Search This Blog

NITAKUFA MARA YA PILI - 2

 







    Simulizi : Nitakufa Mara Ya Pili

    Sehemu Ya Pili (2)





    Mara nilisikia fisi wale wakilia kilio cha maumivu na kutimua mbio kuonesha kuna mtu aliwatupia jiwe lililowaumiza na kuamua kuniacha. Nikiwa bado nimo kwenye shimo, nilimuona mzee Manoni aliyenitoa shimoni na kunipa pole. ?Pole sana kijana.? ?Asante mzee, fisi hawa walipania kunitafuna.? ?Ni kweli Shija, ningechelewa wangekuua.? ?Mungu wangu.? ?Usijali, nitakusaidia ila ukirudi nyumbani usimwambie mtu kitu chochote ulichokiona na kukisikia, sawa.? ?Sawa mzee.? ?Na hili jereha la mguuni?? Mzee Manoni alitema mate na kunipaka, kisha alinieleza. ?Nenda nyumbani wala usihofu, jeraha hili ukiamka asubuhi 

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    halitakuwepo.? Niliagana na mzee Manoni na kurudi nyumbani nikiwa bado na hofu nzito moyoni, nikijiuliza wale fisi walitoka wapi. Niliwaza huenda ni kisasi cha wale wasichana walioniambia nitaona na kuamua kunitumia fisi waniue kwa kunila nyama. Pamoja na kutokewa na tukio lile la kutisha bado sikutakiwa kuwafahamisha wazazi wangu. Niliporudi nyumbani sikutaka kuwa karibu nao kuogopa kuulizwa maswali juu ya jeraha langu ambalo lilikuwa chini ya mguu wa kushoto. Usiku ulikuwa mgumu sana kwangu kwa kusumbuliwa na milio ya fisi waliokuwa wakizunguka nyumba yetu. Hali ilikuwa ikitisha, fisi walikuwa wakiparamia mlango wangu, kilichonishangaza ni wazazi wangu kutulia tuli bila kutoka nje. Hali ile ilinishtusha sana iweje vishindo vyote vya fisi na vilio vyao baba asisikie, mara nyingi kitu chochote kisicho cha kawaida, ilikuwa lazima baba atoke nje. Lakini siku ile sikupata msaada wowote zaidi ya kuingia chini ya uvungu kujificha. Vishindo vya kuuparamia mlango wangu, vilinifanya niamini nimekwisha mtoto wa kiume, niliomba Mungu baba asikie vishindo vile ili aamke kuniokoa. Lakini haikuwa hivyo vishindo na vilio vya fisi ambao walionekana walipania kunitoa roho yangu vilizidi. Nilijaribu kupiga kelele lakini hazikuweza kusikika zilimezwa na kelele za vishindo na milio ya fisi. Niliamini siku ile ndiyo ilikuwa kiama changu. Bado sikujiona nina kosa la kutakiwa kutolewa roho, baada ya muda nilisikia sauti ya mtu akiwafukuza fisi wale. Nilivisikia vishindo vya fisi vikipotea taratibu, niliamini asubuhi kungekuwa na nyayo na fisi hata michubuko kwenye ukuta na mlango wa chumba changu. Kabla sijatoka uvunguni nilipojificha ili nisiliwe na fisi, nilisikia sauti ya baba akigonga mlango wangu huku akiniita jina langu. ?Shija amka kumekucha.? Sikuitikia mara moja, nilitulia ili kuwa na uhakika wa sauti ile, nilinyanyuka huku nikitetemeka na kwenda hadi mlangoni kuchungulia anayeniita kweli ni baba. Nilipoangalia vizuri nilipata uhakika kumbe kweli ni baba yangu mzazi nilifungua mlango na kutoka nje. Baba alinishangaa jinsi nilivyokuwa nimechafuka kwa vumbi la uvunguni nilipojificha vitisho vya fisi. Alinishangaa nilivyotapakaa vumbi mwili mzima, mnajua jinsi sakafu za nyumba za vijijini chini hakuna sementi zaidi ya udongo mtupu. Kama ujuavyo chumbani kwetu bila kukumbushwa kufagia tunaweza kukaa mwaka mzima bila kufagia. Basi chumbani kwangu uvunguni vumbi mtindo mmoja. Nilikuwa kama kinyago bila kujijua huku kichwa kikiwa kizito kwa usingizi, baada ya kukesha usiku kucha kwa vitisho vya fisi. ?Shija mwanangu mbona upo hivyo kama ulikuwa umelala uvunguni?? Baba alinishangaa na kuniuliza huku akinizunguka kunitazama jinsi nilivyokuwa mweupe kwa vumbi. Nami nilijiangalia huku nikijishangaa jinsi nilivyokuwa , nilijiuliza nitamdanganya kitu gani baba ili akubaliane na hali ile. ?Shija kwa nini umekuwa mchafu siku hizi mtu niliyekuwa nikikutegemea kwa usafi, kuna siku ulilala kitandani na matope. Leo unatoka ukiwa umepauka kwa vumbi una tatizo gani?? Nilikaa kimya huku nikitafuta jibu la kumueleza, lakini kila nililofikiria nililiona haliwezi kumkidhi. Ilibidi niseme ukweli wa mambo yaliyonitokea kwa kuamini hata yeye alisikia pengine aliyapuuza. ?Baba, jana fisi walivamia nyumba yetu.? ?Ulijuaje?? ?Baba ina maana vurugu za usiku hukuzisikia?? ?Sikuzisikia.? ?Basi jana fisi walivamia nyumba yetu na kutaka kuingia chumbani kwangu huku wakikwaruza kuta na milango.? ?Hao fisi walifika saa ngapi mimi nisiwasikie?? ?Baba, sijui saa ngapi ila wameondoka muda tu nawe ukagonga mlango.? ?Mmh, na hili vumbi?? ?Niliingia uvunguni kuogopa 

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kuliwa na fisi.? ?Sasa mbona kauli yako inapingana na mazingira halisi?? ?Kweli kabisa baba, mlango usingekuwa mzuri wangenitafuna.? ?Hebu njoo.? Nilizunguka nyumba nzima na baba kutafuta nyayo za fisi hazikuwepo uwanja ulikuwa msafi kama mtu aliufagia. Pia hata kwenye kuta hakukuwa na dalili zozote za mlango kukwaruzwa . ?Haya nioneshe hizo nyayo za hao fisi ulionieleza?? baba aliniuliza baada ya kuzunguka nyumba nzima bila kuona dalili zozote za kuja kwa fisi kwetu. ?Lakini baba, fisi kweli walikuwepo labda wamefuta nyayo .? ?Shija mimi si mtoto mwenzio sitaki kutaniwa, hao fisi unaowasema mbona hata nyayo zao kwenye uwanja wa nyumbani hazionekani au hao fisi walikuwa wakiruka angani?? ?Baba si angani hata vishindo vyao vilikuwa vikisika nikashangaa kwa nini baba hukuamka.? ?Shija siku hizi umekuwa mtoto mtukutu, mchafu wewe , muongo wewe , ona ulivyokuwa kama umelala nje.? ?Baba kweli,? nilitetea kauli yangu.



    ?Ungeniambia umeota unafukuzwa na fisi kwa woga ukaingia uvunguni ningekubali, lakini si kusema kuna fisi walikuwa wakicheza kwenye uwanja wa nyumba yangu. Basi leo ingekuwa ya kwanza toka nianze kuishi hapa huu mwaka wa ishirini na tisa, sijawahi kuona kitu chochote hapa hao fisi huwasikia kwa mbali.? Mmh, maneno ya baba ya kuukataa ukweli wangu kwa upande mwingine niliona kama unanisaidia kumdanganya. Kabla sijamjibu alinieleza. ?Hebu nenda kaoge uwahi shule.? Sikuongeza neno nilikimbilia kuoga ili niwahi shule, baada ya kuoga nilivaa nguo za shule na kupitia vifaa vyangu kuwahi shule. Nikiwa njiani huku kichwa kikiwa kizito kwa usingizi, niliwaza mengi juu ya tukio lililotokea usiku wa kuamkia siku ile. Nilijiuliza ilikuwa ndoto au kitu cha kweli kilichonitokea, sikuamini kama ni kweli kwani kila kilichotokea nilikuwa macho wala si ndotoni. Kingine kilichonishangaza ni hali ya uwanja kuukuta msafi hauna dalili za kuwepo fisi waliokuwa wakicheza huku wakitaka kuingia chumbani kwangu. Nilijikuta katika wakati mgumu huku nikijiuliza nini hatima ya matukio yale, kingine kilichonitisha ni kuvunja amri ya mzee Manoni ya kumueleza baba chochote nitakachokiona au kukisikia. Lakini kwa upande wangu swali la baba halikuwa na jibu la kudanganya zaidi ya kusema ukweli ambao hata hivyo baba hakuuamini. Nikiwa nakaribia eneo la shule, nilishtushwa na sauti za wale wasichana walionifuata wakati nawinda ndege na kunitisha kuwa nitaona. ?Shija,? Helena aliniita. Sikujibu niligeuza shingo na kuwatazama kisha niliendelea na safari yangu. ?Shija si tunakuita?? Sabina aliongezea. ?Mna shida gani?? ?Bado hujakoma kiburi eeh? ?Nakuuliza mna shida gani? ?Tulitaka kukueleza una bahati la sivyo ungetutambua sisi kina nani?? ?Ninyi kina nani,mtanifanya nini?? Siku zote sikupendwa kutishwa na mwanamke. ?Eeh, unatufanyia kiburi, eh'?'' ?Hamuwezi kunifanya lolote hata mkijiunga wote.? ?Shija unatuambia sisi hivyo?? Helena alinitisha. ?Hamna lolote wachawi wakubwa ,? kwa hasira nilijikuta nimeropoka. ?Sisi wachawi ...Sisi wachawi .? Walisema na wakataka kunivamia wanipige. Nilijikuta nikipata ujasiri wa ajabu na kuwa tayari kwa lolote juu ya vitisho vya wale wasichana. Ilitokana na tabia yangu ya tangu utotoni kukataa kuonewa na mwanamke. Baada ya kuhesabu namba tulijichanganya katika kufanya usafi kwenye eneo langu. Nikiwa nafanya usafi nilifuatwa na mmoja wa wale wasichana niliopigana nao na kuwapiga. ?Shija unaitwa na mwalimu.? ?Si amesema atatuita baadaye? nilimjibu bila kumtazama. ?Siyo 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    huyo.? ?Na mwalimu nani?? ?Mwalimu Vene.? Niliacha kufanya usafi na kwenda ofisini ambako kulikuwa na walimu watatu, mwalimu wa zamu, mwalimu Vene na mwalimu mwingine aliyekuwa akikaa karibu na shule. Nilipoingia nilimkuta Sabina amekaa kwenye meza ya mwalimu, nilipoingia mwalimu Vene aliniangalia kwa jicho kali kabla ya kunieleza nikae kwenye benchi lililokuwa mbele ya meza yake. Mwalimu Veneranda au kama tulivyomzoea kumwita jina lake kwa ufupi Vene, ndiye niliyemuota na kumuona kwenye ngoma ya wachawi . Baada ya kukaa aliniuliza. ?Shija umewaitaje wenzako?? ?Sijawaita vyovyote .? ?Mwongo, walimu amesema eti sisi ni wachawi ,? Helena aliingilia mazungumzo. ?Shija, kwa nini umewaita wenzako wachawi ?? Sikujibu nilikaa kimya, kwa vile sikuwa na jibu, niliinama chini. Mwalimu alipaza sauti kutaka jibu langu. ?Shija nakuuliza kwa nini umewaita wenzako wachawi ?? Sikujibu tena nilibakia kimya nimeinama, mwalimu kwa hasira alinyanyuka na kuzunguka meza huku akisema. ?Unanifanyia kiburi, hunijui eeeh.? Baada ya kunisogelea aliniuliza, huku akiunyanyua juu uso wangu. ?Nakuuliza, uliwaona wanawanga ?? ?Mwalimu nilimwona siku ile,? Helena alidakia bila kujua alimaanisha nini. ?Weeeee, shatapu, unataka kuzungumza upumbavu gani, tena ukome nisikusikie siku nyingine,? mwalimu alimkata kauli Helena, na kunigeukia mimi huku akisema. ?Sasa nataka kukukomesha ukome kuwaita wenzako wachawi . Nakumbuka siku za nyuma uliitisha mkutano kwa kuitwa mchawi, leo hii unafurahia kuwaita wenzako. Kama uliona vibaya sasa nataka nikukomeshe usirudie tena,? mwalimu alisema huku akifuata fimbo nyuma ya meza yake, nilijua kumewaka moto ilibidi nijiteteee kabla sijaadhibiwa. ?Mwalimu walikuwa wakinitishia.? ?Kukuroga?? ?Hapana walinieleza nitaona.? ?Sasa mtu akikueleza utaona ndiyo umwite mchawi? Kwa nini hukuwashtaki kwa mwalimu?? ?Mwalimu zilikuwa ni hasira tu.? ?Basi lala chini nizipulize hizo hasira.?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipochelewa kulala, fimbo ya mgongoni ilinipeleka chini, mwalimu alinipiga fimbo zisizo na idadi kisha alinipa adhabu ya kuchimba shimo la taka. Sikutaka kubisha kwa vile niliamini kama nitabisha au kulipeleka mbele lingezua mjadala mkubwa. Nilitekeleza ile adhabu huku vipindi vitatu vya asubuhi vikinipita, baada ya kumaliza adhabu nilirudi darasani kuendelea na masomo huku wanafunzi wakinipa pole, wakisema nimeonewa. Lakini mwalimu wa darasa alinipoza na kuniomba niwe mtulivu na kuniona nisichukue sheria mkononi kama nitachokozwa basi nipeleke mashitaka kwa mwalimu yeyote . Nilijiuliza mambo mengi kutokana na vitendo vingi kufanyiwa nje ya shule huku nikizibwa mdomo na mzee Manoni. Japo niliumia moyoni lakini niliendelea kuumeza mfupa wa siri nzito ambayo sikuamini kama baba angeijua kusingekuwa na usalama. Baba nilimjua vizuri hakupenda kuona mtoto wake akinyanyasika , alishapigana na jirani yetu baada ya kunipiga kutokana na mbuzi wetu kuingia kwenye shamba lake. Niliamini kama nitamweleza kila kilichonitokea kungekuwa na vita kubwa kati yake na mzee Manoni, hata familia ya wale watoto watukutu. Nilikubali niwe mjinga ili kufunika kombe mwana haramu apite. Baada ya masomo nilirudi nyumbani nikiwa na zigo zito la mawazo juu ya mambo yaliyokuwa yakinitokea huku nikikatazwa nisiwaambie wazazi wangu. Nilijiuliza hali ile itaisha lini, nilitembea kwa mwendo wa taratibu kurudi nyumbani. Kila dakika iliyokuwa ikija mbele yangu ilikuwa ya maajabu, baada ya mwendo wa dakika kumi nilijikuta nimetokea sehemu ambayo ilikuwa mbele zaidi na ninapoishi. Nilijishangaa kutembea na kupita kwetu bila kujijua, kabla sijaamua nifanye nini nikiwa najishangaa kufika sehemu ile, akili yangu ilinielekeza kwenye mawazo kiasi cha kushindwa kuona mbele. Lakini sikuwa na mawazo kiasi cha kushindwa kutambua naelekea wapi. Sauti ya mzee Manoni iliyokuwa imezoeleka akilini mwangu iliniita kwa nyuma. ?Shija!? Kabla ya kuitika nilishtuka na kugeuka kutokana na kushtukizwa na sauti ile, eneo lilikuwa jeupe na sehemu niliyokuwepo chini ya mti kulikuwa na majani mengi yaliyokauka . Mtu akija nyuma yako lazima umsikie kutokana na kelele za majani makavu. Kila dakika nilizidi kumwogopa mzee Manoni na kuamini ujaji wake si wa kawaida ni wa miujiza na kuamini siku nitakayomweleza baba huenda akatokea mbele yangu. Ujaji wake sikuweza kumsikia na kumshtukia nyuma yangu, baada ya kushtuka bila kujibu mzee Manoni alicheka mfululizo na kusema...



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shija mbona mwoga hivyo ?? ?Mzee Manoni, umenishtua sana.? ?Ooh, pole na huku umekuja kufanya nini?? ?Hata sijui, nashangaa kujikuta huku.? ?Ooh, pole sana.? ?Asante.? ?Mmhu, nasikia leo umepigana shule?? ?Mmh, hamna; nani kakwambia ?? ?Nijibu sio kuniuliza swali.? ?Ndiyo.? ? Kwa sababu gani?? ?Walinitisha nitaona.? ?Ehe?? ?Basi nami sikukubali ndipo tuliposhikana.? ?Kweli?? Mzee Manoni ilionesha anajua kila kitu. ?Kweli mzee Manoni.? ?Shija nakuamini, mbona unanidanganya.? ?Ni kweli mzee Manoni.? ?Sababu ya kupigana ilikuwa nini, uliwaambia wao ni nani?? ?Wachawi.? ?Kwa nini?? ?Ni hasira tu.? ?Shija nilikueleza nini, mbona siri unaanza kuitoa nje mapema?? ?Nimekosa mzee Manoni ni hasira tu, Lakini sirudii tena,? nilijitetea. ?Basi yamekwisha , ukitoka hapa kama kawaida yetu usimwambie mtu.? ?Sawa, mzee Manoni.? ?Unaweza kwenda nyumbani,? alinieleza huku akiondoka eneo lile. Niligeuka na kuanza kurudi nyumbani taratibu bila kumuangalia tena mzee Manoni aliyekuwa akiyeyuka kama upepo, sikutembea hatua nyingi nilijiona nimetokea kwenye uzio wa nyumbani. Kama kawaida yangu hata lile nililimeza moyoni mwangu. Hata wazazi wangu waliporudi shambani hawakujua nini kilichotokea shuleni, sikumueleza baba nilikaa kimya. Niliendelea kumuomba Mungu kila kitu kilichotokea na kuonekana mbele ya macho ya watu baba asijue. Siku zilikatika huku hali ya utulivu ikijirudia, nililala usingizi mzuri bila vitisho shuleni nilisoma bila usumbufu na wale wasichana walibadilika na kuwa marafiki zangu. Niliamini wagombanao ndio wapatanao. Lakini akili yangu ilikosa amani kwa kushindwa kuutua mzigo mzito wa vitu vilivyonitokea ambavyo baba ndiye angekuwa matatuzi wangu. Kila dakika nilijiuliza kama nikimueleza baba juu vitu nilivyokutana navyo na onyo nililipewa na mzee Manoni itakuwaje? Wasiwasi wangu ulikuwa kwa vile mzee manoni ni mchawi pia chama chao ni kikubwa , kama nilichokiona mara mbili ndotoni ningeweza kumpoteza baba yangu. Niliamua kuumeza mfupa wa siri ili siku ziende mbele, kwa kuamini kila lenye mwanzo lina mwisho, japo sikujua mwisho wake nini. Pamoja na utulivu uliojitokeza bado nilikosa amani moyoni mwangu kila nilipokumbuka yote yaliyonitokea . Uwezo wangu kimasomo haukushuka sana pamoja na matatizo lukuki kichwani mwangu bado niliongoza darasani. Wakati wote huo kaka yangu aliyekataa shule alitoweka bila kujua amekwenda wapi, tuliamini amepotea baada ya kupotea zaidi ya miezi miwili bila kuonekana. Tulijikuta tukisubiri siku atakaporudi, lakini hakukuwa na taarifa zozote za kuonekana au kusikia tetesi kaonekana wapi. Mwezi wa tatu toka kaka atoweke nyumbani, siku moja tukiwa uani tumekaa tukisubiri chakula cha usiku, sote tulishangaa kumuona kaka akirudi. Kitu cha ajabu hakutaka kuzungumza na mtu, aliingia chumbani kwake na kulala. Baba alisema tumuache ajipumzishe akiamka atazungumza naye siku hiyo au ya pili. Tulimuacha alale ili asubuhi tumuulize alikuwa wapi siku zote hizo pamoja na akili yake kuharibiwa na bangi. Hata chakula hakutaka hivyo haikutusumbua, mama alimuwekea chakula kama njaa ingemshika basi angeamka na kula. Baada ya kupanda kitandani kwake na kulala muda wangu wa kulala ulipofika nilipanda kitandani kwangu. Usiku wa siku ile ulikuwa wa mang?amu ng?amu kutokana na kusikia vitu vya ajabu ambavyo sikuwahi kusikia. Pia milio ya ngoma na vishindo vya watu katika nyumba yetu vilikuwa vikubwa , hali ile ya kutisha ilichukua zaidi ya masaa mawili nje ya nyumba yetu huku watu wakichelekea kama siku niliyohudhuria ngoma ya wachawi waliokuwa wakishangilia nyama za watu. Kuna kipindi nilihisi kama ukuta wa nyumba yetu umepasuka eneo kilipokuwa kitanda cha kaka. Lakini sikuona kitu chochote na ukuta 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ulikuwa vile vile japo nilisikia mlio huo, nilijikuta nikisikiliza kwa vile nilianza kuzoea ile hali ambayo ilionesha haikuwa ya kunidhuru. Niliamini pengine ni kujifurahisha katika michezo yao ya kichawi. Baada ya matukio mazito nje ya nyumba yetu yaliyodumu kwa masaa zaidi ya mawili, ngoma ile iliondoka huku nikiwasikia wakiondoka eneo la nyumbani huku wakishangilia. Nilizidi kushangaa baba kutoamka wala kutoka nje kutokana na kelele zilizokuwa nje ya nyumba yetu. Baada ya muda hali ya utulivu ilijirudia nami usingizi haukuchelewa kunichukua. Kwa vile siku ya pili ilikuwa Jumamosi, niliamka saa moja kwa ajili ya kwenda kisimani. Baada ya kuamka nilipitia vyombo ili niende kisimani, kaka alikuwa bado amelala usingizi mzito. Wakati huo wazazi wetu tayari walikuwa wamekwishakwenda shamba, baada ya kutoka kuchota maji nilishangaa kaka kuendelea kulala kitu ambacho siku za nyuma haikuwa kawaida yake, kilichonishangaza mlalo aliolala toka jana hakujigeuza alilala vilevile mpaka asubuhi. Lakini niliogopa kumwamsha kutokana na kiburi alichokuwa nacho kwani ningeambulia makonzi. Lakini mpaka inafika saa tano bado alikuwa kitandani. Niliamua kwenda kumwamsha ili anywe uji, nilipomtikisa ili aamke mwili wake ulikuwa umelegea kila nilimpomtikisa alinifuata. Hali ile ilinitisha nilikumbuka siku moja kuna mtoto alianguka shuleni na kulegea vile. Baadaye tuliambiwa alikuwa ameisha kufa kitambo. Hali ile ilinitisha sana na kutoka mbio hadi shambani na kuwaeleza wazazi wangu hali aliyokuwa nayo kaka.





    ?Ina maana toka jana alipoingia ndani hajaamka?? Mama aliuliza.. ?Ndiyo mama.? ?Mmh, yatakuwa mabangi yake,? baba alisema bila kuonesha kushtushwa sana. ?Baba si mabangi, amekuwa kama Jose aliyeanguka shule na kulegea vile baadaye tuliambiwa amefariki dunia.? ?Mmh, si rahisi, hebu twende.? Niliondoka na baba lakini mama naye hakukubali kubakia shamba tuliongozana wote hadi nyumbani. Tulipofika tuliingia wote chumbani, baba alimuangalia kaka kwa muda kisha alinieleza. ?Shija toka nje mara moja.? Nilitoka nje na kuwaacha wazazi wangu ndani, sikukaa mbali nilikaa pembeni ya mlango kutaka kujua kaka amepatwa na nini. Baada ya dakika kama kumi nilisikia kilio cha mama cha sauti ya juu lakini baba alimzuia kulia. ?Jamani mwanangu wamemfanya nini, Paulo baba ulikwenda wapi mwanangu na kurudi hata salamu hukunipa... Kumbe baba ulikuwa na siri nzito moyoni mwako. Kwa nini baba umeniacha, nilitaka nife unizike sasa kama baba umetangulia nitazikwa na nani mimi jamani?? Maneno ya mama yalinipa picha kuwa kaka alikuwa amefariki, kabla ya kuanza kumlilia kaka yangu nilijawa na maswali yaliyotakiwa kupatiwa majibu na mtu mwingine si mimi mwenyewe . Swali la kwanza kaka alikuwa wapi? Swali la pili alipokuja alikuwa na siri gani moyoni mwake ambayo hakutaka tuijue kabla ya kifo chake? Swali la nne kwa nini hakutaka kuzungumza na mtu? Na swali la mwisho ile ngoma ilikuwa ikiashiria nini? Nilijikuta nikiwaza kitu cha ajabu, huenda ile ngoma ilikuwa chanzo cha kifo cha kaka. Kingine kilichonishangaza ni wazazi wangu na ndugu zangu kutosikia ile ngoma. Kwani hakuna hata mmoja aliyehoji asubuhi kusika ngoma na makelele yakipigwa kwenye uwanja wa nyumba yetu. Yalikuwa maswali ambayo kama nisingekatazwa na mzee Manoni niliamini baba angenipatia majibu. Kilio cha mama kilikusanya majirani, ambao nao waliungana na mama kumlilia kaka, haikuchukua muda wanakijiji walikusanyika na kuanza mipango ya mazishi. Katika watu waliofika msibani alikuwepo mzee Manoni hata wazazi wa wale wasichana ambao niligombana nao na mwishowe kupatana nao walikuwepo . Baada ya maandalizi yote tulimzika kaka kwenye makaburi ya kijiji, baada ya msiba kila mmoja alizungumza lake kuhusiana na kifo cha kaka kutokana na maelezo ya baba 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    aliyosema baada ya kuuzika mwili wa kaka. Japo kuna watu walinong?ona kuwa kifo cha kaka si cha kawaida huenda ni mkono wa mtu. Lakini baba aliamini kile kifo ni cha kawaida kama vilivyo vifo vingine wala hatajishughulisha na upuuzi wowote kutaka kujua nini chanzo cha kifo cha kaka. Baba alisema kwa sauti ya huzuni: ?Jamani, najua kifo cha mwanangu kimewashtua wengi, mazingira ya kutoweka kwake na kuonekana kwa kweli yanatatiza. Lakini bado naamini kifo chake ni cha kawaida. Sitakwenda kuutafuta ukweli popote, kufanya hivyo ni mwanzo wa kutafuta uhasama na watu. Kama amri ya Mungu atajua yeye kama mkono wa mtu vilevile atajua yeye . Hivyo nashukuruni kwa msaada wenu wa hali na mali.? Baba katika maisha yake pamoja na kukaa eneo ambalo lilikuwa likisadikiwa kuwa kuna baadhi ya watu mchana watufisi usiku hakuliamini. Na ndiyo maana minong?ono ya watu kuhusiana na kifo cha kaka aliikanusha. Niliamini hata kama ningemueleza yaliyotokea kabla ya kifo cha kaka bado angeona ni uzushi tu. Baada ya msiba wa kaka nilianza kuweweseka kila siku usiku nilipolala, mambo yaliyotokea siku ambayo asubuhi yake kaka alifariki yalijirudia kila nilipoweka ubavu chini. Hali ile ilinisumbua zaidi ya wiki nzima, kingine kilichoniweka katika wakati mgumu ni sauti ya kilio ya kaka akilalamika kuumizwa na bakora. Nilimsikia kwa sauti yake kabisa akilia huku sauti za bakora akichapwa zikisika, kwa kweli iliniuma kusikia sauti ya kaka yangu aliyekufa akipigwa nje ya nyumba yetu kila siku usiku. Kuna siku uzalendo ulinishinda na kuamua kutoka nje usiku huku nikijisemea liwalo na liwe. Baada ya kufungua mlango sauti ile ilikoma, sikurudi ndani mara moja nilitulia kusikiliza kama ni ya kweli au naota. Nje usiku kulikuwa kunatisha kutokana na kiza kizito na ubaridi kilinipuliza na kuzidisha hofu moyoni lakini sikurudi ndani nilitaka kujua mwisho wake, sikuhofia kitu nilizunguka nyumba, lakini sikuona kitu chochote, zaidi ya milio ya bundi na fisi kwa mbali. Nilirudi ndani na kujilaza masikio yakiwa nje, kusikiliza kama atarudi tena, lakini mpaka kunakucha sikusikia kitu chochote. Kila alfajiri baba aliponiamsha hakuonesha kusikia kitu chochote usiku kwenye uwanja wa nyumba yetu. Nilijiuliza ni kweli yote yanayotokea ni viini macho au kweli, bado niliamini mtatuzi wa yote yale ni baba, lakini nilijiuliza nitaanzia wapi na baada ya kumueleza nitambebea mbeleko gani mzee Manoni. Niliamini hali ile ikiendelea hata kusoma nitashindwa, muda mwingi darasani nilikuwa nasinzia au kuhama kimawazo. Siku moja shuleni tukiwa mapumziko, niliwasikia wanafunzi wenzangu wakizungumzia habari za mtu kugeuzwa msukule. Mtu kuonekana amekufa lakini anakuwepo na kutumikishwa kazi au kuuawa na kugeuzwa kitoweo cha wachawi . Lakini walisema wapo waganga ambao huweza kuwarudisha watu wa aina hiyo. Maneno yale yalinisisimua na kuamini kabisa kaka yangu hajafa kageuzwa msukule, lakini habari zile niliogopa kumueleza baba ningeanzia wapi? Kwani ni mtu aliyekwishasema haamini imani za kishirikina. Ningeanzia wapi mpaka anielewe na akinielewa mzee Manoni angeniacha hivihivi ? Niliendelea kufa kizungu na tai shingoni. Kama kawaida maendeleo yangu ya shule yaliendelea kuporomoka kufikia hatua ya kushika nafasi ya kumi darasani kitu ambacho sikuwahi kukiota. Taarifa zilimfikia baba ambaye alipewa msururu wa matukio yaliyonitokea ambayo toka wakati huo maendeleo yangu yamekuwa yakiporomoka kila siku. Bila kuwa na habari siku moja baada ya chakula cha usiku baba aliniita kuniulizia kwa nini simuelezi matatizo yaliyonikuta kufikia hatua ya kuporomoka kimasomo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya baba kuvuta mikupuo miwili ya sigara alinigeukia na kuniuliza swali. ?Shija vipi maendeleo yako darasani?? Swali lile lilinishtua na kunifanya niiname chini kwa woga, nilijiuliza nitamjibu nini, kuhusiana na mwenendo wangu mbaya wa darasani. Niliamini siri iliyokuwa moyoni mwangu ndiyo chanzo cha yote, lakini nilijiuliza nitaanza je kumueleza baba. ?Shija, nasikia siku hizi umekuwa mtukutu shuleni unagombana na wenzako, darasani husomi unasinzia muda wote tatizo nini mwanangu?? Nilijikuta nikiwa njia panda huenda baba alikuwa amesikia habari nyingi juu yangu, pengine kanifuatilia kwa muda mrefu lakini alikaa kimya kuona kama nitamwambia. Nilijiuliza nikimwambia itakuwaje, nilijikuta nikiamua liwalo na liwe bora nimweleze sikuwa na njia ya kumdanganya. Kabla sijanyanyua mdomo kumueleza baba kinachonisibu, niliisikia sauti kwa mbali ya mzee Manoni akisalimiana na mtu jirani ya nyumba yetu. Woga ulinijaa na kujikuta nanyamaza kimya. Baba baada ya kusubiri jibu langu bila mafanikio alisema. ?Shija huna jibu?? ?Baba wao ndio walionitishia kunipiga ndiyo tukapigana nao, lakini tuliyamaliza yakaisha,? ilibidi nipindishe ukweli ili nisikie ataniambia nini. ?Hivi Shija mtu niliyekuwa nakutegemea leo umekuwa hivyo , umekuwa Mung?unya kuharibikia ukubwani. Na hii tabia ya kupigana imeanza lini tena na watoto wa kike.? ?Samahani baba, ni hasira tu.? ?Shija unakumbuka vizuri hata Father wa Kanisani alikusifia kwa akili yako, alisema kuwa wewe ndiye hazina yetu itakayotukomboa katika umaskini hivyo tukusomeshe kwa nguvu zote. Upo darasa la sita umekuwa mgema tembo unalitia maji au sifa zimekulewesha?? ?Hapana baba, nitajitahidi siwezi kuwa nyuma tena kimasomo, nitajitajidi ili nisiwaudhi ninyi wazazi wangu.? ?Shija mwanangu kumbuka wewe ndiye kichwa cha familia, nimeapa kujinyima ili usome mpaka elimu ya juu. Unakumbuka ahadi aliyokueleza Father Thomas kuwa ukipasi darasa la saba atakupa zawadi nzuuuuri?? ?Ndiyo nakumbuka baba.? ?Sasa hiyo zawadi huitaki?? ?Naitaka.? ?Basi zingatia masomo.? ?Nakuahidi mzazi wangu nitafanya hivyo .? ?Acha utundu ambao ndio unakufanya upungue akili.? ?Sawa baba yangu, nitafanya yote uliyoniagiza.? Baada ya mazungumzo na baba tuliagana, mimi kuingia chumbani kwangu na kumuacha baba naye akiwasha sigara yake iliyozimika wakati wa mazungumzo ili avute kabla ya kwenda kulala. Baada ya kuingia ndani nilipanda kitandani kulala. Lakini kichwani nilikuwa na mawazo mengi sana juu ya taarifa alizozipata baba kuhusiana na matukio yaliyotokea shuleni na kumfikia baada ya muda kupita. Nilijiuliza taarifa zile alizipata zamani na kukaa kimya au baada ya kudorola katika masomo kuna mtu kamweleza habari zile.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini nilimshukuru Mungu hakutaka kuyachimbua sana zaidi kunisisitizia niache utukutu na kuzingatia masomo. Bado wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa matukio yaliyokuwa yakinitokea kila kukicha na kunifanya niwe kwenye msongo wa mawazo kiasi cha kushindwa kuyashika niliyokuwa nafundishwa. Nilipata wazo niende kwa mzee Manoni nimueleze niliyozungumza na baba juu kuporomoka kwangu kimasomo na vitisho vya usiku. Kwenda kwake niliogopa lakini nilipanga akinitokea lazima nimwambie. Usiku wa siku ile ulikuwa mtulivu kuliko siku za nyuma nililala vizuri bila kutokewa na vitu vya kutisha. Siku ya pili nilikwenda shuleni kama kawaida, darasani nilishangaa kuweza kutulia na kuweza kusoma kwa utulivu mkubwa hata kufanya vizuri katika masomo yangu. Baada ya kukusanya kazi na mwalimu kusahihisha kabla ya kwenda ofisini, alinisifia jinsi nilivyofanya vizuri katika somo lake. ?Leo Shija umenifurahisha sana, inaonekana umekuwa mtoto mzuri kuacha utundu na kuzingatia masomo, mpigieni makofi.? Wanafunzi walinipigia makofi, baada ya mwalimu kuondoka Sabina mmoja wa wale wasichana waliokuwa maadui zangu alinifuata kwenye dawati langu. ?Shija nimekuletea kiazi.? ?Asante Sabina,? nilishukuru bila kukichukua. ?Shija, si ulisema ugomvi wetu umekwisha?? ?Ni kweli.? ?Sasa mbona huchuki kiazi?? Niliona aibu kukataa japo sikumuamini moja kwa moja kwa kujua huenda katumwa ili kunimaliza. Lakini nilimtanguliza Mungu mbele na kukichukua kile kiazi. Sabina ili kuhakikisha nakila muda ule alisema: ?Shija nikatie na mimi kidogo maana viazi hivi vilikuwa vichache nikakuchukulia wewe tu kwa mapenzi yangu kwako . ? Nilimkatia kipande tukala wote huku akinieleza nikitoka nisimuache. Tokea siku ile nikawa na uhusiano wa karibu sana na Sabina mpaka akapelekea kuwa mpenzi wangu. Tukawa tukitoka shule tunaongozana na kwenda porini ambako hushinda mpaka jioni na kurudi nyumbani. Uhusiano wetu tuliuficha shuleni ili tusije fikiriwa vibaya , kutokana na baadhi ya wanafunzi kuadhibiwa mbele ya shule kwa kuwa na mahusiano ya mapenzi yaliyotokana na kukamatwa na barua za mapenzi. Hata kutoka kwetu ilikuwa mimi napitia njia nyingine na Sabina naye alipitia yake na kukutana sehemu yetu tuliyoichagua kukutania. Kwa kweli uhusiano wetu japo kwa mila na desturi ni vibaya kwa vijana wadogo kama sisi kuwa na mahusiano ya kimapenzi, lakini kwa upande mwingine ilikuwa ni faida kubwa sana ambayo nilifikiri kama nisingekuwa na mahusiano ya karibu na Sabina ningebakia jina.  


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nayasema haya kutokana na mambo niliyoambiwa na Sabina ambayo yaliufanya moyo wangu utetemeke kwa hofu. Niliamini kauli isemayo cheka nao lakini si wema kwako na adui yako anaweza kuwa rafiki mkubwa. Nimeamini kweli penzi hufungua moyo wa mtu na kuyatoa hata yaliyo chini ya uvungu wa moyo wake na kuwa tayari hata kufa kwa ajili ya kuyalinda mapenzi yake. Japo nilikuwa nakwenda kinyume na maadili yetu ya kujiingiza kwenye uhusiano katika umri mdogo, lakini naweza kusema ilinifungulia nisiyoyajua yaliyokuwa yakinizunguka , ambayo bila kuelezwa na Sabina binti aliyejitoa muhanga ningekufa kifo kibaya. Siku moja baada ya kutoka shule Sabina alinieleza tusikae sehemu tuliyoizoea, nilimuuliza kwa nini, alinieleza kuna kitu anataka kunieleza ambacho kinatakiwa tuwe mbali na maeneo ya karibu na nyumbani. Tulikubaliana kama kawaida tulipita njia zetu na kukutana eneo tulilopanga kukutana kisha Sabina aliongoza kuelekea ndani zaidi ya pori. Tulikwenda mpaka tukayaacha mashamba na kuingia kwenye pori ambalo hakukuwa na watu zaidi ya sauti za ndege. Niliamini sehemu zile kunaweza kuwa na wanyama wakali, kutokana na mwendo kuwa mrefu bila kufika nilianza kuingiwa na wasiwasi . ?Sabina unanipeleka wapi?? woga uliniingia na kuamini huenda kuonesha mapenzi kwangu ilikuwa njia ya kunikomesha. Niliona kama ni kweli alikuwa amenileta kimtego alikuwa amenipatia, kwa eneo lile sikuwa na ujanja wowote . ?Shija wasiwasi wako nini?? ?Mbona tunazidi kwenda ni habari gani za kunileta huku?? ?Shija ungejua wala usingeniuliza ungeweza kuniambia hata tupande gari tuondoke wilaya hii twende tukazungumze sehemu ya mbali zaidi.? ?Ni mazungumzo gani hayo?? ?Utayajua, japo nilionywa nisimwambie mtu yeyote , lakini nimejikuta nikizama kwenye mapenzi yako pia nakupenda sana tusingekuwa wanafunzi ningekueleza unioe,? Sabina alisema kwa sauti ya upole. Mmh makubwa, maneno ya Sabina yalinifanya nisihoji tena kitu na kumfuata kila alichotaka kukifanya juu yangu. Niliridhika na maneno yake tukaendelea na safari iliyochukua nusu saa. Sabina alinieleza tukae chini ya mti wa mkalatusi, baada ya kukaa tulitulia kwa muda kila mmoja akivuta pumzi. Baada ya kupumzika kwa muda Sabina alinitazama kwa muda usoni mpaka nikamuogopa, kilichofuatia kilikuwa machozi. ?Sabina unalia nini?? alinishtua baada ya kuongea machozi yalimtoka. ?Shija dunia hii kweli ina siri kubwa, siamini kijana mzuri kama wewe kuna watu wanautamani uhai wako?? Sabina aliniuliza huku michirizi ya machozi ikiwa mashavuni kwake . ?Uhai wangu?? Niliuliza kwa kushtuka kusikia vile. ?Ndiyo Shija.? ?Mungu wangu, kwa kosa gani?? ?Si unakumbuka kuna siku ulihudhuria ngoma ya wachawi ?? Swali lile lilinishtua kwani kwa upande wangu nilikuwa naota, na swali lile niliogopa kulijibu kama ningelijibu basi ningekuwa nimevunja amri ya mzee Manoni ya kutomwambia mtu siri ile ya kukaa kimya kwa kila nitachokiona au kukisikia. Lakini niliamini mpaka Sabina kunileta kule basi alikuwa na siri nzito ambayo sikutakiwa kumficha ukweli wa kitu kilichokuwa ndani ya moyo wangu. ?Sabina kweli nilihudhuria ngoma ya wachawi , lakini nilikuwa ndotoni,? kwa mara ya kwanza nilitoa siri niliyokatazwa na mzee Manoni. ?Hapana Shija, kwa watu kama ninyi ambao si wachawi huhudhuria ngoma au jambo la kichawi hupitia kwa njia ya ndoto.? ?Kwa hiyo kweli nilikuwa kwenye ngoma ya wachawi ?? ?Kweli kabisa, hata sisi tulipokuona tulishangaa sana na kujua lazima siri yetu itatoka nje. Wachawi walidhamiria wakuue ili siri ile ufe nayo.? Kauli ile ilinitisha sana na kuona kumbe kuna watu wanakufa bila makosa yoyote , sikutaka

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     kuuliza swali nilitulia ili Sabina aendelee kunimwagia siri nzito za wachawi ambazo sikuzijua na nisingezijua. ? ...Lakini mzee Manoni,? kusikia lile jina nilishtuka na kuficha hofu yangu, Sabina aliendelea kuzungumza. ?Lakini mzee Manoni aliwakataza wasikufanye vile kutokana na wewe kuingia bila kujua. Ila alisema atakuonya usimwambie mtu yeyote , kama utakuwa mbishi basi watachukua uamuzi huo wa kukatisha maisha yako.? ?Kwani mzee Manoni ni nani katika hao unaowaita wachawi ?? Nilimuuliza. ?Ndiye mkuu wa kanda ya wachawi .? ?Alaa kumbe, ehe.? ?Basi wachawi ambao ni wakubwa sisi ni wanafunzi ambao tumeingizwa kwa shinikizo la wazazi. Wachawi wakubwa walikubaliana kukuwekea uangalizi wa karibu pindi utakapotoa siri ile basi lazima habari wangeitapa. Wangeitana na kutoa uamuzi wa awali wa kuyachukua maisha yako. Pale kwenu wapo watu ambao huwaoni lakini wapo kwa ajili ya kukusikiliza unazungumza nini na wazazi wako juu yetu. ?Lakini ilivyoonekana hukutoa siri nje muda wote ambao ulikuwa chini ya uchunguzi mkali. Tatizo kubwa lililowatibua wakuu wa uchawi ni siku ile uliyotuita sisi wachawi kibaya zaidi mbele ya wanafunzi. Baada ya kuwapelekea taarifa akiwemo mama yangu ambaye na yeye yumo kwenye kamati ya wachawi wa kanda ambao wapo chini ya mzee Manoni. ?Ilitolewa amri ya wewe uuawe mara moja, lakini kabla ya hapo siku ulipohudhuria sherehe ya sadaka ya nyama ya mmoja wa wanachama, siku ile ndiyo uliyopitiwa usingizi darasani na ulipoamka watu wa kwanza kutuuliza tulikuwa sisi na kitu kibaya nasi tulikuwa kwenye sherehe hiyo. Wasiwasi wetu ulikuwa lazima ungetoa siri kuwa ulituona kwenye ngoma ya kula nyama ya watu.? ?Sabina umeisha kula nyama ya watu?? Nilimuuliza...



    ?Shija huwezi kukwepa ukiingia kwenye chama kile.? ?Mmh haya, endelea? ?Lakini naomba Shija usinifikirie vibaya mimi kuwa na wewe ni mwanzo wa kuachana na kazi ile mbaya.? ?Nimekuelewa Sabina, ehe?? ?Basi siku tulipokuja shuleni tulielezwa yaliyokutokea na kitu cha ajabu hata aliyetupa habari alishangaa kwa kusema baada ya wewe kurudi darasani watu wa kwanza kuwauliza tulikuwa mimi na Helena. Kitu kile kilimshangaza hasa akizingatia siku nile hatukuwepo shule. ?Ndiyo maana tulikufuata kukuuliza sababu ya kutuuliza sisi, lakini ulitujibu kwa kiburi. Kwa hasira baada ya kuondoka tulijigeuza fisi ili tukutie adabu, lakini mzee Manoni alitokea na kutufukuza kisha alitufuata na kutukataza tusikufanye kitu chochote. Baada ya kutukataza alitueleza tuoneshe upendo kwako . Toka siku ile bila kujieleza nilitokea kukupenda Shija hata sijui ni kwa nini, kila nilipolala nilikuota hata Helena nilimueleza. Tulikubaliana kuonesha mapenzi mazito kwako huku nafasi ya nani awe na wewe akaniachia mimi. Kumbe hata Helena naye alikuwa akikupigia mahesabu. Hapo ndipo nilipopata kichaa cha mapenzi mtoto wa kike na kuamua kujiweka wazi mbele yako. Mpaka siku moja nilikuibia kiazi nyumbani na kukuletea, wakati nimejiweka wazi mbele yako na kunipokea na kujikuta nikiingia dunia nyingine ambayo japo kwa umri wetu ni kosa. ?Lakini bado niliamini hakuna moyo unaopenda huku unatambaa kwa vile kina mwanadamu aliyebalehe na kuvunja ungo alikuwa tayari ana matamanio ya mwili vile vile moyo wa kupenda kama mtu mzima. Penzi langu kwako kama mama angejua basi angenifanya kitu kibaya. Nataka nikupe siri hii kumbe yale maneno ya kutuambia sisi wachawi yaliwaumiza wengi akiwemo mama yangu mzazi na baadhi ya wachawi wengine. Na kitu kikubwa alichokitaka kwako ni kukutia uchizi au akuulie mbali, na siri hii ilikuwa ya watu wachache ambao walimficha mzee Manoni ambaye siku zote alikutetea wasikudhuru. Baada ya kumaliza tofauti zetu na 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kumueleza siku hizi tumekuwa marafiki mama alifurahi. Sikujua kumbe furaha yake ilikuwa ya kinafiki, siku ile nilipokuletea kiazi nilipofika nyumbani nilimueleza jinsi tunavyoelewana kiasi cha kukuletea kiazi. Alionesha kufurahi kumbe moyoni alikuwa na dhamira mbaya sana kwako , juzi usiku mama pamoja na wanawake wenzake wa kundi la wachawi waliniita na kuniweka chini kunipa mpango mbaya wa kukumaliza. Niliwashangaa kupanga mpango ule bila kuona kosa lako, niliwauliza kosa lako nini walijibu sitakiwi kujua, nilinyamaza kimya kuwasikiliza bila kujua wewe ni mpenzi wangu. Walinipa dawa ambayo walitaka nikuwekee kwenye viazi ambacho nitakuletea tukiwa shuleni, sikutaka kuwabishia lakini sikuwa tayari kufanya vile labda wakati tukiwa maadui. Basi baada ya kunipa vile vitu nilivichukua na kwenda kuvitumbukiza chooni bila wao kujua. Viazi navyo nilivitupa njiani wakati wa kuja shule, usiku nilipokutana na mama aliniuliza nilikupa nilikubali. Waliamini usiku wa kuamkia leo usingeuona, lakini siri nilibakia nayo moyoni bila kukueleza chochote. Siku ya pili niliporudi nyumbani niliulizwa kama umefika shule niliwajibu ndiyo umefika. Niliwaona wakichanganyikiwa kwa kuamini dawa waliyokulisha haikufanya kazi, baada ya kuona mpango wao wa awali umeshindikana walijipanga upya kwa ajili ya kukuangamiza. Nataka nikueleze kitu kimoja, usikubali kula kitu chochote utakachopewa na mtu si shuleni si njiani. Wanaweza kumtumia mtu mwingine, hata rafiki yangu Helena kwa sasa usimuamini kabisa kwa vile anaweza kushirikishwa na kukubali kukuangamiza. Nakuomba kwa hilo uwe makini sana.? Baada ya kuzungumza kwa muda mrefu alimeza mate, wakati huo nilihisi mwili ukinitetemeka kwa hofu na jasho lilinitoka. Lakini kwa nje nilionekana nipo sawa kama mtu niliyekuwa nikifunuliwa ufunuo wa mambo yaliyojificha . Baada ya kumeza mate aliendelea. ?Basi Shija upo katika wakati mgumu wa vita ya chinichini ambayo mzee Manoni hajui na kama angejua angewapa adhabu kali wote wenye njama mbaya kwako . Shija kuna kitu kingine ambacho kilikuwa kikiniumiza sana akili yangu lakini naamini leo nikikueleza huwezi kuamini.? ?Kipi hicho tena?? nilimuuliza. ?Japo roho itakuuma lakini naomba usimwambie mtu hata wazazi wako.? Sabina ana siri gani nzito anayotaka kumueleza Shija?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kipi hicho tena Sabina?? ?Kuhusu kaka yako.? ?Kaka yangu yupi?? ?Kuna mwingine zaidi ya Luhemeja.? ?Luhemeja! Si ameishakufa kitambo, una habari gani zake?? ?Wewe unajua kaka yako amekufa?? ?Ndiyo.? ?Basi kaka yako hajafa.? ?Hajafa!?? Nilishtuka kusikia vile. ?Ndiyo.? ?Utani huo Sabina hajafa vipi mtu nimemshuhudia mwenyewe akizikwa .? ?Ni kweli yote uliyashuhudia lakini ilikuwa kiini macho.? ?Mmh, mbona sikuelewi?? ?Ni vigumu kunielewa, kilichofanywa kwenu ni kiini macho kumpoteza kaka yako machoni kwenu ili aonekane amekufa.? ?Kama hajafa yupo wapi?? ?Yupo nyumbani kwao Helena.? ?Nyumbani kwao Helena?? ?Eeh, ila ni siri ambayo hakuna anayeijua zaidi ya wachawi wenyewe .? ?Mungu wangu nyumbani kwao Helena anafanya nini?? ?Amegeuzwa mwitunga (msukule) kazi yake ni kuchunga ng?ombe pembeni ya ziwa.? ?Mungu wangu, na muda aliopotea alikuwa wapi?? ?Alikuwa hukohuko, waliogopa kumchukua moja kwa moja kwa kuhofia kutafutwa na siri yao kuvuja ndiyo maana walimrudisha ili wamchukue.? ?Wampeleke wapi?? ?Kwenye kazi yake ya kuchunga ng?ombe.? ?Naweza kwenda kumuona?? ?Unaweza lakini lazima tufanye kwa siri sana wakikugundua watakumaliza.? ?Mbona alirudi bila kuzungumza na mtu na kuingia chumbani kwake ?? ?Wakati ule anarudi kwenu hakuwa Luhemeja bali kivuli chake ndiyo maana hakuzungumza na watu. Aliingia chumbani ili mjue amerudi waliamini hamtamuuliza hadi asubuhi ambapo mngemkuta ameishakufa.? ?Mmh, inatisha.? ?Pia kuna siri moja ambayo familia yenu hamkuijua mapema, kuitwa kwako mchawi kulitokana na mpango wa chinichini uliopangwa bila ninyi kujua ili watu wafiche madhambi yao. Lakini walikuwa na lao jambo, na kuharibika kwa akili kwa kwa kaka yako si bangi bali mchezo wa wachawi walimfanya vile ili waweze kumchukua kwa urahisi. ?Chanzo cha yote ni tatizo ni ugomvi wa shamba kati ya wazazi wako na wazazi wa Helena, baada ya baba yako kushinda kesi ya shamba walilokuwa wakigombea. Mama Helena aliapa kulipa kisasi nacho ni kumchukua mtoto mmoja kumgeuza mfanyakazi katika mashamba yake. Si kaka yako tu kuna vijana wengi waliofariki kijijini na kujulikana wamekufa , lakini ukweli wote wapo pamoja na watu wengine ambao wametoka sehemu mbalimbali za wilaya yetu wapo kwao na Helena kazi yao kubwa ni kufanya kazi mbalimbali kama kulima na kuchunga ng?ombe. Hujiulizi ng?ombe wote wale nani mchungaji wao? Au shamba lile lote nani anayelima? Basi ni kaka yako na wenzake, lakini nakuomba suala hili usimwambie baba au mama yako itakuwa vita ambayo nina wasiwasi pengine wanaweza kumuua kabisa. Ila nakuahidi kukusaidia kumrudisha.? Mmh, nilishusha pumzi na kuzipandisha, nilihisi kuchoka, nilimuangalia Sabina na kuamini kweli ananipenda nami lazima nioneshe upendo kwake . Siri aliyoniambia ilikuwa nzito sana ambayo mzee Manoni ndiyo aliyoiogopa mimi kuitoa kwa watu. Baada ya Sabina kutulia alinitazama kama ananishangaa, nilimuuliza. ?Nini chaanzo cha wewe na Helena kuingia katika uchawi wakati bado ni wasichana wadogo?? ?Shija siyo mapenzi yetu bali shinikizo la wazazi huku tukitishiwa kama tungekataa basi tutatolewa kafara na nyama yetu kuliwa katika kikao cha wachawi . Tuliogopa na kukubali, mwanzo kweli tulifanya kwa kulazimishwa lakini siku zilivyozidi kwenda tulijikuta tukizoea na kuifurahia kazi hiyo. ?Hata siku ya kuja kumchukua kaka yako nilikuwa na Helena.? ?Na mwalimu Veneranda naye mchawi?? ?Kwani kwenye ngoma hukumuona?? ?Nilimuona.? ?Basi naye ni mwanachama mkubwa sana. ? ?Mbona hafanani?? ?Kwani mimi ukiambiwa mchawi utakubali?? ?Siwezi kukubali.? ?Basi huwezi kumjua mchawi kwa kumtazama tu labda uwe mganga au mchawi kwa vile wachawi tuna alama zetu. Ukimuona tu utajua huyu mwanachama.? ?Na wote niliowaona kwenye ngoma ni wachawi?? ?Shija mbona hukumuona baba au mama yako, kila aliyekuwepo ni mchawi.? ?Sasa kwa nini nilipelekwa kwenye mkutano wa wachawi .? ?Hizo ni dalili siku moja utakuwa mwanachama.? ?Mungu wangu, sikubali.? ?Lazima utakubali, utaulizwa uchague kifo au kuwa mwanachana.? 

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mbona kuna wengine wapo katika jumuia ya kanisa na kuonekana wacha Mungu wakubwa ?? ?Hapo ndipo ujue atakayeurithi ufalme wa mbinguni hajazaliwa.? ?Na kwa nini mwalimu amejiingiza kwenye kazi ile?? ?Mmh, kwa kweli sijui, Lakini Shija unajua mwalimu Vene huingia darasani na kufundisha uchi?? ?Uchi?? kauli ile ilinishtua. ?Bila nguo yoyote mwilini huwa kama alivyozaliwa .? ?Mmh, mbona sijamuona.? ?Nasema kama si mchawi au mtaalamu wa mambo hayo huwezi kuona.? ?Wewe huwa unamuona?? ?Ndiyo, hata Helena.? ?Sasa ninyi si watoto wadogo kwa nini anakaa uchi mbele yenu.? ?Shija ulipokuja kwenye ngoma nani ulimuona kavaa nguo kama sio wewe peke yako?? ?Mmh, kweli wachawi hawana aibu.? ?Tena hawajui vibaya , unataka siku moja na wewe umuone?? ?Ndiyo, nitaweza?? ?Utamuona, ila nakuomba kitu kimoja usioneshe kushtuka tulia kama hukuona kitu.? ?Mmh, nitaweza?? ?Basi siwezi kukupa dawa ya kumuona.? ?Hapana nitajitahidi.? ?Basi kesho tukikutana shuleni nitakupa dawa ya kumuona mwalimu Vene anavyomwaga radhi.? ?Hakuna tatizo, Sabina muda umekwenda kiza kimeingia na tunaporudi ni mbali, tufanye tuondoke,? nilimshauri Sabina kutokana na kiza kuanza kuingia. ?Hakuna tatizo mpenzi, nakuomba nipo chini ya miguu yako, japo sikupaswa kutoa siri ya wachawi na nikigundulika ni kifo. Kama utakosa uvumilivu basi kifo changu wewe ndiye utakayesababisha.? ?Sabina moyoni mwangu kuna siri nzito ambayo itaungana na hii ambayo ni nzito yahitaji msaada wa haraka wa kumkomboa kaka yangu.? ?Tusifanye haraka tukikosea tumempoteza au tukimtoa bila kujipanga vilevile tutampoteza.? Baada ya kukubaliana tulirudi nyumbani wakati huo kiza kilikuwa kimetanda, tulirudi nyumbani njiani nilimuuliza. ?Vipi kwenu ukichelewa hugombezwi?? ?Nagombezwa, kwenu vipi?? ?Najua kutakuwa msala, kumbe ule ugomvi wetu wa siku ile baba alikasirika na kutaka kunipiga lakini alinikanya nisipigane tena na niwe mtoto mzuri.? ?Sasa utamwambiaje?? ?Nitajua cha kumwambia hilo usihofu kwa mganga hakuishi nyimbo.? ?Mmh, Shija kwa Kiswahili sikuwezi.? ?Tunajifunza tukitumie.? ?Asikubane ukatoa siri, elewa utakuwa umenimaliza,? Sabina alizidi kunisisitiza. ?Siwezi kufanya hivyo na hata akinibana nitamdanganya lakini ulilonieleza litabakia moyoni mwangu.? Tulipofika njia panda tuliachana wakati huo kiza kilikuwa kimeishaingia, Sabina alielekea kwao na mimi kuelekea kwetu. Nilipofika nyumbani nilimkuta baba amekaa kwenye kiti chake akivuta sigara. Nilipomuona nilishtuka kitu ambacho baba alikiona. ?We Shija muda wote huu, unatoka wapi?? ?Nilikwenda kuwinda ndege baba, shikamoo.? ?Marahaba, ndege gani mpaka usiku wote huu, hujachota maji leo huogi?? ?Nitaoga yaliyopo kesho nitachota kabla ya kwenda shule.? ?Shija mwanangu nazungumza nini? Unafanya nini?? ?Samahani baba.? ?Basi kabadili nguo haraka.? Niliachana na baba na kukimbia chumbani kwangu kubadili nguo huku nikimshukuru Mungu kutoulizwa maswali magumu. Baada ya kubadili nguo nilikwenda kumsalimia mama aliyekuwa jikoni akipika. ?Shikamoo mama.? ?Marahaba Shija, ulikuwa wapi?? ?Mama nilipitia kuwinda.? ?Mpaka usiku?? ?Leo tu mama.? ?Kuwa makini inaonekana siku hizi utundu umekujaa.? ?Nitajitahidi mama.? ?Basi nenda ukaoge chakula si muda mrefu kitakuwa tayari.? Nilikwenda kuoga na kusubiri muda wa kula na baada ya kula nilipanda kitandani, usingizi ulikuwa mbali sana. Niliwaza mambo mengi niliyoelezwa na Sabina juu ya matukio ya uchawi yaliyoizingira familia yetu hasa uchu wa kuutaka uhai wangu bila kosa. Pia ugomvi wa mpaka wa shamba uliozua mtafaruku mkubwa wa watu kutoana roho. Nilijikuta nikitokwa na machozi kila nilipomkumbuka kaka yangu na mambo waliyomfanyia kwa kisingizio cha bangi. Nilijiuliza nitafanya nini mtoto mdogo kama mimi, mdomo wangu ulikuwa na makufuli mawili. La mzee Manoni na la Sabina ambalo ni zito lililoufanya moyo wangu kutetemeka kwa hofu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijiuliza maisha ya kaka yangu ya msukule ataishi mpaka lini, na msaada wa Sabina angenisaidia vipi kumtoa kaka yangu katika kifungo cha kuzimu. Uwezo wake kwa kweli ulikuwa mdogo kwani hakuwa na uwezo zaidi ya kuwategemea watu wakubwa . Niliamini msaada wa Sabina ungekuwa na nguvu kama mzee Manoni, uwezekano wa kunisaidia ungekuwa mkubwa sana. Lingine lililoniumiza akili ni kuhusu uhai wangu unaowindwa na kundi dogo la wachawi ambao wapo tayari kuhakikisha wananipoteza katika sura ya dunia. . Hata kama nilikuwa nimesema kuwa wao ni wachawi , sikuzungumza kwa kuujua huo uchawi zaidi ya kusema kwa hasira tu. Niliwaza mbona mzee Manoni alinielewa hakunipa adhabu yoyote wala kunikanya itakuwa wao, niliamini ule ulikuwa wasiwasi wao tu. Kama jaribio la kumtuma Sabina limeshindikana kwa uwezo wa Mungu bado wasiwasi wangu ulikuwa katika usalama wangu. Bado niliamini msaada mkubwa wa maisha yangu yapo kwa baba yangu. Lakini ningemueleza vipi wakati Sabina kaniomba chonde nisiiseme siri ile ambayo akijulikana yeye kasema basi nitakuwa nimeutoa uhai wake kwa wachawi wa kijijini. Na kukaa kimya nilikuwa nakaribisha matatizo makubwa, wazo la kwenda kumueleza mzee Manoni nililiona linafaa. Lakini bado swali lilikuwa lilelile nikimueleza nilitaka kuuawa na wachawi aliowakataza wasiniue, lazima ataniuliza swali nani kaniambia, nitamwambia nani kaniambia? Lazima atanitisha na kumtaja Sabina ambaye wasiwasi wangu ningempoteza kutokana na kuwa mtu muhimu sana kwa kipindi kile. Nalo niliamua kulikalia kimya kuongeza ukubwa wa mfupa kooni mwangu, ambao kwangu yalikuwa mateso mazito sana yaliyoniweka katika wakati mgumu. Suala la mwalimu kufundisha uchi kwa kweli sikukubaliana nalo japo Sabina alinihakikishia kesho yake angeniletea dawa ya kumuona mwalimu Vene akifundisha darasani bila nguo mwilini. Kuhusu kwenda kumuona kaka yangu Luhemeja, nilijiuliza kama nikimuona nitafanya nini? Nitaweza kuvumilia kumuona akichunga ng?ombe tukijua amekwisha kufa? Niliamini kabisa mwaka ule ulikuwa wangu, mwaka ambao katika maisha yangu ningeuita mwaka wa maajabu. Usingizi ulinipata majira ya saa kumi alfajiri baada ya kukesha kwa mawazo na kumsikia jogoo akiwika kuonesha kumekaribia kupambazuka. Asubuhi kama kawaida baba aliniamsha kuwahi shule, niliamka huku macho yakionekana kuvimba kwa usingizi. Nilitoka nje na kukutana na baba ambaye aliniangalia bila kusema kitu kisha alitikisa kichwa. ?Shikamoo baba,? nilimsabahi bila kumtazama. ?Marahaba.? Baada ya kuitikia nilimpita kwenda kunawa, nilipopiga hatua mbili baba aliniita. ?Shija.? ?Naam baba.? ?Una matatizo gani?? Kauli ya baba ilinishtua na kutulia dakika nzima kabla sijamjibu. ?Sina baba.? ?Mbona sikuelewi?? ?Kivipi?? ?Ni muda mrefu nakuchunguza kutokana na mwenendo wako, muda mwingi ukiwa peke yako unakuwa hapo kimawazo, huna furaha niliyoizoea mara nyingi umekuwa ukinikimbia na kukaa peke yako. Siku za nyuma ulipenda kunidadisi mambo mengi lakini sasa imekuwa tofauti, una tatizo gani?? ?Hapana baba nipo sawa.? ?Hapana niambie mwanangu inavyoonekana siku hizi usiku hulali.? ?Nalala baba.? ?Hapana hii ni mara ya tano nakuona ukiamka macho yamevimba kwa kukosa usingizi kitu kinachosababisha ulale darasani.? Mmh, maneno ya baba yalinifanya niwe katika wakati mgumu wa kumjibu. Kutokana na maneno yake ya kunifanyia uchunguzi ilionesha kabisa amegundua vitu vingi kwangu bila mwenyewe kujua. Niliona kuna maswali ataniuliza lazima ataninasa pengine akijua namdanganya anaweza hata kunipiga. Mara nyingi baba alinionya nijiepushe na uongo kwani ni adui mkubwa wa maisha yangu. Nikiwa bado natafakari cha 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kumwambia, alinisogelea na kusema huku akinishika kichwani. ?Shija mwanangu najua kifo cha kaka yako kimekuchanganya kwa kiasi kikubwa , umepoteza uchangamfu najua jinsi gani ulivyokuwa ukimpenda. Kifo ni kitu ambacho mwanadamu hawezi kukikwepa . Wote tutakufa la muhimu tukubaliane na kilichotokea, kaka yako amekufa la muhimu tuzidi kumuombea kwa Mungu apate makazi mema huko mbinguni.? Sikuamini kama baba atanivua zigo la mawazo la kumjibu juu ya maswali yake mazito. Kunieleza vile nilishusha pumzi baada ya baba kuamini mabadiliko yangu yanatokana na kifo cha kaka. ?Nashukuru baba kwa kunifariji.? ?Basi kanawe uwahi shule.? Nilikwenda kunawa na kubadili nguo kisha nilipitia vitu vyangu na kuwahi namba shule, njiani nilikutana na Sabina aliyeonesha alikuwa akinisubiri aliponiona alitabasamu huku akionesha kunishangaa. ?Shija una tatizo?? ?Hapana.? ?Au jana baba yako amekupiga?? ?Walaa, kwa nini unaniuliza hivyo ??? ?Unaonesha una tatizo.? ?Mbona nipo sawa.? ?Hapana Shija mtu yeyote akikuona atajua una tatizo uso umekuwa mzito unaonesha hukulala kabisa.?



    Ni kweli.? ?Tatizo nini?? ?Mawazo.? ?Ya nini tena?? ?Kwa yote uliyonieleza jana.? ?Shija utaharibu kila kitu, kukueleza umekuwa hivyo je, ukiona itakuwaje?? ?Sidhani kuna mtu atahoji kwa nini sikulala.? ?Basi pole sana.? ?Asante, vipi umeleta?? nilimwuliza. ?Nimeleta, lakini utaweza? Unanitia wasiwasi .? ?Nitaweza,? nilimhakikishia. ?Shija usifanye vituko darasani mwalimu akikugundua vita yenu itakuwa kubwa na pengine kuniponza mimi.? ?Nitajitahidi nina imani nitaweza.? ?Mmh, haya.? Tulikuwa ndiyo tunaingia eneo la shule na kengele ya namba iligongwa, tulikimbilia kuhesabu namba kisha kila mmoja alielekea kwenye eneo lake kufanya usafi. Baada ya usafi kengele ya msitarini ili iligongwa, tulijumuika pamoja. Wakati tunaelekea mstarini Sabina alinifuata na kunipa kikaratasi kidogo na kunieleza kwa sauti ya chini. ?Ndani kuna unga mweupe, paka kidogo chini ya macho yote utaona ya kuyaona.? Sikumjibu nilipokea na kukimbilia msitarini, baada ya ukaguzi tuliingia darasani. Kama kawaida walimu waliingia kwenye vipindi, kipindi cha mwalimu Vene kilikuwa cha tatu cha saa tatu na dakika ishirini mpaka saa nne wakati wa mapumziko. Kama kawaida aliingia darasani kwa macho yangu nilimuona amevaa nguo, nilimuona Sabina akinitazama. Nilijifanya simuoni, nilitulia kama hakuna kitu chochote. Kutokana na hofu yangu sikutaka kuiweka haraka kwa kuhofia kugundulika. Baada ya kuandika na kutuachia kazi, wakati anajiandaa kutoka kwa kutuambia tukusanye daftari, niliutoa ule unga uliokuwa kwenye karatasi na kujipaka kidogo chini ya macho. Mmh, kweli ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni, sikuamini niliyoyaona mbele yangu. Kama isingekuwa kujipaka dawa na kuelezwa nitakayoyaona ningepiga kelele. Mwalimu Vene alikuwa kama alivyozaliwa mkono wa kushoto alikuwa amejifunga hirizi kubwa nyeusi, mkononi alikuwa ameshikilia kitu kama kidole cha mtu. Shingoni alikuwa na kamba iliyokuwa imebeba kichwa cha mtoto mdogo. Moyo ulitetemeka na hofu ilinijaa, nilimuomba Mungu kimoyomoyo mwalimu aondoke mapema. Wasiwasi wangu Sabina aliuona na yeye nilimuona akiingiwa wasiwasi , pengine alidhani naweza kupiga kelele za mshtuko au mwalimu Vene kugundua nimemjua yupo uchi. Ili kukwepana na kile kilichokuwa mbele yangu, sikuangalia mbele tena mpaka mwalimu alipotoka. Kengele ya mapumziko ndiyo iliyoniokoa, baada ya kutoka nilihisi kichwa kizito, nilichoshukuru Sabina muda wote alikuwa karibu yangu kufuatilia kila kilichokifanya .Wakati wanafunzi wote wanatoka alikuja na kuniuliza. ?Vipi Shija?? ?Kichwa,? nilimjibu huku nikishika mkono kichwani. ?Vipi umeona?? ?Ndi..yo..o..o.? ?Pole sana, kanawe na maji utarudi katika hali ya kawaida.? ?


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kaniletee, naweza kukutana naye nje.? ?Si nilikuambia sasa unamuogopa.? ?Hapana hii kufuru.? ?Shija vipo vitu vingi utaviona yataka uwe na moyo mgumu.? ?Mmh, kweli yataka moyo wa ujasiri.? Sabina alinifuatia maji na kunawa uso, baada ya kunawa nilirudi kwenye hali ya kawaida. Pamoja na kurudiwa na hali ya kawaida, bado mazingira ya shule sikuyaelewa . Nilikwenda kuomba ruhusa kurudi nyumbani kusingizia naumwa, kwa vile haikuwa tabia yangu waliniruhusu. Sabina alijitolea kunisindikiza japo wanafunzi walimwita wifi na wengine shemeji. Nilijua nini alichokifanya Sabina alinisindikiza hadi nyumbani. Njiani aliniuliza ninavyojisikia . ?Vipi Shija unajisikiaje?? ?Hata sijielewi.? ?Si nilikuambia?? ?Ni kweli, lakini ni mshtuko tu kwa leo nisingeweza kusoma tena labda kesho.? ?Basi kuna dawa nitakuletea ukiinywa itakutia ujasiri kila kitu atakachokiona utakiona cha kawaida. Sitakupeleka kwa kaka yako mpaka nikupatie hiyo dawa.? ?Nitashukuru.? ?Wacha nikufuatie sasa hivi kwa vile wazazi wapo shamba.? Sabina aliondoka na kuniacha nikiwa nimejipumzisha na yeye kukimbia kwao, baada ya robo saa alirudi. Alikuwa na dawa nyeusi ya unga ambayo niliikoroga kwenye maji na kuinywa kisha alinipa kipande kidogo cha ngozi sikujua ya mnyama gani ambayo alinieleza hata yeye hakujua ni ya mnyama gani.



    Ajabu baada ya Sabina kuondoka nilijikuta narudi kwenye hali ya kawaida maumivu ya kichwa yalitoweka . Niliamua kujilaza kwa vile sikuwa na la kufanya muda ule, usingizi nao haukuchelewa kunichukua. Sauti ya Sabina ilinishtua usingizini na kunifanya ninyanyuke kitandani. Nilipotoka nje nilimkuta Sabina akiwa katika mavazi ya nyumbani kuonesha amekwishatoka shule. ?Vipi umeishatoka shule?? ?Mmh, mbona muda mrefu.? ?Kwani muda huu ni saa ngapi?? ?Karibia saa kumi na moja.? Nilikwenda jikoni na kuchukua viazi ambavyo nilikula na Sabina kisha tuliondoka pamoja kupitia njia ya kwenye vichaka na mashamba ya watu kuelekea ziwani kwenda kumuona kaka yangu. Pamoja na Sabina kunihakikishia kumuona bado sikuamini. Ilitokana na kushuhudia kifo cha kaka yangu hata mazishi yake, muda ulikuwa umekwenda sana ilikuwa inakimbilia saa kumi na mbili na nuru ya anga ilianza kutoweka taratibu kuukaribisha usiku. Tulivuka maeneo ya watu na kuingia kwenye mashamba ya mpunga. Baada ya kuvuka mashamba ya mpunga tuliingia kwenye matete maji yaliyokuwa mengi na kuingia mpaka ziwani kando ya ziwa, woga ulianza kunitawala kutokana na eneo lile kuwa tulivu huku sauti za mawimbi zikisikika. ?Sabina huogopi humu tunaweza kukutana na wadudu wakali?? ?Shija usihofu kitu, niamini. ? Baada ya kunieleza vile tuliendelea kukatiza kwenye matete maji kwa kuyakanyaga maji yaliyokuwa yakitufikia magotini. Nilishangazwa na ujasiri wa Sabina japo msichana mdogo. Tulitembea kwenye matete maji kwa muda huku tukikwaruzwa na majani yake. Baada ya kuyavuka matete hayo tuliingia kwenye maji na nguo zetu ambayo yalikuwa yanatufikia kifuani. Tulitembea ndani ya maji pembeni ya matete kuelekea mbele. Nilijiuliza tunaelekea wapi, Sabina alikuwa mbele yangu akitembea kuelekea mbele bila hofu yoyote , nijikuta naingiwa na wasiwasi na kujiuliza mbona maji yanazidi kwenda juu kwa vile yalikuwa ya tumbo na hatimaye yakafika mabegani. ?Sabina...,? nilimwita. ?Shiiii,? aliweka kidole mdomoni kuonesha ninyamaze. Nilinyamaza kimya nisijue kwa nini kaniambia vile, baada ya kunyamaza 




    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/kimya Sabina alisimama na kunishika mkono kunivutia kwake . Tulikuwa tumeyavuka matete na kufika kwenye majani yaliyokuwa yameota pembeni ya ziwa. Sabina alisita kidogo na kuonesha wasiwasi ; nilijiuliza kaona nini. Mara alinishika kichwani na kunizamisha chini, woga ulinitawala lakini nilitiii amri na kuzama chini ya maji. Tulitulia kwa muda kisha tuliibuka juu, nilitaka kuhoji. Lakini nilipotaka kusema kitu alinishika mdomo nisizungumze lolote. Kila alilofanya aliangalia mbele kama kaona kitu lakini mimi sikuona lolote. Mara alinishika mkono na kunivuta hadi nyuma ya matete maji, alijifuta maji yaliyokuwa yakimtiririka usoni na kusema... Usiondoke Tafadhari....!   



      ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog