Search This Blog

NILIBADILIKA NA KUWA JINI BILA KUJIJUA - 5

 







    Simulizi : Nilibadilika Na Kuwa Jini Bila Kujijua

    Sehemu Ya Tano (5)



    Kazi aliyoachiwa na Fatiha ilikuwa ni zaidi ya mtihani kwake. Hakujua ni kwa namna gani ataweza kuikamilisha, hasa ukizingatia kuwa umri wake ulikuwa bado mdogo, na alikuwa na siku chache tu tangu awasili Bagamoyo akitokea Sumbawanga.



    Hakuwahi kufika Dar es Salaam hata mara moja lakini sasa alitakiwa kwenda kuanza kazi aliyoelekezwa na Fatiha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliishika pete aliyopewa na Fatiha akawa anajaribu kukumbuka maelekezo aliyopewa juu ya namna ya kuitumia.



    “Nataka gari zuri la kifahari litokee!” Gamutu aliiambia ile pete akiwa amekaa mkao wa Atahiyatul Mantra aliofundishwa na Fatiha. Pete ilibadilika rangi na kuanza kung’aa kisha ikafifia.





    Alipofumbua macho, alishangaa mno kuona gari dogo la kifahari, BMW 735 ‘New Model’ likiwa limepaki mbele yake, mlango wa dereva ukiwa wazi huku funguo zikiwa zinaning’inia.



    “Naomba maarifa ya namna ya kuendesha gari, mavazi mazuri na fedha kidogo za matumizi nikiwa njiani,” Gamutu aliiambia ile pete na yote aliyoyataka yakatimia mara moja. Akaibusu ile pete kisha akairudisha mahali pake. Akajiangalia kupitia kioo cha gari, hakika alikuwa amebadilika mno.



    Kitu pekee kilichomuangusha ni nywele ambazo zilikuwa kwenye mpangilio mbovu tangu alipoondoka nazo kule kijijini kwao. Alipanga kuwa kituo cha kwanza itakuwa ni saluni ambapo ataenda kuzinyoa na kuweka kichwa katika hali ya usafi.



    Akiwa anatetemeka aliingia ndani ya gari na kukaa nyuma ya usukani. Hakuwahi kuwaza hata siku moja kuwa anaweza kuja kuendesha gari la thamani kama lile. Akiwa bado anajiuliza aanzie wapi, alisikia sauti ya Fatiha ikimuelekeza namna ya kuliwasha, kuingiza gia na kuondoka.



    Alipofuata maelekezo yale, alishangaa gari likiondoka utafikiri lilikuwa likiendeshwa na dereva mzoefu.



    “Hivi nikifika kwenye taa za barabarani nitafanyeje? Maana hata sijui zinavyotumika,” Gamutu alijisemea kimoyomoyo lakini akajiaminisha kuwa hakuna kitakachoshindikana kwa vile alikuwa na ile pete.



    Akiwa barabarani, alishangaa kumuona Fatiha akiwa amekaa kiti cha pembeni akimuangalia kwa makini alivyokuwa anaendesha gari.



    “Umekuja saa ngapi?”

    “Hilo siyo la msingi, nimekuletea hii dawa, unatakiwa kujifukiza sasa hivi na hii nyingine utaitafuna,” alisema Fatiha na kumkabidhi Gamutu kimfuko kilichokuwa na manukato pamoja na kitezo cha kujifukizia. Alipokifungua kile kimfuko na kuweka manukato kidogo kwenye kitezo, gari zima lilijaa harufu kali, akajifukiza mwili mzima kama alivyoelekezwa.



    Pia alitafuna mizizi kadhaa aliyoletewa na Fatiha. Alipomaliza Fatiha alichukua kile kitezo na kumuelekeza hoteli ya kufikia kisha akamtakia kazi njema na kupotea kimiujiza. Gamutu akaendelea na safari mpaka alipowasili jijini Dar es Salaam.

    ***

    Meza aliyokuwa amekaa Gamutu, ambaye sasa alikuwa amebadilika na kuonekana kama milionea mtoto, akiwa na mvuto wa kimahaba kama si yeye, ilikuwa imezungukwa na wanawake zaidi ya watano ambao wote walikuwa wakitaka kwenda kulala naye.



    “Twende na mimi, si unaniona jinsi nilivyo bomba, nitakupa mambo ambayo hujawahi hata kuyaota,” alisema wa kwanza, akadakia mwingine, kisha mwingine! Ikawa ni vurugu tupu.



    Gamutu hakuwa na haraka, alijua alichokuwa anataka kukifanya kisingefanikiwa kama angekuwa na papara. Kilichomshangaza ni jinsi ambavyo wanawake walivutiwa naye kirahisi. Hata bila kuongea neno lolote, mwanamke ambaye macho yake yaligongana naye, alijipeleka mwenyewe na kukaa jirani naye.



    “Leo kazi ipo!” alijisemea kimoyomoyo wakati akijiandaa kuianza shughuli ile. Ilibidi awadanganye na fedha wale wengine, wakaondoka na kumuacha na mmoja ambaye kiumri alikuwa mkubwa kwake, wakakokotana mpaka ndani ya chumba alichokuwa amefikia Gamutu. Kilichoendelea ilikuwa ni kelele za mahaba za yule mwanamke, ambaye alikuwa akilalamika kwa nguvu mpaka kuwa kero kwa wateja wengine.



    Dawa za kutafuna alizopewa na Fatiha zilimfanya Gamutu kuwa na nguvu kama dume la simba, hali iliyomfanya yule mwanamke ashindwe kuhimili vishindo.



    Baada ya Gamutu kufanya kazi yake ipasavyo, alimbeba yule mwanamke na kushuka naye hadi chini alipokuwa ameegesha gari lake.



    Akamuingiza kwenye siti ya nyuma bila mtu yeyote kumshtukia na kwenda kumtelekeza kwenye mtaro uliokuwa eneo la jangwani. Baada ya kufanikisha zoezi lile, alirejea mpaka pale hotelini, akaenda kubadilisha mashuka ambayo hayakuwa yakitamanika.



    Alipomaliza alienda kukaa kwenye canteen ya hoteli ile, ambapo baada ya dakika chache alikuwa amezungukwa na wanawake wengine kibao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kuwa fedha kwake haikuwa tatizo, aliwanunulia pombe mpaka wote wakawa hoi, akamchagua mmoja aliyekuwa anamtaka na kuelekea naye chumbani kwake.



    Bila hata kupoteza muda, alimsaula na yeye akafanya vilevile, sekunde chache baadaye, miguno ya kimahaba ilikuwa ikisikika wakati wakielea kwenye sayari nyingine. Kwa kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo kelele za kimahaba kutoka kwa yule mwanamke zilivyozidi kuongezeka.



    “Ngo! Ngo! ngo!”

    Gamutu alisikia mlango wa chumba kile ukigongwa.



    “Aaah nani tena huyo?” alisema kwa hasira huku akiinuka na kujifunga taulo. Alipofungua mlango alikutana na mhudumu ambaye alimwambia anaomba wapunguze kelele kwani wateja wa vyumba vingine walikuwa wakilalamika.



    “Okey! Sawa! Nimekuelewa,” alisema Gamutu kwa aibu kisha akafunga mlango.



    Safari hii aliamua kubadili namna ya kufanya kazi, alitumia taulo kumziba yule mwanamke mdomo, akaendelea kama mwanzo. Alipomaliza alifanya kama alivyofanya mara ya kwanza, akaenda kumtelekeza eneo lile lile alilomtupa yule wa kwanza.



    Mpaka inafika saa tatu usiku, Gamutu alikuwa amewaingilia wanawake watano, ambao wote alipomaliza walikuwa hawajitambui kutokana na shughuli nzito. Kibaya ni kwamba alienda kuwatelekeza wote sehemu moja.



    Kuepuka ushahidi, alipomaliza aliamua kuchukua kila kilichokuwa chake na kuhama na kwenda hoteli nyingine.



    “Mh! We mtoto taratibu, nahisi moyo unataka kutoka,” alijitetea yule mwanamke lakini Gamutu alikuwa ni kama hasikii. Aliendelea ‘kumshughulikia’ kwa nguvu mpaka akawa taabani.



    Hakuelewa kilichoendelea mpaka kesho yake alipokuja kuzinduka na kujikuta yuko nyumbani kwake.



    “Mmh! Hivi kumetokea nini?” aliuliza yule mwanamke huku akiwa haamini kujikuta yuko nyumbani kwake.



    “Uliokotwa na wasamaria wema usiku ukiwa hujitambui! Ndiyo wakakuleta hapa nyumbani,” aliongea mtu aliyekuwa pembeni yake.



    Hapo ndipo kumbukumbu zilipoanza kumjia. Alipeleka mkono kwenye ofisi yake, akaguna kwa maumivu makali aliyokuwa anayahisi kwani hakukuwa kukitamanika.





     “Mmh! Jamani, ukatili gani huu,” alisema yule mwanamke huku akijifuta machozi.

    “Kwani nini kimekutokea?”

    “Siwezi kueleza kwa kweli maana naona aibu, nimefanyiwa kitu kibaya na mtu ambaye sikumtegemea kabisa, lakini yote namwachia Mungu.”



    “Usiseme hivyo, hebu nyoosha maelezo maana nasikia kuna wanawake wengine nao wameokotwa eneo ulilookotwa wewe, tena wakiwa na hali kama yako, eleza ukweli ili tujue,” akazidi kusisitiza lakini yule mwanamke akashikilia msimamo wake kuwa hatazungumza kitu chochote.



    Baada ya kubanwa sana, hatimaye alikubali kueleza jinsi alivyokutana na kijana mdogo mwenye fedha ‘kama serikali’ (Gamutu), alivyomrubuni na kufanikiwa kuvunja naye amri ya sita mpaka akapoteza fahamu.

    “Hata maelezo yako yanafanana na mwanamke aliyekuwa anahojiwa redioni asubuhi hii ambaye naye ameokotwa akiwa hajitambui. Halafu nasikia usiku mmoja wa jana wameokotwa wanawake wengi wakiwa wamefanyiwa mchezo mbaya kama wewe.”



    Taarifa juu ya kijana mdogo anayewafanyia ukatili wanawake zilisambaa kwa kasi kama moto wa nyika. Ndani ya siku mbili tu, jumla ya wanawake kumi na nne walikutwa wakiwa hawajitambui, huku mazingira waliyokutwa yakiwa yanafanana.

    Ilibidi jeshi la polisi liingilie kati, likawa linawahoji waathirika wa unyanyasaji ule wa kijinsia, mmoja baada ya mwingine. Kati ya wanawake wote waliohojiwa na polisi, walimuelezea mhusika kwa namna inayofanana, jambo lililodhihirisha kuwa vitendo vile vilikuwa vikifanywa na mtu mmoja.



    Matangazo yakabandikwa kila mahali juu ya watu kuwa makini na mwanaume anayewafanyia ukatili wanawake kwa kuwaingilia kimwili mpaka wanapoteza fahamu, kisha kwenda kuwatelekeza mtaroni au sehemu nyingine za hatari.

    “Mtuhumiwa anatajwa kuwa ni kijana mdogo, mweusi, anatembelea gari la kifahari aina ya BMW 735 “New Model’. Anapendelea kuvaa mavazi ya kisasa huku akiuficha uso wake kwa kofia. Yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwake atapewa zawadi nono na jeshi la polisi,” alisikika mkuu wa polisi akitoa maelekezo kwa wananchi kupitia vyombo vya habari, zikiwemo redio na runinga.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati uchunguzi na upepelezi wa kina ukiendelea, matukio ya namna ile yalizidi kuripotiwa, huku mtuhumiwa akihama eneo moja hadi jingine. Tukio lililoshtua wengi ni pale wanawake saba walipokutwa wametelekezwa juu ya daraja la Manzese, wakiwa wamepoteza fahamu na wakiwa na dalili za kuingiliwa kimwili.



    Walipookotwa na wasamaria wema, wote walieleza kuwa kwa nyakati tofauti walikutana na kijana mmoja mdogo lakini anayeonesha kuwa na fedha nyingi, ambaye aliwarubuni kwa fedha kisha kuwapeleka gesti ambapo hakuna aliyekuwa anakumbuka juu ya nini kilichotokea.



    Mtuhumiwa alizidi kusakwa bila mafanikio, matukio yakawa yanazidi kuongezeka kila kukicha, huku akina dada wanaojiuza nao wakikumbwa na balaa hilo kwa kiwango kikubwa. Hali ilipozidi kuwa tete, ilibidi wanawake waache mazoea ya kutembea usiku, na walipolazimika kufanya hivyo, walikuwa wakitembea kwa makundi.



    Akina dada poa nao wakasitisha kazi yao kwa muda wakihofia kukumbwa na balaa lile. Kilichozidi kuwashangaza wengi ni kuwa, wote waliopitiwa na tukio lile, walianza kuonesha dalili za kunasa ujauzito ndani ya siku chache tangu tukio lilipotokea, hali ambayo haikuwa kawaida.

    ***

    Fatiha! Kazi yako imenishinda! Hivi tunavyoongea ninasakwa na polisi kwa udi na uvumba, wakinikamata si nitaozea jela mimi!”

    “Acha woga Gamutu, wewe ni mtoto wa kiume, lazima uwe jasiri na usikubali kutawaliwa na hofu maishani mwako.”

    “Hapana Fatiha, hebu angalia mpaka mkuu wa polisi anasimama na kuzungumza na vyombo vya habari juu yangu, si lazima nitakamatwa?”



    “Kwa nini unakosa imani kiasi hicho? Kuna jambo ambalo nimewahi kukuahidi na likashindwa kutokea?”

    “Hapana.”

    “Basi amini nakwambia, hakuna atakayekukamata wala kukugusa mpaka utakapokamilisha kazi niliyokupa.”

    “Lakini nitakamilishaje wakati naandamwa kila kukicha? Mi nafikiri nimeshindwa kazi yako.”



    “Hujashindwa! Umeweza tena kwa kiwango cha juu kabisa. Cha kufanya inabidi uhamie Arusha kwa muda, kisha utaenda Mwanza na Mbeya kabla ya kuja kumalizia Bagamoyo. Huko kote unapaswa kuzunguka kwa muda usiozidi siku saba,” alisema Fatiha na kumpa Gamutu kibuyu kidogo kilichokuwa na unga mweusi.



    “Ukiona wanakaribia kukufikia, utakuwa unajipulizia unga huu kidogo na kufanya tahajudi ya kujibadilisha umbo kama nilivyokufundisha, hakuna atakayekusogelea,” alisema Fatiha wakati akimkabidhi Gamutu kibuyu kile, akaenda kukiweka kwenye buti la gari lake.



    Baada ya mazungumzo marefu na Fatiha, wakiwa eneo la Ufukwe wa Bahari la Kunduchi, Gamutu aliagana na Fatiha kwa makubaliano kuwa ahame jijini Dar es Salaam na kuelekea Arusha kuendelea na kazi.

    “Nitakuwa pamoja na wewe kwa kila kitu, wala usiwe na wasiwasi,” alisema Fatiha, Gamutu akaitikia kwa kichwa na kuwasha gari lake.



    Baada ya kuondoka jijini Dar es Salaam, Gamutu alielekea jijini Arusha. Akiwa ndani ya gari la kifahari, aliendesha mwenyewe mpaka alipofika eneo la Chalinze. Akashuka kwa lengo la kutafuta chakula kwani alikuwa akihisi njaa kali.

    “Kaka samahani, naomba msaada wa lifti, mi naenda shuleni Arusha,” binti mdogo, mwenye sura ya kuvutia alijilengesha kwa Gamutu. Kwa jinsi alivyokuwa anaonekana, isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kumfikiria vibaya.



    “Hapana dada’angu, kuna abiria nawapitia hapo mbele, labda nikuongezee nauli upande basi,“ alidanganya Gamutu. Lengo la kumkwepa msichana yule lilikuwa ni kuepusha migogoro njiani kwani alijua lazima atashawishika kumuingilia kimwili na kuifanya safari iwe ngumu.



    Aliingiza mkono mfukoni na kutoa noti mbili za shilingi elfu kumi na kumkabidhi.

    “Ooh, ahsante sana kakaangu, hivi unaitwa nani?“ yule msichana alianza kumhoji Gamutu huku akiziweka zile fedha alizopewa mfukoni.



    “Naitwa G!“ Gamutu alijibu kwa kifupi huku akimuita mhudumu wa hoteli na kumuagiza chakula.

    “Jina lako zuri, hivi unaishi Dar au Arusha?“

    “Naishi Sumbawanga, huku nimekuja kikazi tu,” alijibu Gamutu. Mazungumzo yaliendelea mpaka Gamutu alipomaliza kula, akainuka na kuanza kutembea taratibu kuelekea mahali alipokuwa ameegesha gari lake.







    “Kwani we unafanya kazi gani?”

    “Mimi?”

    “Ndiyo!”



    “Nitakwambia, lakini siyo sasa hivi,” alijibu Gamutu na kuongeza mwendo kuelekea kule alikokuwa amepaki gari.Yule msichana alimfuata, wakaongozana mpaka kwenye gari. Licha ya kujaribu mbinu zote kumkwepa, bado alimganda kama ruba.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Jamani kakaangu, hata kama ni kukaa nyuma mi nitakaa, najisikia kusafiri na wewe, nisaidie tafadhali,” alibembeleza yule msichana, Gamutu akapata wakati mgumu kumkatalia, ikabidi amkubalie huku kimoyomoyo akisema ‘mwache ajitoe kafara’.

    “Hata hao niliotaka kuwapitia nimeghairi, twende sisi wawili tu,” alisema Gamutu huku akimfungulia mlango na kuwasha gari.



    Yule msichana aliingia kwa kupitia mlango wa mbele na kukaa pembeni ya Gamutu. Safari ikaanza huku kila mmoja akiwa kimya. Gamutu aliiacha barabara ya Morogoro na kuingia ya kuelekea Tanga. Akafungulia sauti ya muziki laini kwenye gari.



    Walipofika eneo la Mkomazi, pembeni ya barabara kuu ya Arusha, yule msichana alimuomba Gamutu asimamishe gari kwa madai alikuwa amebanwa na haja ndogo. Gamutu alifanya kama alivyoomba, akasimama karibu na kichaka kikubwa. Yule msichana alishuka huku akimuangalia Gamutu usoni akiwa na tabasamu pana.



    “Nisindikize,” alisema huku akijichekesha, Gamutu akashuka garini na kumfuata huku akichekelea kimoyomoyo.

    “Baada ya kumaliza haja zake, alimfuata Gamutu alipokuwa amesimama, akamkumbatia na kumnong’oneza sikioni.

    “Naomba niwe mchumba wako,” Gamutu alicheka, akamkumbatia kwa nguvu na kumbusu mashavuni.



    Akili yake ilifanya kazi kwa kasi, akamteremsha kufuli na kumkalisha juu ya jiwe kubwa, akapiga magoti na kumwelekeza cha kufanya. Muda mfupi baadaye walizama kwenye dimbwi la mahaba lakini mambo hayakuwa sawa kwa yule msichana. Gamutu alimzidi sana, ukizingatia alikuwa bado ni mwanafunzi, akawa anapiga kelele kwa nguvu huku akiuma meno kama ishara ya kuhisi maumivu makali. Gamutu hakujali, akawa anamuingilia kwa fujo mpaka akaishiwa kabisa nguvu.



    Hakuishia hapo, aliendelea kwa muda mrefu mpaka alipohakikisha hajitambui kabisa. Akapanda juu ya mnazi na kuangua dafu kubwa, alipomaliza akamtelekeza palepale kichakani, akakimbilia alikokuwa amesimamisha gari. Bila kupoteza muda aliliwasha na kukanyaga mafuta, akaondoka kwa kasi huku akijipongeza kimoyomoyo.

    ***

    Safari yake iliendelea huku akiwa tayari ameshaanza kazi hata kabla hajafika. Breki ya kwanza ya Gamutu ilikuwa ni Njiro jijini Arusha. Alipofika alienda moja kwa moja mpaka kwenye Hoteli ya Kitalii ya Planet Link iliyokuwa inatazamana na magofu ya General Tyres, akakodi chumba na kulipia siku kumi. Kwa jinsi ratiba yake ilivyokuwa, ilikuwa ni lazima akae kwa siku za kutosha ili kukamilisha zoezi la kuwaingilia kimwili wanawake wengi kwa ajili ya kuzalisha kizazi kipya cha majini kama alivyokuwa ameleekezwa na Fatiha.



    Tofauti ya hali ya hewa kati ya Sumbawanga, Bagamoyo na Dar es Salaam ilimfanya hata rangi ya ngozi yake ianze kubadilika. Siku chache alizokaa Bagamoyo na Dar es Salaam zilifanya ule weusi wa ajabu aliokuwa nao wakati anatoka Sumbawanga upungue, ukichanganya na fedha nyingi alizopewa uwezo wa kuzimiliki na Fatiha, alinawiri haraka na kuwa tofauti sana.



    Jaribio lake la kwanza alitaka kulifanya kwa watalii lakini akajikuta akishindwa kuwasiliana nao kutokana na kutojua lugha ya Kiingereza.



    “Potelea mbali, watakaopatikana ndiyo hao hao, ila Wazungu wakijichanganya namaliza,” alijisemea kimoyomoyo akiwa amekaa kwenye bustani za nje ya hoteli aliyofikia. Mara alimuona mwanamke ambaye akilini mwake aliona anaweza kufaa kwenye kazi iliyompeleka kule kutokana na jinsi alivyokuwa anavutia. Japokuwa alikuwa amemzidi sana umri, alimpungia mkono kwa ishara ya kumwita, akamsogelea huku akimtazama kwa makini.



    “Habari yako ma’mdogo,” alisalimia Gamutu akijifanya ana heshima.

    “Nzuri mdogo wangu, nikusaidie nini?”

    “Samahani mimi hapa mgeni, nilikuwa naomba kama hutajali, ukae nikuulize mawili matatu,” Gamutu alimuingia kwa maneno matamu na akawa anambembeleza kukaa.



    Alipoona anakuwa mgumu, aliingiza mkono mfukoni kwa siri na kutoa kamzizi miongoni mwa zile dawa alizopewa na Fatiha.

    Akawa anakashikashika wakati akiendelea kuongea naye. Kama alivyokuwa amehakikishiwa na Fatiha kuwa hakuna mwanamke anayeweza kumkataa kama akitumia mbinu alizomuelekeza, kweli yule mwanamke alikubali kirahisi. Uongo aliokuwa anampa ulikuwa mtamu mithili ya asali, wakainuka na kuelekea ghorofa ya pili kulipokuwa na chumba alichopangisha Gamutu.



    “Utaniweza lakini?” yule mwanamke ambaye alikuwa na mwili mkubwa alimuuliza Gamutu wakati akitoa vitu vilivyokuwa mwilini mwake na kuviwekwa kwenye dressing table ndogo iliyokuwa mle chumbani.

    “Nikushindwe una nini?”



    “Nakuona kama bado mtoto, halafu isitoshe mimi nina jini mahab…,” kabla hata hajamalizia sentensi yake, Gamutu alimvaa mwilini na kumtupia juu ya uwanja wa carpenter, akaanza kuhangaika kuung’oa muhogo. Tofauti na yule mwanamke alivyotegemea, Gamutu hakuwa mtoto, bali kidume cha shoka kilichokomaa haswaa!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati akiendelea kumsulubu, alimuangalia usoni kwa makini, akawa ni kama aliyegundua jambo ingawa hakutaka kujionesha. Gamutu aliendelea kushughulika mpaka akaanza kumzidi, ikabidi atumie ujanja uliomuokoa kwani kengele ya hatari ilishalia akilini mwake.



    “Naomba niende toilet mara moja, nakuja sasa hivi,” alidanganya, Gamutu akakubali kirahisi na kujilaza chali huku mkono wake mmoja akiutumia kupasha misuli isipoe. Yule mwanamke alikusanya nguo zake kimya kimya pamoja na viatu, badala ya kufungua mlango wa maliwatoni, alifungua wa kutokea nje, akanyata na kumuacha Gamutu anamsubiri.



    Alipofika kwenye ngazi alivaa haraka haraka, akajikuta kumbe amebeba na za Gamutu. Kwa haraka aliingiza mkono mfukoni na kutoa waleti iliyokuwa imejaa noti nyekundu nyekundu, akaificha kwenye sidiria na kuanza kuteremka kwa kasi kama anayekimbizwa. Hakuonekana tena eneo lile.





    GAMUTU alishtuka baada ya kuona muda unazidi kuyoyoma bila yule mwanamke kurejea. Ikabidi asimame na kuelekea maliwatoni akiamini atamkuta. Cha kushangaza, hakukuwa na mtu. Alipotazama mlango mkubwa wa kutokea nje, alitingisha kichwa kwa masikitiko baada ya kuona ukiwa wazi.



    “Nimefanya uzembe kumuacha mpaka akimbie?” aliongea wakati akirudi kujifunga taulo na kutoka nje kuokota nguo zake zilizokuwa zimetupwa kwenye ngazi na yule mwanamke. Wakati akiokota suruali yake, aligundua kuwa waleti yake haikuwepo mfukoni,akashusha pumzi ndefu huku akifikiria nini cha kufanya.

    Kilichomchanganya ni kwamba kule kwenye waleti kulikuwa na vitambulisho vyake vya bandia ambavyo vilikuwa na picha yake halisi.



    “Potelea mbali nitatafuta vingine,” alijisemea Gamutu. Kitendo cha yule mwanamke kutoroka kabla hajamaliza haja zake za kimwili, kilimfanya Gamutu apandwe na pepo mbaya wa ngono. Mwili wote ulikuwa ukitetemeka huku kijasho chembamba kikimlowanisha.



    Alivaa haraka haraka na kutoka nje, akaingia ndani ya gari lake na kuliwasha akiwa haelewi anaelekea wapi. Baada ya muda alitokezea barabarani, akawa anaendesha gari lake kutokea Njiro kuelekea mjini. Alipofika eneo la Chuo cha IAA (Institute of Accountancy Arusha), aliona kundi la wasichana walioonesha kuwa ni wanachuo wakivuka barabara.

    Kwa jinsi alivyokuwa na hamu ya kucheza gemu la kikubwa, alipunguza mwendo na kusimama pembeni. Akashusha kioo nakuanza kuwasemesha.



    “Habari zenu warembo!”

    “Poa!” walijibu wale wasichana kwa pamoja, akawaambia waingie ndani ya gari lake awape lifti. Wengine walisita lakini watatu kati yao hawakujivunga, wakafungua milango na kuingia, wawili wakakaa nyuma na mmoja mbele. Kwa kuwa shida yake ilikuwa ni kufanya mapenzi tu, alipeleka mkono kwenye dashboard ya gari lile, akatoa kichupa kilichokuwa na dawa ya kienyeji aliyopewa na Fatiha. Akapuliza kidogo ndani ya gari na kuendelea na safari.



    Baada ya muda wale wasichana wote walipitiwa na usingizi mzito kutokana na ile dawa aliyoipuliza. Alichokifanya ilikuwa ni kuegesha gari pembeni ya barabara na kuanza kuwashughulikia, mmoja baada ya mwingine. Aliwaingilia kwa zamu kwa muda mrefu mpaka hamu yake ikapungua, ingawa haikuisha kabisa.



    Japokuwa alikuwa amepaki gari pembeni ya barabara, hakuna aliyeshtukia mchezo uliokuwa unaendelea mle ndani ya gari kwani vioo vyote vilikuwa tinted. Alipomaliza, alifungua milango na kuwasukumia wale wasichana mtaroni bila kushtukiwa na mtu yeyote, akawasha gari na kukanyaga mafuta kwa nguvu, akatokomea mahali kusikojulikana.



    ***

    Baada ya kufanya tukio lile, Gamutu alipita njia za mkato na kurejea Njiro ambapo alipitiliza mpaka kwenye chumba alichokuwa amepanga na kujitupa kitandani.Usingizi mzito ukampitia hadi usiku alipokuja kushtuka.

    Alipoangalia saa yake, ilikuwa tayari ni saa nne za usiku. Japokuwa alikuwa amechoka sana kutokana na safari na mikikimikiki ya kutwa nzima, ilibidi aamke kwa lengo la kuendelea na kazi iliyompeleka Arusha. Aliingia bafuni na kujimwagia maji, akatoka na kuanza kujiandaa. Lengo lake lilikuwa ni kuelekea kwenye klabu za usiku ambapo alikuwa na uhakika wa kupata idadi kubwa ya wanawake wa kuwafanyia kazi usiku ule.



    Baada ya kila kitu kuwa tayari, Gamutu alitoka na kuelekea alipokuwa amepaki gari lake. Akaingia na safari ya kuelekea kwenye ukumbi maarufu jijini Arusha wa Tripple ikaanza. Baada ya kufika eneo la Clock Tower, Gamutu alipunguza mwendo baada ya kuona kundi la akina dada wakiwa wamejazana eneo lile.



    Kwa kuwa alikuwa mgeni wa Jiji la Arusha, hakutambua haraka kuwa wale walikuwa ni machangudoa waliokuwa kazini. Akateremsha kioo cha gari lake, akashangaa kuona wale akina dada wakimkimbilia na kulizunguka gari lake.

    “Nichukue mimi we kaka! Cheki nilivyo bomba!”



    “Huyu hana lolote, nichukue mimi! Si unaona shepu ya kijanja hii!” wale madada poa walizidi kujinadi mbele ya Gamutu ambaye bado alikuwa ameduwaa. Alichokifanya alifungua mlango na kuwaambia waingie wote, wanawake zaidi ya nane wakajaa kwenye gari lake. Alikanyaga mafuta na kuondoa gari kwa kasi kurudi Njiro. Safari ya kuelekea Tripple A ikawa imefikia mwisho.



    Wakiwa njiani,wale madada poa walianza kumfanyia fujo wakimtaka amchague mmoja kati yao ndiyo aondoke naye.

    “Nawataka wote!” alijibu Gamutu lakini walipozidi kumshinikiza, ilibidi asimamishe gari pembeni ya barabara.

    “Sasa kwa kuwa umetusumbua mpaka huku mbali, inabidi utulipe fidia kila mmoja kivyake, kisha uchague mmoja wa kwenda naye,”alisikika mmoja kati yao, aliyeonekana kuwa mkuu wa msafara.



    Gamutu hakuwa mbishi, akaingiza mkono mfukoni kwa lengo la kutoa fedha. Alijikuta akiduwaa baada ya kugundua kuwa waleti yake iliyokuwa na fedha iliibwa na yule mwanamke aliyemkimbia mchana wa siku ile. Alipowaeleza wale wanawake kwamba hakuwa na fedha mpaka afike hotelini alikofikia, walimjia juu na kumvaa mwilini.



    Kwa kuwa walikuwa wengi,walianza kumpekua kwenye nguo zake, wakachukua simu iliyokuwa mfukoni. Kitendo kile kilimpandisha Gamutu jazba, akaanza kurusha mateke na ngumi. Kufumba na kufumbua alishangaa akichomwa na kitu chenye ncha kali tumboni, alipogeuza macho, yule mwanamke aliyeonekana kuwa mkuu wa msafara, alikuwa amezamisha kisu kikubwa tumboni mwake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mamaa nakufa!” Gamutu alipiga yowe kuu wakati kisu kikiwa bado kimening’inia tumboni.

    Damu nyingi zikaanza kumtoka, wale machangudoa wakaanza kukimbia kila mmoja na njia yake. yule kiongozi wao aliingia ndani ya gari, akakaa nyuma ya usukani na kufunga milango yote, akaondoa gari kwa kasi kubwa na kutimua vumbi.



    Kwa jinsi Gamutu alivyokuwa anasikia maumivu makali huku akitokwa na damu nyingi, alianza kukoroma akiwa amelala pale barabarani. Giza nene likaanza kumzingira usoni, akatulia tuli.



    Gamutu aliendelea kukoroma pale chini huku damu nyingi zikimtoka kwenye jeraha alilochomwa kisu, mdomoni, puani na masikioni. Kwa dakika zaidi ya tano, hakuna mtu aliyepita eneo lile, hali iliyofanya maisha yake yawe hatarini. Eneo lote lilibaki kuwa kimya huku wale wanawake wakiwa tayari wameshatokomea kusikojulikana, yule kiongozi wao akiondoka na gari.



    Kitendo cha damu nyingi kumtoka Gamutu kilikuwa na maafa makubwa kwake mwenyewe, kwa Fatiha na wanawake wote aliokuwa tayari ameshiriki nao kuvunja amri ya sita. Kilichotokea ni kuwa, ule mtego wa kichawi uliokuwa umetegwa mwilini mwake ili awape ujauzito wanawake wengi kwa ajili ya kuendeleza kizazi cha majini, uliteguka na kusababisha mimba ambazo zilikuwa zimeanza kutungwa kuharibika.



    Wanawake wote alioshiriki nao mchezo wa kikubwa, walianza kuumwa na matumbo mfululizo. Wakati damu zikimvuja Gamutu, nao walikuwa wakitokwa na damu nyingi kwenye ikulu zao, kuashiria kuwa mimba zote zilikuwa zimeharibika. Ikawa ni vilio mtindo mmoja.



    Fatiha alizinduka kutoka kwenye tahajudi ya kijini aliyokuwa anaifanya akiwa kule ujinini, na kuinuka haraka kuelekea kwenye mlango wa kutokea. Wakati akitembea kwa haraka, alikuwa akiisikia sauti ya Gamutu masikioni mwake akilia kwa maumivu makali.



    “Nini kimemtokea tena?” alijiuliza Fatiha huku akijaribu kujiangalia kwenye kiganja cha mkono wake wa kulia kuona mahali alipokuwa Gamutu. Baada ya kufanya ishara za kichawi, alitokezea kimiujiza eneo alipokuwa amelala Gamutu. Hakuamini macho yake kwa kile alichokiona.



    Gamutu alikuwa amelala kwenye dimbwi la damu huku kisu kikining’inia tumboni kwake. Aligeuka upande mmoja hadi mwingine lakini hakuona mtu yeyote anayeweza kumpa msaada. Kwa jeraha lile, ilikuwa ni lazima apelekwe hospitali kwanza, akashonwe kisha ndiyo asafiri naye hadi ujinini ambako angeendelea kupatiwa matibabu.



    Baada ya muda, aliona gari likija kutokea upande wa Njiro. Fatiha alisimama katikati ya barabara na kupunga mikono, dereva akapunguza mwendo na kusimama kando ya barabara. Hata kabla Fatiha hajaeleza chochote, dereva alishuka na kuelekea pale Gamutu alipokuwa amelala.



    “Nisaidie tumpeleke hospitali,” alisema Fatiha.

    “Kwani amepatwa na nini?” aliuliza yule dereva huku naye akionesha kuogopeshwa na kile kilichotokea. Fatiha alimweleza kuwa hata yeye hajui lakini inavyoonesha alikuwa amechomwa kisu tumboni. Hatuwezi kwenda hospitali mpaka tupitie kwanza polisi,” alisema yule dereva, wazo ambalo Fatiha hakutaka kuliafiki.



    Ilibidi atumie ushawishi wa nguvu zake za kijini kuhakikisha Gamutu anawahishwa hospitali. Hilo lilifanyika kwani dakika chache baadaye walikuwa nje ya Hospitali ya Mount Meru. Bila hata kuulizwa PF3, alipokelewa na kukimbizwa wodini. Fatiha akawa anasimamia kila kilichokuwa kinaendelea.



    “Mgonjwa ni nani yako?” daktari alimuuliza Fatiha, akadanganya kuwa ni mdogo wake.

    “Mazingira ya tukio yalikuwaje?”



    “Sijui chochote kwa kweli, mi nilipewa taarifa na wasamaria wema kuwa mdogo wangu anataka kufa, nilipofika eneo la tukio nikakuta amelala chini huku damu nyingi zikimtoka,” Fatiha alieleza huku akipindisha ukweli wa tukio zima.



    Daktari alimwambia kuwa mgonjwa ana tatizo la damu kutoganda kwani licha ya kushonwa jeraha, bado alikuwa akitokwa na damu nyingi, hali ambayo ingeweza kusababisha mauti yake. Taarifa ile ilimchanganya Fatiha, akajua asipokuwa makini huenda akampoteza Gamutu, jambo ambalo hakuwa tayari kuona linatokea.



    Ilibidi amuombe daktari ruhusa ya kuondoka na mgonjwa wake kwa maelezo kuwa angempeleka kwenye hospitali nyingine kwa matibabu zaidi. Daktari alimshauri kumpeleka KCMC ili akapate huduma bora zaidi. Fatiha alimuandaa Gamutu na kutoka naye hadi nje. Kutokana na kupoteza damu nyingi, hakuwa hata na uwezo wa kusimama mwenyewe, akawa amemshikilia.



    Wazo la kumpeleka KCMC halikumwingia akilini Fatiha, akaona njia bora ni kwenda naye kule ujinini ambako alikuwa na imani kubwa ya kumtibu hadi apone. Baada ya kutoka nje, alizunguka upande wa nyuma kulikokuwa na mbuyu mkubwa, akamshikilia vizuri Gamutu na kufanya ishara za kichawi, wakapotea kimiujiza.



    Kufumba na kufumbua walikuwa tayari wapo kwenye himaya ya majini. Fatiha alimpeleka mpaka kwenye bustani ya maua, mahali walipokuwa wanapenda kukutania kila jioni kipindi Gamutu alipokuwa kule ujinini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alianza kwa kumsafisha kile kidonda kwa maji maalum yaliyokuwa ndani ya kibuyu cheusi. Alipomaliza alitafuta dawa ya mtangetange na kuanza kumkanda nayo. Kwa muda wote huo, bado alikuwa akivuja damu nyingi. Alipomaliza kumkanda, alianza kumnyunyizia unga mwekundu pale kwenye jeraha. Angalau damu ilianza kupungua.



    Baada ya kuhangaika naye kwa saa nyingi, hatimaye alianza kurejewa na fahamu. Akafumbua macho ingawa bado hakuwa na uwezo wa kutambua watu wala mazingira. Aliendelea kutibiwa kwa siku nzima mpaka akapata nafuu kabisa.



    Wakati akiendelea kutibiwa, wanawake wote waliokuwa tayari wamenasa ujauzito wake waliharibikiwa, mimba zikachoropoka. Jambo lile lilimuumiza sana Fatiha kwani tayari alishaanza kuhesabu mafanikio kutokana na kasi aliyokuwa nayo Gamutu.



    Licha ya Fatiha kujitahidi kadiri ya uwezo wake wote kumhudumia Gamutu, bado kuna jambo alishindwa kulirekebisha. Alipochomwa kisu, kiliingia na kwenda kugusa uti wa mgongo, jambo lililosababisha baadhi ya mishipa ya fahamu kuharibiwa vibaya. Hali ile ilimfanya Gamutu apoteze kumbukumbu na uwezo wa kutambua mambo. Kwa kumtazama, alianza kuonekana kama mwendawazimu.



     Baada ya kukaa naye kule kwenye himaya ya majini kwa siku kadhaa, aliamua kumrudisha duniani hasa kutokana na ukweli kwamba, zoezi walilokuwa wamelipanga kulifanikisha la kuzalisha kizazi kipya cha majini lilikuwa limeshindikana na sasa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu na utambuzi.



    Ikumbukwe kuwa baada ya Gamutu kuchomwa kisu tumboni, wanawake wote ambao walikuwa wameshanasa ujauzito wake, walipatwa na tatizo la mimba kuharibika. Vijusi ambavyo vilikuwa vimeanza kutunga ndani ya miji yao ya uzazi vilichoropoka na kufanya zoezi lile lishindikane. Kote alikopita na kuvunja amri ya sita na wanawake kwa staili ya kishirikina, kulibaki na vilio. Damu ilimwagika kutoka kwenye miji ya uzazi.



    Jambo hilo lilimuudhi sana Fatiha kwani lilifanya viongozi wake wamuone mzembe kwa kushindwa kumlinda na kumuongoza Gamutu. Jitihada zote alizofanya zilibaki kuwa historia. Hakuna mimba hata moja iliyobaki salama. Lilikuwa ni zaidi ya janga. Wanawake wengi wakawa wanakimbilia hospitali huku wakilalamikia dalili kubwa ya kutokwa na damu nyingi sehemu za siri.



    Wachache kati yao ndiyo waliogundua kuwa walinasa ujauzito ambao uliharibika. Wengi waliliona tatizo lile kama ni kuvurugika kwa siku zao za mzunguko wa hedhi kulikoambatana na maumivu makali. Nyuma ya pazia kulikuwa na siri kubwa zaidi ambayo ni wachache ndiyo walioitambua.



    Baada ya Gamutu na Fatiha kushindwa kazi, ilibidi akabidhiwe jini mwingine kusimamia zoezi lile. Kwa namna yoyote ilikuwa ni lazima kizazi kipya cha majini kipatikane. Fatiha aliwekwa kwenye chumba maalum kilichokuwa na giza nene na kuanza kupewa mateso kutokana na kufanya uzembe kazini.

    “Kuanzia leo utashushwa cheo ulichokuwa nacho. Inavyoonesha chanzo cha tatizo kilikuwa ni wewe kushiriki mapenzi na binadamu, kisha kumtumia binadamu huyo huyo kwa ajili ya kazi uliyopangiwa, jambo ambalo kimaadili halikubaliki kabisa. Kwa kuwa umeonesha utovu wa nidhamu, kuanzia leo tunakupokonya uwezo wa kwenda duniani na maisha yako yote yatakuwa huku huku.

    “Huruhusiwi kufanya kazi zozote za kutoka nje na ukikaidi amri hii kitakachokutokea kitakuwa ni juu yako mwenyewe,” kiongozi wa majini alikuwa akimsomea Fatiha hukumu baada ya kuonekana alikuwa amezembea kazini.

    Baada ya kushushwa cheo na kupelekwa chumba cha giza, Fatiha alianza kujilaumu kwa kutokuwa makini. Alijuta ni kwa nini alimuelekeza Gamutu aende Arusha wakati alikuwa akifahamu fika jinsi wanawake wa jiji hilo walivyokuwa na roho za kihalifu, hususan kutumia visu au mabeto kama wenyewe walivyokuwa wanaita.

    Aliiweka mikono yake kama anayetabana, akavuta uzingativu kutaka kuona ni nani aliyehusika na kitendo cha kumchoma kisu Gamutu. Japokuwa alikuwa amepewa adhabu ya kutokwenda duniani, kimoyomoyo alijiapiza kuwa ni lazima amshikishe adabu mtu aliyehusika na hujuma zile, hata kama ingemgharimu maisha yake.



    Alijisikia vibaya zaidi kwa sababu alimuacha Gamutu aende duniani wakati akili yake ikiwa haijatengemaa, jambo ambalo liliashiria kuwa Gamutu ataishi kama mwendawazimu kwa siku zote za maisha yake zilizosalia duniani. Alisikitika sana na kujikuta machozi yakimtoka akiwa mle ndani ya chumba cha giza.

    Aliendelea kuvuta uzingativu na mara akaanza kuona picha nzima ya jinsi tukio lile lilivyokuwa. Aliona kuanzia Gamutu alivyoondoka Njiro, Arusha, alivyowanasa wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu cha IAA, alivyojichanganya kwenye kundi la dadapoa, alivyowaopoa wengi kwa mpigo na jinsi walivyoenda kumbadilikia njiani hadi kumchoma kisu.



    Kwa kuwa wakati anashushwa cheo na kuingizwa kwenye chumba cha giza, hakuvuliwa pete yake ya miujiza ambayo ndiyo iliyomuwezesha kufanya mambo ya kijini, alijiapiza kuvunja sheria na kwenda duniani kwa lengo moja tu, kulipa kisasi kwa mwanamke aliyehusika kumchoma Gamutu kisu.

    Sekunde chache baadaye alikuwa kwenye ulimwengu mwingine.



    Alimtafuta yule mwanamke kwa udi na uvumba na kufanikiwa kumkuta akiwa amejilaza na wenzake kwenye geto lao baada ya kufanya biashara ya ngono usiku kucha. Alimtazama kwa jicho la ukali huku wenzake pamoja na yeye mwenyewe wakishindwa kuelewa kuwa kuna kiumbe hatari kilikuwa kikijiandaa kufanya unyama.



    Aliamua kumuua kwa staili ya maumivu makali, akaenda mpaka pale alipokuwa amelala na kumgeuzia juu, akamuweka miguu vizuri na kuingiza mikono yake yote kwa nguvu kwenye viungo vya uzazi vya changudoa yule. Aliingiza mikono mpaka akakishika kizazi, kisha akakinyofoa kwa nguvu huku akiwa hana hata chembe ya huruma.



    Kutokana na maumivu aliyoyahisi mwanamke yule, alipiga yowe huku akiitanua miguu yake, damu nyingi zikaanza kuvuja kama bomba lililopasuliwa. Fatiha hakutaka kuendelea kukaa eneo lile, akaondoka na kile kizazi alichokinyofoa kishirikina. Yule mwanamke alizidi kulia kwa uchungu, wenzake wakaamka na kushangazwa na jinsi hali yake ilivyobadilika ghafla.



    Walijitahidi kufanya jambo ili kuokoa maisha yake lakini haikuwezekana. Damu nyingi zilizomtoka zilisababisha apoteze fahamu ndani ya dakika chache, kisha mauti yakamkuta wakati akiwa njiani kupelekwa hospitali. Baadhi ya wenzake ambao walishiriki pamoja kwenye tukio la kumchoma kisu Gamutu walielewa kuwa mambo yameiva.



    Kila mmoja akaanza kuhaha kivyake kujaribu kuokoa maisha yake. Wengi walikimbilia makanisani na kuamua kuyakabidhi maisha yao kwa Mungu kwa hofu ya kutokewa na tukio kama lile lililouchukua uhai wa mwenzao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gamutu alikuwa akizunguka zunguka kwenye mitaa ya Jiji la Dar huku akiwa na dalili zote za kuwa kichaa. Nywele ambazo siku chache zilikuwa zimetengenezwa kinadhifu, sasa zilibadilika na kuwa timtimu. Nguo alizokuwa amevaa awali ambazo zilikuwa zimepambwa na madoa ya damu, alizivua na kuvaa nyingine chafu ambazo aliziokota kwenye dampo. Kila alipokuwa akitembea alikuwa akiongea peke yake huku akiimba, kucheza na kucheka peke yake. Kichwani alijitwisha zigo la takataka nyingi alizozikusanya dampo.





    Mjomba! Mjomba! Hebu angalia kule!”

    “Kuna nini? Mbona sioni kitu?”

    “Muangalie vizuri yule chizi aliyekaa pale kwenye jalala!”



    “Haaa! Si Gamutu yule? Hebu twende…” aliongea Mzee Mpogole akiongea na mpwa wake, James. Mzee huyu pamoja na ndugu zake wengine walikuwa wakihangaika huku na kule kwa karibu wiki tatu nzima wakimtafuta Gamutu ambaye alipotea kimiujiza wakati walipompeleka kwa mganga, Bagamoyo kutolewa nguvu za kijini alizokuwa nazo.



    Tangu alipotoweka, hawakupata hata usingizi. Muda wote walikuwa wakihangaika huku na kule kumtafuta bila mafanikio. Baada ya kuhangaika sana kwao Bagamoyo, waliamua kwenda jijini Dar es Salaam wakiamini huenda alikimbilia huko na kushindwa kurudi kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika kwenye jiji hilo.



    Baada ya kuhangaika kumtafuta kwa karibu wiki nzima, hatimaye walifanikiwa kumuona lakini hakuwa Gamutu yule waliyemfahamu. Alikuwa na dalili zote zilizoonesha kuwa alikuwa amechanganyikiwa.

    “Gamutu! Gamutu! Unafanya nini hapa? Tumekuja kukuchukua, inuka twende nyumbani,” alisema Mzee Mtogole lakini Gamutu alionesha kuwa alikuwa akielea kwenye ulimwengu mwingine tofauti kabisa. Walizidi kumsemesha lakini hakuwajibu kitu, alipoona wanazidi kumghasi, aliinuka kwa kasi na kutimua mbio kuelekea ndani kabisa ya rundo la takataka.



    Ilibidi mjomba wake na yule ndugu yake mwingine waombe msaada wa wapita njia ili kumkamata. Baada ya purukushani kali, hatimaye walifanikiwa kumkamata na kumfunga kamba mikononi na miguuni, safari ya kurejea Bagamoyo ikaanza mara moja.

    Njia nzima Gamutu alikuwa akisumbua sana mpaka akawa kero ndani ya gari. Mjomba wake alikuwa na kazi ya ziada ya kumtuliza. Walipofika Bagamoyo, ndugu walikusanyana na kukaa kikao cha dharua. Walianza kujadiliana nini cha kufanya baada ya kufanikiwa kumpata ndugu yao akiwa amechanganyikiwa.



    “Mi nafikiri tumpeleke kwa mganga wa kienyeji,” mmoja alitoa wazo.

    “Hapana jamani, bado hatujajifunza tu? Siku ile sote tunakumbuka kizaazaa alichokisababisha kule kwa mganga mpaka sote tukaonekana wachawi, hakuna njia nyingine zaidi ya kumpeleka kanisani akaombewe,” alisema mjomba wake, Mzee Mpogole na wazo lile likaungwa mkono na wengi.



    Walikubaliana kuwa siku ile wapumzike mpaka kesho yake kwani tayari muda ulikuwa umekwenda sana. Wakalala mpaka alfajiri ambapo Mzee Mpogole ndiyo alikuwa wa kwanza kuamka, akaanza kuwaamsha wenzake kwa safari ya kuelekea kanisani.



    Gamutu alianza kuombewa na mchungaji Innocent Mwaluega wa kanisa la kilokole mjini Bagamoyo. Kwa jinsi mchungaji huyo alivyokuwa anasifika kuvunja nguvu za giza kupitia maombi yake, Gamutu hakuwa na ujanja. Kwa kadiri alivyokuwa anazidi kuongeza kasi ya maombi, Gamutu alikuwa akiongea maneno ambayo yalimshangaza kila mmoja.

    Alifichua siri zote za maisha yake, jinsi alivyokuwa na uhusiano na nguvu za giza, jinsi alivyoshiriki kwenye matukio mengi ya kichawi, alivyoshiriki kupoteza roho za watu wasio na hatia na mambo mengine mengi ambayo yaliwaogopesha wote walioambatana naye pale kanisani. Baada ya kusimulia mambo yote, maombi mazito yaliendelea kwa muda mrefu.

    Shughuli ile ilifanyika kwa takribani saa kumi. Baada ya hapo Gamutu akawa hoi bin taaban. Ilibidi ndugu zake wambebe mpaka nyumbani. Mchungaji akawaambia wampeleke tena alfajiri ya siku iliyofuatia. Tangu afanyiwe maombi, Gamutu hakuzinduka mpaka kesho yake. Kitu cha kwanza alichouliza baada ya kuzinduka ilikuwa ni mahali alipo bibi yake.

    Mjomba wake alimweleza kuwa tayari walishamtumia ujumbe na alikuwa njiani kutokea Sumbawanga. Baada ya kuridhika na maelezo yale, Gamutu aliomba mwenyewe apelekwe kanisani alikopelekwa jana yake. Baada ya maandalizi, Mzee Mpogole na ndugu kadhaa wa ukoo wake waliongozana na Gamutu mpaka kanisani ambapo alifanyiwa tena maombi kama jana yake.

    Jioni ya siku hiyo bibi yake aliwasili kutoka Sumbawanga. Akashangaa kumkuta Gamutu akiwa na mabadiliko makubwa tofauti na alivyomuacha. Dalili zote zilionesha kuwa tayari amebadilika na kuwa binadamu wa kawaida.

    ***

    Baada ya kuvunja amri aliyopewa ya kutoenda duniani, Fatiha alifanikiwa kulipa kisasi kwa changudoa aliyemchoma Gamutu kisu na kusababisha mpango mzima uvurugike. Aliporejea ujinini, Fatiha alipewa adhabu kali ambayo ilimmaliza kabisa nguvu zake, akashushwa cheo na kuwa mfagizi wa kasri la majini huku kila mmoja akimdharau kwa uzembe alioufanya kazini.

    Hakuwa tena na uwezo wa kwenda duniani kama awali, hali iliyosababisha azeeke kwa kasi. Baada ya miezi michache alipoteza maisha na huo ukawa ndiyo mwisho wa maisha yake.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog