Simulizi : Kengere Ya Kifo
Sehemu Ya Pili (2)
Upande mwingine kule kwenye Mgahawa wa Mzee Sule walionekana wateja wakiingia na kutoka huku upande wa nje yakionekana magari mengi na Bodaboda zimepaki nje ya mgahawa huo......watu walifurahia supu iliyokuwa inapikwa kwenye mgahawa huo.....pamoja na ugali nyama choma...mishkaki ,,soseji na sambusa...kwa mbali alionekana mteja mmoja akinyanyuka kutoka pale alipokuwa ameketi na kumfuata mke wa Mzee sule......mtu huyo alifoka huku akisema....,,"yani tangu nimefika hamjaja kunisikiliza!!!haya nataka ugali nyama choma...nichomee uenye mafutamafuta kiasi usikaushe sana...weka pilipili nyingi....kisha akarudi kuketi pale alipokuwa ameketi mwanzo...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande mwingine alionekana Mzee Sule....akitika nje ya nyumba yake iliyokuwa katikati ya pori kubwa huku amebeba matulubai matatu yaliyotengenezwa kama gunia,,akayarusha upande nyuma ya gari lake..akaingia ndani ya gari akaliwasha na kuondoka zake......
wakati huhuo kule lilipokuwa limepaki gari la Domy, alionekana Tina kujishangaa huku akijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu!!!!!!
kwa mbali alionekana Domy akizioiga hatua kuja pale lilipokuwepo gari lake huku akiongea na simu..alipofika alifungua mlango na kuingia ndani ya gari....akaendelea kuongea na simu hiyi kwa dakika kadhaa,,alipomaliza akambusu Tina shavuni huku akisema,,"samahani mke wangu,, nilikwenda kununua vocha. Tina alibaki kimya akatabasamu...Domy akaliwasha gari wakaondoka kuelekea nyumbani....
walipotoka tu wakapishana na gari la Mzee Sule.likiingia ndani ya hoteli hiyo...Tina akastuka akamtazama kwa mshangao Mzee Sule...huku akijiuliza moyoni,"Mbona kama namfananisha huyu Mzee!!!sijui nishamuona wapi????Tina akabaki na mshangao kichwani mwake...huku Domy akiendelea kuzipanga gia kuelekea nyumbani.......
*****************
alionekana Mzee Sule akishuka kutika ndani ya gari lake na kuelekea ndani kabisa ya Hotel hiyo....akaimgia ndani ya ngazi ya umeme(lift)akabofya kitufe kilichoandikwa namba(6) alipofika ghorofa ya sita akazipiga hatua kuufuata mlango wa chumba namba(113)huku ameshikilia ile mifuko mitatu mikubwa iliyotengenezwa kwa kutumia tulubai......akafungua mlango na kuingia upande wa nadani.....
baada ya Mzee sule kuingia ndani ya chumba hicho kwa mabali alionekana kijana mmoja akizipiga hatua za harakaharaka kumfuata Mzee Sule.....kumbe kijana huyo ni muhudumu wa Usafi upande wa vyumbani....akanyata mpaka mlangoni akachungulia upande wa ndani kwa kupitia tundu la ufunguo.....akastuka hofu ikamjaa alipogeuka ili akimbie mara ghafla......ikasikika sauti....
WEWE UNAFANYA NINI HAPO??? yule kijana alistuka kumuina Bosi wake...akazipiga hatua kuelekea upande mwingine...bosi akamuita kijana huyo......akazipiga hatua kumfuata bosi wake..alipomkaribia,, Bosi akauliza,,"tabia gani hiyo kuchungulia kwenye vyumba...wakati wateja wamepumzika??? kijana yule akajitetea kwa kusema,,"Bosi nahisi kuna mtu anafanya mauwaji ndani ya chumba hicho.!!!
wakati huohuo alionekana mzee sule mule ndani ya chumba akimalizia kuiweka maiti ya yule muhudumu wa kike,ndani ya ule mfuko mmoja uliobaki...kisha akatoa kichupa kilichokuwa na maji yaliyo onekana na rangi nyeusi..akamimina maji hayo kwenye kiganja na kujipaka mwilini....kumbe mzee sule akifanya hivyo,,hakuna binadamu wa kawaida atakayeweza kumuona yeye pamoja namaiti atakazokuwa amezibebe...
akabeba furushi la kwanza akatokanalo mpanje ya hoteli akaliweka nyuma ya gari lake......alipishana na watu lakini hawakuweza kumuona!!! kwa sababu alikuwa yupo katika hali ya kichawi...
akazipiga hatua kidudi kule ndani ya chumba namba(113) akachukua maiti ya pili akatokanayo na uitupia nyuma ya gari...akarudi tena..akachukua maiti ya yule muhudumu wa kike akatokanayo na kuitupia ndani ya gari...kisha akafungua mlango wa gari akaingia na kuliwasha akaondoka zake...watu waliokuwepo jirani na gari hilo walistahajabu kuina gari linaondoka wakati hawakumuina dereva akiingia ndani ya gari hilo....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
******************
upande mwingine walionekana Seba na Tina wakiwa ndani ya gari wakielekea nyumbani,, wakapitia sehemu kununua Matunda...Seba akasema,,"Ebu nenda kaangalie maparachichi mazuri pia kama utapata ndizi mbivu chukua...akatoa noti ya elfu kumi na kumpa Tina...
Tina akafungua mlango wa gari na kuelekea ule ulande palipokuwa pakiuzwa matunda...
Seba alitoa simu yake ili abadilishe picha kwenye Facebook na kuweka ile picha aliyompiga Tina Tina...Seba alistahajabu kutokuiona picha ile ndani ya simu yake,,akajisemea moyoni,,"au sikuihifadhi??(save) nitampiga picha nyingine....
********************
Upande mwingine kule hotelini alionekana yule kijana muhudumu..akirudi kule ghorofa ya sita...ili akahakikishe kile alichokiona mara ya kwanza akazipiga hata kwa kunyatia alipoufikia mlango akacgungulia kwenye tundu la ufunguo lililokuwa kwenye kitasa....akastahajabu hakuona mtu yeyote yule....ikabidi afungue mlango ili ahakikishe...alipoingia upande wa ndani hakukuta mtu...akajisemea moyoni,,"mbona sijaona mteja yeyote akishuka kutika ghorofani!!!!! akaamua kutoka nje ya chumba hicho na kuendelea na shughuri zake nyingine..
*******************
upande mwingine kule alilipokuwepo gari la Seba alionekana akibofya bofya simu yake....kwa mbali akamuona Tina anakuja huku amebeba mduko uliokuwa na matunda ndani yake...Seba alimtazama Tina kwa macho ya matamanio.....na kwa jinsi Tina alivyokuwa amevaa kapendeza....Seba aliamua kumpiga picha Tina wakati tina akitembea...lakini Seba alishangaa kila anapompiga Tina picha,,haionekani kwenye simu..
Tina aliendelea kuzipiga hatua akafungua mlango na kuingia ndani ya gari.....Seba akamuoba Tina wapige picha ya pamoja kisha akamsogelea na kupiga picha kwa kutumia kamera ya mbele(Selfie) lakini cha kushangaza baada ya kumaliza kupiga picha....Tina hakuonekana kwenye picha hiyo!!! alionekana Seba peke yake...kitendo hicho kilimfanya Seba astuke akawa na masha na mkewe Tina....Seba akaliwasha gari,,wakaondoka zao kuelekea nyumbani...
Tina alionekana kuwa na wasiwasi,,"alijiuliza maswali wa na majibu.....kunamatukio yakawa inazunguka kwenye ubongo wa Tina akawa anaona mauwaji ya kikatiri ya binadamu wakinyongwa kwa kutumia kamba...ghafla Tina akapiga kelele.....baada ya kumuona Mzee mmoja katika hayo matukio yaliyokuwa yakizunguka kwenye ubongo wake!!!! akageuza shingo yake na kutazama upande wa nyuma...kumbukumbu ikamjia kuwa yule mzee waliepishana nae akiingia hotelini huku anaendesha gari aina ya TOYOTA PICK UP..........kipindi wanatoka kule kwenye hotel...Tina alionekana kushangaa kisha akasema kwa sauti ya taratibu kwa kutaja jina,,"SULE...akakumbuka Tukio la miaka Hamsini (50)iliyopita.
Seba alistuka sana kwa kile kitendo cha Tina kupiga kelele....akauliza,,"unatatizo gani??
Tina hakujibu kitu,
baada ya dakika kadhaa wakafika nyumbani..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**************
Upande mwingine alionekana Mzee Sule akiwa ndani ya gari lake akiliendesha huku akionekana kuwa na furaha....
baada ya dakika chache akafika nyumbani kwake akashusha maiti zile tatu na kuziingiza ndani ya kile chumba chake alichokitumia kukatakata nyama....kisha akatoka upande wa nje akaliwasha gari lake na kuelekea kule kwenye Mgahawa wake.
alipofika alilipaki gari na kuingia ndani ya mgahawa...akapitiliza mpaka uoande wa jikoni
Watu waliendelea kunywa Supu matata na nyama choma iliyokuwa na utamu wa aina yake.....akainekana mtu mmoja akiingia ndani ya mgahawa huo...akaketi kwenye kiti..akaagiza supu....baada ya sekunde kadhaa kupita supu ikaletwa.....yule mtu alipoitazama supu ile aliina kuna kipande cha pua ya binadamu...akastuka akaacha kunywa supu na kuzipiga hatua kutoka nje ya mgahawa huo..
kijana mkubwa ambaye ni mtoto wa Mzeee Sule
alimuona mtu huyo ameondoka na kuiacha supu mezani..akazipiga hatua mpaka pale mezani..alipoitazama supu ile alikiona kipande ya pua...ndani ya supu ile akaichukua na kurudi jikoni haraka akamueleza baba yake...
Mzee Sule akatoka jikoni huku akizipiga hatua za haraka kutoka upande wa nje...akamuona yule mtu..akiondoka zake..
Mzee Sule akaingia ndani ua gari lake....na kuliwasha akaliendesha kwa mwendo wa taratibu kumfuata mtu huyo kwa nyuma.....alipo mkaribia
akapunguza mwendo wa gari..yule mtu alipogeuka kutazama nyuma ili aone ni nani anaye endesha gari nyuma yake...ghafla mzee Sule aliongeza mwendo akamgonga na gari mtu yule o chini kisha akarudisha gari nyuma haraka akamkanyaga kwa magurudumu....
mtu yule akapasuka kichwa ubongo ukamwagika chini...mzee sule akashuka haraka kutoka ndani ya gari akachukua maiti ile huku akilalamika kwa kusema,,"yani ubongo wote umemwagika siwezi kuuacha huu ukichanganya kwenye supu inakuwa amazing (supu tamu ya kushangaza) akauzoa ubongo uliokuwa umemwagika chini.akauweka ndani ya mfuko wa plastiki kisha akauweka juu ya maiti ile aliyoiweka nyuma ya gari lake akaimwagia ile dawa iliyokuwa kwenye kichupa kisha na yeye akajipaka mwilini ili asionekane kama kabeba maiti.....akaliwasha gari na kuondoka zake kuelekea kule mstuni,,ilipokuwepo nyumba yake....
***************
Upande mwingine alionekana Domy pamoja na Tina wakiwa chumbani mwao...lakini Domy alioneka kuwa na wasiwasi juu ya Tina..alijiuliza kwa nini Tina akipigwa picha haonekani kwenye picha!!!
Tina aliona kuwa Domy hayupo sawa...yupo katika hali tofauti na alivyozoea kumuona akiwa mchangamfu muda wote..Tina akauliza,,"mbona leo nakuona kama unamawazo!!! nini kinakusumbua???
Domy hakujibu kitu alibaki kimya huku akimtazama Tina...Tina alianza kuhisi huenda kuna jambo baya ambalo yeye kalifanya halijampendeza Domy.....Tina akaanza kuomba msamaha huku akilia.......Domy akauliza mbona nikikupiga picha hauonekani kwenye picha inakuwa kivuli??? Tina akastahajabu sana.....akasema,,"mmh! embu nipige picha tena...
wakati huohuo upande mwingine walionekana watu wawili wakitembea barabarani wakiwa wamelewa...wakakatisha kona na kubofya kengere iliyokuwepo pembeni ya geti.....wakaendelea kubofya kengere hiyo huku wakifoka kuwa,,kwanini watu waliopo ndani wanachelewa kufungua geti..
****************
kule nyumbani kwa Domy alionekana Tina akimwambia Domy ampige picha ili ahakikishe je? ni kweli akipigwa picha haionekani...
wakati huohuo walionekana wale walevi wakiendelea kubofya kengere...ghafla Tina akastuka akainama kutazama chini alipoinua uso wake macho yake yalikuwa yanatoa machozi ya damu...wakati Tina anainua uso wake ndio wakati Domy alikuwa kabofyaa kitufe cha kupigia picha.mwanga ukawaka(flash) mwanga ule uliizuia ile hali ya tina kuendelea kubadilika akarudi katika hali yake ya kawaida....akaonekana kujishangaa.....Domy alipoangalia simu yake ile picha ilionekana kivuli tu.....akastuka sana akamtazama tina akamuona Tina akijishangaa kwa kujitazama mwili wake..
***************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
upande mwingine kule kwenye mgahaw wa Mzee sule..wateja walionekana kulalamika kwamba supu matata leo imekwisha mapema....walitoa lawama hizo kwa mke wa mzee sule.....ikabidi mke wa mzee Sule amwamvie mwanae mkubwa kuwa aende nyumbani akaangalie kama Mzee Sule kaleta nyama...ye kijana akafungua na kuingia kwenye ule mlango wa siri,,,akapitia njia ya chini kwa chini ya aridhi kuelekea nyumbani kufata nyama,,ailete ili supu ibandikwe jikini haraka..
baada ya dakika kadhaa kijana huyo alitokezea nyumbani akafungua mlango wa siri na kuingia ndani ya nyumba..akamkuta mzee Sule akiwa anakatakata na kutenganisha viungo vya maiti...akasema,,"baba fanya haraka wateja wanasubiri supu..alafu pia miskaki imekwisha ugali umebaki mwingi....
mzee Sule akacheka na kusema,,"kunaubongo nimeuweka ndani ya ndoo ebu usafishe kwa kuuosha ili mchanga utoke....kijana yule akafanya kama alivyoagizwa na baba yake....
baada ya dakika tano mzee Sule alikuwa tayari ameshamaliza kukatakata nyama....akaiweka kwenye ndoo na kumpa kijana wake apeleke haraka nyama hiyo kule kwenye mgahawa...
yule kijana aliondoka na kuelekea kule kwenye mgahawa kwa kupitia ile njia ya chini kwa chini ya aridhi...alipofika akaiosha ile myama huku akisaidiana na mama yake pamoja na mdogo wake kisha akachukua nyama kiasi akaiweka kwenye jiko kwa ajili ya kuichoma.......
ghafla kunamteja akaja na kusema nikatie nyama ya elfu kumi isiyokuwa na mifupa...kisha ikaushe usiikatekate.... niletee pamoja na ugali...kijana yule aliichoma nyama na ilipoiva akaiweka kwenye sahani pamoja na ugali...kumbe nyama ile ilikuwa ni sehemu ya kifua,,,yule mtu aliyeuwawa alikuwa kajichora tatuu(mchoro wa rangi usiofutika)....kutokana na harakaharaka ya mtoto wa mzee Sule ili awaishe nyama kwa mteja hakuweza kuona tatuu hiyo...yeye aliweka nyama kwenye sahani akapeleka moja kwa moja mpaka mezani kwa ye mteja aliyeagiza nyama hiyo...
wakati huo huo kule nyumbani kwa Domy...Tina alikosa amani kwa maswali aliyokuwa akiuliza Domy...Tina alishindwa kujibu kutokana yeye hafahamu chochote....haijui siri nzito iliyopandikizwa mwilini mwake......
wakati huohuo walionekana wale walevi wakigonga geti kwa nguvu....ye mle mmojawapo akabonyeza kengere kwa mara nyingine tena...
Domy akiwa anamuuliza Tina maswali mara ghafla Tina akastuka....akainamisha uso wake chini......Dimy alikasirika sana aliona kama Tina kamdharau kuwa yeye anamuongelesha alafu Tina kainamisha uso wake chini....Domy akaamua kumsogelea Tina huku amenyanyua mkono ampige kofi....
Tina alipoinua uso wake, Domy alishtuka macho yakamtoka alistaajabu kumuona tina amebadilika huku macho yake yanayotokwa na machozi ya damu,Domy akatimua mbio kuelekea chumbani wakati huo huo wale walevi waliendea kubofya kitufe cha kengele,Tina akatoweka kimiuzija kuufuata mlio wa kengere.
****************
wakati huohuo ule upande mwingine walionekana wale walevi wawili..kisha mmojawapo akazipiga hatua kadhaa akasimama kando na kuanza kujisaidia haja ndogo...ghafa akajitokeTina akiwa kwa mbali kidogo kutoka hapo walipo walevi hao.....akazipiga hatua kuwafuata.....yule mlevi aliyekuwa akijisaidia haja ndogo akamuona Mwanamke akija upande wao huku ameinamisha uso wake chini.....yule mlevi akaingiwa Tamaa ya kutaka kumtongoza Tina...akafunga zipu haraka haraka.akasimama huku anayumba yumba kwa ulevi...Tina alipomkaribia yule mlevi akamfuata..ghafla Tina akainua uso wake...ye mlevi akastuka akaogopa sana Tina akamkamata na kunyonga kwa kutumia ile kamba yake....wakati huohuo yule mlevi mwingine akageuka akaogopa sana kumuona mwenzake ananyongwa....pombe zikamruka,,akaanza kutimua mbio..alikimbia bila kujua ni wapi anaelekea..Tina akajitokeza mbele yake...akamkamata akamnyonga kwa kutumia ile kamba.......kisha akazipiga hatua kadhaa akatoweka kimiujiza.....baada ya sekunde kadhaa akajitikeza nyumbani..akawa anajishangaa..
********************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wakati huohuo Domy alionekana akiwa kajifungia chumbani huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu...jasho lilimtoka mfululizo...akaona chumbani hapakaliki,,akaamua kufungua mlango wa chumbani akachungulia kule upande wa sebuleni..akamuina Tina yupo katika hali yake ya kawaida huku akionekana kujishangaa....Domy akatoka chumbani huku akizipiga hatua za tahadhari..alitembea huku macho yake yakimtazama Tina...alipomkaribia akamuita Tina kwa sauti ya chini,,Tina...Tinaaaa
Tina akastuka akamtazama Domy...hali yake ya ufahamu ikarudi akaitika," Abee mume wangu.
Domy hakutaka kuuliza kitu chochote akaogopa hata kumsogelea.....Tina alijisikia vibaya,,alitamani kujua ni nini kimetokea lakini alishindwa jinsi ya kumuuliza Domy....Tina akaamua kuzipiga hatua kuelekea chumbani...akamuacha Domy kasimama palepale sebuleni,,Domy akajiuliza,,"yawezekana Tina ni jini...au niliona vibaya...mmh!! lakini sidhani kama macho yangu yalinidanganya....
***************
Upande mwingine kule kwenye mgahawa wa mzee Sule.....alionekana yule mtu aliyeafiza ugali nyama choma akiendelea kula ugali pamoja na nyama hiyo matata....akapaza sauti,,"niletee chumvi na ndimu....pia niongezee pilipili..aliyasema maneno hayo huku akiendelea kutafuna minofu ya nyama......baada ya sekunde kadhaa kupita aliletewa vitu alivyoagiza...akachukua ndimu akakamulia kwenye nyama ile..kisha akaweka na pilipili..akachukua mnofu mwingine akala pamoja na tinge la ugali....ghala kunakipande cha nyama(mnofu) aliuona kama haujaiva vizuri ulikuwa haujakauka...akastuka akakitazama kwa makini akaona mchoro....akajisemea moyoni,,"mmh!!! mbona kama inaonekana ni tatoo! ng'ombe gani huyu alichorwa mchoro wa tatuu ambayo huchorwa kwenye mwili wa binadamu??
kutokana nyama ile ilikuwa imeshachomwa alafu imekatwakawa vipande...mchoro ule haukuonekana wote..ulionekana nusu tena kwa mbali sana...mtu yule akajipa moyo kuwa hiyo ni nyama ya ng'ombe..hakuwa na shaka kuwa kwenye mgahawa huo awawezi kupika nyama ya binadamu.......akajisemea moyoni,,"yawezekana mmiliki wa mgahawa huu ni mfugaji...itakuwa anang'ombe nyingi sana.....hata hivyo wanachoma nyama vizuri tamu sana..ndio maana watu wanajazana kula kwenye mgahawa huu usiku na mchana..
wakati huohuo alionekana mzee sule akiwa barani anaendesha gari lake...akakatisha kona na kutokezea kwenye ile nyumba ambayo wale walevi wawili walinyongwa na Tina..akachukua maiti zao na kuzirusha nyuma ya gari...kisha akaingia ndani ya gari na kuliwasha akaondoka zake.....
******************
Upande mwingine alionekana Domy akizipiga hatua za taratibu kuelekea chumbani...lakini alikuwa na hofu na wasiwasi kuhusu Tina huenda akamdhuru....akafungua mlango na kuingia chumbani akamkuta Tina amevua nguo kabaki mtupu(uchi) kajilaza kitandani......pia Domy akapanda kitandani,,kutokana na umbile la Tina kuwa na mvuto wa aina yake Domy akapata hamasa ya kuanza kumpapasa Tina.....akasahau yale yote aliyotoka kuyaona muda mchache uliopita.....Tina hakutambua wala kujua chochote kilichotokea kwa sababu alikuwa hana uwezo wa kujitambua na kujizuia anaposikia mlio wa kengere.......
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***************
upande mwingine walionekana maaskari wakiwa katika gari la polisi wakifanya doria kwenye mitaa usiku huo.wakakatisha kona na kuliegesha gari lao kando ya barabara kisha wakashuka kutoka ndani ya gari wakasimama barabarani kuhakikisha kila gari inayopita lazima ikaguliwe.....kumbe kunatukio la ujambazi limefanyika muda mchache uliopita ala majambazi wakakimbia na kuondika enei la tukio wakiwa na gari aina ya TOYOTA PICK UP.
wakati huohuo alionekana mzee sule akikatisha kona kuifuata barabara hiyo ambayo wale maaskari walikuwepo...aliliendesha gari lake bila wasiwasi akaingia kabisa kwenye barabara..
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment