Search This Blog

KABURI LA KAZULA - 5

 







    Simulizi : Kaburi La Kazula

    Sehemu Ya Tano (5)



    Mele baada kuhisi kichefu chefu kwa muda mrefu,hatimae alianza kutapika..kitendo ambacho kiliweza kuwashtua wale watu wengine waliokuwa wakiendelea kula zile nyama za binadam. Ghafla wote wakamgeukia Mele na kisha kumtazama kwa macho ya hasira wakati huo mapigo ya moyo ya Mele yalikuwa yakimwenda mbio akiamini kuwa tayali kavunja moja ya mashrati hivyo uwezekano wa yeye kurudi duniani ni ndoto. "Mmmh nitafanya nini mimi? Mele alijilaum mwenye huku machozi yakimtililika mashavuni mwake ikiwa muda huo huo akatokea binadam mmoja ambae miguu yake ilikuwa kama kwato za mbuzi,huku kichwa chake kionekana kuwa na mapembe ya mnyama Swala. Mtu huyo alionekana mbele ya Mele,Mele aliogopa baada kumwona kiumbe huyo wa kutisha,hima alirudi nyuma. Na wakati akizipiga hatua za kurudi nyuma,mala ghafla yule kiumbe aliyetua mbele ya Mele,aliwaamlisha wale watu waliokuwa wakila nyama za binadam kuwa wamshambulie Mele. Kweli punde si punde wale watu walioonekana kuwa na meno marefu,walimfuata Mele kwa kasi,lakini kabla hawajamfikia,ghafla akatokea yule kiumbe aliempokea Mele kule ziwa Victoria. Kiumbe huyo aliwadhibiti wale watu waliotaka kumjeruhi Mele hali iliyopelekea yule kiumbe alietoa amri kukasirika,na hivyo akawataka wale watu watulie ili wao waanze kupigana. Amri ilitoka kwa yule mwenyeji wake Mele,akasema "Ukiniangusha tu chini,hakika nakutunuku huyu mtu mmfanye mtavyo " Alisema kiumbe huyo huku sauti yake ikisikika kwa uzito mkali. Lakini yule kiumbe mwingine nae baada kusikia maneno hayo,alicheka saana kwa dharau huku miale ya mwanga mkali kama radi imulikavyo ..ikamulika kila kona, na punde si punde akanyoosha mkono juu ukatokea upanga makali wa dhahabu...upanga ulionekana kumelemeta kwa makali. Hivyo kiumbe yule ambae ni mwenyeji wake Mele kuzimu, baada kuona adui yake kashika panga kali la dhahabu,nae hakufanya kosa akachukuwa upanga kama uleule na punde si punde mapigano yalianza...viumbe hao wakutisha walipigana,Mele aliogopa sana kwani hao viumbe walipokuwa wakipigana ngurumo kali zilisikika,kitendo kilicho mfanya Mele kuogopa. Vita juu vita..hatimae kengere ilisikika kengere ya kuashiria kwamba muda wa chakula umekwisha amabapo viumbe hao wawili walijikuta wote wako sawa hakana bingwa. Na hiyo ikawa bahati kwa Mele,kwani baada kulia kingere.. yule mtetezi wake ambae ndio mwenyeji wake..aliweza kumwambia Mele afumbe macho na baada ya dakika kadhaa akamwambia afumbue.. hali iliyopelelea Mele kustaajabu kujikuta akiwa kwenye ukumbi mkubwa,ukumbi ulio onekana kupendeza kila kona. "Nifuate huku" Aliambiwa hivyo Mele na yule mwenyeji wake,ambapo Mele alimfuata. Hatimae wakafika kwenye viti wote wakaketi wakati huo kila rugha ikisikika kunako ule ukumbi ambao ulikuwa umesheheni watu mbali mbali,binadam wa kawaida na wasio wa kawaida. Kiukweli Mele alijiuliza maswali mengi kuhusu ule ukumbi,lakini kabla maswali yake haja jijibu..mala ghafla kimya kilitanda mle ndani..na punde si punde mbele ya madhabahu ya ukumbi mahali ambapo kilionaekana kiti kitupu. Ulitokea moshi,ndani ya ule moshi zilisikika sauti ya nyayo za mtu anae tembea. Mele alitaharuki kuona kitendo kile,akajitahidi kupiga moyo konde ili aone nini kitaendelea mbele ya macho yake.

    Yule mtu hatimae alionekana miguu tu..na kimwonekano ilionekana miguu ya mwanamke. "Habari zenu" Ilisikaka sauti hiyo akitoa,sauti ilisika ya kike hivyo Mele akagundua kuwa yule alikuwa ni mwanamke. Baada ya salam, sauti hiyo haikukomea hapo..iliendelea kwa kusema "watu wanaendesha maisha yao kwa raha,watu wanafanya mambo yao kwa raha..lakini ikifikia wakati wa kutoa sadaka,hawatoi.. je, unategemea sisi tufanye nini? zaidi ya kuhitaji damu yako mwenyewe...lakini yote Kwa yote nawashkuru sana wale waliweza kutoa kafara zao kwa wakati mwafaka,pia napenda kuwakumbusha kuwa wale ambao mikataba yao imefikia kikomo,hawataweza kurudi duniani...zaidi kivuli tu nacho kitatafuta sababu ya kifo ili ndugu na jamaa wafaham umauti wako ulivyokukufa" Ilisikika ikisema hivyo hiyo sauti kwa ukali.. Mele akashtuka kusikia hayo..ghafla hofu ikamjaa na kisha kujiuliza "Au inawezekana yule mzee kanitoa kafara pasipo mimi kujuwa?..." Alijiuluza Mele huku moyoni akiwa na wasiwasi.

    Na wakati Mele akiwaza hayo,upande wa pili nako..Duniani. alionekana Marongo akipelekwa na Somela kwa mganga wa kienyeji ili apate kujuwa mahali alipo mke wake ambae ndio Mele..Baada kufika kwa sangoma..Sangoma alifanya mambo yake ya kiganga, na mwishowe akaambia wawili hao yaani Marongo na Somela watazame ukutani mahali ambapo ipo Tv asilia. "Haya tazama embu tazameni ukutani " Alisema mganga huyo,punde akaonekana Mele akiwa katika ule ukumbi Kuzimu. "Wapi hapo..Eeh wapii hapo mzeee " Marongo akiwa na mihemko wa kuogopa,alimuuliza mganga. Hivyo mganga nae huku akicheka alisema "Hahahahaaa...Mkeo yupo kuzimu..kurudi tabu maana yupo hatalini" Alijibu mganga,Somela alishtuka "Kuzimu? .." Alisema hivyo Marongo asiamini kama kweli kile anacho kishuhudia..ghafla akapoteza faham.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Marongo alipoteza faham mala baada kusikia mke wake kaenda Kuzimu, ilichukuwa taklibani masaa mawili Marongo kuzinduka.. na baada kuzinduka,alishtuka kujikuta nyumbani kwa mganga. Marongo akionekana kustaajabu,alimuuliza mganga "Nimefikaje mahali hapa,na wewe ni nani" Alihoji Marongo huku akitazama kila pande,hatimae macho yake yakawa yamegota kwa Somela.. hivyo taratibu kumbukumbu ikawa ikimrudia mwishowe kichwa chake kilirejesha kimbumbuku zote .Marongo akawa amejuwa shida hasa iliyomfikisha pale kwa sangoma.

    "Pole kijana" Mganga alimwambia hivyo Marongo lakini Marongo hukuweza kuitika haraka,zaidi alishusha kwanza pumzi nakisha kuitikia pole ile aliyopewa na mganga. "Ahsante nimeshapowa" Alijibu Marongo,wakati huo mganga nae akiimba nyimbo zake za asiri na kupiga manyanga. Hakika nyimbo hizo za mganga zilidumu ndani ya dakika saba, baada kumaliza kuimba..Alichukuwa pembe la ng'ombe lililo zungushiwa kitambaa chekundu,mganga huyo alie onekana machachari..alilipuza lile pembe. Na mala baada kuhitimisha zoezi hilo,alitulia kisha akamgeukia Marongo. "Kijana mkeo yupo kuzimu je, unataka tumrudishe?..." Aliulizwa Marongo,swali ambalo kwake lilikuwa jepesi kujibu...hivyo haraka haraka Marongo akajibu "ndio mzee hicho ndicho kilicho nileta hapa"

    "Hahahahaaaaaa.. Kijana,safi saaana " Mganga alicheka baada kusikia jibu malidhawa kutoka kwa Marongo...cheko hilo la mganga liliambatana na nyimbo zake...lakini punde si punde alikatisha hiyo nyimbo kisha akasema "Kijana ili mkeo arudi duniani,lazima ufungashe virago umfuate kuzimu " Alisema mganga kwa sauti ya kujiamini. Marongo alishtuka kusikia hivyo..mala ghafla kijasho kikaanza kumtoka "Yani..na...nami..na mimi niende kuzimu?.."

    "Ndio,si unampenda mkeo?..basi lazima ujitose umfuate kuzimu"

    "Aaaah..no..no...nonoooooh! Habari za mimi kwenda kuzimu siwezi,yote namwachia mungu afanye miujiza yake"

    "Hahahaaa..yote namwachia mungu afanye miujiza yake,kama unamwamini huyo mungu wako mbona umenifuata mimi..kwanini hukumpelekea mungu wako hizo shida zako?..Naomba usinichefue,mala moja toweka mbele yangu..towekaaaaa..kabla sijakugeuza ndezi " Kiukweli mganga huyo akionekana kukasirika alimjibu namna hiyo Marongo..Marongo aliogopa maneno ya mganga..hima alijikusanya akasimama,akamtaka Somela waondoke zao.

    "Yani nilijuwa wewe mwanaume,kumbe si lolote si chochote" wakati wakiwa njiani wakitokea kwa mganga wakielekea nyumbani..Somela alimwambia maneno hayo Marongo. "Mmh kwanini Somela unaniambia hivyo,kwahiyo unamaanisha mimi sio mwanaume?

    "Hapana,sina maana hiyo"

    "Ila"

    "Ila ni kwamba wewe muoga sana..huna maamuzi ya kiume"

    "Heeh Somela,kwahiyo wewe unaona kwenda kuzimu kazi nyepesi tu"

    "Hakika kwa kumfuata umpendae?kazi nyepesi kabisa kama kumsukuma mlevi!.."

    "Mmmmmh unasema tu Somela,nadhani hata kama ungekuwa wewe kamwe usinge kubali "

    "Kwanini nisikubali? Yaani niendelee kuteseka moyoni wakati uwezekano wa kuifuata furaha yangu upo?..daah umenipotezea muda wangu bure kumbe mtu mwenyewe huna maamuzi ya kiume"

    "Jamani Somela naomba unielewe kumfuata mtu kuzimu mimi siwezi..tena istoshe mtu mwenyewe mwanamke?..unamfuata leo kesho ukitoka anatembea na mwanaume mwingine ambae humdhanii kabisa..ebo kuzimu siendi,kwanza yeye kafuata nini huko kama marehem? Hakika Marongo aliongea kwa msisitizo...lakini yote kwa yote Somela akaamuuliza "Marongo unampenda mkeo?.."

    "Ndio nampenda sana tena saana"

    "Anha kaa ukijuwa ulipo lalilia ndipo hapo utakapo amkia..Sibiri utaniambia.."

    "Eeh Somela sikuelewi..umemanisha nini sasa?

    "Utanielewa tu..kumbuka damu ya mtu nzito..wewe baada kuzimia,Tv asilia ya mganga ilionyesha Mele akiwa kuzimu..dhamila yake kumrejesha mume wake wa awali duniani"

    "Nani..Kazula?.." Marongo alishtuka kusikia hivyo..na kwa kuwa Somela alikuwa amekalibia nyumbani kwake..hatimae waliagana kila mmoja akaende kwake wakati huo Marongo akionekana kuto amini kama Mele angejitosa kuelekea kuzimu.

    Giza lilikuwa tayali limesha tanda,kiukweli bwana Marongo usiku huo hakupata usingizi..akili yake yoote Ilikuwa ikimfikilia Mele..pumzi kwa kasi alishusha kila mala huku akikumbuka maneno ya Somela aliyokuwa akimwambia..."Mmh hapana lazima na mimi nimfuate Mele kuzimu,siwezi kukubali kirahisi kama kufa nife tu" Alisema Marongo..baada kujishauli kwa muda mrefu.

    Kweli kesho yake asubuhi palipo kucha,Marongo alirudi kwa mganga..lakini kabla hajakalibia kufika,alishtuka kuona umati wa watu kiasi ukiwa umekusanyika nyumbani kwa mganga huyo. Hivyo pole pole Marongo akazipiga hatu kuelekea kwenye umati ule wa watu..na mala baada kukalibia,alimuuliza mtu mmoja kitu kilichotokea hapo nyumbani kwa mganga huyo..Marongo akajibiwa kuwa mganga kafariki. Hakika Marongo aliumia sana,na neno laiti ningejuwa likawa likimrudia akili mwake.



    ******



    Wakati hayo yakijili,Kizimu kwenye ule ukumbi..Mashtaka yalimfikia mkuu aliyekuwa akihutubia na kutoa lahi kwa wanachama wao. Hivyo baada taarifa hiyo kumfikia, mala ghafla mkuu huyo alimtaja mwenyeji wake Mele..mwenyeji wake kwa huko Kuzimu. Hakika kiumbe huyo alitaharuki kusikia akitajwa,hofu ilimjaa akiamini kuwa kitendo kile cha kumtete Mele pindi alipo tapika huwenda kikamghalim maisha,ambapo kiumbe huyo alivua cheni ndogo aliyokuwa nayo akamkabidhi Mele kisha yeye akatoka na kuelekea kule mbele alikoitwa na mkuu wake. "Nikitoka hapa,nifuate kwenye chumba cha nidhanam" Aliambiwa hivyo huyo kiumbe...ambapo chumba hicho cha nidham ndio kile ambacho kilikuwa kikinukia harafu ya damu huku sauti za nafsi nazo zikilia kila kona. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa hakika viumbe wengine waliokuwemo mle ukumbini walitaharuki kusikia kiumbe mwenzao akiambiwa vile,kwani walijuwa dhahili kuwa mtu akifanya kosa na kuingizwa kwenye chumba kile vigumu kutoka. Ukimya ulitawala..na baadhi ya viumbe wengine wa ajabu walionekana kumkodolea macho Mele wakiamini kuwa ndio kampoza mwenzao...lakini wakati viumbe hao walipokuwa wakimkodolea macho Mele,Mele yeye mawazo yake yoote alikuwa akiitazama ile cheni aliyopewa na yule kiumbe alie mpokea huko Kuzimu. "Cheni hii ya nini?.."Alijiuliza Mele huku akiwa ameishika vema kiganjani mwake. Lakini wakati akijiuliza kuhusu cheni ya aliyopewa,ghafla pale alipokuwa amekaa giza nene lilitanda mbele yake na punde si punde kwenye hilo giza aliwaona watu watatu mbele yake,watu hao walikuwa wamevaa mavazi meupe. Kiukweli Mele alihisi woga huku akijiuliza kafikaje fikaje mahala pale,wakati huo mwili wake ukiwa umelowa jasho huku mapigo ya moyo wake yakimwenda mbio. Meleee..." Mele akiwa katika sintofaham alisikia sauti ikimwita..sauti hiyo nzito ilipasa mala mbili bila Mele kuitika kwani alikuwa akiisikiliza..na hapo ndipo alipo gundua kuwa sauti ile ilikuwa ya Kazula..hakika Mele alishtuka sana moyoni akijisemea kuwa "hatimae nadhani muda umefika wa kumaliza mchezo" alijisemea Mele..ila wakati ikisema hayo akakumbuka maneno ya mzee Baluguza " Binti,hirizi mumeo kaivaa kiunoni.. Ili kuipata lazima ufanye nae mapenzi na kisha uikate..itwae kiganjani mwako...muda huo huo bila kuchelewa naenda kwa mwenyeji wako alie kupokea..nae atakuonyesha mlango wa kutokea.



    Mele akiwa katika sintofaham alisikia sauti ikimwita..sauti hiyo nzito ilipasa mala mbili bila Mele kuitika kwani alikuwa akiisikiliza..na hapo ndipo alipo gundua kuwa sauti ile ilikuwa ya Kazula..hakika Mele alishtuka sana moyoni akijisemea kuwa "hatimae nadhani muda umefika wa kumaliza mchezo" alijisemea Mele..ila wakati ikisema hayo akakumbuka maneno ya mzee Baluguza " Binti,hirizi mumeo kaivaa kiunoni.. Ili kuipata lazima ufanye nae mapenzi na kisha uikate..itwae kiganjani mwako...muda huo huo bila kuchelewa naenda kwa mwenyeji wako alie kupokea..nae atakuonyesha mlango wa kutokea.. "mmh nitaanzaje mimi?.." Mele alijiuliza huku akitetemeka mwili mzima,lakini wakati akijiuliza swali hilo punde si punde wale watu watatu waliokuwa wamevaa sanda..walipotea na hapo ndipo ulipo sikika mshindo mkubwa wa hatua. Kiukweli Mele alizidi kuogopa,jasho ndembe ndembe likaanza kumtilika huku mapigo ya moyo wake nayo yakienda kwa kasi yote ikiwa ni woga aliokuwa nao wa kuogopa kile kilichokuwa kikiendelea. Nam! Waakati Mele alipokuwa na hofu na woga moyoni mwake,katika lile lile giza nene ilisikika sauti ikisema "itunze cheni hiyo,kwani ndio msaada wako" Mele alishtuka kusikia sauti hiyo,ambapo alifumbua kiganja chake ili aitazame ile cheni aliyokuwa ameifumba kwa kiganja..cha kustajabisha,Mele baada kufumbua kiganja chake..ghafla ulitokea mwanga mwembamba mrefu,mwanga huo wenye rangi nyekundu uligonga kwenye ukuta,ukuta huo wa jabali ulibomoka mbele ukaonekana mlango uliojengwa kwa dhahabu. "Songa mbele kaguse mlango kwa kutumia cheni" Wakati Mele akistaajabu, ghafla ilisikika sauti ikimwambia hivyo..Kweli Mele alipiga moyo konde kisha akazivuta hatua za pole pole kuufuata mlango,na mala baada kuufikia alifanya kama alivyo ambiwa..kweli mlango ukafunguka.

    Baada mlango kufunguka, Mele kwa mala nyingine alijikuta akitaharuki baada kuona chumba kikubwa mbele yake kilichokuwa kikinuka harufu mbaya ya mizoga pia kuona wafu hai wakiwa wamesimama huku wakitokwa damu midomoni..kucha zao na meno yao yakionekana kuwa marefu..hofu maladufu ilimjaa Mele..lakini licha ya kuwa na hofu,neno ambalo Mele alionekana kuwa nalo makini ni kumtaja mwenyezi mungu. "Hutakiwi kuogopa,ingia kwenye kundi hilo la wafu, tafuta mtu unaemtaka kwa muda wa masaa matano " Ilisikika sauti ikisema hivyo ikimwambia Mele. "Nijitose humu?..Mmh nitaweza kweli? Lakini kwa kuwa nimekuja huku kwa lengo moja,hakika sina budi kutekeleza agizo liwalo na liwe nipo tayali" Mele alijishauli na kujiuliza maswali mwenyewe ndani ya nafsi yake wakati huo akizipiga hatua kuingia kunako kundi lile la wafu walio hai.

    Kiukweli Mele alijikuta akisisimka mwili mzima kwani wafu wale walikuwa wakitoa harufu mbaya mno ya uozo maana kuna wengine walionekana wakitokwa wadudu ila Mele hakujali,bado mwanamama huyo mwenye roho ya chuma alizidi kumtafuta Kazula kwani alienda Kuzimu kwa niaba yake.

    Na wakati hayo yakiendelea, duniani sasa,Marongo alilaani sana maamuzi yake ya kukataa kumfuata mkewe Kuzimu akahisi kuwa wakati wa yeye kumkosa Mele umewadia. "Hapana siwezi kukubali kirahisi rahisi tu,waganga wapo wengi..lazima nimfuate Mele kuzimu" Alijisemea kijana Marongo kwa hasira kali huku akipiga piga kifua chake.

    Kweli muda huo huo alijiandaa,moja kwa moja akaelekea nyumbani kwa shekhe mmoja ambae alifahamika kwa jina Shekhe masoud. Shekhe masoud mzee kutoka unguja alikuwa akijihusisha na mambo ya kiganga na hivyo Marongo Kwa kuwa alimfaham,akaona kuwa Shekhe huyo aanaweza akawa msaada kwake kwa kuweza kumfanikishia safari ya kuelekea kuzimu kumfuata Mele. "Karibu kijana "

    "Ndio mzee Ahsante bwana..mmmh shida yangu mzee mimi nataka kujuwa,hivi kuna uwezekano wa mtu kwenda kuzimu na kisha kurudi duniani" Alihoji kwanza Marongo ili apate uhakika kabla hajachukuwa maamuzi. "Uwezekano upo haswaaa..tena kwa asilimia kubwa,muhimu wewe kufuata masharti..Na je Kuzimu wewe unafuata nini weye " Shekhe Masoud nae alihoji huku akimtazama Marongo kwa jicho la tatu. Marongo baada baada kuulizwa.. alikaa kimya kidogo kisha akashusha pumzi akamgeukia Shekhe na kumjibu "Kuzimu namfuata mke wangu,ana siku tano sasa yuko huko...pia bado mzima yupo hai " Alijibu Marongo.. "Kuzimu kafuata nini yeye?.."

    "Kamfuata aliekuwa mume wake enzi za uhai wake..istoshe mimi bado nampenda sitaki nimpoteze"

    "Aaaah kazi ndogo sana hiyo kijana,cha msingi piga moyo konde...pia naomba kama upo tayali usiku wa leo twende makaburini ili uweze kuanza mala moja safari yako ya kwenda kuzimu"

    "Sawa nipo tayali" Alijibu Marongo kwa sauti kuu. Hakika jibu hilo la Marongo lilimfrahisha sana Shekhe Masoud,na hivyo kilicho baki kikisubiliwa ni muda na wakati wa giza kwisha tanda...Marongo aanze hima safari ya kwenda kuzimu kumfuata Mele ikiwa wakati huo Mele nae akiwa katika hatua ya kumtafuta Kazula kwenye jopo la wafu.

    "Umebakiza dakika nane za kumpata mtu ulie mfuata..zikipita basi hutoweza kuwatoka hao wafu" ilisikika sauti hiyo ikimwambia Mele..hakika Mele alitaharuki moyoni mwake kwa hofu kubwa na woga akajikuta akidondosha chini ile cheni aliyopewa na mwenyeji wake ambae tayali ameshapoteza..hivyo baadala Mele aendelee kumtafuta Kazula, akajikuta akiitafuta kwanza cheni ilihali muda nao ukizidi kutarantadi..maana laiti kama ataiacha cheni kamwe hatoweza kumpata Kazula

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Umebakiza dakika nane za kumpata mtu ulie mfuata..zikipita basi hutoweza kuwatoka hao wafu" ilisikika sauti hiyo ikimwambia Mele..hakika Mele alitaharuki moyoni mwake kwa hofu kubwa na woga akajikuta akidondosha chini ile cheni aliyopewa na mwenyeji wake ambae tayali ameshapoteza..hivyo baadala Mele aendelee kumtafuta Kazula, akajikuta akiitafuta kwanza cheni ilihali muda nao ukizidi kutarantadi..maana laiti kama ataiacha cheni kamwe hatoweza kumpata Kazula..Hivyo Mele alichuchumaa chini kuitafuta cheni,hatimae aliipata ikiwa kwenye mguu wa mmoja wa wafu. Haraka sana Mele aliichukua kisha akainuka ambapo baada kusimama alijikuta akikutana uso kwa uso na marehem mume wake ambae ni Kazula. Kiukweli Mele alisisimka mwili mzima kijasho kikaanza kumtoka asiamini kama kweli kafanikiwa kumwona Kazula. "Hutakiwi kuchelewa, muda umekwisha haraka sana mguse ili mtoke hapo mlipo "Wakati Mele akiwa hajaamini kama kweli kafanikiwa kumwona Kazula, ghafla alisikia sauti ikisema hivyo. Kweli Mele hakutaka kuchelewa haraka akamgusa nao wakafanikiwa kutoka kwenye lile jopo la wafu wakati huo muda ule alio ambiwa Mele baada kutimia, ulizuka moto mkubwa...sauti za vilio zilipasa maeneo mbali mbali kuzimu.. "waooh nafurahi kuiokoa furaha yangu" Alisema Mele huku akitabasam wakati huo akiwa amebakisha sharti moja tu. Nalo ni kufanya mapenzi na Kazula ilihali Kazula akiwa bado hajarejesha kumbukumbu zake za kujua kinacho endelea..Hivyo Kazula alikuwa kama zezeta tu,lakini licha ya Kazula kuwa katika hali hiyo,ila Mele hakuona sababu ya kuacha kufanya kile alicho kusudia kufanya,hivyo kwa kutumia mkono wake alishika Sehem nyeti za Kazula,nae ume wa Kazula ukasimama huku Kazula akionekana kucheka kicheko ambacho kilisikika kwa mwangi hakika kilikuwa kicheko cha kutisha. Mele aliendelea, na mwishowe akafanikiwa kufanya mapenzi na Kazula bila kujali jinsi alivyo kuwa akitoa harufu mbaya ya uozo..Kweli juhudi zake Mele zilimfanya kufanikiwa kuikata hirizi iliyokuwa kiunoni kwa Kazula. "Lazima ufanye nae mapenzi na kisha uikate..itwae kiganjani mwako...muda huo huo naenda kwa mwenyeji wako alie kupokea..nae atakuonyesha mlango wa kutokea "Mele akakumbuka maneno hayo ya mzee Baluguza aliyo ambiwa wakati wa kwenda kuzimu. Hakika huo ukawa mtihani mwingine kwa Mele,kwani ikumbukwe kuwa mwenyeji wake aliempokea kuzimu kashauliwa baada kugundulika kukutetea maovu ya Mele pindi alipo tapika chakula alicho pewa.."nifanye nini mimi? Alijiuliza Mele wakati huo hirizi na cheni anazo kwa viganja vyake..na wakati akijiuliza asijue cha kufanya,ghafla Kazula alitoweka kimiujiza,na punde si punde Mele mbele yake akaona njia ndefu nyembamba iliyo nyooka.."usichelewe kimbia haraka" Safari hiyo ilisikika sauti ya kizee ikimwambia Mele aifuate hiyo njia nyembamba..kweli Mele akionekana kuwa na hofu,alipiga moyo konde kisha akaanza kutembea kwenye ile njia pole pole...ila baada kugeuka nyuma na kuona kuwa kule alikotoka njia ilikuwa ikitokomea na kubaki giza, haraka sana Mele alitimua mbio..

    Mele alikimbia na mwishowe njia hiyo ikafika ukingoni ambapo mbele yake aliona shimo kubwa na ndefu lilikuwa na giza nene..Hakika Mele aliogopa sana akajiuliza afanye nini?wakati huo hiyo njia nayo ilikuwa ikibomoka kuelekea mahali alipo Mele...Mele alizidi kuogopa..akajifunga kiunoni hirizi aliyo itoa kwa Kazula,huku akiwa ameifumba cheni kwenye kiganja chake...hatimae alijitosa kwa kujitupa kwenye lile shimo.



    ********************



    Wakati Mele akiamua kujitosa kwenye hilo shimo ambalo hakujua mwisho wake,upande wa pili nako..Bwana Marongo na shekhe Masoud walijisogeza kunako makaburi usiku huo ulikuwa usiku wa pata saa mbili.. Hivyo shekhe Masoud alifanya matambiko yake kwenye kaburi moja hivi ambalo lilionekana la zamani, kisha akamwambia Marongo asimame juu ya kaburi hilo."kijana,upo tayali kwenda kuzimu? Shekhe Masoud alimuhoji Marongo. "Ndio nipo tayali" Marongo nae akiwa juu ya kaburi alijibu kwa kujiamini. Lakini Shekhe Masoud hakutaka kuridhika na jibu moja,hivyo alirudia kumuuliza mala tatu,nae Marongo alijibu vile vile kwa kujiamini. "Sawa sawa..bwana nimekubali kwa majibu yako,lakini sasa kumbuka huko unakotaka kwenda ni pazuri endapo tu kama utafanikiwa kufuata masharti nitakayo kwambia.." Shekhe Masoud alikaa kimya kidogo huku akichoma udi na bani..kisha akaongeza kwa kusema "Kwanza, lazima uwe jasiri..nikiwa na maana kuwa usiogope chochote kitakacho tokea mbele yako.. pili vyakula,kijana chakula chochote kijacho we kula tu.. vile vile usimtaje mungu wako..tena katika hili kuwa makini sana..endapo ukicheza vibaya huu mchezo,kamwe hutorudi duniani..na endapo ukirudi,basi utakutwa na na matatizo..kwisha kusema hayo,Shekhe Masoud alimfunga hirizi Marongo begani kisha akasema "Kijana masharti mepesi ushindwe mwenyewe..hirizi hii itakusaidi wewe kutimiza kile ulicho kilenga...safari njema" kwisha kusema hivyo,Kaburi lilibomoka Marongo akajikuta akiwa ndani katikatika ya wafu..Marongo aliogopa sana akapiga kelele za kumwita Shekhe Masoud ili amuokoe... hivyo kitendo kile cha Marongo kupiga kelele kwa woga,kiliwafanya baadhi ya wafu walio hai kuamka kutoka mahali walipo lala..hima walimfuata Marongo...Marongo alizidi kupiga mayowe ila mayowe yake hayakumsaidia..zaidi alijikuta akipoteza fahamu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wakati hali hiyo ikimkuta Marongo, upande wa pili nako.. kando ya ziwa Victoria saa za usiku,ulionekana mwili wa Mele ukielea juu ya maji mfano wa mtu aliekufa..Hali hiyo aliipata mzee Baluguza, hivyo haraka alikwenda pale ziwani akambeba na kisha kumpeleka nyumbani kwake kumtibia. Yalipita masaa taklibani sita bila Mele kurudisha faham,lakini mnamo saa tano ya asubuhi..Mele alipata faham baada tiba za mzee Baluguza kufanya kazi ipasavyo. "Pole mama" Mzee Baluguza alimsabahi Mele,lakini Mele hakujibu kwani akili yake ilikuwa bado haijatengamaa vizuri..Na baada liasali moja mbele,hatimae Mele alipata kidogo uelewa wa kugundua kuwa yupo duniani na sio kuzimu tena.



    BAAADA WIKI MOJA.



    Hali ya Mele ilikaa sawa.Mzee Baluguza akafanya mambo yake na kufanikiwa kumrejesha Kazula katika duniani huku akimwambia Mele kuwa akapande mgomba kwenye kaburi alilokuwa amezikwa Kazula,hakika kilikuwa ni kitendo cha kuishangaza dunia..waandishi wa habari walifurika kijijini kushudia miujiza ya mtu aliekufa na kuzikwa kurejeshwa hai...Hata hivyo Kazula licha ya kurudishwa duniani ila bado akili yake ilionekana kutokaa sawa na hivyo basi ikambidi mzee Baluguza kuendelea kumtibia hadi pale alipo pata kumbukumbu vizuri ya kumtambua kila mtu. Hakika machozi yalimtoka Kazula hasa baada kugundua kuwa mama yake ameshafariki kama ilivyokuwa kwake..ila yote kwa alipiga moyo konde akijipanga kuganga yajayo.

    "Mwanangu unajisikiaje kumwona tena huyu kenge asuye na kizazi?

    "Mmmh mama tafadhali,Kazula nilimuua kwa sababu yako,na nimemrejesha kwa kuamua mimi..Kazula kizazi anacho ila mimi ndio ambae sina kizazi..tazama miaka mingapi naish na Marongo? Je, umeniona nikiwa na mtoto? Tafadhali mama naomba uniache mimi na Kazula" Alisema Mele huku akitokwa machozi ikumbukwe kuwa chazo cha umauti wa Kazula ni mama yake Mele baada kumshauli mwanae aende kwa mganga amtengenezee dawa ampe mumewe ili wapate mtoto...ikiwa mama huyo huyo aliongea na mganga huyo huyo ambae ni mzee Baluguza kuwa pindi mwanae atakapo kuja kuchukuwa dawa ampe sumu ya kumuua Kazula ili mwanae apate kuolewa na Marongo kijana ambae kwake maisha yalikuwa mazuri kwa kiasi flani..kweli mtego huo mama wa Mele ulifanikiwa..pasipo Mele kujua..ila mwishowe Mzee huyo Baluguza aligeuza mchezo kwa kumrejesha Duniani Kazula.

    Hakika furaha ilitawala kwa Mele na Kazula....Wakati huo kwingineko Katika majalala ya takataka alionekana Marongo tayali ameshakuwa kichaa adhabu pekee aliyopewa baada kufeli hatua ya kwanza..

    Siku zilisonga..ambapo usiku mmoja Mele alitokewa kwa njia ya ndoto na kivuli cha mwenyeji wake wa kuzimu..kivuli hicho kilimtaka Mele ampe cheni yake..kweli Mele alisimama akafungua droo akaichomoa cheni na kisha kumpa. Usubuhi palipo kucha,Mele alifungua Droo kuitazama cheni..kweli hakuikuta hivyo akajua kabisa yule mtu aliemtokea kaondoka nayo...Maisha yakaendelea kuwa burudani kwa wawili kwa wawili hao...huku Marongo akitaabika na uwendawazim wake majalani..kwani alishindwa kupiga moyo konde kama alivyo fanya Mele.

    "Yaani wewe umenisumbua vibaya mno kukufuata kuzimu" Alisema Mele akimtania Kazula... "Aaah pole ila sindio mapenzi hayo?."

    "Mmh hatakama...mwenzio nimekula vitu vya ajabu,nikikumbuka nahisi kichefu chefu" "hahahaaaa pole mpenzi"

    Yote hayo Kazula na Mele walikuwa wakiongea huku wakiwa kitandani wawili hao wapendanao...

    "sasa" alihoji Mele

    "Kuhusu nini" akajibu Kazula. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ndoa Jamani Kazula sipendi tuachane nakupenda na nitazidi kukupenda tu"

    "Aaanhaa ndoa?!usijali tutafunga tu"

    Mele alifurahi kusikia jibu hilo la Kazula,moyoni akawa akijisemea "Sikuwa na nafasi ya kukushkuru mungu kwa muda wa siku kumi na nne nilizokuwa kuzimu,sasa huu ni wakati wa kukushkuru Ahsante mungu wewe ndio kila kitu,laiti ungeamua basi ningefeli...ila umeamua mja wako nifauru kweli nimefauru...by by Marongo" Alijisemea hayo Mele ndani ya nafsi yake huku akiwa amelalia kifua cha Kazula.

    Kweli hatimae walifunga ndoa,Mungu si athumani Mele alipata tiba ya uzazi na hivyo Kazula na Mele wakawa wamepata mtoto,furaha isiyo kifani ikazidi kutawala..kwa wanandoa hao.



    ◀◀◀MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog