Search This Blog

NITAKUFA MARA YA PILI - 4

 









    Simulizi : Nitakufa Mara Ya Pili

    Sehemu Ya Nne (4)



     Nilijua hata kama watachelewa hawatakaa sana nje kutokana na usiku kuwa na kiza kinene na ubaridi mkali. Baada ya muda kidogo nilimsikia mama akilalamika baridi na mbu na kumuomba baba waingie ndani. Walikubaliana kuingia ndani, hapo kidogo nilipumua na kuamini ni nafasi yangu ya kutoroka. Baada ya kuhakikisha wamelala kwa kupita ukimya bila kusikia sauti zao, huku nikiwa sijui muda ule ulikuwa saa ngapi kutokana kiza kuwa cha kutisha na kibaridi cha kupuliza, nilizima kibatari na kutoka kwa kunyata baada ya kufunga mlango kwa kuuegesha. Nilielekea upande ambao niliamini palikuwa salama, ambako kulikuwa na miti ya miembe. Sehemu yenyewe ilikuwa ikitisha, hakuna mtoto au mtu mwenye moyo mdogo aliyeweza kupita kwenye miti ile usiku. Nililiacha eneo la nyumbani, nikaingia sehemu iliyokuwa na kiza cha kutisha. Kutokana na kiza na miti mingi, hakika palikuwa panatisha sana kwa muda ule japo mchana tulikuwa 

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    tukicheza kwenye miembe ile bila woga. Kama kwenda kwa hiyari yangu nisingekwenda hata kwa bunduki, lakini kutokana na hatari iliyokuwa mbele yangu sikutishika na lolote. Nilitafuta mti mmoja ambao haukuwa mrefu sana na kupanda juu hadi kwenye sehemu iliyokuwa na miti imekaa kama Y, sehemu ile niliiona inanifaa sana kwa kujilaza hata kama usingizi ungenipitia nisingeanguka. Kutokana na kutaka kuokoa maisha yangu nilikuwa na ujasiri wa ajabu licha ya kiza kizito na ubaridi uliopepea majani kama vile kuna mtu. Nilitakiwa kuwa na moyo wa chuma. Usingizi ni kitu cha ajabu, pamoja na hofu nzito iliyokuwa imenitawala, usingizi ulinipitia bila kujielewa. Sauti ya watu kubishana chini ya mti ilinishtua kwenye usingizi wa mang?amung?amu. Baada ya kuwasikiliza vizuri niligundua ni wachawi waliokuja kunifuata nyumbani na kunikosa. Nilimsikia mmoja akisema. ?Jamani atakuwa wapi?? ?Hata sisi hatuelewi,? mwingine alijibu. ?We Helena si ulisema umechukua ile ngozi?? ?Ndiyo mama,? Helena hapohapo nikaitambua sauti yake. ?Sasa mbona haonekani?? ?Sijui.? ?Sasa watakuwa wapi?? ?Jamani mtoto yule anataka kutuzidi watu wazima?? ?Lakini yote mmeyataka wenyewe , si watoto wenu wamemfundisha ujanja wetu!? ?Kwani Sabina yupo wapi?? ?Tumemuacha kwao. Tulimpumzisha safari za hatari kutokana na kusema alikuwa amepoteza ngozi yake kumbe alimpa Shija; mtoto mbaya sana yule na lazima tumpe adhabu kali.? ?Sasa jamani atakuwa wapi, kumbukeni tukishindwa kuitumia nafasi hii, itakuwa tunazidi kujiweka sehemu mbaya.? ?Tulitaka leo tukimpata tumle nyama. Mzee Manoni sijui ana ajenda gani na huyu mtoto ambaye mwisho wa siku atatuvua nguo hadharani?? ?Lakini nilisikia akisema kuwa alimkataza kuitoa siri yoyote kuhusu sisi.? ?Huko ni kujidanganya, hivi mtu amuone kaka yake akiliwa nyama asiseme kitu chochote kwa wazazi wake!? ?Ataanzia wapi kusema, na nani atamkubalia kuwa ameshuhudia kaka yake akiliwa nyama.? ?Jamani yote si muhimu zaidi ya kumpata Shija,? mmoja alibadili mada. ?Jamani, inawezekana Sabina amemficha kwao,? mchangiaji nilimfahamu kwa sauti alikuwa Helena. Ilionesha jinsi gani Helena alivyokuwa adui mkubwa, baada ya kauli ile niliwasikia wakimuunga mkono. ?Itakuwa kweli, lazima Sabina atakuwa anajua Shija yupo wapi.? ?Na kweli, tusipoteze muda, maana Manoni anaweza kuwa anamaliza kikao muda huu na kuanza kurudi.? Walitimka kuelekea nyumbani kwao Sabina kunitafuta. Nilitulia juu ya mti hata kupumua kwangu nilipumua kwa taratibu sana kuogopa kusikika. Kila muda ulioongezeka mbele yangu mambo yalizidi kuwa magumu na kuzidi kuniweka katika hali mbaya. Nilijiuliza kama wakinikosa kwa kina Sabina watafanya nini, na mimi niliapa kupambazukiwa juu ya mti. Baada ya kuondoka nilikaa zaidi ya robo saa ndipo nilipoziruhusu pumzi zangu kutoka bila kuzibana. Nilimuomba Mungu ili kuche haraka niweze kwenda kwa mzee Manoni kumueleza ukweli.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijificha mpaka kijua kilipokuwa kikali ndipo niliporudi nyumbani, sikumkuta mtu palikuwa kimya. Niliingia ndani, kutokana na uchovu nilijitupa kitandani na usingizi mzito ulinipitia. Nikiwa kama nipo ndotoni niliota Helena akinilisha kitu vyeusi ambavyo vilikuwa na uchungu wa ajabu. Niliposhtuka nilijikuta nimelala kitandani lakini midomo ilikuwa michungu sana, niliamka na kusukutua kuondoa uchungu. Baada ya kusukutua nilijiuliza ndoto ile ilikuwa na maana gani na kwa nini nimeota ninalishwa vitu vichungu na Helena na nilipoamka nilijikuta midomo ikiwa michungu? Nilijikuta nikikaa kitako na kujiuliza ile ilikuwa ni ndoto au kweli na kama ni kweli nia yake ilikuwa nini? Nikiwa nimekaa kitako nilishtushwa na sauti ya Sabina aliyekuwa akiita kwa sauti ya juu. ?Shija...Shija.? ?Naam, Sabina.? ?Mmh, siamini upo salama?? Sabina alisema huku akiingia chumbani kwangu katika sare ya shule na kujiuliza muda ule ni saa ngapi. ?Sabina kwanza muda huu ni saa ngapi?? ?Saa tano asubuhi nimetoroka shule baada ya kutokewa na kasheshe nzito kuwa nimekuficha na kujiuliza kama ngozi huna utakuwa umejificha wapi?? ?Kwa vipi Sabina?? ?Shija jana usiku umelala wapi?? ?Kwani vipi mbona unaniuliza hivyo ?? ?Nijibu swali, Shija ngozi ipo wapi?? Nilishindwa kumjibu nilibakia nimeinama chini. ?Shija unanizunguka kwa faida yako?? ?Sio hivyo Sabina.? ?Sio hivyo ngozi yangu iko wapi?? Sabina aliniuliza kwa sauti kali kidogo. ?Hata sijui nani kaichukua, jana baada ya kuachana na wewe niliporudi ndani sikuikuta nilitafuta zaidi ya saa tatu lakini sikuiona.? ?Na usiku ulilala wapi?? Nilimueleza ilivyokuwa baada ya kupoteza ngozi na wazo la kwenda kulala juu ya mti na mazungumzo waliyokuwa wakizungumza wachawi mpaka walipofunga safari kumfuata kumuulizia kuhusu mimi. Sabina baada ya kunisikiliza alishusha pumzi na kusema kwa sauti ya masikitiko. ?Shija ilikuwaje Helena akaipata ile ngozi?? ?Helena ndiye aliyeichukua ile ngozi?? nilijifanya kushtuka ili kujifanya sijui lolote. ?Ukweli ndio huo Helena kaichukua na kuipeleka kwa wachawi ili kuhakikisha unakamatwa na kuliwa nyama kama nilivyokueleza . Shija unajua kabisa Helena kaichukua ngozi, alijuaje umeificha chini ya godoro?? ?Ooh, nimekumbuka kuna siku kabla ya kunieleza kuwa niwe naye mbali alinishauri niiweke chini ya godoro.? ?Si unaona kwa nini ulimwambia? Shija kwa nini unanizunguka najitoa kwa ajili yako lakini unaona kazi bure,? Sabina alisema huku machozi ya uchungu yakimtoka . ?Lakini Sabina ukaribu wangu na Helena ni wewe ndiye uliyeuleta na kunitambulisha kama rafiki yako mkubwa. Pia kunisaidia kumtorosha kaka yangu toka kwao ilinipa imani.? ?Shija kama nilivyokueleza Helena si mtu mzuri jiepushe naye ni mtu mbaya sana. Na dhamira yangu ipo pale pale kwa kitendo alichonifanyia sitamsamehe maisha.? ?Dhamira gani tena?? ?Nakuhakikishia lazima nitamuua Helena na wiki haiishi lazima nimuue.? ?Sabina kwa nini usimuache hujui kuua ni kosa kubwa sana?? ?Shija wewe ni mtu wa aina gani usiyejihurumia, kama usingepata akili ya ziada ya kwenda kulala juu ya mti si watu wangekula nyama? Bado mtu huyo unamuonea huruma? Hata useme nini lazima nimuue Helena kwa mkono wangu.? ?Sabina si watajua kuwa umemuua wewe .? ?Potelea mbali na wajue, kumbuka sasa hivi nina wakati mgumu. naonekana msaliti hata mpango wa kumtorosha kaka yako mzigo kanitupia mimi ili tu nionekane nina makosa. Kama mama yangu asingekuwa mzito kwenye chama cha wachawi ningefanywa kitu kibaya. ?Nilimsikia mama akiwaeleza kwamba mtu atakayenigusa atamjua yeye ni nani?? Wakati nazungumza na Sabina tumbo lilianza kunikata, nilishika tumbo na kuanza kupiga kelele za maumivu. ?Sabina nakufa tumbo linanikata,? nilisema kwa maumivu huku nimeinama. ?Umefanya nini tena?? Sabina alishtuka. ?Hata sijafanya kitu.? ?Umekula nini?? ?Viazi na uji.? ?Ha! Shija mbona ulimi wako mweusi?? Sabina alishtuka kutokana na kugundua ulimi wangu ni mweusi kama nimetafuna mkaa. ?Sabina nimeota nalishwa vitu vyeusi vichungu na Helena kwenye ndoto nilipoamka nilikuta midomo michungu hata mate nilipotema yalikuwa meusi.? ?Hebu,? Sabina alininusa mdomoni. ?Mungu wangu! Unaona sasa.? Sabina bila kunisaidia nilipoanguka chini aliniacha na kutimua mbio bila kujua anakwenda wapi. Nilibaki nimelala chini huku nikiugulia tumbo ambalo lilikuwa likinikata kama kuna mtu anaukata utumbo kwa ndani. Nilianza kuhisi kizunguzungu na kiza kizito mbele yangu. Mauti niliyaona mbele yangu huku nikishangaa kwa Sabina kuniacha bila kunipa msaada wowote . Niliamini kabisa alikuwa amekasirika kutokana na kumdanganya, na uzembe wa kuipoteza ngozi yake muhimu. Nilijiona nikifa, nilijilaumu kwa ukimya wangu wa kuwaficha wazazi wangu na mwisho wa siku nilikuwa nakufa najiona.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikiwa nimeanza kupoteza uwezo wa kusikia na kuona, kwa bali nilisikia sauti ya kilio cha Sabina. Kwa kweli nilichokisikia kilikuwa kilio lakini maneno aliyokuwa akisema sikuyasikia . Niliposhtuka nilijikuta nimelala kitandani pembeni yangu alikuwa Sabina ambaye alikuwa bado katika vazi la shule. Uso wake ulikuwa umetawaliwa na michirizi ya machozi, nilipofumbua macho alishtuka. ?Shija!? ?Eeh.? ?Unajikiaje?? Kabla sijamjibu nilisikia kichefuchefu kilichonifanya ninyanyuke kutoka nje, lakini sikuweza. Niliyumba, mwili haukuwa na nguvu. Sabina alinisaidia kunitoa nje kwenda kutapika. Nilipofika nje nilitapika vitu vyeusi vya ajabu hata sikujua nilikula saa ngapi na vilipitia wapi. Baada ya kutapika nilianza kuharisha kinyesi cheusi. Katika maisha yangu sitamsahau Sabina kwani alinihudumia kwa hatua zote baada ya kunisafisha alinikorogea uji. Kilichonisaidia ni kwamba muda ule wakati wazazi wangu walikuwa bado wapo shamba na muda wao wa kurudi ulikuwa bado. Sabina alinishughulikia kwa kuninywesha uji wa dawa ya kutoa sumu niliyolishwa na Helena nikiwa nimelala. Baada ya kuninyesha uji wa dawa aliniomba nilale ila aliniomba niwaeleze wazazi wangu ibakie siri. Nilikubaliana naye muda nao ulikuwa umekwenda sana aliwahi nyumbani kwao na mimi kupitiwa usingizi mzito. Nilishtushwa na sauti ya baba ambaye alishtushwa kwa kunikuta nikivuja jasho mwili mzima mpaka sehemu niliyokuwa nimelala ilikuwa imelowa. ?Shija unaumwa?? baba aliniuliza huku akiweka mkono wake kichwani kwangu kupima joto la mwili. Nilipojiangalia nilijikuta nikivuja jasho mwili mzima, nguvu zilikuwa kwa mbali. Lakini niliweza kutembea mwenyewe bila msaada wa mtu. Niliangalia nje na kubaini kuingia kwa kiza kutokana na muda kuwa umekwenda sana. ?Vipi mbona upo hivi?? baba aliniuliza. ?Sijisikii vizuri.? ?Tatizo nini?? ?Labda malaria.? ?Asubuhi ulienda wapi?? ?Nilikwenda shule, kumbe niliondoka muda bado na kujikuta nimewahi shule peke yangu, ? ilibidi nitunge uongo ili kuepusha maswali ambayo niliamini nisingeyajibu. Kutokana na kutokwa na jasho jingi nilikwenda kuoga ambapo kidogo hali yangu ilibadilika na kujisikia nikipigwa na hewa safi iliyoupa nguvu mwili wangu. Baada ya kutoka kuoga baba aliniletea dawa ya miti shamba ambayo tulikuwa tukiitumia pale mtu aliposhikwa na malaria. Baada ya kunywa dawa njaa kali ilikuwa imenishika, bahati nzuri kulikuwa na viazi vilivyo bakia mchana; nilivila ili kupunguza njaa na kusubiri chakula cha usiku. Nilipomaliza kula nilirudi tena kitandani na usingizi haukuchelewa kunichukua. Nilishtushwa chakula kilipokuwa tayari, nikala na kurudi tena kulala. Kutokana na mwili kuwa umechoka nilipolala usingizi ulinichukua tena. Katikati ya usiku nilishtushwa na sauti za vishindo vya watu nje ya nyumba yetu, nilijikuta nikiitafuta ngozi yangu chini ya godoro lakini nilikumbuka ilichukuliwa na Helena. Nilijikuta nachanganyikiwa . Niliamini ujio ule ulikuwa wa kuja kunichukua baada ya usiku wa jana yake kunikosa. Akili ya haraka ilikuwa ni kupiga kelele ili baba aamke, lakini kabla sijafanya vile ukuta ulipasuka na kuingia watu wanne ambao walinikamata huku wakisema. ?Leo huna ujanja.? Niliwekewa kipande cha mti mdomoni kilichofungwa na kamba na kuwa kama nimekiuma na meno. Sikuwa na ujanja nilijua kweli nimepatikana. Nilibebwa juujuu na kutolewa nje ambako kulikuwa na mbalamwezi kama mchana. Nje kulikuwa na watu zaidi ya kumi na tano, baada ya kuniona walilipuka kwa shangwe, niliamini baada ya kunitafuta kwa udi na uvumba kwa muda mrefu hatimaye walinipata. Nilimuomba Mungu aniepushe na kifo kile cha kuliwa nyama, japo kifo ni haki ya kila kiumbe, lakini kifo changu nilikiona ni kibaya kwa wanadamu wenzangu kunigeuza asusa. Safari ya kuingia porini ilianza nilijua ilikuwa ya kwenda kwenye mti wa kukutania ili wanigawane nyama. Sikuwa na jinsi kwani mti uliowekwa mdomoni ilinifanya nishindwe hata kumeza mate. Nilijiona nitakufa hata kabla ya kugawanwa nyama. Baada ya kwenda mwendo mrefu kidogo, ghafla nilisikia kitu kama bakora zikitandikwa na watu walipiga kelele.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Walionibeba walinitupa chini baada ya kushindwa kuvumilia ukali wa bakora ambazo zilipigwa kwa nguvu na sauti yake ilipasua anga. Nilipatwa na mshtuko na kujiuliza nini kimetokea, ghafla niliwaona wote waliokuwa wamenibeba wakipiga magoti kama wanaomba msamaha. Sikuamini macho yangu kumuona mzee Manoni akiwa ameshikilia bakora ya mkia wa taa. Kwa sauti ya hasira aliunguruma na kusema; ?Tumekuwa tunazungukana, sasa nasema hivi kila aliyeshiriki kutaka kutoa uhai wa kijana huyu ataleta mtoto wake mmoja aliwe nyama kama adhabu ya usaliti wenu. Tumekubaliana leo tupumzike kumbe mlikuwa na yenu ya kunizunguka?? ?Tusamehe mkuu.? ?Siwezi kuwasamehe kwa kunizunguka kila siku mna kwenda kinyume na maagizo, sasa mama Helena na wenzako nataka mtu mmoja kila ukoo ili muone raha ya kutaka kula nyama za wenzenu.? ?Tusamehe mkuu haturudii tena.? ?Natoa onyo la mwisho kijana huyu akifa au akipotea kwenye mazingira ya kutatanisha mtanijua Manoni ni mtu wa aina gani, uchawi niwafundishe mwenyewe leo mtake kunizidi akili! Chonde chonde muogopeni kijana huyu kama ukoma, haya poteeni.? Baada ya kusema vile wote walikurupuka na kutimua mbio kwa kila mmoja kupitia njia yake. Mzee Manoni alinifungua kamba na kukitoa kipande cha mti. Baada ya kukitoa kipande hicho nilijikuta nikipata shida kumeza mate kutokana kutomeza mate kwa muda mrefu na koo kukauka. Mzee Manoni aliiona hali ile, alichukua majani pembeni aliyoyafikicha na kunikamulia kidogo mdomoni ambapo koo lililainika. Alikiangalia kile kijiti kisha alisema kwa sauti ya chini. ?Pole sana, watu hawa walikuwa wamedhamiria kukufanya nyama, kijiti hiki hutumika kumwekea mtu anayekwenda kuliwa nyama. Ningechelewa kidogo wangekupigilia msumari kwenye utosi na juu ya sikio kabla ya kukufikisha kilingeni kwa kukugawana nyama.? ?Asante mzee wangu.??Nakuhakikishia kila atakayekugusa nitamfanya kitu kibaya.? Baada ya kusema vile alinirudisha hadi nyumbani na kuniingiza chumbani kwangu, aliniacha nilale huku akinisisitiza kuwa nisimwambie mtu kila kitu kilichotokea. Nilijikuta nikijiuliza kama asingetokea mzee Manoni si nilikuwa naliwa nyama? Nilijiuliza mzee Manoni alijuaje kama nimechukuliwa kwenda kuliwa nyama, lakini niliamini huenda ni uwezo wake wa kichawi ndiyo uliomfanya agundue njama za kutaka kunila nyama. Nilimshukuru Mungu usingizi ulinipitia mpaka nilipogongewa na baba asubuhi kutaka kujua hali yangu. ?Shija umeamkaje baba?? ?Sijambo baba, kama hali itaendelea hivi kesho nitaenda shule.? ?Basi pumzika usiende popote sawa baba.? ?Sawa baba.? Mama naye alinijulia hali ikiwa pamoja na kunipa maelekezo ya chakula na dawa ya malaria aliyonipa jana akiamini kutokwa na jasho ilikuwa na malaria kumbe dawa aliyonipa Sabina ilikuwa ikitoa sumu niliyolishwa ndotoni na Helena. Baada ya maandalizi yote, waliondoka na kwenda shambani na kuniacha na mdogo wangu wa kike ambaye naye siku ile hakwenda shule kutokana na kutojisikia vizuri. Kwa vile bado mwili ulikuwa na mchovu nilirudi ndani kulala mpaka niliposhtuliwa na Sabina. Kama kawaida alikuwa katika sare ya shule, aliponikuta nimejilaza alinitazama kwa jicho la huruma. ?Vipi Sabina?? ?Mmh kawaida, pole sana.? ?Asante.? ?Bila mzee Manoni jana ulikuwa unaliwa nyama.? ?Umejuaje?? ?Hivi unafikiri bila kumfuata mzee Manoni ungepona.? ?Sabina! Wewe ndiye uliyemfuata mzee Manoni?? ?Shija mpango wao wote wa kuahirisha kikao cha kila siku cha wachawi ili kumfanya mzee Manoni apumzike na wao kumzunguka ili wale nyama yaako niliungundua. Walipoanza safari ya kuja kukuchukua nilikimbilia kwa mzee Manoni. ?Huwezi kuamini nilipomueleza kilichotaka kufanywa na kundi la wale wachawi kukula nyama alishtuka sana. Nilimueleza na muda ule wamekufuata ili wakakule nyama, ndipo tulipoondoka na mzee Manoni kukufuatilia na kukuona amekubeba wakikupeleka eneo ambalo wangekula nyama yako. ?Kwanza walituchenga njia, lakini tulipita njia nyingine kuwahi eneo ambalo hutumia kutoa uhai wa mtu na kumpigilia msumari au kipande cha mti utosini na juu ya sikio kama ishara kuwa umeishakuwa nyama tayari kuliwa. Muda wote nilikuwa na wasiwasi kabla ya kukuona njia nzima nilikuwa nalia huku mzee Manoni akinituliza kuwa hawawezi kukuua. Nilifurahi kukuona bado wamekubeba japo sikujua upo katika hali gani, mzee Manoni alitoa mkia wake wa taa na kuwasogelea bila wao kumuona mimi nilijificha pembeni ili wasinione na kujua ndiye niliyetoa siri ile. Alipofika kama ulivyoona aliwatandika bakora kisha aliwapa adhabu. Wakati huo mimi nilikimbilia nyumbani kilichoendelea sikukijua. ?Ila elewa mimi na Helena sasa hivi ni chui na paka japo mwalimu Vene alituita kutupatanisha, nilimhakikishia mwalimu sitamsamehe Helena mpaka tunaingia kaburini.? ?Sabina kwa nini umeonesha chuki za wazi kwa adui yako?? ?Alichonifanyia siwezi kukifumbia macho, hivi kama wewe ungeliwa nyama angepata faida gani? Lakini kwa nini Shija huruma zimekuzidi kwa nini unamuonea huruma mtu asiyetaka kukuona ukiendelea kuishi?? ?Najua Helena ni mbaya lakini ukitaka kumpata adui yako muoneshe mapenzi.? ?Katu sitamuonesha mapenzi na wiki hii haiishi utasikia jambo zito.? ?Vipi masomo?? Ilibidi nibadili mazungumzo kwani kila dakika Sabina hasira zilikuwa zikimpanda.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ?Shule safi, vipi mdogo wako leo hakwenda shule?? ?Hajisikii vizuri? ?Na wewe vipi unasendelea?? ?Kidogo sijambo kesho naweza kuja shule? ?Njoo bwana si unajua mtihani umekaribia.? ?Nitakuja usiwe na wasi, lakini Sabina sijui nilikulipe nini umeokoa maisha yangu kila kukicha? ?Ni kweli, lakini vita ni nzito kama unaweza ungekwenda kusomea mjini kwa mjomba wako.? ?Sabina tumechelewa kwa sasa siwezi kuhama zaidi ya kuvumilia mpaka nimalize mtihani.? ?Shija pamoja na jitihada zangu wameanza kunishinda na mwisho wa siku watafanikiwa dhamira ?Basi nikimaliza mtihani nitakwenda kusomea kwa mjomba, kule wapo ndugu zangu wawili mjomba aliwachukua.? ?Vipi na dawa unaendelea kutumia?? ?Namalizia usiku.? ?Tumia tuangalie, uchawi aliokulisha ulikuwa unakukausha.? ?Mungu wangu.? ?Mungu wangu? Ujue Helena alivyonyoka kwanza urafiki wetu unatokana na uchawi si wa moyoni.? ?Sabina sina cha kukulipa.? ?Nataka tukiwa wakubwa unioe.? ?Kwanza naomba tusome kwa bidii na yote ninayokuelekeza kwenye masomo yazingatie ili ikiwezekana uwe mmoja wa wanafunzi watakaofaulu kwenda kidato cha kwanza.? ?Lakini Shija kwani siku hizi darasani unanionaje?? ?Kweli unajitahidi si kama mwanzo.? Tokea siku ile niliishi kwa amani sikuguswa wala kutokewa na mambo ya mauzauza. Darasani Helena aliniogopa hata kunitazama alishindwa, lakini sikutaka kumuuliza chochote kutokana na ubaya wake. Sabina alinieleza jinsi walivyo maadui wakubwa na Helena na kunieleza alivyokusudia kumfanyia kitu cha kuwaacha watu midomo wazi. Sikutaka kumkataza kutokana na kuonekana kunitetea mimi kuliko uhai wake. Siku moja jioni baada ya kutawanyika wanafunzi nilishangaa kumuona Sabina akibakia shule, katika kumbukumbu zangu Helena alitoka mapema baada ya kuitwa na mwalimu Vene. ?Sabina twende zetu.? ?Shija tangulia.? ?Hapana Sabina wawili ni wawili .? ?Shija nielewe we tangulia kwa leo.? ?Au umepata rafiki mwingine?? ?Shija nakuomba uwe muelewa mengi tutaongeza kesho kama Mungu atatufikisha salama.? ?Kwani kuna nini?? ?Shija tutazungumza kesho mpenzi wangu.? ?Kama umepewa adhabu niambie tuifanye wote.? ?Hata ya viboko?? Sabina alinitania hapo kidogo alitabasamu kwa mbali. ?Nipo tayari Sabina hata nichapwe peke yangu viboko vyote .? ?Asante kwa kunijali ila nakuomba kwa leo tangulia ila kesho utajua kila kitu sababu ya mimi kuchelewa kuondoka.? ?Sikutaka kumlazimisha, niliondoka zangu kurudi nyumbani huku nikishangaa hali aliyokuwa nayo Sabina toka nilipomjua sikuwahi kumuona kwenye hali ile. Siku ya pili nilishangaa kutomuona Sabina wala Helena darasani, nilijuliza sana nini kimetokea hasa baada ya Sabina kuchelewa kutoka shuleni pia kuwa katika hali isiyo ya kawaida. Tukiwa darasani nilishangaa kuona gari la polisi likija shuleni. Baada ya gari kusimama polisi mwenye sale na cheo cha nyota moja aliingia kwenye ofisi ya mwalimu mkuu. Haikuwa kawaida polisi kuja shule kutokana na kuwa mbali na tunapoishi. Ofisi za polisi zilikuwa katikati ya mji na sisi kwenda mjini kwa baiskeli tulikuwa tunatumia nusu saa. Kutokana na ushamba wa wanafunzi tuliwashangaa polisi waliokuja shule. Baada ya muda alikuja mwalimu darasani na kuniita. ?Shija.? ?Naam, mwalimu.? ?Njoo mara moja ofisi ya mwalimu mkuu.? Ujumbe ule ulinishtua, nilijuliza naitwa ofisini kwa mwalimu mkuu ambako ndipo alipoingia polisi, kuna nini? Katika maisha yangu yote tulifundishwa polisi hukamata wahalifu. Nilijiuliza nimekosa nini? Nilikwenda huku natetemeka. Nilipoingia darasani mwalimu mkuu alisema: ?Huyu ndiye Shija,? ?Shija hujambo?? askari alinisalimia. ?Sijambo, shikamoo!? ?Marahaba.? ?Shija unatakiwa kituoni mara moja.? ?Ha! Mwalimu nimefanya nini?? ?Shija usiwe na wasi, wewe ni rafiki yangu.? Askari alisimama na kunishika mkono na kutoka naye hadi kwenye gari lao Land Rover 110. Nilipandishwa kwenye gari; kilichonipa moyo kilikuwa baada ya kumuona mwalimu mkuu naye tunaongozana naye. Baada ya mwalimu mkuu kupanda, safari ya kurudi mjini iliiva. Ndani ya gari nilijawa na mawazo mengi toka nizaliwe sijawahi kupelekwa polisi na anayepelekwa polisi ni mhalifu. Lakini sikutaka kuhoji sana baada ya kuongozana na mwalimu mkuu. Safari yetu ilitumia robo saa kufika kituo cha polisi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kufikishwa nilitelemshwa peke yangu, lakini mwalimu aliondoka na baadhi ya askari kwenye gari tulilokuja nalo. Askari niliyetoka naye ofisini ndiye niliyeteremka naye na kuingia polisi. Nilijiuliza mbona tumeteremka wawili wengine wameondoka na gari akiwemo mwalimu mkuu? Baada ya kuingia ofisini niliamrishwa kukaa kwenye kiti, mbele kulikuwa na meza kubwa na nyuma yake kulikuwa na kochi refu kama kiti. Baada ya kuketi polisi alizunguka upande wa pili na kuketi kwenye kiti chake. Kabla ya kuzungumza alifunua faili moja ambalo alisoma kwa muda kisha alinyanyua kichwa chake na kusema: ?Wewe ndiye unayeitwa Shija Matulanya?? ?Ndi..ndi..yo Mkuu.? ?Unasoma darasa la ngapi?? ?La saba.? ?Unamjua Sabina?? ?Ndiyo.? ?Helena?? ?Ndiyo.? ?Unawajua vipi watu hawa?? ?Kama wanafunzi wenzangu.? ?Zaidi ya hapo?? ?Sina zaidi ya hapo.? ?Nikikuambia wale ni wapenzi wako na ni utovu wa nidhamu kujihusisha na mapenzi ukiwa bado mwanafunzi utakataa?? ?Nani, mimi?? swali lile lilinichanganya na kujiuliza kama wapenzi wangu kuna sababu gani ya kuletwa kuhojiwa polisi. ?Humu ndani tumo wangapi?? ?Wawili.? ?Sasa hapa nazungumza na nani?? ? Na mimi.? ?Haya nijibu.? ?Si kweli.? ?Si kweli nini?? ?Sina uhusiano na yeyote .? ?Nikiwaita hapa mbele yako wakakiri kuwa wewe ndiye mpenzi wao utasemaje?? Swali lile lilinifanya niiname chini kwa vile ilionesha labda Sabina ametoa siri yetu, hata hivyo , nisingekuwa tayari kukubali kuwa na uhusiano na Sabina kutokana na kuwa mwanafunzi na kosa lile lazima ufukuzwe shule. ?Shija.? ?Naam.? ?Una taarifa gani kuhusu wapenzi wako?? Sikumjibu neno nilikaa kimya kwa vile swali lile lilikuwa gumu kujibu kwa vile sikujua chochote kuhusiana na wasichana wale, baada ya kuona kimya kimezidi aliniuliza swali jingine: ?Unajua nini kuhusiana na ugomvi wa Sabina na Helena?? ?Sijui chochote.? ?Jana uliachana nao saa ngapi?? Nilitulia kuvuta kumbukumbu na kukumbuka Sabina kumuacha shuleni, ila Helena toka alipoitwa na mwalimu Vene sikumuona mpaka naondoka. ?Sabina nilimuacha shuleni ila Helena toka alipoitwa na mwalimu sikumuona mpaka naondoka.? ?Sabina ulimuacha anafanya nini?? ?Sikujua alikuwa anafanya nini, tuna kawaida ya kuongozana kila siku tukitoka shule, lakini jana nilipomfuata aliniambia nitangulie.? ?Baada ya hapo?? ?Nilikwenda nyumbani.? ?Ulipofika shuleni umepata taarifa gani kuhusu wao?? ?Sijapata taarifa yoyote ,? maswali yale yalizidi kuniweka njia panda na kujiuliza kuna nini? ?Leo shule umewaona?? ?Hata mimi nashangaa leo sijawaona.? ?Unajua kuna mauaji yametokea.? ?Mauaji?? nilishtuka. ?Ndiyo.? ?Mungu wangu mauaji ya nani?? ?Ya Helena.? ?Helenaaaa?? ?Ndiyo na sababu ni wewe . Jana jioni Sabina kampiga Helena na kitu kigumu kichwani na kumsababishia hali mbaya sana.? Kauli ile ilinifungua macho na kujua kumbe kubaki shule Sabina alikuwa na maana yake. Moyoni niliamini wasichana wale kutokana na kazi ya uchawi wamekuwa na mioyo migumu. Mkuu wa upelelezi alinishtua nilipokuwa nimepigwa bumbuwazi. ?Shija.? ?Na..a..m.? ?Kwa taarifa yako wewe ndiye utakayesaidia upelelezi baada ya kutajwa na Sabina kuwa sababu ya ugomvi uliosababisha hali mbaya ya Helena ambaye kwa sasa amehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando. Sabina anashikiliwa na polisi na wewe utasaidia polisi mpaka hapo yatakapopatikana maelezo mengine.? Kauli ile ilinifanya niangue kilio cha juu mlemle ofisini wakati huo askari alinifuata na kunipeleka kwenye chumba kilichokuwa na mtoto mmoja. Niliendelea kulia huku nikijua nitafungwa kwa kosa lisilokuwa langu, kijana niliyemkuta mle ndani aliniomba nisimpigie kelele kwa vile alikuwa akitaka kulala. Sauti yake ya kitisho ilinifanya ninyamaze na kulilia moyoni. Moyoni nilijawa na maswali na kujiuliza Sabina yupo wapi? Na kama Helena atafariki itakuwaje? Nilikuwa nafahamu kila anayeua uhukumiwa kunyongwa nilijiuliza kama wanasema chanzo ni mimi lazima na mimi nitanyongwa . Nilijikuta nikilia tena kwa sauti ya chini kuogopa kumuamsha mwenzangu aliyekuwa amelala pembeni yangu. Nikiwa bado kwenye hofu kuu ya kunyongwa kama Helena atakufa, mlango ulifunguliwa na askari aliyeniingiza mule chumbani aliniita. ?Shija.? ?Naam.? ?Njoo.?



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipotoka nje nilishangaa kumkuta baba na mama ilionekana hata nguo zao za kulimia hawakubadili. ?Shija,? mama aliniita. ?Naam mama.? ?Pole sana.? ?Asante.? Sikuelewa kilichoendelea zaidi ya kumsikia afisa wa polisi akimwambia baba. ?Kesho mumlete asubuhi.? ?Sawa Mkuu.? Baada ya kusema vile baba alitupakia katika baskeli, mama alikaa nyuma mimi kwenye mgomba. Tulirudi nyumbani njiani sikuambiwa kitu mpaka tulipofika nyumbani. Baada ya kufika kabla ya kuingia ndani nilifanyiwa tambiko dogo kisha nilivua nguo za shule nilizoingia nazo mahabusu na kwenda kuoga. Nilipotoka kuoga nguo zangu zililowekwa kwenye maji ili kuondoa nuksi, siku zote ilifahamika kama nuksi kwa mtu kuingizwa polisi au jela. Tambiko lile fupi lilikuwa kama kuisafisha nuksi iliyonipata isirudie tena au kumpata mtu yoyote ndani ya familia yetu. Tambiko dogo lilipokamilika niliruhusiwa kuingia ndani, baada ya muda niliitwa na wazazi wangu kutaka kujua kisa na mkasa na walichoelezwa ni kweli. ?Shija unajua sababu ya wewe kupelekwa polisi?? ?Ndiyo.? ?Sababu gani?? ?Eti wanasema kuwa Sabina na Helena ni wapenzi wangu.? ?Wanasema kina nani?? ?Nimeambiwa na polisi mkubwa.? ?Shija umeambiwa au kuna ukweli?? ?Hakuna ukweli wowote juu ya tuhuma hizo.? ?Mbona kuna tetesi Sabina huwa anaonekana hapa sana.? ?Ni kweli, huwa kwa ajili ya masomo tu na si kingine.? ?Iweje aseme wewe ni mpenzi wake?? ?Sijui, lakini si kweli.? ?Shija hebu tueleze ukweli sisi ni wazazi wako una mahusiano gani na wasichana wale kufikia hatua ya kutaka kuuana?? ?Baba sina uhusiano wowote .? ?Taarifa tulizopewa na mkuu wa polisi alizoambiwa na Sabina kuwa wewe ni mchumba wake na uhusiano wenu ni wa muda mrefu ila Helena ambaye ni shoga yake alitaka kumpindua na kuchukua uamuzi wa kumshikisha adabu.? ?Baba Sabina ni rafiki yangu sana na si mchumba wangu japo huwa tunataniana, kuhusu Helena nilimjua kupitia kwa Sabina. Hakuna kingine juu yangu na wao zaidi ya urafiki.? ?Shija mimi baba yako ninajua mengi, Sabina na Helena ni wapenzi wako, lakini chonde usikubali polisi kuwa wale ni wapenzi wako. Ukikubali umefungwa.? Ajabu baba baada ya kusema vile hakuchukua uamuzi wowote zaidi ya kuendelea na kazi ndogo ndogo za nyumbani. Siku ile kazi ya shamba haikufanyika baada ya kukurupuka walipopata taarifa zangu za kuchukuliwa na polisi. Kesho yake nilirudishwa polisi tena kwa ajili ya kuendelea na upelelezi wao, hali ya Helena ilikuwa bado mbaya kitu kilichosababisha Sabina aendelee kuwa ndani mpaka pale hali ya Helena ingekuwa katika unafuu. Siku nilipopelekwa baba ndiye aliyeingia na kuongea na afisa wa polisi kisha alinipitia na kuondoka na mimi kunirudisha nyumbani. Siku ya pili nikiwa nyumbani peke yangu baada ya baba kwenda shamba na wakati huo shule nilisimamishwa kwa kuchanganya mapenzi na masomo. Nikiwa sina hili wala lile macho yangu hayakuamini kumuona Sabina akija nyumbani. Bila kujielewa nilijikuta nimenyanyuka na kwenda kumpokea Sabina kwa kumkumbatia. ?Ha! Sabina?? ?Ndiyo mimi.? ?Pole sana.? ?Nikupe pole wewe .? ?Siamini ilikuwaje?? ?Yaani Shija najilaumu nimefanya kosa la kijinga sana.? ?Lakini si nilikuambia uachane wa wazo lile.? ?Sijuitii kumpiga Helena.? ?Sasa unajilaumu kwa lipi?? ?Kosa nililofanya kumpiga Helena njia wanayopita watu kila mara, kama ingekuwa kwenye majani wangeokota maiti siku ya pili.? ?Sabina huogopi kunyongwa ?? ?Bora ninyongwe kuliko kuishi na hasidi kama yule.? ?Na mbona umetoka?? ?Nimepewa dhamana.? ?Lakini nasikia hali ya Helena ni mbaya?? ?Tena naomba afe.? ?Sabina si utanyongwa ?? ?Wacha ninyongwe , Shija bado unamuonea huruma Helena mtu aliyetaka kukula nyama?? ?Hapana Sabina, nakuonea huruma wewe sitaki nikupoteze.? ?Nataka kukuhakikishia hata Helena akifa sinyongwi wala kufungwa .? ?Kwa sababu gani unasema hivyo ?? ?Leo siwezi kukueleza tusubiri afe.? ?Je akipona?? ?Dhamira yangu ipo palepale lazima nimuue kwa mkono wangu.?    


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Baada ya wiki Helena alitoka hospitali akiwa hajambo lakini kichwani alikuwa na bandeji kuziba kidonda ambacho kiliendelea kupona. Siku ya pili toka Helena atoke hospitali kiliitishwa kikao cha shule kuzungumzia kilichotokea walikuwepo wazazi wetu wote na wanakamati ya shule. Kwa upande wetu tulikuwepo wote Sabina Helena na mimi, kikao kilifanyika kwenye darasa moja. Baada ya wajumbe kutimia mwalimu mkuu alieleza kilichotokea. Kisha alimuomba Helena aeleze sababu ya ugomvi wao, moyo ulinienda mbio na kujiuliza atasema nini ikifika zamu yangu. Baada ya kusimama aliinama bila kusema kitu. ?Helena hebu eleza kilichotokea,? mwalimu mkuu alimuhimiza. ?Mwalimu mimi sijui lolote nilishtukia tu napigwa na kitu kizito kichwani hata kujitetea sikuweza mpaka nilipopoteza fahamu.? ?Unamjua aliyekupiga?? Mzazi mmoja aliuliza. ?Sabina.? ?Ulimuona?? ?Mama aliniambia.? ?Ina maana hukumuona?? ?Ndiyo.? ?Unafikiria kwa nini Sabina ambaye ni shoga yako alikupiga?? ?Sijui.? ?Siyo kwamba mnamgombania Shija?? ?Hata siku moja, Shija sina uhusiano naye wa kimapenzi lakini Sabina kwa mdomo wake alinitamkia kuwa Shija ni mpenzi wake.? ?Alikuambia lakini hukuona? ? ?Nimewaona wakiwa wawili kila baada ya muda wa masomo.? ?Unaweza kukaa,? Helena aliruhusiwa kukaa, mimi moyo ulinienda mbio nikijiuliza nitasema nini nikiulizwa. Sabina alinyanyuliwa na kuelezwa naye aseme sababu ya kutaka kumtoa roho mwenzake. Sabina baada ya kusimama naye hakusema neno alibakia kimya akiwa ameinama. ?Sabina hebu tueleze sababu ya ugomvi wenu,? mwalimu mkuu alimuhimiza kusema. ?Helena anajua,? Sabina alijibu kwa ufupi. ?Anajua nini?? ?Siwezi kukisema hapa ila mwenyewe anajua.? ?Tunasikia kwa ajili ya kumgombea Shija?? ?Si kweli kuna kitu anakijua Helena awe muwazi na mkweli.? ?Sabina usitake kutufanya sisi watoto wenzio tunataka maelezo yako na si ujinga unaotujibu.? ?Sina cha kueleza mkitaka kujua muulizeni Helena,? Sabina alionesha kiburi cha wazi. ?Eti Helena unajua nini?? ?Mimi sijui lolote.? ?Mmh makubwa, Shija na wewe unajua nini kuhusu ugomvi huu?? Swali lilielekezwa kwangu. Kabla ya kujibu nilijipa moyo kuweza kuzungumza kutokana na mapigo ya moyo kunienda kwa kasi. Baada ya kujipa ujasiri nilisema; ?Sijui lolote.? ?Kuna taarifa kwamba muda mwingi huwa mpo karibu na Sabina ni kwa sababu gani?? ?Siku za nyuma Sabina na Helena niligombana nao na tulipopatanishwa tulikuwa marafiki kwa kushirikiana katika masomo.? ?Lakini mbona tumeambiwa ni mpenzi wako?? ?Si kweli.? Baada ya maelezo yetu sote watatu tulitolewa nje kuwaacha wazazi watujadili, mimi na Sabina tulikaa karibu lakini Helena alikaa mbali wala hakutaka kututazama. Uso wa Sabina ulionesha kujaa hasira na machozi kumtoka tofauti na Helena alikuwa mkavu, niliamini Sabina pamoja na kushiriki mambo ya kichawi lakini moyo wake ulikuwa umejaa utu. Lakini Helena alikuwa na roho ya kinyama ya kula nyama ya mtu bila huruma. Muda wote tuliokaa nje tulikuwa kimya kila mtu akitafakari lake, baada ya kikao tuliitwa wote ndani kuelezwa kulichojadiliwa. Uso wa baba ulionesha kuwa na hasira. Lakini mwalimu alimpoza kwa kumueleza; ?Mzee Matulanya bado una nafasi ya kupinga hukumu hii?? ?Huu ni upumbavu kugombana wagombane watoto wenu adhabu apewe mtoto wangu.? ?Kwa sababu yeye ndiye chanzo.? ?Mna uhakika kuwa yeye ndiye chanzo?? ?Ndiyo maana nikasema bado una nafasi ya kupinga hukumu hii.? ?Hivi kesi ya nguruwe ukimpelekea nyani unategemea kupata haki? Sasa nawaeleza kesi hii haiishii hapa tutafika mbali. Haiwezekani muone mtihani umekaribia mumsimamishe mwanangu kwa vile ana akili ili asipasi.? ?Mzee Matulanya mbona umefika mbali?? ?Sina muda tutajuana muda si mrefu.? Baba alisema kwa hasira na kunishika mkono kunitoa nje ya darasa huku akiendelea kubwata. Sikutaka kumuuliza kitu lakini kwa mazungumzo yake ya sauti ya juu ilionesha wazi mimi peke yangu ndiye niliyesimamishwa shule kwa ugomvi wa watu wengine. Njia nzima alikuwa akifoka kwa sauti ya juu, ilikuwa mara ya kwanza kumuona baba akilalama njia nzima kwa sauti ya juu kiasi kile. Nakumbuka siku aliyofoka lakini si sana ilikuwa siku nilipoambiwa kuwa mimi mtoto wa mchawi. Tulipofika nyumbani bado baba alikuwa na hasira. ?Shija nisubiri hapa ngoja nifike shambani mara moja, ila suala hili nitaliamkia asubuhi kwenda mjini kwa mjomba wako.? Baba aliondoka na kuniacha nikiwa njia panda kuhusu hatima yangu ya muda uliobakia wa kufanya mtihani wa taifa wa darasa la saba. Nilijikuta nikiumia moyoni baada ya kuona kuna kila dalili za kukosa kufanya mtihani. Nilijiuliza walitumia kigezo gani cha ugomvi wa Sabina na Helena kunisimamisha peke yangu. Nilianza kuingiwa na wasiwasi wa ukaribu wangu na Sabina na kuona huenda anatumiwa na wachawi ili kunikwamisha kimasomo kwa kuanzisha ugomvi wa uongo na ukweli ili tu mimi nisimamishwe shule na kukosa mtihani muhimu sana kwangu. Lakini upande wa pili moyo ulionesha dhamira ya ajabu ya Sabina kuhakikisha nipo salama kwa kujitoa kwa kila kitu juu yangu. Nilijikuta nikijipinga mwenyewe mawazo yangu juu ya Sabina. Nikiwa bado namtathmini Sabina mara nilimuona akija mbio nyumbani nikashtuka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Shija... Shija,? aliniita jina langu hata kabla hajafika nyumbani. ?Vipi Sabina mbona hivyo ?? ujio wake ulinitisha. ?Shija... Shija,? Sabina alisema huku akihema kwa kushika magoti, ilionesha amekimbia umbali mrefu. ?Sabina mbona sikuelewi, kuna nini?? ?Mmh, wee acha! Baada ya vitisho vya baba yako kumetokea malumbano mazito, kidogo mwalimu mkuu ashikane na mama Helena ambaye alikuwa akishabikia ufukuzwe kabisa shule. Lakini mwalimu mkuu amesema lazima ufanye mtihani wa mwisho. ?Basi hapo ndipo kazi ilipoanza, baadhi ya wazazi wakitaka usimamishwe kwa wiki na wengine wakitaka ufukuzwe kabisa.? ?Sasa nini kilichoamuliwa?? ?Mwalimu mkuu amesema lazima utafanya mtihani na ile adhabu ya kusimamishwa amesema ataitengua ili kesho uende shule.? ?Wazazi walisema nini?? ?Mama Helena kamwambia mwalimu akikurudisha shule ataona cha moto labda sio yeye . ? ?Mwalimu alisemaje?? ?Alisema hatishiki na lolote.? ?Iliishaje?? ?Baada ya kugundua tupo mle ndani wakati wakiendelea kuzozana, walitutimua nje. Baada ya kutoka nikaona nije huku, vipi baba yupo wapi?? ?Amekwenda shamba.? ?Amesemaje kuhusiana na hukumu kama ile ya kukukandamiza, wahusika hatupewi adhabu unapewa usiyehusika?? ?Lakini Sabina wewe ndiye aliyeitoa siri yetu polisi.? ?Shija polisi wanatisha, baada ya kunibana sana na maswali niliogopa kuitoa siri yetu na kuamua kusema vile.? ?Mmh, kweli ulijitahidi kuunda uongo.? ?Sasa Shija kama wakikuzuia kufanya mtihani utafanya nini?? ?Sina jinsi, itanibidi niende mjini kwa anko nikarudie shule.? Tukiwa katikati ya mazungumzo, sauti ya hodi ilitushtua, tulipoangalia sote tulishtuka baada ya kumuona mwalimu mkuu akiwa katika mlango wa kuingilia nyumbani. Sote tuliingiwa na woga baada ya mwalimu mkuu kutukuta pamoja wakati nikiwa bado na tuhuma za kuwa wapenzi na Sabina. Nilimuona Sabina uso umemshuka kama mchawi aliyekamatwa mchana akiloga. ?Karibu mwalimu,? nilijikaza kiume kumkaribisha lakini mwili kwa hofu haukuwa wangu, niliamini kabisa mwalimu mkuu alishapata ushahidi na kilichobakia ni hukumu. Woga niliokuwa nao niliamini hata kule kunitetea kwake lazima atabadili uamuzi wake kwa kuamini kilichosemwa juu yangu. Nikiwa bado sijiamini, Sabina vidole vilikuwa mdomoni, mwalimu mkuu aliuliza. ?Shija baba yako yupo wapi?? ?Yupo shamba.? ?Unaweza kunipeleka?? ?Ndiyo mwalimu.? ?Basi nipeleke.? Niliongozana na mwalimu kuelekea shamba, Sabina aliyekuwa amekosa raha toka mwalimu mkuu afike pale. Niliongozana na mwalimu hadi shambani, wazazi wangu walipomuona waliacha kulima. ?Karibu mwalimu.? ?Asante.? ?Una taarifa gani tena naona umeongozana na mwanafunzi wako?? ?Mmh, kuna mtafaruku umetokea ambao ndiyo ulionifanya nitengue uamuzi wa kumsimamisha Shija.? ?Mh, baada ya kuutengua ikawaje?? ?Japo nimepata vikwazo vingi toka kwa baadhi ya wazazi baada ya kuitengua adhabu waliyoitaka . Wapo walionitolea maneno ya vitisho kuwa sitakuwa na umri mrefu. Lazima nitakufa.? ?Ni nani?? ?Mama Helena huyo.? ?Ina maana uchawi wake anafikiri utafanya kazi kwa kila mtu? Tunajua yule mama ni mchawi lakini sisi tunamtegemea sana Mungu.? ?Basi mguu huu ni kuja kukutaarifu kwamba kesho mwanao aje shule kama kawaida, nitapambana na yoyote atakayetaka kukwamisha maendeleo ya Shija.? ?Nashukuru sana mwalimu.? Baba na mama walimpa mkono wa shukrani mwalimu kwa uamuzi wake wa busara. Baada ya taarifa ile iliyorudisha furaha moyoni mwangu, nilirudi na mwalimu ambaye alinieleza nizingatie masomo na kuachana na mapenzi. Nilijua alisema vile baada ya kuniona na Sabina nyumbani, mtu niliyekuwa natuhumiwa naye kuwa ni wapenzi. Baada ya kuachana na mwalimu nilirudi nyumbani. Ilikuwa ajabu kwani baada ya kufika nyumbani, hata sijakaa Sabina aliingia. ?Shija vipi mwalimu alikuwa akisemaje?? Nilimueleza yote yaliyosemwa , uso wa Sabina ulijenga tabasamu la matumaini. ?Ooh, afadhali umerudi shule, Shija nikuambie kitu?? ?Niambie.? ?Nilipanga kama wewe usingefanya mtihani na mimi nisingefanya.? ?Kwa nini?? ?Shija siwezi kufanya mtihani wakati mimi ndiye chanzo cha yote, ningeweza kumzuia hata Helena lakini kwa vile kichwani hakuna kitu ningemwacha afanye.? Siku hiyo nilishinda na Sabina kutwa nzima, jioni tuliagana ili tukutane shuleni kesho yake.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ya pili nilikwenda shuleni na kusoma kama kawaida bila kutokea tatizo lolote zaidi ya wanafunzi wa kike kunitania shemeji kwa ajili ya uzushi uliojaa shule kuwa ugomvi wa Sabina na Helena ulitokana na mambo ya mapenzi. Japo sikupenda maneno yale lakini kwa upande wa pili nilishukuru Mungu siri iliyo kati yetu ilibakia kwetu watatu. Sabina alikuwa msichana wa ajabu wala hakuona aibu kuwa na mimi karibu muda mwingi alinisogelea kutaka kujua baadhi ya masomo yaliyokuwa yakimsumbua. Na kweli alikuwa makini sana na masomo tofauti na nilivyomfikiria kipindi kile labda matatizo yale yangemchanganya . Nilikumbuka ahadi aliniyonieleza siku moja kuwa atahakikisha atakuwa mmoja wa wanafunzi watakao ungana nami kwenda kidato cha kwanza. Katika maisha yake yote aliuchukia sana uchawi. Alinieleza ni shinikizo la wajumbe wa baraza la wachawi kutaka kila mwanachana lazima amtoe mtoto wake mmoja atakayefundishwa uchawi ili wakizeeka wapate warithi. Ilikuwa tofauti na Helena ambaye alionesha wazi kuwa katika chama wa wachawi kwake ilikuwa furaha ambayo ilionesha aliitamani muda mrefu. Nami nilimpa moyo kuwa azidi kumuomba Mungu ipo siku atasikiliza kilio chake na kuachana na kazi ile chafu. Na hata nilipokuwa namfundisha alionesha kweli mwanzo alikuwa akicheza na muda ule alikuwa ameamua kusoma. Mawazo ya wengi juu ya ukaribu wetu uliwachanganya hata mwalimu mkuu ni kubadilika kiuwezo kwa Sabina kuweza kuwa mshindani na si mshiriki darasani. Siku zote katika kila kitu kuna washindani ambao kila siku huitafuta namba moja au kuwa katika namba nzuri zitakazo msaidia kuonekana anaweza. Lakini kuna wengine wapo kama wapo kutokuelewa kwao hakuwaumizi kichwa na kuamini maisha si darasani popote wanaweza kuishi hata bila elimu. Hao siku zote wamekuwa washiriki na si washindani. Lakini toka nilipokuwa karibu na Sabina hiyo ilibadilika hata mwalimu alinisifia kwa hilo. Siku ya tatu baada ya kurudi shule asubuhi tukiwa katika usafi baada ya kuhesabu namba, iligongwa kengele kutuashiria tunaitwa. Ilikuwa ajabu kupigwa kengele asubuhi kama ile. Wanafunzi wote tulikusanyika ili kusikia wito ule ulikuwa wa nini. Baada ya kukusanyika mwalimu mkuu msaidizi akiwa na walimu wenzake ambao wote nyuso zao zilionesha kuna jambo fulani kutokana na kila mmoja kushikilia kitambaa mkononi na kufuta machozi kwa muda. Nilijiuliza machozi ya walimu yalimaanisha kitu gani ambacho si cha kawaida. Baada ya kujadiliana walimu, mwalimu mkuu msaidizi alisema kwa sauti ya juu. ?Ndugu wanafunzi kumetokea tatizo zito hapa shuleni kwetu, si jambo la kawaida kuwaiteni muda huu lakini imebidi kufanya hivi ili tuwaelezeni kilichotokea alfajiri ya leo. Mwalimu mkuu wakati akitoka kuoga alianguka na kupoteza maisha.? Kauli ile ilinishtuka kwa kumsikia lakini sikumuelewa hata wanafunzi wenzangu walikuwa kama hawakumuelewa mwalimu mkuu msaidizi. ?Wanafunzi shule yetu imepata msiba mzito mwalimu mkuu hatunaye amefariki dunia alfajiri hii na mwili wake upo hospitali ya wilaya .? Kauli ile ilieleweka vizuri katika sikio la kila mmoja aliyekuwepo pale, kilio cha wanafunzi kilitawala shule huku walimu nao wakishindwa kujizuia kwa kuungana na wanafunzi kumlilia mwalimu mkuu. Sabina alikuwa kama kapigwa butwaa hakulia bali macho yalimtoka pima, alinishika mkono na kunitoa kwenye kundi la wanafunzi waliokuwa wakilia kwa kujitupa chini kwa uchungu. Nikiwa bado nimepigwa na butwaa nisielewe kilichotokea. Tulipofika pembeni Sabina alinieleza kitu. ?Shija umeona?? ?Nini?? ?Mama Helena alichomfanyia mwalimu mkuu kwa ajili ya kukurudisha shuleni?? ?Sabina ina maana mwalimu mkuu hakufa?? ?Sijajua mpaka nihudhurie kikao cha wachawi .? ?Sasa kama kafa kwa ajili yangu unafikiri nitaweza kuendelea kusoma?? ?Kwa nini usisome kwa vile hakuna ushahidi na wewe kuwa na kosa zaidi ya chuki za watu. Sasa hivi utasoma tu labda afe mzee Manoni.? ?Una maana gani?? ?Si kukuua au kukuchukua kwa uchawi, kwani siku hizi mambo ya vitisho usiku yanatokea?? ?Hapana.? ?Basi sasa hivi wanakuogopa kama ukoma ndiyo maana mama Helena alitaka ukose masomo ili iwe njia ya kukukomoa.? ?Shija tuondoke turudi nyumbani hali ya hapa haieleweki.? ?Mmh, sasa hali hii itaendelea mpaka lini na kwa nini kwa hili mzee Manoni asilikemee?? ?Hata mimi sijui, ila nataka kukueleza wachawi wote lao moja, ni ajabu kwako mzee Manoni amekuwa akikukingia kifua ni tofauti na kesi zote zilizowahi kufikishwa kwake . Watu wengi wamechukuliwa misukule kutokana na chuki au hata kuuawa na kuliwa nyama kwa ajili ya ugomvi mdogo mtu akileta mashtaka yake anakubaliwa na kupewa msaada wa kumkomoa mtu.? ?Unafikiri ni kwa ajili gani mzee Manoni amekuwa akinitetea hivyo ?? ?Mzee Manoni amekuwa akikutetea kwa sababu maalum, kuna siku nilisikia akisema kuwa shida yake kubwa ni kukurithisha mkoba wa kichawi.? ?Etiiii?? ? Shija ukweli ni huo hakuna njia iliyo salama kwako ya kukufanya uendelee kuwa salama hata baada ya mzee Manoni kufa zaidi ya kujiunga na chama cha wachawi .? ?Sabina una uhakika gani na hayo unayoyasema ?? ?Shija huna njia ya salama kwa vile unajua siri nyingi za kichawi hivyo hawawezi kukuacha hivi hivi tu, lazima watakulazimisha uingie kwa nguvu la sivyo watakuua au kukugeuza msukule ili usitoe siri zao.? ?Sabina mbona unanichanganya, kwa hiyo kuna siku mzee Manoni atanieleza habari hizo?? ?Hakuna salama yako lazima ujiunge na wachawi kama sisi, mimi sipendi kuwa mchawi lakini nipo kwa usalama wangu japo nafanya makosa mengi. Cheo cha mama yangu ndicho kinachonilinda.? ?Sasa unaniushauri nini?? Nilijikuta nachanganyikiwa . ?Hebu kwanza tuondoke eneo la shule ili tuache kwanza mipango ya msiba wa mwalimu.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nina imani kabisa ilikuwa siku yangu ya kwanza kuhisi kama moyo ulitaka kupasuka na kupiga kelele ambazo niliamini kabisa ndizo zilizokuwa zikipunguza maumivu makali ya uchungu wa kumpoteza mwalimu aliyekuwa mtetezi wangu siku zote za uhai wake, nililia mpaka nikapoteza fahamu. Niliposhtuka nilijikuta nimelala kwenye kitanda na mkononi nilikuwa naongezwa maji, pale palionesha ni hospitali. Nikiwa natafakari ilikuwaje, muuguzi alinisogelea na kuniuliza: ?Unaendeleaje?? ?Sijambo kiasi.? ?Unakumbuka ulipatwa na nini?? Nilitulia kwa muda na kuvuta kumbukumbu lakini sikukumbuka, nilitikisa kichwa na kusema: ?Sikumbuki.? ?Unaitwa nani?? ?Shija.? ?Mara ya mwisho ulikuwa unafanya nini?? Nilitulia tena kuvuta kumbukumbu taratibu nilikumbuka mara ya mwisho tulikuwa tukiuaga mwili wa mwalimu mkuu kabla ya kuusafirisha kwenda kwao kwa mazishi. Kwa sauti ya chini nilimueleza: ?Nakumbuka.? ?Unakumbuka nini?? ?Nilikuwa nauaga mwili wa mwalimu mkuu.? ?Inaonekana peke yako ndiye uliyekuwa ukimpenda mwalimu wako.? ?Kwa nini?? ?Kutokana na maelezo, wakati unamuaga baada ya kuiona sura yake uliangua kilio kilichopelekea kupoteza fahamu kwa saa saba.? ?Mungu wangu!? ?Ndiyo maana nilikuuliza ulikuwa ukimpenda sana.? ?Tena sana, bado siamini mtu adondoke na kufa.? ?Ni jambo la kawaida kitaalamu, kilichomuua mwalimu wenu ni shinikizo la damu na si kingine kama ninavyosikia labda kauawa kichawi. Vipimo vilionesha baada ya kupatwa na mshtuko mishipa ya damu ilipasuka na kusababisha mauti yake.? ?Hata hivyo , mwalimu mkuu alikuwa mtu muhimu sana maishani mwangu bila yeye leo hii nisingefika hapa. Nitaendelea kumlilia siku zote za maisha yangu.? ?Unamfahamu Sabina?? ?Sabina! Sabina gani?? Nilishtuka kusikia jina la Sabina. ?Unayesoma naye darasa moja.? ?Kama huyo kwa nini nisimfahamu?? ?Unamfahamu kivipi?? ?Kama mwanafunzi mwenzangu.? ?Si zaidi ya hapo?? ?Mbona unaniuliza hivyo ? Kuna nini?? ?Sabina naye yupo hapa.? ?Yupo hapa anafanya nini?? ?Jana baada ya wewe kuanguka na kupoteza fahamu kutokana na maelezo ya mashuhuda walisema kuwa, alifikiri umekufa. Alipatwa na mshtuko na kuanguka chini kitu kilichosababisha apoteze fahamu. Mliletwa kwa pamoja, lakini yeye aliwahi kuzinduka na alipozinduka aliendelea kukulilia huku akisema hakubali.? ?Hakubali nini?? ?Hata sisi hatujui lakini baada ya kumueleza unaendelea vizuri alinyamaza na kuwa na hamu ya kukuona kwa kuamini tunamdanganya na ukweli ni kwamba umekufa.? ?Mungu wangu, mbona Sabina ana matatizo?? ?Amkose mwalimu hata mpenzi lazima achanganyikiwe .? Sikumjibu muuguzi ambaye alikuwa mcheshi na mpole, alinijulisha wazazi wangu wapo nje. Aliwaruhusu kuja kuniona huku mama akionekana kuchanganyikiwa sana. ?Shija unaendeleaje baba?? ?Sijambo mama.? ?Pole sana mwanangu, najua ulikuwa ukimpenda sana mwalimu wako.? Baba aliongezea. Muuguzi aliwaeleza ugonjwa wangu si mkubwa ila nitakuwepo pale hospitalini hadi siku ya pili kwa ajili ya uangalizi. Baada ya maelezo yale, muuguzi aliwaomba wazazi wangu anipatie tiba ili nipumzike. Kwa vile chakula kilikuwa kimeletwa, nilikula kwanza kisha muuguzi alinidunga sindano na kuniomba kupumzika. Baada ya muuguzi na wazazi wangu kuondoka nilibakia na mawazo mengi. Ajabu sikumfikiria mwalimu mkuu aliyesababisha niwe pale zaidi ya kumfikiria Sabina. Nilijiuliza Sabina ananipenda kiasi gani kufikia kutaka kufa kwa ajili yangu? Bado moyo wangu haukuwa na kitu ambacho ungeridhika kukitoa kwa Sabina ili kilingane na moyo wake ulivyojitoa kwangu. Niliamini kabisa kama Sabina angeanguka wakati wa kumuaga mwalimu mkuu. Kwa upande wangu nisingeweza kufanya alivyofanya Sabina, kwangu lazima ningeona aibu kumlilia Sabina kwa vile tayari shuleni tulijukana kuwa ni wapenzi. Lakini nilijiapiza kumuonesha najali chochote alichokifanya na atakachokifanya . Dawa nilizodungwa zilianza kufanya kazi, kichwa kilikuwa kizito na usingizi ulinichukua. Nilipozinduka nilikuwa kama nipo ndotoni, mkono ukinipapasa usoni, nilipofumbua macho kweli alikuwa Sabina. Aliponiona nimeamka alishtuka. ?Aah!? ?Vipi?? Nilimuuliza kwa sauti ya chini. ?Unaendeleaje?? ?Mi sijambo sijui wewe ?? ?Mimi mzima hadi nimekuja kukuona, basi ujue nipo fiti.? ?Nashukuru, hata mimi nipo fiti kama si muda ningeruhusiwa leo, lakini kesho mpaka saa nne nitaruhusiwa.? ?Hata mimi nilitaka kuruhusiwa nikaomba tutoke pamoja.? ?Haya mama.? Siku ile muda wote tulikuwa pamoja mpaka usiku ulipoingia kila mtu alikwenda kulala kusubiri siku ya kesho yake kuruhusiwa.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini wakati tukiwa hosptali tulipata taarifa ya kushangaza kuwa, maiti ya mwalimu mkuu iliyopelekwa Mochwari, usiku wa kuamkia siku ya pili ilikutwa nje ya chumba hicho cha kuhifadhia maiti. Tukio hilo liliwafanya wauguzi na madaktari washtuke, hata hivyo habari hazikusambaa sana kwa sababu mganga alionya. Wengi waliamini nguvu za giza zilitumika na kwamba, mwalimu mkuu hakufa. Nilijikuta nikiungana na kauli ya Sabina kwamba lazima mwalimu alikuwa amefichwa mahali akiwa hai na walichokuwa wakikiona watu ni kivuli chake tu. Lakini wakati baadhi ya watu waliamini hivyo , wapo waliosema ni habari za uongo na za kupotosha jamii wakiamini kuwa mwalimu mkuu alikufa sawa sawa na vifo vingine. Nyumbani niliyaanza maisha mapya bila mtetezi wangu, nikiamini kwamba kwa kipindi kilichobaki nilitakiwa kuwa makini ili nifanye mitihani yangu ya mwisho bila tatizo la kiakili. Kama kawaida, niliendelea kuwa karibu na Sabina ambaye alionesha kunijali. Katika uchunguzi wake wa kifo cha mwalimu alinieleza kuwa ni kweli alikufa pamoja na uchawi kutumika kumuondoa duniani lakini waliomuua ambao ni wachawi walishindwa kuchukua maiti ambapo alikuwa mzito kuliko kawaida kitu kilichowafanya waachane naye. ?Shija, mwalimu kweli alikufa na maiti yake ilipopelekwa hospitali, nia ya wachawi ilikuwa kumchukulia kule na kukiacha kivuli chake. Wachawi walifanikiwa kumtoa katika chumba cha kuhifadhia maiti, lakini walipofika nje wakati wanataka kumbeba ili waondoke nayo alikuwa mzito kama kajengewa chini. ?Wachawi walihangaika kumtoa pale chini na kutumia kila mbinu lakini mwili uliendelea kuwa mzito usiobebeka. Huwezi kuamini, kidogo alfajiri iwakute pale, ndipo walipoamua kuondoka. Na asubuhi mhudumu wa chumba cha maiti alishtuka kuona mwili wa mwalimu upo nje wakati mlango umefungwa. ?Ndipo alipoita watu ambao waliushangaa ule mwili, waliubeba na kuurudisha sehemu ulipohifadhiwa mwanzo.? ?Sabina yote hayo ulikuwa unayajua mbona hukuniambia mapema?? ?Shija, nilikuwa sijui lolote,si unajua siku hizi sina kinga ya safari za hatari, walikwenda peke yao na hata waliporudi walikaa kimya. Siku tulipotoka hospitali nilimuuliza mama kuhusu taarifa zilizozagaa kwamba mwili wa mwalimu ulikutwa nje ya chumba cha kuhifadhia maiti. ?Alinijibu ni kweli na kunipa mkasa huu ambao haukuwa mgeni kwangu kwani matukio kama yale tuliishakutana nayo mara nyingi. Si ya maiti kugoma kubebwa tu bali wengine wakishazikwa , kaburi huwaka moto na kushindwa kuwachukua maiti hao. ?Kwa nini inakuwa hivyo ?? ?Mara nyingi watu wa aina hiyo huwa wamezindikwa , maiti hawaliwi nyama.? ?Sabina kama wamezindikwa kwa nini wanakufa ?? ?Shija nataka nikueleze jambo moja huenda unalijua au hulijui, hakuna mwanadamu anayeweza kumuua mwanadamu mwenzake ila kwa ruksa ya Mungu.? ?Sabina ni Mungu gani anayeruhusu mtu amuue mwenzake?? ?Shija hata mimi nilitatizika nilipoelezwa hivyo na mwanzo nilijua binadamu anaweza kumuua binadamu mwenzake. Nafikiri kuna siku nilikueleza msukule huwa anakufa?? ?Ndiyo nakumbuka.? ?Basi katika maisha ya mwanadamu kila kiumbe kina siku yake ya kufa, ila unaweza kufanikiwa kumuua kupitia siku yake na hapo unapata dhambi ya kuua, lakini hata usingemgusa angekufa.? ?Kwa hiyo mwalimu amekufa au ameuawa?? ?Kifo cha mwalimu mkuu mhusika ni mama Helena na washirika wake na baada ya kufa walitaka kumla nyama lakini wameshindwa .? ?Sasa wamepata faida gani?? ?Hakuna faida! Ni roho mbaya tu isiyo na huruma.? Maneno ya Sabina yaliniongezea hofu moyoni na kuamini kama mama Helena amefanikiwa kumuua mwalimu hatashindwa kuniulia baba yangu mzazi. Wasiwasi mkubwa ulitokana na siku ya kikao ambapo aliwatishia wajumbe na mwalimu mkuu ambaye baadaye alijirudi, kitu kilichosababisha kifo chake. Wasiwasi wangu ulizidi na kuamini kuwa kinga niliyopewa na mzee Manoni ili wachawi wasiniguse nilikuwa nayo peke yangu. Kwa wazazi wangu bado nilikuwa na wasiwasi maana kama kweli mwalimu mkuu ambaye ilisemekana alikuwa na kinga ya mwili lakini mwisho wa siku alipatikana na wakamuondoa duniani sembuse wao, hasa baba ambaye siku zote haamini uchawi. Lakini siku zilikatika, muda ukawadia tukafanya mitihani, nakumbuka siku hiyo Sabina alikuwa akisumbuliwa na kichwa hivyo hakuwa katika hali nzuri lakini alijitahidi japo kwa shida na kuacha baadhi ya maswali. Nilimpa pole na kumpa moyo kwamba, kama maswali mengi alijibu vizuri yanaweza kumsaidia katika matokeo, alinishukuru na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Njiani Sabina alishangaa kujiona yupo sawa, kichwa kikikuwa kimepoa: ?Shija kichwa hiki si bure, subiri aliyesababisha kiniume, jasho litamtoka.?



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ugonjwa wa Sabina ulinishtua na mimi, kichwa kupoa baada ya kutoka chumba cha mitihani! Niliwaza moyoni kuwa, aliyefanya vile lazima atakuwa Helena, hakukuwa na mtu mwingine na kama ni Helena vita yao itakuwaje? Wasiwasi wangu, Sabina angemfanyia kitu kibaya ambacho kingechukua muda mrefu kusahaulika akilini mwa watu. ?Shija nikifeli mtihani nakufa na mtu, waombe nisifeli.? ?Sasa unamjua ni nani?? ?Kuna mwingine zaidi ya mama Helena, mchawi asiye na haya.? ?Lakini si ulisema anamuogopa mama yako?? ?Ni kweli, ndiyo maana nashangaa.? ?Lakini....au malaria?? ?Shija acha kujitoa akili, malaria gani ya darasani tu?? ?Hata mimi bado nipo njia panda.? ?Shija kila dakika hasira zinapanda, nakuhakikishia mpaka kunakucha kuna jambo utalisikia.? ?Jambo gani?? ?Lile la mwanzo dogo, hili wataokota maiti.? ?Sabina hupendi uchawi kwa nini unapenda kuua? Kwa nini usiwasamehe tu ili uweze kujipanga upya. Maisha yako si kumuua Helena bali kujipanga kwa ajili ya hatima baada ya mitihani.? ?Ni kweli Shija, lakini nimekuwa na hasira sana pale mtu anaponigeuka kwa kutumia ukaribu wetu.? ?Sawa najua inauma, lakini wakati mwingine izuie nafsi yako kutenda mambo mabaya.? ?Sawa Shija nimekusikia, sitafanya niliyokusudia lakini nitamshikisha adabu.? ?Sabina, mshukuru Mungu kwa kila jambo ili kuupa uhuru moyo wako.? ?Shija, leo nashangaa kila unalolizungumza linaniingia na kupoa kama maji mtungini.? ?Nashukuru Sabina kwa kunielewa.? Niliagana na Sabina kila mmoja alielekea kwao. Nilipofika nyumbani nilijawa na mawazo juu ya kilichomtokea Sabina ndani ya chumba cha mitihani na baada ya kutoka.Nilijiuliza kama wachawi kwa wachawi wanachezeana mimi nitafanyaje? Lakini ulinzi wa mzee Manoni ulinipa kichwa kufanya mambo yangu bila wasiwasi wala kutokewa na mauzauza usiku. Siku zote nililala vizuri na kuamka vizuri hakukuwa tena na vishindo, ngoma wala njozi za kutisha. Siku zilikatika huku wanafunzi wote tuliomaliza darasa la saba tukisubiri majibu kwa hamu kubwa. Hatimaye siku ikafika matokeo yakatoka , shule yetu ilitoa wanafunzi kumi na nne, mimi nikiwa mmoja wa waliochaguliwa . Lakini kwa bahati mbaya Sabina hakuwemo. Kukosekana kwake kulimuumiza na kumfanya alie sana. Nilimbembeleza huku nikimueleza kuwa kuna maisha baada ya shule. Ningeweza kusema labda wazazi wake wangeweza kumsomesha shule za kulipia, lakini haikuwa hivyo , maisha yetu ya kijijini tuliyajua wenyewe . Wacha kufeli hata waliofaulu wengine hushindwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na ukata. Nilichaguliwa nijiunge na shule ya mjini ambayo ilichukua wanafunzi waliofanya vizuri. Kutoka tunapokaa mpaka mjini kwa baiskeli ni mwendo wa robo saa na saa moja kwa miguu. Nilifurahi kusoma shule ile kutokana na sifa zake za ufundishaji mzuri, tofauti na shule nyingi za kata, zilikuwa na walimu wachache. Kuchaguliwa kwangu ilikuwa furaha kubwa kwa familia yangu hata Sabina naye alisema amefarijika. ?Shija heri nimekosa mimi, ningeumia sana kama ungekosa wewe .? ?Sabina nashukuru lakini ndoto zangu hazikutimia.? ?Ndoto zipi Shija?? ?Nilitaka tufaulu wote na siku moja tuweze kukisaidia kijiji chetu.? ?Shija, kijiji hiki hakitaendelea milele.? ?Kwa nini?? ?Na wachawi wa hapa utawaweka wapi?? ?Unataka kuniambia wachawi wa hapa hata maendeleo hawataki?? ?Shija uchawi ni uharibifu, uchawi ni kikwazo , hivyo kila mtu atakayejifanya anajua kijijini hapa lazima afe.? ?Unataka kuniambia Samuel aliyefungua duka mwaka juzi na kufa wiki moja baadaye aliuawa na wachawi ?? ?Shija, Samuel hakufa, aligeuzwa msukule.? ?Mh! Makubwa.? Wakati tukizungumza, Sabina alionesha kuna kitu kinamsukasuka moyoni, nililigundua hilo na kumuuliza: ?Sabina kuna kitu kinaonekana usoni kwako , una tatizo gani?? ?Hakuna kitu Shija,? Sabina alinikatalia akiwa ameangalia chini. ?Hapana Sabina kuna kitu, wewe si mgeni kwangu.? ?Shija sina jinsi, lazima niseme ukweli, ni kwamba matokeo haya yameniumiza sana baada ya kujua sababu ya kuumwa kwangu kichwa, ilikuwa vile ili nifeli.? ?Ha! Kwa sababu gani Sabina?? ?Shija, mwanzo nilijua labda Helena na mama yake kumbe siyo, yaani siamini aliyenifanyia sikutegemea hata siku moja.?



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nani aliyekufanyia mchezo huo?? ?Mama.? ?Mama! Unamaanisha mama yako?? ?Eeh.? ?Mama yako mzazi?? ?Ndiyo.? ?Sabina hebu acha utani,? niliamini Sabina alitaka kunirusha roho. ?Shija naomba uamini ninachokisema hapa ndiyo ukweli wenyewe .? ?Sabina unajua tunazungumza jambo la muhimu, kwanini unaleta mzaha?? ?Najua huwezi kuamini, siku zote kikulacho kinguoni mwako, amini aliyenifanyia mchezo ule mbaya ni mama yangu mzazi.? ?Sasa alifanya ili iweje?? ?Kulikuwa na siri nzito ambayo mwanzo niliona aibu kuisema, lakini kutokana na umuhimu wako kwangu, sina budi kulianika mbele yako leo.? ?Eehe!? ?Shija siku nilipotoka shuleni baada ya mtihani na hali iliyonitokea, nilikwenda kumueleza mama huku nikitangaza vita na familia ya kina Helena. Ajabu mama alipinga na kuniomba afanye mambo yake ili amtambue mbaya, jibu alilonipa lilinikatisha tamaa.? ?Alikueleza nini?? ?Eti alinieleza sijalogwa na mtu ile hali ilinitokea kwa hofu ya mtihani na kuniomba niachane na familia ya mama Helena. Pia Shija naomba nikuombe samahani kwa kutokueleza mambo yaliyotokea siku za hivi karibuni. Baada ya mtihani familia ya mama Helena ilikutana na yetu kuondoa tofauti zilizotokea. Niliwakubalia mdomoni lakini Helena niliapa kuwa adui yangu milele.? ?Sabina nataka kukueleza adui wa leo ni rafiki wa kesho, kila mwanadamu ana upungufu wake hivyo si vizuri kumchukia mtu milele. Tumefundishwa kusamehe ili tusamehewe.? ?Ni kweli, hivi wewe upo tayari kumsamehe Helena?? Sabina aliniuliza akinikazia macho. ?Nipo tayari, na nilikwishamsamehe muda mrefu.? ?Shija wewe ni mtu gani usiyejihurumia, mtu alitaka kukutoa sadaka ukaliwe nyama leo hii unamsamehe?? ?Sabina adui wa leo ni rafiki wa kesho, kumbuka Helena huyo huyo ndiye aliyeshirikiana nasi kumtoa kaka yangu kwa kujitoa kwa hali na mali. Kama jana alikuwa rafiki, leo adui basi kesho atakuwa rafiki mwema zaidi.? ?Shija wewe kiumbe wa ajabu.? ?Siyo wa ajabu siku zote ubaya ukilipwa jema, ubaya hukosa nafasi hivyo kumfanya aliyetenda ubaya ajidharau na kuiga tabia njema.? ?Kwa hiyo unanishauri nimsamehe toka moyoni?? ?Ndiyo maana yangu.? ?Nitajitahidi kufanya hivyo .? ?Ulisema kuwa mama yako ndiye aliyekufanya uumwe kichwa wakati wa mtihani ili iweje?? ?Nisifaulu ili niolewe.? ?Wewe ulijuaje kama aliyefanya vile ni mama yako?? ? Baada ya mtokeo ya darasa la saba, mama alikuwa akizungumza na mtu bila kujua mimi nipo ndani, nilimsikia akijisifia njia aliyotumia nifeli mtihani ili niolewe na baada ya matokeo, harusi iliandaliwa. Bwana anayetaka kunioa anatoka Wilaya ya Bariadi, Mkoa wa Shinyanga, tena ananioa kwa mahari ya ng?ombe 30.? ?Ulijuaje?? ?Baada ya kusikia vile nilisubiri mgeni aondoke ndipo nilipomuangushia kilio mama, kwa kitendo chake cha kuniroga nisifanye mtihani ili niolewe.? ?Mama alinieleza kufanya vile alikuwa na maana kubwa kwa vile nikiolewa nitakuwa nimejitoa kwenye mtandao wa kichawi na kunifanya niishi maisha ya amani.? ?Wewe uliamua nini?? ?Sikuwa na jinsi kwa vile mtihani nimeshindwa na uwezo wa kunisomesha hakuna, wameamua niolewe ili kunitoa kwenye mtandao wa kichawi, wacha nikubali au ulikuwa unanishauri nini?? ?Japo kitendo cha mama yako sikukipenda, nilipenda kukuona ukiwa sehemu ya maendeleo ya kijiji chetu. Lakini hata walichokiamua si kibaya, kitakufanya uishi maisha ya amani.? Baada ya kuagana na Sabina nilirudi nyumbani nikiwa na mawazo mengi juu kitendo alichokifanya mama Sabina kwa mwanaye . Nilijua sababu kubwa ya watu wa vijijini hawathamini elimu zaidi ya mali, wakiamini wakimuoza mtoto wa kike wanapata ngombe. Niliamini kabisa ng?ombe 30 ni mtaji mkubwa katika maisha ya kijijini. Nilijua wingi wa ng?ombe katika mahari ya Sabina ulitokana na rangi yake ya weupe, katika Kabila la Wasukuma, wanawake weupe wana thamani kubwa katika mahari tofauti na wanawake weusi. Wiki moja kabla ya kuanza shule, Sabina aliolewa na kuhamia Bariadi na kuniacha mkiwa. Sikuwa na jinsi, nilijipanga kuanza masomo wa sekondari.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Namshukuru Mungu niliyaanza masomo yangu vizuri huku nguvu zangu zote nikizihamishia huko. Uwezo wangu kimasomo niliokuwa nao shule ya msingi niliuendeleza shule ya sekondari. Hali yangu ya maisha ilikuwa ya kawaida hakukuwa na vikwazo vyovyote vya awali wakati nikiwa shule ya msingi, mauzauza ya wachawi yalikoma. Siku moja nikiwa natoka shule nilishtuka kukutana na Helena njiani, moyo wangu ulinilipuka na kujua si rahisi binti yule kuja kunitembelea kwaheri. Nilipomkaribia nilimpita bila kumsemesha, wazo la haraka lilikuwa baada ya kumpita nitimue mbio. ?Shija,? sauti ya Helena iliniita na kuufanya moyo wangu unilipuke kwa hofu zaidi. Sikumjibu nilikaza mwendo ili nitimue mbio lakini Helena aliendelea kuniita. ?Shija, najua mimi ni adui yako mkubwa, pengine usingependa kuniona machoni mwako, ila nakuomba unisikilize kabla ya kuamua lolote lile juu yangu.? Maneno ya Helena yalinifanya nipunguze mwendo ili nimsikilize, nilisimama na yeye alikuja mbele yangu na kupiga magoti. ?Shija najua kiasi gani nimekufanyia mambo mabaya ambayo hatakiwi kufanya mtu mwenye ubinaadamu, nakubali nimekukosea. Nakuomba unisamehe kwa yote niliyofanya ya kutaka kukuondoa duniani, si mimi, kila nilichokifanya kilikuwa shinikizo la mama na washirika wenzake. ?Nililazimishwa na nilipokataa walinitishia kunitoa kafara, kwa kweli niliogopa na kutii amri yao. Lakini naamini maisha yako ni marefu kwani kila hila imeshindikana na leo hii bado unaendelea kuishi. Shija wewe ni kiumbe wa ajabu ambaye sijawahi kumuona chini ya jua, pamoja na yote niliyokufanyia kwa kunijua bayana bado hukutaka kulipa kisasi kama Sabina. ?Sikuamini siku Sabina aliponieleza dhamira yake mbaya juu yangu, lakini ni wewe ndiye uliyeubadili moyo wake na hatimaye kuurudisha urafiki wetu. Nimekuwa na wakati mgumu kusimama mbele yako kuomba msamaha kwa kuona aibu. ?Huwezi kuamini leo ni siku ya tano nasimama maeneo haya kukusubiri kutaka kukuomba msamaha. ?Lakini kila nilipokuona ujasiri ulinipotea na kuamua kujificha nyuma ya mti na wewe kupita bila kujua kama nipo sehemu hii. Shija nimejiuliza hali hii ya kukosa ujasiri wa kukueleza itaendelea mpaka lini, kama nina uwezo wa kwenda kumtoa mtu ndani mwake au kumfukua maiti kaburini kwa nini nilishindwa kusimama mbele yako? ?Lakini nimeamini kazi ile hujaa nguvu za kichawi na si mtu kamili, tofauti na mimi kusimama mbele yako bila nguvu za kichawi. Kweli uso wa mwanadamu umeombwa na aibu. Shija napiga magoti mbele yako kukuomba msamaha toka chini ya uvungu wa moyo wangu. ?Nakuahidi alilolifanya Sabina ndilo nitakalo lifanya kuhakikisha unakuwa salama siku zote. Najua sasa hivi upo salama sana baada ya adhabu aliyotoa mzee Manoni kwa wote waliotaka kukugeuza kitoweo. Ninavyokueleza mtoto wa kaka yangu mwezi jana ametolewa sadaka kama faini ya kile walichotaka kukufanyia . ?Shija nipo tayari kwa lolote utakalotaka kunifanya hata likiwa zaidi ya alilotaka kunifanya Sabina nipo tayari. ?Nimekutendea mambo mabaya ambayo sikustahili kusimama mbele yako, lakini moyo unanisuta lazima nisimame ili unipe hukumu inayolingana na kosa langu.? Maneno ya Helena yaliufanya moyo wangu usisimke na kujikuta nikitokwa na machozi, niliamini alichokisema kilitoka moyoni mwake na kuzidi kuamini kwamba adui wa jana ni rafiki ya leo. Machozi yangu yalizidisha kilio cha Helena ambaye alijikuta akikaa chini bila kupenda huku akinishika miguu yangu. ?Shija najua roho inakuuma kila ukiniona mbele yako, unatamani kunirarua na kunila nyama. Nakuomba uamini hili nisemalo, sisi wasichana wa kijijini tumekuwa tukilazimishwa kuingizwa kwenye uchawi bila kupenda kwa kisingizio cha kurithi mikoba ya wazazi wetu watakapozeeka . ?Tumekuwa tukifanyishwa mambo ambayo nafsi zetu hayazitaki, lakini siku zote ukiifanya kazi mbaya kwa muda mrefu hatimaye unajikuta umeingia na kuwa mshiriki kamili usiye na chembe ya huruma. ?Sabina kabadilika hivi karibuni baada ya kuzama katika penzi lako, lakini Sabina ndiye aliyeongoza kwenye mambo mazito hasa ya kufukua maiti za watoto, kutoa mimba za wanawake ambao hujiona wana mimba na mwisho wa siku huzaa vitu vya ajabu. ?Kweli nimeamini penzi kitovu cha uzembe, Sabina tangu kuwa na wewe amejikuta akikiuka miiko yote ya uchawi na kuwa tayari kwa lolote, kilichomsaidia Sabina ni uwezo mkubwa wa kichawi wa mama yake tofauti na mimi. Nataka nikueleza kitu kimoja, baada ya zoezi la kumtorosha kaka yako kushindikana, nilitakiwa nitolewe kafara ili niliwe nyama. ?Mama yangu aliwapigia magoti nisifanyiwe hivyo , walikubali kunisamehe lakini sharti kubwa nililopewa ni kuhakikisha nafanikisha kukuua au kukuchukua msukule. Shija ile ilikuwa siri ambayo hata Sabina hakuijua, nina imani angeijua mapema nisingekusogelea. ?Kwa ukaribu wetu Sabina alinipa siri kuwa ngozi ya kinga ya safari za hatari alikupa wewe ili kukukinga. ?Kwenye kamati ya uchawi alisema ameidondosha, kwa vile alikuwa akiaminika kwenye safari zote za kiuchawi, binafsi sikumuamini aliponiambia kuwa amekupa nilidhani amepoteza kweli. ?Lakini kikwazo cha kukupata kilinifumbua macho na kufanya upelelezi na kuamini kumbe kweli. ?Hapo ndipo nilipobahatika kukipata kipande cha ngozi na kuondoka nacho. ?Tukiwa na uhakika wa kukupata, lakini kwa maajabu makubwa, siku tulipokuja tulishangaa kutokukuta, nilijikuta nikichanganyikiwa na kujiuliza wewe ni kiumbe wa aina gani, nilianza kukata tamaa ya kukupata, ndipo nilipotumia njia ya kukutafuta mchana, bahati nzuri nilikukuta umelala ndani na kukulisha dawa za kichawi ili ufe. ?Shija, Sabina kweli aliapa kuyatetea maisha yako, aliweza kuyaokoa tena maisha yako kwa kukutapisha dawa za kichawi, niliamini kupitia ugonjwa wako, basi tungeweza kukupata na kweli tulikupata bado Sabina aliyaokoa tena maisha yako kwa kupeleka taarifa kwa mzee Manoni. ?Shija nakuomba kuanzia leo unione ni kiumbe kipya niliyemsafi mbele yako, nakuahidi kuyafanya yote aliyoyafanya Sabina au pengine mara mbili yake.? Baada ya kumsikiliza Helena na kuona kwamba mengi hayakuwa mageni kwangu zaidi ya kunifafanulia kwa kina, niliamini ni muda mwingine wa msamaha kuchukua nafasi yake. Nilimshika mabegani na kumnyanyua , nilimtazama, alikuwa akiaanza kuvimba macho kutokana na kilio. ?Helena,? nilimwita kwa sauti ya chini. ?Abee Shija.? ?Nimekusamehe.? ?Kweli Shija?? ?Kweli.? ?Au unanifurahisha tu?? ?Helena nilikusamehe tokea siku ya kwanza nilipojua dhamira yako, nina imani msamaha wangu ndiyo uliomfanya Mungu naye anilinde. Amini kweli nimekusamehe tumefundishwa kusamehe ili tusamehewe.? ?Asante Shija, umenipa funzo maishani mwangu.? ?Kwa hiyo umeachana na uchawi?? Nilimuuliza.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Swali langu lilimfanya Helena anyamaze kimya na kutazama chini, nililirudia swali langu la awali. ?Helena mbona hunijibu, kwa hiyo umeacha uchawi?? ?Shija nashindwa nikujibu nini ili unielewe,? Helena alinijibu kwa sauti ya upole akiwa bado ameangalia chini. ?Helena lolote utakalonieleza nitakuelewa.? ?Nikikueleza kuwa nimeacha uchawi nitakudanganya ila kwa asilimia kubwa sitashiriki kwenye kazi za kichawi, muda wangu mwingi nitautumia kuhakikisha usalama wako japo kwa sasa najua huna tatizo lolote kutokana mzee Manoni kukusimamia.? ?Najua una kazi nzito ya kuibadili tabia uliyoizoea lakini kila kitu kina mwisho wake, uchukie uchawi mwisho Mungu atakutoa bila ya wewe kujielewa,? nilimpa moyo. ?Shija nitajitahidi kufanya hivyo .? Tuliongozana na Helena kurudi kijijini, njiani tulizungumza mengi yakiwemo yale tuliyoyafanya wakati tukiwa marafiki. Tulipofika kijijini tuliagana na kila mmoja alienda kwao. Nilipofika nyumbani nilijikuta nikijawa na mawazo mengi juu ya maneno ya Helena ya kuniomba msamaha. Japo nilikuwa na wasiwasi kwa maneno yake na kuyaona kama kweli yalipandikizwa ili kuniteka kimawazo na kunifanyia kitu kibaya. Lakini moyo wangu ulijaa ujasiri kwa kuamini kile nilichomueleza Sabina amsamehe Helena, kuwa adui wa jana anaweza kuwa rafiki mwema wa leo. Nilijikuta nikimuamini Helena kwa kauli yake kwamba kutaka kuniua kulitokana na shinikizo la kutolewa yeye kafara. Nilijikuta nikimuonea huruma, siku zote pamoja na ubaya aliotaka kunifanyia lakini bado niliyakumbuka mema aliyonifanyia pale alipojitolea kwa hali na mali kumtorosha marehemu kaka yangu. Badala ya kujionea huruma mimi nilijikuta nikimuonea huruma Helena kwa masaibu yote aliyopata mpaka kuponea tundu la sindano kuuawa na Sabina. Kumbe hata angemuua angekufa na siri nzito moyoni ambayo ilionesha mimi ndiye mhusika mkuu. Niliamua kusahau yote yaliyopita na kuganga yajayo , nikamchukulia Sabina kama rafiki yangu mwema aliyetaka kujiokoa kwa kuutoa uhai wangu. Siku zote niliamini mwenye uwezo wa kuuchukua uhai wa mwanadamu ni Mungu pekee na si nguvu za giza wala mashetani. Siku zilikatika, niliendelea na masomo yangu vyema huku nikionekana zile nguvu nilizokuwa nazo shule ya msingi nimezihamishia sekondari, Nilikuwa mmoja ya wanafunzi tegemezi kutokana na uwezo wangu niliouonesha darasani ambao ulinifanya niwe maarufu shuleni. Wakati wa likizo kubwa mama alinieleza kwamba mjomba ananiita mjini. Nilikwenda kwa mjomba ambako nilijua muda wangu nitautumia kusoma. Jioni ya siku niliyofika , mjomba aliniita pembeni na kutaka kujua niliyomueleza kuhusu kumleta marehemu kaka akiwa hai yaliishia wapi? ?Anko mbona kimya, harakati zako za kumleta kaka yako ziliishia wapi?? Swali lilikuwa zito, nilijikuta nimebakia kimya nikiwa sijui niseme nini. Sikuwa na cha kumueleza kwa kuamini kila nitakachomueleza atazidi kuniona muongo. ?Shija si nakuuliza? Ulisema kaka yako hakufa yupo hai, si ndiyo?? ?Kuna mtu alinihakikishia lakini mwisho wa siku alisema alikuwa akinidanganya,? nilitengeneza uongo ili kuficha siri nzito ya kifo cha kaka nilichokishuhudia kwa macho yangu. ?Kwa hiyo hayupo hai?? ?Ndiyo.? ?Lakini si ulituhakikishia kuwa ulimuona akiwa hai?? ?Niliwadanganya kwa vile kuna mtu alinihakikishia kamuoa akiwa hai na kuniahidi atamtoa nije kwako nimtafutie nafasi.? ?Yeye alinijuaje?? ?Aliniuliza kama kuna mtu aliye mbali na kijiji ili akimtoa tumlete, nilimueleza upo wewe mjomba ndipo aliponieleza nije nikuambie kwa kunihakikishia kumtoa, hata nilipokuja hapa nilikuwa najiamini kutokana na kauli zake.? ?Mmh! Tulijua huo ni uongo, tulikukubalia ili kukuridhisha lakini hakuna kitu kama hicho. Kaka yako alikufa na tukamzika, hata wewe ulishuhudia.? Sikuwa na jibu zaidi ya kukubali kosa huku nikiendelea kuificha siri nzito moyoni mwangu. Niliamini kama ningemueleza ukweli kuwa kaka yangu hakufa ila ameliwa nyama wakati wa kumtorosha bado asingeniamini. Baada ya likizo nilirudi kijijini kujiandaa na msimu mpya wa kuingia kidato cha pili. Kama kawaida nilikutana na Helena ambaye alionesha ushirikiano wa karibu sana, muda wote nilipokuwa nyumbani tulikuwa pamoja. Huwezi kuamini kila nilipotoka shuleni nilimkuta njiani akinisubiri na kurudi naye mpaka kijijini. Siku zilikatika huku nikiendelea kufanya vizuri katika masomo yangu kiasi cha kila mmoja kunibashiria kufanya vizuri katika mtihani wa mwisho kwa kupata ?division one?. Nilipofika kidato cha nne katika mwezi wa saba, miezi mitatu kabla kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne nilitokewa na jambo jingine la kutisha. Naikumbuka siku hiyo, wakati natoka shule nikiwa katikati ya mashamba sehemu iliyokuwa haina nyumba, wingu zito lilitanda kuonesha muda wowote ingeshuka mvua kubwa. Nilijikuta njia panda kwani kurudi shuleni ilikuwa mbali na kwenda nyumbani ilikuwa mbali. Lakini kwa vile nilikuwa nakwenda nyumbani, nilikaza mwendo kuwahi kabla mvua haijateremka. Sikufika mbali mvua iliyoambatana na upepo mkali ikaanza kunyesha. Nilianza kukimbia lakini upepo mkali ulioambatana na mvua ulinifanya nisione mbele. Niliangalia mti wa karibu ambao niliamini kabisa utanisaidia kupunguza kasi ya upepo japo kwa mvua ningeendelea kunyeshewa . Nilisogea chini ya mti wa mwembe mkubwa na kujibanza na upepo mkali lakini mvua iliendelea kuninyeshea. Mfuko wa madaftari wote ulilowa pamoja na madaftali yote yaliyokuwemo . Kwa muda mfupi giza zito lilitanda kama usiku wa manane. Nilijikuta nikijiuliza kile ni kitu gani? Sikuamini muda wa saa tisa alasiri niliotoka shule mpaka kufika eneo mvua iliponikutia si muda mrefu kisasi cha kuwa na giza zito kama lile. Nikiwa bado nipo chini ya mtu nikimuomba Mungu aniokoe na janga lile, nilishtushwa na sauti za watu waliokuwa wakicheka mfululizo. Nilitetemeka na woga ulinitawala na kukumbuka mambo niliyoyasahau ya kusumbuliwa na wachawi

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sauti za vicheko kila dakika zilizidi kuongezeka na kufanya ziwe kero kwangu kutokana na kuwa kubwa na hivyo kuumiza ngoma za masikio yangu. Nilishindwa kuelewa sauti zile zilitokea wapi, pia giza zito ndilo lilinichanganya zaidi. Nilijiuliza kile kilichonitokea ni nini, kama ni wachawi ina maana wamekaidi amri ya mzee Manoni? Sauti zilizidi kusogea karibu yangu na kufanya nione kama ngoma za masikio zikikaribia kupasuka. Wakati huo mvua ilianza kukatika lakini ubaridi ulikuwa mkali ambao ulifanya nianze kutetemeka na meno kugongana. Kutokana na woga huo nilijikunyata kwenye mti bila kujua sauti zile zinatokea mbele au nyuma yangu. Mara zilianza kupungua huku zikisogea mbali na mimi, nilibaki nikiwa sijui nini hatima yangu. Baada ya muda sehemu ile ikawa kimya ikiacha sauti za vyura na bundi ambaye sauti yake niliifahamu kutokana na kuelezwa na baba. Hiyo ilitokana na siku moja kuisikia juu ya nyumba yetu, nilifahamu karibia sauti zote za ndege kutokana na tabia yangu ya uwindaji. Sauti hiyo ya bundi ilinitisha kwa kujua ni ya uchuro ambayo wengi huamini haina habari njema. Nikiwa bado nipo chini ya mti, kiza kimeendelea kutanda niliamua kuondoka sehemu kwa sababu macho yalishazoea giza na kuiona njia kwa urahisi. Nilitamani kulia lakini niliamini si suluhisho la tatizo langu zaidi ya kupambamba nalo. Nilijipa moyo na kutembea kufuata njia ambayo niliamini ilikuwa ikielekea nyumbani. Baada ya mwendo mfupi nilisikia kitu kama ngoma mbele yangu ikija upande wangu, nilibadili njia na kuingia kwenye mashamba japo sikujua nikipata kule nitatokea wapi hasa kutokana na kiza kilichokuwa kimetanda. Ajabu ya Mungu, nilipoingia tu kwenye shamba milio ya ngoma ilizidi kunifuata, sikukubali kushikwa kirahisi, hivyo nilianza kutimua mbio. Kila nilivyokuwa nikikimbia ndivyo ngoma nazo zilivyokuwa zikisogea kwa karibu yangu. Nilizidi kuchanganyikiwa , niliendelea kukimbia. Kuna kipindi nilifanikiwa kuikimbia sauti ya ngoma ambayo niliisikia kwa mbali, kwa vile nilikuwa nimekimbia kwa muda mrefu bila kupumzika huku nikipiga miereka na kuchubuka baadhi ya sehemu ya mwili na kulitupa begi lililokuwa na vitabu ambalo nililiona kama mzigo. Nilisimama huku nikitweta, sehemu za mbavu zilichoma na kunifanya niiname, mikono ikishika magoti na kuhema kwa shida kutokana na kusikia maumivu makali kila nilipopumua. Nikiwa katika hali ya kukata tamaa nilishtushwa na vicheko ambavyo vilionesha havipo mbali nami. Niliamua kuondoka tena eneo lile huku hali yangu ikiwa mbaya kutokana na kuhisi kizunguzungu, maumivu makali ya mbavu na kifua. Niliandoka kwa kuchechemea angalau nipate sehemu nikajifiche kwa kuamini sitafika mbali kutokana na kupoteza nguvu. Hata hivyo , kutokana na macho kupoteza nguvu nilishindwa kutambua nilipo. Nilifuata kichaka kilichokuwa mbele yangu kama hatua hamsini toka niliposimama. Nilifikiria nikifika pale nitaingia kwenye kichaka kingine ambacho sikuhofia wanyama au wadudu wakali zaidi ya kuokoa uhai wangu ambao ulikuwa unanadiwa kwa bei rahisi. Nilitembea kwa kuchechemea huku mkono mmoja ukiwa kifuani, sauti ambayo haikuwa ngeni masikioni mwangu iliniita: ?Shija...Shija.? Kwanza nilisita kuitika kwa kuhofia kujulikana nilipo, lakini sauti ile iliendelea... ?Shijaaa....Shija usiende huko.? Sikutaka kumsikiliza, niliendelea kwenda huku sauti nazo zikizidi kusogea. Nilipotaka kutimua mbio nilihisi maumivu kwenye goti kutokana na jeraha nililolipata nilipojikwaa na kuangukia shimoni lakini nilinyanyuka na kuendelea kukimbia. Sauti ile ilizidi kuniita: ?Shija usiende huko mbele kuna makaburi, wachawi wanafukua maiti, watakuona.? Sauti ilikuwa ya Helena lakini sikujua alipo, nilijikuta nasimama ghafla na kuitafuta sauti ile inakotokea. ?Shija rudi nyuma,? Helena alinielekeza kwa sauti. Nilifanya kama nilivyoelekezwa kwa kurudi nyuma kuifuata njia niliyokujanayo huku nikiamini kabisa huenda Helena anataka kunifanyia kitu kibaya kutokana na kunirudisha sehemu iliyokuwa na vicheko. Lakini nilipiga moyo konde na kurudi hadi kwenye njia panda. Helena alitokea kwenye kichaka kidogo ambacho nakikumbuka nilikipita kwa kukiona kama nikijificha naweza kuonekana, kumbe yeye alikuwa pale, alijitokeza akiwa katika mavazi yake ya kawaida. Nilijiuliza ilikuwaje nimpite pale na kuniacha mpaka nilipokaribia kichaka kingine. Wakati Helena ananikaribia sauti zilizidi kutusogelea, nilitaka kukimbia lakini aliniwahi na kunishika mkono.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shija unataka kwenda wapi?? Helena aliniuliza kwa ukali kidogo. ?Helena watatukamata,? nilisema huku nikijitahidi kujitoa mikononi mwake ili nikimbilie kule aliponikataza. Lakini Helena alikuwa na nguvu za ajabu zilizonifanya niwe mpole. ?Shija, unataka kwenda wapi?? ?Helena, husikii wanatusogelea.? ?Kina nani?? ?Kelele huzisikii?? ?Unajua zinatoka wapi?? ?Si huku unakotaka kunipeleka.? ?Shija, ulipotaka kukimbilia ndiko ulipokuwa unajipeleka, kelele hizi ni mtego wa kukusogeza walipo wachawi .? ?Helena, mbona imekuwa hivi hawamuheshimu tena mzee Manoni?? ?Shija, kwani mzee Manoni umeacha kumuona kwa muda gani?? ?Mmh! Muda mrefu kidogo.? ?Basi kwa taarifa yako kuna kombora alipigwa katika kazi yetu ya uchawi na kumfanya alale kitandani kwa muda mrefu. Na jana amefariki dunia.? ?Ha!? Nilishtuka kumsikia mlinzi wangu amekufa. ?Shija mzee Manoni kafariki jana usiku, kijijini, tayari taarifa zimezagaa kila kona ila wewe uliyetoka asubuhi kwenda shule, hukuwa na taarifa ile. Baada ya kifo cha mzee Manoni kulikuwa na sherehe kubwa huku mama yangu akiwakumbushia kukutia adabu baada ya kufa mtu aliyekukingia kifua.? ?Mungu wangu nimekwisha,? nilisema nikishika mikono kichwani kwa kukata tamaa. ?Shija nimeapa kukusaidia, jana usiku walipanga wakushughulikie wakati ukitoka shule. Baada ya kupata taarifa hizo nilikuwahi shuleni kwenu, lakini tulichengana kutokana na kupita njia za mkato ili nikuwahi. Nilipofika nilikuta tayari umeondoka. ?Nilijitahidi kuja kwa kasi kukuwahi lakini njiani nilikutana na wingu zito lililonifanya nijue huwezi kufika mbali, lazima utakuwa kwenye hatari ya wachawi , ndipo nilipoanza kukutafuta ili usijiingize kwenye mtego wa wachawi. Kutokana na muda wa kuwanga ulikuwa haujafika, nilijua watakufanyia vitimbi vya kukuchanganya ili usiku uingie na kukutia katika mikono yao.? ?Mungu wangu kama mzee yule amekufa utaweza nini Helena?? Nilizungumza kwa kukata tamaa baada ya kuhisi moyo umekufa ganzi. ?Shija najua upo katika kipindi kigumu hasa muda uliobakia kufanya mtihani, bora mzee huyu angekufa baada ya kufanya mtihani ningekueleza ukimbilie mjini. Lakini kwa udogo wangu, nipo tayari kufa ili kuhakikisha nayaokoa maisha yako.? ?Kwa hiyo huku tunakokwenda ni salama?? ?Ni salama kwa vile sauti ile ipo nyuma wala si mbele yetu.? ?Kama wasiponipata muda huu, usiku si watanifuata?? ?Kazi hiyo niachie mimi, ngoja kwanza nikufikishe kwenu, mambo mengine baadaye.? Helena alinishika mkono na kuniongoza. Kutokana na kuchanganyikiwa , sikujua pale ni wapi kwa sababu ya giza. Ajabu hatukutembea sana, Helena alinieleza. ?Shija tumefika.? Nilishtuka na kujiuliza mambo yote yale yalikuwa yakifanyika wapi.? ?Helena mbona hatukuchelewa kufika?? ?Shija ulichanganyikiwa , matukio yote yalikuwa nyuma ya makaburi.? ?Haya miembeni?? ?Eeh, lile shamba ulimokuwa ni la mzee Masanja.? ?Ha!? Nilishtuka kusikia vile. ?Sasa tuachane na hayo, kama kungekuwa na uwezekano kulitakiwa kupatikane maji ya moto nikukande ili kesho uamke mzima bila hivyo utakuwa katika hali mbaya sana.? ?Helena na usiku utakuwaje?? ?Nitakuletea ngozi yangu, kwa hilo usihofu.? ?Nitashukuru Helena.? ?Shija kama nilivyokueleza , nitahakikisha usalama wako muda wote.? ?Wewe leo hutoki?? ?Sitoki kwa ajili yako, kesho nitajua tutafanye nini.? ?Sasa maji ya moto hakuna, tutafanyaje maana kila dakika maumivu yanazidi?? ?Hakijaharibika kitu, twende kisimani.? Tuliongozana na Helena huku akinisaidia kutembea kutokana na kila dakika maumivu kuongezeka. Tulipofika kisimani, Helena aliniomba msamaha. ?Samahani Shija, nakuja ila usiogope.? ?Sawa.? Helena aliondoka na kutokomea kizani akiniacha nimejiegemeza kwenye mti wa mchongoma uliokuwa pembeni kidogo ya kisima. Muda ule maeneo yale yalikuwa yakitisha sana. Milio ya wadudu na ndege wa usiku ndiyo iliyotawala . Lakini nilikaza moyo kumsubiri Helena bila kuelewa amekwenda wapi. Kutokana na uchovu na kibaridi cha usiku, nilijikuta nikipitiwa usingizi pale kwenye mti. Sauti ya Helena kuniamsha ndiyo iliyoniondoa kwenye usingizi wa mang?amung?amu.? ?He! Shija umelala?? ?Helena wee acha tu, nipo hoi,? nilisema huku nikijitoa kwenye mti. ?Shija tusipoteze muda, vua nguo zote na ulale hapo pembeni ya kisima.? Nilifanya hivyo kwa kuvua nguo zote na kulala pembeni ya kisima. Helena aliingia kisimani na kuchota maji kwenye kindoo kidogo na kukiweka majani mabichi, sikujua ya mti gani. Aliyaingiza ndani ya maji ya baridi na kuanza kunikanda mwili mzima huku nikizidi kutetemeka kwa baridi ya maji.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Helena alinikanda mwili nzima huku maumivu ya majeraha nikiyasikia kila yalipoguswa na maji. Nilishangaa jinsi Helena alivyojitolea kunisaidia kwa kunikanda. Baada ya kumalizaa nilivaa nguo zangu na kunisindikiza hadi nyumbani, tulipokaribia kufika tulisimama na Helena alinipatia kipande cha ngozi kama alichonipa Sabina. ?Shija nakuomba ngozi hii usiitupe, hakikisha muda wote unakuwa nayo, iweke pembeni wakati wa kuoga tu, zaidi ya hapo hakikisha ipo mwilini mwako. Nakwambia hivyo kwa kujua kipindi hiki ni kibaya kuliko chochote kilichotokea. Sasa hivi wachawi hawana pingamizi lolote watafanya watakavyo , hivyo hii ngozi ndiyo kinga yako kipindi hiki cha kujiandaa na mtihani, ukimaliza tu nakuomba uende mjini kwa mjomba wako.? ?Nimekuelewa Helena, nashukuru sijui bila wewe leo ningekuwa katika hali gani, kwani muda huu ni saa ngapi?? Nilipokea kipande cha ngozi na kuuliza.? ?Inakimbilia saa nane za usiku.? ?Mungu wangu! Sijui nyumbani wamenitafuta sana.? ?Lazima watakuwa wamekutafuta .? ?Sijui nitawajibu nini, lakini nimekumbuka nitawaeleza kuwa nililala kwa rafiki yangu kwa ajili ya kujisomea.? ?Na haya makovu?? ?Mmh, hapo sasa sijui nitawadanganya vipi?? ?Sasa, sikiliza wakikuuliza waeleze mlikwenda kucheza mpira wakati wa kurudi aliangukia shimoni ndipo rafiki zako walipokusindikiza , mlipofika usiku ulikuwa mkubwa uliingia chumbani kwako kulala.? ?Mmh! Sidhani kama watanielewa .? ?Basi kapumzike usiku mkubwa, nina imani bado wanakutafuta mwisho watakuja kwako usiogope hawawezi kukuona.? ?Nashukuru Helena.? ?Nilitaka kusahau nakuomba usiwaeleze chochote wazazi wako.? ?Nitafanya hivyo .? Niliagana na Helena kwa kuingia ndani kulala, wasiwasi wangu mkubwa nilijiuliza nitaweza kulala kwa kuhofia maumivu ya mwili. Lakini haikuwa hivyo , nilipogusa ubavu tu usingizi mzito ukanichukua. Nilishtuka siku ya pili pale nilipoamshwa na sauti ya baba. Niliamka kwa kuhofia maumivu, sehemu kubwa ya mwili ulikuwa na maumivu madogo, kasoro kwenye goti kulikuwa na maumivu makali yaliyonifanya nitembee kwa kuchechemea. Baba aliponiona alishtuka. ?Vipi tena?? ?Ajali baba.? ?Ya nini na imetokea saa ngapi?? ?Nilidondokea kwenye shimo wakati wa kurudi nyumbani, kutokana na giza sikuweza kuliona na kupoteza fahamu kwa muda.? ?Mungu wangu! Lakini mchezo wa kutembea usiku umeuanza lini Shija?? ?Imetokea tu baba, roho haikunipa kulala kule kwa kuwa sikuaga.? ?Siku ya pili hata kama hukuaga, lala hukohuko mpaka asubuhi usitembee usiku ni mbaya sana, ona sasa yaliyokukuta , unafikiri ungekufa nani angejua?? ?Samahani baba, nimekuelewa.? ?Na umerudi saa ngapi?? ?Sikujua ni muda gani ila ulikuwa usiku sana.? ?Ona sasa, sisi tulifikiri utalala kwa rafiki zako kujisomea, kumbe umekumbwa na masahibu mazito.? ?Ni kweli nilitaka kulala, lakini sikuaga niliamua kurudi japo usiku.? Mama naye alikuja kunijulia hali na kuniasa kwamba nisitembee usiku, nilimkubalia huku bado nikificha siri moyoni mwangu. Sikuweza kwenda shule kutokana na jeraha la goti lililokuwa likiniuma sana. Ilibidi nitafutiwe mti wa kutembelea. Baada ya wazazi kuondoka nilibakia peke yangu nyumbani, kutokana na kuhisi uchovu, nilirudi chumbani na kujilaza. Niliwaza mengi kutokana na kupoteza mfuko wangu wa shule na kiatu kimoja. Kiatu hakikuniuma sana japo hali yetu ya kujikongoja ilinikatisha tamaa kukipata haraka. Kilichoniuma sana ni ?counter book? zangu zilizokuwa na ?notice? nyingi nilizotumia kujisomea kila nilipopata muda. Nikiwa katika lindi la mawazo, sauti ya Helena alinizindua. ?Shija...Shija.? ?Helena.? ?Abee,? Helena aliitikia huku akisukuma mlango. ?Vipi Shija, umeamkaje?? ?Sijambo ila jeraha la kwenye goti ndilo linanisumbua.? ?Hebu,? niliusogeza mguu karibu yake. Nilipojaribu kujinyanyua na kutembea maumivu yalinifanya nishike ukuta. ?Basi Shija, pole eeh.? ?Asante.? ?Vipi wazazi wako umewambiaje?? ?Nimewadanganya wameniamini.? ?Ooh, afadhari,? Helena alishusha pumzi ndefu. ?Vipi mbona hivyo ?? Nilimuuliza baada ya kushusha pumzi kama ameshusha mzigo mzito. ?Nilikosa usingizi juu ya maswali ya wazazi wako, nilijua wangekubana lazima ungesema ukweli.? ?Helena, mpaka mzee Manoni anafariki nimebaki na siri nyingi ambazo wazazi wangu hawazijui, kama wangezijua, baba yangu angemkata mapanga mama yako.? ?Ooh, asante Shija kwa kuficha siri hizo.? ?Helena huu mguu ni wa kawaida au wa kichawi?? ?Wa kawaida, wachawi hawakuwahi kukugusa, ila kuna dawa nitakuletea itakusaidia, ambayo hutumiwa na wachawi wanapopata majeraha kwenye kazi zao na wakiumia hupona kwa muda mfupi.? ?Nitashukuru, Helena nataka kusoma, nikikaa nyumbani nitapitwa na vitu vingi hata couter book zangu na kiatu kimoja vimepotea.? ?Ooh kweli nilisahau, nilitaka kukuuliza jana kuhusu kiatu na mfuko wa madaftari.? ?Kiatu sijui nilivuka wakati gani, ila mfuko wa madaftari niliutupa wakati nakimbia baada ya kuuona mzigo.? ?Basi hebu niachie hiyo kazi nitakutafutia nina imani kuwa asubuhi hii hakuna aliyeviokota .? ?Vipi usiku hukutoka?? Nilimuuliza. ?Shija hayo si muhimu kama kutafuta vitu vyako vya shule.? ?Sawa.? Baada ya mazungumzo Helena aliondoka huku nikiamini ni vigumu kuvipata vitu vile. Nilijilaza kitandani kumsubiri, kutokana na uchovu usingizi ulinipitia, nilishtushwa tena na sauti ya Helena. ?Shija umelala?? ?Si unajua uchovu vipi za huko?? ?Nzuri vitu vyako nimevipata, wala sikupata shida kuviona,? Helena alisema huku akiwa ameshikilia mfuko wa madafutari na kiatu. ?Ha! Siamini umevipata wapi?? ?Ulipoviangushia? Kilichonishangaza kilikuwa ni mfuko wangu wa madaftari, ulikuwa mkavu pamoja tofauti na mvua ilivyonyesha . ?Helena mbona mfuko unaonesha kama hakukuwepo na mvua jana. ?Shija mbinu za kichawi huziwezi, hakukuwa na mvua yoyote zaidi ya kiini macho.? 



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati vishindo vikiendelea kuizunguka nyumba, nilijua kabisa nimezidiwa ujanja. Bado sikuamini kama kweli kipande cha ngozi kimepotea, nilirudia kutafuta katika mfuko wa kaputula. Jibu lilikuwa lile lile hakukuwa na kipande cha ngozi. Nilijikuta nimetumia nguvu nyingi kutafuta, jasho lilinivuja kama nimemwagiwa maji, mapigo ya moyo yalikuwa juu kwa hofu. Nilishika kiuno kuwaza kipande cha ngozi nimekipotezea wapi. Nilifikiria kama ingekuwa mapema ningekwenda kwa Helena kuomba msaada lakini ulikuwa usiku mkubwa niliokatazwa na wazazi wangu kutembea muda huo. Nilijiuliza nitafanya nini, kwani vishindo vilizidi kuisogelea nyumba yetu, nilitamani kupiga kelele kuomba msaada kwa wazazi wangu lakini nilichelewa. Ghafla upepo mkali ulivuma uliosababisha kibatari kuzimika. Haikuchukua muda, mvua kubwa iliteremka. Sauti kali ya mvua ilinifanya nisisikie chochote kilichokuwa kikiendelea nje. Nilisimama wima huku nikitetemeka kwa kuamini ile haikuwa mvua ya kawaida bali ya kichawi ya kuja kunichukua. Nilimuomba Mungu aniokoe na balaa la wachawi , mvua ilinyesha kwa muda mrefu sana na ilipokatika nje kulikuwa kumepambazuka. Nilipoangalia nje ilionesha kweli kulikuwa na mvua kubwa iliyonyesha kiasi cha kuweka madimbwi. Nilitoka nje na kwenda msalani na kukuta mlango wa chumba cha wazazi wangu bado umefungwa kuonesha kuwa bado hawajaamka. Nilijiuliza muda ule utakuwa ni saa ngapi? Nilirudi chumbani kwangu na kukaa kitandani huku nikikisikia kichwa kizito kutokana na kukesha kwa hofu ya wachawi . Niliamua kujilaza kidogo kuvuta muda kutokana na kuhisi uchovu kila kona ya mwili. Wakati naanza kusinzia mlango uligongwa na kusikia sauti ya baba. ?Shija amka kumekucha.? Nilitaka kuitikia lakini midomo ilikuwa mizito kutokana na usingizi ulionijaa kichwani, baba aliendelea kuniita. ?Wee Shija, mvua zinakudanganya amka kumekucha.? Nilijilazimisha kunyanyuka huku nikisikia kichwa kizito na kizunguzungu. Nilifungua mlango na kutoka nje. ?Vipi mbona hivyo ?? ?Kichwa kinaniuma.? ?Nawe unasoma sana punguza kusoma, kama hukuelewa miaka yote minne utaelewa kwa hizi wiki mbili zilizobaki?? ?Nitapunguza baba.? ?Sasa shule utakwenda?? ?Lazima niende, muda uliobaki si wa kukosa hata kidogo.? Nilikwenda kuoga kuondoa uchovu, baada ya kuoga nilielekea zangu shule huku mwili ukiwa umechangamka kiasi lakini kichwa bado kilikuwa kizito kwa usingizi. Nilipofika shule bado sikuwa nimechangamka kama nilivyozoeleka , hata darasani muda mwingi nilisinzia na nilipoulizwa, nilisingizia naumwa. Lakini nilijitahidi kusoma mpaka muda wa kuondoka, kama tulivyokubaliana siku ile ya Ijumaa tulitakiwa tusome pamoja, sikuweza kurudi nyumbani kwenda kwa mwanafunzi mwenzangu wa kike ambaye pia alikuwa mpenzi wangu tuliyepeana mikakati mingi, baada ya kumaliza elimu yetu ya chuo kikuu kama tukifika. Kwa vile sikupata muda wa kulala, nilipofika kwa rafiki yangu alinielekeza chumba cha wageni ambako nilala kupunguza usingizi kabla kuanza kujisomea. Hakuwa tofauti na Sabina, alikuwa mdadisi mzuri sana na mtu mwenye uchungu wa kufika mbali. Pamoja na kuwa mpenzi wangu, wakati wa kujisomea tuliweka urafiki pembeni na kusoma kwa bidii. Rusia alinishtua saa mbili usiku, wakati huo chakula cha usiku kilikuwa tayari, nilijumuika na familia yake kula chakula na baada ya chakula tulipumzika mpaka saa tatu na nusu, tuliingia kwenye chumba tunachokitumia kujisomea. Tulijisomea huku nikimsaidia baadhi ya vitu ambavyo yeye vilimtatiza, ilipofika saa sita usiku, kichwa kilianza kuniuma kwa mbali. Rusia aliniletea dawa ya kutuliza maumivu, nikameza. Kilitulia kidogo na kutufanya tuendelee kusoma lakini ilipofika saa nane usiku, maumivu yalirudi tena kwa kasi. Rusia alinishauri tupumzike ili kesho tuendelee kusoma, alinisindikiza chumba cha wageni na kuniacha nikijilaza na yeye kwenda chumbani kwake . Nililala vizuri hadi asubuhi, kwa vile haikuwa siku ya shule, niliamua kurudi nyumbani kutokana na hali yangu nilivyoisikia . Japo Rusia aliniomba anipeleke hospitali, nilimueleza ule ulikuwa ni usingizi tu wala si kitu chochote na baada ya muda, ningekuwa katika hali ya kawaida. Niliagana na Rusia na kurudi zangu nyumbani tukiahidiana kuonana Jumapili ambapo tulipanga kusoma kuanzia saa nane hadi saa mbili usiku, kisha tungepumzika kwa ajili ya chakula na kuendelea tena saa nne hadi saa nane usiku. Nilirudi hadi nyumbani ambako nilifika majira ya saa nne asubuhi, bado mwili ulikuwa na uchovu. Nilipanga nilale kidogo nikiamka nijisomee mpaka kiza kitakapoingia. Nilipoingia chumbani kwangu, kichwa kilinipasuka katikati ya utosi na kuhisi maumivu makubwa. Nilishika mikono kichwani kama nitaweza kukizuia kisipasuke, nilijivuta mpaka kitandani na kujilaza huku maumivu ya kichwa yakizidi kuongezeka kama kuna mtu ananichokonoa na mti kwenye ubongo. Nilitaka kupiga kelele kuomba msaada lakini sauti haikutoka. Mlangoni niliwaona watu wakiingia wakiwa uchi, sikushangaa kwani nilijua wale ni wachawi . Mmoja alinifuata kitandani na kunilisha kitu ambacho kilinifanya niuone ulimi wangu mzito kama jiwe. ?Jamani tufanyeni haraka, tusifanye tena kosa,? alisema jamaa mmoja aliyeonekana kiongozi wao aliyekuwa amejifunga pembe ndogo mkono wa kushoto. Walitoa kitu kama unga na kunipulizia kisha kuniondoa kitandani, baada ya muda kiliingizwa kitu sawa na urefu wangu ambacho nilikitambua ni kipande cha mgomba na kulazwa kitandani kwangu. Baada ya kulazwa, ulitolewa unga kama niliopuliziwa na kupulizwa kwenye ule mgomba ambao uligeuka na kuwa mtu aliyeonekana amelala. Mtu mwenyewe nilikuwa mimi, vitu vile havikuwa vigeni kwangu niliamini tayari nimegeuzwa msukule.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya zoezi la kuugeuza mgomba kuwa na taswira yangu kumalizika, walinichukua na kunisimamisha nyuma ya mlango. Baada ya hapo waliondoka na kuniacha. Baadaye niliisikia sauti ya Helena ikiniita kutokea nje, alipokosa jibu aliingia ndani lakini hakuniona. Nilimuona akinitafuta kitandani, lakini sikuwa na uwezo wa kutoa sauti kumwambia nipo nyuma ya mlango. Baada ya kunikosa ndani, alitoka huku akiendelea kuita kwa kuzunguka nyuma ya nyumba. Nilimsikia akisema kwa sauti. ?Atakuwa amekwenda wapi?? Baada ya muda nilisikia sauti ya kuondoka kwa Helena ambaye aliamini kabisa sipo nyumbani. Muda ulikatika huku hali ya ukimya ikitawala, juu ya kitanda mgomba wenye taswira yangu ulikuwa umelazwa na kufunikwa shuka. Majira ya jioni niliwasikia wazazi wangu wakirudi kwa kuzisikia sauti zao. ?Shija atakuwa amerudi au na leo anaendelea kusoma?? Sauti ya mama iliuliza. ?Mmh! Sijui lakini mlango wake unaonesha kama amerudi.? Ulipita muda huku wakizungumzia mambo ya shamba, giza liliendelea kuumeza mwanga na nuru ya mchana ilipotea. Niliusikia mlango ukifunguliwa na kuingia mtu aliyekuwa na kibatari mkononi ambaye nilimtambua kuwa ni baba. ?Shija...Shija,? aliniita lakini hakukuwa na jibu. Baba alisogea karibu na kitanda na kuanza kukitikisa kipande cha mgomba kilicholazwa bila kujua sikuwa mimi. ?Shija...Shija,? aliendelea kuniita, lakini hapakuwa na jibu, nilijitahidi nifunue mdomo wangu kumueleza nipo nyuma yake lakini sikuweza. Baba aliendelea kunitikisa huku akiniitaka kwa kuongeza sauti lakini sikuweza kuitika. Baba alionekana kuongeza nguvu ya kutikisa huku akiniita kwa sauti ya juu ambayo hata mama aliisikia. ?Baba Shija vipi?? Mama aliuliza. ?Usingizi gani huu, mtu namtikisa na kumuita kwa sauti lakini haamki.? ?Labda kachoka na masomo, muache apumzike si unajua mwanao amepanga kufanya vizuri kwenye mtihani wake?? ?Mmh, hata hivyo hatuwezi kumuacha, alipotoka jana alfajiri hadi leo tumuache, lazima tumjulie hali yake.? ?Si ungemuacha mpaka chakula kitakapoiva .? ?Mke wangu hata sielewi, leo roho yangu imekuwa na hamu ya kuzungumza na mwanangu.? ?Haya muamshe,? mama alisema huku akitoka nje. Baba aliendelea kuutikisa ule mgomba bila kuonekana dalili zozote za kuamka. Ndipo alipotoka na kurudi na maji ambayo aliumwagia ule mgomba aliodhania ni mimi, lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote . Nilimsikia akisema: ?Usingizi gani wa namna hii, mpaka nammwagia maji bado tu haamki.? Aliendelea tena kuutikisa kwa nguvu huku akiita. ?Shija... usingizi gani huu?? ?Baba Shija kwani kuna nini?? Mama alirudi tena ndani baada ya kuona baba katumia muda mrefu sana kuniamsha. ?Yaani haya ni maajabu, haijawahi kutokea kumuamsha Shija kwa kipindi kirefu hivi, nimemwagia maji kichwani lakini bado tu haoneshi kushtuka.? ?Sasa ni usingizi huo? Hata kama angekesha anasoma, mtu umwagiwe maji bado uendelee kulala, hebu muamshe kwa kumnyanyua .? Baba alifuata maelekezo ya mama, aliunyanyua mgomba ambao ulionekana ni mimi kabisa. Lakini hakuonesha dalili zozote za uhai, kulegea kwa ule mgomba ambao wazazi wangu waliamini ni mtu kuliwatisha. Katika kuuchunguza mwili ule waligundua haukuwa na uhai. ?Mama Shija kuna usalama kweli hapa?? ?Kwani vipi mume wangu?? ?Hebu subiri,? baba bado hakuamini kama kweli nimekufa, alipima mapigo ya moyo ambayo niliamini kabisa yatakuwa yamesimama. Haikuwa tofauti na siku kaka aliporudi, siku ya pili nikakuta amefariki kumbe tuliwekewa ?danganya toto?. Baba alitoka nje, haukupita muda mama alirudi kutaka kupata uhakika. Mama hakuwa na simile, aliangua kilio cha sauti ya juu kunililia. Haikuchukua hata dakika kumi majirani walifika kutaka kujua kuna nini, mama aliwaeleza kuwa sipo tena dunia. Hapo ndipo vilio vilipoongezeka kutokana na jinsi nilivyokuwa nikiishi na majirani. Nilisikia sauti za wanaume wakizungumza kuhusu kifo changu. Kila mtu nilimsikia akisema lake, baada ya muda waliingia wanaume watatu ambao waliuweka vizuri mwili wa bandia na kuufunika shuka nyeupe. Nje vilio viliendelea kutawala, sauti ya mama ndiyo iliyokuwa juu kuliko wote waliokuwa wakilia. Moyo uliniuma jinsi watu walivyokuwa wakinililia kama nimekufa kumbe nipo nyuma ya mlango. Walipotoka watu walioteuliwa kuitengeneza maiti, niliona ukuta ukipasuka na kuingia wachawi waliokuja asubuhi wakiwa na tunguri mkononi. Mmoja ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wao, alimimina unga mweusi kiganjani kwake , kisha aliinyunyizia ile maiti ya bandia kwa kuanzia kichwani mpaka miguuni. Baada ya kumaliza, unga uliobakia alinisogelea na kunipulizia usoni kisha walitoweka . Waliponipulizia nilihisi kama mwili umekufa ganzi, nilitamani kulia lakini nilihisi machozi yamenikauka . Nini kitaendelea? Ni kweli Shija ndio ameshakuwa msukule? 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA..





0 comments:

Post a Comment

Blog