Search This Blog

NYOKA WA KUTUMWA - 2

 





    Simulizi : Nyoka Wa Kutumwa

    Sehemu Ya Pili (2)



    …………….ilipoishia………………………

    Baada kuruhusiwa akakimbia haraka na akafanikiwa kufika nyumbani kwake na kumkuta mke wake akiwa amekaa kwenye mkeka ajui hili wala lile linaloendelea kwenye mkutano kule kwa mfalme.

    ............ inaendelea …………………….

    Alipofika alikuwa anahema haraka haraka kutokana na kukimbia kwa speed { haraka } Baada ya kukaa sawa ndipo akamsimulia mke wake kwa ufupi kilchotokea kwa mfalme.

    MZEE SUBE: Mke wangu tumefanikiwa tena kwa asilimia elfu kumi maana mia ni ndogo.

    BIBI SUBE: Kwanini maana umenishtua sana ulivyokuwa unakuja nilihisi unakimbizwa.

    MZEE SUBE: Sio nakimbizwa ila hii ni furaha maana mfalme amekubalia nikamtibu mtu ambae kang'atwa na yoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    BIBI SUBE: Heee! Mume wangu kweli ?

    MZEE SUBE: Kweli Hivi hapa unavyoniona nimekuja kuchukua dawa na kuondoka.

    BIBI SUBE: Kama ndio hivyo na mimi ninakuja huko huko.

    MZEE SUBE: Yani hata kama utataka kuibeba mpaka nyumba uje nayo wewe beba twende, Kwanza ngoja nikachukue dawa ili twende kabla sijachelewa.

    Akaingia ndani na kwenda kuichukua ile dawa yake, alipotoka bibi sube na yeye akaenda chumbani akuchelewa akatoka wakaanza safar yao ya kwenda kwa mfalme. Kutokana na mwendo wa haraka waliokuwa wanatembea wakafanikiwa kufika mapema nyumbani kwa mfalme na kuwakuta watu wakiwa wanasubiria. Ndipo mzee sube akamuweka vizur yule mgonjwa huku akisaidiwa na mke wake, akachukua ile dawa yake na kumtia kwenye kidonda na nyingine akamnywesha. Walikaa kwa dakika kadhaa wakisubilia yule kijina apate afadhali ila cha ajabu hali yake ilizidi kuwa mbaya jambo ambalo lilimshangaza sana mzee sube. Bibi sube alipoona vile akatoa ile dawa yake na kumpatia mume wake ili amnyweshe yule mgonjwa, Sube akachukua ile dawa na kumnywesha zikapita dakika kama mbili yule kijina akazinduka maana alikuwa kama mtu aliezimia. Jambo lile llmshangaza sana mzee sube na kujikuta akimuangalia mke wake kwa jicho la mshangao kumaansha kuna kitu alihitaji kumuuliza lakini alishindwa kutokana na kuwepo kwa watu karibu yao. Wanakijiji pamoja na mfalme walifurahi sana kuona yule kijana amepona, ndipo mfalme akaanza kuongea na wanakijiji huku akiwa anamshukuru sana sube pamoja na mke wake.

    MFALME: Wakijiji kwanza nina furaha sana juu ya uponyaji ambao kaupata huyu kijna pia napenda kutoa shukrani zangu nyingi kwa huyu mzee pamoja na mke wake maana jambo ambalo wamelilifanya sio kwamba limemsaidia huyu kijana tu bali na wanambaka wote. Maana huyu kijina anaweza kuwa askari au mfalme na akasaidia hiki kijiji chetu huko mbeleni. Kwahyo jambo alilolinya huyu mzee la kupongezwa sana na kila mtu.

    .

    Mfalme aliposema hivyo wanakijiji wakaapiga makofi kwa ajili ya kumpongeza mzee sube, Lakini wakatii wanakijiji wanapiga makofi, Sube alikuwa mbali sana kimawazo kutokana na kile kitendo ambacho amekifanya mke wake. walipoacha kumpongeza, mfalme akamtangaza rasmi mzee sube ndie atakaekuwa tabibu mkuu pale kijijini kutokana na ule msahada ambao alikuwa ameufanya.

    MFALME: Sasa baada ya kumpongea kwa maneno na kwa kumpigia makofi, mimi nataka nimpe zawadi nyingine nampa cheo cha kuwa tabibu mkuu hapa kijijini kwetu maana inaonesha anazijua dawa nyingi ambazo zitaweza kutusaida.

    .

    Maneno ya mfalme yalimfanya mzee sube afurahi sana maana aliona malengo yake yamekwisha timia. Mfalme alihailisha ule mkutano na kuwaambia watu wakaendele kufanya shughuli za zingine za kuleta maendelea pale kijini kwao, Wanakijiji baada ya kuondoka ndipo akamuita mzee sube na kuanza kuongea nae.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MFALME: Mzee wangu kutokana na cheo ambacho nimekupa unatakiwa ukae karibu na hapa nyumbani kwangu ili wanakijiji wakipatwa na matatizo iwe rahisi kukupata.

    Wazo la mfalme na maneno yake yalikuwa ni mazur sana ila kwa upande wa Sube alikuwa wazo zuri hata kidogo maana aliona kama angeamia karibu na mfalme ingekuwa rahisi kumgundua kuwa yeye ndio msababishaji wa yote maana asingekuwa na sehemu ya kumtunza yule nyoka wake.

    MZEE SUBE: Ni wazo zuri mtukufu mfalm ila mimi ninaona bora nibaki kule kule maana ni karibu na msituni kwahiyo nitakuwa napata dawa kwa urahisi kuliko nikija kukaa huku itakuwa mbali na msituni.

    Sube baada ya kupinga wazo lile, mfalme alimlazimisha lakini haikuwezekana alizidi kupinga na kutoa sababu zake nyingine ambazo zilifanya mfalme akubali kumuacha aendelee kukaa kule nyumbani kwake.

    MFALME: Sasa kama ukihitaji dawa utakuwa unawatuma vijana ambao watakuwa wakikusaidi.

    MZEE SUBE: Sawa ila kwa hizi kazi sio rahis kumtuma mtu akakuchukulie dawa msituni na akakuletea kama unayohitaiji wewe. Kwahiyo usijari mtukufu mfalme nitafanya kazi kwa ufasaha zaidi japokuwa nitakuwa naishi mbali na eneo lako na mda wowote utakao nihitaji haraka nitawaslii.

    MFALME: Sawa nimekuelewa.

    Walipomaliza maongezi yao sube akamchukua mke wake na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao, wakiwa njiani ndipo akaanza kuuliza kuhusu ile dawa.

    MZEE SUBE: Ehe mke wangu nimekumbuka kitu nataka uniambie ile dawa wewe uliipata wapi?

    BIBI SUBE: Hahaha wewe unajifanya kujua dawa sasa ilikuwaje ukashindwa kuigundua ile, tena bila mimi leo ungeumbuka. { Aliongea kwa kumdhihaki huku akiwa anacheka }

    MZEE SUBE: Yani bila wewe mwanamke leo mimi sijui ningekuwa mgeni wa nani sijui na jinsi kijijini wasivyo tupenda mh.

    BIBI SUBE: Na ndio maana nimekuwa mke wako ili endapo utakwama na jambo lolote nikusaidie.

    MZEE SUBE: Mmmmh mwanamke una maneno mazuri wewe ila shida yangu kubwa nataka kujua ile dawa umeipata wapi?

    BIBI SUBE: Nliipata kule msituni na ilitokana na ule mti mwingne.

    MZEE SUBE: Haaaa kumbe sasa uliujuaje ule mti ni dawa.?

    Bibi sube baada ya kuulizwa vile ndipo akaanza kutoa histori juu ya kuufahamu ule mti na kazi yake.

    BIBI SUBE: Bibi kabla ajafariki siku moja alinchukua kule msituni kwa ajili ya kumsaidia kuchimba dawa zake, tukiwa msituni kwa bahati mbaya mimi nikang'atwa na nyoka ambae aliniambia kuwa ana sumu kal,. Akaniambia kuna mti mmoja tu ambao mizizi yake ndio itaweza kunisaidia kupona. Kutokana na uadimu wa ule mti ilfanya bibi kuangaika huku mimi hali yangu ikizidi kuwa mbaya zaidi. Alijitahidi kuutafuta ule mti bila ya kukata tamaa maana akupenda aone mimi nikipoteza maisha nikiwa bado mdogo tena mbele macho yake, Katika kuangaika sana akafanikiwa kuupata ule mti na kunitengenezea dawa, nilipoitumia mda mfupi mbele nikaanza kurudi kwenye hali ya kawaida.

    MZEE SUBE: Mh! Sasa ikawaje baada ya hapo maana hiyo hstoria yako nimeipenda.

    BIBI SUBE: mmmh na wewe kwa kupenda hadithi. {akaendelea kusimulia} Mda ukivyozidi kwenda na mimi nilizidi kupata uafadhari na hatimae nikapona kabisa, ndipo bibi akanichukua na kunipeleka kwenye ule mti na kuniambia ndio ulio nsaidia endapo nitapata ugonjwa wowote au kuumwa na mdudu wowote awe wa kutumwa au sio wakutumwa lazima nipone na hiyo sio kwangu tu bali kwa watu wote. Ila aliniambia kuwa ule mti una kawaida ya kupoteapote na huwa unaletwa na mzimu kwa mda fulani na hatimae unatoka pale ulipo na kwenda sehemu nyingine na tangu niuone wakati nipo mtoto ndio nimeuona tena ile siku na nilishindwa kukuambia chochote kutokana na sheria za pale msitu.

    MZEE SUBE: Hapa nilipo kichwa chote kinawaka moto maana huo mti kama una kawaida ya kupotea sasa itakuwaje na wakati ule mti ndio dawa ya kuzuia sumu ya YOka ?

    BIBI SUBE: Ndio hivyo ila nakumbuka aliniambia kitu kingine kama unataka uupate ule mti kwa urahisi inabidi uende usiku tena ukiwa umevaa zile nguo za kazi na unatakiwa uombe ile mzimu ikuonyeshe ule mti ulipo kwa mda ule.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MZEE SUBE: haaa! Kama ndio hivyo basi leo usiku inatakiwa twende kule msituni kwa ajili ya kuutafuta huo mti Maana Isije Yoka akamng'ata mtu tukashndwa kumsaidia kwa sababu dawa tayari imeisha.

    BIBI SUBE: Sawa mume wangu.

    Waliendea na safari yao huku wakiendelea kuiongelea ile dawa na hatimae wakafanikiwa kufika nyumbani kwao na kuanza kupanga dhana ambazo watazitumia hapo usiku kule msituni. Walipomaliza wakaendelea kufanya shughuli zao za kila siku huku wakiwa wanasubiria kwa hamu ufike usiku ili wakachukue ile dawa. Masaa yakapita na hatmae usiku ukafika na ndipo mzee sube pamoja na mke wakaanza kujiaanda kwa ajili ya safari yao ya kwenda msituni. Walipomaliza Sube akatoka nje na kwenda kwenye kile kichaka na kumruhusu Yoka akafanye kazi yake, ndipo na wawo wakaanza safari yao ya kwenda msituni mda huo ilkiwa yapata saa sita usiku. Walitembea kwa miguu kutoka kwao mpaka karibu na kutoka nje ya kijiji kisha wakasimama na kushikana mikono huku wakiwa wanaangalian wakiwongea maneno fulani ya kichawi ghafla wakapotea pale ambapo walikuwa wamesimama na kutokea moja kwa moja ndani ya msitu huku wakiwa bado wameshikana mikono.



    Wakaachana mikono na kuanza kuimba na kucheza nyimbo zao za kichawi, Sasa wakati wao wanafanya mambo yao, Yoka na yeye alikuwa kazini. Baada ya kutoka kichani akaanza kuzunguka katika kile kijiji akitafuta mtu wa kumng’ata. wawili wale walipomaliza kuimba nyimbo zao ndipo bibi sube akaanza kuongea na mizimu ili wapate kuuona ule mti kwa urahisi.

    BIBI SUBE: Mababu na mabibi zetu sisi ni wajukuu zenu tumekuja tunashida tunaomba mutusaidie.

    Akanyamaza na kuanza kusikiliza nini mizmu itasema kama itawapokea au laa, lakini kwa bahati mbaya kimya kilitawala na hakuna ishara yoyote ambayo ilijionyesha kuashiria mizimu kukubari ombi lao ndipo bibi sube akarudia tena.

    BIBI SUBE: Mababu na mabibi sisi ni wajukuu zenu tumekuja tunahitaji msahada wenu.

    Baada ya kurudia ghafla akatokea bibi yake ambae alimuonyesha ule mti kipindi ameng'atwa na nyoka, alikuwa amevaa kaniki na kujifunika kitambaa chekundu kichwani, aliwatama na akaanza kuongea na wawili wale huku wakiwa wameinamsha vichwa vyao chini.

    BIBI: Karibu wakuju zangu karibuni sana. Mizimu imekubari kuwasikiliza na imejua nini shida yenu na ipo tayari kuwasaidia ila hii iwe siri yenu.

    Alipomaliza kuongea ghafla akapotea ndipo mzee sube na mke wake wakainua vichwa vyao na kuanza kuangalia huku na kule wakiwa wanamtafuta yule bibi, wakiwa kwenye haraka za kumtafuta bibi sube akauona ule mti uikiwa mbele yao. Akamshtua mzee sube kisha wakaenda kuuchimba mizizi ya ule mti. Walipomaliza waliiaga mizimu na hatamae wakashikana mkono na kupotea pale mstuni na wakatokea nyumbani kwao huku wakiwa na furaha sana. Mara baada ya kufika walisikia mtu akipiga hodi kwa nguvu kwenye mlango wa nyumba yao. Kitendo kile kiliwatisha sana walikaa kimya kwa mda kigodo huku wakiwa wanabadirsha zile nguo zao za kazi ambazo walikuwa wamevaa kule mstuni na kuvaa nguo zao za kawaida ndipo wakaende kufungua mlango. Walimkuta baba mmoja akiwa analia kwa uchungu kama mtu aliefiwa na mwae mpendwa au mke wake, mzee sube alipoona vile ikabidi amuulize kulikoni maana ni kitu cha ajabu kidogo mwanaume kulia kama mtoto mdogo

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MZEE SUBE: Heee! kulikoni mbona upo hivyo?

    BABA: Nina shida baba yangu ninahitaji msahada wako.

    MZEE SUBE: Shida gani hiyo mwanangu na mbona usiku sana?

    BABA: Mwanangu kang'atwa na nyoka nimempa dawa ya kuua sumu ila hali yake bado mbaya.

    MZEE SUBE: Pole sana mwanangu ila usijari mwanao atapona na atakuwa mzima kama kawaida.

    BABA: Nitashukuru sana kama utayasaidia maisha ya mwanangu.

    MZEE SUBE: Basi subilia kidogo nitengeneze dawa.

    BABA: Sawa.

    Akaingia ndani na kumsubili mzee sube atengeneze hiyo dawa, mzee sube akachukua ile mzizi ambayo walikuwa wamechmba katika ule mti na kuanza kuipondaponda kwenye jiwe ambalo alikuwa anatumia katika kutengenezea dawa zake. Alipomaliza kuitengeneza akaongozana na yule baba kwenda nae nyumban kwake. Waliwakuta watu wengi kidogo wakimuangalia yule mtoto ambae kwa mda huo hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi, ndipo mzee sube akaanza kufanya mambo yake na hatimae yule mtoto akapona kabisa tena kwa mda mfupi sana. Kitendo kile kiliwafurahisha sana wanakijiji ambao walikuwa pale na kumuona mzee sube ndio mtu anae faa sana pale kijijini kwao na kumbe walikuwa awajui kuwa yeye ndie chanzo. Alipomaliza kazi yake akarudi nyumbani kwake huku akiwa na furaha kubwa sana, ile siku ikawa imepta. Siku iliyofuatia asubuhi habari zilimfikia mfalme juu ya jambo ambalo amelifanya mzee sube juu ya kumtibu yule mtoto, habari hiyo ilimfurahisha sana mfalme na kumfanya amuite mzee sube nyumbani kwake kwa ajili ya maongozi fulani. Mzee sube baada ya kupata taarifa ya kuitwa kwa mfalme haraka aliwasili na kumkuta mfalme akiwa amekaa pamoja na viongozi wengine wa kile kijiji, walisalimiana na ndipo mfalme akaanza kumuambia lengo la kumuita pale.

    MFALME: Nimekuita hapa kwa ajili ya kukupa pongezi kwa jambo ambalo umelifanya jana kumtibu yule mtoto. Pia nimejuita kwa ajili ya kukupa zawadi kutokana na wema ambao umekuwa ukiufanya kwa hawa wanakijiji wenzako.

    MZEE SUBE: Lazima nifanye hivyo mtukufu mfalme.

    MFALME: Sawa, kwahiyo nimeona bora nikupe zawadi ya eneo ambalo utakuwa unafanya shamba lako pia nitakupa na watu ambao watakuwa wakulimia hilo eneo na nina fanya hivi kama shukrani zangu kwako.

    Mzee sube baada ya kusikia vile alifurahi sana na kumshukuru mfalme kutokana na zawadi ambayo amempatia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MZEE SUBE: Nashukuru sana mfalme wangu hata sijui nsfanye nini ili nionyeshe hii furaha yangu. Ila mimi nakuahidi nitakuwa bega kwa bega na wanakijiji na nitatoa msahada wangu kadri niwezavyo.

    MFALME: Sawa na mimi nakuahidi kuwa karibu sana na wewe katika kuwasaidia awa wanakijiji. Ila mzee unaweza kuniambia huyo nyoka atakuwa ni wa aina gani mpaka awe na sumu kali kiasi kile maana sijawai kusikia wala kumuona nyoka wa aina hiyo.

    Mzee sube alishtuka kidogo maana alihisi kama mfalme ataweza kuhisi kitu juu ya huyo nyoka ikabidi amdanganye.

    MZEE SUBE: Huyo nyoka hatari sana mfalme pia nyoka kama huyu mara nyingi huwa anaishi mistun na kuonekana kwake ni nadra sana na ndio maana wewe umeshindwa kumfahamu na hata kusikia habari zake maana watu wamekuwa wakimsahau mara kwa mara.

    MFALME: Heee kumbe sasa huyo nyoka anaitwa jina gani.

    MZEE SUBE: Huyo nyoka anaitwa RUKA.

    MFALME: Ahaa sasa tunatakiwa tufanyaje ili tumkamate.

    MZEE SUBE: aa huyu nyoka huwa awindwi maana ni mkali sana ila huwa anakaa sehemu moja na baadae anatoka yeye mwenyewe bila ya kufukuzwa na mtu.

    MFALME: Kwahiyo ataendelea kuwadhuru watu mpaka atakapotoka yeye mwenywe.

    MZEE SUBE: Ndio hivyo mtukufu mfalme maana atuna jinsi.

    MFALME: Mh! Sawa.

    Jibu lile lilimfanya mfalme akose raha maana aliona kuwa kijiji kipo katika wakati mgumu juu ya jambo lile, Walipomaliza Kuongea na waliagana ili kila mtu akaendele kufanya shughur zake, ila ajaondoka alimsihii mfalme asimwambie mtu kuhusu yule nyoka wala kupanga mipango ya kumtafuta.

    MZEE SUBE: Mtukufu mfalme nakuomba usimwambie mtu yoyote kuhusu huyu nyoka maana tutakuwa tumevunja miiko ya mababu na mabibi zetu. Pia usisubutu kumtafuta RUka maana utasababisha matatizo makubwa zaidi hapa kijijini.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mfalme alishangaa kidogo maana aliona kama mzee sube amekuwa akimlinda yule nyoka asiuawe lakini kutokana na ukubwa wa mzee sube, mfalme ilibidi akubari tu maana aliona kuwa inawezekana kuwa kweli kama atafanya vile atakuwa amevunja miiko ya kijiji chao. Baada ya hapo ndipo mzee akarud nyumban kwake huku akiwa na furaha kubwa maana amefakiwa kumdanganya mfalme pia kapewa shamba pamoja na wafanyakazi wa kumlimia hilo shamba . Alipofika nyumbani alimkuta mke wake akiwa anapika uji kwa ajili ya kupasha matumbo moto, mzee sube akamuita mke wake huku akiwa na furaha na kuanza kumsimulia kilichotokea kwa mfalme. Wakati huo mfalme na yeye alikuwa akiwaza na kuwazua njia gani atumie kulitatua lile tatizo lililoingia kijijini kwao, ila aliishiwa nguvu kila alipokuwa akiyakumbuka maneno yam zee sube.

    MZEE SUBE: Mke wangu akuna siku ambayo nina furaha kama leo .

    BIBI SUBE: Ehe nambie unafuraha ya nini?

    MZEE SUBE: Yani hauwezi amini hapa tulipo tumepewa shamba na mfalme isitoshe ametupatia mpaka na wafanya kazi wa kulima hilo shamba.

    BIBI SUBE: Hee ! Mume wangu kweli au unantania tu?

    MZEE SUBE: Sikudanganyi alafu kuna kitu hicho yani da hata sijui nisemaje hivi unajua kuwa mfalme akitafuta ya njia ya kumuangamiza YOKA?

    BIBI SUBE: Aaaaa! Sasa imekuaje mbona naogopa.

    MZEE SUBE: Sasa unaogopa nini wewe mfalme hawezi kufanya kitu chochote kusuhu yoka maana jinsi nlivyomwambia nahisi wala hata taka kumtafuta.

    BIBI SUBE: Kwahiyo kasitisha hilo zoezi?

    MZEE SUBE: Ndio hvyo yan leo ni siku ya kufuraha alafu kuanzia leo Nimataka nimruhusu yoka afanye kazi mpaka mchana.

    BIBI SUBE: Mume wangu hauoni kma itakuwa hatari kwa upande wetu pamoja na yoka?

    MZEE SUBE: wala usiogope mke wangu nakuahid nitakuwa makini juu ya jambo hli .

    Aliposema vile akanyanyuka na kwenda mpaka kwenye kichaka na baada ya kufika akaangalia kushoto na kulia kwake il aone kma kuna mtu anakuja au anamuona na baada ya hapo ndipo akaanza kusema maneno fulani huku ukiwa ameinamia kile kichaka. Baada ya kufanya hivyo mara akatoka nyoka kwenye kile kichaka na kuanza kutembea pale kijijini, Mzee sube alifurahi sana akarudi tena kwa mke wake na kuendelea kupiga story huku wakiwa wanasubiria uji uive il wanywe. Siku hiyo watu waliumwa sana na nyoka maana aliruhusiwa afanye kazi mpaka mchana Kwahyo watu wengi walikuwa kwa mfalme wakisubilia dawa ifike il wapone. Hali hiyo iliendelea kwa siku kadhaa na watu wengi walidhurika na wengine kupoteza maisha kutokana na kukosa kupata dawa kwa wakati. kwa upande wa mzee sube na mke wake wao walijitahidi kwa nguvu zao zote kusaidia wana kijiji lakini ile speed ya nyoka kuuma watu ilikuwa kubwa na kupelekea kushindwa kuwasaidia watu wote. Wazee wa kijiji baada ya kuona lile tatizo limezidi kuwa kubwa walikusanyana na kwenda kuzungumza na mfalme juu ya yule nyoka maana alikuwa amezid balaa.

    MZEE.1: Mfalme tumekuja hata tunashida ya kuzungumza na wewe.

    MFALME: kuweni huru wazee wangu mimi ninawasikiliza.

    MZEE 2: Mtukufu mfalme sisi tumekuja hapa kwa ajil ya kuongelea kuhusu hili tatizo lilokumba hiki kijiji chetu cha mbaka kwasasa.

    MFALME: Tatizo gan tena ?

    MZEE 3: kuhusu huyu nyoka ambae amekuwa akisumba sana hapa kijijini kwetu.

    MFALME: kweli huyu nyoka kwa sasa amekuwa tishio hapa kijiji kwetu ila mimi nimepata maelezo yote kuhusu huyu nyoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MZEE 2: Kwahiyo umeamua kufanya nini baada ya kujua kuhusu huyu nyoka.

    Mfalme kabla ajajibu mara mzee sube akafika maana alipelekewa taarifa kuhusu kikao kilichopo kwa mfalme, mfalme baada ya kumuona mzee sube alijkuta na yeye akiwa anamtete yule nyoka.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog