IMEANDIKWA NA : JAFARI MPOLE
*********************************************************************************
Simulizi : Sara (Msaada Wa Mateso)
Sehemu Ya Kwanza (1)
Wanafunzi wote walianza kusogea paredi baada ya kengere kusikika ikiwaamuru wafike eneo hilo kupata mawili matatu kabla ya kuingia darasani kuanza vipindi vya asubuhi ile ya Jumanne.Mwalimu Isack ambaye ni mwalimu wa taaluma katika shule hiyo ya Butiama Secondary School mkoani Mara,alikuwa ni mwalimu wa zamu kwa wiki hiyo na kusimama pale mbele ya umati wa wanafunzi ambao walikaa kimya na kuanza kuzungumza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Habari ya asubuhi"alisalimia wanafunzi na wakamuitikia kwa kumpa heshima yake na akaipokea.
"Tushukuru Mungu tumefika salama leo na kama kuna anayeumwa Mungu amsaidie apone haraka,yah jana nakumbuka nilitoa tangazo kuhusu kuleta maji ili tumwagilie miti tuliyoipanda na bustani,wote mmeona kulivyo kukame maana huku maeneo ya shule ni shida ndio maana jana tuliwaruhusu mapema mkatafute maji mlete tumwagilie hii miti....sasa kama unajijuwa huna maji...tafadhari usitake tutafutane huko wewe ruka mbele huku haraka"alisema Mwl.Isack na kauli yake hiyo ikawafanya wanafunzi waanze zogo huku taratibu baadhi yao wasiokuwa na maji wakitoka mbele.Walimu wanne walitoka ofisini wakiwa wameshika burungutu la fimbo na kusogea pale paredi hali iliyofanya wanafunzi wengi wastaajabu huku idadi ya wasiokuwa na maji ikiongezeka.Taratibu walimu wakaanza kukagua galoni za maji kwa wale walioleta maji siku hiyo na kuwasogeza sehemu moja wawe mbali na wale wasioleta,walimu waligawana majukumu na kuanza kuwaadhibu wale wakaidi kwa kuwachapa bakora 4 za nguvu kila mmoja huku wakiwarudisha wakalete maji ndio waingie madarasani..
"kama huyu yupo karibu na kisima kwao lakini hakubeba maji...njoo hapa Ester"alisema mwalimu mmoja akimuita mmoja wa wanafunzi wale,Ester alimaogelea mwalimu yule akiwa amekuja sura.
"Mwalimu mimi nili..."hakumalizia sentensi akashuhudia bakora ikitua begani kwake.
"sitaki porojo nyoosha mkono haraka ukalete maji"alisema mwalimu yule.
"Nisikilize basi mwalimu....jana mwenye kisima hakutaka kuuza maji yake hivy..."
"aisee unajua unanichelewesha...."
"yaani wewe kila siku huishiwi visingizo leo lazima tukuadhibu,mlete hapa"alisema Mwl.Isack na kumfanya yule mwalimu amkamate mkono Ester akimsogeza kwa mwalimu huyo wa taaluma na alipomkamata tu Ester akaanza kufurukuta kwa uwoga wa fimbo huku mguu wake mmoja kuonekana kuwa na tatizo,hakupenda kabisa kupigwa kwa uwoga wake hali iliyofanya hata Mwl.Isack abaki akimtazama tu maana kwa hali ile asingeweza kumuadhibu ikambidi ampe adhabu pale assemble apige magoti huku wanafunzi wale walioleta maji waingie madarasani.
"na leo utakaa hapa uite mvua mpaka ije ndio unyanyuke uingie darasani,si unajifanya wewe hutaki kupigwa sasa unashika adabu leo...nyanyua mikono hiyo ita mvua"alisema Mwl.Isack na kumfanya Ester ainyanyue mikono yake huku akikunya sura kuichukia adhabu ile,walimu wote wakaingia ofisini na kuchukua vitabu vyao kujiandaa kuelekea madarasani,hata walipotoka walimpita tu Ester pale paredi akiwa amepiga magoti huku mikono ikiita mvua ambayo kwa ukame wa kipindi kile kwa jua lile hakukuwa na hali wala dalili ya kutokea mvua kwa muda ule.
"Denis hayo siyo mapenzi...we wifi anasurubika pale assembly wewe hata kuumia wala kumjali yaani dah"alisema mwanafunzi mmoja wa kike aliyetambulika kwa jina la Magreth na kuwafanya wanafunzi wa darasa lile la Form 3A waangue vicheko na wengine walipiga mayowe hali iliyomfanya Denis abaki akimtazama Magreth.
"Hivi "Magaga" unanitafuta nini mimi,tangu umeota Mavuumba unaongeeeea mwenyewe unaona sifa,tafadhari achana na mimi boya wewe!!"alilalama Denis baada ya Magreth kusema mbele ya darasa mahusiano yake na Ester.
"Asa unakasirika nini kaka mbona unanitania mimi Magaga na sikasiriki kwakuwa ninayo miguuni,halafu kwani uongooo si ukamuombee basi hata msamaha jamani mwenzako anaumia pale maskinii"alisema Magreth huku akitabasamu kwa utani, Ile hali iliyomfanya Denis azidi kukasirika na kutaka kumfuata ampige lakini wenzake walimzuia huku Magreth aliona ni utani tu na kuzidi kucheka.
"mwalimu huyo!!"alisema mmoja wa wanafunzi na kuwafanya wenzake warudi sehemu zao na kutulia,akaingia mwl.Isack na kuendelea na kipindi chake cha History.
Huku nje Ester alizidi kuitumikia adhabu yake isiyokuwa na muda mwalimu,alijitahidi kukaza mikono isishuke lakini baada ya muda akajikuta anashindwa ingawa anaendelea kujitahidi kuinyanyua mikono huku jasho likimtoka jua kali linapiga asubuhi ile ya saa mbili na nusu.Akiwa kwenye adhabu hiyo kuna mwanafunzi wa kike alionekana kuingia shuleni pale na taratibu akaanza kupiga hatua kusogea mbele huku macho yake yakiangalia majengo ya shule ile kila sehemu yakiwa yamependeza sana,alionekana ni mgeni ndio anawasili shuleni pale na alimuona mwanafunzi akiwa amepiga magoti na alikuwa ni Ester aliyekuwa akizidi kuita mvua tu kwa uchovu,yule mwanafunzi mgeni alimtazama Ester kisha akatazama juu mbinguni kukionekana jua linawaka.Alimtazama Ester na taratibu akamsogelea pale alipopiga Magoti.
"Pole sana Ester ..."alisema yule mwanafunzi na kumfanya Ester ageuke kumtazama,hakuweza kumjuwa kabisa na kubaki kushangaa.
"Wewe ni mgeni?"aliuliza Ester.
""ndio...mimi ndio nafika leo shuleni hapa."alijibu yule mwanafunzi.
"Haah!!sasa umenijuaje kama naitwa Ester.?"
"nimekujua kwakuwa unaitwa Ester Philemon "alisema yule mwanafunzi akimuita kabisa jina la baba yake na Ester ,alistaajabu sana Ester ikambidi amtazame yule mwanafunzi kwa makini.
"usijali utanijua tu taratibu,jiandae uende darasani kipindi kinakupita mimi ngoja nkaonane na mwalimu mkuu nipate muongozo wa hapa,baadae..."alisema yule mwanafunzi na kupiga hatua kuelekea ofisini kwa mwalimu mkuu huku akizidi kuangalia mazingira ya shule ile kama mgeni,alipopiga hatua kadhaa mbele hali ya hewa ikabadilika mawingu yakajaa na kuwa meusi ghafla na mvua kuanza kunyesha tena kali,Ester alibaki kushangaa ile mvua na kubaki akifurahi,haraka akanyanyuka na kukimbilia darasani kwake maana adhabu yake iliyekuwa kuisha mpaka mvua inyeshe na sasa imenyesha kweli,alipofika kwenye korido kabla hajaingia darasani aligeuka nyuma kumtazama yule mwanafunzi aliyeelekea ofisini kwa mkuu,alimuona amesimama naye nje ya ofisi na kuanza kumpungia mkono Ester ambaye alibaki akimshangaa yule mgeni .
"amelijuaje jina langu?...amelijuaje jina la baba yangu?....mbona kaniambia nijiandae kuingia darasani na mvua ikanyesha gafla?ina maana alijua kuwa ikanyesha?mmhhh huyu ni nani?"ni maswali ambayo Ester hakuyapatia majibu muda ule huku mvua kali ikizidi kunyesha muda ule.
NI NANI HUYU MWANAFUNZI?
Yule mwanafunzi aliingia moja kwa moja ofisini kwa mwalimu mkuu baada ya kupiga hodi akaingia hadi ndani ambapo alimkuta mkuu wa shule hiyo akiwa anaandika ripoti za kazi zake,akasogea na kukaa kwenye kiti baada ya kumsalimia mkuu wa shule kisha akafungua begi lake na kutoa bahasha ya kaki na kumkabidhi mwalimu ambaye aliifungua na kuanza kutoa karatasi zilizokuwa kwenye bahasha ile na kuanza kuzisoma kwa muda machache tu akapata kufahamu.
"ahaa kumbe ndio wewe,baba yako alikuja Ijumaa niliongea akasema atakuleta leo."alisema mwalimu mkuu aliyefahamika kwa jina la Malamba.
"ndio,alipaswa kunileta lakini hali ya afya yake alivyoamka haikuwa sawa ndio akaamua kunikabidhi hivi vithibitisho vya uhamisho nikuletee Mwalimu"alisema yule mwanafunzi.
"aisee mpe pole yake ukirudi....jina lako ndio Sara....!"
"ndio mwalimu....naitwa Sara Junior Temba."alijitambulisha Sara.
"sawa...nlitaka kupata uhakika wa jina lako,nakuona hapa limeandikwa kama ulivyolitamka,basi haina shida karibu sana shuleni kwetu na kuwa na amani muda wote na ufuate zile sheria zote za shule kama inavyotakiwa,ukitoka hapa utapitia kwenye ubao wa matangazo usome sheria 20 za shule yetu ya Butiama Secondary,unapaswa kuzifuata na kuzitii muda wote na kwakufanya hivyo utakuwa ni rafiki na mwanafunzi mzuri hata kwa walimu watakupenda Sara"alisema mwalimu mkuu Malamba.
"nimekuelewa vema mwalimu"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"basi sawa nitamuita kiongozi wa darasa lako atakuchukuwa akuelekeza mahala pa kukaa darasani"alisema mwl.Malamba na kunyanyuka kuelekea nje,alimuagiza mwanafunzi mmoja akamuite kiongozi wa kidato cha 3 aje ofisini na yeye akarudi ofisini kwake kukaa akiendelea kuongea na Sara.
Muda mchache baadae akapiga hodi mwanafunzi mmoja nakuingia ofisini kwa mwalimu mkuu.
"Good morning Sir..!"alisalimia yule mwanafunzi.
"Morning how ar you? "
"I'm well"alijibu yule mwanafunzi na kusimama kumsikiliza mkuu.
"nilikuona muda fulani ukiwa umepiga magoti pale assemble....what's happen there?"aliuliza mwalimu mkuu akiwa anaandika mambo yake.Maneno yake yalimfanya Sara ageuke kumtazama yule mwanafunzi na kutambua kuwa alikuwa ni Ester ndio muda ule alimuambia ajiandae kuingia darasani.Hata Ester mwenyewe alipomuona Sara alibaki kuangalia chini tu akitaka kumjibu mwalimu.
"Nilikuwa ninakosa,sikuwa na maji ambayo tuliagizwa tulete"alisema Ester.
"na una bahati mvua imenyesha"alisema mkuu na kumfanya Ester amtazame Sara kwa kuibia ibia.
"sasa fanya hivi Ester,huyu mtakuwa naye darasani ni mgeni na anahitaji ushirikiano wenu darasani,kamtafutia kiti na meza umuwekee sehemu yake sawa"alisema mkuu.
"Sawa mwalimu nitafanya hivyo"
"hiyo rozali yako nilikuambiaje Ester?!"alisema mwalimu na kumfanya haraka Ester aivue ile rozali na kuiweka ndani ya mfuko wa sketi.
"haya ongozana naye apite hapo kwenye ubao asome sheria za shule kisha uende naye darasani,"
"sawa mwalimu"alijibu Ester na kuongozana na Sara wakapitia kwenye ubao wa matangazo akamuacha Sara akianza kusoma sheria za shule ile kama zilizo orodheshwa kwenye karatasi maalumu iliyochapishwa nabkubandikwa pale ubaoni.Ester mida wote alikuwa nyuma amesimama akimtazama tu Sara akiwa anasoma zile sheria,Sara alisoma sheria zote 20 na alipozimaliza akabaki akitabasamu tu huku akigeuka nyuma kwa Ester ambaye naye aliongoza njia kwenda darasani.
Walipoingia tu darasani ndio mwl.Isack alikuwa anatoka baada ya kumaliza kufundisha somo lake la History.
"Huyu ni mgenieee"aliuliza Mwl.Isack baada ya kumuona Sara akiwa na Ester pale mlangoni wakitaka kuingia darasani.
"Ndio mwalimu"alijibu Ester.
"Karibu sana...unaitwa nani?"
"Naitwa Sara"
"Haya karibu...ila uwe na nidhamu shuleni maana ukiwa ni jeuri dawa ninayo mimi utanyooka tu,haya ingieni darasani"alisema Mwl.Isack na kuondoka zake,Sara akimtazama yule mwalimu kwa jicho la aina yake na baadae akaingia darasani akiongoza na Ester.
"mlete kwa hapa Ester akae kuna nafasi"
"Meza na kiti hivi hapa Ester aje akae hapa"
"na nyie msione mwanamke mbili yenu inawasha msivyo na aibu,watoto wa kike kibao humu darasani wamejaa mmewashindwa mnajifanya vidume waone"alisema mwanafunzi mmoja aliyefahamika kwa jina la Aisha.Ester aliwaangalia tu na kubaki akitabasamu,alichukua kiti kimoja na kuweka sehemu pamoja na meza kwa pamoja na kumuita Sara akae pale.
"Haya sasa Hilali useme huna bahati..."walisema wavulani kadhaa wakimwambia mwenzao ambaye ndoto Sara aliwekwa karibu yake,akabaki akicheka kwa utani wa wenzake.
Sara alikaa kwenye kiti na hapo hapo akatia daftari moja kwenye begi lake na kuliweka mezani kwa kulifunua,alitoa peni yake na kuanza kuandika mambo yake hali iliu wafanya baadhi wa aliachana wenzake wakunje midomo kumuona kama anajishauwa kusoma.
"Wasomi mpoo..!hiyo ni salamu jamani..."alisema msichana mmoja na kufanya nusu ya darasa kuangua kicheko hali iliyomfanya Ester ashindwe kuvumilia kama kiongozi wa darasa.
"Jamani hebu tukue basi...mnapiga kelele kama watoto wa msingi!sasa kipi cha kushangaza hasa,hebu acheni mambo yasiyo na msingi."alisema Ester kwa ukarimu.
"haya sawa mama mchungaji,mwambie asimame basi ajitambulishe tumjuwe."alisema mwanafunzi mmoja wa kiume na kuwafanya baadhi ya wenzake wamuunge mkono kwa alichokisema..Akiwa anataka kujibu Ester aliona tu Sara amesimama na kusogea mbele ya darasa amesimama.
"Sawa,nipo hapa kwa ajili ya kujitambulisha...naitwa Sara Junior,ni mgeni na ndio naingia leo hapa shuleni kwahiyo naombeni ushirikiano wenu mimi ni mwanafunzi mwenzenu wa darasa hili."alisema Sara kwa tabasamu lililoonesha uzuri wake wa asili,darasa lilimpigia makofi kama kumkaribisha,alifurahi na kurudi zake kukaa na kuendelea zake kuandika mambo yake,wengine wakaendelea na kujisomea na wengine wakipiga tu stori.
"mimi watu wanaojishauwa siwapendi,yani unaingia tu darasani siku ya kwanza unajionesha kuwa wewe ni msomi saaana ili tukuogope au!!"alisema msichana mmoja akiwa na wenzake wanne wakiweka genge la umbea.
"Sasa na lile lihereni na shule wapi na wapi anajua kutuletea usistaduu humu"alidakia mwengine wakizidi kumsengenya Sara.
"mmmh na nyie mmezidi kwa umbea,mtu katokea ofisini kwa mkuu akiwa vilevile yeye hajamuona kwani?tupunguze mdomo loh!"alisema mmoja wao na kuwafanya wenzake wanyamaze kuona lisemwalo ni kweli.Sara alikuwa anacheza tu na karamu akiandika kwenye daftali lake.
Vipindi viliendelea baadae na hata muda wa mapumziko ulipofika wanafunzi wote walitoka madarasani na kwenda kupata chai kwenye migahawa ya wanakijiji pembezoni na shule huku wale wasiokuwa na pesa wakipumzika tu kwenye bustani za shule wakisubiri muda ufike waingie darasani,Ester alikuwa miongoni mwa wanafunzi hao ambapo alitafuta mahali na kukaa pekeake akiimba na kumsifu bwana Yesu kwa imani yake,hisia zilimfanya hata afumbe macho kwa ile imani anayoihisi ikitawala kwenye roho yake huku akiwa ameishikilia rozali yake,hata alipofumbua macho yake tu akamuona mbele Sara akiwa amesimama huku ameshika mkate kwa tabasamu.
"una sauti nzuri sana Ester Mungu amekubariki kwa hilo"alisema Sara na kuukata kati mkate ule,akanyoosha mkono wake kumpatia Ester kipande kimoja,akakipokea huku akimtazama Sara.
"unaniruhusu nikae nawewe tafadhari!"alisema Sara na kumfanya Ester atabasamu na kumruhusu wakae pamoja.
Akaanza kuangalia mandhari ya shule ile iliyokuwa imetanda wanafunzi kila kona kwa muda ule wa mapumziko.Waliongea mambo mengi sana ya kielimu na hata baadae Ester akahitaji kumjua zaidi Sara.
"hivi Sara kabla ya hapa kufika ulikuwa unaona shule gani?"aliuliza Ester huku Sara akiwa anatafuna tu mkate akiyatazama mazingira ya shule,kulikuwa kimya kama dakika moja hivi kasi cha kumfanya Ester amtazame Sara vizuri akihisi huenda hakusikia.
"mandhari ya huku ni nzuri sana na nimeyapenda kwakweli tofauti na kule nilikotoka Ester,huku kuna amani,watu wametulia na nahisi nitaishi nao kwa furaha,"alisema Sara na kumtazama Ester."mimi ni rafiki yako Ester naomba tuwe pamoja,tutafika mbali,turudi darasani muda umeisha wa kukaa nje"alisema Sara na muda huo huo kengele ikagongwa kuamrisha wanafunzi waingie darasani muda wa mapumziko umeisha,Ester alibaki njia panda juu ya Sara kwa maneno yake aliyoyaongea bila kujibu swali aliloulizwa."huyu mbona simuelewi?"alijiuliza mwenyewe Ester bila kupata jibu,akaamua kumalizia mkate wake kisha akaingia darasani na muda ulipofika vipindi vikaendelea.
Wakiwa kwenye kipindi kuna wakati Ester anamtazama tu Sara aliyekuwa mbele yake upande wa kulia na kubaki akitabasamu kwa umakini anaouonesha Sara kumsikiliza mwalimu,alipenda sana watu anapoenda kusema na kujituma kwenye taaluma yao na ndio alivyosema rafiki nao siku zote huku akijipa tumaini kuhusu Sara huenda akawa miongoni mwa marafiki zake anaowahitaji.Vipindi viliendelea hadi mchana na muda ulipoisha iligongwa kengele kama kawaida na wanafunzi walianza kutoka madasani kuelekea paredi kupata matangazo kabla hawakupata ruksa ya kuelekea majumbani kwao.Mwalimu Isack alisimama na kuongea mawili matatu huku hali ya hewa ikionesha kuna dalili za kunyesha mvua,alizungumza machache na wanafunzi wakaruhusiwa kurudi makwao.Wachache walikuwa wakikaa vijiji vya karibu na shule huku wengi wao wakikaa Rorya mbali kidogo na shule,Sara alikuwa miongoni mwao naye akianza safari ya kutembea kurudi nyumbani,Ester alipata kumuona Sara akiwa mbele kidogo na kumfanya amkimbilie kuongea naye.
"mbona unatembea haraka sana?"aliuliza Ester baada ya kumkuta Sara na kuanza kutembea wote.
"Ah kuna kazi za kufanya nahitaji niwahi kuzifanya."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Eh lakini mama yako si anaweza kukusaidia kufanya baadhi ya kazi?"aliuliza Ester na kumfanya Sara amtaze kidogo na kuendelea kupiga hatua bila kujibu.Hali ile sasa ya kukaa kimya ikamkera Ester maana sio mara moja kunyamaziwa,akamkamata Sara mkono gafla wasimame.
"Mbona una tabia mbaya Sara kila ninalokuuliza hujawahi kunijibu,tatizo nini?"alisema Ester kwa ukali kidogo hali iliyomfanya Sara akasirike na kujikuta akibadilika gafla macho kwa sekunde kadhaa kwa hasira na baadae yakarudi hali yake na hasira zile zikatokomea gafla hali iliyomfanya Ester atahaluki kwa kuachama mdomo baada ya kuona macho ya Sara yakiwa tofauti na kawaida.Hata Sara alielewa kuwa Ester ameiona hali ile akautoa mkono wa Ester na kugeuka kupiga hatua za haraka kuondoka zake huku akitoa kitambaa chake kujifuta macho yake....
Njia mzima Sara alijutia kuonesha wazo hasira zake zilizomfanya aonekane muonekano wake akikasirika,mbaya zaidi hata Ester amepata kutambua hali ile,alijutia sana huku akizidi kutembe njiani akielekea nyumbani.
Na kwa Ester ni hivyo hivyo,hakuamini kile kitu alichokiona huku akitembea taratibu njiani akitafakari.
"Sara atakuwa ni mtu wa aina gani?au ni jini?"akijiuliza Ester mwenyewe akilinganisha na matukio ya nyuma aliyohisi muhusika atakuwa ni Sara kwa siku ile mvua kuonyesha gafla hata akijiuliza shule alipotokea anajibu mambo mengine kumaanisha hataki undani wake.
"ushindwe kwa jina la Yesu....pepo lipite mbali nami daima damu ya Yesu itanilinda na kuniongoza milele."alikemea sana Ester baada kuamini huenda Sara si mzuri kwake.Gafla akajikuta akishikwa mkono na kumfanya ashtuke sana huku akigeuka kumtazama aliyemshika,alikuwa ni rafiki mmoja wa Denis aitwaye Frank.
"Ah shem vipi.."alisema Frank huku akiwa anatabasamu.
"Frank nakuona tena sana mtaani yenu yaishe kuanzia leo nitawaripoti kwa mwalimu mkuu mpewe adhabu munichukie,nawaheshimu sana mjuwe "alisema Ester akijuwa wanamdhihaki kwa kuwa mguu wake mmoja ni mfupi kidogo uliyomfanya atembee kama kilema.
"asa Ester ukatusemee kwa kisa gani?jamaa kafa kaoza kwako ujue."
"usiniambie upumbavu wenu,kama kafa si mumzike mnaniambia mimi nina mazoea naye, tena nasema mara ya mwisho ukiniambia ujinga wenu sikwepeshi napeleka taarifa kwa mkuu."alisema Ester akionekana kuchukizwa na tabia ile ya akima Frank ambaye alivyoambiwa hivyo akapoa na kumuacha Ester huku akitabasamu kwa kumtania,akapiga hatua mbele na kuungana na group la wenzake akiwemo Denis mwenyewe.
"Dah aisee Denis shem wetu mkali kweli nmeongea naye kakasirika mpaka kanitishia kwenda kwa mkuu n kaona isiwe tabu nkamuacha"alisema Frank na wenza wakawa wanacheka tu.
"achana naye anajiona Queen hana lolote na uchiba wake ule,mimi nlitaka kukata nyuzi nitembee si anasema mlokole yule ana bk,angekubali kunipa tu ningemtema mapema siwezi kutembea na chiba mim i wakati mademu wakina kibao wapo kiskuli"alisema Denis kwa kujiamini na wenzake wakamsapoti na stori zai zikawa ni za wanawake tu mpaka wanafika makwao.
Sara aliweza kufika kwao ambapo alikuwa anaishi na baba yake tu ambaye kweli alikuwa anaumwa,hivyo baada ya kumsalimia na kumjulia hali akienda kubadilisha nguo za shule mchana ule na kuanza kuongea jikoni kuandaa chakula huku akisogeza vyombo kuviosha,hadi jioni ilipofika alishamaliza kazi zote za pale ndani ikiwa ni pamoja na kufika nguo zake za shule,akaandaa chakula mezani na kumuona baba yake wakae wale.Baba yake alikuwa mzee umri umekwenda kidogo ,alijifunika blangeti kwa kuhisi baridi hali ya kuwa hakukuwa na baridi sana yote ikiwa ni hali ya kuumwa,wakakaa na kuanza kula pamoja.Sara akaanza kukumbuka BAADHI ya matukio ya siku ile akianza kuingia shule,akiwa darasani,akiwa na Ester hadi wakati wa kuondoka alipokuwa naye Ester kukatokea hali ile ya hasira,akabaki akivuta pumzi na kuishusha baada ya kujua alikosea.
"jaribu kuzuia hasira zako Sara,umeanza shule tena yale mambo uliyoyafanya kipind kile sebuleni acha,soma tuliza akili yako ukijua unawaangali yule binti na wenzake.Hasira za haraka ziache kabisa,ona sasa ameshakuwa na wasiwasi na wewe baada ya kuonyesha hasira zako,yataka kumuelewesha kweli kweli hadi akuelewe akuamini"alisema mzee Junior akitazama mwanaye,alishafahamu yote yaliyotokea shuleni kwa mwanaye.
"Sikutaka afahamu ndani wangu kwa sasa ndio maana alivyokuwa akinilazimisha nlikasirika,lakini nlishakwambia baba hizi nguvu za m......."
"shhhhhhhhh......usiseme tena maneno hayo,hiyo ni bahati mwanangu uliyozaliwa nayo hupaswi kuichukia,kikubwa ni kujizuia mwenyewe naamini utakuwa mtu wa watu"alisema mzee Junior baada ya kuona mwanaye akaanza kuongelea kutozipenda nguvu ile ya kichawi aliyokuwa nayo.
Sara alibaki ameinamia tu kwenye meza huku akibembelezwa na baba'ke kula.
Huku kwa Ester usiku wa siku ile kabla hajalala akapiga magoti karibu na kitanda na kuanza kupiga maombi sana baada ya kupata na mashaka moyoni mwake.Ilimchukuwa nusu saa nzima kukemea mabaya na kuiombea familia yake izidi kuwa na amani milele na alipojirizisha akapanda kitandani na kuutafuta usingizi.Muda wote akiwa kitandani alikumbuka tu Sara siku alipoingia shuleni akafanya tukio la ajabu ambalo kwa Ester aliamini muhusika ni Sara,kwa upande fulani alimchukulia ni rafiki mzuri sana kwake hasa muonekano wake na maongezi yake lakini kitendo cha kubadilika macho kuwa kama macho ya jini yakianza kumuogopesha Ester na kuhisi huenda Sara si mtu wa kawaida na kuna jambo linaloendelea maana amekuja shuleni gafla,alijipa moyo kwa kuwa moyoni anaamini analindwa na Yesu na punde tu usingizi ukamchukuwa.
Asubuhi ya Jumatano wanafunzi walisogea maeneo ya shule huku baadhi yao waliowahi akianza kufanya usafi,muda ilipofika walisogea Paredi baada ya kengele kugongwa walipata matangazo kutoka kwa walimu na baadae akaingia darasani kuanza vipindi.Walimu walijitahidi kuingia kwenye vipindi vyao kwa wakati kila darasa kuhakikisha wanatoa elimu iliyo bora na inayoeleweka kwa kila mwanafunzi.Mida ulienda na kengele ya mapumziko ilipolia wanafunzi kama kawaida walielekea kupata chai.Siku hiyo Sara alikuwa ametulia sememu karibu na mti wa mjohoro akipumzisha akili yake,alishuhudia kuona Ester akisogeza upande ule aliko nabkujua lazima atakuja kuuliwa jambo lile lililotokea jana.
"Mbona umekaa huku mbali na wenzio?"aliuliza Ester akionesha tabasamu lislo na woga usoni mwake.
"Ah nimeamua tu,nimeipenda sehemu hii ndio maana.."alisema Sara akitazama pembeni,aliona alichokifanya jana si izuri hasa kwa Ester na kuhisi akakuona ni mchawi.
"Sara...."aliita Ester na kumfanya Sara ageuke kumtazama.
"Hakika bwana Yesu anakupenda,na amenipa maono kwamba utakuja kuwa msichana mzuri sana kwa jamii."alisema kwa pole Ester na kumfanya Sara ajue yote anayosema ni kwaajili ya lile jambo la jana lililotokea.
"Ester....naomba unisamehe kwa kile kilichotokea jana maana hata mimi sijielewi ilikuwaje,na sio kwamba napen a kuwa vile."alisema Sara kutoka moyoni na kumfanya Ester amsogelee na kukaa karibu yake akashika bega.
"hebu niambie ukweli Sara usinifiche maana mimi ndio rafiki kwako hapa shuleni,...ni kweli una nguvu za kishetani??"aliuliza Ester na kufanya ile hereni aliyovaa Sara kucheza cheza mfululizo hadi akashangaa,Sara akainama chini na kuishika ile hereni ikatulia,akanyanyua uso wake na kumtazama sasa Ester kwa macho yale ya kijini hadi Ester akaogopa kutaka kukimbia lakini akamshika mkono.
"Ester usinikimbie tafadhari maana siku nitakapokukimbia wewe unaumia sana,nizoee hivi nilivyo ndio hivi hivi,sikupenda kuwa hivi ila nimezaliwa nikiwa hivi."
"ni habari sana Sara ujue,naogopa..."
"Usiniogope Ester,sijawahi kufanya kitu kibaya kwa mtu hata siku moja ila inaponibidi nafanya japo naumia maana mimi si mtu wa kawaida kama wengine,Nina hasira sana tena sana,hii heleni tangu nazaliwa hadi kukua kwangu haijawahi kutoka sikioni mwangu na ndio kitu pekee kinachozuia hasira zangu na baba alinambia endapo nikiivua sitakuwa Sara tena na sijui nitakuwa kiumbe gani,hivyo nakwambia yote haya kama rafiki yangu naomba usiniogope,nampenda kumjua zaidi Mungu wangu,napenda sana kuwa kama wewe lakini najikuta nakuwa tofauti sana na nyie hata mimi sijui kwanini,tafadhari usinikimbie Ester."alisema Sara huku alitoa machozi kwa macho yale ya kutisha.
Ester alijikuta akielewa tatizo alilonalo Sara hivyo moyo wake ukajikuta ukiwa na amani baada ya kuyaelewa maneno ya Sara,akamsogelea na kumkumbatia kama kumfariji hali uliyomfanya Sara afarijike na punde tu macho yake yakarudi hali ya kawaida.Ester alimuachia Sara na kumtazama usoni na kuona hali ya macho yale yametoweka na kurudi kama awali,akabaki anatabasamu tu kuona ni hali ya kawaida.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"nimekuelewa Sara,nitakuwa nawe muda wote rafiki yangu"alisema Ester.
"nashukuru kwa hilo"alijibu Sara kwa tabasamu na gafla tu wakasikia makelele makali kwenye darasa moja,wanafunzi waliokuwa amekaa mule darasani walianza kukimbia ovyo.Haraka Ester pamoja na Sara wakanyanyuka na kuanza kukimbia kuelekea eneo la tukio...
Walipofika eneo lile waliona wanafunzi wengi wamejazana eneo lile la darasa la kidato cha kwanza.
"Eti kuna nini?"aliuliza Ester kwa mwanafunzi mmoja aliye pembeni yake.
"Yule Natasha wa Form one amepandisha mashetani,ananyanyua vitu na kuvitupa tupa humo ndani hadi wenzake wamekimbia na kumuacha mwenyewe humo"alisema yule mwanafunzi kwa sauti kidogo hadi Sara akasikia.Kwa kujiamini Ester akaanza kusogea kwenye lile darasa huku akiwaambia wenzake wampishe aingie.
"Mpisheni aingie"ilisikika sauti ya mwalimu wakike Madam Magdalena na kuwafanya wanafunzi waache njia Ester akapita na kusimama mlangoni akimtazama Natasha akiwa amefura akirusha viti tu.
"UHIMIDIWE BWANA MUNGU ULIYE MBIGUNI,KWA JINA LAKO BABA NAKEMEA MAPEPO YA BINTI HUYU NATASHA YAWEZE KUTOKA MWILINI MWAKE AWE SALAMA,AWEZE LITOKA KWENYE KIFUNGO CHA SHETANI NA KUWEZA KULITUKUZA NA KULITAKASA JINA LAKO.....PEPO TOKA,MUACHE NATAKA ASOME,MUACHE HURU NATASHA AISHI KWA AMANI....TTTOKKAAA"alikemea sana Ester na kuzidi kuomba huku Natasha akionekana kucheza kwa dharau asikiapo maneno yale japo alionekana kudhoofika na kujikuta akienda chini na kuanza kulia,Ester alimsogelea na kumshika kichwani na kuendelea kumwaga maombi ya nguvu yaliyochukuwa muda kidogo,walimu wakawaamuru wanafunzi wengine waingie madarasani huku wanafunzi wa Form one A wa darasa lile la Natasha wakichanganywa na wenzao wa B,hata Sara naye alirudi darasani kwao akimuacha Ester akiendelea kutoa maombi kwa Natasha.
"Hapana chezea shemeji wewe.."alisema Magreth aimchokoza Denis makusudi na darasa likaanza kuangua kicheko.Denis alimtazama tu Magreth kujikuta akimnyooshea kidole cha kati kama kumtusi,hakupenda maneno ya Magreth.Sara alitoa daftari lake na kukamata kalamu akaanza kuandika,kuna mambo anayaandika kila siku na ni siri yake mwenyewe,akiwa kwenye kazi hiyo hereni yake kuanza kutikisika na kumfanya anyanyuke mkono wake na kuziba sikio lake lote ili isionekane hereni ile ikiwa kwenye ile hali,aliinama na kuweka kichwa kwenye meza aliyoweka lile daftari na kulilalia,alifumba macho na taratibu akaanza kuonesha matukio kadhaa yatakayotokea hapo mbele,alipata kumuona Denis akiwa kwenye pori ametupwa huku mwili wake ukiwa hautamaniki kwa kuharibiwa vibaya damu mwili mzima,alioneshwa pia Magreth akiwa anamcheka Ester aliyeonekana kama kutokwa na akili na kudondosha tu maudenda mdomoni yaliyoichafua shati yake ya shule.
Alikurupuka pale alipolala kwenye lile daftali na kuangalia huku na kule hadi wanafunzi wenzake wakamshangaa.Alimtazama Denis akiwa anacheka tu wenzake wakiwa wanapiga stori hawana habari,aligeuka kumtazama Magreth ambaye naye alikuwa akimuangali Sara baada ya kukurupuka pale.Hakujua ni kitu gani kitamfanya Magreth amcheke Ester hapo baadae,hakujua ni nini kilimpata Ester na wala ile hali ya Denis kule porini.Akajawa na wasiwasi na haraka akanyanyuka na kutoka nje kuelekea kule aliko Ester kwenye lile darasa.
Alipofika nje aliona walimu watatu wakiume wakiwa wamembeba kwa nguvu Natasha aliyeonekana bado kufurukuta huku akikoroma kama simba dume.Walimpeleka kwenye chumba kimoja kule ofisini huku Ester akiwa nyuma naye anafuata,haraka akamkimbilia huku moyoni akiwa anahisi huenda yaweza kuwa ndio siku hiyo Ester atakuwa chizi.
"Ester...!!"aliita Sara akiwa akamkimbilia Ester ambaye baada kusikia aliita aligeuka na kumuona Sara.
"Haya vipi anaendeleaje Natasha?"
"Aisee bado,ana mapepo makali sana nikiyaombea yatoke yanatulia kwa muda halafu baadae yanacharuka tena,tumemuhamishia huku tuache kidato cha kwanza warudi darasani kwao kuanza kupanga viti,ngoja nikajaribu tena nione itakuwaje"alisema Ester na kuendelea kupiga hatua kuelekea ofisini huku Jasho likimtoka.Sara alimtazama Ester kwa jinsi anavyowajali wenzake na kujitolea hata kukosa vipindi ili kusudi tu atoe msaada kupitia imani yake, naye akawa nyuma yake tu anamfuata huku akitafuta namna ya kumueleza Ester yale mambo aliyoyaona na kubadilika yanaweza kutokea hapo mbele.
Wale walimu walimuingiza Natasha kwenye chumba kimoja na Ester akaingia pia kuendelea kumuombea huku wale walimu pamoja Sara wakiwa wamesimama mlangoni wakisubiri matokeo.Aliumiza kichwa Sara akikumbuka yale aliyoyaona na kuhisi huenda kuna jambo linaweza kuwa chanzo ya haya yote,akwatazama wale walimu kisha akageuka na kufumba macho yake kwa sekunde kadha na kugeuka.Haikupita hata dakika moja wale walimu wakaondoka zao na kumuacha Sara pale mlangoni,alimtazama Ester akiendelea kuomba na kuona kuomba ni kazi bure,akasogea mpaka pale na kumwambia Ester atulie huku Natasha akiwa amebadilika macho kwa kulia sana,Sara alimshika Natasha kwenye paji la uso na papo hapo Natasha akazimia na kudondoka chini.
"we Sara nini unafanya??"aliuliza Ester akioneka kuogopa.
"kuna kitu kimemuingia huyu Natasha tena si muda mrefu leo hii hii,katupiwa jini"alisema Sara na kumfanya Ester ahamaki,akaambiwa akafunge mlango na haraka Ester akafanya hivyo kisha akarudi.
Sara aliweka mikono yake masikioni mwa Natasha na kuanza kusema maneno yasiyosikika akawa ana non'gona pekeake na kumfanya Ester aangalie tu,moshi mweusi ulianza kutoka masikioni mwa Natasha huku Sara akiendelea kunon'gona tu."haya wataje..."alisema Sara akimwambia Natasha aliyekuwa chini amelala.
"Natasha,mwalimu Eddy,Juma,Ester na Denis"alisema Natasha akiwa pale chini amelala.
"Haah!Ester mimi au?tumefanyaje?"alidakia Ester baada ya kusikia jina lake limetajwa.
"shhhhhh..."alitoa ishara Sara ya kwamba anyamaze Ester.
"na kwanini wawe hao na sio wengine?"aliuliza Sara.
"nimetumwa niwauwe hao tu na wala sijui kwanini...mimi nimeagizwa tu natekeleza.."alisema Natasha na kumfanya Ester aishiwe nguvu akajikuta akikaa chini tu kusikia waliotajwa wanahitajika kufa.
"Nani kakutuma?"aliuliza Sara.
"Mfalme....Mfalme.....Mkuu wa wakuu"alisema Natasha huku akiachia tabasamu.
"Sasa nakupa dakika moja utoke rudi kwa huyo mkuu wako ukamwambie yule aliyewasaliti ameiingilia tena kazi yake,nitafanya nilichokifanya mwanzo.
"HAAA! KUMBE NI WEWE SARA!!!"akashangaa Natasha.
"kumbe unanijuaeee,sasa nahesabu hadi tatu ukusanye vitu vyote ulivyoanza kuviweka kwenye mwili wa Natasha la sivyo nakuteketeza.. MOJA......MBIL...."
"Basi basi natoka Sara....ila huyu hataishi kwa amani una kazi ya kumlinda"
"sitaki kusikia maneno yako...tokaa"alisema Sara kwa hasira na muda ule ule kikatoka kivuli ndani ya mwili wa Natasha na kupotea gafla,Sara naye akajirudi hali yake ya awali baada ya kuitoa mikono yake kwenye masikio ya Natasha,akawa anahema sana huku akimtazama Ester aliyebaki akikodoa macho haamini kile alichokiona na kusikia.
"Ungeweza kumtoa huyu kiumbe?"aliuliza Sara akimtazama Ester aliyebaki kutikisa kichwa,alijibu asingeweza.
"Ndio maana ulikuwa unaomba anatulia halafu anaanza tena kucharuka maana hata wewe upo miongoni mwa hao watu wanaowahitaji."alisema Sara.
"sasa jamani mimi nimewafanya nini hawa viumbe?,eh Yesu mwokozi niokoe kwa hili"alilalama Ester.
"hakuna haja ya kulalamika,hawa wananijua sana na ndio maana huyu ameondoka mwilini mwa Natasha,anajua kitakachoendelea endapo angekataa kutoka."alisema Sara na muda huo huo Natasha akaamka baada ya mambo hayo yote kutokea,alishangaa kuona yupo kwenye chumba kile cha wazi akamtazama Sara hakuweza kumfahamu sana,alipomtazama Ester alimjua na kujikuta alipata nguvu ya kuamka kukaa.
"Dada Ester nini kimenitokea mimi?"aliuliza Natasha huku akishika kichwa chake kuonesha anahisi maumivu.
"ah usijali Natasha nitakueleza baada ya kutulia vizuri,vipi kichwa kinauma?"alisema Ester akijenga tabasamu la kumfariji Natasha.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndio kinauma huku pembeni"
"Pole sana,ngoja nikakuchukulie dawa kwa Madam uje umeze maumivu yapungue sawa"alisema Sara na kunyanyuka kwenda kwa Madam..
"Eti dada nini kilitokea mpaka niletwe huku?"aliuliza Natasha kumwambia Sara ambaye alibaki kumtazama Natasha tu usoni akionesha kweli hana analojua,alimshika shavuni.
"Umshukuru sana Ester amekusaidia,amesema uliingiwa na pepo hivyo akakufanyia maombi na yametoka yote tumeshuhudia hapa upo salama sasa."alisema Sara anatabasamu.
"Ila sikuwa na mapepo mimi hapo mwanzo?"
"ni kweli...ulipokuwa unaombewa yenyewe yalisema yamekuingia leo asubuhi na kwa bahati nzuri E ster amekuombea yanaweza kupotea kabisa."alisema Sara.
"Eh jaman Mungu amzidishie sana dada Ester."alisema Natasha na muda huo huo Ester alifika sambamba na walimu watatu akiwa na Madam Magdalena aliyeshika kikombe cha maji ya kunywa.
"Eh jamani dada Ester asante sana dada yangu umenitendea jambo nisilolisahau maishani,Mungu akulinde sana dada yangu"alinyanyuka Natasha na kumkumbatia Ester kwa kumpa pongezi hadi Ester mwenyewe alishangaa,chozi likimtoka Natasha baada ya kujua alipitia majaribu yale ambayo aliambiwa na Sara kuwa yameisha,alipokea dawa na kunywa pale pale huku walimu wakimpa pongezi Ester kwa kile kilichofanyika,alipokea shukran hizo japo alijua mwenye kustahili kupewa ni Sara,kutokana na hali ile mwalimu alimpa ruhusa ya siku tatu Natasha arudi nyumbani kupumzika kutokana na yale aliyoyafanya kule darasani.Sara na Ester walirudi zao darasani ambako wanafunzi wa darasa Lao wakaanza kumpigia makofi Ester kwa kile alichokifanya,Sara akabaki amefurahi tu akarudi zake kukaa kwenye kiti na yeye akaanza kumpigia makofi Ester kama kumpongeza....
Ester alikubali kupokea sifa zile na shukrani kisha akaelekea kwenye kiti chake na kukaa akitabasamu,alimtazama Sara ambaye naye alitabasamu tu na kuendelea na mambo yake.Siku hiyo ilikuwa ni gumzo shule nzima juu ya tukio la Natasha kuonekana akipandisha mashetani jambo ambalo siwkawaida yake hasa kwa wanaomjua,haikuishia hapo hata alipofika nyumbani kwao Natasha na kuwaeleza wazazi wake nao hawakuamini juu ya tukio hilo,baadhi ya wanafunzi waliokuwa na rafiki na Natasha walipita kwao kumjulia hali na kutoka ushahidi wa kweli kwa wazazi wake Natasha wakaamini na kubaki kumkumbatia tu mtoto wako na kuzidi kumuombea kwa Mungu.
Usiku wa siku hiyo mwalimu Eddy akiwa ametulia na familia yake baada ya chakula walipumzika kidogo na baadae akamchukuwa mwanaye anayesoma darasa la pili na kwenda kumlaza chumbani kwake na kumuaga kisha yeye akarudi kuelekea kupumzika na mkewe,waliongea mambo yao ya kifamilia na kutokana na uchovu wa siku nzima mwl.Eddy usingizi ukamchukua mapema,mkewe naye kuona vile naye akaanza kuutafuta usingizi taratibu.
Usiku wa man and kukiwa kumetulia,gafla kukaonekana kivuli cha mtu ndani ya nyuma ya mwalimu yule,taratibu kile kivuli likaanza kutembe mule ndani na kuingia kila chumba na kutoka,kiliufungua mlango wa chumba cha yule mtoto kidogo na kutazama kitandani kuona mtoto yule anakoroma tu hana habari,kikagairi kuingia na kuufunga mlango ule kisha kikaanza kuelekea chumbani kwa wazazi wenyewe,mlango ulifunguka na kikaingia taratibu kikisogea hadi pale kitandani,kilizunguka kile kitanda mara tatu kisha kikisogea upande alipolala mwalimu Eddy nacho kikapanda kitandani na kulala pembeni ya mwalimu kama alivyolala yeye na gafla kikapotelea mwilini mwa mwalimu kwa kumuingia,mwalimu akiendelea tu kuuchapa usingizi bila yeye kujua usiku ule,kitendo cha kile kivuli kuingia ndani ya mwili wa mwalimu Eddy kukifanya hata Sara aliyekuwa amelala chumbani kwake kashtuka gafla baada ya kuhisi jambo,moyo ulimuenda mbio sana usiku ule hadi yeye mwenyewe akashangaa ile hali baada ya kuota ndoto fulani iliyomtisha hadi macho yake yakabadilika gafla,alikaa na kuitafakari ndoto ile lakini hakupata muafaka,taratibu akarudisha mwili wake kitandani huku akianza tena taratibu kuutafuta usingizi japo ndoto ile ilikuwa bado kichwani mwake.
Asubuhi kulipopambazuka Sara alidakia na kuanza kufanya usafi wa ndani,akawasha jiko na kuanza kuchemsha chai huku akiandaa nguo zake za shule,baada ya kazi zote kuzimaliza akatenga chai mezani na kuanza kunywa kabla ya kwenda shule,na baada ya kumaliza alimuaga baba yake na kuanza safari ya kuelekea shuleni.
Wanafunzi walionekana kufanya usafi kila kuona ya shule asubuhi ile huku baadhi ya viongozi wakisimamia usafi huo hadi pale ulipokamilika na kengele ikagongwa na wote wakaelekea paredi kujuzwa kunachoendelea.Mwalimu wa zamu ya wiki hiyo mwl.Isack alisimama nabkuongea machache ikiwa ni pamoja na kuwahimiza wenye taaluma yao kisha akawaruhusu kuelekea madarasani kusubiri vipindi kuanza siku hiyo.Ester alichukuwa ufutio nabkusogea ubaoni na kuanza kusafisha ubao na muda huo huo mwalimu Eddy alikuwa akiingia darasa hilo kuanza kipindi chake,alimkuta Ester pale mbele.
"yaani muda wote tangu asubuhi hamkufuta ubao ndio maguta saa hizi?Monitor and monitress piteni mbele."alisema mwalimu Eddy na kutoka nje,akamuagiza mwanafunzi mmoja kwenda kuchukua viboko ofisini huku darasa likaanza kunon'gona..
"Mh leo mwalimu Eddy anachapa?makubwa"
"asa jamani kuna kosa gani wakati ndo tunaingia darasani saizi?"
"Leo kajisikia kuchapa huyu"yalikuwa ni maneno ya wanafunzi wakiamhizana kimya kimya kujadili kosa lile.Ester alibaki amebaki ameduwaa tu huku ameshika dasta lililomchafua usoni kwa vumbi la chaki,taratibu Denis alinyanyuka na kusogea mbele kusimama karibu ya Ester.Mwalimu Eddy alirudi darasani baada ya kupata viboko na kusogea pale waliposimama viongozi wa darasa.
"huu ujinga sitaki ujirudie tena nikiingia darasani nikute ubao upo safi,monitor kaamka hapa haraka..."alisema Mwl.Eddy kwa hasira hata Sara aliyekuwa amekaa akitazama lile tukio alibaki anashangaa.Taratibu Denis alimshika ukuta na kuanza kutembezewa bakora Sita za matako hadi wanafunzi wakashangaa,haikuwa kawaida kwa mwalimu huyo ndani ya shule ile hakuwahi kuonekana akimuadhibu mwanafunzi kwa kumchapa hata siku moja.Denis alivumilia Kitendo cha Denis kupigwa kila fimbo kilimfanya Sara aanze kukumbuka ile ndoto aliyoota usiku na kufahamu kitu kinachoenda kutokea hapo mbele,alibaki kuhamaki Sara baada ya kujua lile tukio linaweza kutokea kweli.Denis alivumilia zile bakora na alimaliza akarudi zake kwenye kiti kukaa na kubaki Ester pale.
"lakini mwalimu mimi ndio naingia na kuanza kufuta ubao wewe ndio unatokea.."alijitetea Ester akionesha uwoga wake.
"Nyoosha mkono bwana...halafu tena ndio...hebu nyoosha"alisema Mwl.Eddy kwa hasira hadi wanafunzi wote wakaogopa,alitoa jasho jingi sana kwa kumuadhibu tu Denis na Sara alipoona Ester anataka kuadhibiwa akajikuta akiliziba lile sikio lake na Kufumba macho,alipofumbua yalibadilika na kuwa ya kutisha huku akishuhudia Ester akinyoosha mkono,bakora ilishuka kwa kasi na kumfanya hata Ester acumen macho lakini cha ajabu hakusikia maumivu yoyote huku mwalimu Eddy akiendelea kuzishusha fimbo kwa nguvu,Ester alifumbua macho na kushuhudia kweli mwalimu anamuadhibu tena kwa hasira lakini yeye hasikii maumivu yoyote,akili za haraka zikamjia na kujikuta akimtazama Sara na kumuona akiwa kwenye macho yale ya kutisha na kufahamu aliyofanya haya ni Sara.Wanafunzi wote walikuwa wakishuhudia zile fimbo zikitua mkononi mwa Ester na K ubaki wakimshangaa Ester hali wala hafurukuti kama iliyo kawaida yake mpaka bakora zile sita zilipoisha akaruhusiwa Kurudi kukaa,kwa kufahamu kuwa amesaidiwa na Sara akaamua kuushika mkono wake wanafunzi wenzake wajue kwamba ameumia kweli.Sara alirudi kutoka hali ya kawaida na kumsikiliza mwalimu huyu akiendelea kufundisha somo lake la English,muda wote huo hadi kipindi chake kinaisha Ester alikuwa akilifikiria tukio lile la kupigwa fimbo za nguvu lakini hakuweza kusikia maumivu,kwa kujuwa kuwa Sara ndiye aliyefanya yote akajikuta akitabasamu tu na kushukuru moyoni,kuna wakati alijiuliza kama uwezekano wa kuzuia asipigwe Ester kwanini asingemsaidia hata Denis?...akipata jibu la haraka na kujikuta asilitilie maanani sana jambo lile huku akiushika mkono wake kuuangalia,hakuamini.
Baadhi ya rafiki zake baadae walimfuata na kumfanya kwa kumpa hongera ya kuvumilia fimbo sita bila kulia hata Denis pia alishangaa.Ester hakutaka kusubiri kutoka shukran alinyanyuka muda ule na kumfuata Sara pale alipo kwenye meza na kiti chake na kuanza kuongea taratibu bila yoyote kujua.
"Unajua siamini Sara kwa ulichokifanya,yaani leo ningegaragara hapa zile fimbo zingeniingia wewe mwenyewe ungenicheka,asante sana"alisema Ester akionesha tabasamu.
"usijali mambo ya kawaida Ester.."alisema Sara na kumfanya Ester amsogelee karibu.
"kwani ilishindikana kutusaidia wote tusiadhibiwe?"aliuliza Ester na kumfanya Sara amtazame kwa muda,akwatazama darasa na kuona baadhi yao wanajisomea,akavuta kiti nyuma na kunyanyuka.
"Njoo.."alisema Sara na kuongoza njia kutoka nje.Ester alimtazama tu na yeye akanyanyuka kutoka nje asijue kinachoendelea.Walienda kukaa mbali kidogo na darasa wakasikia bila yeyote kuwaona.Sara akabaki anamtazama tu Ester usoni hammalizi hadi mwenyewe Ester akashangaa.
"Mbona unaniangalia sana Sara kuna nini?"aliuliza Ester na yeye akiwa anamtazama Sara.
"leo ungekufa pale darasani!!"alisema Sara na kumfanya Ester ashangae.
"NINGEKUFAA???"
"shhhhhh....acha kelele,nashangaa nini sasa!jana tu lile jini lililomuingia Natasha aliwataja watu wote wanaotakiwa kuuliwa na wewe ukiwemo,sasa ulipaswa kuanza kufa wewe na wengine war hate na kifo chako kilitengenezwa sababu mdogo tu ndio zile fimbo za yule mwalimu Eddy ambaye naye ni miongoni mwa watu wanaopaswa kuuliwa"
"haa jamani Sara.....M bona anaanza kuogopa hivi...sina amani kwa sasa,mwalimu Eddy alitaka aniuwe mimi..?"alisema Ester akianza kuonesha kulia.
"Yule sio mwalimu Eddy tena,kilichotokea kwa Natasha kumuenda tena kwa mwalimu,mwalimu Eddy ameingiliwa na jini ndio linamtuma kufanya haya,so umeona watu walikuwa wanashangaa leo mwalimu Eddy ameshika fimbo wakati sio kawaida yake,yule ni jini ndio atantumia mwili wa mwalimu kuwapunguza nyie mnaohitajika,Denis hakupaswa kufa kifo kile na yeye atatafutiwa sababu,ile ilipangwa na mlengwa alikuwa ni wewe Ester,kutofuta ubao sio kupigwa bakora zote sita zile tena za nguvu hushituki tu!,na laiti ungepoteza maisha yule jini angetoka mwilini kwa mwalimu Eddy na kesi inahamia kwake kosa la kuua ndivyo mnavyopungua hivyo"alisema Sara na kumfanya Ester aelewe lengo hasa.Wakakaa na kuongea mengi sana huku Sara akimueleza Ester mambo mengi aliyoyaona hapo mbeleni hata yeye Ester kuja kuwa chizi,hakutaka kuuficha lolote na hapo ndipo Ester akaona kuna umuhimu na kila sababu ya kuwa karibu na Sara mana anamsaidia kwa mambo mengi sana.Sikh hiyo vipindi bingo sana viliwapita bila wao kujali maana hali ya shuleni pale inakoelekea sio nzuri.Baadae walirudi darasani kuambulia vipindi vilivyobaki.Kwa Ester haikuwa kawaida kwake muda wote alikuwa mwenye kuwaza tu,hata aliporudi nyumbani kwao alijikuta akitumia muda mwingi kukaa chumbani akizidi kufanya maombi juu ya mabalaa yale yaliyo mbele yake na kuweka dhamira kila atakapofika eneo la shule lazima amuombe Mungu ampe nguvu na kumlinda kwa siku hiyo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi ya siku iliyofuata kulipopambazuka baadhi ya wanakijiji walianza kukamata majembe yao kuelekea kwenye mashamba yao kufukua mihogo iliyokuwa tayari kwa biashara na matumizi ya nyumbani kama chakula.Asilimia nyingi ya wa kazi wa mkoani Mara walitegemea sana zao hilo pamoja na mahindi kidogo kama njia ya kupata pesa za kujikimu kimaisha na kuwasomesha watoto wao,wanafunzi nao wa shule za msingi na sekondari walianza kupiga hatua kusogea mashuleni kupata elimu ya kuwafaa maishani,Ester kama alivyosema nadhiri yake alipofika tu karibu na shule yao akaanza kukamata rozali yake na K ufumba macho kuomba kwa bwana Mungu aweze kumlinda na mabaya na Shari zinazonyemelea,hata baadhi ya wanafunzi wengine waliompita W alibaki kumshangaa kwa kile kitendo anachokifanya na kuamini kweli dada huyo amemuweka Mungu moyoni,alipomaliza akielekea moja kwa moja darasani kwake na kuungana na baadhi ya wanafunzi wenzake kadhaa kusafisha darasa,alichukua ufutio na kuufuta ubao mapema kusudi yasitokee yaliyomkuta jana.Muda ulienda na baada ya mambo yote kwenda sawa wanafunzi Wakaingia madarasani kutulia wakisubiri walimu wa vipindi vya asubuhi kuanza kazi yao na muda mchache tu masomo yakaanza.
Baada ya vipindi viwili kumalizika asubuhi alionekana walimu wote wakitoka ofisini wakiwa wameshika makaratasi kila mmoja jambo lililowafanya baadhi ya wanafunzi kuulizana kuna nini kinachoenda kutokea.Kila mwalimu aliingia kwenye darasa lake alilopangiwa kuingia,Madam Magdalena aliingia kidato cha tatu A na kuwakuta wanafunzi wametulia,alivuta kiti na kukaa mbele ya darasa.
"Monitor....Denis njoo"alisema Madam na kumfanya Denis anyanyuke kusogea pale mbele,akapewa karatasi moja.
"waandike wenzako wote waliofika siku ya leo"alisema Madam na kuwafanya wanafunzi wabaki na sintofahamu huku Denis akifanya kama alivyoagizwa.
"Okay habari za asubuhi wanangu."alisalimia Madamu na kuitikiwa kwa kupewa heshima ya salamu.
"Bila kupoteza muda naomba niende kwenye point muhimu,hiyo karatasi uhakikishe kila hapa shuleni na tangu nifike hapa shuleni nmemuona jana tu akimtandika mtoto wa form One fimbo za uhakika hadi nkashangaa lakini haikuwa mchapaji...kwahyo basi kama kuna aliyeazima kitabu au kitu chochote kutoka kwake aje hapa kwenye karatasi aandike mbele ya jina lake kitu alichopewa akirudishe haraka,pia kama kuna wanaomdai pia waje ila hii ni kwa wote,kama umeguswa na msiba huu tafadhari kutoa ni moyo wanangu hebu ile hela ya chai baadae toa japo shilingi mia uchangie kiasi hicho tukawakabidhi wafiwa familia ya marehemu iwe ni kama mchango kutoka kwa wanafunzi,nadhani nimeeleweka."alisema Madam Magdalena na maneno yake ya hekima yaliwagusa wanafunzi wengi,taratibu wakaanza kunyanyuka na kuanza kusogea pale mbele kutoa kile walichonacho,hata Denis alisogea na kutoa mia tano yake yote aliyoiweka kwaajili ya kula baadae huku akimkumbuka marehemu mwalimu Eddy kwa bakora alizochapwa jana tu darasani huku moyo wake ukiwa mweupe kwa kusahau yale yaliyopita.
Basi siku ilikuwa ni huzuni kwa walimu pamoja na wanafunzi juu ya tukio hilo la ajabu lililowashangaza wengi.Wanafunzi wengi waliguswa na msiba huo wa mwalimu wao na kuanza kutoka kile mtu alichojaaliwa.Walimu kila darasa walikusanya pesa za wanafunzi na kuzichanganya pamoja baada ya kurudi ofisini na kuacha minon'gono ya wanafunzi madarasani.Ester aliamua kutoka nje kabisa na kwenda kukaa sehemu akianza kutafakari ile jana alivyoadhibiwa na mwalimu huyo marehemu lakini Sara akazuia asiumie na baadae akawa kuambiwa alipaswa kufa Ester siku ile na yule mwalimu angepata kesi ya kuuwa kwa kuwa wote waliokuwa miongoni mwa watu waliotajwa na lile jini lililoingia mwilini mwa Natasha kuwa watauawa,sasa tukio hili la kufariki kwa mwalimu huyo kulimfanya Ester aamini kifo chake kinakaribia,akaogopa sana na kuanza kukimbia kurudi darasani haraka akaelekea kwenye nafasi yake na kukaa huku akihema hali iliyowafanya wenzake wa karibu amtazame kwa makini.
"Ester...upo okay?"aliuliza mwanafunzi mmoja wa karibu na Ester ambaye aliitikia kwa kichwa kwamba hana tatizo,yule mwanafunzi akimuacha na kuendelea na mambo mengine.
Aliumiza kichwa sana siku hiyo hasa akiangalia sehemu ya Sara upo wazi alizidi kuumia.
Kengele ilisikika asubuhi ya saa nne nabkuwafanya wanafunzi atambue muda wa break fast umefika,walitoka baadhi kuelekea kupata kifungua kinywa huku wengine wakiwa ametulia madarsani na kwenye baadhi ya bustani za shule.Siku hiyo Ester aliamua kwenda naye kunywa chi aondoe yale mawazo yanayomtawala kichawi mwake,akaanza kufuata njia kuelekea kwenye mgahawa akiongozana na wanafunzi wengine..Akiwa wanatembea kuelekea kwenye Migahawa na wenzake walipishana na mwanafunzi aliyeonekana kubana sare Maya kabisa akiwa na begi lake akiongozana na baba mmoja akaingia shuleni hapo.
Sara muda wote alikuwa akimhudumia baba yake aliyekuwa kitandani akiwa na hali mbaya,alikuwa ameshamsaidia baba yake kumnywesha uji huku akimuongelesha kumfariji,alipomaliza alichukua vyombo vile na kuelekea jikoni kuviweka lakini alipopiga hatua kadhaa aliona ile sahani ikiwa nzito na kumponyoka hadi chini ikapasuka vipande vinne ,hali ile ilimfanya Sara abadilike macho na kuvitazama vipande vile na kushangaa kuona kila kipande kuna sura ya mtu,alipoangalia cha kwanza aliona mwili wa mwalimu Eddy ukigombaniwa na viumbe vya ajabu na kile kipande gafla kikapotea,alipotazama kipande cha pili aliona wanafunzi wawili wa jinsi tofauti wakiwa kwenye jumbo bovu wakiwa wameangika chini miili yao ikilowana damu,alitazama na vipande vilivobaki na kuona vile alivyoona ndotoni siku ile ndio kama anavyoona kuhusu Denis na hata Ester kuwa na ile hali ya utaahira.
Alipomaliza kutambua yote yale kwa maajabu ya aina yake ile sahani ikarudi na kuwa nusu sahani na kuanza kuonesha watu wawili mwanafunzi wa kiume akiwa anaongozana na baba mmoja wakiingia maeneo ya shule.
Hapo ndipo Sara anapata kujua kuwa kuna ugeni mbaya shuleni unaingia,aligeuka kumtazama baba yake ambaye naye alishudia tukio lile na kubaki kutikisa kichwa tu kwa masikitiko,Sara akaishusha pumzi kwa nguvu na kuiweka sahani ile ya dongo pembeni kisha naye akakaa kuanza kutafakari.
"Ina maana washamchukuwa mwalimu?"aliuliza mzee Junior akiwa pale kitandani.
"ndivyo inavyoonyesha,na sijui wametumia njema gani hadi mimi sikujua"alisema Sara akionekana mwingi wa kufikiri.
"una kazi mwanagu ya kulinda roho za watu waliobaki ila usichoke kuna siku tu utayashinda yote haya...Koh...koh"alisema mzee Junior huku akikohoa na kumfanya mwanaye asogee pale kitandani kumuweka sawa baba'ke.
"Sara mwanangu...wewe bado mdogo sana kiumri na nakutegemea kwa K ipindi hiki kigumu,baada ya mama yako kufariki sina mwengine wa kunianfalia na kunijali zaidi yako wewe mwanangu,anasema hivyo nina maana,kuwa majini sana na yote ufanyayo,muamini yule umuonaye ni bora kwako wengine achana nao watakuweka pabaya,fanya mambo yote hayo asijuwe mtu kuwa upo na hali hiyo uliyonayo maana wakijuwa wawili au watatu basi jamii nzima itaanza kukuangalia kwa hicho mengine huku wakijumlisha na matukio haya wataanza kukuhisi vibaya mwanangu ukaniacha baba yako pekeangu...nakutegemea Saratambua hilo"alisema Mzee Junior kwa sauti ya huruma akimsihi mwanaye,Sara alimsogelea baba yake na K ubaki kumkumbatia tu baada ya kuyaelewa maneno yale.
Huku shuleni,mwalimu mkuu alimuagiza mwanafunzi akamuite kuongoza wa kidato cha pili waweze kuja ofisini kwake na muda machache tu yule mwanafunzi alifika.
"Ramadhani...."aliita mwalimu mkuu.
"Yes Teacher....!"aliitika Yule mwanafunzi akiwa amesimama.
"Ongozana na huyu mwenzenu mgeni,ukampeleke kwanza apitie kuziona sheria za shule kwenye huo ubao kisha ukamtafutie kiti pamoja na meza,ni Form II mwenzenu huyu ntajuwa naye"alisema mwalimu mkuu na kumkabidhi Ramadhani yule mwanafunzi mgeni,ni yule aliyeonekana akiongozana na baba yake wakiingia shuleni hapo,alinyanyuka na kutoka nje na Ramadhani akiongozana mahala pa kwenda.
"nadhani mambo tumeyamaliza sawa sawa,na mimi naweza kurudi sasa"alisema yule baba wa yule mwanafunzi.
"ndio hapa kila kitu kipi safi kikubwa tu ni ushiriano wako kwetu sisi juu ya kufuatilia taaluma ya kijana wetu,"alisema mwalimu mkuu.
"BASI sawa haina shida,nikutakie kazi njema mwalimu."
"haya asante,karibu tena"alisema mwalimu Malamba na yuleb mzee akafunguanmlango na kuondoka zake,alipofika mbele baada ya kuondoka kwenye eneo la shule yule baba mwili wake ukaanza kubadilika na kuwa kama jini huku likicheka pekeake kwa sauti ya kutisha na punde tu likapotea gafla.
Mpaka jioni ya siku ile inaingia Polisi hawakuweza kupata uhakika wa chanzo cha kifo cha mwalimu Eddy na kubaki kuwa ni utata kuhu wengine wakihisi huenda alidhuliwa na mnyama kule bafuni lakini haikuwa na ukweli wowote,kwa kuujali mwili wa ndugu yao usizidi kuharibiwa ndugu waliamua kuufanyia maziko kesho yake Alasiri,ni baada ya kukubaliana na Polisi baada ya kuhaingaika kupata chanzo lakini ikashindikana,ndugu wa marehemu walifungua nafsi na kauchuna na upelelezi huo ili wausitiri mwili wa ndugu yao.Ni majonzi sana na uchungu alionao mkewe marehemu huku akizimia kila mara akikumbuka mapenzi na upendo wa mumewe.
Siku iliisha hivyo na kesho yake maandalizi ya main a yakafanyika,ilikuwa ni Ijumaa wanafunzi wote waliruhusiwa mapema tu asubuhi ile ile walipokuja shule wakiagizwa kwa walioguswa na main a huo waelekee huko kusaidia kazi.Muda yulisogea na umati wa watu walitokea kwenye msiba huo,Ester alikuwa pamoja na Sara wakiwa na wanafunzi wenzao wamekusanyika mahali wakiomboleza.Jeneza lilitolewa likiwa na mwili wa marehemu aliyeonekana kuanzia kifuani akiwa amevalishwa nguo takatifu na kulazwa ndani ya nyumba yake hiyo ya milele.Taratibu watu wakaanza kupanga mstari na kusogea kuuaga mwili wa marehemu kabla ya kwenda kupumzika,wanafunzi wengi pia waliokuwa miongoni mwa waliosimama wakipita karibu na jeneza lile na kushuhudia mwalimu wao akiwa amewekwa pamba puani na masikioni,ilikuwa ni huzuni tupu siku hiyo.Ester akiongozana na Sara nap walisogea kwenye jeneza lile kuuaga mwili wa mwalimu wao na cha ajabu alipofika pale ni Sara pekee ndiye aliyeona utofauti,hakukuwa na mwili wa marehemu pale kwenye jeneza liliwekwa gogo la mtu mbichi kasi cha kumfanya Sara ashangae hadi Ester aliye mbele yake akageuka kumtazama,akazuga tu anakohoa na anaendelea kutembea mbele.Muda ulipowadia wa kwenda makaburini wanaume walilibeba lile jeneza la marehemu mwalimu Eddy na kuanza kuelekea mazikoni huku umati wa watu wakifuata nyuma wakiusindikiza mwili wa marehemu kwa kuomba nyimbo za kumuagaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda wote Sara alikuwa amesimama mikono na Ester huku akitahaluki juu ya tukio lile baada ya kufahamu si mwili wa mwalimu Eddy uliokuwa mule ndani japo watu wote waliuona mwili huo hadi walipofika makaburini baadhi ya wanawake walihudhuria maziko hayo walisogea pembeni,mke wa marehemu pamoja na ndugu kwa ujumla walionekana kulia sana pale makaburinina kuwapa kazi baadhi ya watu waliohudhuria maziko yale kuwanyamazisha,ndugu wa marehemu waliingia kwenye kaburi na kupotea jeneza wakalaza ndani ya kaburi na kutoka,mkewe alikabiziwa chepe na kuagizwa atupe udongo ndani ya kaburi la mumewe ishara ya kumzika mumewe,alilia sana na kujitahidi kujikaza lakini hakuweza maana haaminin kama mumewe ndio anaondoka kweli,akazimia pale pale ikawafanya baadhi ya ndugu wamchukuwe na kumuweka pembeni.Ndugu walichukuwa jukumu hilo na kuanza kurusha udongo kwenye jeneza wakafuata watu wengine na hata wanafunzi pia,Sara alibaki kumtazama tu tukio lile akiwa sambamba na Ester ambaye aliomba kwa imani yake Mola ampokee mwalimu huyo kwenye makazi ya baraka,alisogea mchungaji pale karibu na kaburi lile baada ya kufukiwa vema,alitoa kitabu cha Biblia na kufunua ukurasa kadhaa na kuanza kutoka neno mbele ya umati wa watu pale makaburini ambao walisimama wakimsikiliza.Wakiwa kwenye zoezi hilo la ukimya wakimsikiliza mchungaji Sara akianza kuona utofauti mahala pale na gafla tu heleni yake ikaanza kucheza kwa kasi na kumfanya afumbe macho na azibe sikio lake kusudi asionwe na mtu na ni Ester pekee ndiye aliyemuona Sara vile,alitambua kuna kitu huenda kimetokea akabaki akimtazama tu,alipofumbua tu macho yake yalibadilika na kuanza kutazama huku na kule.Ester alivyoona vile haraka akasimama mbele ya Sara kusudi Ester asionekane macho yake.Sara akawa amejibana nyuma ya Ester huku akiangalia kila kuona kama kwamba anatafuta kitu na nn alipomtazama vizuri akaona watu wa ajabu kama sita wakionekana kuugombania mwili wa mtu mmoja,akaja kijana mdogo akawatuliza na kugeuka kumtazama Sara huku akitabasamu wakabaki wakiangaliana kwa macho makali hadi Sara pale alipo hasira zikampanda...
Yule kijana aliendelea kutabasamu tu na macho yake makali kama paka."ndio tumeanza kazi tena upya,huyo uliyenaye atafuata tu muda ukifika usione umeshika kumkomboa"maneno hayo ya yule kijana aliyasikia Sara tu masikioni mwake.
"sitakubali muendelee kuwachukuwa watu wasio na kosa lolote,na huyo mtamrudisha tu"maneno hayo ya Sara yalipenya masikioni mwa kijana yule na kubaki wakiongea kwa hisia zao wenyewe bila yeyote kusikia wala kuwaona wale viumbe.Mazishi aliendelea na hata askofu alipomaliza watu wakaanza safari ya kuondoka pale makaburini huku Sara akarudi hali yake ya kawaida baada ya wale viumbe kutokomea katika mazingira ya ajabu,akaongozana na Ester kurudi makwao.Siku hiyo Sara alimshawishi Ester waende nyumbani kwa akina Sara,wakiwa njiani wakiongea mambo mengi hasa kuzungumzia kifo cha marehemu mwalimu Eddy.
"Kama yale majina tuliyotajwa na lile jini lililomuingia Natasha ni kweli basi maisha yangu namkabidhi bwana Yesu anilinde na niwe naye milele."alisema Ester na kumfanya Sara atabasamu.
"kuna mambo ambayo Mungu anatulinda juu ya mabaya lakini kuna vitu vengine yakupasa ujisaidie mwenyewe uwe ni changamoto kwenye maisha yako"alisema Sara.
"Ah weee....changamoto enyewe ndio hizi za kufa ki mazingira ya ajabu,unakuja gafla tu "
"Esterrr....kuna mambo wewe huelewi yakupasa uyafahamu kidogo kidogo.."alisema Sara na kumfanya Ester ainame kumtazama,naye Sara akasimama.
"Hebu niambie ukweli Sara....pale makaburini umeona nini hadi kubadilika gafla?"aliuliza Ester na kumfanya Sara avute pumzi na kuishusha kwa nguvu huku a kiangalia pembeni.
"Niliona viumbe wa aina nyengine,waliokuwa tofauti na sisi,ni majini kama yule aliyemuongia Natasha siku ile,na ndio hao waliomuuwa mwalimu."alisema Sara.
"hee...jamaaaaani.....walikuja hadi huku makaburini?,walifuata nini sasa huku wakati washaua?"
" "Ndio wamekuja,wameuchukua mwili wa marehemu Mwalimu Eddy"mameno haya ya Sara yakamfanya Ester ahamaki kwa sauti,akabaki akicheka tu haamini.
"huo ndio ukweli Ester sijawahi kukudanganya,walikuja kuubeba mwili wa marehemu Mwalimu Eddy na pale limezikwa gogo tu hakuna aliyefahamu."alisema Sara na kumfanya Ester abaki kuduwaa na kukosa hata nguvu ya kuendelea kuuliza.Sara aligeuka na kuanza kupiga hatua kuondoka zake akimuacha Ester akiwa amesimama pale kwa muda,alichokifanya Sara ni kumtoa yale mawazo ya kufikiria jambo lile Ester,akazama pembeni kwa macho makali na kuyatikisa majani ya mti pembeni kwa Ester ambaye kuona vile alishtuka na kuanza kukimbia kumfuata Sara kule mbele huku alipiga mayowe kwa uwoga.
Safari iliendelea kuelekea kwa akina Sara,hata walipofika Ester alikaribishwa na kuingia hadi ndani ambapo alionyeshwa hali ya baba yake na Sara akiwa kitandani.
"Huyu ndio Ester!!?"aliuliza mzee Junior baada ya kumuona Sara akiwa pamoja na Ester.
"ndio mimi baba Shikamoo"alisalimia Ester na baba yule akaitikia huku akitabasamu.
"Umekuwa siku hizi..."alisema baba yule na kumfanya Ester abaki kushangaa.
"kwani unanifahamu baba?"aliuliza Ester na kumfanya baba yule amtazame Sara ambaye alifahamu baba yake nini anamaanisha,akatoa zake nje na kumuacha Ester akiwa na mzee Junior mule ndani.
Siku mbili zilipita na siku hiyo ya Jumatatu wanafunzi wakionekana kwenda kupata chai asubuhi ile,Sara alikuwa nyuma ya jengo la shule yao pamoja na Ester ambaye alionekana kuwa mwenye mawazo mengi sana.
"Unajua siamini kwa yale niliyoambiwa na baba yako,moyo unaumia sana baada ya kuniambia vile"alisema Ester baada ya kuambiwa mambo fulani siku ile na mzee Junior.
"hali ndio kama hiyo,vile ulivyoambiwa ni ukweli mtupu na wala sio utani"alisema Sara.
"Lakini inawezekana vipi Sara,mpaka najielewa tokea udogoni mimi ni mtu wa kumjua Mungu na wazazi wangu ndio walionifundisha siku zote hadi hapa nikioa,iweje tena uniambie wao ndio.....ah siamini Sara siamini kabisaaa"
"usitake kubisha kitu ambacho ni kweli,kipindi hicho wazazi wako walikuwa na shida,na mambo yote ushaambiwa sasa kinachokufanya usiamini ni kipi Ester."alisema Sara.
"ina maana na mimi ni JAMII YA HAWA VIUMBE? kweli Sara maneno haya unayaamini?"alisema Ester akionesha huzuni.
"haina haja ya kuhuzunika Ester, wazazi wako pia usiwalaumu maana walifanya hivi ili uishi mtoto wao salama,yashatokea haya na huna haja ya kulia,vumilia,tuliza akili yako kwenye masomo,hata mimi ni kama wewe na sijapenda niwe hivi,nipo nawewe siku zote rafiki yangu."alisema Sara na kumfanya Ester amtazame,walikumbatiana tu mabinti hao wawili na kuzidi kupeana moyo.Wakiwa kwenye hali hiyo Sara alimuona kijana mmoja wa kidato cha nne akielekea chooni huku nyuma akionekana akifuatwa na mwanafunzi mmoja,yule mwanafunzi aliyekuwa akimfuata yule kijana akageuka nyuma moja kwa moja akampiga jicho Sara na kubaki kuangaliana huku akitabasamu.
"wa pili huyu hapa....."alisema mwanafunzi yule na sauti ile ikapenya masikioni mwa Sara.Haraka akamuachia Ester walivyokuwa wamekumbatiana na kuanza kukimbia kuelekea kule chooni kwa wanaume.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"We...we...we...wewe Sara....!!,"ilisikika sauti ya mwanamke na kumfanya Sara asimame,alikuwa ni Madam Magdalena akiwa natembea kuelekea vyoo vya walimu.
"tabia gani hiyo umeanzisha!mtoto wa kike kutaka kuingia kwa wanaume unatafuta nini huko?umeanza tabia mbaya nikakuripoti kwa Malamba?"alisema Madam na kumfanya Sara abaki akiangalia tu kule chooni kwa wanaume akiwaona wale wanafunzi wakiingia kule chooni.Akamgeukia Madam na kakubali kosa akapiga magoti,Ester alibaki alishangaa tu lile tukio.
"nsamehe Madam sikuwa na nia mbaya kuingia chozi cha wavulana,kuna mwanafunzi nlimfananisha tulikuwa tunasoma wote sasa nkawa namkimbilia kabla hajaingia chooni ndio na wewe ukahisi nataka kuingia."alijitetea Sara.
"Usinifanye mu mimi mtoto mwenzako Sara hizo janja wenzako tulipitia sana enzi hizo,mwanafunzi gani uliyesoma naye?"alisema Madam Magdalena.
"Ngoja nimsubiri akitoka nitakuonesha."alisema Sara kwa kujiamini.
"sasa ole wako?"alisema Madam na yeye akasimama na Sara wakisubiri watoke wale vijana wawili walioingia.Haikupita dakika tatu akatoka yule mwanafunzi aliyekuwa akitazamana na Sara na kuanza kutembea kuelekea darasani.
"we njoo hapa"aliita Madam kumuita yule mwanafunzi ambaye alitii na kusogea pale waliposimama Madam na Sara ambaye alimtazama yule mwanafunzi alikuwa na hasira.
"Unamjuwa huyu msichana?"aliuliza Madam kumwambia Yule mwanafunzi ambaye alibaki kumtazama tu Sara."hahaha Saraaaaa."alisema yule mwanafunzi moyoni na Sara akasikia.
"kama umemuuwa yule kijana huko chooni utanijua mimi ninani!"alisema Sara akimwambia yule mwanafunzi wa imani yao.
Yule mwanafunzi aligeuka kumtazama Madam.
"hapana Madam simfahamu"
"haya unaweza kwenda!"alisema Madam na yule mwanafunzi akaondoka zake.
"Sara....endapo akitoka huyo wa mwisho aseme naye hakujui nitakuwa adhabu usiyoisahau la sivyo nimeamini mkuu wa shule ajue la kufanya.!"alisema Madam Magdalena akiwa kama mwalimu wa kuwaangalia wanafunzi wa kike,Sara akabaki kugeuka na kuangalia tu kule chooni kumsubiri yule kijana.
Walikaa takribani dakika kumi mbele hadi Madam akashangaa,alimuita mwanafunzi mmoja na kumtuma aingie mule chooni aangalie kila choo kama kuna mtu,yule mwanafunzi akiingia chooni na kuanza kufungua milango ya kila choo kutazama...
"MADAM.....MADAM......NJOO HARAKA."ilisikika sauti ya yule mwanafunzi akipiga kelele mpaka Madam akaogopa,bila kuhofia Madam alikimbia kuingia mule chooni huku Sara akimfuata nyuma, Ester naye aliyekuwa kushuhudia mambo yakiendelea naye akaanza kukimbia kuelekea kule chooni kujua nini kimetokea.
Walipoingia kule chooni walibaki kuhamaki baada ya kumuona yule mwanafunzi waliyokuwa wakimsubiri amedondoka chini huku mapovu mdomoni yakimtoka.
"kawaite walimu haraka.."alisema Madam baada ya kuona ile hali na kuanza kushirikiana kumtoa chooni yule kijana na kumuweka nje,walimu walipopata taarifa ile haraka walitoka na kwenda eneo la tukio akiwa sambamba na mwalimu mkuu.Haraka walisogeza pikipiki ya mwalimu mkuu na kumuweka juu akae yule kijana huku akakaa nyuma mwalimu mmoja kumshikilia asianguke na haraka wakaanza taratibu za kumpeleka hospitali huku wanafunzi walibaki kushangaa pikipiki ile ikitokomea na kuacha maswali mengi pale shuleni.Kengele ya dharura iligongwa haraka na wanafunzi wote wakasogea pale paredi kusimulia walichoitiwa huku Madam akimfuata Sara.
"unamfahamu yule kijana Sara."aliuliza Madam na kumfanya Sara amtazame usoni Madam.
"Mimi simjui yule mwanafunzi Madam."
"Hata kama humjui nahitaji tu kama unaikumbuka sura yake?"alisema Madam na kumfanya Sara ashangae.
"lakini Madam na wewe si ulimuona,umeisahau sura yake?"aliuliza Sara huku akimtazama Madam aliyeonekana kutokumbuka kitu,Sara alipata kutambua kuwa Madam amepigwa changa la macho alimuona yule mwanafunzi kweli lakini katolewa kumbukumbu gafla tu hali ya kuwa yeye hajui kinachoendelea,Sara alitambua ni yule mwanafunzi ndiyo aliyefanya haya yote.
"kama nitamkumbuka nitamwambia."alisema Sara na hapo hapo Madam akamshika mkono wakaelekea paredi ambapo wanafunzi wote walikuwa wamesimama,Madam alisimama pale mbele na Sara nabkuwaangalia wanafunzi.
"kuna jambo la gafla na la ajabu limetokea hivyo nawaomba sana msimame kama mlivyo kuna mtu tunamtafuta na atakapo patikana wengine mtaingia darasani...haya twende anzia kule Form One."alisema Madam akimuamuru Sara waanze kupita kila mstari kumtafuta yule mwanafunzi huku walimu wote wakiwa wamesimama tu wakisubiri maana mashahidi walikuwa wawili Sara na Madam.
Zoezi hilo likaanza kufanyika la kuwaangalia sura wanafunzi wote huku Madam akijaribu kuvuta kumbukumbu kama ataweza kumkumbuka yule mwanafunzi.Sara alianza kupita kuangalia kila sura ya mwanafunzi wa kidato cha kwanza wote na kuhamia kidato cha pili.
"utajisikiaje akifuata Ester endapo ukinitaja?yule sijamuua nimekuonesha tu kuwa nipo ndani ya shule hii kutekeleza kazi yangu,nikiwamaliza ninao wataka nitaondoka."akasikia sauti ikipenya masikioni mwake Sara na kumfanya ashike sikio lake kuiziba hereni yake.Kitendo kile kilimfanya Ester aliyekuwa kwenye mstari na wenzake afahamu kuna jambo linaendelea hapo ndio maana Sara yupo na hali ile.
"kwanini unawadhuru watu ambao hawana hatia MICHAEL?kwanini?"alisema Sara kwa imani yao akiongea na yule mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la Michael.
"usijifanye hujui Sara,hawa ni damu yetu na tunairudisha ilipotoka na huwezi kunizuia"alisema Michael kwa hasira wakiongea wao wawili tu kwa hisia.
"sasa umemdhuru huyu kijana wa watu ili iweje?"
"hapo nimekuonya tu,muache Ester kama alivyo using hate na usimzoeee,ni damu yetu ile hupaswi kuingilia Sara,laa sivyo nitawaangusha wengi tu na hata nikutengezee kesi wewe."alisema Michael akimtisha Sara.
"siwezi....siwezi kumuacha binti wa watu aliyezoea maisha ya ubinaadamu aje kuwa shetani kama nyie,natetea haki zao kama nilivyoagizwa na marehemu mama yangu."alisema Sara.
"ahaa sawa kama unamfuata mama yako,pita hapa nilipo halafu nitaje ndio utajua nini namaanisha"alisema Michael na kumgeukia Ester kumtazama bila yeye kujua lolote.Sara alipoona vile akamtazama Ester ambaye alikuwa naye anamuangalia Sara na kumbinyia jicho ili ajue kama kuna hatari yeyote pale aweze kukimbia.Sara akaendelea na kazi ile ya kuangaliwa wanafunzi pamoja na Madam.
Alipozidi kusogea alifika karibu na Michael na kubaki kuangaliana kwa chuki kila mmoja,Sara alibaki kutimiza kichwa amtaje Michael au la!!,kuna moyo ukawa unamwambia mtaje ili walimu wachukue hatua huku upande mwengine ukimkanya asithubutu kusema ili kuyaokoa maisha ya Ester na wanafunzi wengine,alimtazama Michael kwa hasira na bila kupepesa macho akampita na kuendelea kuangalia wanafunzi wengine huku roho inamuuma kumpita muhusika.Huku Madam alipita kwenye madarasa mengine bila kufanikiwa na kukutana na Sara akamwambia hakumwona.Madam aliwaamuru wanafunzi aingie madarasani wakiwa hawaelewi kinachoendelea.
"we nenda darasani Sara ngoja tujue maendeleo ya yule mwanafunzi hapo baadae"alisema Madam akionesha kuchoka kwa kazi ile.Sara aligeuka na kuelekea zake darasani kwake ambako wanafunzi wenzake walimganda kutaka wajue kumetokea nini,akawaeleza habari za kuanguka kwa yule kijana chooni baada ya mwenzake mmoja kutoka chooni jambo lililowafanya baadhi ya wanafunzi waga kuhofia kwenda chooni.Sara alirudi kwenye sehemu yake na kujikuta akilalia meza yake kwa uchovu huku akitafakari mambo anayofanya Michael kwa siku chache tu aliingia shuleni pale,Ester alinyanyuka pale alipo na kumfuata Sara akijaribu kumuongelesha lakini Sara alinyanyuka tu mkono kumaanisha hataki kusumbuliwa,Ester alirudi zake kwake na kutulia huku akimtazama tu Sara aliyekuwa amelala,Ester alikuwa na shauku ya kufahamu ilivyokuwa hadi jambo lile likatokea. Sara hakutaka kuongea na yeyote hadi muda wa kurudi nyumbani ulifika akaanza safari ya kurudi,Ester haikuwa mbali naye na kuamua kumfuata Sara kuongozana naye na kuanza kuongea mambo ya kawaida,hakuonekana mwenye furaha siku hiyo Sara jambo lililomfanya Ester abaki kukuangalia tu Sara.
"kwani kimetokea kitu gani Sara hadi umekosea raha kabisa hivyo?"aliuliza Ester na kumfanya Sara akunu tu niweke zake.
"Ah we acha tu yaani Ester...."alisema Sara na kumuangalia Ester."ulimuona yule mwanafunzi pale chooni akiwa anaongea na Madam.
"ndio nlimuona...si yule aliyeingia chooni ukiwa unamkimbilia?"
"ndio ....yule sio mtu mzuri hata kidogo.....ndio anayewataka nyie wote mliotajwa ili awauwe.....anaitwa Michael na yeye ndiye aliyemuuwa mwalimu Eddy,na kule chooni alimjeruhi yule mwanafunzi...."alisema Sara.
"HAAA!.....kweli?....."
"ndio hivyo Ester"
"sasa yule aliyekuwa mbele yake kwani naye yupo kwenye wale watu tuliotajwa?"
"hapana...yule hayupo ila alifanya vile makusudi,akinikanya mimi niwe mbali nawewe ili atekeleze kazi yake."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hee..."
"ndio hivyo....mtu anayefuata ni wewe Est...."
"bwana usiniambie Sara maneno hayo,hujui najisikiaje hapa"alisema Ester akionesha kuogopa sana baada ya kuambiwa vile,hata Sara akitumia na kuona kuna kazi ya kuilinda rafiki yake pamoja na watu wengine,hali ile ikawafanya wawe kimya kila mtu akitafakari kwa namna yake swala lile hadi waliofikwa makwao.
Siku zilizidi kusonga mbele huku yule mwanafunzi aliyekuwa ameondoka chooni akionekana kurudi afya yake ya awali,walimu walimuita ofisini wakiongozwa na Madam kutaka kujua kimetokea nini siku ile kama anakumbuka.Mwanafunzi yule hakuwa anafahamu lolote na kubaki kusema hata yeye hajui kilichotokea pale na kujikuta yupo hospitali ametundikiwa dripu tu.Hawakuweza kupata ukweli na kubaki kuachana na jambo hilo baada ya kumshukuru tu uzima wa kijana yule. Kwa Natasha naye japo kuwa na uzuri alio nao na kuwafanya baadhi ya wanafunzi wa kiume wa Madarasa ya juu kumtamani,kitendo cha siku ile alivyo oonekana kupandisha mashetani kiliwafanya waanze kumuogopa na kumuacha kumsumbua japo rafiki zake walikuwa pamoja naye wakimpa moyo,mara nyingi Sara huwa karibu na Natasha lengo ni kuhakikisha anamlinda juu ya mambo yanayo muandama.Akiwa kwenye harakati hizo upande wa pili Michael anaendelea kuhakikisha watu waliopangwa awaangamize wanapotea kweli,alianza kupiga hatua kuelekea kidato cha tatu na kuingia hadi darasani ambapo aliwakuta wanafunzi wanajisomea wengine wanapiga soga tu,moja kwa moja alielekea hadi kwenye dawati la Magreth ambaye alikuwa akiandika mambo yake ya masomo.
"samahani dada...wewe ndiyo Magreth?"aliuliza Michael na kumfanya Magreth amtazame.
"Ndio una shida gani?"alisema Magreth.
"kuna mkaka yupo nyuma ya darasa la form 4 ameniagiza nikuite mara moja"alisema Michael.
"anaitwa nani?"
"anaitwa Emanuel"alisema Michael na kumfanya Magreth atabasamu.
Ester alipomuangalia kwa makini yule mwanafunzi aliyeingia alifahamu ni Michael,mwanafunzi ambaye alishaambiwa na Sara kuwa ndiyo muhusika kwa mambo yote mabaya yanayotokea pale shuleni,aliohopa na kujikuta akisimama na kuropoka.
"We mwanafunzi hebu toka humu darasani,rudi darasa lenu"alisema kwa ukali Ester baada ya kujua Michael ni mbaya na hakuja kwa uzuri.
"Ester na wewe niiini...dogo si kaja kuongea na mtu kwani akapiga kelele mpaka ufoke hivyo."alisema mmoja wa wanafunzi mule darasani.
"mimi ni monitres na ninahaki ya kufanya hivi,amekuja kwanza bila kusalimia na laiti mnge...."alisita Ester baada ya kuona anataka kuropoka mambo ya siri.
Magreth alinyanyuka na kumshika mkono Michael na kuanza kutoka nje ili Ester asiendelee kuongea.
"We Mage..."alisema Ester baada ya kuona Magreth anaondoka na Michael,alijuwa tu kuna jambo linaendelea,haraka akaanza kuweka madaftari yake kwenye begi na kuyaweka sawa na yeye akaanza kutoka kutembea kuelekea nje,alipokaribia tu mlangoni Mwalimu Isack alitokea akiwa ameshika kitabu na kuingia darasani.
"Ester hebu njoo mara moja hapa kuna kazi nahitaji nikuachie ya kuondoka ubaoni"alisema Mwalimu Isack na kumfanya Ester akasirike,aligeuka na kumfuata mwalimu akaanza kumsikiliza na kupewa kile kitabu akielekezwa sehemu za kuandika na mwalimu akaondoka zake.Alipohakikisha mwalimu ameondoka akamuomba mwanafunzi mmoja afanye kazi ile na yeye akataka zake nje kuelekea kule alipoenda Magreth,alifika eneo lile nyuma ya darasa alimuona Magreth akiwa pekeake amekaa kama ana mawazo kichwani...taratibu Ester akaanza kumsogelea pale alipokaa.
"Magreth...vipi?"aliuliza Ester huku akimtazama Mage kwa makini akionesha kuwa na huzuni huku akiwa ameshika karatasi mkononi,mara tu chozi likaanza kumtoka na kumfanya Ester ashangae.
"Mage...una nini mbona unalia sasa,kuna nini kimetokea.?"aliuliza Ester na kukaa karibu na Magreth.
"Ester.....Ema hawezi kunifanyia hivi mimi....!!"alisema Magreth huku akionesha kulia.
"Nyamaza basi kwanza...nini akakufanyia Emmanuel kwani?"alisema Ester na kumfanya Magreth atoe ile karatasi kumpa Ester aisome ajue kilichoandikwa,Ester akaipokea ile karatasi.
Na kitendo cha kupokea karatasi ile tu kule aliko Sara alisikia makelele ya mtu akicheka tena kwa sauti na kumfanya azibe masikio yote mawili,aliposikia kucheka kile kwa makini akakumbuka siku ile alipolala lile daftari lake pale darasani na kushuhudia Magreth akimcheka Ester ambaye alionekana kuwa kama chizi na kutema tu maudenda kulichafua shati lake la shule.Alivyokumbuka hivyo alishtuka pale alipo akimuangalia Natasha.Haraka akanyanyuka mbiombio kuelekea darasani baada ya kuhisi kuna tatizo,aliing is darasani kama alikuwa anakimbizwa na moja kwa moja akaangalia anapokaa Ester na kweli hakumuona,alipopiga macho kwa Magreth naye hayupo,hapo ndio akajua kweli lile tukio lawezakuwa limetokea kweli,haraka akatoka mbio kuelekea kule alipoona lile tukio kimaajabu akiachia wanafunzi wamshangae.
"Halafu unajua Sara huwa simuelewagi muda mwengine kama chizi,siku ile alikurupa alivyoona kulala na kuanza kukimbia kwenda nje."alisema Denis akiwa na wenzake.
"utajuaje kama alibanwa na mkojo!"
"Sasa na leo je utasema nini na katokea hukohuko nje."alisema Denis na kuwafanya wenzake washinde kusema lolote.Denis alinyanyuka na kuelekea naye nje kukuangalia Sara Liu ajilizishe baada ya kumhisi vibaya.
Kule nyuma ya darasa baada ya kupewa karatasi ile Ester alianza kuisoma kilichoandikwa,lakini alishangaa kuona maneno ni magum kutamka na kuanza kuyasema kwa tabu.Kila anavyozidi kuyasoma ndio Magreth anavyopata furaha na kuanza kucheka, Ester alimshangaa Magreth akiendelea kucheka vile na hata dakika mbili hazikupita karatasi ile ikamdondoka kutoka mikononi Edter na kuanza kuuona mdomo ukiwa mzito,akasikia baridi kali mwilini na kupotea gafla huku alifumba macho,alipofumbua........hakuwa Ester yule wa mwanzo,udenda mfululizo ulimtoka mdomoni huku akimuiga kucheka Magreth aliyeoneka akimnyooshea kidole Ester na kumcheka,Ester naye akaanza kucheka cheka tu bila kujielewa pale.
Sara alipofika eneo lile kama hatua 15 mbele walipo wakina Ester na kuona sasa lile tukio,mwili wake ulisisimka na kupandwa na gazabu hadi macho yakabadilika kumtazama Magreth kwa macho yale yaliyotoa mwanga mkali kummulika Magreth ambaye alianza kuonekana kuunguzwa na mwanga ule na gafla tu Magreth akapotea kimazingira ya kutatanisha.Haraka Sara akamkimbilia Ester aliyeonekana tayari kuwa zuzu.
"Ester...Ester....oh my God......Ester nitazame vizuri...ni mimi Sara rafiki yako"alisema Sara akimshika mashavu Ester aliyeonekana kuzidi kumwaga udenda mzito uliochafua shati lake.
"Saaaraaa...veeeve...Saaraa"sauti ya uchizi aliyotamka Ester akimuita Sara ilimfanya Sara atoe chozi,akamshika Ester ambaye alionekana kucheka cheka tu na kumkalisha chini,akatazama huku na kule hakuna anayemuona,akamlaza Ester chini na kuanza kuyabadilisha macho yake kila aina ya rangi huku akisema maneno kadhaa na kumtemea temea mate Ester kwenye mwili wake.
"HAAAAAAH...SARAAA!!!?!!"ilisikika sauti ya mtu akionekana kushangazwa na ile hali na kumfanya Sara amtazame,alikuwa ni Denis aliyeonekana kushangaa vile alivyomuona Sara akiwa kwenye macho ya ya kutisha,alitazama chini akaona mwili wa Ester ukiwa umelazwa na Ester pale chini.Moja kwa moja akapata jibu kuwa Sara si kiumbe cha kawaida,ni mchawi na anataka kumdhuru Ester,hakuamini kile anachokiona hata Sara naye hakutegemea kama Denis angeweza kumuona kwenye hali ile maana alikuwa kwenye harakati za kumsaidia Ester rafiki yake,alipomtazama Denis mdomoni alionekana kutaka kupiga kelele ajaze watu,haraka akamuwahi kwa kwa kumgandisha pale aliposimama asifanye lolote Denis kisha akaendelea na kujaribu kusaidia Ester.Hakumaliza hata kufanya lolote alishangaa kumuona Madam Magdalena akiwa na Michael walisogea eneo lile..
"umeona Madam....yule pale....ona anavyofanya..."alisema Michael akimuonesha Madam jinsi Sara alivyo..
"We mtoto....kumbe ndivyo ulivyo?Sara....ni wewe kumbe....unamfanyaje mwenzio jamani.!!?"alisema Madam akiwa haamini kile anachokiona mbele yake.Sara alibaki kushangaa tu baada ya kuona Michael amemleta Madam kwa makusudi ili ambambikizie ile kesi,kwa vile anavyoonekana tu pale akiwa kamlaza mwenzio chini huku akiwa kwenye hali ile ya macho makali ni wazi kwamba yeye ndiye muhusika wa yale yaliyotokea chooni siku ile.Kwa kuona vile amekutwa pale,aliamua tu kupunguza kesi kwa kumgandua Denis pale aliposimama,akarudisha macho yake na kurudi kama kawaida huku aliona aibu kwa kile kilichotokea.
Madam alibaki alishangaa huku akisogea pale alipolazwa Ester na kumuona akiwa kwenye hali ile ya uchizi.
"We Sara...umemfanyaje mwenzio mbna yupo hivi..."aliuliza Madam huku akiinama kumnyanyua Ester.
"Madam....Madam....nimemshuhudia kwa macho yangu Sara anamtemea temea mate Ester huku macho yake akiwa kama paka."alisema Denis baada ya kumuona Madam pale.Sara alikuwa mpole baada ya kuona hana jinsi amekutwa kwenye tukio lile,alimtazama Michael aliyekuwa anatabasamu tu kuonesha mambo yake yanafanikiwa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wewe Sara ni MCHAWI!!?"alisema Madam kwa hasira.
"Hapana Madam naomba nisikilize mar......"
"Denis kagonge kengele haraka!!!"alisema Madam na kumfanya haraka Denis aelekee alipoagizwa.
"Nilimuona akiishika hiyo hereni yake sikioni ikibadilika badilika sasa sijui ina kazi gani"alisema Michael na kumfanya Madam amtazame Sara kwa hasira.
"Vua hiyo hereni!!!"alisema Madam na kumfanya Sara asite huku kutikisa kichwa kuashiria hataki.
"unajifanya jeuri si ndio? sasa ngoja.!!"alisema Madam na muda huo huo kengele ikasikika kuwaamuru wanafunzi waelekee mstarini, Taratibu Madam akamshika mkono Ester aliyeonekana na hali ile kama zuzu kwa kuchafuka shati lake kwa udenda uliozidi kumtoka tu mdomoni,wakaanza kuelekea mstarini ambako wanafunzi wengi waliokusanyika eneo lile walishangaa kumuona Ester aliyeshikwa na Madam akiwa na hali ile,walimu nao walishangaa kuona vile na kushuhudia Madam alisimama pale mbele sambamba na Ester.
Kule nyuma ya darasa Sara alibaki amesimama tu hana la kufanya baada ya kuona amejitia matatizoni,moyo ulimuuwa na kujikuta akipiga magoti chini na kufumba macho huku chozi likimtoka.
"Mama.....sina la kufanya tena hapa nishajulikana na watu zaidi ya mmoja,na bado naendelea kuingia matatizoni hapa shuleni,nifanyeje!"alisema Sara akiwa amepiga magoti pale,mara tu akasikia sauti ya mwanafunzi."Sara unaitwa mstarini...."sauti ilimfanya moyo umuende mbio na kumfanya akose nguvu,alijua atakapoenda mstarini lazima atajulikana mbele ya wanafunzi wote,akitumia sana huku akiendelea kutafakari namna ya kufanya.
"Sara mwanangu...ondoa shaka kuhusu hilo.."ilisikika sauti na kumfanya Sara anyanyue macho.
"Mama..."aliita Sara baada ya kuijua sauti ile.
"Pole mwanangu...hiyo no mtihani tu na unapaswa kuvumilia,nyanyuka tu uende ulipoagizwa na ufanye kile unachoambiwa wala usibishe...ni hatari kwako"alisema mama Sara na kumfanya mwanaye ashangae.
"Maaama....wanafunzi wote watanijua kuwa mimi ni nani so ndio itakuwa mbaya zaidi?"
"hujui kinachoendelea....wewe fanya kama nilivyokwambia.,Michael sio yule unayemdhani wa zamani,sasa ameshamuingia Magreth na anaelekea kwa wengine,chochote kitakachotokea kuhusu wewe ndivyo ilivyopangwa na wala usishtuke"ilisema ile sauti ya mama Sara na papo hapo ikapotea ile sauti na kumuacha Sara akiwa pale,alijishauri sana lakini alijikuta akuamini sauti ile ya mama yake,taratibu akanyanyuka na kufuta vumbi lililopo kwenye senti yake magotini na taratibu akaanza kupiga hatua kuelekea paredi,kitendo cha kutokea tu alishuhudia macho ya wanafunzi wakimtazama sana hadi akaona aibu na kuangalia chini.
Mwalimu mkuu Malamba alikuwa pia pale mbele akiwa amesimama karibu na Ester aliyeonekana na hali ile ya uchizi.
"kumbe ndio huyu..."
"halafu hata umzanii"
"demu mzuri kumbe MCHAWI"
"jamani watu wana roho mbaya..."
"siamini kama ni Sara aliyefanya hivi?"yalikuwa ni maneno ya wanafunzi ya chinichini yakimtazama Sara akiwa akasogea pale mbele,kila mwanafunzi alibaki kuishika mdomo hata Natasha alibaki kushangaa kwa kile kilichotokea.
"Sogea hapa..."no sauti ya Madam iliyomuamuru Sara asogee pale waliposimama.
"Piga magoti hapo....yani hata mwezi kujamaliza Sara umeonesha dhahiri kuwa wewe ni nani"alisema mwalimu mkuu na kumfanya Sara atii kama alivyoambiwa na mama yake akapiga magoti.
"Tangu naanza kufundisha hii shule hadi kuwa mkuu wa hapa sijawahi kuona wala kusikia kuna uchawi ndani ya shule hii wala kushuhudia,leo ndio naona hii hali baada ya kuambiwa kuwa Sara ndiyo mhusika wa jambo hili,sitaki kuamini kama ni kweli,...Sara.."aliita mwalimu mkuu na kumfanya Sara ageuke kumtazama."mimi ndio nilikuamuru na kukupa ruhusa wewe pekeako uvae hiyo hereni baada ya baba yako kuniomba hivyo....sasa nakuona tena sana....vua hiyo hereni sasahivi"alisema Mwalimu mkuu na kuwafanya wanafunzi wote wamuangalie Sara wajue nini kitatokea,Michael alibaki akiangalia tu huku akitabasamu baada ya kujua tayari kashamdhalilisha Sara ambaye baada ya kuambiwa vile aligeuka na kuangalia tu chini ya ardhi huku akiwa amepiga magoti.
"Toa hiyo hereni au husikii...?"alichangia Madam na kumfanya Sara ajisikie vibaya,alinyanyua sura yake na kuwatazama wanafunzi wakishuhudia kinachoendelea,alimuona pia Michael akiwa mwenye kumtazama tu Sara baada ya kumpa kesi ya hatari lengo ni kumzuia Sara awe mbali ili afanye mambo yake kwa amani.
Wakiwa kwenye zoezi hilo kuna bibi mama mmoja alionekana binti yake mmoja akiingia shuleni pale,walipofika tu karibu na paredi wakashuhudia wanafunzi wote wamesimama pale na walimu,mwalimu mkuu akigeuka alimuona mama yule akiwa ameshika binti yake mkono wakisimama,akawaonyesha tu kwa isharaya mkono kuwa waelekee karibu na ofisi yake wamsubiri.Mama yule akafanya kama alivyoagizwa na kukaa kwenye benchi kubwa nje ya ofisi ya mkuu wakisubiri.
Huku kwa Sara aliyakumbuka maneno ya sauti ile ya mama yake ikimsihi afanye vile anavyoagizwa na walimu,akajikuta akinyanyua mikono yake na kuipeleka kwenye lile sikio lililokuwa na hereni ile ambayo haijulikani ina kazi gani,wanafunzi na walimu wote wakatoa macho kutazama mikono ya Sara inapoelekea kwenye sikio lile hata yeye mwenyewe alikuwa akihofia,akaivua ile hereni na kubaki ameishika huku akilia,shule nzima ilikuwa umetulia kimyaa akisikika Sara tu akilia huku akiinama chini...akaanza kuangua kicheko cha dharau na kuzidi kucheka haki Michael aliyekuwa mstarini na wanafunzi wengine aanze kushangaa.Mwalimu mkuu alibaki naye kumtazama tu Sara huku akiwa ameshika Ester aliyeoneka na ile hali ya uchizi haelewi kinachoendelea..
"AR AR AR AR ARRRRRRRRRRRRRRRRRR.....Wala msiogope kuhusu mimi jamani,mimi ni mwema tu nipo hapa kwa Sara nina miaka 16 sijawahi kupata ukiona Dubai...tazama sasaaaaa nimerudi tena....Kauthar nimerejea tena duniani!!....sina haja ya kurudi kwa Sara tena namuacha na maisha yake na ilimfanya Ester taahira nikijua kwa vyovyote mtamkamata Sara mkimuhisi ni mchawi,ala hashaa...Sara ni msichana mwema sana mababu zake ndio walimfanya kuwa nyumba yangu niishi mwilini mwake na kufuli ilikuwa hiyo hereni ndio maana Mwalimu uliombwa na baba yake asivuliwe hereni hii akijua lazima nitataka endapo mtamvua,na kweli.....leo natoka tena anaondoka nikaishi mbaaali na hapa,nawaachieni Sara wenu mimi anaondoka na vitu changu nilivyoviachav kwake pamoja na vitu nilivyoviweka kwa Ester......"alisema Sara na muda huohuo Sara akaondoka chini gafla huku wanafunzi wakiogopa wengine wakitaka hata kukimbia baada ya kusikia vile,hata Michael alishangaa kuona vile wakati hajapanga iwe vile,gafla naye Eater a kadondoka pale aliposimama na kuzidi kumchanya Michael,alitamani afanye jambo palepale lakini aliona itakuwa amejiweka wazi na yeye.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Maneno yale yaliyozungumzwa na Sara yaliwaacha watu mdomo wazi huku wengine wengi tu walishapata jibu kwann Sara naye aaliingiliea na jini na siyo yeye, mstarini pale kukata na sintofahamu kila mtu akisema la kwake huku aliachana wale wawili wakiwa chini hakuna aliyewagusa wawasubiri hapo watakapoamka.Walimu wakabaki nao wanaulizana na kupeana mawazo baada ya zoezi lile.Haikupita hata dakika tano Mwakiwa wanazidi kutafakari lile jambo,Ester alikuwa wa kwanza kuinuka ambapo alipotazama na kufahamu kuwa yupo shuleni alishangaa,akaangalia wanafunzi kibao wakiwa wote pamoja na walimu wakimtazamahata yeye alishangaa,akaingia juu na yeye akaanza kuwatazama wanafunzi haelewi,alisikia harufu mbaya gafla na kuanza kujiangali,alishangaa kujiona yupo kama chizi tena mbele ya wanafunzi,aliona aibu sana akiendelea kupeleka macho ndipo alipomuona Sara akiwa naye ameondoka pale chini,haraka Ester akipata nguvu na kuanza kumkimbilia Sara kutaka kumnyanyua..
"Sara...nini kimenikuta best yangu jamaaaanii,"alisema Ester akionesha kuwa na uchungu hali iliyomfanya Michael zaidi kukasirika.
"mwalimu ina maana hamumuoni Sara jamani kadondoka!mbona mnaangaliana tu hamtoi msaada?"alisema Ester huku akianza kulia na kuwafanya watu waamini kweli Sara hakuwa yeye aliyefanya mambo yale mabaya laiti angefanya yeye Ester asingemlilia kiasi kile zaidi ya kumshtaki.BASI Ester alilia pale kwa muda na hatimaye Sara akapata kurudisha fahamu pale alipodondoka na kuanza kutazama pale alipo,naye akaanza kuwashangaa watu pale kuonesha hajui lolote kilichotokea,watu wote pale wakabaki wakishangaa hali ile na kuwafanya walimu waanze kujadili lile swala huku Sara na Ester wakibaki wamekumbatiana pale.
Hali ile ilimfanya Madam awaruhusu wanafunzi warudi madarasani kwao na walimu wakaingia nao ofisini pia wakiwaacha wawili wale pale chini.
Si Magreth muongeaji na mropokaji daradani wala Denis aliyethubutu kuongea lolote juu ya jambo lile wote walitulia,darasa lilitulia kila mtu akiwaza kwa namna alivyolipokea yeye swala lile huku wengine wakilijadili.
Mwalimu mkuu aliwaita walimu wote na kukaa ofisini kwa dakika kadhaa wakijadili swala lile kwa kina,kila mtu alizungumza ya kwake vile alivyolipokea jambo lile kwa uzito na hatimaye mwalimu mkuu akatoa neno la mwisho na wote wakaliafiki ili kuweka swala hili muafaka.Mwalimu mkuu akarudi ofisini na kumkaribisha sasa yule mama wakawa wanaongea, Mama yule amemleta mwanaye pale shule baada ya kuwasiliana na mwalimu mkuu siku chache kabla ya siku hiyo hivyo alienda kukamilisha tu mambo sawa.
"basi haina shida maadamu mambo yamekamilika ni yeye tu kama kuja kesho jar tu aanze masomo,sare si ushashona?"alisema mwalimu mkuu.
"ndio jana ametoka kuichukuwa sketi yake kwa fundi ipo tayari"alisema yule mama.
"Basi sawa afike kesho shuleni aanze"
"Sawa mwalimu...side ngoja twende basi atakuja Sasha kesho mweyewe"alisema mama yule na kusimama na yule binti yake wakaagana na mwalimu nao wakaondoka zao.Wakipita pale paredi na kuwaona Sara na Ester wakanyanyuka kuelekea ofisini kwa mkuu baada ya kupata taarifa kuwa wanaitwa,mama yule aliwatazama huku akiwa anaondoka zake na mwanaye.Waliingia moja kwa moja kwa mwalimu mkuu na kumkuta anaandika karatasi moja maelezo fulani,walisimama na kubaki kumuangalia huku wakimsubiri amalize kazi ile,baada ya robo saa Mwalimu mkuu akamaliza kuandika ile karatasi na kuiweka kwenye bahasha ndogo kisha akwatazama Ester na mwenzake Sara ambao baada ya kuona mwalimu anawatazama aibu ikawajaa wakainama chini.
"Nadhani mshapata kidogo kuelewa jinsi hali ilivyokuwa japo ina sadikika haikuwa mnatambua lolote,hivyo tumekaa na walimu na kuona bora tufanye jambo ili hali hii hata wale wanaoipata habari hii wataichukuwa kwa namna nyengine,hivyo basi walimu umeamua jambo moja....Ester utaenda kupumzika nyumbani wiki hii nzima ili kutuliza hili zogo ambalo linaendelea shuleni hapa...Sara..."aliita mwalimu mkuu huku akinyanyua mkono ulioshika ile bahasha na kumpatia Sara."kwa hili lililotokea limeonesha sura nyengine hapa shuleni,japo tunakuhitaji kuendelea na kupata taaluma ya shuleni hapa lakini hatuna jinsi,tumekusimamisha shule kwa muda usiojulikana hadi hapo hali itakapokuwa nzuri huku uchunguzi ukiendelea, maana baadhi ya wenzio na walimu wanaanza kukuhisi vibaya huenda hata matukio ya nyuma ya Natasha na hata marehemu mwalimu Eddy ni wewe unahusika,kwahiyo bora ukapumzike nyumbani Sara hadi hapo tutakapokuita uje...hakuna Mandalay kwa hilo,geukeni muondoke"alisema Mwalimu mkuu na kuendelea na mambo yake.Ester alitamani kulia kutaka kumuombea msamaha Sara lakini alishangaa kuona Sara mwenyewe anafungua mlango na kutoka nje,hali iliyomfanya na yeye kuamua kutoka..
"We Sara...wewe..."alisema Ester na kuishika mkono Sara aliyeonekana kukasirika."mbona upo hivyo wewee....umekubali kabisa adhabu hiyo hujui kama ndio ushafukuzwa h ivyo?turudi tukamuombe msamaha mkuu atakuelewa tu,hukuwa wewe pale ujuwe"alisema Ester.
"Ester nisikile kitu kimoja...ulikuja hapa shule ukiwa mwenyewe soma kwa moyo wako na mimi nimekuja hapa shule nikiwa pekeangu na leo naondoka mwenyewe...Jay yako"alisema Sara na kumfanya Ester ashangae....Sara aligeuka na kwenda kuchukua madaftari yake darasani na kuondoka zake huku Ester alibaki kumshangaa,machozi yalimtoka na kujikuta anapiga magoti chini akimsindikiza Sara kwa macho,alijuwa umuhimu wa Sara pale shuleni,yeye ndiyo aliyekuwa anawalinda dhiki ya mambo mabaya yanayofanywa na Michael na leo anaondoka kumaanisha Michael anakuwa huru kufanya mauaji aliyoyapanga.
Hata Michael naye alikuwa darasani akimtazama tu Sara akiiaga shule ile na kubaki kutabasamu.
"nipo huru sasa....naanza kazi rasmi kesho."alijisemea Michael akiwa darasani huku Ester akiwa kule nje akiendelea kulia pale chini.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule mama na mwanaye walifika mbali sana na shule ile na walipofika sehemu tu gafla mama yule akabadilika gafla na kuwa mwaume mtu mzima,yule binti Sasha naye alipomtazama baba yule akabaki kutabasamu tu na yeye akajibadilisha kuwa na mwili wake halisi,sura ya SARA ilijitokeza na mwili ule ule wake akionekana na ile hereni yake,akaivua na kuitupa mbali akimtazama yule baba ambaye alionekana ni baba yake mzee Junior....safari ikaendelea kurudi makwao.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment