Search This Blog

KABURI LA KAZULA - 2

 







    Simulizi : Kaburi La Kazula

    Sehemu Ya Pili (2)



    Mele alionekana kushtuka baada kuona dawa aliyokuwa ameiweka juu ya meza,imepotea kimaajabu.Hivyo akiwa na hofu kubwa,Mele alisema.Marongo unajuwa ya kuwa tangu tumzike kazula,nyumba hii imekuwa chungu? "Ndio mke wangu nafaham hilo,ila usijali tatizo kama hili kwangu la kawaida sana" Akajibu Marongo huku akijionyesha kujiamini,ambapo baada kujibu hivyo alijinyanyua kutoka kitandani,kisha akazama uvunguni.akatoka na mkoba uliochakaa,mkoba huo marongo aliufungua akachomoa kitambaa kilichokuwa kimefungwa fundo.akafungua lile fundo.Baada kulifungua lile fundo,Marongo akasema.Mimi ndio marongo,naomba mizimu ya ukoo wangu mlisimamie suala hili.Alisema Marongo huku akijipakaa unga flani alioukuta kwenye lile fundo lililokuwa limefungwa kwenye kitambaa.. ambapo kwisha kusema hayo,Marongo alirudisha mkoba wake uvunguni..na hapo ndipo Mele aliposema.Marongo unajuwa mimi sijaelewa ulichokifanya,naomba uniambie unamaana gani? Hujaelewa nini sasa Mke wangu? Naomba ukae kimya kwanza,ndio maana nimekwambia mambo haya yakawida kwangu! Alijibu Marongo kisha akachukuwa mkuki na panga,akaelekea kwenye zizi la wanyama wake,ambapo ndani ya zizi,alimchagua fahali mmoja akawa ameondoka nae moja kwa moja mpaka kwenye mti mkubwa kuliko yote kijijini kwao.Mti ambao ulikuwa maalumu kwa kufanyia matambiko.Marongo akiwa na fahali wake yaani ng'ombe dume.aliusogeleCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    a ule mti kisha akamfunga kamba yule ng'ombe miguu yote minne kisha akamwangusha chini ya ule mti mkubwa.Upepo mkali ulivuma,giza na mwanga hafifu ukatanda kwenye ule mti,na punde si punde vicheko vya kila lika vilisikika kutoka kwenye ule mti.Marongo hakuteteleka,kwa ustadi wa hali ya juu aliukamata vyema upanga wake akiwa tayali kabisa kumchinja Ng'ombe wake ikiwa kama kutoa kutoa sadaka kwa mizimu yao.

    Lakini kabla Marongo hajamjicha fahali wake,ghafla kwenye ule mti alitokea mtu mrefu.Mtu wa ajabu akiwa amevaa mavazi yake ya sanda..Mtu huyo alimsogelea Marongo kisha akasema.Tunatambua kibarua kizito kilichopo mbele yako,nasi tupo tayali kukusaidia kwa sababu umejali kitu tunacho hitaji,pia pongezi kwako kwa kuwahi kufika mahali hapa,kwa maana jopo la mizimu likiongozwa na kazula lipo katika haraki za kulipa kisasi juu ya kile ulicho kifanya wewe na mkewe..Marongo alistaajabu kusikia maneno yale ya ule mzimu uliomtokea chini ya mti..Ambapo punde si punde ule mzimu ulipotea,na hapo ndipo marongo alipomchinja ng'ombe wake huku akijisia huru kabisa ndani ya moyo wake akiamini kuwa huo ndio utakuwa mwisho wa mauzauza ya kitokewa na Marehem Kazula.

    Hivyo wakati Marongo alipokuwa akifanya tambiko,upande mwingine nako.alionekana kazula juu ya kaburi.Kazula alikuwa ameketi huku akitazama kila pande ya dunia..kitu ambacho kilipelekea wapita njia kushtuka kumwona akiwa kwenye kaburi..ambapo habari hiyo iliweza kusambaa kijini huku baadhi ya wanakijiji wakionekana kutokukubaliana na habari ile ya kuonekana kazula kwenye kaburi..wakati hajawahi kusikia msiba wa kazula zaidi wao walikuwa wakijuwa mama kazula ndio aliefariki..Wingi wa wanakijiji walijisogeza nyumbani kwa Marongo kwenda kumshuhudia Kazula ambae alizikwa kimyakimya baada kuuliwa na Mele...Hivyo Mele baada kuona wingi ule wa wanakijiji wakija nyumbani kwake,alishtuka

    .Wakati huo tayali jopo la wanakijiji limeshafika nyumbani kwake,,ambapo moja kwa moja walizunguka nyuma ya nyumba mahali alipozikwa kazula..Kwa hakika walistaajabu kumwona kazula.wakati huo Kazula alisimama,akatabasam na punde si punde akapotea pale kaburini..

    "Jamini Mele na mume wake wako wapi" ilisikika sauti ya mmoja ya wanakijiji akisema hivyo,baada kuona kitendo kile cha kushamgaza katika macho ya watu.Hivyo alitaka kujuwa ukweli kuhusu kazula na ukweli kuhusu kaburi la siri lilopo nyuma ya nyumba yao.

    Lakini kabla mwanakijiji yule hajajibiwa,kwa mbali alionekana Marongo akiwa na upanga pamoja na mkuki huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu kila kona kona..Marongo alishtuka na wingi wa watu uliokusanyika nyumbani kwake..maswali kibao alijiuliza kichwani mwake,ila yote kwa yote alipiga moyo konde kisha akazipiga hatua za pole pole akizidi kujongea nyumbani kwake..Na punde si punde wanakijiji waliokusanyika pale kwake,waligeuza nyuso zao kumtazama Marongo..ambapo ilisikika tena sauti kutoka kwa mwanakijiji,sauti hiyo ikisema "lazima huyo leo atuambie ukweli kuhusu hili kaburi,pia yeye na mke wake watueleze mahali walipo muweka Kazula.." Alisema hivyo mwanakijiji mmoja ambae jina lake aliitwa Mzee mkavu. .ambapo mzee huyo aliongea kwa ukali,kauli ambayo iliungwa mkono na wanakijiji wenzake haswa wale ambao waliomjuwa kiundani zaidi Kazula ambae alisifika kwa upole aliokuwa nao

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wanakijiji walionekana kuwa na shauku ya kutaka kujuwa ukweli kuhusu kaburi lilopo nyuma ya nyumba ya bwana Marongo,,lakini cha kushangaza Marongo hakutaka kusema ukweli kama kaburi lile lililopo nyuma ya nyumba yake,,ni kaburi la Kazula..kijana waliomzika kimya kimya pasipo kutambua mtu yoyote. Hivyo baada wanakijiji kushindwa kupata ukweli,hakika walifadhaika saana mioyoni mwao..kwani ilifikia hatua wakataka kumpiga Marongo,,ila Marongo alisimama kidete huku akidiliki kumtishia mwana kijiji yoyote atakae thubutu kumpiga. Na kwakua marehem baba Marongo alisifika kwa uganga wa kienyeji enzi za uhai wake,,hivyo wanakijiji walimwogopa sana Marongo..wakaamua kumuacha huku wakiamini kuwa hakuna siri chini ya jua..kwa kuwa Mele alimuuwa kijana kazula,,basi ipo siku itajulikana tu na haibu kubwa itawakumba wanandoa hao Bwana marongo na Mele.

    Naam! Siku zilikwenda mapenzi ya Marongo na Mele yakizidi kunoga..kwa hakika Mele alidiliki kusema kwa kinywa chake..Afadhali nilivyo muondoa kazula nyoka kibisa..kumbe wewe ndio ulikuwa sahihi katika maisha yangu! Alisema Mele wakati huo akiwa ameketi chini ya mti uliokuwa kando kidogo na nyumba yake huku akimwambia maneno hayo mume wake ambae ni Matongo..Marongo alifurahi kusikia maneno yale matamu yakitoka mdomoni kwa mke wake..kisha baada kuachia tabasam..Marongo akasema. Unamaana gani mke wangu? Alijibu Marongo huku akiachia kicheko chenye furaha ndani yake. Mele alishusha pumzi kisha akasema. Kiukweli miaka mingi sana niliishi na kazula,lakini licha ya kuingiliana kimwili mala kwa mala kama mke wake..ila hata siku moja sikuwahi kujihisi mjamzoto..hivyo nadhani kwako wewe unaweza kunipatia mtoto..kwa maana dalili zote naziona. Aliongeza kwa kusema hivyo Mele..kiukweli Marongo alifurahi saana kusikia maneno yale,,sifa nyingi alijisifia akasubutu kumponda Kazula ambae tayali ni marehem..utani kadha wa kadhaa uliendelea kwa wapenzi hao..Na mwishowe habari hiyo njema,Mele aliona bora akamueleze mama yake..lakini wakati akijiandaa kuondoka,,hatimae mama yake alifika..hivyo safari ya Mele ikawa imeota mbawa. Ambapo waliamua kukaa sehem tulivu chini ya mti,,kisha mazungumzo yakafatia kati ya mama na mtoto. Na katika mazungumzo hayo,habari ya Mele kunasa mimba ilimfurahisha sana mama Mele,,akacheka sana huku akipiga vigelegele asiamini kama kweli mwanae kapata mimba.

    "Mwanangu,,naweza kusema kufa kwa kazula ni neema kwako..hakika uwanaume kazi,,na sio kuvaa suruali tu khaa.." Alisema mama Mele huku furaha kubwa akiwa nayo ndani ya moyo wake.. "kweli mama mimi nakuunga mkono" Alisema Mele.



    Mama Mele hiyo taarifa ya mwanae kunasa ujauzito ilimfurahisha sana..hadi akatangazia baadhi ya marafiki zake..hivyo nao wakawa wamefaham kuwa Mele mtoto wa mama Mele amimba..Lakini kadri siku zilivyozidi kwenda,,cha kushangaza mimba ya Mele haikuweza kukuwa wala kupungua..hali iliyompelekea kupata wasiwasi..hata Marongo nae alishtuka..na hivyo siku mojs usiku..Marongo aliamua kumuliza Mke wake kuhusu miezi ya ujauzito..lakini kabla Mele hajajibu, ghafla kule kwenye kaburi la Kazula ilisikika sauti ya mtoto mchanga akilia,,Marongo alishtuka..huku akiisikilizia ile sauti kwa makini,,sauti hiyo ambayo alikuwa akiisikia yeye peke yake..ila mwishowe ile sauti aliisikia na Mele..ambapo punde si punde ikakata. Kisha ikasikika sauti ya Kazula ikisema. "Mele bado nipo hai..na kwa hakika maisha yako yoote na mume wako yapo kiganjani mwangu" Ilisikika ikisema hivyo sauti ya marehem Kazula..sauti ambayo iliambatana na mwangwi mkali.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mele aliogopa sana kusikia maneno yale ya Kazula,,na punde si punde punde mimba yake ambayo ilikuwa changa ilipotea kimiujiza..Mele akionekana kustaajabu aligusa tumbo lake baada kujihisi tofauti.."mungu wangu,nitaificha wapi sura yangu mimi mbele ya mama yangu? " Alijisemea Mele ndani ya nafsi yake,,wakati huo Marongo nae akiendelea kumwaga dawa zake za asiri ndani ya chumba chake,,na mala baada kumaliza alimtoa wasiwasi mke wake huku akiupeleka mkono wake kwenye tumbo,,lakini Mele aliushika ule mkono wa Marongo,,hali iliyomfanya Marongo kushangaa,,na punde si punde akasema. Kwa nini unanizuia nisimguse mwanangu ndani ya tumbo lako? Ah embu niache nimguse japo nisikie akihema" Alisema Marongo huku akiongeza na utani kiasi. Ila bado Mele alionekana kukataa,,kwani wakati ule tayali tumbo lake lilikuwa lipo kawaida tofauti na awali ambapo ilikuwa mimba ya ndogo ya kawaida.



    "Nitaificha wapi sura yangu,mbele ya mama yangu? Au nitamueleza nini mume wangu ili anielewe maana nimeshamwambia kuwa tayali nimenasa mimba! Daah Eeh mungu wangu nisaidie" Mele aliwaza hivyo baada kujiona yupo katika wakati mgumu baada mimba yake kutoweka kimaajabu. Na wakati Mele akiwaza hivyo,Marongo nae alionekana akizidi kuwa king'ang'anizi kwa mke wake akitaka kumgusa tumboni ili asikie japo mtoto akihema. "Marongo mume wangu jaribu kuwa na staha basi, mimi mkeo na sio hawala yako. Hivyo nakuomba uniheshimu sawaee.. kwanza kwa vitisho vinavyo endelea humu ndani. Tafadhali nakuomba tuhame haraka sana" Alisema Mele kwa msisitizo mkali huku akiurudisha nyuma mkono wa mume wake ambao tayali ulikuwa ukiukalibia tumbo lake. Kiukweli Mele alikereka sana,na mwishowe Marongo alilitambua hilo. Hivyo akatulia.

    Baada Marongo kutulia kiukweli aliwaza akajiuliza ni kitu gani kinachomfanya Mele akatae kuguswa tumbo lake? Swali ambalo lilimfanya achukie moyoni mwake ambapo aliamua kunyanyuka kutoka kitandani akazipiga hatua kuelekea sebleni kulala. Mele baada kuona hali ile akajuwa kabisa amemchukiza mume wake labda huwenda alikuwa anahitaji tendao. Mele alijilaum sana kiukweli akatamani kwenda kumuomba msamaha..wazo ambalo aliliona lifaa saana hivyo alinyanyuka haraka sana kutoka kitandani akitaka kumfuata mume wake ili amuombe msamaha. Lakini kabla hajatoka chumbani,ghafla akamuona Marongo kalejea tena chumbani. Kwa sauti ya upole Mele akasema "samahani mume wangu kama kweli nimekuudhi. Hakika halikuwa tegemeo langu" alisema Mele Kwa sauti ya upole. Nae Marongo baada kuambiwa hivyo,alicheka kisha akamjibu "usijali mke wangu hayo mambo ya kawaida tu" Marongo alijibu hivyo huku akijalaza kitandani ambapo Mele nae ili kuyasawazisha makosa yake,aliamua kumpapasa mumewe na punde si punde tendo la ndoa lilifuata. Tendo hilo lilidumu kwa muda wa dakika tano. Na wakati wawili hao wakiendelea kufanya mapenzi, ghafla chumbani aliingia mtu mwingine aliefanana na Marongo. Mele alistaajabu kuona hali ile akamsukuma M arongo yule aliekua juu ya kifua chake. Akamtazama Marongo yule aliekuwa amesimama kando yake. "Mele nini sasa unafanya " Marongo aliekuwa kando ya kitanda alimuhoji Mele wakati huo huo Marongo yule aliekaa kitandani nae akimuuluza Mele "kwani huyo nani kwako? Daah Mele alichanganyikiwa kiukweli akashindwa amjibu yupi amuache yupi maana wakina Marongo hao wote walikuwa wamefanana kila kitu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini wakati Mele ikiwa amepigwa na butwaa akishindwa amjibu yupi amuache yupi,ghafla yule Marongo aliefanya nae mapenzi alipotea kimaajabu. Mele alishtuka hali iliyompelekea kupotezea faham hapo hapo mpaka asubuhi.

    "Maisha gani haya ambayo tunaishi mume wangu? Tazama mimba yangu imetoweka kimaajabu! Ee kwanini lakini" Mele alimwambia mume wake mala tu alipozinduka. Ambapo katika sentensi zake akaamua kuingizia na suala la mimba kutoweka kimaajabu. Marongo alishtuka sana akalaani mizimu ya ukoo wao kuwa haimsaidii licha ya kuitolea sadaka Kwa kuichinjia fahali wake. Na mwishowe kabisa Marongo akamwambia mke wake. "Kwahiyo mke wangu ulipenda tuhamie wapi?

    Mele kwa haraka haraka akajibu "Ili kukwepa haya mauzauza,nakushauli mume wangu tuhamie mjini tu kiukweli hapo tutakuwa tumemaliza kila kitu"

    "Aaaah Mele kwa kupenda mji? Hahahaaaaa sawa bwana mke wangu usijal kwanza hapa kijijini wameshaanza kutuhisi vibaya juu ya kifo cha kazula,kwahiyo wazo lako ni nzuri sana..pia hilo suala la mimba kupotea kimaajabu. Huo woga wako tu amini mwanetu bado yupo sawa mke wangu"

    "Sawa ahsante kwa Kwa maneno yako mazuri mume wangu,ndio maana nakupenda sana"

    "Mmh kuliko kazula?

    "Aaah Jamani mume wangu mbona hivyo sasa nitampendaje mtu ambae ameshakufa? Wewe ndio kila kitu kwangu sio huyo marehem Nyoka kibisa " Marongo na mke wake walicheka sana baada kuongea maongezi hayo..



    Marongo alifanya mikakati ya kuhama katika imaya ile ya Kazula. Ambapo alifanikiwa kupata nyumba ya kupanga mjini kama mke wake alivyopendekeza. Hakika amani ilitawala baada wawili hao kuanziasha maisha mapya mjini. Hivyo Marongo akaona hana mpango wa kuishi kijijini ambapo aliamua kuuza mifugo yake akapata fedha nyingi ambazo aliweza kufungua biashara mjini alikohamia.

    Maisha yake na mke yaliendelea kuwa raha mstarehe. Wakasahau kuwa kuna dhambi kumbwa waliyoitenda yote ikitokana na amani tele kutawala juu yao. Lakini siku moja asubuhi wakati Mele akiwa katika manunuzi yake sokoni. Kwa mbaali alimuona mtu aliefanana na Kazula, Mele alishtuka akawa haamini kama kweli yule mtu aliemuona ni Kazula au laa.. hivyo akionekana kuwa na Hofu kubwa moyoni alizipiga hatua kuelekea sehem ile aliyomuona yule mtu aliefanana na marehem Kazula, ,lakini kabla hajamkalibia ghafla yule mtu alitoweka kimaajabu. Kiukweli Mele alistaajabu. Haraka sana akarejea nyumbani kwake huku akimsubilia mume wake kwa hamu kubwa ili amwambie kile alichokishuhudia sokoni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na wakati Mele akiwaza hayo,upande wa pili nako Marongo akiwa katika biashara yake ya kuuza duka. Ghafla dukani kwake alitokea mtoto mdogo wa makamo ,mtoto huyo alimpa Marongo fedha shilling miambili kisha mtoto huyo akahitaji sigara. Marongo Kwa masihara akamuuliza yule mtoto. "Nani kakutuma sigara? Mtoto yule aliachia tabasam kisha akanyoosha kidole akimwonyesha Marongo mtu aliemtuma sigara. "Mungu wangu yule si kazula? Alisema Marongo huku akionekana kushtuka baada kumuona marehem Kazula akiwa amekaa kando kidogo na eneo lilipo duka lake. Na wakati Marongo akiwa amepigwa na butwaa..ghafla yule mtoto alitoweka kimaajabu pia muda huo huo Kazula nae alipotea. Hali iliyomfanya Marongo kupagawa zaidi,ambapo siku hiyo aliamuwa kufunga duka lake mapema akarudi nyumbani kwake . Na wakati Marongo akiwa njiani akirejea nyumbani kwake,upande wa pili alitokea marehem kazula punde si punde akajibadilisha kwa kuchukuwa taswira ya Marongo kisha akazivuta hatua kuelekea nyumbani kwa Marongo. Mele baada kumuona alimpokea akijuwa kuwa kweli yule ni mume wake...hivyo kabla ya yote alimpelekea maji ya kuoga bafuni huku akimsubili kwa hamu ili amueleze kile alichokiaona sokoni . Ila wakati Marongo huyo alipokuwa bafuni kuoga,kwingineko alionekana Marongo mwingine ambae ndio mume wake Mele. Hakika Marongo alionekana kuchoka saana kwani alipakimbia kijijini kwa nia ya kuyakwepa mauza uza. Lakini cha kustaajabu akajikuta yule waliomkimbia kawafuata hadi mjini. Amakweli damu ya Mtu nzito. Mele akiwa ndani aligongewa hodi na mumewe,hivyo akajuwa dhahili mume wake atakuwa ametoka bafuni..Lakini baada kufungua mlango alishtuka kumuona mume wake ndio amerejea kutoka kazini...





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog