Search This Blog

KABURI LA KAZULA - 4

 







    Simulizi : Kaburi La Kazula

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mele alizidi kuweka nia pale pale..nia ya kuelekea kuzimu kufuata hirizi ili ampe mzee Baluguza, nae mzee huyo ambae ni mganga wa kienyeji..aweze kumrejesha Duniani Kazula.

    Hivyo siku zilisonga amani kidogo ikionekana kutawala malangoni kwa Mele..na hatimae ikafika siku ya alakhamisi..ambapo usiku wa siku hiyo,alitokea mzee Baluguza chumbani kwa Mele akawa amewakuta Mele na mume wake wakiwa wamesinzia fofofo. Mzee Baluguza akiwa ameshika kibuyu kidogo mkononi mwake...kibuyu ambacho ndani kilikuwa na dawa..alichovya kidole chake cha Kati ndani ya kibuyu kile alichokuwa ameshika,kisha akampaka usoni Marongo kitendo kilicho mfanya Marongo kuendelea kusinzia pasipo kutikisika. Mzee baluguza alicheka kwanza baada kufanya kitendo kile kisha akamwita Mele "Binti...Binti...Bintiiiii" Aliita mzee Baluguza,sauti hiyo Mele aliisikia kwa mbaaali ambapo aliweza kushtuka na kugundua kuwa sauti ile ilikuwa ya mzee Baluguza, Mele aliyafikinya macho yake ili apate kuona vizuri kwa Maana alikuwa ametoka usingizini. Kweli hatimae macho yaliona vizuri...akaweza kumuona mzee Baluguza akiwa amesimama kwenye kona ya chumba,huku akiwa amevaa nguo nyeusi..na usoni akiwa amejichora alama mbali mbali watumiazo waganga wa kienyeji. "Hahahahaaa...Binti simama na kisha nifuate " Alisema mzee Baluguza kwa sauti ambayo ilisikika ikijirudia mala mbali mbali. Hivyo Mele akionekana kuwa na hofu kubwa moyoni mwake,alijifunga khanga yake moja vizuri kwa mwili wake kisha akazipiga hatua kumfuata mzee Baluguza pale kwenye kona ya chumba...na mala baada Mele kumfikia mzee Baluguza, punde si punde walitoweka mle chumbani,wakaibukia kwenye makaburi ya mji. Mele aliogopa sana lakini mzee Baluguza alimtuliza akimwambia "usihofu ondoa shaka kabisa sawa binti?...." Alisema mzee Baluguza huku wakiwa tayali wamesimama juu ya kaburi. Lakini licha ya mzee Baluguza kumwondoa hofu Mele kwa kumwambia hivyo,ila baado Mele alionekana kuogopa...kitendo ambacho kilimfanya mzee Baluguza kumhoji "Kabla hatujaendelea...unaonekana huna ujasiri wa kwenda kusimu je, utaenda au huendi? Alihoji mzee Baluguza kwa sauti iliyo ambatana na hasira. "Babu mimi nipo tayali kwenda..wala sina hofu kabisa" Mele alijibu. "Ok kama huogopi,ngoja nianze kukuelekeza sasa. "Kitu cha kwanza,tafuta mayai ya ya kuku matatu. Nenda nayo moja kwa moja mpaka ziwa victoria,utakapofika kando ya ziwa Victoria, yatupe hayo mayai matatu ziwani huku ukinuia maneno fulani nitakwambia baadae maneno hayo. Na baada kufanya hivyo,pale ziwani patatokea barabara..kwahiyo wewe cha kufanya,ifuate barabara hiyo bila kuogopa..ambapo utakapo piga hatua mbili au tatu,barabara hiyo itapotea.. hivyo usiogope kwani huko utakutana na mwenyeji wako ambae nae atakuwa mtu mwenye jicho moja usoni nywere zake zitakuwa vichwa vya nyoka huku miguu yake nayo ni kama kwato za ng'ombe. ... Kwahiyo Wala usimwogope Binti maana huyo ndio atakupa mbinu zote za kumpata Memeo huko kuzimu"

    Mele baada kusikia maelekezo hayo,kiukweli moyoni alizidi kujawa na hofu ingawa usoni mwake alionekana kuwa kawaida.. hivyo mzee Baluguza hakuweza kujuwa kama Mele anahofu na safari hiyo ya kuelekea kuzimu. "Kitu kingine ambacho nakuasa, tafadhali usiogope wala usikatae kula chakula au kinywaji chochote utakacho letewa..maana endapo ukikataaa,basi kurudi duniani kwakweli itakuwea vigumu...hivyo chunga sana usicheze vibaya katika huu mchezo wa kufuata hirizi aliyo ivaa mumeo" aliongeza kwa kusema hivyo mzee Baluguza, Mele akashusha pumzi kwa nguvu kisha akauliza swali" sasa babu hiyo hirizi mume wangu kaivaa wapi? Shingoni..au kiunoni? .."

    Mzee Baluguza alicheka kwanza baada kusikia swali la Mele, na baada kumaliza kucheka akasema "Binti,hirizi mumeo kaivaa kiunoni"

    "Kwahiyo nitaichukuaje?

    "Lazima ufanye nae mapenzi na kisha uikate..itwae kiganjani mwako...muda huo huo naenda kwa mwenyeji wako alie kupokea..nae atakuonyesha mlango wa kutokea " Alisema mzee Baluguza, Mele alishtuka akataka kuuliza swali lingine lakini akahofia Kuwa anaweza kumkera mzee huyo. Hivyo Mele akakaa kimya wakati huo akiwa amejiinamia,na mwishowe aliinua uso wake na kisha kusema "Naomba uniambie basi hayo maneno nitakayo nuia"

    "Naaam kabisa kumbe nia unayo. Hahahahaaa..binti utakapo fika pale ziwa Victoria..tupa yai la kwanza huku ukisema..zisonye umokoye mugabo...eenhee sema hivyo kila utakapo kuwa ukirusha yai moja baada ya lingine..na mwishowe utatokea hiyo barabara niliyokwambia hapo awali" mzee Baluguza alimwambia hivyo Mele...ambapo Mele nae alianza kuyaongea hayo maneno huku akirudia mala mbali mbali ilimladi ayakariri ili asiyasahau. Baluguza alicheka kidogo kisha akamwambia "simama binti tuondoke...kesho fanya kama nilivyokwambia..safari utaianza jioni saa kumi na moja" Mele alisimama akaambiwa afumbe macho punde si punde akaambiwa afumbue...hatimae akajikuta yupo chumbani...na hivyo mzee Baluguza akamkabidhi Mele kitambaa ambacho kilikuwa na fundo...ndani ya lile fundo kulikuwa na unga fulani mwupe. "Chukuwa hiki kitambaa,katika hilo fundo kuna unga maalum mweupe...unga huo utajipakaa kabla hujaanza kurusha mayai ziwani..sawaa?.." CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa babu" Mele alimjibu mzee Baluguza ikiwa mzee huyo nae akimgusa kwa mala nyingine Marongo...kitendo kilicho mfanya Marongo kutikisika kwa kugeukia upande wa pili wa ubavu wake... kwisha kufanya hivyo... mzee Baluguza alipotea mle chumbani kwa Mele...ikasalia sauti ikimuhimiza Mele kwa kusema "kesho kuzimu" ilisema hivyo hiyo sauti huku ikimaliza kwa kicheko kizito.



    Kiukweli Mele alionekana kukosa usingizi...muda wote alikuwa akiitafakari safari hiyo ya kwenda kuzimu. Maswali mengi Mele aliweza kujiuliza,na kitu pekee ambacho kiliweza kumwogopesha ni kuhusu urejeo wa kurudi tena duniani pindi atakapo kosea sharti. "Mmh sijui itakuje nikikosea mashart..au ndio utakuwa mwisho wangu wa kuendelea kuishi duniani? Ee mungu nisaidie niweze kuupiku mtihani huu mzito uliopo mbele yangu" Alijisemea hivyo Mele ndani ya nafsi yake, nakisha kujivutia vizuri shuka yake ili aanze safari ya kutafuta usingizi. Hakika shunguli haikuwa ndogo..shughuli ya kutafuta usingizi..kwani kila alipokuwa akijaribu kuliondoa wazo la kwenda kuzimu,ila baado lilimjia. Hali iliyofanya mapigo ya moyo wake kwenda mbio na kisha usingizi uliokuwa ukimnyemelea kwa mbali hutoweka. Hivyo Mele aliendelea kujitahidi kutafuta usingizi kwa mbinde,wakati huo nao muda ndivyo ulivyokuwa ukizidi kwenda..na hatimae ikafika saa tisa usiku..usiku wa siku ya ijumaa,siku ambayo saa za jioni Mele ataanza safari ya kuelekea kuzimu. Ghafla Marongo akaamka kutoka usingizini,huku akionekana kuwa na furaha..ambapo alimshika Mele kiunoni akionekana kutaka haki yake ya ndoa. Hivyo kutokana na Mele kuwa na mawazo ya kuiwazia safari ya kuzimu..hatimae aliona endapo akifanya tendo la ndoa na mume wake itampelekea kusahau kuhusu safari ya kuzimu,ambapo walau ataweza kupata usingizi kwa muda ule wa saa tisa japo masaa yote alikuwa tongo macho. Kweli Marongo akajaa katika kifua cha Mele na hatimae wakatimiza azma yao. Baada ya tendo kila mmoja alikuwa hoi..kitendo kilichompelekea Mele kupata usingizi mzito...alisinzia mpaka saa tatu asubuhi. Hivyo baada kuanika alifanya usafi wa nyumba na mazingira..alipomaliza alikwenda dukani kununua mayai matatu kama alivyo agizwa na mzee Baluguza, Saa kumi ilipo timia,Mele akaanza safari ya kuelekea ziwa Victoria..ambapo alipanda daladala alipofika kituoni akashuka kisha akapanda bodaboda ambayo ilimfikisha mpaka pembezoni mwa ziwa Victoria...Kwa hakika ziwa lilonekana kutulia kwa muda ule wa saa kumi na moja ikikimbilia saa mbili jioni..mawimbi makubwa kiasi yalionekana huku upepo nao wakawaida ukivuma kwa utadi kabisa...Mele alitazama huku na kule huku mkono akiwa ameshika mfuko mweusi,na punde si punde akaingiza mkono wake wa kulia ndani ya ule mfuko alio ushika. Akatoa kitambaa kilichokuwa na fundo,hivyo Mele akalifungua lile fundo akaona unga mweupe. "Chukuwa hiki kitambaa,katika hilo fundo kuna unga maalum mweupe...unga huo utajipakaa kabla hujaanza kurusha mayai ziwani..sawaa?.." Mele alikumbuka alivyo ambiwa na mzee Baluguza pindi alipokuwa akimkabidhi kitambaa hicho chenye fundo. Hivyo baada kukumbuka,hatimae akaanza kujipakaa usoni.. baada kumaliza kujipaka usoni unga huo,hatimae akaanza kuyatupa yale mayai matatu ziwani huku akinuia maneno aliyo ambiwa na mzee Baluguza. Kweli punde si punde..pale ziwani palitokea barabara kubwa huku magari nayo yakipishana kama ilivyo katika jiji la Dar es salaam. Hakika Mele alistaajabu sana kuona maajabu yale...na mala ghafla katika barabara ile,ilionekana gari aina ya DCM..gari ambayo ilikuwa imebeba abiria ambao kimwonekano hawakuwa binadam wa kawaida..kwa maana wengi wao ngozi zilikuwa na rangi za kijani huku wengine wakiwa na nasikio mrefu na jicho moja. Mele aliendelea kushangaa..lakini punde akasikia sauti ikimuhimiza kuwa asimamishe ile gari ya DCM. "Binti hutakiwi kuogopa..simamisha hiyo gari..nayo ndio itakupeleka kuzimu " ilisema hiyo sauti kwa uzito zaidi.

    Mele akashtuka kusikia hiyo sauti ya kutisha,kwani aliemwambia hivyo hakumwona bali alisikia sauti tu. Hakika Mele alishusha pumzi kwa kasi huku akisita kuisogelea ile barabara..lakini mwishowe aliipungia mkono ile gari DCM ambapo nayo ilisimama..baada kusimama Mele alipanda na punde si punde ziwa Victoria likajifunga..na barabara ile ikawa imetoweka.



    Ndani ya ile DCM aliyopanda Mele,ndani aliwakuta watu wa maajabu ajabu...ambapo kuna baadhi ya watu walikuwa na Rangi nyekundu ngozi zao, pia wengine walikuwa na macho kama ya nyoka na hata ngozi zao pia zilikuwa mfano wa ngozi ya Nyoka...Na chakustajabisha zaidi ni baada Mele kumwona binadam mwenye jicho moja huku mkononi akiwa na vidole vitatu"Mungu wangu" Mele alijisemea mwengewe ndani ya nafsi yake huku akitetemeka. Lakini baada kusema hivyo...mala ghafla alisikia sauti ikisema "hupaswi kutaja jina la mungu wako huku" Ilisema hiyo sauti ambayo ilisikaka ikiwa na mwangwi. Hakika Mele alishtuka kusikia hivyo...akishindwa kuelewa ile sauti imetokea wapi...na imejuaje kama kamataja mungu? "Mmmh" Mele aliguna wakati huo ile DCM ikasimama akashuka abilia mmoja kisha safari ikaendelea. Kiukweli Mele alipokuwa ndani ya ile gari,kitu pekee kilichomshangaza ni baada kuona utaratibu katika vyombo vya usafiri..upo vilevile kama ilivyo duniani. Kwani aliweza kuona abilia wakingojea magari vituoni... pia biashara ndogo ndogo nazo zikiendelea kufanyika..zilinunuliwa bidhaa zao ingawa wanunuzi ndio hao watu walioonekana kutisha kulingana na maumbile yao..kiukweli Mele alipiga moyo konde Safari ikaendelea..anako kwenda hapajui,hivyo ilimbidi atulie kama mzigo.

    Gari hiyo ainana ya DCM..ilitembea kwa umbali mrefu,na hatimae ilifika mwisho ambapo abiria wote walishuka kunako gari ile..na baada abiria wote kushuka,ghafla ikawaka moto..na katika ule moshi mzito wa gari iliyokuwa ikiteketea kwa moto,walitokea watu kumi na wawili. Watu hao kumi na mbili,wote walikuwa wamevaa nguo nyeupe yaani sanda. Mele alishtuka akahema kwa nguvu huku akiogopa. Lakini alipokumbuka kuwa akifanya mchezo hatorudi duniani,ilibidi atulie aangalie kipi kitajili. Hivyo wale watu walio vaa sanda walizipiga hatua kuelekea kule alipo simama Mele na wanzake aamabao walishuka kwenye ile gari DCM. Na mala baada kuwafikia,ghafla kila mmoja alimshika mwenzake..yaani wale jamaa waliovaa sanda kila mmoja alimshika abiria na kisha kupotea nae. Mwishowe wote wakawa wametoweka ila akabaki Mele. Hakika Mele aliogopa sana akajiuliza atafanya nini? Hali yakuwa kaachwa peke yake? Lakini wakati akiendelea kujiuliza,punde si punde ilisikika nyimbo ya kiarabu. Nyimbo hiyo Mele aliisikia kwa mbali ila kadri muda ulivyozidi kwenda,ndivyo ile sauti nayo alizidi kuisikia kwa ukaribu zaidi. Kiukweli hofu mala

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    dufu ilizidi kumjaa Mele lakini alijitahidi asitaje neno mungu..kwani neno hilo alionywa tangu hapo awali alipokuwa ndani ya DCM. Hivyo hiyo nyimbo ya kiarabu iliendelea kusikika kwenye masikio ya Mele,na punde si punde giza nene likatanda sehem ile aliyosimama Mele.. giza hilo kwisha kutanda, ile nyimbo ya kiarabu ilikata... wakati huo huo ikasikaka sauti nzito. Sauti hiyo ikisema ikianza kwa kicheko" Hauna haja ya kuogopa,usihofu jisikie uko nyumbani" Ilisema hiyo sauti. Lakini Mele akaishia kuguna tu...na mwishowe akajitahidi kuhoji japo kwa wasiwasi "kwani wewe nani? Na uko wapi? Alihoji Mele.. swali ambalo lilimfanya yule mtu kucheka kwa mala nyingine..safari hiyo kicheko chake kiliambatana na upepo mkali na ngurumo nzito zilizo mfanya Mele kuogopa sana. "Unataka kuniona? Yule alihoji. "Ndio" Mele nae akajibu hivyo. Ambapo kimya kidogo kilitawala. Baada kimya hicho kutoweka,ghafla Mele aliona mwanga hafifu..na katika mwanga ule Mele alimwona mtu akitembea kuja mahali alipokuwa amesimama. Mele alizidi kuogopa kwa maana huyo mtu hakuwa wa kawaida. "usiogope kwani huko utakutana na mwenyeji wako ambae nae atakuwa mtu mwenye jicho moja usoni nywere zake zitakuwa vichwa vya nyoka huku miguu yake nayo ni kama kwato za ng'ombe. ... Kwahiyo Wala usimwogope Binti maana huyo ndio atakupa mbinu zote za kumpata Memeo huko kuzimu" Mele alikumbuka maneno hayo aliyo ambiwa na mzee Baluguza....Baada Mele kukumbuka hatimae akashusha pumzi kwa kasi huku akimeza mabunda ya mate kila sekunde yote ikiwa dalili ya woga. Yule mtu alizipiga hatua za polepole kumfuata Mele.. Na baada kumfikia, akasema "Fumba macho"

    Mele alifumba macho,ghafla akasikia joto kali..akataka kufumbua macho lakini nafsi ikamsuta akiamini kuwa huwenda akapata madhala. Hivyo aliendelea kuyafumba macho yake mpaka pale alipo ambiwa fumbua. "Fumbua" Mele alifumbua macho,hakika hakuamini baada kuona yupo katikati ukumbi mkubwa,ukumbi ambao ulikuwa umepambwa na maua ya kila aina huku marashi mbali mbali nayo yakiupendezesha ule ukumbi. Mele hakuwa peke yake...aliyainua macho yake kutazama kila upande katika ule ukumbi,akaona kila kiti kina mtu. Na watu hao hawakuwa wa kawaida kama ilivyo binadamu...kwani kuna baadhi walikuwa hawana hata Nyama katika miili yao zaidi ya mifupa mitupu huku wengine wakionekana nusu mtu nusu binadamu..si wote walikuwa hivyo,la khasha wengine walikuwa binadam wa kawaida.. Na siku hiyo kumbe ilikuwa siku ya Sherehe kuzimu. "Twende huku" Mele wakati akiendelea kustaajabu,aliambiwa hivyo na yule mwenyeji wake aliemfikisha kuzimu kwa kupotia njia ya ziwa Victoria. Mele aliambatana na yule mtu,moja kwa moja wakaingia mpaka kwenye chumba ambacho kilikuwa kikinukia harufu ya damu huku sauti za nafsi za watu zikisikika kila kona.



    Baada Mele kuingia katika kile chumba kilichokuwa kikinukia harufu ya damu..huku zikisika sauti za nafsi za watu waliokufa.. sauti ambazo zilikuwa zikilia wakati wote. Hatimae yule mtu ambae alikuwa nae wakati wote, alimwambia Mele "Tazama mbele " Mele akatazama akaona mlango mkubwa ulijengwa kwa dhahabu...wakati Mele akishangaa,ghafla ule mlango ukajifungua mbele wakaonekana watu wakila nyama za binadam..kiukweli alistaajabu sana,mwemgewe akajiuliza je, nitafanikiwa kweli? Akiwa bado hajapata jawabu juu ya kile alicho jiuliza,punde akadikia tena sauti ikisema "ingia kwa hicho chumba" Mele aliambiwa aingie mle chumbani..hivyo Mele hakusita,hara sana akazivuta hatu akaingia kwenye kile chumba...kisha lango lile la dhahabu liliokuwa limepambwa kwa nembo mbali mbali za mashetani likajifunga."keti kwenye kiti " Sauti iliyosikika kwa uzito,ilimwambia hivyo Mele ikiwa Mele akiendelea kuwashangaa wale watu waliokuwa wakishambulia nyama za binadamu. Hatimae Mele alikaa,na punde si punde akaletewa bilauli lililojaa nyama za binadamu,ambapo Mele alipozigeuza geuza akakuta ni Sehem ya siri za mwanaume. Kwa hakika Mele alijikuta akitaharuki ghafla kinywa chake kikajaa mate,kichefu chefu nacho hakikuwa mbali. Mele akajihisi kutapika,lakini kabla hajatapika Mele akakumbuka " Kitu kingine ambacho nakuasa, tafadhali usiogope wala usikatae kula chakula au kinywaji chochote utakacho letewa..maana endapo ukikataaa,basi kurudi duniani kwakweli itakuwea vigumu...hivyo chunga sana usicheze vibaya katika huu mchezo wa kufuata hirizi aliyo ivaa mumeo" kwisha kukumbuka hayo,ile hali ya kichefu chefu ilimpotea Mele ambapo alianza kula zile nyama bila kuogopa. Na hayo yote Mele aliyafanya kwa kutaka kumrejesha Kazula duniani.

    Mele alikula zile nyama kwa tabu sana ambazo zilikuwa ni makorodani na ume. Kabla hajamaliza akaletewa kikombe kikubwa kilicho sheheni damu ambayo ilikuwa bado ya moto kwani ilionekana kutoa mfuke. Hakika Mele alishtuka akajisemea "Kweli mtaka cha uvunguni sharti ainame,uko wapi Kazula nafanya yote haya kwa ajili yako" Alijisemea hivyo Mele huku akitafuna Makorodani,ikiwa mbele yake bado kuna kikombe cha damu kikimngojea. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na wakati hayo yalipokuwa yakimkuta Mele kuzimu,upande wa pili nako duniani. Alionekana Marongo akihaha kutafuta namba ya Simu ya Mele ili apate kumpigia baada kuona taklibani siku tatu hamuoni nyumbani kwake kwa maana safari ya Mele kwenda kuzimu,Marongo hakuijuwa. "Mmh huyu nwanamke siku hizi kabadilika saana,yaani haiwezekani siku tatu zote asirudi nyumbani " Alijisemea Marongo mume wake Mele huku akiweka Simu sikioni kwake,na punde si punde simu ya Mele ikaita bila kupokelewa. "Unaona? wanawake wengine bwana bora ukaishi na sokwe. Inakuaje unaondoka bila kuaga harafu hata simu hupokei! Aah " kwa hasira zisizo kuwa na mfano Marongo aliyasema hayo maneno huku akipiga ukuta kwa kutumia mkono wake wa Kulia... lakini mwishowe akaamua kutoenda kazini siku hiyo,moja kwa moja akaelekea kwa rafiki yake Mele ambae alifahamika kwa jina la Somela. Marongo akafika nyumbani kwa Samela kwa lengo la kutaka kujuwa mahali alipo Mele,hivyo kwa kuwa Somela ndio rafiki yake wa karibu Mele..Marongo akaona Somela huwenda akajuwa Mele alipo kwenda. "Habali yako Somela" Marongo akionekana kuwa na hofu alimsalimu Somela ambae nae alionekana kuwa bize kupika chapati,maana Somela kazi yake ilikuwa ni hiyo kuuza chapati kwa wapita njia. "Salama tu shemeji, vipi mbona wanaonekana hauko sawa?.." Somela alijibu hivyo huku akikomea na swali lililomfanya Marongo kushasha pumzi na kisha kusema. "Somela,nimekufuata hapa ili uniambie wapi alipo mke wangu.. siku tatu sasa haonekani nyumbani na hata nikimpigia simu hapokei "

    "Nani Mele?..kiukweli shem mimi sijui chochote kuhusu Mele,nakumbuka mala ya mwisho kuonana nae ilikuwa juma tano..na siku hiyo aliniambia kwamba ulimpiga sana kwa kigezo eti hazai..kwahiyo tangu siku hiyo sijamtia tena machoni"

    "Oooh Mele wangu weee...Ni kweli tangu nijuwe kuwa Mele hazai,ghafla Upendo wangu wa dhati ukapungua,nikawa simpendi hata kidogo...lakini baada kufikilia sana nikaona sio vizuri kwani hata yeye huo ugumba hakuupenda" Alisema Marongo kwa masikitiko makubwa huku machozi yakimtoka.

    "Sawa shem,lakini ngoja nikushauli kitu" Somela alisema akimwambia Marongo.

    "Ndio ndio...nishauli shemeji yangu"

    "Kuna mganga mmoja hivi,yupo vizuri nadhani anaweza kukusaidia tukajua mahali alipo mkewe, hapa mjini huwezi juwa. Kama kachukuliwa msukule,utajuaje sasa?.." Somela alisema hivyo kwa kukazia hilo jambo. "Ok nitashukuru sana...kwahiyo lini sasa nije ili twende?..."

    "Tungeenda hata leo, lakini nina oda ya chapati hamsini za wakandarasi..kwahiyo kesho jioni asubuhi we njoo" CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa..Ahsante " Aliaga Marongo kisha akaondoka zake akimwacha Somela akiendelea kazi yake "mmmh wanaume mnashida sana,yaani unategemea mwanamke ukimpiga kama punda atavumilia tu kila siku?..aawapi hatakama ni mimi siwezi" Alibaki akijisemea hayo Somela huku akigeuza geuza chapati iliyokuwa kwenye flampeni.

    Wakati hayo yakijili duniani,kuzimu sasa kule alipo Mele..alijikuta akiwa katika wakati mgumu baada kumaliza chakula na damu lakini punde akaanza kutapika..Harufu ya damu ilimshinda...akajikuta akitapika sana huku akiwa amegusa tumbo lake kwa mikono miwili..ambapo watu wale wa kawaida na wakutisha waliokuwemo ndani ya kile chumba..ghafla walimgeukia Mele huku wakimtazama kwa hasira kali.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog