Search This Blog

MALAIKA WA KIFO - 3

 





    Simulizi : Malaika Wa Kifo

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Mara baada ya kupokea simu ile, usingizi wote ukapaa, akainuka kutoka kitandani na kuelekea sebuleni kwani ingawa alimuita mama yake aliona kama anachelewa kuja. Uso wake ulikuwa na furaha kupita kawaida, simu ile aliyokuwa ameipokea aliiona kubadilisha maisha yake yote.

    “Nimechaguliwa,” alimwambia mama yake ambaye hakuonekana kuelewa kitu.

    “Unasemaje?” aliuliza mama yake.

    Hata kabla hajajibu swali hilo, Filbert akaanza kukimbia kuelekea barabarani. Alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa, simu ambayo aliipokea kutoka kwa watu wa Kampuni ya Panorama ilimchanganya sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bado alikuwa akiendelea kukimbia kuelekea barabarani. Hakuweza kusalimiana na watu waliokuwa wakimfahamu ambao walimuona akikimbia, alionekana kuwa mwingi wa haraka kupita kawaida.

    Mara baada ya kufika barabarani, daladala zikawa na ugumu kupatikana. Kila wakati alikuwa akiuma meno yake kwa hasira kwani alijiona kama anachelewa kufika huko alipokuwa ameitwa.

    Alisimama kituoni kwa zaidi ya dakika kumi, daadala moja iliyokuwa imejaza sana ikafika, hakutaka kuchelewa, japokuwa hata konda naye alikuwa akining’inia, naye akajitosa, alichokuwa akikihitaji wakati huo ni kuwahi tu.

    Kichwa chake kikaanza kufikiria mambo mengi, mama yake alikuwa mgonjwa huku yeye mwenyewe akiwa masikini wa kutupwa, simu ile aliyokuwa amepigiwa, ikaonekana kuyabadilisha maisha yake kabisa.

    Akajiona akipata fedha, akimiliki magari na mama yake kwenda kutibiwa nchini India. Zaidi ya hapo, akajiona akianza kupata usupastaa na kuwa muigiaji mkubwa duniani.

    “Hatimae nimekuwa supastaa,” alisema Filbert huku akionekana kutokuamini kilichokuwa kikiendelea.

    “Mama atakwenda India kutibiwa, nitamiliki magari, jina langu litatumika katika biashara, na nitakuwa na fedha nyingi mno, eeh! Mungu, naomba basi hizi ndoto za mchana zitimie,” alisema Filbert, daladala lilikuwa safarini ambapo baada ya dakika ishirini, likafika Afrika-Sana, akateremka na kuanza kupiga hatua kuelekea katika Hoteli ya Atriums ambayo haikuwa mbali na hapo aliposhukia.

    ***

    Sheila aliumizwa na kile alichokisikia kutoka kwa Ignas, hakukuwa na mtu aliyekuwa akimchukia kwa wakati huo kama alivyokuwa Edmund. Mawazo yake yakarudi nyuma na kukumbuka kile alichofanyiwa na mwanaume yule, kiliuumiza moyo wake na kamwe asingeweza kuyasahau maumivu yale.

    Akazidi kububujikwa na machozi kwani ile filamu ya Golden Angel aliyoizungumzia Ignas ilimkumbusha kila kitu kilichotokea miaka ya nyuma alipokuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Edmund.

    Ignas hakulielewa hilo, kubadilika kwa ghafla kwa Sheila kulimshtua, hakujua ni kitu gani kilimsibu mpaka kuanza kulia ghafla, hakujua kama msichana huyo aliwahi kuumizwa na Edmund, mtu aliyekuwa ameigiza filamu hiyo na Waafrika Kusini.

    “Kuna nini Sheila?” aliuliza Ignas huku akijitahidi kumbembeleza Sheila.

    Msichana huyo hakunyamaza, bado moyo wake ulikuwa ukimuuma mno, kumbukumbu za maisha ya nyuma na Edmund zilimtesa na kumuumiza mno, moyo wake ulijawa na chuki kubwa dhidi ya mwanaume huyo.

    “Hakuna kitu,” alijibu Sheila.

    “Sasa kwa nini unalia?”

    “Kuna mengi nimekumbuka.”

    “Yapi hayo?”

    “Naomba uniache Ignas, sipo sawa.”

    “Sawa. Hakuna tatizo. Ila hebu niambie Sheila ili siku nyingine nisirudie kosa langu,” alisema Ignas.

    Sheila hakuwa radhi kuzungumza kile kilichokuwa kimemsibu, moyo wake tayari alijisikia kuwa na mapenzi kwa mvulana huyo japokuwa hakutaka kumwambia hilo, kitendo cha kumwambia kwamba katika kipindi cha nyuma aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Edmund, hilo lilikuwa jambo gumu.

    Ignas akapata kazi zaidi ya kuendelea kumbembeleza. Moyo wake bado ulikuwa na uhitaji wa kuwa na msichana huyo. Alimpenda mno na hakuwa tayari kuona akimkosa, alikuwa tayari kufanya lolote ili mradi msichana huyo awe naye.

    “Upo tayari kwenda kutazama muvi na mimi?” aliuliza Ignas, hakutaka kushindwa.

    “Nipo tayari ila si kuangalia muvi za Kibongo,” alijibu Sheila.

    “Sawa. Hakuna tatizo. Unataka nini?”

    “Labda kuangalia muvi za Kizungu,” alijibu Sheila.

    Hilo halikuwa tatizo kwake, kitu pekee alichokuwa akikitaka kwa wakati huo ni Sheila kuelekea nyumbani kwake tu, alihitaji kufika ndani ya nyumba hiyo kwani aliamini kwamba kwake ingekuwa rahisi sana kumfanya msichana huyo kuvutika naye zaidi. Baada ya dakika kadhaa, wakaanza safari kuelekea huko.

    Ndani ya gari, Ignas alishikilia usukani lakini akili yake muda wote ilikuwa kwa msichaana huyo, kila alipokuwa akimwangalia, alionekana kuwa msichana mrembo ambaye alistahili kuwa naye.

    “U mzuri sana Sheila,” alisema Ignas.

    “Umekuwa ukiniambia hilo kila wakati.”

    “Najua. Uzuri wako ndiyo unaonifanya nilizungumze hili kila wakati, hakika sitochoka kukwambia hilo,” alisema Edmund huku akiachia tabasamu.

    “Nashukuru.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ningependa sana uwe msichana wangu Sheila.”

    “Yaani bado tuhaujachoka kuniambia hilo!”

    “Siwezi kuchoka na kamwe sitochoka. Nitaacha kukwambia hili endapo utakubali kuwa nami, baada ya hapo, nadhani hautosikia nikikwambia tena kwamba nataka kuwa nawe,” alisema Ignas.

    “Naomba nijifikirie.”

    “Daah! Yaani kujifikiria miezi yote hiyo jamani!”

    “Ndiyo, si ninataka kupanga maamuzi sahihi.”

    “Najua, ila umenipa muda mrefu sana Sheila, ni zaidi ya miezi sasa, kipindi chote hicho nakusisitizia kwa kitu kimoja tu” alilalamika Ignas.

    “Tutaongea tukifika nyumbani.”

    “Sawa. Hakuna tatizo.”

    Hiyo ikaonekana kuwa faraja kwa Ignas, moyo wake ukaanza kukusanya matumaini kwa kuona kwamba hatimae Sheila alikubali kuwa msichana wake. Hakutaka kuonesha matumaini hayo usoni, alijifanya kutokuwa na uhakika kama angekubaliwa au la.

    Baada ya dakika chache, wakafika, wakateremka na kuanza kuelekea ndani.

    “Niambie sasa.”



    ‘Una haraka mno, hata kula hatujala.”

    “Sawa. Karibu jikoni.” alisema Ignas.

    Wakaelekea jikoni ambapo huko wakaanza kupika na baada ya muda fulani, wakaanza kushikana hapa na pale na mwisho wa siku kujikuta kitandani. Hiyo ikawa siku ya kwanza kwa wawili hao kulala pamoja, wakafanya kila kitu kiichotakiwa kufanywa na wapenzi kitandani.

    “Naomba usiniumize,” alisema Sheila mara baada ya kumaliza kila kitu.

    “Siwezi kufanya hivyo, niamini,” alisema Ignas kwa kujiamini.

    ***

    Alipolifikia geti la Hoteli ya The Atriums, Filbert akaingia ndani. Muonekano wa hoteli ile, Filbert akashindwa kuamini kama leo hii alikuwa akiingia ndani ya eneo lililokuwa na mandhari mazuri kama yalivyokuwa katika hoteli ile.

    Kila alipokuwa akiyaangalia, hasa kwa kijana kama yeye aliyekulia uswahilini, hakuamini, akabaki kutokuamini tu.

    Mara baada ya kuona hakukuwa na mtu yeyote aliyeonesha kwamba alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakijihusisha na filamu kutoka katika Kampuni ya Panorama, Filbert akaanza kupiga hatua kuelekea mapokezini.

    “Karibu sana,” alisema dada aliyekuwa mapokezini, uso wake ulipambwa na tabasamu pana.

    “Asante. Kuna watu nimekuja kuwaulizia,” alisema Filbert.

    “Wakina nani?”

    “Wazungu kutoka katika kampuni ya filamu Marekani.”

    “Wewe ndiye Filbert?”

    “Ndiyo.”

    “Niliachiwa maagizo yako, unaweza kwenda chumba namba 14,” alisema yule dada na kuanza kumpeleka katika chumba hicho.

    Katika kila sehemu anayopita ndani ya hoteli hiyo hakuamini kile alichokuwa akikiona, mandhari mazuri ya hoteli ile yalimfanya kutokuamini kama masikini yeye aliyezaliwa katika familia masikini siku hiyo alikuwa akikanyaga katika marumaru yenye kung’aa.

    “Kumbe kuwa na fedha raha,” alijisemea Filbert.

    Safari yao ikaishia katika chumba hicho ambapo mlango ukafunguliwa na kijana aliyekuwa akihusika na uratibu wa shindano la kuwatafuta wasanii kuufungua mlango, alipomuona Filbert tu, akamtaka kuingia ndani.

    Msanii mwenzake, Thomas alikuwa ndani ya chumba hicho, Wazungu zaidi ya watano walikuwa wamemuweka Thomas huku wakiongea naye mambo mengi yakiwepo ya tamthilia hiyo iliyotakiwa kuchezwa nchini Tanzania.

    Kila kitu kikapangwa ndani ya chumba hicho na ni utayarishji tu ndiyo uliokuwa ukisuburia. Waigizaji wengine katika tamthilia hiyo walitarajiwa kuingia baada ya wiki moja, walipoingia tu, mchakato mzima ukaanza siku hiyo.

    Ilikuwa ni ndoto iliyoonekana kutimia, kwa sababu alikuwa akijua sana kuigiza, alijitahidi kuigiza kwa uwezo wake wote ndani ya filamu hiyo kiasi kilichowafanya Wazungu hao kumfurahia hata zaidi ya walivyomfurahia Thomas.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “He knows how to act, I think we have to do something for him (Anajua namna ya kuigiza, nafikiri inatupasa tufanye kitu kwa ajili yake,) alisema Mkurugenzi mkuu, Mc Kenzie.

    “Should we tell him?” (Tumwambie?)

    “No. We have to wait” (Hapana. Tusubiri kwanza)

    Hicho ndicho walichokuwa wamekipanga kwa wakati huo, uigizaji wa filamu ile ukaanza na Filbert akawavutia kiasi cha kutamani kufanya naye kazi zaidi, hawakutaka kumwambia kwamba walitakiwa kuendelea kufanya naye kazi kwani hilo walitaka kulifanya na kuwa ‘supise’ kwake.

    Kupitia uigizaji wake, hata waigizaji wa tamthilia hiyo kama Edward Lambert, Phillip Powell walionekana kuvutiwa naye kiasi ambacho wakatamani Filbert ajiunge naye kwa ajili ya kufanya naye kazi zaidi na si kuishia katika tamthilia hiyo tu.

    “Anavutia, anaweza sana, natumaini tukiwa naye, kuna mengi ataonesha,” alisema Lambert.

    “Sawasawa. Kwa hiyo tufanye nini?” aliuliza Mkurugenzi, Mc Kenzie.

    “Tumchukue, tumfundishe zaidi, atakuja kuwa mkali sana” alishauri Edward.

    Hilo likapita na hakukuwa na kipingamizi chochote kile, uigizaji wa Filbet uliendelea kuwavutia na hata walipokuwa wakiangalia tamthilia ile, katika kila kipande ambacho Filbert aliigiza, alionekana kufunika.

    Filbert hakuwa mtu wa kuonekana nyumbani, kwa kiasi fulani maisha yake yalianza kubadilika. Hakuwa akikaa nyumbani, katika muda wote wa kuigiza, alikuwa amepangiwa hoteli Bagamoyo ambapo filamu hiyo ilikuwa ikiendelea.

    Katika kipindi chote cha usiku, mawazo yake yalikuwa juu ya mama yake aliyekuwa mgonjwa, Alimpenda mno kwani ndiye aliyekuwa mtu pekee aliyembakiza katika maisha yake, ugonjwa wa kansa ya koo aliokuwa akiumwa, ulimuumiza.

    “Nitafanikiwa tu, hata kama nitaigiza tamthilia hii tu, bado naamini nitafanikiwa,” alisema Filbert huku akiwa hajui kama tayari wenzake walikwishamuwekea mipango endelevu katika kipaji chake cha kuigiza.



    Ignas alirudisha furaha yake iliyopotea kipindi cha nyuma kilichopita, wanaume wote waliokuwa wakimfuata, aliamua kuwapiga chini na kuwa na mwanaume mmoja ambaye alimchagua kwa moyo wake wote, huyu alikuwa Ignas.

    Pengo la mapenzi ambalo aliliacha Edmund moyoni mwake likazibika, kidonda kikubwa alichokuwa amekipata kutoka kwa mwanaume huyo aliyekuwa akimchukia, katika kipindi hicho kilikuwa kimepona kabisa.

    Mapenzi yao hayakuwa siri, chuoni, kila mtu alikuwa akifahamu, wanaume waliokuwa wakimfuata wakaonekana kukosa nafasi hiyo tena kwani tayari msichana Sheila alikuwa amechukuliwa, walitakiwa kujiweka pembeni kabisa.

    Siku ziliendelea kukatika, mapenzi yao yaliendelea kukua kila siku, Sheila hakutaka kumkumbuka tena Edmund aliyeuumiza moyo wake, mawazo yake na malengo yote aliyaweka kwa mpenzi wake huyo ambaye mpaka kufikia kipindi hicho alionekana kuwa kila kitu kwake.

    Jina la Edmund bado liliendelea kuvuma zaidi, aliendelea kuigiza filamu nyingi zilizomuingizia kiasi kikubwa cha fedha. Edmund, mwanaume aliyekuwa akiishi katika maisha ya kimasikini, kwa wakati huo alikuwa akiogelea fedha tu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Umaarufu wake ukaongezeka, baada ya kutoa filamu na Waafrika Kusini, hapo akahamia nchini Nigeria. Akawakusanya wasanii wote wakubwa na kuigiza nao, aliamua kujitangaza na kwa kiasi kikubwa akawa amefanikiwa.

    Kila alipopita alinukia fedha, hakukuwa na msanii mkubwa kama alivyokuwa, shida hazikuwa sehemu ya maisha yake tena, aliendelea kujitangaza huku jina lake klikianza kuwa miongoni mwa wasanii walioingiza kiasi kikubwa cha fedha kila mwaka.

    “Fedha na umaarufu, hakika nimezaliwa masikini, halipingiki, ila kwenye kufa, nitakufa nikiwa tajiri mkubwa,” alijisemea Edmund.

    Huo ndiyo ulikuwa mtazamo wake, makampuni mengi yalimuona kuwa kisima chao cha kuingiza fedha, kila walipotaka kuzitangaza bidhaa zao basi ilikuwa ni lazima kumuita Edmund na kumfanyia matangazo.

    “Naomba nafasi ya kuigiza Ed,” ilisikika sauti ya msichana simuni, kwa jinsi ilivyosikika, ilitosha kabisa kugundua kwamba huyo alikuwa miongoni mwa wasichana warembo, mwili wa Edmund ukasisimka.

    “Unataka kuigiza?” aliuliza Edmund japokuwa alisikia vema sauti ya msichana yule.

    “Ndiyo. Ninaomba kuigiza.”

    “Sawa. Upo wapi?”

    “Naishi Tanga Barabara ya 13.”

    “Sasa nitaweza kuuona vipi uwezo wako?”

    “Kama ukinihitaji, naweza kuja Bongo.”

    “Sawa. Itakuwa vizuri. Njoo,” alisema Edmund.

    Moyo wake ulikuwa na uhakika kwa asilimia mia moja kwamba msichana ambaye alikuwa amempigia simu alikuwa moja kati ya wanawake warembo waliobarikiwa waliokuwa wakiishi katika nchi hii ya Tanzania, hivyo alitaka kumuona.

    Hakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea, kuanzia hapo, kichwa chake kikaanza kumfikiria mno msichana huyo huku muda mwingi akiutumia kumtengeneza msichana wake kichwani mwake, na kila msichana aliyekuwa akimtengeneza, alikuwa mrembo.

    Ndani ya siku mbili, msichana huyo akawasili Jijini Dar es Salaam. Kitu cha kwanza tu alichokifanya ni kumpigia simu Edmund ambaye akaomba kuonana naye ili aweze kumwangalia kama alikuwa bomba au alikuwa akikipa kazi kichwa chake kumtengeneza msichana mrembo na wakati alikuwa wa kawaida.

    Wakapanga sehemu ya kukutania, hotelini Atriums kulionekana kufaa kabisa. Saa kumi jioni Edmund alikuwa akiegesha gari lake ndani ya eneo la hoteli hiyo, akateremka na kuanza kuyapitisha macho yake huku na kule, sehemu ya kupumzikia kulipokuwa na majani, macho yake yakatua kwa msichana mmoja mrembo, moyo wake ukamwambia kwamba ndiye alikuwa msichana huyo.

    Kwa mwendo wa kujiamini, Edmund akaanza kupiga hatua kumfuata, alipomfikia, tabasamu pana likaonekana usoni mwa msichana huyo, mwanya wake na vishimo vidogo mashavuni mwake vikaupendezesha uso wake.

    “Mambo,” alisalimia Edmund.

    “Safi. Karibu,” alimkaribisha msichana huyo.

    “Asante. Bila shaka ninayeongea naye ni Yasnat?” aliuliza Edmund.

    “Yeah! Ndiye mimi, karibu Edmund,” alisema Yasnat, Edmund akakaa kitini.

    Kwa jinsi Yasnat alivyokuwa, Edmund hakuwa amekosea, uzuri wa msichana yule ulifanana na taswira za wasichana wote warembo ambao alikuwa amewatengeneza ndani ya kichwa chake.

    Yasnat alikuwa msichana mweupe aliyebadirikiwa na shepu nzuri, sura yake ilikuwa ya kitoto huku kila wakati akiwa mtu wa kutabasamu tu. Umbo lake lilikuwa la kimisi huku kifuani mwake, matiti makubwa na mazuri yaliyokuwa na mvuto yakionekana kumpendezesha na kuwavutia wanaume waliokuwa na uchu. Kwa kumwangalia tu, Yasnat alistahili kuonekana kwenye filamu zake.

    “Ulisemaje vile?” aliuliza Edmund.

    “Nilitaka kuigiza nawe.”

    “Usijali, bila shaka unajua kuigiza. Ila ili nijiridhishe, unaonaje ukiigiza mbele yangu mahali hapa?” aliuliza Edmund.

    “Niigize hapa? Mbele za watu hapa?”

    “Ndiyo.”

    “Jamaniiiiii.”

    “Unaogopa?”

    “Yeah! Au kama tungekuwa wawili,” alisema Yasnat.

    Katika kila hatua aliyokuwa akipitia msichana huyo, hasa maneno aliyokuwa akiyazungumza, akili ya Edmund ilikuwa ikihama kabisa, kitendo cha kuambiwa kwamba angeweza kuigiza mbele ya macho yake endapo tu wangekuwa wawili, kichwa chake kikafikiria harakaharaka kwamba alitakiwa kuchukua chumba hotelini hapo.

    “Basi twende ukaigize chumbani mbele ya macho yangu peke yangu,” alisema Edmund, Yasnat akakubaliana nae.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tayari Edmund alijiona mshindi, msichana aliyekuwa mbele yake alionekana demu bomba kwa kumwangalia, kitendo cha kukubali waende chumbani ili aigize mbele ya macho yake kilimpa uhakika kwamba ilikuwa ni lazima afanye naye ngono tu, iwe isiwe.

    Walipofika chumbani, Edmund akavua nguo zake na kubakiwa na boksa tu, akaanza kumwangalia Yasnat kwa macho yaliyojawa na matamanio. Yasnat akavua nguo zake na kubaki na nguo ya ndani, hapohapo, akaanza kuigiza.

    Ndiyo, alijua kuigiza lakini wakati huo akili ya Edmund ilikuwa imehama kabisa, hata kama Yasnat asingekuwa anajua kuigiza lakini tayari kwa jaji mkuu kama Edmund msichana huyo alikuwa amekishapita, hivyo hakuhitajika kuigiza zaidi.

    “Unajua.”

    “Kweli?”

    “Niamini. Umepita,” alisema Edmund, tayari mikono yake ilifika mwilini mwa msichana huyo, akaanza kumtomasa hapa na pale, mwisho wa siku, hata ile nguo moja aliyobaki nayo, akaichojoa, Edmund akachanganyikiwa, kifua kizuri cha msichana Yasnat kikamchanganya.

    “Asanteeeeee.....” alisema Edmund mara baada ya kifua cha Yasnat kuwa mbele ya macho yake, alikuwa huru kufanya chochote alichokitaka, kitu ambacho hakuwa akikifahamua, Yasnat hakuwa msichana wa kawaida kama walivyokuwa wengine, huyu, alikuwa tofauti kabisa.



    Tetesi zilikuwa zikisikika kwamba kulikuwa na mwanamke jini aliyekuwa akiua watu mjini Tanga. Idadi kubwa ya wanaume waliokuwa wakiuawa usiku ilisadikiwa kwamba walikuwa wakiuawa na mwanamke huyo jini ambaye tetesi zilisema kwamba alikuwa mzuri kwa kumwangalia tu.

    Wanaume wakaogopa, hofu ikawaingia na hata wale waliokuwa wakichukua wanawake nyakati za usiku wakapacha tabia hiyo, na kama waliifanya, waliifanya kwa umakini mkubwa sana.

    Wanawake wazuri wote waliokuwa wakiishi Tanga hasa wale waliokuwa Waarabu walipata wakati mgumu mno kwani kila walipopita, walikuwa wakiitwa ‘Jini wa Uarabuni’.

    Idadi ya watu waliokuwa wakiuawa ilizidi kuongezeka kila siku. Wale waliokuwa wakipenda kwenda klabu nyakati za usiku, hawakwenda tena, wakabaki nyumbani kwao wakiendelea kufanya mambo yao.

    “Nimekutana na Jini wa Uarabuni jana usiku,” alisema jamaa mmoja.

    “Acha masihara kaka.”

    “Kweli tena.”

    “Yupo vipi?”

    “Demu wa Kiarabu, mkali sana, yaani nilivyomuona jana, japokuwa alikuwa akitaka nisimame, sikusimama, nikaunganisha zangu kwani mwili ulikuwa ukinisisimka mno,” alisema jamaa huyo.

    “Hasa barabara ya 13, hapo ndipo kunapotisha zaidi, ukipita usiku tu, umeula wa chuya,” alisema jamaa mwingine.

    Taarifa zikatolewa kwamba halikuwa jambo zuri kutembea nyakati za usiku na kuchukua wanawake hovyo, kila mmoja akatakiwa kuwa makini kwani Jini wa Uarabuni bado alikuwa akiendelea kuua kama kawaida yake.

    ****

    “Mke wangu, unakuwa unalalamika sana, tatizo kwani nini hasa kipenzi?” aliuliza mzee Yusufu, mzee mwenye ndevu nyingi nyeupe zilizomfanya kuonekana mzee mno, alikuwa akiongea na mke wake, bi Arafa.

    “Nimechoka na hayo madude yako, kila siku mtoto wetu analia tu, naomba uyatoe hayo madude, sitaki kuyaona wala kuyasikia,” alisema bi Arafa, aliongea kwa jasira, tena kwa sauti ya juu.

    “Mke wangu, mbona ni viumbe wazuri tu, tena yananipa heshima sana hapa Tanga Mjini, hulioni hilo?” aliuliza mzee Yusufu.

    Siku hiyo ilikuwa ni kama ugomvi, bi Arafa alikuwa akimlalamikia sana mume wake kwa tabia yake aliyokuwa nayo ya kufuga majini ambayo kwake aliyaita viume vizuri ambavyo havikuwa na madhara yoyote yale.

    Majini aliyokuwa nayo aliyafunga kwenye chupa, yalikuwa majini mawili ambapo moja aliitwa Maimuna na mwingine Makata.

    Uwepo wa majini hayo ndani ya nyumba yakamkosesha amani mtoto wao aliyekuwa na miaka kumi, kila siku usiku alikuwa akilia kwa kusema kwamba alikuwa akiona vitu vya hatari kila alipokuwa akilala.

    Japokuwa watu wengi waliokuwa na matatizo mbalimbali walikuwa wakifika nyumbani hapo na kusomewa dua na mzee Yusufu lakini bado mke wake hakufurahishwa na uwepo wa majini yale, kila siku alikuwa akimlazimisha mume wake ayaondoe nyumbani hapo na kwenda kuyatupa.

    Majini hayakuwa kama binadamu, yalikuwa ni roho ambayo chakula chao kikubwa kilikuwa ni damu. Mara kwa mara mzee Yusufu alikuwa akienda machinjioni ambapo alinunua damu za ng’ombe au mbuzi kisha kurudi nyumbani na kuweka kwenye bakuli kubwa, alikuwa akisoma dua, majini yale yalitoka chupani na kisha kunywa damu ile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake ya kila siku. Kupitia majini hayo, alijikuta akifanikiwa, akiingiza fedha lakini bado nyumba yake haikuwa na amani hata kidogo.

    Kila siku mke wake alikuwa akilalamika kwamba majini yaliyokuwa ndani ya nyumba hiyo hayakuwa mazuri na ndiyo maana mtoto wao alikuwa akilalamika sana kwamba alikuwa akiona vitu vya ajabuajabu.

    Baada ya malalamiko hayo kuongezeka, mzee Yusufu akaamua kuzichukua zile chupa zilizokuwa na majini na kwenda kuzitupa baharini, hakutaka kuwa nayo tena.

    Huko baharini, watoto waliokuwa wakichezacheza walipozioan chupa hizo, wakavutiwa nazo, wakazichukua na kuzifungua vifuniko kwa lengo la kwenda kuzijaza maji, majini hayo yakatoka na kuingia mitaani.

    Kitu cha kwanza kabisa kufanya ni kuchukua miili ya binadamu, jini Maimuna akachukua umbo la msichana mrembo wa Kiarabu na kisha kuanza kufanya mauaji, hakuwa amekunywa damu kwa kipindi kirefu, hivyo alihitaji damu na hakukuwa na njia yoyote ya kuipata zaidi ya kuua.

    Wanaume waliogopa sana, mauaji hayo yaliwatisha sana lakini hakukuwa na jinsi ya kukiepuka kifo hicho zaidi ya kuwapuka wanawake waliokuwa wakijiuza usiku, hasa msichana wa Kiarabu ambaye alikuwa gumzo Tanga nzima.

    ****

    Edmund hakujua ni kitu gani kilichokuwa kikimtokea chumbani hapo, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi kutokana na mzunguko wa damu yake kuwa mkubwa mno.

    Jasho likaanza kumtiririka huku kwa mbali akiwa na hofu kubwa iliyoanza kumuingia. Hakujua ni nini kilisababisha hali hiyo, kila alipojiuliza, hakupata jibu lolote lile.

    Alimwangalia Yasnath kwa macho ya tamaa, kifua cha kilimchanganya mno, tofauti na hicho kifua, hata umbo lake lilionyesha ni kwa jinsi gani msichana huyo alikuwa mrembo mno.

    Mtoto wa Kiarabu mwenye ngozi nzuri isiyokuwa hata na kovu lolote lile, hakika lilimpagawisha kupita kawaida.

    “Mbona natokwa na jasho sana? Yaani ina maana sikuwahi kukutana na msichana mrembo kama alivyokuwa Yasnath au?” alijiuliza lakini hakupata jibu.

    Mwili wake ukaanza kumtetemeka pia, alikuwa kama mtu aliyesikia baridi kali, katika kila mabadiliko yaliyokuwa yakitokea chumbani humo, alikuwa akijishangaa lakini hakutaka kuzungumza.

    Akaanza kumsogelea Yasnath, moyo wake ulizidi kuwa na hofu, japokuwa msichana yule alijitahidi sana kutoa tabasamu lakini halikuweza kuubadilisha moyo wa Edmund, hofu haikuweza kumtoka kabisa.

    Kwa kipindi hicho akili yake ilikuwa kama imefungwa, hakuwa na wazo la kutoka nje, kitu kilichokuwa kimemtawala ni kufanya mapenzi na msichana huyo ambaye alidiriki kusema kwamba hakuwahi kukutana na msichana mrembo hapo kabla kama alivyokuwa Yasnath.

    “Mwaaaa...” Yasnath akambusu Edmund shavuni mwake.

    Katika hali ambayo hakuitegemea kabisa, mapigo ya moyo wake yakapungua na kuwa kama kawaida, mwili wake ukaacha kutetemeka na hofu yote kumuondoka moyoni mwake, busu lile likabadilisha kila kitu.

    Wakakumbatiana na kulala kitandani, kilichofuata ni milio ya kimahaba na miguno ya hapa na pale, yaani walikuwa kama watu waliotamaniana kwa kipindi kirefu.

    Edmund hakujua kama alikuwa akifanya mapenzi na Jini Maimuna aliyejulikana kwa jina la Jina wa Uarabuni.



    Wazungu wale kutoka katika Kampuni ya Panorama walichukua mwezi mzima kuwepo nchini Tanzania ambapo tamthilia ya Wicked Journey bado ilikuwa ikiendelea kuigizwa kama kawaida.

    Hawakuishia jijini Dar es Salaam tu bali walikwenda mpaka katika sehemu nyingine kama Zanzibar, kigoma, Kilwa na sehemu nyingine ambapo filamu hiyo iliendelea kuigizwa kama kawaida.

    Katika waigizaji wote wageni ambao walifanya vizuri alikuwepo Filbert, japokuwa alionekana kuwa kijana mdogo lakini uwezo wake haukuweza kujificha, alikuwa akiigiza vizuri kiasi kwamba Wazungu wale walionekana kuvutiwa naye.

    Huo ukawa mwanzo wa safari yake ndefu, tamthilia ile ilipoanza kurushwa katika majumba mbalimbali ya sinema, Filbert alipata mashabiki wengi kwani kazi ambayo ilifanyika ilikuwa kubwa na ilimletea heshima kubwa.

    Malipo ambayo alilipwa baada ya kuigiza tamthilia ile ilikuwa ni dola elfu ishirini ambazo zilikuwa ni zaidi ya milioni thelathini, fedha ambazo zilikuwa kubwa mno na hivyo kuanzisha biashara.

    Kwa kuwa hakuwa na utaalamu wa kufanya biashara hasa kubwa, akamkabidhi mama yake fedha hizo na kisha kuanza kuzipanga kwa ajili ya biashara ambazo waliamini kwamba zingewaingizia vipato.

    Mama yake, Bi Imelda akaamua kufungua duka la kuuza vitenge ambavyo alikuwa akivuitoa nchini Kongo kwa kupitia mkoani Kigoma na kuvipeleka Dar es Salaam. Ilikuwa biashara nzuri ambayo ilimuingizia fedha nyingi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mbali na biashara hiyo, pia wakafungua biashara ya kuuza nguo na viatu Manzese, sehemu ambayo kwa kipindi hicho hakikuwa na nguo nyingi hivyo kupata faida kubwa. Hiyo tu haikutosha, walichokifanya ni kuanza biashara ya kuchukua mazao kutoka mikoani na kuyaleta jijini Dar es Salam.

    Ilikuwa ni biashara nyingine ambayo iliwaingizia sana fedha. Kiasi kile alichokuwa amepewa Filbert kama malipo ya kuigiza filamu ile iliyoingiza mamilioni ya shilingi iliyabadilisha maisha yake kabisa.

    Maisha yao yakabadilika, wakahama Manzese walipokuwa wakiishi na kuhamia maeneo ya Kijitonyama. Waliyajua maisha ambayo walipitia kabla hivyo hawakutaka kurudi tena, umasikini ambao walikutana nao katika maisha yao ya nyuma wakatamani kuuacha na kubaki historia ambayo kamwe isingejirudia tena.

    Japokuwa kidogo alikwishaanza kupata maisha mazuri na mama yake lakini bado kichwa chake kilikuwa kuhusiana na uigizaji tu. Aliigiza tamthilia ya Kizungu na kutegemea kwamba angepata jina kubwa lakini hiyo wala haikumpa nafasi kubwa kwani tamthilia hiyo ilitazamwa zaidi katika nchi za Ulaya na Marekani.

    “Mungu ametutoa mbali sana, kama tukiendelea hivi, tutakuja kuwa na maisha mazuri zaidi ya hapa,” bi Imelda alimwambia Filbert.

    “Najua mama lakini bado moyo wangu haupo kwenye kufanya biashara hizi,” alisema Filbert.

    “Haupo kwenye kufanya biashara hizi?”

    “Ndiyo mama, bado ninataka kuwa muigizaji.”

    “Kwani si unataka kuwa muigizaji ili upate fedha? Sasa fedha si umekwishapata!”

    “Hapana mama, fedha pekee hazitoshi na ninaamini nikipata umaarufu, fedha zitakuja nyingi mara mia ya hizi.”

    “Sasa itakuwaje? Mrudie tena Edmund.”

    “Ni ngumu mama.”

    “Kwa nini? Uligombana naye?”

    “Hapana.”

    “Kumbe?”

    “Basi tu, jamaa ana maringo sana, alinionyeshea nyodo fulani ambazo kwangu hazikunivutia,” alisema Filbert.

    Ndoto yake haikufutika moyoni mwake, bado alikuwa akifikiria kuwa muigizaji mkubwa ambaye angeingiza kiasi kikubwa cha fedha katika maisha yake. Aliamini katika uigizaji, kwa jinsi Edmund alivyokuwa akiingiza fedha kupitia uigizaji, aliamini kwamba hata na yeye angeweza kuingiza fedha hivyohivyo.

    Siku zikaendelea kukatika, hakuacha kuigiza peke yake kila awapo chumbani au anapokwenda ufukweni kutembea, uigizaji ulikuwa damuni mwake na hakika hakutaka kuachana nao.

    Mara baada ya watu kutazama Tamthilia ya Wicked Journey, hapo ndipo walipogundua kwamba ndani yake kulikuwa na Watanzania na ilikuwa imechukuliwa baadhi ya vipande kutoka nchini Tanzania.

    Hapo ndipo watu walipoanza kuizungumzia, ilizungumziwa mno katika mitandao ya kijamii na hata kutangazwa katika redio mbalimbali nchini Tanzania bila kusahau televisheni.

    Pasipo kutarajia, Filbert na kijana mwingine, Thomas wakajikuta wakianza kupata umaarufu na kuanza kuzungumziwa katika sehemu mbalimbali. Umaarufu ambao alikuwa akiutaka ukaanza kumnyemelea, aliitwa kwenda kufanya interview na redio, televisheni na hata magazeti, alionekana kijana mdogo mwenye kiu ya kutaka kuwa na mafanikio makubwa nchini Tanzania.

    Uigizaji wake ukapendwa hata zaidi ya Thomas, alionekana kuwa na uwezo mkubwa na huku wengine wakidai kwamba hata Edmund hakuwa akiufikia uwezo wake kitu ambacho kikaanzisha bifu kubwa moyoni mwa Edmund.

    Alimfahamu Filbert, alikumbuka siku ambayo alimfuata nyumbani kwake na kumwambia kwamba alikuwa akitaka kuigiza na hivyo alihitaji nafasi, alimdharau kwa kuwa alijiona kuwa juu lakini mwisho wa siku, kile alichokuwa akikitaka, kuwa maarufu na kuigiza filamu na Wazungu nchini Marekani, hakukipata, bahati hiyo ikaenda kwa mtu ambaye alimfuata nyumbani kwake na kumuomba sana, Filbert.

    Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, hakuamini kama kweli nafasi aliyokuwa ameipata Filbert aliitafuta kwa kipindi kirefu lakini hakuweza kuipata. Wakati mwingine alikaa na kumlalamikia Mungu kwamba kwa nini hakutaka kumpa nafasi kama ile ambayo kila siku alikuwa akiitaka sana.

    Vyombo vya habari ndivyo vilivyokuwa vikimchanganya zaidi na kumuongezea chuki dhidi ya Filbert. Jina na picha ya Filbert vilipokuwa vikitolewa gazetini na kwenye televisheni, alijisikia kuumia kupita kawaida.

    Jina lake likaanza kufutika japokuwa alikuwa muigizaji mkubwa tu. Kitu ambacho kilimuumiza zaidi ni pale alipomsikia Filbert akiwaomba Watanzania wamuombee kwa kuwa alikuwa akijiandaa na safari ya kuelekea nchini Marekani kusaini mkataba rasmi na Kampuni ya Panorama na baada ya hapo, anaingizwa moja kwa moja katika uigizaji wa filamu za Hollywood.

    Hakukuwa na siku ambayo aliumia maishani mwake kama siku hiyo, aliuma meno yake kwa hasira na kumlaumu Mungu kwa kisingizio kwamba alikuwa akimpendelea Filbert bila kujua kwamba maisha ambayo aliyapitia kijana huyo mpaka kufika hapo alipokuwa amefika, alipitia maisha ya shida na dhiki kubwa kuliko yeye.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nitamuua hata kabla hajakwenda nchini Marekani,” aliwaza Edmund huku pembeni akiwepo Yusnath.

    “Hakuna haja ya kumuua, achana naye, kila mtu ana bahati yake Edmund,” alisema Yusnath, Edmund akashtuka kwani jambo hilo hakulitamka zaidi ya kuliwaza kichwani mwake.

    “Nani?”

    “Huyo Filbert, hakuna haja ya kumuua, achana naye,” alisema Yusnath.

    “Yusnath, nani amesema anataka kumuua?”

    “Wewe mwenyewe.”

    “Hapana. Siwezi kuwaza kitu kama hicho.”

    “Huwezi kunificha mpenzi, achana naye,” alisema Yusnath na kutoka chumbani hapo.

    ****

    Maisha yalibadilika ghafla na kwa haraka mno, Filbert yule masikini ambaye kila Jumamosi ilikuwa ni lazima kuelekea katika Viwanja Leadres Club kwa ajili ya kuzungumza na wasanii ili wamtoe hakuwa huyu Filbert wa kipindi hiki.

    Jina lake lake likaanza kuwa kubwa nchini Marekani, katika kila sehemu ambayo uzinduzi wa tamthilia ile ulipokuwa ukifanyika, Filbert alikuwa huko kitu kilichomfanya kujulikana zaidi.

    Mbali na tamthilia ile kuwa na mhusika mkuu lakini katika vipande ambavyo Filbert alivicheza, alionekana kuvitendea haki na kuongeza ubora katika tamthilia hiyo. Huo, kwake ukawa kama mwanzo, kuanzia siku hiyo akaanza kuitwa na kuigiza katika filamu mbalimbali nchini Marekani.

    Umaarufu ukawa juu, fedha alizokuwa akilipwa, akanunua jumba kubwa nchini Marekani katika Mji wa Miami uliokuwa katika Jiji la Florida. Waigizaji wengi nchini Marekani wakataka kuigiza pamoja naye, filamu yake ya kwanza kuigiza mbali na tamthilia ile ilikuwa Travelled With Aunt Penny.

    Ilikuwa filamu nzuri iliyompa sana jina, kila aliyekuwa akiiangalia alikiri kwamba Filbert angekuwa muigizaji mkubwa sana siku za usoni.

    “Ni ndoto mama,” alisema Filbert.

    “Hapana mwanangu, kila kitu kinachoendelea ni maisha halisi, umekuwa maarufu, una heshima na fedha pia, mshukuru Mungu kwa kila kitu,” alisema bi Imelda.

    “Mama, unakumbuka kipindi kile tulichokuwa tukilala bila kula, ulipokuwa ukiumwa na kukosa fedha za dawa?” aliuliza Filbert.

    “Nakumbuka kila kitu Fil, siwezi kusahau kitu chochote kile,” alisema bi Imelda.

    “Kila kitu kimepita, maisha ya mateso na dhiki kuu tuliyopitia, acha yapite na kubaki ndoto tu, Mungu amefanya, nitaendelea kujituma zaidi mama mpaka niwe zaidi ya hapa,” alisema Filbert.

    Filamu ziliendelea kumiminika zaidi, jina lake likaendelea kuwa kubwa, kampuni mbalimbali za biashara zikaanza kujitokeza kwa ajili ya kujitangaza kupitia yeye. Kinywaji cha pombe kali, Ciroc wakamfuata na kuwekeana naye mkataba kwa ajili ya kufanya matangazo naye.

    Huo haukuwa mwisho, kila kitu kilichofanyika kwake kilikuwa ni fedha tu, jina lake likazidi kuongezeka, majarida mengi nchini Marekani kama PlayBoy, Fantasy, Forbes, Vogue na mengine mengi yalikuwa yakitawaliwa na picha zake huku yakimsifia kwamba ni kizazi cha nyoka, yaani aliyekuwa mkali, mwenye sumu kali kama nyoka.

    Alikusanya fedha, alizilalia fedha, alitumia fedha kadiri alivyotaka na wala hazikuisha. Alimiliki magari ya kifahari na kununua nyumba tatu ambapo mbili akaamua kuzipangisha.

    Huyu alikuwa Filbert, muigizaji mkubwa aliyekulia kwenye maisha ya kimasikini, baada ya kuishi sana Manzese Midizini, leo hii alikuwa akiishi Miami, sehemu iliyokuwa na fukwe nyingi ambazo zilitembelewa na masupastaa wengi wakiwepo Jay Z, Kanye West, Tom Cruiz, Madonna na watu wengine waliokuwa maarufu.



    Watu wakaachana na Edmund, Filbert ndiye aliyekuwa habari ya mjini kipindi hicho. Aliitangaza nchi ya Tanzania kila sehemu aliyokuwa. Ilionekana kuwa kama kosa la jinai kama ungeizungumzia tasnia ya filamu bila kumgusia Filbert.

    Alitikisa dunia nzima, kila mtu aliyesikia stori ya maisha yake kwamba alikuwa kijana masikini aliyeishi na mama yake, kula kwa manati lakini leo hii alikuwa hivi, hakukuwa na aliyeamini.

    Kitu kama msumali mzito wenye moto ulikuwa moyoni mwa Edmund, kila siku alikuwa akisikia maumivu makali kitu kilichomtesa sana maishani mwake. Alikuwa amejijengea heshima kubwa lakini kwa kitendo cha Filbert kuwa maarufu mkubwa kilimfunika kabisa.

    Kisasi chake bado kilikuwa moyoni mwake, alijua fika kwamba kijana huyo ndiye aliyeizima ndoto yake, hivyo naye alitaka kumzima milele. Hakujua angefanya nini, alijaribu kwenda kwa waganga mbalimbali kwa ajili ya kummaliza mtu huyo lakini alimbiwa kwamba uchawi waliokuwa nao usingeweza kuvuka bahari.

    “Nitamuua vipi sasa, haiwezekani mtu kaja juzijuzi tu leo hii yupo Hollywood halafu mimi nipo Tanzania, hizi dharau” alisema Edmund.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bado kichwa chake kilikuwa na mawazo lukuki juu ya Filbert, moyo wake ukamfurukuta huku wivu kumtafuna kila siku. Hakupenda kumuona Filbert akiendelea kupata umaarufu na fedha na wakati yeye alikuwepo toka kitambo.

    Hakutaka kumshirikisha mtu yeyote juu ya suala alilokuwa nalo kipindi hicho, alitaka ibaki siri moyoni mwake na hata ikitokea siku mtu akijua basi awe mtu wake wa karibu mno.

    Kila kitu alichokuwa akikifikiria, mpenzi wake, Yusnath alikuwa akifahamu kila kitu kwa sababu hakuwa binadamu wa kawaida, alikuwa jini aliyetoroka ndani ya chupa aliyokuwa amefungiwa na kuanza kuua watu kwa kuwanyonya damu.

    Kwa macho ya kibinadamu, Yusnath alionekana msichana mrembo, binadamu halisi aliyekuwa akiishi katika dunia hii kitu ambacho hakikuwa sahihi.

    Toka alipoanza kuwa na msichana Yusnath, alijiona mambo yake yakimuendea vizuri tofauti na alivyokuwa kipindi cha nyuma. Katika kila dili alilokuwa akilifanya, alikuwa akifanikiwa kwa kiasi kikubwa kitu ambacho kilimfanya kumuona Yusnath kuwa msichana wa kipekee kabisa.

    Alimpenda sana Yusnath ila kama msanii kuna wakati alikuwa na tamaa ya kuwafuata wasichana wengine, kila alipokuwa akitaka kufanya hivyo, sura ya Yusnath ilikuwa ikimjia kichwani, mwisho wa siku hakuwa akifanya kile alichokuwa akipanga kukifanya.

    Moyo wake ulipigwa upofu, bado hakujua kama kila siku alikuwa akilala na Jini Maimuna kitandani kwake. Siku zote alikuwa akipanga mipango yake mwenyewe, kitu kilichokuwa kikimchanganya zaidi, kila alichokuwa akikifikiria, kesho Yusnath alikuwa akimwambia.

    “Nitatafuta mganga mwingine, ngoja nimshirikishe Yusnath, inawezekana huko Tanga kukawa na waganga wazuri,” aliwaza Edmund.

    Hakuwa na jinsi, kwa sababu alimpenda mno msichana Yusnath, kesho yake akaamua kumuita na kuzungumza naye. Aliongea huku muonekano wake ukionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa ameumia moyoni mwake.

    Kwa macho ya huruma yaliyokuwa na mvuto, Yusnath akaanza kumwangalia Edmund, akaonekana kupagawa, alimuona Yusnath kuwa msichana mrembo zaidi ya siku nyingine.

    “Ninahitaji unisaidie jambo fulani,” alisema Edmund.

    “Jambo gani?”

    “Ninatafuta mganga mwenye uganga unaoweza kuvuka bahari,” alisema Edmund.

    “Mmmh! Mbona hapa Dar waganga wengi!”

    “Wote wamechemka, wamesema uganga wao hauwezi kuvuka bahari,” alisema Edmund.

    “Wewe unataka uvuke bahari ili iweje?”

    “Ninataka kum....daaah!” alisema Edmund, hata kabla hajamalizia sentensi yake, akakaa kimya.

    “Niambie, naweza kukusaidia.”

    “Ninataka kuua, moyo wangu upo kwenye maumivu makali mno.”

    “Hebu kuwa muwazi mpenzi, bado sijakuelewa,” alisema Yusnath, japokuwa alikuwa akifahamu kila kitu, hakutaka kujiweka wazi.

    Edmund hakuwa na jinsi, akaanza kumuhadithia Yusnath ni jinsi gani alikuwa akiumia moyoni kila alipokuwa akimuona Filbert akipata mafanikio makubwa zaidi ya aliyokuwa akiyapata.

    “Ninaumia, ninataka nimuue ili niendelee kuwa na heshima,” alisema Edmund.

    “Nitahakikisha nafanikisha katika hilo,” alisema Yusnath.

    “Utafanikishaje?”

    “Ni siri yangu, ila tunatakiwa kwenda sehemu fulani.”

    “Wapi?”

    “Sehemu fulani, si hapa duniani.”

    “Ni wapi? Mbinguni au Kuzimu?”

    “Utapafahamu tu. Leo tunaondoka mahali hapa, jiandae, kila kitu kitafanikiwa na mtu wako atakufa,” alisema Yusnath.

    Edmund akaridhika, akaonekana kuwa na furaha tena mara baada ya kugundua kwamba mpenzi wake, Yusnath angeweza kumsaidia. Ilipofika usiku wa saa sita, Yusnath akamwambia ajiandae kwani safari hiyo ingefanyika usiku huo.

    Haikuwa tatizo, akajiandaa na kuambiwa avae mavazi yenye rangi nyekundu, akavaa, baada ya kukamilisha kila kitu, akaambiwa achukue mayai manne kisha wakaondoka na kuelekea karibu kabisa na bahari.

    Edmund hakujua ni kitu gani kilichotakiwa kufanyika mahali hapo, alikuwa kimya huku akifuata maelekezo yote ambayo alikuwa akiambiwa na Yusnath. Akaambiwa ayachukue mayai yale na kuyatupa baharini, akafanya hivyo na kisha kuanza kuingia baharini hapo.

    Alikuwa akiogopa, waliendelea kupiga hatua mbele tena huku akiwa ameshikwa na msichana huyo. Mapigo yake ya moyo yalikuwa juu, kila alipokuwa akimwangalia Yusnath, msichana huyo hakuonyesha hofu yoyote ile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Maji yalipofika shingoni, ghafla akajikuta akizama, katika hali ambayo aliishangaa, walitokea sehemu ambayo ilionekana kuwa kama duniani, akaanza kujishangaa, ilikuwaje mpaka kufika hapo.

    “Mungu wangu! Nini kimetokea?” alijiuliza lakini hakuwa na jibu.

    Walikuwa kwenye ulimwengu mwingine, ulionekana kama ulimwengu huu wa kawaida lakini kule ulionekana kuwa wa tofauti sana. Watu waliokuwa wakipishana nao hawakuwa watu wa kawaida, walikuwa ni watu wa kutisha ambao walikuwa katika maumbo tofauti.

    Kuna wengine walikuwa na vichwa vya ng’ombe, paka, mbuzi na wanyama wengine lakini ukiviangalia vifua vyao, vilikuwa ni vya binadamu wa kawaida ila miguu yao haikuwa ya binadamu, ilikuwa ni kwato za wanyama.

    Kila alichokuwa akikiona, alikuwa akihofia sana, kuna kipindi alitamani kumuomba Yusnath amrudishe katika ulimwengu wa kawaida kwani kule alipokuwa, kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda mbele na ndivyo alivyokuwa akihofia zaidi.

    Walitembea mpaka kufika katika jumba moja kubwa, lilionekana kama jumba la kifalme ambalo kwa nje lilikuwa na sanamu kubwa la kutisha, la mtu mwenye kichwa cha paka chenye mapembe, manyoya, kwato za ng’ombe na kifua cha binadamu kilichokuwa na ufaufa kama ukuta.

    Wakatingia ndani. Idadi ya watu wengi ilikuwepo ndani ya jumba hilo tena wote wakiwa wanasujudu kama kutoa heshima kwa jitu la kutisha lililokuwa mbele kabisa, kwenye kiti kikubwa kilichokuwa na alama nyingi za kutisha, hapohapo naye Yusnath akainamisha kichwa kama ishara ya kusujudu, naye Edmund akafanya hivyo.

    “Karibuni sana, leo ni siku ya kutoa majukumu kwa kila mtu,” ilisikika sauti ya kiumbe huyo wa ajabu.

    Haikuwa sauti ya kawaida, ilikuwa sauti nzito na yenye kutisha ambayo ilijaa utetemeshi mzito uliyoyafanya masikio ya Edmund kuanza kuuma. Kiumbe huyo wa ajabu, alikuwa akizungumza huku akiwa kitini, mkononi mwake alikuwa na glasi iliyokuwa imejazwa damu, kila alipokuwa akiinywa, alipata nguvu zaidi ya kuzungumza. Edmund alikuwa amefikishwa kuzimu, na kile kiumbe kilichokuwa kikisujudiwa, alikuwa shetani mwenyewe.



    Moyo wa Filbert ulikuwa ukitetemeka, hakuamini kama katika maisha yake yote angeweza kukutana na msichana aliyekuwa mzuri kupindukia, msichana aliyeonekana kuwa kama malaika, mwenye umbo la kimisi, sura nyembamba huku tabasamu lake likimfanya kumpendezesha zaidi.

    Kwa jina aliitwa Stacie, alikuwa msichana mwenye mchanganyiko wa sehemu mbili, baba yake alikuwa Mmexico huku mama yake akiwa Mmarekani mweusi. Alimvutia kila mtu aliyemwangalia, urembo wake ukamfanya kwa marafiki na wacheza muvi wengi nchini Marekani kitu kilichomfanya kuitwa na kushiriki filamu nyingi ikiwepo Dear Samantha iliyoigizwa nchini Italia.

    Jina lake lilikuwa kubwa, urembo wake ulimdatisha kila mtu. Alijitambua, alijua kwamba ni msichana mrembo hivyo alitaka kujinufaisha kupitia urembo wake.

    Maisha yake yalitawaliwa na mapenzi, alikuwa na mahusiano na watu wengi wakiwepo mastaa wa kikapu, wacheza filamu na hata wanamuziki. Katika kila kitu alichokuwa akikifanya, alikifanya kwa kuwa kuna mengi alikuwa akiyataka.

    Umaarufu wake ukaongezeka na hivyo kupewa michongo mingi ya kuingiza fedha kitu kilichomfanya kuzidi kujirimbikizia mali nchini Mexico.

    Baada ya kuwa na mahusiano na watu wengi na kuachana nao, leo hii alikuwa ameangukia mikononi mwa Filbert. Kwa kumwangalia, alionekana kuwa mwanaume mzuri tofauti na wengine, mwanaume ambaye alikuwa na uhakika kwamba angeweza kuwa naye na hatimae kufunga ndoa.

    Aliwahi kuwa na mastaa, huko alipenda kwa kuwa alihitaji vitu fulani, baada ya kuvipata, leo hii aliamua kuwa na Filbert huku akiwa na lengo la kuwa naye mpaka watakapofunga ndoa.

    Kichwa chake hakikutulia, kila wakati alikuwa akimwangalia Filbert, alionekana kuwa mwanaume makini aliyekuwa akijielewa mno, kila alipojitahidi kutengeneza naye ukaribu, Filbert alikuwa akimkwepakwepa.

    “Pleaseeee, I want to talk to you!” (Tafadhali, ninataka kuzungumza nawe!) alijisemea Stacie huku akimwangalia Filbert.

    Siku hiyo alijitahidi kufanya kila linalowezekana ili apate muda wa kuzungumza na Filbert lakini ilishindikana kabisa. Moyo wake ulikufa ganzi, kila alipokuwa akimfikiria Filbert alijisikia kuwa na uhitaji mkubwa wa kuwa na mwanaume huyo.

    Usiku hakulala vizuri, mawazo juu ya Filbert yaliutesa moyo wake, japokuwa alikuwa na namba yake ya simu lakini alihofia kumpigia kwani hakuwahi kuzungumza naye hata mara moja.

    Hali hiyo haikumpata yeye tu, bali hata Filbert alikuwa hivyohivyo. Wawili hao walikuwa wakipendana lakini hakukuwa na yeyote aliyetaka kumwambia mwenzake. Filbert alibaki na mawazo, alikuwa na fedha, umaarufu lakini kumwambia ukweli Stacie alikuwa akihofia mno.

    “Mama,” alimuita mama yake.

    “Abeee.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kuna kitu nataka unishauri.”

    “Kitu gani?”

    “Kuna msichana ninampenda mno, lakini ninahofia, kuoa wanawake wa Kimarekani kunaweza kunigharimu sana, unadhani nifanye nini?” aliuliza Filbert.

    “Kuna mwanamke umempenda?”

    “Ndiyo mama.”

    “Mwanamke yupi?”

    “Anaitwa Stacie.”

    “Yule muigizaji na mwanamitindo?”

    “Ndiye huyohuyo.”

    “Mmmh!”

    “Nini tena?”

    “Si ndiye yule aliyetembea na wanaume lukuki?”

    “Mama, mbona umekimbilia kuuliza hivyo? Kwa nini usingeuliza ndiye yule anayeigiza muvi nzuri?” aliuliza Filbert.

    “Ndiye huyo?”

    “Yaaap!”

    “Mmmh!”

    “Mama, naomba unishauri kwanza.”

    “Unataka nikushauri nini tena?”

    “Ninaataka kuwa naye, unaonaje?”

    “Sidhani kama ni wazo zuri. Yule mwanamke hajatulia hata kidogo, achana naye,” alisema bi Imelda.

    “Mama, tupo Marekani hapa, tumefuata fedha, hii ni fedha, amini hilo,” alisema Filbert.

    Huo ndiyo mpango aliokuwa nao, ukiachana na mapenzi, kitu pekee alichokuwa akikihitaji ni kuandikwa sana na magazeti pia kutangazwa na vyombo mbalimbali vya habari kwa kuamini kwamba jina lake lingekua kwa kasi sana.

    Hakutaka kuchelewa, alichokifanya ni kumkubalia Stacie kuonana naye katika Mghahawa wa McDonald na huko ndipo mapenzi baina yao yalipoanzia.

    Walipendana na kuheshimiana, mara ya kwanza walifumwa na waandishi wa habari wakiingia katika Hoteli ya Bavarian iliyokuwa katikati mwa Jiji la New York, taarifa hiyo ikatolewa na wao kupinga kwamba hawakuwa wakitoka kimapenzi.

    Huo ndiyo ulikuwa mpango mzima wa biashara, hawakutaka kukubali kwa kuamini kwamba kwa jinsi walivyokuwa wamekataa, basi waandishi wangeendelea kuwafuatilia zaidi kutaka kufahamu ukweli, hivyo ndivyo ilivyokuwa.

    Hicho ndicho kilichofanyika, baada ya wiki kadhaa tena kwa kufuatiliwa sana, wawili hao wakabambwa wakibusiana mghahawani, mapaparazi hawakuwa mbali, walichokifanya ni kuwapiga picha na kisha kuziweka katika magazeti yao, siri kama ilikuwa imevuja.

    “Hivi ndivyo ninavyotaka, hapa ni kupiga hela tu. Kwanza mwezi huu ngoja nirudi Tanzania, naamini wamenimisi sana, nisipotee sana kwa Wazungu,” alisema Filbert bila kujua kwamba tayari Edmund alikuwa ameweka mikakati kabambe ya kumtoa roho.

    ****

    Kati ya marafiki wote ambao alikuwa nao, rafiki yake wa karibu kabisa alikuwa Thomson Petersen. Huyu alikuwa tajiri mkubwa nchini Marekani ambaye alikuwa akijishughulisha na uuzaji mkubwa wa meli za kifahari, ndege na biashara nyingine nyingi.

    Mbali na biashara hizo, pia bwana Thomson alikuwa mmiliki wa mitandao mbalimbali na televisheni ambazo zilikuwa zikitazamwa sana nchini Marekani. Katika maisha yake, bwana Thomson alikuwa akiogelea fedha, hakuwahi kufilisika hata siku moja, fedha zake hazikupungua hata mara moja, kila siku aliendelea kutengeneza fedha kadiri alivyotaka.

    Japokuwa alikuwa tajiri lakini bwana Thomson alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakimuabudu shetani. Kazi yake kubwa kwa kipindi hicho ilikuwa ni kuwalaghai watu wengi kujiingiza katika dini ya kumtumikia shetani kwa kisingizio cha kupata utajiri kama aliokuwa nao.

    Kupitia fedha alizokuwa nazo, watu wengi wakajikuta wakiingia mkenge na kuungana naye katika dini hiyo ya kumtumikia shetani. Ingawa baadhi walikuwa wakipata utajiri mkubwa lakini wengi wao walikuwa wakifa kwa kutolewa kafara kwa sababu damu zao zilionekana kuwa nzuri zaidi.

    Kupitia bwana Thomson, waigizaji wengi wakaingia katika dini hiyo, wanasiasa na watu wengine maarufu wakajikuta wakiingia katika dini hiyo maarufu ya kumtumikia shetani. Ilikuwa ni vigumu mno kukutana na mtu maarufu nchini Marekani ambaye hakuwa ndani ya dini hiyo ya kumtumikia shetani.

    Kwa mtu yeyote ambaye alikuwa akichipukia, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kushawishiwa ili ajiunge na dini hiyo ambayo kila siku ilizidi kushika kasi na kupata wafuasi wengi zaidi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bwana Thomson alikuwa mzizi mkubwa, yeye ndiye aliyekuwa kiunganishi cha watu hao katika dini hiyo.

    Mtu pekee ambaye alikuwa akimtaka kwa kipindi hicho alikuwa Filbert. Alijua kwamba alikuwa muigizaji mkubwa ambaye kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo alivyozidi kupata jina zaidi.

    Alikuwa mtu muhimu ambaye angewafanya hata watu wengine kuingia katika dini hiyo kitu ambacho kingekuwa sifa nzuri zaidi kwake. Kwa sababu alimtaka sana mtu huyo, alichokifanya ni kuanza kutengeneza ukaribu naye.

    Urafiki ukawa urafiki, mara kwa mara walikuwa wakitoka, wakitumbua maisha pamoja na mwisho wa siku kushirikiana katika mambo yao mengi. Bwana Thomson ndiye alikuwa mshawishi mkubwa kwa Filbert kumkubalia Stacie na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi.

    “Utakwenda kuwa tajiri mkubwa, umaarufu wako utaongezeka na kukua kwa kasi,” alisema bwana Thomso.

    “Natakiwa kufanya nini? Au nijitume zaidi?”

    “Hapana, unaweza kujituma na kazi ikawa sawa na ziro, kuna la msingi ambalo unatakiwa kulifanya, ukiwa tayari, nicheki simuni,” alisema bwana Thomson.

    “Kwa nini usiniambie sasa hivi?”

    “Ni habari ndefu sana.”

    “Lakini mwezi ujayo nataka kuondoka kwenda Tanzania.”

    “Kwani hautorudi?”

    “Nitarudi.”

    “Basi sawa, ukirudi tutaongea tu.”

    “Daaah! Lakini ungeniambia sasa hivi tu, umekuwa rafiki yangu mkubwa, napenda kupokea ushauri mbalimbali, niambie Thomson, ninataka kusonga mbele zaidi ya hapa,” alisema Filbert.

    “Usijali, nitakwambia.”

    Siku hiyo bwana Thomson hakutaka kumwambia kitu chochote kile, alikuwa kimya huku kila siku akimwambia kwamba kuna siku angeweza kumwambia.

    Moyo wa Filbert ulikuwa kwenye mawazo tele, kila wakati alikuwa akifikiria ni mbinu gani ambazo bwana Thomson alitaka kumpa ili kufanikiwa zaidi.

    Kila siku katika maisha yake alitaka kuwa juu, hakutaka kabisa kuona mwaka ujao akiwa pale alipokuwa katika mwaka huo, kiu yake ya mafanikio aliyokuwa nayo ilikuwa kubwa mno, hakutaka kurudi kule alipokuwa kipindi cha nyuma, alitaka kuwa zaidi ya pale alipotaka kuwa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog