Search This Blog

SARA (MSAADA WA MATESO) - 3

 







    Simulizi : Sara (Msaada Wa Mateso)

    Sehemu Ya Tatu (3)





    "Denis....unajisikiaje?"aliuliza Ester na kushuhudia Denis akiitikia kwa kutikisa kichwa kumaanisha yupo salama.Ester akamgeukia Sasha kumuangalia vizuri maana haamini,hakujua kama Sasha ana nguvu zile za maajabu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sa..sha.....kumbe na wewe unanguvu za ajabu kama yule rafiki yangu Sara?"alisema Ester na kumfanya hata Denis sasa afumbue macho vizuri baada ya kusikia kumbe Sara alikuwa na nguvu za ajabu kweli.Sasha alimtazama Ester na kubaki akitabasamu tu.

    "kwa sasa naitwa Sasha...ila jina langu halisi naitwa SARA..Sara yule rafiki yako unayemjuwa wewe ndio mimi,mwanzoni akitaka kumueleza ukweli nlitaka kuficha mambo kadhaa ambayo huenda yakawafanya wewe Ester na wenzako msiweze kunielewa."alisema Sasha nabpapo hapo akajikunyata na kugeuka rasmi kuwa Sara,hali iliyomfanya Denis aliyekuwa pale chini anyanyuke haraka kutaka kukimbia,Ester akamshika.

    "Usikimbie Denis,Sara sio mbaya,hebu rudi utulie umsikilize."alisema Ester na kumfanya Denis arudi lakini bado akiwa na wasiwasi alimshangaa Sara,hakutegemea.





    "Hupaswi kuniogopa Denis mimi sio kama hao wanaowaandani muda wote,hebu tuambie kitu gani kilikuleta huku porini?"aliuliza Sara na kumfanya sasa Denis aanze kukumbuka nyuma kuwa alikuwa na Natasha waliwa wanaongozana wote wakiwa kwenye hisia nzito zilizowafanya watamaniane miili yao,ikapelekea Winnie vichakani na kutaka kufanya lile tendo,lakini walipokuwa wakiandaana Denis alipata kumuona Natasha alibadilika gafla sura na hata baadhi ya sehemu za mwili wake huku makucha yalimtoka vidoleni na kuanza kumkwaruza Denis mwilini mwake kwa kudhamiria kuua, Denis alipiga mayowe sana baada ya kukamatwa koo lake na makucha yale yaliyomfanya adondoke chini asijuwe kilichoendelea,a kashtuka sana.

    "Jamani Natasha jinii.....kweli ni jini Natasha,"alisema Denis kwa wasiwasi huku akipeleka mkono wake miongoni kuangalia majeraha aliyopata,alishangaa kuona hana hata jeraha moja huku akiendelea kulishika sehemu nyengine,alihisi ni ndoto anaota ama..!

    "Ina maana ulikuwa na Natasha huku?mnafuata nini sasa na nyie huku maporini Denis mnajitafutia matatizo wenyewe?!"alisema Ester na kumfanya Denis aangalie chini kwa aibu.

    "Ester usimlaumu Denis wala nani,wewe unajua kinachosababisha haya,..Denis naomba uelewe yule hakuwa Natsha mwenyewe,aliingiwa na kitu kilichomfanya akuyendee haya na hapa wewe unajulikana ushakufa."alisema Sara.

    "Nimekufa?haah.....yanii...mimi nime....."

    "ndio hivyo nilivyokwambia na elewa hivyo,na kwa hili lililotokea hapa litaleta upinzani mkubwa sana.Denis...tambua kuwa wewe,Natasha,Magreth na Ester ambaye anafahamu haya...wote mnatafutwa na viumbe si binadamu wa kawaida ili wawauwe"

    "Sara unaongea nini mbona sikuelewi?"

    "Elewa hivyo Denis...tunatafutwa kweli tuuliwe,kuna mtu pale shuleni ndiyo anayafanya mambo yote haya,siku ile kama unambuka tulichapwa na marehemu mw.Eddy kisa hatukufuta ubao,sasa yule hakuwa mwalimu halisi aliingiwa na kivuli cha jini kilichomfanya afanye mambo yale hadi wanafunzi tukashangaa kuona ni mara ya kwanza mwalimu anachapa,na ile siku ndio nilipangiwa mimi kufa pindi tu nitakapochapwa zile fimbo"alisema Ester na kumfanya Denis amshangae.

    "Haah....sasa ikawaje?imekuwaje sasa hadi ukawa mzima.?"aliuliza Denis.

    "Ni Sara...Sara ndiyo aliyeyafahamu hayo mapema ndiyo maana alimuacha wewe upigwe japo na wewe ni mmoja wa wanaopaswa kufa lakini haikuwa muda wako,yeye ndiyo alitumia nguvu zake kuzuia lile tukio,na ilisadikika kumbe Natasha alikuwa akitamaniwa sana na mwalimu Eddy,alikuwa akimsumbua sana binti huyo ndiyo maana aliuliwa mwalimu kwa tamaa zake,alimpenda binti ambaye naye anapaswa kufa."alisema Ester na maneno yale sasa yakamfumbua macho Denis ambaye alikuwa hajui.

    "Ah makubwa,sasa tunauliwa rumefanya nini?na nani huyo anayeuwa watu hivi?"aliuliza Denis kwa mkupuo akionesha simanzi usoni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "kuna kijana anapenda kuingia darasani akimfuata Magreth,anaitwa Michael."alisema Sara.

    "Haah....kale kadogo kaMichael ndio kanatuumiza sisi akili?"alishangaa Denis.

    "yule sio binadamu,usimchukulie ni wa kawaida...anauwezo mkubwa sana kuliko unavyomfikiria.Ngoja niwaweke kitu ambacho hakuna anayekijua kati yenu....Ester,wewe Denis na wezenu tambueni kuwa nyie ni damu ya hawa viumbe wa ajabu nikiwemo na mimi Sara"alisema Sara na kuwafanya wenzake amtazame na kumsikiliza kwa makini maana ni kitu kipua wanakisikia."baba yangu mzee Junior alikuwa akiishi mwanamke ambaye ndiyo mama yangu kwa muda mrefu sana na kufanikiwa kumpa ujauzito,baadae ndio mama akaja kumwambia baba kuwa yeye ni kiumbe chengine so binadamu ila amempenda baba kwa dhati na hataki kurudi kwenye jamii yao,sasa jambo lile limewakera jamii yake maana hairuhusiwi wao kuwa na mahusiano na binadamu,hivyo baada ya kujuwa kuwa kuna wenzao wengi walikuwa na mahusiano na binadamu ikawafanya sasa waingie duniani kuwachukuwa watu wote waliozaliwa wenye asili ya jamii yao,wawauwe ili wawarudishe wakaishi kwenye jamii yao mbali kabisa na dunia yetu.na nyie ni miongoni mwa watu hao huenda akawa baba yako au mama yako ndiyo alikuwa jamii ya viumbe hao ndio maana mnasakwa sana ili mrudi huko,nyie ni damu yao na hawataki kuacha mbegu duniani"alisema Sara na kawaacha midomo wazi Denis pamoja na Ester pale walipo"baba yangu mzee Junior ni miongoni wa binadamu waliozaa na mwanamke wa jamii hiyo na ndio alikuwa Malkia wao huko kwenye jamii yao mwenye uwezo mkubwa,yeye alipinga sana hili jambo kwakuwa naye ni miongoni mwa waliokuwa na upendo kwa binadamu ambaye ni baba,huyo ndio alikuwa mama yangu Malkia Aznaty Sheeran."alisema Sara na kuwaeleza mambo mengi sana kuhusu jamii hiyo lam alivyoelezwa na mzee Junior kule makaburini na kuwafanya sasa waelewe ni kwanini wanafuatwa namna hiyo,taratibu Denis alianza kuelewa hayo mambo maana alikuwa akiishi na mama yake lakini hakuwahi hata siku moja kumuona baba,na siku zote mama yake alimficha ili asijuwe chochote mwanae mpaka naye alipofariki na kumuacha Denis mikononi mwa shangazi yake ambaye hadi sasa ndiyo anakaa naye,alifahamu huenda baba yake ndio atakuwa wa jamii hiyo ya viumbe vya ajabu,alimtazama Sara huku akionesha majonzi.

    "ina maana na sisi utakufa kama wengine ndiyo turudi huko kwao?"aliuliza Denis.

    "Ndio....lazima utakufa tu urudi kule,lakini kuna watu wanaoitwa wasuriati hao ndio wanawataka kwa namna ya tofauti hao ndio wakina Michael,inasadikika kuwa hadi sasa hiyo jamii yao haina kiongozi baada ya yale mambo kutokea yule Mfalme akapewa kazi ahakikishe mwanaye ndiyo anawarudisha ninyi na watu wengine walizaliwa huku duniani wenye asili ya kule ili wapate kuongoza falme ikiwa chini ya mtoto wa Mfalme,Michael.Ndio maana Michael anawasaka kwa nguvu zote awamalize ili sense kukabidhiwa falme waimiliki kwa mabavu,jambo lilimuumiza sana mama yangu kwa kuona falme yao inaenda kumilikiwa na wasuriati ambao hawapaswi kabisa kumiliki maana watakuwa kuwanyanyasa sana hapo baadae,ndio maana alimueleza baba yangu kuwa mimi ndiyo mtetezi wa watu kama nyie,natetea haki ya mama yangu,natetea falme yangu,nihakikishe anawalinda msife umuende kuwa watumwa wa wasuriati"alisema Sara na wenzake sasa wakaelewa kila kitu,walikaa sana pale huku Sara akiwafariji wenzake ambao nao taratibu walianza kuelewa lengo.



    Hata jioni ilipofika baada ya kila mtu kurudi makwao Ester alikuwa na bibi yake mezani baada ya kumaliza kula wakawa wanaongea.

    "hata mimi sikuwa najua lolote mjukuu wangu hadi kifo cha mama yako kilivyotokea tihuzunika sana na baba yako ambaye ni mwanangu,th law tunaendelea na maisha yetu nikiwa nakulea mimi,baba yako naye akaanza kuumwa gafla tu na siku alipoona hali sio nzuri akamwita na kunieleza kuwa yule mkewe aliyekaa naye alikuwa sio binadamu,alikuwa ni kiumbe cha jamii nyengine,mwanangu alifarikibpale na kuniachi mtoto wake nimlee ambaye ndio wewe Ester,tangu alivyoniambia kuwa yule mkewe no kiumbe chengine nikawa nahofu sana ndio maana nikakulea kimazingira ya ya kumjuwa Yesu Kristo aweze kukuongoza kwenye maisha yako,nashukuru hadi sasa una afya tele japo vikwazo ni vingi ila usivunjike moyo mjukuu wangu"alisema bibi yake Ester kwa upole huku mjukuu wake akimsikiliza kwa makini.

    "sasa ndio hivyo bibi na sisi tinahitajika kwenda kwenye jamii hiyo alipotokea mama yangu"alisema Ester.

    "Ester mjukuu wangu....hayo mambo ni ya kuhisi huenda ikawa au laa,muombe Mungu sana"alisema bibi na kumfanya Ester aelewe,akamsogelea bibi yake na kukaa karibu yake.

    "hebu tufumbe macho tuombe bibi,haya mambo tuyakemee kabisa."alisema Ester na kumfanya bibi yake kweli afumbue macho kwa imani,Ester naye akafumba macho na kuanza kuomba.

    "Mungu baba uliye mbiguni, jinablako litukuzwe na ufalme wako udumu milele,wewe ndiye Ebenezer,wewe Alpha na Omega na hakuna kiumbe chochote kinachoweza kuzuia Mari zako baba,baasi najikabidhi kwako baba mimi na bibi yangu update kuwa salama usiku huu na hata milele,baaba mwanao napita kwenye mitihani migumu ambayo kwa umri niliyo nao siwezi kumiliki tabu za mitihani hiyo,na niwewe pekee tunayeweza kukukimbilia kwa kunyeyekea baba uweze kututia nguvu,uweze kuingilia swala hili la mimi pamoja na wenzangu wale tunaosoma pale shuleni baba ukapate kutia nguvu zako na baraka zako yule adui ,shettani ashindwe katika jina lako Yehova, walinde wale rafiki zangu baba hata na yule tunayetaraji hi mwema kwetu Sara uweze kumpindua naye azidi kutete haki,amekutwa kujitolea sana kutulinda lakini pia naye alipitia kwenye mateso makubwa sana,ni MSAADA WA MATESO aliyoupitia kwa kipindi kile hadi kufukuzwa shule kwa kuhisi alinidhuru mimi,ni MSAADA WA MATESO aliyoupitia pia mama yake akitetea upendo kwa mumewe,yote hayo baba unayajua na ni wewe ndiye mwenye amri kuu ya kuutuliza hili jambo,na naamini wewe ndiye mmliki wa viumbe vyote ulimwenguni naamini utatenda muujiza baba,ni katika jina la Yesu Kristo bwana na mwokozi aliye hai ......EIMEN..."alimaliza kuomba Ester pale akiwa na bibi yake ambaye aliguswa na maneno ya mjukuu wake hadibchozi likamtoka na kubaki kumkumbatia tu mjukuu wake pale walipo.



    Usiku kabisa watu wote wakiwa wamelala Natasha alianza kujiwa na njiani mbaya akikumbuka namna ilivyokuwa kule kichakani akiwa tayari kufanya tendo lile na Denis.

    Njozi ile ilimuonesha Muda ule akionekana kukumbatiana na Denis na kuanza kuchojoa nguo zao taratibu,Denis alimvamia Natasha nabkuanzabkuupapasa mwilibwa binti yule ambaye naye hisia zilimuandama akilifurahia lile tendo na kujikuta akimkumbatia Denis kwa hamu ya kufanya lile tendo,gafla tu akaanza kubadilika mwilini,makucha yalimtoka huku meno makali na marefu yakichomoza mdomoni mwake,akaanza kumkwarua Denis na nakucha yale mgongoni na sehemu nyengine hali iliyomfanya Denis apige kelele,alimcharanga na makucha yale mfululizo hadi usoni kasi cha kumfanya Denis akose nguvu,taratibu akaanza kulegea na kudondoka chini,Natasha alichukuwa mti mkavu pembeni na kukamata mkononi kisha kwa nguvu zote akakishusha kichwani kwa Denis ambaye papo hapo akapoteza maisha,Natasha alionekana mwenye hasira akiwa kwenye sura ile ya kutisha sana akiwa amelishika lile gongo,mara tu akabadilika nabkurudi kama alivyo mwanzo,alijishangaa mwenyewe kuona amelishika mti,alipotazama mbele akabaki amefumbwa mdomo baada ya kumuona mwili wa Denis ukiwa pale chini umetapakaa damu,aliogopa sana baada ya kuona hali ile ambayo hata yeye haelewi ilikuwaje,kwa kichanganyikiwa vile palepale akaanza kukimbia mbali na eneo lile.Alishtuka pale kitandani na kukaa huku akiangalia huku na kule Natasha,hivyo ndivyo ilikuwa muda ule kabla ya wakina Sara hawajafika eneo lile.Natasha alitetemeka kwa kuhisi huenda amemuua Denis muda ule japo yeye haelewi jinsi ilivyokuwa,akitafakari hapo asubuhi kukicha itakuwaje atakapofuka shule asikie hizo taarifa za msiba,na itakapojulikana mhusika ni yeye itakuwaje?alitoa kabisa Natasha hata usingizi ukapotea kabisa.



    Asubuhi kulipokucha wanafunzi kama kawaidia waliendelea kufanya usafi,muda wote huo Michael alikuwa amehakikisha kuwa Natasha ametulia vema kule maporinibkwa kumuingiza roho ya kichawi iliyomfanya Denis kwa sasa aitwe marehemu,hivyo akawa anangoja tu taarifa za kufa kwa mwanafunzi Denis ziweze kutangazwa pale paredi Muda wa usafi ulipomalizika wanafunzi walielekea zao paredi na kupewa matangazo machache kisha wakarudi za madarasani kwao,Michael alishangaa kuona kimya walimu hawakupata taarifa za kuuawa Denis au vipi?,hata alipofika darasani kwake hakutaka kabisa kukaa,alinyanyuka na kuelekea darasani kwa Natasha,alipofika nje ya dirisha alimshuhudia Natsha akiwa ametulia kwenye kiti chake huku akionesha kuwa na wasiwasi moyoni,alijuwa bado atakuwa na woga wa kile alichodhani yeye ndiye mhusika wa mauaji wale ya Denis,aligeuka kuelekea kidato cha tatu kuangalia kinachoendelea.Naye Natasha hakutaka kuamini kile kilichotokea,taratibu naye akanyanyuka kuelekea darasani kwa Denis kuhakikisha kama ni kweli amekufa au laa!.

    Michael alipofumbua tu mlango wa darasa lile macho yake yakagongana na macho ya Denis aliyekuwa amekaa kwenye kiti chake akapanga madaftari yake,alishangaa sana Michael na kugeuka uso wake kumtazama Sasha aliyeonekana akitabasamu tu huku akiwa ameshika kitabu cha riwaya ya TAKADINI.Kwa kuzuga tu Michael alipiga hatua kuelekea kwa aliyemzoea Magreth akitengeneza tabasamu la kinafki kuongea naye.Ester naye alibaki kumtazama kwa hasira sana Michael hampatii jibu.BAADA ya muda kidogo Michael akitoka zake kuelekea darasani kwao huku akiwa amekasirika kuona Denis yu hai,alimtazama Sasha pale alipokaa na kujua ni yeye ndiye aliyemuongilia kwenye kazi yake,alipokamata tu mlango ili stoke nje alisikia sauti ikimuamuru.

    "We dogo hebu subiri hapi"sauti ile ilimfanya hata Sasha na wanafunzi wengine ageuke kuangalia,alikuwa ni Denis aliyeonekana alinyanyuka pale alipo na kumfuata Michael mkuku mkuku na alupomfikia akamkamata shati lake na kufungua mlango w akatoka nje akionesha kuwa na hasira,watu walianza kucheka na wengine wakaanza kuhisi vibaya huenda wivu ukawa unasumbua Denis,lakini kwa Sasha na Ester haikuwa hivyo wakabaki kushangaa kwa kitendo alichokifanya Denis na kubaki kutazamana tu,ikawabidi na wao wanyanyuke kutoka nje huku wanafunzi wenzao wakiwatazama.

    Huku Denis alimchukua Michael kwa hasira zote akiwa amumkunja shati lake kumpeleka nyuma ya darasa,akamuweka ukutani na kubaki kumuangalia kwa hasira.

    "Hivi wewe mtoto unakichaa?unaona raha kuuwa wenzake ili upate unachokitaka si ndio,huna hata chembw ya huruma unaleta matatizo shuleni hapa watu hawasomi kwa amani kila siku matatizo tu hayaishi,kwanini?naongea na wewe kwaniniii?"alisema Denis kwa hasira na muda ule wakina Ester wakatokea na kuanza kumtukuza hasira Denis,hali ile pia ilimfanya hata Magreth kuwa na mashaka pale darasani maana ni yeye ndiye anafuatwa na Michael kila siku akahisi huenda Denis akamuumiza Michael kisa yeye,naye akanyanyuka na kutoka nje,alipotokea tu amekumbana na Natasha ambaye naye alipofika sehemu ile akasikia kelele nyuma ya darasa ambapo Magreth alikuwa akielekea huko,naye akafuata kujua nini kinaendelea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hebu tulia kwanza basi Denis nakuomba,usiwe na hasira za hivyo ndugu yangu"alisema Ester akiwa ameukamata mkono wa Denis uliyokunja shati la Michael,muda huohuo Magreth na Natasha ndiyo walikuwa wanafika eneo hilo na kila mmoja akabaki kustaajabu,Magreth alishangaa kuona Denis amesikia hatua ile ya kuwa na hasira hadi kumkunja Michael,alijuwa kwa vyovyote Denis alihisi vibaya kuhusu Michael na Magreth.Lakini kwa Natasha alibaki kushangaa kumuona Denis akiwa salama kabisa hana hata dowa la jeraha mwilini mwake,hakuamini ikabidi amkimbilie kumshika Denis na kuanza kumuangalia kila sehemu huku wote wakibaki kimya kumtazama tu,hata Michael alikuwa akitazama tu.

    "Denis.....upo salama kweli....nikiwa naotaaa au?"alisema Natasha akiwa haamini,Denis akivuta pumzi na kuishusha kwa nguvu huku akimtazama Natasha.

    "sikia Natasha nikwambie,mimi niko salama kabisa na wala hukuwa unaota....Yale yote ni ya kweli na aliyefanya unyama ule ni huyu dogo hapa anaonekana Mpole kumbe ni muuwaji"alisema Denis.

    "We Denis umerogwa?kijana wa watu mtuli...."

    "wewe Magreth hujui lolote linaloendelea hapa,huyu ni muuwaji,na uzuri wake wote tumekutana hapa,alitaka kutuuwa sisi site hapa,alianza kwa Natasha huyu akamuingia mwilini na kumfanya Natasha aonekane amepandisha mashetani,kila mtu saivi anakuwa kuwa Natasha Ana mashetani,watu wanamuogopa,akaja kwa mwalimu Eddy ndio yeye alim....."Sasha akamfumba mdomo Denis baada ya kuona anataka kuongea maneno ambayo hayapaswi kuongelewa hadharani.

    "Denis...inatosha."alisema Sasha na kumfanya Denis atulie japo jasho la hasira likimtiririka.Kwa uchache wa maneno aliyoongea Denis yalianza kumshtua Natasha na kujuwa kuwa yale mashetani kumbe aliekewa anahusika ni huyu Michael.

    "kama unaniamini Denis naomba umuache Michael sasahivi."alisema Sasha kwa sauti ya unyenyekevu,kwa mambo aliyofanya Sasha kwa Denis ilimfanya kweli Denis amuamini,akautoa mkono kifuani kwa Michael ambaye alionekana kukasirika sana kukunjwa shati.Sasha akamsogeza Denis pembeni na yeye akisimama sasa kutazamana na Michael aliyeonekana kukasirika.Wakiangalia wawili hao kwa macho ya hasira.

    "kwa hali hii huwezi kufanikiwa jambo lako hata siku moja,leo hawa wote watakujuwa kuwa wewe ni nani?unategemea nini kitatokea hapa shuleni ukijulikana?jiandae sasa tena uwaambie na wenzio narudi,narudi kukuletea kiti cha MAMA yangukwa yote mliyomfanyia mama yangu mtalipa kwa damu na sitomuacha hata kiumbe mmoja,hawa ni binadamu na sio watu wenu,kila mmoja Ana haki ya kupenda pale alipopenda wala usimchagulie,amependa binadamu sawa,amependa shetani sawa,amependa jini sawa wala msitake kuweka mipaka kwenye mapenzi."alisema Sasha kwa hisia ambayo hakuna yeyote kati yao pale walipo alisikia kinachoongelewa zaidi ya Michael na yeye tu,ila Ester alishajuwa kuwa kuna mazungumzo yanaendelea maana alikaa sana na Sara na kujua baadhi ya mambo hivyo ikamfanya awatulize wenzake waliokuwa wakiulizana nini kinaendelea mbona watu wanaangaliana tu hawaongei?.

    "kati ya siku ambayo nimekasirika ni leo,sijawahi kushikwa kwa kudhalilishwa namna hii tena na binadamu mdogo tu,mwambie ana kazi nzito nilipanga kumuua hapa shuleni lakini sasa nitamfuata hata kwao nimuangamize,sikuhofii Sara hata kidogo,mama yako alikuwa Malaya kama wengine ndio maana akavaa na binadamu,na nishakula kiapo cha kuwauwa watoto wa Malaya wote huku duniani niwaeudishe kwao,nikiwamaliza hawa watoto wa Malaya wenzako unafuata wewe,huwezi kunivurugia kila mipango ninayoipanga"alisema Michael kwa kujihami na kushuhudia kofi zito likuwa shavuni mwake hadi damu kumtoka.Ester na wenzake walishangaa kuona Michael anatokwa na damu mdomoni,alifuta kwa mkono wake na kumtazama Sasha kwa makini.

    "nashukuru kwa hiki kibao...no changamoto kwenye kazi yangu,ila utakuja kulipa kwa hiki ulichokifanya mtoto wa Malaya wewe,jipange."alisema Michael na muda huo huo akaanza kuondoka zake,kwa kuonesha amekasirika kweli aliutazama mtu iliyokuwa pembeni akajiangalia kwa macho makali hadi ule mtu ukakatika na kuanza kudondokea waliposimama wakina Natasha na wenzake,Sasha alipoona vile naye akanyanyua mkono wake kujizuia ule mti ukabaki umeelea tu juu haukuwadhuru,ndiyo kwa mara ya kwanza Natasha na Magreth wanamshuhudia Sasha akiwa na nguvu zile,walishangaa sana.Sasha akau elekeza ule mti ukadondokea pembeni kabisa.Magreth akawa haamini kwa kilebalichokiona na kumshangaa Ester akiwa hana hata hofu.

    "we Sasha....kumbe...una nguvu za ajabu namna hii?"hakuamini kabisa Magreth,ikambidi sasa Sasha awaweke wote chini na kuanza kuwaelewesha mambo yote hasa Mage na mwenzake Natsha ambao hawakuwa wanajua lolote,walipoteza vipindi vya darasani asubuhi ile hadi ilipogongwa kengele ya kuwaruhusu wanafunzi kwenda kuoata chai,hakuna hata mmoja kati yao pale aliyekuwa na hamu ya kwenda kwenye chai,machozi yalimtoka sana Natasha baada ya kuona amepitia kwenye matatizo makubwa sana hadi kufika pale,hata Magreth naye alihisi kuumwa maana alishaanza kumzoea mtu ambaye alikuwa sumu hapo baadae muda wake ukifika,walimshukuru sana Sasha ambaye aliwaeleza ukweli kuwa yeye ndio Sara yule aliyefukuzwa shuleni pale.Wakiongea mambo mengi sana na baadae Sasha akawaambia muda wa kutoka kuna kitu atawapa,walimuamini na baadae kila mmoja akielekea sehemu yake.





    Kwa Michael ilikuwa ni hasira tu kwa kile kilichotokea,mipango yake mingi anakaribia kukamilisha lakini Sara ndio anakuwa kikwazo na kmrudisha tena nyuma,alifikiria sana siku hiyo akitafuta namna ya kudhibiti Sara Liu amalize ile kazi iliyomleta duniani.Kuona muda aliona ni bora amshuhulikie kwanza Sara kwa namna yeyote ile amuangushe ilikiwa rahisi kwa yeye kuwamaliza wale waliobaki.



    Huku darasani kila mmoja alichukulia lile swala kwa namna alivyolipokea,si Ester wala Denis wala Magreth aliyeweza kuwa sawa mara baada ya tukio lile waliloshuhudia la Michael,alionekana mwenye hasira sana na kuwafanya wapate hofu hadi muda ule.Sara ikambidi atoke kwenda kwa Natasha na kuanza kumpa moyo wa ujasiri na kumtoa woga kwa kumuhakikishia usalama,alimtoka nje ya na kukaa nyuma ya darasa kisha akaanza kumshika kichwa huku akinena maneno fulani yaliyomfanya Natasha ahisi kizungu zungu na baadae akatulia.

    "Kwasasa utakuwa na uwezo wa kutambua baya lolote litakalotokea hapo mbele ili ujuwe namna ya kulikwepa mapema"alisema Sasha na kumfanya Natasha atabasamu baada ya kuwekwa kitu kinachoweza kumsaidia.Vivyo hivyo aliwafanyia wale wengine wote na kuwaeleza kama alivyofanya kwa Natasha ikiwa ni kuwapa msaada was kukwepa tatizo au kitu kibaya pindi kitakapotokea,na hii akifanya kwa makusudi baada ya kujua sasa Michael a naweza akawafuata hata majumbani kwao ambako watakuwa mbali na Sara ikawa ni tatizo,kwa kufanya hivyo wanaanza wakaepukuana na mitihani hiyo na hicho ndicho alichoahido kuwapa kabla ya kuondoka shuleni siku hiyo.Muda uliyoyoma na muda wa masomo ulipoisha kengele iligongwa kuwafanya wanafunzi waelekee sehemu husika na kupewa baadhi ya matangazo kisha wakaondoka zao kurudi makwao.



    Siku hiyo Michael alikaa na baba yake na kumueleza yale yaliyotokea shuleni siku hiyo.

    "Kwanini anatusumbia akili yule paka?hapana hatuwezi kukaa kimya,Michael mwanangu...wewe ndiyo utakuwa Mfalme wa jamii yetu,Mfalme wa kwanza wa wasuriati kuomiliki falme kuu,na hakuna yeyote atakayezuia hili,tulimhofia Malkia Aznaty kipindi kile lakini siyo huyo mtoto anayesadikika ni damu yake"alisema babake Michael ambaye ndiyo alikuwa Mfalme enzi zile akipangiwa kumuoa Malkia Aznaty,na ni yeye ndiye alizaa na mfanyakazi na kumuweka sumu Malkia Aznaty iliyompelekea kufa.

    "HAPA nafikiria kitu kimoja tu na lazima tukifanye maana haina jinsi na muda unazidi kuupoteza,kama mlimuua mama yake kwa sumuwbasi hata Sara naye anapaswa kufa ili mambo yetu tuyakamilishe"alisema Michael kwa kudhamiria akionesha kweli hataki masihara,baba yake alimtazama na kubaki kutabasamu tu,akamshika bega kumpongeza kwa kile alichosema.

    "unazidi kukuuwa mwanangu...nahisi ushajuwa umuhimu wa wewe kuwa Mfalme.Nakubaliana na wewe kwa kile ulichosema,tutafanya hivyo mapema tu."alisema baba mtu na kuendelea kutabasamu tu.



    Nyumbani kwa akina Sara akiwa na baba yake walikuwa wamepumzika nje wakiangalia uzuri wa mbalamwezi ya usiku ule kwa jinsi ilivyokuwa inawaka.

    "washajua kuwa wao ni akina nani,sikutaka tena kuwa msiri maana kila kitu kitu kipo wazi na Michael amedhamiria kuwamaliza kweli,ila kuna nguvu nimewawekea mwilini mwao wenyewe wakijua ni ya kuepuka na mabaya tu lakini ni zaidi ya nguvu hiyo nihakikishe wanakuwa salama,naamini tutashinda vita hii kwa kutompoteza yeyote miongoni mwao"alisema Sara na kumfanya mzee Junior akubali kile anachosema binti yake "Uamuzi mzuri uliofanya Sara,na utambue kuwa hao ni watu wako wewe,wewe ndiye utakaye kuwa Malkia wao yakupasa uwatetee watu wako ili use kuwa Malkia bora"alisema Mzee junior.

    "usijali baba,nitafanya hivyo"alisema Sara na wakiendelea kuongea mambo hayo.



    Huku kwa Denis naye usiku ule alikuwa mwenye mawazo sana hasa akimfikiria Michael,mwanafunzi ambaye amekutwa akiwanyima amani siku zote,kuna muda alifikiria ni bora kwenda kuripoti Polisi kusudi Michael akamatwe lakini hakuna ushahidi wowote unaoweza kumfanya Michael anaitwa ni mtuhumiwa.Aliumiza kichwa sana bila kupata muafaka wa hilo japo kuna wakati akapata wasiwasi sana kuhusu h ili hasa akifikiria muda ule Michael alipotumia nh uvu zake za ajabu kuuangusha ule mti,ndipo alipojuwa swala hili sio la masihara.



    Asubuhi ya kesho yake masomo yaliendelea kama kawaida katika kila darasa huku miezi ya kufikia muhula wa kwanza ikikaribia.Kwa Michael alitaka amalize kazi yake mapema ili wanapokwenda tu likizo basi awe anaondoka na watu wake aliwakusudia na kwenda kuwa Mfalme wa ile jamii yao.Lea jupania kufanikiwa katika hilo alishirikiana na wenzake wengine ambao na kuwataka wakae njia ambayo Sara anapendelea kupita kutoka shule lengo no kumdhibitibkwa namna yeyote ile maana amekutwa ndio kikwazo katika mambo yao.N.a. kweli baada ya masomo kumalizika Denis akawa yu karibu na Sara baada ya kujua ndiyo tumaini pekee lililobaki katika kuyalinda maisha yake,sio kwake tu....hata Natasha pamoja na Magreth aliyekuwa ni muoga sana hasa baada ya kufahamu kuwa yu miongoni mwa watu wanaopaswa kuuliwa ili warudi kwenye jamii yao.Siku ile alitembea wote kwa pamoja walitoka zao shuleni huku Ester akiwapa wenzio moyo ili wawe katika hali ya kawaida tu siku zote.Wakiongea mambo mengi sana na kufurahi pamoja hadi walipofika kijijini kila mtu akakamata njia ya kuelekea kwao baada ya kuagana huku Sara akitaka baadae Ester aweze kuja kwao kama akiwa na muda.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Alikuwa mwenye furaha sana baada ya kuona hali ile aliyowaona hawakuwa watu wa kubisha sana kuhusu uzao wao maana kila mmoja wao alienda kwao na kuuliza kwa kudadisi na kupata ukweli wa kile walichoambiwa,mtu pekee aliyemuona ni jasiri na mpaka haki ni Ester,mtu aliyekuwa naye kwa kipindi chote cha misukosuko hadi kufika hapo na ndio maana anamtaka and hapo baadae huenda kuna mambo ya kuongea.Akiwa kwenye hali ya kuyafikiria hayo alishangaa kuona mwili wake unaingiwa na hofu gafla,mwili unasita kabisa kuendelea na safari,akajua kuna jambo baya lipo mbele na alipotambua hilo alibaki kuachia tabasanu na kumuona nywele zake,aliangalia panda zote na kuona hakuna mtu yeyote eneo lile,akapiga hatua kuendelea na safari yake lakini gafla tu anaonekana mtu akipita mbele yake vup kama umeme na kupotea gafla,alipogeuka kutazama alipopotelea alishangaa akipigwa kofi la shavuni la nguvu lililomfanya adondoke chini kumfanya apandishe hasira,ikawa ni kama mchezo anaona kama watu wanamchezea bila kuonekana,alipotaka kusimama akipigwa kofi la kichwani tena hadi Sara akabadilika macho kwa kupandisha hasira,alitazama kulia na kushoto kisha akasimama na kuangalia chini kwa macho yale makali akivushusha pumzi kwa nguvu,haikupita sekunde kadhaa akipita mtu tena kwa kasi mbele yake na kwa wepesiwna haraka wa Sara akamtaka yule mtu mkono uliyomfanya yule jamaa ashindwe kufanya tena ujanja wake,Sara alimtazama kwa macho makali na kujuwa ni watu wa Michael wasuriati wenzake.

    "sasa wewe na wenzako mlioko hapa mtapeleka salami zangu kwa huyo aliyewatuma."alisema Sara na kumminya mkono yule kamaa pale pale akakauka kabisa,wenzake wawili walivyymoona hivyo ikawajaa hasira wakawa wanakuja kwa kasi kutaka kumdhuru Sara lakini wapi. ...hawakuwa na uwezo wa kumjua Sara,aliwazidi na wao walikamatwa kila mmoja na kuwanyongelea mbali,akabaki amewatazama tu hawapatii jibu,akamgeukia yule aliyemgandisha na bila huruma Sara akaunyofoa mkono wa yule jamaa kisha akamganduana kumuacha ayasikie maumivu yale,alipiga mayowe kwa sauti lakini hakuna wenzake washaelewa kila kitu na kwa hata binadamu yeyote akiyasikia kelele zile,kelele zilizomfanya hata Michael na baba yake waliokuwa nyumbani kwao washtuke baada ya kusikia sauti ile na kubaki kuangaliana.

    Yule jamaa alilia sana na kumfanya Sara amsogelee.

    "nadhani watakuwa wamesikia hui ujumbe,nakutumia ukawaambie natetea ufamle na heshima ya mama yangu,na ni mimi ndiye nitakayerithi na kuwa Malkia wenu na sio nyie wenye mikono ya zambi,potea haraka. ..!!"alisema Sara akionesha bado kuwa na hasira,yule jamaa alipoteza kimaajabu akiwa hana mkono mmoja.Sara aligeuka nyuma na Kuwait wale aliyowaua,papo hapo akawasogelea na kutoa moto kitandani mwake akawachoma kabisa wateketee pale hadi walupopotea na yeye akarudi hali yake ya ubinadamu na kurudi zake nyumbani ambapo alimkuta baba yake anepumzika.



    Taarifa zile zilifika kwa Michael akiwa na baba yake,yule jamaa alionekana kuzidi kulia baada ya mkono wake mmoja kukatwa na Sara hali ilimfanya hasa Michael ashangae.

    "ndio hivyo Mfalme,amewaua wanangu wote na mimi kanileta mkono wangu akisema niwaeleze kuwa ye......yeye ndio....yeye ndiyo eti ni Malkia wetu"

    "PUMBAAVU"alisema Michael na kuchomoa kisu akakipitisha shingoni kwayule jamaa naboapo hapo akadondoka chini na kupoteza maisha,Michael alinyanyuka kwa hasira baada ya kusikia maneno yale aloambiwa kuwa Sara anataka kuwa Malkia wao jambo ambalo hawataki kabisa kusikia wasuriati,kwa hasira alizonazo akataka kutoka nje jioni ile lakini baba yake akamzuia.

    "A..aaah....unaenda wapi sasa Michael?"

    "Niache baba,yule mtoto wa malaya aliyekaa na binadamu ndio anatufanyia sisi tusifanikiwe mambo yetu, tumekaa muda gani hapa duniani mambo yetu hana haribika hayaendi kisa yeye,amekutwa nani hasa?atatushindaje sisi mtu aliyezaliwa duniani huku?wacha nimfuate nkuonyeshe nini tunamaanisha!!"alifoka kwa hasira Michael akitaka kuondoka lakini baba yake amemzuia.

    "huna haja ya kukurupuka mwanangu,mimi naamini asilimia zote lazima wewe utakuwa Mfalme tu maana tuna nguvu za watu wengi,yeye hana wa kumsaidia lazima atachoka tu mimi nawajuwa jinsi walivyo,hawawezi kuhimili kupambana me amid mrefu wewe endelea kuwatuma wasaidizi wako wazidi kumsumbua kuna muda tu utaiona anaishiwa nguvu ndiyo hapo utakapommaliza bila hata kutumia nguvu nyingi."alisema baba mtu na kumfanya mwanaye kidogo aanze kupata tumaini kipua,akazidi kumsuka mwanaye na kumpa mbinu na udhaifu wa nguvu ambayo anazo Sara,Michael taratibu akaanza kutabasamu na kucheka baada ya kujuwa kuna muda lazima Sara choke tu na ndio muda wa yeye kummaliza kabisa,alipanga tena watu kadhaa wamvizie tena Sara kesho yake wazidi kumchosha.





    Basi wakaafikiana iwe hivyo na kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha mambo ya yanaenda sawa.

    Baada ya muda kwenda na usiku kuchukuwa Nafasi yake,Ester alionekana kuwasili nyumbani kwa akina Sara akimkuta akaandaa chakula cha jioni huku mzee Junior amepumzika kwenye mkeka,alitoa heshima kwa mzee huyo kisha akaingia jikoni alipo Sara akiendelea kukaangiza,wakasaidiana kufanya kazi muda ule na baadae walimaliza kazi hizo pamoja na kupika,wakaanza chakula na wote wakisogea kuanza kula kwa pamoja huku wakipiga stori za hapa na pale hadi walipomaliza,baada ya muda kupita mzee Junior akanyanyuka zake na kuwaaga anakwenda zake kulala kawaacha Sara na Ester pale wakiendelea kuongea mambo yao.

    "kuna muda nilikaa nkakumbuka siku ile Denis alivyomkwida Michael kiasi kile sijui alikuwa na moyo gani yule mvulana hakumuhofia kabisa Michael"alisema Ester na kumfanya Sara atabasamu.

    "Pale Michael asingefanya chochote maana ni sehemu ya uwazi muda wowote watu wanatokea,yule akapanga sehemu mwalimu ya kukutia mikononi mwake anajiandaa Denis alimshutikiza pale ndio maana hakufanywa lolote japo amepandisha hasira."alisema Sara.

    "Hivi Sara...hakuna njia yeyote ya kuharibu kunaweza kumuulia mbali huyu Michael apotee kabisa maana anawakosesha amani wengine ujuwe,nahofia hata wewe huenda akakutengenezea kesi nyengine iliyo kubwa zaidi kuonekana mwenye hatia ukaisha sehemu mbaya.!"alisema Ester kwa upole,Sara alimtazama Ester kwa tabasamu na kumshika shavu lake.

    "wala usijali Ester,niko vizuri sana japo kuna mambo nimepitia kamabchangamiro ila ndiobwajibu wangu kufanya hivyo,wewe na wenzako ni kama watu wangu hivyo napaswa kuwalinda watu wangu nyie ,hata nikidhurika mimi lakini nihakikishe nyie mpo salama na niweze kutokomeza hili kabisa la wasuriati wenye kukazania desturi yao ya kuwauwa watu pasi na huruma,hata kama narudi kwenye jamii hiyo basi muwe ni watu kama binadamu wa kawaida wasiokuwa na ubaya kwa binadamu wengine,hicho ndicho ninachokijenga sasa,amani baina ya sisi tuliyozaliwa pande mbili na wale wa jamii hiyo ya viumbe wasio binadamu,nataka nitoe ile Mila na desturi yao ya kutotaka wao kupenda binadamu na kuchaguliwa mtu wa kumuoa au wa kukuoa,tutabanwa hata sisi tuliozaliwa binadamu tukichaguliwa wa kukupenda jambo ambalo sidhani kama kuna mmoja wetu ataliafiki,muhimu tu ni kuwa na moyo wa ujasiri na kujitolea kwa lolote litakalotokea,hawa ninawachukia kuliko unavyodhani...wameniulia mama yangu mpendwa ambaye hata sijafaidi kuliona tabasamu lake,naisikia tu sauti yake ukiniambia nifanye hiki na kile ili kuweka mambo sawa,yeye ndio aliyenituma kazi hii na ni lazima niitekeleze kuirudisha heshima yake,na kwa hili nimeona nikupe kitu ambacho itakubidi iwe ni lazima kwako"alisema Sara na kumfanya Ester amtazame kwa makini,alifunua mkeka waliokalia na kukitoa kitabu kidogo akakikabidhi mikononi mwa Ester huku akimtazama."yakupasa kuanzia leo ukisome hicho kitabu ndani ya wiki mbili ujuwe kuyatamka hayo maneno yaliyopo kwenye kitabu hicho,nakuomba tena sana Ester yasome kwa bidii sana hayo maneno uyaweke kichwani japo nusu tu"alisema Sara na kumfanya Ester akitazame kile kitabu,akamtazama Sara kwa makini.

    "Nakuamini sana Sara,nitafanya ulivyoniambia rafiki yangu"alisema Ester kwa ujasiri hadi Sara akafurahi,walisogeleana na kukumbatiana marafiki hao,na muda ulipofika Ester akataka kuondoka zake usiku ule,alisindikizwa na Sara hadi karibu na kwao kisha wakaagana na Sara akarudi zake kwao.

    Usiku ule Ester kabla ya kupanda kitandani alifanya maombi yake kama kawaida na baada ya hapo alipanda kitandani akiwa na kile kitabu alichopewa na Sara,taratibu alikifungua na kushangaa kuona lugha ambayo hakuweza kuitambuwa,ikambidi acheke tu maana hajawahi kuisoma lugha ile na kubaki kukiangalia tu kile kitabu.



    Kesho yake shuleni kama kawaida wanafunzi wakiendelea kupata taaluma shuleni pale, Kwa Michael hakutaka kupoteza muda alikuwa akitafuta namna ya kumuingia Sara kwa namna yeyote ile lengo ni kumdhibiti kama sio kumuua kabisa,muda mwingi sana alikuwa akimfuatilia Sara kuhakikisa anafanikiwa jambo lake lakini mhusika anaonekana kuwa makini muda wote kiasi cha kuzidi kumpa kazi Michael.Ikawa ni kama tabia ya Sara pamoja na wenzake kutoka pamoja shuleni hadi wanapofika kijini kila mtu anafuata njia yake kuelekea kwao,Michael alikuwa akishuhudia hilo na kumfanya atabasamu baada ya kuona amewatia presha.Alizidi kumuandama Sara kila muda wa kutoka shuleni baada ya kuachana na wenzake,baada ya siku kama nne kupita huku Michael akizidi kumuandama Sara kwa kuwatumia watu wake kimiujiza lengo ni kumuua moja kwa moja Sara ambaye naye kitendo kile kilimchosha sana kila Siku anauwa tu wale viumbe wanaotumwa na Michael kila wakati,siku hiyo akiwa darasani alifikiria sana Sara akaona Leo ni bora amtolee uvivu Michael maana anampanda kichwani,alitoka zake darasani na kwenda kukaa mahali akitafakari Mambo Fulani.

    Huku nako wa Michael akiwa darasani alikuwa akitafari namna ya kumdhibiti Sara kwa namna yoyote ile,alipata wazo moja ambalo alihisi huenda kikawa ni sahihi likamsaidia kumpindua Sara,alinyanyuka na kutoka darasani moja kwa moja akaelekea chooni akiwa na Jambo kichwani kutaka afanye,Sara alimuona Michael akaelekea kule msalani na kuona ndio muda pekee wa yeye kufanya alichokiamua,alitazama pande zote hakuna mtu yoyote anayemuona pale alipo,gafla tu akapotea mahali pale.

    Aliingia zake chooni Michael na kuangalia kila choo hakuna mtu kisha akatulia na kuanza kutamka maneno kadhaa ambayo gafla tu yalimbadilisha na kugeuka kuwa mtu wa ajabu,alionekana kama mtu aliye fufuka ,alitoa kioo na kukitazama huku akicheka,akachukuwa kile kioo na kujikata kidole kwa makusudi damu ikaanza kumtoka,akanyanyua kile kioo na kuanza kumimina ile damu huku akiliandika jina la Sara hadi herufi zile nne zilipokamilika.Alinyanyua tu mkono wake juu na gafla kikatokea kisu na kutua kwenye mkono ule, alicheka sana Michael huku kile kioo kikimuonesha Sara akiwa darasani hana hata habari,.

    "leo ndio mwisho wako mtoto wa malaya wewe,huwezi kunizuia Mimi nisifanikiwe kwenye mbio hizi za kuwa mfalme, mfuate mama yako Sara safari Njema" alisema Michael na kuanza kukishusha kile kisu kukipasua kile kioo na gafla tu lile jina la Sara likabadilika palepale na kuonekana kuwa jina la Baba yake na Michael ambapo bila kujua Michael alitua kile kisu kwenye kile kioo kikapasuka vipande vipande kuonesha kazi aliyoitegemea imekamilika.

    Haikupita hata dakika moja akatokea Sara kimiujiza mule mule chooni huku akimtazama Michael ambaye alikuwa kama mtu aliyefufuka,Michael alishangaa kumuona Sara pale ikabidi aangalie chini vile vipande vya vioo vilivyopasuka pasuka maana alikuwa tayari kammaliza Sara kwa namna ile.,hammad......alisikia tu sauti ya Baba yake ikimlilia."Michael....umeniuwa Mwanangu.....umeniuwa Baba yako....kwanini?..."sauti ile ilimfanya Michael gafla abadilike na kuwa kama kawaida,alishangaa kusikia vile.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Huna haja ya kushangaa,umemuua Baba yako,....atafuata mwingine na mwingine na mwingine hadi muishe wote,hamna haki ya kumiliki falme takatifu hali ya kuwa nyie ni watenda zambi,hamfai kabisa na ni lazima niwaangamize wote,huu ni mwanzo tu" alisema Sara huku akimtamzama Michael aliyekuwa haamini kikichotokea,Sara akapotea gafla na kumuacha Michael pale akiangalia chini kwenye vile vipande vya kioo kilichopasuka,hakutaka kuamini na muda huo huo akapotea kimaajabu kuelekea kwao kuhakikisha kama ni kweli amemuua Baba yake?..



    Na kweli baada ya muda mchache alitokea moja kwa moja chumbani kwa Baba yake na kumkuta ameshikilia tu shingo yake kana kwamba kuna kitu kinamoaba tena sana,macho yalimtoka Baba huyo kiasi cha kufanya Michael amsogelee huku akiwa na Huzuni.

    "Micha....el Mwan....angu...una....ni...ua.." alisema Baba mtu kwa tabu huku jasho likimtoka pale chini ya sakafu.

    "Hapana Baba...siku taka kukuua kabisa baba yangu....niliandika kabisa afe Sara na sio wewe Baba yangu." alisema Michael alitokea na machozi.

    "Sara.....ana uwezo mkubwa sio kama unavyofikiri,jitahidi sana Mwanangu wasuriati wote wanakutegemea wewe,Umebeba nguvu za wazee wote waliopita na una nguvu,pigana usichoke....na Sara huenda ndio aliyemfanya yote haya,nakuachia Mwanangu....sijaku...ona te...na.." alisema Baba Michael na kufanya mwanaye azidi kulia.

    "hapana Baba usiseme ivyo...huwezi kufa Mimi nipo,tutamshinda Yule hawezi kutupindua." alisema Michael.

    Baba mtu akabaki kulia tu akimtazama mwanaye maana hali yake sio nzuri,alitaka kusema neno lakini hakuweza kulitamka na papo hapo akapoteza maisha,Michael alibaki akiita tu baba huku akilia mchana ule.

    Huku shuleni muda wakutoka wanafunzi ulipofika waliruhusiwa na kurudi makwao,kama ilivyo kawaida yao waliongozana wote wakina Magreth na wenzake wakiongea mambo yao.Kwa kitendo alichokifanya Sara aliona sasa amewapa salamu wakina Michael na kujua kwa vyovyote vile hawatavumilia wakina Michael.Na kweli muda mchache kule kwa akina Michael walitokea baadhi ya viumbe jamii yao na kuahudia mwili wa baba Michael ukiwa pale chini,waliusujudia pale kama heshima,ndiye aliyekuwa mfalme kabla hajatolewa baada ya Malkia Aznaty kufariki kwa kusadikika ni yeye ndio aliyemuwekea sumu hadi kufa.

    Michael naye alisogea pembeni na kusujudu huku akionesha kuwa na simanzi moyoni mwake.Alipandwa na hasira sana baada ya kujuwa Sara ndiye mhusika wa kifo cha baba yake,macho yake yakibadikika gafla kama paka pale alipo na kujikuta akisimama huku akiangalia mwili wa baba yake pale chini huku akikunja ngumi kwa hasira zilizomjaa juu ya Sara."LAZIMA NIKUUE SARAAAAA"alipiga ukelele mkali Michael uliopenya hadi kwenye ngoma ya masikio ya Sara akiwa anatoka shuleni na wenzake wakiwa njiani.Alisimama gafla baada ya kusikia sauti ile ambayo aliijuwa ni Michael,wenzake wakamshangaa kuona amesimama gafla hali ya kuwa walikuwa wakipiga stori pamoja.

    "vipi Sara mbona umestop gafla kuna tatizo?" alisema Denis na kuwafanya wenzake wakina Ester wabaki kumuangalia Sara,taratibu aliachia tabasamu na kuanza kutembea kuendelea na safari,nao wenzake wakafuata tu wakisubiri aseme lolote.

    "Yule Michael mnayemjuwa nyie sasa amezidi mara mbili yake,ana hasira zaidi ya maelezo"alisema Sara na kuwafanya wenzake wote wasimame,aliwageukia na yeye na kuwashangaa.

    " vipi?nimewashtuwa?"aliuliza Sara lakini hakuweza kujibiwa,kila mmoja alibaki akimtazama mwenzake baada ya kujuwa kuwa Michael amekuwa hatari zaidi.

    "Sara....maneno gani hayo unayotuambia?unajuwa fika wewe ndiyo tunayekutegemea kumdhibiti Michael halafu unatuogopesha kwa maneno hayo,unategemea nini?eti!" alisema Magreth huku wenzake wakionekana kuwa na wasiwasi kweli,Sara aliwasogelea karibu na kuanza kumuangalia kika mmoja.

    "Eleweni kuwa na nyie ni kama yeye,msimuogope kiasi kwamba unakata tamaa ya kuishi kabisa,ni kweli Michael ana hasira kwa sasa,baba yake amefariki,Leo akitaka kuniuwa mimi baada ya kuona nipo karibu sana na nyie,alielekea chooni na kuchukuwa kioo ambacho akiandika jina langu kwa maandishi ya damu kwenye kioo kile,akachukuwa kisu ili akichome kioo kile kusudi mimi nife,hapo ndipo nilipomfanya akasirike,nina kisasi na baba yake,ndiye aliyempa sumu mama yangu afariki angali bado ana malengo mazuri na falme ile pamoja na kutaka kuiondoa desturi ya kubaguwa wao kuwa na mahusiano na binadamu,mimi ndiyo nilibadilisha jina langu pale kwenye kioo kile na nikaandika jina la baba yake,alipochoma kioo kile akijuwa kaniuwa mimi kumbe kamuuwa baba yake,kwake ni kilio na hasira ila kwangu ni furaha ni moja ya hatua nilizopaswa kuzitimiza,amekufa aliyemuuwa mama yangu,bado wengine pia watafuata,"alisema Sara akionekana kutabasamu hana hata wasiwasi huku akiwatazama wenzake waliokuwa hawaamini yale wanayoambiwa.

    "Sara...huoni ulichokifanya kitatuweka sisi kwenye matatizo?" aliukiza Natasha kwa upole.

    "Natasha....kwa sasa nyie mpo huru,na eleweni kuwa nimefanya hili kusudi asiwafuatilie nyie kwanza,sasa ana vita na mimi akitaka kuniua kwa kuwa nimemuulia baba yake" alisema Sara na kumgeukia Ester."nakusihi sana Ester usome kile kitabu,kama umeweka ratiba yako ya masomo basi lile pia ni somo na ukumbuke utalifanyia mtihani"alisema Sara na kugeuka zake kuendelea na safari,akawaacha wenzake pale wakiwa wanatazamana tu hawaelewi hatma ya maisha yao.



    Kwa Michael....akiwa na wenzake wa jamii ile mule chumbani kwa baba yake,walishapanga mambo ya kufanya na kuamua kuondoka na mwili ule urudi kule walipotoka,hakutaka kabisa arudi huko kama hajamuulia mbali Sara ambaye ndiye aliyekuwa kikwazo hadi leo hii hawakufanikiwa,tena ndiyo akuyesababisha na Leo anampoteza baba yake kipenzi,hakika alikuwa na uchungu sana lakini wenzake walimtuliza na kumbembeleza warudi kwanza wakaupumzishe mwili wa marehemu.Siku hiyo hiyo waliondoka kimaajabu hadi kufika kwenye dunia yao ambapo taarifa ziliwafikia wasuriati wengine waliobaki,taratibu za mazishi zilifanyika huku wazee wa wasuriati wakizidi kumfariji Michael ambaye ndio alikuwa mbele kwenye maziko hayo,mwili wa maregemu ukiwekwa kwenye kuni zilizopangwa kama jukwaa,ukaletwa moto akakabidhiwa Michael ili amalizie mazishi yake,Michael aliukataa ule moto gafla tu na kuwafanya wazee pamoja na wasuriati wengine washangae,alisogea karibu kabisa na alipolazwa baba yake na kunyoosha mkono wake ambao ulianza kutoa moto kuelekea kwenye zile kuni zikaanza kuungua.

    "kapumzike baba yangu,ila kwa hili lazima nilipize lazima nimuue Sara kwa mikono yangu lazima niwe mfalme ushindi urudi kwetu,hiki ni kiapo nakiweka mbele yako baba"alisema Michael kwa uchungu huku watu wote wakisikia,aligeuka nyuma na kuwaona watu wote wanamtazama.

    "Apewe heshima mfalme mpya wetu!!" alisema mzee mmoja na kushuka chini kusujudu,wote nao wakamfuata kwa kusujudu mara tatu kumpa heshima Michael ambaye ndio anabeba mikoba yote ya baba yake ambaye ndiye alikuwa mfalme wao siku zote,hali ile ilimfanya Michael ajiamini na kuona sasa amekuwa mtu wa kuheshimika,akigeuka kutazama jinsi kuni zinavyozidi kuuteketeza mwili wa baba yake kama mazishi ya jamii yao kisha akageuka kuwatazama wasuriati ambao walinyanyuka na kukaa kumsikiliza.

    "aliyesababisha kifo cha baba yangu ni SARA....ndiye yule mtoto wa malkia Aznaty" alisema Michael na kuwafanya wengine wasiojuwa wafahamu kuwa Sara ndiye aliyemuuwa mfalme wao.

    "Kama baba yangu ndiye aliyefanyiwa hivi basi siwezi kuvumilia lazima nimmalize kwa mikono yangu na nishaweka kiapo hicho mbele ya baba yangu hapa,nitamuuwa SARA" alisema Michael akidhamiria.

    "AFE...AFE...AFE...AFE..." zilisikika sauti za wasuriati wote wakimuunga mkono Michael kuonesha nao wameguswa kwa msiba huo,Michael alijisikia amepata ushindi baada ya kuona ameungwa mkono,basi baada ya maziko hayo wazee walimuita Michael sehemu wakawa wanamueleza mambo na namna ya kufanya kama mfalme wao,waliitwa wale wazee wazito kabisa waliobobea kwa uchawi,wakamchukuwa Michael na kuingia kwenye chumba cha maombi wakawa wanamwingiza nguvu za kuchawi zaidi mwilini mwa Michael ili aweze kufanikiwa kwenye mambo anayoyapanga hadi kuwa Mfalme mkuu wa jamii yao na sio tena mfalme wa wasuriati tu.

    Na kweli baada ya mambo kwenda sawa alitolewa kwenye chumba kile akiwa amekamilika kwa nguvu za ajabu,wazee walimuweka sehemu wakawa wanamueleza mambo mengi ya kifalme ambayo anapaswa kufanya.

    "Kikubwa ni kuelewa kuwa zimebaki siku nne tu ili falme nzima iweze kupata kiongozi wa kuongoza muda wote maana hadi sasa hakuna kiongozi yeyote pale falme ipo wazi na anayeweka kizuwizi ni mmoja tu,Sara.Hawezi kupata nafasi ya kuja kutuongoza sisi angali yeye hakuzaliwa huku,tena kazaliwa na uzao wa binadamu jambo ambalo kamwe haliwezi kuwepo kwenye koo hii,unapaswa Michael umuangamize huyu binti mapema kabla ya siku hizo hazijafika" alisema mmoja wa wazee wale na kumfanya Michael aelewe,alikubaliana na mambo yale aliyoambiwa kisha akasimama hadi na kusogea mlangoni, alijiangalia mwenyewe na kujiona ana mabadiliko kweli kwenye mwili wake,akabaki akitabasamu tu huku kichwani akimuwaza Sara tu lengo ni kumuangamiza,basi alipanga kundi la wenzake waweze kurudi tena duniani na muda ulipofika walianza safari hiyo wakiongozwa na Michael mwenyewe.





    Huku duniani....Ester alikuwa akisoma masomo yake ya darasani usiku ile wa saa sita ikiwa ni pamoja na kumalizia mazoezi waliyoachiwa na mwalimu siku hiyo,akipohakikisha yamekamilika aliviweka vitabu na madaftari yake kwenye begi lake la shule na yeye akapanda zake kitandani,taratibu akaanza kuutafuta usingizi ambao dakika chache tu ukamchukuwa,akiwa kwenye usingizi mnono Ester alipata kuota ndoto moja akimuona Michael amekalia kiti cha kifalme huku akicheka kwa dharau miguu yake ikiwa juu ya Sara aliyeonekana kulala pale chini ya sakafu akiwa hoi hajitambui,taratibu akaja mwanamke mmoja akiwa amebeba sahani ya dhahabu ikiyokuwa na kisu kikubwa juu,Michael alikichukuwa kile kisu huku sura yake ikiwa imebadilika kuwa na hasira,alikishika kile kisu kwa mikono miwili na kukinyanyuwa juu akiomba mambo yake kusudi kitakaposhuka kituwe mija kwa moja usawa wa moyo wa Sara kifuani,Ester alianza kutazama eneo lile na kuona wasuriati jinsi walivyo na furaha baada ya kumuona mtu wao waliyokuwa wakimtaka awe mfalme yupo juu ya kiti cha kifalme na uzuri ni kwamba aliyekuwa akikwamisha mambo yao amedhibitiwa,aliangalia pembeni na kuwaona Magreth,Natasha,Denis na baadhi ya watu wengine waliohisiwa ni damu ya kibinadamu wote walifufuliwa na kuwa kama bina damu muda ule ili washuhudie anachofanywa Sara siku hiyo.Michael alizidi kuomba tu na baada ya muda akaanza kushusha kile kisu taratibu kuelekea alipolala Sara pale chini,

    "Anza....anza Ester..utafeli mtihani wako wewe Ester anza haraka!!" kwa mbaali aliisikia sauti ile Ester akiwa anaangalia kisu kile kikielekea kushuka kifuani mwa Sara na kukita kifuani pale hadi Sara akapiga ukelele wa maumivu makali,...gafla tu akakurupuka kutoka usingizi Ester baada ya kuiota ndoto ile,akawasha taa,alitazama huku na kile kuangalia alipo,alichoka baada ya kuona alikuwa usingizini anaota,ah alishusha pumzi baada kuona ndoto ile imempa hofu kubwa,akaanza kutuliza akili yake kufikiria mambo yanavyoenda,alifumba macho na kuanza kupiga maombi kwa dakika kadhaa kuitoa hofu ile iliyokuja gafla moyoni,akakumbuka kile kitabu alichopewa na Sara akisome,akinyanyuka kitandani na kusogea hadi mezani na kuanza kukishika kile kitabu na kukifunua,akakaa kabisa na kukiangalia kwa umakini,mwanzoni alikisoma sana lakini hakuweza kuelewa hata moja wala kushika hata neno,lakini kwa ile ndoto aliyoota alihisi kuna jambo litatokea hapo mbelena kukumbuka maneno ya Sara anapaswa kukusoma ajuwe kuyatamka maneno yaliyo mule ndani ya kitabu kabla ya wiki mbili,alianza kutoa chozi baada ya kuona kwenye ile ndoto Sara akichomwa bisu la kifuani karibu na moyo kabisa kuonesha Sara atakufa ,akajifuta machozi kwa kujiamini kisha akaanza kuyasoma maneno yale taratibu tena na tena yaanze kukaa kichwani akihisi huenda yakawa na maana kubwa hapo baadae,alianza kuyasoma maneno yake kwa hisia japo hayajuwi maana yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asubuhi kulipo pambazuku wanafunzi wakisogea mashuleni kwako kupata elimu itakayowafaa maishani,bibi yake Ester alitoka zake chumbani na kuelekea sebuleni kuanza kufanya zake usafi,alimpenda sana mjukuu wake huku akimsaidia hata kazi nyengine,alipomaliza kufanya usafi wa nje akaelekea chumbani kwa mjukuu wake kuweka vitu sana,akipoingia tu alishangaa kumuona Ester akiwa ameweka kichwa mezani huku amelalia kitabu,alionekana kupitiwa na usingizi tokea jana usiku,.

    "Haa wewe Ester!!" alisema bibi akiwa anashangaa kumuona Ester pale."wewe ....wewe Ester....huendi shule?"alisema Bibi na kufanya Ester ashtuke pale alipo,akaangalia dirishani na kuona jua lilivyochomoza.

    "Mama weeeee....kumbe kumekucha hivi!"alisema Ester na kukurupuka pale alipo na kuanza kuchukuwa nguo zake za shule akaanza kuzivaa haraka haraka huku bibi akimtazama tu na kubaki kucheka.

    " wahi viboko vinakusubiri huko"alisema bibi kama utani na kuzidi kumpa presha Ester.



    Huku shuleni wanafunzi walielekea madarasani baada ya kufanya usafi wa mazingira ya shule.Magreth akishangaa kutomuona Ester darasani siku hiyo na sio kawaida yake,hata Denis naye alishangaa kwa hiyo hali na kuanza kutilia shaka huenda ikawa ndio Michael ameanza kazi rasmi,walimuangalia Sara akionekana kuwa bize akiandika masomo yake.Mage hakuwa na amani kabisa akanyanyuka na kumfuata Sara hadi pale alipo.

    "Sara...ujuwe nanihii....Ester hajafika ujuwe hadi muda huu,huenda kuna jambo limemkuta huko!" alisema Mage kwa sauti ya chini wakificha siri zao mwengine asijuwe.

    "Mh sidhani kama kuna kitu kibaya kimemkuta,ila si ndio kwanza asubuhi watu wanaingia darasani huenda kachelewa tu kuamka labda,ngoja tumsubiri usijali Magreth" alisema Sara akiendelea kuandika mambo yake hana hata habari,punde tu akaingia mwalimu mkuu akiwa amekamata bakora na kuwafanya wanafunzi wasimame kumpa heshima,Magreth akarudi sehemu yake na mwalimu akawaruhusu wakae.

    "Haya kama unajijuwa ulikosa namba asubuhi tafadhari pita mbele kwa usalama wako"alisema mwalimu mkuu Malamba akionekana kuchukizwa,kwa kuogopwa kwake wanafunzi waliochelewa walianza kunyanyuka kwenye viti vyao na kusogea pale mbele.

    "Ona sasa....ona .....watu wote nyie mmechelewa shule mnategemea Malamba ndio awafanyie usafi si ndio!" alisema mwalimu Malamba akiangalia idadi kubwa ya wanafunzi waliochelewa.

    "Haya anapita mmoja mmoja hapa na kila mtu anajuwa kinachoendelea," alisema Malamba na kuwafanya wanafunzi wachelewaji waanze kuvua kiatu kimoja mguuni jambo likilomfanya hata Sara ashangae,mmoja wa wanafunzi akisogea alipo mwalimu na kusimama kwa mguu mmoja huku mguu mwengine akiuelekezea kwa mwalimu ambaye alinyanyua fimbo yake na kuushuka kwa nguvu kwenye unyayo wa yule mwanafunzi na kuwafanya wale waoga washike midomo yao kwa kuhamaki.Sara alishangaa kuona staili ya uchapaji wa mwalimu yule na kubaki akitabasamu tu maana ilikuwa ni ajabu kwake.Wanafunzi waliendelea kuadhibiwa na mwalimu huyo na muda mchache tu akatokea Ester na kuaingia darasani,alihamaki kumuona mwalimu mkuu akiwa anawaadhibu wanafunzi.

    "Yaani wewe monitres wa darasa ndio unafika sasahivi!" alisema mwalimu mkuu akiwa anammalizia kumuadhibu mwanafunzi mmoja wa kike.

    "Mwalimu nilipata dhalula kidogo ndi....."

    "sitaki kusikia maneno yako,huishiwagi maneno wewe ujitetee tu Leo sitaki,lete unyayo huo" alisema Mwalimu kwa hasira na kufanya Ester anune,taratibu akavua kiatu chake na kumsogelea mwalimu,alimtazama Sara na kumkonyeza ili afanye kama siku ile alivyomsaidia,Sara akakubali na kumfanya Ester ajiamini na kuuweka mguu wake tayari kwa kupigwa,aliisikia fimbo ya nguvu ikituwa kwenye unyayo wake,maumivu aliyoyasikia yalimfanya amtazame Sara ambaye alionekana kucheka,chozi likimtoka Ester kuona Sara amemdanganya na bado fimbo tatu,akaona leo kapatikana,Sara alibaki kushika mdomi kwa kicheko maana Ester nibmuoga sana wa fimbo na alimfanyia tu kusudi asimsaidie ili aone utamu wa fimbo za unyayo,lakini aliingiza nguvu zake kwa viboko vile vilivyobaki ambavyo Ester hakuweza kusikia maumivu na kujuwa Sara ndiye aliyefanya hivyo.Baada ya kuadhibiwa akarudi zake kukaa kwenye kiti chake na kumsikliza mwalimu mkuu akiwahasa kuhusu uchelewaji maana inapelekea utendaji wa kazi pamoja na kusafisha baadhi ya mazingira ya shule kuwa machafu kutokana na uchache wa wanafunzi,aliongea mengi sana na wanafunzi wakamuelewa na baada ya muda akaondoka zake kwenda darasa lengine.

    Michael alionekana kutoka darasani kwake akielekea kidato cha tatu huku akionrsha kuwa na hasira usoni mwake,hatavalipofika na kuingia darasani humu akawafanya wanafunzi wa darsa hilo wamshangae,aliwatazama wote nabjuwaona wakimuangalia,walipojuwa ni Michael waliendelea na mambo yao wakimzoea huwa anaenda kwa Magreth,Michael alimtazama Sara aliyeonekana akiwa bize na kuandika mambo yake,taratibu akaanza kumsogelea na kuwafanya Denis,Magreth na Ester wamtazame kwa makini Michael waone atafanya nini kwa Sara,Michael akabaki akimtazama Sara kwa jicho la hasira sana huku Sara mwenyewe hana hata habari akiendelea kuandika masomo yake hapo alimuona Michael yupo pembeni yake.

    "Kwa kile ulichokifanya kwa baba yangu kamwe siwezi kukaa kimya mtoto wa makaya wewe,lazima nikuue kwa mikoni yangu miwili,nitaanza na wewe nifuate na wale unaojiganya unawalinda" alisema Michael kwa hisia zao bila ya wengine kusikia na maneno yale yalimfanya Ester ahamaki kwa sauti hadi wenzake wa karibu wakashtuka,hata yeye mwenyewe alishangaa kusikia vile na kuona ameangaliwa sana na wenzake akazuga kukohoa na kuwafanya wenzake wajue amepatwa na kikohozi wakaendelea na mambo yao,Ester hakuamini.

    "Sikia Michael nikwambie,sioni ajabu kwa kufa kwa baba yako,uchungu ulionao wewe na mimi pia nilikuwa nao vivo hivyo,na hivyo ndivyo nlikuwa nataka maana nimefanikiwa kufanikisha moja ya malengo yangu niliyoyapanga,lazima niteketeze azma yangu ya kuteketeza wasuriati wote" alisema Sara na kumfanya Michael atabasamu.

    "Kamwe haitakuja kutokea,mimi ndiye mfalme wa wasuriati na ninatarajiwa kuwa pia mfalme wa jamii yetu nzima,nitawarudisha hao unaowalinda wewe sasa ili niwaue mbele ya jamii yetu iwe fundisho na onyo kwa yeyote atakaye taka kujenga ukaribu au mahusiano na binadamu,hamna nafasi nyie malaya kwenye jamii yetu,na kifo chako kitakuwa cha kustaajabisha kwa kila mtu,jiandae." alisema Michael kwa hasira na maneno yake yakapenya moja kwa moja masikioni mwa Ester aliyekuwa mbali na pale alipo simama Michael na Sara,kumbe maongezi yote Ester aliyasikia maongezi yote waliyokuwa wakizungumza Michael pamoja na Sara,alishangaa kuona na yeye amesikia yale maongezi hali ya kuwa anaelewa hana uwezo ule ambao anao Sara na Michael tu,alibaki haamini kabisa huku akimshuhudia Michael akiondoka zake akimuacha Sara akiwa anaendekea kuandika masomo yake hana hofu kabisa.Denis alikuwa anaangalia tu namna Michael alivyoonesha kukasirika,alianza kumuogopa baada ya kuambiwa hasira za Michael hasa baada ya kifo cha baba yake.

    Ester naye hakutaka kuamini kile akichosikia,haraka akanyanyuka na kumfuata Sara pale alipokaa.

    "Sara...Unajua siamini!!!"alisema Ester akiwa ana kiwewe.

    " huamini nini Ester?"

    "yaani huwezi amini... nimesikia yale yote mliyokuwa mkiongea na Mi...." alijikuta akizibwa mdomo asiendelee kuongea maneno yale.,alinyanyuka Sara na kumshika mkono Ester wakatoka nje hadi nyuma ya darasa wakabaki kuangakiana.

    "una uhakika Ester????" aliuliza Sara akionesha kushangazwa na taarufa zile.

    "siwezi kuongopa Sara nasema kweli,nimemsikia Michael akikueleza kuhusu kukuua wewe na sisi atatuua mbele ya watu wa kisuriati iwe ni fundisho kwa yeyote atayekuwa na mahusiano na binadamu,na mengine mengi tu nimesikia Sara" alisema Ester na kumfanya Sara atabasamu,alijikuta akimkumbatia Ester kwa furaha kiasi cha kumfanya nayeye Ester atabasamu,Sara akataka aamini kama ni kweli Ester naye ana uwezo wa kusikia sauti ambazo binadamu wa kawaida hawezi kuzisikia.

    "Ester...sema lolote lile moyoni mwako kwa hisia bila kufungua kinywa chako.....umeanza kuwa MTU muhimu sana kwangu...na nahakika utazidi kubadilika kila siku zinavyozidi best yangu.." alisema Sara kwa hisia bila kutamka maneno kinywani mwake,sauti ile aliisikia kweli Ester na kumfanya na yeye aamini sasa kweli naye ana uwezo wa kusikia kwa hisia,akafanya kama alivyoambiwa.

    "Unajua siamini Sara.....mbona kama naota" alisema Ester kwa hisia wakiwa wamekumbatiana.

    "huoti Ester...ni kweli kabisa...umepata bahati ya kuwa hivyo...hiyo ni bahati ,ndio maana nakusihi sana uyashike maneno ya kwenye kitabu kile nilichokupa huenda ukafanya jambo moja kubwa sana hapo baadae,"alisema Sara na kumfanya Ester ajisikie faraja,akazidi kumkumbatia Sara.

    "Nakupenda sana Sara,na nashukuru kwa kuwa pamoja nasi kwa kipindi hiki,bila wewe sijui tungekuwa wapi sasahivi" alisema Ester.

    "Usijali best,tutakuwa pamoja siku zote" alisema Sara na kuachiana wakabaki kuangakiana baada ya kuongea kwa hisia wawili hao,wakabaki kucheka tu maana ni kama utani tu Ester anapata uwezo wa ajabu kama huo.





    Siku hiyo ilikuwa ni ya furaha sana kwa Ester baada ya kufahamu ana nguvu flani inayomuwezesha kufahamu sauti za siri zinazoongelewa na viumbe jamii ya akina Michael.Hata wakati wa kuondoka kama desturi wanaongoza kwa pamoja njiani wakitoka shuleni huku wqkiongea mambo yao,baada ya Denis kumuuliza Sara kuhusu muda ule akupoingia Michael darasani na kusimama karibu yake Sara alimpa moyo tu na kumueleza vile Michael alivyokuwa akiongea,

    "wala msijali yule hana uwezo wa kufanya anachokisema,tutaishi kwa raha na amani na itafika tu muda Michael atatokomea kabisa na mambo yote yatakuwa sawa" alisema Sara na kumfanya Ester adakie.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "haya mambo jamani ni mitihani tu na naamini tutashinda kwa uwezo wa bwana,tuendelee kuomba tu wala tusiwe na hofu na mashaka juu ya maisha yetu,kama alivyosema Sara tutaishi kwa amani nabhaya mambo yataondoka tu wala msijali" alisema Esterna kuzidi kuongea maneno ambayo yaliwatia moyo wenzake wakawa na matumaini mapya,Sara alifurahi baada ya kuona ushitikiano anaoutoa Ester kwa wenzake,wakawa wanaendelea na safari yako huku kila MTU akiongea LA kwake hadi walipofika kijijini kila MTU akakamata njia yake ya kuelekea makwao.

    Njia aliyokuwa akielekea Sara alikuwa Michael amewaandaa wenzake wamejificha kwaajili ya kumfanyia vitimbi lengo ni kumuua,na kweli Sara alipokaribia eneo lile hisia zilimcheza na kufahamu kuwa eneo lile sio salama,alipunguza mwendo na kuanza kutembea taratibu huku akiangalia kwenye kiatu chake cha shule,gafla akatokea mtu akiwa amekamata kisu akakirusha kwa kazi kukuelekeza kwa Sara ambaye alipokiona haraka akakikwepa na kukiangalia kikitua kwenye mti pembeni,Sara aligeuka kumtazama yule mtu lakini zamani yule mtubakishaooyea wala haijulikani alitokomea,hakukaa vizuri akahisi nyuma yake kuna kitu kinakuja kwa spidi lakini aliinama haraka vikapita visu viwili kwa pamoja ambavyo havikuonekana kutuwa sehemu yeyote vikapotea kiajabu.Hali ile ilimfanya hata Sara ashanagae kuna mambo ambayo hata yeye mwenyewe alishangaa,hakukaa sana akasikia kisu kikimchana begani hadi akapiga ukelele wa maumivu aliyoyasikia baada ya kukatwa,alipata hasira iliyomfanya abadilike gafla na kupotea kimaajabu,hazikupita hata sekunde kumi akatokea tena akiwa amemkamata mtu shingoni akimnyonga huku macho yake yakiwa makali kama chui,alzidi kumnyonga yule mtu ambaye ni mmoja wa waliokuwa wakimzingira muda ule wakitaka kumuua,almuachia yule jamaa ambaye zamani tu alikuwa kashapoteza maisha baada ya kukabwa koo kwa muda mrefu,Sara alibaki amesimama huku akiangalia huku na kule akiwa amekasirika sana damu zikimtoka mkononi.aliona sasa wanazidi kumpanda kichwani,alibadilika kabisa na kuwa na sura ya ajabu akaanza kupambana nao japo walikuwa ni wengi sana,kila akiua watano wanaongezeka tena kumi hali iliyomfanya hata yeye ashangae,yote hayo alikuwa akiyafanya Michael ambaye muda wote alikuwa pembeni tu akiwaangalia watu wake wakipingana nguvu na Sara ambaye baada ya muda akaanza kuonekana kuchoka maana anatumia nguvu nyingi sana kupambana na ule umati wa watu,ilichukuwa muda sana na kwa uwezo wake alifanikiwa kuwamaliza baadhi ya viumbe wale japo mwili wote ulikuwa hoi huku akionekana kukatwa na visu kwenye baadhi ya mwili wake huku mgongoni akiwa amelibeba begi lake la shule,hali ile ilimfanya Michael atabasamu baada ya kumuona Sara huko hoi taabani,alinyanyua upanga mkubwa na taratibu akaanza kumsogelea Sara huku akikumbuka kifo cha baba yake,hasira zilimpanda sana Michael huku akizidi kumsogelea tu,alipomkaribia akaanza kuunyanyua upanga wake ammalize Sara ambaye alikuwa amesimama tu akitafakari na kuona njia sahihi kwake ni bora kuondoka tu akubali kushindwa kwa siku ile,akatazama chini na kunena maneno Fulani na gafla akapotea pale aliposimama na muda huohuo upanga wa Michael ukapita kichwani kwa Sara lakini haikusaidia,alikuwa ameshapotea muda ule Sara na kumuacha Michael aanze kupiga makelele ya hasira kwa kumkosa Sara ambaye alionekana kushindwa kabisa na ilikuwa ni yeye tu Michael kummaliza ili mambo yaishe,alilalama sana na kuwafanya watu wake waangalie tu chini kwa kumheshimu,hawakukata tamaa wakapanga tena wamvizie siku nyengine waendelee kuhakikisha wanampoteza Sara.



    Sara alikuja kutokea chumbani kwake akiwa yupo hoi kwa kazi ile ya kupambana na wale viumbe ambao walidhamiria kumuua,alishusha begi lake lililo kuwa mgongoni muda wote na kulibwaga chini huku akionekana kutiririka damu kwenye baadhi ya sehemu za mwili wake,alikitazama kioo kikubwa kikichokuwa kwenye ukuta na taratibu akaanza kukisogelea,alijiangalia jinsi alivyofanywa hadi kuwa vile,alinyanyua mkono wake uliokuwa ukidondosha matone ya damu sehemu ile aliyokatwa na kisu na wale viumbe,aliishika damu yake huku akionekana kuishangaa sana,ndio kwa Mara ya kwanza anaiona damu yake ikimwagika tena kwa kuumizwa na viumbe ambao ndio jamii ya wasuriati,aliyakumbuka sana maneno ya baba yake vile aliambiwa kuwa mama yake alifariki kwa kuwekewa sumu kwenye kinywaji na chakula lengo ni kumuua ili wasuriati wamiliki falme ile iliyokuwa chini ya utawqla wa marehemu Malkia Aznaty,Leo tena wasuriati hao hao wakiongozwa na Michael wanamuumiza,wakiwa na lengo la kumuua kabisa Sara ili waimiliki vizuri ile falme,Sara aliona ni ujinga juu kufumbia macho swala hili.

    "Japo sina wa kunisaidia lakini nitapambana nao mpaka tone la mwisho kuhakikisha nawamaliza wasuriati wote ambao wanaenda kinyume na kushikiria desturi mbaya,siwezi nikakubali niwaache wqkae sehemu ambayo hawana hadhi ya wao kukaa,nutailinda na kuiheshimu heshima ya mama yangu kama Malkia wao,Mimi ndiye mhusika na ndiyo ninayepaswa kuwa Malkia kama alivyo mama yangu.,Michael....nimekuachia sana tena sana....sasa inatosha..." alisema Sara na kushika sehemu aliyokatwa,akaiziba kwa mkono na kuifuta sehemu ile papo hapo ile sehemu ikajifunga na kurudi kama alivyo awali,alivua nguo zake za shule na kuchukuwa kanga yake akitaka kuelekea zake bafuni kuoga lakini gafla tu akajikuta akidondoka chini kwa kukosa nguvu,jambo ambalo hata yeye mwenyewe alilishangaa,alijitahidi kunyanyuka na kuanza kupiga hatua kuendelea na safar yake ya bafuni.



    Ester aliendelea kukisoma kile kitabu alichopewa na Sara huku taratibu akaanza kuyashika baadhi ya maneno yaliyomo kwenye kitabu kile,alipata shauku ya kuyajuwa baada ya kuona matumaini Mara tu alipojuwa kuwa naye ana uwezo wa kusikia kwa hisia kama ilivyo kwa Sara na Michael,alikumbuka muda ule alivyoingia Michael darasani kwao akasimama karibu na Sara akiwa anamuangakia kwa husda huku wakiongea kwa hisia na hakuna mwanafunzi yeyote aliyesikia wala kujuwa kinachoendelea,ndio hiyo siku Ester alipata kusikia maongezi Yale yaliyomfanya abaki kushangaa maana haamini kama ni yeye,hata baada ya kuondoka kwa Michael alimfuata Sara na kumweleza hali ile na ndipo akaelezwa ni kweli,na yeye kwasasa anauwezo wa kuongea kwa hisia,hiyo ndiyo ilikuwa furaha ya Ester kwa siku hiyo ambayo kila akikumbuka anazidi kusoma kile kitabu na kuona kumbe kuna umuhimu na lipo tumaini hapo mbele juu ya kuishinda mitihani inayowakabili,alijuwa kuwa Sara ni mtu wa muhimu sana kwao ambaye muda wote amekuwa ni msaada mkubwa katika mambo fulani,alizidi kusoma kile kitabu usiku kucha hadi usingizi ukamchukuwa.



    Asubuhi kulipokucha wanafunzi walionekana wakiingia madarasani kuanza masomo yao,Sara alipoingia tu darasani akimtazama Ester pale anapokaa lakini hakumuona,akabaki kushika kichwa baada ya kujua jambo,akaelekea zake kwenye sehemu yake kuanza kupanga meza yake na kiti kwaajili ya kukaa,kutoonekana kwa Ester asubuhi ile kuliwafanya baadhi ya wanafunzi wa lile darasa kuanza kuongea ya kwao maana sio kawaidai yake Ester kuchelewa ,wakiwa kwenye mada hiyo aliingia Madam Magdalena tayari kwa kuanza kufundisha somo lake la Kiswahili,wanafunzi walimsikiliza na kuanza kupewa elimu hiyo huku wakiandika baadhi ya mambo muhimu ya somo hilo wanalofundishwa.

    Wakiwa katikati ya kipindi Ester alionekana kuchungulia chungulia kwa nje,wanafunzi wqliomuona wakaanza taratibu lakini Madam akasikia,aligeuka na kuwatazama.

    "kinacho wachekesha nini?au nguo yangu imetoboka nyuma?" alisema Madam na kuwafanya wanafunzi wanyamaze kimya,Ester kuona vile akaamua kuingia tu mwenyewe hadi ndani na kumfanya Madam abaki kumshangaa.

    "haaa wewe mtoto ndio unaingia saahizi kweli!yaani wenzako tunamaliza wewe ndio unaingia,SAA ngapi saizi?"aliuliza Madam akimtazama Ester ambaye alibaki kuangalia chini,kama kawaida yake hakosi cha kujitetea,alinyanyua uso wake na kumtazama Madam kwa huruma.

    "Madam kiukweli tu nikubali nimechelewa ndio na sasa ni saa mbili na nusu ika si kufanya kusudi,Mimi naishi na bibi yangu tu na na anaumwa ni mzee hivyo ikanibidi nifanye usafi pamoja na kazi zote za pale ndani peke yangu hadi nimalize,nimpikie Bibi chai ndio nijiandae kuja shule ila sio kwa makusudi Madam,naomba tu unisamehe," alisema Ester na kutii kabisa akapiga magoti,ni muoga wa fimbo na adhabu na kila MTU anamjuwa.Kwa maneno yake matamu yakamganya Madam amtazame tu na kuamua kumsamehe akaenda zake kukaa sehemu yake na kuungana na wenzake kumsikiliza Madam ambaye muda mchache tu akamaliza kipindi chake na kuondoka zake ofisini baada ya kuwaachia kazi ya kufanya darasa.

    Baadhi ya wanafunzi walianza kuiga kile alichofanya Ester pindi alipoingia kwa kuyarudia maneno yale yaliyokuwa akiyasema kumwambia Madam na kufanya darasa zima liangue kicheko,hata Ester mwenyewe alibaki kutabasamu tu baada ya kuona utani ule,Sara aligeuka kumtazama Ester na kufahamu sio kosa lake kuchelewa shule,analala muda mbovu sana akikesha kukisoma kile kitabu alichompa,alimsikitikia lakini hakuwa na jinsi,lazima afanye hivyo akiwa na maana yake mwenyewe.Basi muda ulisogea na baada ya vipindi vya asubuhi wanafunzi wakaenda kupata kifungua kinywa kwa wale kwenye hela,wengine walitulia tu kwenye bustani za shuleni wakiongea mambo yao muda ule.

    Magreth alikuwa na Sara pamoja na Ester wakiongea mambo yao,Sara alikuwa msiri kwa kile kitu kilichotokea jana, alijuwa fika akiwaambia atawatisha waanze kuingia na woga kwenye nafsi zao.

    Muda huo Michael naye alikuwa sehemu anawatazama tu wakiwa Ester pale walipokaa hawana habari,mtu wake wa muhimu kwa sasa ni Sara na amempania kumuua kwa namna yeyote ile.Akikumbuka jinsi alimkosa jana kumuua alizidi kupandwa na hasira akitamani muda ufike waanze kazi.Basi baada ya muda wanafunzi wakarudi madarasani kwao na kuendelea na vipindi vyao,Denis alionekana kutoka darasani akielekea zake chooni kujisaidia,alimaliza haja yake akatokea zake na kuanza kuelekea zake darasani lakini gafla tu akakutana na Michael mbele akiwa naye anaelekea kule chooni,wakabaki wakitazamana jika mtu uso wake ukionesha kuwa na hasira na mwenzake,waliangaliana kama dakika mbili hivi huku Denis akikumbuka alivyofanyiwa na Michael kule porini alivyoutumia mwili wa Natasha na kumdhuru kabisa Denis mpaka kufa lakini kwa miujiza tu na msaada wa Sara aliweza kumuinua hadi Leo anaishi,huku naye Michael alimtazama Denis na kuikumbuka ile siku aliyomtowa darasani kwa aibu akiwa amemkunja shati hadi nyuma ya darasa akimkoromea,aliona ni dharau kubwa sana aliyofanyiwa siku ile akaona leo amfundiahe adabu kidogo kabla ya mambo mengine,wote kwa pamoja wakaanza kupiga hata walisogeleana kila MTU akionekana kuwa na hasira na mwenzake,Denis aliiandaa ngumi nzito pindi Michael atakapomkaribia tu amtwange ya uso.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Michael naye alikuwa akimtazama Denis kwa hasira,alikunjua vidole vyake na kufungua nguvu za ajabu na kuanza kuonekana kama moshi flani kwenye vidole vyake ili ampige Denis aweze jupooza mwili taratibu maana kile alichomfanyia siku ilikuwa ni fezeha,walipokaribiana karibu kila mmoja akanyanyuma mkono wake kumpa ga mwenzake Mara ikasikika kengele ikigongwa mfululizo kuashiria wanafunzi wote wanahitajika paredi mara moja,Denis na Michael wakabak wakiangaliana tu kila mmoja akimtamani mwenzake,Michael akashusha mkono wake akimtazama Denis kwa dharau kisha akaondoka zake kwenda chooni na kumuacha Denis pale akiwa amesimama,alibaki akishusha pumzi ya hasira baada ya kengele ile kuwafanya wasitishe kile walichotaka kukifanya,aliona wanafunzi wakianza kutoka madarasani wakielekea paredi asubuhi ile baada ya kusikia kengele ile ya dharura,naye akaanza kupiga hatua kuelekea huko na wenzake.



    Baada ya wanafunzi wote kukusanyika eneo lile mwalimu mkuu Malamba akisimama mbele ya paredi akiwatazama wanafunzi wake.

    "Naam habarini za asubuhi kwa Mara nyengine" alisema Mwalimu mkuu na wanafunzi wakaitikia na kumpa heshima yake ambayo aliipokea.

    "nadhani hakuna anayefahamu ni kipi kilichowaleta hapa wakati huu baada ya kusikia kengele ya dharura,ila nina jambo moja na ni la heri tu katika kuiendeleza taaluma yetu,kuna Tour(safari ya kutalii) tumeiandaa walimu wote baada ya kukaa pamoja na kuona ni vema tuwataarifu mapema walengwa ambao ndio nyie wanafunzi kwamba tutataka mkae madarasani,kila darasa najuwa lina monitor na monitres,hivyo kila mwalimu wa darasa atakuja akishirikiana na ciongozi wenu wapate maoni yenu ni sehemu ipi mngependa twende kutalii na utaje sababu zinazokifanya uichague hiyo sehemu halafu maoni yenu yote yatakusanywa ili tuanze kuyachambua tujuwe mmependelea sehemu gani ili tuanze kupanga mikakati ya safari hiyo,nadhani tumeelewana"alisema mwalimu mkuu na jambo lile liliwafanya wanafunzi waanze kufurahi sana kwa kupiga mayowe na makofi,wakaruhusiwa warudi madarasani kwao ili wafanye hiyo kazi.Kila mtu alikuwa akiongea la kwake kwa kile walichoambiwa,hata walimu walipoingia madarasani wakaanza kushirikiana na viongozi wa darasa kuandika maoni ya wanafunzi wa kila darasa.

    Magreth alikuwa wa kwanza kuongea kwenye darasa lao maana alikuwa ni mpenda safari sana.

    "Mimi mwalimu nisiongee sana ngoja niende kwenye main point,kwangu Mimi naona Tour ambayo utakuwa ni ya kihistoria kuliko zote zilizowahi kutokea hapa shuleni ni kwenda kuukwea mlima maarufu hapa Tanzania mlima wa Kilimanjaro,hapo tutapata kujifunza mambo mengi sana kuhusu asili ya mlima ule,hadi sasa umeingiza kipato gani kwenye sekta ya utalii na vengine vingi ambavyo sisi hatuvijuwi,Mimi nachaguwa kwenda kutembelea mlima Kilimanjaro" alisema Magreth na kuwafanya baadhi ya wanafunzi wenzake akiwemo Sara wampigie makofi.Ester kama kiongozi wa darasa akiyaandika maoni yale ya Magreth kwenye karatasi.

    "Haya asante Mage kwa wazo lako zuri...mwengine" alisema Madam Magdalena kama mwalimu wa darasa la kidato cha 3.

    Basi wanafunzi wengine walitoa nao maoni yao juu ya swala hilo la safari ya kishule na maoni hayo yakaandikwa kwenye karatasi moja na kiongozi wa darasa Ester huku Madam akisimamia kuhakikisha zoezi hilo linakwenda sawa.Ikafika muda na Denis naye japo alikuwa mbele kama kiongozi wa darasa alisimama juu na kutaka kuchangia na yeye.

    "Kiukweli Tanzania yetu ina sehemu nyingi sana za kutalii hasa kwa wanafunzi kama sisi,ila hapa kila mmoja anaeleza ile sehemu anayoiona inafaa,kwa upande wangu sehemu ambayo inafaa sana hasa kwa shule yetu ni mkoani Tanga....mkoa ambao una kila sifa ya vivutio na sehemu nyingi za kujifunza kama sisi wanafunzi,kule kuna sehemu tunasoma kwenye vutabu vya kihistoria,kuna viwanda vikubwa sana vya Cement kama kiwanda cha Simba na chengine kinachoanzishwa cha Rhino,vile vile kuna bandari kubwa,mbuga ya Saadan na Yale mapango ya Amboni tunayosomaga kwenye History hapo huko Tanga,na isoshe wana tumia umeme wao wenyewe unaozalishwa Pangani na Hale kutokana na vyanzo cha maji,huo ndio uzuri wa mkoa wa Tanga ambao ninaupa asilimia zote kuwa unatufaa sana kuelekea huko" alisema Denis na kumfanya hata Madam Magdalena atabasamu,baadhi ya wanafunzi wakasikika wakimpigia makofi Denis aliyetoa wazo lile,naye Ester aliliunga mkono wazo lile na kuwafanya darasa zima likubaliane na kuuchagua mkoa wa Tanga kwenda kishule kutalii sehemu muhimu.

    Kwenye madarasa mengine yakiandika maoni yao na baada ya kazi hiyo ya kukusanya maoni ya kila darasa walimu waliondoka zao na kuwaacha wanafunzi madarasani wakiendelea kujadili ya kwao.Walimu walikusanyika na kukaa sehemu moja ofisini akiwemi mwalimu mkuu,walianza kusoma maoni ya wanafunzi wote yaliyokusanywa kimadarasa,huwezi amini mkoa uliopendekezwa na wanafunzi wengi ni mkoa wa Tanga na kila mmoja alizitaja zile sifa za sehemu za kutalii mkoani hapo,walimu wakawa na kazi ya kuujadili mkoa huo kuangalia kama ni sahihi kwa wanafunzi wao kuelekea kwa ajili ya taaluma na mwalimu pekee aliyeungana na wanafunzi kwa kuusopoti mkoa huo alikuwa ni Madam Magdalena ambaye naye alipata kuzungumzia uzuri wa mkoa wa Tanga hasa kwenye sehemu za vivutio kama Saadan,bandari ya Tanga na hata mapango ya Amboni vitu ambavyo vipi kwenye vitabu vya kihistoria,aliongea maneno mengi yaliyowafanya wenzake waanze kuafiki kwa hilo wazo,hata mwalimu mkuu akakubaliana na wazo hilo na taratibu za kuanza kuandika barua za maombi kwenye baadhi ya sehemu za vivutio mkoani Tanga zikaandaliwa huku wanafunzi wakakusanyika tena paredi ili kusikiliza kilichoamuliwa na walimu,mwalimu mkuu alisimama na kuwaeleza yote wanafunzi.

    "....huo ndio mkoa ambao wengine wenu mmeuchagua na sisi walimu tumekaa tukauona unafaa kwakuwa na vivutio vingi vya kutalii na tumepitisha kuwa tutakwenda Tanga" alisema mwalimu mkuu na wanafunzi wengine wakafurahi kusikia hivyo huku wengine wasiafiki walikaa kimya.

    "Kila mwaka shule yetu inatoka nje ya mkoa juu wa Mara kwenda sehemu zengine mikoani lengo ni kupitia sehemu nyingi za kihistoria,na kizuri zaidi tuna kiasi cha pesa kidogo tunachopatiea na mfadhiri wetu na tunatumia kudumisha taaluma ya hapa shule,na kwa safari kama hizi kazi LA mwanafunzi anayehitaji kushiriki basi atachangia kiasi kidogo cho pesa ili kufanikisha safari hii,najua hakuna asiyeifahamu Tanga ilipo,umbali wa kutoka hapa Mara hadi Tanga ni mbali mno na kwa haraka haraka tumekaa na walimu tukaona garama za mwanafunzi ambaye anayehitaji kwenda itambidi atoe shilingi elfu 30 kila mmoja ili tuichanganye na hili fungu tulilo nalo kufanya safari hiyo ifanikiwe,hivyo kwa yeyote anayetaka kwenda safari hii afahamu anahitajika kutoa elfu 30,kama utaingia shambani kulima kibarua haya,kama utaenda kuuza mihogo sawa,kama utapewa na wazazi sawa ila tu siku tutakayopanga ya safari hiyo kuanza basi kusiwepo na mtu ambaye ataleta vikwazo tena,na tushaanza kutuma barua za maombi kwenye baadhi ya sehemu kama Amboni Caves(mapango ya Ambono),bandari kuu ya Tanga,mbuga ya Saadan na vyanzo vya umeme pale Hale na Pangani,hivyo mkienda kwenu muwaeleze wazazi wenu hivyo hiyo hela ni ndogo sana kwa wewe mwanafunzi wa Butiama ufike sehemu hizo zote muhimu mkoani Tanga kwa hela hiyo,na mkumbuke ni kama kumbukumbu kwako wengine mtazeeka hapa hamtaujua mkoa wa Tanga ukoje mtaishia kusoma tu kwenye vitabu na kusikia maredioni,"alisema Mwalimu mkuu na kuwafanya wanafunzi na walimu wafurahi.

    "basi nawaomba Leo muwafikishie wazazi wenu hili swala mapema,barua ya maombi itwafikiwa huko tunapokusudia kwenda hivyo kuanzia leo uanze kutafuta pesa usaidiane na wazazi,Mimi nimemaliza niwatakie maandalizi mema kila mmoja" alisema Mwalimu mkuu na kugeuka kuelekea zake ofisini,wanafunzi wakaruhusiwa kuelekea kupata kifungua kinywa asubuhi ile baada ya muda huo kufika,ikawa stori ni kuhusu suala hilo la safari.

    Wengi walilipokea swala hilo ni la kipekee na walifurahi sana kusikia hivyo huku wakiahidi kwenda safari hiyo,hata kwa Ester na wenzake walikaa sehemu wakawa wanaongelea uzuri wa mbuga ya Saadan na mapango ya Amboni na kila mtu akiahidi kwenda akiwemo Sasha.

    Kwa upande wa Michael alionekana mwenyewe furaha sana tena isiyo na maelezo,swala LA safari ile aliona ni kama jambo jipya kwake na ni la muhimu sana hasa kwenye kufanikiwa kumpindua Sara,alifikiria sana na kuona ndio wakati pekee wa yeye kumaliza kazi endapo kama Sara na wenzake watakuwepo kwenye safari hiyo,alikuwa amekaa sehemu pekeake huku akiwa ameshika kitabu cha kihistoria akisoma habari za mapango ya Amboni ambayo yalioneshwa kwa michoro ambayo ilionekana kutisha kwa vile ilivyokaa,alipiga macho sehemu za shule hiyo na kuona jinsi wanafunzi wakivyokuwa na furaha juu ya swala hilo la kutembelea sehemu za kihistoria katika mkoa wa Tanga.



    Basi wanafunzi wakawa na jambo hilo kichwani mwao kwamba kuna safari ya kuelekea mkoani Tanga kishule hivyo walizifikisha taarifa hizo kwa wazazi wao kuhusu suala hilo,baadhi ya wazazi waliona muhimu wa safari hiyo kwa watoto wao na kulipokea kwa mikono jambo lililo wafanywa watoto wao wapate faraja na kujiwekea asilimia kubwa ya kuwepo kwenye safari hiyo,kuna ambao pia kwa upande wao waliona kama ni kupoteza pesa tu za kuchezea wakisingizia hali ni ngumu kisa kumpeleka mwanafunzi mkoa tofauto na ule wa pale huku wakiona sio jambo la muhimu sana na haina ulazima na kuwafanya watoto wao wabaki kuwa wapole kwa kukata tamaa ya kuelekea safari hiyo ya kishule,hivyo kukawa na makundi tofauti juu ya safari hiyo.

    Kwa upande wa walimu walijitahidi kuhakikisha barua zile za maombi zinafika sehemu husika na kubaki wakisubiria majibu waambiwe ni siku gani ya kufika kama wakikubaliwa,na kweli Mungu si Athumani majibu yaliyokuja yaliwafanya walimu pamoja na wanafunzi wafurahi baada ya kuruhisiwa kutembelea mkoani Tanga kishule kwa baadhi ya sehemu muhimu walizozichaguwa,hivyo ikawa kazi ni kukusanya michango kwa wanafunzi ndani ya wiki tatu wakizopanga,na kweli wanafunzi walioelewana na wazazi wao wakaridhia mapema tu walianza kupeleka pesa hiyo wakizidi kuwahamasisha wenzao kuhusu safari hiyo,hadi wiki mbili zilipokatika walishapatikana wanafunzi 37 waliokamilisha mchango huo wa safari akiwemo Magreth,Denis pamoja na Ester.Kwa kuona wako wao tu wakaanza kumhimiza Sara afanye kila linalowezekane awepo kwenye safari hiyo,huku Magreth naye alimfuata Natasha kumueleza umuhimu wa safari hiyo na kumfanya aelewe.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa upande wa Michael naye alikuwa nyuma hakuweza kutoa pesa hiyo ya safari akiwa na maana yake,muda wote alikuwa akielekea ofisini na wanafunzi wanaoenda kulipia hela ya safari hiyo na kuiahia kuangalia majina tu ya waliotoa na kuwaona wakina Denis na wenzake lakini jina la Sara halioni,basi wakawa anarudi na kila siku ikawa ni desturi yake lazima akaangalie kama Sara yupo maana ndio mtu mlengwa anayemtamani kwa hamu kubwa ni Sara lengo hasa ni kumuua,alipopokea taarifa hiyo ya safari kuelekea Tanga alifurahi na kuona sehemu ambayo atammaliza kwa urahisi Sara ni pindi watakapoingia kwenye mapango ya Amboni na ndio siku ambayo hata wakina Ester na wenzake wote wote atawamalizia huko kabisa maana muda waliopewa kumaliza kazi hii umekwisha ,alishawaandaa vijana wake wa nguvu za giza wake na kiwaagiza mapema kabisa waelekee mkoani Tanga moja kwa moja kwenye mapango ya Amboni ili waanze kuangalia ustaarabu wa njia za mule ndani ya mapango wakipanga jambo lao watakalo lifanya siku hiyo,na kweli siku zilienda na kubaki siku mbili ili daftari lifungwa safari iandaliwe,bado Sara alikuwa hajapata hela ya kupeleka shule kuhusu safari hiyo,siku hiyo alikaa na baba yake wakiwa wanakula.

    "Ndio maana hadi sasa sitaki kupeleka hiyo hela maana yule Mjinga hajalipa nayeye hadi leo,sasa sijajuwa ana maana gani maana Natasha hajalipa na huenda asiende,sasa nikisema mimi nilipe halafu nimuache Natasha itakuwa kama mchezo wa kuigiza maana nitakuwa nimempa Uhuru na wepesi Michael amdhuru Natasha kwa urahisi,na nikikaa hivi hivi hadi dakika ya mwisho Michael anaweza kubadilika yule akalipa ikawa nimebaki Mimi na Natasha na kuwaacha wakina Ester wakiwa kwenye matatizo mengine." alisema Sara akiwa ameweka mikono tu mezani.

    "Sara mwanangu.....haya yote unayopitia ni mitihani tu na ujuwe kuwa hata mama yako aliipitia mitihani kama hii hadi anakuja kuwa Malkia hivyo usiumize kichwa saaana ukashindwa kupata jibu sahihi,kula chakula mwanangu ulale naamini mpaka asubuhi utakuwa ushapa jibu sahihi juu ya hili jambo" alisema mzee Junior akiwa anamuamini kabisa binti yake,wakaendelea kula na baadae kila MTU akaelekea kumpumzika chumbani kwake.

    Akiwa chumbani kwake mzee Junior alimuonea huruma sana mwanaye jap ndio wajibu wake kufanya hivyo,laikumbukua siku akiwa na mama Sara enzi za uhai wake wakiwa duniani kabla ya kuzaliwa Sara.



    (#alikumbuka)



    "kwa hiyo ufalme wenu mnafanya kurithishana wenyewe kwa wenyewe?"aliuliza Junior akiwa amelala mapajani kwa Aznaty.

    "ndio ilivyo Junior,yaani inaenda kizazi hicho hicho hadi mwisho,kama sasa baba yangu ndiyo mfalme na kwakuwa hana mtoto wa kiume basi mimi ndiyo nitakuwa kiongozi pindi baba yangu akitoka,na ndio hivyo hivyo inavyoenda nikijaaliwa mtoto awe wa kiume au wakike basi ndio atakuja kuwa mbadala wangu na yeye hivyo hivyo akiwa na familia yake mwanaye ndio atakuja kuongoza falme hiyo" alisema Aznaty.

    "Kwahyo mwanangu naye anakuja kuwa Malkia huko?alisema Junior baada ya kujua Aznaty yumja mzito.

    " ndio atakuwa Malkia,japo hadi uitwe wewe ni Malkia lazima upitie mambo mengi sana kwenye maisha yako,huwezi kuwa Malkia wa kuitwa tu lazima uwe imara,na hakuna msaada wowote unaoupata kwa mtu wa karibu zaidi ya akili yako mwenyewe ndio inayohitajika hapo uionyeshe ili wahakikishe kwamba wewe unafaa kuwa Malkia."alisema Aznaty na kumfanya Junior aelewe umakkia unapatikana vipi.



    Hayo yote alikuwa akiyakumbuka Mzee Junior usiku ule akiwa kitandani,alijuwa kuwa hadi Sara kuitwa Malkia lazima apitie kwenye matatizo mengi sana na kitu pekee alichokioata kama msaada ni zile nguvu za mama yake Malkia Aznaty lakini hatakuja kusaidiwa tena zaidi ya akili yake mwenyewe.Huku kwa Sara naye alikuwa chumbani kwake akitafakati namna mambo yanavyoenda,alifikiria sana hasa kuhusu Natasha endapo akabaki hali ya kuwa wenzake wamesha jihakikishia safa,kitu kinachomuumiza kichwa zaidi ni Michael hadi sasa haeleweki kama naye ataenda au laa,alibaki akiwaza lakini baadae akapata wazo na kuona huenda likawa zuri,alipanda kitandani na taratibu akavuta shuka kuanza kutafuta usingizi usiku ule.

    Asubuhi kulipo pambazuka alianza kufanya kazi zake zote na baada ya kumaliza akajiandaa tayari kwa kuelekea shule,hata alipotoka chumbani kwake alimsalimia baba yake akiwa amekaa nje baada ya kufungulia mifugo yake mbuzi na kuku wake.

    "vipi ulishapata wazo namna ya kufanya?" alisema mzee Junior akiwa anawarushia mahindi kuku wake asubuhi ile.

    "ndio nishapata wazo,ndio naenda kulifanya nikifanikiwa nitakueleza baba wala usijili wacha niwahi shule baba baadae" alisema Sara huku akikimbia zake na kumfanya baba yake atabasamu tu,anampenda sana mwanaye.



    Siku hiyo wanafunzi wengi wakionekana wakiongelea swala la safari hiyo ya kuelekea Tanga huku wengine wakizidi kutoa mchangi huo huku ikiwa imebaki siku moja tu ya kukusanya pesa hiyo,siku hiyo Sara alimchukuwa Natasha na kukaa sehemu moja wakiongea wenyewe.

    "nilimweleza mama akasema hana hela kabisa japo alitamani kunisaidia lakini ndio hivyo imeshindikana maana si unajuwa baba mwenyewe ni wa jambo na ni mlevi balaa ukimwambia swala hilo hakuelewi kabisa" alisema Natasha kwa huruma.

    "Ila umeridhia wewe kwenda hiyo safari au kwakuwa umewaona wenzako na wewe ndio unatamani?" aliuliza Sara akionesha kuwa siriasi.

    "Yaani Sara sikufichi,tangu siku ile tulivyo tangaziwa nikawa Nina hamu sana ya kwenda,napenda nipajuwe Tanga kwanza,nijue mapango ya Amboni,bandari ya Tanga na vitu vengine kama sehemu za kihistoria,ni muhimu kwa mtanzania kama Mimi inakuwa kqma kumbukumbu kwangu." alisema Natasha na kumfanya Sara aelewe.

    "basi sawa nimekuelewa,tutaenda tu usijali" alisema Sara na kumfanya Natasha amshangae,alifurahi kusikia hivyo,basi ikawa ni furaha kwa Natasha baada ya kuambiwa kuwa Sara atajitolea kumlipia ili tu waende wote katika safari hiyo.

    Basi baadae masomo yaliendelea madarasani kama kawaida hadi muda wa kuondoka shule siku hiyo ulipowadia kengele iligongwa na wanafunzi wakaelekea paredi kusikiliza matangazo.Mwalimu mkuu alisimama mbele na kuanza kuongea mwili matatu na wanafunzi.

    "nafurahi sana kwa wale waliotoa michango yao ili safari ya kuelekea Tanga ikamilike,maandalizi yako vyema na naomba nitangaze kwamba Leo ni Jumanne kesho ni mwisho wa michango hiyo,Ijumaa ndio safari inaanza hivyo kwa wale waliotoa tayari jiandaeni mnaondoka Ijumaa kurudi hapa ni Juma tatu mchana hivyo mjiandae,na ieleweke mnaenda kishule hivyo uhuni pamoja na mambo ambayo hayaendani na sheria za shule hazitaruhusiwa kwenye safari,hivyo basi kama wewe umejiandaa kufanya uhuni wowote huko muendako utakapo bainika aisee utajuta kuifahamu hii shule ya Butiama,Mimi napenda amani na ndio maana naihimiza iwepo katika safari yenu,na nyie ambao hamuendi tutaendelea kuhudhuria kama kawaida maana walimu watakao ondoka ni wacgace tu kusiwe na visingizio hutakuja shule kwakuwa hakuna walimu,hata mimi nitabaki,zaidi ya haya niliyo ongea niwatakie mchana mwema kesho muwahi."alisema Mwalimu mkuu na kuwarugus wanafunzi kurudi zao majumbani,hapo ndio wanafunzi wakaamini sasa kweli safari imepamba moto,njiani ilikuwa stori ni hiyo tu kwa wanafunzi ambao wqlikiwq tayari washatowa pesa hiyo ya safari,walirudi majumbani kwao na kutoa taarifa kwa wazazi wao kuhusu siku hiyo ya safari ambayo ni Ijumaa.Kwa upande wa Ester yeye alikuwa hana shaka baada ya kuhakikishiwa safari ile alimueleza bibi yake kuhusu siku ya kuondoka Tanga,akawa yupo tu chumbani kwake akijisomea masomo yake ya shuleni,hata baada ya kumaliza alupanda zake kitandani na kile kitabu alichopewa na Sara akawa anapitia pitia kukisoma akiwa atayari ameshakizhiyo,haikupita hata dakika 30 usingizi ukamchukuwa.

    Asubuhi kulipokucha wanafunzi kama kawaida walionekana wakisafisha mazingira ya shule yao,na baada ya kazi zote za asubuhi kumalizika waliingia zao madarasani,siku hiyo vipindi vyote vya asubuhi vilivunjwa kwa kuwa na kikao cha walimu wakizungumzia juu ya safari hiyo,huku wanafunzi wengine wakimalizia malizia kulipia hela hiyo ambazo zilikuwa zikikusanywa na Madam Magdalena.

    Sara na Natasha walionekana wakielekea ofisini kwa ajili ya kulipia hela hiyo,walipoingua tu ofisini kwa Madam walimkuta Michael ndio anamalizia kuandikwa jina lake,walisogea hadi pale na kumfanya Michael ageuke kuwatazama na kubaki wakiangaliana tu,alitabasamu tu Michael na baada ya kuhakikisha ameandikwa alianza kuondoka zake akawaacha Sara na Natasha mule ofisini.

    "yaani wewe Sasha usingeenda shoga yako Ester sijui angejisikiaje maana mwenzako mapema tu kashalipa" alisema Madam akipokea hela ya Sara ambaye anajulikana kama Sasha shuleni,alibaki akitabasamu tu kwa maneno yale ya Madam maana urafiki wake na Ester hakuna asiyeujuwa,basi na Natasha naye akalipia na baada ya kumaliza wakarudi zao sasa wakisubiri hiyo kesho siku ya safari,.

    Basi muda ulienda na mchana wakati wa kuondoka wanafunzi waliitwa wale wote waliolipa hela zao wakaambiwa wabaki na wale wasiolipa wakaruhiswa kuondoka.Ni wanafunzi 74 tu waliolipia hela hiyo wakaingia kwenye darasa moja na walimu wote wakawa wanapanga mambo yao kwaajili ya siku ya kesho ya safari.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "basi ndio kama nilivyowaambia,walimu watakao kuwa na nyie ni mwalimu Isack,mwalimu Mhando na Madam Magdalena na kila mmoja atahakikisha nidhamu kwa kila mwanafunzi inakuwepo,usafiri utakuja hapa shuleni asubuhi saa 1 kamili na safari itaanza saa 3 asubuhi hivyo ukichelewa shauri yako,kuna mahala mtafika huko ndio mtakaa hapo kwa siku hizo mbili na kuhusu chakula tunashukuru kuna mfadhili wetu tumemueleza suala hili na amesgatoa kiasi cha pesa ambacho kishatumwa mkoani Tanga kwenye sehemu mtakayofika watawahudumia kuhusu chakula,na kwenye mavazi...naomba nirudie kwenye mavazi,muda wote ukiwa safarini unatakiwa uwe na uniform za shule hata siku mtakayoanza kwenda sehemu za kihistoria mtakuwa na uniform zenu,ila mtaruhusiwa kubeba nguo za heshima pindi mkiwa pale mnapokaa basi na nirudie tena ziwe za heshima,mwalimu wa taaluma na nidhamu mwalimu Isack yupo nadhani atasimamia hilo,Mimi nawaombea safari njema wanangu na muende huko kujifunza na si vingine ili mkija muwe na cha kusimulia....niwatakie safari njema" alisema mwalimu mkuu Malamba na wanafunzi wakampigia makofi kama kumshukuru kwa maneno yake ya busara,basi walimu wengine nao waliongea yao na kuagana kwa amani na wanafunzi wakaruhusiwa kurudi nyumbani kwao wawe tayari asubuhi kwa ajili ya safari hiyo,ilikuwa ni furaha sana kwao na kuisubiri siku ya kesho kukuche haraka.



    Kila MTU alirudi zake kwao na kujiweka sawa kwa ajili ya safir ya kesho,Sara akiwa kwao aliutumia muda huo kuongea sana na baba yake jioni ile waliongea mengi sana na kumweleza maamuzi aliyochukuwq ya kumlipia Natasha lengo ni kuwa nao wote wale wenzake na cha kushangaza hata Michael naye yumo kwenye safari hiyo,wakaanza jutilia mashaka huenda kuna jambo analikusudia na sio bure.

    "ila Sara kabla hujaondoka nenda kamuage mama yako kwanza upate baraka zake huenda ukaepushwa na mitihani inayokukabili uaijiamini sana kupitiliza mwanangu" alisema Mzee Junior na kumfanya mwa naye amuelewe,basi hakutaka hata kupoteza muda aliondika na kuanza safari ya kuelekea kuelekea makaburini lakini alipitia nyumbani kwa akina Ester akimuomba amsindikize sehemu na hakutaka kumwambia ni wapi,Ester hakuwa na kipingamiI mbele ya Sara wakaongozana wote hadi sehemu ya makaburini jioni ile na kumfanya Ester ashangae baada ya kujuwa kaletwa sehemu ile.Walielekea hadi kwenye kaburi husika na kumfanya Sara alitazame kaburi la mama yake kisha akapiga magoti na kuanza kung'olea majani yaliyoanza kuota,Ester naye akafanya hivyo.

    "mama...shikamoo....vipi upo salama,ni Mimi mwanao mama tumekuja hapa kukutembelea na rafiki yangu Ester,tumekuja kukupa taarifa kuwa kesho apendapo Mungu tuna safari ya kwenda mkoani Tanga kishule,najua kuna mambo mazuri tutayaona huko na kufurahi kila wajuwa fika kulipo kuzuri hakukosi ubaya hivyo kama kuna jambo litakalotufanya sisi na wenzetu ulioniambia niwe nao pamoja,kama kuna nguvu nisizoziweza Mimi basi nisaidie mama lengo ni kukamilisha kile ulichoniambia...naamini utakuwa umetuelewa nini shida yetu...." alisema Sara na kufumba macho kisha akainamisha kichwa kama anafanya maombi,hata Ester naye ikambidi afumbe tu macho akimuiga Sara,wakiwa wako bize na maombi hayo huwezi amini........Malkia Aznaty alipata kuonekana akiwa juu ya kaburi lake amekaa akimtazama mwanaye Sara akiwa bize na kuomba,akabaki tu akitikisha kichwa kama hali fulani kisha akamgeukia Ester aliyekuwa naye amefumba tu macho,alimtazama sana na mwishowe akabaki akitabasamu tu,alinyanyua mkono wake na kumyooshea Sara kwa muda kadhaa kukionekana kama moshi fulani wa rangi ukitoka mwilini mwa Sara kisha Malkia Aznaty akageuka kwa Ester na kunyanyuka pale alipo akasimama mbele ya Ester na kumshika kichwa huku akiongea maneno fulani yaliyomfanya Eater mwenyewe ashike kichwa chake hana anachokiona wala kujuwa kama ameguswa,Malkia alisendelea kuongea maneno yake na baada ya dakika kadhaa alimaliza na kubaki kumuangalia Ester kwa tabasamu huku alirudi zake kwenye nyumba yake ya milele,alijilaza kama kawaida na wakati huo huo Ester alikuwa akifumbua macho yake na moja kwa moja akashuhudia mtu akiwa analala juu ya lile kaburi,kwa vile alivyomuona tu akahisi ni mama yake Sara tu japo moyoni alijawa na woga,akamgusa Sara begani na kumfanya ageuke kumtazama,akamuoneaha kwa kidole kule kabulini,na kweli Sara alupogeuka aliuona mwili wa mama yake ikiwa umelala pale juu ya kaburi taratibu ukianza kudidimia kwenda chini,haraka Sara akanyanyuka kwa furaha na kuanza kumuita mama yake lakini aliambulia patupu baada ya mwili wa mama yake kupotea ,kidogo Sara alifarijika juuona mwili wa mama yake japo hajamuona kwa sura na ni tangu ajijuwe kuwa yeye ni Sara hajawahi mumuona mama yake hata siku moja,haijui sura yake,aligeuka zake na kumtazama Eater aliyekuwa amesimama akiwa naangalia tu.Sara alimweleza Ester huku akiwa hana uhakika kuwa huenda mama yake akawa amefanya kitu ambacho kitakuwa msaada kama wakikumbana na matatizo kwenye safari yao ndio maana amejitokeza vile maana sio bure.Basi walirudi zao majumbani kwao baada ya kusindikizana na kila mtu akawa anajiandaa kwa ajili ya safari ya kesho.Wakiwa wao wanajiandaa kwa safari kwa furaha huku Michael alikuwa akiwasiliana na wenzake kuhakikisha mambo yakwenda kama walivyopanga.Safari hii ameiamulia kwa nguvu zote akihakikisha anampoteza Sara.

    Huku kwa Sara alikuwa akijiandaa na safari hyo usiku ile,alikuwa na imani sana baada ya kutoka kulizulu kaburi la mama yake jioni ile akiwa na Ester ambaye naye muda huo alikuwa akipanga vitu vyake kwenye begi lake LA mgongoni,alikichukuwa kile kitabu alichopewa na kukiangalia tu,hakutaka kabisa kukisoma siku hiyo maana kila akikisoma lazima achelewe shule,hivyo akahisi huenda akachelewa hata siku ya kesho ya safari endapo akikisoma,alikichukuwa na kukiweka kwenye begi lake la safari kisha akapanda zake kitandani kutafuta usingizi taratibu.

    Na hatimaye asubuhi ya safari magari mawili yalionekana maeneo ya shule yamepaki yakiwafanya wanafunzi wazidi kufurahi baada ya kuona safari imewadia kweli,miongoni mwa wanafunzi wale 75waliokuwa tayari kwa safari walikaa mahala pao wakizidi kusubiri muda ufike safari ianze.Natasha,Denis,Magreth,Sara pamoja na Ester walikuwa tayari washawasili na kusimama mahali fulani wao mwenyewe wakiwa wenye furaha.

    "najisikia furaha kwa kweli maana sikutegemea kama nitakuwa na nyie Leo hii nakushukuru sana Sara kwa wema wako." alisema Natasha akionekana kufurahi siku hiyo akiwa amebeba begi lake mgongoni.

    "Natasha...hupaswi kunishukuru hivyo kana kwamba nimefanya jambo kubwa,ni wajibu kwangu kuhakikisha wewe unakuwa karibu na wenzako,laiti ungebaki halafu wenzako tungeondoka unahisi vp tukamuacha na Michael huku,utakuwa salama wewe?,hivyo swala la wewe kuwa pamoja nasi ni kama jambo LA kawaida tu wala usijali" alisema Sara na kumfanya Natasha aelewe.

    Michael naye alikuwa amejichanganya na wenzake wakiongea mambo kuhusu safari yao,alifanya hivyo kusudi asionekane ubaya wake mapema dhidi ya wakina Sara ambao nao walikuwa makini naye muda wote baada ya kujuwa si mwema kwao hata robo.

    Basi muda ulipokaribia Madam Magdalena aliwaita wale wanafunzi na kuanza kuota jina mmoja mmoja na kuingia kwenye gari kukaa kwenye siti hadi wote walipoisha,na kama majina yalivyopangwa kutokana na mtu alivyowahi kutoa pesa yake,hivyo wakina Ester,Magreth na Denis walikuwa kwenye gari la kwanza na kuwaacha Sara na Natasha wakiingia kwenye gari lengine ambalo ndio Michael alipoingia na kwa bahati nzuri kama sio mbaya Madam akaanza kuwapanga watu wasikae kwa kubaguana,akajikuta akimuweka Michael na Sara wakiwa sawa kwenye siti zinazobandana jambo lililomganya Sara ashangae,hata Michael naye alitahaluki kuona Sara anakaa pembeni yake,.Basi walimu waliagana na wenzao watakaobaki shuleni huku nao wanafunzi wakiwapungia mkono wenzao waliokuwa nje ya madarasa na dakika chache baadae magari Yale yakaanza kuondoka shuleni hapo huku mwalimu mkuu akiwapungia mkono kwa kwaheri wanafunzi na walimu waliokuwa kwenye magari hayo.Ilikuwa kama utani vile lakini ndio imetokea tena Sara kukaa pamoja na Michael,ambaye muda wote safarini alikuwa akiangalia tu nje kuishangaa miti ikipitwa tu na gari,alijikuta akitabasamu tu baada ya kuona leo ndio mwisho wa yule wa pembeni yake,aligeuka na kumtazama Sara akiwa bize na kuangalia mbele.

    "Naona Leo kwa Mara ya kwanza Ndugu wawili wamekaa pamoja,kila mmoja anataka kuwa juu ya mwenzake hali ya kuwa ukweli unajulikana,kwa nini usiamue kuachana na haya mambo Dada yangu kulikoni ukaendelea ukajitafutia matatizo yasiyo na lazima,?!" alisema Michael huku akimtazama Sara wakiwa ndani ya gari safari ikiendelea.Sara alimtazama Michael na kubaki akicheka tu kwa yale maneno ya Michael ambaye alivyoona Sara anacheka na yeye akaamua kucheka.

    Hali ile ilimfanya Natasha aliyekuwa nyuma yao ashangae kuona maadui wawili wanacheka kwa furaha,alistaajabu.

    "sikia nikwambie Michael,unajuwa wewe ni mdogo kwangu,licha ya umri kukupita hata fikra pia nimekupita japo ubishi na ujinga ndio umekujaa kichwani,hivi unavyodhani utaweza kunishawishi Mimi niachane na hili,ili iweje kwanza baada ya kuachana nalo,uje kuwa kiongozi gaidi,muendelee na mila na desturi zenu za matabaka!sikia wewe Mimi naitwa Sara Junior mtoto wa Malkia Aznaty ambaye alikuwa akiwa anatetea nafasi yake,kwa kulichotokea kwa mama yangu siwezi kufumbia macho,nitamdondoaha mmoja baada ya mwengine hadi nihakikishe sijaacha hata msuriati yeyote ambaye yupo akikumbatia mila zenu za kipumbavu,hata nisipokipata kiti cha uongozi lakini nihakikishe tu watu mnaotaka Kuwaua wanaishi kama wengine,na kwa hili kamwe siwezi kurudi nyuma" alisema Sara kwa kujiamini huku sauti ya radio ya gari ikiwa juu na kufanya maongezi yao yasisike na MTU yeyote zaidi yao.Maneno yake yalimtia sana hasira Michael baada ya kuona Sara anazidi kupanda kichwani,alimtazama kwa hasira pale walipokaa.

    "sawa....endelea kuwalind.....jibu litapatikana siku sio nyingi" alisema Michael na kumfanya Sara abaki akitabasamu tu kuonesha anajiamini.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Safari iliendelea huku baadhi ya wanafunzi wakiwa na furaha sana wakioneshwa sehemu kadhaa ambazo hawakuweza kuzijuwa hapo awali,safari ilizidi kupamba kasi huku walimu wakizidi kuwapa faida na uzuri wa sehemu ambao watapata kufika na kuzidi kuwasisitiza wawe na adabu pindi wakifika.

    Yote hayo alikuwa akiyasikia Michael na kuona ni ujinga tu huku lengo lake hasa ni kuwaangamiza wake wote aliowakusudia wakiongozwa na Sara aliyekuwa pembeni yake.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog