IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilisikika taarifa ya habari katika kituo cha habari hapa nchi. taarifa hiyo ilielezea kuhusu binti mmoja aliyezikwa miaka 50 hiliyopita...binti huyo alifufuka na kuanza kuonekana sehemu mbalimbali huku macho yake yakionekana kuwa na machozi ya damu iliyoganda...inasemekana kuwa binti huyo anajitokeza kila unaposikika mlio wa kengere yoyote ile.....anabadilika sura na kufuata mlio wa kengere ulipotokea,,na akifika eneo hilo anafanya mauwaji ya kikatiri kwa kunyonga shongo kwa kutumia kamba aliyokuwa anatembeanayo muda wote.kila anapobadilika....hakuna aliyekuwa akifahamu kuwa binti huyo alifufuka na anaishi katika maisha ya binadamu wa kawaida,lakini huwa anabadilika na nacho yake hutoa machozi ya damu kila inaposikika sauti ya kengere...
Usiku wa leo,binti huyo aitwae Tina..alionekana akiwa ndani ya clubu akiwa na mpenzi wake Domy....walikuwa wameketi kaunta huku wakinywa
karinya(pombe)Domy alikuwa hajui kuwa Tina alishakufa miaka hamsini (50)iliyopita akazikwa huko,Nigeria lakini alifufuka Tanzania..Domy aliishi na Tina miaka mitano lakini hakuwahi kuwajua wazazi wala ndugu wa tina..pia hakuwahi kumjua rafiki wa tina hata mmoja..hata simu ya tina ilikuwa na namba moja tu ya Domy.
waliendelea kunywa pombe...Tina akanyanyuka ili aende chooni kujisaidia haja ndogo..alipoingia chooni ikasikika kwa mbali sauti ya kengere ikitokea upande wa nje ya club..uso wa Tina ukaanza kubadilika macho yake yaanza kutoa machozi ya damu....akatoweka kimiujiza na kuelekea kule ulipotokea mlio wa kengere....
akajitokeza nje ya nyumba moja akaanza kuzipiga hatua..
kwa mbali kidogo walionekana wanafamilia wakiwa wamesimama mlangoni wakisubiri mlango ufunguliwe...walipo ona kijakazi wa ndani anachelewa kufungua mlango baba wa familia hiyo akabofya tena kitufe cha kengere ili yule kijakazi kama amelala basi aisikie kengere hiyo...
wakastuka kunamwanamke kasimama nyuma yao
akamkamata baba wa familia hiyo na kumnyonga kwa kamba aliyokuwa ameishikilia mpaka akafa.
mkewe akaamua kutimua mbio huku amewashika mikono watoto wake wawili wa kike... tina akajitokeza mbele yao na kuwanyonga wakafa papohapo...kisha akaingia uoande wa ndani na kumuuwa kijakazi wa nyumba hiyo....akatoka upande wa nje na kutoweka kimiujiza.....akajitokeza ndani ya choo cha cha wanawake ndani ya ile club aliyomuacha Domy...akarudi katika hali yake ya kawaida akatoka chooni na kurudi kule kaunta.. wakaendelea kuzitandika karinya(kunywa pombe)
ilipofika majira ya saa saba za usiku Domy alisema waondoke wakalale....wakatoka nje na kuingia ndani ya gari wakaianza safari ya kurudi nyumbani...
*****************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
asubuhi palipokucha alidamka na kuandaa chai..
alipomaliza kuandaa chai wakaanza kunywa huku wakitaza Runinga...ikaoneshwa taarifa ya habari ikisema kunafamilia imeuwa na mtu asiyejulikana.
kisha wakainesha ile nyumba ya wanafamilia hao.
Tina alichukia akakaza macho kuitazama runinga ghafla ikavunjika kioo.. na kuanza kutoa moshi...
Domy alistuka sana lakini hakujua kuwa Tina ndiye kavunja Runinga hiyo kimiujiza..Domy akaanza kulalamika kwa kusem,,"Yani hili shirika la tanesco hawapo makini na kazi yao,ona sasa Runinga yangu imeeungua....Domy alikasirika sana akahairisha kunywa chai akaondoka na kuelekea kazini....kabla hajafika mbali aliamua kwenda nyumbani kwa rafiki yake...hakuna umbali mrefu kutoka nyumbani kwake...alipofika alipaki gari na kuufuata mlango akagonga hodi..akasubiri kwa sekunde kadhaa alipo ona hakuna mtu anayekuja kufungua mlango,,akahisi huenda hawajasikia akigonga mlango akaamua kubofya kengere iliyokuwepo kando ya mlango kwenye ukuta.
****************
Kule nyumbani kwa Domy alionekana Tina akiendela kufanya usafi wa nyumba...ghafla ukasikika mlio wa kengere akili ya tina ikabadilika pamoja na uso wake...macho yake yakaanza kutoa mchozi ya damu...akatuoa kitambaa alichokuwa anakitumia kuduta vumbi kwenye kabati la sebuleni......akatoweka kimiujiza na kuufuata mlio wa kengere.......
Domy akabofya kitufe cha kengere, akasubiri kwa sekunde kadhaa kumbe rafiki ake alikua dukani anaoga, domy alitazama saa yake mkononi ilikua ni saa tatu kasoro za asubuhi, akaingia ndani ya gari lake akaliwasha na kuelekea kazini. Domy alipoondoka Tina kajitokeza kimiujiza akasimama nje ya mlango huo, wakati huo huo rafiki yake Domy alionekana akitoka bafuni huku akizipiga hatua za haraka haraka......alipofungua mlango akakutana uso kwa uso na Tina alistaajabu kuona macho ya Tina yakitoa machozi ya damu akafunga mlango kwa haraka. . alipogeuka alistuka kumkuta Tina ndani ya nyumba, Tina alimnasa alimnyonga kwa kamba mpka akafa.... kisha akatoweka kimiujiza, akajitokeza nyumbani kwake, baada ya sekunde kadhaa akarudi katika hali yake ya kawaida...akajishangaa sana...hali hiyo humtokea pasipo yeye kujua. akakimbia na kuelekea bafuni akanawa uso huku akijitazama kwenye kioo kilichokuwa ukutani.....kumbukumbu ikamjia akahisi kaona tukio la mauwaji ya mtu akinyingwa kwa kamba....
akatoka bafuni akaingia jikoni akaendelea kufanya usafi...alipomaliza...akatoka na kuelekea sokoni kwa ajili ya manunuzi ya chakula cha jioni...
alipofika sokoni alinunua vitu mbalimbali..kisha akaelekea super market kununua vitu vingine alivyokuwa amepanga kununua......
akiwa ndani ya super market....alionekana mama mmoja akiwa na mtoto wake mdogo..mama huyo alikuwa akinunua midoli kwa ajili ya mtoto..
katika midoli hiyo kunamdoli mmoja ulikuwa na kegere ndogo iliyofungwa shingoni mwa mdoli huyo.....yule mama alipoutikisa mdoli...kengere ikatoa mlio...
Tina akastuka...ghafla akaanza kubadilika...macho yake yakaanza kutoa machozi ya damu hata uso wake ukaonekana kutisha....akatuoa kikapu alichokuwa amekishikilia na kuanza kuzipiga hatua kuufuata ule mlio wa kengere....
ghafla kuna mtoto mdogo aliyekuwemo ndani ya super market hiyo alikuwa na kamera ya kitoto(toy) alipomuona Tina,,mtoto huyo aliamua kumpiga picha....camera ile ikawaka mwanga(flash) Tina akajiziba uso huku akipiga kelele akabadilika na kurudi katika hali yake ya kawaida.....akastuka huku akijishangaa..... hata watu waliokuwemo ndani ya super market hiyo,,walishtushwa na kelele za Tina wakageuka na kumtazama......Tina aliakota kikapu chake akazipiga hatua za haraka kutoka upande wa nje..
hakuna aliyemuona Tina kipindi alipobadilika zaidi ya yule mtoto aliyempiga picha...kumbe mwanga wa kamera unauwezo wa kumzuia Tina kipindi anapobadilika.....mwanga huo akiuona unamchoma kama kamwagiwa maji ya moto....sekunde hiyo hiyo anarudi katika hali yake ya kawaida..
******************
Alizipiga hatua huku akijiuliza kwa nini hali hiyo hujitokeza bila yeye kujua..akawa anajiuliza,"mimi ni nani???alijiuliza maswali mengi bila kupata jibu
baada ya nusu saa kupita alifika nyumbani..akaanza kuandaa chakula...tayari kwa kukipika jikoni.
****************
upande mwingine alionekana mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la SULE mzee huyo alikuwa anaishi porini familia yake mke na watoto wawili wa kiume.....ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na njia ya siri iliyopita chini kwa chini. nakutokezea kwenye jiko la mgahawa mmoja uliokuwa ukiuza supu na nyama choma....watu wengi walijazana kwenye mgahawa huo...kwa ajili ya kujipatia supu na nyama choma...
mgahawa huo ulikuwa nje kidogo ya Mji...na ulikuwa wazi na huduma inapatikana masaa 24..
mgahawa huo ulikuwa na siri nzito ambayo hakuna mtu aliyekuwa anafahamu zaidi ya Mzee Sule na mke wake pamoja na Watoto wake wawili wa kiume..ambao ndio walikuwa wapishi katika mgahawa huo......
***************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
upande mwingine watu walionekana mtaani wakijiuliza kwa nini mtu akikutwa amenyongwa baada ya muda maiti yake inapotea na hakuna anayejua nani muuwaji......hata vyombo vya dola vilipata wakati mgumu sana kumtafuta muuwaji lakini mpaka sasa bado hawajafanikiwa kumjua wala kumpata...
***************
ilipofika majira ya jioni Alionekana Domy akiwa ndani ya gari lake baada ya kutoka kazini..aliliendesha gari kwa mwendo wa taratibu..
akaelekea nyumbani kwa rafiki yake....alipofika alipiga honi ya gari lakini hakuona mtu akija kufungua mlango akahisi huenda rafiki yake bado hajarudi.....Domy hakujua kuwa rafiki yake ameuwawa asubuhi ya leo....na muuwaji ni Tina ambaye ni mpenzi wake. Domy akaamua kuondoka zake na kuelekea nyumbani kwake.alipofika alikuta tayari Tina kamaliza kuandaa chakula cha jioni........Tina alimpokea Domy kwa mabusu kama kawaida yake huwa anamfanyia hivyo kila siku....
ilipofika majira ya saa mbili za usiku Tina alipakua chakula wakaanza kula...
**************
upande mwingine alionekana mzee sule akiwa ndani ya gari lake aina ya TOYOTA PICK UP..
iliyokuwa wazi upande wa nyuma.....kulionekana kuwa na furushi refu kiasi.....Mzee Sule aliliendesha gari mpaka kule porini ilipokuwepo nyumba yake...alipofika alishuka kutoka ndani ya gari kisha akalivuta furushi lile na kuliweka begani
akazioiga hatua kuingia ndani ya nyumba yake...akapitiliza mpaka ndani ya chumba kilichokuwa kimejitenga peke yake...akalitupia juu ya meza lile furushi...akachukua kusu pamoja na shoka na Upanga mkali sana....akachana furushi lile na kutoa lile turubai alilokuwa amelifunga...alipo litoa turubai hilo,,ndani yake ilikuwemo maiti ya yule rafiki yake Domy......Sule akachukua shoka na kuanza kuikata kata maiti ile..na kukata nyama isiyokuwa na mifupa na kuiweka ndani ya ndoo..
akakata viganja na miguu na kuviweka kwenye mashine ya kusagia nyama unayotumia umeme...mzee sule alikuwa na mtambo maalumu unaofua umeme kwa kuakisi mionzi ya jua.mashine hiyo ilikuwa na nguvu..inauwezo wa kusaga mpaka mifupa ikawa unga mlaini kabisa...
viganja pamoja na miguu iliyosagwa aliitumia kutengenezea soseji pamoja na sambusa.....
alipomaliza kukata kata nyama hiyo alichukua shoka akakipasua kichwa na kutoa ubongo akauweka pembeni vilipokuwepo utumbo pamoja na maini na figo....ambavyo huvichanganya kwenye supu matata...
alipomaliza alichukua ndoo iliyojaa maji na kiisafisha meza kwa kufuta damu zilizomwagika....kisha akabeba ile ndoo iliyokuwa imejaa nyama pamoja na ndoo nyingine iliyokuwa na utumbo pamoja na maini,,figo na ubongo...akazipiga hatua kuelekea kwenye chumba chake cha kulala aka vuta kochi kulisogeza kando...akafungua mlango mdogo uliokuwa kwenye sakafu..mlango huo ulitengenezwa kwa mbao ngumu...... akaingia uoande wa ndani kisha akazichukua ndoo hizo mbili akaanza kuzioiga hatua kwa kupitia nja hiyo ya chini kwa chini kuelekea kuke kwenye mgahawa...
*****************
upande mwingine alionekana Domy akiingia nyumbani kwake....Tina alimpokea mumewe wakazipiga hatua kuelekea chumbani..walipoingia Domy alisema anahisi uchovu..hivyo anahitaji kupumzika.....akapanda kitandani akajipumzisha
Tina akatoka na kuelekea jikoni.....akaandaa chakula cha jioni...
*****************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
upande mwingine kule kwenye mgahawa wa mzee sule ilisikika sauti ikisema,,""Niongezee supu nalafu ongeza sambusa mbili....
wakati huohuo alionekana mzee sule akitokezea jikoni kutoka kwenye mlango wa njia ya chini kwa chini ya aridhi....mke wake alichuku ile ndoo iliyokuwa na nyama akaiweka kwenye sufulia kubwa akaweka maji na kuliweka juu ya jiko....
kisha akachukua sufulia lingine akaanza kuosha utumbo kisha akaubandika jikoni huku akisema,," mme wangu leo umechelewa yani supu ilikuwa imekaribia kuisha alafu leo wateja ni wengi sana si unajua ni weekend(siku ya mapumziko)
*****************
Upande mwingine alionekana muuza maziwa akiwa amebeba mitungi iliyokuwa na maziwa ndani yake....mitungi hiyo iliyotengenezwa kwa bati la aluminiamu...alikuwa kaifunga vyema kwenye kiti cha nyuma........huku akiendesha baiskeli.....akapiga kengere huku akipaza sauti,,"MAZIWA MAZIWA MAZIWA....mtu huyo hakuwa mbali na nyumbani kwa Tina..
wakati huo huo Domy alionekana akinyanyuka kitandani ili akamwambie tina kuwa yeye anajisikia kula mboga kavu isiyokuwa na mchuzi..
Wakati huo huo Tina alionekana akiendelea kuandaa chakula..ghafla akastuka baada ya kusikia sauti ya kengere akaanza kubadilika,,macho yake yakaanza kutoa machozi ya damu......ghafla kisu alichokuwa amekishikilia mkononi kikadondoka chini kutoka mkononi.....akanyanyuka na kusimama wima akazipiga hatua za taratibu ghafla akatoweka kimiujiza na kujitokeza mbele ya yule muuza maziwa....
yule muuza maziwa akastuka akashika breki ya ghafla baiskeli ikaserereka na kuanguka chini....Tina akamkamata na kunyinga kwa kutumia kamba yake....kisha akatoweka kimiujiza.....akajitokeza nyumbani kwake.....baada ya sekunde kadhaa akarudi katika hali yake ya kawaida...akawa anajishangaa ghafla Domy aliingia jikoni akamkuta Tina kasimama huku anaonekana kuushangaa mwili wake..
Domy akauliza,,,"umepatwa na nini mbona unainekana kujitazama mwili wako????
Tina hakujibu kitu alibaki kimya...ghafla fahamu zikarudi akastuka sana nusu akimbie....
***************
upande mwingine kule aliponyongwa muuza maziwa......kwa mbali lilionekana gari la Mzee sule likiishirizi kwenye kona huku limebeba baiskeli upande wa nyuma ya gari.....
Kule nyumbani kwa Domy....Tina aliamua kumdanganya Domy kuwa kichwa kinamuuma..huku akijishika usoni..Domy aliogopa akaamua ampeleke hospitali haraka..akamchukua Tina huku ameuweka mkono wa Tina Begani kwake wakazipiga hatua kuelekea kwenye gari ili waende hospitali....Domy aliliwasha gari na kuliondosha kwa kasi.
wakiwa njiani karibia kwenye mataa...walikuta foleni ikawalazimu wasubiri foleni...
pembeni kulikuwa na gari jingine limesimama..ndani ya gari hilo kulikuwa na familia alikuwemo Mwanamke Mtoto pamoja na baba wa mtoto ambaye aliyekuwa akiliendesha gari hilo....kulikuwa na vitu vingi vya kuchezea mtoto wao ndani ua gari hilo ghafla yule mtoto akachukua kengere ya kuchezea watoto.......mtoto hiyo aliitingisha kengere ile kwa kuigonga gonga kwenye kiti cha gari....ghafla Tina akasikia mlio wa kengere hiyo.....akastuka
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Domy alitoa simu yake aina ya SAMSUNG NOTE 4
akampiga picha Tina...kitendo cha mwanga wa flash kuwaka kikazuia hali ya tina kubadilika...ghafla taa za alama za barabarani zikaruhusu magari yaliyokuwa uoande wa kushoto kuendelea na safari...kabla hawajafika mbali tina akasema,," turudi nyumbani najisikia nafuu...Domy hakutaka kumpinga Tina...akakatisha kona na kuingia kwenye barabara nyingine...akiiacha ile barabara iliyokuwa ikielekea hospitali....Domy aliendelea kuzipanga gia huku akiliendesha gari lake kwa mwendo wa wastani.....
wakiwa njiani Tina akasema,,"Tupitie kariakoo kuna duka fulani hivi nikaangalie kama wameshaleta mapazia mapya....Domy akajibu,,"Sawa mke wangu kilenzi kisha akaliendesha gari mpaka kariakoo.....kutokana na msongamano wa magari kuwa mengi..Domy aliamua kulipaki gari kwenye hotel moja....ili Tina asguke aende dukani kwa sababu hapakuwa na umbali.......
wakati huo huo alionekana muhudumu wa hotel kwa upande wa jikoni akifunika chakula na kuzipiga hatua huku amekibeba chakula hicho kuelekea kwenye ngazi ya umeme(Lift) akaingia upande wa ndani mlango ukajifunga,,akabonyeza kitufe kilichoandikwa namba (6) lift ikaanza kupanda kuelekea juu....alipofika ghorofa namba sita akazipiga hatua kuufuata mlango ulioandikwa chumba namba (113) akabofya kengere iliyokuwa pembeni ya mlango huo..
****************
kule upande wa nje alionekana tina akizipiga hatua kuelrekea dukani..mara ghafla akastuka...akasita kuendelea kutembea akasimama...akaanza kubadilika macho yake yakaanza kutoa machozi...ghafla akatoweka kimiujiza kuufuata mlio wa kengere.....akajitokeza kwenye ile hotel juu ghorofa ya sita.....akazioiga hatua kuufuata mlango ulioandikwa chumba namba(113) alipofika akaingia upande wa ndani kimiujiza.....akamnyonga yule muhudumu pamoja na Mwanaume aliyekuja Hotelini humo kupumzika na mpenzi wake....baada ya Tina kufanya mauwaji hayo akatoweka kimiujiza na kujitokeza pale alipokuwa amesimama....Tina alionekana kujishangaa sana.....akahairisha kwenda dukani akazioiga hatua za harakaharaka kurudi kule lilipokuwepo gari la Domy...
wakati huohuo kabla Tina hajafika...alionekana Domy akiongea na simu,,ghafla salio likakakata akifungua mlango wa gari na kutoka upande wa nje ...akazipiga hatua kuelekea madukani kununua vocha....
baada ya Domy kutoka Tina akafika akafungua mlango haraka na kuingia ndani ya gari.....akabaki humo akimsubiri Domy...
**************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande mwingine kule kwenye Mgahawa wa Mzee Sule walionekana wateja wakiingia na kutoka huku upande wa nje yakionekana magari mengi na Bodaboda zimepaki nje ya mgahawa huo......watu walifurahia supu iliyokuwa inapikwa kwenye mgahawa huo.....pamoja na ugali nyama choma...mishkaki ,,soseji na sambusa...kwa mbali alionekana mteja mmoja akinyanyuka kutoka pale alipokuwa ameketi na kumfuata mke wa Mzee sule......mtu huyo alifoka huku akisema....,,"yani tangu nimefika hamjaja kunisikiliza!!!haya nataka ugali nyama choma...nichomee uenye mafutamafuta kiasi usikaushe sana...weka pilipili nyingi....kisha akarudi kuketi pale alipokuwa ameketi mwanzo...
*****************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment