Search This Blog

KABURI LA KAZULA - 3

 







    Simulizi : Kaburi La Kazula

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Kiukweli Mele alijikuta akistaajabu baada kumuona mtu mwingine aliefanana na mume wake..asijue kuwa yule aliempelekea maji bafuni hakuwa mume wake bali ni marehem kazula aliechukuwa taswila ya Marongo ambae ndio mume wake Mele. Kwahiyo wakati Mele akistaajabu, Marongo nae alimshangaa sana Mele akishindwa kujua kipi kinacho msibu mkewe . Hivyo basi kwa sauti ya ukali kiasi..bwana Marongo akamuuliza mkewe hivi "Mele unanini leo? Mbona sikuelewi badala unilaki na kisha unihoji kilicho nifanya nirudi nyumbani mapema! Unanishangaa kama vile me mgeni kwako" alisema hivyo bwana Marongo lakini Mele hakujibu kitu,zaidi alizipiga hatua kuelekea bafuni ambako alimpelekea maji Marongo mwingine ambae ndio Kazula aliechukuwa taswila ya Marongo. Lakin baada Mele kufika bafuni,cha kustajabisha aliukuta mlango wa bafu ukowazi. Mele akashtuka mapigo ya moyo wake yalimwenda mbio..ila alipiga moyo konde akaendelea kuzivuta hatua za kunyata na punde si punde aliukalibia mlango wa bafu ambao ulionekana kuwa wazi.. Baada kuukalibia zaidi,Mele alichungulia ndani ambapo hakuweza kumuona yule Marongo aliempelekea maji ya kuoga bafuni. Kiukweli Mele hofu ilizidi kumjaa moyoni wakati huo ile sauti ya mwisho aliyoitoa Marehem Kazula ilikuwa ilikuwa ikijirudia akili mwake..sauti ambayo ilikuwa ikisema "Nakufa na ndoto zangu Mele, ila ilaa. ." Neno "ila" ndilo neno ambalo lilionekana kumtesa mno Mele kwani lilikuwa kwenye fumbo. Mele alisononoke kiukweli. Na wakati Mele akiwa na sononeko moyoni mwake, ghafla kwenye kona ya chumba bafuni alitokea Kazula akiwa katika mavazi yake meupe yaani Sanda. Mele alishtuka akataka kutoka mbio bafuni lakini mlango wa bafuni ukajifunga kitu ambacho kilimpelekea Mele kupasa sauti "Mama nakufaaa" Sauti ambayo ilimshtua Marongo haraka sana akakimbia kuelekea bafuni ambako alisikia mayowe ya mke wake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Marongo baada kufika bafuni, alikuta mlango bado umefungwa lakini punde si punde mlango ule ulijifungua...bwana Marongo akatazama bafuni akaona mwili wa mke wake ukiwa chini. Kiukweli Marongo alishtuka sana kwa woga aliusogelea mwili wa Mele kisha akaugusa Sehem ulipo moyo akakuta mapigo ya moyo yakiwa yamesimama..daah Marongo alitaharuki ghafla kijasho chembamba kilianza kumtoka wakati huo huo akimnyanyua na kisha kumtwaa begani..moja Kwa moja akampeleka chumbani.

    Baada Marongo kumfikisha chumbani mke wake ambae tayali alikuwa amepoteza faham..hara haraka akatoka ndani akazipiga hatua kwenda kwa jirani yake kuomba msaada wa usafiri,na kwakuwa jirani yake huyo alikuwa na gari ndogo ya kutembelea hivyo ikawarahisi sana kwa bwana Marongo kusaidiwa.

    Ndani ya hospital Mele akafikishwa vipimo vilifanyika ikiwa wakati huo huo faham zilikuwa zimemrudia Mele ambapo neno la kwanza kuongea ilikuwa ni"Nisamehe Kazula" alisema hivyo huku akionekana kuwa na wasiwasi lakini Doctor alimtuliza wakati huo akiendelea kumfanyia vipimo vingine ambavyo vinahusu mambo ya uzazi na mengine kadha wa kadha.

    Baada ya masaa mawili kila kitu kilikuwa tayali..na katika vipimo vyote alivyopemwa Mele,jibu moja tu ndio lililoweza kumshtua Marongo baada mke wake kugundulika kuwa hana uwezo wa kuzaa. Kwa hakika Marongo alifadhahika sana moyoni mwake akakumbuka kuwa Mele alishawahi kunasa mimba sasa iweje leo hii aambiwe kuwa Mele tasa?

    "No sikubali " Alisema Marongo kwa hasira kali huku akiwa amejiinamia chini.



    Sikubali ndilo neno aliloweza kusema Marongo baada kupewa report ya doctor ambayo ilionyesha kuwa Mele tasa. ..yaani hatoweza kuzaa. Kiukweli Marongo alionekana kuchanganyikiwa mno ambapo alinyanyuka kutoka mapokezi kisha akatoka nje ya hospital, huku akiwa na kuwaza ni jinsi gani mke wake ataweza kumpatia mtoto. Wakati huo akiwaza hayo..Marongo alishusha pumzi kwa kasi na mwishowe akaano njia pekee ni kuachana na Mele pindi atakapo pona kwani aliona atamshawishi kwenda pasipo stahili mwishowe ajikute akisababisha madhala kama yaliyomkuta kazula..."siwezi kupanda mmea usio zaa " Alisema Marongo.

    kweli baada siku kadhaa Mele kupata ahueni,ghafla mambo yakaanza kubadilika. Mele akaona wazi kabisa kuwa Marongo wa zamani sio wa sasa kwani ilifikia hatua Marongo akawa anamjibu mkewe kivyovyote anavyo jisikia. Hali ambayo ilimfanya Mele kukosa amani, na hivyo akawa anajutia mamuzi yake ya haraka ..mamuzi ambayo yaliyomuondoa duniani kijana Kazula baada kupewa chakula chenye sumu na mke wake ambae ndio Mele alie kimbilia kwa mganga wa kienyeji kutafuta dawa ya kupata mtoto baada kuona miaka ikisonga wao bila kupata mtoto. Hakika Mele alilia sana huku akimtaja Kazula kila mala..wakati huo Mele akilia, alikumbuka maneno fulani aliyowahi kuambiwa na mume wake siku za nyuma baada kutofautia kauli "Kamwe sitoweza kuishi na mwanamke asie zaa " Ni maneno hayo ambayo yalikuwa yakijirudia kichwani kwa Mele huku akibubujikwa na machozi. Kiukweli Mele aliumia sana moyoni mwake akawaza ataishi vipi endapo akiachwa na Marongo. Lakini wakati akiwa katika dimbwi zito la mawazo,mala ghafla alimuona mume wake kwa mbali akirejea kutoka kazini. Hiyo tayali ilikuwa saa kuminambili jioni. Kiukweli macho ya Mele hayakuamini baada kumwona mumewe akirejea nyumbani huku akiwa amelewa, Mele alistaajabu sana kwani haikuwa kawaida yake Marongo kulewa pombe na istoshe zaidi bwana Marongo alikuwa akitoa matusi mabaya kwa mke wake..lakini kwa kuwa Mele alikuwa hana kimbilio . hivyo alikaa kimya licha ya Marongo kumtukana sana huku akikazia saula la kumtimua mele nyumbani kwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Naam baada kufoka kwa muda mrefu hatimae Marongo alitulia kitandani ambapo punde si punde akapitiwa na usingizi..na hivyo Mele akawa amepata unafuu ingawa alifaham fika kuwa yeye sio mali ya Marongo tena baada kugundulika kuwa hazai. "Nitafanya nini mimi? Mele alijiuliza wakati huo tayali giza limeshatanda. Na kabla hajapata ghafla alisikia mtu akitembea sebleni. Mele alishtuka mwili ukaanza kumsisimka na punde si punde mume wake nae alishtuka kutoka usingizini hivyo akadai apelekewe maji bafuni ili aoge...kiukweli licha ya Mele kusikia vishindo vya mtu akitembea sebleni cha ajabu alipiga moyo konde hakutaka hata kumwambia mume wake...na hivyo alishuka kitandani kisha akazipiga hatua kuelekea sebleni ,na wakati anafungua mlango wa chumbani ili aingie sebleni..alishtuka baada kumwona mtu alievaa sanda akiishia kwenye kona ya seble. Mele alipiga kelele lakini alipewa jibu moja tu na mumewe "acha kuleta uchizi wako hapa..peleka maji nikajimwagie tasa wewe nitakubomoa sasa hivi ebo" Alisema hivyo Marongo kwa sauti ya ukali..Mele aliumia sana chozi lilimtoka ila alijikaza kisabuni kisha akampelekea mume wake maji bafuni kama alivyo ambiwa.

    "Kukaribia maji mume wangu yapo tayali" Alisema Mele baada kurejea ndani na kumkalibisha Marongo maji..na Kwa chuki aliyokuwa nayo Marongo kamwe hakuweza kuitikia ile karibu,bali zaidi alichukuwa taulo yake akajifunga kwa kiuno kisha akazipiga hatua kuelekea bafuni kuoga. Dakika zisozidi kumi zilikamilika Marongo akiwa bafuni kuoga,na mala baada kumaliza alitoka ambapo alipokuwa akirejea ndani,ghafla alitokewa na mtu nyuma yake..mtu huyo alikuwa kifua wazi huku macho ya huyo mtu yalionekana kuwa mekundu mfano wa mtu aliekula pilipili vilevile mtu huyo alikuwa na kucha ndefu na nywere ndefu pia..yani kimsingi mtu huyo alionekana kutisha " Kaka kaka kaka" yule mtu alimwita Marongo kwa sauti ya kunong'ona. Marongo nae baada kuisikia hiyo sauti,alishtuka hima akageuka nyuma..cha kushangaza hakumuona huyo mtu aliyekuwa akimwita ...hivyo Marongo akaamua kukazana ili aingie ndani lakini kabla hajaukalibia mlango wa kuingilia ndani...ghafla akageuka nyuma kwa mala ya pili ambapo alitaharuki baada kuona jopo la wafu wakimfuata na katika wafu wale alikuwemo Kazula. .kwa hakika Marongo aliogopa sana hima akatimua mbio kuusogelea mlango punde akaukalibia lakini mlango ulikuwa umefungwa...hivyo Marongo akapasa sauti kwa ukali akimwambia Mele afungue mlango ikiwa wakati huo Mele nae alikuwa kaketi kitandani akiyatafakali maisha ambayo anaishi na mume wake ambae alionekana kubadilika kwa asilimia kubwa tangu agundulike kuwa tasa...hivyo hata sauti ya kuitwa na mumewe kamwe hakuweza kuisikia kwani wale wafu waliifanya sauti ya Marongo isambae mahala popote.



    Hofu na woga ulimjaa Marongo akiwaogopa wale wafu waliokuwa wakizipiga hatua kumfuata..hivyo Marongo aliendelea kupiga kelele za kumwita mkewe Mele ambae nae alikuwa yupo chumbani kaketi kitandani akiyatafakali maisha anayo ishi na mume wake ambae ndio Marongo, kwani tangu bwana huyo agundue kuwa Mele tasa..upendo wa dhati ulipungua hadi kufikia hatua Marongo kumtolea maneno mabaya Mele. Na hivyo Mele akajikuta akikosa amani. Na wakati Mele akiwa bado yupo katika dimbwi la mawazo, upande wa pili nako Marongo aliendelea kupiga kelele akimwita mkewe aje kumfungulia mlango,,lakini sasa kutokana na wale wafu waliokuwa wakimfuata Marongo kuzuia sauti isiweze kupasa mahala popote,hatimae Mele hakuweza kuisikia ile sauti Kwani laiti angelisikia,hima angemfungulia mlango mumewe ili ajiokoe dhidi ya wale wafu waliokuwa wakizipiga hatua kumfuata. "Mele nifungulie mlango mumeo nakufa! Mele nifungulie mlango mumeo nakufa!" Alisema hivyo Marongo huku akipiga mayowe,ila bado mayowe hayo hayakuweza kusaidia. Naam punde si punde wafu tayali wakawa wamemkalibia Marongo ,na katika wale wafu alijitokeza mfu mmoja ambae ni Kazula. Kazula alijitokeza akionekna kachakaa kila sehem ya mwili wake...huku kucha na nywere zake zikiwa ndefu,na mdomoni alikuwa akitokwa damu. Hakika Marongo aliogopa sana baada kumwona Kazula, haraka sana alirudi nyuma..lakini kutokana na kuisogelea nyumba jirani zaidi..hivyo akashindwa kurudi nyuma sana,hali iliyomfanya marehem Kazula kumsogelea zaidi. "Marongo Marongo unanikumbuka? " Kazula akiongea kwa taabu saana,alimhoji hivyo Marongo...lakini kwa sababu ya woga aliokuwa nao Marongo. .kiukweli alishindwa kujibu na zaidi aliishia kuhema kwa kasi huku akimwomba msamaha Kazula. Kazula nae baada kumeona Marongo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akiomba msamaha,aligeuza shingo yake akiwataza wafu wenzake.. na hapo Kazula akawa amekutana na uso wa mfu mmoja alieonekana mzee kuliko wote...mfu huyo alionyesha ishara fulani. Ishara ambayo Kazula alitambua kuwa muda wa kuendelea kutembea duniani umekwisha. Kiukweli kazula baada kugundua hilo aliinamisha uso wake chini ...akionekana kukerwa..ila hakuwa na budi. Zaidi alisema "Bado nipo hai popote mlipo nipo lazima nilipe kisasi " kwisha kusema hayo Kazula pamoja na jopo la wafu wenzake walipotea.

    Hakika Marongo alibaki ameduwaa alicho kiona asiamini kama kweli ama ndoto. "Kazula! kazula! " Alijisema Marongo huku akijifunga taulo yake sawa..kwani kutokana na woga aliokuwa nao..taulo yake ilimdondoka. Hivyo wakati Marongo akijifunga sawa taulo yake kwa kiuno chake,upande wa pili nako. .. ghafla Mele akatoka kwenye dimbwi la mawazo,ambapo alishtuka baada kutomuona mume wake chumbani..hivyo Mele akiinuka kutoka kitandani..alisikika akijusemea "mungu wangu..kakutwa na nini mume wangu tangu muda ule hadi sasa hajarudi" alisema Mele huku akiusogelea mlango,na punde akafungua ambapo alikutana na kipigo kizito kutoka kwa mumewe..kipigo ambacho Marongo alikuwa akikitoa huku akimtukana matusi mabaya "unataka kumwambia kuwa hujanisikia nilipokuita? Mbona unadharau sana malaya mkubwa wewe.. hakika wewe mchawi sana na ndio maana umemuua Kazula pumbafu" Alisema Marongo kwa sauti kali akimfokea Mele huku akiendelea kumpiga. Maskini Mele alilia sana akiomba msamaha..ila Marongo hakujali msamaha wa Mele hivyo aliendelea kumpiga hadi Mele akapoteza faham.

    Hali ile ya Mele kuzimia, ilimshtua bwana Marongo kwani alijuwa kuwa tayali kauwa. Hivyo ili kukwepa jela kwa kuhusishwa na mauaji,Marongo aliamua kumbeba Mele na kisha kwenda kumtupa mbali kabisa na nyumbani anakoishi...kisha akarudi nyumbani kwake huku akijutia ndani ya nafsi yake juu ya unyama alioutenda.. aliogoapa sana kiukweli Marongo .

    Lakini wakati marongo akirejea nyumbani kwake baada kumaliza shughuli yake ya kuutupa mwili wa mkewe Mele , ghafla njiani alikutana na mzee mkongwe mno. .mzee huyo mkononi alikuwa ameshika kifurushi kidogo na kibuyu kilicho zungushiwa shanga. Hivyo mzee huyo akamsimamisha Marongo kwa upole ikiwa wakati huo wameshapishana kama hatua mbili. Marongo akiwa na hofu alisimama. "Habari yako kijana" mzee huyo alimsabahi Marongo. Hivyo Marongo nae akiwa bado na wasiwasi ..akaitikia kisha akamwongeza na heshima yake. "Malakhabaa..kijana samahani nimetoka kijijini leo nikija kumwona mwanangu ambae jina lake anaitwa Adnani, sasa kwa sababu muda mrefu sana sijaja huku! Kiukweli mazingara yamebadilika yamenipotea kichwani.. sana kwahiyo nahitaji msaada wako kwa usiku huu ili kesho asubuhi nimtafute" alisema Mzee huyo alionekana kula chumvi nyingi. "Daah mzee umenisimamisha nikijuwa unajambo la maana kumbe ushenzi tu.. achana na mimi hapa mjini bwana na nyinyi ndio wachawi" Marongo alimjibu hivyo kwa hasira mzee huyo.. kisha akaondoka zake. Cha ajabu baada Marongo kuondoka zake,huyo mzee aliyeomba msaada kwa Marongo...alicheka saana kisha akasema "naam mimi ndio Baluguza" kwisha kusema hayo mzee huyo ambae anaitwa Baluguza alichuchumaa chini kisha akapotea.. akaibukia kule alikotupwa Mele akiwa hana faham...napia ikumbukwe kuwa Baluguza ndio yule mganga aliempa Mele sumu ya kumuua kazula baada Mele kwenda kwa mganga huyo kutafuta dawa ya kumpatia mtoto baada kuishi na Kazula kwa muda mrefu bila kupata mtoto.

    Hivyo wakati Baluguza akiibukia kule alikotupwa Mele...upande wa pili nako Marongo alifika nyumbani kwake..moja kwa moja akaingia mpaka chumbani kwake...na alipowasha taa ili alale na kesho afanye mpango wa kutoroka...mala ghafla kitandani aliona mwili ukiwa umelazwa huku umevishwa sanda..na pembeni ya mwili huo palikuwa na jeneza ambalo lilionekana kuchakazwa na damu.

    Ikiwa kwingineko napo..mzee Baluguza alifanya uganga wake akawa amemrejeshea faham Mele...ambapo Baluguza aliweza kumtuliza Mele kwa kumtowa woga...kweli Mele akatulia ingawa sio kiviile kama inavyotakiwa...na mwishowe Mzee Baluguza akamwambia Mele hivi "kumbuka ulikosea masherti na ndio maana ukamuua mumeo " Mele hakujibu kitu zaidi aliishia Kulia usiku ule. "Huna haja ya kulia. .amini mumeo bado yupo ila kuna kitu inabidi ukifanye na ndipo utafanikisha kumrejesha mumeo duniani " Wakati Mele akilia kwa uchungu mzee Baluguza aliongeza kwa kusema hivyo...Mele alishtuka na papo hapo faham ikamjia vizuri ..kwanza akahoji nipo wapi hapa? Mzee Baluguza alicheka kisha akamshika kichwa Mele kitendo ambacho kilirudisha kumbukumbu nyuma...na hivyo Mele akakumbuka kuwa kabla ya kufika hapo alipigwa vibaya na mume wake.

    Baada kukumbuka hayo,Mele alishusha pumzi kisha akahoji "Ni kweli unaweza kumrejesha Kazula wangu duniani? Alihoji Mele kwa masikitiko "ndio ila mpaka ufanye jambo fulani" mzee Baluguza alijibu.

    "Jambo gani hilo! Kabla mzee Baluguza hajamwambia Mele jambo hilo analotakiwa kufanya..Alicheka kwanza kisha akasema..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee Baluguza alicheka kwanza,kisha akasema.

    "katika mwili wa marehem mume,wako kuna hurizi kaivaa...hirizi hiyo endapo ukiipata na kisha kuniletea..amini unaweza kumrudisha duniani Kazula " Alisema mzee Baluguza akimwambia Mele. "Hirizi? kwa hiyo nitaipataje hurizi hiyo" Mele akionekana kuwa na mshangao Alihoji hivyo..

    "Hahahaaa Mele kuipata hirizi hiyo...lazima umfuate kazula kuzimu je,uko tayali? Kiukweli lilikuwa swali gumu sana kwa Mele kuweza kujibu kwa haraka. Hivyo alishusha pumzi huku akijishauli mwenyewe akilini mwake, kitendo ambacho kiliweza kuchukuwa muda kutoa jibu. "Binti inaama huna haja ya kumrejesha mumeo duniani? Maana naona hukubaliani na masharti hayo ya kuelekea kuzimu " aliongeza kwa kusema hivyo mzee Baluguza huku akimtazama Mele ambae nae aliinamisha uso wake chini kwa kuhisi haibu. "Hapana babu,kumbuka mimi ndio niliekufuata ili unipatie dawa ya kuweza kutupa mtoto..lakini kama unavyodai kwamba kukosea masharti kwangu ndio kulisababisha kifo cha mume wangu..kwahiyo naomba unipe muda nikajifikilie" Mele alijibu kwa upole "Hahahaaaa binti unampenda mumeo? " Baluguza alimuuliza Mele ."ndio bado nampenda na bado najutia maamuzi yangu" "Ok kama bado unampenda..jambo ni moja tu lakifanya...hahahaha mfuate kuzimu ukachukue hirizi aliyoivaa kisha niletee mimi mganga kati ya waganga kuwahi tokea balani Africa na Dunia kiujumla" Mzee Baluguza aliongea hivyo kwa sauti ya chini chini mfano wa mtu anaemnong'oneza mwenzie.

    Kiukweli Mele aliendelea kujishauli kuelekea kuzimu..amabapo alienda mbali zaidi kwa kukumbuka maisha anayo ishi na Marongo...akakumbuka na maisha aliyo kuwa akiishi na Kazula enzi za uhai wake..akaona heri ya Kazula licha ya kuishi kwa taklibani miaka miwili bila kupata mtoto ila Bado kwa kiasi fulani amani ilikuwepo ambapo tafuti na Marongo ambae muda huo alikuwa amempiga mpaka kuzimia. "Babu nipo tayali " Mele akajitaidi kujibu ingawa usoni mwake bado alionekana kuwa na hofu. Hivyo mzee Baluguza baada kusikia jibu hilo la Mele,kwa hakika alicheka sana. Na mwishowe akamwambia hivi "sikiliza binti...yaani wewe bonge la shujaa unafaa sana maana unaroho ya chuma cha pua " alisema mzee Baluguza huku akiachia tabasam. Lakini licha ya mzee Baluguza kutabasam ila Mele hakuweza kutasam kwani akili yake ilikuwa mbali mno akifikiia safari hiyo ya kuelekea kuzimu kwa lengo la kufuata hirizi je, nitafanikiwa? Ndilo swali liloweza kumuumiza akili Mele.

    Baada ya Mele na mzee Baluguza kukubalia hayo,hatimae mzee Baluguza alimwamlisha Mele asimame. Mele akasimama. Mzee Baluguza akamshika mkono Mele kisha akamwambia Mele afumbe macho. Punde si punde mzee Baluguza akarudia kumwambia Mele kuwa afumbue macho yake ambapo Mele alifumbuka akajikuta kafika nyumbani kwake."haya upo nyumbani kwako binti..na kabla hujaingia ndani,napenda nikwambie kuwa safari ya kuelekea kuzimu itakuwa siku ya ijumaa..kwa sababu ijumaa kutakuwa na sherehe huko kuzimu hivyo siku ya alhamisi usiku nitakuja ili nikufunde mambo kadhaa ya kutakiwa kufanya kabla hujaenda na baada kufika huko kuzimu! Sawa binti "

    "Sawa nimekuelewa" Mele aliitikia kwa huku akiwa bado hajiamini.

    "Ok unaweza kuingia ndani"

    "Ndani? Hapana babu siwezi mala hii ataniua kabisa huyu mwanaume" kiukweli licha ya kurudishwa nyumbani baada kutupwa na Marongo ambae alimpiga hadi kuzimia,Mele bado aliogopa kuingia ndani akimhofia Marongo kumpiga kwa mala nyingine. Hivyo mzee Baluguza baada kuona Mele anaogopa kuingia ndani..ghafla alipotea pale nje akaibukia chumbani ambapo alimkuta Marongo kalala usingizi mzito. Hivyo kwa kutumia mkono wake,mzee Baluguza alimgusa Marongo kichwani...wakati huohuo Marongo akaota ndoto nzuuri akifurahia maisha na Mele ...ndoto ambayo ilikomea baada kutoka kwenye starehe ghafla Mele akawa amegongwa na gari huku akiwa na ujauzito. Hivyo hiyo ndoto ilimkurupusha Marongo kutoka usingizini huku akimwita Mele "Meleeeeee "

    Marongo alishtuka akatoka usingizini ..akatazama kitandani hakumwona Mele..muda huo huo akakumbuka kuwa alimpiga na kisha kumtupa mbali kabisa na nyumbani kwake akihofia kuwa amumuua. "Mele..Mele. ..Mele " Marongo alimtaja Mele moyoni akijutia kwa kitendo kile alicho kifanya...na punde machozi yalimtoka huku huku akishuka kitandani ili aelekee kule alipo mtupa ili ahakikushe kama kweli Mele kafa au alizimia tu.

    "Mungu wangu nisaidie ili nimkute akiwa hai " alijisemea Marongo huku akifunga mifungo vya shati ili aelekee kule alipomtupa Mele.

    Na wakati Marongo akipanga suala hilo la kumfuata Mele, upande wa pili nako nje...mzee Baluguza alimwambia Mele "tayali nimesha mvuruga,na muda huu anataka kukufuata kule alikokutupa,,kwahiyo basi wewe kaa hapa ili akifungua mlango tu akuone. ..kamwe hawezi kukupiga tena" kwisha kusema hayo,mzee Baluguza alitoweka..ikabaki sauti nzito ikimsisitiza Mele kuwa siku ya ijumaa ni safari ya kuelekea kuzimu... Na wakati sauti hiyo ilipokuwa ikimuhimiza Mele kuhusu suala la kwenda kuzimu, ghafla Marongo akafungua mlango ambapo alishtuka kumuona Mele,hima Marongo akamkumbatia na kisha kumwambia "nisamehe mke wangu.. zile zilikuwa hasira tu" CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Usijali nimesha kusamehe " Mele alimjibu Marongo, lakini akili mwake alikuwa akijisemea" Marongo siri ya furaha yako hii ya madakika,naijuwa ...hivyo msimamo wangu utabaki kuwa pale pale...nipo tayali kuelekea kuzimu kuifuata furaha yangu niliyo ipoteza pasipo kujuwa"



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog