Search This Blog

NILIBADILIKA NA KUWA JINI BILA KUJIJUA - 4

 









    Simulizi : Nilibadilika Na Kuwa Jini Bila Kujijua

    Sehemu Ya Nne (4)



    Matukio ya ajabu aliyoyasababisha Gamutu yalivuta hisia za wengi kwenye eneo lile. Japokuwa hakuna aliyejua mhusika wa matukio yale, taarifa ziliposambaa kwenye vijiji vinavyopakana juu ya matukio ya wanawake wawili kukutwa wakiwa wameuawa huku miili yao ikiwa na alama za kutisha, kila mmoja alichukua tahadhari.



    WANAUME wenye silaha wakaingia mitaani kumsaka muuaji, wakiwa hawajui adui yao ni nani. Wakati hayo yakiendelea, Gamutu alikuwa akihaha kutafuta mahali pa kutorokea akiogopa kuhusishwa na tukio lile. Bado hamu kali ya kufanya mapenzi ilikuwa ikimsumbua kupita kawaida.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Fatiha uko wapi? Ulinizoesha mwenyewe, angalia sasa ninavyopata taabu,” aliongea Gamutu huku akijaribu kuiweka vizuri sehemu ya mbele ya kaptura aliyokuwa ameivaa ambayo ilikuwa imeinuka.



    Akiwa bado haelewi aelekee wapi, alipata wazo jipya akilini mwake. Alitambua fika kuwa alikuwa na tatizo kubwa ambalo bila kupatiwa ufumbuzi huenda lingemsababishia madhara makubwa. Akaamua mwenyewe kujipeleka kwa wale waganga ambao awali walimfanyia matambiko mawili, tambiko la maisha na tambiko la pili la kumvunja nguvu za kijini alizokuwa nazo baada ya kushiriki ‘mchezo wa kikubwa’ na jini Fatiha.



    Baada ya kutembea umbali mrefu, akikwepa kuonana na mtu yeyote, hatimaye alikaribia nyumbani kwa wale waganga.

    “Yule anayekuja kule ni nani?”

    “Amefanana na Gamutu, mjukuu wa Bi. Lubunga tuliyetoka kumfanyia dawa hivi karibuni.”

    “Mmh, ujio wake ni wa heri kweli, si unakumbuka alikuwa anakataa kabisa tusimfanyie tambiko?”

    “Nakumbuka vizuri, sijui kafuata nini? Ngoja tumuone.”



    Waganga wawili wanawake walikuwa wakijadiliana wakati wakimtazama Gamutu aliyekuwa anapandisha kilima kuelekea nyumbani kwa wale waganga.

    “Shikamooni.”

    “Marahaba Gamutu, hujambo? Bibi yako hajambo?”

    “ Hajambo.”



    Baada ya kukaribishwa ndani, Gamutu alijieleza kuwa amekuja kwa ajili ya kutaka msaada kwani mambo yalikuwa magumu. Alieleza kila kitu, hali iliyowafanya wale waganga watazamane kwa hofu.

    “Mh, kama hali ndiyo hiyo akiamua kutubadilikia hapa ndani akatutaka na sisi kimapenzi, tutafanya nini?”

    “Hawezi bwana, mbona unakosa imani kiasi hicho?”



    “Mh, mwenzangu lazima kujihami, ameshajieleza mwenyewe, unafikiri hilo pepo likimpanda tutaweza kumzuia?”

    “Mimi ndiyo kiboko yake, nimewahi kukutana na hali kama hii nilipoenda Kongo, tena mwanaume mwenyewe alikuwa mtu wa miraba minne lakini nilifanikiwa kumtuliza, atakuwa huyu mtoto aliyezaliwa tunamuona? Akipandisha ya kwake na mimi napandisha ya kwangu.”

    “Mh! Sasa tutamsaidiaje?”



    “Kuna dawa ya kunywa tukimpa mwenyewe atatulia. Ila ingekuwa vizuri kama bibi yake angekuwepo kwani hataweza kutembea kurudi nyumbani mwenyewe kutokana na ukali wa dawa.”

    “Sasa tufanyeje?”

    “We nenda kampe taarifa bibi yake, ngoja mimi nimshughulikie.”

    “Utaweza peke yako?”



    “Hilo siyo tatizo, hakikisha wakati mnarudi mnakuja na dawa ya Mtangetange, si unajua miti yake inapoota?”

    “Najua, ngoja niwahi,” aliongea mganga wa kwanza na kutoka kuelekea nyumbani kwa bibi yake Gamutu, Lubunga. Ndani ya nyumba akawaacha Gamutu na mganga wa pili.



    Ukweli ambao hakuna aliyekuwa akiujua ni kuwa, yule mganga wa pili naye alikuwa na pepo ambalo kila lilipomkumba, alikuwa akipatwa na hamu ya ajabu ya kukutana kimwili na mwanaume lakini kila aliyethubutu kulala naye, hakuamka tena.



    Hali ile ilimfanya aishi maisha ya kipweke sana kwani kila mwanaume aliyemuoa, alifariki siku chache baada ya kufunga ndoa. Akaamua kuelekeza nguvu zake kwenye mambo ya tiba za jadi. Ni hapo ndipo alipokutana na yule mwenzake aliyetoka, ambaye walikubaliana kufanya kazi za kiganga kwa kushirikiana.



    Baada ya kuona mganga wa kwanza ametoka, Gamutu alianza kujisikia hali kama ile iliyomfanya afunge safari hadi mahali pale. Kwa kulitambua hilo, yule mganga aliyesalia alichoma aina fulani ya ubani ambao huamsha mapepo yake. Gamutu aliposikia harufu ya ubani ule, alijikuta akiishiwa nguvu na kunyong’onyea, yule mganga akambeba kirahisi na kumuingiza kwenye chumba cha kulala.



    Japokuwa Gamutu alikuwa ameishiwa nguvu, alikuwa akielewa kila kilichokuwa kinaendelea.

    “Gamutu!”

    “Mmh!”

    “Usiogope, najua ulipatwa na tatizo hili ulipoanza kufanya mapenzi na jini Fatiha. Lakini nikutoe waiwasi kuwa hali yako itatulia kabisa kama utafuata masharti nitakayokupa,” aliongea yule mganga huku akiwa ameusogeza uso wake karibu na wa Gamutu.



    “Masharti gani mganga?”

    “Nataka uwe mume wangu ila watu wengine wasijue kwa sababu na mimi nina tatizo kama lako. Niliwahi kubakwa na majini nikiwa mdogo, kuanzia siku hiyo kila mwanaume ninayelala naye anakufa kama ilivyokutokea wewe.”

    “Sasa na mimi nikilala na wewe si nitakufa?”

    “Hapana, kwa kuwa tumekutana watu wenye matatizo yanayofanana, hakuna atakayekufa kati yetu, ila tutakuwa tukibadilika baada ya kufanya tendo hili.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unamaanisha nini?”

    “Wewe si uliwahi kubadilika na kuwa jini? Hata mimi niliwahi ingawa siku nyingi zimepita.”

    “Mmh! Lakini si mlishanifanyia tambiko la kuzuia nisibadilike tena?”

    “Nguvu nilizonazo mimi zinazidi zile za tambiko, usiogope bwana,” aliongea yule mganga huku akianza kumfungua Gamutu vishikizo vya shati lake kisha vya kaptura aliyokuwa ameivaa.



    Muda mfupi baadaye, Gamutu na yule mganga ambaye kiumri alikuwa sawa na mama yake walikuwa kwenye ulimwengu tofauti. Walikuwa wakielea kwenye ulimwengu wa mahaba ya kishirikina. Hata Bi. Lubunga na yule mganga wa kwanza walipowasili, hakuna aliyewasikia, wakajibanza mlangoni na kushuhudia kila kitu kilichokuwa kikiendelea ndani.



    Walitaka kuingia ndani kwa nguvu kwenda kumuokoa yule mganga kutoka kwenye mikono ya Gamutu lakini walishangazwa na hali iliyoonesha kuwa hata yule mganga naye alikuwa akifurahia mchezo ule kutokana na jinsi alivyokuwa amemkumbatia Gamutu.



    Kilichowashangaza wote ni kwamba, kila mmoja alikuwa akitokwa na damu nyingi huku wakitoa miguno kama wanyama wakali wa porini. Baada ya muda mrefu kupita, walimaliza mchezo wao na kila mmoja akaangukia upande wake, fahamu zikiwa zimewatoka.



    Chumba kizima kilikuwa kimejaa damu, kuanzia shuka walilokuwa wametandika hadi kitanda chenyewe. Hazikuishia hapo bali zilichuruzika hadi chini ambapo ziliweka dimbwi kubwa. Kila mtu aliogopa kuingia chumbani mle.



    Baada ya muda wa takribani saa zima kupita, Gamutu na yule mganga walirejewa na fahamu zao na kujikuta wamelala katikati ya dimbwi la damu. Kila mmoja alishtuka na kuanza kumwangalia mwenzake.

    “Wewe kweli ni mwanaume wa shoka.”

    “Kwa nini unasema hivyo?”



    “Mtu akikuangalia kwa nje anaweza kukudharau, lakini duh! Ndiyo maana jini Fatiha alikuwa anakung’ang’ania,” aliongea yule mganga, maneno yaliyopenya mpaka kwenye masikio ya Bi. Lubunga na yule mganga mwingine.



     “INA maana umenileta ili kunionesha uchafu mnaofanya na mjukuu wangu, mi nilijua mko pamoja na mimi kunisaidia kumbe mna lenu jambo?”



    “Hapana usiseme hivyo ndugu yangu, mimi na wewe si tumekuja pamoja na kushuhudia uchafu huu, iweje unigeuzie kibao? Sijui lolote, hata mimi nashangaa,” yule mganga alijitetea kwa sauti ya chini huku naye akishangaa kilichokuwa kikiendelea.



    Kengele ya hatari ililia kichwani kwa Bi. Lubunga. Kwa hali ilivyoonesha, kama asingechukua hatua za haraka, huenda Gamutu angeharibikiwa kabisa. Matukio ya ajabu yalikuwa yakitokea kwa kasi ambayo ilimfanya ashindwe kuelewa nini cha kufanya kumuokoa mjukuu wake.



    Tatizo la kwanza la Gamutu kuwa na nguvu za kijini baada ya kutoroshwa na kupelekwa kwenye himaya ya majini kisha kuanza kukutana kimwili na jini fatiha lilikuwa bado halijaisha. Akiwa bado analihangaikia ndiyo lile lingine likaibuka.



    “Huyu dawa yake ni kumuondoa kabisa huku na kumpeleka Bagamoyo kwa ndugu wa mama yake, huenda kule akawa salama na kurejea kwenye maisha ya kawaida, ikibidi aendelee na shule, huku hakumfai kabisa,” Bi. Lubunga alijisemea kimoyomoyo huku akiwa bado haamini kama Gamutu anaweza kudiriki kufanya mambo ya ajabu kama yale.



    “Lakini usitulaumu sisi wala mjukuu wako Gamutu, we mwenyewe unafahamu kila kitu kuhusu hili eneo tunaloishi, kwani wewe ni mgeni wa Sumbawanga? Umekulia hukuhuku na unajua kila kitu,” yule mganga aliongea na kujaribu kumrejesha Bi. Lubunga kwenye hali yake ya kawaida.



    “Yaani hakuna chochote utakachoongea nikakuelewa, na afadhali yako, huyo mwenzako ndiyo kabisa? Yaani anajua ninavyohangaika na huyu mtoto halafu na yeye badala ya kunisaidia anazidi kuniongezea matatizo,” aliongea Bi. Lubunga huku akilengwalengwa na machozi. Hakutaka kuendelea kushuhudia uchafu ule, akaondoka kimyakimya bila hata kuaga.



    Wakati Bi. Lubunga na mganga wa kwanza wakiendelea kujadiliana pale mlangoni walipokuwa wamejificha, Gamutu na yule mganga wa pili walikuwa hawajui kuwa walikuwa wakitazamwa. Waliendelea na mazungumzo yao ya kimahaba, huku yule mganga akimpa Gamutu ahadi nyingi za kuyabadilisha maisha yake.



    Wakiwa bado palepale kitandani, Gamutu alikumbuka jambo lililofanya mapigo yake ya moyo yaanze kumwenda mbio kuliko kawaida.



    “Usije ukanisaliti Gamutu kwa kujihusisha na mapenzi na binadamu yeyote, ukithubutu kufanya hivyo na nikagundua, nitakuua wewe na huyo mwanamke wako,” Gamutu alikumbuka maneno aliyokuwa akiambiwa mara kwa mara na Fatiha wakiwa kule kwenye himaya ya majini kabla ya kukombolewa na kurejeshwa duniani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitendo cha yeye kulala na yule mganga na kushiriki mchezo wa kikubwa, kama fatiha alivyokuwa akimsisitizia lilikuwa ni kosa kubwa ambalo adhabu yake ni kifo kwa wote wawili. Hali hiyo ilimfanya Gamutu aanze kuingiwa na hofu kwani alikuwa akiujua vyema ukatili wa Fatiha.



    “Mbona unatetemeka halafu mapigo yako ya moyo yamebadilika?” yule mganga alimuuliza Gamutu huku akiwa amemkumbatia kimahaba.



    “Niache nirudi nyumbani, kuna jambo nimekumbuka limeniogopesha.”

    “Jambo gani?”

    “Fatiha aliniambia nikimsaliti ataniua,” alijibu Gamutu huku akijaribu kujinasua kutoka mikononi mwake.

    “Achana na mawazo ya Fatiha, nguvu zangu ni kubwa sana, hawezi kukufanya lolote, siyo wewe wala mimi. Amini nitakuwa upande wako na nitahakikisha hakuna baya lolote linaloweza kukupata.



    “Hapana, Fatiha namjua mwenyewe, kwa siku chache tulizokaa naye kule kwenye himaya ya majini nimemsoma vitu vingi. Ni kiumbe hatari sana,” alisema Gamutu huku akizidi kujinasua kutoka kwenye mikono ya yule mganga.



    Licha ya kumtoa hofu, Gamutu hakumuelewa, akafanikiwa kujitoa na kushuka kitandani, akakutana na dimbwi la damu ambayo ilikuwa imeanza kuganda.

    “Mh! Hiki nini?”



    “Usiogope Gamutu, hiyo ni hali ya kawaida. Unajua watu wenye nguvu za kishirikina mnapofanya mapenzi kikamilifu lazima kuwe na umwagaji wa damu kama huu, wala usiogope,” aliongea yule mganga hali iliyomfanya Gamutu akumbuke jinsi hali ilivyokuwa alipokutana kimwili kwa mara ya kwanza na Fatiha.



    Hakutaka kupoteza muda, baada ya kuvaa shati lake na kaptura, alitoka mbio na kuanza kuelekea nyumbani kwa bibi yake. Tayari kigiza cha jioni kilishaanza kuingia. Akawa anakatiza vichaka kwa kasi kuelekea nyumbani. Alipofika sehemu yenye njia panda ambayo pembeni yake kulikuwa na mti mkubwa wa Mbuyu, alianza kusikia sauti za ajabu.



    “Alisikia mtu akimuita kwa kulitaja jina lake huku wengine wakicheka na kusindikizwa na sauti ambazo hakuzitambua kama zilikuwa ni za ndege wa usiku na wanyama wa porini. Aligeuka huku na kule lakini hakuona mtu. Zile kelele zilizidi kuongezeka na sasa akawa anazisikia kutokea jirani kabisa na pale alipokuwa amesimama.



    Ghafla alishangaa hali kama ya kimbunga ikija kwa kasi pale alipokuwa amesimama, akiwa anahangaika kujiokoa na kimbunga kile, alishtukia akipigwa na kitu kizito kichwani, akadondoka chini na kuanza kutokwa na damu nyingi puani na mdomoni. Hakuelewa kilichoendelea.



    ***

    Bi. Lubunga alikuwa akitembea kwa kasi kurejea nyumbani kwake. Akili yake ilikuwa ikiwaza mambo mengi kwa wakati mmoja. Mabadiliko ya tabia ya Gamutu yalimfanya awe kama mwendawazimu.



    Akilini mwake alikuwa akifikiria jambo moja tu, kumsafirisha Gamutu hadi Bagamoyo kwa ndugu wa ukoo wa mama yake. Aliamini huenda yale yalikuwa yakimtokea kwa sababu ya kuishi kwenye eneo lililokuwa likisifika kwa kuwa na mambo mengi ya kishirikina na matumizi ya nguvu za giza.



    Aliamini akimpeleka sehemu yenye mazingira tofauti na yale aliyoyazoea, huenda akabadilika kwa kila kitu. Wakati anatembea, alikuwa akifikiria namna ya kupata fedha kwa ajili ya safari ya Bagamoyo.

    “Nikiuza yule ng’ombe wangu mmoja aliyebakia nitapata nauli ya kutosha kumpeleka. Ni heri aondoke vinginevyo ataniua kwa presha,” Bi. Lubunga alikuwa akijisemea kimoyomoyo wakati akipandisha kilima cha kuingilia nyumbani kwake.



    Alipofika alipitiliza mpaka kwenye banda la ng’ombe na akawa anamuangalia ng’ombe wake ambaye awali alipanga aje kutumika kutoa mahari pindi Gamutu atakapofikisha umri wa kuoa.

    Hakutaka kupoteza muda, jioni ile ile alienda kuwasiliana na wafanyabiashara wanaonunua mifugo na kwenda kuiuza mnadani. Walikubaliana bei na wakawa wanasubiri asubuhi ifike ili wakabidhiane.



     Akiwa katika hali ya kupoteza fahamu, Gamutu alitokewa na Fatiha aliyeanza kwa kumuuliza mahali alipokuwa ameiweka pete aliyompa.

    Gamutu hakuwa na jibu kwa sababu hata yeye hakuwa akikumbuka kilichotokea mpaka pete ile ikaondolewa mwilini mwake.



    Alijaribu kuvuta kumbukumbu lakini hakukumbuka chochote. Hakujua atamjibu nini Fatiha aliyeonekana kuwa na hasira kali kwani miongoni mwa vitu ambavyo alimsisitiza sana ni kutoivua pete ile.



    “Naona umeshindwa kuitumia bahati niliyokupa, pete yangu umewapa wanawake wako na bado unanisaliti kimapenzi. Sasa ni lazima ufe kwa kuvunja masharti. Kifo chako kitakuwa gumzo kila kona, nataka nikuoneshe kuwa mimi ni nani,” alisema Fatiha kisha akapotea kimiujiza.



    Muda mfupi baada ya kupotea, Gamutu alirejewa na fahamu na kujikuta akiwa amelala pembeni ya kinjia kidogo kilichokuwa kinaelekea nyumbani kwa bibi yake, jirani na mti mkubwa wa mbuyu. Alikuwa bado anahisi maumivu makali kichwani, sehemu aliyopigwa na kitu kizito. Aligeuza macho huku na kule kama asiyeamini kilichotokea lakini bado ukweli uliendelea kuwa ule ule.



    Aliinuka na kujikongoja mpaka kwa bibi yake, akakuta mlango umerudishwa bila kufungwa na komeo, akausukuma na kuingia moja kwa moja mpaka chumbani kwake. Alijilaza kwenye kitanda kichakavu kilichokuwa mle chumbani mwake, mawazo kibao yakawa yanapishana kichwani.



    Maneno ya Fatiha yalikuwa yakijirudiarudia kichwani mwake kama mkanda wa video. Hakuna kitu alichokuwa anakiogopa kwa wakati ule kama kufa, tena kifo cha kishirikina. Akiwa amejilaza kitandani huku macho yake yakifanya kazi ya kulisanifu dari, alisikia mlango wa chumbani kwake ukisukumwa, bibi yake akaingia.



    “We mtoto shetani sana, wazazi wako wangekuwa hai ningekupeleka maana nimechoshwa na vitendo vyako. Yaani kila siku ni matatizo tu, hili halijaisha unazua lingine,” alisema Bi Lubunga kwa sauti ya masikitiko.



    Gamutu hakujibu kitu, akageukia ukutani na kuendelea kulala huku akiwa bado anasikilizia maumivu makali ya kichwa. Hakuwa na taarifa kuwa bibi yake alishuhudia kila kitu alichokifanya akiwa kule kwa waganga.

    “Sasa utamuoa nani? Huyo jini wako Fatiha au yule mganga wa kienyeji?” alihoji Bi Lubunga huku akionesha hali ya kukatishwa tamaa na vitendo vya Gamutu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gamutu hakuyaamini masikio yake, akamgeukia bibi yake akihisi labda alikosea kuuliza swali lile. Aliamini alichokifanya na yule mganga ni siri yao na hakuna anayefahamu. Alibaki kumkodolea bibi yake macho huku akijihisi aibu usoni.



    “Nilichoamua ni kwamba lazima tusafiri pamoja mpaka Bagamoyo kwa ndugu zako, labda ukifika kule utabadilika, jiandae kwani kila kitu kipo tayari, kesho alfajiri na mapema tunaianza safari,” aliongea Bi Lubunga na kuondoka.



    Japokuwa Gamutu hakuwa amejibu kitu, taarifa kwamba siku inayofuatia alitakiwa kusafiri, zilimfanya ajisikie furaha kubwa ndani ya moyo wake. Hata yeye alikuwa amechoka sana kuishi maisha ya aina ile, akaona labda akibadilisha mazingira atarejea kwenye hali yake ya kawaida kama alivyokuwa awali.



    Usingizi wote ulimpaa, akawa anafikiria kitu kimoja tu, safari. Aliamini akiwa Bagamoyo Fatiha hawezi kumtokea tena hivyo atakuwa ameepukana na vitisho vya kuuawa. Aliamini pia atakuwa mbali na yule mganga ambaye naye hakuwa akimpenda lakini alilazimika kufanya naye mapenzi ili kutuliza hali ile iliyokuwa inamtokea ya kutamani kukutana kimwili na mwanamke.



    ***

    Alfajiri na mapema, Gamutu na bibi yake, Lubunga walikuwa tayari wako barabarani kusubiri basi ambalo lingewasafirisha hadi Mbeya. Baada ya kufika Mbeya wangelala mpaka siku inayofuatia ambapo wangepanda mabasi ya kuelekea jijini Dar es Salaam, kisha Bagamoyo.



    Gamutu alikuwa amebeba mfuko wa plastiki (Rambo) ambao ndani yake kulikuwa na nguo zake chache ambazo nazo zilikuwa kuu kuu. Bibi yake alikuwa amebeba mkoba mdogo ambao ndani yake aliweka fedha alizozipata baada ya kuuza ng’ombe wake.



    Dakika chache baadaye, basi la Sumry lilitokea, wakapanda na kukata tiketi wakiwa ndani ya basi. Safari ikaanza. Wakiwa safarini, hakuna aliyekuwa akimsemesha mwenzake. Bi Lubunga alikuwa akiwaza yake na Gamutu alikuwa akifikiria yake.



    “Mkufu wako ulioachiwa na marehemu baba yako nimekuchukulia, tukifika nitakupa,” alisema Bi Lubunga lakini Gamutu hata hakujali. Kwake mkufu ule haukuwa na maana kuliko pete aliyopewa na Fatiha ambayo wale waganga kwa kusaidiana naye walimvua.



    “Sitaki huo mkufu, nataka pete yangu.”

    “Nayo nimekuchukulia, nitakupa tukifika,” alisema Bi Lubunga lakini Gamutu hakutaka kumuelewa. Akawa anamng’ang’ania ampe ili aivae mle mle ndani ya gari. Kisingizio kikubwa alichokuwa anakitoa ni kuwa, barabarani kuna nguvu nyingi za kishirikina na michezo ya kichawi.



    Kuepusha watu kuwafikiria vibaya, Bi Lubunga alifungua mkoba wake na kutoa pete pamoja na mkufu, akampa Gamutu lakini cha kushangaza akaukataa mkufu alioachiwa na marehemu baba yake na kuichukua pete.

    Ilibidi Bi Lubunga atumie busara za kiutu uzima kumuelewesha.



    Alipovaa pete yake na kukubali kuuchukua na ule mkufu, alianza kuona mambo ya ajabu barabarani. Kwa kuwa siti aliyokuwa amekaa na bibi yake ilikuwa karibu na dereva, Gamutu aliweza kuona kila kilichokuwa kinaendelea mbele.

    Tofauti na watu wengine, Gamutu alikuwa na uwezo wa kuona hata yale ambayo hayaonekani kwa macho ya kawaida.



    Kila mara alikuwa akipiga kelele lakini bibi yake alikuwa akimtuliza kimyakimya. Abiria waliokuwa wamekaa nao jirani walikuwa wakimshangaa sana Gamutu. Bibi yake kukwepa aibu, akawa anadanganya kuwa mjukuu wake anasumbuliwa na malaria iliyopanda kichwani.



    “Dereva simama, simama tafadhali. Nimeona kitu kibaya mbele yetu kinakuja, ukiendelea na safari tutapata ajali mbaya. Simama mimi nishuke,” aliongea Gamutu kwa sauti ya juu na kuwashtua abiria wengine ambao walianza kuhoji kumetokea nini.



    “Kwani ameona nini?” Abiria mmoja alihoji kwa sauti ya juu, mwingine akadakia: “Hawa ndiyo wachawi wenyewe, mbona sisi sote tumekaa siti za mbele lakini hatuoni hayo anayoyasema?” Mwingine kutoka nyuma aliibuka na kushinikiza Gamutu ashushwe.



    Kauli zote zilizokuwa zinatolewa zilikuwa zikigonga kwenye kichwa cha Bi Lubunga. Kauli pekee aliyoitoa ilikuwa: “Mjukuu wangu ana matatizo ya akili, tunampeleka hospitali.”

    Angalau baada ya kauli ile ya Bi Lubunga abiria pamoja na dereva waliamua kumpuuza Gamutu na safari ikaendelea.



     Safari iliendelea mpaka kwenye mji mdogo wa Tunduma kisha jijini Mbeya. Kila kitu kilikuwa kigeni kwa Gamutu, alikuwa akishangaa kuanzia mazingira ya nje na ndani, watu na kila kitu alichokiona.



    Baada ya kuwasili jijini Mbeya, kwa kuwa muda ulikuwa umeenda walilazimika kulala hadi kesho yake ndipo waendelee na safari.

    “Kwa nini ulikuwa unasumbua watu kwenye gari?” Bi Lubunga alimuweka chini mjukuu wake. Vitendo alivyovifanya kwenye basi vilimkera sana bibi yake.

    “Bibi nilikuwa naona watu wakifanya mambo ya ajabu barabarani ndiyo maana nikawa napiga kelele.”



    “Mambo ya ajabu kama yapi?” alizidi kuhoji Bi Lubunga.

    “Mwanzo nilikuwa naona watu ambao hawajavaa nguo wakicheza barabarani, baadaye nikaona watu wengi wakiwa wanachimba kaburi katikati ya barabara,” Gamutu alizidi kujitetea.



    “Sasa hayo machache ndiyo yaliyokufanya uwe unapiga kelele njia nzima? Kumbuka kuwa wewe ulifanyiwa tambiko la maisha ukiwa mdogo. Hakuna mtu anayeweza kukuchezea kirahisi, kuwa na roho ya kiume,” alisema Bi Lubunga na Gamutu akatingisha kichwa kama ishara ya kuelewa kile alichoelezwa.



    Siku ile walilala Mbeya mpaka kesho yake ambapo walipanda basi la kuelekea jijini Dar es Salaam kisha Bagamoyo.

    Alfajiri iliyofuata Bi Lubunga na Gamutu wakawa ndani ya basi la Planet Safari wakitokea Mbeya. Lengo lilikuwa ni kuwasili Bagamoyo jioni ya siku ile ile. “Sasa ina maana tukifika Bagamoyo mimi utaniacha peke yangu, nikipatwa na matatizo nani atanisaidia?” alihoji Gamutu wakati basi walilopanda likizidi kuchanja mbuga.



    “Kuna ndugu zako wengi kule, hutapata shida kabisa. Huo mkufu aliokuachia baba yako nao utakuwa unakulinda usiku na mchana,” alisema Bi Lubunga.

    Basi lilipofika maeneo ya tambarare ya Igawa, eneo linalosifika kwa ajali kutokea, Gamutu alianza tena kupiga kelele kwamba anaona vitu vya ajabu barabarani. Safari hii bibi yake alimuwahi na kumtaka asipige kelele kwani huenda wangeshushwa kwenye basi na kusababisha safari yao kuishia pale.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naona barabara yote imejaa mitego ya kichawi ambayo husababisha ajali. Dereva punguza mwendo tafadhali, tupo jirani na ukanda wa kifo,” kabla hata Gamutu hajamalizia maelezo yake, abiria waliokuwa mbele walishuhudia ajali mbaya ikitokea mbele yao. Basi dogo la abiria lililokuwa likitokea Makambako kuelekea Mbeya lilimshinda dereva kutokana na mwendo kasi na kulivamia lori la mafuta limeegeshwa pembeni ya barabara. Wote walioshuhudia ajali ile walishika vichwa vyao na kumtazama Gamutu aliyekuwa kama amepigwa na shoti ya umeme.



    Abiria waliokuwa wamekaa pembeni ya bi Lubunga na Gamutu walikonyezana na kuanza kuzungumza kwa sauti ya chini.

    “Huyu kijana mchawi nini? Mbona ameongea tu na ajali imetokea?”

    “Yawezekana ana majini, si unajua watu wenye majini wanaona kila kitu?”

    “Mmh mi amenitisha aisee! Akiongea jambo tena kuhusu basi hili tulilopanda mi nateremka,” alisikika abiria mmoja.



    Gamutu aliendelea kueleza kuwa anaona kundi la watu eneo la ajali wakikusanya damu na mifupa. Alitahadharisha kuwa hata basi walilopanda nalo limewekewa mtego wa ajali, hivyo uwezekano wa kufika salama ulikuwa mdogo.

    Kauli ile ilisababisha baadhi ya abiria kuteremka.



    Baadaye safari iliendelea, huku dereva akiwa makini baada ya kupewa angalizo na Gamutu.

    Walipofika kwenye milima ya Udzungwa, eneo liitwalo Kitonga ambalo lilikuwa na kona nyingi kali na miteremko ya kutisha, ambalo pia lilikuwa likisifika kwa ajali za kutisha, Gamutu alianza tena kuweweseka akidai kuna watu wanataka kusababisha ajali.



     Walokole na watu wenye imani nyingine tofauti walianza kusali kila mmoja kwa imani yake wakiomba Mungu awanusuru na kile alichokuwa anasema Gamutu kinataka kutokea. Basi zima lilijaa kelele za sala ya kila mmoja akimuomba Mungu kivyake. Kilichofanya safari hii wasafiri wote kuingiwa na hofu ni kile kitendo cha Gamutu kuzungumza jambo kuhusu ajali kisha wote wakashuhudia basi dogo la abiria likigongana na gari la mafuta.



    “Mbona husali ndugu yangu, huyu kijana akiongea jambo linatokea kweli, unakumbuka tukiwa kule Igawa alitabiri jambo na kweli ajali ikatokea?” abiria mmoja alimwambia mwenzake waliyekuwa wamekaa naye siti moja.



    “Mi namwamini Mungu, siogopi utabiri wa kichawi, kama anaona jambo baya si wote tungeliona?” yule abiria alimjibu mwenzake, wote wakanyamaza.



    Dereva aliongeza umakini akiwa kwenye usukani, akawa anazihesabu kona za Mlima Kitonga huku mguu wake ukicheza kwenye breki. Licha ya kuwa gari halikuwa likienda kwa mwendo kasi, abiria bado hawakuwa na amani. Mara kwa mara walikuwa wakigeuka na kumtazama Gamutu ambaye al;ikuwa amekaza macho barabarani, kama anayeona mambo ya kutisha.



    Tukio lililowashtua wengi, ni pale basi walilokuwa wakisafiria lilipogonga paka wawili weusi. Kwa mujibu wa imani nyingi za Kiafrika, gari au chombo chochote cha usafiri kinapogonga mnyama kama paka au bundi, basi safari hiyo huwa na mikosi na uwezekano wa ajali kutokea huwa mkubwa.



    “Jamani eeh, hao paka wawili waliogongwa ni majini wanaotafuta damu zetu, lazima ajali itatokea mbele,” aliongea Gamutu kwa sauti ya juu na kusababisha taharuki ndani ya basi. Wapo waliopinga na kusema kuwa Gamutu alikuwa anatumiwa na shetani kuwatia hofu wasafiri, wengine wakasema alikuwa na karama ya utabiri wakati wengine walimuita mchawi.



    Licha ya kila mmoja kuzungumza lake, ukweli ni kwamba hofu ilikuwa imewajaa kwenye mioyo yao, kila mmoja akawa anafikiria nini hatma yake ikiwa kweli ajali itatokea.



    “Sasa kama una uwezo wa kuona ajali kabla haijatokea, kwa nini usiwe na uwezo wa kuzuia isitokee?” abiria mmoja aliyekuwa amekaa siti ya nyuma ya Gamutu alimuuliza kwa sauti ya chini huu bibi yake, Lubunga akisikia kila kitu.



    “Sina uwezo huo, anayeweza kuzuia majanga ya aina hii ni Mungu pekee,” Gamutu alijibu kwa sauti ya chini pia. Wakati huo huo akakumbuka jambo. Aliikumbuka pete ya miujuza aliyokuwa amepewa na Fatiha alipokuwa kule kwenye himaya ya majini.



    Alikumbuka maelezo ya Fatiha kuwa pete ile ilikuwa na uwezo wa kufanya chochote ambacho angekiomba. Akaingiza mkono mfukoninakuanza kuitafuta. Kumbukumbu zake zilimuonesha kuwa kabla hawajaondoka Sumbawanga kwa safari ile ya Bagamoyo, bibi yake alimkabidhi kila kitu chake. Aliendelea kujipekua mwili mzima na hatimaye akaipata.



    Kwa kutumia mikono yote miwili, aliishika pete ile, akainamisha kichwa nakuanza kuzungumza maneno ambayo hakuna aliyeyaelewa. Ilikuwa ni lugha inayotumiwa na majini wanapofanya tahajudi. Aliendelea kufanya vile kwa muda wa takribani dakika kumi, kisha akatulia na kuendelea kuangaliambele huku ile pete ikiwa mikononi mwake.



    Yale mauzauza aliyokuwa anayaona kabla ya kuiambia jambo pete ile, yalitoweka ghafla na sasa akawa na imani kubwa kuwa kuna nguvu inayomlinda yeye na wote waliokuwa ndani ya basi lile. Safari iliendelea huku kila mmoja akiwa kimya, akimuomba Mungu wake kimoyomoyo.



    Baada ya kumaliza Mlima Kitonga, abiria wote walimshukuru Mungu wao na sasa angalau wakawa na imani ya kufika salama. Dereva akaongeza mwendo kufidia muda waliopoteza Kitonga. Baada ya masaa kadhaa wakawa wanakatiza kwenye mbuga za wanyama za Mikumi. Walipofika eneo lile, Gamutu alianza tena kuona mauzauza, lakini kwa kuwa pete yake ilikuwa bado mikononi, akaiambia jambo na mambo yakarejea kuwa shwari.



    Walipowasili Morogoro, abiria wengi walishuka kwenye basi lile na kuhamia magari mengine, wakihofia kuwa huenda ule mkosi wa kugonga paka weusi ukaendelea kuliandama basi lile na kusababisha ajali kama Gamutu alivyokuwa akitabiri.



    Safari iliendelea na hatimaye Gamutu na bibi yake, Lubunga wakawasili mkoa wa pwani ambapo walitafuta usafiri wa kuwafikisha Bagamoyo. Hatimaye wakawasili kwenye kitongoji cha Mtakuja, ilipokuwa asili ya ukoo wa marehemu mama yake Gamutu pamoja na ndugu wengine.



    Walipokelewa kwa shangwe na nderemo kwani tangu Gamutu azaliwe, hakuna ndugu yake hata mmoja wa upande wa mama yake aliyekuwa anamfahamu. Siu ya kwanza ugenini ikapita. Kesho yake Bi Lubunga akaomba kufanyike kikaocha wanandugu wote ili awaeleze matatizo ya Gamutu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hilo lilifanyika, ndugu wote wa ukoo wao wakaitwa na kikao kikafanyika.

    “Hatujawahi kuwa na mtu mwenye matatizo kama ya Gamutu kwenye familia yetu, lazima tukafanye tambiko na kuiomba mizimu kama kuna jambo tumekosea tusamehewe,” aliongea mzee Mpogole ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikao kile.



    Wazo lile lilikubaliwa na kila mmoja, wakapanga kwenda kuwatafuta waganga mashuuri katika ukanda wa bagamoyo kwa ajili ya kuongoza tambiko lile. Bi Lubunga aliomba udhuru kuwa wakati wao wanajiandaa kwa ajili ya tambiko hilo, yeye anaomba arejee kwake Sumbawanga kwa ajili ya kutunza mifugo pamoja na nyumba yake.



    Ombi lile lilikubaliwa na siku ya tatu akaianza safari ya kurejea Sumbawanga akimuacha Gamutu mikononi mwa ndugu zake. Taratibu zote kwa ajili ya tambiko lile zikawa zinaendelea. Ndugu wakachangishana nafaka kama mtama na ulezi na fedha kwa ajili ya kuwalipa waganga ambao wangefanya kazi ile.



    “Atakuwa ametupiwa vitu vya ajabu huko Sumbawanga alikokulia, lakini ilimradi ameletwa kwetu kila kitu kitaenda sawa,” aliongea mzee Mpogole. Kwa sikuzote tatu alizokaa pale Bagamoyo, hakutokewa na jambo lolote kama ilivyokuwa alipokuwa Sumbawanga, jambo lililomfanya hata yeye mwenyewe aamini kuwa alikuwa akielekea kupona.



    Usiku wa nne, Gamutu akiwa usingizini, alitokewa na Fatiha kwa njia ya ndoto.

    “Afadhali umeondoka kule na kuja huku kwani nilikuwa nipo mbioni kukuua wewe pamoja na yule mganga wako mliyevunja amri ya sita. Mshukuru sana bibi yako kwa kukuleta huku,” aliongea Fatiha na kumfanya Gamutu angalau awe na amani moyoni mwake.



    Fatiha alizidi kumwambia kuwa, ndugu zake walikuwa mbioni kumfanyia tambiko ambalo bila msaada wake yeye (Fatiha) angepoteza maisha.



    “Tambiko hilo litahusisha kuondolewa kwa nguvu zako zote mwilini ambazo kimsingi ndiyo zinazofanya uendelee kuishi. Hakuna anayejua kuwa ulkizaliwa tayari ukiwa na nguvu za kijini isipokuwa bibi yako, na kwa kuwa hakuwaambia jambo lolote, ukipelekwa kufanyiwa tambiko basi lazima ufe,” alisema fatiha.

    “Sasa nitafanya nini Fatiha, niokoe tafadhali!” alisema Gamutu.



    “Siwezi, wewe mkaidi sana, nipindi kile nimekusaidia lakinimwishowe umeishia kunifanya mjinga, safari hii nitaacha dunia ikufundishe, kwa heri, ” alisema Fatiha na kupotea kimiujiza. Muda mfupi baadaye Gamutu alishtuka usingizini na kupiga kelele zilizowaamsha wote waliokuwa wamelala mle ndani.



    “Kwani kuna nini kilichotokea?” aliuliza mzee Mpogole ambaye ndiye aliyekuwa amepewa jukumu la kumsimamia Gamutu mpaka matatizo yake yaishe.



     ALFAJIRI na mapema, Bi Lubunga aliaga na akasindikizwa mpaka stendi kwa ajili ya kuianza safari ya kurejea Sumbawanga yalipokuwa makazi yake.Kichwani alikuwa akijisifu akiamini ameutua msalaba mzito uliokuwa ukimuelemea. Aliamini Gamutu atakuwa salama Bagamoyo kuliko kule Sumbawanga, akawa anaomba kwa mizimu yake mambo yote yaende kama yalivyopanga.



    Mzee Mpogole aliniahidi kuwa watakuwa wakiwasiliana mara kwa mara kumjuza yote yatakayokuwa yanaendelea. Baada ya Bi Lubunga kupanda basi, Mzee Mpogole pamoja na ndugu wengine waliokuwa wamemsindikiza, walirejea nyumbani tayari kwa kazi ya kumpeleka Gamutu kwa mganga wa kienyeji.



    Akiwa bado na usingizi mzito, Gamutu alishtuka baada ya kusikia mlango wa chumba chake ukigongwa kwa nguvu. Akilini mwake aliamini huenda ni bibi yake amekuja kumuamsha kama ilivyokuwa kawaida yake. Aliinuka kichovu na kuvaa nguo zake, akausogelea mlango, alipofungua macho yake yakagongana na ya Mzee Mpogole.



    “Vipi mjomba, bado umelala? Amka bwana, mtoto wa kiume hutakiwi kulala hivyo, tayari kumepambazuka,” alisema mzee yule, Gamutu akatoka chumbani na kuanza kujinyoosha.

    “Bibi yuko wapi?”



    “Mbona ameshaondoka? Hivi unavyotuona tumetoka kumsindikiza, lakini amesema atarejea baada ya siku chache kuja kukuchukua,” alisema Mzee Mpogole na kumtoa hofu Gamutu. Kitendo cha bibi yake kuondoka bila hata kuagana naye kilimfanya Gamutu awe na mawazo mengi kichwani mwake. Alitambua fika kuwa bibi yake hakuwa akipendezewa na vitendo vya ajabu alivyokuwa akivifanya kule Sumbawanga. Kuondoka bila kumuaga kulitosha kuonesha jinsi alivyokuwa amemchoka.



    “Lakini hata mimi sipendi hali hii, nitaendelea kuteseka mpaka lini? Nitakuwa mgeni wa nani?” Gamutu alikuwa akijiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu. Alijiandaa kama mjomba wake alivyomwambia na muda mfupi baadaye wakaondoka wakiwa sambamba na wajomba zake wengine wawili.



    “Kwani tunaenda wapi?”

    “Tunakupeleka kwa mtaalam mmoja akakuangalie, inavyoonesha kuna mtu alikuchezea tangu ukiwa mdogo ndiyo maana unatokewa na mambo ya ajabu,” alisema Mzee Mpogole na kuungwa mkono na wale wajomba zake wengine.



    “Unajua marehemu mama yako alilazimika kuhama huku na kwenda kuolewa mbali na mwanaume mwingine (marehemu baba yake Gamutu) kwa sababu alikuwa akirogwa sana akiwa huku. Kila alipokuwa akipata ujauzito, alikuwa akijifungua watoto wafu au ujauzito kuharibikia tumboni, ni wewe peke yako ndiye uliyesalimika. Hii inamaanisha huenda ulichezewa tangu ukiwa tumboni.



    Bila sisi wajomba zako kukuhangaikia na kukupeleka kwa wataalamu wa tiba za jadi mwisho wako utakuwa mbaya sana, usije kuhisi kuwa tuna nia mbaya na wewe... tunataka kukusaidia,” aliongea Mzee Mpogole kwa busara wakati wakikatiza vichaka kuelekea ka mganga wa kienyeji.



    Wakati akizungumza maneno yale, Gamutu alikuwa akikumbuka maneno aliyoambiwa na Fatiha usiku alipomtokea ndotoni. Alibaki njia panda akiwa hajui nini cha kufanya. Alishindwa kujua kama afuate ushauri wa Fatiha wa kukataa kupelekwa kwa waganga au asikilize yale aliyokuwa anaambiwa na wajomba zake. Hakupata jibu.



    Baada ya kutembea umbali mrefi, hatimaye waliwasili kwa mganga Njiwa Manga aliyekuwa akisifika Bagamoyo yote na maeneo ya jirani. Walipofika nyumbani kwake, japokuwa ilikuwa bado ni asubuhi, walikuta idadiu kubwa ya wagonjwa wakiwa wamekaa nje kusubiri huduma ya mganga yule. Ikabidi nao wake kwenye foleni kusubiri zamu yao.



    Wakiwa kwenye foleni, macho ya Gamutu hayakuwa yakitulia.Muda wote alikuwa akigeuka huku na kule kama anayemtafuta mtu.

    “Mbona hutulii mjomba?” Mzee Mpogole alimuuliza baada ya kuona hali aliyokuwa nayo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hamna kitu mjomba,” Gamutu alidanganya. Ukweli ni kwamba alianza kusikia mambo ya ajabu yaliyoashiria kuwa hali yake ilikuwa ikitaka kurejea kama mwanzo. Alikuwa akisikia sauti ya Fatiha ikimuita mazikionimwake, akahisi huenda tayari atakuwa amefika eneo lile kichawi, akawa anageuka huku na kule akihisi huebda atamuona.



    Hakuna muda aliokuwa anahitaji msaada wa Fatiha kama ule. SIku zote bibi yake ndiye aliyekuwa akimpa mwongozo wa nini cha kufanya, kitendo cha kuondoka na kumuacha mikononi mwa wajomba zake kilikuwa sawa na pigo kubwa kwani hakujua kama hali yake itabadika nani atakayemsaidia.



    Alitamani Fatiha atokee kimiujiza ili ampe maelekezo ya nini cha kufanya kwani hakuwa tayari kufa kwa kuvunja masharti. Akiwa bado anajishauri nini cha kufanya, sauti ya Fatiha ilizidi kuongezerka na sasa akawa anamsikia kama yupo jirani kabisa na pale alipokuwa.



    Alitamani kuitikia ili apewe maelekezo ya nini cha kufanya lakini akaogopa kueleweka vibaya na wajomba zake.

    “Naomba nikajisaidie mara moja, nakuja sasa hivi,” Gamutu alidanganya kwa lengo la kutaka kwenda kumsikiliza Fatiha alichotaka kumwambia.



    Aliporihusiwa alisimama na kujifanya anaelekea chooni lakini badala yake akazunguka nyuma ya nyumba na kwenda mpaka kwenye miti ya mikorosho. Akiwa pale Fatiha bado alikua akimuita, akamuitikia na kumsikiliza alichotaka kumwambia. Alisikia sauti tu na hakuwa na uwezo wa kumuona.



    “Kwa nini hutaki kusikiliza ushauri ninaokupa. Umeshafanya makosa mengi lakini nikiajitolea kuadhibiwa mimi ili wewe ubaki salama. Hii yote ni kudhihirisha mapenzi wangu kwako.



    Sasa ukishindwa kusikiliza hiki nitakachokuambia shauri yako. Ondoka haraka hapo kwa huyo mganga.



     KATIKA kumthibitishia kuwa kile alichokuwa anakizungumza kilikuwa kweli, Fatiha alimwambia Gamutu kuwa ateme mate kwenye kiganja chake cha mkono wa kushoto kisha ajipake machoni na kutamka neno Mantra mara kumi na tatu kisha atakuwa na uwezo wa kuona kila kilichokuwa kinaendelea pale kwa yule mganga.



    “Ukimaliza kutamka neno Mantra, tembea kinyumenyume mpaka ukauguse ukuta wa nyumba ya mganga kwa nyuma. Utaona mazingaombwe yote yanayoendelea,” sauti ile ya Fatiha ilipotea baada ya kutoa maelekezo kwa Gamutu. Kilichofuatia ilikuwa ni utekelezaji wa kile alichoelekezwa.



    Katika hali ambayo hata mwenyewe hakutaka kuiamini, baada ya kufanya kama alivyoelekezwa na Fatiha, Gamutu alishangaa kuona watu wote waliokuwa wamejipanga foleni nje ya nyumba ya mganga wakiwa hawana nguo. Alishangaa zaidi kwani awali kabla hajafanya kama alivyokuwa ameelekezwa na Fatiha, alikuwa akiwaona wamevaa nguo kama kawaida.



    Alizidi kupigwa na butwaa zaidi baada ya kugundua kuwa kumbe hata yeye hakuwa amevaa nguo. Akawa na kazi ya ziada ya kuficha maumbile yake nyeti kwa kutumia kiganja cha mkono wa kushoto. Alipoangalia pale wajomba zake walipokuwa wamekaa, alitahayari kuona nao wako uchi.



    “Mhh!” Gamutu aliendelea kuwashangaa watu waliokuwa pale nje. Ni dhahiri hakuna aliyekuwa anajua kuwa hajavaa nguo kwani hakuna aliyeonekana kujali wala kujificha kama alivyokuwa anafanya Gamutu. Kwa mwendo wa kunyata alitembea hadi pale alipokuwa amekaa kabla hajatokewa na Fatiha, akajichomeka katikati ya wajomba zake ambao hawakumuona wakati anarejea.



    Akawa anaendelea kushangaa. Mlango wa kuingilia ndani kwa mganga ambao awali aliona kama umetengenezwa kwa miti ya porini, alishangaa kugundua kuwa kumbe ulikuwa umetengenezwa kwa mifupa ya binadamu. Hata miti iliyotumika kujengea nyumba ile, ilikuwa ni mchanganyiko wa mifupa na miti, ingawa awali alikuwa anaona imejengwa kwa miti.



    Mahali walipokuwa wamekaa palikuwa na mafuvu mengi ya binadamu ambayo awali alikuwa anaona kama ni vifuu vya nazi. Kila kitu ambacho awali alikuwa anakiona cha kawaida sasa alikiona kwa mtazamo tofauti. Alijikuta mapigo ya moyo yakimuenda kasi kuliko kawaida.



    Akiwa bado anashangaa mazingaombwe yaliyokuwa yanafanywa na mganga yule, alishangaa mlango wa kuingilia ndani ukifunguliwa, mzee mfupi wa makamo ambaye bila hata kuuliza Gamutu alimtambua kuwa ndiyo mganga mwenyewe kwa jinsi alivyokuwa amejichora usoni, alitoka kwa kasi huku sura yake ikiwa na makunyanzi kuonesha kuwa alikuwa amekasirika. Akaanza kupepesa macho huku na kule kama anayetafuta kitu.



    Baadhi ya wagonjwa waliokuwa kwenye foleni walimsabahi lakini hakuitikia, akawa anazidi kupepesa macho mpaka alipomuona Gamutu. Akamkazia macho na kuanza kutembea kwa kasi kuelekea pale alipokuwa amekaa. Ieleweke kuwa baada ya Gamutu kufanya kama vile alivyokuwa ameelekezwa na Fatiha, hakuwa akionekana kwa macho ya kawaida.



    Hata pale alipokuwa amekaa, hakuna mtu mwingine yeyote aliyekuwa na uwezo wa kumuona zaidi ya yule mganga.



    Yule mganga alipomkaribia, Gamutu alisimama, wakawa wanatazamana machoni.

    “Umetumwa kuja kunivurugia biashara yangu siyo? Kwa nini unataka kuniadhiri? Unataka kuona uwezo wangu siyo? Sasa nisubiri hapohapo,” aliongea yule mganga kwa sauti nzito yenye kutetemesha, akageuka kwa kasi na kuanza kutembea kwa hatua za haraka kuelekea ndani kwake.



    Wagonjwa wote walibaki wamepigwa na butwaa wakiwa hawaelewi mganga wao alikuwa anaongea na nani. Sekunde chache baadaye, sauti ya Fatiha ilimjia Gamutu ikimhimiza kuondoka eneo lile haraka iwezekanavyo. Gamutu hakutaka kupoteza muda, aliinuka na kuondoka kwa kasi akiwa haelewi anaelekea wapi. Alipotoka kwenye eneo la mganga yule, alijiangalia tena mwilini lakini tofauti na awali, alikuwa amevaa nguo zake kama kawaida.



    Baada ya kutembea kwa umbali mrefu akiwa haelewi anakoelekea, Gamutu alijikuta ametokea kwenye msitu mkubwa. Kwa kuwa alikuwa ametembea kwa umbali mrefu, alilazimika kukaa na kuegamia kisiki cha mti kwa lengo la kupumzika. Kichwani mwake alikuwa akiyatafakari yote aliyoyaona kule kwa mganga, akawa anatikisa kichwa kama mtu aliyegundua jambo zito.



    Akiwa amekaa pale chini, alihisi akianza kunyemelewa na usingizi, akalala. Alikuja kuzinduka baada ya kuhisi kitu cha baridi kikimtambaa shingoni. Alipofumbua macho, almanusra afe kwa kihoro kwani aliona nyoka mkubwa mweusi akijiviringisha shingoni mwake. Sauti ya Fatiha ikasikika ikimwambia kuwa atulie vilevile bila kutingishika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gamutu alitii, lile joka likaendelea kumviringisha mwili mzima kisha likakielekeza kichwa chake kwenye usawa wa uso wa Gamutu.

    Kwa jinsi ilivyokuwa, kama asingefanya jambo kwa haraka, joka lile lingeweza kumgonga na kumuachia sumu ambayo huenda ingeuchukua uhai wake ndani ya muda mfupi.



    “Nani amekutuma kuja kunipima nguvu?” alishangaa sauti kama ya binadamu ikitoka kwenye kichwa cha yule nyoka, jambo lililomuongezea hofu kuu moyoni mwake.



    Kufumba na kufumbua alishangaa lile joka likianza kujinyonganyonga likiwa bado limemviringisha vilevile, hali iliyosababisha maumivu makubwa kwa Gamutu kwenye shingo na mbavu zake. Baada ya kujinyonganyonga, alishangaa likianza kubabuka ngozi kama limemwagiwa tindikali, likamuachia Gamutu na kuanza kutambaa kwa kasi kuekelea vichakani huku likitoa sauti za kutisha.

    Lilipomwachia na kuondoka tu, alishangaa kuona Fatiha akitokea nyuma ya mti mkubwa na kusimama mbele yake.



    “Pole! Najua umeumia kidogo,” alisema Fatiha na kumuinamia Gamutu pale alipokuwa amekaa, akamshika mkono na kumuinua kisha wakakumbatiana.

    “Ooh Gamutu wangu, nimefurahi kukutana tena na wewe, vipi za siku nyingi?” aliongea Fatiha huku akizidi kumkumbatia kimahaba, jambo ambalo lilianza kuamsha hisia za Gamutu zilizokuwa zimepoa. Ni kweli siku nyingi zilikuwa zimepita tangu walipokutana kwa mara ya mwisho.



    “Japokuwa umenitesa na kunidharau kwa siku nyingi, bado upendo wangu kwako uko palepale na ndiyo maana napigania kuokoa maisha yako,” alisema Fatiha huku akimpiga busu Gamutu kwenye shavu la kushoto.



    Gamutu hakuweza kujibu kitu kwani alikuwa bado analifikiria lile joka lililotaka kumtoa uhai pamoja na yule mganga. Fatiha alilitambua hilo, akazidi kumkumbatia kimahaba na kumtaka waingie ndani kabisa ya msitu ule wakatimiziane haja zao za kimapenzi.



    “Hapana Fatiha, siko tayari kufanya chochote na wewe japokuwa umenisaidia sana,” alijitetea lakini Fatiha akazidi kumvuta huku akimfanyia michezo ya kimahaba. Licha ya kujivunga, kiukweli hata Gamutu mwenyewe alikuwa akitamani kushiriki mchezo wa kikubwa na Fatiha kwani siku nyingi zilikuwa zimepita.





    Wakawa wanapashana joto, kila mmoja akitoa miguno ya kimahaba. Sekunde chache baadaye walikuwa wakielea kwenye ulimwengu wa mahaba. Kila mmoja aliwajibika kisawasawa kwani walipotezana kwa siku nyingi, kwa hamu na uchu wa hali ya juu wakaendelea kulifaidi tunda haramu la mti uliokatazwa. Miguno ya kimahaba ndiyo kitu pekee kilichokuwa kinasikika wakati Gamutu akilishambulia shamba la Fatiha na kuchimba kwa fujo huku kijasho kikimtoka.



    Gamutu na Fatiha wakiwa kwenye hali ile, walishtukia yule mganga akiwatokea na kuanza kuzungumza kwa ukali. Alikuwa akilalamika kuwa wameamua kumharibia kazi yake bila sababu kwa kuvunja amri ya sita kwenye msitu mtakatifu aliokuwa anautumia kuchimba dawa za asili. Akaapa kuwa atawaonesha jeuri yake na watamtambua kwa nini anaitwa Njiwa Manga Concord. Baada ya kuongea maneno yale, alipotea kimiujiza na kuwaacha Gamutu na Fatiha wakiwa wamepigwa na butwaa.



    “Hawezi kutufanya lolote, nguvu zake ni za kiwango cha chini sana. Anachoweza ni kuwafanyia watu viini macho na kuwatapeli fedha zao. Waganga wengi wako hivyo!” alisema Fatiha na kumtoa hofu Gamutu ambaye alishaanza kutetemeka. Waliendelea na walichokuwa wanakifanya mpaka wote walipotosheka, wakainuka na kuanza kutembea taratibu huku wakiwa wameshikana mikono kimahaba.



    “Unaweza kuniambia ni kwa nini bibi yako aliamua kukuleta huku Bagamoyo na kukuacha peke yako?”

    “Sababu kubwa ilikuwa ni wewe kwani uliponitelekeza nilipatwa na hali ya ajabu ya kutamani kufanya ngono kuliko kawaida. Nikasababisha vifo vya wanawake kadhaa. Bibi alipogundua ndiyo akaamua kunisafirisha haraka kuja huku,” alijibu Gamutu huku akikwepa kutazamana na Fatiha kwani aliyatambua makosa yake.



    “Ulipatwa na hali gani?”

    “Nilikuwa nikijisikia hamu kali ya kukutana kimwili na wewe, kwa kuwa hukuwepo, ikabidi niwe namvamia mwanamke yeyote ambaye anakuja mbele yangu.”

    “Kwa hiyo ukakiuka masharti niliyokupa ya kutokutana na mwanamke mwingine yeyote zaidi yangu!”

    “Nisamehe Fatiha! Nilikuwa nashindwa kujizuia.”

    “Baada ya hapo nini kilitokea?”



    ”Kama ulivyokuwa umeniambia awali, wanawake wote niliokutana nao walipoteza maisha tukiwa kwenye tendo, isipokuwa yule mganga aliyenifanyia tambiko.”

    “Kwani naye ulikutana naye kimwili?”

    “Nisamehe Fatiha, baada ya kuona hali ni mbaya, niliamua kwenda kwake kuomba msaada, badala ya kunisaidia akaniambia anataka niwe mume wake.”



    “Sasa kwa taarifa yako, kuanzia siku mliyofanya huo ujinga wenu, alipoteza nguvu zote za kiganga na hivi ninavyoongea na wewe tayari nimeshamgeuza msukule, anafanya kazi na misukule wenzake kule kwenye himaya yetu.”



    “Haaa!” Gamutu alishtuka kupita kiasi kusikia kauli ile kutoka kwa Fatiha. Hakutaka kuamini kuwa ni kweli yule mganga anaweza kuwa ameshageuzwa msukule. Alimtazama Fatiha kwa jicho la woga, akawa anatetemeka.



    “Hata wewe ni kwa sababu nakupenda ndiyo maana niliamua kuahirisha nilichokuwa nimekipanga. Ilikuwa ufe kwenye ajali ya gari wakati mkisafiri na bibi yako kuja huku, nikaahirisha mpango wangu,” alisema Fatiha, kauli iliyozidi kumuongeza Gamutu hofu.



    “Hutakiwi kuniogopa, cha msingi ni kufuata maagizo ninayokupa, ukifanya hivyo utafurahi mwenyewe, lakini ukiwa unakaidi ninachokwambia nitakufunza adabu. Kibaya zaidi kila unachokifanya huwa nakiona, usije ukafikiri unaweza kunificha jambo,” Fatiha alizidi kuchimba mkwara huku macho yake yakibadilika rangi na kuwa mekundu na ya kutisha.

    “Lakini Fatiha, mbona badala ya kuniambia mbinu zitakazoniweka salama wewe una kazi ya kunitishia maisha?”



    “Sikutishii maisha ila nakwambia ukweli. Nimetokea kukupenda sana kiasi ambacho najihisi wivu kukuacha wakufaidi wanawake wengine.”

    Wakati wakiendelea na mazungumzo yale, walisikia upepo mkali ukivuma kutokea nyuma yao, ukiambatana na ngurumo kama za radi. Fatiha akamwambia Gamutu asigeuke kwa sababu alishagundua kuwa ni yule mganga Njiwa Manga ndiyo alikuwa akiwajaribu kwa nguvu za kishirikina.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usigeuke nyuma Gamutu, we tazama mbele tu, ukiona unashindwa fumba macho,” alisema Fatiha huku ule upepo ukizidi kuwakaribia. Milio ya miti iliyokuwa inavunjwa na kurushwa juu na upepo ule pamoja na milio ya radi kali vilimfanya Gamutu apatwe na hofu kuu. Alijitahidi kujikaza kiume lakini hofu ikamzidi nguvu. Alipogeuza kichwa pembeni kumtazama Fatiha, hakumuona, akajikuta amebaki peke yake.



    Bila kujitambua akajikuta akikiuka masharti ya kutogeuka nyuma aliyopewa na Fatiha. Alipogeuza kichwa tu, alishangaa akizolewa na kimbunga kikali, akarushwa juu na kuchanganywa na takataka nyingine zilizokuwa zimezolewa na upepo ule, akapoteza fahamu.



    Hakuelewa kilichoendelea mpaka alipozinduka na kujikuta yupo ufukweni mwa bahari, akiwa hana nguo hata moja. Alijaribu kukumbuka kilichomsibu lakini kumbukumbu zake ziligota kwenye upeo wa kufikiri. Hakuna alichokikumbuka. Akiwa bado anajiuliza amefikaje mahali pale ambapo wala hakutambua ni wapi, alisikia sauti ya mtu akilitaja jina lake. Alijaribu kugeuka huku na kule lakini wala hakumuona mtu.



    Sauti ile iliendelea kumuita huku ikimbembeleza aitike. Sauti nyingine ambayo aliitambua kuwa ni ya Fatiha ilikuwa ikimnong’oneza sikioni kuwa asiitike kwani kwa kufanya vile atakuwa amekubali mwenyewe kuchukuliwa msukule na yule mganga. Safari hii hakutaka kufanya uzembe kama mara ya kwanza, akaisikiliza sauti ya Fatiha na kuamua kutomuitikia yule mtu aliyekuwa anamuita.



    Baada ya kukaa pale ufukweni kwa muda mrefu, alitamani kusimama ili apeleleze vizuri pale ni wapi kwani hakuwahi kufika kabla. Katika hali ya ajabu, alipojaribu kusimama alishindwa kutokana na miguu yake kuishiwa nguvu, akawa anasikia baridi kali kwenye mifupa ya miguuni kama amewekwa ndani ya friji. Alijaribu kusimama tena lakini hali ilikuwa ileile, akasikia vishindo vya mtu akija kutokea upande wa nyuma.



    “Pole! Lakini haya yote umeyataka, hivi kwa nini huwa hupendi kusikiliza maelekezo ninayokupa? Siku nyingine utakufa huku unajiona,” alisema Fatiha huku akiinama pale Gamutu alipokuwa amelala. Mkononi alikuwa ameshika majani ambayo Gamutu hakuwahi kuyaona.



     “Haya majani yanaitwa kahungo, huwa yanatibu tatizo la kupooza miguu na hayapatikani sehemu nyingine yoyote zaidi ya chini ya bahari. Yule mpuuzi alikuwa anataka kukuweka kilema cha miguu ili usiwe na uwezo wa kutembea tena wala kufika nyumbani kwake. Ameshaona wewe ni adui kwake kwani baada ya kushuhudia anayoyafanya pale kwake, dawa zake zote za mazingaombwe zimeisha nguvu, wateja wote wamemkimbia ndiyo maana ana hasira,” alisema Fatiha huku akianza kumchua Gamutu miguu.



    Katika hali iliyozidi kumshangaza Gamutu, baada ya Fatiha kumchua miguu, alisikia kama moto unawaka kwenye miguu yake, kisha ule ubaridi aliokuwa anauhisi mwanzo ukaisha, miguu ikawa na nguvu kama awali, akasimama kwa msaada wa Fatiha, wakashikana mabegani na kuanza kutembea taratibu ufukweni.



    “Gamutu!”

    “Naam!”

    “Nataka nikupe kazi ya kufanya, unajua unazidi kukua na huna dira yoyote maishani. Mwanaume kujishughulisha!”

    “Mmh, nitaweza kufanya kazi gani mimi? Hata shule sikumaliza na sina ujuzi wowote kichwani, labda unifundishe dawa za mitishamba niwe mganga wa kienyeji.”



    “Yaani akili zako ndiyo zimeishia hapo! Uwe mganga halafu iweje? Siyo lazima uwe umesoma mpaka chuo kikuu ndiyo unaweza kujitegemea na kuwa na mafanikio. Mi nataka uwe msimamizi wa mradi mmoja ninaotaka kuuanzisha na kama ukifanya kazi inavyotakiwa utakuwa na mafanikio.

    “Mradi gani?”



    “Nimegundua kuwa kule kwetu (ujinini) kuna upungufu mkubwa wa watoto wanaohitajika kuandaliwa kwa ajili ya kurithi utawala wa kule. Inajua wengi wa watu waliopo kule umri wao wa kuishi unahesabika. Kuna wazee wengi ambao hawawezi kufanya kazi kama zamani. Tunahitaji kizazi kipya kwa ajili ya kazi ya kuijenga upya himaya yetu. Mkuu ameniambia kuwa baada ya kipindi fulani kupita, mimi nitatawazwa kuwa malkia, ndiyo maana nimeamua kuanza kuandaa mikakati mapema.”



    “Mmh! Mbona unaongea mambo mazito kirahisi namna hiyo? Unataka mimi nifanye kazi gani?”

    “Kwa kuwa wewe ni kidume cha shoka, na uwezo wako kwenye mambo ya kikubwa naufahamu vizuri, pia una nguvu za kijii ulizozaliwa nazo, nataka nikuongezee vitu fulani kasha kwa pamoja tutaifanya kazi ya kutafuta wanawake wazuri ambao watafaa kutuzalia watoto wengi kwa ajili ya kizazi kipya cha majini.”



    “Noo! Hapana Fatiha! Siwezi kuifanya hiyo kazi.”

    ‘Tatizo lako wewe mpaka nitumie nguvu ndiyo tutaelewana. Kwa taarifa yako, hii kazi utaifanya kwa hiyari yako au kwa kulazimishwa, wewe ndiyo utachagua. Kwanza siyo ngumu, ngoja nikueleweshe vizuri,’ aliongea Fatiha huku macho yake yakianza kubadilika.



    Alimweleza Gamutu kuwa, anachotakiwa kukifanya ni kufanya mapenzi na idadi kubwa ya wanawake ambao wote watabeba ujauzito, kisha kipindi cha kujifungua kitakapofika, watawachukua watoto kimazingara na kuwapeleka kuzimu ambapo wataandaliwa kuwa majini.



    “Unatakiwa kufanya mapenzi na wanawake na mabinti wengi kwa kadiri uwezavyo, na kila utakayekutana naye kimwili, atapoteza fahamu kwa kipindi cha miezi tisa mpaka kiumbe kilichopo tumboni kitoke. Baada ya kuzaa, tutawachukua watoto wetu na tutawaacha huru hao wanawake,” alisema Fatiha huku akiwa hana hata chembe ya mzaha.



    “Ile pete si bado unayo?”

    “Ndiyo!”

    “basi hiyo ndiyo itakuwa silaha yako kubwa. Hakuna atakayekushtukia mpaka kazi yetu itakapokamilika. Nakuahidi ukiifanya kazi vizuri, nitakufanya uwe tajiri kuliko watu wote wa duniani.



    Gamutu na Fatiha walijadiliana kwa saa nyingi, Fatiha akawa anamtoa wasiwasi Gamutu. Akamweleza kuwa, atampa dawa itakayompa uwezo wa kubadilika sura na umbo kwa kadiri atakavyo ili iwe rahisi kuwanasa wanawake wa kila aina na kuvunja nao amri ya sita.

    “Mi nitapata wapi nguvu za kuwapa ujauzito wanawke wote hao?”



    “Usiwe na wasiwasi, nitakupa dawa ya kuongeza ukubwa wa maumbile yako ya kiume ili ukimuingilia mwanamke mara moja tu apate ujauzito, pia nitakupa dawa ya kuongeza nguvu ambapo utakuwa na uwezo wa kufanya mapenzi na wanawake wengi kadiri utakavyo kwa siku.

    “Lakini wewe si ulishaweka nadhiri kuwa kila mwanamke nitakayefanya naye tendo la ndoa atakufa? Unataka niwe muuaji?”



    “Hapana Gamutu, hawa kwa kuwa tunafanya kazi maalum, hawatakufa bali watapoteza fahamu kuanzia siku utakayokutana nao kimwili, mpaka watakapojifungua. Nitahakikisha nawalinda wote, hakuna atakayekufa na wakishajifungua watarejea kwenye hali zao ya kawaida.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tutawatumia wanafunzi wa kike ambao bado hawajazaa, wake za watu, machangudoa na mahausigeli. Maeneo ya kukutana nao kimwili itakuwa ni kwenye nyumba za kulala wageni (Guest). Pia utakuwa na uwezo maalum wa kuwatambua wanawake wanaoweza kuzaa mapacha, hao watatusaidia sana.



    “Kwa kuwa tunahitaji wanawake wengi ndani ya kipindi kifupi, ni lazima kazi hii ikafanyikie mijini. Dar es Salaam, Arusha na Morogoro kutafaa zaidi. Tanga hakutufai kwani kuna wanawake wengi ambao siyo binadamu halisi, bali majini. Hao watakusababishia matatizo,” alihitimisha Fatiha na kumwambia Gamutu aanze safari ya kuelekea Dar es Salaam wakati yeye akirudi kuzimu kwenda kuweka mambo sawa.



    “Sasa nitaendaje Dar es Salaam wakati sijawaaga wajomba zangu wala bibi? Si watakuwa na wasiwasi sana?”

    “Achana nao, na wala usithubutu kurudi tena kwa wajomba zako kwani yule mganga atakuwa anakuwinda, bado ana hasira na wewe. Fanya kama nilivyokuekekeza. Itumie pete kukuletea gari la kifahari na nguo za kisasa, mi nitakuwa pamoja na wewe kwa kila hatua.”



    “Lakini sijui hata kuendesha gari. Hata kuvaa nguo nzuri hii ndiyo itakuwa mara yangu ya kwanza, nitawezaje?”

    “Mbona una uhaba wa imani namna hiyo Gamutu! Fanya nilivyokwambia na utaona unajua kila kitu ukishaanza kukifanya. Kama unauliza kila kitu mwisho utasema nikufundishe hata namna ya kutongoza!” alisema Fatiha na kupotea kimiujiza akimuacha Gamutu ana maswali mengi kichwani yasiyo na majibu.



    “Kazi aliyoachiwa na Fatiha ilikuwa ni zaidi ya mtihani kwake. Hakujua ni kwa namna gani ataweza kuikamilisha, hasa ukizingatia kuwa umri wake ulikuwa bado mdogo, na alikuwa na siku chache tu tangu awasili Bagamoyo akitokea Sumbawanga. Hakuwahi kufika Dar es Salaam hata mara moja lakini sasa alitakiwa kwenda kuanza kazi aliyoelekezwa na Fatiha.

    Aliishika pete aliyopewa na Fatiha akawa anajaribu kukumbuka maelekezo aliyopewa juu ya namna ya kuitumia.



    “Nataka gari zuri la kifahari litokee!” Gamutu aliiambia ile pete akiwa amekaa mkao wa Atahiyatul Mantra aliofundishwa na Fatiha. Pete ilibadilika rangi na kuanza kung’aa kisha ikafifia.



    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog