Search This Blog

SARA (MSAADA WA MATESO) - 4

 







    Simulizi : Sara (Msaada Wa Mateso)

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mkoani Tanga,mkoa unaosadikika kuwa na idadi kubwa ya watu wa dini ya kiislamu,na kweli kona siku ya mtaa wanawake walionekana kujistiri miili yao kwa kuvaa mabaibui,wengine nguo ndefu na kufunika nywele zao kama desturi ya mwanamke wa kiislamu,kwa upande wa wanaume baadhi yao walionekana kutembea na kanzu zao huku wakiwa kwenye usafiri wao baiskeli wakielekea sehemu mbali mbali siku ile ya Ijumaa baada ya kutoka kwenye ibada kuu ya swala ya Ijumaa,walionekana ni wakarimu na wenye mapenzi na watu hasa wao kwa wao na kila siku ya Ijumaa huwa na desturi ya kufanya sherehe za dini pindi ifikapo muda wa Magaharibi(jioni).Walionekana watu wanne wakiwa kwenye shule moja ambayo ilisadikika siku hiyo inategemea kupokea wageni kutoka mkoani Mara,ni wanafunzi ambao wanakuja mkoani hapo kwaajili ya kutalii kwa siku mbili kisha watarudi zao,watu hao wanne walikuwa ni walimu wakiongozwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo,walikuwa wakiandaa mazingira ya kufika wageni wao kusudi kusitokee adha yeyote pindi wakifika.Ukaribu wa mwalimu huyo na mwalimu mkuu wa Butiama Malamba uliwafanya wayaweke mambo sawa ili wanafunzi wale wafike sehemu salama,shule hiyo ilikuwa ina mabweni ya kutosha ambayo bado hayajaanza kupata wanafunzi wa kukaa hivyo zilitumwa pesa kwa mwalimu huyo ili awapokee wanafunzi hao wakae hapo kwa siku hizo mbili kisha watarejea,swala hilo likawa limekamilika na wakawa wanawasiliana tu na walimu waliokuwa safarini wakiwasubiri kuwapokea.

    Masaa yalisogea sana hadi kufika usiku wa saa moja hatimaye magari yale mawili ya wanafunzi yaliingia mkoani Tanga na kuwafanya wanafunzi wazidi kufarijika,hawakuamini.

    "Na hatimaye jamani tumeingia mkoani Tanga,kikubwa kilichotulita huku ni kujifunza na sio kingine,huu ni mji wa watu naomba tuwe makini,tutaelekea moja kwa moja sehemu ambayo tumeapangiwa kufika,kila mtu ahakikishe hajasahau kitu chake kwenye gari,muda sio mrefu tutakuwa tumefika" alisema Mwalimu Isack akiwa amesimama kwenye gari akiwaambiwa wanafunzi wake,hata kwa Madam Magdalena naye aliwaeleza wanafunzi waliokuwa naye kwenye gari kuhusu kuwa makini.Na kweli waliweza kufika kwenye shule ile waliyoandaliwa kufika wakakaribishwa na walimu wale kwa furaha sana hadi wanafunzi wote waliposhuka kwenye magari na kusimama mahala pamoja.Walimu walichukuliwa na kwenda kuonyeshwa Yale mabweni ya wanafunzi ambayo yqlikuwa mengi sana na kila chumba kuna vitanda viwili ambavyo kila kitanda wanalala wanafunzi wawili mmoja juu na mwengine chini,hivyo ikawa ni rahisi sana kuanza kuwapanga wanafunzi kwenye kila chumba wanafunzi wanne.Hadi walipokamilisha zoezi hilo walimu walichukuliwa tena na kuelekezwa sehemu ya kula iliyoandaliwa kabisa baada ya kudhaminiwa na mtu kutoka kule Mara,baada ya muda kidogo wanafunzi waliitwa na kuanza kupata chakula cha jioni kwa pamoja kabla ya kulala ili kesho waanze jambo lao lililowaleta,ilikuwa ni furaha sana kwa wanafunzi kuwa pamoja huku wakibadilishana mawazo ya hapa na pale,wale walimu wenyeji walianza kuwaeleza uzuri na faida za kuja kutembelea sehemu za kihistoria na kuwasihi wawe waangalifu sana mjini Tanga,wanafunzi walielewa na wakashukuru pia kwa ukaribu wa wenyeji wao,baadae kila mmoja alirudi alipopangwa kulala wakisubiri siku ya kesho wakashuhudie vile walivyoambiwa.

    Michael alikuwa zake amepangwa amepangwa chini huku mwenzake mmoja akiwa juu ya kitanda chao huku na wenzao pembeni wakipangwa hivyo,alikuwa alifikiria tu siku ya kesho itakuwaje kuhusu mambo yake na sio vingine,hakuja Tanga kwaajili ya kutalii na kuona sehemu hizo za kihistoria bali kaja kwa kukamilisha kazi yake ya ya kuwaua wakina Sara na wenzake kabla hawajarudi shule.

    "kwa siku mbili zinanitosha kabisa kufanya kazi hii na wenzangu,lazima niwauwe wote hawa nimechoka kukaa duniani muda wote kama mtumwa wakati Mimi ni mtu mkubwa kwetu,hakutakuea na haja ya kurudi tena shuleni kama nikimaliza kazi huku huku narudi kwenye ardhi yangu nianze rasmi kuitawala,wacha nisubiro kukiche nijue tunaanzia wapi"alijisemea moyoni Michael akiwa kitandani amelalia mto ,taratibu akaanza kutafuta usingizi usiku ule.

    Kwa bahati iliyoje,Ester na wenzake walikikuta wamepangwa wote kwenye chumba kimoja hivyo ikawa nafuu kwao kuongea mambo yao ya siri bila yeyote kujuwa,usiku ule walikuwa wamekaa tu vitandani wakiongea mambo yao.

    "ujio wa Michael huku Tanga nina wasiwasi nao wenzangu hivyo muda wote mnatakiwa muwe makini,ukiona kiti chochote hukielewi jaribu kuepukana nacho mara moja hasa sehemu ambazo tutapelekwa kutembelea,naomba tuwe karibu muda wote kama sio kukaa wawili wawili kusudi tumpe wakati mgumu adui yetu"alisema Sara na kuwafanya wenzake Natasha,Magreth na Ester wamuelewe,basi walizidi kuongea mambo yao hadi usiku sana na huenda wao ndio wakawa watu wa mwisho kulala siku hiyo,kwa Ester haikuwa hivyo,wenzake walilala lakini yeye alichukuwa kitabu chake kile na kupitia pitia kidogo miatari kadhaa ambayo alishaijuwa kuitamka kwa wepesi,ilisemekana ni lugha tofauti na kiswahili,haikuwa inaeleweka kwa wepesi hasa kwa mtanzania wa kawaida,alizidi kukisoma usiku ule na kujikuta akipitiwa na usingizi huku akiwa amekikumbatia kitabu chake.

    Usiku wa manane ile ndoto kwa Ester ilijirudia tena,alimuona Michael akiwa kwenye kiti cha kifalme huku akicheka kwa dharau,chini alikuwa Sara akionekana kuteswa sana hajielewi,muda huohuo alikuja mwanadada mmoja akiwa na sahani ya dhahabu iliyokuwa imebeba kisu kikali sana na kumkabidha Michael ambaye alipo kipokea tu akanyanyuka na kumfuata Sara,kwa sura ya kikatili Michael alinyanyua kisu kile akimuelekezea Sara aliyekuwa akikitazama tu kile kisu bila kufanya lolote na papo hapo kikatua tumboni mwake na kumfanya apige kelele za maumivu.Ester alikurupuka kutoka kitandani na kupiga kelele akimtaja Sara hadi wenzake wote wakastuka kutoka usingizini na kumshuhudia Ester akionekana kuwa na wasiwasi,Sara alimtazama Ester akiwa kwenye hali ile hata yeye mwenyewe hakujuwa nini kimemkuta Ester,alikuwa chini na kuwafanya wenzake Magreth na Sara waliokuwa juu kwenye vitanda washuke na kukaa karibu yake.

    "Ester....niambie kulikoni,!umeota ndoto mbaya?" alisema Sara kwa taratibu kwa kuwa kulikuwa kimya usiku ule, bila kujizuia Ester alijikuta akimkumbatia Sara huku machozi yakimtoka na kuanza kulia, ikawa kazi ni kumbembeleza hadi pale aliponyamaza,wakamtuliza na maneno ya busara na baada ya kumuona amekuwa sawa wakamuuliza sasa awaeleze kilichomfanya yeye apige makelele usiku ule.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "kama ulivyo sema Sara kuwa Michael hakuja kwa nia nzuri,amekuja kukumaliza Sara" alisema Ester kwa huzuni na kuwafanya wenzake wamshangae,Sara mwenyewe alibaki akimtazama tu Ester machoni .

    "sawa Michael atqnimaliza,hebu niambie sasa hicho ulichokiota" alisema Sara kwa upole.

    "Mara ya kwanza tulipokuwa nyumbani niliota ndoto hii na nlipoamka nikapuuzia tu kwa kuwa sikuwa naamini ndoto za namna hiyo, lakini leo naiota tena ndoto hiyo hiyo nahisi kuna jambo laweza kutokea," alisema Ester na kuanza kuwaadisia yale yote aliyoota hadi pale Sara alipoonekana anachomwa kisu.

    Ndoto yake iliwafanya hata wakina Natasha waanze kuogopa baada ya kujuwa kuwa mwisho wa Sara sio mzuri.

    "Hapana...siiamini ndoto hiyo hata kidogo,Ester....ulivyoota sio...haiwezekani Ester,Sara sio wa kupotea kwa namna hiyo na bora tu uaingeaema umeanza kututia hofu sasa" alisema Magreth akionesha kuchukizwa ndoto ile.

    "na itawezekana vipi kwanza?" alisema Natasha akichangia wote wakiioinga ndoto ile.

    "jamani msianze kuongea maneno sio,Ester ameota hivyo,na ndoto ieleweke kuwa yaweza kuwa kweli au isiwe kweli"

    "hiyo sio...sio kabisa Sara nakwambia,haiwezekani kabisa" alisema Magreth akiwa naamini kabisa,.

    "sawa Magreth nimekuelewa,ila hili sio swala la kuanza kupuuzia hivi,kama Ester kaota inatokea hivi inatakiwa tukae tuangalie namna ya kulizuia hili swala na sio kuanza kulipuuzia"alisema Sara na kuwafanya sasa wenzake wawe kimya,akazidi kuongea maneno ya busara ya kuwatoa hofu wenzake kuhusu jambo hilo hadi Ester naye akatulia na kuondoa wazo hilo la ndotoni,basi baadae walirudi zao vitandani na kuanza kutafuta usingizi,Sara akawa anatafakari maneno ya Ester aliyoongea kuhusu hiyo ndoto,aliyapokea na kuamuwa kuyafanyia kazi.



    Asubuhi kulipo pambazuka wanafunzi waliamka na kuanza kuosha nyuso zao na kufanya mambo mengine,hadi kufika saa nne asubuhi kila mtu alikuwa tayari kashajiandaa kwa ajili ya kuanza kuelekea sehemu walizo takiwa kwenda,wote walivaa sare zao za shule kujitambulisha kuwa wametokea shule gani huko waendako,waliingia kwenye magari na muda mfupi baadae safari inaanza wakiongozana na wale wale walimu wenyeji wakiwapeleka,Michael alimeza mate na kuona sasa ameingia kazini hivyo anatakiwa kila jitihada kukamilisha kile alichokusudia kwa siku hizo mbili kabla hawajarudi Mara.





    Safari iliwapeleka mpaka kwenye bandari kuu ya Tanga ambapo wanafunzi walianza kujifunza hapo,moja kwa moja baada ya kushuka kwenye usafiri wakaanza kupiga hatua ya kuelekea ofisi ya kiongozi wa idara ya bandari ambaye alipokea taarifa ya ujio huo wa wanafunzi,aliwakaribisha akishirikiana na kamati yake na kuanza kuwapeleka wanafunzi hao kwa makundi wakiwaonesha sehemu muhimu za bandarini pale huku maswali ya hapa ma pale kwa wanafunzi wakitaka kujua namna ilivyoanza na maswali mengine kama hayo na kwa umakini wa uwelewa walipata kufahamu mambo mengi yanayohusiana na bandari hiyo,muda wote huo wakina Ester walihakikisha wanakuwa pamoja kama walivyopanga lengo ni wanakuwa salama kwenye safari hii hadi wanarudi.Michael alikuwa akiwatazama tu na kupanga namna ya kuwaingia kwa kuwatenganisha,aliwaacha tu waendelee kujisahau huku akipanga tayarimahala pa kuanza kazi yake.Baada ya kumaliza mambo yao eneo lile waliwashkuru idara ile kwa kuwapokea na kuwa nao pamoja muda wote wakielekezana mambo,basi waliaga na kupewa ruhusa wakaondoka zao na safari ikaendelea wakielekea kwenye mapango ya Amboni,hapo ndio Michael alipoonyesha tabasamu baada ya kupanda gari wanafunzi wote wakiambiwa na walimu wao,tabasamu lake lilimfanya Sara amshangae kwa maama si kawaida kwa Michael kuonesha tabasamu kwa kiasi kile.Basi safari iliendelea huku Michaelakiwa na yake ya moyoni.

    "hatimaye nilichokuwa nakifikiria kinaenda kuwa,naiona kabisa safari ya kwenda kuwa mfalme inakaribia kabisa,wacha nilimalize hili mapema."alijisemea moyoni mwake Michael huku akimuangalia Sara kwak kuibia.

    Huku alipo Denis akiwa na wenzake Magreth na Ester ambaye muda wote alikuwa anakipitia kile kitabu hasa baada ya kuota ndoto ambazo kwake yeye amekuwa akizitilia shaka,tangu ajitambue kuwa na yexe anahisia kama za Sara amekuwa akianza kuamini imani fulani waliwashkuru idara ile kwa kuwapokea na kuwa nao pamoja muda wote wakielekezana mambo,basi waliaga na kupewa ruhusa wakaondoka zao na safari ikaendelea wakielekea kwenye mapango ya Amboni,hapo ndio Michael alipoonyesha tabasamu baada ya kupanda gari wanafunzi wote wakiambiwa na walimu wao,tabasamu lake lilimfanya Sara amshangae kwa maama si kawaida kwa Michael kuonesha tabasamu kwa kiasi kile.Basi safari iliendelea huku Michaelakiwa na yake ya moyoni.

    "hatimaye nilichokuwa nakifikiria kinaenda kuwa,naiona kabisa safari ya kwenda kuwa mfalme inakaribia kabisa,wacha nilimalize hili mapema."alijisemea moyoni mwake Michael huku akimuangalia Sara kwak kuibia.

    Huku alipo Denis akiwa na wenzake Magreth na Ester ambaye muda wote alikuwa anakipitia kile kitabu hasa baada ya kuota ndoto ambazo kwake yeye amekuwa akizitilia shaka,tangu ajitambue kuwa na yexe anahisia kama za Sara amekuwa akianza kuamini imani fulani ambazo hapo awali hakuwa akiziamini kwa kuona kwake ni mbaya ukizingatia yeye ni msichana aliye lelewa kwenye misingi ya kikristo.Kwa kuzidi kupitia maneno ya kwenye kitabu akajikuta akiyakariri na kuyasema kwa ufasaha kama yanavyo tamkwa japo hakuwa na uhakika sana kama ni kweli,wenzake aliokaa nao karibu walimuona akikipitia kitabu kile lakini hawakuwa wanajua lolote hadi walipofika kwenye eneo hilo la mapangoni,walishuka kwenye magari yao huku wakiwa na furaha.Hiyo ndiyosehemu pekee wanafunzi wengi walikuwa wakiingojea kufika ili wajionee yale waliyokuwa wakisomakwenye vitabu vya kihistoria kuhusu mapango hayo.Moja kwa moja waliongozana hadi sehemu ambayo ni kama mapokezi kwa wageni,walikaa wote sehemu hiyo na kukaribishwa na kiongozi wa mapango hayo Aliongea nao na kuanza baada ya kujitambulisha na kuwapa maelekezo kuhusu mapango hayo kabla ya kuingia.

    "kwa mujibu wa wanasayansi na wanahistoria ilisadikika kwamba mapango haya yalianza kujiunda kwa ujumla miaka milioni moja na hamsini iliyopita huku kukidaiwa kuwa eneo hili lilikiea kwenye mkondo wa bahari hivyo maji yalikiwa yakifika hapa kwa kasi yakawa yanachonga miamba hii kwa miaka hiyo milioni moja na hamsini iliyopita hadi sasa kunaonekana hivi,na humo ndani ya mapango hayo kuna vitu vingi vya ajabu ambavyo ndivyo vimekuwa vivutio ulimwengu mzima,baada ya maji hayo ya baharini kuzidi kutawala eneo hili yalizidi kupiga hadi huko ndani kwenye miamba na kuonesha vitu mbalimbali kama bawa LA ndenge ambalo kwa haraka tu ukiliangalia waweza kuhisi huenda ndege alikufa pale na kubaki vile lakini ni mwamba uliochongwa kwa maji hayo,pia kuna picha ya mwamba uliyojichonga na kutengeneza sofa na kufanya iwe ni kivutio kwenye mapango haya,mlima Kilimanjaro,picha ya Chui iliyojichonga kwenye mwamba na I na vitu vingi ambayo mtazidi kuonesha na viongozi watakao ongoza kuingia humo" alielezea kwa ufasaha msimamizi huyo huku akiulizwa maswali na wanafunzi ambao walipewa majibu ya maswali yao waliyokuwa wakiandika kwenye madaftari yao iwe kama nakala.Muda wote huo Michael alikuwa akiangalia pande zote za pango lile,aliona kama anacheleweshwa kwa maongezi yale,basi baada ya muda wakatengwa kimakundi ya watu Ishirini Ishirini na hapo ndio ikawa furaha kwa Michael baada ya kuona watu aliokuwa akiwawinda wamewekwa tofauti tofauti,hata Sara alivyoona vile wamewekwa tofauti akaanza kuwa na mashaka,alipomtazama Michael alimshuhudia naye akimtazama huku akitabasamu kwa dharau kumaanisha kuna jambo linakwenda kutokea.

    "haya kundi LA kwanza tupite tianzie huku" alisema kiongozi wa msafara huo akiwa amekamata tochi kubwa huku wanafunzi Ishirini wakifuata akiwemo Natasha na Denis huku akimalizia mwalimu Isack,kundi lengine likapita kwenye pango lengine wakiongozwa na kiongozi wa msafara huo wa wanafunzi huku Ester na Magreth wakiwa sambamba pamoja na Michael ambaye alimfanya Magreth awe na wasiwasi,akamtonya na mwenzake Ester ambaye naye alipomuona Michael akabaki akimtazama tu kwa kujiamini kisha akaachana naye huku akimshika mkono Magreth.

    "Hupaswi kuwa muoga namna hiyo Mage kwani utamfanya aone udhaifu wako,jiamini tupo wengi hapa wala ondoa wasiwasi wako my" alisema Ester na kuzidi kumpa moyo Magreth,dakika chache mbele kiongozi wao akawaweka tayari na kuanza kuingia ndani ya pango kwa utaratibu maalum,Sara alikuwa akimtazama tu Michael akiwa nyuma nyuma na kuanza kuhisi jambo,alifumba macho yake na kuwa makini,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ester...Ester...nawaomba sana muwe makini na Michael...hakikisha muda wote unakuwa karibu na mwenzio wala msiachane hata point maana nahisi Michael kuna jambo anataka kulifanya" alisema Sara kwa hisia kali na sauti ile ikapenya masikioni mwa Ester ambaye akiyasikia maneno Yale na kujuwa ni Sara,kila kwa bahati mbaya Michael naye aliyasikia maneno Yale na kumfanya ashtuke akasimama kabla ya kuingia,akageuka nyuma kumuafuta Sara,akamuona yupo na wenzake wakiwa wanaandaliwa nao waingie mapango ni hapo,aligeuka kuangalia mapangoni ambapo wenzake walikuwa wanazidi kuingia.

    "Ina maana na Ester ana upeo wa kuhisi kama sisi?????haaa!!!"" hakuamini kabisa Michael baada ya kujuwa maneno Yale walikuwa wakiwasiliana Sara na Ester,hakujuwa mwanzo kama hisia zile hata Ester kwa sasa naye anazo hivyo ikimfanya awe na wasiwasi juu ya mpango wake akihisi anamuanza Sara kwakuwa ndiyo ana uwezo kumbe huenda hata Ester naye akawa na nguvu hizo,aliingia ndani na kuwa sambamba na wenzake lakini kichwani tayari kashachanyikiwa kwa kuhisi na yeye yaweza kuwa anawindwa maana sio rahisi tu MTU wa kawaida akawa na nguvu za kwao.Basi wakizidi kuingia ndani zaidi na kuonyeahwa mambo Yale waliyoambiwa kule nje kuhusu bawa LA ndege,picha ya Chui,mlango wa ndege wa abiria na vengine vingi ambavyo wanafunzi walipata kustaajabu baada ya kuona,huku Michael akizidi kuangalia mahala pa kuanza kazi yake,walipofika ndani ndani huku yule kiongozi akiwa mbele na lile chochi kubwa lililowafanya watu wote kuona vitu vya mule kwenye pango,Michael alitazama pembeni na kuanza kuwasiliana na wale wenzake aliowatuma yangu awali na kiwaamuru sasa waanze kazi yao kwa watu maalumu,kule nje nao wakiwa na kiongozi wao walianza taratibu kuingia akiwemi Sara huku akiwa nyuma Madam Magdalena,alipoingia tu Sara kwenye lile pango alisikia kelele za watu wakisikika wanalia tena kwa sauti kali hadi yeye mwenyewe akaogopa,aligeuka nyuma gafla na kumfanya hata Madam amshangae.

    "we ushaanza uoga wako hapa hata kuingia ndani hatujaingia unakodoa macho" alisema Madam Magdalena.

    "Madam...haisikii kelele za watu wakilia?" aliuliza Sara na kumfanya Madam atege sikio kusikiliza lakini wapi.

    "we unaumwa?kama una mashetani yako bora usiingie maana huko ndani ndio kuna mambo mengi ya kujifunza." alisema Madam baada ya kutosikia lolote.Sara aligeuka huku akiwa na mashaka na taratibu akapiga hata kuingia ndani,.

    Lile kundi la kwanza akiwemo Denis na Natasha walifika sehemu ambapo wakiongozwa na yule kiongozi,kulikuwa na mwamba uliochongwa na kuwa kama sofa,akaanza kuwaeleza jinsi ilivyotokea hadi kuwa vile,akiwa kwenye maelekezo hayo gafla tu tochi yake ikazima na kufanya eneo lile liwe giza totoro tena LA kutisha.

    "msiogope jamani humu ni salama tu tochi imezima gafla" alisema kiongozi huyo akiwatoa woga wanafunzi huku mapopo yakisikika kuruka ruka kwenye miamba,hata mwalimu Isack aliwatuliza wanafunzi wake huku akiwasha mwanga wa simu yake na kufanya upatikane mwanga japo sio sana,baada ya dakika kama mbili tochi kubwa lile LA kiongozi wa msafara likawaka na kufanya wanafunzi wawe na amani sana wakaendelea na kupata darasa juu ya lile sofa la mwamba.

    Kule kwa Sara bado zile kelele anazisikia tu baada ya kufahamu kuwa hakuna yeyote anayesikia sauti zile akajuwa kwa vyovyote vile Michael ameanza mambo yake,alijaribu kuongea na Ester na kuambiwa kuwa wapo salama na mwenzake Natasha.

    "Hebu piga macho hapo muangalie kama Michael yupo hapo" alisema Sara na kumfanya kweli Ester ageuke kuanza kumuangalia Michael,kila kona akipeleka macho wapi,Michael hakuonekana kwenye kundi lao,akabaki amedumwaa tu Ester huku Sara akimsubiria amueleze kulikoni.

    "Sara......" aliita Ester akiwa ameduwaa.

    "nini...."

    "Michael haonekani hapa...Yesu wangu!!!"alisema Ester akiwa haamini na kumfanya Sara aliyekuwa kule mwili umsisimke kwa kuambiwa vile,alivyozisikia sauti zile walipo kuwa wakiingia na sasa ameambiwa Michael haonekani aliona kwa vyovyote Denis na Natasha wapo matatizoni..





    Maneno ya Ester yalimfanya Sara aanze kumhisi Michael kuwa ni yeye ndio aliyofanya hivyo,alitazama wenzake wakiwa eneo fulani wakioneshwa baadhi ya vitu huku Madam Magdalena akiwa naye yupo bize akisikiliza maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na yule kiongozi,Sara alianza kurudi nyuma na kuwaacha wenzake wakiwa mbele,alipoona hakuna anaye muangalia akapotea gafla pale walipo.Alikuja kutokea pembeni kabisa na kundi la wakina Denis na kuanza kupiga macho kuwatafuta wakina Natasha na mwenzake Denis lakini cha ajabu hakuweza kuwaona,moyo ulimdunda kwa hofu kuona jambo hilo limekuwa zito,hakuwa anajua njia wala mapango yale yalivyo,lakini kwakuwa ni jambo ambalo linamhusu alijitolea kuwatafuta wenzake huku kwa mbali zikisikika sauti zile za watu ambao hawajulikani,alipotea pale alipo na kuanza kuwatafuta wakina Denis na Natasha kila kona ya pango lile huku akibadilika na kuwa na macho makali yaliyo kuwa yakimulika kila alipokwenda akiifuata ile sauti inaposikika,alipoikaribia ile sehemu hakuamimi alichokiona,Michael alikuwa amebadilika kabisa huku akiwa amemkamata Natasha shingoni akimmaliza na papo hapo mwili wa Natasha ukidondoka chini kama gunia la pumba huku mwili wa Denis ukionekana pale chini huku damu zikimtoka puani.Sara alichoka baada ya kuona vile,hasira zilimpanda pale alipo kwa kuona wenzake washauliwa ikiwa na maana Denis na Natasha tayari washarudishwa kule kwenye jamii hiyo ya Michael.Aligeuka nyuma baada ya kumaliza kazi hiyo Michael ma kumtazama Sara aliyeonekana haamini kwa kile kitu,akiwa kwenye hali hiyo alijikuta akizungukwa na watu wa Michael zaidi ya 20,Sara akabaki akizunguka tu akiuangalia umati ule na mwishowe akabaki kutazamana na Michael aliyeonekana kutabasamu kwa dharau.

    "unajisikiaje kwa hili tukio?hawapo... Washatangulia Denis na Matasha,

    huu ndio mwanzo tu wala usishangae,nilishakwambia ninakwenda kuwa mtu mkubwa siku ya Leo,umekuwa ukiniharibia Mambo yangu siku zote,umekuwa mpinzani wangu kila siku ukijaribu kuwatetea binadamu ambao napaswa kuwachukuwa ili Jambo langu litimie,nimesubiri sana lakini Leo ndio wakati muafaka wa Michael kupewa Utukufu wa kifalme,sidhani kama utakuwa na nguvu ya kunizuia hadi wakati huu maana wawili kati yao nishawachukuwa,wamebaki wawili wengine pamoja na WEWE MWENYEWE,niliapa nitakumaliza kwa mikono yangu mwenyewe maana hupaswi KUISHI kwenye ardhi ambayo nakwenda kuitawala maana najua tutakuwa mwema kwangu,....pole sana Sara"alisema Michael kwa kujiami I huku akitabasamu kwa Furaha,wakatokea watu wake na kumzukunguka Sara pale alipo tayari kwa kupambana naye,waliokuwa zaidi ya 20 huku Michael mwenyewe akiwa pembeni tu nakuangalia,alitazama ile miili ya Natasha na Denis iliyokuwa pale chini na kuanza kuisemesha maneno fulani huku Sara akianza kuonyeshana Ubavu na watu wale wa Michael.

    Michael aliiamuru miili Ile kurudi kule waliko kwenye Makundi yao japo kama vivuli tu lakini Denis na Natasha halisi amewachukuwa yeye na kiwakabidhi watu wake wawili wawarudishe kule kwenye Jamii yao wakiwasubiri na hawa wengi yaani Ester na Magreth,kazi iliyobaki sasa ni kuhakikisha wanammaliza Sara kwenye mapango mule mule.



    Sara mwenyewe alizidi kupambana na watu wale kwa kutumia nguvu za kichawi tu,alikuwa aimebadilika kabisa na kuwa kama Shetani huku akiunguruma kama simba lakini wale watu walizidi kuja tu japo walianza kupunguza taratibu na Sara kwa kutupiwa Uchawi Mwilini mwao.Hata wao walibahatika kumshambulia sehemu kadhaa za mwili wake,walizidi kumfuata hadi Sara mwenyewe akashangaa maana wamekuwa na nguvu zaidi ya vile alivyotegemea awali,naye akaziachia nguvu zake zote na kuendelea kupambana nao,akawa anaangalia tu kiongozi yule aliyekuwa anaongoza akiendelea kuwaelekeza wanafunzi mambo kadhaa ndani ya mapango yale, hakuwa kabisa anaelewa kinacho zungumzwa pale

    Huku kwa Ester muda wote alikuwa ana wasiwasi muda hana Amani baada ya kuhisi kuna tatizo huenda kimetokea mule mapangoni,akiwa kwenye hali hiyo huku akiwa na kitabu chake akianza kusikia kwa hisia sauti ya mtu anayemjuwa akisikika akipiga kelele za maumivu,akaanza kutega sikio vizuri na kuisikia sauti ile kwa makini na ilipojirudia tena akashtuka baada ya kuifahamu sauti Ile ni ya Sara akisikika kama amepatwa na tatizo Hali iliyomfanya Ester ashangae na papo hapo moyo ukaanza kumuenda mbio huku moyoni akimtaja Sara rafiki yake na gafla tu sauti ile akakisikia kwa nguvu mule mapangoni humu akizisikia sauti za watu wengine wakisadikika kama wanampiga mtu,alipoangalia kwa pembeni aliona mwanga kwa mbali uliokuwa ukionesha vivuli vya watu wakionekana kupambana,alijuwa Yule ni Sara akipambana na watu wale wa Michael,kwa moyo wa Upendo kwa rafiki yake Sara taratibu akaanza kupiga hatua bila kuonekana na Magreth na wanafunzi wenzake na kuanza kusogea pale alipoona vile vivuli vya watu wakipilingishana,kadri anavyosogea ndivyo anavyozidi kuisikia sauti zile.

    Huku akiwa amewaacha wenzake wakiendelea kuelimishwa na Yule kiongozi aliyeongoza kundi lao,akiwa anaendelea kuwaonesha wanafunzi vitu vilivyomo kwenye pango lile gafla tu lile tochi aliloshika likazimika na kufanya Giza nene litawale eneo lile huku wanafunzi wakibaki kushangaa,aliwatuliza kwa kuwaambia hakuna Jambo baya litakalotokea mule,na kweli baada ya dakika mbili tu lile tochi likawaka baada ya kuligonga gonga na kuwafanya wanafunzi waondoe wasiwasi wakiendelea kuelekezwa.

    Huku kwa Ester alizidi kumuata tu ule mwanga na alipoukaribia tu zike sauti zikazima na kuwa kimya,hata ule mwanga ukapotea gafla na kufanya Ile sehemu kuzidi kuwa giza totoro,akaanza kushangaa humu na kule bila ya kuona kitu chochote akisikika tu sauti za mapopo wakiruka ruka kwenye miamba ya pango lile. Kwa woga na wasiwasi akaanza kutetemeka huku akiitoa rozali yake ilikuwa shingoni mwake na kuishika tu huku akiomba asidhurike,akawa ameaimama tu hana pa kwenda maana haoni hata njia wala mwanga wowote pale alipo Simama na gafla tu akasikia kitu kizito kikituwa kichwani mwake na papo hapo akanikuta akipoteza nguvu na kudondoka hadi chini kama mzoga.



    Huku kwa Sara hali ilikiwa tete maana akianza kuchoka baada ya kuwamaliza wale viumbe lakini cha ajabu anaona wanazidi kuongezeka tu,alijikuta mwili wake unaanza kuuma kwenye baadhi ya sehemu alizojeruhiwa Jambo ambalo mwanzo halikuwahi kutokea,Hali Ile ilimfanya hata Michael atambue na kuona sasa ni wakati wa kufanya jambo lake alokusudia,taratibu sasa akaanza kusogea pale alipo kuwa Sara ambaye akiendelea kujitahidi kuwamaliza viumbe wale,alisogea Michael pale huku akiwa ameshika fimbo iliyokuwa ikitowa mwanga mkali na kuanza kuminyana na Sara ambaye alikuwa akikwepa tu fimbo ile ambayo Michael aliitumia kupambana na Sara.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Sara alijikuta akimshangaa sana Michael ambaye hakumdhania kama atakuwa vile,alionekana kuwa na nguvu za ziada huku nakutumia kila mbinu kuhakikisha anamuweza Sara,watu wa Michael wote wa wakasogea pembeni na kuwaachia uwanja watu wawili Sara na Michael.Kibaya ni kwamba Sara alikuwa ameshapambana na idadi kubwa ya watu wa Michael hadi kufika pale tayari ameshapoteza nguvu zake na ndivyo udhaifu huo aliutumia Michael baada ya kuona Sara ameahamxhosha hivyo yeye anakuja kukamilisha zima yake aliyoipanga.Na kweli haikuchuwa hata muda sana Sara akajikuta anashindwa hata kuendelea na kupambana huku jasho jingi likichanyika na damu zilizokuwa zikimchuruzika mwilini mwake na kufanya shatiblake aliolivaa lipoteze rangi yake halisi,taratibu akajikuta akidondoka chini kwa kupiga magoti huku mikono yake ikilowa damu kwa kuua viumbe waliotumwa na Michael,akabaki akimuangalia tu Michael aliyeonekana kutabasamu,alicheka sana na taratbu anaanza kumsogelea Sara pale alipopiga magoti,alipofika aliitoa ile fimbi yake na kuunyanyua uso wa Sara uliochakaa kwa damu na kuanza kumsikitikia.

    "ah ah ah ah ah ah.....mbina mmemuumiza kiasi hiki Malkia wangu jamani....eti Malkia Sara....nini kimekukuta jamaniii" alisema Michael kwa dhihaki na kucheka sana baada ya kuona jambo alilokuwa akilisubiria kwa muda mrefu linakwenda kukamilika,akiwa anaendekea kumtazama Sara kwa ile hali aliyonayo,aligeuka na kuwatazama watu wake.

    "mchukweni tuondoke naye,leo ndio siku ambayobnimekuwa nikiisubiri kwa muda mrefu,nataka niwaoneshe watu wa jamii yetu kwamba Mfalme wao habahatishi kwenye kitu kiamuwa,mbebeni" alisema Michael na watu wake wakasogea pale alipo Sara na kumnyanyua,wakaweka duara la pamoja na papo hapo wakapotea kimaajabu pamoja kuelekea kwenye jamii yao.

    Nje ya falme walijaa viumbe wa jamii ya wasuriati walio changanyika na jamii ya falme ile,ilikuwa ni siku ambayo walikiwa wakiisubiri kwa muda mrefu sana,siku ambayo inasadikika jamii hiyo inapata kiongozi mpya baada ya miaka mingi kupita bila ya kuongozwa na Mfalme ama Malkia wa jamii hiyo,tangu kufariki kwa Malkia Aznaty na yule aliyesadikika kuwa ni Mfalme kufukuzwa kwenye madaraka hakukutokea mtu mwengine aliyediriki kukalia kiti kimoja wapo.

    Wasuriati walukuwa na furaha sana baada ya kupata taarifa ya kijana wao Michael kukamilisha zoezi ambalo alikuwa akisubiriwa kulimaliza ili aje kuitawala ardhi yote ya jamii yao,huku upande mwengine ile jamii iliyokuwa ikitawaliwa Malkia Aznaty wakawa nao wanafurahi kwa kuona bora aje kiongozi awatawale maana tangu kuondoka kwa utawala wa mwanzo hakukuendelea jambo la maana lolote kwenye ardhi yao.Wakiwa wanaendelea kusubiria kuona kiongozi mpya aweze kufika wazee ambao walikuwa muda wote wakiilinda falme ile walisimama mbele ya jukwaa kubwa sana lililoandaliwa na walianza kuwapa imani maelfu ya watu waliohudhuria eneo lile kuwa muda si mrefu kiongozi wao atakuwa amewasili pale,na ndio wazee hao waliokuwa wakishirikiana na wasuriati kuhakikisha wanampa nafasi kijana Michael kuwa kwenye kiti kile cha Mfalme,na kweli sekunde kadhaa mbele wakatokea watu wa Michael kama sita pale mbele ya jukwaa wakiwa wamemshika Sara aliyekuwa hoi ajielewi,watu wote walikaa kimya baada ya kuona vile,na papo hapo akatokea Michael mwenyewe kimaajabu na kuwafanya jamii yote imshangilie kwa furaha baada ya kujuwa kuwa yule ndio Mfalme mtarajiwa,hata yeye mwenyewe hakuamini kuona halaiki ya watu waliokuwepo pale wakimsubiria yeye kwa heshima wazee walinyanyuka na kumpa heahima yake kama kiongozi wako na kuwafanya watu waoote waliokuwa eneo lile wainame kwa kumpa heshima Michael,alifurahi sana maana ndio kitu pekee alichokitaka kwa miaka yote hiyo akisubiri kupata heshima kama hiyo,alisogelewa na mzee mmoja kwa tabasamu akiwa ameishika ile kofia ya heshima ya Mfalme,na taratibu Michael akainama kisha yule mzee akamvalisha ile kofia ya ufalme Michael na kuwafanya watu waliohudhuria pale wote washangile japo kuna baadhi yao walikuwa hawawapendi wasuriati na kubaki kunyamaza tu wakishuhudia mambo yanavyoenda.



    Lililetwa vazi la Mfalme ambalo lilimuenea Michael baada ya kuvalishwa mbele ya umati wa watu kisha akakaribushwa kwenye kiti cha ufalme kilichokuwa mbele yake,alikitazama hukubakioneaha furaha aliyonayo na taratibu akaanza kukisogelea na kukishika huku akikizunguka kama mata tatu hivi kisha akakilia na kuwafanya watu woote waende chini kwa kisujudu kama heshima kwa Mfalme hiyo mpya.Alijisikia furaha sana Michael baada ya ndoto yake kutimiasiku zote alikiwa akiwaza jinsi ya kuwa mtu mkubwa na leo amekiwa Mfalme kweli,aliwaamuru watu wanyanyuke na wakakaa kimya kumsikiliza.

    Naamini kila mmoja wenu anafahamu kinachoendelea hapa kwa sasa,mimi ndio Mfalme kwa sasa na nyie ndio watu wangu,kwenye harakati za kupigania ufalme huu nimepitia changamoto nyingi sana hasa kuwapoyeza watu muhimu sana akiwemo baba tangu mzazi ambaye ndio alikuwa Mfalme hapa akiongozana na Malkia Aznaty ambaye alileta uvutani kutaka kupindua mila na desturi za jamii yetu,hakuna asiyefahamu kwamba hairuhusiwi kuwa na uhusiano wa kimapenzi au wowote ule na binadamu wa kawaida,lakini Malkia Aznaty alivunja sheria hiyo na kudiriki kuzaa kabisa na binadamu kisha mtoto hiyo akampa uwezo mkubwa tu kama alivyo yeye ili aweze kutupindua sisi na kuja kuitawala ardhi hii alete sheria mbovu za duniani,na mtoto wake hiyo ndio aliyekuwa akileta changamoto nyingi na ndio aliyemuuwa Mfalme wenu ambaye ni baba yangu"alisema Michael mbele ya watu na kuwafanya watambue kwamba kumbe Mfalme wao aliuliza na mtoto wa Malkia Aznaty,walikasrika sana kwa tukio hill.

    "hivyo basi mimi kama Mfalme wa sasa nimefanikiwa kumdhibiti binti huyo anayeitwa Sara na hadi sasa ninavyoongea tunaye tumemdhibiti,na ili niwahakikishie ufalme wangu ulivyojiandaa kuwa makini nitamleta hapa mbele yenu mseme wenyewe tumpatie adhabu gani wakiwemo na wenzake ambao walizaliwa kwa kuchanganya asili yetu na binadamu." alisema Michael na kuwaamuru watu watu wake wawalete Denis,Magreth,Natasha na Sara pale wakiwa wamefungwa kamba mikononi.

    Na kweli baada ya dakika kadhaa waliletwa pale mbele huku Sara akisukumizwa na kuangukia miguuni mwa Michael pale alipokaa kwenye kiti,Denis na wenzake wakawa wanashangaa tu sehemu ile walipo maana hawajawahi kufika eneo lile.Muda huo huo Ester naye ndio alikuwa akiletwa na watu wa Michael wakitokea kule mapangoni na kumuweka sehemu,alishangaa kuona umati wa watu eneo lile ambalo hakuweza kuelewa ni wapi,lipotazama pembeni aliwashuhudia wenzake Denis,Magreth na Natasha wakiwa wamefungwa kamba mikononi kama yeye,alipotazama kwa mbele alimuona Michael amekaa kwenye kiti cha kifalme huku akiwa amemkanyaga Sara ambaye alikuwa hajitambui kwa kipigo alichopigwa na watu wa Michael ambaye aliamuru awalete pale mbele ya halaiki ya watu ili awauwe iwe ni onyo kwa jamii hiyo kujenga mahusiano na binadamu.

    Muda huohuo alikuja mwanadada mmoja akiwa na sahani ya dhahabu iliyokuwa imebeba kisu kikali sana na kumkabidha Michael ambaye alipo kipokea tu akanyanyuka na kumfuata Sara,kwa sura ya kikatili Michael alinyanyua kisu kile akimuelekezea Sara aliyekuwa akikitazama tu kile kisu bila kufanya lolote,hapo ndipo Ester akaikumbuka ile ndoto aliyoiota siku mbili na kufahamu jambo linalokwenda kutokea ni Sara kuchomwa kile kisu,akajikuta akianza kupata ujasiri moyoni mwake kuna roho inamsukuma kufanya kitu ambacho hakuwa na uhakija nacho,alipokikumbuka kile kitabu alichokuwa akikisoma siku zote,hapo ndipo akajuwa kuwa huenda kile kitabu ndio ikawa njia pekee ya msaada kwa siku hiyo,alipiga hatua mbili mbele huku mikono yake ikiwa imefungwa kamba,akafumba macho na alipofumbua gafla tu macho yake yalibadilika na kuwa makali kama jini yakitowa mwanga mkali sana hadi watu waliokuwa eneo lile kuanza kushangaa wakimnyooshea kidole Ester akiwa kwenye hali ile,Michael akiwa amenyanyua kile kisu alishangaa kuona watu wanashangaa,alipogeuza macho hata yeye hakuamini kumuona Ester akiwa kwenye hali ile,Ester akazidi kusogea mbele na kuwafanya hata wakiwa Denis,Natasha na Magreth wamshangae maana hawakuwahi kuona Ester akiwa kwenye hali ile,Ester akawatazamaule umati wa watu waliokuwa pale wakimuangalia maana hawaamini kama binadamu anaweza kuwa kama wao.

    "O,popor..cu sigurantâ câ nu esti privind proasta gestionare conducerea sclavie,clase de conducere între om si Jinn afirmâ câ fiecare creaturâ are dreptul de a trâi si de a iubi aerul asa cum se simte din inimâ.Traditiile si obiceiurile acestui teren despre unul dintre lagârele si a societâtii umane se presupune cà nu este permis abuzul,fiecare dintre noi are dreptul de a iubi.Spun toate astea reginà Aznaty Sheraan....m-am dus la corpul fetei pentru a aràata cá,chiar si o fiintâ umanâ are dreptul de a locui cu noi de a iubi si a pãcii.Ïncepànd de astãzi,începând permiteti-mi sã obtine un lider aun este cel care iubeste pacea între cele douã párti,nu omor si caracteristicile acestui regat sunt dintr-un clan numai,acestea sunt familiare Sheeran.(Enyi watu.,hakika mpo kwenye uongozi mbovu,uongozi wa utumwa,uongozi wa matabaka baina ya watu na jamii yenu hali ya kuwa kila kiumbe ana haki ya kuishi na kumpenda yeyote vile anavyojisikia kutoka moyoni.Mila na desturi za ardhi hii kuhusu mtu wa jamiii hii kuwa na mahusiano na binadamu eti hairuhusiwi ni unyanyasaji kila mmoja wetu ana haki ya kupenda,nasema hayo.Nasema hayo Mimi kama Malkia Aznaty Sheeran.....na mtashangaa kwa kuona naongea nikiwa kwenye mwili wa huyu binti hii ni kuonyesha hata binadamu ana uwezo na ana nafasi ya kuishi na sisi kwa upendo na kwa amani.Kuanza Leo na kuendelea naomba kila mmoja aelewe hilo na hii ndio sheria ambayo nimeiacha kama Malkia,kiongozi niliyekuwepo madarakani kipindi cha nyuma na naamini mwanangu Sara atakuja kuwaongoza vema maana nimemkabidhi vitu vyote ambayo Malkia anapaswa kuwa navyo,nafahamu amepitia tabu nyingi lakini ndivyo ilivyopangwa kwa kiongozi yoyote anayetawala jamii hii....na daima ukoo wa Sheeran ndio utakaoongoza siku zote Kama ilivyomiwa enzi za mababu na mababu huku nyuma,kwa maneno haya naomba niwakabidhi kiongozi ambaye ataleta furaha ya awali na si mauaji wala matabaka,kuanzia sasa kila mmoja wenu ana haki ya kwenda kokote aendako na ana haki ya kupenda popote apendapo....SARA NDIO MALKIA WENU"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    aliyatamka maneno hayo Ester na kuwafanya watu wote walio kuwepo pale wabaki kimya wakishangaa,hata Michael na jopo la wazee wote walibaki midomo wazi kwa maneno ambayo Ester ameyatamka,haikuwahi kutokea hata siku moja tokea karne na karne kwa mtu au binadamu kuyatamka maneno hayo kwa ufasaha wa hali ya juu.Ni maneno ambayo yalisadikika kuandikwa kweli na Malkia Aznaty kabla ya kifo chake,ilisadikika hapo nyuma Malkia huyo aliwakusanya watu wote wa jamii hiyo na kuwaeleza kuwa ameshaandika sheria yake hivyo anangoja tu siku za kutokea madarakani ili sheria hiyo ifuatwe,watu walimpenda sana kutokana na ukarimu na ukaribu kwa jamii na baada ya kuona wasuriati wameanza kuweka ukaribu sana na baba yake Mfalme Sheeran na kuhisi kuna siku ufalme wao utakuja kupinduliwa hivyo aliandika kitabu cha sheria ambayo kila kiongozi anayetoka madarakani lazima aache sheria yake na ni lazima kuifuata na itaendelea kutumika hadi kiongozi mwengine atakapoachia madaraka na yeye ataacha sheria yake na ni sheria moja tu ambayo haikupaswa ivunjwe ambayo ndio hiyo ya kutokuwa na ukaribu na binadamu yeyoye.Hivyo kuja kwa wasuriati wakishirikiana na wazee ambao walikuwa wakimtumikia Mfalme Sheeran enzi za jamii hadi wake hadi kuja kuuacha uongozi huo kwa mwanaye Aznaty kumbe walikuwa ni wasaliti siku zote wakawa wanatoa siri na namna ya kumuingia Mfalme Sheeran lengo hasa ni kutaka kupata kabisa uongozi wa kurithi kwa falme hiyo na wasuriati wawe wanaitawala ardhi hiyo kwa kuwa wanaogopeka sana kwa kuwa na nguvu za kichawi sana maana wao walikuwa wakimhofia Malkia Aznaty tu ndiye aliyekuwa jeuri yao lakini baada ya kumuwekea sumu kwenye vyakula hawakuwa na sababu ya kumuogopa mtu yeyote ndio maana wakaitaka falme kwa nguvu zote.Kila mtu maneno yale yalimuingia moyoni na kuona kuna haja kweli ya kubadili desturi za pale,hawakuona haja tena ya kuweka matabaka baina ya binadamu na jamii yao.Denis,Natasha pamoja na Magreth walibaki kumshangaa tu Ester kwa namna alivyoiongea lugha ile ambayo wao hawakuweza kufahamu zaidi ya kuona watu wa jamii ile wakionesha kushangaa tu huku wengine wakitikisa kichwa kuoneaha maneno yale yamewaingia,watu wote walimtazama Michael aliyekuwa amekishikia tu kisu kile baada ya kukumbwa na tahaluki baada ya kumuona Ester ambaye hakumtegemea wala kumdhahini kama anaweza akaja kuongea lugha ambayo binadamu wa kawaida hawezi kuitamka hata iweje,aligeuka kiwatazama watu wa jamii yao waliojaa eneo lile wakionesha sura za kukasirishwa na kitendo ambacho Michael anataka kukifanya,alivyoona kuwa watu wameanza kuingiwa na moyo wa huruma baada ya kuelewa maneno aliyosema Ester akaona amuue kabisa Sara anayepaswa kuwa ndio Malkia ili lengo litimie watawale kimabavu,alinyanyua kile kisu kwa hasira na kupeleka tumboni kwa Sara lakini gafla ukatokea mkono wa mtu uliyozuia kisu kile ambacho kilishaanza kidogo sana kuingia tumboni mwa Sara aliyekuwa hoi pale chini.



    Michael alishangaa kuona mkono wake ulioshika kisu kikali umezuiwa kutua tumboni mwa Sara aligruka kuangalia aliyemzuia,alihamaki kumuona Denis akiwa anamuangalia kwa macho makali sana yaliyotisha,hali iliyomfanya Michael azidi kushangaa maajabu hayo.

    "hata siku moja haiwezi kutokea,utuulie Malkia wetu angali sisi tunakutazama!hapana inatosha sasa" alisema Denis kwa ujasiri wa hali ya juu na kumsukuma huko Michael na kisu kikadondokea miguuni mwa Ester,Michael pamoja na jopo lote la wazee pamoja na wasuriati wakuu walibaki kushangaa hali ile namna inavyoenda,wakaona sasa mambo yanataka kwenda kuharibika wakati walikuwa wanamalizia kumtangaza Mfalme mpya,huku kwa mbali makelele ya watu wakianza kuamini maneno yale ya Ester na kuanza kuamini kuwa yawezekana Sara ndiye akawa kiongozi wa Taifa lao,zikaanza kusikika kelele zikimtaka Sara ndio awe Malkia wao na si vingine,kelele zile zikasambaa kote na wote sasa wakawa wanasema kwa pamoja.

    "UTUKUZWE UKOO WA SHEERAN,ATUKUZWE MALKIA SARAAA........ATUKUZWE MALKIA SARAA" zikawa ni kelele eneo lile sasa na wote wakawa wakisema kwa pamoja na kuwafanya jamii ya wasuriati waone aibu sasa kule waliko changanyika na wenzao wakiwa wameshajipa nafasi ya MTU wao Michael kukabidhiwa madaraka ya kifalme siku hiyo.

    walibaki Wazee nao wakawa hawaamini kwa kuona imekiwa gafla tu mambo yamebadili na kubaki wakiangaliana na kutafakari namna ya kufanya ili kumaliza mzozo ule,wote wakamuangalia Michael ambaye ndio ana maamuzi ya mwisho,akageuka kumtazama Sara pale chini na kuona yule ndio kila kitu na ndio anayeleta vikwazo akiwa hai ni bora afe,aliachia vidole vyake vyote vikawa vinaangalia chini huku ukionekana mvuke wa ajabu kiganjani make kana kwamba kuna nguvu anaivuta kutokea ardhini,hali ile Ester aliiona na kuona Sara yu matatizoni,akaanza kukimbia haraka sana kusogea pale alipo Sara chini akiwa na Denis ambaye alikuwa amemshika akitaka kumnyanyu bila kujuwa kinachoendelea,Michael aliandaa shambulizi lake na alipohakikisha limekaa sawiya alinyanyuwa mkono ule kwa nguvu zote na na kuuachia ule mkono uchawi uliyonyooka kuelekea alipo Sara lakini haraka na upesi Ester akafika alipokuwa Sara na Denis akawazuia kwa kukinga mgongo wake na papo hapo ule uchawi uliotupwa kwa nguvu zote na Michael alimkusudia Sara ukapenya mwilini mwa Ester ambaye alijukuta akitapika damu nzito zilizo mdondokea Sara pale chini na kufanya watu woote waliokuwepo eneo lile wanyamaze kimya baada kushudia tukio lile kwa macho yao Michael akifanya jambo lile,Natasha pamoja na Magreth wakabaki khamaki baada ya kumuona rafiki yao Ester mgongoni anaanza kutokea na damu huku mdomoni zikizidi kumtiririka,Denis aliyekuwa amemshika Sara pale chini hakuamini kabisa kushuhudia taratibu Ester akienda chini na kumdondokea Sara pale alipolala,Ester akawa anamuangalia Sara huku chozi likimdondoka kuchanganyika na damu zilizaza kusambaa eneo lile,haraka Magreth na Natasha wakaanza kukimbia kusogea eneo lile alipodondokea Ester aliyekuwa akiunyanyua mkono wake uliotapakaa damu na kumshikika Sara shavuni.....kitendo cha kuguswa damu ya Ester kilimfanya Sara aanze kupata kurejesha kumbukumbu zake zote tokea anaanza kuingia shuleni kule hadi kujuana na Ester pamoja na wengine,gafla likaja tukio la muda mchache tu wakiwa mapangoni na kuona jinsi alivyokiwa akipambana na wasuriati vijana wakiongozwa na Michael kwa lengo la kumuua......alifumbua macho gafla na muda huo huo Ester taratibu alianza kupoteza nuru macho ni mwake,giza likamtanda machoni na papo hapo macho yake yakafumba huku mapigo ya moyo yakisimama kuashiria safari yake imeishia pale.

    Sara alinyanyuka gafla na macho yake yakaelekea kwa Ester ambaye alionekana kuanza kupoa.

    "Ester....Ester......ESTERRRRRRR AMKA BWANA......ESTER AMKAAAAAAAAAA AHHHHHH" alijikuta akianza kumsogelea Ester na kuanza kumtikisa kujaribu kumuamsha swahiba wake Ester,Denis kuona vile alichoka gafla na kujikuta akikaa kabisa chini huku akihamaki,Natasha na Magreth wakaanza kuungana na Sara kumtikiza Ester aliyekuwa pale chini tayari mwili ushatengana na roho.Hali ile iliwafanya wananchi wote waliokuwa eneo lile waanze kuwa na moyo wa ubinadamu wa huruma baada ya kutokea tukio lile,hali ile iliwafanya Michael pamoja na wazee waliokuwa wakishirikiana naye kutahamaki baada ya kuona SARA AMEAMKA TENA UPYA,wakajikuta wakimeza tu mate ya wasiwasi hawajui nini kitatokea.

    Sara alilia sana lakini haikusaidia kitu,akanyanyuka kusimama na kugeuka kuwaangalia wananchi wa jamii ile wakiwa wametulia kimya wakimuangalia.

    "NANI AMEMUUA ESTER WANGU......NAULIZA NANI...." alisema Sara na gafla sura yake ikabadilika kwa hasira huku macho yakionekana kuwa makali,wazee waliokuwa wakimjuwa vizuri Malkia Aznaty waliogopa sana kuona hali ile aliyonayo Sara waliwahi kuiona kwa mama yake Malkia Aznaty na kufahamu kuwa kinachofuata hapo ni kifo tu....mmoja wao akanyoosha kidole kumuoneshea Michael kuwa ndiye aliyefanya tukio lile,mwengine naye akanyoosha kidole kukielekeza kwa Michael,wakafuata wengine na mwengine likawa kundi kubwa likimuelekezea vidole Michael aliyebaki kushangaa,wazee waliokuwa wakishirikiana naye baada ya kuona vile wakajuwa wazi kwamba Sara amepandwa na hasira za mama yake ambaye wanamuogopa kupita maelezo,walimshika Michael mkono.

    "tunakuomba sana tena sana....ondoka hapa haraka....huyo hapo sio Sara tena ni nguvu za Malkia Aznaty Sheeran mama yake,hakuna anayeweza kumuweza kwa nguvu za kichawi hata kidogo,tafadhari ondoka haraka sana" alisema Mzee mmoja na kumfanya Michael atazame pembeni huku akiwa amechukia kupita maelezo.Sara baada ya kuona watu wote wakinyoosha vidole vyao nyuma yake ikambidi ageuke kuangalia ni nani huyo alifanya mauwaji hayo,alupotazama aligongana macho kwa macho na Michael ambaye alipomuona Sara usoni alishangaa,alikuwa ni zaidi ya jini tena mweupe huku damu ikimtoka taratibu mdomoni,akaanza kupiga hata kumsogelea Michael huku akisindikizwa na makelele ya watu wakimuhimiza amuuwe Michael pale pale maana washamkataa mazima kwa matendo ya kinyama aliyoyaonesha pale mbele ya watu,angali wao walishaanza kuona umuhimu wa kuwa na kuishi kama wanavyoishi binadamu.

    Na kweli Michael alivyoona anakaribiwa akaamuwa kuondoka kwa kupotea kimiujiza na kuwafanya watu washange huku wakibaki wazee wengine na watu wa kisuriati,walishindwa kuvumilia watu na kuanza kupanda pale juu walipo wale wazee kutaka kuwatia adabu,ikawa ni vurumai eneo lile huku wengine wakiwageukiwa watu wa suriati na kuanza kupambana nao wakionekana ndio lao moja kutaka kuitawala falme hiyo kwa maslahi yao wenyewe,hasira hizo ziliwafanya hata wakina Natasha na Magreth kuungana na wenzao kuwashambulia wasuriati,muda wote huo Sara alibaki kuwaangalia tu wakipambana akionekana kuna kitu,alisogea kwa Magreth aliyekuwa amekamata gongo akiendelea kupambana na watu wale,Sara alimkamata mkono na kubaki kumuangali.

    "eti wewe....yule aliueoneshwa kidole akapotea gafla NI NANI?" aliuliza Sara na kumfanya Magreth aache kwanza kupambana amtazame Sara usoni,alimuangalia sana akawa hamuelewi.

    "we Sara...ina maana humjuwi Michael wewe?kijana ambaye ametusumbia siku zote hizo hadi leo tupo hata ni kwaajili yake,Michael ndio muuaji,amemuua Ester yule pale" alisema Magreth na kumfanya Sara abaki kumuangalia Ester.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "MICHAEL......MICHAEL NDIO NANI.....?"alisema Sara na kumfanya Magreth as hang a, alichoka kabisa baada ya kusikia maneno ya Sara akionesha hamjuwi Michael,kiukweli tangu Sara apigwe na watu wa Michael kwa kumchangia kiasi kile hakika hadi kupoteza fahamu na kumfanya apoteze kumbukumbu ya mambo yote yaliyopita,ni Ester pekee tu ndio MTU pekee anayemkumbuka.Hadi hapo anaongea na Magreth lakini hamfahamu ni nani,alitazama pembeni na kuuona mwili wa Ester ukiwa magotini mwa Denis,alianza kutokwa na machozi huku akimfuata Ester pale alipo na kumfanya Magreth abaki akimtazama tu haamini anachokiona kwa Sara,alitoka na kwenda kwa Natasha kumueleza hali ya Sara kwa sasa na wakaanza kusogea pale alipo Ester akiwa na Sara aliyekuwa akimlilia,Magreth alimchukuwa Denis na kumpeleka pembeni na kuanza kumueleza kuhusu yaliyomkuta Sara,wote watatu wakabaki wakimtazama tu Sara akiwa analia tu pale kwa Ester Basi baadae baada ya vulumai kuanza kutulia huku baadhi ya wasiriati waliokuwa na nguvu zao za ajabu waliondoka kwa kupotea kabisa eneo lile huku wengine wakishiliwa na wananchi wa ardhi hiyo baada ya kuelewa kuwa wasuriati hawana nia nzuri na taifa laoTaratibu baadhi ya viongozi waliokuwa kwenye falme hiyo tangu kipindi kile cha Malkia Aznaty wakintii na kumheshimu waliwakaribisha Denis pamoja na wenzake huku mwili wa Ester pamoja na Sara wakapelekwa kwenye chumba maalumu ambapo wanafanyia maombi yao.Taarifa za kutojitambua kwa Sara zikaanza kuenea ndani ya falme hiyo kwa wafanyakazi wote waliokuwa mule ndani kwa siku zote wakiusubiri uongozi mpya wautii,siku hiyo hiyo waliwaeleza watu wote wa taifa hiyo kwa kuwaambia hali ya Malkia mpya sio nzuri hivyo waliwaomba kwa pamoja kuhidhuria kwenye maombi maalumu ya kuiomba miungu ya kwao ili Sara aweze kisaidiwa na kurudi kwenye hali yake ya awali.Basi muda ulipofika watu wengi walihudhuria kwenye maombi hapo yakiongozwa na waganga wao waliokuwa wakiiheshimu falme ile na muda mchache maombi yalianza.

    Hakika hakutaka kabisa akubali kushindwa kirahisi kwa maana alishajitolea kabisa kutetea nafasi hiyo hivyo haikuwa rahisi kumuachia Sara aiongoze falme ile kirahisi,aliingia ndani na kuvaa nguo zake kisha akatoweka kimaajabu bila wenzake kufahamu.

    Usiku ule walionekana idadi kubwa ya watu wakiwa mahala fulani wakiongea mambo,kila mtu akiwa anajibizana na mwenzake na muda huo huo akatokea Michael mbele yao na kuwafanya watu wote wanayamaze kimya.

    Michael aliwatazama na kuona kila mmoja anaangalia kwa chini.

    "vipi kuna jambo linaendelea hapa?" aliuliza Michael akisubiri majibu,wote walinyamaza tu kimya wajihofia kuongea ila mzee mmoja tu alisimama na kumtazama Michael.

    "Michael....sisi sote unaotuona hapa tunakusikiliza wewe kama kiongozi wetu,wewe ndio Mfalme wasuriati woote na tunakuheshimu kwa cheo chako,tumekuwa wote kuhakikisha unapiga hatua ya mbele hadi kuimiliki Falme juu ambayo kwa ushirikiano wetu tukafanikiwa kuichukuwa Falme ile na hata nguo za kifalme ukavakishwa lakini kukatokea ya kutokea pale mambo yote yakaharibika.Sasa basi...tumepokea taarifa kuwa wananchi wote,kiongozi ,wafanyakazi wa falme ile wamekubaki kuungana na Sara pamoja na wenzake kuhakikisha upendo bila ya kuleta matabaka baina ya waliozaliwa kibinafamu na wao wenyewe,na kwakuwa wana watu wengi tumeona ni bora UWAACHIE TU FALME YAO,haina haja ya kusumbuana nao ukizingatia nguvu za Malkia Aznaty zinazunguka tu eneno lile hatutawaweza walw ,tuanzishe makazi mapya na wewe ndio utakuwa Mfalme wetu kwa siku zote" alisema yule mzee na kuwafanya wenzake wengine wamuunge mkono kwa Yale aliyoyasema,Michael akabaki kuwatazama tu,alianza kuangua kucheko cha muda mrefu hadi wasuriati waliokuwa pale washangae,baadae alinyamaza na kuwatazama.

    "hivi mnafahamu ni ndugu zetu wangapi wameuliwa kwa ajili ya kuhakikisha tunaichukuwa falme ile na inakuwa chini ya wasuriati?hivi mmewahi hata siku moja kufikiria kwamba mmempoteza Mfalme wenu ambaye ni baba yangu,amekufa kuhakikisha Mimi nawaongoza nyie kupata nafasi ya kuwa Mfalme ili tuwe na jina kubwa?muda tuliyoutumia miaka na miaka kuhakikisha tunapindua Koo ya Sheeran kuongoza falme ile,aliyebaki kwenye koo ile ni yule binti Sara,tena ni binti tutashindwaje sisi jamani wanaume kwa ajili ya binti mmoja ndio turudi nyuma tuiache Falme aiongoze yeye,kwanza hana haki ya kushika nyazfa ile,nyie kama mmeshindwa ni nyie lakini Mimi bado na ninao uhakika wa kurudi tena kwenye falme ile na nikawa Mfalme kwa vyovyote vile,na eleqeni nafafanya haya yote kwaajili ya wasuriati tupate kuiongoza falme na si vingine,Mimi najua tumekuja hapa kuangalia namna ya kuingia tena kwenye ufalme tuwapindue wale watu kumbe ndio mmekata tamaa ya kupata ufalme wenyewe,dah dah dah...sasa kama nyie wakubwa wa umri kwangu mmeogopa hivyo na kukata tamaa mnaleta taswira gani sasa kwa vijana wenu?kama nguvu tunazo,nini sasa turudi nyuma kwa ajili ya MTU mmoja?Mimi naamini tunashinda safari hii na kupata uahindi mkubwa tu"alisema Michael kwa kujiamini akiwasisitiza wenzake ambao walikuwa wamekata tamaa,kwa maneno yale ya Michael yaliwafanya waanze kukumbuka kweli wamepoteza wenzao wengi waliojitolea kwenye jambo hilo,kitendo cha kukata tamaani kama kuwasaliti wenzao,walinyanyuka na kuungana na Michael kwa pamoja wakala kiapo cha kurudi tena kwenye Falme kuleta mapinduzi.Michael alifurahi sana kuona sasa ana nguvu ya watu wa kufanya kazi,walikaa kidogo wakaanza kusuka upya mipango yao namna ya kuanza kazi rasmi.



    Asubuhi kulipokucha wanafunzi walikuwa tayari kwa ajiri ya safari baada ya kupata kifungua kinywa,safari ikaanza moja kwa moja kuelekea kwenye hifadhi ya mbuga ya Saadan ,wanafunzi walishudia na kuona wanyama mbalimbali waliokuwa kwenye mbuga hiyo,walifurahi sana siku hiyo maana asilimia kubwa ya wanafunzi hawakuwahi kuona na na wanyama wakubwa kama tembo na wanyama wengine hivyo siku hiyo ikawa ni furaha kwako na kuweka historia katika maisha yao,walizunguka sehemu nyingi hata kwenda fukweni mwa bahari wakaoga maji kwa furaha ya siku hiyo ya mwisho ya safari yao,siku hiyo baada ya kumaliza sehemu zote walizopaswa kwenda walirudi mahala waliweka makazi yao mapema na kuanza kuandaa mizigo yako kwaajili ya safari kurudi mkoani Mara,waliwashkuru sana wale walimu waliowapokea kwa ukarimu na kushirikiana nao siku zote hadi siku hiyo ya mwisho wakitaka kuondoka.

    Hatimayesiku ya safari ilipowadia kila mwanafunzi alikiwa ameshajiandaa kwa ajili ya safari, usafiri ulikuwa tayari na kila wanafunzi aliambiwa akakae kwenye siti kama walivyokuja, hi hiyo iliyomfanya Sara amtazame Michael wakiwa chini, taratibu wanafunzi walianza kupanda kwenye magari na safari ikaanza sasa kurudi makwao baada ya kumaliza Tour yao ya siku kadhaa mkoani Tanga. Njiani Michael alikuwa akitazama tu pembeni hataki kabisa kumuangalia Sara kwa yale yaliyo tokea nyuma.Alitamanu kukaa mahala pengine lakini ilikuwa ni kama sheria vile mlivyokuna ndio hivyo mnavyo ondoka,Sara alibaki kutabasamu tu baada ya kuona kile alichokitafuta kwa muda mrefu sasa amekipata,alikumbuka siku ile alipoingizwa kwenye maombi na Ester wakawa wanaombewa huku Ester akiwa kama amekufa,hata yeye alimuwa hajitambui maana alipoteza kabisa kumbukumbu.

    Basi maombi ya nguvu yalifanyika siku ile baada ya muda Sara akapata kunyanyuka akiwa sasa anajitambua na kushangaa kumuona Ester akiwa amelala eneo lile akionekana kabisa kutohema wala kupumua,alijikuta amipata wasiwasi sana baada ya kumsogelea ndipo wale wazee walio kuwa wakifanya maombi yale wakamueleza gali halisi ilivyo kuwa,maneno yao yalimfanya sasa Sara atambue yote yaliyotokea akiwa hajielewi,alimsogelea Ester pale alipo kisha wakafuata wale wazee ,alipeleka mkono wake kwenye paji la uso la Ester na kufumba macho huku akianza kusema maneno fulani,nao wale wazee wakawa wanamshika Sara kichwani wakizidi muomba sana na kuchumuwa kama dakika Ishirini hivi kwa zoezi hilo kukamilika na hatimaye Ester akanyanyuka akiwa mzima wa afya,hata yeye alishangaa kuona yupo kwenye mandhari yale lakini kumuona Sara eneo lile alijisikia amani,baadae Sara akapata kumueleza kila kitu kuhusu mambo yalivyo tokea na kumweleza Ester kuwa kuna nguvu nyingi sana za Sara mwenyewe alipata kuziweka mwilini mwa Ester bila yeye kufahamu akijuwa fika kuna kipindi wasuriati watamzidi nguvu hivyo ni bora kuhifadhi uwezo wake mahala ambapo ndio kwa Ester na leo hii amezirudiaba rasmi kwake kuonesha asasa amekuwa Sara yule wa mwanzo humu akilini akiweka azma kuwa lazima amuue Michael pamoja na wenzake kwa namna yeyote ile huku akiweka mbele kisasi cha mama yake mzazi marehemu Malkia Aznaty.

    Yote hayo alikuwa akikumbuka Sara akiwa kwenye gari wakirudi Mara na kubaki kutabasamu,tabasamu la kutengeneza lenye chuki,hasira na kisasi ndani yake.



    Siku ya Jumatano asubuhi,baada ya viongozi wa shule wakishirikiana na walimu kubamimisha mazingira ya shule yamekaa kwenyesehemu nzuri yenye kuvutia kwa usafi,kengele iligongwa na muda mchache tu wanafunzi wakaanza kuelekea paredi kusikiliza kinachoendelea,Mwalimu mkuu Malamba alisogea pale na kisimama mbele ya wanafunzi wake ambao walikaa kimya kumsikiliza mwalimu.

    "Ok sina mengi saana ya kuongea kwa sasa ila nimekuja tu kueapa taarica kwambaaa....wale wenzetu walio elekea mkoani Tanga kwa Field basi tayari wameshaingia Mara na baadae tutawaona wakiwasiri hapa shuleni kama kituo ambacho ndicho walichoanzia safari yao,naa kupitia hao wenzenu mtapata kuuliza uliza kidogo walau wawaeleze uzuri wa kwenda Tour kwenye mikoa nje ya hapa tulupo,nadhani wakiwaeleza walichokipata wao huko basi hata nyie ambao hammupata nafasi ya kwenda naamini mwakani tutaenda,basi niwatakie masomo mema na nkae mtulie madarasani maana mitihani si mida mrefu itaanza shuleni hapa...kaeni mjisomee"alisema Mwalimu mkuu na baada ya hayo akaelekea zake ofisini kwake akiwaacha walimu wakimalizia matangazo yao na baadae wanafunzi wakaingia madarasani na vipindi vikaendelea kama kawaida.

    Muda uliyoyoma na baadae mengele ikagongwa muda wa mapumziko kwa wanafunzi kwenye kupata chai uliwadia,na hatimaye magari yale ya wanafunzi wakitokea mkoani Tanga yalikuwa yakiwasiri shuleni pale na kuwafanya wanafunzi waliobaki na waliokuwa kwenye magari kubaki kupungiana mikono kwa furaha huku shangwe za hapa na pale zikisikika baina ya wao kwa wao kuoneaha furaha,Magreth,Denis,Natasha na wenzao walionesha kufurahi na marafimi zao baada ya kuonana aiku hiyo huku walimu wakipeana pongezi zao.Wakati furaha hiyo ikiendelea kwa Michael haimiwa hivyo,dhumuni lake hasa lililompeleka kule baada ya kubakikisha ameweka watu wake ndani ya mapango alikiwa akisubiria sasa kazi yake aimalize kwa wepesi lakini badala yake imeenda kumshusha tena chini na kushuhudia anaambulia mukaa kwenye kiti cha Mfalme,alijitenga pembeni kabisa na wenzake akiyafikiria mambo yake,aligeuka na kuwaona wakina Ester na kundi lake wakionesha furaha tu muda wote,alikunja ngumi ya hasira kuona amewakosa mizembe sana.

    "yaani safari hii sitarudia makosa niliyo fanya nyuma,Sara.....utalipa tu kwa kifo cha baba yangu lazima nikuue kwa mikono yangu ndipo nipate kutulia..."alisema Michael akimtazama Sara kwa macho ya haaira balaa..Siku hiyo iliishia hivyo huku wanafunzi wote waliotoka safarini walikusanywa pamoja na mwalimu mkuu na kuwataka waelezee mapunguvu waliyoona huko tokea mwanzo wa safari hadi wanarudi tena kwao wakiwa wazima,wanafunzi watatu tu walinyanyuka na kuongelea kuhusu uendeshaji wa gari dereva kwa spidi sana tu lakini tofauti ha napo hakuna aliyeongea wala kunyanyua kidole kuongea lolote,wakina Denis na wenzake walibaki wakibaki kutazamana na Michael akionekana kutokuwa na raha kabisa,walikaa kimya bila kusema lolote kuhusu yale yaliyotokea mapangoni. Basi waliongea mambo machache muda ule na baada ya kuhakikisha hakuna matatizo yaliyotokea wanafunzi wale waliruhusiwa kurudi makwao kupumzika baada ya safari ndefu ya siku kadhaa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Siku zilizidi kwenda huku Sara akiwa na jukumu la Malkia wa jamii yao,kila kipindi anaenda kuangalia maendeleo ya kule namna inavyo kwenda,kuna muda alitamani kukaa kule moja kwa moja lakini akifikiria wenzake wakina Ester kuwa bado wapo mikononi mwake,isotoshe Michael bado yupo hai hivyo huenda akaendelea kuwaandama.Akiwa anaendelea kutafakari kuhusu hayo na ndivyo Michael naye alikuwa akifikiria hivyo,siku hiyo akiwa shuleni amekaa sehemu alikiwa akitafakari namna ya kuwaingilia watu wake,safari hii hakutaka kabisa kusikia la mtu,vile anavyo panga ndivyo hivyo anavyotaka iwe.Siku hiyo alipanga kumfuatilia Ester siku hiyo lengo ni kutaka kummaliza ili aendelee na wengine,safari hii hakutaka kumuonea huruma mtu yeyote,aliwaandaa vijana wake njiani lengo ni kumteketeza Ester siku hiyo,na kweli muda wa wanafunzi kuondoka Sara aliongozana na kundi lake kama ilivyo ada lakini alishangaa kuona Michael yupo mbele yao tena anakazana kutembea kana kwamba kuna mahali anawahi,hali ile Sara aliiwekea wasiwasi na kuhisi huenda ndio Michael ameanza tena kuwaandama.Basi stori za hapa na pale ziliendelea njiani huku wakifurahi na baada ya muda waliweza kufika kijijini,waliagana na kila mmoja akashika njia ya kuelekea kwao.Akiwa hana hata habari Ester alikuwa akitembea zake kurudi kwao,alipofika mahala fulani alihisi kuna mtu anamfuata kwa nyuma hvyo ikambidi ageuke kutazama nyuma lakini hakuona kitu,akaangalia kulia na kushoto lakini hamukuwa na dalili ya kuonekana kitu chochote,akageuka na kuendelea na safari lakini alipoliga hatua kama tano mbele akaanza kusikia sauti za watu zikilia kwa mbali,ilimbidi asimame na kuanza kuisikiliza sauti ile lakini cha ajabu kulikuwa kimya gafla,hali ile ikamfanya Ester aanze kupata mashaka juu ya swala lile,akafumba macho yake kutaka kuwasiliana na Sara amuelezee hali ile.

    "Sara..."aliita Ester kwa hisia na kitendo cha kumuita Sara jina lake zile kelele zikaanza kusikika yena kwa ukali sana huku Ester akisikia milio ya hatua za watu zikija pale aliposimama,aliogopa sana na kuanza kutetemeka na gafla wakatokea watu wa ajabu asili ya waafu wakikimbia kumfuata Ester ambaye naye kuona kikosi kile cha wale wafu wanamfuata akaanza kuchanganya miguu kukimbia spidi.Sara baada ya kuisikia sauti ile ya Ester aliitikia huku akiikaribia kwao.

    "Vipi Ester niambie....umeahafika kwenu?"aliuliza Sara akiwa anaongea kwa hisia na sauti yake ikapenya masikioni mwa Ester aliyekuwa akizidi kukimbia..

    "Sara nisaidiee.....wananikimbizaaa...nisaidie Saraa nakuomba...."maneno yale yalimshtuwa Sara baada ya kusia vile,akakumbuka muda ule alimuona Michael akiwa anawahi mahali hivyo huenda ndio alikiwa amepanga kumdhuru Ester....alivyotambua hilo huku akiwa amefika kwao akatupa begi lake la shule na kuanza kukimbia kurudi alikotoka na gafla tu akapotea kimaajabu.



    Huku Ester alizidi kuokoa maisha yake akikimbia kupita maelezo huku kundi la wafu kama kumi na watano wakimfukuza kwa kasi na kwa bahati mbaya Ester aligonga kisiki kidogo kilichokuwa ardhini na kumfanya kuanguka hadi chini,aliumia sana mikononi na magotini kwa kuchubuka sana,maumivu yale yalimfanya ajikute akilia kwa hofu na alipogeuka nyuma tu wale wafu aliwaona wamesimama,wakaanza kuangua kicheko cha kebehi sana kumfanya Ester azidi kuogopa,huwezi amini alijitahidi kuamka lakini miguu ilikosa nguvu kabisa na kumfanya sasa aamini kuwa huo ndio mwisho wake,taratibu wakaanza kumsogelea Ester pale alipojikwaa na kuanza kuanza mumzunguka mduara huku wakizidi Ester akaona sasa mwisgo wake ndio umefika na kuamua kufumba macho aanze kumkumbuka mwokozi Yesu huku akianza kusoma sala ya toba,.





    Alibaki kufumba macho tu akisubiri kumalizwa tu,ikapita sekunde kadhaa,dakika lakini haoni kitu kinachoendelea Ester ikambidi afumbue jicho moja kutazama imekuwaje,alipofumbua alishangaa kuwaona wale wafu wakirudi nyuma taratibu kana kwamba kuna kitu wanakiogopa,hata Ester aloshangaa kuona vile na kuamua kuwaangalia wanavyozidi kusogea nyuma na kubaki kujiuliza maswali lakini kuna sauti ya kuunguruma nyuma yake aliisikia na kumfanya ahofu, alipogeuka kuangalia nyuma alishangaa kuona Simba mkubwa sana amesimama akiwatazama wale wafu,taratibu alianza kusogea kuwafuata sasa wale wafu huku akiunguruma hadi Ester akaogopa na kutaka kunyanyuka akimbie lakini hakuweza kutokana na mguu wake kuumia sana alipo dondoka,akabaki akimshuhudia tu yule Simba akiwasogelea wale wafu na alipo wakaribia akaanza kuwakimbiza na kupambana na wafu wale kwa kuwakwaruza sana na makucha makali,kila aliye taka kukimbia alimzuia kwa kumrukia na kuanza kumtafuna kwenye sehemu za mwili wake huku wengi wao akiwadhibiti kwa kiwanyonya damu shingoni hadi kifa.Yote hayo alikiwa akiyatazama Ester kumuona Simba yule mmoja akipilingishana na viumbe zaidi ya 15 ambao baada ya muda Simba yule alowateketeza wote na kumbakisha mmoja ambauye alikiwa tayari kashaumia mguu hawezi kutembea vizuri kama Ester,yule Simba akawa anamfuata tu huyo jamaa huku likijiramba tu na ulimi wake baada ya kiwamaliza wale wengine wote,kwa bahati mbaya sasa yule mfu akawa anatambaa kusogea kule alipo Ester ambaye naye alikuwa ameumia na kushindwa kukimbia,yule jamaa alimsogelea Ester huku akimuhofia yule Simba,Ester naue kuona vile akaona heri tu kuyaokoa maisha yake naye asije kuliwa na Simba yule,aligeuka na kujaribu kunyuanyuka kuondoka lakini mlio wa Sauti ya Simba ukiunguruma kwa nguvu hali iliyomfanya Ester aamini kuwa sasa ndio mwisho wake wake,yule simba alimrukia yule jamaa pale chini na kumparua,chana nguo zake kwa makucha makali na mwishowe kwa meno yake makali akaikamata shingo ya yule mtu na kunyofoa pande la nyama lililomfanya mtu yule kupoteza maisha,Ester alikishudia kifo kile cha kikatili na kuona sasa zamu yake imewadia,hakujali kuwa ana maumivu makali miguuni alijitahidi kusimama,akageuka na kuanza kujikokota kukimbia.



    waje kunimaliza sijui walikiwa ishirni vile....eti uliwatuma wangapi..???ok sijali hilo ila nilitaka uwaongeze mara tatu yake ili nimpunguzie kazi Sara maana amesema lazima atawamaliza kizazi chenu cha wasuriati wote,sasa tafadhari sana...najua kwa hilo jambo nililo fanya hujategemea na utakuwa umekasirika sana ila nakuomba sana uwatume wengi zaidi ili tukamilishe zoezi hili kwa haraka Michael,wacha nipumzike saahizi maana kesho tunatakiwa kule kwenye Falme kuna maana ndio siku MALKIA SARA anakabidhiwa rasmi kuwa kiongozi wa JAMII YETU,kama utataka karibu ila tambua siku zote kuwa hata watu wa jamii ile wanakuchukia sana kwa matendo yako,usitegemee kabisa kwamba utakuja kumpindua Sara uje uongoze jamii ile kamwe...hawakuelewi kabisa na kwa moyo mmoja wamempokea Sara,yule aliye zaliwa na pande mbili ya binadamu na ya jamii yenu,kesho anakuwa Malkia wao,ndio uje kuwa kitu kizuri hata kifichwe vipi kitabaki kiwa kizuri tu,wasuriati nyie mkamuulia mama yake kwa tamaa zenu tu za kutaka madaraka,ona sasa.....mmekata mti mkasahau mizizi...na sasa hiyoooo inaota tena na mti safari hii umezungushiwa fensi ya chuma hamuwezi kuukata,leo hii Ester naongea nina nguvu za ajabu kutoka kwa MALKIA AZNATY,Denis,Natasha hata Magreth hakuna aliyekuwa mpuuzi kwa sasa kama ilivyo zamani kila mtu anajiweza sidhani kama utampindua mmija wetu,nakwambia unajisumbua...tafuta njia mbadala ndugu yangu....Ma rog buna seara(nakutakia jioni njema)"alisema Ester na sauti maneno yake yalipenya barabbara masikioni mwa Michael ambaye alibaki kuduwaa tu,hakika hakuamini kabbisa kusikia vile,Ester amewaua watu wake kumi na watano?alishangaa sana na kuanza kujiwa na woga baada ya kutambua kama ni kweli basi amekwisha maana Denis,Natasha na Magreth nao yasadikika wana nguvu kama mwenzao Ester,alijikuta akijibwaga kitandani kama zigo la mahindi akikosa kabisa raha huku hasira zikichangia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ina maana hawa wameingizwa nguvu wote ili waje kunimaliza kirahisiii au?nakaa muda wote kusubiri watu twende kwa mwengine kumbe nafanya kazi bure!ahhh"alikasirika sana Michael kuona mipango miingu anayo panga i afeli na kuanza kuhisi ni dalili mbaya kwake,alianza kuamini kuwa wakina Ester kweli wana nguvu nao maana tokea siku ile alimshangaa Ester akiongea lugha ya kichawi ambayo hakuna mtu wa jamii yao anaye iweza kuitamka kwa ufasaha zaidi ya wazee waliobobea kwenye nguvu za ajabu hivyo kuifahamu Ester lugha hiyo ni wazi kwamba huenda akawa kweli ana nguvu za marehemu Malkia Aznaty ambaye ndio alikuwa anaitumia sana lugha ile kuo gea na wazee,hakika alichanganyikiwa kabosa Michael akitafakari namna itakavyo kuwa.



    Huku kwa Ester moyo ulikuwa ukimdunda,.wili wote umelowa jasho kwa kitendo alichokifanya.Hakuamini kama anaweza kusema maneno yale yote kwa Michael akamnyamazisha namna ile,aliya pangilia maneno sawa sawa na kuchanganya na lugha ya kichawi kumfanya Michael aamini kuwa ni kweli kumbe hana nguvu zozote wala hao wenzake wakina Denis na muda ule wale wafu waliuliwa na Sara baada ya kubadilika kuwa mnyama mkali Simba.

    Naye Sara akiwa kitandani usiku ule, maongezi yoote ya Ester na Michael alikuwa akiyasikia tu kwa hisia zao,kumbe muda ule aliokuwa akiingia kwao alipata wazo na kuamua kurudi tena nyumbani kwa Ester na kumpa kazi ya kuongea na Michael amtishe kwa namna hiyo ili wampoteze malengo yake Michael ya kuwafuatilia wakina Denis na wenzake waliobaki,Sara alicheka sana akiwa chumbani kwake kwa kuona sasa wamemdhibiti Michael walau kwa staili hiyo,taratibu akaanza kuutafuta usingizi.



    Asubuhi kulipo pambazuka Michael alijiandaa vema kwa ajili ya kuelekea shuleni,aliyakumbuka sana maneno ya Ester aliyosema jana huku akijiamini kabisa,akaona kuna kazi ngumu ya kufanikiwa jambo lake,aliamua kuelekea zake Shuleni huku akiwa na mawazo ni njia gani ataitumia kuwapiku wakina Sara na wenzake.

    Baada ya kumaliza kufanya usafi kwenye madarasa na mazingira yote ya shule wanafunzi waliingia kwenye madarasa yao na vipindi vikaendelea kama kawaida,kwa Michael haikuwa kawaida yake maana mawazo yote hayakuwa shuleni kabisa,tangu walipotoka Tanga na wenzake hakuwa na raha kabisa kila akikumbuka mambo yaliyotokea kule Amboni pindi alipo wadhibiti wakina Sara na kufika nao hadi kwenye jamii yao akiwa na asilimia zote za kuwa Mfalme,hata muda ule alipokaa kwenye kiti cha kifalme na kuvalishwa kabisa kofia ya kifalme.....alipokumbuka ile kofia akapata wazo ambalo lilimfanya kuanza kutabasamu na kuona kwa namna fulani amewaweza.

    Hakuwa na hamu hata ya kuwa darasani kwa ajili ya masomo hali iliyompelekea aage kwa mwalimu aliye kuwa anafundisha na kutok zake nje walau kupumzisha akili.Akatafuta mahala patulivu na kukaa pekeake na kuanza kutafakari matukio kadhaa ya nyuma aliyofeli,alikumbuka hata siku ile alipoliandika jina la Sara kwenye kioo ili ammalize kwa kumchoma kisu lakini kwa uwezo wa Sara akabadili jina lile na kuweka jina la baba wa Michael na kumfanya amuue baba yake kwa mikono xake mwenyewe,hasira zilimpanda Michael na kudhamiria kamwe hatomuacha Sara akiwa mzima.Akiwa kwenye hasira hizo gafla tu mbele akashangaa kumuona Sara akiwa mbele yake,alishtuka sana Michael na kumfanya asimame kumtazama Sara kwa hasira.

    "nadhani ushapata salamu kutoka kwa Ester,labda nikwambie tu kwamba siku zote umekuwa ukinifanya niwe na mashaka ya kuhofia kuwadhuru wenzangu,sikuwa na amri ya kukufanya kitu kibaya ndio maana nimekuwa nikinyamaza tu kuwatetea wanyonge,sasa mimi ni Malkia..nina uhuru wa kufanya lolote lile ninalo taka liwe ni la haki ndio maana siku zote nilikuwa nikiipigania nafasi hii ili nhfanye nilichokikusudia,na leo nakueleza dhahiri kwamba wewe pamoja na wasuriati wote waliokuwa wakikusapoti kwa unyama ulho ufanya lazima niwamalize kwa mikono yangu mwenyewe,kawape taarifa na wenzako waambie Malkia Sara amesema hivyo,nikuacge uendelee kuwaza.."alisema Sara akiwa amemkaribia kabisa Michael kumweleza ukweli huku sura yake ikionyesha kuwa na hasira,aligeuka nyuma na kuondoka zake akimuacha Michael pale alipo akibaki kumsindikiza tu kwa macho tu Sara mpaka alipoingia darasani kwao.Alipandisha pumzi na kuishusha kwa kasi baada ya maneno ya Sara kuzidi kumtia hofu,akajikuta akipiga ngumi mti uliokuwa pembeni yake kwa kupunguza hasira zake,alihisi kuchanganyikiwa kabisa.

    "HUWEZI KUNIPANDA KICHWANI WEWE MTOTO WA MALAYA TU, ,nitapigana mpaka nihakikishe ninafika pale ninapo pataka,kamwe sitasita wala kukatisha msimamo wangu,nina kisasi pia cha baba yangu lazima nikumalize Sara sitakuacha nakwambiaaa"aliongea Michael kwa hasira huku akihema sana,alibaki kulitazama tu darasa la akina Sara huku mkononh akitokwa na damu baada ya kupiga ngumi ule mti.





    Basi masaa yalisogea mbele na muda wa kuondoka uliwadia wanafunzi walirudi makwao,siku na ilikuwa ni kweli Sara anaenda kutangazwa kweli kuwa ndiye Malkia wa jamii yao nzima,siku hiyo aliwaeleza wenzake wakina Denis,Natasha,Magreth na Ester na wakapanga muda wa kukutana kuweza kwenda huko kwenye ile jamii ambao nao pia wanahusika.

    Huku kwa Michael nae taarifa za Sara kwamba ndio siku hiyo anafanywa kuwa Malkia rasmi wa jamii yao aliipata,mida huo alikuwa na watu wake wakipanga namna ya kufanya,baadhi yao hawakutaka kabisa jambo hilo la Sara kutawazwa kuwa Malkia lifanikiwe hivyo wakataka bora watoe maisha yao ili kuhakikisha wanakatisha jambo hilo,na lengo hasa ni kumuua Sara kwa hali yeyote ile ili tu asipate kuiongoza ardhi ile.Wazo hilo lilimtia Michael nguvu na kuona bado ana nafasi ya kumpindua Sara pindi wakifanikiwa kummaliza.Basi waliandaliwa watu watano waende kufanya kitu kule bila ya kujulikana huku Michael akiwa ana furaha na kubako kusibiria matokeo ya watu wake wakielekea kule kwenye ardhi ya jamii yao.



    Ilikuwa ni furaha sana kwa viumbe wa jamii ile siku ile ambayo wazee pamoja na waganga wakuu waliokuwa mbele ya mimbari pamoja na Malkia mtarajiwa Sara aliyekuwa kwenye vazi takatifu la kimalkia na kukaa kwenye kiti chake,Denis,Natasha,Eater na Magreth walikuwa na furaha tu wakiwa pembeni wakishuhudia rafiki yao anavyotawazwa kuwa Malkia wa jamii hiyo.Alisimama mzee mmoja huku akiwatuliza watu waliokuwa wakipiga kelele za furaha,wakatulia kumsikiliza.

    "hatimaye ile siku tuliyokiwa tunaisubiri imewadia,kuanzia leo tunapata kuongozwa na kiongozi,Malkia aliyekuja kuweka pembeni utofauti baina yetu na binadamu na nina imani naye kuwa atakiwa mwema kwetu na kutujali katika kila hali"alisema mzee yule mida mfupi wakasogea wasichana watatu waliorembwa wakiwa nyuma ya wenzao mmoja aliyeshika kofia ya Umalkia na kumkabidhi yule mzee,aliipokea kwa tabasamu na wale wasichana wakasogea pembeni na kumfanya Sara aliyekuwa amekaa kwenye kiti chake anyanyuke na kusogea mbele ya yule mzee,taratibu akapoga magoti na kumfanya yule mzee asogee taratibu na kuanza kumvisha kofia ile huku akitamka maneno kadhaa kama mila yao.

    "Kuanzia sasa wewe ndiye Malkia wa jamii yetu,tutakuskiliza na kutii amri zako kama ilivyo kawaida....UBARIKIWE MALKIA SARA...."alisema mzee yule kwa sauti kuu na kuwafanya watu wote wasujudu chini kumpa heshima yake Malkia wao mpya hali iliyomfanya Sara afurahi sana,baada ya kuvishwa kofia ile alisimama kuongea na watu wake na kuwasisitizia upendo na kuwa wenye kusaidiana kwenye matatizo yanayo jitokeza.Akiwa anaendela kuhutubia watu wale watu wa Michael walikiwa nao washawasiri eneno lile hivyo kazi ikawa ni kupanga wapi waanzie na wapi wamalize ile tu wasijulikane na yeyote,walikumbuka kitu kimoja walichoambiwa na Michael kwamba hapo mwanzo marehemu Malkia Aznaty aliwekewa sumu kwenye vinywaji na chakula na alipokula tu hakukaa muda akapoteza maisha.....hivyo kwa njia hiyo kwao ikawa ndio njia pekee waitumie kummaliza naye Sara kama alivyokufa mama yake.Walilitazama jengo la kifalme na kuona baadhi ya wafanyakazi wakipita huku na kule kuandaa vyakula vya Malkia Sara,wakaona njia ya pekee ndio hiyo,bila kujulikana wakanyata na kuwaminya kimya kimya wakawaua,waliwaweka sehemu ya siri na kisha wakachukwa mavazi ya wale wafanyakazi wakayavaa wao kisha wakajochanganya na wengine kiendelea kuandaa andaa mambo bila kujulikana,walitafuta chumba cha Malkia Sara anachopumzikia na kumtuma mmoja kati yao aingie mule,alichukuwa matunda na Juisi akaelekea chumbani kwa Malkia wakionekana ni wafanyakazi wa kawaida tu,hata alipoingoa haraka akaanza kuweka matunda sehemu yake pamoja na juisi,alipomaliza aliangalia huku na kule hakuna mtu anayemuona,akatoka kimfuko kidogo ambacho kilikiwa na unga kidogo akauchota na kuuchanganya kwenye juisi na kukoroga kisha akaunyunyizia kwenye matunda yale na kuanza kumwagia maji kodogo yaonekane yametoka kuoshwa na baada ya kumaliza kazi hiyo taratibu akafungua mlango na kuondoka zake,alirudi kwa wenzake na kuwaeleza kuwa kazi imekamilika hivyo wasubiri matokeo tu.

    Basi huku mambo yalienda sawiya na hatimaye Sara akatawazwa kuwa Malkia wao,walimaliza taratibu za pale na Malkia akaruhusiwa kurudi chumbani kwake kumpumzika,Sara hakuwa na walinzi wa pembeni aliongozana na kundi lake wakina Ester moja kwa moja hadi chumbani kwake na kukaa .

    "aisee siamini ujue Sara.....hivi naona kama ni mchezo wa kuigiza vile! yaani hapa tupo kwenye ufalme sijui...umati mkubwa wa watu hapo njee umefurika kumshuhudia Sara kiongozi wao...aisee hongera sana Sara maana yataka moyo kuongoza umati wa watu namna hii....mimi huo umonitor wa darasa tu wenyewe unanishinda"alisema Magreth na kuwafanya wenzake watabasamu tu. Asi waliongea mambo mengi sana pale huku wakiangalia namna chimba cha Malkia wao kilivyo pambwa na kuwa safi,walifurahi kuona vile.Natasha alinyanyua ndizi moja na kuanza kuimenya huku wenzake wakiwa wanaongea,hata alipomaliza kuimenya taratiibu akaanza kuipeleka mdomoni lakini Magreth alimuona.

    "muone naye huyu cha uroho...anapenda kula huyuuu"alisema Magreth na kumfanya Natasha asimame zoezi lake na kubaki kucheka tu kama utani huku wenzake na o wakimcheka.Wakiwa kwenye hali hiyo akabisha hodi mfanyakazi mmoja wa kiume akionekana kushika kinywaji na kumpelekea moja kwa moja Malkia Sara,akammiminia kwenye glass ya dhahabu na kumtengea pembeni hadi wakina Ester na wenzake wakaona ni jinsi gani Sara anavyo heshimika kweli,Sara alitabasamu tu huku Natasha akiwa bado ameishikilia ndizi ile akimtazama Sara ambaye taratibu akainyanyua glass ile huku akiiangalia kwa tabasamu,yule mtu aliyeleta kinywaji kile akanyanyuka na kugeuka nyuma kuanza kuondoka zake huku usoni akioneaha tabasamu,alipoukaribia tu mlango akasikia sauti.

    "hebu subiri...."alisikika sauti ya Sara pale alipo na kunyanyuka kumfuata yule jamaa ambaye alishtuka kusikia vile,Sara akasogea mpaka pale alipo na kusimama karibu ya mlango akiuzuia huku mkononi akiwa ameshika kile kinywaji.

    "kwanza niseme nashkuru sana kwa kuonyesha utendaji wako wa kazi maana nilikiwa kweli nina kiu,"alosema Malkia Sara.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ah usijali Malkia wangu...hii ni kazi yangu kuhakikisha unapata kile unacho kitaka hapa kwenye Falme"aliaema yule kijana akionesha tabasamu la unyenyekevu.

    "unaitwa nani wewe?"aliuliza Sara na kumfanya yule kijana aanze kujin'gatan'gata huku wakina Denis na wenzake wakimuangalia tu.

    "Ah hehe...naitwa Razul....."alilitaja jina lake yule kijana.

    "ahaa Razul...nashkuru kukufahamu.....unaoneka mtu wa watu sana wewe hupendi kuona watu wanapata tabu wewe,unawajali sana wenzako."alisema Sara akimtazama tu yule jamaa usoni.

    "ahh ni kweli....ni kweli kabisa Malkia...unajua ukarimu ni jambo la msingi sana baina mtu na

    wakina Magreth,Natasha,Denis na Ester wote wakiwa wana muangalia kwa tabasamu,akageuka na kuanza kupeleka taratibu ile glasi kinywani macho yote yakimtazama Malkia Sara,alipokaribia mdomoni tu akachomoa kile kiau chake kwa haraka na kukipitisha haraka shingoni mwa Malkia Sara lakini wapi.....Sara alikuwa mwepesi sana na kufanikiwa kuukamata mkoni wa Razul kwa nguvu zote huku akimtazama usoni na papo hapo mkono ule ukaanza kuonekana kuoza taratibu ukielekea mabegani umalizikie mwili mzima,Ester na wenzake walishangaa kuona hali ile na kubaki kushika midomo yao tu hawaamini.

    "nakupa nafasi moja tu uniambie....umekuja pekeako au una wenzako uliokuja nao?"aliaema Sara kwa hasira akionekana kubadilika kabisa macho.Razul aliogopa sana huku akishuhudia mkono wake ukizidi kusogea tu kuoza.

    "nisamehe Sara....nisamehe tu Malkia wangu.....nimetumwa tu na Michael mimi nisamehe bure"aliaema Razul akianza kuoneaha kulia,wakina Ester waliahangaa kusimia kuwa Michael ndio aliyemtuma kufanya hivyo..

    "a. aaaaah sijakwambia aliyekutuma kufanya hivi.....huyo namjua na wewe pia nimekujua tokea mwanzo ila nimekuuliza umekuja na wenzako au upo pekeako?"alisema Sara kuonesha yupo siriasi kwa hilo,Razul akaona bora aseme ukweli tu akamtazama Sara na kutaka kusema lakini gafla tu ukapenya mshale mmoja na kutua shingoni mwa Razul papo hapo akapoteza maisha,Sara kutazama ulipotokea aliona jamaa mmoja dirishani na baada ya kumaliza kazi ile akapoyea kimaajabu tu gafla hivyo ikamfanya Sara aelewe kuwa hakuja pekeake kuna wenzakw alikuja nao na walipoona mwenzao kashikwa wakaamua wammalize ili asizidi kutoa siri zengine.Magreth alibaki kuziba mdomo tu kwa hofu ya jambo lile analoliona mbele yake,yaani hadi ndani ya Falme watu wanavamia na kufanya mauaji ni jambo lililomfanya apate wasi wasi sana,basi Sara aliwaita walinzi na kuwaeleza namna ilivyokuwa huku akiwahimiza wawe makini na kila mtu wanaye muhisi vibaya,waliuchuwa mwili wa Razul na mwenda kuutupa mbali maana ulishaanza kutoa harufu ya kuoza kwa kile alicho kifanya Sara...Aliumiza sana kichwa na kuona akifanya masihara Michael anaweza kumuangamiza,aliwasogelea wenzake na kuwaeleza kuwa vyakula vyote pamoja na vinywaji vilivyo kuwepo pale vilitiwa sumu lengo ni yeye kuuawa kama alivyokufa mama yake marehemu Aznaty,maneno yale yalimshtuwa sana Natasha na kuona hata yeye angekufa pale tu angeila ndizi ile,alipata wasiwasi lakini Sara aliwatuliza na kuahidi hakuna kitakacho haribika



    Taarifa za kuingia wasuriati kwenye falme ile ilifika kwa wazee na kuona kuna haja ya kuzidi kuweka ulinzi ili lisitokee tena hali hiyo,Sara alikasirika kuona bado anafuatiliwa na wasuriati na kujua kuwa mhusika mkuu ni Michael,basi walipanga namna ya kufanya na muda ulipofika aliwachukuwa wenzake na kurudi tena duniani.

    Kesho yake wanafunzi waliendelea na masomo yao kama kawaida huku Michael akionekana mwenye hasira sana mara baada ya kupata taarifa za wale watu aliyo watuma kule kwenye falme kwamba wameshindwa kutekeleza kazi waliyofanya,aliona sasa ni wakati wa yeye mwenyewe kuchukua uamuzi wa kumpindua Sara maana kila akiwatuma watu wake analetewa habari ambazo hazimpendezi,alikaa muda mwingi sana akitafakari afanye jambo gani ambalo anaweza kupata wepesi wa kumzidi mpinzani wake,aliumiza kichwa sana baadae akapata wazo ambalo aliona ndio njia ya wepesi kummaliza Sara,akapata hata nguvu ya kuendelea kusoma huku moyoni akiwa na wazo lake lililomfanya awe na matumaini.Basi muda ulienda na kengele ya mapumziko ilipogongwa kama ilivyo ada wanafunzi wakaelekea kupata kifungua kinywa,muda huo Michael aliutumia kuelekea kwa mwalimu wake wa darasa na huku akionesha hali ya utofauti akisingizia anaumwa,mwalimu alimtazama na

    kumshika alionekana kweli kuwa na joto kali,haraka akampa ruhusu arudi kwao mpaka hapo atakapo pona,Michael alitoka ofisini na kurudi zake darasani ambako muda huo wanafunzi wote walikuwa washatoka kuelekea kupata chai,alibaki akitazama tu lile darasa huku akitabasamu.

    "kwa siku hizi tatu nisipo kumaliza wewe mwanaharamu itakuwa ni bahati yako,ngoja nifanye hili tuone."alisema Michael na kugeuka zake kuondoka.Muda huo ndio Denis na wakina Magreth nao walikuwa wakielekea kupata chai,Michael alikuwa nyuma yao tu anawafuata taratibu,basi walifika na kununua chai pamoja na mikate wakatafuta mahali na kuanza kula huku wakiongea mambo yao,muda wote huo Michael hakuwa mbali na walipokaa wakina Magreth na kuona hapo ndipo sehemu sahihi ya kufanya kile alichopanga,alimtazama Denis akiwa ameushika mkate akiupeleka mdomoni,kwa nguvu za kichawi akaanza kuyatamka maneno fulani na kuonekana vumbi fulani likitoka mdomon i mwake na kuelekea kwenye ule mkate wa Denis ambaye bila kujua lolote alitafuna na kushushia na chai,zoezi hilo lilipo kamilika Michael alitabasamu tu na kugeuka kuondoka zake na kuwaacha wakiendele kula.

    "yaani nikikumbuka matukio ya nyuma yaliyo tokea hadi kuambiwa leo Denis mimi naishi sina budi kumshukuru Sara kwa mambo aliyoyafanya,ametusaidia sana tena sana"alisema Denis akimsifia Sara.

    "na kweli aisee,eti kipindi kile nakuja kuambiwa nimepandisha mashetani maskini ya Mungu hata siyajui mambo hayo kumbe ni hila tu na njama za shetani Michael,namchukia yule mvulana basi tu"

    "ah yashapita hayo mambo jamani ni kumshukuru Mungu tuwazima wote na tumeshajitambua kuwa matatizo yote yanatokea kwasababu gani,nusu binadamu nusuuu sijui niite viumbe gani ila yote kwa yote ni kuzidi kuomba Mungu tu na tuwe na imani hiyo maana tuseme tumtegemee Sara hata yeye pia ni bnadamu ana kushinda na kushindwa tuelewe hivyo"alisema Magreth na wenzake wakamuelewa na kuyapokea mawazo yake,wakawa wanaendelea kunywa chai lakini gafla tu Denis akaanza kujiwa na upendo kwa Sara,alianza kumfikiria na kuona upole,ukarimu na kujiamini kwa msichana huyo hali iliyomfanya aingiwe na matamanio ya kimwili hasa akifikiria uzuri wa Sara,akajikuta ana tabasamu tu mwenyewe huku akinywa chai tu na kuwafanya wakina Natasha wamshangae.

    Huku kwa Sara alikuwa na rafiki yake wa dhati Ester wakiwa wanajadili jambo.

    "yakupasa uwe makini sana Sara juu ya uongozi wako,duniani unaonekana ni msichana mdogo wa kawaida tu lakini kwenye jamii yako wewe ni kama Rais wa nchi,wewe sasa ni Malkia na unatakiwa uwe na maamuzi yaliyo sahihi hasa kwa wananchi wako,usikilize pia mawazo yao juu ya kuijenga nchi yako,mimi kama kama mmoja wa wananchh wako nakushauri umteketeze kabisa Michael kusudi watu waishi kwa amani,kama nguvu,uwezo mkubwa unao kinachokufany a umcheleweshe kiumbe kama huyu?unataka azidi kukutia matatizoni,kama hapo tu umekoswa kuuliwa kwa sumu iliyowekwa kwenye kwenye kinywaji,namchulia huyu mtu sana maana ametufanya tuisi kwa mashaka muda wote,tafadhari MALKIA WANGU jaribu kufikilia haya ninayo yasema"alisema Ester kwa hisia kalh akionesha kuchoka na usumbufu wa Michael,maneno yake yakampa ujasiri sana Sara na kujiona amejisahau kuwa yeye ndiye mweny amri ya kufanya chochote,alimtazama Ester na kumshika mkono.

    "ndio maana najivunia kuwa na wewe Ester,upo sahihi kabisa kwa maneno uliyoniambia na nitafanya hivyo wala usijali."alisema Sara namfanya Ester aachie tabasamu.Baadae muda wa kuingia madarasani ulipofika walirudi na vipindi vikaendelea,aliingia Madam Magdalena na kuendelea kufundisha kipindi chake cha Kiswahili.Muda wote Denis alikuwa akizidi kuushawishi moyo wake akiwa ana muangalia tu Sara kwa uzuri alio nao,hakika akatokea kumpenda Sara bila kujielewa.Basi muda ulizidi kwenda hadi vipindi vilipokwisha wanafunzi waliruhusiwa kurudi makwao,muda huo ndio Denis akaona ni njia pekee ya kumuonesha ishara Sara kwamba anahitaji nini kutoka kwake,na kweli Sara akiwa anaweka madaftari yake vizuri kwenye begi alimuona Denis akimsogelea pale alipo.

    "ah niambie jembe langu Denis uko powa!"alisema Sara kwa uchangamfu akiwa anafunga zipu ya begi,uchangamfu ule ukamfanya na Denis naye auige ili waende sawa.

    "ah safi tu Malkia wangu naona ndo safari hiyo"

    "kama kawaida ngoja nikamuwahi mzee Junior nikampikie."alisema Sara huku akianza kutembea na kuwaona wakina Ester na wenzake wakiwasubiri.

    "ok sawa but....kuna jambo nataka tuongee kidogo wawili kama hutojali ila kwa mazingira ya leo naona hayaruhusu hivyo kesho kunako majaaliwa kesho tutaongea vizuri Malkia wangu"alisema Denis kwa kujiamini akionesha kweli anamaanisha na kumfanya Sara atabasamu tu bila kujua lengo hasa la Denis ni nini.

    "basi sawa jembe nitakukumbusa kesho ikifika"alisema Pasa na Denis akubali,wakaungana na wenzao na kuanza safari ya kurudi makwao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huku kwa Michael alionekana akiwa kwenye chumba chenye giza akiangalia beseni lililokuwa na maji yaliyo tulia akiangalia mambo yanavyoenda.

    "safi sana Denis kwa kazi nzuri,ataingia tu mwenyewe kwenye mtego wangu na sitomuacha"alisema Michael huku macho yake yakiwa makali akitazama lile beseni lenye maji ambalo liliweza kumuonesha vile Denis akiwa anaongea na Sara kule darasani na kuahidiana kuongea kesho,alibaki akicheka sana kwa kuona mbinu yake inaanza vema.

    Basi jioni ile Sara alipanga safari ya siri kurudh kwenye falme yake,kwa maneno ya Ester aliyoongea mchana ule yalimfanya aone kuna haki ya yeye kama Malkia kufanya kitu kwaajilh ya wenzake,akiwa chumbani kwake alinena maneno fulani na kupotea gafla na kuja kutokea kwenye falme yak e ambapo alipokelewa kwa heshima zote,aliwaita wazee wote wa falme hiiyo na kukaa nao kwenye chumba kimoja wakijadili mambo.

    "kubwa hasa nililo waitia hapa ni kuhusu hatma ya hawa wenzangu,ukweli ni kwamba naheshimu taratibu za falme hii lakini kwa hili naomba niwashirikishe hata nyie kwa maana mnafahamu zaidi mambo ya hapa yanavyoenda,Michael licha ya kushindwa kuwa kiongozi wa hapa amekuwa bado ana njama za kuendelea kunipinga kwa kupanga kuniua,si mimi tu hata wenzangu ambao ndio kabisaa amekuwa akiwaandama kutaka kuwaua,sasa najikuta nafanya kazi ya kuwalinda wote wanne pamoja na kujilinda mwenyewe...hivyo basi kama MALKIA ninahitaji wapewe nguvu za ziada waweze kujilinda wao wenyewe kusudi niwe nina uhuru wa kupanga mipango mengine ya kimaendeleo ya nchi yetu,au mnaonaje?"alisema malkia Sara huku akiwatazama wazee wale wakionekana kuangalia chini wakilitafakari jambo lile,kimya kilitawala kama dakika mbili hivi bila ya mtu yeyote kuongea na badae mmoja wa wazee aliongea.

    "Malkia wangu,tumeyapokea maneno yako na tuta tekeleza kama ulivyotaka,lakini swala hili lina masharti ambayo inabidi yafanyike,wewe ni wa kipekee uliye bahatika kuwa na nguvu zaidi kisha ukaishi duniani,lakini kama unataka wenzako wawe na nguvu za kujilinda wenyewe yatakiwa pindi wakipokea nguvu hizi watapewa siku saba tu za kuishi duniani zitakapo malizika watalazimishwa kurudi huku kama makazi yao ya milele hawatarudi tena duniani."alisema mzee yule na wenzake wakatikisa vichwa kumaanisha yanayoongelea ni ya kweli.Sara alishangaa baada ya kusikia masharti yale,alitaka kuwasaidia wenzake wawe na nguvu kama za kwao lakini kutokana na maneno aliyoambiwa aliumiza kichwa sana na kutafakari atafanyaje.Hakutaka kutoa jibu papo hapo ikambidi atoke kuelekea kwenye chumba chake kama Malkia na kujitupa kitandani akianza kutafakari kwa kina,mtu wa karibu na anaye muamini alikiwa ni Ester hivyo ikambidi tu aage na kurudi zake duniani apate kumueleza Ester naye ili apate mawazo yako.





    Basi alirudi tena duniani akiwa amebeba kitu kichwani kwamba ili wenzake wapate kubarikiwa kuwa na nguvu kama zao basi ni lazima warudi kuanza maisha yao kule kwenye Falme jambo ambalo kwa Sara alifiki jinsi ya kulifikisha kwa wahusika kama watalipokea jambo hilo.Kesho yake shuleni alimchukuwa Ester na kukaa zao kama ilivyo kawaida pindi wenzao wakienda kupata kifungua kinywa asubuhi ile.

    "basi hali halisi ndio kama hivyo ndio maana nikaamua kukujuza kwanza wewe nategemea utanishauri kwa hili"alisema Sara baada ya kumueleza yote Ester yale yote aliyoambiwa na wazee.Hata Ester mwenyewe alichukuwa muda kidogo hadi kutoa wazo lake.

    "kiukweli Sara mimi nakuamini sana,wewe ni zaidi ya rafiki kwangu,mimi niko tayari hata kuishi huko lengo tu ni kutaka amani maishani mwangu,kama mzazi wangu alitokea huko na kuzaa na mzazi wangu huku duniani kwanini nikatae kuishi popote pale,huku ni kwetu na kule pia ni kwetu wala usijali Malkia wangu,madam na wewe upo sioni kama nitakuwa mpweke huko kuanza maisha mapya"alisema Ester kwa moyo mkunjufu na kumfanya Sara apate faraja kuona kumbe inawezekana.

    "cha muhimu nh kuwaambia tu na wenzetu wapate kujua hali halisi na kusikiliza mawazo yao,tukiafikiana hata kesho tunaweza kwenda tukafanyiwa hicho kitu"alisema Ester akionyesha kweli amedhamiria,Sara alimuelewa na kupanga kuwaeleza muda ukifika,na muda ule Sara alipata kumuona Denis akiwa amekaa mahali akimtazama tu Sara pale akiwa na Ester,akakumbu jana waliahidiana kukutana kuna mambo wayazungumze,alimuaga rafiki yake na taratibu akamsogelea Denis pale alipokaa.

    "vipi mbona umejibanza huku pekeako jembe!"alisema Sara na kuketi kwenye jiwe moja lililipo karibu na Denis.

    "nilijuwa tu utakuja ndio maana nikatafuta mahala patulivu kama hapa"alisema Denis.

    "hahha,haya bwana nimekuja kweli maana jana ukaniweka kwenye mabano, hukuniambia lolote nkaona muda ndio huu"alisema Sara akiwa hana wasi na kubaki kumsikiliza Denis ambaye hakutaka kupoteza hata pointi moja.

    "Sara.."aliita Denis na kumfanya Sara aitike na kugeuka kumtaza Denis.

    "kiukweli tangu nikufahamu hapa shuleni umekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu,bila wewe sidhani kama ningefika hapa hasa nikikumbuka jinsi nilivyoingia na jini na kujikuta namtamani Natasha bila kujielewa,niliumia sana kipindi kile kulikuwa na kitu moyoni mwangu ambacho nilikipanga kukueleza,hivyo siku zote nikawa najiuliza nitakapo kueleza utanifikiliaje,lakini kiukweli Sara...."alisema kwa hisia Denis na kuushika mkono wa Sara ambaye alishangaa..."nimeshindwa kuzuia hisia zangu kwako kwa kujikuta nakuweka moyoni pasi na kujali kile kilicho nitokea japo si kwa ridhaa yangu,nakuomba uniweke moyoni mwako ili nipate kupoa kwa hili,hiki ndicho kitu nilichokiweka moyoni kwa muda wote na kuona bora nikua mbie ukweli mwenzangu upokee hisia zangu,NAKUPENDA SANA SARA"alisema maneno hayo Denis huku akiwa ameushika mkono wa Sara ambao kwa mbali ulianza kutetemeka kwakuwa hakuwahi hata siku moja kuambiwa maneno hayo,kama msichana aliyeumbwa aibu alijitahidi kukwepa macho ya Denis yaliyokuwa yanamtazama muda wote.

    "Denis....mbona unaongea maneno ambayo sikutarajia kama utanambia!na kwanza...eh"alishindwa kuzungumza Sara akihisi kutetemeka mwili,alishindwa kuongea.

    "Sara ninacho kisema namaanisha kweli kutoka moyoni,nakupenda kutoka moyoni na ndio maana nikawa mchoyo wa kutamka maneno haya kwa msichana mwengine,tafadhari Sara fikiria kuhusu hilo wangu."alizidi kuongea Denis na kumfanya ampe wakati mgumu Sara,muda huo huo kengele ya kuingia madarasani ikagongwa na kumfanya Sara ashukuru na kupata pointi ya kuondokea.

    "Denis hebu twende darasani muda wa masomo huu haya mambo tuyaache kwanza ila nikwambie tu ukweli, sikupanga kabisa kujihusisha na mambo hayo nikiwa hapa shuleni,tumekuja kusoma haya mambo yapo tu Denis,na sio kwamba sikupendi jembe langu nakuheshimu na nakupenda sana kama ninavyo wapenda wakina Natasha,Magreth na Ester,tusivunje urafiki wetu kwa mambo ambayo hayana umuhimu kwa umri wetu,nimezipokea hisia zako,nimekuelewa yote uliyo sema lakini tambua tu kwamba Sara kwa sasa hayupo tayari kwa mambo hayo kwa sasa,nisamehe sana jembe langu na wala usinichukie....tuelekee darasani"alisema Sara akiwa tayari amesimama,aligeuka na kuondoka zake huku akiwa ameukunja mdomo kuonesha yale yaliyoongelewa na Denis hayana maana kwake,Denis alibaki pale akimsindikisa kwa macho tu Sara hadi alipoingia darasani,alibaki akitabasamu tu na kujipa moyo tena huenda akimueleza kwa mara nyengine atajua kuwa kweli amedhamiria kupenda,naye akanyanyuka na kuelekea darasani.Basi vipindi viliendelea madarasani kama kawaida.

    Huku kwa Michael akiwa kwenye chumba chake cha siri baada ya kuona yale majibu ya Sara akaona kuna namna ya kuzidisha uwezo wa kumtumia Denis kumlaghai Sara kwa kuziteka hisia zake,hakukubali kushindwa mapema na kuamua kujipanga tena upya kwakuwa anamtumia Denis popote pale anapoenda na popote pale alipo Michael anafahamu.

    Siku hiyo Sara akiwa na wenzake wakirudi nyumbani aliwapata tu taarifa kuhusiana na vile alivyoambiwa.

    "jamaniee kuna jambo tunapaswa kulijadili kwa kina na kila mtu ataongea wazo lake ni kuhusu kule kwenye falme,nadhani kila mmoja wetu anafahamu kuwa yeye ni nani na anahusika vipi kule kwenye jamii nyengine,hivyo basi kama tutakuwa tayari tujadili huku tunatembea."alisema Sara akiwa na wenzake wanatoka shule.

    "mh Sara,tusimwage mchele kwenye kuku wengi hapa,njia hii wanapita bado wanafunzi wengi tu hapa hivyo haitakuwa vzuri tujadili huku tukiwa na mashaka wakipita watu watasikia,bora tupan ge siku na mahala pa kujadili ili tuelewane"alisema Magreth na kuwafanya wenzake wakubaliane nae.

    "ah lakini kwanini tusiliseme tu hapa hapa kila mmoja wetu awe ameshajua hapa hapa?"alichangia Denis ambaye kashatekwa akili na Michael hivyo mambo yote anayofanya si yeye ni Michael ambaye alionesha kutaka kufahamu kinacho endelea ni kitu gani hicho.Wenzake wakawa na kazi ya kumuelewesha muda wote japo alionekana kuwa mbishi lakini hakuwa na jinsi akawasikiliza watoto wa kike wazo lao.

    "basi sawa kwakuwa kesho ni ijumaa tukitoka tu shule jioni tutaenda kule kwenye falme tukaongee vzuri maana ndio sehemu yenye utulivu na amani"alisema Sara na wenzake wakakubaliana naye.Basi kila mmoja akakamata njia ya kuelekea kwao huku wakisubiri siku ya kesho jioni waelekee kule kwenye falme.Natasha na Magreth walikuwa ni majirani wa karibu hivyo waliongozana njia moja wakiendelea kuongea mambo yao.

    "haya asubuhi ukasema kuna jambo unataka kuniambia,haya niambie sasa"alisema Magreth akiwa na shoga yake Natasha.

    "ah shogawee...sio jambo geni sana lakini ni zito kidogo kwangu mimi.."alisema Natasha na kumfanya Mage awe kimya kumsikiliza."kiukweli yani nimeshindwa kuzuia kabisa hisia zangu na kuona ni bora tu nimweleze mtu ajue tu ili niutue huu mzigo,Mage.... nampenda Denis kupita maelezo,tangu kipindi kile yaliuyo tokea yaliyo tokea nikawa najaribu kabisa kumsahau lakini najikuta siwezi mwenzio,sasa ya nini kuumia mwenyewe wakati anaye sababisa yupo,eti si bora nimwambie tu!au atanionaje?"aliongea Natasha akionesha kweli maneno asemayo yanatoka moyoni.

    "mh aisee Natasha unanistaajabisha,unajua sikutegemea kama wewe au Denis angeongelea swala la mahusiano tena baina yenu maana kile kilicho tokea haikuleta picha mzuri kwa kweli..ila ni kweli uyasemayo yanatoka moyoni?"

    "bila kupepesa macho Mage nasema ukweli wa moyo nampenda sana Denis na naamini hata yeye ananipenda,tulianza kupendana hata kabla ya jambo lile kutokea,sasa ugumu unakuja kwenye kumwambia maana haoneshi kabisa kama anakumbuka kuwa tulikuwa wapenzi na mimi ndio mdhaifu wa mwisho kwenye kuongea,naogoopa ndio maana nimekwambia wewe unisaidie kwa hili."

    "mh unanipa mtihani sasa shoga....ila sawa nitajaribu kumwambia akiwa pekeake kama atanielewa sawa nitakwambia ila yakupasa kuwa jasiri na wewe uoga wako huo utajikuta unapoteza ukipendacho ukabaki unalia,..haya basi kama vipi kesho"alisema Magreth wakiwa wamesimama karibu na kwao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "basi sawa Mage nimekuelewa, kesho basi"alisema Natasha na kila mmoja akaelekea kwao.



    Basi baada siku mbili walipanga jioni ya siku hiyo waelekee kule kwenye falme huku Sara na Ester pekee ndio waliokuwa wanafahamu kinachotakiwa kuongelewa,siku hiyo asubuhi Ester alitoka kuelekea msalani na kumuacha Sara pale walipokuwa wamekaa,muda huo Denis ndio aliutumia kumfuata kwa mara nyengine Sara akizidi kumshawishi kimapenzi,Natasha alikuwa hayuko mbali na kushuhudia Denis akiongea na Sara na kuonekana kama anabembeleza jambo,hakuweza kusikia yanayo zungumzwa baina ya Denis na Sara ambaye hakuonyesha kabisa kuyafurahia maongezi yale hivyo ikambidi ajisogeze kuweza kusikia kinachoendelea maana ameanza kuwa na mashaka,Sara kuona bado analazimishwa alinyanyuka na kumgeukia Denis.

    "Denis naomba tusivunjiane heshima,elewa mara moja mtu akikwambia kitu usipende kufosi,niache kama nilivyo"alisema Sara akionesha kukwazika akaondoka zake,Natasha ndipo akapata kusikia kile kinachoendelea baina ya watu hao wawili,hakuamini kuona mtu anayempenda Denis anahangaika kuanzisha mapenzi kwa Sara,moyoni aliumia sana na kubaki kukumbuka maneno ya Magreth kuwa uwoga wake wa kukaa kimya ipo siku atapoteza kile akipendacho,alibaki akimtazama tu Denis pale alipoachwa na Sara,

    "Denis,yani mimi nahangaika nitakupataje kumbe wewe upo kwengine kabisa!"alisema Natasha akionesha kutopendezwa na kitendo kile, moyo wake ukamtuma bora aanze tu kujionesha kwa Denis kama anampenda ili amuondoe fikra Denis za kumfuata fuata Sara,taratibu alijisogeza mpaka pale alipo Denis na kuanza kuachia tabasamu.

    "Vipi Denis uko powa?"aliuliza huku akikaa karibu na Denis ambaye aligeuka na kumtazama.

    "ah shwari nambie"

    "poa.. naona umekaa pekeako hapa kuna usalama?"

    "ndio niko poa tu,nlikuwa na malkia wetu hapa nkawa namuuliza kuhusu safari yetu hiyo ya jioni na kidogo nkataka nijue ni nini tunaenda kujadili lakini hakuweza kunambia."alisema Denis akionesha yupo siriasi lakini Natasha alijua kuwa sio kweli anamdanganya,alimuitikia tu yaishe na baada ya sekunde kadhaa wakaa kimya wote,Natasha moyo ukawa unamdunda akitamani kuongea kilicho mleta lakini moyo unakataa,alijipa matumaini na kuvaa moyo wa ujasiri kuona potelea pote bora atoe la moyoni....





    "Denis..."aliita Natasha na kumfanya Denis ageuke kumtazama na kubaki wakiangaliana tu.Natasha alihisi kutetemeka mwili huku akiwa na woga moyoni mwake,kwa ujasiri akaamua kujikaza tu.

    "samahani kama nitakuuzi kwa hili nisemalo japo ndio ukweli halisi,kiukweli Sara hana mpango na wewe kabisa na hajawahi kufikiria kuwa na mtu kimapenzi unajisumbua tu bure,lakini kwanini uhangaike kutaka kuanzisha penzi kwa mtu asiyekuwa na hisia na wewe wakati kuna mtu anakupenda na kuijali thamani yako...Denis,tusahau yale yaliyo pita hatukuwa sisi pale tulipandikizwa tu mapepo mabaya lakini ukweli kwamba nakupenda sana,naumia nikikuona una hangaika kwengine wakati mimi nipo,tafadhari hebu nielewe jamani nakupenda."alisema Natasha na kuushika mkono wa Denis ambaye alikuwa akishaa.

    "wewe....wewe....wewe,unaumwaee?una pepo la ngono ndio linakutuma ujitongozeshe kwangue!yaani muda wote umekuwa ukinifuatilia tu nikiwa na Sara ujue nitajibiwa nini ili upate pointi ya kujiingiza kwangu,sasa sikia tena unisikilize kwa makini,SIKUPENDI,SIKUTAKI,SIKUHITAJI na uniache tu niendelee kumfuata Sara kila siku maana ndiyo nimemchagua yeye kwa sasa na sio NYIE wa..."alisema Denis na kujikuta akitaka kuropoka.

    "sio sisi?mbona sikuelewi Denis!"aliuliza Natasha akiwa hajamuelewa Denis alimaanisha nini,hakumjibu chochote akageuka na kuondoka zake akimuacha Natasha akifikiria kauli ile,lakini aliachana nayo na kuanza kukumbuka alivyoambiwa kuwa hapendwi,moyoni aliumia sana na kubaki na huzuni.Muda huohuo akatokea Magreth aliyemkuta Natasha akiwa kwenye hali ile.

    "Natasha...haya kulikoni mbona huna raha."aliuliza Mage akiwa amemshika bega Natasha.

    "Mage we acha tu,Natasha nimependa nisipopendwa,hanitaki,hanipendi,hanihiji ndio kauli aliyo niambia Denis."

    "wewee Natasha,hicho ndicho kinakufanya unune na kuifanya sura yako iwe na majonzi muda wote? kuambiwa hivyo tu siku moja ndio unakata tamaa kabisa."

    "sio hivyo Mage,nimemshuhudia kwa macho yangu akimbembeleza Sara wawe wapenzi,unafikiri nitakosa kuwa mnyonge?"alisema Natasha kwa hisia kali huku kwa mbali machozi yakimlenga,hata Mage alimuonea huruma.

    "lakini Natasha,bado una nafasi ya kumbadilisha Denis akakuelewa,sidhani kama Sara atakubali kirahi tu kuwa na mahusiano Denis,muda huu sio wa kuanza kulia,kama unampenda kweli usichoke kumfuata we kubali tu kuwa chini ili upate unacho kihitaji."alisema Magreth na kuzidi kumpa moyo kwa maneno yaliyomfanya kidogo Natasha awe na matumaini mapya.Basi walirudi madarasani na kuendelea na masomo.Siku hiyo ndio walipanga kwenda kule kwenye falme wakakae kikao kujadili jambo waliloambia na Sara kwamba linahusiana na falme,hivyo kwa Michael alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua ni jambo gani wanalokwenda kuongea akimtumia Denis kama kupata habari zinazo endelea.Na jioni ilipofika walikusanyika wote watano na kukaa sehemu moja wakijenga duara kwa kushikana mikono na muda mfupi wakapotea,muda mfupi tu wakatokea ndani ya falme na bila kupoteza muda Sara aliongoza njia akifuatwa na wenzake hadi kwenye meza kuu.Kule duniani Michael alikuwa ndani ya kile chumba chake na kuwa makini akiwatazama tu wakina Sara na wenzake wanayo ongea kule..wenyewe kule wakaa na kumsikiliza Malkia Sara.

    "nadhani kila mmoja wenu anajitambua kuwa yeye amezaliwa kwa mazingira gani na ndio maana hadi sasa anapitia mitihani kadhaa maishani mwake kubwa hasa ni kuhusu hofu iliyopo kwenye mioyo yetu juu ya maadui wanao tuzunguka,mmekuwa mkinitegemea kwenye mambo mengi yanayo watokea,itafika mahala nitakuwa mbali mmoja wenu atapata tatizo ikawa ni hatari sana tukajikuta kunapungua kwa kutegemea msaada sehemu moja,sasa ili kuondoa hili nilikaa na wazee wa falme hii nikawaomba wafanye jambo ambalo linaweza likatusaidia wote,lengo hasa nikawataka wafanye mpango wa kuwapatia nguvu ya kujitegemea kila mmoja wenu muwe kama sisi ili muweze kujilinda."alisema maneno hayo Sara na kuwafanya wenzake wafurahi kusikia hivyo,ni Denis tu aliyeonekana kutofurahia wazo hilo hali iliyomfanya hata Natasha amshangae.

    "basi jambo lenyewe ndio hilo nililo waitia lakini nguvu hizo zina masharti ambayo sasa nitahitaji kila mmoja wenu aseme kutoka moyoni mwake..."maneno hayo yaliwafanya washangae kusikia kuna masharti,wakamtazama Sara kumsikiliza kwa makini.

    "nilipo waambia wazee kuhusu hili wakasema linawezekana lakini inampasa kila atakaye patiwa nguvu hizi maisha yake yawe ni ya huku huku,ataishi kwenye falme hii pasi na kurudi duniani."alisema Sara na kuwatazama wenzake ambao walibaki kushangaa huku wakitazamana tu,kila mmoja alikuwa kimya na kubaki kuangalia tu chini akitafakari mara mbili mbili kuhusu swala hilo maana sio la kukurupuka kuamua.Kwa Ester yeye hakuwa na shaka maana alishaamua tokea siku ile alivyoambiwa na Sara na kuona ni bora kukaa huku kwenye falme akiwa amejizatiti kwa nguvu za ajabu aanze maisha yake ya amani na sio kukaa duniani kwa mashaka,haikupita hata dakika tatu Denis alisimama na kumtazama Sara.

    "nilizaliwa duniani,nitaishi na nitakufa duniani,kamwe siwezi kuja kukaa huku,kama umechoka kutusaidia useme na sio kutumia triki hiyo ya kutuleta huku tuishi,tutawaeleza nini wazazi tunao ishi nao pindi tukiamua kuja huku,hapana kwangu hilo mimi siwezi na sipo tayari"alisema Denis na kuwafanya wenzake washangae kwa majibu yake,akasimama Ester

    "mimi sioni sababu ya mtu kukataa hili swala,kumbukeni hili swala ni kwaajili yako mwenyewe,kumbukeni pia mmoja wa wazazi wako alitokea huku,alikuwa akiishi huku na ikatokea muda wakashuka duniani na kuweka mahusiano na binadamu ndipo tukapatikana sisi tutamtegemea Sara mpaka lini,yeye pia ni binadamu kuna matatizo yanaweza kumkuta,akazidiwa kwamfano na kupoteza maisha,nani atatusaidia sasa wakati tumekataa wenyewe kupokea nguvu hizi,au mmeridhika kuendelea kusumbuliwa kila kukicha na wasuriati wanao ongozwa na Michael?hapana mimi napinga unayosema Denis na hupaswi kumsema Sara wakati amefanya hivi ili atusaidie,mimi niko tayari hata sasa kuwa huku ili niish kwa amani"alisema Ester kwa msisitizo akionesha kudhamiria kweli,maneno yake yakamfanya hata Magreth akubaliane na maneno ya Ester."amani ndio kila kitu katika maisha na nakubaliana na Ester,nitaishi huku"alisema Magreth na kuwafanya Ester na Sara wafurahi,wakamtazama Natasha naye ambaye alikuwa ametizama tu chini akiendelea kutafakari.

    Maongezi waliyokuwa wakiongea yalimshtua sana Michael kule alipo na kukumbuka siku ile alipofuatwa na Ester ambaye alikuja kwa kujiamini na kusema yeye ndio amewaua wale wafu waliotumwa na Michael siku ile ambayo alikimbizwa na kudondoka,alitoke Sara kwa umbo la Simba na kuwaangamiza wale wote,hivyo akaja kumdanganya Michael kuwa yeye Ester pamoja na wenzake wana nguvu kama alizonazo Sara,hali iliyomshtua Michael akaamini kuwa ni kweli kumbe alidanganywa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ina maana alinidanganya siku ile,kumbe hawana hata nguvu nakaa naumiza akili siku zote kuhangaika na Sara wakati hawa wapo"alisema Michael na kuanza kutambua kuwa laiti Denis angekuwa na nguvu kweli asingeweza kumuwekea uchawi kwenye ule mkate,alikasirika sana kuona amedanganywa vile akabaki akimtazama tu Ester kwenye lile beseni la kichawi kwa hasira,muda ule kule kwenye falme Natasha alinyanyuka na kuwatazama wenzake ambao walibaki kumsikiliza.

    "kama Mungu amenipangia kuwa nitakufa Mara basi hata niende wapi haitasaidia,nitabaki tu duniani na wala sitohitaji chochote."alisema Natasha na kuwafanya wenzake washanga e,hata Michael naye alishangaa kusikia uamuzi ule wa Natasha maana yeye ndio anampelekesha Denis hadi kukataa kuishi kule kwenye falme akijua fika wakiwa kule watapata nguvu na kuwa kama yeye akashindwa kuwamaliza.Natasha alimtazama Denis kwa tabasamu,alimpenda sana Denis na ndio maana alipoona Denis amekataa kuishi kwenye falme akaona ndio muda pekee wa yeye kumpata Denis maana Sara,Magreth na Ester watakuwa huku kwenye falme,hakika kauli yake iliwafanya wenzake kujiuliza maswali mengi na kujikuta kunatokea pande mbili za kuto kuelewana baina yao wenyewe.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog