Search This Blog

NYOKA WA KUTUMWA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : DAVIS NYANDINDI



    *********************************************************************************



    Simulizi : Nyoka Wa Kutumwa

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Katika kijiji kimoja kulikuwa na mzee mmoja aitwae mzee sube , Pia mzee sube alikuwa na mke ambae alikuwa anaitwa Dae { Bibi sube }. Mzee sube pamoja na mke wake walikuwa wanajishughulisha na kilimo maana awakuwa na uwezo, Maisha ya mzee sube pamoja na mke wake yalkuwa ni magumu japokuwa walikuwa wanajishughulisha na kilimo. Mzee sube pamoja na mke wake walikuwa ni wachawi wakubwa sana hapo kijijini kwao ila watu wa hiko kijiji walikuwa awafahamu kuhusu jambo hilo. Siku moja mzee sube alimuita mke wake na kuaanza kuongea nae kitu fulan kuhusu maisha yao.

    MZEE SUBE: Mke mimi nimekuita hapa kuna kitu nataka tuongee.

    BIBI SUBE: Kitu gani hiko mume wangu.?

    MZEE SUBE: Kuna wazo nimelipata maana naona aya maisha tunayoishi sio mazur hata kidogo na wakati sisi ni watu wakubwa sana hapa kiijini.

    BIBI SUBE: Ni kwel mume wangu yani hata mimi aya maisha nimeyachoka kabisa.

    MZEE SUBE: Basi leo ndio itakuwa mwisho wa haya maisha magumu.

    BIBI SUBE: Aya basi nambie hilo wazo lenyewe mume wangu .

    MZEE SUBE: Mke wangu kuna kitu nataka tukifanye na kitu kitatufanya sisi tujulikane na tuwe watu wakubwa sana hapa kijijini na kila mtu ajue kuwa sisi ni wakina nani na huo ndio utakuwa mwanzo wa kujulikana kwetu na kufanikiwa pia.

    Bibi sube baada ya kuambiwa vile akajikuta akiwa anashauku kubwa ya kutaka kujua hiko kitu chenyew kitakacho wajulisha wao katika kile kijiji chao.

    BIBI SUBE: Bas niambie kitu chenyewe mume wangu maana unafanya niwe na furaha hata kabla sijambiwa kitu chenyewe.

    MZEE SUBE: Mimi nataka kutengeneza nyoka ambae atakuwa anang'ata watu .

    BIBI SUBE: Heee!! Ili kiwe nini mume wangu?

    Bibi sube alishangazwa kidogo na lile wazo la mume wake maan akutegemea kama angesema wazo kama llile.

    MZEE SUBE: Na mimi nilijua tu kuwa nikikuambia lazima ushangae kwa kuwa aujajua faida yake hapo baadae. nataka kumtengeneza nyoka na awe anauma watu na endapo utakuwa umeumwa na huyo nyoka itabidi uje uchukue dawa kwangu na hiyo dawa sitatoa bure bali nitakuwa naiuza kwa kubadilisha na chakula, je hilo sio wazo zuri ?

    Bibi sube baada ya kuulizwa vile alikaa kimya kidogo na kisha akajibu.

    BIBI SUBE: Unajua mume wangu mimi wala sikufkilia kama unataka kufanya hivyo nilidhani unataka kuwakomoa wanakijiji ili wakujue kuwa wewe ni nani ila kama ndio hivyo basi ni vizur tu mume wangu.

    MZEE SUBE: Na ndio maana nakupenda sana mke wangu kwa kuwa ni muelewa na unapenda sana kusikiliza mawazo yangu na kuyafanyia kazi.

    BIBI SUBE: Sawa nashukuru mume wangu kwahiyo hyo kaza ya kumtengeneza uyo nyoka itaanza lini?

    MZEE SUBE: Inatakiwa tufanye leo hii hii tena usiku katika ule mda wetu wa kazi.

    BIBI SUBE: Aha sawa nimekuelewa mume wangu na nitafanya utakalo wewe.

    Basi baada ya kukubaliana vile kila mtu akaendelea na shughul zake za kila siku. Masaa yalipita na hatimae ukafika ule mda ambao mzee sube pamoja na mke wake walipanga kufanya shughuli yao ya kumtengeneza huyo nyoka wako. Mda ulipofka mzee sube alivaa kaniki na kichwan akajifunga kitambaa chekundu, pia bibi sube alikuwa amevaa kitambaa chenye rangu nyekundu na kichwani akajfunga kaniki. Mzee sube alikuwa ameshika ukili pamoja na nyumbu huku bibi sube akiwa amebeba vibuyu viwili vyenye unga wenye rangi ndani yake, kibuyu kimoja kiliwa na unga mweusi na kibuyu kingne kIlikuwa na unga mwekundu. Baada ya hapo wakatoka na kwenda nyuma ya nyumba yao ndipo mzee sube akachukua ule ukili na kuuweka chini kisha akachora chini kitu chenye umbile la nyoka likiwa limeizunguka ule ukil. Baada ya hapo bibi sube akachukua ule unga mweusi na kuanza kutia kwenye ule ukili, baada ya hapo ndipo mzee sube akaanza kuongea maneno fulan ya kichawi na baada ya kumaliza ndipo bibi sube akachukua unga mwekundu na kumiminia tena kwenye ule ukili. Baada ya kufanya vile mzee sube akachukua ule ukili na kwenda kwenye kichaka ambacho kilikuwa karibu sana na ile nyumba yao. Wakaanza kukizunguka kile kichaka huku wakiwa wanaimba nyimbo zao za kichawi. Sasa wakiwa wanafanya vile ghafla waliona manyasi ya kile kichaka yakiwa yanatikisika kumaanisha kuwa ule ukil alikuwa ushabadilika na kuwa nyoka kama walivyodhamilia wao. Mzee sube alienda kwenye kile kichaka na kumtoa yule nyoka. Kiukwel alikuwa ni nyoka mkubwa sana mwenye rangi ya blue yenye kung'aa huku mkian kwake pamoja na akichwan akiwa na rangi ya njano. Mzee sube baada ya kumchukua yule nyoka akaenda kumuweka sehemu ya wazi na kuanza kumnuia maneno fulani ya kumuongoza yule nyoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MZEE SUBE: Wewe nyoka nimekutengeneza kwa ajili ya kazi moja tu ya kuwadhuru watu wa hiki kijiji cha MBAKA. Pia nataka ufanye kile nitakachokuambia ufanya na mimi ndio nitakae kuongoza na hiki kichaka ndio itakuwa nyumba yako na kuanzia leo nakupa jina lako ni YOKA .

    Alipomaliza kumnenea, akambeba yule nyoka na kumrudisha tena pale kwenye kichaka ila alipomuweka tu ghafla yule nyoka akabadlika na kurudi tena kuwa ukili. Jambo lile lilimfurahisha sana mzee sube maana aliona kuwa kafankiwa kwa asilimia mia katika kumtengeza yule nyoka. walipo maliza kufanya vile ndipo mzee sube pamoja na mke wake wakaondoka na kwenda ndani kupumzika huku wakiwa wanafuraha sana ya kufanikisha jambo lao, kwahiyo ile siku ikapta na kuja siku nyingne. Iipofka asubuhi mzee sube aliamka mapema sana na kuelekea kweye kile kichaka kwa ajili ya kumuangalia yule nyoka wake. Alipofika kwenye kile kicha aliukuta ule ukili kama alivyouacha jana usiku. Baada ya kuona vile ndipo mzee sube akasema maneno na kuuambia ule ukili.

    MZEE SUBE: Usibadilike mpaka nitakapo kuruhusu mimi na endapo utakimbizwa na mtu wowote kimbilia hapa nyumban kwako.

    Baada ya kusema vile ghafla ule ukili ukabadilika na kuwa nyoka na mda huo huo ukubadilka tena na kuwa ukili. Kitendo kile kilmfurahsha sana mzee sube maana alijua moja kwa moja kuwa Yoka amekubali kile kitu alichoambiwa. Baada ya hapo mzee sube alitoka pale kwenye kichaka na kurudi zake ndan. Alipofka alimkuta mke wake akiwa anachemsha uji kwa ajili ya kupasha tumbo joto ila waendelee na majukumu mengne. Mzee sube alipofka akaanza kuongea na mke wake.

    MZEE SUBE: Habar yako mke wangu.?

    BIBI SUBE: Mzuri tu mume wangu.

    MZEE SUBE: Umeamkaje?

    BIBi SUBE: eeee mume wangu kwani tulilala pamoja jaman ila maswal unayo niulza utazan nilienda kulala kwa jirani ( bibi sube aliongea kwa kumdhihaki mumewe )

    MZEE SUBE: Hata kama tumelala pamoja je kama umeamka huku ukiwa unaumwa?

    BIBI SUBE: Si ningekuambia mume wangu kipenz.

    MZEE SUBE: Aya mama umeshinda wewe maana uking'ang'ania kitu ukubali kushindwa.

    BIBI SUBE: Hahahaha sawa. Ehe mume wangu tuachane hii mada vipi ulienda kumuangalia YOKA?

    MZEE SUBE: Ndio tena sahizi ninatoke huko huko kumuangalia.

    BIBI SUBE: Ehe anaendeleaje?

    MZEE SUBE: Nimemkuta yupo kama tulivyomuacha jana usiku kwahiyo inaonesha kuwa ile sehemu ni salama.

    BIBI SUBE: Mh afadhali maana usiku wala sikulala kwa amani maana nilikuwa nahofia sana ile sehemu maana siunajua ni njiani pale ?

    MZEE SUBE: Basi ndio hivyo pale ni sehemu salama japokuwa n barabarani .

    BIBI SUBE: Basi kushukuru.

    MZEE SUBE: ndio hivyo ila leo tuna kazi ya kwenda msituni kuchimba dawa ya kuwatibia watu baada ya kubanwa na YOKA.

    BIBI SUBE: Alafu ni kweli basi ngoja nipike haraka haraka twende.

    Basi baada ya hapo bibi sube alipika haraka haraka kama alivyo sema alipomaliza walikula na baada ya kumaliza ndipo safari ya kwenda msituni ikaanza. Sasa wakiwa njia mzee sube alianza kumwambia mke wake dawa ambayo inatafaa kumtibia mtu ambae ameng’atwa na yoka.



    MZEE SUBE: Ehe unaijua dawa ambayo tunatakiwa tukaichukue kule msitun?

    BIBI SUBE: Ndio naijua si ile dawa ya kuondoa sumu ya nyoka mwilini.

    MZEE SUBE: Hapna sio hiyo, dawa inayotakiwa ni ile inayoweza kumrudisha Yoka kwenye ile hali ya ukil. Hiyo ndio dawa ya kuitafuta na ndio itaponyesha mtu.

    BIBI SUBE: e kumbe mimi nilikuwa sifahamu.

    wawili wale waliendelea kupiga stori na hatimae wakafika msitun, mzee sube alielekea moja kwa moja mpaka kwenye mti mmoja mkubwa na kuanza kuchimba mizizi ya ule mti. Bibi sube alipoona kuona vile na yeye akaanza kuchimba ile mizizi ya ule mti. Mda wote wakati wanachimba ule mti akukuwepo na hata mmoja wa kumuongelesha mwenzake wote walikuwa bize na kuchimba ile mizizi pia ilikuwa ni sheria ya ule msitu, endapo unaenda kuchimba mizizi ya dawa hautakiwi kuongea na mtu wowote wala kitu chochote pale msituni. Wakati wanachimba ile mizizi ghafla bibi sube aliona mti fulan mbele yake ambao ulitokea kumvutia sana, kwahiyo alipomaliza kuchimba ule mti wa kwanza ndipo akaenda kuchimba mizizi miwili ya ule mti alio uwona . Jambo lile llmshangaza sana mzee sube na kumfanya awe na maswali mengi sana maana ule mti akiochimba mwenzake sio ambao ukitakiwa. Kitendo kile kilmfanya mzee sube atamani kumuulza maswali mke wake lakini alishindwa kumuuliza kwa sababu ya taratibu ziliZopo pale msituni . Bibi sube aliendelea kuchimba ule mti na hatmae akamaliza Ndipo wakachukua vile vifaa vyao na kuanza kurudi nyumbani kwao. Walitumia mda mrefu kidogo kutoka nje ya ule msitu maana huo mti ulikuwa katikati na mara baada ya kutoka ndipo mzee sube akaanza kutoa lile dukuduku lake kutaka kujua kwanini alikuwa anachimba ule mti na wakati alikuwa lengo lao kufanya vile.

    MZEE SUBE: nataka nikuulze kitu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    BIBI SUBE: Mh kitu gani hiko ( bibi sube aliongea kwa wasiwasi )

    MZEE SUBE: Hivi unaweza kuniambia kuwa kwanini ulikuwa unachimba ule mti mwingine na wakati aikiwa lengo, Tena nilitamani nikulize pale pale ila sheria za mzimu ndio zilinibana.

    BIBI SUBE: Na mimi nilijua tu lazma uniulize maana nilikuona jinsi ukivyoniangalia kwa kunishangaa ila ule mti mimi nlikuwa nataka kufanyia kazi yangu Fulani tofauti na hii.

    MZEE SUBE: Aha maana nilishangaa sana kuona vile.

    Walipomaliza kuongelea ile mada, waliendelea na safari yao huku wakiendelea kupiga stor zingine za hapa na pale. Walitumia masaa mawil kutembea na hatimae wakafika nyumban kwao na moja kwa moja wakaanza kuitengeneza ile dawa yao. Wakati wanatengezea ile dawa ndipo bibi sube akaanza kumuongelesha mume wake juu ya ile jambo lao.

    BIBI SUBE: Mume wangu hivi wewe unajisikiaje tunavyofanya jambo hili .

    MZEE SUBE: Ninafura kupita kiasi maana najua siku sio nyingi na sisi tutakuwa tunaishi kama wafalme hapa kijijini.

    BIBI SUBE: Ni kweli lakini kwa upande wangu nusu nafurahia ila nusu nyingine sifuriha. Maana unakumbuka kilchompata mzee sui pamoja na mtoto wake Ama { mzee sui na Ama ni wahusika katika simulizi ya kwanza ihusuyo hiki hiki kijiji cha mbaka }. Sasa mimi naogopa sana maana isije ikatutokea kama yaliyowapata wenzetu na kama unavyojua jinsi sheria za hiki kijiji chetu cha mbaka zinavyowabana watu wabaya.

    MZEE SUBE: Sawa ila siku zote kwenye maisha ukitanguliza kufikiria hasara hauwezi kufankiwa kamwe.

    BIBI SUBE: kwahiyo unamaanisha nini maana sijakuelewa.

    MZEE SUBE: Nina maanisha ukitaka kufanya jambo lolote usianze kufikilia madhara au matatizo yanayoweza kukupata katika utendaji wa hilo jambo na kuhusu mzee sui na mwanae ule ulikuwa ni uzembe wao wenyewe na ndio maana wakauawa. Ila mimi sitakuja kufanya uzembe kama ule.

    BIBI SUBE: Sawa nimekuelewa.

    Waliendelea kutengeneza ile dawa na hatimae wakafanikiwa kumaliza ndipo mzee sube akaanza kumwambia mke wake juu ya jambo ambalo wanatakiwa kulifanya ifkapo usiku.

    MZEE SUBE: Kama unavyoona dawa ipo tayari kwahiyo leo usiku tunatakiwa tuanze kumruhusu Yoka kufanya kazi yake maana dawa iko tayari.

    BIBI SUBE: Sawa.

    MZEE SUBE: Sawa basi ngoja nikuache ninaenda kule mwemben kucheza bao.

    BIBI SUBE: Sawa mume wangu ila usichelewe kurudi maana mda sio mrefu chakula kitakuwa tayari.

    MZEE SUBE: sawa nmimekuelewa.

    Mzee sube akaondoka na kumuacha mke wake akiwa anaanda chakula cha mchana ila baada ya kuona mume wake ameondoka ndipo akachukua ile dawa yake ya mti mwingine na kuanza kuitengeneza na hatimae akamaliza akaichukua na kwenda kuificha ndani sehemu ambayo mzee sube asingeweza kuiyona. Baada ya hapo akaendelea na mapishi na hatimae akamaliza na mara mume wake akarudi nyumban kwa ajili ya kula. Bibi sube akapakuwa kile chakula na kuanza kula walipomaliza wakaenda kupumzika huku wakisubiria kwa hamu usiku uingie ili wakaifanye ile kazi yao. Kuanzia hapo masaa yalinda haraka hatimae ikafika usiku, Ndipo mzee sube pamoja na mke wake wakavaa zile nguo zao za kichaw na kwenda nyuma ya nyumba yao huku bibi sube akiwa amebeba vile vtu alivyokuwa amebeba ile siku ya kwanza. Walipofika ndipo mzee sube akaanza kumuita yule nyoka kwa jina ambalo alikuwa amempatia, ila alikiwa anaita kwa sauti ya chini huku akipiga na mluzi. Alipofanya vile ghafla ule ukili kule kichakani ukabadilka na kuwa YOKA na kuelekea nyuma ya nyumba ambako alikuwa ameitwa. Alipofika ndipo mzee sube akaanza kuongea na yule nyoka wake.

    MZEE SUBE: Nimekuita hapa kwa ajili ya kukupa ruhusa ya kuanza kuifanya kazi ambayo imefanya mimi nikutengeneze yani ni kuwadhuru watu wa hiki kijiji cha mbaka. Ila kumbuka kitu kimoja kile kichaka ndio nyumba yako na kila ifikapo saa kumi na moja alfajiri unatakiwa uwe usharudi pale kichakani .

    Baada ya kusema vile akachukua unga mweusi ambao alikuwa ameushika mke wake na kuanza kumpaka huku akimnuia maneno fulani.

    MZEE SUBE: Huu unga niliokupaka utakuwa unakusaidia wakati ukiwa katika matatizo, utakusaidia kupotea au kubadilika na kuwa ukili.

    Aliposema vile akachukua unga mwekundu na kumpaka kinywani huku akimnuia maneno mengine.

    MZEE SUBE: Huu unga nakupaka kwa ajili ya kukufanya uwe mkali na uwe na hasira mda wote na kwa kila mtu unaemuona kasoro mimi pamoja na mke wangu.

    Baaada ya kufanya vile akamruhusu aende.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MZEE SUBE: Aya sasa uko huru kwenda kokote ila usisahau kila kitu nilchokuambia.

    Baada ya kusema vile akamalizia kuongea maneno ya kichawi na ndipo Yoka akaondoka na kwenda kuianza kazi yake aliyotumwa. Yoka baada ya kuondoka ndipo mzee sube pamoja na mke wake na wao wakaelekea ndani kwa ajili ya kupumzika maana walikuwa washamaliza kazi yao kwa siku ile. Sasa Yoka akiwa akatika mawindo yake akapita karibu na nyumba moja ambayo ilikuwa karibu sana na nyumba ya mfalme na kubahatika kumuona kijana mmoja akiwa anatoka ndani ya nyumba yao, ndipo akaanza kummendelea { kumvizia } yule kijana ili akamuume. Huyo kijana bila kujua akasogea mpaka karibu na sehemu ambayo Yoka alikuwa amekaa akimvizia, ndipo yoka akaruka na kumbana yule kijana mguuni , kijana aligumia sana na kuanza kuangalia chini ili aone ni kitu gani ambacho kilikuwa kimemng'ata ila kwa bahat mbaya akufanikiwa kuona maana yoka baada ya kufanya vile tu akapotea. Ndugu wa yule kijana baada ya kusikia ile sauti ya ndugu yao ikipga kelele walitoka nje haraka na kwenda kuangalia kilichompata. Walipofika walimkuta ndugu yao akiwa amekaa chini huku akiwa amejishika mguuni, wakaanza kumuuliza maswali nini kimempata ndipo akaanza kueleza kilichomtokea.



    NDUGU 1: Kaka kwani umepatwa na tatizo gani?

    KIJANA: Mimi sijui jamani ila nahisi kuna mdudu ameniuma lakini sijajua ni mdudu gani nilipoangalia chini sikumuona.

    NDUGU 2: sasa itakuwa nini hiko?

    KJNA: hata sijui . { alijibu huku akiwa analia kutokana na maumivu makali ambayo alikuwa anayapata }

    NDUGU 1: Basi tumpeleke ndani ili tuone hiyo sehemu aliyobanwa maana hapa atupaoni kutokana na hili giza.

    Ndugu yake mwingine alitoa hilo wazo baada ya kushindwa kuona sehemu alipokuwa ameumia kutokana na giza nene lililope sehemu ile. Walimchukua yule kijina na kumpeleka ndani kuangalia hiyo sehemu ambayo alikiwa ameng'atwa, wakamuweka karibu na taa na kuanza kumkagua wakabahatika kupaona sehemu ambayo yule ndugu yao alikuwa ameng'atwa maana ilikuwa inamatobo manne pia ilikuwa nyeusi kama amepaka masizi. Kutokana na ile hali walioina kwenye kile kidonda moja kwa moja wakagundua ndugu yao alikuwa kabanwa na nyoka tena mwenye suma kali, ndipo wakaanza kutafuta dawa za kumsaidia kupunguza maumivu na kufanya ile sumu isiendee kumletea matatizo zaidi mwilini mwake. Waliangahika huku na kule kwa majirani zao wakitafuta dawa ya kumsaidia ndugu yao hatimae wakafanikiwa kuipata kisha wakampatia. Kwa mawazo yao walidhani kama wamefanikiwa kumsaidia ndugu yao kwa kumpatia ile dawa kumbe ilkuwa tofauti kabisa maana siku iliyofuatia asubuhi walimkuta ndugu yao akiwa ana hali mbaya na kile kidonda kikiwa kimechimbika na nyama ya ile sehemu kuoza. Jambo lile liliwashangaza sana wale ndugu zake maana ile dawa ambayo walimpatia usiku ilikuwa mzuri kwa kutibia sumu ya nyoka. Walipoona vile wakamchukua ndugu yao na kwenda nae kwa tabibu wa kijiji kwa ajili ya kupata dawa ambayo ingezeweza kumsaidia ndugu yao, walipofika wakamuelekeza kila kitu kilichompata ndugu yao.

    NDUGU 1: Tabibu tumekuja tumemleta huyu ndugu yetu kapatwa na matatzo.

    TABIBU: Matatizo gani ? { Aliuliza huku akimtazama mgonjwa }

    Baada ya kuuliza vile ndipo wale ndugu wa yule kijina wakaanza kumsimulia.

    NDUGU 1: Hayo matatizo amepata usiku wakati ameenda kujisadia na mwenyewe amesema kuna mdudu amemng'ata na sisi baada ya kumuangalia vizuri tukagundua kuwa kabanwa na nyoka. Kwahyo tukamtafutia ile dawa ya kutulizia maumivu pamoja na kupunguz a makali ya sumu tukampatia tukiamini kuwa tumemsaidia ndugu yetu cha ajabu leo asubuhi tumeamka tumemkuta akiwa kwenye hii hali.

    Walipomaliza tabibu akaanza kuangalia kile kidonda cha yule kijana na kuwaeleza alichokiona yeye.

    TABIBU: Jamani nimekiangalia kile kidonda inaonyesha ni kweli kang'atwa na nyoka tena mwenye sumu kali ila sasa kinacho nishangaza, kama mulimpa dawa kwanini awe kwenye hali kama ile maana mimi ninavyoijua dawa ile hata kama ukabanwa na nyoka wa aina gani endapo utaitumia lazima upate uafadhali sasa imekuaje kwa huyu mwenzenu ? { Aliongea kwa mshangao mkubwa }

    NDUGU 1: Na ndio maana hata sisi tumeshangaa.

    TABIBU: Alafu mbona kile kidonda chake kimechimbika vile na nyama yake naona imekuwa nyeusi sana imekuwaje ?

    NDUGU 2: Hata hatufahamu na ndio maana tumekuja kwako ili utusaidie.

    TABIBU: Mh hili ni tatizo kubwa na mimi wala sina dawa ya kumsaidia kutokana na tatizo lake maana dawa niliyonayo mimi ndio kama mliotumia huko kwenu.

    Walipojibiwa vile waliumia sana na kuanza kumuangalia ndugu yao kwa huzuni, lakini hawakukata tama waliendelea kumuuliza tabibu maswali zaidi ili wapate msaada kwa ndugu yao.

    NDUGU 2 : Kwahiyo tufanye nini maana sisi tunakutegemea wewe.

    TABIBU: Mimi ninaona bora tumpeleke kwa mfalme ili atangazie watu kama kuna mtu atakaweza kumsaidia kabla ajapata madhara makubwa.

    Aliposema vile wote walikubali na kumchukua yule ndugu yao na kumpeleka nyumbani kwa mfalme kwa ajili ya kuwatangazia watu ili wamsaidie kumpa dawa za kumponyesha.

    Walipofka kwa mfalme wakasalimiana nae kisha tabibu akaanza kumwambia mfalme juu ya tatizo lililomkuta yule kijana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    TABIBU: mtukufu mfalme huyu kijina kapatwa na matatizo jana usiku.

    Mfalme alishangaa kusia vile maana hata siku moja yule tatbibu hakuwai kumpeleka mgonjwa pale kwake,.

    MFALME: Matatizo gani hayo tabibu?

    TABIBU: Jana usiku huyu kijana alitoka nje kujisahdia ila kwa bahati mbaya aling'atwa na mdudu na baada ya kumchunguza vizuri tukagundua aling'atwa na nyoka. Ila cha ajabu amepewa ile dawa ya kuzuia sumu ya nyoka ila hali yake bado imekuwa mbaya zaidi.

    MFALME: Sasa wewe ndio tabibu wa hiki kijiji cha mbaka unamsaidiaje huyu kijana?

    TABIBU: Kusema kweli mtukufu mfalme mimi nimeshindwa kumsaidia kwa sababu dawa niliyonayo mimi ndio ambayo amepewa na haikumsaidia ndio maana nikaona bora nimlete kwako ili uwatangazie wanakijiji wengi waje kumsaidia.

    MFALME; Sasa kama wewe umeshindwa nani ataweza kumsaidia na wakati wewe ndio unategemewa hapa kijijini.

    TABIBU; Ni kwel mtukufu mfalme ila kwa hili lpo nje ya uwezo wangu na ndio maana nikaona bora uwatangazie watu wengine ili waje wamsaidie kama wao wataweza.

    MFALME: Sawa nmekuelrwa.

    Mfalme akamuagiza kijina apige ng'oma ya dharula kwa ajili ya kuwaita wanakijiji katika ule uwanja wao wa mkutano, kijana akafanya kama alivyo agizwa. Wakati inapigwa ile ng'oma mzee sube pamoja na mke wake walibahatka kuisikia ile sauti na moja kwa moja wakahisi kuwa labda Yule nyoka wao mwenye jina la YOKA alikuwa kafanya kazi yake ambayo alikuwa ametumwa, mzee sube akamuomba mke wake abaki pale nyumbani na yeye aende huko kwa mfalme.

    MZEE SUBE : Mke wangu hiyo ng'oma inayopigwa huko nahisi kunatatizo limetokea kwa mfalme alafu kichwani mwangu naona hilo tatizo kama kalisababsha Yoka.

    BIBI SUBE: Yani kama ulikuwa kichwani mwangu hivi maana hata mimi ninmehisi hivyo hivyo

    MZEE SUBE: Sasa tufanye kitu kmoja mimi ngoja niende alafu wewe baki hapa nyumbani chochote kitakachotokea kule nitakuja kukuambia.

    BIBI SUBE: Sawa safari njema ila kuwa makini.

    MZEE SUBE: Wala usijari mke wangu.

    Mzee sube akatoka nje na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwa mfalme, alijtahi kutembea haraka sana na hatimae akafika na kuwakuta watu wengine wameshafika pale uwanja ndipo mfalme akasimama akawasalimia wanakijiji na kuanza kuongea juu ya jambo ambalo limfanya awaite pale.

    MFALME: Jamani wananchi wa hiki kijiji cha mbaka nimewaita hapa kwa ajili ya jambo moja na ninahitaji msaada wenu juu ya jambo hili.

    Mfalme baada ya kusema vile ndipo wanakijiji wakaanza kutazamana huku wengine wakiwa wananong'ona wakiulizana Ila kwa upande wa mzee sube moyo wake ulikuwa unaenda mbio na hakutaka kuongea na mtu yoyote bali alikuwa makini kusikiliza anachokisema mfalme, wanakijiji waliponyamaza mfalme akaendelea kuongea.

    MFALME: Jambo lenyewe ni hili , hapa kuna kijana ameletwa ameumwa na nyoka na alipewa ile dawa ambayo huwa tunaitumiaga kuuwa sumu ya nyoka ila bado hali yake mbaya .Kwahiyo mimi sipo tayari kumpoteza huyu kijina kama kuna mtu anadawa ya kumsaidia naomba ajitokeze ila iwe tofauti na ile dawa ya kijiji iliyotengenezwa na mababu zetu.

    Mzee sube aliposikia vile moyo wake ulilpuka kutokana na furaha ambayo alikuwa nayo, haraka bila uwoga akapita mbele na kumueleza mfalme kuwa yeye anaweza kumsaidia yule kijana, Mfalme alifurahi sana kusikia vile mda huo wananchi walikuwa wakinong’onezana kutoka na mzee sube kujitokeza.

    MZEE SUBE: Mtukufu mfalme mimi ninaweza kumsaidia huyo kijana.

    MFALME: Kweli mzee ?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MZEE SUBE: kweli mtukufu mfalme.

    MFALME: Aya mzee anza kazi na endapo utafanikiwa kumsaidia huyu kijana nitakupatia zawadi.

    MZEE SUBE: Sawa mtukufu mfalme ila naomba uniruhusu nikachukue dawa yangu nyumbani ninakuahidi huyu kijna atakuwa mzima kabisa.

    MFALME: Sawa fanya haraka kabla hatujampoteza huyu kijana.

    Baada kuruhusiwa akakimbia haraka na akafanikiwa kufika nyumbani kwake na kumkuta mke wake akiwa amekaa kwenye mkeka ajui hili wala lile linaloendelea kwenye mkutano kule kwa mfalme. Alipofika alikuwa anahema haraka haraka kutokana na kukimbia kwa speed { haraka } Baada ya kukaa sawa ndipo akamsimulia mke wake kwa ufupi kilchotokea kwa mfalme.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog