Simulizi : Kengere Ya Kifo
Sehemu Ya Tano (5)
upande mwingine kule nyumbani kwa mzee Sule alionekana,,akishuka kutoka ndani ya gari,,akaweka mitego,,ya miti iliyochongoka,,ili kama kunamtu atakanyaga eneo la nyumbani kwake kuanzia sasa hivi..basi atauwawa kwa kuchomwa na mitego hiyo hatari..alipomaliza kutega mitego hiyo,akazipiga hatua,,kikakamavuCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
na kuingia ndani ya nyumba yake,,,akapitiliza mpaka chumbani kwake huku ameshikilia upanga....
akauweka chini akachukua shoka kubwa.
akatoka chumbani....akaanza kukagua vyumba vyote....ili ahakikishe kama vitu vyake vipo sawa...
akatoka upande wa vyumbani akaelekea sebuleni..
Upande mwingine kule kwenye mgahawa watu walizidi kuingia....kwa ajili ya kujipatia chakula na supu matata...wakaanza kulalamika kuwa huduma inacheleweshwa......
mke wa mzee Sule hakuwa na namna..kwa sababu nyama ilikuwa imekwisha...hata supu ilikuwa imekwisha......
kwenye sufulia la kupikia Supu....ilibaki kwa ajili ya familia ya mzee Sule...masikio,,pua,na viganja vya mikono ya binadamu.....ghafla yule kijana mkubwa,,ambaye ni mtoto wa mzee Sule akasema.,,"mama ninawasiwasi,,kunamtu ameingia kwenye njia ya siri..anayoitumia baba kuleta nyama huku jikoni...tunaweza kukamatwa muda wowote...ni vyema tukakimbia kwa usalama wa maisha yetu...kabla hajamaliza kuongea....
mke wa mzee Sule akadungua mlango wa nyuma wa kutokea nje kabisa...wakatimua mbio kuelekea kule mstuni,,ilipokuwepo nyumba yao....baada ya dakika arobaini(40)kupita walianza kuikaribia nyumba yao...walipoanza kukanya ardi ya mazingira ya nyumba hiyo..ghafla yule kijana mkubwa,,,pasipokujua akakanyaga ule mtego uliotegwa na mzee Sule ambaye ni baba yake
mara ghafla ile miti iliyochongoka na kutengeneza ncha kali ikafyatuka na kuruka upande wao pasipo wao kujua...wakatahamaki kusikia sauti kama ya vitu vilivyorushwa kwa kasi mara ghafla..
miti hiyo iliruka na kuwachoma....
miti miwili ilikwenda moja kwa moja mpaka tumboni mwa mke wa sule ikatokezea mgongoni akadodoka chini na kupoteza uhai papohapo..
miti mingine mitatu ikaruka kuelekea kwa kijana mkubwa wa mzee Sule...mmoja ukaingia kwenye jicho na kutokeza kisogoni....mti mwingine ukamchoma kwenye ubavu,,,na ule mti wa tatu ukatoboa shingo yake na kutokeza upande wa nyuma...akadondoka na kupoteza uhai papohapo..
pia alionekana yule mtoto wa mwisho wa mzee sule,,,akidondoka chini,,akapoteza uhai baada ya kuchowa na miti miwili ikaingia tumboni na kutokezea mgongoni..
*************************
Upande wa ndani ya nyumba hiyo,,alionekana mzee Sule akiendelea kutazama na kuvikagua vitu vyake kama vipo sawa.....akazipiga hatua kuifuata kabati aliyokuwa amejificha Muki.....akashika mlango ili aufungue mlango wa kabati hiyo...ghafla akahisi kama ile mitego aliyoitega nje.. imefyatuka....akatabasamu,,....akiamini kuwa,, mitego hiyo imemnasa mtu aliyekuwa ameingia kwenye eneo la nyumba yake na kujaribu kuchunguza vitu vyake........akaacha kufungua mlango wa kabati akazipiga hatua kuelekea nje,,ili akamtazame mtu huyo..
***********************
Upande mwingine,, kule kwenye mgahawa, walionekana wateja wakiendelea kusubiri huduma,,,wengine walihitaji supu,na wengine walihitaji ugali nyamachoma,,kuna mteja mmoja alikuwa kaagiza Supu,,akaambiwa asubirie supu inaletwa lakini akastahajabu,,,inakaribia kupita lisaa limoja haoni dalili yoyote ya muhudumu kuleta supu aliyomuagiza....akaamua kunyanyuka na kuelekea kule jikoni ili akaulize kama kuna tatizo!!! kwa sababu supu imecheleweshwa,,alipoukaribia mlango wa jikoni,,akasema,,"jamani mbona nimeagiza supu,,lakini hamjaleta mpaka sasa hivi ni lisaa limoja limepita....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hakuna mtu aliyemjibu...akaamua kufungua mlango, akaingia upande wa ndani ya jiko..hakuona mtu!!! akaangaza angaza macho,,ghafla akaina sufuria kubwa likiwa jikoni,,ndani yake kulikuwa na supu panoja na viganja vya mikono ya binadamu!! akastuka...akazipiga hatua za tahadhari kulisogelea sufuria hilo...akaona pia kuna masikio ya binadamu pamoja na pua ya binadamu!.....macho yakamtoka,,ghafla akahisi kichefuchefu akatapika,,,akasema,,"MUNGU WANGU!!! INAMAANA SIKUZOTE NAKUNYWA SUPU KWENYE MGAHAWA HUU KUMBE NAKULA NYA YA BINADAMU MWENZANGU...akatoka haraka na kurudi kule kwenye viti walipokuwa wameketi wateja wengine..akatapika tena kwa mara nyingine!!!wale wateja waliokuwemo ndani ya mgahawa huo wakamshangaa mtu huyo.....mteja mmoja akamfuata na kumuuliza ,,"Unaumwa??
mtu huyo hakujibu kitu chochote akanyoosha kidole kukielekezea kule jikoni...wale wateja wakajiuliza ,,mtu yuho anamaanisha nini?? mteja mmoja akaamua kwenda kule jikoni akafungua mlango na kuingia upande wa ndani,,akaangaza angaza macho akaona sufuria kubwa,,ndani yake kuna supu pamoja na viungo vya binadamu,,viganja,,masikio na pua...akastuka akatoka haraka huku akitimua mbio...wale wateja wengine walipo ona mtu huyo anatimua mbio,,wakaamua kwenda kushuhudia...kuna nini huko jikoni..kwa sababu ni kama huduma ya supu na chakula imesitishwa kwa muda wa lisaa limoja sasa...wakafungua mlango wa jikoni,,,,baadhi ya wateja wakaingia upande wa ndani...wakastuka kukuta kunasufuria lina supu ndani yake...pia kuna viungo vya binadamu!!! wakakasirika sana........ikasikika sauti ya mchaga mmoja miongoni mwa wateja hao,,walioingia humo jikoni akaropoka,,,"YELEUUUWI..YESU NA MARIA,,AISEE MEKU...huyu mama anatulisha nyama ya BINADAMU....
wale wateja wakaamua kuchoma moto mgahawa huo..kisha wakatoka nje kwa pamoja na kuingia mitaani kumtafuta MAMA MUUZA SUPU wamuangamize..kwa kitendi hicho cha kuwalisha nyama za binadamu kwa miaka mingi...pasipo wao kujua..
***********************
Upande mwingine kule kwa mzee Mbega alioneka
alionekana,,,Tina akiwa bado ameketi kwenye kiti,,sebuleni,,akaonekana mzee Mbega akitokea chumbani kwake,,Tina akamtazama Mzee mbega wakakutanisha macho,,Tina akastuka,,, akahisi hali ya hatari,,,ghafla kuna fikra ikamuingia kwenye mawazo yake....akukumbuka matukio ya mauwaji yaliyofanywa na mwanamke akinyonga watu kwa kutumia kamba...mawazi hayo yalizunguka ndani ya ubongo wake,,ghafla akamuona mzee Mbega ndani ya fikra hizo zilizokuwa zikizunguka kwenye ubongo wake,,kuwa mzee mbega katoa kipande cha mbao ya mti wa MKARATUSI anamuangamiza yule mwanamke aliyekuwa anafanya mauwaji akinyonga watu kwa kutumia kamba....
TINA akastuka!! akarudi katika fikra zake za kawaida....wakati huo mzee Mbega alikuwa tayari kamkaribia Tina.....
Tina akaona mzee Mbega anaingiza mkono wake ndani ya mfuko wake wa suruali.. ghafla akatoa kipande cha mbao ya mti wa MKARATUSI....
akastuka akauliza kwa mshangao,,"Unataka kufanya nini???kabla hajamaliza kuongea Mzee mbega alipeleka mkono wake uliokuwa umeshikilia kile kipande cha mbao,,moja kwa moja mpaka kwenye kifua cha Tina..
Macho yakamtoka Tina,,huku mdomo wake ukiwa wazi,,akabaki kasimama kama sanamu....ngozi ya Tina ikaanza kubadilika na kuwa ngozi ya mzee,,nywele zake zikaanza kubadirika rangi,,zikawa mvi...uso wake ukakunjamana,,akadondoka chini....akaanza kupukutika kama vumbi linalopulizwa na upepo...hatimae akatoweka kimiujiza...akarudi katika hali ya umauti.....ukawa ndio mwisho wa Tina......wakati huo macho ya mzee Mbega yalikuwa yakitazama ile sehemu alipodondoka Tina na kutoweka....akajisemea moyoni,,"ni bora umerudi mavumbini kuliko ulivyokuwa unaishi duniani bila kujitambua kuwa wewe ni mfu uliyefufuliwa..aliyasema maneno hayo kwa sauti yake ya kizee....akazipiga hatua kurudi chumbani kwake...akakirudisha kile kipande cha mbao,,ghafla ukavuma upepo mkali sana!!! upepo huo ukaezua bati la nyumba yake ukaendelea kuvuma kwa kasi kubwa....Mzee mbega akaingiwa na hofu kubwa...akaamua kutoka nje ya nyumba..kwa kuhofia huenda nyumba ikabomoka akafunikwa na kifusi cha matofali akafa......
alipotoka nje bado aliona upepo ukivuma kwa kasi,,pia vumbi lilikusanywa na upepo huo likawa linapepea hewani...upepo ulikuwa mkali sana ulinyanyua hata vitu vizito..vikawa vinapelekea na angani....huku vikirusha huku na kule...
wakati mzee mbega anatahamaki..kuna kipande cha chuma kilichokuwa kimechongoka,,kilirushwa na upepo huo kikaenda moja kwa moja mpaka kwenye paji la uso la mze Mbega akapoteza maisha papohapo...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****************
Upande mwingine,, kule nchini Nigeria...kule kwenye kaburi alilozikwa Tina...likatikisika na kutoa nyufa za mpasuko kutoka chini ya aridhi...likatokea tetemeko kubwa la aridhi,,tete meko hilo lilisababisha makaburi mengine yakapasuka na kuzama chini ya aridhi...pia baadhi ya nyumba zilizokuwa jirani na maeneo ya makaburini....zilibomoka kwa mtikisiko huo......
watu wakaanza kutimua mbio,,huku wakipiga mayowe kwa hofu.....ndani ya dakikaka chache mji mzima ulikuwa kimya..haikusikika hata sauti ya ndege warukao.....
wakati huo huo..kule kwenye himaya ya mganga matata OBINA....akaanza kupata misukosuko.......kilitokea kimbunga kikiambatana na upepo uliovuma kwa kasi ya ajabu!!!!upepo huo ulitoa mngurumo mkubwa wa kutisha....
Macho yakamtoka Obina...akaamua kuuzuia upepo huo kwa kutumia nguvu zake za kichawi lakini akashindwa....akachukua Tunguri zake na baadhi ya vitu vyake vya muhimu vinavyompa nguvu za kichawi,, ili atimue mbio baada ya kuona mambo yamekuwa magumu....kabla hajafika mbali...ule upepo ukamfuata ukamvuta!! akawa katikati ndani ya kimbunga hicho akizunguka hewani....kisha ukamrusha kule kwenye kaburi la Tina,,Mganga Obina akatumbukia ndani ya kaburi hilo,,,likajifunga na kurudi katika hali yake ya kawaida,,ukawa ndio mwisho wa mganga Obina.....,, kimbuga hicho pamoja na upepo uliokuwa unavuma kwa kasi..ukatoweka,hali ikawa shwari na ukimya ukatawala......
****************
upande mwingine kule mitaani,,walionekana wale wateja waliokuwa wakinywa kila siku supu,, pamoja na nyama choma katika mgahawa wa mzee Sule...wakiwa wameshikilia mapanga na marungu..wengine wamebeba mawe na madumu yaliyokuwa na petroli ndani yake....waliizungukia mitaa yote lakini hawakufanikiwa kumpata Mama muuza supu,,ambaye ndiye mke wa mzee sule..
wakakata tamaa!! wakaanza kutawanyika kila mmoja akipitia njia yake kwenda kuendelea na shughuri zake.....hatimae mkusanyiko huo wa watu ukaisha kabisa......
************************
Upande mwingine kule nyumbani kwa mzee Sule..alionekana akitoka nje ya nyumba yake..akazipiga hatua za tahadhari huku kashikilia shoka kubwa..kuelekea kule alipokuwa ametega mitego ya kumnasa mtu atakayeingia kwenye himaya yake....hakuwa na wasiwasi na familia yake..kwa sababu...huwa wanarudi nyumbani kwa kupitia ile nja ya chini kwa chini ya aridhi...hivyo hakuwa na shaka kabisa....alipokaribia lile eneo alilotega mitego,macho yakamtoka,,,hakuamini kile alichokiona!!! alikuta mkewe kalala chini amekufa kwa kunaswa na ile mitego aliyokuwa kaitega yeye mwenyewe!! alipoangaza angaza macho yake akawaona watoto wake wa pekee nao wakiwa wamekufa kwa mitego hiyo!!! akapiga kelele zaaumivu ya moyo kwa kuiangamiza familia yake yeye mwenyewe pasipo kutarajia......akapaza sauti kwa kusema,,"WEWE ULIYEINGIA KWENYE NJIA YANGU YA SIRI INAYOPITA CHINI YA ARIDHI,,NDIO CHANZA CHA KUONDOKEWA FAMILIA YANGU.....HAKIKA SITOKUACHA UKIWA HAI....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wakati huo huo alionekana Muki akiwa bado kajificha ndani ya kabati la mzee Sule lililokuwela sebuleni,,akitafakari namna ya kufanya ili ajiokoe..kutoka mikononi mwa mzee sule....
kule nje alionekana mzee Sule kazipiga hatua kuelekea mstuni....ghafla akasita akasimama kwa sekunde kadhaa....akaamua arudi ndani kwake akachukue mashine ya kukatia miti(chain sow) iliyokuwa ndani kabati lake kule sebuleni....akaingia ndani,,Uso wa mzee Sule ulionekana kuwa na hasira kali....mpaka mwili wake ulikuwa unatetemeka...macho yake yalikuwa mekundu huku machozi yakimlenga.....akaikaribia kabati akanyanya mkono wake kuushika mlango wa kabati hilo...
Ndani ya kabati alionekana Muki..akitetemeka kwa uwoga..hofu kubwa ilitanda juu yake....akakishikilia kisu chake sanjari..tayari kwa lolote litakalotokea..
Mzee Sule lipotaka kuufungua mlango huo...ghafla akasikia sauti ya mngurumo wa upepo ukivuma kwa kasi!! akasita kufungua kabati hilo..akazipiga hatua kutoka nje ili ashuhudie ni nini kimetokea...
akastahajabu kuona Kimbunga kikubwa angani kimeambatana na vumbi kali....ndani ya kimbunga hicho kulionekana vitu vingi vilivyobebwa na upepo mkali....macho yakamtoka mzee Sule baada ya kuona kimbunga hicho kikija upande wa nyumba yake!!! kutokana na upepo mkali..miti iling'oka na kupeperuka kuelekea angani katikati ya kimbunga hicho....upepo uliendelea kuvuma kwa kasi ya ajabu huku ukizunguka kama gurudumu!!! Mzee Sule akalitupa shoka alilokuwa amelishikia akaamua kutimua mbio akatokomea mstuni....
mule ndani ya kabati alionekana Muki,,akiendelea kusubiri mzee Sule adungue kabati..amchome kisu cha kwenye koo...ghafla akasikia sauti ya mngurumo...akajiuliza,,"mngurumo huo ni wa kitu gani!!? wakati bado anajiuliza..akasikia sauti ya kitu kungo'ka kwenye nyumba hiyo..kumbe kile kimbunga kiliezua batu la nyumba ya mzee Sule..
vitu vilivyokuwa ndani ya nyumba hiyo vikaanza kusombwa na upepo,,, kuvitwa kuelekea angani..ghafla lile kabati likavutwa na kimbunga hicho kuelekea angani......Muki akaingiwa na Hofu kubwa..akahisi anaelea hewani...alipojaribu kufungua mlango wa kabati akashindwa..
kumbe mlango huo ukiufunga haufunguki bila kuzungusha kitasa....na kitasa hicho kipo nje ya mlango!! Muki akahisi kuchanganyikiwa.....
kutokana na upepo kuvuma huku ukizunguka....
vitu vilivyokuwa vimevutwa na kuwekwa katikati ya kimbunga hicho pia vilizunguka....hata lile kabati ambalo alikuwemo Muki ndani yake lilizunguka kwa kasi!!!,, kitendo hicho cha kabati kuzunguka kwa kasi....ule msumeno wa kukatia miti mikubwa(hain sow)ulimgonga Muki sehemu ya kichwani akahisi kizunguzungu akapoteza fahamu akiwa huko angani,,ndani ya kabati hilo!!!
watu walistahajabu...wakaingiwa na hofu wakidhani ni MWISHO WA DUNIA....mji mzima ulichafuka...watu walikimbia mbio kila mtu akipita njia yake..ili kutetea nafsi yake.....
ghafla vikaanza kudondoka vitu kutoka angani.kuja kwenye ardhi!!!.ikiwemo miti mingi mikubwa isiyokuwa na idadi....pamoja na vitu vingi vizito......
***********************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
upande mwingine alionekana mzee Sule akitimua mbio,,,macho yalimtoka! alikimbia bila kujua ni wapi anaelekea..ghafla akaanza kukutana na maiti nyingi zisizokuwa na idadi zikiwa katika hali ya nafsi,,,maiti hizo zilionekana kuwa na huzuni kwenye nyuso zao...zilimtazama mzee Sule kwa macho ya msisitizo....Mzee Sule akapagawa...akaanza kukimbia ovyo..akawa anajikwaa na kudondoka chini mara kwa mara...kila alipokua ana kimbilia bado umati wa maiti hizo zilimfuara kwa nyuma zikitembea....Mzee Sule akazidi kuchanganyikiwa..alikimbia mpaka akachoka..alipokuwa akisimama na ule umati wa maiti ukisimama pia...Mzee Sule akaanza kupiga mayowe ya kuomba msaada lakini hakuna hata mtu mmoja aliyesikia sauri yake..kutokana alikuwa katikati ya pori.....alikimbia mpaka nguvu zikamuishia akasimama...akakata tamaa....alipotazama kushoto kwake...akamuona mkewe pamoja na watoto wake wakiwa wanazipiga hatua muja pale alipokuwa amesimama.....akaanza kuingiwa na amani...alijua familia yake imekuja kumpa msaada.....ghafla familia yake ikatoweka...ikajitikeza tena....
kumbe...hayo yalikuwa ni mawazo ya mzee Sule...akakumbuka kuwa familia yake haipo tena duniani....akaingiwa na hofu,,,akaanza kulia kwa uchungu,,ghafla akaona ule umati wa maiti...ambao ni wale watu aliokuwa akiwauwa kikatiri kwa kumtumikisha Tina kichawi pasipokujijua......na kuwanyonga watu hao......ule umati wa maiti hizo ukaanza kumzunguka mzee Sule na kumuweka katikati...akawa hana sehemu ya kukimbilia.......Akainekana Domy akiwa katika hali ya umauti...akizipiga hatua kumfuata mzee Sule....alipomkaribia akamkamta mzee Sule akamnyofoa macho kwa kumtoboa na vidole vyake..akavuta macho hayo na kuzipiga hatua akasimama kando....Mzee Sule alipiga mayowe....alihisi maumivu makali,yaliyosababisha haja ndogo kumtoka mfululizo...damu nyingi zilimtoka...ikaonekana maiti nyingine..ammbaye alikuwa mmoja kati ya wale walevi wawili akizipiga hatua kumsogelea mzee Sule...alipomkaribia..akamnyofoa mkono kwa kuuvuta mpaka ukang'oka kwenye bega....mzee Sule akapiga mayowe ya kuomba msaada,,lakini hakuna aliyemsaidia......
maiti nyingine ikamfuata na kumnyofoa mkono mwingine...mzee Sule akahisi maumivu ya hali ya juu...alipiga kelele mpaka saiti ikakauka...ikaonekana maiti ya yule jirani yake Domy ikizipiga hatua kufuata mzee Sule na kumnyofoa mguu...Mzee Sule akadondoka chini...alihisi maumivu makali..mpaka mwili ukawa na ganzi,,,akawa ahisi maumivu tena....
ikainekana maiti ya yule fundi aliyekuwa anatengeneza kengere kwenye nyumba ya jirani yake Domy..akizipiga hatua kumfuata mzee Sule kamnyofoa mguu wa pili.....ikaonekana maiti ya Tina ikimfuata mzee Sule kumtoboa kifuani na kuunyofoa moyo wake...Mzee Sule akatulia tuli.. mati zilizobaki zikawa zinanyofoa baadhi ya viungo vya mwili wa mzee Sule mpaka akaisha kabasa..pale alipokuwa amelala pakabaki tupu.....umati huo wa maiti ukatoweka kimiujiza..ukawa ndio mwisho wa mzee Sule....
************************
upande mwingine kule angani...kilipokuwepo kimbunga .....kikatoweka ghafla...ni baada ya mzee Sule kufa... .likaonekana kabati likishuka kutoka angani likatumbukia kwenye bahari.....likawa linaea juu ya maji!!!! kwa mbali walionekana wavuvi wawili wakiwa kwenye mtumbwi
(Wood boat) wakapiga kasia kuifuata kabati hiyo..wakafungua kitasa cha mlango huo..wakastahajabu kukuta binadamu...wakasikiliza mapigo yake ya moyo kifua...wakasikia bado uanapiga....mvuvi mmoja akasema,,"mtu huyu kapoteza fahamu..wakamchukua na kumuingiza ndani ya mtumbwi.....wakaanza kupiga kasia..kuelekea nchi kavu.....kabla hawajafika Muki akazinduka,,alipoangaza macho yake..akastahajabu kujikuta yumo baharini ndani ya mtumbwi...mvuvi mmoja akasema,,"pole ndugu..tumekukuta ndani ya kabati lililokuwa likielea juu ya maji....Muki akashusha pumzi baada ya kugundua kuwa yupo katika mikono salama....baada ya dakika kadhaa Muki alijisikia nafuu kabisa...akaanza kuwasimulia wale wavuvi kilichomtokea......walimuonea huruma ......mvuvi mmoja akasema,,"MUNGU NI MWEMA,HAKUNA LINALOSHINDIKANA MBELE YAKE...POLE SANA NDUGU...KWA MISUKOSUKO ILIYOKUPATA..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muki akasema,,"Asante sana nashukuru kwa msaada wenu MUNGU AWABARIKI..
Muki alifika nyumbani kwake akiwa salama kabisa...akaamua kuacha kuendelea kuifanya kazi ya ufundi seremala...akawa mfanya biashara...aliishi kwa amani na furaha...
*************MWISHO WA HADITHI******
0 comments:
Post a Comment