Search This Blog

KENGERE YA KIFO - 3

 





    Simulizi : Kengere Ya Kifo

    Sehemu Ya Tatu (3)



    pande mwingine walionekana maaskari wakiwa katika gari la polisi wakifanya doria kwenye mitaa usiku huo.wakakatisha kona na kuliegesha gari lao kando ya barabara kisha wakashuka kutoka ndani ya gari wakasimama barabarani kuhakikisha kila gari inayopita lazima ikaguliwe.....kumbe kunatukio la ujambazi limefanyika muda mchache uliopita ala majambazi wakakimbia na kuondika enei la tukio wakiwa na gari aina ya TOYOTA PICK UP.



    wakati huohuo alionekana mzee sule akikatisha kona kuifuata barabara hiyo ambayo wale maaskari walikuwepo...aliliendesha gari lake bila wasiwasi akaingia kabisa kwenye barabara.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akaliendesha gari mara ghafla akasimamishwa na maaskari waliokuwa kwenye doria..Mzee Sule akastuka...akajisemea moyoni,,"nimefanya ujinga sijajipaka dawa...akaonekana askari mmoja akizipiga hatua pale lilipokuwepo gari la mzee Sule......mzee sule akafungua mlango na kutoka nje ya gari akajifanya anajisaidia haja ndogo nyuma ya gari akatoa haraka ile dawa iliyokuwa ndani ya kichupa kidogo akaimwaga kiasi kwenye zile maiti mbili za wale walevi kisha akajipaka dawa hiyo mwilini haraka..yule askari alipolikaribia gari la mzee Sule,,,,akastahajabu kutomuona mzee Sule wakati kamuona sekunde kadhaa zilizopita akitoka ndani ya gari na kuelekea upande wa nyuma ya gari....yule askari akaanza kuingiwa wasiwasi akawa na mashaka na mzee Sule....akaiweka bunduki yake mkao wa tahadhari...akazipiga hatua za taratibu huku kaielekezea bunduki yake lilipokuwepo gari la mzee Sule......alipotazama kwa makini hakuweza kumuona mzee Sule kwa sababu mzee Sule alikuwa amejipaka ile dawa yake ya kichawi ili asionekane.....



    wakati huo mzee Sule alikuwa akimtazama yule askari huku akimcheka kwa kejeri...lakini askari hakuwa na uwezo wa kumuona mzee Sule...ghafla akaona gari linawashwa bila kumuona dereva anayewasha gari hilo....mzee Sule akaweka gia na kuliondosha gari kwa mwendo wa wastani....

    yule askari alipo ona hivyo akaogopa sana akajiuliza,,"yawezekana vipi gari kujiendesha lenyewe pasipo dereva!!!! akaamua kutimua mbio kuelekea kule walipokuwepo wenzake...alipowakaribia akapaza sauti kwa kusema,,"jamani jiniii......

    wale maaskari wenzake wakatimua mbio wakasahau kama walikuja na gari.....walikimbia na kutokomea kusikojulikana.....mzee Sule akacheka sana kisha akapiga mluzi huku akiliendesha gari lake na kuelekea kule mstuni ilipokuwepo nyumba yake...aliendesha gari kwa mwendo wa nusu saa akaanza kuingia kwenye msitu.....baada ya dakika kadhaa alifika nyumbani kwake....akazishusha zile maiti mbili kutoka ndani ya gari na kuziingiza ndani ya nyumba,,akazivuruta mpaka kwenye kile chumba anachokitumia kuandaa nyama kwa ajili ya mishkaki na soseji,,,sambusa pamoja na supu flani hivi amazing(supu matata) akachukua maiti moja akaibeba na kuilaza juu ya mweza....akachukua shoka akaanza kukata miguu na mikono.....akaweka kando,, kisha akachukua upanga akakata shingo na kukitoa kichwa akakiweka pembeni...akachukua kisu akatoboa tumbo akatoa utumbo huku akisema,,"huyu mtu inaonekana alikuwa mlevi sana..kinyesi chake kinanuka pombe tupu....kisha akauweka utumbo kwenye ndoo...akachukua shoka akapasua kichwa akatoa ubongo na kuuweka kenye sufuria..kisha akaanza kukatakata kata maiti ile vipande vipande kwa kutumia uoanga mkali..huku akijisemea moyoni..,,"huyu mlevi alikuwa hali vizuri nyama yake kavu haina mafuta mafuta......alisema maneno hayo huku akikatakata nyama na kuiweka ndani ya ndoo.



    ***************



    upande mwingine kule kwenye mgahawa walionekana watu wengi wakipata huduma ya chakula..wengine wakila ugali nyama choma,,wengine wakila soseji..na wengine walila sambusa na supu matata....watu walikuwa wengi sana,,hakuna kiti kilicho onekana kipo tupu..watu wengine walikuwa wakinywa supu huku wamesimama....sauti za watu zilisikika wakiisifia supu na nyama choma walisema chakula kinachopikwa kwenye mgahawa huo ni kitamu sana.....



    *********************



    Asubuhi palipokucha Tina alidamka amechelewa kuliko siku zote..akanyanyuka kitandani akaingia bafuni kuoga...akamuacha Domy bado kalala..kwa sababu siku ya leo ilikuwa ni jumamosi hivyo Domy hakwenda kazini kwa ajili ya mapumziko..



    wakati huohuo nyumba iliyopo kando kando ya nyumba ya Domy alionekana jirani aingia nyumbani kwake akiwa na fundi umeme...siku ya leo jirani huyo aliamua kuweka kengere mlangoni kwake....fundi akatoka nje na kuanza kuifunga kengere ile kwenye ukuta kando kidogo ya mlango.



    kule nyumbani kwa Domy alionekana Tina akitoka bafuni nakuanza kujifuta maji..akavaa nguo na kutoka akaelekea jikoni kuandaa chai....

    wakati huohuo ule upande mwingine alionekana

    yule fundi akimalizia kuifunga kengere ile pale ukutani....kisha akajaribu kubofya kitufe cha kengere aone kama itatoa mlio....alipobofya kengere ile haikutoa mlio wowote,,akahisi huenda atakuwa amegeuza nyaya..akaamua kuifungua na kuanza kuifunga upya..

    wakati huohuo alionekanna Domy akiamka kutoka usingizini...akazipiga hatua kuingia bafuni kuoga...



    wakati huohuo kule jikoni alionekana Tina akiendelea kuandaa chai.....

    kule nje akaonekana yule fundi akimalizia kuifunga ile kangere..kisha akabofya kitufe cha kengere..ikatoa mlio......yule fundi akakusanya vifaa vyake na kumuita yule jirani ili amlipe pesa ya ufundi aondoke zake....



    kule nyumbani kwa Domy alionekana Tina kustuka

    akainamisha uso wake chini akaanza kubadilika..macho yake yakaanza kutoa machozi ya damu..akaatoweka kimiujiza kuufuata mlio wa kengere....akajitokeza mbele ya yule fundi

    wakati huohuo alionekana Domy akitokea upande wa chumbani na kuelekea upande wa jikoni ili amuage Tina...alipofika alishangaa kutomuona Tina...akaamua kupaza sauti huku akimuita Tina...alipo ona Tina haitiki akaamua kutoka upande wa nje huenda Tina akawa huko...alipotoka upande wa nje..akaangaza angaza macho...mara ghafla akasikia sauti ya mtu akikoroma kama amekosa hewa au pumzi....akageuza shingo yake ukutazama ule upande ilipokuwa ikitokea sauti hiyo....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tina akatoweka kimiujiza kabla Domy hajageuka akajitokeza sebuleni.....Domy alipotazama akastuka kumuona fundi anadondoka chini...akaogopa sana akaamua kurudi ndani haraka..hakutaka kuwa shuhuda kabisa...alipoingia upande wa ndani akastuka kumuona Tina anajishangaa mwili wake...Domy akafoka kwa kusema,,"Leo nataka uniambie kwa nini huwa unajishangaa mwili wako!!!unamatatizo gani???

    Tina alibaki kimya bila kujibu kitu chochote..Domy akauliza tena,,,kwa sauti ya ukali zaidi..,,"Hivi Tina mbona umeanza kuwa na kiburi? yani nakusemesha alafu wewe unakaa kimya unamaana gani???kama umechoka kuishi na mimi ni bora uondoke..na sio kunifanyia Dharau...UMENISIKIA??

    Tina akastuka hali yake ya ufahamu ikarudi..akastuka kumuona Domy akifoka kwa sauti ya ukali..



    *********************



    Upande mwingine kule kwenye nyumba iliyopo kando ya nyumba ya Domy...alionekana yule jirani akitokea ndani kuja upande wa nje...alipofungua mlango.akastuka akaogopa sana kumuina fundi amelala chini huku ulimi wake uko nje..na macho yamemtoka kama anatazama kitu kwa mshangao.

    jirani akaingiwa na hofu akaamua kurudi upande wa ndani ili apige simu kwenye vyombo vya dora..wakati anaingia ndani kwa pupa akatereza kwenye marumaru/vigae nusu adondoke akawahi kushika ukuta..akabofya kitufe cha kengere bila yeye kujua...kengere ikatoa mlio....



    wakati huohuo kule ndani ya nyumba ya Domy alionekana Domy kuendelea kufoka mara ghafla Tina akastuka..baada ya kusikia mlio wa kengere.

    akainamisha uso wake..akaanza kubadilika,macho yake yakaanza kutoa machozi ya Damu..aliponyanyua uso wake Domy alistuka akapata uwoga wa hali ya juu..hakuwahi kumuona Tina akiwa hivyo katika sura ya kutisha..ghafla Tina akatoweka kimiujiza kuufuata mlio wa kengere....Domy akatimua mbio ...... tangu azaliwe hakuwahi kuona binadamu akitoweka katika mzingira ya kutatanisha ndani ya sekunde moja....alihisi kuchanganyikiwa akasahau mlango wa kutokea upande wa nje akakimbilia chumbani.

    akajifungia..



    wakati huohuo alionekana Tina kujitokeza nje ya nyumba ya jirani...akazipiga hatua mpaka mlangoni..akatoweka kimiuhiza akajitokeza upande wa ndani ya nyumba...akamkamata yule jirani akamnyonga kwa kutumia ile kamba...



    *****************



    upande mwingine alionekana mzee Sule akiwa ndani ya gari lake akiliendesha kwa kasi ya ajabu utadhani anaendesha gari la kubeba wagonjwa mahututi(AMBULANCE),,,akakatisha kona kuelekea kwenye barabara inayokwenda kwenye mtaa anaoishi Domy....

    wakati huohuo alionekana Domy akiwa chumbani kwake kasimama..huku akitazama huku na kule..kwa kuhofia huenda Tina ataingia chumbani na kumdhuru...akaona ndani hapakaliki akaamua kutoka chumbani akatembea hatua za kunyatia..huku macho yake yakitazama kwa tahadhari kubwa...mapigo yake ya moyo yalipiga kwa kasi ya ajabu....hofu ikazidi kuongezeka..alipoukaribia mlango akafungua haraka akatoka upande wa nje na kuanza kutimua mbio...Domy alikimbia kwa kasi,utadhani anakimbia kwenye mashindano ya mita mia(100)

    akaliparamia geti akafungua harakaharaka..akatoka upande wa nje...akaendelea kukimbia kwa kasi huku akitazama upande wa nyuma..mara kwa mara huenda Tina akawa anamfatilia.....wakati huohuo alionekana mzee Sule akiliendesha gari lake kwa kasi ya ajabu....Domy aliendelea kukimbia huku akigeuza sgingi yake upande wa nyuma...alipofika kwenye kona..ndio wakati mzee Sule alikuwa anakatisha kona kuelekea uoande aliotokea Domy..ghafla akamgonga na gari!!Domy akarushwa juu kutokana gari lilikuwa kwenye mwendo wa kasi...alipotua chini alidondoka na kuangukia kichwa akavunjika shingo pamoja na uti wa mgongo..Domy akafa palepale...



    ****************



    upande mwingine alionekana Tina akijitokeza ndani ya nyumba ya Domy...na baada ya sekunde kadhaa akaanza kujishangaa huku akiutazama mwili wake.....



    wakati huo huo kule barabarani alionekana Mzee Sule akishuka kutoka ndani ya gari..huku akijisemea moyoni,,"mungu mkubwa yani kitoweo kimejileta chenyewe bila kutafutwa..akaichukua maiti ya Domy na kuirusha upande wa nyuma ya gari..kisha akaingia ndani ya gari..akaliwasha na kuendelea na safari yake.....akaonekana akilipaki gari nje ya nyumba ya jirani yake Domy....akashuka na kuichukua maiti ya fundi pale nje ya mlango..akaipeleka kwenye gari lake na kuirusha upande wa nyuma....akazipiga hatua mpaka kwenye mlango wa jirani yake Domy..akaufungua akaingia upande wa ndani..

    baada ya sekunde kadhaa kupita akatika na maiti huku ameibeba begani..akazipiga hatua kulifuata gari lake...akairusha maiti ile nyuma ya gari....



    wakati huohuo alionekana Tina amerudi katika hali yake ya ufahamu...akakumbuka kuwa mume wake Domy alikuwa akimfokea akagisi huenda amemkosea akaamua kuingia chumbani kwenda kumuomba msamaha....akastahajabu hakumuona Domy mule chumbani..akaamua kutoka upande wa nje huenda Domy yupo nje ili amuombe msamaha..alipotoka nje akaangaza angaza macho huku na kule ghafla akamuina mzee Sule...CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akili ya Tina ikaanza kuzungukwa na kumbumbumbu ya ya tukio la miaka Hamsini (50)

    iliyopita.....katika mawazo hayo yaliyokuwa yakizunguka kwenye ubongo wake akamuona mze Sule!!! ndani ya fikra hizo akasema kwa sauti ya chini chini Sule!!!!..Tina akastuka.....alipotazama tena ule upande lilipokuwepo gari la mzee Sule ili aende amuulize kitu...akamuona analiwasha gari na kuliondosha kwa kasi....Tina alipojaribu kuita..akasita macho yakamtoka alipomuona mumewe Domy akiwa amelala nyuma ya gari huku akionekana kutapakaa Damu.....Tina aliweza kumtambua Domy kutokana na nguo alizokuwa amezivaa siku hiyo...Tina akapiga kele kwa sauti kali akisema,,"simamisha gari.....

    mzee sule aliliendesha gari bila kusimama akatokomea kusikojulikana.......Tina akarudi upande wa ndani huku akilia kwa uchungu..ghafla akasita akanyamaza kulia...kumbe Tina hatakiwi kuwa na hali ya mshtuko wa ghafla...hali hiyo ya mshtuko ikamfanya akaanza kubadilika..na kuwa kiumbe wa kutisha zaidi... akazipiga hatua kadhaa akatoweka kimiujiza...



    Upande mwingine alionekana mzee Sule akiliendesha gari lake kwa kasi..kabla hajafika mbali...akapunguza mwendo akalipaki kando ya barabara..akashuka kutoka ndani ya gari akatoka nje haraka akatazama kushoto kulia,,ili aone kama kuna mtu anamuona...alipogundua eneo hilo hakuna mtu yeyote anayeshuhudia..akatoa kile kichupa kidogo akanyunyizia zile maiti kisha akajipaka mwilini mwake....akafunga mfuniko wa kichupa hicho akaingia ndani ya gari na kuondoka zake......akaelekea kule mstuni ilipokuwepo nyumba yake....

    baada ya nusu saa kupita Mzee Sule alifika nyumbani kwake akachukua zile maiti na kuziingiza ndani ya nyumba yake moja kwa moja kwenye kile chumba chake anachokitumia kama bucha ( butcher) akaanza kukatakata nyama.....akatoa utumbo maini moyo na ubongo akaviweka pembeni kwa ajili ya supu matata..

    akilpomaliza alichukua toroli dogo akaliingiza kwenye mlango wa njia ya chini kwa chini...akachukua nyama na kuiweka kwenue toroli,,akaianza safari ya kuelekea kwenye mgahawa wake kwa kupitia njia hiyo ya siri..



    *************



    upande mwingine alionekana mtu mmoja akiwa mstuni.......ndani ya gari lake..mtu huyo alifahamika kwa jina la MUKI...anajishuggurisha na fundi seremala..

    siku ya lei alikwenda kwenye msitu huo kwa lengo la kukata miti iliyokomaa kwa ajili ya kuchana mbao..ili zimsaidie katika kazi zake za useremala.

    akashuka kutoka ndani ya gari akachukua(CheanSaw) msumeno wa kutumia umeme..ndani yake kuna betri inayochajiwa katika umeme na kuhifadhi umeme kwa muda wa masaa sita(6) mfululizo huku ukiwa unafanya kazi ya kukata magogo makubwa.... kabla hahaanza kukata miti ghafla likatanda wingu kubwa na upepo mkali mvua ikaanza kunyesha....ilinyesha mvua kubwa sana akaamua kuingia ndani ya gari lake akaliwasha na kuondoka zake ili akapange siku nyingine aje kuchana mbao ......akiwa njiani ndani ya msitu huo gari lake lilikwama kwenye udongo ulietifutifu,,,akakanyaga mafuta kwa nguvu magurudumu yakazunguka kwa kasi huku yakichimba aridhi..mpaka gari ikatitia.....Muki akakasirika sana...akawaza jinsi ya kufanya ili aweze kulitoa gari lake....akazima gari kutokana na mvua kubwa na maji kuwa mengi pamoja na uzito wa gari likaanza kutitia kuelekea chini ya aridhi .



    kumbe hiyo sehemu lilipokua limekwama gari la Muki na kutitia ,,ndio sehemu ambapo ile njia ya siri inayopita chini kwa chini aliyoitengeneza mzee sule kwa ajili ya kupitisha nyama za biadamu kwa ajili ya kuzipeleka kwenye mgahawa wake.

    mvua iliendelea kunyesha na maji yakawa mengi zaidi udongo ulilainika kutokana na maji hayo ukameguka na gari la Muki likatumbukia chini ya aridhi na kudondoka ndani kabisa kwenye ile njia ya chini kwa chini ya aridhi, mzee Sule alisikia kishindo cha gari hilo kudondoka, akastuka aliogopa sana akalitelekeza toroli lililokua na nyama za binadamu akatimua mbio ili kuokoa maisha yake.....alihisi ni kifusi kimedondoka,,akapata hofu ya kufunikwa na kifusi.....alikimbia bila kugeuka mpaka akatokezea kwenye mlango wa kuingilia ndani ya nyumba yake...mlango huo ulikuwa kwenye sakafu ya chumbani kwake......



    Muki alionekana kustahajabu sana..baada ya gari lake kutumbukia chini ya aridhi ba yeye akiwemo ndani yake.....akashangaa sana kuona kunanjia inayopita chini ya aridhi....akaamua kufungua mlango akachukua tochi,,na kisu akatoka ndani ya gari...akaanza kuifatilia njia hiyo ili aone inatokezea wapi......akatembea kwa mwendo dakika kumi..Muki alizipiga huku macho yake yakitazama kwa tahadhari kubwa sana...

    huku akimulikamulika pande zote kwa kutumia tochi yake.....kwa mbali kama hatua kumi hivi akaona kuna kitu..alipomulika na kutazama kwa umakini akagundua kuwa ni toroli....akazipiga hatua kulisogelea toroli hilo..akamulika ili aone toroli hilo limebeba nini ndani yake.....akaona kuna nyama..akastuka..akatazama kwa makini akaona makalio ya vinadamu yamekatwakatwa vipande vipande...akaona maini na moyo pamoja na utumbo..akagundua kuwa ni binadamu waliouwawa na kukatwakatwa vipande vipande...akajiuliza,,"mbona hakuna viungo vingine kama miguu mikono na kichwa...inamaana kuna watu wanakula nyama za binadamu!!!! ni nani huyu aliyefanya mauwaji haya??

    Muki alikuwa jasiri sana, aliwahi kuwa mwanajeshi akaacha kazi hiyo ya uwanajeshi kutokana aliugua ugonjwa wa akili........mkuu wa jeshi akaamuru Muki asimamishwe kazi akatibiwe,,Baada ya kutibiwa Muki alipona kabisa akili zake zikarudi katika hali ya kawaida(TIMAMU) akaamua kuachana na kazi ya jeshi akawa mjasiliamali wa kutengeneza vitanda,,makabati,,meza na vitu vingine vinavyotengenezwa kwa mbao..Muki hakuogopa akaendelea kuifuata njia ile...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****************



    Upande mwingine kule kwenye mgahawa..walionekana watu wakiingia na kutoka...walipishana utadhani sokoni..Mgahawa wa mzee Sule ulizidi kupata umaarufu......kutokana watu wengi waliowahi kula kwenye mgahawa huo waliusifia sana...

    kwa mbali alionekana mwanamke mmoja akitembea hatua za kikakamavu...mwanamke huyo alikuwa kavaa miwani yenye kioo cheusi huku nywele zake zimeanguka mgongoni...akaingia ndani ya mgahawa wa Mzee Sule.



    kutokana na watu kuwa wengi kuliko viti vya kukalia...Mwanamke hiyo alisimama....

    kwa mbali akaonekana yule kijana mkubwa wa mzee Sule akimfuata mwanamke huyo..ili kumuuliza anahitaji huduma gani? alipomkaribia akamuuliza...yule mwanamke akasema,,"niletee sambusa tatu na supu...weka nyama yenye mafutamafuta.....yule kijana akazipiga hatua za haraka haraka akaingia jikoni...akaandaa supu pamoja na sambusa tatu...akapeleka kwa mwanamke yule.....akaweka kwenye meza iliyokuwa imejaa vyakula juu yake...

    yule mwanamke akachukua sambusa moja akaitafuna,,,akachota supu kwa kijiko akasita kuipeleka mdomoni...alipoitazama kwa makini..aliona kucha ya binadamu ikielea kwenye mchuzi...akaacha kula..akamuita yule kijana akatoa noti ya shilingi elfu kumi..yule kijana aliipokea pesa hiyo akarudi jikoni kuchukua chenji ili amrudishie mwanamke yule......

    alipokuwa anarudi akamuona yule mwanamke akizipiga hatua kuelekea upande wa nje.....akamuita lakini hakugeuka..akaamua kumfuata kwa nyuma....alipotoka nje hakumuona mwanamke yule...akaangaza angaza macho lakini hakufanikiwa kumuona,,akabaki na mshangao...akajiuliza inamaana kayayuka au!!!? mbona hakuna hata kichochoro,,,atakuwa kapitia wapi....

    hakujali akaamua kurudi ndani ya mgahawa akapitiliza moja kwa moja mpaka jikoni....akaendelea kuwahudumia wateja wengine waliokuwa wanaingia....



    ********************



    upande mwingine alionekana Muki akiwa chini ya aridhi,,kwenye ile njia inayopita chini kwa chini..

    akaona kunamlango wakutokea ndani ya njia hiyo ya siri...akausogelea,,,alipojaribu kuusukuma,,haukufunguka ulikuwa umefungwa kwa ndani...akaanza kuupiga kwa mateke ili uvunjike..lakini akashindwa....mzee Sule aliutengeneza mlango huo kwa mbao za mti wa MPINGO..akaweka komeo kubwa la chuma.... mlango huo ulikuwa umezungukwa na zege iliyochanganywa kwa simenti kali...haikuwa rahisi kuuvunja.....Muki akaamua kurudi kule lilipokuwepo gari lake



    Mzee Sule alisikia kama kuna mtu anagonga ule mlango wake wa siri...akastuka akafunua chini ya kitanda,,akatoa upanga...akatoka nje haraka ili aende akatazame ni wapi mtu huyo ameingilia, amuuwe kabla hajatoa siri...



    *****************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    upande mwingine kule kwenye mgahawa Nyama ikaanza kupungua huku wateja wakizidi kuingia..hatimae supu ikaisha....Mke wa mzee sule akachanganyikiwa...akajiuliza mpaka muda huu mumewe Mzee Sule hajaleta nyama kulikoni??

    akaamua kumtuma kijana wake mkubwa apitie kwenye mlango wa njia ya siri..awahi nyumbani angalau akalete nyama ndoo moja,,,na utumbo,maini,bandama pamoja na ubongo aweke kwenye ndoo nyingine.....

    Yuele kijana akachukua tochi akafungua mlango na kuianza safari ya kwenda nyumbani.kwa kupitia njia hiyo ya siri....kwa mbali aliona kama kuna kitu kimeziba njia..akasita kuendelea kukimbia..akaanza kutembea kwa hatua za tahadhari....alipokaribia akagundua kuwa ni gari limetumbukia..na limeziba njia..hivyo hawezi kutokezea upande wa pili...yule kijana akaamua kuvuta mlango wa gari ukafunguka,,akaingia ndani ya gari akafungua mlango wa upande wa pili ili atoke aendelee na safari yake ya kufata nyama kule nyumbani kwao...kabla hajatoka ndani ya gari..aliona kuna mwanga wa tochi ukilifuata gari..yule kijana hakujali alijua ni Mzee Sule...akatoka ndani ya gari na kuanza kuzipiga hatua...pia Muki aliona mwanfa wa tochi ukitokea kule lilipokuwa gari lake,,akastuka akaamua kuizima tochi yake...



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog