IMEANDIKWA NA : GLOBAL PUBLISHERS
*********************************************************************************
Simulizi : Nitakufa Mara Ya Pili
Sehemu Ya Kwanza (1)
Katika familia ya watoto Matulanya wengi hakuwakupenda elimu hasa walionitangulia akiwemo kaka yangu mkubwa na dada zangu yupo aliyeishia darasa la pili mpaka leo hata kusoma hajui. Mwingine aliishia darasa la sita baada ya kupata ujauzito. Maisha tuliyokuwa tukiishi yalikuwa ya hali ya chini kutokana na ukubwa wa familia na udogo wa kipato... Kwa kweli tulitegemea kilimo na mifugo ambayo kwa kiasi kikubwa vilituwezesha kupata chakula na pesa za kimaendeleo. Kwa upande wangu nilijiona kama nabii fulani niliyeshushwa ndani ya familia ya mzee Matulanya. Naweza sema nilikuwa na tofauti kubwa na ndugu zangu wote walionitangulia na walionifuata. Toka nikiwa darasa la kwanza nyota yangu ilionekana, nilikuwa na uwezo mkubwa kuliko hata wanafunzi walionizidi umri. Shuleni sikupelekwa nilijipeleka mwenyewe kwani umri wangu ulikuwa mdogo sana, siku aliyopelekwa kaka yangu nami nilikuwepo. Kutokana na michezo ya watoto waliokuwa wamekwenda kuanza darasa la kwanza, nilivutiwa nayo na kung?ang?ania kubakia shule. Mwalimu aliamini ningeweza kushindwa kurudi siku ya pili kwa kumwambia mama aniache tu nikichoka nitarudi nyumbani. Siku hiyo nilishinda pale hadi muda wa kurudi nyumbani, siku ya pili nilikuwa wa kwanza kuamka kuwahi shule tofauti na kaka aliyetakiwa kuamka kwa vile yeye ndiye aliyekuwa muhusika mkuu. Mama alitaka kunikataza lakini baba alimwambia aniache kwa vile ile ilikuwa nguvu ya soda. Lakini siku zilikatika nikiwa mwanafunzi mwenye bidii na mdogo darasa zima, katika mtihani wa darasa la kwanza
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nilikuwa wa sita katika darasa la watu 45. Hiyo iliwashtua wengi hasa walimu ambao siku zote walinidharau kwa kuamini hasa kuandika kwangu nilisaidiwa na kaka yangu. Ajabu ilikuwa kaka yangu alikuwa wa thelathini mimi mdogo wake wa sita, ilikuwa kioja na kuwashtua watu wengi. Ukweli ulibakia pale pale katika mtihani wa kufunga muhula nilikuwa wa pili, nilizidi kujijengea heshima na kuwashangaza watu wengi. Kila penye zuri hapakosekani wabaya , watu walianza kusema eti kwetu wachawi tunatumia uchawi mimi kushinda. Hawakuchoka kuzusha kwa kusema kwa vile kaka yangu alionekana yupo yupo, walisema eti familia yetu tumemgeuza ndondocha ili mimi nionekane nasoma zaidi. Maneno yale nilipowapelekea wazazi wangu walinieleza niachane na maneno ya kunikatisha tamaa. Niliwasikiliza wazazi wangu kuanzia hapo nilianza kushika nafasi ya kwanza mpaka naingia sekondari. Nilichaguliwa kujiunga na sekondari ya kutwa. Nikurudisheni nyuma kidogo, tulipofika darasa la tatu, wakati mimi nashika nafasi ya kwanza kaka yangu alikuwa kifunga darasa yaani wa mwisho, imani ya uchawi ndani ya familia yangu ndipo ilipoanza kutawala na kuonekana wazi tunamtumia kaka yangu kama msukule ili mimi niwe na akili sana. Hawakuamini mtoto mdogo kama mimi kuwazidi akili watu wazima niliokuwa nao darasa moja. Kutokana na ufinyu wa akili iliyotawala vijijini vingi visivyojua elimu ni nini, waliamini mwenye umri mkubwa ndiye mwenye akili. Kila kona nilipotembelea niliitwa mtoto wa kichawi
Kitendo cha kaka yangu kushika mkia darasani huku akitaniwa na wanafunzi kwa kuitwa msukule aliamua kuacha kusoma. Pamoja na kupigwa na baba ikiwa ni pamoja na kunyimwa chakula, kaka yangu alikataa katakata kurudi shuleni. Baada ya wazazi kushindwa waliamua kumuacha afanye anavyo taka, tokea hapo kaka yangu alianza kupoteza mwelekeo kwa kuvuta bangi. Alikuwa nusu mwendawazimu , hali ya kaka yangu na maendeleo yangu shuleni yalitafsiriwa kama tumemgeuza kaka yangu ngazi ili mimi nionekane nina akili, kuzidi kutaniwa mtoto wa mchawi. Kwa kweli jina lile lilinikosesha raha hata kuogopa kutembea peke yangu wanafunzi wenzangu walinitania kwa kuniita mtoto wa mchawi. Nilimshukuru mwalimu mkuu ambaye aliwachapa wote waliniotania na wengine kuwapa adhabu kali. Ile kidogo ilisaidia kupunguza kutaniwa, haikuishia hapo nilitengwa kucheza na wenzangu kwa kuhofia kuwageuza mandondocha kama tulivyomgeuza kaka yangu. Maisha yangu ya shule yaligeuka subiri na kufikia hatua ya kuichukia shule. Bado mwalimu mkuu alikuwa chachu yangu ya mafanikio kwa kunifuata nyumbani na kuniomba nisife moyo. ?Shija mwanangu usife moyo, hizi ni imani potofu kuamini mwenye akili ni mtu mwenye umri mkubwa. Lakini nakuhakikishia kukupigania na kuwaelimisha, wewe ndiye roho ya shule utakayetubeba huko tuendako.? Nilikubaliana na mwalimu na kurudi kuendelea na shule huku mwalimu akiwalazimisha wanafunzi wenzangu wacheze na mimi. Mwalimu mkuu hakuishia hapo aliitisha mkutano wa wazazi na wanafunzi ambao ulifanyika siku ya Ijumaa jioni. Baada ya wazazi kukusanyika mwalimu mkuu alisimama na kuzungumza machache kisha aliniomba ninyanyuke . Baada ya kunyanyuka mwalimu mkuu aliwageukia wanafunzi wenzangu na kuwauliza. ?Wanafunzi.? ?Mwalimu,? waliitikia wote kwa sauti kubwa. ?Mnamjua huyu?? ?Ndiyoooo,? waliitikia wote. ?Nani?? ?Mchawiiiii.? Maneno yao yalitaka kuupasua moyo wangu na kujiona kama mchawi wa kweli aliyekamatwa mchana kweupe akiwanga. Nilimuona mama yangu akitokwa na machozi, baba naye uzalendo ulimshinda alikuja nilipokuwa nimesimama nikiwa nimeshikwa mkono na mwalimu mkuu na kutaka kunikwapua ili tuondoke. ?Mwalimu kweli umetuchoka yaani kutuita kote huku ni kuja kutudhalilisha?? ?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapana mzazi, ndiyo sababu kubwa ya kukuiteni hapa kutaka kuondoa dhana hii mbaya. Nakuomba ukae tafadhali sana.? Baba alikubali kukaa mimi nilikuwa bado nimesimama nimeshikiliwa mkono na mwalimu, sikujua mwalimu alitaka kufanya nini. Baada ya hali ya utulivu kurudi, mwalimu alisema kwa sauti ya juu; ?Ndugu wazazi nimekuiteni ili tusawazishe ili ambalo tusipoliangalia siku za mbeleni kijiji chetu kitakosa hata msomi mmoja. Nasema hayo nikiwa na maana gani? Kumekuwa na imani ambayo imejengeka toka kwa wazazi na kuipandikiza kwa wanafunzi kuwa hakuna mwenye umri mdogo kuwashida watu wazima ni uchawi. Ndugu zawazi nataka kuwaeleza Shija ni tunu tuliyotunukiwa wanakijiji, toka shule yetu ianzishwe hakuna kijana mwenye akili kama Shija. Ni Mungu ametutunukia msomi mwenye upeo mkubwa japo umri wake ni mdogo. Nayasema haya hasa nikizingatia ujaji wa Shija shuleni ulikuwa na tofauti kubwa na wenzake
Wanafunzi wengi wa kijiji chetu hawapendi shule, wamekuwa watoro mpaka watafutwe na fimbo. Lakini kwa Shija kuna tofauti kubwa, kijana mpenda shule mdadisi. Asichokijua huuliza tofauti na wanafunzi wengine. Hii imemsaidia sana Shija kufanya vizuri darasani. Mimi nafikiri uchawi wa Shija ni uwezo wa kujua mambo na kuyafanya kwa usahihi. Na si kushika tunguri nakuombeni muondoe imani potofu wazazi wa Shija si wachawi bali wana bahati ya kupata mtoto mwenye kipawa toka kwa Mungu na si kingine. Wazazi wenzangu nawaomba mumchukulie Shija kama kioo ili wanafunzi wenu nao wafanye vizuri, tuhahitaji akina Shija zaidi ya mia si mmoja. Tuliye naye mnamvunja nguvu. Narudia uwezo wa Shija darasani si uchawi bali kipaji alichopewa na Mungu, wafanyeni watoto wenu wawe karibu na Shija ili kupata alichonacho. Waswahili wanasema aliyekaribu na uaridi hunukia. Nataka leo mbadili kauli yenu nataka kuanzia leo mseme Shija si mchawi, haya kwa pamoja, Shija si mchawi.? ?Shija si mchawi,? walisema wanafunzi wote. ?Ni rafiki yetu.? ?Ni rafiki yetu.? ?Hatutamtenga tena Shija.? ?Hatutamtenga tena Shija.? ?Haya mwanafunzi mmoja mmoja anakuja kumkumbatia Shija huku akimwambia pole rafiki.? Wanafunzi wote walisimama katika mstari mmoja na kwenda kumkumbatia huku wakisema; ?pole rafiki?. Walipita wanafunzi wote na mwisho mwalimu mkuu aliwaeleza wazazi wampende na kumlinda kwani ni zao adimu shambani wakilipoteza ni vigumu kulipata. Baada ya kikao kile ambacho nilimshukuru mwalimu mkuu kwa kurudisha amani ya moyo iliyopotea katika familia yetu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimshukuru Mungu hali ya utulivu ilijirudia tena shuleni kwa wanafunzi kuniona kama mwanafunzi mwenzao kwa kushirikiana katika shughuli zote za ndani na za nje ya shule. Utulivu ule uliweza kunifanya nisome kwa utulivu. Wakati huo kaka alikuwa amegoma kabisa kuendelea na masomo, nilimuomba Mungu usiku na mchana ili kaka arudi shuleni. Lakini dua zangu zilikwenda bure kwani kaka alipolazimishwa kusoma kwa nguvu aliamua kukimbia nyumbani na kuamua kulala porini kitu kilichofanya wazazi na walimu waamue kumuacha. Katika masomo darasani niliendelea kuyamudu vizuri na mtihani wa kuingia darasa la tano nilishika nafasi ya kwanza. Nilimshukuru Mungu pamoja na kuzidi kuwaongoza darasani hakukuwepo na minong?ono tena ya uchawi zaidi ya kupongezwa. Palipo na wengi pana mengi hapakukosekana maneno ya chini, wapo ambao hawakuamini mimi kuwa na akili kiasi kile ni uwezo wangu mwenyewe na si uchawi. Katika akili zao kama nilivyokwishasema mwanzo, waliamini mtoto mdogo kama mimi siwezi kuwashinda watu wazima kama kaka zangu. Kwa umri na umbo nilitakiwa niwe darasa la pili, kama nilivyosema king?ang?anizi changu ndicho kilichonifanya niwe pale na uwezo wa akili yangu ndio uliomfanya mwalimu aniruhusu kuendelea kusoma. Ilikuwa kama kichekesho darasani kwa jinsi wanafunzi wakubwa walivyokuwa wamenizidi umbo na umri kisha mimi niwaongoze darasani katika masomo yote. Kibaya zaidi si kuwazidi kidogo bali kwa mbali sana, pamoja na ninong?ono ya chinichini bado haikuwa na nguvu sana kunikatisha tamaa, maneno mengi yaliongelewa chinichini. Rafiki zangu waliokuwa wamenitenga mwanzo upendo ulirudi kama mwanzo na kushirikiana nao kama kawaida kitu kilichonipa faraja kubwa moyoni mwangu na kusahau maisha ya mateso kwa kipindi kirefu cha kuitwa mtoto wa mchawi. Nakumbuka siku moja nikiwa nimelala nilisikia jogoo akiwika , nilishtuka usingizini na kutulia kitandani. Mara nilisikia sauti kama za watu wakipita huku wakizungumza. Mawazo yangu yaliniambia kumekucha, niliamka na kutoka nje ambako nilikuta kweli kumekucha kutokana na mwanga wake
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
sikuwa na haja ya kuangalia juu kujua ule mwanga wa jua au mwezi, hali ya nje ilijionesha kwa uwazi zaidi kila kilichokuwa mbali kilionekana. Niliamini ilikuwa ni asubuhi. Kutokana na kuona kumepambazuka muda mrefu, niliamini nimechelewa namba shule. Nilinawa maji harakaharaka kisha nilipitia kidumu changu cha lita tatu cha kubebea maji ya kumwagilia maua na ufagio kuwahi shule. Nilitembea kwa mwendo wa kukimbia kuwahi namba, ilikuwa kama ukichelewa namba lazima upigwe fimbo kabla ya kuingia darasani. Katika watoto walioongoza kuwahi namba mimi nilikuwa mmoja wapo, lakini siku ile nilijua ndiyo siku yangu ya kwanza kuchelewa. Nilitembea kwa haraka wakati mwingine nilikimbia kidogo kwa kuamini kabisa nimechelewa. Ajabu nilitembea njia nzima bila kuona mwanafunzi yoyote , kitu kile hakikuwa cha kawaida kukosekana mwanafunzi njiani hata walimu ambao huungia shuleni saa mbili. Hali ile ilionesha wazi nilikuwa nimechelewa sana. Nilianza kukimbia kuwahi shule. Kila hatua niliyopiga nilizidi kushangaa kuona mbona hata sauti za wanafunzi, shuleni kulikuwa kimya. Mpaka naingia eneo la shule sikuona mtu wala kusikia sauti ya mtu yoyote , nilijiuliza ina maana nimechelewa kiasi kile cha kukuta wanafunzi wote wameishaingia madarasani. Niliamini kama ni kweli lazima hata familia yangu imechelewa kwenda shamba, mara nyingi baba ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamka na kutuamsha watoto wake. Baada ya kuamka baba hutangulia shamba kisha mama humfuata baadaye. Mama baada ya kutuandaa sisi kwenda shule, humuandalia baba cha kudanganyia tumbo shamba na kwenda kuungana naye shamba mpaka jioni. Niliingia eneo la shule huku moyoni nikiwa nimeishaingiwa woga, shule nzima ilikuwa kimya kitu ambacho hakikuwahi kutokea toka nianze darasa la kwanza. Ukimya ule ulizidi kunizidisha hofu moyoni, ulikuwa ukimya wa ajabu. Lakini kila hatua niliyopiga nilihisi mwili kunisisimka na nywele kunisimama, nilipoangalia ndani ya madarasa sikuona mwanafunzi yoyote . Nilijiuliza wanafunzi wamekwenda wapi, nilipatwa na hofu kubwa moyoni mwangu na mwili kunisisimka. Kibaridi kilichokuwa kikisafiri muda ule kilinipiga mwilini na kuamini ubaridi ule si wa asubuhi bali usiku wa manane. Wazo la haraka lilikuja niangalie juu, nilinyanyua macho yangu juu kuangalia mbinguni na kukutana na mwezi wa saa tisa za usiku. Moyo ulinilipuka na kuanza kwenda mbio kwa hofu kunijaa moyoni, nyuma yangu nilisikia sauti za watu wakizungumza, nilipogeuka nyuma sikuona kitu. Nilijiuliza watu waliokuwa wakizungumza wapo wapi? Kwani sehemu waliyokuwa wakizumngumzia hakukuwa na kitu cha kusema nisiwaone. Mara nilisikia watu wakikimbia na vishindo vya watu waliokuwa wakikimbia vilipita karibu yangu lakini sikuwaona. Woga ulizidi na kujikuta nikitokwa na haja ndogo bila kupenda, ghafla nilisikia kelele za watu wakishangilia kwenye uwanja wa shule, mara ngoma zilianza kupigwa kwenye uwanja wa shule lakini sikuona kitu. Nilijikuta najiuliza ile ngoma ni kweli inachezwa kwenye uwanja wa shule au mlio wake unatoka mbali. Lakini akili yangu haikukubali hata kidogo mlio ulionesha unatoka kwenye uwanja wa shule japo wapiga ngoma na wachezaji hawakuonekana machoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijiuliza zile ni ngoma gani zinazochezwa usiku wa manane, wazo la kutaka nisogee uwanja wa shule kupata uhakika, nililipinga haraka kwani kila dakika ilivyokwenda ndivyo nilivyozidi kujaa hofu moyoni. Nikaona pale hapanifai niliondoka taratibu kurudi nyumbani. Kilichonishangaza kupita katikati ya uwanja wa shule bila kuona kitu chochote wala kusikia sauti, lakini nilipofika shuleni ngoma zilizokuwa zikipigwa na vishindo vya watu kucheza kusikika pale uwanjani vilizidi kuniweka njia panda. Kurudi na njia ile niliogopa nilitafuta njia ya kupita mbali na uwanja kwa kupitia kwenye majani kwa kuzunguka kutokea njia ya kuelekea nyumbani, nilitembea kufuata njia ya kurudi nyumbani huku nikitetemeka. Hofu iliyokuwa moyoni mwangu ni kwamba kitu chochote kingetokea mbele yangu na kunitisha, niliamni ningekufa palepale kwa presha iliyokuwa juu sana. Nikiwa narudi nyumbani huku nikitetemeka na kumuomba Mungu anifikishe salama, kwa mbali nilimuona mzee akija taratibu ameshikilia mkongojo. Nilitaka kukimbia. Wasiwasi wangu ulikuwa nikirudi nilipotoka huenda si salama kuliko kukutana na yule mzee. Nilisimama kama sanamu nisijue nifanye nini na wakati huo mzee yule alizidi kunikaribia. Lakini mwanga mkali wa mwezi ulinifanya nimfahamu, alikuwa mmoja wa wazee wa kijijini kwetu anayeheshimika, mzee Manoni.
Shija unatoka wapi usiku wote huu?? Mzee Manoni aliniuliza baada ya kusimama mbele yangu. ?Shu...shu...leni,? nilijibu kwa kubabaika. ?Shija shule gani ya usiku wa manane?? ?Nilifikiri kumekucha kumbe bado.? ?Umeona nini?? ?Sijaona kitu.? ?Umesikia nini?? ?Sauti za watu.? ?Umewaona? ?Hapana.? ?Ni hichohicho umesikia?? ?Na...na...ngoma.? ?Ngomaa?? ?Ndiyo.? ?Wapi?? ?Kwenye uwanja wa shule.? ?Ni kweli hukuona kitu chochote?? ?Sikuona babu.? ?Shija unakuwaje unasikia ngoma usione watu au ilikuwa haipigwi kwenye uwanja wa shule?? ?Hapana babu ilikuwa inapigwa kwenye uwanja wa shule.? ?Sasa mbona hukuona?? ?Labda wachawi .? ?Shija unaujua uchawi?? ?Hata!? ?Sasa mbona unasema wachawi bila kuwa na uhakika na unachokisema?? ?Nilisikia siku moja baba akisema wachawi huwa hawaonekani kwa macho ya kawaida ila unaweza kuwasikia .? ?Sasa sikiliza ulichokiona na kukisikia kiache huko huko sawa?? ?Sawa babu.? ?Narudia tena ukiisema siri hii kwa mtu yeyote utapatwa na jambo zito.? ?Hata mama nisimwambie? ?Siyo mama yako tu, hata baba yako, ulichokiona na kukisikia kiache huko huko, nenda nyumbani ukalale hutadhuriwa na kitu chochote.? ?Sawa babu.? ?Usisahau niliyokueleza sawa babu?? ?Sawa babu simuelezi mtu yeyote .? Niliagana na mzee Mamoni na kuelekea njia ya nyumbani, baada ya kutembea hatua nne kwa woga niligeuka nyuma kumuangalia mzee Manoni anaelekea wapi. Wasiwasi wangu huenda akaelekea kwenye ngoma ile ambayo niliamini kabisa ilikuwa ya wachawi . Kingine kilichonishangaza mzee Manoni usiku mkubwa kama ule alikuwa akienda wapi na kwa nini hakuonesha wasiwasi japo usiku ulikuwa mkubwa sana. Ajabu nilipogeuka babu sikumuona, nilijiuliza amekwenda wapi, eneo lote lilikuwa wazi hata angebadili njia bado ningemuona. Nilijiuliza babu ile kasi ya kutembea na kupotea alipata wapi? Sikutaka kumfikiria sana nilikaza mwendo kuwahi nyumbani. Nilipofika nyumbani kulikuwa kimya kila mtu alikuwa amelala, kwa vile chumba chetu watoto wa kiume kilikuwa cha uani, niliusukuma mlango na kuingia chumbani kwangu bila mtu yeyote kujua kama kuna mtu alitoka. Baada ya kuingia ndani nilivua nguo zangu za shule na kupanda kitandani. Nilipatwa na usingizi wa ajabu, na kujikuta
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nikiota ndoto ya kutisha, eti nimeamka usiku toka nyumbani kwenda shuleni. Nilipofika uwanja wa shule nilikuta kuna ngoma ya watu waliokuwa wakicheza uchi wanawake kwa wanaume. Katika ngoma ile hakuna aliyenijali walicheza kwa mtindo wa kuzunguka mduara huku wengine wakiwa wamepanda wanyama ambao sikuwahi kuwaona. Wengine walirusha mioto juu bila kuungua kweli ilikuwa sherehe kubwa sana. Katika kundi la watu wale waliokuwa wakicheza uchi walikuwemo watu ninaowafahamu akiwemo mzee Manoni na baadhi ya wazee wa kike na kiume waliokuwa wakiheshimika sana pale kijijini. Pia walikuwepo wasichana wadogo ambao baadhi yao tulikuwa tunasoma nao shule moja na wengine darasa moja. Kulikuwa na mgao wa nyama ambayo sikujua ilikuwa ya nini, ila kila aliyenyakua kipande cha nyama iliyokuwa mbichi ikivuja damu aliibugia mdomoni na kuitafuna huku akizunguka na kucheza kwa furahi
Kilichonishangaza si ngoma bali watu wote kucheza uchi bila aibu ya wakubwa na watoto, wanawake kwa wanaume wote kucheza bila kujali utupu wao. Sauti kali ya baba kuniamsha kujiandaa kwenda shule ndiyo iliyoikata ile ndoto ya kutisha. Ilikuwa kawaida alfajiri anapoamka kwa ajili ya kwenda shamba. Ilikuwa kawaida ya baba kabla ya kwenda shamba kutuamsha tujiandae na shule, nilishtuka na kujikuta mapigo ya moyo yapo juu na jasho jingi kunitoka. Sikuitikia haraka nilinyanyuka na kukaa kitako kuangalia pande zote ili kupata uhakika nilikuwa naota au kweli. Sauti ya baba nje iliendelea kuniita, lakini kutokana na hofu iliyokuwa imenitanda moyoni. Sikuamini kama kweli ni sauti ya baba yangu au bado nipo ndotoni, nilijiuliza yote yaliyotokea ilikuwa ni ndoto au kuna lenye ukweli wowote , macho yangu yalitua kwenye nguo zangu za shule ambazo nilizivua jana yake na kuamini kweli niliamka usiku. Baada ya baba kuniita bila kuitikiwa kwa muda alisukuma mlango na kuingia ndani, alinikuta nimekaa kitandani nikiwa bado nimeshangaa kama mtu aliyepigwa bumbuwazi. ?Shija vipi leo huendi shule? ?Nakwenda,? nilijibu kwa mkato. ?Mbona bado umekaa kitandani?? Sikumjibu kitu nilitelemka kitandani kwenda kunawa ili niwahi shule, kila kona ya mwili ulikuwa umechoka sana. Baada ya kumsalimia baba nilipitia kikopo cha maji kwenda kunawa. ?Shija,? baba aliniita. ?Naam baba.? ?Mbona mwili wako unamikwaruzo hivyo ?? Nilijitazama na kujikuta nimekwaruzwa sehemu za tumboni miguuni na chini miguu ilionesha ina matope. Nilikumbuka jana nilipowakwepa wachawi wakicheza ngoma na kuingia kwenye majaruba ya shule kabla ya kukutana na mzee Manoni. ?Shija mbona upo hivi umejikwaruza pia miguu ina matope, umeanza kuwa mchafu kulala bila kuoga?? Nilipotaka kumjibu, nilikumbuka kauli ya mzee Manoni nisimueleze mtu yoyote juu ya mambo niliyoyaona na kuyasikia usiku ule. Nilijifanya simsikii na kwenda kunawa ili niwahi shule, nilishukuru baba aliachana na mimi na kuelekea shamba. Baada ya kunawa nilipitia vifaa vya shule, dumu la maji na fagio kisha nilikimbia shule. Mara nyingi muda aliokuwa akituamsha baba hata ukienda kwa mwendo wa taratibu shuleni unawahi namba. Hali ya asubuhi ilinionesha kweli ile ndiyo asubuhi sahihi sio niliyoamka usiku. Hata wanafunzi walionekana mmoja mmoja njia niliyopita, sikutaka kujisumbua kuwaza kuamka kwangu usiku wa manane na vitu nilivyokutana navyo pamoja na njozi nilizoota zenye kukaribiana na ukweli ambazo nilikatazwa kumuelezea mtu yoyote na mzee Manoni
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilihamishia mawazo yangu shule kuwaza masomo hasa somo la jiografia ambalo jana yake nilikosa maswali mengi tofauti na nilivyojiamini kwa kuyaona maswali mepesi. Sikutaka kuumiza akili yangu kuwaza nilioyaona na kukutana nayo, kwani niliamini hata kama nisingekatazwa bado hakuna mtu angeniamini na kuniona mtu niliyekuwa nikiona ndoto na vitu visivyo na ukweli. Kingine nilichokiogopa ni kuonekana mchawi wa ukweli kuyasema mambo ya usiku watu wamelala. Nilitembea kwa mwendo wa kawaida kwa kuamini bado sijachelewa kutokana na wanafunzi wengi kuonekana kutembea bila wasiwasi wowote . Nilipokaribia uwanja wa shule nilianza kusikia mlio wa ngoma niliyoisikia usiku iliyokuwa ikipigwa palepale uwanjani. Lakini nilipokaribia sauti ile ilipotea akilini taratibu na mwisho wake ilipotea kabisa. Nilifanikiwa kuwahi namba, baada ya kuhesabu namba nilikwenda kwenye eneo langu kufanya usafi na kumwagilia maua. Baada ya usafi ilipigwa kengele na wanafunzi wote tulikusanyika kwa ajili ya usafi, baada ya usafi muda wa kuingia darasani ulipofika tuliingia madarasani. Nilipoingia darasani nilikwenda kukaa kwenye dawati langu. Dawati nililokuwa nakaa lilikuwa la wanafunzi wawili . Kutokana na uwezo wangu darasani, katika dawati nilikuwa nakaa na mtoto wa mwalimu mkuu wa kike. Japo hakuwa na akili sana lakini tulisaidiana japo sehemu kubwa ya masomo alinitegemea mimi. Ajabu ilikuwa baada ya mwalimu kuingia darasani, tulimsalimia vizuri kama kawaida alituruhusu tukae chini . Baada ya kukaa chini mwalimu wakati anaanza kufundisha somo lake, nilipitiwa na usingizi mzito uliopelekea niote yote niliyoyaota jana yake baada ya kurudi kutoka shuleni baada ya kuamka muda usio wa kawaida. Ilikuwa ndoto nyingine iliyonipeleka tena kwenye ngoma ya wachawi , ilikuwa ajabu ile ngoma haikuwa tena kwenye uwanja wa shule. Ilikuwa chini ya mti mkubwa, ngoma ilikuwa imepamba moto kila mtu kucheza anavyojua . Watu walikimbia na fisi na wengine kupaa na kutua na ungo. Mara moja sikujua sherehe ile inahusu nini kwa wachawi kufurahi namna ile, kitu kingine kilichonishtua kwenye njozi yangu ilikuwa kumuona mmoja wa walimu wetu naye akiwa anacheza ngoma ile huku vumbi likiwa kubwa sana. Kutokana na vumbi kubwa kutimka nilijikuta nikiingiwa na vumbi mdomoni na puani na kusababisha nikohoe mfululizo. Kumbe kukohoa kwangu ndiko kulikowashtua wanafunzi na mwalimu darasani kuwa nimelala, hata mwalimu alipokuja bado nilikuwa nimelala sijitambui. Kila walivyoniita sikuweza kuwasikia , nililala juu ya dawati huku nikiendelea kukohoa sana. Walinichukua na kunitoa nje na kuniweka chini ya mti wenye hewa. Mwalimu aliwaeleza wanafunzi waliokuwa wamepagawa na hali yangu, waniache nipigwe na upepo huku akiwekwa msichana mmoja pembeni yangu aniangalie.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Njozi yangu iliendelea hadi kulala na kuamka siku ya pili kwenda shule ndipo niliposhtuka na kujikuta nimelala chini ya mti. Pembeni yangu alikuwepo msichana aliyekuwa amenipa mgongo, kwa vile nilimfahamu nilimwita. ?Leti,? alishtuka na kunikuta nimekaa kitako. ?Haa! Shija!? ?Vipi?? ?Mmh, hata siamini, kwani ulikuwa ukijisikiaje?? ?Kivipi, kwani hapa nimefikaje?? ?Wenyewe tulishtuka tukiwa darasani ulipokohoa mfululizo. tuliposogea na mwalimu, tulikuona umelala, hujitambui hata tulipokubeba kukutoa nje bado ulikuwa hujitambui.? ?Mungu wangu.? ?Kwani ulipatwa na nini Shija?? ?Hata najua!? Nilikumbuka masharti niliyopewa na mzee Manoni ya kutokusema kitu chochote nilichokiona wala kusikia. ?Pole sana.? ?Asante.? Tulinyanyuka kuelekea darasani, mwili wote ulikuwa umechoka sana japo ilikuwa ndotoni lakini niliamini kutokana na ngoma ya kichawi niliyocheza. Nilipoingia darasani wote walishtuka, wakaja kwenye dawati langu kunipa pole huku wakitaka kujua nilipatwa na kitu gani, kwani toka nianze shule sijawahi kutokewa na hali kama ile, si mimi hata wanafunzi wenzangu, hakuna aliyewahi kukumbwa na sakata kama langu. Nikiwa darasani nilipepesa macho kuwatafuta wanafunzi ambao niliwaona kwenye ngoma ya wachawi , nilipowakosa niliuliza. ?Jamani Sabina yupo wapi?? ?Leo hatujamwona.? ?Helena?? ?Mmh, hata yeye leo hajaja shule.? Majibu yale yalinishtua kidogo kutokana na njozi niliyoota muda mfupi na kukosekana kwa wale wasichana. ?Shija, kwani vipi! Mbona unawaulizia hao?? ?Hata, basi tu, maana wote nimewaona kasoro wao.? Mwalimu aliyeshuhudia tukio lile aliniita ofisini kwake na kunihoji juu ya mkasa ulionikuta. ?Shija upo sawa?? ?Nipo sawa, ila nahisi uchovu.? ?Jana umelala saa ngapi?? ?Kama kawaida baada ya kula tuliingia chumbani kulala.? ?Saa ngapi?? ?Saa tatu mwalimu.? ?Kweli?? ?Kweli mwalimu.? ?Unaweza kunieleza nini kilikutokea darasani kilichosababisha ulale na kupoteza fahamu?? Nilitulia kidogo kabla ya kumjibu huku nikiyakumbuka maneno ya mzee Manoni, nilitikisa kichwa kama ishara ya kukataa kuwa, siwezi kumwambia. ?Kweli mwalimu sikumbuki chochote.? ?Ni hali gani ilikutokea kabla ya kupoteza fahamu?? ?Mwalimu kusema kweli wakati unaingia darasani na kutwambia tukae chini, ghafla usingizi mzito ulinijia, kilichoendelea sikijui mpaka nilipojikuta nimelazwa chini ya mti.? ?Ooh, pole sana.? ?Asante.? ?Unasema mwili unajisikiaje?? ?Nimechoka sana, kama nilikuwa nalima.? ?Basi itakubidi urudi nyumbani ukapumzike, lakini usisahau kuwaeleza wazazi wako kilichokutokea, sawa?? ?Sawa mwalimu.? Kabla ya kutoka, nilimuulizia mwalimu yule niliyemwona kwenye ngoma ya wachawi .
Mmh, aliomba ruhusu toka juzi, lakini kesho atakuwepo, kwani vipi?? ?Hapana, ila sijamwona tokea jana.? ?Kweli upo makini, wanafunzi wengine wapo hawajui nini kinaendelea shuleni.? Nilitoka ofisini huku walimu wengine wakiniuliza maswali mengi juu ya tukio lile lililowashtua wengi. Kilichonishtua zaidi kilikuwa ni kukosekana kwa wote niliowaona kwenye ngoma ya wachawi . Nilibaki na maswali mengi, kuna ukweli gani katika njozi zangu na matukio ya kweli. Wengi waliamini huenda nachelewa kulala, niliomba Mungu wote waamini hivyo kuliko tofauti, kwani wangeniweka kwenye wakati mgumu na mzee Manoni. Baada ya
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kuniuliza na kuwajibu ya uongo nilirudi nyumbani taratibu huku nikijiuliza kule, wazazi wangu nitaanzaje
kuwaeleza kilichonitokea shuleni? Wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa kwa baba, kama ningemweleza uongo, akanibana kwa maswali na kujikuta nasema ukweli ambao ungegharimu maisha yangu. Njiani kama kawaida, nilikutana tena na mzee Manoni ambaye sikumwona alipotokea ila ghafla alisimama mbele yangu. Nilishtuka sana na kutaka kutimua mbio, lakini miguu ilikuwa mizito kama imefungwa mawe. Aliniangalia kwa muda bila kuniambia kitu, ikabidi nijifanye natazama chini kwa aibu na woga, mwili ulinitetemeka kwa hofu. ?Shija,? aliniita. ?Abee babu,? nilijikuta nakosea kuitikia kwa woga. ?Shija wewe mtoto wa kiume unaitikiaje hivyo ?? ?Samahani babu, naam.? ?Mbona unatoka shule mapema?? ?Sijisikii vizuri.? ?Kama nilivyokueleza , kila ulichokiona na kukisikia kiache moyoni mwako, sawa?? ?Sawa babu nitafanya hivyo ,? nilimjibu kwa unyenyekevu . ?Haya kwa heri.? Niliagana na mzee Manoni, kama kawaida baada ya hatua tatu nilipogeuka sikumwona, kitendo kile kilizidi kunitia hofu moyoni. Sikufanya lolote, nilifika nyumbani na kuingia chumbani kwangu. Kutokana na mwili kuchoka sana nilijitupa kutandani ambako nilishikwa na usingizi mzito sana. Niliota ndoto za kawaida mpaka waliporudi wazazi wetu jioni kutoka shamba ndiyo walioniamsha. Nilifikiria kuwaeleza kilichonitokea, niliogopa vitisho vya mzee Manoni, niliamua kukaa kimya kama hakuna kitu kilichonitokea
Vipi mbona umelala,? baba aliniuliza. ?Uchovu tu baba,? nilimjibu kwa kuficha kilichonitokea mchana. ?Mbona umelala na nguo za shule au kesho huendi?? ?Naenda, niliporudi shule nilijilaza kidogo usingizi mzito ukanipitia.? ?Basi nenda kisimani ukachote maji ya kuoga.? Sikumjibu kitu nilipitia dumu la maji kuelekea kisimani kwa kuhofia baba kuniuliza kitu ambacho angekiona kigeni kwangu. Nilikwenda hadi kisimani na kuchota maji, wakati narudi nilikuwa na mawazo mengi juu ya uamuzi wangu wa kumueleza baba yaliyonitokea shuleni kwa kuhofia kunichimba sana. Nilimuomba Mungu, baba yangu asijue lolote juu ya kilichonitokea shuleni kwa kuamini lazima atataka kujua kwa undani. Hata nikijitahidi kuficha lazima angegundua kitu, kwa vile yeye ni mtu mzima siwezi kumficha au kumdanganya kutokana na kujua vitu vingi. Nilipofika nyumbani nilikwenda kuoga, wakati huo mama alikuwa jikoni akiandaa chakula cha usiku, usiku ulipofika tulijumuika pamoja kupata chakula cha usiku. Siku ile nilikuwa muoga kupita kiasi baada ya chakula tu, niliingia chumbani kwangu na kupanda kitandani. Nikiwa chumbani nimejilaza, nilishtushwa na sauti ya baba aliyokuwa akiniita huku akiingia chumbani kwangu. Moyo wangu ulishtuka na kujua nilichokificha kimemfikia baba hivyo anataka kujua ukweli. ?Shija!? ?Naam baba.? ?Vipi baba unaumwa, mbona leo mapema kitandani wakati muda si mrefu umetoka kulala?? ?Basi tu leo mwili nahisi uchovu.? ?Pengine maralia?? ?Sidhani, nahisi ni uchovu tu.? ?Basi pumzika usiku mwema.? ?Na wewe pia.? Nilishukuru baba aliondoka bila kunidadisi wakati moyoni nilikuwa na wasiwasi wa siri ya shule kumfikia baba. Nilijilaza kitandani huku nikiwaza vitu ambavyo hunitokea huku nikikatazwa nisimwambie baba. Niliamini kama baba angejua matatizo ninayokumbana nayo angeweza kunisaidia. Nilijiuliza kwa nini mzee Manoni hataki wazazi wangu wajue na wakijua itakuwaje. Swali lingine nilijiuliza kama nikimwambia baba nini kitanitokea, katika habari nilizowahi kusikia juujuu kuhusu wachawi nilielezwa ni watu wabaya wanaoweza kuua na kula nyama. Niliogopa pengine kuitoa siri na kumueleza baba nitauawa na kugeuzwa kitoweo cha wachawi . Kwa kweli nilijikuta kwenye wakati mgumu maishani mwangu, mzigo niliobebeshwa haukulingana na umri wangu. Niliamini walikuwa wakinionea pengine walihofia siri yao kutoka nje, ni kweli ningeweza kuwaeleza wazazi wangu niliyokutana nayo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bado wazazi wangu wasingejua nani anayehusika katika uchawi, kujitokeza kwa mzee Manoni kulijidhihirisha wazi wasiwasi wao pengine nimewajua. Nilimuomba Mungu aniepushe na janga lile kwa kuamini kama wataendelea kunifuata, nitashindwa kusoma vizuri. Usingizi nao haukuchelewa kunichukua baada ya kitu kizito kunipitia na kunifanya nilale usingizi wa pono. Siku ya pili kama kawaida baba aliniamsha kujiandaa kwenda shule, niliamka nikiwa na nguvu kama kawaida. Nilijiandaa kuwahi namba shuleni, niliwahi namba na kufanya usafi kama kawaida. Muda wa kuingia darasani ulipowadia tuliingia. Ajabu siku ile wale wanafunzi niliowaota wakicheza ngoma ya wachawi katika ndoto na nilipoamka sikuwakuta darasani na kuwauliza kama walikuwepo darasani. Hata mwalimu aliyekuwepo kwenye ngoma alikuwepo siku hiyo shule, kila sekunde ya pumzi yangu nilijiona kama sipo katika dunia ya kawaida ambayo naishi peke yangu. Sikutaka kuhoji lolote nilikaa kimya na kuendelea na masomo kama kawaida. Siku ile nilisoma kama kawaida hakuna kilichonitokea cha ajabu. Jioni ilipofika nikielekea nyumbani, mara nyingi nilipenda kuwinda ndege kila nikitoka shule. Niliacha njia ya kuelekea nyumbani na kuingia vichakani kuwinda ndege, nikiwa katikati ya kichaka, nilisikia sauti ya wale wasichana niliowaota wakicheza ngoma ya wachawi . ?Shija.? Kabla ya kuitika niligeuka kuwaangalia, nilishtuka kuwaona ni wale wale, nilijiuliza wamefuata nini kule porini. Niliwaitikia huku nikitabasamu kuficha hofu yangu. ?Naam, aah Helena na Sabina,? Helena na Sabina walikuwa wakubwa kwangu kiumri. ?Mbona uko huku peke yako?? ?Nawinda ndege.? ?Eti jana ulituulizia?? ?Eeh, kwani mlikuwa wapi jana?? ?Mmh, nyumbani.? ?Wote?? ?Kwani vipi mbona unauliza hivyo ?? ?Si rahisi wote muwe nyumbani kwa pamoja bila sababu, ikizingatiwa hamkai pamoja.? ?Kwani wewe wasiwasi wako nini?? ?Hakuna tatizo, ila niliwaulizia kama wanafunzi wenzangu.? ?Shija ilianza lini na jana iwe ya pili, ina maana mimi na Sabina ndiyo jana kukosekana kwa pamoja?? ?Tena nasikia sijui ulipitiwa usingizi na kuanza kukohoa na ulipopata fahamu watu wa kwanza tulikuwa sisi. Tunaomba utueleze ukweli nini kilichokufanya utuulize. ? Helena aliongezea.
Jamani kuna ubaya mtu kumuuliza mwanafunzi wenzake?? nilijitetea. ?Hakuna ubaya lakini kuuliza kwako kuna sababu, haiwezekani ukurupuke toka nje ulipolala kitu cha kwanza kutuuliza sisi. Huoni unatutengezea picha mbaya shuleni?? ?Jamani si nimewaeleza au kuna kingine ambacho mnajua mimi sikijui?? ?Halafu unataka kutuambia tuliokosa darasani jana ni sisi wawili , mbona Emma, Mihayo, Koleta na God hawakuwepo darasani jana hukuwauliza ukatuuliza sisi?? walizidi kunibana kwa maswali. ?Nataka kuwauliza swali, kwani ninyi mnafikiria nini?? ?Unakijua lakini hutaki kukisema.? ?Naomba mnisaidie ili nijue mnachokitaka kwangu.? ?Tunataka kujua kwa nini jana ulituuliza sisi tu?? ?Sina jibu zaidi la nililowaeleza.? ?Unajifanya mjanja sio, utaona.? ?Hamna lolote msinitishe.? Baada ya kusema vile waliondoka na kuniacha nikijiuliza ndoto ile kukosekana kwao shuleni na maswali yao yalikuwa yakiashiria nini. Nilianza kupata picha kuwa wale wasichana wanahusika katika masuala ya kichawi, wasiwasi wao mkubwa kuitoa siri yao. Nilijiuliza walikuwa na maana gani kunitishia kuwa nitaona, baada ya kujifanya mjanja kamna walivyosema . Sikutaka kuwapuuza kusema vile walikuwa na maana gani na kwa nini wanitishe. Nilingiwa na wasiwasi kutokana na kusikia eti kati ya wale wasichana kuna mmoja alimuambia mwanafunzi mmoja kuwa utaona siku ya pili hakuamka wakamzika . Nilijiona naingia kwenye mtihani mwingine, mzee Manoni alinikataza nisimwambie mtu. Na wale wasichana walikuwa wakinilazimisha huku wakinitisha nitaona, nilijiuliza nini hatima yangu. Wazo la haraka lilikuwa kwenda kwa mzee Manoni kumueleza jinsi nilivyotishwa na wale wasichana. Nilikumbuka katika njozi tulionana uso kwa macho na wale wasichana wote katika ile ngoma
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ambayo ilinitatiza kuwa ya kweli tofauti na njozi yenyewe . Niliamua kuachana nao na kuendelea kuwinda ndege, kwa kuamini ilikuwa ni kunitisha tu ili nisimwambie mtu, japo bado niliamini huenda wakanigeuzia kibao. Nilijikuta nikibadili mawazo na kuona kuna umuhimu wa kuonana na mzee Manoni jioni ile kabla usiku haujaingia ili yasijenikuta kama yaliyomkuta mmoja wa wanafunzi waliotishiwa na Sabina na mwisho wa siku alikufa kifo cha ghafla. Kwa vile nilikuwa nimeingia katikati ya vichaka kuwinda ndege, niliamua kurudi ili niende kwa mzee Manoni kumueleza nilivyotishwa na wale wasichana. Kama isingekuwa hivyo ningerudi nyumbani kumueleza baba jinsi nilivyotishwa na Helena na Sabina. Wakati najiandaa niliona wanyama wawili weusi kama mbwa waliokuja mbio mbele yangu wakinifuata niliposimama. Nilipoangalia vizuri niliwafahamu ni fisi, woga uliniingia na kuanza kukimbia kuingia ndani ya vichaka kuwakimbia . Wale fisi walinifuata mbio nyuma yangu. Toka nizaliwe sikuwahi kukimbia vile kwani fisi waliponikaribia niliongeza mwendo, wapotaka kunishika walikosa kwa kuwaponyoka . Walionekana wamenipania kunimaliza. Kila waliponikosa walilia
0 comments:
Post a Comment