Search This Blog

NILIBADILIKA NA KUWA JINI BILA KUJIJUA - 3

 







    Simulizi : Nilibadilika Na Kuwa Jini Bila Kujijua

    Sehemu Ya Tatu (3)





     “Kwa nini wewe hunywi kinywaji kama wenzako na una kazi ya kushangaa shangaa?”

    “Sijui ni nini? Siwezi kunywa kitu nisichokijua,” alijibu Gamutu kwa mkato lakini kwa woga huku akizidi kupepesa macho mahali Fatiha alipo ili aje kumsaidia kwani ni yeye ndiye aliyemwambia asinywe.



    “Yaani na ugeni wako umeshaanza kujifanya mjuaji siyo? Sasa kwa taarifa yako utakunywa huku nikikusimamia, halafu usiku utapangwa zamu ya kwenda kutafuta damu na wenzako usiku wa leo, ukianza kuleta ujuaji maisha ya huku yatakushinda na utaishia kuwa msukule,” aliongea kwa ukali yule mzee wa ajabu, kisha akamshika Gamutu kwa nguvu na kuanza kumnywesha.



     “Duuh! Kweli ni damu… lakini mbona nyingi kiasi hiki? Wameipata wapi?”

    Gamutu alijiuliza wakati akimeza funda la pili. Ladha yake ilimkumbusha siku zilizopita, alipojikuta kwa mara ya kwanza akitamani kunywa damu alipokuwa shuleni, kabla hajapotelea ujinini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yule mwanaume alishangaa kuona Gamutu akijilamba midomo, tofauti na alivyotegemea kuwa ataitema.

    “Sasa ulikuwa unaogopa nini, mi’ nilishakuona wewe ni kidume na ndiyo maana nimekupanga zamu leo usiku. Inaonesha wewe ni mzoefu, wenzako wote wakinyweshwa kwa mara ya kwanza huwa wanatapika sana, lakini nashangaa wewe unajilamba, utakuwa msaada mkubwa kwetu,” aliongea yule kiumbe kwa sauti ya furaha huku akimuongeza Gamutu kikombe kingine.



    “Wale viumbe wengine ambao awali walikuwa wakimshangaa Gamutu, baada ya kuona anakunywa damu bila wasiwasi nao waliendelea na shughuli zao na hawakumshangaa tena kwani walishaamini ni mmoja kati yao.

    Baada ya kumaliza vibuyu viwili, Gamutu aliruhusiwa kuendelea na utaratibu mwingine na ni hapo ndipo alipomuona tena Fatiha.



    “Kwa nini ulinikimbia?”

    “Nilitaka nione ukomavu wako.”

    “Kwa hiyo umeshauona!”

    “Umenishangaza kweli.”

    “kwa nini?”



    “Kuona unakunywa damu ya watu bila wasiwasi, nakumbuka mimi mara ya kwanza nilikamatwa kwa nguvu na kunyweshwa lakini niliitapika yote. Kwani ulishawahi kuinywa kabla hujaja hapa?”

    Fatiha alimuuliza Gamutu swali gumu ambalo hakuwa tayari kulijibu, badala yake akamdanganya.

    “Walaa, leo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza, halafu yule mzee amesema usiku na mimi nitaenda na wenzangu kutafuta nyingine.”



    “Wee! Kweli?” Kauli ile ilizidi kumshangaza Fatiha.

    Kwa utaratibu wa kule ujinini, ni wazoefu pekee ndiyo waliokuwa wakitumwa duniani kwenda kutafuta damu kwa ajili ya majini wote. Hiyo ilikuwa ni kwa sababu zoezi la ukusanyaji damu lilikuwa likihusisha matukio mengi ya kutisha ambayo kama huna moyo wa jiwe huwezi kumudu. Alishangaa ni kwa nini Gamutu achaguliwe kwenda wakati alikuwa bado mgeni.



    Hata hivyo, aliona muda huo ndiyo utakaokuwa muafaka kwa yeye na Gamutu kufanya mapenzi kwani wakiwa duniani watakuwa na uhuru mkubwa kuliko kule ujinini.



    “Tutaongozana na mimi, ni kazi ngumu lakini nakuahidi nitakuwa na wewe bega kwa bega,” aliongea Fatiha huku akimkumbatia. Saa zilizidi kuyoyoma na hatimaye giza kuanza kukolea. Giza lilipokuwa totoro, sauti kama ya king’ora kikubwa ilisikika kisha baadhi ya majini wakawa wanaelekea kwenye lango kuu la kuingilia kwenye himaya ile.

    Fatiha alimwambia Gamutu kuwa kile ni king’ora kuashiria kufika kwa muda wa wale waliopangiwa kwenda duniani kusaka damu.



    “Inuka twende,” aliongea Fatiha huku akimshika mkono Gamutu. Baada ya sekunde chache, umati wa viumbe wasiopungua sabini walikuwa tayari kwa safari ya kuelekea duniani. Kila mmoja alipewa kibuyu kikubwa na kuelekezwa kuwa, muda wa kurudi kiwe kimejaa. Wakatawanyika kila mmoja na njia yake.



    “Twende huku,” Fatiha alimshika mkono Gamutu na kusogea naye pembeni.

    “Fumba macho,” aliongea Fatiha na Gamutu akatii.

    “Usifumbue mpaka nitakapokwambia,” alizidi kusisitiza Fatiha.

    Gamutu alisikia kama upepo mkali ukipuliza kisha akawa ni kama asiyeelewa kinachoendelea. Alijihisi ni kama wanapaa angani.



    “Fumbua macho, tumefika,” aliongea Fatiha na kweli Gamutu alipofumbua macho alijikuta yuko jirani na nyumba ya bibi yake. Mwanzo alikuwa haamini lakini alipofikicha macho aligundua kuwa ni kweli tayari yuko kwenye ulimwengu mwingine.

    “Nisikilize, kabla ya kufanya lolote nataka unipe penzi kwanza kisha ndipo kazi itakapoendelea,” aliongea Fatiha huku akimkumbatia Gamutu.



    Waligusishana ndimi zao na kuanza kuwekana sawa, tayari kwa kula tunda la mti uliokatazwa.

    “Kwa kuwa Fatiha alikuwa hajakutana kimwili na mwanaume kwa kipindi kirefu, alikuwa akipiga kelele za kimahaba kila alipofanyiwa kitu na Gamutu. Kwa kuwa alishahakikishiwa kuwa akimpa penzi la dhati anaweza kumfundisha mbinu za kurudi duniani moja kwa moja, Gamutu alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake wote kumfurahisha, wakawa wanaelea kwenye ulimwengu wa mahaba.



    “Kelele alizokuwa anazipiga Fatiha zilimfanya bibi yake Gamutu, Bi Lubunga aliyekuwa amelala ndani ya nyumba peke yake, kushtuka na kuanza kunyata kuelekea nje.

    “Alipofika mlangoni aliufungua mlango taratibu na kuchungulia nje lakini hakuona kitu, akaamua kutoka kabisa kufuata sauti zile zilikokuwa zinatokea.

    Gamutu na Fatiha wakiwa kwenye bahari ya mahaba, walishtuka baada ya kusikia Bi Lubunga akiliita jina la Gamutu kwa sauti kubwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yule ni nani? Aliuliza Fatiha huku akionekana kuchukizwa na kitendo cha kuingiliwa kwenye starehe yao, akatoa kitu kama unga mweusi kutoka kwenye nguo zake na kutaka kumpulizia Bi Lubunga.

    “Hapana, usifanye hivyo, huyu ni bibi yangu.”

    “Tuondoke haraka,” aliongea Fatiha huku akionekana kukasirika.

    “Hapana, naomba japo nimsalimu, nilimkumbuka sana bibi yangu.”



    “Twende kwanza tukamalizie kule pembeni, ukinifikisha mwisho wa safari yangu nitakuruhusu kuja kumsalimia bila tatizo.

    Aliongea Fatiha huku akimvuta Gamutu kwa nguvu. Walipofika kwenye vichaka vilivyokuwa pembeni ya nyumba ya Bi Lubunga, Fatiha alimvutia Gamutu mwilini mwake, wakaendelea na mchezo wao. Hakuna aliyegundua kuwa muda ulikuwa ukienda kwa kasi na saa ya kurejea ujinini wakiwa na damu ulikuwa umekaribia. Walizidi kuogelea kwenye bahari ya huba hadi wakawa taaban kwa uchovu. Fatiha bado alikuwa akimuhitaji Gamutu na hakuwa tayari kumuachia.



    Baada ya kufika mwisho, alimwachia Gamutu huku wote wakiwa wameloana jasho chapachapa.

    “Sasa unaweza kwenda kumsalimu bibi yako, mimi nitakusaidia kutafuta damu, lete kibuyu chako,” aliongea Fatiha huku akihema kwa nguvu. Gamutu alimshukuru na kumpa kibuyu chake, kwa kasi ya ajabu akainuka na kuanza kukimbilia nyumbani kwa bibi yake huku Fatiha naye akipotea kimiujiza.

    Alipofika, alimkuta bibi yake akiwa amesimama mlangoni.



     “Ni wewe Gamutu?”

    “Ndiyo bibi! Nimekuja kukusalimu.”

    “Enhee, habari za ulikokuwa?” Bi Gamutu aliongea kwa furaha huku akitaka kumkumbatia Gamutu mwilini lakini akawa anajikwepesha ili wasigusane.



    “Huko nilikokuwa nimeambiwa nisigusane na mtu wa kawaida, eti nitapata madhara.”

    “Haa! Hata mimi bibi yako niliyekulea tangu una siku moja mpaka leo? Kwanza hebu niambie ulikuwa wapi na umefikaje hapa.”



    “Ni stori ndefu bibi, nimehamishiwa kwenye ulimwengu wa majini lakini kuna mtu ameniambia anaweza kunisaidia kunirudisha.”

    “Acha uongo we mtoto, tangu lini majini wakawa kama wewe? Kwanza huna kwato, huna umbo la ajabu, macho yako hayang’ai na unaweza kuelewana vizuri na mimi kwa lugha ya kawaida, wewe siyo jini ila umepumbazwa akili na viini macho.”



    “Kwa hiyo bado mimi ni binadamu wa kawaida?”

    “Ndiyo, hakuna mwenye uwezo wa kukubadilisha kuwa jini labda mimi bibi yako niwe nimekufa, nakuhakikishia nitakupigania hadi mwisho wa uhai wangu, lazima urudi nyumbani,” aliongea Bi Lubunga kwa kujiamini.



    “Halafu zile kelele nilizokuwa nazisikia zilikuwa za nini?”

    “Ni Fatiha, yeye ndiyo ameahidi kunisaidia kutoroka kurudi duniani.”

    “Kwa nini alikuwa anapiga kelele? Au umeanza tena michezo yako ya kupenda wanawake?”

    “Mhh…” Gamutu alishindwa kujibu, akabaki kubabaika huku akitazama chini, bibi yake akaelewa kilichokuwa kinafanyika.



    “Ina maana unashirikiana kimapenzi na majini?”

    “Fatiha siyo jini, ni binadamu wa kawaida.”

    “Hata kama! Wewe matatizo yako si unayajua, unakumbuka ulivyofanya mapenzi na yule mwanafunzi mwenzako kilikutokea nini? Leo umehamia kwa majini na kuendeleza mchezo wako, mbona hujionei huruma mjukuu wangu?”



    “Ameniahidi kuwa nikimfurahisha kimapenzi atanifundisha mbinu za kutoroka na kurudi huku duniani.”

    Wakiwa bado wamesimama palepale mlangoni wakizungumza, walisikia sauti kama ya upepo mkali ukivuma kuja eneo lile, Bi Lubunga akakimbilia ndani kuchukua dawa zake za kinga dhidi ya wachawi lakini Gamutu akamzuia kwa kusema yule ni Fatiha waliyekuja naye.



    “Amekuja kunipitia tuondoke.”

    “Muondoke kwenda wapi?”

    “Mimi nimeambiwa eti duniani siyo sehemu yangu ya kuishi, natakiwa kuishi ujinini.”

    “Wewe! Hivi umechanganyikiwa na nini mjukuu wangu? Au mapenzi na huyo jini wako ndiyo yamekuchanganya! Hata sikubali, lazima nikuokoe.”



    Wakati wakiendelea kubishana pale mlangoni, Fatiha alikuwa ameshawasili na kusimama pembeni ya Gamutu bila ya Bi. Lubunga kumuona. Kauli yake aliyoitoa kuwa Gamutu amenogewa na penzi la jini ilimkasirisha Fatiha, akataka kuondoka haraka eneo lile.

    “Twende, muda umekwisha!”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ngoja niongee kwanza na bibi yangu.”

    “Twende bwana, tutakuja tena kesho, nitakuleta, tukichelewa tutaadhibiwa.”

    Japokuwa Gamutu alikuwa mbishi, Fatiha alitumia nguvu kumuondoa eneo lile, Bi Lubunga akawa anapiga kelele za kuomba msaada bila mafanikio. Gamutu na Fatiha wakapotea kimiujiza huku wakiwa na vibuyu viwili vikubwa vilivyojaa damu.



    “Mbona hivi vibuyu vizito namna hii?”

    “Kwa sababu vimejaa, unajua damu inayopatikana kwenye ajali huwa ni nzito sana.”

    “Unamaanisha nini? Mbona sikuelewi?”

    “Nilipokuacha pale na bibi yako nilienda kwenye barabara inayotoka mjini, nikaandaa mtego wa ajali, muda mfupi baadaye magari mawili yakagongana uso kwa uso, nikachukua kilicho changu na kuondoka.”



    “Ina maana umeua?”

    “Hapana, mimi huwa siui kama wenzangu, nikisababisha ajali kichawi nahakikisha hakuna anayekufa bali wote wanapata majeraha makubwa yanayovuja damu nyingi, nikishajaza vibuyu kadhaa basi nawaacha wakatibiwe na kupona.”

    “Kwani wengine huwa wanafanyaje?”



    “Mambo mengine siwezi kukwambia, utajionea mwenyewe.”

    Waliendelea na safari kimyakimya, sekunde chache baadaye wakawa tayari wameshawasili kwenye himaya ya majini.

    “Mbona mmechelewa sana? Mlipitia wapi?”

    Sauti kali ya yule mzee aliyeonekana kuwa kiongozi wao ilisikika kama muungurumo wa radi akiwafokea Gamutu na Fatiha.



    Kwa kuwa Fatiha alikuwa akifahamu taratibu za kule, aliinamisha kichwa chake chini, Gamutu naye akamuiga, wakasujudu mara tatu kisha wakainuka. Kwa majini ile ilikuwa ni ishara ya kuomba msamaha, yule kiongozi wao akapokea vibuyu vyao viwili vilivyokuwa vimejaa mpaka juu, akawaruhusu kuendelea na taratibu nyingine.



    “Mimi bado sijaelewa ulivyopata damu nyingi kirahisi namna ile,” Gamutu alianza upya mazungumzo lakini Fatiha akamkatisha wakati wakielekea kwenye bustani nzuri ya maua.

    “ Tuachane na hayo bwana, hebu tuzungumzie mapenzi yetu, unajua umenifurahisha sana leo! Sikuwahi kudhania kuwa una uwezo mkubwa wa kumridhisha mwanamke kiasi hiki kwani kiumri bado unaonekana mdogo. Nani alikufundisha?”



    “Sijafundishwa na mtu, halafu huwezi kuamini kuwa leo ni mara yangu ya pili kukutana na mwanamke maishani mwangu.”

    “Wewe ni mwanaume wa shoka,” aliongea Fatiha huku akimkumbatia Gamutu kimahaba, akawa anampapasa mgongoni huku akipumua kwa nguvu.

    Walipofika ndani kabisa ya bustani ile ya maua, Fatiha alimuomba Gamutu warudie tena ‘mchezo wa kikubwa’.



    “Lakini si ulisema huku ni hatari kufanya mapenzi, tukikamatwa?”

    “Huku hakuna anayefika kwa urahisi. Nipe haki yangu mpenzi,” aliongea Fatiha huku akijiweka vizuri tayari kumpokea Gamutu kwenye himaya yake. Wakaanza tena kulila tunda la mti uliokatazwa.



    Wakiwa wamekolea kisawasawa kwenye ulimwengu wa mahaba, kila mmoja akitoa miguno na sauti za huba, walisikia sauti ya mtu ikiwakaripia kwa ukali.

    “Mnafanya nini hapa? Hamjui sheria za himaya hii? Simameni hivyohivyo jinsi mlivyo.”



     Niliinuka kwa hofu huku nikitetemeka, Fatiha akanivutia pale chini na kwa kasi ya ajabu akatoa kichupa kilichokuwa na unga mweusi, akajipulizia na kunipulizia, kisha akaniambia:

    “Acha wasiwasi, hawezi kutuona tena, atahisi ameona maluweluwe, tuendelee kula raha.”



    Nilishangazwa sana na yaliyokuwa yanatokea. Moyoni nilikuwa bado nina hofu lakini Fatiha akawa ananihamasisha kuwa hawezi kutuoana tena. Alichokisema Fatiha kilikuwa kweli, nikaona yule mzee mkali akijishtukia mwenyewe, akageuka na kuondoka zake.



    Kwa hofu niliyokuwa nayo, sikuwa na hamu ya kuendelea kucheza mchezo wa kikubwa na Fatiha lakini aliniganda kama ruba, akanivutia kwake na kuanza kunihamasisha upya.

    Dakika chache baadaye akili yangu ilitulia, tukaendelea kuchakachuana.



    Kilichonishangaza ni kwamba, kadiri tulivyozidi kuzama kwenye dimbwi la mahaba na Fatiha alianza kuonesha dalili ambazo zilinishtua. Alianza kutokwa na damu puani, mdomoni na masikioni huku akilalamika kwa sauti ya ajabu. Macho yake yalianza kung’aa kama ya paka awapo gizani na sura yake nzuri ya kuvutia ilibadilika na kuonekana kama bibi kizee wa kutisha. Nilishangaa kucha zake zikibadilika na kuwa kama za mnyama, miguu nayo ikawa na manyoya mengi, akawa anazidi kulalamika kwa sauti ya kutisha.



    Niliogopa kiasi cha kuishiwa kabisa msisimko wa mapenzi, nikawa najitahidi kujinasua ili nikimbie lakini Fatiha ambaye sasa alibadilika na kuwa kama kiumbe wa ajabu alizidi kuning’ang’ania.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya dakika kadhaa, alipiga yowe kuu kisha akatulia tuli. Ni hapo ndipo nilipopata nafasi ya kujinasua kutoka mwilini mwake na kukimbilia pembeni, nikasimama kwa hofu huku nikitaka kujua kitakachoendelea.



    Fatiha alitulia pale chini kwa zaidi ya dakika tano huku akiendelea kutokwa na damu nyingi, kisha nikamuona akianza kujigeuza geuza huku akijinyonganyonga, akaanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida. Zile kucha ndefu zikabadilika na kuwa za kawaida, macho yakaacha kung’aa na uso wake mzuri ukarudi kuwa vilevile. Alifumbua macho akawa anaangalia huku na kule kama aliyejiuliza alikuwa wapi.



    Alipoona nimesimama kwa pembeni huku nikitetemeka kwa hofu, aliinuka haraka na kunivamia mwilini, akanikumbatia kimahaba huku akinipiga mabusu mengi, akili yangu ikawa bado imejawa na hofu kwa yale niliyoyaona.

    “Nakupenda sana Gamutu, ooh Gamutu wangu! Kwa nini nimechelewa kukujua?” Aliongea Fatiha kwa sauti ya kimahaba na akawa ananitazama machoni. Niligeukia pembeni na nikawa nawaza yangu.



    “Wewe umekuwa mwanaume wa kwanza kunifurahisha maishani mwangu, nitakupa chochote unachokitaka.

    “Nataka kurudi nyumbani, nataka nikaendelee kumsaidia bibi yangu kazi pia nikaendelee kusoma.”

    “Sawa Gamutu, nikakutimiza yote unayoyataka, baadaye nitakupa zawadi nzuuuri ambayo itakufanya muda wote uwe unanifikiria.”



    “Zawadi gani?”

    “Utaiona hiyo baadaye.”

    “Lakini Fatiha, mimi nimeanza kukuogopa mwenzio, siyo siri umenitisha sana.”

    “Nimekutisha nini mpenzi wangu?”



    “Wakati tunaduu ulibadilika na kuwa kama jini kabisa, nimeogopa sana na sijui kama nitakuja kurudia kufanya mapenzi na wewe.”



    “Tafadhali sana Gamutu, nitunzie siri yangu, raha za mapenzi uliyonipa ndiyo imenifanya niwe hivyo.”

    “Halafu ulikuwa unatokwa na damu nyingimasikioni, puani na mdomoni.”

    “Hiyo ni hali ya kawaida, unajua kazi ya kukusanya damu duniani ni ngumu sana, muda mwingine tunakutana na watu ambapo wamefanyiwa matambiko makali ambayo ndiyo yanayotufanya tutokwe damu kiasi, lakini wala usiopgope, ni hali ya kawaida tu, na isitoshe kwetu sisi damu siyo kitu cha kutisha.”



    “Lakini hata kucha nazo zilibadilika… uso na macho vyote vimenitisha sana, nakuogopa Fatiha.”

    “Hapana usiniogope mpenzi, hata wewe ukishazoea kazi za huku utakuwa unabadilika wakati wa kufanya mapenzi.”



    “Mhh! Ina maana na mimi nitakuwa kama wewe?”

    “Usiogope, nitakufundisha mbinu nyingi zaidi za kujidhibiti, mimi leo nimeshindwa kwa sababu ya utamu wa penzi lako, lakini hali kama hii huwa naweza kuizuia isitokee.

    “Na vipi kuhusu yule mzee aliyekuja wakati tunaanza.”

    “Nilimpumbaza akili, hata hawezi kukumbuka aliona nini.



    “Lakini ahadi yako ilikuwa nikikufurahisha utanifundisha mbinu za kurudi duniani.”

    “Sijakataa Gamutu lakini utamu wa penzi lako nao umeninogea, najua ukienda duniani utaanza kutembea na wanawake wengine, sitaki jambo hilo litokee.

    “Hapana, siwezi… nitakutunzia heshima yako.

    ”Niahidi kitu kimoja na ukiwa mwaminifu nitakupa utajiri mkubwa sana duniani.”

    “Mh! Nakusikiliza.”



    “Niahidi kuwa hutashirikiana kimapenzi na mwanamke mwingine yeyote zaidi yangu. Ukiwa mkweli hata usiku wa leo naweza kukurudisha nyumbani kwenu.”

    “Nakuahidi kuwa mwaminifu kwako.”

    “Kweli?”

    “Ndiyo!”



    ***

    Bi. Lubunga ilibidi arudi nyumbani kwa waganga wa jadi waliomfanyia tambiko Gamutu kwa ajili ya kuomba msaada. Aliwaeleza kila kitu kilichotokea hadi mjukuu wake alipochukuliwa kimiujiza usiku wakiwa wamelala. Aliwaeleza pia jinsi jaribio lake la kumuokoa lilivyoshindikana mara mbili mfululizo na kuomba msaada wa haraka.



    “Watakuwa wamemficha chini ya bahari kwenye makazi ya majini, kule kuna mji mkubwa sana wenye kila kitu. Ni vigumu sana kumkomboa mtu anayeishi kule, labda tujaribu lakini kaa ukifahamu kuwa tukishindwa lazima mmoja kati yetu afe.”

    “Nani?”



    “Mmoja kati yetu, wewe au Gamutu mwenyewe, majini wana nguvu kubwa sana ambazo zinahitaji umakini mkubwa kupambana nazo.”

    Jitahidini jamani, mjukuu wangu hawezi kupotea kimiujiza kiasi hiki, nimehangaika naye sana tangu anazaliwa, siwezi kuishi bila yeye.”

    Wale waganga walikubali kuifanya kazi ile ngumu kwa masharti ya kupewa ng’ombe wawili na kondoo mweupe.



    Wakaanza kwa kulirudisha nguvu tambiko la maisha walilomfanyia akiwa bado duniani. Kazi ile ilikuwa ngumu kwani kila walilolifanya, Fatiha alikuwa akiliona kupitia nguvu zake za kijini, akawa hataki Gamutu aondoke haraka kwani alimuonjesha penzi tamu. Ikawa ni vita ya kimya kimya, waganga wakijitahidi kumrudisha Gamutu duniani na Fatiha akizuia asiondoke ili aendelee kumfaidi.



     “Nasikia sauti kama za mtu ananiita jina langu.”

    “Hata mimi nasikia, nahisi bibi yako ameenda kwa waganga wa kienyeji kutaka kukukomboa kutoka kwenye mikono yangu.”

    “Sasa tutafanyaje? Niruhusu niende halafu kama utakuwa unanihitaji utakuwa unakuja duniani, bibi yangu anateseka sana.”



    “Hapana, lazima tukae pamoja kwa kipindi kifupi kisha nitakuruhusu.”

    “Lakini ulisema utaniruhusu mapema, kwa nini unamtesa bibi yangu Fatiha?”

    “Yeye ndiyo ananitesa kwa sababu hao waganga wake eti wanataka kuniua ndiyo wakuokoe wewe, mimi naona kila kitu lakini sitaki kuwaonesha jeuri yangu kwani wataumia sana. Pia leo usiku kuna kazi kubwa ya kwenda kuifanya duniani, lazima tuiikamilishe tukiwa wote.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Basi fanya kama ulivyoniahidi Fatiha, niko tayari kukutunzia heshima yako na nakuahidi sitatembea na mwanamke yeyote duniani ila niruhusu kitu kimoja tu, niache nirudi kwa bibi yangu.”



    Baada ya malumbano ya muda mrefu kati ya Gamutu na Fatiha, ilibidi akubali kumrudisha duniani baada ya siku tatu kupita lakini kwa masharti magumu. Alimwambia kuwa akifika duniani hatakuwa binadamu wa kawaida kama ilivyokuwa awali. Atakuwa katikati ya hali ya ubinadamu na ujini na kwamba, atakuwa akiwajibika kwa majini kuliko binadamu.

    “Zawadi niliyokuwa nimekuahidi ni hii!” Aliongea Fatiha huku akitoa pete ya dhahabu iliyokuwa inang’aa sana.



    “Utaiambia chochote unachokitaka nayo itakutimizia, ila usiiombe vitu haramu.”

    “Vitu haramu ndiyo vipi?” Alihoji Gamutu kwa mshtuko huku akiipokea pete ile.

    “Cha kwanza ni fedha, usije kuthubutu kuiomba ikuletee fedha badala yake unaweza kuiomba ikuletee kitu ulichotaka kukinunua.



    Kwa mfano kama unataka nyumba nzuri, we iambie na utashangaa kuona nyumba inatokea. Pia usiiombe ikuletee vitu ambavyo tayari vinamilikiwa na watu wengine, hivyo ni haramu. Ukitaka gari we sema unataka la namna gani na litakuja ila usiseme nataka gari la fulani liwe langu. Pia usiitumie kutongozea wanawake kwani uwezo huo inayo lakini madhara yake ni kuwa kila utakayemtongoza atakufa wakati mkifanya mapenzi.”



    Gamutu alishusha pumzi ndefu wakati Fatiha akizidi kumpa maelekezo ya namna ya kuitumia pete ile. Alipomaliza alimvalisha Gamutu kisha akampiga busu kwenye paji la uso na kutamka maneno ambayo hakuyaelewa. Wakati hayo yakiendelea, Gamutu alikuwa akizidi kusikia sauti za ajabu masikioni mwake zikilitaja jina lake.



    “Gamutu! Nakupenda na sitaki kukupoteza ila naomba ukakae na bibi yako na kumweleza kuwa asinichukie kwani sina tatizo lolote naye. Mwambie asiende tena kwa waganga kwa lengo la kunidhuru kwani sina nia mbaya na wewe wala yeye bali nataka kuwasaidia. Akiendelea kuhangaika kwa waganga nitakasirika na nikichukia nitakunywa damu yake.



    Wakati Gamutu na Fatiha wakiendelea na mazungumzo yao walisikia king’ora kikali kutoka ndani ya himaya ile, wakainuka haraka na kuanza kukimbia kuelekea kule kilikotokea.

    “Muda wa kwenda duniani kukusanya damu umefika, sipendi hii kazi basi tu!”

    “Ina maana mimi pia naenda? Afadhali nikaonane na bibi yangu.”



    “Leo hutaweza kuonana naye kwani itabidi tukusanye damu nyingi sana maana nimeambiwa kutakuwa na sherehe, mtoto mkubwa wa mfalme amepata mke, watafunga harusi usiku wa kesho.”

    Gamutu na Fatiha walikuwa wakiongea huku wakikimbia kuwahi eneo la tukio. Walipofika walikuta wenzao wameshajipanga, nao wakainamisha vichwa vyao na kuanza kusubiri kupangiwa kazi ya kufanya.



    ***

    Miongoni mwa matukio ambayo yaliwashtua watu, zilikuwa ni ajali mbili zilizotokea eneo moja kwa nyakati tofauti ndani ya usiku mmoja. Ya kwanza ilikuwa ni ya basi lililokuwa limebeba abiria 32 ambalo liligonga ng’ombe wawili waliokuwa wanavuka barabara usiku na kusababisha vifo vya watu wote isipokuwa dereva.



    Mita chache kutoka ajali ya kwanza ilipotokea, gari dogo lililokuwa limebeba waombolezaji waliokuwa wanasafirisha maiti, liligongwa vibaya na gari kubwa la mizigo. Watu wote 11 waliokuwa kwenye gari dogo wakapoteza maisha palepale, gari la mizigo likapinduka na kwenda kuangukia nyumba iliyokuwa pembeni ya barabara na kuwaua mama na wanaye sita waliokuwa wamelala ndani.



    Eneo la ajali lilikuwa linatisha kama machinjioni, viungo vya watu vilitapakaa huku damu ikiweka madimbwi makubwa barabarani. Dereva wa gari la kwanza kupata ajali ndiye mtu pekee aliyebakia hai eneo lile, akawa anakimbia huku na kule kuomba msaada kama aliyepagawa. Kilichomchanganya ilikuwa ni mauzauza aliyoyaona barabarani muda mfupi kabla ya ajali kutokea.



    “Sitaki kazi ya udereva tena, sitakii! Barabara imejaa majini yanayosababisha ajali, sitaki tenaaa!” Alisikika dereva yule akipayuka kama mwendawazimu. Alikuwa akiropoka yote aliyoyaona kabla ya ajali na kusisitiza kuwa zile hazikuwa ajali za kawaida.

    “Nini cha kufanya?”



    “Wewe kusanya mifupa na meno, mimi nakusanya damu,” Fatiha alimjibu Gamutu na wakaanza kazi eneo ajali ile ilipotokea. Kwa mtu wa kawaida isingekuwa rahisi kuwaona kwani walikuwa kwenye sura za kijini.



    “Lakini mimi naogopa… siijawahi kushika mifupa na meno ya binadamu kama hivi.”

    “Kaza moyo Gamutu, yaani we kila siku utakuwa mgeni tu! Kuwa kama mwanaume.”



     Kazi ile ya kutisha iliendelea kwa muda mrefu, Fatiha akakusanya damu nyingi na Gamutu akapata mifupa na meno ya kutosha. Walipomaliza kazi yao, walifanya ishara ya kichawi kisha wakayeyuka kimiujiza.



    Kufumba na kufumbua tayari walikuwa wamewasili ujinini. Tofauti na siku zote, wao ndiyo waliokuwa wa kwanza kufika na kukuta wenzao wote bado hawajarudi. Mkuu wa himaya ile alifurahishwa na ujasiri wao kwani licha ya kuwahi, walipata mzigo wa kutosha wa damu, meno na mifupa.



    “Kazi nzuri, kijana umekuja juzi tu lakini naona unayamudu vizuri majukumu, nakupandisha daraja,” aliongea kwa sauti ya kutisha yule mkuu wa himaya ile, ambaye kichwa chake kilikuwa kimejaa mvi nyingi na ndevu za kutisha, huku mwili wake nao ukiwa na vinyweleo vingi.



    Fatiha alimuelekeza namna ya kuitikia yale mkuu wao aliyokuwa anayasema, akainamisha kichwa na kusujudu, kisha akasema maneno yafuatayo kwa lugha ya Kilingala huku akiwa ameinamisha kichwa:

    “Bolingo nayo ekoma mokonzi ya bandoki.”

    (Mapenzi yako yatimie mkuu wa himaya).



    Kitendo kile kilimfurahisha sana mkuu wa himaya ile ya majini kwani alivutiwa pia na nidhamu aliyoionesha Gamutu katika kuitikia.

    Moyoni mwake Gamutu hakuwa akipenda kupandishwa daraja wala kuzoeana na yule mkuu wao kwani alijua kwa kufanya hivyo zoezi la kurudi duniani litazidi kuwa gumu.



    Fatiha alikuwa akitabasamu kwa furaha huku akimwangalia Gamutu usoni. Baada ya kuzungumza mawili matatu na mkuu wao, Fatiha na Gamutu waliruhusiwa kuendelea na taratibu nyingine. Wakaondoka na kuelekea kwenye bustani ya maua, mahali walipozoea kukaa wakiwa wawili.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tafadhali sana Gamutu, nitunzie heshima yangu, ukienda duniani usithubutu kushirikiana na mwanamke yeyote kimapenzi. Raha ya mapenzi uliyonipa imenichanganya na niko tayari kufanya lolote ilimradi niwe na wewe siku zote.”

    “Nimekuelewa Fatiha, sitafanya. Lakini mbona unanipa ahadi hewa kila mara, niambie siku yangu ya kurudi duniani.”



    “Subiri hii sherehe iishe, ukiondoka saa hizi mkuu anaweza kukuulizia halafu akibaini kwamba haupo, ataniadhibu mimi kwa sababu alinikabidhi siku ya kwanza uliyoletwa huku.”



    “Lakini bado nasikia sauti za watu wakiniita jina langu kila mara, namsikia bibi yangu akiniita mpaka analia. Niache niende bwana, nitatimiza masharti yote uliyonipa.”

    “Najua jinsi bibi yako anavyohangaika kwa waganga, lakini kama nilivyokwambia mapema, ukienda kamwambia aache kwenda kwa waganga kwa lengo la kunidhuru kwani sina nia mbaya kwako wala kwake, bali nataka kuwasaidia.”



    ”Nimekuelewa Fatiha, mbona unaongea jambo moja mara nyingi?”

    Wakati wakizungumza hayo, Gamutu alizidi kusikia sauti zikimuita kwa nguvu masikioni mwake. Kila alipojaribu kugeuka na kuangalia ni nani aliyekuwa anamwita, hakumwona mtu yeyote.



    Katika hali ambayo hakuitegemea, alishangaa kumuona Fatiha akianza kulalamika kwa maumivu makali, damu nyingi zikawa zinamtoka masikioni, puani na mdomoni.

    “Mbona unatokwa na damu nyingi masikioni, puani na mdomoni?”



    “Nahisi kuna watu wananijaribu, bahati yao leo wamenikuta nimetoka kufanya tukio kubwa la kusababisha ajali za kutisha hadi nguvu zimeniishia. Lakini nikipata nguvu lazima niwaoneshe kuwa mimi ni nani,” aliongea Fatiha huku akizidi kutokwa damu.



    “Nikumbatie Gamutu, najisikia vibaya sana,” alizidi kuongea Fatiha huku akitetemeka mwili mzima. Muda mfupi baadaye Fatiha akalegea mwili mzima, akalala kwenye mikono ya Gamutu huku damu nyingi zikimtoka.



    ***

    Waganga wa kienyeji walikuwa wakihangaika kumkomboa Gamutu kutoka kwenye himaya ya majini, wakisaidiana na bibi yake, Lubunga. Walikesha makaburini siku mbili mfululizo wakifanya matambiko na mizungu ya kichawi kwa lengo la kuvunja nguvu za kijini ambazo tayari zilikuwa zimemuingia Gamutu na kuanza kufanya kazi.



    Kazi ngumu waliyoifanya ilisababisha Fatiha ambaye ndiye aliyepewa jukumu la kumlinda Gamutu kuzidiwa nguvu. Kilichotokea ni kuwa, baada ya wale waganga kumzidi nguvu Fatiha, alizimia huku akitokwa na damu nyingi puani, mdomoni na masikioni. Waliitumia nafasi hiyo vizuri kwani mganga mmoja aliweza kupenya hadi kwenye himaya ya majini na kuanza kumsaka Gamutu kwa lengo la kumchukua kwa nguvu.



    Baada ya kufika eneo alilokuwepo, yule mganga alishangaa kumkuta Gamutu akiwa amemkumbatia Fatiha ambaye hakuwa na fahamu. Kwa mujibu wa nguvu zao za kichawi, kitendo cha kumgusa Fatiha, hata kama alikuwa amep-oteza fahamu kingesababisha arejewe na nguvu zake, jambo ambalo lingekuwa hatari kwa Gamutu na yeye mwenyewe. Ikabidi aanze kutumia mbinu za kumshawishi amuachie mwenyewe ndipo waondoke.



    “Gamutu! Gamutu! Gamutuuu! Mwachie huyo jini, bibi yako amenituma nije kukuchukua,” aliongea yule mganga kwa sauti kubwa, Gamutu akawa anamsikia lakini hamuoni.



    “Wewe ni nani?” Aliuliza Gamutu. Yule mganga ikabidi ajitambulishe kuwa ni ndugu yake na ametumwa na bibi yake kuja kumchukua. Licha ya kujitambulisha, Gamutu alikuwa ni kama aliyepagawa kwani hakutaka kumwachia Fatiha, akawa anamfuta damu nyingi zilizokuwa zinamvuja.



    “Mwachie huyoo twende!”

    “Hapana, siwezi kumuacha akiwa kwenye hali kama hii, yeye ndiye aliyenipokea na kunifanyia mambo mengi mazuri, lazima nihakikishe amepona kwanza ndiyo nirudi kwa bibi.”



    Mabishano makali yaliendelea kwa muda, ikabidi yule mganga ajibadilishe sura na kuanza kuonekana kama bibi yake Gamutu, Bi Lubunga kisha akajitokeza mbele yake ili aamini.

    “Haa kumbe ni wewe bibi?” Alihoji Gamutu huku akimuachia Fatiha na kuanza kuelekea kule yule mganga alikokuwa amesimama. Akachomoa kichupa kilichokuwa na unga mweusi, akaupuliza angani, Gamutu akaanza kujihisi kulegea viungo vvote vya mwili wake.

    Akaanza kuhisi kizunguzungu kikali, akamuona yule mganga akimsogelea na kubadilika sura tena, akamshika mikono kisha akazungumza maneno kadhaa ambayo hakuyaelewa, wakapotea kimiujiza.



    Kituo cha kwanza kilikuwa ni makaburini, mahali walipokuwa wanafanyia tambiko la kumkomboa Gamutu. Yule mganga alipomfikisha Gamutu akiwa hajitambui, kila mmoja alipiga vigelegele kwa furaha kwani hatimaye kazi ile nzito ilikuwa imekamilika.

    Wakaendelea na tambiko usiku kucha, Gamutu akiwa amepoteza fahamu. Kulipopambazuka, wakambeba na kuanza kumrudisha nyumbani kwa Bi Lubunga.



     Mganga wa kwanza alitangulia mbele akiwa na chungu kilichokuwa kinawaka moto ndani yake, yule wa pili akawa ameshika kitanda cha kamba pamoja na Bi Lubunga ambacho walikuwa wamemlaza Gamutu aliyekuwa amepoteza fahamu. Kwa pamoja walikuwa wakiimba mapambio ambayo haikueleweka yalikuwa ni ya dini gani, huku yule wa mbele akimwaga vitu kama dawa njia yote waliyokuwa wanapita.



    Waganga hawa wanawake ndiyo waliyomfanyia Gamutu tambiko la kwanza la maisha. Nguvu zao zilikuwa zikiaminika Sumbawanga yote, na hata miujiza waliyokuwa wanaifanya ilisababisha wengine kuwaita ‘mapacha wa moto’. Hii ndiyo sababu iliyofanya Bi Lubunga aende kuomba msaada moja kwa moja kwao kwani ndiyo pekee waliokuwa wanamuelewa vizuri pamoja na nguvu alizozaliwa nazo.



    Mapambazuko yaliwapokea vizuri kwani kwa kadri walivyozidi kusogea nyumbani kwa Bi Lubunga ndivyo kulivyozidi kupambazuka. Kazi nzito waliyoifanya makaburini kwa siku mbili mfululizo ilikuwa imezaa matunda na sasa kila mmoja alikuwa akimshukuru Mungu wake kwa yaliyotokea.



    “Gamutu! Gamutu! Amka mjukuu wangu…,” Bi Lubunga alikuwa akimuita mjukuu wake wakati wale waganga wamemlaza kwenye kitanda cha kamba chumbani kwake huku chini wakiwa wameweka karai lenye maji yaliyochanganywa na dawa za kienyeji, ambayo mvuke wake ulikuwa ukimpitia Gamutu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mpaka inatimu saa moja asubuhi, Gamutu alikuwa bado hajazinduka. Wale waganga walikuwa wakizidi ‘kufanya mambo’ huku wakitumia ujuzi wao wote kuhakikisha muunganiko wa nguvu za Gamutu na majini unavunjika. Hakuna aliyekuwa na jibu la moja kwa moja kwamba kwa nini Gamutu amevutwa kirahisi namna ile na nguvu za kijini.



    Haikuwa kawaida kwa binadamu kwenda kuishi kwenye himaya ya majini kisha kurejea. Binadamu siku zote huishi duniani na majini ujinini, kwa Gamutu ilikuwa ni zaidi ya maajabu. Ilipotimu saa tatu asubuhi, Gamutu alifumbua macho na kwa mara ya kwanza akazungumza.



    “Bibi yangu yuko wapi?”

    “Nipo Gamutu, nipo mjukuu wangu, pole!”

    “Kwani bibi unanipa pole mimi nimefanyaje?

    “Hapana Gamutu, hamna kitu, nakupa pole kwa safari ndefu,” aliongea Bi Lubunga huku akimsogelea pale kitandani na kutaka kumkumbatia… wale waganga wakamzuia na kumweleza kuwa kwa kufanya vile na yeye ataambukizwa nguvu za kijini kwani zilikuwa bado hazijaisha mwilini mwake.



    Alisikia maelekezo aliyopewa, akarudi nyuma, dawa ikazidi kuchochewa na sasa mvuke mwingi ukawa unamlowanisha Gamutu na kumfanya apige chafya nyingi. Wale waganga waliendelea kufanya mambo yao, hawakuchoka na hawakuwa na dalili hiyo. Bi Lubunga aliwashangaa kwani kwa siku mbili mfululizo hawakupata hata muda wa kupumzika.

    Akajua kweli walikuwa na lengo la kuhakikisha mjukuu wake anakombolewa. Kwa moyo mkunjufu akaongeza malipo ya ng’ombe na kondoo mwingine mweupe kama nyongeza ya makubaliano ya awali.



    Mpaka inatimia saa kumi na moja jioni, Gamutu alikuwa tayari amerejewa na fahamu zake timamu, akawa na uwezo wa kuwatambua watu na kuzungumza lugha inayoeleweka. Hata hivyo, wale waganga hawakuondoka. Walitaka kuhakikisha nini kitatokea usiku wa manane. Kama siku hiyo ingepita bila chochote kutokea, hiyo ingemaanisha kuwa tayari Gamutu yuko huru. Hakuna ambaye alikuwa na uhakika wa nini ambacho kitatokea, lakini kwa kuwa wote walikuwa na imani kali juu ya mizimu na nguvu za giza, waliamini watavishinda vikwazo vyote.



    ***

    Fatiha aliendelea kulala akiwa hajitambui pale alipochukuliwa Gamutu. Nguvu zilikuwa zimemwisha kabisa kwani wale waganga walimvizia akiwa ametoka kusababisha ajali duniani ambazo zilimlazimu kutumia nguvu zake zote za kijini, akabaki mwepesi. Wakamvamia na kumzidi kete kwenye ulimwengu wa giza. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kumwokoa Gamutu kirahisi, vinginevyo wasingeweza.



    Usiku mzima ulipita bila Fatiha kurejewa na fahamu. Hata wenzake walipoamka kwa ajili ya sala ya alfajiri, yeye alikuwa bado hajarudi kwenye hali yake ya kawaida. Mapambazuko yalimkuta akiwa bado hajitambui.



    “Kuna mmoja wenu hajaonekana tangu alfajiri, yu wapi malkia wa uvumilivu Fatiha? Ewe mkuu! Fatiha alionekana bustanini na ‘kiti mgeni’, wakicheza michezo ya kimahaba, kisha harufu ya damu ikafuatia, sote tuliisikia… ilikuwa inafanana na ya malkia wa uvumilivu Fatiha.”



    Maelezo yale yalifanyiwa kazi ndani ya sekunde chache, bustani nzima ilizingirwa na Fatiha akaonekana kando ya waridi akiwa amelala huku damu nyingi zikiwa zimeganda pembeni yake na kutengeneza mfano wa bwawa la damu.



    “Nini kimempata?”

    “Atakuwa ameponzwa na mapenzi!”

    “Hapana, amefanya kazi kubwa kuliko ninyi nyote usiku uliopita akiwa sambamba na ‘kiti mpya’. Atakuwa amekumbana na nguvu mbaya duniani, mpelekeni joshoni haraka akaoge na kutoa nuksi. Fanyeni haraka,” sauti yenye mamlaka ilisikika, kundi kubwa likajipanga kufanya kazi ile.



    Ilipangwa kuwa akizinduka tu, aeleze nguvu mbaya kutoka duniani zimempataje, kisha kisasi kingetekelezwa haraka kabla ya usiku wa manane haujaisha. Akiwa kwenye usingizi ule wa kifo, Fatiha alijishangaa akiweza kuuvaa ubinadamu wa kawaida kama Gamutu na kukaa pembeni yake, ingawa kwa kutumia sura ya kijini ambayo inaweza kubadilika na kuwa binadamu endapo mhusika ataamua.



    Alisimama kando ya kitanda cha kamba alichokuwa amelazwa Gamutu akifanyiwa tiba na waganga wa kienyeji. Kwa kuwa nguvu zake za kijini zilikuwa zimenyonywa na mabaki yake kubakizwa ndani ya bustani ulipokuwa mwili wake wa kijini, hakuwa na nguvu duniani zaidi ya kubakia mtazamaji.



    Akawa anaangalia kila kitu anachofanyiwa Gamutu. Moyoni alijua kuwa kama hatarejewa na nguvu zake za kijini haraka kabla wale waganga hawajamalizia tambiko lao, asingeweza kumpata tena kipenzi cha moyo wake. Machozi yakawa yanamtoka huku akisubiri huruma ya majini wenzake kuutafuta mwili wake kisha kuuongezea nguvu kama wafanyavyo majini siku zote.



    Kilichokuwa kikimliza ni mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa Gamutu. Hakutaka kumkosa kwa namna yeyote ile. Alijiapiza moyoni kuwa akirejewa na nguvu zake atawafunza adabu wote walioshiriki kumchezea.



    Hali ya Gamutu iliendelea kuimarika taratibu. Kitu kikubwa kilichokuwa kinamsumbua ilikuwa ni kushtuka mara kwa mara na kulitaja jina la Fatiha. Muda mwingine alikuwa ni kama anawasiliana naye ingawa hakuna ambaye alikuwa na ushahidi wa hilo. Wale waganga waliendelea kumtibu wakitaka kumtenganisha kabisa na nguvu za uvutano wa kijini alizozipata kwa Fatiha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda ulizidi kusonga na giza likaingia. Kila mmoja alikuwa na shauku ya kutaka kuona kama zindiko lile limezaa matunda ya kudumu kwani kama usiku wa manane ungepita na hatimaye siku mpya kuanza, wangekuwa na uhakika kuwa Gamutu ameokolewa moja kwa moja kutoka kwenye himaya ya majini.



    Waliendelea kumuangalia kwa karibu kutaka kuona nini kitatokea. Bi. Lubunga naye alikuwa akiiomba miungu yake kufanya miujiza kwani hakuwa tayari kuona mjukuu wake anarudi tena kwenye himaya ya majini.



    ”Gamutu, lala mjukuu wangu, kesho nitakupa zawadi nzuuri niliyokuwa nimekuandalia wakati haupo,” aliongea Bi. Lubunga huku akimbembeleza mjukuu wake pale kitandani. Wale waganga walikuwa wakiimba nyimbo za kichawi huku wakikizunguka kile kitanda alichokuwa amelala Gamutu.



    Maneno yale aliyoambiwa na bibi yake kuhusu zawadi yalimkumbusha kitu. Alianza kuvuta uzingativu kama anayekumbuka jambo. Kumbukumbu zake zilimrudisha muda mfupi kabla ya kuachana na Fatiha ambapo alimpa pete ya maajabu na kumwambia kuwa ina uwezo wa kumpa chochote alichokuwa anakitaka.



    Alijaribu kukumbuka ni wapi alipoiweka kwani wakati anachukuliwa na mganga na kurudishwa duniani, akili yake haikuwa kwenye hali ya kawaida. Alijaribu kuvuta kumbukumbu kwa muda mrefu lakini hakukumbuka ni wapi alipoiweka.



    “Unatafuta nini?” Bibi yake alimuuliza baada ya kumuona hayuko sawa.

    “Hamna kitu!” alijibu Gamutu kwa kifupi kisha akatulia kitandani. Alijibu vile kwa kuwa hakutaka wajue alipewa nini. Kitendo cha kukumbuka kuhusu pete ile, kilimfanya aanze kumfikiria upya Fatiha.



    “Sasa hata kama ni jini, ikiwa ameweza kuniamini na kunipa zawadi kubwa kama pete ya maajabu, kwa nini na mimi nisioneshe fadhila kwake?” Mawazo yalikuwa yakipita kwa kasi kwenye kichwa cha Gamutu kama mkanda wa video uliokuwa unapelekwa mbele. Kwa upande wake hakuona tatizo lolote kuwa na uhusiano na Fatiha na akajikuta akizidi kumpenda kwa dhati kutoka moyoni mwake.



    “Lakini siyo kiumbe wa kawaida? Mambo niliyoshuhudia akiyafanya ujinini yanatisha sana, kazi zake ni za hatari na hata mimi siku nikimkosea anaweza kunifanyia unyama wa kutisha… Lakini nampenda!”

    Gamutu aliongea kwa sauti na kumfanya bibi yake na wale waganga kuacha kila walichokuwa wanakifanya na kubaki wanamkodolea macho.



    Kumbe muda wote alikuwa akiwaza kimoyomoyo lakini alipotamka maneno…

    “lakini nampenda,” aliongea kwa sauti kubwa, hali iliyowashtua bibi yake na wale waganga.

    “Wee Gamutu! Lakini unampenda nani?” Gamutu alishtuka baada ya kusikia bibi yake anamuuliza swali lile.



    Hakudhani kuwa aliongea kwa sauti mpaka wakamsikia, kwa aibu akajifanya kubadilisha mada. Licha ya kukwepesha ukweli, bibi yake akisaidiana na wale waganga waliendelea kumbana aseme alikuwa anamzungumzia nani.



    Licha ya kumbana sana, hakuwa tayari kuongea. Walichokifanya wale waganga ilikuwa ni kumnywesha dawa ya kienyeji ya usingizi. Alipolala wakaanza mjadala juu ya kile alichokizungumza.

    “Anasema anampenda nani?”

    “Atakuwa ni yule jini niliyemkuta amempakata nilipoenda kumkomboa kule ujinini.”

    “Kwani ilikuwaje?”



    Ilibidi yule mganga aliyeenda kumchukua kwa nguvu kule ujinini aanze kuwaeleza Bi. Lubunga na yule mganga mwenzake juu ya hali halisi aliyoikuta wakati alipoenda kumuokoa kule ujinini. Kila mmoja alishangaa kusikia kuwa Gamutu hakutaka kuondoka kule mpaka yule mganga alipojibadili na kuwa na sura kama ya bibi yake.

    “Kwa mazingira niliyowakuta, wanaweza kuwa tayari wameshakutana kimwili.”

    “Sasa kama ni hivyo itakuwaje?”



    “Kama ni kweli walishashiriki mchezo wa kikubwa, hatari kubwa iliyopo ni kwamba nguvu za kijini haziwezi kuisha mwilini mwake, labda zitakuwa zinapungua taratibu.”

    “Huyu mtoto! Yaani hata haogopi?”



    “Na kwa kawaida mtu akishaanza kufanya mapenzi na jini, mwanamke yeyote wa kawaida atakayekutana naye kimwili lazima apoteze maisha wakiwa kwenye tendo.”

    “Hii sasa hatari! Nisaidieni jamani kumuweka huru mjukuu wangu, vinginevyo nitashindwa kuishi naye sehemu yoyote chini ya jua.”



    “Usiwe na wasiwasi, tutajaribu kwa kadiri ya uwezo wetu wote.”

    Wakati wakijadiliana hayo, Gamutu alikuwa kwenye usingizi mzito baada ya kunyweshwa dawa ya kienyeji. Akiwa usingizini, Fatiha alimtokea kwa njia ya ndoto na akawa anamueleza nini cha kufanya ili wote wawili wasidhurike.



    “Pete niliyokupa ipo wapi?”

    “Siioni Fatiha, nimeitafuta sana lakini siioni.”

    “Huioni vipi wakati uko nayo mwilini mwako? Mbona mimi naiona,” aliongea Fatiha na kuingiza kidole chini ya ulimi wa Gamutu na kuitoa pete ile.”



    “Niliificha hapa kwa makusudi, nilijua lazima utaipoteza wakati ukiwa mikononi mwa waganga wa bibi yako. Ivae kwenye kidole cha mkono wako wa kushoto na usiivue. Zingatia masharti yote niliyokuwa nimekuelekeza.”



    Akiwa bado usingizini, Gamutu alivalishwa pete ile kimiujiza na Fatiha. Alipozinduka alijikuta akiwa na pete inayong’aa kidoleni. Akawa anaitazama huku akitabasamu, hali iliyozidi kuwashtua bibi yake na wale waganga.



    “Hicho ulichovaa kidoleni ni nini?”

    “Ni pete!”

    “Umeipata wapi wakati muda wote hukuwa nayo?”

    “Amenipa na…ni…!”



    “Nani?”

    Gamutu alishindwa kusema, akawa anajiumauma. Wale waganga walishaelewa kila kitu, wakawa wanajadiliana nini cha kufanya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waliendelea kujadiliana bila kupata majibu. Kwa jinsi ilivyoonekana, nguvu iliyokuwa kwenye pete ile ilikuwa kubwa kuwazidi wale waganga kwani kila mara walipokuwa wanataka kumvua, walikuwa wakishindwa.

    “Mh! Leo kazi ipo. Kuna uwezekano mkubwa usiku wa leo kukatokea miujiza mikubwa, lazima tufanye kazi ya ziada kumdhibiti.”



    “Lazima tufanye kila linalowezekana kumpokonya hiyo pete, vinginevyo anaweza hata kutudhuru sisi kwa kutumia nguvu zilizopo ndani yake.”

    Mjadala uliendelea kwa muda huku Gamutu akiwa kimya. Akili yake yote ilikuwa kwa Fatiha. Hali aliyomuacha nayo mara ya mwisho ilimfanya awe na wasiwasi, akahisi kuwa lazima atakuwa matatizoni.”



    “Lakini mbona aliponitokea ndotoni hakuonesha hali yake ya kawaida?” Alijisemea Gamutu kimoyomoyo huku akiwa amekishika kile kidole kilichokuwa na pete. Hakutaka mtu yeyote amvue na akatishia kuwafanyia kitu kibaya kama wangeendelea kumng’ang’aniza.

    “Sasa mtu mwenyewe tunayemsaidia hataki kutupa ushirikiano, unafikiri tutafanyaje kazi?”



    “Jamani msameheni, huyu bado mtoto na akili yake haijakomaa na hapa hajui alitendalo.”

    “Usimtetee mjukuu wako, unasema bado mtoto wakati tayari anashiriki michezo ya kikubwa mpaka na majini. Sasa ongea naye pembeni, kama hataki tumsaidie basi sisi tuondoke maana kazi yetu ilikuwa ni kumkomboa kutoka ujinini na hilo limetimia, kama mwenyewe anatamani kuendelea kuishi huko unafikiri tutafanya nini? ”



    Wale waganga walimbana Bi. Lubunga kutokana na tabia za ajabu alizokuwa anazionesha Gamutu. Ilifika mahali wakataka kukata tamaa na kuondoka zao lakini Bi. Lubunga alizidi kuwasisitiza kuwa wasiondoke.



    Wakiwa bado wanajadiliana, walisikia kishindo kikubwa nje ya nyumba kisha zikaanza kusikika sauti za watu kama wanacheka. Dakika chache baadaye eneo zima lilitawaliwa na ukimya wa ajabu.

    “Mambo yameanza! Yule jini ameshapata nguvu mpya na sasa amemfuata Gamutu.”

    “Bila kuivua hiyo pete atachukuliwa sasa hivi, hebu ongea na mjukuu wako ili tumsaidie.”



    Licha ya Bi. Lubunga kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote kumshawishi Gamutu aivue pete ile, hakuwa tayari, jambo lililofanya wale waganga waanze kufungasha vitu vyao tayari kwa kuondoka kwani hawakutaka kushiriki kwenye vita ile ngumu iliyokuwa mbele yao.



    Gamutu alikuwa ni kama amechanganyikiwa akili kwani hakutaka kabisa kuivua, alichokitaka ilikuwa ni kuonana tena na Fatiha. Ilibidi Bi. Lubunga atumie busara za kiutu uzima kuwaelewesha wale waganga wambo tayari walishakusanya vifaa vyao vyote vya kazi. Wakakubaliana kumnywesha dawa ya usingizi Gamutu kisha waivue pete ile ndiyo waendelee na matambiko yao.



    Hilo lilifanyika ndani ya sekunde chache, Gamutu akanyweshwa dawa ya usingizi na kulala. Alipolala ile pete kidoleni mwake ilivuliwa na wale waganga wakawa ni kama wameanza upya kazi, safari hii kwa nguvu zaidi kwani tayari kulishakuwa na dalili mbaya.



    Baada ya kumvua ile pete Gamutu, kilisikika kishindo kingine kikubwa, kisha sauti za watu kucheka kama pale awali zikasikika tena, safari hii zikawa zinatokomea mbali na nyumba ile ya Bi. Lubunga.



    “Amekuja jini mmoja, tena nahisi ni yule aliyekuwa naye kwa mara ya mwisho lakini tumemuweza. Labda akaite wenzake,” aliongea mganga mmoja na kuungwa mkono na mwenzake. Bi. Lubunga alikuwa akishangaa kila kinachotokea kwani hakuwa na uelewa wowote juu ya mambo ya majini.



    Wale waganga walifanikiwa kudhibiti nguvu za kijini zilizokuwa zinamuandama Gamutu kwani mpaka kunapambazuka, hakuna muujiza mwingine wowote uliotokea zaidi ya milio ya kutisha ya bundi juu ya paa na paka waliokuwa wanalia kama watoto wachanga.



    Walipohakikisha kuwa wametengua kwa kiasi kikubwa nguvu za kijini ndani ya mwili wa Gamutu, waliaga na Bi. Lubunga akawaruhusu kwa moyo mkunjufu. Walimpa angalizo kuwa asikubali Gamutu akaivaa tena ile pete kwani atakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na yule jini aliyekuwa anamsumbua, Fatiha.



    ***

    Dawa ya usingizi aliyonyweshwa Gamutu ilimfanya alale masaa mengi mfululizo bila kuzinduka. Mpaka inatimu saa saba za mchana siku iliyofuatia, alikuwa bado hajazinduka. Bibi yake hakuwa na hofu kwani alishaelekezwa na wale waganga kuwa atazinduka saa tisa alasiri.

    Kama walivyosema, kweli ilipofika saa tisa, Gamutu alizinduka na kitu cha kwanza alichokikumbuka ilikuwa ni pete yake.



    “Nataka pete yangu!”

    “Pete wameichukua wale waganga waliokuwa wanakushughulikia, wamesema hutakiwi kuivaa tena kwa sababu itakufanya urejee kwenye hali ya ujini.”

    “Bibi kwa nini umewaruhusu waondoke nayo? Hujui kuwa ile ina uwezo wa kuyabadilisha maisha yetu na sisi tukaonekana watu kwenye hii dunia.”



    “Acha mambo yako ya kitoto Gamutu, kama ni umasikini bora tufe nao kuliko kupata utajiri wa kijini. Madhara yake ni makubwa sana kwa siku za baadaye ingawa unaweza kuwa hulioni hilo. Hayo mambo sitaki kuyasikia, nataka uwe mtoto mzuri kama ulivyokuwa awali.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maneno yale ya bibi yake yalimuingia kidogo akilini, akatulia ingawa mawazo juu ya Fatiha hayakumuisha. Siku ya kwanza ikapita bila ya jambo lolote baya kutokea. Bi. Lubunga muda wote alikuwa akikaa jirani na mjukuu wake kumchunguza asije akatoweka.

    Kilichomshangaza ni kwamba tabia za Gamutu zilikuwa zimebadilika mno. Hakuwa tena Gamutu aliyependa kuongea na kufanya mizaha. Akawa muda wote yuko kimya. Hata bibi yake alipokuwa akimsemesha alikuwa mgumu wa kujibu chochote.



    Baada ya siku ya tatu kupita, Gamutu alianza kuhisi hali tofauti. Muda wote alikuwa akitamani kukutana kimwili na wasichana. Kikwazo kikubwa kikawa ni masharti aliyoachiwa na Fatiha ya kutojihusisha na mapenzi na mtu mwingine zaidi yake.

    “Mbona hutulii, unataka nini?” Bi. Lubunga alimuuliza Gamutu baada ya kuona hatulii sehemu moja.



    Hakujibu chochote zaidi ya kunyamaza na kujifanya kutulia kwa muda. Ilifika hatua hata yeye mwenyewe akawa anajishangaa kwani haikuwahi kumtokea akawa na hamu ya mchezo wa kikubwa namna ile.

    “Pete yangu ingekuwepo ningemwambia Fatiha aje anichukue, mateso gani haya ninayoyapata,” aliongea Gamutu kwa sauti bila kutambua kuwa bibi yake alikuwa anamsikiliza.



     “WEWE! Unazungumzia nini?”

    “Wewe! Unazungumzia nini?”

    “Hamna kitu bibi, nilikuwa nawaza tu mwenyewe.”

    “Unawaza ndiyo useme bora aje akuchukue? Au umemkumbuka huyo jini wako?”

    “Hapana bibi, naomba nisamehe.”



    “Nikusamehe umefanya kosa gani?”

    “Bibi basi yaishe?”

    Licha ya Gamutu kutaka mambo yale yaishe, bibi yake aliendelea kumshikia bango akitaka ufafanuzi wa kile alichokizungumza, jambo lililomkasirisha. Akaamua kuondoka kwa hasira. Alipotoka na kubamiza mlango, huku nyuma bibi yake alibaki na maswali mengi ambayo hakuna hata moja ambalo alilipatia jibu.



    Mabadiliko ya mjukuu wake yalimfanya amkumbuke mwanaye mpendwa , Isambi ambaye ndiye aliyekuwa baba mzazi wa Gamutu. Alikumbuka mara ya mwisho alipompeleka Gamutu Kalemie, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo walipowasili tu, Isambi akaaga dunia. Alikumbuka jinsi alivyomkabidhi mkufu na pete kama urithi pekee ambao utamlinda.



    “Hivi ile pete na mkufu alivyopewa na baba yake niliviweka wapi?” alijiuliza Bi Lubunga wakati kumbukumbu za siku mwanaye alipoaga dunia zilipomjia. Alikumbuka pia jinsi Gamutu alivyozaliwa kwa kutanguliza kichwa, akatoka akiwa tayari ameshaota meno, hali iliyosababisha kifo cha mama yake.



    “Ndiyo maana kwenye kabila letu mtoto akizaliwa hivi huwa anatupwa porini ili aliwe na wanyama wakali! Usumbufu kama huu unaweza kusababisha mtu akafa kabla ya siku zake. Maskini Gamutu mjukuu wangu, hivi mwisho wake utakuwa ni nini?” Bi. Lubunga aliendelea kuwaza huku akijifuta machozi yaliyokuwa yanaulowanisha uso wake wa kizee.



    Alisimama kinyonge ne kwenda kwenye sanduku lake kujaribu kutafuta vile vitu ambavyo Gamutu aliachiwa na baba yake wakati anafariki. Aliamini akiupata mkufu na ile pete aliyoachiwa, huenda mauzauza yanayomkabili yangefikia mwisho.

    Alianza kupangua vitu vyote na akajiapiza kuwa atavitafuta mpaka avipate ili kumnusuru mjukuu wake.



    ***

    “Oyaa sista mambo?”

    “Wee Gamutu, yaani leo umekuwa mkubwa unaniita mimi mama’ako mdogo ‘oya sista’, ama kweli watoto wa siku hizi hamna adabu.

    Aliongea mwanamke mmoja aliyekuwa anaishi kijiji kimoja na Gamutu. Licha ya kumshushua sana Gamutu, bado aliendelea kumganda huku mazungumzo yake yakionesha kuwa alikuwa akimtaka kimapenzi.



    “Lakini mimi ni mkubwa sana kwako Gamutu, isitoshe wakati unakua sisi ndiyo tuliokulea,” alizidi kusisitiza yule mwanamke lakini Gamutu hakutaka kuelewa. Akawa anamshinikiza wafanye mapenzi vinginevyo angemfanyia kitu kibaya na ikibidi kumtoa uhai.



    “Kwa kuwa eneo walilokuwepo hapakuwa na mtu mwingine yeyote zaidi yao, Gamutu aliamua kutumia nguvu kwani hamu ya kufanya mapenzi sasa ilikuwa imefika kwenye kilele. Akamkaba yule mwanamke shingoni na kumlazimisha wafanye mapenzi kwa lazima.

    Kwa kuwa alitishiwa maisha, yule mwanamke aliamua kutulia na kumwacha Gamutu afanye alichokuwa anakitaka. Akambeba juu juu mpaka pembeni kwenye kichaka, akamchania nguo yake ya ndani na kuanza kumuingilia kwa nguvu.



    Yule mwanamke alijaribu kupiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna aliyemsikia, Gamutu akawa anaendelea kujisevia. Katika hali ambayo hata Gamutu mwenyewe hakuielewa, wakiwa katikati ya tendo lile, yulemwanamke alianza kubadilika na kuwa kiumbe wa ajabu kama ilivyowahi kutokea wakati akifanya mapenzi na Fatiha.



    Licha ya mwili kubadilika, alianza kutokwa na damu nyingi puani, mdomoni na masikioni, hali iliyomfanya Gamutu kuacha kila alichokuwa anakifanya na kutimua mbio. Alimuacha yule mwanamke palepale kichakani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikimbia umbali mrefu akihofia kuhusishwa na lolote baya ambalo lingemtokea mwanamke yule, akajikuta ametokezea kwenye kijiji cha pili. Alipofika, alijichanganya na wanakijiji wengine waliokuwa wamekusanyika kwenye klabu ya pombe za kienyeji, akakaa kwenye benchi na kuagiza lita moja ya pombe ya kienyeji aina ya kimpumu. Japokuwa hakuwa mlevi, aliamua kuagiza ili aonekane sawa na wanakijiji wale, fedha kidogo alizomuibia bibi yake zilimpa jeuri.



    Akilini mwake bado alikuwa akisumbuliwa na mawazo ya tukio lililotokea muda mfupi uliopita. Hakujua nini itakuwa hatima ya mwanamke yule. Kimoyomoyo alikuwa akiombea akipona asimtaje kwani kijiji kizima kisingemuelewa.



    Akiwa kwenye lindi la mawazo, bado hisia za kimapenzi zilikuwa zikimtesa. Hamu yake haikuwa imefika mwisho ila alilazimika kukatisha kutokana na hali ile iliyojitokeza.

    “Nitapata wapi mwanamke mwingine nimalize hamu yangu? Sitaweza kulala leo kabisa, najisikia kufanya mapenzi na mwanamke yeyote atakayejitokeza mbele yangu,” alikuwa akiwaza Gamutu huku akipepesa macho huku na kule ndani ya klabu ile ya pombe za kienyeji.



    “Mbona unashangaa watu, unamtafuta nani?” aliuliza mama muuza pombe ambaye kiumri alikuwa ni mwanamke wa makamo.

    “Aaah mama muuza, nilikuwa nakutafuta wewe mwenyewe, njoo tuongee pembeni kidogo,” aliongea Gamutu na kuinuka pale alipokuwa amekaa. Yule muuzaji ambaye alionekana kukolea kwa kilevi, alimfuata huku akipepesuka, wakatoka mpaka eneo ambalo watu wengine hawakuwa wakiwasikia.



    Bila kupoteza muda Gamutu alieleza shida yake.

    “Wee mtoto, yaani unanitaka mimi, mbona wewe ni sawa na mwanangu wa kumzaa, makubwa!”

    “Nitakupa fedha, we sema unataka shilingi ngapi,” Gamutu aliongea kwa sauti iliyoonesha jeuri ya fedha. Kwa kuwa yule mwanamke alikuwa amelewa, alipotajiwa fedha hakufikiria mara mbili, akakubaliana naye na wakaelewana waende kwenye kichaka kilichokuwa nyuma ya klabu ile.



    Kwa hamu kubwa aliyokuwa nayo Gamutu, walipofika tu kichakani, alimvamia na kumchania nguo yake ya ndani, akaanza kumuingilia kwa nguvu. Sekunde chache baada ya kuanza kufanya kitendo kile, alishangaa yule mwanamke akianza kupiga kelele kwa nguvu, mwili wake ukaanza kukakamaa.



    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog