Simulizi : Nilibadilika Na Kuwa Jini Bila Kujijua
Sehemu Ya Pili (2)
Mipango yote ilipokamilika, Bi. Lubunga alimchukua mjukuu wake Gamutu na safari ya kuelekea Kalemae na baadaye Bukavu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikaanza. Kwa kuwa walikuwa wakiishi katika kijiji ambacho hakikuwa mbali sana na Ziwa Tanganyika, walitembea umbali mfupi wakawa tayari wamefika ziwani. Usafiri ambao ulikuwa ukitumika eneo lile ulikuwa ni mtumbwi au majahazi.
Endelea mwenyewe…
“Leo hakuna usafiri, ziwa limechafuka sana, pepo zinavuma kwa kasi na watabiri wa hali ya hewa wanasema mvua kubwa itanyesha mfululizo,” alizungumza mmoja wa wasafirisha abiria kwenye Ziwa Tanganyika aliyekuwa anamiliki jahazi.
Taarifa ile ilimchanganya B. Lubunga, alichokitaka ilikuwa ni kuvuka kuelekea ng’ambo ya pili. Hakutaka kupoteza muda.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliendelea kuuliza uwezekano wa kupata usafiri lakini kote alijibiwa vilevile, kwamba hali ya hewa haikuwa ikiruhusu chombo chochote kusafiri majini. Akiwa amembeba Gamutu mgongoni, alianza kukata tamaa. Alizunguka kwenye fukwe za ziwa hilo kwa muda mrefu bila mafanikio. Mwishowe akawa anataka kuahirisha safari baada ya kukosa usafiri.
“We bibi, kuna usafiri umepatikana, kama unaweza kusafiri kwenye mtumbwi twende nikupeleke,” aliongea mwanaume mmoja baada ya kumuona Bi. Lubunga amekata tamaa na anataka kuondoka.
Bila hata kufikiria mara mbili juu ya hatari ambayo ingetokea kwa kusafiri na mtumbwi kwenye ziwa lililochafuka, tena akiwa na mtoto mdogo, Bi. Lubunga alikubali na haraka haraka akaanza kumfuata yule mwanaume kuelekea mahali uliko mtumbwi.
“Tarif yango faranga nini? Takokoma na ngonga nini? mwana moke azali na mokongo,”
(Nauli ni faranga (shilingi) ngapi? Tutafika saa ngapi? Niko na mtoto mdogo mgongoni ), alihoji Bi. Lubunga kwa lugha ya Kilingala maana ndiyo iliyokuwa ikitumika kwa mawasiliano eneo lile lililokuwa na mchanganyiko wa Watanzania na Wakongo.
“Ngai nazali Nzambe te, nakoyeba makambo ekozala na lac te,”
(Mimi siyo Mungu, siwezi kujua yatakayotokea ziwani,) alijibu yule nahodha wa mtumbwi ambaye baadaye aliambiwa kuwa anaitwa Mutembe, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Baada ya makubaliano na kulipana kabisa nauli, Bi. Lubunga alimfunga mjukuu wake Gamutu vizuri mgongoni na kupanda ndani ya mtumbwi. Kulikuwa na abiria wengine ndani ya mtumbwi ule wapatao saba, akiwemo mzee mmoja aliyeonekana kuwa na umri mkubwa kuliko wote. Kila kitu kilipokamilika, safari ya kulivuka Ziwa Tanganyika hadi ng’ambo ya pili, upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilianza. Mutembe ndiye aliyekuwa kiongozi wa msafara.
Injini ndogo iliyofungwa nyuma ya mtumbwi, iliifanya safari angalau iwe na unafuu. Mtumbwi ukawa unakata mawimbi kuelekea kwenye mji maarufu wa Kalemie, uliokuwa unapakana na Ziwa Tanganyika kwa upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Safari iliendelea kwa masaa mengi majini.
Jua lilianza kuzama na kigiza cha jioni kulipamba Ziwa Tanganyika, ziwa linalosifika kuwa na kina kirefu kuliko yote barani Afrika, likiwa ni la pili duniani. Mutembe alizidi kuongoza chombo majini, huku abiria wake wakionekana kuzidiwa na uchovu.
Baadaye watu wote ndani ya mtumbwi walilala, isipokuwa Bi. Gamutu na Mutembe, nahodha wa mtumbwi ule. Hakuna aliyemuongelesha mwenzake chochote, kila mtu alikuwa anafikiria kuimaliza safari ile ndefu na ya hatari.
Kwa mwendo wa mtumbwi ule, ingewachukua masaa kati ya 13 hadi 17 kuufikia Mji wa Kalemie. Hiyo ilimaanisha kuwa, wangesafiri masaa mengi majini, tena usiku. Muda ulizidi kuyoyoma huku chombo kikikata mawimbi.Kwa muda wote huo, Gamutu alikuwa amelala mgongoni kwa bibi yake, Bi. Lubunga kutokana na dawa ya mitishamba aliyonyweshwa kabla ya safari ili asisumbue njiani.
Ilipotimu saa sita usiku, wakiwa bado safarini, Gamutu alishtuka kutoka usingizini na kuanza kushangaa mazingira waliyokuwemo. Kwa maneno ya kubahatisha, Gamutu alimuuliza bibi yake pale walipokuwa ni wapi.
Bi. Gamutu alitumia ujanja kumdanganya Gamutu kwani alijua akimwambia ukweli angeanza kusumbua. Wakati wakiendelea na safari, Gamutu alianza mambo yake ya ajabu. Jambo la kwanza lililowashangaza wote, ni pale alipoanza kunyooshea kidole mbele yao, huku akionekana kufurahia kile alichokuwa anakiona.
Bi. Lubunga alikazia macho kule mjukuu wake alikokuwa ananyooshea kidole lakini hakuona kitu. Ilibidi amuulize Mutembe maana ya kile mjukuu wake alichokuwa anakifanya. Mutembe kwa kuwa alikuwa mzoefu wa safari za ziwani, alimweleza kuwa mwanaye alikuwa anauona mji mkubwa wa wachawi uliokuwa unaelea katikati ya Ziwa Tanganyika.
“Pale ndiyo kituo kikuu cha wachawi wa nchi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
zote za Maziwa Makuu. Huwezi kuuona mji huo mpaka uwe na uwezo wa ziada. Mchana huwa hauonekani kwani hushuka chini mpaka kwenye ukuta wa chini wa ziwa, na usiku hupanda juu na kuelea,” alieleza Mutembe.
Bi. Lubunga alikuwa akisikia simulizi juu ya mji huo wa kichawi lakini hakuwahi kuuona hata mara moja. Alishangaa kwa nini yeye asiwe na uwezo wa kuuona mji huo lakini mjuu wake Gamutu auone wakati alikuwa bado na umri mdogo.
Gamutu aliendelea kunyooshea kidole upande ule, Mutembe naye akakazia macho huku akionekana kama anaona mambo yanayotendekea kwenye mji huo.
Ghafla Gamutu alianza kulia kwa sauti huku akijificha mgongoni kwa bibi yake, Mutembe naye akawa anahangaika kubadili uelekeo wa mtumbwi baada ya kuwa ni kama ameona jambo baya mbele yao. Kelele za Gamutu ziliwashtua abiria wengine ambao walianza kuhoji kuna kitu gani.
Miongoni mwa abiria wale, kulikuwa na mzee kikongwe ambaye muda wote alikuwa amelala. Aliposhtuka tu, naye alianza kutazama upande ule aliokuwa anatazama Gamutu na Mutembe muda mfupi uliopita, akawa anaonesha wasiwasi mkubwa machoni mwake.
Wale abiria wengine hawakuona chochote, hali iliyozidi kuwatia hofu.
“Bovanda polele! Tokoleka ekolo ya bandoki, soki bovandi tokoleka malamu polele.”
(Tulieni jamani! Tunavuka mji wa wachawi, mkitulia tutavuka salama,” aliongea kwa sauti kubwa yule mzee kwa Kilingala, abiria wote wakatulia huku kila mmoja akikodolea macho kule walikoambiwa ndiko iliko himaya ya wachawi, katikati ya ziwa Tanganyika.
Muda mfupi baadaye wakashuhudia upepo mkali wa ziwani ukianza kuvuma kwa kasi, huku wingu zito likijikusanya angani.
Tukiwa katika hali ya kuchanganyikiwa kutokana na upepo mkali uliokuwa unavuma kutokea kule tulikoambiwa ndiyo kwenye makao makuu ya wachawi, tulianza kuona mwanga ukimulika anga lote mithili ya radi.
Mwanga ule ulikuwa unakuja na kupotea, nilimfunga vizuri mjukuu wangu Gamutu na kujishikilia vizuri kwenye kingo za mtumbwi. Maji yalianza kuingia ndani na kufanya Mutembe awe na kazi ya ziada ya kupiga kasia na kumwaga maji yaliyoingia kwenye mtumbwi.
Muda mfupi baadaye alifanikiwa kuugeuza mtumbwi, sasa upepo ukawa unatupiga kwa mgongoni, hali iliyosababisha mtumbwi uanze kwenda kwa kasi kubwa.
Mutembe alisisitiza kuwa lazima kila mmoja ajishikilie vizuri na atulie kwani ilivyoonesha ziwa lilikuwa linataka kuchafuka. Muda mfupi baadaye manyunyu ya mvua yakaanza kudondoka kuashiria mwanzo wa mvua kubwa.
Mvua iliendelea kunyesha kwa muda mrefu, maji yakawa yanazidi kujaa ndani ya mtumbwi licha ya jitihada kubwa za kujaribu kuyatoa. Watu wote ndani ya mtumbwi waliloana na kuanza kutetemeka, utulivu ukamwisha Gamutu, akaanza kulia kwa sauti ya juu huku akitetemeka kwa baridi.
Baada ya Mutembe kuhangaika kwa muda mrefu kuudhibiti mtumbwi, hatimaye juhudi zake zilianza kuonekana kugonga mwamba. Upepo ulikuwa mkali kiasi cha kuurusha rusha mtumbwi huku na kule. Kila mmoja alianza kulia kwa hofu kwani kwa jinsi ilivyoonekana, sekunde chache baadaye mtumbwi ungepinduka.
Kila mmoja alikuwa akisali na kuomba kwa imani yake, kama walivyotabiri, mtumbwi ulipigwa na wimbi kubwa, ukarushwa juu na kuwafunika wote waliokuwa ndani yake, watu wakaanza kuhaha kuokoa maisha yao. Gamutu alikuwa bado mgongoni kwa bibi yake aliyeanza kukumbushia enzi zake kwa kupiga mbizi kuokoa maisha yake na ya mjukuu wake. Miongoni mwa vitu vilivyokuwa ndani ya mtumbwi uliopigwa na wimbi, ilikuwa ni mikungu ya ndizi.
Bi. Lubunga alipiga mbizi kwa nguvu zake zote, akafanikiwa kuushika mkungu mmoja.
“Hapa siuachii, nitaushikilia kwa nguvu zangu zote,” alijisemea Bi. Lubunga huku akiukamata vizuri ule mkungu wa ndizi. Mjukuu wake Gamutu alikuwa mgongoni akizidi kulia na kutetemeka kwa baridi.Mvua iliendelea kunyesha na giza kuwa totoro. Hakuna aliyejua hatma ya mwenzake kati ya watu wote waliokuwa ndani ya mtumbwi ule. Kila mtu alikuwa akihangaika kuokoa nafsi yake.
***
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Waganga wawili wa jadi waliokuwa wakisifika kwa umahiri wa tiba zao kwenye fukwe za ziwa Tanganyika upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, walikuwa wamekizunguka kitanda cha mgonjwa aliyekuwa mahututi. Tiba mfululizo walizompatia kwa takribani wiki saba hazikuzaa matunda na hali yake ilizidi kuwa mbaya kwa kadri muda ulivyokuwa unazidi kuyoyoma.
Kila aina ya tiba za mitishamba na dawa za kienyeji zilishindwa kutoa nafuu kwa mgonjwa. Taarifa zilishatumwa kwa ndugu zake kuwa waje kumchukua nakujaribu kumpeleka kwa waganga wengine lakini hakukuwa na mwitikio wowote kutoka kwa ndugu zake.
“Nakufa… nakufa jamani, kabla sijafa nataka kuonana na mama yangu mzazi, Bi. Lubunga. Fanyeni kila mnachoweza nionane naye mapema…” aliongea mgonjwa ambaye kumbe alikuwa ni mtoto wa Bi. Lubunga, Isambi kutoka upande wa Tanzania. Ni huyu ndiye aliyekuwa baba mzazi wa Gamutu ingawa mwenyewe alishaaminishwa kuwa mkewe na mtoto wake walifariki.
Alipewa taarifa kupitia watu waliokuwa wanavuka ziwa kutoka upande wa Tanzania kuwa mkewe na mwanaye walifariki wakati wa kujifungua. Hilo lilikuwa ni pigo jingine kwake kwani tayari maradhi yaliyokuwa yanamsumbua yalimmaliza kabisa.
Alitaka kuonana na mama yake mzazi kabla hajafa. Alijua kamwe hawezi kupona kutokana na hali yake ilivyokuwa. Mwili wake ulikuwa umedhoofika sana, mbavu zilikuwa zinahesabika. Kwa kumtazama alikuwa anatisha na kutia huruma. Kitu pekee alichotaka ilikuwa ni kuonana na mama yake kabla hajafa.
***
Baada ya mvua kubwa iliyonyesha kwa saa nyingi mfululizo, hatimaye hali ya hewa ya ziwa Tanganyika ilianza kutulia. Zile pepo zilizokuwa zinavuma kwa kasi kutokea katikati ya ziwa zilitulia, wingu zito lililokuwa limetanda lilipungua na sasa mapambazuko yalianza kuonekana upande wa mashariki wa ziwa Tanganyika. Bi. Lubunga alikuwa ameshikilia mkungu wa ndizi kwa masaa mengi, hali iliyosababisha mikono yake ianze kufa ganzi.
Maji ya ziwa yaliyokuwa na baridi kali kutokana na mvua kubwa iliyonyesha tangu usiku, yaliifanya miili ya Bi. Lubunga na mjukuu wake Gamutu ife ganzi. Walikuwa wakitetemeka kutokana na baridi kali. Wakati wakielea ziwani, bila kutambua upande waliokuwepo, kwa mbali walianza kusikia muungurumo wa boti ikija upande wao.
Bi. Lubunga aliinua mkono mmoja juu, akajivua kitambaa alichokuwa amejifunga kichwani na kuanza kukipunga huku akiita kwa nguvu. Boti ya uvuvi kutoka mji wa Kalemie, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuwa ikirejea kutoka ziwani ilikokuwa ikifanya kazi ya uvuvi usiku kucha.
Ile boti ilipowakaribia mahali Bi. Lubunga na Gamutu walipokuwepo, ilipunguza mwendo baada ya wavuvi kuona vitu mfano wa binadamu ziwani. Boti iligeuza mwelekeo na kuanza kumulika kule Bi. Lubunga alikokuwa na mjukuu wake.
“Tusaidieni jamani, tunakufa! Msaada!” Bi Lubunga alizidi kupunga mkono hewani huku akipiga mayowe ya kuomba msaada.
Ile boti ilisogea karibu yao, wazamiaji wawili wakiwa na maboya wakarukia majini na kuanza kuwafuata Bi. Lubunga na mjukuu wake.
Muda mfupi baadaye walifanikiwa kuwaokoa na kuwaingiza ndani ya boti yao.
“Huyu mtoto yuko salama kweli? Mbona haoneshi kama bado anapumua,” alihoji mmoja kati ya wale wavuvi.
Kauli ile ilimshtua Bi. Lubunga, akaanza kumchunguza vizuri mapigo ya moyo wake.
Alimgusa kifuani lakini mapigo yalikuwa yanasikika kwa mbali sana, hali iliyomfanya achanganyikiwe. Wale wavuvi wakamtuliza na kumweleza kuwa ni kwa sababu ya baridi ya ziwani ndiyo maana mapigo ya moyo ya mjukuu wake yalikuwa chini kiasi kile.
“Mpelekeni vyumba vya juu, kisha mfunikeni kwa nguo nzito, mwili ukipata joto kidogo atatulia,” alisema kiongozi wa wale wavuvi.
Kilichofuatia ikawa ni utekelezaji. Gamutu alipandishwa kwenye vyumba vya juu vya ile boti ya wavuvi, akalazwa mahali pakavu, akafunikwa kwa mablanketi mazito.
Baada ya dakika kadhaa, mapigo ya moyo ya Gamutu yalianza kurudi kwenye hali yake ya kawaida. Bi Lubunga aliyekuwa amekaa pembeni akiwa amejishika tama na kujiinamia, aliruka juu kwa furaha baada ya kuona mjukuu wake amefumbua macho na ameanza kuchangamka.
Tukiwa katika hali ya kuchanganyikiwa kutokana na upepo mkali uliokuwa unavuma kutokea kule tulikoambiwa ndiyo kwenye makao makuu ya wachawi, tulianza kuona mwanga ukimulika anga lote mithili ya radi.
Mwanga ule ulikuwa unakuja na kupotea, nilimfunga vizuri mjukuu wangu Gamutu na kujishikilia vizuri kwenye kingo za mtumbwi. Maji yalianza kuingia ndani na kufanya Mutembe awe na kazi ya ziada ya kupiga kasia na kumwaga maji yaliyoingia kwenye mtumbwi.
Muda mfupi baadaye alifanikiwa kuugeuza mtumbwi, sasa upepo ukawa unatupiga kwa mgongoni, hali iliyosababisha mtumbwi uanze kwenda kwa kasi kubwa.
Mutembe alisisitiza kuwa lazima kila mmoja ajishikilie vizuri na atulie kwani ilivyoonesha ziwa lilikuwa linataka kuchafuka. Muda mfupi baadaye manyunyu ya mvua yakaanza kudondoka kuashiria mwanzo wa mvua kubwa.
Mvua iliendelea kunyesha kwa muda mrefu, maji yakawa yanazidi kujaa ndani ya mtumbwi licha ya jitihada kubwa za kujaribu kuyatoa. Watu wote ndani ya mtumbwi waliloana na kuanza kutetemeka, utulivu ukamwisha Gamutu, akaanza kulia kwa sauti ya juu huku akitetemeka kwa baridi.
Baada ya Mutembe kuhangaika kwa muda mrefu kuudhibiti mtumbwi, hatimaye juhudi zake zilianza kuonekana kugonga mwamba. Upepo ulikuwa mkali kiasi cha kuurusha rusha mtumbwi huku na kule. Kila mmoja alianza kulia kwa hofu kwani kwa jinsi ilivyoonekana, sekunde chache baadaye mtumbwi ungepinduka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila mmoja alikuwa akisali na kuomba kwa imani yake, kama walivyotabiri, mtumbwi ulipigwa na wimbi kubwa, ukarushwa juu na kuwafunika wote waliokuwa ndani yake, watu wakaanza kuhaha kuokoa maisha yao. Gamutu alikuwa bado mgongoni kwa bibi yake aliyeanza kukumbushia enzi zake kwa kupiga mbizi kuokoa maisha yake na ya mjukuu wake. Miongoni mwa vitu vilivyokuwa ndani ya mtumbwi uliopigwa na wimbi, ilikuwa ni mikungu ya ndizi.
Bi. Lubunga alipiga mbizi kwa nguvu zake zote, akafanikiwa kuushika mkungu mmoja.
“Hapa siuachii, nitaushikilia kwa nguvu zangu zote,” alijisemea Bi. Lubunga huku akiukamata vizuri ule mkungu wa ndizi. Mjukuu wake Gamutu alikuwa mgongoni akizidi kulia na kutetemeka kwa baridi.Mvua iliendelea kunyesha na giza kuwa totoro. Hakuna aliyejua hatma ya mwenzake kati ya watu wote waliokuwa ndani ya mtumbwi ule. Kila mtu alikuwa akihangaika kuokoa nafsi yake.
***
Waganga wawili wa jadi waliokuwa wakisifika kwa umahiri wa tiba zao kwenye fukwe za ziwa Tanganyika upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, walikuwa wamekizunguka kitanda cha mgonjwa aliyekuwa mahututi. Tiba mfululizo walizompatia kwa takribani wiki saba hazikuzaa matunda na hali yake ilizidi kuwa mbaya kwa kadri muda ulivyokuwa unazidi kuyoyoma.
Kila aina ya tiba za mitishamba na dawa za kienyeji zilishindwa kutoa nafuu kwa mgonjwa. Taarifa zilishatumwa kwa ndugu zake kuwa waje kumchukua nakujaribu kumpeleka kwa waganga wengine lakini hakukuwa na mwitikio wowote kutoka kwa ndugu zake.
“Nakufa… nakufa jamani, kabla sijafa nataka kuonana na mama yangu mzazi, Bi. Lubunga. Fanyeni kila mnachoweza nionane naye mapema…” aliongea mgonjwa ambaye kumbe alikuwa ni mtoto wa Bi. Lubunga, Isambi kutoka upande wa Tanzania. Ni huyu ndiye aliyekuwa baba mzazi wa Gamutu ingawa mwenyewe alishaaminishwa kuwa mkewe na mtoto wake walifariki.
Alipewa taarifa kupitia watu waliokuwa wanavuka ziwa kutoka upande wa Tanzania kuwa mkewe na mwanaye walifariki wakati wa kujifungua. Hilo lilikuwa ni pigo jingine kwake kwani tayari maradhi yaliyokuwa yanamsumbua yalimmaliza kabisa.
Alitaka kuonana na mama yake mzazi kabla hajafa. Alijua kamwe hawezi kupona kutokana na hali yake ilivyokuwa. Mwili wake ulikuwa umedhoofika sana, mbavu zilikuwa zinahesabika. Kwa kumtazama alikuwa anatisha na kutia huruma. Kitu pekee alichotaka ilikuwa ni kuonana na mama yake kabla hajafa.
***
Baada ya mvua kubwa iliyonyesha kwa saa nyingi mfululizo, hatimaye hali ya hewa ya ziwa Tanganyika ilianza kutulia. Zile pepo zilizokuwa zinavuma kwa kasi kutokea katikati ya ziwa zilitulia, wingu zito lililokuwa limetanda lilipungua na sasa mapambazuko yalianza kuonekana upande wa mashariki wa ziwa Tanganyika. Bi. Lubunga alikuwa ameshikilia mkungu wa ndizi kwa masaa mengi, hali iliyosababisha mikono yake ianze kufa ganzi.
Maji ya ziwa yaliyokuwa na baridi kali kutokana na mvua kubwa iliyonyesha tangu usiku, yaliifanya miili ya Bi. Lubunga na mjukuu wake Gamutu ife ganzi. Walikuwa wakitetemeka kutokana na baridi kali. Wakati wakielea ziwani, bila kutambua upande waliokuwepo, kwa mbali walianza kusikia muungurumo wa boti ikija upande wao.
Bi. Lubunga aliinua mkono mmoja juu, akajivua kitambaa alichokuwa amejifunga kichwani na kuanza kukipunga huku akiita kwa nguvu. Boti ya uvuvi kutoka mji wa Kalemie, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuwa ikirejea kutoka ziwani ilikokuwa ikifanya kazi ya uvuvi usiku kucha.
Ile boti ilipowakaribia mahali Bi. Lubunga na Gamutu walipokuwepo, ilipunguza mwendo baada ya wavuvi kuona vitu mfano wa binadamu ziwani. Boti iligeuza mwelekeo na kuanza kumulika kule Bi. Lubunga alikokuwa na mjukuu wake.
“Tusaidieni jamani, tunakufa! Msaada!” Bi Lubunga alizidi kupunga mkono hewani huku akipiga mayowe ya kuomba msaada.
Ile boti ilisogea karibu yao, wazamiaji wawili wakiwa na maboya wakarukia majini na kuanza kuwafuata Bi. Lubunga na mjukuu wake.
Muda mfupi baadaye walifanikiwa kuwaokoa na kuwaingiza ndani ya boti yao.
“Huyu mtoto yuko salama kweli? Mbona haoneshi kama bado anapumua,” alihoji mmoja kati ya wale wavuvi.
Kauli ile ilimshtua Bi. Lubunga, akaanza kumchunguza vizuri mapigo ya moyo wake.
Alimgusa kifuani lakini mapigo yalikuwa yanasikika kwa mbali sana, hali iliyomfanya achanganyikiwe. Wale wavuvi wakamtuliza na kumweleza kuwa ni kwa sababu ya baridi ya ziwani ndiyo maana mapigo ya moyo ya mjukuu wake yalikuwa chini kiasi kile.
“Mpelekeni vyumba vya juu, kisha mfunikeni kwa nguo nzito, mwili ukipata joto kidogo atatulia,” alisema kiongozi wa wale wavuvi.
Kilichofuatia ikawa ni utekelezaji. Gamutu alipandishwa kwenye vyumba vya juu vya ile boti ya wavuvi, akalazwa mahali pakavu, akafunikwa kwa mablanketi mazito.
Baada ya dakika kadhaa, mapigo ya moyo ya Gamutu yalianza kurudi kwenye hali yake ya kawaida. Bi Lubunga aliyekuwa amekaa pembeni akiwa amejishika tama na kujiinamia, aliruka juu kwa furaha baada ya kuona mjukuu wake amefumbua macho na ameanza kuchangamka.
Safari iliendelea ziwani na alfajiri na mapema wakawa tayari kwenye Ufukwe wa Kalemie, upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wale wavuvi waliwasaidia kushuka na kuwapeleka mpaka nchi kavu, wakawakabidhi kwa wavuvi wenzao walioahidi kuwafikisha mpaka mahali walikokuwa wanaenda.
“Tuna mgonjwa wetu kwa mganga Dongola, yule mzee maarufu anayesifika kwa kutibu magonjwa yaliyoshindikana. Nilimleta siku nyingi zilizopita lakini tumeletewa taarifa kuwa hali yake siyo nzuri,” alijieleza Bi. Lubunga kwa wale wavuvi. Haikumuwia vigumu kwani mganga yule alikuwa akifahamika sana katika mwambao wa Ziwa Tanganyika.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bi. Lubunga na mjukuu wake Gamutu wakapakizwa kwenye baiskeli na safari ya kuelekea kijijini kwa mganga Dongola ikaanza. Walipita misitu mikubwa na mapori ya kutisha. Bi. Lubunga hakushangaa kwani alikuwa na uzoefu na safari za Kongo.
Kitu pekee alichokuwa anakiombea moyoni ni kutokutana na waasi waliokuwa wanaushikilia mwambao wa Kalemie kwani alijua watakwamisha safari ile napengine kuwapiga risasi na mjukuu wake. Misukosuko aliyoipata ziwani hadi alipookolewa na wavuvi, ilimfanya Bi. Lubunga awe sugu. Wakazidi kuchanja mbuga na hatimaye wakawasili kijijini anakoishi Mganga Dongola na wasaidizi wake.
Yule mvuvi aliyewapeleka aliwafikisha jirani na nyumba ya mganga yule kisha yeye akarejea ziwani. Kwa mbali Bi. Lubunga akaona watu wakiwa wameizunguka nyumba ya mganga.
Alijikuta moyo ukimlipuka paaah! Kwa jinsi hali ilivyoonesha kulikuwa na tatizo.
Waganga mashuhuri watatu waliokuwa wanasifika katika ukanda wote wa mwambao wa Ziwa Tanganyika walikuwa wamekizunguka kitanda cha mgonjwa aliyekuwa katika hali mbaya wakiongozwa na mkuu wao, Dongola. Ilivyoonesha, mgonjwa alikuwa katika hatua za mwisho za uhai wake na ni kama alikuwa anapambana na malaika mtoa roho.
Waganga walikuwa wakiendelea kumfanyia tiba za kienyeji kwa kipindi cha miezi kadhaa lakini kila siku hali yake ilizidi kuwa mbaya kadiri siku zilivyosonga mbele. Licha ya kujaribu karibu mitishamba yote iliyokuwa inapatikana katika misitu ya Kongo, bado hali ya mgonjwa ilikuwa mbaya kiasi cha kuwakatisha tamaa.
Hakukuwa na matumaini ya mgonjwa kupona, kilichokuwa kinasubiriwa ilikuwa ni hitimisho tu na tayari wazee wa kijiji kile, kwa heshima ya Dongola walishaanza kujadiliana nje ya nyumba ile juu ya nini cha kufanya ikitokea mgonjwa yule akifa. Hakuna ndugu yake wa karibu aliyekuwa anafahamika zaidi ya mwanamke mzee aliyempeleka pale.
“Nakufa! Nakufa Isambi mimi! Niitieni mama yangu Lubunga!” Yalikuwa ni maneno yaliyomtoka mgonjwa karibu kila siku. Alikuwa ni Isambi, mtoto pekee wa Bi. Lubunga kutoka upande wa Tanzania akiwa katika siku za mwisho za uhai wake.
Ni Bi. Lubunga ndiye aliyempeleka mwanaye kwa waganga wa kienyeji huko Kongo baada ya kushindwa kupata tiba ya maradhi yake upande wa Tanzania.
“Isambii! Isambiii! Amka mwanangu, mama yako nimekuja, nimekuletea zawadi nzuri sana!” aliongea Bi. Lubunga kwa sauti ya juu baada ya kuwasogelea wale watu waliokuwa nje ya nyumba ya mganga na kubaini kuwa kumbe walikuwa wamemzunguka mwanaye Isambi, aliyekuwa akihangaika kupambana na malaika mtoa roho.
Sauti ya mama yake ilimfanya Isambi awe kama anaota. Alishtuka na kukaa juu ya kitanda, hali iliyowashangaza hata wale waganga. Kwa miezi kadhaa, Isambi hakuwa na uwezo hata wa kugeuka mwenyewe kitandani bila kusaidiwa, lakini baada ya mama yake kuwasili na kumsemesha aliweza kukaa mwenyewe huku tabasamu lake lililopotea likirudi kwa mbali.
Mwili wake ulikuwa umedhoofika sana, mbavu zilikuwa zinahesabika, sura ilibakia mifupa mitupu huku shingo na mikono vikiwa vyembamba kiasi cha kutisha.
Ungemtazama kwa haraka ungeweza kudhani ameathirika kwa ugonjwa wa kisasa, lakini haikuwa hivyo.
Bi. Lubunga alimkumbatia kwa nguvu huku machozi yakimbubujika kama chemchemi. Hakuamini kama mwanaye anaweza kuwa katika hali kama ile licha ya kujitahidi hadi kumfikisha pale.
“Huyo mgongoni ni nani?” aliuliza Isambi kwa sauti ya kukosa matumaini.
“Hii ndiyo zawadi niliyokuletea! Anaitwa Gamutu!” Aliongea Bi. Lubunga huku akimfungua Gamutu kutoka mgongoni, akamuweka mikononi mwa mwanaye na kuanza kumueleza kuwa huyo ndiye mtoto aliyemwacha tumboni mwa mkewe kabla hajasafirishwa na kupelekwa kule kwa waganga.
“Mbona amekuwa haraka namna hii! Au unanitania?” Aliongea Isambi huku akimsogeza vizuri Gamutu na kuanza kumtazama kwa makini usoni.
Alijikuta akiachia tabasamu hafifu baada ya kuona alikuwa akifanana naye kwa vitu vingi. Alimsogeza karibu yake na kumpiga busu kwenye paji lake la uso, akamshika sikio moja na kuanza kumuongelesha maneno fulani ambayo hakuna aliyeyasikia wala kuyaelewa.
Alifanya vile kwa dakika karibu tatu nzima, kisha akamuachia. Bi. Lubunga hakutaka kumpa taarifa kuwa mtoto yule alizaliwa kwa matatizo makubwa hadi kusababisha kifo cha mama yake (Mke wa Isambi). Alijua kwa hali aliyokuwa nayo, kumpa taarifa kama zile ilikuwa ni sawa na kumsogeza jirani na kifo.
Isambi aliingiza mkono chini ya kitanda alichokuwa amelazwa juu yake, akatoa kitu kama mkufu wa rangi nyeusi, akatoa na pete ya shaba, akamshikisha Gamutu mkononi huku akisema maneno ambayo hakuna aliyeyaelewa. Baada ya kukabidhiwa vitu vile, Gamutu aliving’ang’ania mkononi na ghafla akaanza kupiga kelele kwa sauti ya juu. Alishuka kitandani na kumkimbilia bibi yake huku akiwa bado ameshikilia vile vitu alivyokabidhiwa na baba yake.
“Naomba maji ya kunywa!” Alisema Isambi kwa sauti kavu, wale waganga wakazuia asipewe kwani kuna dalili mbaya walishaziona.
“Naomba maji ya kunywa jamani, nakufa kwa kiu!” Bado hakuna aliyekubali kumpa na badala yake wakatoa wazo kuwa awekewe maji kwenye kata kisha apewe Gamutu ndiyo amkabidhi. Kweli walifanya hivyo, alipoyanywa tu yale maji kwenye kata, akajinyoosha taratibu na kulala kama alivyokuwa amelala mwanzo, akatulia tuli. Pumzi zake zilikuwa zimefika ukingoni na moyo ukasimama kufanya kazi, alikuwa amekufa.
HatimayeBi Lubunga na mjukuu wake Gamutu wanafanikiwa kufika kijijini Kalemie, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alikopelekwa mtoto wake wa pekee, Isambi kupatiwa tiba kwa waganga wa kienyeji. Kitendo cha Bi Lubunga na mjukuu wake kuwasili ilikuwa ni kama wanamruhusu Isambi aianze safari yake, kwani muda mfupi baadaye alikata roho na kumkabidhi mkufu mweusi na pete ya shaba mwanaye Gamutu. Upande wa pili, baada ya miaka mingi kupita na Gamutu kuwa mkubwa, anaanza kutokewa na mambo ya ajabu baada ya kuvunja masharti aliyowekewa tangu akiwa mdogo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Naona alikuwa anamsubiri huyu mwanaye ndiyo akate roho, ametusumbua kwa kipindi cha wiki tatu mfululizo akitaka akuone wewe mama yake. “Yametimia, ila wasiwasi wangu ni huu mkufu mweusi na pete ya shaba, huyu mtoto amekabidhiwa bila kuandaliwa, inaweza kuja kumletea matatizo mbeleni.”
“Tutafanya nini sasa! Mjukuu wangu ndiyo atakuwa liwazo la moyo wangu, buriani mwanangu Isambi!” Aliongea Bi Lubunga huku akilia kwa uchungu.”
“Namna ya kumnusuru huyu mjukuu wako ni kumfanyia matambiko mawili akiwa mkubwa. Leo tutamfanyia dawa kidogo ya kuzuia tatizo lake la kuwasiliana na wachawi usiku wanaomchukua na kwenda kumfundisha mambo ya ajabu.
“La kwanza litakuwa ni tambiko la maisha, hili atafanyiwa akishakuwa na akili zake timamu na la pili ni tambiko la mapenzi, hili inabidi afanyiwe kabla hajaanza kuwajua wanawake. Hii ni muhimu kwani mizimu inaonesha alizaliwa katika laana,” aliongea mganga Dongola na Bi Lubunga akawa anamsikiliza kwa makini.
Baada ya hapo taratibu za mazishi zilianza kufanywa. Kwa kuzingatia umbali uliokuwepo hadi kwao Sumbawanga na ugumu wa safari ya ziwani, walikubaliana kuwa azikwe kule kule Kalemie, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mipango ikaanza kufanywa kwa haraka. Kwa umaarufu aliokuwa nao mganga Dongola, vijana wengi walijitokeza kwa ajili ya shughuli ya kuchimba kaburi.
Masaa kadhaa mbele, kaburi lililokuwa na urefu wa futi sita lilikamilika, Isambi akazikwa kwenye makaburi ya Kitongoji cha Kalemie, jirani na nyumba ya mganga Dongola.
Bi Lubunga na mjukuu wake walikaa pale nyumbani kwa mganga kwa siku moja, kesho yake wakasafirisha msiba hadi Sumbawanga.
Walipokelewa kwa huzuni kuu pale kijijini kwao kwani Isambi alikuwa akifahamika sana. Ndani ya kipindi kifupi, Gamutu alibakia yatima, akiwa hana baba wala mama. Bi Lubunga ndiyo akawa kila kitu kwake.
Baada ya kumaliza kabisa matanga ya mwanaye Isambi, Bi Lubunga aliendelea na maisha yake ya kawaida, huku suala la mahali alikotokea Gamutu likiendelea kuwa siri. Wengi waliamini kuwa ni mtoto wa ndugu yake aliyekuja kuishi naye. Hakuna aliyekuwa na taarifa kuwa Gamutu ni mtoto wa marehemu Isambi. Wote walijua kuwa mke wa Isambi alifariki wakati akipelekwa kujifungua na kichanga nacho kikafia tumboni.
***
MIAKA 17 BAADAYE
“Bibi mi nimeshasema siwezi tena kurudi kwa wale waganga, walinifanyia tambiko la kutisha sana, nikienda tena wanaweza kuniua.”
“Hapana Gamutu, wale lengo lao ni kukusaidia. Baba yako wakati anafariki alikuachia vitu vizito ambavyo kutokana na umri wako inabidi usaidiwe kwa kufanyiwa matambiko mawili. La kwanza ulishafanyiwa, la pili ilikuwa ufanyiwe hivi karibuni kabla ya kuruhusiwa kukutana na wasichana, kwa uzembe wako umemwingilia mtoto wa watu Sabina kabla hatujakukamilishia tambiko la pili. Hili ni tatizo kubwa.”
Bi Lubunga alikuwa akiongea kwa hisia baada ya kuona mjukuu wake amekiuka masharti aliyopewa. Kwa jinsi alivyoelekezwa, kukiuka moja kati ya masharti aliyowekewa kungeweza kumsababisha abadilike na kuwa jini. Bi Lubunga hakutaka kumwambia mjukuu wake nini ambacho kingempata zaidi ya kumsisitiza kuwa ni hatari sana.
Kesho yake taarifa zilisambaa shule nzima kuwa Gamutu alifanya mapenzi na mwanafunzi mwenzake aitwaye Sabina, tena akiwa kwenye siku zake baada ya kuvunja ungo kwa mara ya kwanza akiwa shuleni na Gamutu kujifanya anatoa msaada kwake. Hakuna aliyejua kuwa, mbali na kumwingilia kimwili bila ridhaa yake, pia alimnyonya damu na kuihifadhi kwenye chupa ndogo.
“Hee nyie, mbona maajabu! Sijawahi kumsikia Gamutu hata mara moja akizungumzia stori za wasichana, lakini eti leo ametembea na Sabina! Mi siamini!”
“Kama huamini shauri yako, wenzako tumeona mpaka mahali walipofanyia, pametapakaa damu kama machinjioni.”
“Kwani ilikuwaje”
“Sabina alikuwa analalamika tumbo linamuuma, tulipoenda mapumziko walibaki darasani na Gamutu. Tuliporudi tukakuta wamekaa kiti kimoja. Hata wakati wa kuondoka walisubiri wanafunzi wote waondoke ndiyo na wao wakaondoka, tena walipitia njia ya kule vichakani.”
“Ndiyo maana leo hawajaja shule wote wawili! Mwalimu mkuu akijua atawafukuza shule.”
Kitendo alichokifanya Gamutu kwa mwanafunzi mwenzake kilikuwa gumzo shule nzima. Taarifa zilisambaa kwa haraka miongoni mwa wanafunzi. Kila mtu akawa anawazungumzia wao. Licha ya taarifa hizo kuzagaa, hazikufika kwa walimu wao.
Gamutu mwenyewe baada ya kuona siri imevuja, hakutaka kukaa shuleni. Alisingizia anaumwa na hakwenda kwa siku tatu mfululizo, Sabina naye vivyo hivyo.
Kwa siku zote hizo, Bi Lubunga alikuwa akimbembeleza mjukuu wake warudi kwa waganga wa kienyeji haraka kwani alikuwa ameshaharibu mambo kwa kukutana na mwanamke kabla tambiko la mapenzi halijakamilika, lakini Gamutu alikuwa mbishi sana. Umri wa miaka 17 aliokuwa nao ulimfanya ajione tayari ni mtu mzima anayeweza kujiamulia mambo yake mwenyewe.
“Lakini ujue ukipatwa na matatizo utanisikitisha sana Gamutu! Wewe ndiyo mtu pekee ninayekutegemea. Lakini kwa nini hutaki kunisikiliza?”
“Bibi mi nimeshasema, huko kwa waganga wako mi’ siendi tena, siku ile walinitesa sana. Watanifukiaje kaburini na kunibebesha moto wakati bado niko hai,”
“Tambiko la pili ni jepesi, wala halitakuwa kama lile la kwanza. Jikaze mjukuu wangu twende. Ni tambiko la siku moja tu, wala hutalala makaburini tena kama siku ile.”
Licha ya kumbembeleza kwa kadri ya uwezo wake wote, bado Gamutu hakutaka kukubali.
Usiku wa siku ya tatu tangu Gamutu alipofanya dhambi ile ya kukutana kimwili na Sabina, alianza kutokewa na mambo ya ajabu usiku.
Usiku wa manane akiwa amelala kwenye chumba chake na Bi Lubunga akiwa kwenye chumba chake, ilisikika sauti ya mvumo wa upepo mkali.
Upepo ule ulidumu kwa dakika kadhaa na ukawa unapuliza kwa nguvu kuelekea kwenye chumba cha Gamutu. Mwenyewe akiwa usingizini alishtuka baada ya kusikia mlango wa chumba chake ukifunguliwa kwa nguvu. Alipoinua kichwa kuangalia ni nani aliyefungua mlango, hakuona chochote zaidi ya kukumbana na upepo mkali. Ghafla akashangaa mwanga mkali ukimmulika mwili mzima kutokea kule upepo ulikokuwa unatokea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akiwa bado haelewi nini cha kufanya, alishangaa kuona anashikwa mkono na mtu asiyeonekana, akaanza kuvutwa kupelekwa nje. Alijaribu kupiga mayowe ya kuomba msaada kwa bibi yake lakini sauti haikutoka.
Alivutwa mpaka nje, akawa anatapatapa huku na kule na kujaribu kujishikilia mlangoni bila mafanikio. Alipofikishwa nje, alijaribu kutazama ni nani anayemvuta lakini hakuona chochote zaidi ya vivuli vya watu wengi waliokuwa wanaonekana warefu kuliko kawaida.
Aliendelea kuburuzwa na kupelekwa kusikojulikana. Kutokana na hofu na woga aliokuwa nao, alijikuta mwili wote ukimwisha nguvu, kisha akapoteza fahamu. Hakuelewa kilichoendelea.
Bi Lubunga alishtuka usingizini baada ya kusikia upepo mkali ukivuma ghafla ndani mwake. Alichokifanya ilikuwa ni kukimbilia chumbani kwa mjukuu wake Gamutu kuona kama yuko salama, kwani kwa uzoefu aliokuwa nao, upepo ule ulimaanisha jambo.
Katika hali ambayo hakuitegemea, hakumkuta Gamutu chumbani, akajua mambo yameanza. Kwa haraka alitoka mpaka nje, hakumkuta yeyote zaidi ya kuona alama ya kitu kilichokuwa kinaburuzwa ardhini.
Akarudi ndani haraka, akachota chumvi nyingi kwenye kopo dogo na kukimbilia jikoni, lengo lake likiwa ni kwenda kuichoma motoni.
Kwa imani za kwao, unapotokewa na mauzauza yanayoashiria uchawi hasa nyakati za usiku, dawa ya kwanza ilikuwa ni kuchoma chumvi motoni.
Kama uchawi husika ulikuwa unahusisha majini, moshi wa chumvi uliaminika kwenda kuwamaliza nguvu na kuwazuia kufanya walichotaka kukifanya. Alipofika jikoni mbiombio, aligundua kuwa tayari moto ulikuwa umezima.
Akashusha pumzi ndefu kwa ishara ya kukata tamaa. Aliumiza kichwa tena juu ya nini cha kufanya ili kumwokoa mjukuu wake. Alipata wazo, alirudi haraka chumbani kwake na kuchukua ubani uliokuwa kwenye kitezo, chini ya kitanda. Alitaka kuuwasha ili kuvunja nguvu zote za uchawi eneo lile, lakini bado kikwazo kikawa kilekile, hakukuwa na moto. Alijikuta akiishiwa nguvu.
Katika hali ya kuchanganyikiwa, Bi Lubunga alitoka na kuanza kukimbia ovyo kufuata alama zile za kitu kilichokuwa kinaburuzwa ardhini. Alikimbia umbali mrefu lakini hakuona chochote zaidi ya zile alama ambazo zilikuwa zinazidi kutokomea porini. Alizidi kuchanganyikiwa.
***
“Tumekuchagua kwa kuwa tumeona unaweza kuziba pengo lililoachwa miaka mingi na marehemu baba yako, Isambi. Uko tayari kushirikiana na sisi?”
“Kwani nyie ni akina nani? Siwezi kushirikiana na watu nisiowajua wala nisiowaona.”
Gamutu alikuwa akizungumza ndani ya pango kubwa ambalo hakujua aliingiaje. Aliokuwa akizungumza nao walikuwa hawaonekani zaidi ya kusikia sauti za kutisha zilizokuwa zikiambatana na mwanga na ngurumo kali kama za radi.
Hakukumbuka alifikaje mahali pale. Kitu pekee alichokumbuka ni kwamba mara ya mwisho alikuwa chumbani kwake amelala, akashangaa upepo mkali unavuma na ghafla akashikwa mkono na mtu asiyeonekana. Akaanza kuburuzwa kutolewa nje kabla ya kupoteza fahamu akiwa bado anaburuzwa.
“Unataka kutujua? Njoo huku! Iliongea sauti kama ile ya kwanza, akajikuta akiushikwa tena mkono na kutolewa nje. Safari hii hakuburuzwa, alitembea mwenyewe lakini mkono wake ulikuwa umeshikwa kwa nguvu. Akazungushwa mpaka nyuma ya pango lile.
“Nawa kichwa chako na uso kwenye haya maji!” Aliamrishwa na sauti ile ya mtu asiyeonekana. Bila ubishi akatii amri. Akainama kando ya mfereji uliokuwa unapitisha maji mengi kwa kasi. Kwa kutumia mikono yake miwili, akaanza kunawa kichwa na uso. Katika hali isiyotegemewa, alishangaa mandhari ya eneo alilokuwepo yakibadilika ghafla.
Ule ambao awali aliuona kama mfereji, ulibadilika na kuwa mto mkubwa, lile aliloona kama ni pango lilibadilika na kuwa kasri kubwa mithili ya makazi ya mfalme. Alishangaa kuona kumbe kulikuwa na watu wengi sana eneo lile waliokuwa wakiendelea na shughuli zao.
Baadhi walikuwa wakifanya usafi huku wengine wakiandaa kitu kama chakula. Wote walikuwa wamevaa mavazi meupe tofauti na binadamu wengine aliozoea kuwaona, hawa walionekana kuwa warefu zaidi.
Mabadiliko yale ya ghafla yalimfanya abaki kama zezeta. Kuna wakati alihisi anaota, akajifikicha macho lakini hakuzinduka, akajua ni kweli. Akiwa bado amepigwa na bumbuwazi, akashikwa begani kutokea nyuma, akasikia amri ikitolewa:
“Si umeshanawa uso na kichwa? Nifuate.”
Alipogeuka alimuona mwanaume mrefu akiwa amevalia mavazi meupe, akaanza kumuongoza mahali pa kuelekea. Alimrudisha uelekeo ule ule aliokuja nao, wakafika kwenye lango kubwa ambapo kulikuwa na watu wengine wengi waliofanana kwa kila kitu na yule aliyekuwa anamwongoza.
“Kwani hapa ni wapi?”
“Mwanzo ulisema unataka kutujua, kabla hata hujapata jibu la swali lako, tayari unaulizwa swali lingine, sikiliza! Lazima ujifunze kukaa kimya wakati mambo yanatendeka, vinginevyo utageuzwa kitoweo, si unaona wenzako wote wako kimya? Tena huko ninakokupeleka ndiyo hatari zaidi.”
“Basi kama ndiyo hivyo nirudisheni mlikonichukua, nirudisheni kwa bibi yangu.”
“Hakuna atakayekurudisha, utabaki huku hadi mwisho wa maisha yako. Unaonekana kuwa na uwezo mkubwa sana utakaotusaidia sisi majini na binadamu wenzako.”
“Haaa! Ina maana wewe ni jini?”
“Siyo mimi tu, hawa wote unaowaona ni kama mimi, hebu angalia,”
Aliongea mtu yule na kufunua joho jeupe alilokuwa amevaa na kuonesha miguu yake…”
“Mungu wangu?” Aliongea Gamutu kwa sauti kubwa baada ya kuona kitu cha ajabu miguuni mwa yule mtu, hali iliyowafanya wengine waliokuwa pembeni wakiendelea na kazi zao kusimama na kuanza kumwangalia Gamutu. Neno ‘Mungu wangu’ alilolitamka ndilo lililovuta usikivu wa wengi.”
“Kwani na nyie binadamu mnamjua Mungu?” Alihoji yule kiumbe ambaye sasa Gamutu alitambua kuwa ni jini. Wakati akiwa bado hajajibiwa swali lake, ilisikika sauti kali ambayo Gamutu aliifananisha na adhana anayoisikia msikitini. Tofauti ilikuwa ni lugha iliyotumika, Gamutu hakuelewa kitu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya adhana ile, alishangaa kuona wale viumbe wote wakikimbilia mtoni na kuanza kufanya kitu kama kuchukua udhu, ingawa hakuwa na uhakika. Baada ya hapo aliona wote wakiinamisha vichwa vyao na kujishika mikono kwa mbele, wakaanza kuingia ndani ya lile jumba kubwa. Yule kiumbe aliyekuwa amesimama na Gamutu alimwamuru na yeye kufanya kama wenzake lakini Gamutu akakaidi.
Sekunde chache baadaye wale viumbe wote walikuwa wameingia ndani ya lile jumba kubwa, Gamutu akabaki peke yake pale nje. Akiwa amesimama wima, alisikia sauti kama ya bibi yake akimuita kutokea ng’ambo ya ule mto. Alijaribu kupepesa macho huku na kule lakini hakumuona. Sauti ilizidi kusikika na sasa akawa anapewa maelekezo kuwa aingie ndani ya ule mto na kuvuka ng’ambo ya pili.
Wakati akishuhudia mambo yale ya miujiza, Gamutu alisikia sauti ya bibi yake, Lubunga kutokea upande wa pili wa ule mfereji ambao ulibadilika na kuonekana kama mto mkubwa. Alijaribu kukodoa macho akiamini atamuona bibi yake lakini wapi!
Kwa muda huo, wale watu wa ajabu wote walikuwa wanaendelea kusali kwa namna ambayo Gamutu hakuwahi kuiona. Walikuwa wakisimama na kuinama kwa pamoja, kisha kurukuu na baadaye kurudi kama walivyokuwa awali. Alishindwa kuelewa nini cha kufanya kwani ile sauti ya bibi yake ilikuwa ikiendelea kusikika ikimuita.
Akiwa katika hali ile, alishangaa anashikwa mkono na mtu ambaye hakumtambua mara moja, akaanza kuvutwa kuelekea kule kwenye ule mfereji. Alijaribu kumtazama vizuri aliyekuwa anamvuta lakini hakumtambua zaidi ya kumuona kama kivuli.
Walipoufikia ule mfereji ambao sasa ulikuwa unaonekana kama mto mkubwa, yule mtu alimtangulia kuingia kwenye maji, akawa anamvuta. Woga ulimzidi kwa kudhani huenda wangesombwa na maji ya mto ule ambayo yalikuwa yakipita kwa kasi, lakini yule mtu akampa ishara kwamba asiogope. Walipofika kwenye kina kirefu, Gamutu alishangaa yale maji yakibadilika rangi na kuwa mekundu kama damu. Hofu ilimzidi lakini yule mtu akazidi kumvuta.
Dakika kadhaa baadaye wakawa tayari wameshavuka mpaka ng’ambo ya pili.
“Kwa nini nilikuwa nakuita lakini unakataa?”
“Sikukataa, nilikuwa nashindwa kuvuka?”
Ni hapo ndipo Gamutu alipotambua kuwa kumbe yule aliyekuwa amemshika na kumvusha kwenye ule mto alikuwa ni bibi yake, Lubunga.
“Hee bibi! Kumbe ni wewe? Umefikaje na ulijuaje kuwa nimeletwa huku?”
Maswali mengi tutaenda kuulizana nyumbani, hapa cha msingi ni kuwahi kuondoka eneo hili kabla hawajamaliza kusali.”
“Wakina nani?”
“Kwani wale uliokuwa nao ni kina nani?”
“Mi sijui lolote, ila nilishangaa kuona hawana miguu kama tuliyonayo sisi, wao chini wana kwato kama za punda.”
“Wale ni majini, tuondoke haraka hapa maana wakimaliza kusali lazima wataanza kukutafuta.”
Bi. Lubunga na Gamutu walianza kukimbia kutokomea gizani. Walikimbia kwa umbali mrefu, wakawa wanakatiza vichaka namapori ya kutisha. Kilichowasaidia kulikuwa na mbalamwezi iliyowaangazia njia.
“Umeona faida ya ubishi? Nilikwambia twende nikupeleke kwa waganga wakumalizie tambiko la pili mapema ukawa unakataa, matokeo yake ndiyo hayo.”
“Sasa kwani mimi nimewakosea nini mpaka waje kunichukua nyumbani wakati nimelala?”
“Hilo siyo la kuuliza, nilishakwambia ukikosea masharti uliyopewa utapatwa na matatizo makubwa na huenda ukabadilika na kuwa jini.”
“Nibadilike na kuwa jini? Mbona sikuelewi?”
“Mpaka yakutokee ndipo utakapoelewa namaanisha nini,” Gamutu na bibi yake walikuwa wakiongea wakati wakikatiza vichaka kuelekea kwao. Maneno aliyokuwa anaambiwa na bibi yake sasa yalianza kumuingia kichwani kwani mwanzoni alikuwa anaona kama uzushi.
“Sasa bibi, nifanye nini ili yasinitokee haya, mi nimeanza kuogopa!”
“Hakuna njia nyingine zaidi ya kurudi kwa wale waganga wakakumalizie tambiko la pili?”
Wakati wakiongea hayo, walishangaa kuona wanamulikwa na mwanga mkali kama wa radi kutokea kwenye mti mkubwa uliokuwa mbele yao.
“Simameni hivyohivyo!” Sauti kali ilisikika ikiwaamrisha kutokea kwenye mti mkubwa uliokuwa mbele yao. Gamutu alijificha nyuma ya mgongo wa bibi yake huku akitetemeka kwa hofu kuu.
Katika hali ambayo hakuelewa, bibi yake alianza kuzungumza kwa lugha asiyoielewa akiongea na yule mtu aliyewapa amri ile ya kusimama. Kila alilokuwa akiongea bibi yake, upande wa pili nao ulikuwa ukijibu, hakuelewa wanazungumza nini kwani lugha ile ilikuwa ngeni kabisa kwake. Kitu pekee alichokielewa ni pale aliposikia ile sauti ikilitaja jina lake.
Mazungumzo kati ya bibi yake na yule kiumbe ambaye alikuwa haonekani kwa macho yaliendelea kwa dakika kadhaa. Ilivyoonekana walikuwa wakibishana jambo kwani alimshuhudia bibi yake akiongea kwa ukali na msisitizo huku akimshika vizuri Gamutu.
Kufumba na kufumbua Gamutu alishangaa wakimulikwa tena na mwanga mkali kisha bibi yake akadondoka chini kama mzigo, Puuuh!
Alijaribu kumuinua huku akimtingisha bila mafanikio, akashangaa akishikwa tena mkono kama ilivyokuwa awali alipochukuliwa chumbani kwake akiwa amelala.
Alichokiona ni mkono wenye manyoya mengi na kivuli kirefu, akawa anavutwa kurudi kule alikokuja kuokolewa na bibi yake. Safari haikuwa ngumu kama wakati wanatoroka kwani sekunde kadhaa Gamutu alishangaa kuona tayari wameshaufikia ule mto wenye maji yanayobadilika. Safari hii hawakuvuka kwa kuingia kwenye maji bali alishangaa akinyanyuliwa juu juu na kurushwa hadi ng’ambo ya pili.
Akadakwa na kuanza kupelekwa ndani. Miujiza aliyokuwa anaiona ilimfanya ashindwe kustahimili, akajikuta fahamu zikianza kumtoka taratibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa nini ulitaka kutoroka? Wewe ni wa hukuhuku, duniani hakukufai kwani nyota yako inaonesha wewe siyo binadamu wa kawaida. Unatakiwa kusahau kila kitu ulichokiacha ulikotoka na kuanza maisha mapya ndani ya himaya hii,” alisikia sauti kama ile ya kiumbe aliyekuwa anabishana na bibi yake kule porini. Wakati anaambiwa haya, alikuwa katika hali ambayo mwenyewe alihisi kama ni ndotoni. Alijifikicha macho lakini wapi, fahamu zikawa zinazidi kumtoka, akadondoka chini na kulala kifudifudi.
Kulipopambazuka, Bi Lubunga alishtuka na kujikuta akiwa msituni. Alijishangaa kwani awali jioni ya siku hiyo alilala akiwa nyumbani kwake pamoja na mjukuu wake Gamutu. Cha ajabu alijikuta akirejewa na fahamu eneo ambalo Gamutu alizaliwa… mahali yalipomfika mauti mama yake mzazi… siku alipozaliwa.
Pumzi zilikuwa zikimwenda mbio kwa sababu katika siku zote za maisha yake hakuwahi kukutana na mambo kama yale. Yaani alale nyumbani kwake usiku halafu ajikute anaamkia porini… haikuwahi kutokea. Kwa kasi ya ajabu aliinuka na kuanza kusonga mbele.
Alitembea kwa haraka hadi alipofika nyumbani kwake. Kitu cha kwanza kukigundua ni kukuta mlango mkubwa ukiwa wazi. Alipitiliza hadi chumbani alikokuwa amelala mjukuu wake Gamutu, chumba kilikuwa kitupu. Ni hapo ndipo kumbukumbu zilipoanza kumrudia na kukumbuka matukio ya ajabu yaliyotokea usiku uliopita.
Alikumbuka jinsi nyumba yake ilivyoanza kupigwa na upepo mkali, akakumbuka jinsi mjukuu wake alivyochukuliwa kimazingara hadi alipokwenda kumuokoa kutoka mikononi mwa majini. Alikumbuka pia jinsi walivyokamatwa tena wakiwa porini, hakukumbuka kilichoendelea zaidi ya hapo.
Alikaa chini na kuegemea ukuta wa nyumba yake, akiwa haamini kama kweli Gamutu ametoweka katika mazingira ya kutatanisha. Alijaribu kutazama chanzo cha matatizo yale… akashusha pumzi ndefu baada ya kukumbuka jambo ambalo kimsingi ndiyo lilikuwa chanzo.
Alikumbuka miaka mingi iliyopita, jinsi marehemu mwanaye, Isambi ambaye ndiye baba mzazi wa Gamutu, alivyohangaika kwa kipindi kirefu kutokana na tatizo lililokuwa likimkabili yeye na mkewe la kukosa mtoto. Marehemu Isambi na mkewe waliishi kwa kipindi kirefu bila kupata mtoto, jambo lililosababisha matatizo makubwa katika ndoa yao.
Ili kuokoa jahazi, Bi Lubunga aliamua kumpeleka mwanaye na mkewe kwa waganga wa kienyeji, ambako walifanyiwa tiba za asili zilizohusisha matumizi ya nguvu za kishirikina hadi mkewe akapata ujauzito. Ni ujauzito huo uliopatikana kwa waganga wa kienyeji ndiyo uliomleta duniani Gamutu. Sijui ni kwa kukiuka masharti au kitu gani, lakini ujauzito huo ulipofikisha miezi saba, mikosi ikaanza kuwaandama.
Isambi alianza kuugua magonjwa yasiyoeleweka huku mke wake akiota ndoto za mauzauza kila siku. Alikuwa akilalamika kuwa mtoto alikuwa hatulii tumboni, siyo usiku wala mchana. Mikosi iliendelea hadi kufikia Isambi kuwa hoi bin taaban.
Walizunguka kwa waganga kadhaa kujaribu kumtibu bila mafanikio. Mwishowe mama yake (Bi Lubunga ) akaamua kumsafirisha hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwenye mji mdogo wa Kalemie. Alikumbwa na mauti akiwa huko na mazishi yakafanyika kwenye makaburi ya Kalemie.
Mkewe naye alipoteza maisha wakati wa kujifungua.
Kumbukumbu zake zilimuonesha kuwa lazima tatizo lilianzia pale alipowapeleka kwa waganga kwa ajili ya tatizo la kutopata mtoto. Madawa yaliyotumika aliamini ndiyo chanzo cha yote yale. Akiwa bado anakumbuka, alijikuta akipitiwa na usingizi mzito palepale chini alipokuwa amekaa.
***
Akiwa amelala kifudifudi, Gamutu alirudiwa na fahamu zake na kujikuta yuko katikati ya watu wengi wenye sura za kung’aa na macho mekundu. Kila mmoja alikuwa kimya akimtazama usoni. Alipozinduka almanusra atimue mbio lakini akajikuta akirudishwa chini vilevile alivyokuwa, akapewa amri ya kutulia. Gamutu aliendelea kushangaa mazingira yale aliyokuwepo akiwa haamini kama ni kweli au yuko ndotoni.
“Wewe ni wa hukuhuku, duniani hakukufai kwani nyota yako inaonesha wewe siyo binadamu wa kawaida. Unatakiwa kusahau kila kitu ulichokiacha ulikotoka na kuanza maisha mapya ndani ya himaya hii…” maneno yale aliyoambiwa punde alipoingizwa mle ndani yalikuwa yakijirudiarudia kichwani mwake kama mkanda wa video ya kutisha.
Mwili mzima ulikuwa ukimtetemeka akiwa hajui nini hatima yake. Muda mfupi baadaye, akiwa bado katika hali ya kutaharuki, alikuja mwanaume mzee ambaye kichwa chake kilikuwa kimejaa mvi nyingi. Alipokaribia eneo lile Gamutu alipokuwa amelazwa, wale watu wa ajabu waliokuwa wamemzunguka waliinamisha vichwa vyao na kusujudu chini, kisha wakainuka na kutawanyika wakimuacha peke yake na Gamutu.
Alimsogelea mpaka pale alipokuwa amelala na kuanza kuzungumza naye kwa sauti kubwa ya kutisha iliyokuwa inatoka kama muungurumo wa radi.
“Kijana usiogope, haya ndiyo yatakuwa makazi yako mapya. Utaishi nasi na kushirikiana na wenzako kwa kila kitu. Ukizoea utapangiwa majukumu mengine, lakini kwa sasa nakukabidhi kwa mwenyeji wako atakayekuwa nawe kwa siku zote utakazokuwa nasi,” aliongea yule mzee kwa sauti ya kutisha, kisha akainua kidole cha shahada juu, kwa haraka akatokea msichana mrembo kutoka nyuma yake, akaja kwa kasi na kusujudu mbele yake na Gamutu.
“Huyu ndiyo atakayekuongoza kwa siku zote za maisha yako utakazokuwa nasi,” alisema huku akimtambulisha yule msichana kwa Gamutu, kisha akaaga na kutoweka ghafla kama upepo. Gamutu akawa anamtazama yule msichana kwa hofu… alianza kwa kumtazama miguuni akitegemea kukutana na kwato kama ilivyokuwa kwa wale watu waliokuwa wamemzunguka muda mfupi uliopita.
Tofauti na wengine, yeye hakuwa na kwato bali miguu ya kawaida kama binadamu wengine.
“Karibu kwenye makao mapya…” aliongea yule msichana kwa sauti laini ya kike huku akiachia tabasamu pana usoni kwake. Gamutu alikuwa kama asiyeamini kinachoendelea, yule msichana akamuinamia pale alipokuwa amelala kifudifudi na kumshika kichwani, akawa anakipapasa kichwa chake na mikono yake laini huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni.
“Unaitwa nani?”
“Gamutu! Kwani hapa ni wapi?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Usiwe na haraka, nitakuelekeza kila kitu. Nimekabidhiwa niwe mwenyeji wako, inuka twende kule bustanini nikakuoneshe mazingira ya hapa,” aliongea yule msichana na kumshika Gamutu mkono, akamvuta na kumuinua. Wakaanza kuondoka eneo lile kuelekea nje kupitia lango la nyuma kulikokuwa na bustani kubwa ya kupendeza.
“Nataka kurudi kwa bibi yangu! Naogopa kila kitu kilichopo hapa!”
“Hee! We wa ajabu kweli, wenzio wote wanaoletwa huku huwa hawatamani kurudi tena walikotoka. Hata mimi nilipoletwa mara ya kwanza niliogopa lakini nilipozoea sitamani kuondoka kwani napata kila ninachokitaka ndani ya muda mfupi sana,” aliongea yule msichana wakati akimtembeza Gamutu kwenye bustani.
Walipofika mahali ambapo hapakuwa na mtu mwingine yeyote, yule msichana alisimama mbele ya Gamutu na kuanza kumwangalia kwa macho ambayo yalionesha ana jambo analotaka kumwambia.
Nimeishi maisha haya nikiwa jini huu ni mwaka wa saba sasa. Nakumbuka siku yangu ya mwisho kuishi duniani ilikuwa ni ile niliyopata ajali mbaya ya kudondoka kutoka kwenye mti wakati tukitafuta kuni na dada zangu. Tangu siku hiyo, niliporejewa na fahamu nilijikuta huku, nikaambiwa ile iliyonipata haikuwa ajali kama wengine walivyofikiria bali ulikuwa ni mpango maalum wa majini.
Tangu siku hiyo, maisha yangu yote yamekuwa hapa, na kwa kweli najisikia furaha na amani tofauti na maisha ya kibinadamu niliyokuwa naishi awali. Sitamani kabisa kuishi duniani.
Ila naomba nikuambie kitu kimoja ambacho ndiyo pekee kimekuwa kikinisumbua siku zote za maisha yangu ya huku,” aliongea yule msichana aliyepewa jukumu la kumpokea na kumzungusha kwenye makazi mapya Gamutu.
“Kitu gani hicho?” Gamutu alihoji baada ya kuona kweli jambo alilotaka kuambiwa na yule msichana ambaye baadaye alijitambulisha kuwa anaitwa fatiha.
‘Mapenzi”
“Una maana gani? Mbona sikuelewi?”
“Huku ujinini haturuhusiwi kufanya mapenzi na binadamu wa kawaida. Lazima tukutane sisi kwa sisi, hata hivyo majini wanavyokutana ni tofauti kabisa na binadamu wa kawaida.”
“Una maana gani? Mbona unazidi kunichanganya?”
“Sikia, majini hufanya mapenzi kwa hisia za kishirikina na wala huwa hawagusani kama binadamu. Inawezekana mmoja akawa nchi kavu mwingine akawa ng’ambo ya pili ya bahari lakini wakawa wanafanya mapenzi bila kujali umbali kati yao.”
“Hee! Makubwa… kwa hiyo na wewe uko hivyo?”
“Ukishaingia huku lazima utii maelekezo yote. Mkuu wetu ametutahadharisha kuwa tukikiuka masharti adhabu yake ni kubwa sana ila kwa mateso ninayoyapata niko tayari kwa lolote.”
“Kwa hiyo ulikuwa unataka mimi nikusaidie nini?”
“Kwa kuwa wewe ndiyo kwanza umeletwa huku na bado unasifa za binadamu, nilikuwa naomba tuwe tunakutana kimwili na kuridhishana kimapenzi bila mtu yeyote kujua.”
“Mhh! Unasema?” Gamutu alihoji tena kama hakusikia kile kilichozungumzwa na Fatiha. Alirudia kilekile alichokisema awali. Baada ya kuongea vile, alimkumbatia Gamutu kwa nguvu na kuanza kumfanyia vituko vya kimahaba. Licha ya kufanya yote hayo, akili ya Gamutu haiukuwepo kabisa mahali pale. Alikuwa akimfikirias bibi yake na jinsi alivyohamishwa kimazingara kutoka kwenye ulimwengu wa kawaida hadi ujinini.
Alikuwa akiwaza namna bibi yake anavyohangaika kumtafuta, akafikiria ataishi kule hadi lini kwani kila kitu kilikuwa kigeni kwake. Kitu pekee alichoona kinafaa ilikuwa ni kumtumia Fatiha kufahamu siri zote za kule na kutafuta namna ya kutoroka.
“Kwani wewe umeishi miaka mingapi huku?”
“Huu mwaka wa saba sasa, nimeona mengi na ninajua mengi, nafahamu siri zote za huku.”
“Kwa hiyo unafahamu hata namna ya kutoroka kurudi duniani?”
“Nafahamu ila kwa kuwa maisha ya huku nimeridhika nayo, na hakuna ninachokikosa zaidi ya mapenzi, sioni haja ya kurudi duniani.”
Kauli ile ya Fatiha iliamsha matumaini mapya kwa Gamutu. Alitambua fika kuwa, endapo atamtimizia Fatiha kile alichokuwa anakitaka, uhakika wa kurejea salama duniani ulikuwepo. Hakutaka kujivunga…
“Sasa umeshasema majini wanafanya mapenzi tofauti na binadamu, na wewe umeshakaa miaka saba huku, si umeshakuwa jini kama wengine?”
“Hebu niangalie miguu yangu! Unaona unafanana na majini wengine?”
Swali lile la Fatiha liliamsha shauku kubwa moyoni mwangu ya kutaka kujua kwa nini Fatiha hakuwa na kwato kama majini wengine aliowakuta kule.
Akazidi kumbana kwa maswali:
“Kwanini wewe uko tofauti na wengine?”
“Nina siri kubwa moyoni mwangu ambayo ndiyo inayonilinda na kunifanya nisibadilike na kuwa na miguu yenye kwato. Ukikubali kuwa wangu ipo siku nitakueleza.’
“mazungumzo yao yaliwachukua muda mrefu hadi giza lilipoanza kuingia. Wakainuka kutoka katikati ya bustani ya maua walikokuwa wamekaa, Fatiha akauzungusha mkono kiunoni kwa Gamutu na wakawa wanatembea kimahaba.
“Tukionekana tumeshikana hivi, yule mzee mkali si ataniadhibu?”
‘Wala usihofu, mimi ndiyo mwenyeji wako, fanya kile ninachokuelekeza na utakuwa salama,” aliongea Fatiha kwa kujiamini huku akimtazama Gamutu machoni. Japokuwa alikuwa na sura nzuri, macho yake yalitisha sana kwani yalikuwa mekundu sana na giza liingiapo yalikuwa yakiwaka kama ya paka. Hali ile ilimfanya Gamutu awe anamuogopa ingawa hakuonesha moja kwa moja.
Fatiha naye alitambua kuwa lazima Gamutu alikuwa na hofu kubwa, akawa anajitahidi kumfariji aone kila kitu kiko sawa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda mfupi baada ya kuondoka kule bustanini, walisikia sauti kama ya kengele na adhana vilivyokuwa vikisikika kwa wakati mmoja. Fatiha akamwambia kuwa muda wa kusali magharibi na kunywa kiburudisho chekundu ulikuwa umefika. Akamwambia Gamutu amfuate kule alikokuwa anaenda.
Aliongoza mpaka ndani ya lile jengo kubwa lililokuwa linaonekana kama makazi ya mfalme, likiwa limenakshiwa kwa vito vingi vya thamani. Walipoingia walikuta tayari majini wengine wengi wamejipanga mstari wakiwa wanasubiri maelekezo kutoka kwa mkuu wao.
Baada ya muda alishangaa kuona wote wakifunga sala na kuanza kusali kwa lugha ambayo Gamutu hakuielewa. Fatiha alikuwa pembeni yake na alikuwa akimuelekeza kila kitu cha kufanya.
Baada ya sala ile iliyodumu kwa takribani dakika thelathini, wote walitawanyika na kuanza kuelekea upande ambao kulikuwa na mapipa makubwa matatu yenye kinywaji chenye rangi nyekundu.
Kila mmoja akawa anachukua kikombe mfano wa kibuyu na kukinga kisha kuanza kunywa. Fatiha alimkonyeza Gamutu kuwa wakifika pale nayeye achukue kikombe chake lakini asinywe kwani ile ni damu ya watu.
“Kauli ile ilimshtua Gamutu na kumfanya mwili wote uanze kutetemeka; mapipa matatu ya damu za watu, wameyapataje?” Alijiuliza bila majibu.
Gamutu alifuata maelekezo aliyopewa. Baada ya kukinga kwenye kikombe chake, alizugazuga kama anakunywa lakini hakufanya hivyo, akageuka kumuangalia Fatiha mahali alipo ili amuelekeze kitu kingine cha kufanya. Wakati akiangaza macho huku na kule, alishangaa kuona wale majini wote wakimkodolea macho kama waliojiuliza “Huyu ni nani?”.
Alijaribu kupepesa macho kumtazama Fatiha lakini hakumwona. Akasikia sauti nyuma yake ikimuuliza; Mbona wewe hunywi una kazi ya kushangaa shangaa?”
Kabla hata hajajibu alishangaa akivutwa na mwanaume mwenye mwili mkubwa na nywele nyingi mwilini.
“Njoo huku! Eboo…”
Vilio vilianza kusikika eneo la tukio. Bi Lubunga akawa analia kwa uchungu wa kuondokewa na mwanae aliyemwachia mjukuu mwenye matatizo na anayetakiwa kuuawa mara moja. Wenzake walimtuliza kwa muda, akatulia na kuanza kuulizana na wenzake nini cha kufanya.
Tubebe maiti ya mama, huyu mtoto tumwache hukuhuku porini. Ni bora tukadanganye kijijini kuwa mtoto kafia tumboni kuliko kusema kazaliwa na meno huku akiwa ametanguliza miguu. Ukoo wetu utatengwa na huenda tukapata matatizo makubwa.
“Hapana, nyie ondokeni kurudi kijijini, mi niacheni na mjukuu wangu. Siwezi kukubali afe, ataziba pengo la mama yake.
“Lubunga umechanganyikiwa nini? Atazibaje pengo wakati huyu ni wa kufa? Tangu lini Kashinjeghe (mtoto aliyezaliwa na meno na kutanguliza miguu) akaishi?”
“Najua nitakachokifanya, nyie niachieni kila kitu mimi, naomba tu mnitunzie siri.
Kilichofanyika ilikuwa ni kumficha mtoto porini, Bi. Lubunga na wale wanawake wengine wakakubaliana kuitunza siri ya kuzaliwa mtoto yule wa ajabu. Waliuchukua mwili mama kachanga ambaye alikuwa ni mke wa mtoto wa Bi. Lubunga na kuanza upya safari ya kurudi kijijini. Taarifa zilienea haraka juu ya kufariki kwa mama mjamzito akiwa na kachanga tumboni wakati akipelekwa kujifungua.
Hakuna aliyefahamu kuwa marehemu alikuwa tayari ameshajifungua kabla ya kufikwa na mauti, ikabaki kuwa siri kati ya Bi. Lubunga na wale wanawake watatu waliomsindikiza muda ule. Walipofika kijijini, mipango ilifanywa na mazishi yakafanyika. Muda mfupi baada ya mazishi, Bi. Lubunga aliondoka bila kuaga, akaelekea kule porini alikomficha mtoto mchanga.
Aliwasili jioni, wakati jua likianza kuzama huku anga likipambwa na rangi ya wekundu. Aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye pango alilokuwa amemficha mtoto na kuingia ndani, huku mkononi akiwa na kibuyu cha maziwa fresh.
Baada ya kumchukua, alitoka naye nje huku akimgusa kifuani kuangalia kama bado alikuwa hai. Alikuwa bado anapumua ingawa mapigo yake yalikuwa chini. Hakuonesha dalili zozote kuwa alilia wakati Bi. Lubunga akiwa hayupo, jambo lililomshangaza.
Haraka haraka alianza kumnywesha maziwa yaliyokuwa kwenye kibuyu. Alifanya hivyo mpaka maziwa yalipoisha, akamfunika na shuka kubwa alilokuwa amelibeba kutoka nyumbani kwake ili apate joto.
“Sitaki mtu yeyote akudhuru, nitakulinda kwa moyo wangu wote hata kama mama yako ametutoka, jina lako utaitwa Gamutu kama kumbukumbu ya jina la msitu uliozaliwa ndani yake,” aliongea Bi. Lubunga akiwa amemshika sikio kachanga yule.
Alikaa naye mpaka giza lilipoanza kuingia. Akamvingirisha kwenye shuka kubwa huku akiongezea vitenge na kanga kuukuu alizotoka nazo nyumbani kwake ili kumuongezea joto kachanga.
Aliogopa kurudi naye kijijini kwani kama mila za kwao zilivyokuwa, endapo Gamutu angeonekana na hali aliyokuwa nayo lazima angeuawa. Hakutaka kuona mjukuu wake anauawa kwa sababu ya mila na desturi zilizopitwa na wakati. Aliamini mtoto yule atakuwa msaada mkubwa kwake siku za mbele maishani mwake.
Baada ya kuhakikisha kuwa amemficha mahali ambapo asingeweza kudhurika na wanyama wakali wala baridi, Bi Lubunga alianza safari ya kurudi kwake. Hakuna aliyegundua kuwa alitoka porini, ikawa siri yake. Siku iliyofuatia alidamka asubuhi na mapema na kuanza safari, mkononi akiwa na vibuyu viwili vya maziwa. Alipofika msituni, alienda mpaka pale alipokuwa amemficha mjukuu wake. Alimkuta akiwa salama salmini. Akaanza kumnywesha maziwa haraka.
Aliendelea vile hadi mtoto aliapoanza kuchangamka na kufumbua macho vizuri. Bi. Lubunga akawa anautumia muda wake mwingi kushinda na kachanga porini. Hakuna aliyekuwa anajua juu ya kilichoendelea. Alipotimiza siku saba, aliamua kubadilisha utaratibu.
Aliona haitakuwa vizuri mtoto yule kuendelea kulala porini peke yake, akaona ni bora awe anarudi naye nyumbani kwake usiku bila ya mtu yeyote kufahamu na asubuhi kabla hakujapambazuka akawa anakwenda naye msituni alikoshinda naye kutwa nzima.
Bi. Lubunga alisimamisha hata shughuli zake za shamba kwa ajili ya kupata muda wa kumlea mjukuu wake, Gamutu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MIEZI SITA BAADAYE
Mtoto Gamutu aliendelea kukua kwa kasi huku kukiwa hakuna anayemjua zaidi ya Bi. Lubunga. Kitu kilichomshangaza hata Bi. Lubunga mwenyewe ni jinsi mtoto huyo alivyokuwa akikua haraka mwili na akili. Katika umri mdogo wa miezi sita tu, alikuwa na uwezo wa kuzungumza maneno yanayoeleweka. Kama ungeambiwa ana umri wa miaka miwili au zaidi usingebisha wakati kiukweli alikuwa na miezi sita tu.
Bi. Lubunga akaona hakuna haja ya kuendelea kumficha kwani yale matatizo aliyokuwa nayo wakati anazaliwa yasingeweza kuthibitika tena. Haikuwa rahisi tena kuthibitisha kwamba mtoto huyo alizaliwa akiwa ameota meno na kutanguliza miguu.
Bi. Lubunga alipojiridhisha, aliamua kuweka mambo hadharani huku akidanganya kuwa mjukuu wake huyo alikuwa ameletwa na wazazi wake kuja kumsalimia.
Mbinu yake ilifanikiwa kwani hakuna aliyejua mahali alikotokea Gamutu. Ikabaki kuwa siri ya Bi. Lubunga peke yake. Hata wale wanawake waliokuwa wamemsindikiza siku ile mkwe wake alipojifungua, nao walishasahau na wasingeweza kumtambua Gamutu kwa jinsi alivyokua haraka.
Wakati Gamutu akizidi kukua, upande wa pili, baba yake mzazi ambaye ni mtoto pekee wa Bi. Lubunga, Isambi Mwakatika alikuwa akiugua ugonjwa wa ajabu. Tangu mke wake alipokuwa na ujauzito, Isambi alianza kuumwa maradhi yasiyoisha. Alijaribu kwenda kwa waganga kadhaa wa jadi bila mafanikio. Mama yake, Bi. Lubunga aliamua kumsafirisha hadi ng’ambo ya pili ya ziwa Tanganyika, upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa matibabu.
Waganga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walikuwa wakiaminika kuwa na nguvu kubwa ya kutibu na kutegua mitego ya kichawi. Kwa jinsi mwanaye alivyokuwa akiumwa, Bi. Lubunga aliamini moja kwa moja kuwa amechezewa michezo ya kishirikina kwa sababu alikuwa akiandamwa sana na majirani zake.
Hata kifo cha ‘mkamwana’ wake aliyefariki wakati akijifungua, alikichukulia kuwa kilisababishwa na ushirikina ndiyo maana alipania kwa nguvu zake zote kuhakikisha mtoto Gamutu anakua bila matatizo ili awe ‘kifuta machozi’.
Taarifa alizotumiwa kutoka kwa waganga waliokuwa wakimtibu mwanaye zilieleza kuwa hali yake ilizidi kuwa mbaya kadiri siku zilivyokwenda, jambo lililomchanganya sana Bi. Lubunga.
Kitu kingine kilichokuwa kikimshtua Bi. Lubunga juu ya maendeleo ya mjukuu wake, ilikuwa ni tabia ya mtoto huyo kuamka usiku wa manane na kuanza kuzungumza lugha zisizoeleweka. Mara ya kwanza aliona kama ni kawaida ya watoto lakini kadiri siku zilivyokuwa zinaenda, wasiwasi ulizidi kumwingia.
Alipoenda kutafuta ushauri kwa wataalamu wa jadi, walimweleza kuwa yawezekana mtoto huyo akawa anawasiliana na majini na wachawi ambao humtembelea nyakati za usiku wakati watu wote wakiwa wamelala. Alipewa dawa za kumnywesha na kufukiza kabla ya kulala ambazo nazo hazikusaidia kitu.
Hali ile iliendelea kwa muda mrefu, ikafika mahali mtoto akawa anapotea kimiujiza nyakati za usiku na kurudi alfajiri akiwa amechafuka mwili mzima. Hali ile ilimtisha sana, ikabidi afunge safari kuvuka Ziwa Tanganyika kuelekea upande wa pili wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Alipanga kwenda kwa mganga ambaye alikuwa akimtibu mtoto wake Isambi (baba mzazi wa Gamutu), aliyekuwa akiishi Bukavu, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mipango ya safari ilipokamilika, Bi. Lubunga alimchukua mjukuu wake Gamutu na safari ya kuelekea Kongo ikaanza. Kwa kuwa walikuwa wakiishi katika kijiji ambacho hakikuwa mbali sana na Ziwa Tanganyika, walitembea umbali mfupi wakawasili ziwani. Usafiri uliokuwa ukitumika eneo lile ulikuwa ni mitumbwi na majahazi.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment