Simulizi : Sara (Msaada Wa Mateso)
Sehemu Ya Pili (2)
Siku hiyo jioni mzee Junior alikaa na mwanaye Sara wakiongea mambo yao ndani.Ni yeye ndiyo aliyejibadilisha na kuonekana na sura ya mwanamama na kuingia ofisini kwa mwalimu mkuu akionekana kuongozana na binti aliyetambulika kwa jina la Sasha.
"Unatakiwa kuwa makini Sara safari hii,usioneshe sura ya Sara shuleni tena,wewe ni Sasha na utakuwa hivyo siku zote wapo shuleni,fanya ulivyoambiwa na mama yako."alisema mzee Junior akiwa ameshika kisu na chungwa akimenya kuonesha kidogo hali yake inaimarika.
"Lakini baba...bado mnanificha hapa Kati,sielewi ilikuwaje hadi watu hawa wanawataka baadhi ya wanafunzi shuleni pale na sio watu wengine huku kijijini?mwalimu Eddy wamemchukua na hadi sasa sielewi alipo"alisema Sara na kumfanya mzee wake amtazame,Sara alionekana kuna mambo naye hayafahamu yeye anafuata kile anavyoaguzwa na marehemu mama yake ambaye huwasiliana naye kwa siku moja moja.
"Sara mwanagu,elewa tu una kisasi cha kulipia kuhusu mama yako,viumbe hawa ndio waliomuuwa mama yako miaka 13 iliyopita baada ya kufahamu mama yako ana uwezo mkubwa wa miujiza kushindwa wao,alitamani kuwa nawe siku zote akuonyeshe jinsi walimwengu wanavyoishi lakini haikuwa hivyo ,waliyakatisha maisha ya mama yako na kutaka kuzichuma zile nguvu wawe nazo wao."alise mzee Junior na kukata chungwa lile vipande viwili akampa kimoja mwanaye.
"Inamaana walikuwa wanamjuwa vema na mama yangu?"
"ndio,na walikuwa naye siku zote kwenye kazi za kawaida,ipo siku utajua ulipozaliwa,utajua kwanini hawa wanawataka wale watu,ila tambua kuwa wewe hukuzaliwa dunia hii ndio maana upo tofauti na wengine."alisema mzee Junior.
"kwani nimezaliwa wapi mimi?"aliuliza Sara akionekana kuna mambo hayajui.Mzee Junior alibaki kumtazama mwanaye huku akitabasamu tu.
"muda ikifika nitakuambia,nenda kapumzike kesho uwazi shule mwanangu...usiku mwema."alisema mzee Junior na kuingia zake chumbani kwake jkupumzika,hata alipofika chumbani alikaa tu kitandani akiyakumbuka mambo ya nyuma hasa kifo cha mkewe kipenzi aliuemuachia mtoto Sara kipindi hicho akiwa mdogo .Usiku ule Sara alibaki akitafakari mambo mengi ambayo hakuweza kuyapatia majibu papo hapo,naye akanyanyuka kuingia chumbani kwake kujipumzisha.
Upande wa pili kuna sauti za watu wawili akisikika wakiongea mambo yao.
"..ndio itakuwa safi maana akianza yeye itamfanya Sara azidi kuwa matatizoni mbele ya watu"ilisikika sauti ya kiume ikisema .
"usijali baba na ndio nishapanga uwe hivyo,Sara alikuwa yupo naye muda mwingi sana lakini kwakuwa ameshaondoka pale shuleni nitalikamilisha hili,Ester lazima tumchukue naye kesho"ilikuwa ni sauti ya Michael akiwa anaongea na baba yake wakiwa ndani ya nyumba,waliendeleawkupanga mambo yao baada ya kujua Sara hayupo tena pale shuleni huku mtu wa kwanza kulengwa alikuwa ni Ester.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi kulipokucha wanafunzi baada ya kumaliza usafiri wa maeneo ya shule na baadae wanafunzi waliingia madarasani.Ester alionekana akitoka ofisini kwa mwalimu mkuu akiwa na bibi yake ambaye alipata kusikia habari ile iliyomtokea mjukuu yake,mwalimu mkuu alimueleza yote na kimwambia kuhusu uamuzi ule aliouchukua,bibi yule alimuomba sana mwalimu juu ya mjukuu wake aweze kurudi shule siku hiyo na kutaka ile wiki isifike,mkuu alifikiria swala hilo baada ya moyo wa ubinadamu na huruma ya bibi yule aliifuta ile akili yake ya awali na kumruhusu Ester arudi tena darasani jambo lililomfurahisha bibi yake ambaye alibaki akimshukuru mkuu na baadaye akaondoka zake.SIKU hiyo Sasha aliweza kuwasili na kuelekea moja kwa moja mwalimu mkuu ambaye alimpokea na kumuita Ester ofisini na muda mchache tu aliwasili.
"Ester haya mwenzenu huyo mtakuwa naye darasani,anaitwa Sasha mumpe ushirikiano wenu...."alisema mwalimu mkuu na Ester akaitikia huku akielezwa ampitishe kwenye ubao ule wa kuzisoma na kuzijua sheria za shuleni pale,baada ya hapo walielekea darasani ambapo kama ulivyo kawaida kwa mwanafunzi mgeni wa kike lazima baadhi ya wavulana wamshadadie,Ester alimchukua Sasha na kumuandalia kiti pale pale alipokuwa anataka Sara zamani.
"Ah Hilali naona unapendelewa wewe tu alikuja Sara kaondoka hata siku mbili hazijaisha umeletewa chombo kingine. ..kazi kwako nyima ya chipsi"alisema Magreth na kumfanya darasa zima liangue kicheko,hata Ester mwenyewe ikambidi afurrahi maana darasa lake haliishi vitimbi.
Kama ilivyo kawaida kwa mwanafunzi mgeni darasani anapaswa kujitambulisha darasa limjuwe...Sasha alisimama na kuanza kujitambulisha kwa jina la Sasha Dominick huku akiona ushirikiano na wenzake,walikaribisha kwa kumpigia makofi kisha akarudi zake kukaa.Alibaki ametulia tu akiangalia angalia baadhi ya wanafunzi wa darasa lile,muda mwingi alikuwa akitazama tu darasa hali iliyomfanya Ester aliyekuwa anajisomea kubaki kumuangalia tu Sasha.
"mh mbona haonekani kama amekuja kusoma,anaonekana zuzu zuzu hata kuishika daftari!"alijisemea Ester moyoni akizidi kumtazama yule mwanafunzi na kuendelea kujitolea.Muda uliyotuma na vipindi vya asubuhi viliisha na wanafunzi wakaelekea kunywa chai,Ester alielekea kupumzika sehemu ambayo alipendelea sana kukaa na Sara wakiongea mambo yao,moyoni alikuwa amejawa na uwoga tangu kuondoka kwa Sara na kujua mambo yale ya nguvu za Giza yanaweza kutokea kwake muda wowote hasa akiikumbuka sauti ya Natasha siku ile alipoingia na jini ambaye aliwataja watu wote wanaotakiwa kuuawa na mtu wa kwanza tayari ni mwalimu Eddy,hata yeye naye alikoswakoswa baada ya kupata uchizi ule na kubaki kuishika rozali yake,akiwa akiyakumbuka hayo ndipo akili zikamjia siku ile alimfuata Magreth kule nyuma na kumkuta akilia huku mkononi akiwa ameshika karatasi fulani,na baada ya kupewa karatasi ile asome alianza kuona mabadiliko na ndio hapo hakujua kilichotokea,haraka akanyanyuka na kuanza kukimbia kumtafuta Magreth popote alipo.Wakati wote tu akiwa anafanya hayo Sasha alikuwa sehemu anamuangalia tu huku akionesha huruma usoni mwake,alishusha pumzi Sasha na kufumba macho,akakumbuka maneno kadhaa ya nyuma ambayo alipata kuambiwa." "Unatakiwa kuwa makini Sara safari hii,usioneshe sura ya Sara shuleni tena,wewe ni Sasha na utakuwa hivyo siku zote wapo shuleni,fanya ulivyoambiwa na mama yako"yalikuwa ni maneno ya baba yake akimuuliza sana asijioneshe tena kwa watu,alibaki akimtazama tu Ester akielekea sehemu anayopendelea kukaa Magreth lakini alipitazama pembeni alimuona Michael akimtazama Ester kwa macho ya uchu na muda ule ule Michael akapotea gafla,Sasha alipotazama na kuona vile akajua kuna jambo baya linaenda kutokea,akanyanyuka ila akikumbuka maneno ya baba yake akawa anasita kufanya lolote huku akizidi kumuangalia Ester akienda kwa Magreth.
Moyo wake ukawa mzito Sasha akanyanyuka pale alipo na kuanza kutembea haraka kuelekea kule anapoenda Ester kule kwa Magreth,Ester mwenyewe alimuona Mage akiwa amekaa na rafiki zake wakipiga soga lakini cha ajabu Ester akajikuta anapita pale alipo Mage na kuanza kukamata njia ya kuelekea nje ya shule ambako kuna mashamba ya watu na mapori.Sasha alishangaa kumuona Ester akielekea kule ambako hakuna mwanafunzi yeyote aliyeonekana kumshangaa walijua kuna anapoenda tu,Sasha akawa nyuma tu anafuata tena kwa kuongoza spidi.Alizidi kuingia tu ndani kwenye pori ambapo mbele kulikuwa na mti mkubwa wa mbuyu ndipo Ester akakomea hapo na kubaki kuangalia tu huku na kule.
"Umepotelea wapi Mage...rudi nikuulize mara moja...!"alisema Ester na kumfanya Sasha aliyekuwa anamkaribia kumshangaa,alipotazama pembeni aliona dege kubwa lenye makucha marefu likitoka juu ya mti mmoja na kuelekea alipo Ester,haraka Sasha akaanza kukimbia kwa kasi kumfuata Ester ambaye hakuwa anajua lolote,na alipomfikia akamsukuma pembeni Ester yule ndege
kwa kasi alipita na kumkwaruza Sasha mkononi na kumfanya augumie,yule ndege alipiga ukelele wa hasira na kutokomea zake lengo likiwa ni kumzuru kabisa Ester macho yake aweze kupata urahisi wa kuendelea kumkwaruza sehemu nyengine.
Ester alishangaa kuona yule ndege anaondoka zake,akageuka kumtazama Sasha aliyeonekana kujeruhiwa vibaya mkononi.
"Eh jamani polee..!"alisema Ester kwa upole na kutoa kitambaa chake kwenye sketi cha kufutia jasho na kuanza kumfuta Sasha damu zilizokuwa zikitoka mkononi.
"usijali ndugu."alisema Sasha.
"Huyu ndege sijui ametumwa?alitaka kunidhuru mimi.!"alisema Ester.
"Na wewe umefuata nini huku porini unajitafutia matatizo?"alisema Sasha.
"kuna mwanafunzi mwenzetu anaitwa Magreth aliponiona namfuata akaanza kukimbilia huku nikaanza kumfuata,anajua kuna jambo alilifanya"alisema Ester akiendelea kumfuta futa damu Sasha.
"alikufanya nini?"aliuliza Sasha na kumfanya Ester amuangalie usoni kisha akatazama chini na kuendelea kumfunga kidonda.
"kuna tatizo lilitokea hapa shule juzi tu hapa kabla ya wewe kufika hapa "alisema Ester na kuanza kusimulia yote yale ya nyuma yaliyotokea akiwa na rafiki yake Sara ambaye kwa sasa anajua amefukuzwa.
Alimueleza mambo mengi sana hata kuhusu uwezo alionao Sara kipindi kile japo amekaa naye kwa muda mchache tu na kuona umuhimu wake.
"nilimchukulia kama ndugu yangu maana amekuwa msaada kwangu juu ya mambo haya yanayoendelea kuniandama,ameondoka ila naamini mwalimu mkuu atamsamehe na kumrudisha shuleni."alisema Ester kwa hisia kuonesha jinsi gani anavyompenda Sara.
Sasha alibaki kumuangalia tu Ester akimfunga ile sehemu aliyojeruhiwa na yule ndege,aliona jinsi gani Ester alivyokuwa na upendo kwa watu,alitamani kumwambia ukweli Ester kuwa yeye ndiyo Sara mwenyewe lakini hakutaka kusema lolote ili aweze kuikamilisha kazi yake,alibaki kutabasamu tu baada ya kuona kumbe Ester bado anamjali na alimpokea kama ndugu zaidi ya rafiki kwa kuujuwa umuhimu wake.Walimaliza kufunga lile jeraha na kanyanyuka huku Ester akimfuta vumbi kwenye nguo za Sara ambaye kwa sasa anajulikana kama Sasha na baadaye wakaanza safari ya kurudi darasani.
Ester alipokaa kwenye sehemu yake aligeuka kumtazama Magreth ambaye hakuonesha hali yeyote ya wasiwasi kiasi cha kumfanya Ester ageuke kuendelea na mambo yake akipanga baadae amfuate Mage apate kumuuliza mambo kadhaa.Alimtazama Sasha na kuona vile alivyoumia ni kwaajili yake,akamkumbuka Sara ndiyo alikuwa msaada wake kwenye matukio yale,hapo ndipo akaanza kujiuliza sasa Sasha amejuaje kama anaenda kule maporini?hadi yule ndege mkali anataka kumdhuru Ester ina maana Sasha alikuwa anaona au?...ni maswali madogo lakini kichwani kwake yalianza kumuogopesha kiasi fulani,hata yule ndege alianza kumuogopa baada ya kuhisi huenda alikuwa ana nia ya kumuua na kuona bila ya Sasha sijui angekuwa wapi kwa sasa,akabaki kumtazama tu Sasha aliyeonekana kujiangalia sehemu aliyojeruhiwa.
Huku kwa Michael alionekana amekaa darasani amenuna sana,alikuwa akitafakari jinsi alivyofeli tena kwa mara nyengine,alikuwa akijiuliza kuhusu yule msichana aliyemsaidia Ester kule porini,alifumba macho na kuanza kurudisha nyuma kumbukumbu zake aone kama kuna mtu alikuwa amemuona pale alipopotea gafla,akaanza kuona eneo lile lote alipokaa muda ule akimtazama Ester akiwa anamfuata Magreth,kila anapotazama kwa pembeni kila upande haoni mtu aliyeona tukio lile,aliona vile alivyopotea kimaajabu na kujigeuza kuwa ni Magreth na kusimama karibu na mti ambapo Ester alipofika pale alipokaa Magreth na wenzake alimuona Mage akimtazama na kusimama kuanza kuondoka kuelekea kwenye ule mti hali ya kuwa Magreth alikuwa palepale amekaa na wenzake wanapiga stori,ujanja huo wa kutumia uchawi ulimchanganya Ester na akawa anamfuata tu Michael ambaye alijibadilisha kuwa ni Magreth na hakuna mtu yoyote aliyemuona Magreth huyo wa uongo ndio maana Ester akawa anaenda tu mwenyewe kule porini yeye akiona anamfuata Magreth kumbe alizugwa tu na Michael alipofika ndani zaidi ya lile pori akapotea na kujibadilisha kuwa ndege mwenye makucha na kukaa juu ya miti akimvuta Ester akae sehemu nzuri na aliposhuka kutaka kumpofua macho Ester akashanga kuona kuna mtu ametokea na kumsukuma pembeni Ester lakini aliambulia kumkwaruza mkononi...
Michael aliumiza sana kichwa kumtambua yule aliyemsaidia Ester baada ya kuwaona wakitoka kule porini na kuingia darasani,alinyanyuka pale alipokaa baada ya kukumbuka mambo hayo pale darasani na kutoka kuelelea kidato cha 3 ambako ndiko anasoma Ester na Sasha pia..
Akiwa anakaribia kuufikia mlango wa kidato cha 3 kule ndani Sasha akahisi kitu,akageuka kumtazama Ester akionekana kujisomea,alinyanyuka na kumfuata Ester,akasogeza kiti na kukaa karibu yake jambo lililomfanya Ester atabasamu,wakavuta daftari la somo la History na wakaanza kupitia mambo fulani kwenye baadhi ya Topic.
Michael muda ule akaingia mule darasani na kuanza kutembea kuelekea kwa Magreth kwa mara nyingine jambo ambalo Ester alipata kuliona na kubaki kumtazama Michael aliyeonekana kama mshamba fulani hivi akimsogelea Mage ambaye alionesha tu tabasamu.Ester pale alipo alijihisi kumropokea yule Michael alitamani kumfukuza lakini akaona itakuwa jambo lengine maana mwanzo alipomfukuza wanafunzi waliongea kumtetea Michael.
Sasha muda wote alikuwa akiangalia tu tukio lile na kumuona Ester alivyobadika gafla kuonesha kununa.Kwa Michael nayeye alikuwa akiongea mambo na Magreth ambaye alianza kumzoea Michael gafla tu na kujikuta anamuamini,Michael alikuwa akiibia kumtazama Sasha kila muda lengo likiwa ni kumjuwa kwa kuangalia mwili wake mzima,wenyewe wanajuana wakionana na mtu mwenye nguvu za kichawi lazima kuna hisia fulani azisikie lakini kwa Sasha haikuwa rahisi,Michael alikuwa akimtazama tu Sasha baada ya kujiridhisha ninkiumbe wa kawaida tu na kubaki kujiulizia maswali kama yale aliyokuwa amejiuliza Ester muda ule kuwa kabla ya lile tukio la Ester kuuawa na yule dege ambaye ni Michael,Sasha amejuaje kama itatokea hivyo?:alijiuliza maswali kadhaa bila kupata jibu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya muda kidogo tu Michael akaanza kuondoka kutoka nje kisha sekunde kadhaa akafuata Magreth naye akatoka kumfuata Michael jambo ambalo lilimfanya Ester akumbuke mara ya kwanza alipoona Magreth akitoka na Michael na ndio ile siku alipo geek kuwa chizi,japo aliyakumbuka lakini moyo wa imani ulimjaa Ester na kuona huenda Magreth leo ndio ikawa ile siku yake yake ya kufa,akatamani anyanyuke amfuate lakini alishangaa mkono wa Sasha ukimkamata.
"Hii Topic ya SRAMBLE FOR AND PARTITION sijaisomaga vizuri ujei,hebu utilities kidogo nipate aidia kidogo"alisema Sasha akionesha kutaka kuelekea,Ester akageuka na kumuangalia Sasha akionesha kutaka kweli kufundishwa lakini moyo wa Ester ushahama kimasomo pale baada ya kuhisi hatari ua ukapoteza mmoja wa wanafunzi ambao walishatajwa kufa mwanzo,alijuwa Sasha ni mgeni na hawezi kuelewa mambo mengine yanayoendelea mocha ya kumueleza baadhi hasa kuhusu habari za Sara,hakutaka kumwambia Sasha kuhusu tukio lile la Magreth na Michael kutoka nje kunaweza kuleta matatizo hivyo alitaka kwenda mwenyewe bila mwengine kujua.
"Sasha ngoja niende uwani mara moja nikirudi tunaendelea"alisema Ester na kunyanyuka zake.
"Ah na mimi mkojo umenibana kweli, twende tuongozane."alisema Sasha na kunyanyuka kuanza kuongoza njia na kumfanya Ester anti same tu,hakuwa na jinsi ikambidi aongozane naye kuelekea chooni lakini hakutaka kwenda chooni ilikuwa ni kama zuga tu amkimbie Sasha kule darasani lengo likiwa ni kuwafuatilia wakina Michael na Magreth. Waliookamata njia ya kuelekea uwani walipata kushuhudia Magreth akiwa amekaa nyuma ya darasa na Michael wakiongea mambo yao.
"Yule mkaka simpendi yule we acha tu!"aliropoka Ester wakielekea chooni na Sasha.
"he kwanini?"aliuliza Sasha bila kupata jibu la haraka wakaingia chooni,na baada ya kumaliza haja zao akatoka kuelekea darasani,alipotazama walipokaa wakina Magreth hawapo,Ester kashtuka kidogo na kuanza kupiga mwendo wa haraka kuelekea darasani huku Sasha alibaki kumuangalia tu baada ya kusimama.
Ester alipofika mule darasani akaanza kumtafuta Magreth leak ni hakuweza kumuona,akajua kuna jambo baya kitakuwa limemtokea Mage,akatoka haraka kwenda kumueleza tu ukweli Sasha.
"Sasha...Sasha....Mage atakuwa matatizoni nahofia sana,yule mvulana aliyeongozana naye sio mwema...anaitwa Michael ni mc....."hajamalizia sentensi yake akajikuta amefumbwa mdomo na Sasha asiongee tena.
"Ester...una moyo wa huruma kuwasaidia wenzio... lakini usijiingize matatizoni rafiki yangu,utakufa mapema kabla yya siku zako...nakuomba tena sana jali maisha yako niangalie mwenyewe Ester.."alisema Sasha maneno yale na kumuachia Ester kisha akaondoka zake kwenda darasani.
Ester akabaki ameduwaa baada ya kuambiwa maneno yale ambayo kwa upande mwengine aliyeona ni ya maana sana na kujiona anataka kuwasaidia wenzake hali ya kuwa nayeye anahitaji msaada juu ya jambo hili,maneno yale yakamfanya ageuke alipoelekea Sasha baada ya kuona maneno yale aliyoongea ni mazito na yana maana kwake.
"Mbona anaongea kana kwamba anayajua haya mambo!anaonesha kunijali na mwenye upendo kama wa Sara....hakika huyu ni rafiki yangu wa dhati baada ya Sara,alisema Ester na kuanza kurudi zake darasani baada ya kuouuzia mambo yale kuhusu Magreth,aliamua tu liwalo na liwe maana hana nguvu za kumpindua Michael hasa akifikiria na yeye muda mchache tu alikoswa koswa kuuliwa na dege kule porini na kuokolewa na Sasha,akaanza kumuamini Sasha na kuona amepata rafiki wa kuelezana matatizo yao.
Wakati mambo yote yanaendelea Michael alikuwa amekaa sehemu akiwaangalia tu anavyofanya,lengo lake lilikuwa ni kumjuwa huyu Sasha kiundani zaidi baada ya kumuhisi lakini alijikuta akigonga mwamba,Sasha akionesha dalili zozote za yeye kuwa na nguvu za ajabu kama za Michael,aliona anayehaha kuangaika muda wote no Ester ambaye no mmoja wa watu wanaohitajika kuuliwa,yote ya kumtoka darasani Mage kwenda naye nyuma ya darasa kuongea ilikuwa ni Janna tu ili ajuwe kama Sasha a naweza kufanya kitu cha tofauti lakini alimuona hana hata habari.
Akajiridhisha kwa kuona Sasha aliyekuwa akimuhisi hana lolote linaloweza kumzuia yeye kutekeleza mambo yake hivyo lile la kule porini ilikuwa bahati tu kumuokoa Ester,akapanga kufanya jambo lengine tena kwa Ester maana yeye ndiye mtu anayefuata kufa baada ya marehemu mwalimu Eddy na ndio maana muda wote hawafuati wakina Natasha,Magreth na monitor wa darasa Denis,alinyanyuka pale alipokaa na kuanza kuelekea darasani kwake Michael.
Akiwa amekaa sehemu yake Sasha alibaki akitabasamu tu baada ya kujua kuwa haya yote anayafanya Michael lengo ni kutakabkumjuwa Sasha kwa ndani zaidi baada ya kuanza kumhisi na kuamua kufanya jambo ili kumuona kama Sasha atafanya lolote,lakini Sasha alishayajua haya na kufahamu njema zote anazotumia Michael ni za kichawi ili asijulikane,alikuwa anacheza na hisia za Ester tu mule darasani ndio maana muda ule alipoingia darasani na kwenda kwa Magreth kuanza kuongea naye na baada ya muda alionekana kuondoka kisha Mage akafuata,kumbe haikuwa hivyo alimzuga tu Ester,vile vilikuwa ni vivuli tu vya Mage na Michael wakionekana ni watu wakitoa nje na Ester alijua ni watu halisi ndio maana hata pale Mara ya kwanza alivutwa kwa namna hii kumbe Magreth alikuwa yupo palepale darasani mwenyewe hana hata habari na tukio lile la mwanzo Sara hakuwepo darasani alikuja kushtuka Ester kashaingia matatizoni.Lakini kwa tukio hili la pili Ester alipotaka kunyanyuka kuwafuata nje alishangaa kuona Sasha amemshika mkono akitaka wasome,kumbe alishajua kuwa wale waliotoka sio watu ni vivuli tu na wenyewe walikuwa palepale wakiendelea kupiga soga,yote ilikuwa ni janja ya Michael ambayo Sasha alipata kuijua mapema na kubaki akitabasamu tu pale darasani.
Baada ya muda kidogo aliingia darasani akitokea zake chooni mara moja hali iliyomfanya Ester abaki kumuangalia tu usoni baada ya kufahamu huenda Magreth alikuwa kwenye matatizo.
"Mage upo sawa?"aliuliza Ester baada ya Mage kupita pembeni yake.
"ndio...kwani vipi?"alisema Mage akionesha hana analojua.
"Ah hapana...nakuona kama haupo sawa ndio maana"
"mh na we mama mchungaji una visa kweli...au unataka uniombee!"alitania Mage huku akielekea zake kukaa kumuacha Ester akitabasamu tu baada ya kujua hakuna kibaya chochote kilichomkuta Mage kwa Michael.
BASI masaa yalizidi kwenda na mchana ulipofika muda wa kuondoka wanafunzi waliruhusiwa kurudi zao makwao.Ester aliongozana na Sasha njiani wakiongea mambo yao hasa kuhusu taaluma,hata walipokafika kijijini waliagana na kila mtu akakamata njia yake kuelekea kwao,Sasha alipofika kwao alisalimiana na baba yake kisha akaingia chumbani kwake ambapo aliweka begi mezani na yeye akakaa kitandani na kuanza kutoa viatu na nguo za shule huku akibaki na nguo ya ndani tu,alinyanyuka na kusogea hadi kwenye kioo kikubwa kilichowekwa ukutani akajiangalia Sasha huku akitabasamu kujiona,akainama chini na kuchutama huku akiangalia chini na kuanza kunena maneno ya lugha fulani ambayo haikuweza kufahamika na baada ya sekunde kadhaa akanyanyuka na kujitazama tena kwenye kioo,alirudi kuwa Sara mwenyewe na sio Sasha tena,akajishika tu sura yake huku akionekana kutafaki mambo fulani yanayomkabili,kuna wakati anatamani amueleze Ester kuwa yeye ni nani maana ametokea kumuamini na kuwa zaidi ya rafiki,lakini akikumbuka mambo kadhaa aliyoelezwa na mama yake roho ile ya mazoea tena na watu inapotea taratibu,aliachana na hayo mambo na kugeuka kuchukua kanga yake kuelekea bafuni kuoga.
Jioni ya siku ile Ester akimkumbuka rafiki yake Sara na kuamua kuelekea kumuona,alipofika Sara alimpokea na kuigiza kwa tabasamu zito kana kwamba kweli hawakuona kwa siku kadhaa,waliingia chumbani na kuongea mambo yao.
"...ila nashukuru Head Master baada ya kuombwa na bibi alikubali na mimi asubuhi ile ile nkaingia darasani kuendelea na masomo."alisema Ester kumueleza Sara ambaye alifukuzwa shule pamoja na Ester ambaye yeye alipumzishwa wiki moja tu lakini alirudi na bibi yake kuomba msamaha.
"hongera umerudi shuleni kabla ya wiki yako kuisha,vipi lakini maendeleo ya shuleni"alisema Sara kana kwamba hakwenda kweli shuleni akitaka asijulikane kama yeye ndiyo Sasha.
"Ah tunaendelea hivyo hivyo leo tumepiga Maths,Kiswahili na Biology tu basi....halafu dah nlitaka kusahau....unajua bwana duniani kweli watu wanafanana sura na wengine tabia..aisee kuna mwanafunzi wa kike mgeni amekuja darasani anaitwa Sasha,ukimuona hivi utasema muongeaji mapepe flani hivi lakini ni mtu mmoja safi sana na mpaka nikakukumbuka wewe,yale matukio naona bado yanaendelea na leo kuna jambo la ajabu limetokea ndio maana nkamkumbuka huyo Sasha na kukufananisha naye"alisema Ester na kuanza kumueleza Sara yale yaliyotokea kule porini alipokuwa akimfuata Magreth hadi Sasha akamsaidia,alimueleza hata alipokuja Michael darasani muda ule na kuonekana akitoka huku Mage akimfuata nyuma.Sara baada ya kuambiwa vile hakutaka hata Ester ajue kuwa ni yeye ndiye aliyemsaidia kule porini asidhulike na yule ndege,alimshika mkono Ester na kumtazama usoni kwahisia ya huruma.
"Ester nakuomba sana kwa kipindi hiki ambacho sipo shuleni kuwa makini sana na Michael,zidi kumuomba Mungu akupe nguvu uweze kushinda mitihani inayokuandama...Mimi naamini utakuwa salama tu siku zote na kama huyo rafiki yako Sasha amekusaidia kwa siku ya leo basi kuwa naye muda wote ili usiwe mpweke.Hivi ulivyoniambia nimejua mambo mengi sana,huyo ndege unayesema wewe ni Michael yule alikuwa amedhamiria kukumaliza na umshukuru Mungu Sasha amekusaidia bila hivyo ungeitwa jina lengine la marehemu,swala la Sasha kukusaidia lilimkera sana Michael ndio maana akaja darasani alinifanya amekuja kwa Mage kumbe sio alikuja kumpima Sasha akimhisi huenda akawa ana nguvu za ajabu kama mimi au kama yeye Michael, na pale uliposema alipotokea darasani na Mage akafuata sio kweli,kilichotokea pale ni vivuli yao tu alijuwa kuwa kama Sasha atakuwa na nguvu zile lazima atoke ajue Mage anaelekea wapi na Michael,ndio maana hata wewe ulipoona vile ukijua Mage anaenda kuingia matatizoni kumbe sio,Mage alikuwa palepale kwake amekaa,usijifanye mtoa amani wakati wewe mwenyewe unaitafuta amani,usipende kuwa mwema muda wote vitu vingine unatakiwa kuwa makini,nlishakwambia mtu anayefuata kuuliwa ni wewe na kamwe hataanza Mage wala Natasha wala Denis..wewe ndio mtu wa pili baada ya Mwalimu Eddy hivyo Michael hata amchukuwe Mage wewe fanya mambo yako hawezi kumdhuru"alisema Sara na kumfanya sasa Ester aelewe hali halisi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Michael ninamchukia tokea siku ile ya kwanza uliyonambia,umri alionao ni tofauti na mambo anayofanya,na tumemkosea nini sisi hadi anatufanyia hivi,hata huruma hana kijana yule"alisema Ester akionesha kuumia kwa yale matukio,Sara alibaki kumtazama tu maana hata yeye hajui ni kwanini wakina Ester na wenzie wanatakiwa kuuawa kama alivyotangulia mwalimu Eddy,yeye alipewa kazi ya kuwatetea hawa wasidhurike lakini hadi sasa mwalimu Eddy ameshafariki.
Marafiki wale walibaki wameshikana mikono tu muda ule wakiendelea kutokana moyo kwa mambo hayo,muda uliyoyoma na baadae Ester akaaga kutaka kuondoka kurudi kwao,Sara alimsindikiza rafiki yake hadi mahala fulani kisha wakaagana na kila mtu akarudi kupumzika kwao usiku ule.
Siku zilizidi kuyoyoma huku Michael akizidi kumuandama Ester kila siku lakini akijaribu kumfanyia kitu Sasha anakuwa yupo karibu na Ester hali inayomfanya Michael azidi kufanikiwa kazi yake,siku hiyo aliamua amtie adabu Sasha kusudi akae mbali na Ester ili afanikiwe kumaliza Ester.Siku hiyo Sasha akitoka darasani kwao akielekea uwani,Michael alikuwa akimtazama tu anapoelekea.Sasha alitembea kuelekea uwani na alipotaka kuukaribia mlango wa choo alishangaa pale aliposimama anadidimia chini baada ya kutokea shimo kubwa lililomfukia kabisa kumpoteza Sasha baada ya kidumbukia.
Shimo lile lilimpeleka mbali Sana Sasha na kumtupa sehemu ambayo alipofika alipoteza fahamu.
"Sara...Sara mwanangu.."iliisikia kwa mbali sauti ile iliyomfanya Sara pale alipo aisikie japo hakuweza kunyanyuka
"Hapa ulipo sio sehemu ya kawaida...kuna viumbe vya ajabu na hupaswi kuvihofia...nimekupa uwezo wangu wote mwanangu ambao hakuna kiumbe chochote kwa hawa atakakaye kuzidi ila wanafanya ubishi tu...huku umeletwa ili wakutishe na wakuzuie usimfuatilie Ester,usiwaogope waeleze kuwa wewe ni nani na watakuogopa hawatakudhuru."sauti ile ilisikika masikioni mwa Sara akiwa pale chini ya lile shimo refu sana amezimia na ile sauti haikusikika tena.
Kelele za ajabu zikaanza kusikika zikimfanya Sara pale alipo chini afumbue macho taratibu baada ya fahamu kumrudia,akaanza kuona vivuli vinapita huku na kule vikizidi kumcheka sana hadi kelele zikazidi na kumfanya Sara akurupuke pale alipolala na kusimama ,akaanza kuangalia lile shimo lililokuwa na giza totoro,vivuli vilionekana mwanga na kupotea vilipita kumzunguka Sara mfululizo hadi mwenyewe akashangaa...
"Nyie ni akina nani na mnataka nini kwangu."aliuliza Sara kwa sauti huku akiwa kwenye umbile na sura ya Sasha.
Maneno yake hayakuwa na maana kwao hakujibiwa na kuzidi kusikia baadhi ya milio ya wanyama tofauti tofauti wa kutisha huku vicheko vikishika kasi.Sara alibaki kuziona masikio kwa kelele zile.
"Mbona hamjibu nyie ni nani,na nani kanileta huku?"alisema Sara.
"FUATA KULICHOKULETA SHULENI ACHANA NA ESTER....UMELETWA HAPA ILI UKANYWE UACHE URAFIKI NA ESTER KAA MBALI NAYE,LAA SIVYO UTAJUTAAAA"ilisikika sauti nzito yenye muungurumo ikisema na kumfanya Sara atafute inapotokea.
"yule ni rafiki yangu na nasomea naye darasa moja,siwezi kuwa nimemtenga..."alisema Sara.
"ACHA KUBISHA BINTII...UTAKUFA BURE KWA UJINGA WAKO..ACHANA NA ESTER MARA MOJA"
"amefanya nini kwani hadi niachane naye.?"aliuliza Sara akitaka kujua maana ni kweli hafahamu ni kwanini Ester na wenzake wanaandamwa hivyo.
"YULE NI DAMU YETU...NI MWENZETU NA HAPASWI KUWA BINADAMU KAMA NYIE,YEYE NA WENZAKE WANATAKIWA KURUDI WALIKOTOKA"
"kwani walikuwa wanaishi huku?"aliuliza Sara swali ambalo ilifanya ile sauti inyamaze na kuonekana viumbe vya ajabu kama wafu waliofufuka wakiwa na manguo yaliyochakaa huku wakitepeta damu.
"HAO NI BAADHI YA WENZETU TULIOWARUDISHA HUKU,NDIO MAANA TUNAWAHITAJI NA HAO WALIOBAKI TUWEZE KUKAMILISHA JAMBO LETU."ilisikika ile sauti huku Sara akizidi kusogelewa na wale wafu baadhi yao walionekana kuanza kuoza na wengine ndio hawatamaniki,alipotazama kwa makini alipata kumuona mwalimu Eddy akiwa miongoni mwa wafu wale huku akiwa ameanza kuoza usoni na sehemu nyengine,Sara alibaki kuweza mate tu ya hofu maana yale mambo ndiyo anayaona kwa mara ya kwanza,alikuwa ni jasiri sana maana yote haya anaoneshwa ili aogope aachane na kumfuata Ester wakijua yeye ni Sasha binadamu wa kawaida.
"SASA BASI TUTAKUACHA ENDAPO UTAKAPO TUHAKIKISHIA KAMA KWELI UTAMUACHA ESTER UKAE MBALI NAYE,ILA KAMA HUTOKUBALI UTAKUWA CHAKULA CHA HAO VIUMBE"ilisikika ile sauti huku wale wafu wakimsogelea Sara...hadi akubali ndipo wamuache huru,wale wafu wakamzunguka na kuweka duara kumuweka kati Sara na kuanza kumsogelea lengo ni kutaka kumdhuru kama atakataa kuachana na Ester,Sara alipoona vile wale wafu wanamkaribia kabisa akajikuta akifumba macho yake na sekunde kadhaa mbele akayafumbua na kubadilika gafla kuwa na sura yake ya Sara halisi huku macho yakiwaka mwanga mkali uliomulika lile shimo lote.
"WEWE NI NANI,?"iliuliza ile sauti na kufanya wale wafu wasimame gafla.
Sara alicheka kwa dharau kisha akatulia."Mimi ndiye mtoto wa Malkia AZNATY SHEERAN,malkia kumi na tisa (19) wa Majini na viumbe vya ajabu....naitwa SARA JUNIOR"alipojitambulisha tu kwa maneno yale pale pale wafu wote waliomzunguka wakapotea na gafla tu akajikuta yupo ardhini pale karibu na chooni alipokuwa anataka kwenda na akajikuta anadidimia chini muda ule.Hata yeye mwenyewe alijishangaa na palepale akajirudisha sura ya Sasha,alitazama huku na kule hakuna aliyeona tukio lile,aligeuka na kurudi zake darasani maana hakuwa na hamu ya kwenda tena msalani.
Kwa Michael yeye alikuwa zake darasani,baada ya kumuingiza Sasha kiuchawi kwenye lile shimo alikuwa akingoja tu majibu kwa wale viumbe vya ajabu kuwapa kazi ya kumtisha Sasha. Alipokuwa akiendelea na kujisomea pale darasani alishangaa amepigwa kofi la maana hadi akshtuka na kushika shavu lake pale lile kofi lilipofika,wanafunzi wenzake wote wakawa wanamshangaa maana ameshika sana.
"Michael vipi?"aliuliza mmoja wa wanafunzi wenzake aliyekuwa karibu yake.
""dah jini huwaga linanisumbua mara nyingi naona ndo limeanza tena."alidanyanga pale ili asijuwe kilichotokea huku akichezesha ulimi wake mdomoni kuonekana ni kweli,walimpa pole na muda huo huo akatoka zake nje na kuelekea chooni huku akiangalia nyuma kukamilisha hakuna anayekuja,alishajuwa aliyemzaba kofi ni nani hivyo alipofika tu chooni baada ya kuhakikisha hakuna mwanafunzi aliyekuwa eneo lile akatulia.
"nini nigefanya baba mbona unaniadhibu nikiwa darasani?"alisema Michael na muda ule ule akitokea baba yake kimazingara akionesha kununa,alimtazama mwanaye kwa hasira sana.
"yaani kati ya vitu vya kijinga ulivyovifanya ni leo,umewafanya wakuu wakimbie sana kwaajili ya yule binti Sara.,"alisema baba.
"Sara????Sara yupi tena baba mbona unanichanganya,nimewaletea Sasha binti anayetembea na Es......"
"ACHA upumbavu Michael zinduka,yule sio Sasha ni Sara...baada ya kufukuzwa shule amerudi kwa aina ile na hakuna angeweza kufahamu lolote hata wewe hujui."alisema baba mtu na kumfanya mwanaye ashangae,ndipo akaanza kupata picha kuona yaweza kuwa kweli maana kila siku Sasha lazima atembee na Ester kama ilivyokuwa zamani kwa Sara na Ester huwa wapo wote,hata ile siku alipogeuka kuwa ndege mkali akitaka kummaliza Ester alitoka Sasha kumsaidia.
"kumbe Sasha ndiyo Saaara"alifahamu sasa Michael.
"na sasa huwezi kuamini...wakuu wamekasirika sana wakijia umefanya makusudi,Sasha anauwezo mkubwa sasahivi na hutakiwi kumuendea kijinga,na tuna nafsi chache ya kukosa kiti kile kwahiyo kazi kwako mwanangu wewe ndiyo mhusika wa hili,acha kufuata mpangilio sasahivi,mchukuwe yeyote hata Magreth,Natasha....yeyote yule aliyekaa kwenye mstari sio lazima na Ester sasahivi ili tumpotoshe Sara si amekariri anaye fuata ni Ester,hapo ndio utafanikiwa lakini useme un'gan'gani kwa Ester kuanza hutaweza Michael."alisema baba mtu na kumfanya mwanaye aelewe sasa,alikubali na kuchukua shauri huo wa kupunguza yeyote kati ya wale wanafunzi waliopangwa kuuawa,baada ya baba yake kuondoka alirudi darasani huku akiwa ameshajuwa kuwa Sara amerudi tena shuleni kuendelea kumkwamisha mambo yake anayopanga.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sitakubali unizidi wewe mtoto wa malaya,mimi ndiyo nastahili kukaa pale,ngoja uone matokeo
yake"alisema Michael moyoni mwake akiwa amesimama nje akiliangalia darasana anakosoma Sara kwa hasira sana,alisimama muda sana akitafakari namna ya kumaliza kazi yake kwa urahisi na haraka,muda huo huo alimuona Denis akitoka darasani akiwa ameshika madaftari ya wenzake ya somo na kupeleka ofisini kwa mwalimu yakasahihishwe,akaona njia bora na ya haraka ni kuua watu wawili anaowahitaji kwa pamoja na kwa mazingira tofauti,alimtazama Denis huku amefurahi sana na kufanya maajabu pale,alikituma kivuli cha mwili wake na gafla tu kikapotea pale aliposimama kimaajabu na kutokea mbele kabisa anapoelekea Denis ofisini,hakikuweza kuoneka na yeyote hali iliyomfanya Denis bila kujua wala kuona lolote azidi kupiga hatua tu kutembea alipita muelekeo ule ule kilipo kile kivuli cha Michael akakivaa kile kivuli bila kujijua na kuzidi kuelekea ofisini,alimkabidhi mwalimu Isack yale madaftari na yeye akarudi kuelekea darasani,alipofika mbele zaidi alishangaa kuona mwili wake unaanza kupata na hisia za ajabu hadi mwenyewe alijishangaa na kuanza kumfikiria Ester,akabaki anajichekesha tu mwenyewe baada kufikiri huenda amempenda kweli Ester,aliingia darasani na kuelekea kukaa zake akipiga stori na wenzake lakini muda wote macho kwa Ester hadi mwenyewe Ester alishtuka baada ya kuona anaangaliwa sana na Denis..
Ester aligeuka tu na kuendelea kujisomea baada ya kuona macho ya Denis yamezidi kumuandama.Muda uliyoyoma na baada ya masomo kumalizika wanafunzi walirudi zao makwao,Ester aliongozana kama kawaida na Sasha wakipiga stori za hapa na pale,wakiwa kwenye furaha yao Ester akaona mkono wake unashikwa na alipotazama alishangaa kumuona Denis huku akionesha tabasamu.
"Mbona umeshtuka hivyo Ester...?"alisema Denis na kumfanya Ester ashangae kweli.
"hebu niache bwana Denis nini?"alisema Ester akitoa mkono wa Denis.
"kuna kitu nataka nikwambie mara moja Ester niruhusu dakika mbili tu tafadhari."alisema Denis kwa sauti ya ushawishi.
"haya sema nakusikiliza"alisema Ester kwa kujiamini wakiwa wanatembea na kumfanya Denis amtupie macho Sasha.
"dada samahani ninaweza kutupisha kidog...."
"wewe sikia...KAMA maneno yako ni siri mpaka umfukuze Sasha sitaki...ongea hapahapa kama umeshindwa waweze kwenda Denis...na samahani sana nakuheshimu usitake tufike mbali."alisema Ester kwa hasira.
"Lakini Ester...mbona unanifanyia hivyo mwenzio!,moyo wangu u...."
"Denis....Denis....tafadhari tena sana....nlishakukanya na hiyo tabia yako mara ya tatu na leo ni ya nne...sitaki MA HU SI A NO na mtu yeyote niache nisome mwenzenu,wewe kama umefuata mapenzi shule wafuate hao wengine sketi fupi na sio mimi,na leo ni mara ya mwisho nakukanya utakaporudia kunisumbua nakushtaki kwa mkuu unione mbaya."alisema Ester huku akimnyooshea kidole Denis kumaanisha hataki kabisa mambo hayo,hata Sasha alibaki kutazama tu pembeni akisikia Ester anavyomporomoshea maneno Denis ambaye akupata hata nafasi ya kumshawishi Ester, alibaki anamtazama tu Ester kisha akamuangalia Sasha kwa jicho baya hadi Sasha akashangaa,taratibu akashika njia na kuondoka zake bila kusema lolote.
"kuna mijitu mibishi kweli,alinifuataga kipindi cha nyuma mara tatu ananitongoza namkatalia lakini halisikii,wanaume wabishi kweli hawakubaligi kushindwa yani"alisema Ester wakiendelea kuongea na Sasha ambaye alibaki kumshauri tu akae mbali na wavulana kuepuka vishawishi visivyokuwa na lazima na kufanya aharibikiwe na kumpoteza rafiki elimu.Stori ziliendelea hadi walipofika kijijini kwao wakaagana kila mtu akafuata njia yake ya kufika kwao.
Kwa Michael jioni ya siku ile akiwa kwao alikuwa amekaa hana raha baada ya kuona ujanja aliyoutumia kwa kumtumia Denis umefeli huku akihisi huenda Sara alilijua hilo ndio maana Ester alikuwa ana nguvu ya kuongea maneno ya ujasiri,alikaa akitafakari kwa muda kisha akapata wazo ambalo alihisi huenda litafanikiwa,akatabasamu tu kisha akanyanyuka na kuingia chumbani kwake kupumzika,kuna sababu zinazofanya yeye ndio afanye kazi hiyo ya kuhakikisha anawapoteza wakina Denis na wenzake.
Naye Ester alikuwa akifanya maombi na bibi yake usiku ule,na baada ya kumaliza wakawa wanaongea mambo yao kabla ya kwenda kulala.
"kesho yakupasa uwahi kurudi ili tukafanye usafi makaburi ya wazazi wako,so unajua kesho ndio kumbukumbu yao."alisema bibi na kumfanya Ester atabasamu.
"Tena nilisahau kumwambia rafiki yangu leo kama atakuwa na muda kesho nije naye makaburini anisaidie"alisema Ester baada kukumbuka kuwa kesho ni siku muhimu sana kwake kuwakumbuka wazazi wake.
Nyumbani kwa akina Sara alikuwa mezani anakula pamoja na baba yake.
"haya niambie kile ukisema unataka kuniambia..."alisema Sara akimwambia mzee Junior.
"kesho unapaswa uwahi kurudi kuna mahala nahitaji kukupeleka."alisema mzee Junior na kumfanya Sara atabasamu tu.
"huyo itakuwa out hiyo"alisema Sara akitania na kumfanya baba yake naye acheke,wakiendelea na kula lakini mzee Junior alibaki akimtazama tu binti yake muda mrefu na kujikuta akitabasamu me huruma,alinyanyuka baada ya kukosa hamu ya kula gafla na kumuaga binti yake anaenda kupumzika huku akimhimiza kuhusu safari hiyo ya kesho.
Sara akabaki pale mezani akimalizia kula,baadae alirudi chumbani kwake kupumzika.Alianza kuwakumbuka matukio ya siku hiyo alipokuwa shuleni na kukumbana na ule mikasa uliyomfanya adumbukie kwenye shimo lile na kukutana na viumbe wa ajabu,alishuhudia kumuona marehemu mwalimu Eddy akiwa miongoni mwa wafu walioweza kutokea muda ule kule Shimoni,hakujua ni kwanini na kwasababu gani wafu wale wapo kule,akitafakari sana lakini hakupata jibu usiku ule na usingizi ukamchukuwa.
Asubuhi na mapema wanafunzi walielekea mashuleni,kama ilivyo kawaida yao usafi unawekwa kipaumbele kuiweka shule iwe kwenye mazingira mazuri,wanafunzi walishirikiana kusafisha kila sehemu ya shule ile na kuipendezesha huku wengine wakichukuwa maji na kuanza kumwagilia baadhi ya multi iliyoanza kupandwa ya vivuli na sehemu za bustani,baada ya kumaliza kazi zote asubuhi ile waliingia madarasani na masomo yakaanza.Asubuhi ile ile wakiingia tu darasani Ester alimfuata Sasha akionekana ndio anaanza kutoa daftari zake alizopanga kusoma.
"shosti vipi"alisalimia Ester na kumfanya Sasha atabasamu.
"Powa nambie Ester "
"Ah safii naona unaandaa silaha"
"Ah si unajua tena tunajiandaa kuitafuta ONE"alisema Sasha na Ester akawa anachangia wakiendelea kuongea.
"leo Sasha utakuwa na kazi nyingi nyumbani kwenu?"maana nitahitaji nakuchukuwa ukanisaidie kitu"aliuliza Ester.
"Kiti gani tena Ester? "
"Tarehe na siku kama ya leo wazazi wangu walifariki hivyo nahitaji kuelekea makaburini walau nikafanyie usafi nyumba zao za milele wazazi wangu,NDIO maana nikakutaka na wewe ujumuike nami ukanisaidie,samahani lakini"
"aise Ester samahani tena sana,maana leo kuna safari baba ameipanga anipeleke na sijajua ni wapi."alisema Sara.
"ah basi sawa kama utakuwa na safari wala usijali,nitamshitua yule rafiki yangu Sara naye nimweleze akikubali nitaenda naye"alisema Ester na Sasha akamuitikia tu,Ester akarudi zake kukaa huku akigeuka kumuangalia kiongozi mwenZake wa darasa Denis,aliishia kumsonya kwa kile alichokifanya jana.
Muda,Masaa yalizidi kuyoyoma siku ile na ilipokaribia mchana Ester na Sasha walitoka darasani na kuelekea ofisini kila mmoja akienda kuomba ruksa kivyake ili waweze kuondoka,baada ya kufanikiwa kuruhusiwa walirudi darasani na kuchukuwa mabegi yao kuondoka zaoeneo la shule.Michael alikuwa akiwatazama tu wakaondoka zao na kumfanya atabasamu mwenyewe pale ali pokuwa,alisotafuta sehemu nzuri na kuangalia hakuna anayemuona,akainama chini na kusema maneno ya kichawi yalifanya kuonekana kivuli cha Michael kutokea pembeni.Mwenyewe alikiangalia na kuanza kukiamrisha taratibu likaanza kutembea kuelekea darasa la kidato cha tatu bila yeyotebkuona kinachoendelea,kile kivuli kiliingia na kufuata sehemu alipo Denis ambaye alikuwa ameweka genge lake wakiongea na wenzake,kile kivuli kikasogea karibu na Denis na gafla tu kikazamia mwilini mwa Denis bila yeye kuelewa lolote akiendelea kuongea tu.Dakika chache tu Denis alianza kujiona wa tofauti,zile hisia zikamrudia tena zikaanza kumpelekesha pale alipo huku kichwani mwake kukija sura ya Natasha kuonesha anamtaka kimahusiano.
Stori waliokuwa wakipiga pale na wenzake zilikuwa ni za wanawake tu hali iliyomfanya abaki akitabasamu tu.
"ila jamanieeh...Natasha huko vizuri sio utani,mtoto akimuangalia hivi na macho yake ya aibu yale lazima tu umsimamishe"alisema Denis na kuwafanya wenzake wamshangae.
"we umerogwa nini?yule demu uliyekuwa unamponda baada ya kupandisha mashetani ndio leo unamsifia hivyo,acha ufala wewe"alisema mmoja wa rafiki zake.
"Ah hayo yalishapita Elisha, demu mzuri tumpe sifa zake bwana acheni majungu"alisema Denis.
"Kwahiyo una maanisha nini labda hebu funguka"
"Mimi yule leo ninaye mguu kwa mguu hadi kieleweke "alisema Denis na wenzake wakaanza kutabasamu.
"we jamaa nyoko sana nakukubali kwa umalaya wa chinichini,haya siye yetu macho"alisema kijana mwengine na kuwafanya wenzake wote wafurahi.
Uzuri na umbo la kuvutia la binti Natasha liliwafanya wanaume wengi pale shuleni wamtamani kuwa naye japo yeye alionekana kuwa mkali mbele yao na kuwafanya watu warudi nyuma kumfuatilia,na ile ishu ya binti huyo kuonekana kupandisha mashetani na kuharibu vitu darasani ndio kabisa wavulana wakarudi nyuma kabisa na kutomfuatilia kwa kuona kumbe uzuri wote mwilini ana mashetani, hata baadhi ya wasichana wenzake walianza kuwa mbali naye hali iliyomfanya mwenyewe awe mnyonge kwa kukosa ushirikiano na baadhi ya wanafunzi wenzake.
Muda wa masomo ulipomalizika wanafunzi walikusanyika paredi na kupewa maagizo kadhaa kisha wakaondoka zao,wanafunzi waliongozana vikundi vikundi kuelekea makwao wakifurahi hali iliyokuwa tofauti kwa Natasha aliyeoneka kupowawakitembea mwenyewe njiani wanafunzi wenzake wakipita tu kwa yeye kutembea taratibu akitafakari kuona amekosa marafiki,alihamaki kuona mkono wake wa kushoto umeshikwa,na alipogeuka nyuma akaonana na sura ya Denis iliyo na tabasamu pana. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Unajua binadamu tunavyoishi ni mdani wa maigizo,itapangwa sehemu ya upendo,itapangwa sehemu ya chini,itapangwa sehemu ya chanzo cha chuki hiyo,itapangwa mvurugano na mwisho itatokea hitimisho la igizo hilo liwe ni Jena au baya,Natasha...usiwe na mawazo salama kuhusu ukapoteza marafiki wa kuongea nao,na si uwe na marafiki wengi maana marafiki pia waweza kuwa maadui, kile kilichotokea siku ile kuhusu wewe chukulia ni bahati mbaya na naamini haitatokea tena,wewe bado ni mrembo,una kila sababu ya kujiamini usihofu kulengwa na watu wewe furahia kuwa wewe kama wewe,jipe furaha mwenyewe usihofie watu kujitazama tofauti,hupaswi kuwa hivyo bwana Natasha muda wote unakosa raha...utauharibu uzuri wako jamanii"alisema Denis akiwa ameshikana na Natasha ambaye maneno yale ya Denis yalimfanya atabasamu na kuona ni kweli,wakawa wanatembea.
"Lakini hata mimi najishangaa...sijawahi kuwa v....."
"Shhhh....usiseme tena mambo hayo,hebu fanya kama umesahau hakijatokea kitu,wewe ni Natasha mpya sasa hupaswi kukumbuka ya zamani,usiwaze sana Natasha."alisema Denis kwa upole hadi Natasha akabaki kumtazama usoni Denis kwa muda na kubaki kutabasamu tu.
"nashukuru kwa kunifariji "alisema Natasha.
"wala usijali Natasha."
"na umelijuaje jina langu hali ya kuwa ni mara ya kwanza tunaonana?"
"sidhani kama kuna mwanaume hapa shuleni asiyekufahamu kwa tabia na uzuri ulio nao,"alisema Denis akianza kusifia Natasha.
"mmmh sio kweli bwana mbona mimi ni wa kawaida tu"
"wewe unajiona wa kawaida ila sisi tunao ujua uzuri wako ndio tunasema hivyo"alisema Denis.
"haya asante mwaya....kumbe unaitwa nani?"aliuliza Natasha.
"Naitwa Denis...nipo Form Thee"
"ahaa sawa...nashukuru kukufahamu pia."alisema Natasha na wakaendelea kuongea mambo yao hadi walipofika kijijini wakaafana na kila mtu akashika njia yake.
Upande wa pili..Sara alikuwa akifuata tu anakopelekwa na baba yake,hakujua mahali wanapoenda.Walikaribia maeneo fulani ya makaburi na kumfanya Sara ashangae huku akizidi kufuata tu.
"baba....huku wapi tena?"aliuliza Sara akiwa haelewi kinachoendelea.
"wewe nifuate..!"alisema mzee Junior kwa ufupi na kuongoza njia ya kuingia makaburini,walisogea hadi kwenye kaburi moja ambapo mzee Junior alichuchumaa na kukushika kibao kichokuwa kimeandikwa jina la marehemu aliyezikwa pale kikiwa kina vumbi lililofanya jina lile lisionekane,taratibu huku machozi yakimlenga alianza kukifuta kile kibao huku mwanaye Sara kushuhudia tukio lile,alipomaliza lile jina likaonekana vizuri na kumfanya Sara abaki ameduwaa tu,aliishiwa nguvu gafla na kujikuta akidondoka kwa kupiga magoti haamini....lilikuwa ni kaburi la mama yake mzazi, miaka 12 imepita hajawahi kuona kabiri la mama yake leo ndio anapata kulitambua kwa kuona jina la mama yake AZNATY SHEERAN likisomeka kwenye kibao kile,alimgeukia baba yake ambaye alionekana kuwa mwenye majonzi baada ya kumkumbuka mkewe.
"baba....kwanini ulinidanganya.?kumbe mama yangu amezikwa kabisa miaka yote hiyo imepita hata siku moja umeshindwa kunionyesha mama yangu alipozikwa.?"alisema Sara kwa uchungu huku akilia machozi kabisa,hali iliyomfanya Mzee Junior amshike mkono binti yake na kumsogeza karibu yake akamkumbatia.Kila mtu akawa angalia kwa uchungu wake kana kwamba msiba imetokea siku hiyo,muda wote Sara alikuwa akilia kwa kumlaumu baba yake kwa kumdanganya na kutomuonesha alipozikwa mama yake miaka yote hiyo.Kilio kilipoisha baadae wakaanza kun'golea majani yaliyoota pembeni ya kaburi lile kama ishara ya kumkumbuka na kumjali marehemu kiroho japo kimwili hayupo nao.Baada ya zoezi hilo walisogea pembeni ya kaburi na kukaa huku Sara akionesha hakupendezwa na kile alichokifanya baba yake,mzee Junior alimtazama tu mwanaye.
"Sara mwanangu..."aliita mzee Junior na kumfanya Sara amtazame pembeni kabisa.
"Hupaswi kumlaumu mimi mwanangu,kuna mambo mengi huyafahamu ndio maana nikakuficha hata usipajue hapa miaka yote hiyo,Leo ndiyo siku aliyofariki mama yako na ndiyo siku na mwaka niliyoagizwa nikulete hapa kaburini ulione."alisema Mzee Junior na maneno yale yalimfanya Sara ageuke kumtazama baba yake.
"umeagizwa?nani kakuagiza?yaani nipangiwe masharti na mtu kuja kumuona mama yangu?"alisema kwa hasira Sara.
Mzee Junior alikuwa mpole huku akiangalia kaburi la mkewe,kuna mambo yalitokea nyuma na kumfanya asimwambie lolote mwanaye.
"Aznaty mkewangu...mwanao amekuwa sasa...na leo ndio ile siku ambayo uliniambia nimlete hapa kwenye nyumba yako...wacha nifanye kile ulichoniagiza..."alisema Mzee Junior na kumgeukia mwanaye.
"Sara...leo nitakueleza ukweli mwanangu ili ujijuwe wewe ni nani"alisema mzee Junior na kumfanya Sara ageuke kumsikiliza baba yake.
"ni miaka mingi sana imepita nikiwa naishi na mama yako mjini Dar Es Salaam,nilikuwa bado kijana nikiwa nachakarika ili nihakikishe napata cha kutumia na mkewangu Aznaty kipindi hicho bado hatujaoana.Maisha yetu yalikuwa na raha sana na tulipendana kiasi cha mimi kuufikia hatua ya kutamani ndoa hata kupafahamu kwa wazazi wake Aznaty.Kwangu ilikuwa niko tayari kwenda lakini mama yako hakuwa na utayari wa kutaka kupafamu kwao,kila siku nikizungumzia swala hilo anakuwa mnyonge sana na sijajua ni kwanini.Siku moja akaniomba aanze kupafahamu nyumbani kwetu maana tayari alikuwa ni mjamzito,sikuwa na hiyana tulijipanga baada ya kupata nauli nilimchukuwa na kumleta huku Mara,wazazi wangu wakifurahi sana kumuona make wao na wanataka tufanye haraka kukamilisha swala la ndoa.Siku ya kurudi Dar iliwadia na tukawaaga wazazi na kurudi zetu,tukiwa kwenye gari njiani mama yako alianza kuhisi halo fulani ambayo haikuwa kawaida.
(#alianza_kusimulia_ilivyokuwa_wakiwa_kwenye_basi_wakirudi_Dar).
"Junior...!!"aliita Aznat huku akitazama nje ya basi lile likiwa lipo kwenye mwendo pamoja na abiria wengine,Junior aligeuka kwa tabasamu kumtazama mpenzi wake aliyekuwa anashangaa nje.
"safari hii sio salama..."alisema Aznat na kumfanya Junior ashangae.
"We unaongea ujinga gani mbona unaombea mabaya!!"alisema Junior.
"Nielewe Junior hii safari so nzuri...kuna viumbe vinatufuata"alisema Aznat na kuzidi kumchanganya Junior.Wakiwa wanaendelea kuongea hayo walishangaa tu gafla gari linaanza kwenda kulia na kushoto likitanda barabara nzima huku likiyumba,abiria wakaanza kupiga makelele huku wakielekea huku na kule hata dereva mwenyewe alishangaa kuona usukani hautulii kana kwamba anashindana na mtu kuukamata usukani ule,gari liliyumba na kuyumba hadi likatoka kabisa barabarani na kuanza kushika kasi kuelekea kwenye maporomoko likadondoka na kupondeka vibaya ubavu wa kondakta,...
Ilikuwa ni ajali mbaya sana ambayo haikuweza kufahamika chanzo chake,basi lile lilipoporomoka chini hakukuonekana mtu yeyote kutoka wala kelele ya kuomba msaada.Ndani ya pori moja kuna mtu anaonekana amelala pembeni ya mti mmoja wenye kivuli kizuri,baada ya dakika kadha alianza kufumbua macho yake taratibu na kuanza kuangalia huku na kule pale alipo,alinyanyuka na kukaa,aliwatazama yale mazingira yakioneka kupendeza kwa maua kila sehemu huku ndege Wazuri wakisikika sauti zao zilizomfanya yule mtu anyanyuke na kuanza kuangalia huku na kule mahali pale,alipotazama kwa mbele zaidi aliona bwana zuri lenye maji ya kuvutia na taratibu akaanza kulisogelea, alianza kuyachezea yale maji kwa mikono,ndipo kumbukumbu zikamjia kuwa mara ya mwisho alikuwa safarini na mkewe Aznaty na muda mchache baada ya Aznat kumwambia kuhusu salama wa safari ile kulionekana basi lile walilopanda kuanza kwenda tofauti na muelekeo huku kila abiria akipiga makelele,hakujua kichotokea pale na kuanza kumkumbuka mpenzi wake Aznat,akageuka nyuma sasa na kuanza kutembea kumuita Aznat,aliita takribani dakika tano nzima na kujikuta akianza kutoa machozi kuona huenda ameshampoteza mtu ampendaye.Akiwa kwenye hali hiyo alisikia tu kwenye lile bwawa kama kuna mtu anaibuka ndani ya maji yale,alipogeuka kuangalia alihamaki kumuona Aznaty akitokea akiwa na nguo ya ndani tu huku akitabasamu,alimtazama Junior huku akimuita kwa kumnyooshea mkono.Junior moyo wake kidogo ikatulia baada ya kuona Aznaty yu mzima,taratibu akaanza kusogea hadi pale kwenye bwawa,akiachia tabasamu na yeye akaivua nguo kuingia mule kwenye maji kuoga.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baadae walitafuta sehemu na kukaa,Junior alikuwa bado anaitazama ile sehemu hakuipatia mfano wake."hapa ni wapi?aliuliza Junior akizidi kushangaa sehemu ile,ni nzuri.
"vipi umepapenda tuwe tunaishi hapa,"aliuliza Aznaty na kumfanya sasa Junior akumbuke jambo,akamtazama Aznaty.
"na tumefikaje kwanza hapa wakati ulikuwa kwenye gari tunarudi nyumbani?"
"usiwe na wasi kuhusu hilo Junior,ni mimi ndiyo niliyekuleta hapa na ni mimi ndiye niliyekutoa kwenye lile basi mapema kabla ya ajali kutokea."alisema Aznaty akimtazama Junior.
"ajali?ina maana lile gari liipata ajali?"
"ndio...na wote walikufa na naomba nikujulishe kitu ili ujuwe Junior...nakupenda sana na naomba usiniogope hata kidogo maana nimekuzoea mpenzi wangu...."alisema Aznaty na kumshika mkono Junior."Mimi ni kiumbe tofauti na binadamu,nimezaliwa katika dunia nyengine tofauti na hii,ila anaishi kama binadamu kama wewe."alisema Aznaty na kumfanya Junior amshangae.
"wewe Aznaty...unaumwa au?maneno gani ya kuongea hayo?"
"sitanii Junior ni kweli,mimekaa na wewe muda wote kwa upendo na sijawahi kukuonesha kwamba mimi ni nani,naomba unizoee tu Junior maana siko tayari kutengana na wewe kiukweli...ndio maana tukiwa ndani ya gari mapema tu nlikuambia safari ile haina usalama,niliwaona viumbe wa ajabu wakilifuat ila basi lile,shida yao kubwa ilikuwa ni sisi."
"U...naju.....a......unajua Aznaty...sui..sikuelewi ujue....yaani w...wewe ni..."
sina nia mbaya Junior na wala usiniogope,nimeishibna wewe muda mwingi sana sijawahi kukufanyia kitu kibaya,hata nilipojua kutokea kwa ile ajali nimeshindwa kuokowa watu wote nikaona ni bora nikutoe kwenye kifo mpenzi wangu...nakupenda sana Junior...lakini...."alisema Aznaty kwa pole."lakini sheria na taratibu zetu zinatubana sisi kuwa na mahusiano na binadamu wa kawaida,na nlishakupenda wewe siwezi kukuacha nipo radhi lolote litokee nisikukose Junior,tafadhari naomba unizoee...nidhanie kwa namna yeyote ile iwe mimi ni jini,mchawi au shetani lakini tambua kuwa mimi sio binadamu kama wewe lakini nakupenda"alisema Aznaty na kumfanya Junior amtazame Aznaty vizuri usoni na kuona macho yake yamebadilika na kuwa ya kijani kabisa huku yakitoa machozi.Hakuamini siku zote hizo alikuwa anaishi na jini kiumbe kisicho bi binadamu,alifikiria mapenzi waliyokuwa wakipeana wawili hao siku zote kumbe anapata penzi la jini,hadi kuamua kwenda Mara kwao kumtambulisha kwa wazazi.Hakuweza kuamini kabisa akawa anamtazama Aznaty aliyekuwa ni mwingi wa aibu akiangalia chini kumuacha Junior amuangalie muda wote.Lea moyo wa huruma na upendo Junior akajikuta akimsogeza Aznaty na kumkumbatia kwa upendo kuonesha ameridhia kwa chochote kile,akitafakari amefanya mambo mengi sana na mrembo yule na hakuweza kumdhuru hhata siku moja,kwanini amuogope sasa hivi kwakuwa ameambiwa kweli?kwanini amkatae hali yakuwa ameepushwa na ile ajali?hakuona sababu ya kumkataa Aznaty,alijuwa kweli Ana mapenzi ya dhati,akaamua kujitolea kwa chochote kile kitakachotokea hapo mbele.Aznaty alifarijika sana baada ya kuona upendo wa Junior,siku hiyo walifurahi sehemu ile huku Aznaty akimuonesha Junior uwezo na maajabu yake anayoyaweza,taratibu ile hali Junior akawa anaizoea taratibu,na kuonesha anampenda sana Junior,Aznat alitoa baadhi ya uwezo wake na kumuwekea mwilini Junior ambaye t a aibu alianza kujishangaa na kuhisi utofauti mwilini,hata ikafika kipindi Junior akawa anapata kuhisi jambo ambalo linaweza kutokea hapo baadae,hali ile ilimfanya Aznaty afurahi na kuona amempa zawadi muhimu ampendaye.Siku hiyo wakiwa wawili wametulia Aznaty aliweza kumueleza amefanya siku ampeleke huko anapoishi huko kunakosadikika kuna viumbe tofauti na binadamu,Junior akaogopa kwa kuhisi a naweza akafanyiwa baya huko lakini Aznaty alimuuliza na kumuondoa shaka.
Usiku wa kuamkia safari hiyo Junior akiwa amelala zake alihisi kuamshwa na Azanaty,alipotaka kunyanyuka alihisi mwili mzito na macho hayawezi kufumbuka akabaki alisikia tu sauti za watu wakisikika kuongea usiku .uk wa manane.
"amekupa nini huyu binadamu mbona hatukuelewi Aznaty?baba amechukia kwa kitendo ulichofanya hali ya kuwa wewe ushapangiwa kuelewa na ukoo wasuriati."ilisikika sauti ya kike ilisema kwa sauti.
"Najma sikia nikwambie mdogo wangu,nimempenda Junior kutoka moyoni mwangu,na nimeridhika japokuwa ni binadamu na katu sitakubali niolewe na ukoo ule wakibabe na maguvu,wale wanataka kuipindua tawala ya baba na kila nikimwambia hanielewi ananilazimisha niolewe kwa watu watakaokuja kumpindua,nitamuweka wapi sura yangu siku niolewe na wale watu halafu nimshuhudie baba yangu anavyokatwa kichwa?hapana Najma siwezi...bora niolewe na binadamu kuliko wale wanayama wasio na huruma"alisema Aznaty kwa uchungu akimuelewesha mdogo wake aliyemtembelea usiku ule kwa miujiza,hata yeye Najma alikuwa akimsikiliza sana dada yake kwakuwa ni yeye pekee ndiye anauwezo wa kupata kutambua mtu fulani Ana lengovgani kuhusu wewe,Aznaty alikuwa na uwezo wa kipekee wa kumjuwa mtu vile vyote anavyofikiria.
"sawa dada nimekuelewa,lakini kwa hili la kuwa na binadamu na kutaka akuoe sidhani kama litakupa amani siku zote,si baba wala wale wasuriati watakaokubali huyo binadamu akuoe,wewe ni malkia mtarajiwa na baba ameshakuwekea n afasi hiyo akijuwa kuwa utakuja kuolewa na ukoo ambao anauheshimu"
"wale wanafuata masilahi Najma hawana lolote wanajua baba afya yake unazidi kuzorota."
"sasa dada unafikiri utafanyaje,baba maneno hayo hayaelewi kabisa na hivi ninavyokwambia wanaanza kumsumbua baba kwa akili yako wakikutaka"
"Kiukweli Najma kumuacha Junior siwezi hata watumie nguvu gani,lolote na liwe sisikilizi la mtu na hiko cheo cha umalkia bora nikikose kuliko kumkosa Junior,na yeyote atakayemgusa huyu atanijua kuwa mimi ni nani sitojali la mtu nadhani unanijuwa"alisema Aznaty akionesha kweli akampenda binadamu yule.Yote alikuwa akiyasikia Junior akiwa pale kitandani na kukaa kimya kuyasikia,aliona kweli hili swala ni zito na huenda kuna vita itatokea kisa tu kupendwa na Aznaty ambaye si binadamu wa kawaida.
Huku Aznaty aliendelea kumweleza mdogo wake ambaye baada ya kupewa maneno ya kutosha akimuacha dadake na kumuaga huku akiambiwa na dadake akayafikishe maneno hayo kwa Mfalme ambaye ni baba yao.
Na kweli taarifa zile zilimfikia Mfalme ambaye alizipokea kwa Kali akikasirika,hasira zile zilimfanya atibue maradhi yake ambayo yaliwafanya wapambe wake wamrudishe kupumzika kitandani.
"mpumbavu sana huyu mtoto...anapinga desturi za mababu wa enzi...binadamu atamsaidia kitu gani zaidi ya matatizo anajitafutia,hakikisheni mnamuuwa huyo mtu asitake kuniletea balaa mimi wakati nishakaa na wasuriati tumeshayamaliza kila kitu,auliwe huyo mtu na mumlete hapa haraka Aznaty ndoa ifanyike,yeye ndiyo Malkia wa hapa asilete ujinga wake.....harakaaa!!"alifoka Mfalme wa viumbe wale na kuwafanya watu wake watii na kuanza safari ya kurudi duniani kumchukuwa Aznaty kwa namna yeyote ile huku wakipewa idhini ya kumuuwa binadamu Junior.
Usiku wa siku ile hakuwa na raha ikambidi Junior aamke nab kuanza kuongea naye,Aznaty alishafahamu kwa uwezo aliyompa Junior yale yote atakuwa ameyasikia lakini angekuwa mtu wa kawaida asingesikia chochote kilichoendelea muda ule.
"Junior...naomba uniamini mimi....nakupenda sana na siwezi kakubali wanacjotaka."alisema Aznaty huku akimshika mkono Junior.
"nakuhofia wewe pamoja na kiumbe kilichopo tumaini mwako Aznaty,hao wenzako anaonekana kabisa kutonihitaji m...."alifumba mdomo Junior na Aznaty.
"nielewe mpenzi wangu....hakuna kibaya chochote kitakacho kukuta,aliyekupenda ni mmoja tu na ni yeye ndiyo atakulinda muda wote,muamini Aznaty..niaminii"alisema Aznaty na kumkumbatia Junior,hakika akampenda upendo wa kweli jambo lililomfanya hata Junior kuutoa moyo wake naye na kuamua lolote litakalotokea mbele sawa japo hajui vizuri kuwa amepangiwa afe na Aznaty aweze kurudishwa kwenye ulimwengu wao.
Usiku ule waliutumia vizuri wapendao wale wakipeana mapenzi ya dhati huku akijaribu kusahau mambo yanayoendelea.Baada ya kumaliza mambo yao walipumzika wakiongea mambo yao hasa kuhusu kiumbe kilichopo tumboni mwa Aznaty.
"ndio nshawahi sasa...huyo ni dume na nshamuandalia jina la Kareem"alisema Junior akiwa amelishika tumbo la Aznaty lililoanza kuwa kubwa,.
"mh jina balaa...Ikram ndiyo jina zuri au unalionaje?"alisema Aznaty akionesha tabasamu.
"mmhh kweli...unajua kuchagua kumbe!"alisema Junior akimsifia."akiwa mama je"alisema Junior.
"mh tena hapo mengi kuna Najati,Nazhaty,Kauthar...yapo mengi sana...tumuite Kauthar..."alisema Aznaty.
"Mh sitaki...akiwa mwanaume umempa jina wewe huyu wa kike nampa mimi.....mmmmmmmmmmmmm ataitwa SARA!!!"alisema Junior na kumfanya Aznaty abaki akitabasamu tu,muda ule ule akifumba macho na liloshika tumbo lake kwa mikono miwili akimuacha Junior akiangalia tu,alilipapasa tumbo lake kwa dakika kadhaa kisha akafumbua macho na kumtazama Junior,akamsogelea Junior na kumpigia busu la shavunu.
"Sara wako anakusalimia"alisema Aznaty kwa utani japo ni kweli,kwa uwezo wake tu alishajuwa kuwa kiumbe kilichopo tumboni ni jinsi ya kike,alimfanya Junior asiamini lakini ukweli ndio huo.Amefurahi sana baada ya kujuaanakwenda kuitwa baba Sara siku za usoni na kubaki kumkumbatia Aznaty wakawa wanafurahi..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakiwa kwenye hali hiyo kila mmoja alihisi kitu,kwa kuwa Junior alipata kupewa nguvu za Aznaty naye alipata kujua kuna jambo baya inatokea muda si mrefu.Aznaty akabadilika gafla huku akitoa sonyo kali,akainuka na kuanza kuvaa nguo.
"sio salama hapa jiandae tuondoke"alisema Aznaty akichukua gauni lake lililokuwa na mipasuo mikubwa pembeni huku ndani akiwa amekaa suruali,haraka haraka na Junior akavaa nguo zake kisha akashikwa mkono na Aznaty ambaye alisema maneno fulani wakapotea mule chumbani.Hazikupita hata dakika mbili watakatokea kimaajabu viumbe vya ajabu mule chumbani walikotoka Aznaty na Junior,waliangali kile chumba kila kona hawakuona mtu,wanakuwa wameshaondoka na wao bila kumpoteza muda wakapotea.
Upande wa pili Mfalme alikuwa meza juu pamoja na viongozi wake wengine na baadhi ya ule ukoo wa wasuriati ambao walionekana kukasirika sana.
"nishawatuma vijana wangu wameanza kumchukuwa wala msijali,yule ni mali yenu wala ondoeni shaka."alisema Mfalme akionesha kujenga tabasamu.
"tumechoka Mfalme ni mara ya ngapi tunafika hatumuoni Malkia mwenyewe?au hadi swala hili tuingilie sisi?"alisema Mkuu wa wale wasuriati akiwa pembeni na kijana wake ambaye ndiyo mlengwa anayetakiwa kuwa mume wa Malkia Aznaty.
"ataletwa tu wala msijali jamani,hata kijana wako atafurahi kumuona mwenzake."alisema Mfalme kuwafariji wale watu ambao kidogo walianza kumuamini Mfalme na kuendelea kupiga vinywaji vilivyoandaliwa mezani pale.Wakiwa kwenye furaha hiyo wakimsubiri Malkia aletwe walianza kuona uwepo mkali ukijua eneo lile na kuanza kuzunguka pale mezani kama kimbuga cha ajabu kilichosambaratisha kila kitu pale mezani huku wat u wote wakiondoka chini na viti v yao wakiwa hawaelewi chanzo,Mfalme kwa nguvu zake akaanza kuutuliza upepo ule lakini wapi,ikawabidi watu wasuriati nao watumie nguvu zao kudhibiti kimbuga kile cha ajabu lakini nao hawakuweza,kiliendelea kupeperusha vitu kwa dakika kama kumi tu kisha taratibu kikaanza kutulia na kwenye kile kimbunga katikati akatokea Aznaty akiwa amekasirika huku akiwa na Junior wameshikana mikono.Watu wote walishangaa kumuona ni Aznaty akiwa binadamu pale mbele yao,Aznaty akaanza kuwatazama wote waliokuwa kwenye eneo lile kwa hasira kisha akaishia kwa baba yake.
"WEWE Aznaty una kichwa??"alifoka Mfalme na kubaki kukohoa kuonesha hana hali nzuri.
"sina huo ukichaa na wala siujui....baba...sijawahi kukukosea hata siku moja baba yangu hata kosa dogo....lakini kwa hili nahisi litakuwa la kwanza...."alisema Aznaty na kugeuka kuwatazama wasuriati.
"siwezi kuolewa na hawa wanaopanga kukuuwa pindi mtoto wao atakaponipa mimi...hawa sio watu wazuri....wanailazimisha ndoa hii kwa masilahi yao ili mtoto wao awe Mfalme mimi niwe Malkia na hawana upendo wa kweli hata kidogo....."alisema Aznaty na kugeuka kumtazama Junior."huyu ndiyo mume ninayemtarajia awe na sitakuwa na mtu yeyote kwa hili nililochagua,nahitaji amani,nahitaji kuwa mwenye upendo na familia yangu muda wote,"
"Wewe binti unaongea maneno gani huna hata aibu mbele ya wazee wako?"alisema baba wa yule kijana wa kisuriati me kufika,Aznaty alimtazama kwa dharau.
"tena wewe....wewe.....usiongee lolote maana unazidi kunifanya nikuchukie"alisema Aznaty na kulishika tumbo lake.
"Nimekuja hapa kuwakanya...hakuna anayeweza kunigusa hata kidogo na hata huyu niliyesimama naye,yeye ndiye nilimchagua na nampenda kuliko huyo mtoto wenu,na nyie si mnafuata desturi za wasuriati...haya nina ujauzito wa huyu binadamu...vipi nafaa kuolewa tena?"alisema Aznaty kwa makusudi kabisa na kuwafanya wazuriati wote waliokuwa pale wartime mate kuonyesha ni haramu kwao kile kitu.
"nadhani mshapata jibu...hivyo akahitaji kufuatwa ninapoenda mniache,sifai kuwa mke wa mtu."alisema Aznaty na kumtazama baba yake,hakumuongelesha tena akageuka na Junior na kupotea zao eneo lile wakiwaacha wasuriati kubaki kushangaa na Mfalme,taratibu wakaanza kunyanyuka zao pale walipodondoka wakijifuta vumbi,mkuu wa wale wasuriati alimtazama Mfalme kwa muda kisha akamkamata mwanaye wa kiume na kuanza safari ya kuondoka zao kwa hasira na wengine wakafuata .
Kwa Mfalme yeye ilikuwa ni fedheha sana kwa kile kitendo alichokifanya binti yake na kubaki akipiga ukelele kwa nguvu akimuita Aznaty kwa hasira,hali iliyomfanya apandishe matatizo yake ya kiafya na kubaki akianza kukohoa damu,wahudumu wake wakaribu alimchukua na kumsaidia kumpeleka akapumzike huku wakifuta damu zile mdomoni.Mfalme Sheeran alikuwa ndiye kiongozi wa viumbe vyote vya ajabu yenye uwezo mkubwa tofauti na binadamu,yeye ndiye aliyekuwa akiamuru sheria zote za watu wake huku ikiwekwa mipaka ya kutojenga urafiki na binadamu yeyote,alifanikiwa kupata watoto wawili na mkewe ambaye naye alikuwa anauwezo wa aina yake na hakuna kiumbe mwenye akili yao anayeweza kuufikia uwezo huo na walibahatika kupata mtoto mmoja ambaye ni Aznaty huku Mfalme akizaa nje na mwanamke mmoja ambaye alifariki baada ya kujifungua na kumuachia mtoto Mfalme aliyeitwa Najma,baada ya masiku kadhaa Malkia alianza kuugua ugonjwa wa gafla ambao ulimla taratibu hadi pale hali iliyokuwa tete Malkia akamwita mwanaye Aznaty na kumkabidhi nguvu zote alizonazo na ndio siku hiyo alifariki na kumuacha Mfalme akiwa na watoto wawili Aznaty na mtoto wa nje Najma.
Siku hiyo Mfalme alikuwa hoi taabani baada ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya alianza kuota jopo la viongozi na kuwaeleza mambo ya flame ile na mtu pekee anayepaswa kuwa kiongozi endapo atakapotoweka kwenye ulimwengu wao.
Taarifa za kuwa taabani mfalme ziliwafanya wasuriati waamke na kutaka kuichukuwa nafasi ile ya ufalme jambo ambalo lilileta mtafaruku wakileta kisingizio cha kuwa walipaswa kuoa kwenye koo ile ya kifalme hivyo yule kijana wa kisuriati aliyetakiwa kuwa mumewwa Aznaty ndiyo anayepaswa kuwa mfalme lazima ile mimba ya Aznaty lazime iharibiwe ili aje kuwa mke wa mfalme huyo anayetarajiwa wa kisuriati.
Muda ulipoenda huku mfalme alipoona Jana mud mrefu wa kuishi akaamua kuvuta kitabu chake na kukiweka pale kitandani alipolala,kwa uwezo wake wa ajabu alianza kufunua karatasi na kuanza kutamka Manson anayoyataka huku yakionekana kujiandika kwenye kile kitabu yoke anayoyazumza,alichukuwa mud mchache kuongea na alipomaliza n.a. kunyanyuka kwa tabu n.a. kuanza kuembea kuelekea kwenye kiti chake cha kifalme, watu wake wa Karin walimtaka kumsaidia walau wamsogeze Latino hakutaka,aliyaka a file mwenyewe,alipokitikia kiti kile cha kifalme akakaa na kugeuka kuangalia kiti cha pembeni yake ambacho alikuwa akikaa marehemu mkwewe,alitabasamu tu pale alipokaa akikumbuka alivyokuwa anampenda mkewe,alihisi yup naye pale wamekaa wakifurahi,machozi yalimtoka huku akiweka Kiel kitabu kwenye kiti cha malkia n.a. mud mfupi th kukawa kimyaa kumaanisha tayari mfalme amemfuata mkewe,mwili wake ulitengana na roho gafla tu na kuwafanya watu wake wapige goti chini kwa pamoja kama kumpa heshima yake kama ufalme, taarifa za kifo cha mfalme ziliwafikiwa wasuriati ambao waliona ndio muda muafaka wa kwenda kugombea nafasi ile ya ufalme na haraka wakaelekea kunako msiba.
Aznaty alipata kupokea taarifa ile ya kufariki kwa baba yake akiambiwa n.a. Najmawambaye alimtembelea siku hiyo akimtaka yeye ndiyo anayetegemewa kwenye mazishi kama mtoto wa pekee wa kifalme.Na kweli hakuwa na kipingamizi Aznaty alimuacha Najma arudi huku yeye akiongea na Junior akimuiga kuelekea kule kwenye jamii ya kwao na kumuahidi kurudi punde watakapozika maana binadamu hawezi kuhudhuria mazishi wa viumbe wale.Junior alikubali na kumuacha Aznaty aanze safari kwenda kwao huku akiwa na ujauzito wa Junior.
Mazishi yalifanyika siku hiyo huku watu wa jamii hiyo wakushuhudi Mfalme wao anavyozikwa kwa desturi ya kuuchoma moto mwili huo uliyowekwa juu ya kumi nyingi.BAADA ya mazishi Aznaty hakutaka kusikia la mtu akataka kurudi duniani kuendelea na maisha yake lakini wazee wa karibu na baba yake walimzuia na kumtaja akae kwanza ili aelezwe mambo ambayo marehemu baba yake aliacha kabla hakufa,basi aliwasikiliza na kuingia sehemu ambayo Mfalme aliweka kiti chake cha kufalme pamoja na kiti cha Malkia,Aznaty akasogea na kukaa kweny kiti cha Malkia na kuchukua kofia ya kimalkia akaivua kama ilivyo destuli,kitendo cha kuvaa tu ile kofia kile kiti kilimbana chini miguu na huku kwenye mikono na tumboni kwa minyoro mikubwa ya kichawi ambayo haikujulikana ilipotokea,akabaki ku kukuruka ukitaka itoke lakini wapi,waliingia wazee watano waliokuwa ni hodari kwa nguvu za kichawi,wakaingia na jopo la wazee wa wale wasuriati wakiongozwa na yule baba mwenye kutaka mwanaye awe Mfalme,alishangaa sana Aznaty kumuona yule kijana aliyepaswa amuoe amevalishwa kofia ya marehemu baba yake kuonesha yeye ndiye atakaekuwa Mfalme kwa muda huu..
"nini mnafanya nyie...mbona siwaelewi...nmalazimisha vitu visivyowezekana..?!"alisema Aznaty kwa hasira na gafla macho yake yakabadilika na kuwa ya kutisha akizipandisha nguvu zake kutaka kukata ile minyororob lakini wazee wale waliitupia uchawi na kumfanya Aznaty ashindwe kutoka pale.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"mnamuumiza mwanangu jamaniii,toeni hizi nyororo!!"alisema Aznaty kwa uchungu akiona tumbo lake linabanwa na huenda kiumbe kilichopo tumboni kikapoteza uhai.
"Unaweza ukapoteza kweli huyo mwanao endapo hautakubaliana na maneno ya marehemu baba yako,"alisema mzee mmoja na kuchukua kile kitabu alichokuwa amekiandika Mfalme,akakisimamisha hewani kwa nguvu za kichawi kisha akakisogeza kwa Aznaty karibu kabisa na uso wake ili asome,Aznaty alikitazama na kuona maandishi kweli.
"#Aznaty binti yangu,wewe ndiye tegemezi langu siku zote hata nisiwepo kwenye jamii hii,baba yako naondoka sasa namfuata alipo mama yako,tumeishi naye kwa miaka mingi sana na tukipinga mtu yeyote wa jamii yetu kuwa na mahusiano na binadamu,ni kosa June sana na unastahili kufa,na hao unaowaona mbele yako wapo kwaajili ya wajibu wa jambo hilo,huwezi kukwepa adhabu hiyo mwanangu.Nimefikiria sana baba yako nikaona hatuwezi kuondoka wote tukauacha ufalme huu upotee,nimewaomba wazee wasikuadhibu na kuona ni bora kukubali uwe mke wa kijana wa kisuriati,awe Mfalme na wewe use Malkia ili tu uwe hai bila hivyo kifo kinakusubiri binti yangu,kama nimekukosea mwanangu nsamehe sana ila nakupenda sana ndio maana nayajali maisha yako uendelee kuishika,wewe ni zawadi pekee ya mkewangu kipenzi...acha nikapumzike na Malkia wangu...nikuombee maisha mapya mwanangu.
#$Mfalme SHEERAN#$"
Aznaty alikisoma kile kitabu huku machozi yakimtiririka,yalikuwa ni maneno yaliyomkata maini hasa akifikiria ameshapenda binadamu ambaye tayari anategemea kuitwa mama,alitazama tumbo lake likiwa inazidi kubanwa na minyororo,kuna muda aliona maneno yale bora ayafuate maana ataponyeka adhabu ya kifo na kuiendeleza falme ile izidi kuwa upande wao,lakini nafsi inamsuta akimfikiria Junior aliyemuahidi baada ya mazishi atarudi duniani,aliumiza kichwa sana.Kile kitabu kikatolewa na mnyororo wa tumboni unazidi kubanwa na kumfanya Aznaty alie.
"Sawa.....sawa......nimekubali...."alisema Aznaty na kuanza kulia kwa uchungu baada ya kuona hali tete,watu wa suruali walifurahi na taratibu yule kijana akasogea hadi kwenye kiti cha Mfalme na kukaa,wakawa ni Malkia na Mfalme pale mbele.
Mzee mmoja alitoa kichupa kidogo kilichokuwa na maji fulani ndani yake,akakipeleka kwa Aznaty kama kilivyopelekwa kile kitabu.
"Hiyo ni dawa ya kumuondoa kabisa huyo kiumbe kichafu tumboni mwako,unapaswa unywe maana Malkia hapaswi kuolewa akiwa na mimba ya nje tena ya binadamu,unatakiwa unywe"alisema yule mzee na kumfanya Aznaty ahuzunike kuona mwanaye wa tumboni anauliwa muda si mrefu,akiinama chini na kuanza kufikia alivyopanga mambo mengi na Junior,moyo ulimsuta,akaona bora afanye kitu...kwa uwezo alionao aliiteka haraka akili na hisia za Junior na kumjaza hisia za ajabu za kutaka kufanya mapenzi.
Usiku huo Junior alikuwa zake akitoka kwenye mihangaiko yake akiwa ameshika mfuko wake alioweka vitu yake,akauweka mezani na kunawa mikono baada ya kuandaliwa chakula na binti wa kike wa mamantilie,alianza kula pale Junior huku akimfikilia Azanty wake,alikumbuka kuwa ana mtoto tumboni huku akifikiria mambo ya kule,alikosa amani gafla na kushindwa kuendelea kula,alitoa hela na kisha akaondoka zake kuelekea kwake ambapo ni nyumba tatu mbele tu ya kile kibanda cha mamantilie,hata alipoingia zake ndani kwa mawazo aliyonayo alijitupa tu kitandani huku akianza kumkumbuka Aznaty wake hisia za mapenzi zikaanza kumtawala gafla tena hadi alishangaa,alijitahidi kufanya jambo lengine lakini wapi.Akiwa kwenye hali hiyo alisikia mlango ukigongwa,taratibu akasogea mlangoni na kujifungua mlango,akakuona na msichana yule wa mamantilie alimleta mfuko wa Junior ambao aliusahau
akiwa anakula,Junior alizipokea mfuko ule lakini kwa hisia alizonazo alianza kumuachia yule msichana me nguvu zote hadi akakubali,kamuongoza ndani na kujikuta wanashiriki tendo la ndoa siku ile japo walichukuwa muda mchache tu kisha yule msichana akarudi kazini na kujikuta alipokea lawama nyingi me kuchelewa akabaki akiomba msamaha na ikawa ni siri yake na Junior.
Alibaki akilia tu mwenyewe kitandani baada ya kuona amemsaliti Aznaty,alilaumu moyo na hisia zake kumponza kufanya jambo lile lakini ndio ishatokea.
Huku kwa Aznaty alikubali kuinywa ile dawa ila kuna jambo alinifanya ambaye hakuna yeyote aliyeweza kujua kilichoendelea,ni yeye ndiye aliyefanya Junior azini na yule mfanyakazi wa mamantilie akiwa na maana,kabla ya kunywa dawa ile alilitazama lile tumbo lake huku akilia.
"Sara mwanangu...sina budi ya kukuhamisha ukae kwa mama mwengine....nitakuomba na wewe mwanagu endapo siyokubali kufanya wanachotaka,nenda mwanangu...naamini kuna siku nitakuona tu"alisema Aznaty yale kisha akanena maneno fulani ya kichawi na kutoka kitu tumboni mwake,alipoteza ile dawa haikufanya kitu chochote maana mtoto tayari kashamtoa kimiujiza na kumuweka yule msichana aliyefanya tendo la ndoa na Junior na mimba ile ikaanza tena moja kwa yule msichana.
Iliipita siku,masiku,miezi lakini hakukuwa na dalili za kurudi kwa Aznaty ambaye muda wote Junior alikuwa akimsubiri japo mazoea na yule binti muuza chakula yakizidi kushika kasi,siku hiyo wakiwa chumbani wamepumzika yule msichana akamueleza Junior kuhusu hali yake alihisi ni mimba jambo lililomfanya Junior abaki ameduwaa, kesho yake asubuhi iliwabidi waelekee hospitali kupima na kukuta ni kweli mimba ya miezi mitatu.Walirudi zao na hali ile ilimfanya Junior abaki na mawazovsana akifikiria kuhusu Aznaty ambaye alimuahidi kurudi,istoshe wanafurahi nao kupata mtoto.Alifikira pia endapo Aznaty akijua kuwa Junior alipata mwanamke na kumpa mimba nini atafanya maana so kiumbe cha kawaida?,alibaki hana amani tu huku mimba ile ya msichana yule ikizidi kukuwa tu.
Huku upande wa pili hadi leo hii Aznaty hakuwa tayari kuolewa na yule kijana maana kama mimba alishawaridhisha kuwa imetoka,japo alikuwa akiishi na yule mwanaume kama Mfalme na Malkia lakini hakukuwa na tofauti na mtu na dadake maana hawakuwa wakishiriki ten do la ndoa hata siku moja jambo ambalo liliwakera hata wasuriati ambao lengo Lao ni kupata mjukuu ambaye wanajua atakuja kuwa Mfalme hapo baadae na kuweka kuitawala falme hiyo,na jambo hilo ndio Aznaty alipokuwa mapema na kukamata katakata kuolewa.
Siku huyo Mfalme aliitwa na wazee wake wakaa kibao cha muda mfupi wakitaka bora azae na kijakazi wa mule ndani ili baadae wafanye lolote kwa Aznaty ili aonekane amezaa na Mfalme yule wa kisuriati.,basi ikambidi wafanye hivyo wakaanza kumshawishi mfanyakazi mmoja na kila siku akawa anajuana na Mfalme yule kimwili bila Aznaty kujuwa.
Miezi kibao ilipata na siku ya kujifungua kwa yule mwanamke wa Junior ilipowadia Aznaty alipotea kule kwenye jamii yao na kuja duniani,alienda moja kwa moja hospitalini bila yeyote kumjuwa wala kumuona,baada ya zoezi la kujifungua kumalizika mtoto akawekwa pembeni na mama yake ambaye alikuwa hoi muda ule,Junior akitabasamu baada ya kuona amekuwa baba,alishaanza kusahau kuhusu Aznaty, alielekea kwa daktari kwenda kupata maelezo kuhusu mkewe na mtoto aliyezaliwa.
Aznaty alitokea kimiujiza kwenye chumba alichokuwa yule mwanamke na mtoto,akasogea alipo mtoto na kumnyanyua huku chozi likimtoka,."Sara mwanangu,mimi mama yako,huu ndio msaada wangu kwako kuhakikisha upo hai, nisingekubali ice tumboni mwangu siku ile ndio maana nimekuweka kwa huyu mama yako mwengine,nakupenda mwanagu maana nimekuwa nikikusubiri na baba yako kwa muda mrefu sana,hata nikifa mimi nahitaji wewe uje kuwa Malkia wa jamii yetu na so vingine,sisi tuna haki pia ya kuchagua tumpendaye,nimempenda baba yako kutoka moyoni na sitaki nimpoteze hata siku moja,nakupenda mwanangu,wewe ndiye utakayeokoa kizazi chako kilichozaliwa na binadamu kama baba yako,natarajia utakuwa salama Sara na utakuwa msaada kwa wenzio japo utapitiabmatesonmengibkama niliyopitia mama yako lakini yakupasa uvumilie ili ufikie lengo lako,terra watu wako utakao waongoza wewe,nakupenda Sara.."alisema Aznaty huku machozi yakimtoka akiwa amembeba yule mtoto,macho yake yakabadilika gafla na kuanza kumuangalia mtoto yule huku miale ya mwanga ikitoka mwilini mwake kote na kuingia kwa yule mtoto kwa dakika kadhaa,nguvu zake zote alimtupia mtoto yule siku hiyo na kumrudisha pale kitandani na kubaki kumuangalia tu huku akihuzinika,alijuwa kuna wenzake wa jamii yao wengi nao walizaa na wengine kuwapa mimba binadamu wa kawaida na kufanya kizazi chao kianze kusambaa duniani.
Jambo hilo ilipofika hadi kwa wazee wa jamii yao na kukaa mahali wakijikusanya wazee wote wa kichawi na kuanza kufanya maombi kwa miungu yao ikitaka kupoteza nguvu zote za watoto ambao waliozaliwa na binadamu ambao walikuwa na mahusiano na ile jamii yao bila wao kujua ili mtoto akizaliwa awe binadamu wa kawaida,lakini cha ajabu kila wakiomba miungu yao inakataa.Siku hiyo wakiwa kwenye maombi ndiyo siku ambayo yule mfanyakazi aliyezini na Mfalme alikuwa akijifungua naye mtoto huku wazuriati wakitamani awe ni mwanauwe are kuwa Mfalme wao,baada ya Aznaty kurudi ndio akapata kuelezana kuwa Mfalme alikuwa na mahusiano na kijakazi wa pale na leo ndio anajifungua yule mwanamke,kwake ilikuwa ni kawaida kwakuwa hakuwa alimpenda yule Mfalme lakini moyoni aliona ni kama dharau aliyofanyiwa,hakutaka kuonesha ubavu wake hata siku moja maana anaishi kwakuwa amekubali yule kijana awe Mfalme lakini angekataa angeuliwa siku ile na mwanaye kwa minyororo ya kichawi,kwa kuona hilo ndio maana akaamua kuziacha nguvu zake zote kwa mtoto yule aliyezaliwa wa Junior.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule mfanyakazi alibahatika kujifungua na ikawa furaha kwa wasuriati kuona mwanaume amezaliwa na kuona ndio mwanzo wa wao kuimiliki falme..taratibu Mfalme akaanza kupanda juu kwa kutoa amri akitaka yule aliyekaa naye awe ni mke wake wa kwanza baada ya Malkia Aznaty ambaye alikataa kuolewa.Kwa Malkia alibaki kuwa kama zoba hana la kusema desturi zao zinamfunga,hakuwa na nguvu tena baada ya kuona yeye ni dhaifu amedhibitiwa na desturi zao na kuamua nguvu zote kuzihamishia kwa mwanaye wa duniani.Wazee walianza kumkalia kikao Malkia wakiona amekutwa kimya siku zote haumii wala hapingi lolote,ndipo wakaanza kuhisi jambo na kuamua kuzipima nguvu zake...walimfanyia uchawi ambao wanajuwa angeweza kuutegua kuirahisi lakini cha ajabu walishangaa hana analoweza.Wakapata kutambua kuwa Malkia kuna sehemu alipoweka nguvu zake sio bure,taarifa zile zikawafikia hata Mfalme na baba yake,kwao wakiona ndio muda pekee wa kumuangamiza Malkia waweze kuimiliki falme rasmi,wakapanga kumuua kabisa usiku huo,walichukuwa sumu kali sana na kumuwekea Malkia kwenye vinywaji anayopendelea kunywa,vyakula na hata matunda na kuviweka sehemu yake,jioni ilipofika kwa kuwa hana uwezo wowote Malkia Aznaty akivuta chupa moja ya juisi anayopendelea na kuanza kuinywa bila kufahamu lolote,alichukuwa tundra moja na kuenda nalo hadi kitandani na kuanza kulia huku akitafakari mambo yake baada ya Mfalme kuwa chumba chengine na yule mwanamke aliyezaa naye wakibembeleza mtoto,gafla tu yakasikika kelele za wahudumu wakilia kumtaja Malikia Aznaty.,Mfalme kusikia vile waliangaliana na yule mwanamke wake."unaenda kuwa Malkia sasa,ameshakufa huyo"alisema Mfalme na kumfanya yule mwanamke wake atabasamu.
Povu jingi lilimtoka Malkia mdomoni huku taratibu damu zikianza kutoka puani,wahudumu walianza kumfuta huku wakimlilia Malkia wao,mwili wake ulikauga gafla,moyo ulisimama kumaanisha tayari ameshakata roho,rafi zilipiga mfululizo na gafla tu mvua ikaanza kunyesha ya kutisha hadi wazee wenyewe wakaogopa,haraka wakaenda zao kwenye miungu yao kuomba.
Huku duniani nako yapata siku sita sasa yule mwanamke aliyezaa na Junior haonekane,alipotea kimazingira ya ajabu hata hakuna aliyekuwa alikoenda,Junior akawa na kazi ya kulea mtoto mdogo mwenyewe,siku hiyo alimuacha mtoto ndani amelala na kuelekea kuchukuwa mazoea ili aje kumpa mwanaye maana yeye ndio baba na yeye ndio mama,lakini aliporudi alishangaa kuona viatu vya kike pale mlangoni mwake akajipa tumaini atakuwa amerudi mkewe anajifungua mlango na kuingia hadi ndani......alishtuka sana kumuona Aznaty akiwa anamnyonyesha mtoto yule ambaye hakuwa hana hata tabu,Aznaty akiachia tu tabasamu zito baada ya kumuona yule ampendaye hali iliyokuwa tofauti kwa Junior ambaye alibaki kushangaa hata kujikuta chupa ya maziwa ikimdondoka mikononi,Aznaty alimtoka hofu na kumuita asogee karibu yake jambo ambalo kwa Junior lilikuwa ni gumu,alimuweka mtoto kitandani na kumfuata Junior pale aliposimama wakaenda kukaa pale kitandani.Alianza kumweleza mambo yote alivyokuwa tangu siku ile alikoenda kumzika baba yake hadi yeye kuamua na kumfanya Junior awe na hisia zilizompelekea kufanya mapenzi na yule msichana,na ni yeye Aznaty ndiye aliyeoneka mimba ile ya huyu mtoto na kumweleza Junior kuwa mtoto huyu ndiyo yule wa kwao waliyotarajia kumuitajina la Sara,na yule mwanamke aliyezaa na Junior hawezi kurudi tena pale kwa Junior ameenda kuanza maisha yake.Ilikuwa vigumu kwa Junior lakini taratibu akaanza kuamini,alilia sana na kumkumbatia Aznaty wake maana ni muda mrefu hawakuonana na kuona kweli Aznaty ana mapenzi ya kweli,wakarudi na kuanza kunilea mtoto wao.
Baada ya miezi kama sita kupita hali ya Aznaty ilianza kudhoofika taratibu,magonjwa yanamuandama kila kilich na kumfanya Junior awe na wasiwasi kuhusu mkewe.
Kule kwa wasuriati miungu ilikasirika sana na kutaka Mfalme aondoke na viti vya Malkia na Mfalme viachwe wazi huku wakiwapa mtihani wawarudishe mabegi zote za jamii yao zilizosambaa duniani na zoezi hilo lifanywe na yule mtoto wa Mfalme aliyezaa na mfanyakazi wake,basi falme ikaachwa na wazuriati wakaanza kazi ya kuingia duniani kuua watu wanaosadikika ni mabegi zao ili warudi nao kuanza maisha Maya kwenye ile jamii yao.
Usiku wa siku hiyo Aznaty alimuita Junior na kumweleza ukweli kwamba yeye alishakufa kule alipokuwa kwenye jamii yao kwa kupewa sumu,akamueleza hata yale mambo aliyofanya Mfalme kufanya njama ya umuua ili tu wapate kuimiliki falme,alimpa mimba mfanyakazi kusudi aje kuwa Malkia ili wamuondoe kabisa Aznaty.
"Ukweli ndio huo Junior,sina muda sana wa kuishi maana nimepewa kama zawadi tu ya kuishi hadi muda huu.Nakuomba pindi Sara atakapokuwa mkubwa umsomeshe awe kama binadamu wengine japo anauwezo wangu wote na ana nguvu za kupambana na watu wa jamii yangu,atakapofikisha miaka 15,mwambie kuwa ana wenzake anahitaji kuwalinda wasidhulike na hawa wasuriati wanaotaka kuuwa kizazi cha watoto waliozaliwa na jamii yetu huku duniani lengo lako ni kuwachukuwa warudi kuishi kule kwenye falme ambayo sasa inanuka damu ya laana,japo atakuwa bado mdogo lakini haina jinsi mueleze mimi ndiye nimemuagiza na naamini atafanya hivyo."alisema Aznaty na kumfanya Junior aelewe hali halisi.
Na kweli haikupita hata siku kadhaa Aznaty alifariki,alisikia uchungu sana Junior lakini haikuwa na jinsi, taratibu za kuusafirisha mwili wa mkewe huyo zilifanyika na kumpeleka Mkoani Mara ambapo ndipo alipozikiwa Aznaty.....??
(alimaliza kusimulia mzee Junior akiwa na mwanaye Sara wakiwa pale makaburini huku giza likiwa totoro wala hawakujali.)
"Ndivyo ilivyokuwa mwanangu,ndio maana umepewa kazi ya kuwasaidia wenzako ambao hawaelewi kinachoendelea, yule Michael ndiyo mtoto wa yule Mfalme aliyefukuzwa na ndio yeye na mwanaye wanataka kuwamaliza haowatu.Ester na wenzake wote nao walizaliwa kama wewe yaani kama sio baba basi ni mama aliyekuwa na jamii kama ya mama yako,wasaidie wenzako na utokomeze kabisa huu ukoo wa wasuriati,nguvu na uwezo unao umwagiwa na mama yako."alisema mzee Junior na kumfanya sasa aelewe yote aliyoambiwa,kumbe yeye na Michael washindana kuhakikisha mmoja kati yao anakaa kwenye kiti cha kuiongoza falme ile,.
"imekuwaje hadi na mwalimu Eddy naye amekufa?"aliuliza Sara.
"ilikuwa ni adhabu yake,alikuwa akitaka kujenga mahusiano na mwanafunzi Natasha,binti ambaye naye anahitajika kurudi kwenye ile jamii"alisema mzee Junior na Sara akaelewa,akanyanyuka pale alipo na kumsogelea kaburi la mama yake akapiga magoti.
"Pole sana mama kwa ulichofanyiwa...nitakujakuongea na wewe tena kwa kirefu ila wacha nikafanye ulichoniagiza,na naamini nitashinda"alisema Sara na kuamka,akamshika mkono baba yake."tuondoke baba...usiku umeingia..."alisema Sara na kumfanya baba yake anyanyuke na wakaondoka zao usiku ule huku Sara akijua nini cha kufanya.
Kulipopambazuka asubuhi wanafunzi walionekana kama kawaida kusafisha mazingira yao ya shule na baadae wakaingia madarasani kuendelea na vipindi.Ester alimfuata Sara pale anapokaa na kuanza kuongea naye.
" Haya nlienda ile safari yenu uliyoniambia baba yako atakupeleka"aliuliza Ester huku Sasha akiwa anapanga madaftari yake.
"Yah tulienda...ila ilikuwa ni kama surprise kwangu,unajua tangu nijijuwe mimi sijawahi kumuona mama yangu na baba alishaniambiaga kuwa alifariki zamani sana nikiwa bado mtoto,sasa leo ndio alinipeleka alipotokea mama yangu na nafuraha kuona kaburi la mama yangu mmmaana sijawahi kuona hata siku moja."alisema Sasha na kumfanya Ester astaajabu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"siku zote hizo ina maana baba yako alikuficha walau kukuonesha jamani?"
"alikuwa na sababu zake na alinieleza nikamuelewa,sikuwa na shaka naye maana kuna mambo hapo nyuma yalitokea ndio maana akawa kimya"alisema Sasha."na vipi wewe ulipata mtu wa kwenda naye kuzulu makaburi ya wazazi wako?"
"hapana,ilipotoka hapa jana nilienda kwa yule rafiki yangu Sara sikumkuta nkaamua niende tu mwenyewe nikiwa na bibi yangu,tulifanya usafi wenyewe tu wala hakukuwa na shida."alisema Ester na kumfanya Sasha amuelewe,baada ya muda kidogo Madam Magdalena akaingia na kuanza kipindi chake cha Kiswahili.
Masaa yalisogea huku walimu wakiendelea kutoa taaluma madarasani,vipindi vya asubuhi vilipoisha wanafunzi wakielekea kupata kifungua kinywa kwenye migahawa nje ya shule ile kwa baadhi ya wanafunzi waliokuwa na pesa ya kula asubuhi ile,wengine walitulia zao kwenye bustani za shule wakipumzika kwa muda ule wa mapumziko.
Natasha alionekana nyuma ya darasa akiwa na Denis wakiongea mambo yao faragha.
"nyie wanaume nawajuwa hamna ukweli wowote,hapa unaongea maneno matamu lakini nikishakupa unachotaka mnatuona kama takataka."alisema Natasha akiwa ameshikwa mkono na Denis.
"sio wote Natasha,na sidhani kama kuna mwanaume ambaye amempenda msichana kwa dhati ya moyo wake akaja kufanya jambo kama hilo kwa kudhamiria kabisa,hao sio na hawajui thamani ya pendo....Natasha...nimekupenda kwa moyo mmoja na kukubali changamoto zote unazopitia sasa ili tu nikufanye uwe na faraja muda wote,naumia hata mimi kukuona una simanzi, usoni huna raha,naweza kusema huenda nikawa nakujali kuliko unavyojijari wewe Natasha,tafadhari...usinifananishe na wanaume wasiojuwa umuhimu wa kupenda,niamini Natasha nakupenda sana"alisema Denis akiwa anachezea vidole vya mikono ya Natasha,alibaki akitazama tu chini kwa aibu akazidi kumfanya Denis ajiamini,aliinyanyua sura ya Natasha wakawa wanatazamana.
"nakupenda Natasha..."alisema Denis kwa sauti ya akshi hadi Natasha akashindwa kuvumilia kuachia tabasamu baada ya kuyaelea maneno ya Denis.
"Naomba usinifanye niumie Denis,nakukabidhi moyo wangu usinitese"alisema Natasha kwa upole na kumfanya Denis atabasamu,akasogea na kumlaza kifuani akimpa maneno matamu yakiyomtuliza mtoto wa kike.
Yote hayo Michael alikuwa sehemu akiwatazama tu huku akifurahi tu mwenyewe kuona jambo analolikusudia linaenda kukamilika.
Muda huo Sasha alikuwa mahala fulani amekaa akiyatafakari sana yale maneno aliyosimuliwa na baba yake hasa kuhusu kifo cha mama yake na,alijua sababu ya wasuriati ambao ndio wakina Michael walivyokusudia kuwarudisha wakina Ester pamoja na wenzake ambaovinasadikika ni damu ya wasuriati.Moyoni alikuwa na hasira juu ya wasuriati kwa kile kitendo cha kumuua mama yake kwa sumu,aliangalia pembeni na kuona kipande cha chupa,akakikamata na kujikata kiganjani kwa makusudi ikiwa ninkiapo cha kulipiza kwa kile alichofanyiwa mama yake.
Siku hiyo ilikuwa ni furaha kwa upande wa Michael baada ya kuwaweka karibu Denis na Natasha lengo ni kuwamaliza kwa pamoja.
Alitoka darasani kwake na kuelekea hadi darasa ambalo anasoma Natasha,akaingia na kuelekea kwa mwanafunzi mmoja akizuga kumuulizia mambo fulani,alimtazama Natasha akiwa hana habari,taratibu akaanza kunena maneno fulani huku akizidi kumtupia jicho Natasha,hazikupita hata dakika mbili Natasha akaanza kuhisi kitu mwilini mwake,akawa ana tabasamu mwenyewe huku akijikunyata,hali ile ilimfanya Michael ajue jambo alilofanya linaenda vema na taratibu akageuka kuondoka zake.
Hisia za mapenzi zilimtawala Natasha mule darasani,akashindwa kujizuia na taratibu akanyanyuka na kuanza kupiga hatua kuelekea chooni baada ya kuhisi kuna kitu tofauti mwilini mwake.Alipofika tu akashusha sketi yake na kujiangalia,alikuwa amejichafua na kubaki kushangaa hisia zile zinavyompelekesha,moyoni alikuwa huenda ni upendo aliyouanza kwa Denis ndio imepelekea hayo yote,akajikuta akitabasamubmwenyewe kule chooni baada ya kuamini huenda ikawa hivyo.
Huku darasani ikiwa dakika kadhaa muda wa vipindi uiage kwa siku ile,Ester alimfuata kwa mara nyengine Sasha wakawa wanapiga stori zao.
"Sasha..unajuwa wewe ni kama ndugu kwangu,sijawahi kuwa mpweke toka aondoke Sara rafiki niliyempenda sana kwa muda mchache tu,nahitaji na leo nipitie kwenye kaburi la wazazivwangu tena,naomba niongozane na wewe kwa muda mchache tu hatutachelewa."alisema Ester na kumfanya Sasha amuelewe,alikubali na swala hilo wakaliafiki.
Muda ulipowadia wa kuondoka wanafunzi walianza kurudi zao nyumbani Denis alikuwa akiongozana na rafiki yake mmoja wakirudi zao nyumbani,akiwa njiani aliona akishikwa shati nyuma na kufanya ageuke kuangalia,alikuwa ni Natasha akionesha kutabasamu.
"Mbona unatembea haraka hivyo jamani"alisema Natasha na kumfanya Denis atabasamu.
"Ah nipo na jamaa yangu hapa ndio maana...vipi lakini"alisema Denis na kumshika mkono Natasha wakawa wanaendelea kutembea,yule jamaa kawaacha wawili hao wakitembea polepole.Walibadili njia na kupita njia nyengine wenyewe,kwa hisia alizokuwa nazo Natasha taratibu akaanza kumpa hamasa Denis ambaye naye alizipokea hisia zile wakawa wanatamaniana,zile hisia zilizomsumbua Natasha muda ule zikamjia na kujikuta kumkumbatia Denis ambaye alibaki kutabasamu tu.
"Denis..."aliita Natasha kwa sauti laini."
"Niambie.."
"Mmmmmhhhhhhh"alishindwa kujizuia Natasha na kujikuta akimvamia Denis kupeleka kinywa chake mdomoni kwa Denis ambaye naye aliupokea na kubaki wamekumbatiana pale,kila mtu hisia zilimkamata na kuamua kuingia pembeni ya kichaka kila mmoja akiwa na hamu ya kuujuwa mwili wa mwenzake,Denis alijikuta akivua shati la Natasha na yeye akaanza kuvua nguo zake.Gafla tu Natasha akaanza kubadilika,alimkumbatia Denis huku kucha ndefu zikiota gafla vidoleni,alimkamata mgongoni Denis na kuanza kumparua na kucha zile kiasi cha kufanya Denis apige kelele za maumivu,kelele ambayo zilipenya hadi masikioni mwa Sasha akiwa njiani na Ester wakielekea huko makaburini kama walivyopanga,Sasha alisimama na kuanza kuisikiliza ile sauti kwa makini na kumfanya Ester amshangae,Sasha alihamaki na gafla tu akaanza kukimbia kukamata njia iliyoonekana kuingia maporini,Ester alibaki kushangaa hakujuwa nini inaendelea naye ikambidi amfuate kwa nyuma Sasha ajue anaelekea wapi.Sasha aliifuata ile sauti akiisikia mwenyewe mtu akipiga mayowe tu,akazidi kukimbia tu huku Ester akiwa nyuma hadi walipofika eneo la tukio,akabaki kutahamaki,kuona mwili wa Denis ukiwa hautamaniki kwa damu zilizotapakaa kwenye nguo zake,Ester aliogopa sana hadi akajificha nyuma ya Sasha akionesha kuwa na woga moyoni mwake.
"Ah tuondoke Sasha haraka....!!!kesi hii ujuwe"alisema Ester na kumfanya Sara ageuke kumtazama.
"ina maana humjuwi huyu ni nani?na moyo wako umeridhia kabisa tumuache,hebu mtazame vzuri!"alisema Sasha na kumfanya Ester aangalie vizuri tena sura ya yule mtu,alishamjuwa ni Denis lakini moyo wake ulikuwa una hofu sana hakutaka tena kukaa pale.Sasha alimsogelea Denis pale chini na kuanza kukagua vizuri mwili wa Denis bila woga na kumfanya Ester amshangae kwa kuwa na ujasiri ule,alianza kuuangalia vizuri mwili ule ukionesha kujeruhiwa sehemu nyingi hasa mgongoni na shingoni,akiikumbuka ile ndoto ya siku ile ikimuonesha Denis akiwab porini huku mwili weak ukiwa hautamaniki kwa damu,Leo ndio kweli anaona kile kitu,akabaki kuushika kifuani kwa Denis kuonesha mapigo ya moyo kusimama kabisa kuashiria amekufa,hakutaka kabisa kuamini kama amekosa mtu wa pili tena,ikambidi atulie akimtazama tu mwili ule ukiwa pale kichwani.Ester alibaki kumshangaa sana Sasha maana hakutegemea kama anaweza kuwa na moyo wa ujasiri kama ule wa kumsogelea mtu aliyekufa,akabaki akimtazama tu Sasha aliyekuwa amepiga magoti karibu na ule mwili wa Denis,Sasha alimtazama Denis sana na kugeuka kumtazama Ester,aliona liwalo na lile,akageuka kumtazama Denis na kuanza kunyanyua mkono wake na kuuweka kichwani kwa Denis.
"#di_ahora_nitro_gen_akgouraawq"aliyanena maneno hayo kwa sauti na kuyaridia mara tatu mfululizo huku alipata sauti,mwanga mikononi mwake ulitoka na kuingia kwenye paji la uso kwa Denis na kuanza kusambaa mwili mzima hali iliyomfanya Ester atoe macho huku akishika mdomo kwa taharuki,taratibu kikaonekana kivuli cha kiume wa ajabu aliyeonekana kama mzimu ulitoka kwenye mwili wa Denis kana kwamba unabutua japo wenyewe ukitaka kuingia tena,Sasha alibadilika macho na kuwa makali kama paka huku akikuangalia kivuli kile na kumtemea mate muda ule ule kikawaka moto na kupotea gafla.Muda huo huo Ester alishangaa kumuona Denis anakohoa damu pale chini,damu iliyo nyeusi na papo hapo akafumbua macho yake na kuona tena dunia,alitazama pembeni na kuiona sura ya Sasha ikiwa kwenye macho makali,akaanza kuogopa lakini Sasha akamtuliza huku alifuta zile damu kwa kitambaa chake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda wote huo Ester hakuamini kumuona ni Sasha ndiye
0 comments:
Post a Comment