Simulizi : Nitakufa Mara Ya Pili
Sehemu Ya Tatu (3)
-?Unajua nini Shija?? ?Hata sijui.? ?Wakati tunafika eneo lile mama Helena alikuwepo na shoga zake, niliogopa anaweza kutuona. Kama angeniona mimi asingekuwa na tatizo ila angekuona wewe na mazingira haya ungeleta utata mkubwa.? ?Mbona asikuwaona?? ?Walikuwa kikazi usingewaona, sijakupaka dawa kwa kuhofia hali ambayo ungeiona lazima ungepagawa, pengine ungepiga kelele.? ?Sasa kama ulijua hivyo kwa nini ulinileta huku?? ?Lazima kila kitu utaona tu mpenzi wangu.? ?Kwa hiyo?? ?Turudi tena.? ?Si watatuona?? ?Walikuwa wakiaga ili waondoke, sasa hivi najua hawapo.? Muda ulikuwa unazidi kuyoyoma kigiza nacho kilizidi kuchukua nafasi yake, ubaridi ndani ya maji nao ulizidi kuongezeka. Ujasiri wa Sabina ulinifanya nami nifiche hofu yangu japo niliamini maeneo tuliyokuwepo hata kama tungetokewa na tatizo asingekuwepo wa kutusaidia. Alitoa kikaratasi kilichokuwa na unga mweusi ambao haukuwa mgeni tena kwangu, alichovya kidole na kunipaka chini ya macho. Baada ya kujipaka tulirudi tena taratibu, tulipokaribia lile eneo nilishangaa kuona kuna ng?ombe wengi waliokuwa wakila majani na wengine wakinywa maji pembeni ya ziwa. Nilijiona kama nipo dunia nyingine tofauti na ya mwanzo, nikiwa bado nipo katika dimbwi la mawazo. Sabina alininong?oneza. ?Umeona mabadiliko yoyote ?? ?Ndiyo.? ?Umeona nini?? ?Ng?ombe wengi.? ?Mchungaji umemuona?? ?Hataa.? Mara nilimuona kijana mmoja akiwa katika vazi la rubega la kaniki, nilipomuangalia vizuri nilimtambua. Alikuwa akiswaga ng?ombe wasiingie ndani ya maji. ?Ha! Huyu si Samweli tuliyekuwa tunasoma naye?? nilisema kwa sauti kidogo. Alikuwa ni mwanafunzi mwenzetu aliyegombana na Helena na kumuapia ataona, na siku ya pili Samweli alianguka akicheza na kupoteza maisha. Kila mmoja alijua Samweli amekufa baada ya kuhudhuria mazishi yake. Japo baada ya mazishi maneno yalienea kuwa Samweli hakufa. Pamoja na maneno ya chinichini, hakukuwa na ukweli wowote , siku zilikatika watu tukaamini kweli Samweli amekufa. Nilibakia nimetokwa na macho pima.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
?Unamjua?? Sabina aliniuliza. ?Eeh, si Samweli yule.? ?Si nilikueleza, Shija kila kitu nilichokueleza kina ukweli, nilipoamua kuusema ukweli wa wachawi nilijitoa mhanga wa uhai wangu. Kama wakijua nimekueleza haya ujue lazima nitapoteza maisha yangu? ?Sabina, nina siri nzito moyoni mwangu hivyo usihofu kitu, nitailinda mpaka mwisho wa uhai wangu.? ?Ni kweli lakini nina wasiwasi na baba yako kutokana na mabadiliko yako.? ?Sabina we nione hivi siwezi kutoa chochote ulichonieleza na kunionesha.? Wakati huo tulikuwa bado tumo ndani ya maji ya mabega, kuogelea nilikuwa najua lakini wasiwasi wangu mazingira yalikuwa yakinitisha sana hasa baada ya kiza kutukutia kwenye maji huku yakizidi kuwa baridi. Muda wote sikumuona kaka yangu, nilijiuliza kwa nini nilikuwa simwoni. ?Mbona simuoni?? ?Hata mimi nashangaa lakini yupo.? ?Sabina usiku unaingia nasikia sehemu hizi zina viboko tunaweza kudhurika.??Shija acha woga, hebu nisubiri nikamuangalie.? Sabina alitoka nje ya maji na kuelekea eneo lililokuwa na ng?ombe wengi, aliingia ndani ya kundi lile la ng?ombe. Nilibakia kwenye maji peke yangu huku baridi ikizidi kunipiga. Nilijikuta nikiingiwa na wasiwasi baada ya Sabina kuchelewa kurudi. Nilijikuta najiuliza kama asingerudi nigefanya nini. Kurudi njia tuliyoijia nisingeweza kuitambua kutokana na eneo lake kuwa la hatari hasa muda ule wa kiza kuanza kuingia. Kwenda mbele niliogopa kutokana na kuwepo kundi la ng?ombe bila kujua usalama wake ulikuwa vipi. Nilibakia nimeganda kwenye maji huku nikimuomba Mungu ashushe miujiza yake. Baada ya muda Sabina alitokea kwenye kundi la ng?ombe na kusogea karibu na maji, alinionesha ishara ya mkono nitoke ndani ya maji nimfuate. Nilifanya vile kwa kusogea pembeni ya ziwa na kutoka ndani ya maji kumfuata alipokuwa amesimama. Alinishika mkono na kunipitisha katikati ya kundi la ng?ombe. Nilimfuata nyuma hadi tulipowavuka wale ng?ombe na kuingia kwenye mashamba ya mpunga kisha kuelekea kwenye makazi ya watu. Nilichoshukuru ni kwamba giza lilikuwa limeanza kuingia, hivyo kutoka kwetu na nguo zetu na maji hakuna aliyetuona. Nilishangaa kufika mapema barabarani na kuona kumbe kulikuwa na njia ya karibu kuliko kuzunguka njia ya hatari kama ile. Kingine ni kwamba mpaka tunaondoka eneo la ziwani sikumuona kaka yangu. ?Sabina mbona tumepita mbali kumbe kulikuwa na njia fupi?? ?Shija nilikuwa na maana yangu tusingeweza kuja moja kwa moja tungeweza kuonekana na wao kutufuatilia na wangejua umewatambua usiku wa leo usingelala.? ?Sasa mbona tumerudi na njia hii?? ?Sasa hivi wameisha ondoka.? ?Na kaka yangu mbona sikumuona?? ?Hata mimi nashangaa, lakini mara nyingi huwa huku lakini nitamuuliza Helena.? Tulivuka barabara na kuanza kuitafuta njia ya kurudi nyumbani, kama kawaida niliingia nyumbani muda ukiwa umekwenda. Siku hiyo baba hakunivumilia alinichapa sana na kutaka kujua nilikwenda wapi. Nilimdanganya kwamba nilikwenda kucheza mechi kijiji cha mbali kidogo. Alinipa onyo kali la kuwahi kurudi nyumbani na kwamba kila nikitoka shule lazima nirudi nyumbani. Niliona kwa onyo lile lazima baba angeniona mkaidi na sina adabu kutokana na ukweli kwamba harakati zangu na Sabina zilikuwa zikifanyika jioni. Siku ile nililala salama mpaka siku ya pili. Asubuhi kama kawaida baba aliniamsha kuwahi shule, kama ilivyokuwa ada yangu nilinawa kisha nilipitia vitu muhimu vya shule na kuwahi namba ambapo njiani kama siku zote nilikutana na Sabina. ?Za asubuhi Shija.? ?Nzuri kiasi.? ?Kivipi?? Nilimuelezea yaliyonikuta jana yake na onyo kali nililopewa na baba. Sabina alinionea huruma lakini wasiwasi wake mkubwa ulikuwa ni mimi kuitoa siri hiyo nje. ?Pole sana mpenzi wangu, lakini hukumweleza ukweli?? ?Sabina niamini mpaka nakufa siri hii itabakia moyoni mwangu.? ?Asante sana Shija naamini kuwa na wewe ni chaguo langu sahihi.? ?Hata mimi kuwa na wewe ni chaguo langu sahihi.? Tilicheka na kugongeana mikono huku tukielekea shule, tulipokaribia shule Sabina aliliita jina langu na kunigeukia, kitu kilichonifanya nisimame. ?Basi jana nilipofika
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nyumbani nilikwenda hadi kwa kina Helena kumwulizia kaka yako? ?Mmh!? ?Kumbe jana hakwenda kuchunga kutokana na kuamka anaumwa!? ?Unataka kuniambia hata ndondocha wanaumwa ?? ?Kwa nini wasiumwe ? Kwani wale ni binaadamu kama binadamu wengine, sema wanaishi katika mazingira ya kichawi tu.? ?Na wanakufa ?? ?Kila kinachomtokea mwanadamu nao huwatokea.? ?Sasa wakifa mnawafanya nini?? ?Wanaliwa nyama!? ?Mmh,? niliguna.? ?Shija kuna kitu nilikuwa nakifikiria leo? ?Kipi?? ?Nilikuwa na wazo la mimi kujifanya naumwa ili na wewe unisindikize kisha tukishatoka maeneo ya shule twende kwa kina Helena? ?Kufanya nini?? ?Nikakuoneshe kaka yako.? ?Utawezaje na wenyewe wapo??
Muda huo huwa hakuna mtu yoyote nyumbani hivyo itatusaidia kuingia mpaka ndani na kumuona.? ?Wazo zuri lakini huoni wataona kama mchezo, mimi jana leo wewe ?? ?Sasa ulikuwa unanishauri nini?? ?Fanya hivi, mimi kesho siji shule nitajifanya naumwa nitakapoamshwa asubuhi. Wewe jifanye unaumwa ili urudi nyumbani peke yako? ?Mmh, lazima Helena atanisindikiza na kuharibu kila kitu.? Wazo la Sabina lilikuwa zuri lakini utekelezaji wake ulitaka akili sana, wazo la haraka lilikuwa Sabina asije shule na mimi vile vile nisiende shule kisha anipitie twende kwa kina Helena kumuona kaka. Baada ya kukubaliana tulikimbia mstarini kuhesabu namba baada ya kengele kulia. Baada ya usafi tuliingia darasani, na kipindi cha mwalimu Vene kilikuwa cha kwanza. Aliingia kama kawaida yake akionekana kavaa gauni la maua. Niliamini huenda siku ile hakuwa uchi, baada ya kutuachia kazi alirudi ofisini. Nilimfuata Sabina kwenye dawati lake huku wakitutania mtu na mkewe. Hilo halikunitisha kwa vile hawakuwa na vithibitisho, kwani si mimi na Sabina tu tulikuwa katika mwonekano huo, bali kulikuwa na wasichana na wavulana wengi waliokuwa karibu sana. Nilipomsogelea nilimuuliza kwa kumnong?oneza. ?Vipi na leo hakuvaa?? ?Shija mwalimu Vene huwa havai nguo siku zote!? ?Mmh, halafu!? ?Poa, kesho nikuletee tena?? ?Acha tu la muhimu ni kupata uhakika zaidi ya hapo itanichanganya.? Niliachana na Sabina baada ya mwalimu wa somo jingine kuingia. Muda wa kurudi nyumbani ulipofika nilirudi nyumbani nikiongozana na Sabina kama kawaida. Tulikaa sehemu ya kujificha karibu na nyumbani ili nisichelewe, muda ulipofika tuliachana kwa yeye kurudi kwao na mimi kwenda kwetu. Kabla ya kuacha Sabina alinikumbushia mpango wetu wa kutokwenda shule kwa pamoja. Siku ya pili nilipoamshwa na baba nilisingizia kuumwa kichwa naye akanipa dawa ya maumivu ambayo niliimeza lakini bado niliendelea kushikilia kwamba kichwa kilikuwa bado kinaniuma. Kwa vile sikuwahi kutokewa na hali ile aliniacha nipumzike nyumbani kusikilizia hali yangu. Hivyo , watu wote nyumbani walielekea shamba na kuniacha nimelala. Majira ya saa nne Sabina alibisha hodi nyumbani, nilitoka na kukutana naye. ?Vipi upo tayari?? ?Nipo tayari.? ?Basi twende zetu.? Tulielekea nyumbani kwao Helena, nyumba ambayo ilikuwa umbali kama viwanja viwili vya mpira kutoka nyumbani kwetu. Eneo la nyumba lilikuwa kimya, hakukuwa na mtu yeyote . Sabina aliniambia nimsubiri aende akaangalie hali ya hewa. Alikwenda kwa kujiamini hadi kwenye nyumba moja iliyokuwa pembeni kidogo na kuingia ndani. Nilijiuliza Sabina alijiamini nini kuingia nyumba ya watu? Kama wenyewe wangerudi muda ule angewaeleza nini? Nilibaki nimesimama huku nikitetemeka na kujiuliza kama mama Helena angetokea ningemwambia nini? Nikiwa katikati ya lindi la mawazo, Sabina alitoka ndani ya ile nyumba na kuniita kwa kunipungia mkono. Kwanza nilisita kwenda lakini alizidi kuniita kuonesha nifanye haraka. Kwa wasiwasi mwingi nilijikuta nikikimbia huku miguu ikipandana, hivyo nikaanguka mweleka. Nilinyanyuka haraka na kumfuata Sabina pale mlangoni nilipofika aliingia ndani na mimi nilimfuata. Tuliingia ndani kisha aliufunga mlango. Ndani ya nyumba ile kulikuwa na
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mitungi mingi, na wala sikuona kitu kingine. Sabina alifungua kikaratasi chake na kunipa dawa ya kuona na kujipaka. Mmh! Sikuamini vitu nilivyoviona mle ndani. Nyumba kwa nje ilionekana ndogo sana lakini ndani lilikuwa jumba kubwa sana. Ndani ya jumba lile kulikuwa na watu wengi waliokuwa na kazi nyingi tofauti. Wapo waliokuwa wakitwanga , wengine walikuwa wakipasua magogo ya kuni ya kupikia pombe ya kienyeji. Wengi waliokuwemo mle ndani nilikuwa nawafahamu, ambao walikufa na tukawazika . Walikuwa buheri wa afya; tofauti yao nywele na kucha ndefu na wote walikuwa vifua wazi huku chini wamejifunga kipande cha kaniki. Lakini kila kona sikumwona kaka yangu. Nilimgeukia Sabina na kumuuliza. ?Yupo wapi sasa?? ?Yule pale chini amelala kwenye ngozi ya ng?ombe.? Tulisogea mpaka alipokuwa amelala kaka yangu. Sikuamini macho yangu; alikuwa kaka yangu kweli! Nilitaka kupiga kelele lakini Sabina alikuwa makini kwa kuniziba mdomo huku akinitoa nje. Tulipofika nje na kutoka eneo la kina Helena nilikaa chini na kulia kama ndiyo siku ya msiba wa kaka yangu. ?Shija unataka kuniangusha, nilikueleza nini na unafanya nini?? ?Inauma Sabina.? ?Najua inauma lakini wewe ni mwanaume, la muhimu tujipange tujue tutamtoaje.? ?Tutaweza?? ?Tutaweza japo ni kazi nzito la muhimu kama tutafanikiwa kumtoa basi akafichwe mbali na hapa.? ?Siamini, siamini! Kumbe kaka yangu anateseka hapa wakati tunajua amekufa!? ?Shija kuwa mwanaume wa kweli, ukijichanganya tutampoteza. Siri hii usimwambie mtu yoyote .? ?Nitajitahidi, lakini katika siku zote leo nimeumia sana!? ?Utazoea tu; pole sana mpenzi wangu.? Baada ya kutoka kwa kina Helena tulikwenda mbali na eneo la nyumbani ambako Sabina alisema alikuwa na mengi ya kunieleza juu ya wachawi .
Wakati tunatoka eneo lile tulikutana na mzee Manoni, japo tulishtuka lakini kila mmoja alificha hofu yake na kumsalimia. ?Shikamoo mzee Manoni.? ?Marahaba, vipi leo hamkwenda shule?? ?Mi naumwa.? ?Hata mimi.? ?Sasa mbona mpo pamoja?? Swali lile lilitufanya sote tuangalie chini, baada ya kimya kifupi mzee Manoni alisema. ?Haya jamani baadaye.? Bila kumjibu tulijikuta tukikanyagana kwa kugongana wakati wa kuondoka, baada ya kupoteana na mzee Manoni Sabina alinieleza kitu. ?Shija nikuambie kitu.? ?Niambie.? ?Leo tusizungumze lolote, inaonekana kuna kitu mzee Manoni amekitilia wasiwasi.? ?Mmh, sawa.? ?Kuna kitu kingine nataka nikueleze kuhusu Helena.? ?Kitu gani hicho tena?? ?Kama nilivyokueleza , usionesha kitu chochote kwa Helena lazima atashtukia na akigundua nimekupeleka kwao lazima msala utakuwa kwangu.? ?Nitajitahidi, japo chuki yangu ilikuwa ni kubwa sana kwake .? ?Shija kama nilivyokueleza kuhusu ushiriki wetu na Helena katika uchawi ni wa kulazimishwa, hata mimi siku ya kuuchukua rasmi mwili wa kaka yako nilikuwepo lakini si mapenzi yetu bali shinikizo la wazazi wetu.? ?Nimekuelewa Sabina.? ?Niite mpenzi.? ?Nimekuelewa mpenzi.? ?Kuna kitu kingine nataka kukueleza kuhusiana na Helena na kaka yako.? ?Kitu gani hicho?? ?Toka tulipoanza mahusiano ya kimapenzi, Helena amekuwa akitoa unafuu wa kazi hata kutomfanyisha kazi ngumu. Pia katika misukule, kaka yako ndiye anayelala pazuri hata kula chakula kizuri.? ?Maskini nilitaka kumchukia bure Helena kumbe mtu muhimu sana kwetu.? ?Hata mpango wa kumtoa kaka yako mtu mwenye msaada mkubwa ni Helena kwa vile yeye ndiye aliyeshika mpini. Toka tulipoanza
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mahusiano nilianza mipango ya chini chini ya kumtoa kaka yako huku Helena akionesha ushirikiano mkubwa. ?Kilichochelewesha ni kujipanga kwa umakini mkubwa kuhakikisha hakuna mtu atakayegundua siri yetu. Kingine kigumu kinatokana na kuogopa kama kaka yako ataonekana itakuwaje?? ?Mmh, hata mimi nachanganyikiwa ? ?Shija jambo hili tungewashirikisha watu wazima ingekuwa vizuri, kumbuka sisi ni watoto tunajua uchawi juujuu lakini kuna mambo mazito ya kichawi ambayo hatujafundishwa kwa vile umri wetu bado.? ?Lakini Sabina unafikiri suala hili kuna umuhimu wa kuwashirikisha watu wazima?? ?Shija huo ndio ugumu, tukiwashirikisha watataka kutumia nguvu na hapo ndipo tutakapompoteza kabisa kaka yako.? ?Sasa unafikiri tutafanya nini?? ?Hili jambo tutajipanga, ila kuna kitu nataka kukufundisha ili tusaidiane katika mpango wetu.? ?Kitu gani hicho?? ?Nikufundishe uchawi ili tuweze kumtoa kaka yako.? ?Mmh, nitaweza?? ?Kwani sisi tumewezaje?? ?Sabina naomba suala hilo tuachane nalo kwanza, siwezi na sitaki kujifunza uchawi.? ?Basi itabidi usiwe na haraka ili tujipange.? Tulijikuta tumefika sehemu yetu kama kawaida bila kujijua kutokana na mazungumzo, tulikaa kule mpaka muda wa kukaribia kurudi wazazi wetu shamba. Usiku wa siku ile ulikuwa mzito sana kwangu kuwaza mateso mazito niliyoyaona kwa misukule akiwemo kaka yangu. Nilijiuliza kama kaka yangu anapendelewa yuko vile, wasiopendelewa wapo katika hali gani? Nilijiuliza dunia wanayoishi watu wale ni ipi tofauti na ya kwetu? Kingine kilikuwa nyumba niliyoingia ilikuwa ndogo lakini baada ya kujipaka dawa lilikuwa jumba kubwa kama godauni la kiwanda. Katika watu niliowaona wachache niliwafahamu ila wengi walikuwa wageni. Kingine kilichonistaajabisha ni mchanganyiko wa rangi wa misukule niliyoiona ilikuwa ya Wazungu, Waarabu, Wahindi na Wasomali; wote walikuwemo na kufanya kazi kama punda. Kilichonifanya nijiulize kama kule wapo vile kwa kina Sabina pako vipi japo sikupenda kumuuliza swali kama lile. Siku ya pili nilikutana Sabina shuleni ambaye alionekana kujitahidi kunichangamsha muda wote mwalimu alipokuwa nje ya darasa. Muda mwingi nilifikiria hatma ya vitu vilivyokuwa mbele yangu kutokana na kulazimishwa kuitunza siri ambayo kwangu ilikuwa nzito kama kumeza mfupa. Muda mwingi darasani nilipokuwa peke yangu nilihama kimawazo kutokana na msongo mkubwa wa mawazo. Lakini sikuwa na jinsi, nilikubali kuificha siri huku nikijiuliza nitawezaje kumpata kaka yangu. Muda wa kutoka shule Sabina na Helena walinifuata. Nilimshangaa Helena kunipa pole, nilishindwa kuelewa pole ile ililenga kitu gani. ?Pole Shija.? ?Pole ya nini Helena?? ?Kwa yote uliyoyaona , lakini nakuhakikishia kila kitu kitakwenda kama alivyokueleza Sabina.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
?Yapi tena hayo Helena?? ?Shija hii si sehemu ya kuyazungumzia haya twende sehemu yetu,? Sabina aliingilia kati mazungumzo. Tuliacha njia ya kwenda nyumbani na kuingia kwenye pori na kwenda sehemu yetu ya kila siku chini ya mti kuendeleza mazungumzo yetu. Tulipofika tulikaa chini ya mti, Sabina alikuwa wa kwanza kuzungumza. ?Sasa tunaweza kuendelea.? ?Ehe, Helena ulikuwa unanipa pole ya nini?? nilimuuliza. ?Kuhusu kaka yako, najua kiasi gani umeumia baada ya kumuona hai kaka yako. Shija, si mimi ni wazazi wangu walikuwa na ugomvi mzito na familia yenu ambao umekuwa ukitengeneza kisasi ambacho ninyi hamjui lakini mama na washirika wake wamekuwa wakiiandama familia yenu kila kukicha.? ?Nashukuru kusikia hivyo , hata hivyo nashukuru kwa msaada wako mkubwa wa kumtunza kaka yangu katika mazingira magumu kama yale.? ?Shija nina mipango mikubwa kuhakikisha kaka yako tunamtoa salama.? ?Sabina aliniambia.? ?Basi nakuomba suala hili ulifanye siri usimwambie mtu ukifanya hivyo utakuwa umeharibu kila kitu.? ?Helena nina siri nyingi nzito moyoni mwangu lakini bado zitaendelea kuwa siri mpaka hapo Mungu atakapochukua uhai wangu,? nilimhakikishia Helena kuificha siri ile. Sabina aliamua kubadili mazungumzo ambayo yalituhamisha katika mambo ya kichawi, tulijikuta tukicheka pamoja na kusahau majonzi ya muda mfupi juu ya kifo chenye utata cha kaka yangu kumbe bado yu hai. Jioni ilipotimu tulirudi wote na tulipofika njia panda tuliagana na mimi kurudi nyumbani na wao kuelekea makwao, kwa vile muda ulikuwa bado na giza ndiyo kwanza lilikuwa linaanza kuingia nilipitia dumu kufuata maji kisimani. Njia nzima nilikuwa peke yangu, niliamini pengine ilikuwa ni kutokana na muda wenyewe kuwa umekwenda, watu wengi walikuwa wamechota maji mapema. Hali ile ilinifanya nikute maji mengi, bila kuchelewa nilichota maji kwenye dumu na kujitwisha kichwani ili nirudi nyumbani. Wakati nanyanyua dumu niondoke nilishtushwa na sauti toka nyuma yangu. ?Shija,? sikuitikia mara moja niligeuza shingo nimuangalie aliyeniita. Kumbe alikuwa mzee Manoni akiwa na mkongojo wake mkono wa kushoto alikuwa na majani mabichi. ?Shikamoo mzee Manoni.? ?Marahaba, hujambo Shija?? ?Sijambo.? ?Naona unachota maji.? ?Ndiyo mzee wangu.? ?Eti jana nilipokuoneni na Sabina mlikuwa mnatoka wapi?? ?Tulikuwa tunatembea tu.? ?Bado hujanijibu swali langu, mlikuwa mnatoka wapi?? ?Kutembea.? ?Mmh, una uhakika na ukisemacho?? Swali la mzee Manoni lilinitia mashaka kidogo, sikujua alitaka nimjibu nini. ?Mzee Manoni kwani vipi, mbona unaniuliza hivyo ?? ?Nyumbani kwa kina Helena mlikwenda kufanya nini ikiwa wenyewe hawapo?? Mmh, niliona tumeumbuka na siri yote ilikuwa nje, lakini sikutaka kumjibu kwa kuamini huenda anajua kila kitu.?Yapi tena hayo Helena?? ?Shija hii si sehemu ya kuyazungumzia haya twende sehemu yetu,? Sabina aliingilia kati mazungumzo. Tuliacha njia ya kwenda nyumbani na kuingia kwenye pori na kwenda sehemu yetu ya kila siku chini ya mti kuendeleza mazungumzo yetu. Tulipofika tulikaa chini ya mti, Sabina alikuwa wa kwanza kuzungumza. ?Sasa tunaweza kuendelea.? ?Ehe, Helena ulikuwa unanipa pole ya nini?? nilimuuliza. ?Kuhusu kaka yako, najua kiasi gani umeumia baada ya kumuona hai kaka yako. Shija, si mimi ni wazazi wangu walikuwa na ugomvi mzito na familia yenu ambao umekuwa ukitengeneza kisasi ambacho ninyi hamjui lakini mama na washirika wake wamekuwa wakiiandama familia yenu kila kukicha.? ?Nashukuru kusikia hivyo , hata hivyo nashukuru kwa msaada wako mkubwa wa kumtunza kaka yangu katika mazingira magumu kama yale.? ?Shija nina mipango mikubwa kuhakikisha kaka yako tunamtoa salama.? ?Sabina aliniambia.? ?Basi nakuomba suala hili ulifanye siri usimwambie mtu ukifanya hivyo utakuwa umeharibu kila kitu.? ?Helena nina siri nyingi nzito moyoni mwangu lakini bado zitaendelea kuwa siri mpaka hapo Mungu atakapochukua uhai wangu,? nilimhakikishia Helena kuificha siri ile. Sabina aliamua kubadili mazungumzo ambayo yalituhamisha katika mambo ya kichawi, tulijikuta tukicheka pamoja na kusahau majonzi ya muda mfupi juu ya kifo chenye utata cha kaka yangu kumbe bado yu hai. Jioni ilipotimu tulirudi wote na tulipofika njia panda tuliagana na mimi kurudi nyumbani na wao kuelekea makwao, kwa vile muda ulikuwa bado na giza ndiyo kwanza lilikuwa linaanza kuingia nilipitia dumu kufuata maji kisimani. Njia nzima nilikuwa peke yangu, niliamini pengine ilikuwa ni kutokana na muda wenyewe kuwa umekwenda, watu wengi walikuwa wamechota maji mapema. Hali ile ilinifanya nikute maji mengi, bila kuchelewa nilichota maji kwenye dumu na kujitwisha kichwani ili nirudi nyumbani. Wakati nanyanyua dumu niondoke nilishtushwa na sauti toka nyuma yangu. ?Shija,? sikuitikia mara moja niligeuza shingo nimuangalie aliyeniita. Kumbe alikuwa mzee Manoni akiwa na mkongojo wake mkono wa kushoto alikuwa na majani mabichi. ?Shikamoo mzee Manoni.? ?Marahaba, hujambo Shija?? ?Sijambo.? ?Naona unachota maji.? ?Ndiyo mzee wangu.? ?Eti jana nilipokuoneni na Sabina mlikuwa mnatoka wapi?? ?Tulikuwa tunatembea tu.? ?Bado hujanijibu swali langu, mlikuwa mnatoka wapi?? ?Kutembea.? ?Mmh, una uhakika na ukisemacho?? Swali la mzee Manoni lilinitia mashaka kidogo, sikujua alitaka nimjibu nini. ?Mzee Manoni kwani vipi, mbona unaniuliza hivyo ?? ?Nyumbani kwa kina Helena mlikwenda kufanya nini ikiwa wenyewe hawapo?? Mmh, niliona tumeumbuka na siri yote ilikuwa nje, lakini sikutaka kumjibu kwa kuamini huenda anajua kila kitu. Nilitulia ili aamue anachotaka kuamua, nilijikuta nikipata ujasiri wa ajabu na kuwa tayari kwa lolote toka nilipomuona kaka yangu yupo hai tukijua familia nzima amekufa. ?Shija najua kila unalofanya naomba uniambie ukweli.? ?Mzee Manoni kila ninalofanya unalijua sasa nikuambie nini?? Nilitulia ili aamue anachotaka kuamua, nilijikuta nikipata ujasiri wa ajabu na kuwa tayari kwa lolote toka nilipomuona kaka yangu yupo hai tukijua familia nzima amekufa. ?Shija najua kila unalofanya naomba uniambie ukweli.? ?Mzee Manoni kila ninalofanya unalijua sasa nikuambie nini?? ?Sasa sikiliza tena sikiliza kwa makini, unachokifanya sasa hivi ni sawa na kuchezea sharubu za Simba. Una bahati moja kubwa unayoyafanya kwa sasa nimekuwa nafahamu peke yangu. Lakini ukijulikana kwa wenyewe ujue jina lako litabakia historia midomoni mwa watu. ?Nataka nikuambie kitu kimoja kuwa maisha yako kwa sasa yapo mkononi mwangu, siku nikiyaachia utafutika kama vumbi kwenye upepo mkali, kuna watu hawalali kwa ajili ya kukupoteza katika tumbo la dunia. Lakini nimekuwa mtetezi wako mkubwa, sasa nakuonya kuanzia leo achana kabisa kufuatilia nyendo hizo ni hatari itakayoweza kukupoteza. ?Huwezi kuuchunguza uchawi, kumbuka hao wanaokudanganya uwezo wao ni mdogo sana hawajui lolote katika uchawi hivyo . Ninachokuomba mnachokipanga muda huu kitakupoteza, wenzako mama zao wana nguvu ya giza mwenzangu na mimi utafanya nini zaidi ya kupotea?? ?Mzee Manoni inauma sana kujua mtu amekufa kumbe anatumikishwa kazi.? ?Ndio maana nikakueleza uachane na tabia za kuchunguza uchawi utajikuta siku moja unawaona wazazi wako nao wachawi utafanya nini?? ?Mzee Manoni ina maana baba na mama ni wachawi ?? ?Sijasema hivyo ila ukichunguza sana utakujapata majibu usiyotegemea.? ?Sasa mzee Manoni utanisaidia vipi kuhusu kaka yangu?? ?Kwani wale wasichana walikueleza nini juu yangu?? Nilijua swali lile lilikuwa la mtego, sikutaka kumjibu zaidi ya kumdanganya. ?Siwajawahi kukuzungumzia nao lolote linalo kuhusu, kwanza hawajui kama mimi na wewe tuna ukaribu.? ?Vizuri, sasa nakuomba kitu kimoja, kila ulichokiona na kukisikia kiache kama kilivyo na ibaki kuwa siri yako, najua upo katika kipindi kigumu lakini jitahidi kukishinda, hiki ni kipindi cha mpito kitapita tu wala usisumbue akili yako. ?Sawa mzee Manoni nitafanya hivyo .? Niliagana na mzee Manoni na kurudi nyumbani kuwahisha maji huku nikizidi kuwa katika wakati mgumu wa karipio la mzee Manoni juu ya mpango wetu wa kumtoa kaka yangu katika hali ya umsukule.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipofika nyumbani niliona kichwa kitapasuka kwa mawazo kutokana na vitu vyote vilivyokuwa vikinitokea vyenye maswali yasiyo na majibu. Nilijikuta nikishindwa nifanye nini kutokana na onyo la mzee Manoni kuwa niachane na mpango niliopanga na kina Sabina wa kumtoa kaka yangu kwenye umsukule, nilijiuliza kajuaje yote niliyofanya na Sabina bila yeye mwenyewe kuwepo zaidi ya kutuona kwa mbali. Lakini kitu kimoja kilinishangaza, ni kutoniuliza kuhusu safari yangu ya kwenda ziwani na Sabina kumuona kaka yangu. Sikutaka kuumiza sana kichwa niliiacha siku ile ipite ili siku ya pili nikawasimulie kina Sabina japo mzee Manoni alinikataza chochote nitachosikia au kuona nisimwambie mtu. Niliona kuna umuhimu wa kuanza kukaidi baadhi ya vitu alivyonikataza baada ya kuona vilikuwa havinisaidii zaidi ya kunikandamiza. Suala lililonijaza ujasiri lilikuwa la kumkomboa kaka yangu, niliamini kwa mtindo ule siwezi kumsikiliza. Sabina na Helena kwa kipindi kile walikuwa watu muhimu sana kwangu, niliapa kutomsikiliza mpaka nimpate kaka yangu. Siku ya pili nilikwenda shuleni kama kawaida, nilipofika nilikutana na Sabina na Helena ambao nyuso zao muda wote zilijaa furaha kila waliponiona. Kipindi cha mapumziko walinivuta pembeni kuzungumza, ilionesha walikuwa na jambo zito lililowasumbua akili zao. Baada ya kukaa sehemu ya peke yetu, sehemu iliyokuwa salama kwetu Sabina kama kawaida alianza kuzungumza. ?Shija kuna kitu tunataka kukueleza lakini kisikuvunje moyo, tunakuhakikishia japo sisi wasichana wadogo tutatimiza tulichokuahidi.? ?Kwani kumetokea nini?? ?Si huyu mzee Manoni eti anatutisha!? maneno ya Sabina yalinipa picha nzima ya kauli za jana yake za mzee Manoni kuwa nisiwasikilize wao. ?Kawatishia nini tena?? ?Eti tusimtoe kaka yako kwenye umsukule na kutuonya tukijaribu atatuchukulia hatua kali.? ?Mmh, jamani hamuoni tuna kazi nzito?? ?Ni kweli lakini tunataka kukuhakikishia mzee Manoni ni wa kawaida, kuwa mkuu wa wachawi wa kanda wala kusikutishe kile cheo kwani kuna wachawi wenye nguvu kuliko yeye .? ?Kwa hiyo mnaniambia nini?? ?Wewe tulia kila kitu tutakifanya tena haraka tofauti na tulivyopanga .? ?Lakini nataka kuwaeleza kitu kimoja mzee Manoni ana uwezo mkubwa wa kujua tunapanga nini, hivyo atatuvurugia kabla hatujafanya.? ?Ujanja huo autoe wapi?? Sabina alibisha. ?Mbona juzi alijua tuliingia ndani kumuona kaka japo alituona tukiwa nje.? ?Ndivyo alivyokwambia ?? Sabina alikuja juu. ?Ndiyo, amekuwa akifuatilia mambo yangu na kunieleza kila kitu.? ?Helena, mzee Manoni muongo huyo hana lolote mzee yule sema tu humjui, lakini hajui lolote. Ya juzi alinibana na kunitishia kunishtaki kwa mama ndipo nilipomwambia kuwa tulikwenda kumuona kaka yako. Alinikanya nisifanye tena kitendo kama kile.? ?Kumbe, mbona amesema anajua mambo mengi bila yeye kuwepo.? ?Hana lolote, tena mzee yule simpendi kweli,? Helena alisema kwa hasira. ?Sasa kama mambo yetu yapo nje namna hiyo hamuoni hatuwezi kufanya jambo lolote?? ?Nakwambia hivi yule mzee hana lolote kwanza maisha yake ya kubabaisha, haishi nyumbani kwetu kuomba misaada mbona hana misukule wa kumlimia?? ?Kwa hiyo mnaniambia nini?? ?Hiyo kazi ya kumtorosha tutaifanya kesho usiku wa mapema kabla hawajaingia kwenye kazi yao.? ?Lakini hamuoni kama ni haraka sana kumtoa tutampeleka wapi?? ?Mmh, na kweli,? alisema Sabina. ?Kwa hiyo tutafanyaje?? ?Kweli huu mtihani, Shija una nduguyo ili tukimtoa tumkimbizie huko?? Helena aliuliza. ?Kama hivyo basi zoezi hili tusimamishe mpaka nitakapokwenda Mwanza kwa mjomba.? ?Basi jitahidi mwisho wa wiki hii uende,? Helena alisisitiza. ?Lakini bado sijui kama nitapewa ruhusa na baba.? ?Kwani si utamwambia unakwenda kumsalimia.? ?Mmh, sijui; hata nauli pia sina.? ?Nauli tutakuchangia, au sio Sabina. ?Nauli usiwe na wasi? ?Basi niachieni kazi hiyo.? Wakati huo kengele ilikuwa imekwishalia kuashiria muda wa kurejea madarasani umewadia. Tulirudi darasani wote. Masomo yaliendelea kama kawaida huku nikishangazwa na ujasiri wa wasichana wale wawili , kila dakika moyo wangu ulijikuta ukijaa kiburi na kuwa tayari kwa lolote. Sabina na Helena pamoja na vitisho bado hawakurudi nyuma katika mpango wao wa kunisaidia kumrudisha kaka yangu, jioni tulipotoka tulikubaliana waniletee nauli niende Mwanza kwa mjomba nikamweleze ampokee kaka. Tulikubaliana kwa pamoja kwa wao kusubiri baba atasemaje kuhusu safari ya kwenda Mwanza kwa mjomba aliyekuwa akikaa Ilemela. Usiku wa siku ile nilikuwa na wakati mgumu sana kumuomba baba ruhusa ya kwenda mjini kwa mjomba. Siku ile sikuweza, kwani moyo wangu ulikosa ujasiri wa kukabiliana na baba na kuamua kuiacha siku ile ipite. Siku ya pili tulipokutana shule walikuwa na hamu kujua baba amenijibu nini juu ya ombi langu la kwenda Mwanza kwa mjomba. Niliwaeleza jambo lile halikutakiwa kulifanyia haraka kwa vile kulikuwa na siku zingine mbili kabla kufika siku ya mapumziko ya mwisho wa wiki. Wenzangu walikuwa wamejiandaa walinipa nauli ya kwenda na kurudi na pesa ya kula njiani japo kutoka kwetu mpaka Mwanza haizidi dakika 45. Niliipokea ile pesa na kuwaahidi jioni ya siku ile nilipanga kumuomba baba ruhusa japo sikuwa na uhakika wa kuruhusiwa. Lakini Helena alinipa wazo. ?Shija yule wa Mwanza ni mjomba wako?? ?Ndiyo.? ?Wa toka nitoke na mama yako?? ?Ndiyo.? ?Sasa fanya hivi muombe ruhusa mama yako kuwa unakwenda kumuona mjomba wako, lazima atakubali hata kukuombea hurusa kwa baba yako.? ?Wanaweza kukubali wakiniuliza nauli nitawajibu nini?? ?Waeleze kuna mwanafunzi wenzio naye anakwenda Mwanza atakulipia.? ?Mmh, nitajaribu.? Baada ya kunipa mbinu zile ambazo bado niliziona nyepesi sana kwangu, niliamua kujaribu ili nijue wazazi wangu wataamuaje. Kama wangekataa nisingekuwa na jinsi. Usiku ya siku ile baada ya chakula nilimfuata mama jikoni alipokuwa akisugua mwiko baada ya kuusongea ugali. ?Unasemaje Shija?? ?Mama nilikuwa naomba kwenda kwa mjomba Mwanza Jumamosi.? ?Mmh, leo umemkumbuka mjomba wako?? ?Ndiyo mama ni muda mrefu sana sijamuona.? ?Mmh, wazo zuri lakini sijajua baba yako ataamua nini.? ?Basi niombee ruhusa Jumamosi niende ili nirudi jumapili jioni kuwahi shule.? ?Basi nikimaliza kazi hii nitakuombea ruhusa.? Niliachana na mama na kuelekea chumbani kwangu kulala.?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku ya pili kama kawaida baba aliniamsha niwahi shule, wakati nanawa uso baba alinifuata na kuniuliza. ?Eti unataka kwenda mjini kwa mjomba wako?? ?Ndiyo baba, nimemkumbuka sana.? ?Umemkumbuka au umekumbuka kuangalia tivii.? ?Walaa.? ?Sasa ni hivi kuna pesa ipo kwa Ng?wana Maria akinipa nitakupa nauli.? ?Hata kama ukikosa, John anaelekea mjini katumwa na baba yake amesema kama nitataka kwenda atanilipia nauli, alichosubiri ni ruhusa yako.? ?Ruhusa umepata tena kanipunguzia mzigo, imekuwa vizuri nami nilikuwa na wazo la kwenda kwa mjomba wako aliniahidi kunipa pesa za kulimia hivyo imekuwa vizuri wewe kwenda.? ?Nashukuru baba.? Niliachana na baba na kwenda kubadili nguo kisha kuwahi shule, njia nzima nilikuwa mtu mwenye furaha. Sabina kama kawaida nilimkuta akinisubiri. ?Shija za asubuhi?? ?Nzuri.? ?Hata mimi naona nzuri.? ?Kwa nini?? ?Uso wako leo unaonesha furaha tofauti na siku mbili zilizopita.? ?Baba amenipa ruhusa.? ?Amekupa nauli?? ?Aliniambia kuna pesa anamdai Ng?wana Maria kama akimlipa atanipa.? ?Asipompa.? ?Nilimueleza kama mlivyonieleza .? ?Alisema nini?? ?Alinikubalia.? ?Sabina.? Sauti toka nyuma yetu ilitufanya wote tugeuke, alikuwa Helena ambaye alionesha anakuwa akikimbia kutokana na jasho kumtoka kwa mbali. ?Vipi shoga ulichelewa?? Sabina alimuuliza Helena. ?Mmh, shoga weee acha jana kidogo tuumbuke.? ?Kivipi?? ?Jana si tuliifuata ile nyama.? ?Ehe.? ?Basi amini usiamini, ngoma ilikuwa nzito mpaka saa kumi na nusu ndio tumetoka makaburini na nyama hatukupata. Basi hapa nilipo nina usingizi sijui kama nitasoma vizuri.? ?Ukizidiwa si unasingizia unaumwa tu ili urudi nyumbani.? ?Nikizidiwa nitafanya hivyo .? Wakati wote nilikuwa kimya nikiwasikiliza wachawi hao watoto wakizungumza. Tuliingia eneo la shule na kubadili mazungumzo. Tulihesabu namba na kutawanyika kwenye maeneo yetu kufanya usafi. Baada ya usafi tuliingia darasani. Jioni kama kawaida tuliondoka wote na kuwaeleza ombi langu kwa baba alivyolikubali bila pingamizi lolote. Sabina na Helena walifurahi sana kusikia vile, tulipanga kuifanya ile kazi baada ya majibu ya mjomba kukubali kumpokea kaka yangu ambaye hata yeye anaamini alikwishakufa na kumzika. Siku zilikatika huku nikiendelea kuwa karibu ya Sabina na Helena, mwisho wa wiki nilielekea Mwanza kwa mjomba. Nilifika Mwanza salama salimini na kupokelewa na mjomba ambaye alikuwa akinipenda sana. Pamoja na kupewa kila kitu huku nikikutana na vitu ambavyo huwa navikosa ninapokuwa kijijini. Moyo wangu ulikuwa katika wakati mgumu wa kumueleza mjomba ili anielewe kitu ambacho ataona ni cha kusadikika. Siku niliyofika niliiacha ipite sikuzungumza lolote zaidi ya kucheza na watoto wa mjomba ambao usiku walikuwa wakijisomea. Kutokana na uwezo wangu mkubwa darasani walikuwa wananiomba niwafundishe masomo yanayowashinda . Kitendo kile kilifanya mjomba afikirie kunihamishia kwake ili niwe karibu na watoto wake katika masomo. Siku ya pili ambayo ilikuwa Jumapili nilipiga moyo konde na kumwita mjomba pembeni kabla hajatoka kwenye mizunguko yake ya kawaida. Baada ya kunikubalia kunisikiliza tulisogea pembeni ili tuzungumze kwa siri. ?Mmh mjomba, una lingine au la kutumwa na baba yako?? mjomba aliniuliza. ?Kuna lingine lililonileta.? ?Lipi hilo tena mjomba?? ?La kuhusu kaka Luhemeja.? ?Luhemeja, amefanya nini tena, si ameishakufa?? ?Ni kweli sote tunajua amekufa.? ?Sasa una habari gani kuhusu marehemu kaka yako?? ?Mjomba kaka hajafa.? ?Hajafa! Yupo nyumbani?? ?Hapana.? ?Yupo wapi?? ?Alichukuliwa na wachawi .? ?Wachawi! Wewe umejuaje?? Nilimueleza yote niliyokutatana nayo na yote niliyoelezwa na Sabina na Helena mpaka kumuona kaka yangu kwa macho yangu mawili na mpango niliopanga na kina Sabina wa kumtoa kwenye umsukule.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilionekana kama mjomba alinisikia nikizungumza lakini hakunielewa, baada ya kunitazama kama ananishangaa aliniita jina langu. ?Shija.? ?Naam mjomba.? ?Akili zako zipo sawa?? ?Tena timamu.? ?Uliyozungumza muda mfupi umeyaona au umeota?? ?Nimeyaona kwa macho yangu, na sababu ya kuja huku ni kuja kukuomba tukimtoa kaka nije nimfiche huku.? ?Mmh, wazazi wako wanajua?? ?Hakuna hata mmoja nyumbani anayejua siri hii, kuitoa siri hii ni kuvunja masharti ya mkuu wa kanda ya uchawi mzee Manoni kuwa nisimwambie mtu kuhusu kila kitu cha ajabu nitakachokiona au kusikia.? ?Mmh, huu mtihani, kwa nini hukumwambia baba yako?? ?Naamini kabisa baba nikimwambia kutakuwa ugomvi mzito ambao lazima utasababisha kumpoteza kabisa kaka na mimi kujiweka kwenye wakati mgumu.? ?Sasa itakuwaje kama ukimleta huku wazazi wako wasijue?? ?Mjomba watajua baadaye, la muhimu nimtoe kaka kwenye dunia ya wafu.? ?Mmh, sawa lakini lazima nizungumze na shangazi yako.? ?Mjomba naomba iwe siri kwanza.? ?Itakuwa siri, lazima ajue nini kitafuata asije akatimua mbio.? ?Sawa, lakini asijue mtu yeyote zaidi yetu.? ?Basi wacha nikazungumze naye kisha nije nikusindikize uwahi kwenu kabla ya usiku haujaingia.? Mjomba aliniacha nje na kwenda kuzungumza na mkewe, nilisubiri jibu la shangazi ataamua nini baada ya kuelezwa ninachokikusudia. Mara alirudi mjomba ameongozana na shangazi. Shangazi alipofika aliniuliza. ?Wee Shija una uhakika na unachokisema?? ?Nina uhakika shangazi.? Nilimueleza kwa kifupi mikakati yetu na wenzangu, baada ya kunisikiliza alishusha pumzi ndefu na kusema. ?Mmh sawa, tupo tayari kama utamleta, unasema ulimuona vipi hali yake?? ?Hajambo kiasi.? ?Wanasema msukule huwa na kucha ndefu na nywele zisizo chanwa?? ?Ni kweli kaka ana nywele na makucha marefu.? ?Sasa utampitishia wapi katika hali hiyo lazima watu watakushangaeni?? ?Tumejiandaa kumuogesha, kumnyoa nywele na kumbadili nguo kabla ya kumpandisha gari.? ?Sawa, kama unasema kweli mlete tumuone.? Baada ya makubaliano na mjomba yaliyokwenda vizuri, mjomba alinipa mzigo wa baba na kunisindikiza kituo cha daladala ambako nilipanda hadi mjini na kurudi zangu nyumbani. Nilifika nyumbani majira ya saa moja usiku, baba aliponiona cha kwanza kuniuliza kilikuwa mzigo wake, nilimpatia pesa zake akafurahi pia zingine nilimpa mama nilizopewa na kaka yake. Usiku wa siku ile niliona kama unachelewa kutokana na kuwa na hamu ya kuonana na akina Sabina kuwaeleza majibu ya mjomba. Siku ya pili nilikwenda shule na kukutana na Sabina aliyekuwa na Helena wakinisubiri. Waliponiona walifurahi, hata bila ya salamu waliniuliza. ?Vipi ulienda kwa mjomba wako?? Sabina aliniuliza katika uso wa shauku la kujua nini kinachoendelea. ?Ndiyo.? ?Vipi imekuwaje?? Helena naye aliuliza. ?Imekwenda vizuri.? ?Usituambie!? walisema kwa pamoja. ?Mjomba amekubali.? ?Shija au unatudanganya?? Niliwaeleza yote niliyozungumza na mjomba. ?Kama ndiyo hivyo basi Ijumaa tutaifanya kazi hii,? Helena alisema. Tulikubaliana kuifanya kazi ya kumtorosha kaka siku ya Ijumaa usiku. Helena alituahidi kutengeneza mipango kwa umakini mpaka siku ya Ijumaa, ibakie kazi ya kumtorosha. Helena na Sabina walinieleza niandae nguo za kumbadili baada ya kumtoa na kwenda kumuosha na kumnyoa nywele . Mipango ilipangwa vizuri na kutia matumaini ya kumpata kaka yangu akiwa hai. Kila siku tulipokutana Helena alitueleza maendeleo yake katika kuhakikisha mpango unakwenda vizuri bila kikwazo chochote Siku ya Ijumaa tulikutana saa moja usiku sehemu tuliyopanga kukutana. Nilizibeba nguo za kaka ambazo tulipanga avae baada ya kumtoa kwenye umsukule. Tulipokutana Helena alitueleza mambo yamekwenda vizuri sana anasubiri giza lichanganye aweze kumtoa. Tulipanga kwenda kumuosha kwenye mto uliokuwa kwenye mpaka na kijiji cha pili kisha tuelekee barabara kubwa ambayo haikuwa mbali kutoka pale. Kila dakika niliushangaa ujasiri wa ajabu waliokuwa wakiuonesha wasichana wale. Niliamini hata mimi natakiwa niwe na ujasiri ili nisiwaangushe, baada ya nusu saa Helena alikwenda kwao na kutuacha tumejificha sehemu iliyokuwa karibu na kwao. Tulisubiri kwa muda bila kumuona Helena akitokea, hivyo tulianza kuingiwa na wasiwasi na kuona mpango unaweza kushindikana. Baada ya nusu saa Helena alirudi peke yake. ?Vipi?? Sabina alimuuliza kwa sauti ya chini. ?Mmh, mambo magumu,? kauli ya Helena iliufanya moyo wangu ilipuke kwa mshtuko. ?Tatizo nini?? Sabina alimuuliza. ?Kila kitu kipo sawa mpaka kumuandaa, njia ninayotaka kumtolea kuna watu hivyo siwezi kumtoa kwa mbele, lazima tutaonekana.?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda unakwenda tutamtoa saa ngapi?? Sabina aliuliza. ?Wakati wowote wakiondoka tu namtoa.? ?Kwani kina nani? ?Yupo mzee Manoni na wazee wengine wawili .? ?Ooh, kila kitu kimeharibika,? Sabina alizungumza sauti ya kukata tamaa na kunivunja nguvu. ?Walaa, hajui lolote si nilikueleza mtu wa mizinga amekuja kuomba ugoro kwa mama, lakini inaonekana wataondoka muda si mrefu, anamsubiri mama ampe ugoro aondoke zake.? ?Sasa ataondoka saa ngapi si unaona tunachelewa muda unakwenda?? Wakati huo wingu zito lilikuwa limeanza kutanda angani kuonesha wakati wowote mvua kubwa ingedondoka. ?Jamani mvua si itaharibu kila kitu?? niliuliza. ?Shija usiwe na wasi mvua hii haiteremki.? ?Kivipi?? ?Nikiingia ndani nitaifunga hainyeshi.? ?Kama vipi nije nikusaidie umtoe mzee Manoni kwenye njia ili mimi nitoke na Luhemeja.? Sabina alisema. ?Ngoja nikacheki nikishindwa nitakufuata.? ?Fanya haraka muda unakwenda.? ?Hakuna tatizo.? Baada ya kuzungumza vile Helena aliondoka na kutuacha tukiwa tumejibanza, muda ulionesha unakimbilia saa tatu kutokana na kibaridi cha usiku kilivyokuwa kikizidi kutupiga. Tulimsubiri Helena kufikia hatua ya kukata tamaa ya kuona mpango ule hautafanikiwa . Nilijiuliza kwa muda ule hata tukimtoa bado tutakuwa na kazi ya kwenda kumuosha kisha tumfanyie usafi na wao kunisindikiza mpaka barabara kuu ya kuelekea Mwanza. Baada ya Helena kuchelewa tena Sabina aliamua kumfuata ndani na kuniacha peke yangu. Baada ya kuondoka woga ulinitanda kubaki peke yangu, niliona mambo yanazidi kuwa magumu. Sabina naye alipotelea huko na kuniacha na maswali yasiyo na majibu. Nikiwa katikati ya maswali yasiyo na majibu, nilishtushwa na sauti ya mzee Manoni na kunifanya nijisaidie haja ndogo bila kupenda. Mapigo ya moyo yalinienda kwa kasi na kujua nimekwisha, lakini ajabu kumbe alikuwa akipita huku akizungumza na mwenzake bila kuniona. Kiza ndicho kilichonisaidia kutoniona; alinipita karibu kabisa nilipokuwa nimesimama huku nimebana pumzi zangu. Zilipita dakika tano alikuja Sabina mbio huku akihema. ?Shija twende huku.? Alinishika mkono na kuanza kunivuta kuelekea kwenye giza kwa kuiacha njia na kuingia kwenye majani. ?Vipi mmemtoa?? nilimuuliza. ?Ndiyo.? ?Yupo wapi?? ?Ametangulia na Helena.? Kwa mbele niliona vivuli vya watu wawili nilipowasogelea niliwatambua, kweli alikuwa Helena na kaka yangu Luhemeja. ?Sasa jamani tusipoteze muda tufanye kila tuwezalo kabla jamaa hawajaingia kazini,? Helena alisema huku akihema kutokana na kukimbia na Luhemeja kutoka nyumbani kwao. Muda wote Luhemeja alikuwepokuwepo tu, tulishika njia ya bondeni kwenye mto kwenda kumuosha kaka. Tulipofika tulimuingiza majini na kuanza kumsugua kwa pamoja na sabuni waliokuja nayo. Ilionesha jinsi gani Helena na Sabina walivyokuwa wamejiandaa na mpango ule. Taratibu wingu lilianza kutawanyika na nuru ya mbali ilipatikana na kuweza kuonana. Baada ya kumsafisha tuliingia kwenye kazi ya kumnyoa nywele bila kuzingatia tunamnyoa vipi, cha muhimu kilikuwa kuzitoa nywele ndefu. Baada ya kuzitoa kwa kumnyoa bora-liende, Sabina na Helena walimkata kucha na kisha tulimvisha nguo. Kingine ambacho sikukitegemea kumbe Sabina aliiba kofia ya baba yake kwa ajili ya kumvisha Luhemeja. Baada ya kuhakikisha Luhemeja yupo katika hali nzuri, tulianza safari ya kuitafuta barabara kuu ili kutafuta usafiri wa kwenda Mwanza. Kwa muda ule niliamini ningepata gari lolote linalokwenda Mwanza. Kutoka eneo tulilokwenda kumsafisha kaka mpaka barabara kuu ya kutoka Musoma ilikuwa nusu saa. Tukiwa njiani Helena alimpaka dawa kaka kwenye utosi na nyingine alimlambisha na kumnusisha, Kaka alipiga chafya mfululizo baada ya chafya nilishangaa kumsikia akiuliza. ?Jamani mnanipeleka wapi?? ?Aah, kaka mimi Shija tunakupeleka kwa mjomba Mwanza.? ?Mmh, mtaweza?? aliuliza swali ambalo lilinishtua. ?Tutaweza,? alijibu Helena. Kauli yake ilifuatiwa na upepo mkali ulioambatana na wingu zito, haikuchukua muda mvua kubwa ilitelemka. Sabina na Helena walijitahidi kuizuia lakini iliwazidi nguvu iliendelea kunyesha kwa kasi ya ajabu. Nilimsikia Helena akisema. ?Mvua hii si bure lazima wameshtukia mchezo.?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sasa itakuwaje?? niliuliza. ?Hatuna jinsi, tuingie tu kwenye mvua tukiisubiri mpaka ikatike lazima watatupata, wametumia mvua ili kutuzuia tusifike mbali,? alisema Sabina huku akifuta maji usoni, kauli ile ilinivunja nguvu na kuona lazima nitakuwa katika wakati mgumu maishani mwangu kwa kuharibu kila sehemu. Nilikumbuka maneno ya mzee Manoni kwamba Sabina na Helena ni watoto tu hawawezi kitu chochote. Kila dakika mvua ilizidi kuongezeka ukali wa manyunyu yake ulifikia hatua ambapo matone yake yakimpiga mtu mwilini unahisi maumivu. Tulikubaliana kutembea na ile mvua kuelekea barabara kuu ambapo hakika ilinitia hofu kuhusu usalama wetu. Ukali wa mvua ulitufanya tusione tunapokwenda kutokana kunyesha kwa nguvu. Baada ya kuona kila hatua ilikuwa ni lazima mtu aanguke kwenye maji, tulikubaliana tusimame sehemu tusubiri mvua ikatike. Lakini Helena aligoma kwa kuamini tukisimama sehemu watu waliokuwa wanatufuata wangetukuta. Nilijiuliza watu hao wangetukuta wapi? Na kama walikuwa wametugundua niliamini hatukuwa na ujanja wa kufika popote kabla hawajatukamata. Tulikubali kuendelea na safari kwa shida huku mvua ikizidi kutunyeshea na kutufanya tuhisi maumivu makali. Tuliendelea mbele na kiza nacho kilizidi kutuchanganya. Kilichotokea muda ule sikuwahi kukiona katika maisha yangu. Mvua ilikuwa kali iliyoambatana na upepo mkali, na kiza kizito kilichokuwa hakielezeki kwa maneno. Nilitamani kulia lakini ajabu Sabina na Helena walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunaushinda mtihani ule. Niliamini maisha yetu yalikuwa kwenye hatari, lakini Sabina na Helena walionesha ujasiri muda wote kumnyanyua kaka kila alipoanguka. Kuna kipindi tulitumbukia kwenye shimo na kutoka bila kujua tulikuwa tunaelekea wapi, akili yangu ilinionesha kabisa tumeishakosea njia kutokana na kutembea muda mrefu kwenye mvua bila kufika. ?Jamani hatujapotea?? niliuliza. ?Shija si suala la kuuliza hii ni vita tujitahidi tu tutashinda,? Sabina alisema. ?Hatuna jinsi twendeni tu mpaka tujue mwisho wake,? Helena alisema kwa msisitizo. ?Na kweli tukikosea leo tumeharibu kila kitu,? Sabina aliongezea. Maneno yale yalinivunja nguvu na kuona tumeishauvaa mkenge kwa kuamini ubishi wa kina Sabina ndio uliotufikisha pale. Tuliendelea kutembea kwenye mvua kwa kuanguka na kunyanyuka . Kaka alikuwa amechoka kiasi cha kumshika na kumburuza kwa kutembelea magoti. ?Jamani niacheni mimi nimechoka,? kaka alilalamika. ?Luhemeja mateso yote haya ni kwa ajili yako jikaze, tunaweza kufika sehemu tukapona,? Helena alimueleza kaka ambaye alikuwa hoi kwa safari isiyo na mwisho . Si yeye hata mimi niliona aibu kusema nimechoka kwa vile kazi ile ilinihusu mimi. Niliuweka mkono wa kaka mabegani kwangu na kuanza kwenda naye huku mvua ikizidi kuwa kali sana, mbele kiza kilikuwa kizito cha kutisha. Baada ya mwendo mfupi tulishtukia wote wanne tukiangukia kwenye mto uliokuwa ukipeleka maji kwa kasi. Kila mmoja alipiga kelele kutetea nafsi yake. Kasi ya yale maji yalitupeleka kwa kutuburuza bila kujitetea. Kitu kibaya zaidi ni kwamba kulikuwa na kiza kizito ambacho kilitufanya tusione sehemu ya kuweza kujitetea kuyaokoa maisha yetu. Nikiwa napelekwa na maji nilimuomba Mungu aipokee roho yangu kwani sikuwa nafanya jambo isipokuwa kumtetea kaka yangu aliyekuwa mzima lakini akiishi maisha ya wafu. Ghafla nilihisi kupigwa na kitu kizito kichwani kilichonifanya nipoteze fahamu. Kilichoendelea sikukijua. Niliposhtuka nilijikuta nimefungwa chini ya mti mkubwa, sehemu ambayo wachawi hufanya mkutano wao. Sehemu hiyo haikuwa ngeni kwangu kwani niliishawahi kufika katika sherehe ya wachawi kwa njia ya ndoto iliyokuwa na ukweli . Pembeni yangu walikuwepo Sabina na Helena ambao nao walifungwa kama mimi. Chini alikuwa amelala kaka yangu akiwa amefungwa kamba huku akiwa amepigiliwa msumari mkubwa katikati ya kichwa na mwingine pembeni ya kichwa. Ilionesha kaka yangu alikuwa amekufa, na alikuwa katika vazi lile lile nililomchukulia nyumbani na kumvisha. Moyo uliniuma nikijua na mimi muda si mrefu nitamfuata kaka yangu, ila sikuamini kama Sabina na Helena nao wangenifuata nyuma yangu. Bado Sabina na Helena walinitia moyo hawakuonesha kutishika na adhabu ile. Mara lilitokea kundi la wachawi wakiwa wanatoka makaburini ambako walipata miili miwili ya watu ambayo siku hiyo ingeliwa nyama. Walikuja huku wakiwa wamebeba maiti za watu wawili waliokuwa kwenye sanda ambayo ilionekana mpya. Baada ya kuitua pale, mkuu wa wachawi mzee Manoni alisema: ?Nafikiri kazi imekwenda vizuri, ila kuna nyama imeongezeka kutokana na kiburi cha kitoto,? mzee Manoni alisema huku akinigeukia na kunitazama kwa muda kisha alisema: ?Shija nilikueleza usiingilie nguvu za watu utapotea sasa ona umesababisha kaka yako kugeuzwa kitoweo usiku huu.? ?Kwa nini na yeye asiliwe?? mchawi mmoja aliuliza. ?Shija hana kosa, hajui lolote kuhusu uchawi bali watoto wenu.? ?Lakini ameisha ua siri zetu lazima tumgeuze asusa leo,? mwingine alichangia. ?Bado hiyo haitoshi, wa kulaumiwa ni watoto wenu, Shija namjua vizuri.? ?Kwa hiyo na yeye ageuzwe msukule,? kauli ile ilinivunja nguvu na kujua Shija mimi nimekwisha. ?Hapana huyu haguswi na kitu chochote ila nataka akitoka hapa atoke akijua kaka yake hayupo tena wala asisumbuke kumtafuta. Leo atamshuhudia akiliwa nyama pamoja na maiti nyingine tulizo pata leo.? Baada ya kusema vile walimchukua kaka na kuanza kumkata vipande ambavyo waligawiana na kuanza kumla mbele yangu. Maumivu yalikuwa makali kuliko siku aliyokufa kwa kiini macho. Baada ya kumaliza kumla kaka yangu huku wakicheza ngoma, waligawana na maiti zingine mbili ambazo zilikuwa zimelazwa. Baada ya zoezi lile, nilifunguliwa pamoja na wenzangu Sabina na Helena na kupewa onyo zito. ?Shija leo itakuwa mwisho wangu wa kukutetea tena, ukifanya chochote kinyume na ninavyokueleza utayamaliza mwenyewe . Haya arudishwe kwao ili wazazi wake asubuhi wamkute chumbani kwake .? Baada ya kusema vile nilihisi kizunguzungu na usingizi mzito ulinipitia palepale nilipokuwa nimefungwa kamba, kilichoendelea sikujua
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sauti ya baba ilinishtua asubuhi, niliposhtuka nilijikuta nipo kitandani kwangu. Kabla ya kunyanyuka nilijawa na mawazo juu ya ndoto niliyoota, lakini akili yangu bado haikuamini kama ilikuwa ndoto bali kitu cha kweli. Bado sikutaka kuamini nilisubiri wazazi wangu waende shamba niende kwa kina Sabina kupata ukweli sikuwa na woga tena moyoni mwangu. Baada ya baba na mama kwenda shamba, mimi kiguu na njia kuelekea nyumbani kwao Sabina kutaka kuuliza kilichotokea jana kilikuwa ndoto au kweli. Kwa mbali niliwaona Sabina na Helena, walipofika cha kwanza kilikuwa kunipa pole. ?Pole Shija.? ?Ya nini?? ?Si ya kumpoteza kaka yako jana.? ?Mmh, hivi yaliyotokea jana ni kweli au ndoto?? ?Lazima utajua ilikuwa ndoto ulipoamka na kujikuta upo umelala kwenu, lakini kila ulichokiona ni kweli kabisa. Makosa yalikuwa muda tulichelewa sana ndiyo yaliyosababisha tumpoteze kaka yako.? ?Kweli, Shija nitajitahidi kukufundisha jinsi ya kukabiliana na wachawi najua sasa hivi watakutafuta kwa udi na uvumba wakuangamize.? ?Sasa jamani mjomba akiniuliza nitamjibu nini?? ?Mwambie hatukufanikiwa kwenda.? ?Na akitaka kutumia nguvu za dawa?? ?Hawezi kupata kitu zaidi ya kupata ukweli kuwa kweli kaka yako amefariki.? ?Mmh, sasa itakuwaje maana mpaka sasa hivi siamini kama wazazi wenu watataka muwe karibu yangu.? ?Yote hayo tuachie sisi, tunakuhakikishia kukulinda kwa nguvu zetu zote japo tunaonekana watoto, najua lililotokea jana kuna makosa tuliyafanya . Tulisahau kumfuta mhuri wa kichawi ambao uliwafanya watujue tupo wapi kwa urahisi, tumuachie Mungu,? Helena alinipa moyo. ?Nitashukuru.? ?Ila najua leo tuna kikao kizito kitachozungumzia kukushirikisha kuijua siri ya wachawi , lazima kuna mkakati mzito wa kukuondoa duniani kwa kifo au kukugeuza msukule. Lakini pia nguvu za mzee Manoni zinakulinda ila lazima uwe makini lazima watatumia ujanja ili wakutie adabu,? Sabina aliongezea. Tukiwa katikati ya mazungumzo mara Sabina na Helena walitimua mbio na kuniacha nimesimama peke yangu kama sanamu nisijue nini kinachoendelea. Wakati najiuliza wamekimbia nini nilimuona mzee Manoni akipita, ajabu baada ya kunisalimia alipita bila kuongeza neno lolote. Nilimsindikiza kwa macho mpaka alipopotea niligeuka na kuelekea nyumbani. Mbele nilikutana na kina Sabina. ?Vipi amekuuliza kitu?? ?Hataa, amenisalimia tu na kuendelea na safari zake.? ?Ooh, afadhali mzee yule mbeya kama mwanamke.? ?Kama angewaona?? ?Tumekatazwa kuwa karibu na wewe , kama angetuona angekwenda kuwaambia na lazima tungepewa adhabu kali.? ?Mmh, hamuoni vita yangu ni kubwa?? ?Ni kweli lakini tutajitahidi na udogo wetu kukulinda.? ?Basi jamani tutaonana baadaye maana kichwa kizito kwa usingizi pia kinaniuma sehemu niliyopigwa na kitu wakati tunapelekwa na maji.? ?Mmh, pole ngoja nikakuletee dawa,? Sabina alinieleza huku wakigeuka na kuelekea kwao nami nilirudi nyumbani kulala, kichwa kikizidi kubeba mambo mazito ambayo wazazi wangu hawakupaswa kujua. Wakati najiandaa kulala Sabina aliingia na kuniletea dawa ambayo alinipaka ilikuwa imechanganywa na mafuta ya ng?ombe. Baada ya kunipaka alinipa nyingine ya kunywa kisha aliniaga na kusema angerudi mchana kunijulia hali. Alipoondoka nilipitiwa na usingizi mzito sana. Usiku wa siku ile nikiwa katikati ya usingizi nilishtushwa na kishindo kizito ukutani. Nilishtuka na mapigo ya moyo yalinienda kwa kasi na kuanza kutetemeka. Sikuamini macho yangu kuuona ukuta ukipasuka na mwanga mkali ulinipiga usoni. Baada ya mwanga ule kunipiga ulinifanya nione kiza kizito mbele yangu, nilijitahidi kushindana na kiza kizito hicho mbele yangu. Baada ya muda niliweza kurudi katika hali ya kawaida kuizoea hali iliyokuwepo . Nje kulikuwa na mwezi mkali ulionifanya nione nje kupitia sehemu ya ukuta iliyopasuka. Woga ulinitawala nilijikunja ukutani kabisa pembeni ya kitanda huku nikijitahidi kuangalia ukuta ule umepasuka kweli au kiini macho. Mara niliwaona watu wanne waliokuwa uchi wakiingia chumbani kwangu. Nilinyanyuka kitandani na kupiga kelele ambazo zilipasua anga. Lakini kuna kitu chenye nguvu kali kiliniingia mdomoni na kuifunga sauti yangu. Wawili hao walinisogelea kitandani nilipokuwa nikifunua mdomo kupiga kelele ambazo zilikuwa hazitoki. Wakati wananivuta ili wanitoe nje, sauti ya mlango wa chumba cha wazazi wangu iliwashtua. Niliwasikia wakisema. ?Mambo yamekwisha haribika tuondokeni.? Baada ya kusema vile mmoja wao alifanya kama anaondoa kitu mdomoni kwangu ambacho sikukiona na kutoka mbio huku ukuta ukirudi katika hali yake ya kawaida.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ajabu sehemu ya kooni iliyokuwa imekauka iliachia na kuwa katika hali ya kawaida. Nikiwa bado natafakari kilichonitokea, mlango wangu uligongwa ukifuatiwa na sauti ya baba. ?Shija,? japo sauti ile ilikuwa ya baba bado sikuiamini kutokana na hofu nzito iliyokuwa moyoni mwangu. Sikuitikia mara moja mpaka baba aliporudia kwa sauti ya juu huku akiugonga mlango. Sauti ya mama ndiyo iliyonifanya niitikie na kufungua mlango. Nilimsikia mama akisema: ?Inawezekana anaota, turudi tukalale.? ?Mmh, kelele zile si za kawaida, ngoja kwanza aamke tumsikie. Nimewahi kusikia kelele nyingi lakini hizi zina jambo.? Baba alipogonga tena mlango huku akiita jina langu, niliitikia na kutoka nje. Kwa vile mwanga wa mwezi ulikuwa mkali nilimuona baba akinichunguza kabla ya kuniuliza kitu. Wa kwanza kuniuliza alikuwa mama. ?Shija eti umetokewa na nini?? ?Kwani vipi?? niliuliza. ?Baba Shija labda kelele zile si za Shija.? ? Hapana, Shija hebu tueleze nini kimekutokea?? Kabla ya kujibu nilijikuta nikifikiria masharti niliyopewa na mzee Manoni kuhusiana na kuitoa siri yoyote nje. ?Shija umetokewa na nini?? ?Baba ni ndoto tu.? ?Ndoto gani uliyoota?? ?Niliota nafukuzwa na simba ndio maana nilipiga kelele.? ?Basi rudi ukalale.? ?Hapana mume wangu huyu hawezi kulala tena peke yake tuingie naye ndani tukalale naye.? ?Wazo zuri.? Kimoyomoyo nilishukuru kuchukuliwa na wazazi wangu kwani niliamini kama ningelala peke yangu wachawi wale wangerudi kunichukua na sikujua walitaka kunipeleka wapi. Lakini nilikumbuka niliyoelezwa na kina Sabina kuwa uhai wangu unawindwa usiku na mchana baada ya kuzigundua siri za wachawi . Na lingine baya lilikuwa kutaka kumtorosha kama yangu na kuonekana nayajua mengi. Kutokana na kauli ya kina Sabina wachawi walipanga kumzunguka mzee mzee Manoni na kunitoa kafara. Niliwashukuru wazazi wangu nililala salama mpaka asubuhi. Kama kawaida baada ya wazazi wangu kwenda shamba Sabina na Helena kwa njia za siri walikuja nyumbani. Walipokuja walitaka kujua hali yangu, niliwaeleza yaliyonitokea usiku. ?Ha! Mungu wangu ndio maana nilisikia wakijilaumu kwa kosa walilofanya , sikujua kumbe walikuwa wamekufuata wewe .? ?Ina maana mtu waliomkosa alikuwa Shija?? Sabina alishtuka. ?Ndiyo mimi, msishangae siku moja mkaniona nimegeuzwa msukule nyumbani kwenu!? ?Haitatoke na ikitokea siku watakayokuingiza usiku asubuhi nakutoa na lolote wanifanye ,? Sabina alisema kwa msisitizo. ?Sabina tutafute njia ya kumsaidia Shija hali ni mbaya wamempania lazima watampata. Si unajua uwezo wetu si mkubwa kama tulivyofikiri .? ?Mmh, nimepata wazo? ?Lipi hilo?? ?Shija nenda kwa mzee Manoni mueleze ukweli yeye ndiye mwenye uwezo wa kukusaidia. Kama ukishindikana uhamie mjini kwa mjomba wako.? ?Basi ngoja nimalize mtihani wa mwisho nikiwa nasubiri majibu ya darasa la saba nihamie mjini.? ?Shija muda uliobakia si mkubwa sana, lakini watu wale hawaaminiki. Sasa hivi nawaogopa kama ukoma. Basi mtafute mzee Manoni ndiye mtu mwenye kukusaidia kwa sasa hivi.? ?Nitafanya hivyo .? ?Lakini kabla ya yote tutakupa dawa ambayo kila ukitaka kulala unajifunga mkononi, kila atakayekuja kwako hakuoni.? ?Basi kama dawa hiyo ipo hakuna haja ya kwenda kwa mzee Manoni.? ?Basi subiri.? Baada ya kusema vile Sabina alitimua mbio na kuniacha na Helena, kwa woga wa kuonekana tulijificha chumbani kwangu. Baada ya muda Sabina alirudi na kupande cha ngozi ambacho kilikuwa kimetobolewa na kuwekewa kipande cha uzi. Alipofika alikitoa; nilimuona Helena akishtuka. ?Sabina hii si kinga yako?? ?Ee, lakini kwa kipindi hiki lazima tumlinde Shija la sivyo tutampoteza.? ?Na wewe ?? ?Nitapata.? ?Sabina si unajua ngozi hii sasa hivi haipatikani?? ?Wakijua nimeipoteza watanipumzisha kwenye safari za hatari.? Nilimshukuru Sabina kwa jinsi alivyojitolea juu yangu na kuwa tayari kwa lolote ili kuhakikisha nipo salama. Baada ya kina Sabina kuondoka, nilifuta wazo la kwenda kwa mzee Manoni kwa kuangalia kile kipande cha ngozi cha kujifunga kwenye mkono. Baada ya muda Sabina alirudi peke yake, nilimshangaa na kumwuliza. ?Vipi mbona umerudi peke yako?? ?Shija kuna kitu nataka kukuambia lakini kisikutishe sana.? ?Kipi hicho?? ?Jichunge sana na Helena.? ?Kivipi?? ?Inaonekana bado anatumiwa na wachawi .? ?Kivipi?? ?Njia nzima alikuwa akinilaumu kukupa ngozi hii kwa kusema eti hata ukifa kuna hasara gani.? ?Wewe umemjibu nini?? ?Nimemwambie heri nife mimi kuliko wewe .? ?Yeye akasemaje?? ?Nimemwona kama kakosa raha, na wasiwasi huenda akawaeleza kuwa nimekupa kinga hii.? ?Sasa tutafanyaje?? ?Ndio maana nikasema usihofu, nitajua njia ya kufanya lazima nitamfanyia kitu kibaya.? ?Kipi tena Sabina?? ?Nitamuua.? ?Noo, usifanye hivyo , Sabina.? ?Hapana Shija, Helena sio mtu mzuri hata kidogo, ni rafiki yangu lakini ana roho mbaya sana.?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Roho yake mbaya nini?? ?Kuna wanafunzi aligombana nao ugomvi wa kawaida alipofika kwa mama yake waliwageuza , walikubaliana kuwageuza msukule na siku ya pili walikufa katika mazingira ya kutatanisha kama kaka yako mara ya kwanza.? ?Mmh, sasa kwangu roho yake mbaya ipi?? ?Shija nimezuia vitu vingi sana vya kukuangamiza kutoka kwa Helena alivyotumwa na kundi la wachawi lililokupania kukutoa duniani au kukugeuza msukule. Mara nyingi alikuwa akinishirikisha kwa kujua wewe ni mpenzi wangu lakini nilimgomea na kumpiga mkwara mzito kama angekugusa.? ?Sasa unaniambiaje? Maana kila kitu changu kwa Helena kipo wazi, lakini mbona alikuwa mstari wa mbele kunisaidia kumtoa kaka yangu?? ?Kwa shinikizo langu.? ?Kwa hiyo wasiwasi wako nini?? ?Wa kunizunguka, kwa hiyo tuwe naye makini sana naye.? ?Hakuna tatizo Sabina nimekuelewa.? ?Shija usifikirie utani utakuja kumbuka kauli zangu,? Sabina alionesha msisitizo juu ya kumshtukia shoga yake. Siku zote Sabina alioneka yupo mstari wa mbele katika kunipigania, nilijifikiria ujasiri gani uliomfanya kunifanyia yote yale kwa kuwa tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili yangu. Dawa na ngozi aliyoniletea Sabina vilinifanya nirudi katika hali ya kawaida, huwezi kuamini tukio la kushuhudia kaka yangu akiliwa nyama liliichanganya sana akili yangu na kunifanya nisiende shule kwa wiki nzima. Ila usiku nililala safi japo nilikuwa nikisikia vishindo vya watu wakiizunguka nyumba huku wakisema hawanioni kila walipoingia ndani. Walipokuwa wakija nilishtuka usingizini kutokana na vishindo huku miale ya moto ilitanda juu, baada ya vishindo ukuta hupasuka na kuwaona watu zaidi ya sita wakiingia ndani. Nilijikunyata ukutani kuogopa kuonekana, lakini kwa maajabu huondoka bila kuniona huku wakisema sionekani inawezekana siku hizi silali mle. Kila usiku kulikuwa na vishindo kuzunguka nyumba na kuingia ndani bila kuniona na siku ya pili nilipokutana na Sabina nilimueleza kuhusiana na vishindo vya usiku hata sauti za ukuta kupasuka na watu kuwaona wakiingia ndani lakini hawakuniona na kuondoka. ?Shija una vita nzito sana shukuru hiyo ngozi bila hiyo walikuwa na nia mbaya, ila nakuomba fanya mpango wa kumueleza mzee Manoni.? ?Nitafanya hivyo .? Nilizidi kumshukuru Sabina mara mia jinsi alivyoonesha kunijali na kuwa tayari kutoa uhai wake kwa ajili yangu. Dawa zake zilinisaidia sana kurudi katika hali ya kawaida kiasi cha kuweza kwenda shule kama kawaida. Niliweza kusoma shule kwa mazingira magumu kwa kumuogopa Mwalimu Vene na Helena japo Helena hakuonesha mabadiliko yoyote kwangu. Wasiwasi wangu mwingine niliamini huenda maneno ya kunitahadharisha na Helena yanatokana na wivu . Nilishindwa kuonesha kumbagua Helena kwa vile muda wote walikuwa pamoja. Masomo yaliendelea kama kawaida, miezi miwili kabla ya kufanya mtihani wa darasa la sana, nakumbuka siku hiyo Helena alikuja peke yake. Sikushangaa kwa vile na yeye alikuwa sehemu ya urafiki wetu pamoja na kuelezwa niwe naye makini. Helena alionesha uchangamfu kama kawaida kitu kilichozidi kunitoa hofu na kuamini maneno ya Sabina ni wivu tu. Tukiwa katika mazungumzo nilimuona Helena akikimbilia chumbani huku akinieleza Sabina akifika nisimwambie kama yupo pale. Baada ya muda mfupi Sabina alifika na kuniuliza. ?Shija, Helena kafika huku?? ? Sijamuona kwani vipi?? ?Nimepita kwao wamesema ameelekea huku.? ?Mmh, sijamuona,? nilimdanganya. ?Ni hivi....,? nilimwekea kidole mdomoni kumnyamazisha. ?Kuna nini?? aliniuliza kwa sauti ya kunong?ona. Nilimshika mkono na kumuondoa eneo la pale nyumbani ili tu Helena asisikie alichotaka kunieleza Sabina nilijua anaweza kuropoka. Sabina naye hakuwa mbishi alinifuata mpaka nje ya uzio wa nyumbani kwetu nyuma ya mti mkubwa wa mwembe. ?Vipi Shija kuna nani?? Sabina aliniuliza huku uso wake ukijaa shauku ya kujua kuna kitu gani kwani kitu kile hakikuwahi kutokea. ?Baba.? ?Ooh, wacha niondoke.? ?Anaondoka sasa hivi kuna kitu nilikuwa nimetumwa nikaona nipite mara moja.? ?Kwa hiyo?? ?Hebu subiri nikamtazame.? Nilimuacha Sabina nyuma ya mti na kurudi hadi nyumbani ili kumuondoa Helena kama bado yupo ndani. Nilipoingia ndani sikumkuta, nilizunguka nyuma ya nyumba vile vile hakuwepo. Niliamini ameisha ondoka, nilimwita Sabina kwa sauti kwa vile hakuwa mbali alinisikia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikuja kwa tahadhari, nilimtoa hofu. ?Ameishaondoka.? ?Mmh, niliogopa sana, hivi baba yako akinikuta hapa kwenu atasemaje?? ?Nitamwambia mwanafunzi mwenzangu ambaye nashirikiana naye darasani.? ?Mmh, haya.? ?Helena ulikuwa unamtafuta wa nini?? ?Nilikuwa na wasiwasi labda amefika huku.? ?Wasiwasi wa nini?? ?Si nilikueleza kuna kikao cha siri kuhusiana na wewe kuijua siri ya wachawi , basi kuna mpango mkubwa umepangwa kuhakikisha wanakufanyia kitu kibaya.? ?Na mzee Manoni yumo?? ?Wala hajui lolote, si ndiyo maana nilikueleza ukamueleze mapema.? ?Na ile ngozi haitanisaidia?? ?Itakusaidia, ndio maana nilikuwa na wasiwasi na Helena kuja hapa anaweza kuja na kukuibia ngozi hiyo na usiku wakija wakuchukue kirahisi.? Kauli ya Sabina ilinitisha sana na kunitia wasiwasi wa Helena kuingia ndani, niliogopa kumueleza ukweli kuwa Helena alifika na kuingia ndani. Lakini ilibakia siri yangu moyoni kuwa Helena alifika na kuingia chumbani kwangu. ?Mmh sawa, basi itabidi niende kwa mzee Manoni mapema,? nilimjibu huku wasiwasi wangu ulikuwa kwenye ngozi yangu niliyoiweka chini ya godoro. ?Kwa leo huwezi kumpata amekwenda katika kikao cha wachawi kinachofanyika Kasungamile, Geita, kurudi inaweza kuwa karibu na alfajiri.? ?Kwa hiyo itakuwaje?? ?Tumia hiyo kwa leo akirudi jitahidi kumuona la sivyo utapotea, uwezo wangu ni mdogo pia hata Helena amekuwa akinikimbia katika mambo yake.? ?Basi lazima tuwe naye makini.? ?Shija mi si mkaaji nilikuja tu ili kukueleza hili, ila kuwa makini sana na Helena.? ?Nimekuelewa.? ?Nilisahau, sasa hivi sitakuwepo kuna kazi moja tumetumwa kwenda kuifanya muda wote, hivyo sitaonana na wewe mpaka kesho. Kuwa makini tu na yote niliyokueleza, usiku najua unaweza kuwa mbaya kama utafanya makosa.? ?Nimekuelewa mpenzi.? Baada ya mazungumzo Sabina aliondoka na kuniacha nikiwa na shauku la kwenda kuiangalia ngozi yangu chini ya godoro. Niliingia hadi chumbani kwangu. Hali ya godoro langu kuwa tofauti na lilivyokuwa ilinishtua na kunifanya nifunue godoro. Sehemu niliyoweka ngozi yangu hapakuwa na kitu, sikuamini macho yangu na kunifanya nishtuke. Nilianza kupekua kila kona bila dalili zozote za kuiona ngozi ya kinga niliyopewa na Sabina. Nilijiuliza inawezekana kweli Helena kaichukua, lakini kajuaje kama nimeificha chini ya godoro? Nilikumbuka siku moja kabla ya kuelezwa na Sabina niwe naye mbali aliniuliza kuhusu kuiweka ngozi yangu. Katika ushauri wake alinieleza sehemu salama ni chini ya godoro baada ya kumueleza naiweka kwenye ubao wa batini. Wazo la haraka lilinifunua akili kuwa yote niliyoelezwa na Sabina yalikuwa na ukweli mkubwa. Jasho la hofu lilinitoka na woga ulinijaa moyoni kuhofia mpango wa kunifanyia kitendo kibaya. Kibaya muda ulikuwa umekwenda sana kutokana na kuhangaika kutafuta ngozi kila kona ya chumba kwa zaidi ya masaa mawili. Kutokana na maelezo ya Sabina muda ule niliamini asingekuwepo. Nilijikuta nikichanganyikiwa na kujiuliza ngozi nimepoteza sijui usiku utakuwaje? Nilipata wazo usiku ukiingia nikalale kwa wazazi wangu kwa kuhofia kuchukuliwa na wachawi . Lakini kutokana na historia ya wachawi lazima wangenichukua bila wazazi wangu kujua na asubuhi wangenikuta nimekwishakufa . Wazo la kutolala ndani lilizidi kuniweka katika wakati mgumu sana. Siku ile niliishi kwa shida kutokana na hofu kunitanda moyoni mwangu. Nilijiuliza nitafanya nini usiku ukiingia kwani kwa macho yangu niliwashuhudia wakinitafuta lakini hawakufanikiwa kuniona na kilichonisaidia kilikuwa ngozi? Kulala kwa wazazi nilijua si dawa ya kuwazuia kunichukua. Kwa mara ya kwanza toka nianze kutokewa na mauzauza ya wachawi siku ile ilikuwa nzito kwangu, wasiwasi wangu niliamini lazima watatumia nafasi ile kunifanyia kitu kibaya kama kulipa kisasi cha kugundua mambo yao ya kichawi. Nilijikuta nikimchukia Helena kwa kitendo chake cha kuniibia ngozi niliyopewa na Sabina. Wazo la haraka nilifikiria kuwaeleza wazazi kuhusiana na mpango wa usiku. Bado onyo la mzee Manoni lilinitisha na kujikuta kwenye wakati mgumu kuwaeleza wazazi wangu tukio lililotaka kunitokea usiku. Pamoja na udogo wangu nilijikuta nikiwaza mambo mengi. Nilipata wazo moja la kutolala ndani ili wakija wasinikute. Wazo hilo nililiona linafaa kulifanyia kazi, baada ya wazo lile niliendelea na shughuli zangu kama kawaida. Usiku ulipoingia kama kawaida baada ya chakula cha usiku niliingia chumbani mwangu, nilikuwa chumbani lakini akili yangu ilikuwa mbali sana. Nilisubiri mpaka wazazi wangu walipoingia ndani ili nitoke, ajabu siku ile wazazi wangu walichelewa kuingia ndani kulala. Nilishangaa siku ile kuchelewa kuingia ndani walikuwa wakizungumza nini. Nilijikuta nikiwachukia wazazi wangu na kuwaona labda nao wanahusika kwa namna moja au nyingine, siku zote walikuwa wakiwahi kulala au kuingia ndani lakini siku ile ilikuwa tofauti. Niliamua kujilaza kusubiri mpaka watakapotaka wenyewe kuondoka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment