Simulizi : Kengere Ya Kifo
Sehemu Ya Nne (4)
akalete nyama ndoo moja,,,na utumbo,maini,bandama pamoja na ubongo aweke kwenye ndoo nyingine.....
Yuele kijana akachukua tochi akafungua mlango na kuianza safari ya kwenda nyumbani.kwa kupitia njia hiyo ya siri....kwa mbali aliona kama kuna kitu kimeziba njia..akasita kuendelea kukimbia..akaanza kutembea kwa hatua za tahadhari....alipokaribia akagundua kuwa ni gari limetumbukia..na limeziba njia..hivyo hawezi kutokezea upande wa pili...yule kijana akaamua kuvuta mlango wa gari ukafunguka,,akaingia ndani ya gari akafungua mlango wa upande wa pili ili atoke aendelee na safari yake ya kufata nyama kule nyumbani kwao...kabla hajatoka ndani ya gari..aliona kuna mwanga wa tochi ukilifuata gari..yule kijana hakujali alijua ni Mzee Sule...akatoka ndani ya gari na kuanza kuzipiga hatua...pia Muki aliona mwanfa wa tochi ukitokea kule lilipokuwa gari lake,,akastuka akaamua kuizima tochi yake..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule kijana wa mzee Sule alipo ona ule mwanga wa tochi hauonekani tena...akaingiwa na hofu..akapaza sauti kumuita baba yake,,"BABA..
Muki akauliza kwa sauti ya ukakamavu,"WEWE NI NANI??
yule kijana aligundua hiyo sio sauti ya baba yake..akaamua kutimua mbio akaingia ndani ya gari akafungua mlango wa upande wa pili akatoka na kuendelea kutimua mbio kurudi kwenye mgahawa..
******************
Upande mwingine alionekana mzee Sule akizipiga hatua za haraka haraka..kuifuata ile njia ya siri akiwa upande wa juu ya aridhi...alitembea mwendo wa dakika kumi..huku macho yake yakitazama kwa umakini akastuka,,kwa mbali akaona kuna gari limetumbukia chini ya aridhi huku likionekana kiasi kutokeza upande wa juu ya aridhi..amzee Sule akatimua mbio kuelekea kwenye gari hilo...
wakati huohuo..kule chini ya aridhi alionekana Muki akizipiga hatua za tahadhari huku kashikilia kisu chake,,tayari kwa lolote litakalotokea,,alipolikaribia gari lake akawasha tochi akamulika huku akitazama kwa umakini...akagundua kuwa hakuna mtu ndani ya gari lake...akaingia ndani ya gari..alipomulika kwenye kioo cha dirisha akaona bado njia hiyo inaendelea..akafungua upande wa pili akatoka na kuanza kuifuata njia hiyo....
**************
kule juu ya aridhi,alionekana mzee Sule akilisogelea gari la Muki akavunja kioo cha nyuma akaingia ndani ya gari. ...akafungua mlango akatoka ndani ya gari...nia na lengo lake amuwahi yule mtu kule aliposikia mlango unagongwa...akawasha tochi akaanza kukimbia kuelekea kwenye mlango wa kutokezea ndani ya nyumba yake.
upande mwingine alionekana Muki akiendelea kusonga mbele zaidi..kuelekea ule upande ambao ulikuwepi mlango wa kutokezea kwenye mgahawa...
Macho ya muki yalikuwa makini kutazama..alizipiga hatua kwa tahadhari kubwa...
huku akimulika kwa tochi...kwa mbali akaona kama kunamlango...akazipiga hatua za haraka haraka...alipoukaribia...akazima tochi..akachungulia kwenye upenyo wa mlango huo uliotengenezwa kwa mbao...alipotazama kwa makini,, akaona kunawatu wanapika...akaangaza angaza macho..akaona kiganja kimoja cha binadamu kikiwa kimekatwa....akastuka..akaona kunanyama imetundikwa....nyama hiyo ilikuwa imekatwa kwenye sehemu ya paja la binadamu....Muki akasikitika sana akajisemea moyoni.."inamaana...humo ndani wanakula nyama za watu....hakujua kuwa nyama hizo za binadamu zilikuwa zikipikwa kwenye mgahawa....akaamua kurudi kule lilipokuwepo gari lake...
*******************
ule upande mwingine alionekana mzee Sule akirudi baada ya kutokumkuta yule mtu aliyekuwa anagonga mlango wake wa siri...akazipiga hatua kuelekea kwenye lile gari lililokuwa limetumbukia kwenye hiyo njia yake ya siri..inayopita chini kwa chini....
wakati huo huo,, alionekana Muki akiingia ndani ya gari akapanda kwenye viti akatoka upande wa nje.kwa kupitia kwenye kile kioo kilichovunjwa na mzee Sule....akazipiga hatua za harakaharaka..kuifua njia hiyo inayopita chini kwa chini ya aridhi..yeye akiwa upande wa juu ya aridhi.....alitembea umbali mrefu kidogo kwa muda wa dakika kumi natano...akaona kuna nyumba imejitenga porini....akaamua kuifuata nyumba hiyo..alipofika..akapiga hodi kwenye mlango..lakini hakuona dalili yoyote ya mtu kufungua mlango...akajaribu kusukuma mlango ukafunguka..akaingia ndani ya nyumba hiyo...akakuta kuna radio ndogo ikipiga mziki...akapaza sauti.."HIDI HUMU NDANI!!....
hakusikia mtu akimjibu..akajisemea moyoni....inaonekana mwenye nyumba hayupo mbali,,kwa sabavu radio ilikuwa ikipiga mziki..akaamua kuzipiga hatua kutoka nje..ghafla akaona kuna damu kwenye sakafu,,damu hiyo ilikuwa ikitokea ndani ya chumba ikitiririka kupitia chini ya mlango...akastuka.akazipiga hatua kadhaa akafungua mlango wa chumba hicho....CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akastuka kukuta miguu sita na mikono sita ya binadamu ikiwa imekatwa...imekusanywa sehemu moja..alipotazama juu ya meza aliona kuna vichwa vitatu vikiwa vimepasuliwa katikati..na kutolewa ubongo...kumbukumbu ikamjia akakumbuka..lile toroli aliloliona kule kwenye njia inayopita chini kwa chini ya aridhi...lilikuwa na nyama ya binadamu ikiwa imekatwakatwa....akagundua kuwa mtu anayeishi ndani ya nyumba hiyo ndiye aliyeweka toroli lile..lililojaa nyama za binadamu. ..
**************
upande mwingine..kule chini ya aridhi..alionekana mzee Sule akifungua mlango wa gari la muki akaingia ndani akafungua mlango wa upande wa pili..akatoka na kuelekea kule ulipokuwepo mgahawa...alipoukaribia mlango hakuona mtu yoyote...akajisemea moyoni,"lazima nimnase mtu huyu..Lah! si hivyo.. titakuwa matatani...kwa sababu mtu huyu ameona lile toroli..na ameshajua kuhusu hii njia yangu siri....ngoja nirudi nyumbani nikachukue gari nimtafute..nina imani bado hajatoka nje ya msitu huu.
mzee Sule akakasirika sana..akarudi kule lilipokuwepo gari la Muki.akaingia ndani ya gari akafanda juu ya viti..akatoka nje kwa kupitia kwenye kioo alicho kivuja......akazipiga hatua za haraka haraka kuelekea nyumbani kwake......
*************
wakati huohuo alionekana Muki bado yumo ndani ya nyumba ya mzee Sule...akiendelea kuchunguza,,vyumba vyote vilivyomo ndani ya nyumba hiyo....akainfia kwenye chumba kingine..akakuta kuna pesa nyingi sana....pesa hizi alizihifadhi mzee Sule ndani ya chumba hicho...kutokana na mauzo ya kila siku kule kwenye mgahawa wake.....Muki alistahajabu sana alijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.....akatoka nje ya chumba hicho..akaingia kwenye chumba kingine....akakuta kuna mashine...ya kusagia nyama......pia kuna diaba kubwa likiwa limejaa nyama iliyosagwa...Muki akazidi kustahajabu.....akajiuliza nyama hiyo iliyosagwa bila shaka pia itakuwa ni ya binadamu.
akaisogelea mashine hiyo akawasha swichi..lakini haikuwaka akaamua kutoka ndani ya chumba hicho bila kuizima ile swichi......akaanza kuutafuta ule mlango unaitokezea kwenye ile njia ya chini kwa chini ya aridhi....
********************
upande mwingine alionekana yule mwanamke aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha kule kwenye mgahawa wa mzee Sule... akiingia ndani ya Taxii...kisha akamwambia Dereva ampeleke....KIBAHA..dereva akawasha gari na safari ya kwenda Kibaha ikaanza...
****************
upande mwingine alionekana mzee Sule akizidi kusonga..alipoikaribia nyumba yake..akasikia mashine yake ya kusagia nyama ikiwaka na kuanza kunguruma....akastuka akaanza kutimua mbio kuufuata mlango wa kuingilia ndani ya nyumba ili amuwahi huyo mtu aliyewasha mashine yake kabla hajatoka nje.....kumbe mashine hiyo ikiwashwa inachukuwa muda kuanza kuzungusha injini na kuanza kufanya kazi.
tangu ule muda ambao Muki aliiwasha ile swichi,,sasa hivi ndio mashine imewaka..
wakati huohuo alionekana Muki akiwa ndani ya nyumba ya mzee Sule...akastuka kusikia mngurumo wa mashine hiyo,!!akahisi kuna mtu huenda kaingia na kuiwasha mashine hiyo...
Muki akachomoa kisu akajificha chini ya uvungu wa kitanda kwenye chumba cha mzee Sule..
kule nje ya nyumba hiyo akaonekana mzee Sule akiingia ndani ya nyumba huku kashikilia upanga..tayari kwa kumuangamiza mtu aliyeingia ndani ya nyumba yake.
Akafunga mlango akaanza kuzipiga hatua kuelekea kwenye kile chumba kilichokuwa na mashine ya kusagia nyama...akaangaza angaza macho pande zote lakini hakuina mtu...akatoka akaingia chumbani kwake.......akasita kutafuta akatoka nje haraka akaingia ndani ya gari lake.....akamtafute huyo mtu aliyejaribu kucheza kwenye Himaya yake....akajisemea moyoni hatakuwa hajafika mbali....
kumbe kamuacha Muki kule ndani...chini ya uvungu wa kitanda, kwenye chumba chake cha kulala......
*******************
kule ndani ya nyumba ya mzee Sule,, alionekana Muki akiwa bado yumo chini ya uvungu wa kitanda..akatoka uvunguni haraka...akachungulia upande wa nje kwa kupitia dirishani....akaona gari la Mzee Sule likitokomea mstuni....akazipiga hatua kutoka nje.....akaparamia sanduku dogo la mbao..likadondoka na kufunguka....alipolitazama akaona kuna picha Tatu...pamoja na nyaraka za siri za Mzee Sule.. akazichukua zile picha...akazitazama....picha hizo zilionekana za kizamani...akazirudisha..akachukua zile nyaraka akazisoma.....macho yakamtoka...
nyaraka hizo zilieleza hivi,,,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Miaka hamsini iliyopita.....wakati huo mzee Sule alikuwa na umri wa miaka kumi na moja... alianza kupata na hali ya kutamani kula nyama mbichi tena alipendelea zaidi nyama ya binadamu....hali hiyo iligundulika baada ya mzee Sule kudondoka wakati anaendesha baiskeli...akapata jeraha la mchubuko kwenye mkoni wake wa kushoto.....baada ta wiki mbili kupita,,wazazi wake wakaanza kuingiwa na wasiwasi kwa nini kidonda cha Sule hakiponi,,wala hakuna dalili yoyote ya kidonda hicho kukauka.....kila kukicha kinaonekana kuwa vilevile kibichi,,alafu kinazidi kuongezeka uchimbika kwenda ndani zaidi........
ikafika kipindi Sule akaanza kuwa na tatizo la kupungukiwa damu...akawa anapelekwa hospitali mara kwa mara,,kwa ajili ya kuongezewa damu...madaktari walistahajabu sana...kwa sababu sio jambo la kawaida kwa binadamu kuongezewa damu kila baada ya wiki moja.......kila wakikifunga kindo cha Sule kwa bandeji...haichukui muda..wanakuta Sule kaitoa bandeji hiyo...na kidonda kuonekana kuwa kibichi...ikabidi wazazi wake watafute njia mbadala,,ya kumsaidia mtoto wao Sule......
kumbe Sule alikuwa anaifyonza damu yake kwa kupitia kidonda hicho....wazazi wake hawakulitambua hilo...kwa sababu Sule alikuwa hafanyi kitendo hicho mbele yao.....
hali ya kidonda cha Sule ilizidi kutisha kadri wiki zilivyozidi kusonga.....
siku moja baba Sule..alishauriwa na rafiki yake kuwa ampeleke Sule NIGERIA kwa mganga matata aitwae OBINA...baba Sule aliandaa hati mbili za kusafiria....yake pamoja na Sule...akaongozana na Rafiki yake...huyo aliyempa ushauri huo.....
baada ya siku kadhaa safari ikawadia...wakapanda ndege kuelekea NIGERIA.
wakafika salama...wakaelekea mpaka kwenye msitu ISAKABA alipokuwa anapatikana Mganga matata OBINA...walipofika baba Sule akaeleza tatizo la Sule kupungukiwa damu kila wiki...na kidonda hakiponi..kadri siku zilivyozidi kusongo..ndivyo kiliongezeka ukubwa utadhani kaumia muda huohuo......hata madaktari walipomfanyia vipimo haikugundulika tatizo ni nini...linalosababisha Sule kupungukiwa damu kila wiki....
OBINA akasema "tiba ya Sule ni kubwa sana,,,kuna masharti ya kuyafuata...na Tiba hiyo itachukua muda wa wiki tatu...Sule atapona.....Mganga OBINA aliongea maneno hayo huku akipiga TUNGURI zake za kichawi....akasita akabaki kimya kwa sekende kadhaa,,kisha akasema..."mtoto wako anasumbuliwa na mzimu wa JIGO..mzimu huo unanyonya damu ya mwanao kwa kupitia,,Sule mwenyewe....baba sule akastuka..kwa sababu JIGO ni jina la UKOO wake...jina hilo ni la muazilishi wa ukoo ambaye ni babu wa mababu katika ukoo wa baba Sule.....
mganga OBINA akasema,,"ili mzimu huu usiendelee kumsumbua mtoto wako...inabidi Sule amuuwe binti wa umri kama wake..ndani ya siku tatu...........na baada ya wiki tatu kupita,,,,, mzimu huo utaacha kumuandama Sule...pia baada ya miaka hamsini(50) kupita...binti huyo atafufuka akiwa katika umbile la mwanamke mwingine...huko kwenye nchi yenu....na atakuwa mtumwa wa Sule.....sharti sule asithubutu kumkasirisha binti huyo........Mganga OBINA akamnywesha dawa Sule.....dawa hiyo ni maalumu ya kumpa Sule ujasiri wa kufanya mauwaji ya binti wa umri kama wake....
*************************
Rafiki yake baba sule akawaongiza mpaka kwa kaka yake aliyekuwa anaishi hukohuko NIGERIA
wakaishi hapo mpaka Sule atakapo maliza kutibiwa....ilipofika majira ya usiku...Sule aliamka bila yeye kujitambua akafungua mlango na kutoka nje..akazipiga hatua za kikakamavu mpaka kwenye nyumba ya jirani.....akabofya kengere.....iliyokuwa ukutani kando ya mlango
ndani ya nyumba hiyo alikuwema...mama moja mgonjwa aliyekuwa akiishi na binti yake aitwae TINA...
Tina alisikia mlio wa kengere..akastahajabu...ni nani anayebofya kengere hiyo usiku kama huo...akanyanyuka kitandani..akaenda sebuleni..alipofungua mlango....Sule akamkamata na kumkaba shingo....Tina akakosa pumzi...akatapatapa mpaka akafa....Sule akazipiga hatua na kurudi ndani ya nyumba akalala......
Baada ya siku tatu kupita....Ile hali ya Sule kunyonya damu yake ikatoweka...akaanza kuhisi maumivu kwenye kile kidonda....
na baada ya mwezi mmoja kupita....tiba ya Sule ilikamilika mganga Obina akasema,,"sasa mnaweza kurudi nchini kwenu.....
*****************
Muki akastuka baada ya kuisoma stori ya mzee Sule iliyokuwa imeandikwa kwenye nyaraka hizo za siri..kwa mkono wa mzee Sule mwenyewe.... Muki akarudisha haraka nyaraka hizo...
akazipiga hatua za harakaharaka kutoka upande wa nje...kabla hajatoka akasikia mngurumo wa gari likija kwenye nyumba hiyo......alipochungulia akaona ni gari la mzee Sule.........akiliendesha kwa kasi..
akatoka haraka ndani ya chumba hicho akakimbia sebuleni...na kujificha ndani ya kabati kubwa lililo na vitu vichache ndani yake....
*********************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
upande mwingine alionekana yule mwanamke aliyekwenda Kibaha...mwanamke huyo alikuwa akimtafuta mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la
MBEGA.........mzee huyo ndiye yule aliyemshauri baba sule miaka hamsini (50)iliyopita..ampeleke Sule kwa mganga OBINA kutibiwa huko Nigerea....
mwanamke huyo akazipiga hatua mpaka kwenye duka lililokuwa linauza vinywaji baridi..akanunua maji ya chupa..akaketi kando ya duka hilo...akiwa ameketi...kunatukio akawa analiona katika fikra zake likizunguka ndani ya ubongo wake....akamuona mzee Mbega,,kwenye frikra hizo,,pia akamuona Sule ambae kwa sasa anaumri wa miaka sitini na moja(61).....akakumbuka siku ile Sule alipobofya kengere ya mlango wa nyumba yao na kumkaba shingo mpaka akafa,,,akakumbuka lile tukio aliloliina hivi karibuni la mume wake Domy akiwa amelala nyuma ya gari la Mzee Sule, huku ametapakaa damu mwili mzima baada ya kugongwa na gari la mzee Sule.....pia katika fikra hizo hizo akaona mtaa na nyumba anayoishi..mzee mbega...
kumbe mwanamke huyo ni Tina,,kwa sasa yupo katika umbile lingine la mwanamke tofauti na muonekano wa Tina wa mwanzo.....alibadirika pasipo yeye kujijua,,baada ya kupata mstuko,,alipomuona mumewe kafa na kuingizwa ndani ya gari la mzee Sule....likasirika sana...akatoweka kimiujiza....akarudi kivingine katika umbile la mwanamke mwingine...sasa hivi hii ndio sura na umbile halisi la Tina yule aliyeuwawa miaka hamsini(50) iliyopita,,,
Tina akanyanyuka kutoka pale alipokuwa ameketi,,akazipiga hatua kuelekea ule mtaa anaoishi mzee Mbega bila kujitambua....alipofika kwenye nyumba ya Mzee mbega akastuka,,,akajiuliza,,"hii nyumba kama nimeshawahi kuiona mahala fulani,,lakini sikumbuki ni wapi...akawa anashangaa pasipo kujielewa....akamua kuufuata mlango wa nyumba hiyo akagonga hodi....ikasikika sauti ya kizee ikisema,,"karibu,, ingia mlango upo wazi....Tina akafungua mlango na kuingia ndani....Mzee Mbega akastuka sana,,kumuona mwanamke huyo,,,akajaribu kuvuta akamkumbuka,,,kuwa huyo ni yule binti,,aliyeuwawa miaka hamsini iliyopita....kwa sababu sura ndio ile ile,,,ya yule binti aliyekutwa kauwawa kwa kunyongwa shingo...jirani na nyumba ya kaka yake aliyekuwa anaishi kule Nigeria,ambaye kwa sasa pia ni marehemu....
Tina akaketi kwenye kiti.....akauliza,"Samahani wewe ni nani??
yule mzee akabaki kimya kwa sekunde kadhaa akajibu mimi naitwa Mbega...nikusaidie nini binti??
Tina akabaki kimya kisha akasema,,"kho Aaam....ee..hata sijui nataka nini,,pia sijui hapa nimefikajefikaje??? mzee Mbega akastuka akajisemea moyoni,"bila shaka binti huyu bado hajajitambua yeye ni nani.....akasema,,"Tina...
Tina akastuka..akakumbuka alishawahi kuitwa jina hilo.....lakini hakumbuki ni wapi....akauliza,,"wewe umejuaje jina hilo? mzee Mbega akazidi kustahajabu,,akajisemea moyoni....inamaana Sule bado yupo hai?? na atakuwa wapi kwa muda huu....kwa sababu yule mganga Obina alisema baada ya miaka hamsini kupita huyo binti atafufuka huko nchini kwenu....mzee Mbega akastuka akasema,,"nisubiri nakuja,,akazipiga hatua za kizee akaingia chumbani kwake.....alipofika chumbani kwakeaka,,akajiuliza,,"kama amefufuka basi itakuwa balaa,,,akakumbuka maneno ya mganga Obina kuwa...mwanamke huyo akifufuka atakuwa mtumwa wa sule....pia akakumbuka....jinsi ya kumdhibiti Mzimu aliyeingia katika kiwiliwili na kuonekana ni binadamu wa kawaida...ni kumchoma na kipande cha mbao ya mti wa MKARATUSI....akaamua kuchukua kipande hicho cha mbao akakiweka kwenye mfuko wa suruali yake,,ili Tina asikione,,,,mzee Mbega aliamua kufanya hivyo ili kuikoa maisha ya wengine...kwa sababu mwanamke huyo hakufufuliwa kwa nia nziri akaona ni vyema akamuuwe ili arudi kwenye kifo.....mzee Mbega akazipiga hatua kurudi sebuleni..kule alipokuwepo Tina.
************************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
upande mwingine kule nyumbani kwa mzee Sule alionekana,,akishuka kutoka ndani ya gari,,akaweka mitego,,ya miti iliyochongoka,,ili kama kunamtu atakanyaga eneo la nyumbani kwake kuanzia sasa hivi..basi atauwawa kwa kuchomwa na mitego hiyo hatari..alipomaliza kutega mitego hiyo,akazipiga hatua,,kikakamavu
na kuingia ndani ya nyumba yake,,,akapitiliza mpaka chumbani kwake huku ameshikilia upanga....
akauweka chini akachukua shoka kubwa.
akatoka chumbani....akaanza kukagua vyumba vyote....ili ahakikishe kama vitu vyake vipo sawa...
akatoka upande wa vyumbani akaelekea sebuleni..
**********************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment