Simulizi : Sara (Msaada Wa Mateso)
Sehemu Ya Tano (5)
Maamuzi yale yalimfurahisha sana Michael na kuona hata Natasha naye anaweza kumsaidia kwenye mambo yake.Basi malkia Sara akalazika kusitisha kikao hicho baada ya kutoafikiana baina yao,walirudi zao duniani kila mtu akiwa ameongea kile alichokiona kinafaa kwa upande wake.Jambo lile likawa limekaa moyoni kwa kila mmoja wao pindi walipofika majumbani kwao kuanza kufikiria kwa kina zaidi,Natasha usiku huo alikuwa akitabasamu tu kwa kuona kupitia njia hiyo ya kubaki duniani na Denis anaweza akamshawishi kwa wepesi na kutimiza lengo lake.Huku Sara muda wote alikuwa akiumiza kichwa kuona kumekuwa na kutokuelewana na baadhi ya wenzake Denis na Natasha,alitafari ni njia gani atumie kuwaelewesha ili wakubali,nia na lengo lake ni kutaka kila mmoja awe huru kwenda popote pale akiwa na nguvu zake mwenyewe pindi atakapopatwa na jambo,aliendelea kutafakari hadi usingizi ukamchukuwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kesho yake wakiwa shuleni Magreth alimfuata Natasha na kumuona yupo darasani hakukuwa na mwalimu,aliingia hadi mule na kukaa karibu na Natasha wakawa wanaongea wenyewe.
"lakini ujue kuwa yale ni maisha yako Natasha,unajisaidia mwenyewe na yule naye ana maisha yake,wewe unakata kupata msaada wa nguvu ukabiane na mabaya unakataa kisa mtu aliyekwambia hakutaki,sasa una uhakika gani kama yeye atakupenda baada ya kukataa kuishi kule!"alisema Magreth akiwa amekuja kwa lengo la kumshawishi Natasha.
"Magee eh,mbona unaongea sana wakati nishaamua mambo yangu,we acha tu mambo yaende kama yalivyopangwa,mkienda nyie kuishi kule na Sara nitapata uhuru wa kuwa karibu na Denis,hicho tu ndicho ninacho kitaka mimi na si vingine"alisema Natasha akiwa hana wasi.
"hivi Natasha unaongea umedhamiriaaa umerogwa!maana unaongea upuuzi ujue,nilikuwa nakushaurh kuhusu kumpata Denis lakini kwa jambo lililo jitokeza yakupasa uangalie kwanza maisha yako,kama umepangiwa kuwa naye hata ukiwa huko utakuwa naye tu Natasha hebu amka ulipolala"
"hee Mage, haya nafanya ili nimkwepe Sara maana akiwa karibu na Denis ndio wanazidi kuniumiza,ni bora yeye akaanza maisha ya kimalkia amuache Denis huku niwe naye."alisema Natasha na kumfanya Mage ashindwe hata kuongea,alichoka baada ya kuona mtu anayetarajia kumuelesha ndio kwanza ameshikilia msimamo wake,alichoamua Mage ni kunyanyuka na kuondoka zake akimuacha Natasha pale darasani.Moja kwa moja akarudi zake darasani na kukaa mahala pake,Ester na Sara walimfuata na kutaka kujua kilichoendea maana walimtuma Mage makusudi kwakuwa ni rafiki wa karibu na Natasha.
"amekataa katakata,hataki kusikia habari ya kwenda huko,nina mashaka naye Natasha hawezi kuwa mbishi hivi"alisema Magreth na kuwafanya wenzake wachoke kusikia bado kuna kazi.
Walirudi kukaa sehemu zao wakiwa na wamechoka kusikia kuwa Natasha amekataa.Basi masaa yalisonga mbele na muda fulani wanafunzi wakiwa nje Sara alimuona Denis akiwa amekaa mahala pekeake,taratibu akaamua kumfuata walau amshawishi akubali kupata nguvu zile,akiwa anamkaribia huku nyuma Natasha alishuhudia jambo lile na kujikuta akikasirika kuona watu hao wawili bado wana ukaribu.Sara alikaa pale wakawa wanapiga stori za hapa na pale na Denis ambaye hakuonesha kuchukia kabisa maana bado ana upendo kwa Sara.
"hivi unajua rafiki bora anayekupenda na kuyajali maisha yako ni yule anaye kuelekeza pale unapo kosea ana kusahihisha,na pale unapofanya vema ana kusifia kwa kile ulicho fanya,..Denis kile tunacho kueleza kipo sahihi yatupasa kila mmoja wetu aweze kujilinda mwenyewe,mimi sasa ni Malkia hivyo nitakuwa na kazi nyingi za kijamii napaswa kuzifanya hivyo sitoweza kuwalinda na nyie kila wakati kama ilivyo awal i,tafadhari hebu kubali tufanye jambo hili kwa pamoja Denis,wewe ndio unapaswa uwe mbele kama mwanaume uoneshe mfano"alisema Sara.
"Sara hebu nielewe,mimi kule siwezi kuishi nimezaliwa huku Mara na nitazikiwa huku,nyie kama mtaenda nendeni tu mimi niacheni."alisema Denis kwa kujiamini,Sara akabaki kumtazama tu Denis,alishangaa sana kuona ubishi wa Denis umetokea wapi hali ya kuwa hakuna na hali hiyo,moyoni akapata wasi wasi juu ya Denis,hakumwongelesha chocite akageuka nyuma na kuondoka zake.Alimtafuta Ester wakakaa mahala na kuongea.
"nimetoka kuongea na Denis naye amekataa katakata ila kuoa kitu nakihisi nimepata mashaka nacho,mpaka leo Michael hajarudi shule maana nilipata kuulizia nikaambiwa ameaga anaumwa,na ninavyo mjua Michael hawezi kuwa kimya kwa muda wote huu lazima atafanya jambo,na huenda kama sio Denis basi ni Natasha atakuwa anatumiwa na Michael ili afahamu tunafanya jambo gani."alisema Sara.
"sasa hapa tunatakiwa kufanya jambo kuhakikisha wenzetu wanarudi kwenye hali ya kawaida"alisema Ester na kuwafanya wenzake waanze kuumiza kichwa kutafakari namna ya kuwasaidia wenzao na baada ya muda Sara alipata wazo na kuwashirikisha wenzake.
"hapa sasa tufanye kitu ili kukamilisha zoezi hili,na huu ndio uwe mwisho wa Michael kabisa na wasuriati,..Ester...Magreth...tunaingia vitani sasa kila mtu aweke hilo moyonh mwake,kama sisi watatu ndio tumekubaliana kuishi kule basi tufanye hili kama sisi kisha tuje kuwasaidia na wenzetu,tukitoka leo shuleni safari ni kwenye falme,mkafanyiwe maombi maalum za kuwajaza nguvu za ajabu ili kusudi tuwe na nguvu za kuwamaliza adui zetu,na kabla hatujaenda tuwaambie wakina Denis na Natasha kuwa tumegairi tutaishi huku wote."alisema Sara,alichokisema kiliwaingia akilini wenzake na kuona ni bora iwe hivyo,wakasogeleana na kukumbatiana kama kukubali kufanya jambo hilo kwa pamoja.Basi walirudi na kuendelea na kusoma na baada ya masaa kupita muda wa kuondoka wanafunzi kama kawaida yao waliongozana wote watano kuelekea makwao,njiani walikuwa wakipiga tu stori za kawaida tu na walipofika mahala Sara ikambidi aongee.
"unajua siku zote umoja wetu ndio furaha kwetu sasa tunapokwenda tofauti na kutokuelewana baina yetu inakuwa sio vizuri kama tumeamua kufanya jambo kwa pamoja hebu tulifanye wote,Natasha na Denis.. Hebu tumalizeni jambo hili jamani kwa faida yenu wenyewe"alisema Sara.
"jamaniee mimi nilishakataa tangu mwanzo na siwezi full stop"alisema Denis akiwa anatumiwa na Michael ambaye muda wote amekuwa anaendelea kuwasikia tu mazungumzo yao,hata kwa Natasha majibu yalikuwa hivyo hivyo wakionesha msimamo wao.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sara,mimi naona haina haja ya kubishana wenyewe,tuache tu hili jambo lipite tuishi na wenzetu kwa amani,tutavumilia tu kitakacho tokea"alisema Ester na kuwafanya wakina Natasha washangae kusikia hivyo,hata Michael kule alipo alistaajabu kusikia hivyo,alijikuta akitabasamu na kusikia raha kuona hata Ester naye anajitoa kwenda kwenye falme.
"si ndio hapo bwana,tumekuwa tukiishi vizuri tu na kama matatizo yanayo tokea tunasaidiana tu hivyo hivyo maisha yanaenda."alisema Denis akimuunga mkono Ester,hata Magreth naye akaamua kukubaliana nao tu,Sara kuona vile akaamua tu kusitisha mpango ule.
"basi sawa kama tumeamua hivyo tutakuwa wote kama awali,tusameheane tu kwa yale yaliyo tokea mwanzo sisi nh kama ndugu tuendelee kupendana"alisema Sara huku akimtazama kwa makini Denis akionesha kutabasamu.
"safi sanaaaa"alisema Michael kwa sauti ya juu kule alipo lakini sauti yake ikapenya masikioni mwa Denis ambaye alihisi maumivu yaliyo mpelekea kuyaziba masikio yake,hali ile ilimfanya Sara atambue kuwa ni Denis ndiye aliyeshikwa na kutumiwa na Michael.Lakini kwa Natasha jambo lile la wakina Sara kugairi jambo lao lilimkera sana,hii ni kutokana na wivu wake wa mapenzi juu ya Denis na kuona ukaribu wa Sara na Denis utazidi kuendelea,alijikuta akimchukia Sara bila sababu.Basi walimaliza tofauti zao kwa kuamua kuwa pamoja,walipofika kijijini kwao waliagana kila mmoja akaelekea makwao.
Basi jioni ile Sara alikuwa akiongea na baba yake mzee Junior akiwa amemshirikisha kwenye mambo waliyokuwa wamepanga na wenzake.
"wewe ndio unayepanga Sara,wewe ndio malkia kuwa na maamuzi kama kiongozi,mtu kama Michael anakusumbua kiasi hiki wakati una uwezo wa kumdhibiti lakini unaacha mpaka analeta madhara mengine,kuwa makini mwanangu jitambue,wewe sio Sara tena bali ni Malkia,una kazi ya kuwaongoza watu zaidi ya maelfu huko uendako"alisema mzee Junior akimuelewesha mwanaye.Maneno yake yakamfanya Sara apate ujasiri mwengine wa kujiona ni mkubwa kimadaraka,baada ya muda kupita waliwasili Ester na Magreth pale na kumfanya Sara anyanyeke pale sebuleni akiwa na baba yake.
"haya basi baba,siye ngoja twende muda umefika."alisema Sara na kumfanya mzee Junior awape ruhusa waende salama.Sara aliingia na wenzake chumbani kwake kama kawaida walishikana mikono huku Sara akisema maneno fulani na gafla tu wakap otea na baada ya muda wakatokea kwenye meza kuu kule kwenye falme.Waliona kundi la wazee likiwa linawangoja pale hivyo walipofika tu moja kwa moja wakachukulia na kupelekwa moja kwenye chumba maalumu cha maombi,Ester na mwenzake Magreth walipata wasiwasi huku miili yao ikitetemeka wa woga pindi walipoingia kwe chumba kile na kuona jinsi kilivyo pangwa vitu vya kiasili,mafuvu ya watu yakiwa yamewekwa kwenye kila kona ya chumba kile,mbele kuliandaliwa viti viwili vya chuma ambavyo wazee wale waliwaamuru Ester na Magreth wakakae kila mtu kiti chake.Basi walifanyanya hivyo kama walivyo ambiwa,kila mmoja akakaa kwenye kiti chake huku Sara akiwafuata pale walipo.
"msiwe na wasi rafiki zangu na muwe wavumilivu,kuna maombi yatafanyika hapa mara moja tu hapa na mkitoka hapa mtakuwa wapya tena."alisema Sara kwa kunyenyekea akiwapa moyo wenzake wakapata ujasiri kweli,Sara akasegea pembeni na kuwapisha wale wazee wen ye madaraka na uwezo wa kuziachia nguvu za ajabu,wakisogea pale kwenye vile viti walivyokaa wakina Mage na kuanza kuwashika shingoni hadi kwenye mishipa masikio ambapo waliiminya gafla na kuwafanya wapoteze fahamu,wazee watatu walikuwa kwa Mage na wengine watatu wakawa kwa Ester,walichukua kamba na kuwafunga miguuuni na maombi yakaanza muda ule,kila mmoja akawa anaingiza nguvu zake kwenye miili ya mabinti hao huku wakiongea maneno ya kichawi,mikono yao ilitoka miale ya mwanga ikizidi kuzama mwilini mwa akina Ester na mwenzake huku Sara akiwa pembeni anashuhudia zoezi lile na kubaki kuyakumbuka maneno ya baba yake yaliyomfanya azidi kupata ujasiri,alikumbuka kifo cha mama yake kikisababishwa na wasuriati na kuona kweli haina haja ya kuwa mpole kwa jambo hili,hali ya kuwa wanaumia kila muda,aliwatazama wakina Ester pale walipokaa na kushuhudia wakitokwa na jasho jingi,gafla tu wakafumbua macho yao yakioneka na makali sana kama paka,hali ile ilimfanya Sara atabasamu kuona wenzake wamekuwa tayari na nguvu zile.Basi alitoka zake nje na kuwaacha wazee wakimalizia kazi yao.
Huku duniani Michael baada ya kupata habari mpya kuwa wakina Sara wamepuuzia swala la kwenda kwenye falme kuwasaidia wenzake kupata nguvu,hivyo kazi kwake ikawa ni rahisi ni kuamua tu aanze na nani,safari hii naye alijipanga kuhakikisha ana wamaliza wote,alijiamini kuona tayari Denis ameshamteka kiakili hivyo alichokifikiria ni kumtumia na Natasha ambaye ameonesha kumpenda Denis kiukweli.
"hii kazi nitaifanya kesho nikiwa shuleni,sitaki nipoteze hata pointi moja kwa hili."alisema Michael akiwa chumbani kwake usiku ule akidhamiria kweli jambo lake.
Kule kwenye falme baada ya mambo yote kukamilika walionekana wakina Ester na mwenzake Magreth wakitoka kwenye kile chumba wakiwashikwa na kupelekwa chumbani kupumzika kwanza,Sara aliwafuata na kukaa nao kidogo waongee,aliwatazama machoni na kuona bado wana macho ya kutisha,aliwachukua na kuwapeleka kwenye kioo wajiangalie walivyo kwa sasa.
"hivo ndio muonekano wenu kwa sasa pindi ukiwa na hasira,hivyo yawapasa mzuie hasira zenu mbele ya macho ya watu,na muelewe kuwa mmepewa nguvu hizi ikiwa ni moja ya sababu ya kuitokomeza kabisa jamii ya wasuriati ambao wamekuwa wakituandama kila kukicha na ninaamini tukifanya hili kwa pamoja tutashinda"alisema Sara akiwapa maelezo wenzake juu ya nguvu zile,walimuelewa na taratibu wakapoa maana walitoka kwenye kile chumba wakiwa na maumivu makali,Sara alinyoosha mikono yake kuwapa wenzake,walishikana tayari kwa kuanza safari ya kurudi duniani.
"ina maana tutaishi duniani tena au tutarudi huku?"aliuliza Magreth na kumfanya Sara atabasamu tu,alitamka maneno fulani na papo hapo wakapotea kurudi duniani bila kumjibu Magreth.
Huku kwa Michael alionesha na tumaini jipya hasa baada ya kujua kuwa ameanza kuwavuruga kundi lao na kuhakikisha wote wamekubaliana kuishi kama awali,alijivunia kumuendesha Denis vile atakavyo na sasa Natasha amejisogeza mwenyewe kwa kumpenda kiukweli Denis akaona nayeye amjumuishe awe wawe wawili hibyo hawatamsumbua,akapanga jambo usiku ule ambalo aliona linaweza kumuweka Sara pabaya pindi akimtumia Natasha.
Siku hiyo Denis alikuwa mahala amefungwa kamba na Sara aliye onekana kubadilika kwa hasira huku akiwa ameshika kisu kikali,pembeni walikuwa wakina Eater na Magreth wakimtazama tu Denis lengo lao akubaliane nao.
"nikiwa mimi kama Malkia wenu nina amri ya kusema ufanye jambo na wewe ukalitekeleza,sasa nakupa nafasi ya mwisho uamue,unakubali kwenda kuishi kule kwenye falme?"aliuliza Sara huku akimtazama Denis ambaye alionekana damu zikimtoka mdomoni kwa kupigwa,alicheka sana kwa dharau huku naye akimtazama Sara.
"sikia nikwambie Sara,uwe ni Malkia uwe rais uwe sijui mtu gani kamwe huwezi nipeleka kule nikaishi ni bora uniue tu hapa nijue moja,niue...niue tu na sio kunilazimisha mimi nifanye kitu ambacho sikitaki,nyie nendeni mtaniacha mimi na Natasha wangu na kwa kuwa nampenda na yeye ananipenda tutaishi kwa furaha,na kama ukiniua mimi basi kamuue na Natasha kabisa maana utakuwa umeanikisha azma yakobya kutumaliza sisi tuliokataa amri yako...tuuweni tu wala msisite kufanya hilo,maana hatutokubali kwenda huko mnapotaka twende,niue tuuuu"alisema Denis na kumfanya Sara atambue kuwa kweli Denis ameamua,alinyanyua kisu chake huku akimtazama Denis kwa hasira.
"haya sawa kama umeamua hilo itakuwa vizuri,wacha nikutangulize wewe halafu huyo Natasha wako atafuata,wasalimie huko"alisema Sara na kumchomeka kisu cha tumbo Denis ambaye alipiga kelele za maumivu,wakina Ester na mwenzake Magreth wakawa wanatabasamu tu kuona vile.................
"DENIIIIIS"alikurupuka Natasha kitandani na kuanza kutazama huku na kule kwa hofu,mapigo ya moyo yakawa yanamwenda mbio usiku ule,ilikuwa ni ndoto akiota Denis anauliwa kikatili na Sara kisa tu kugoma kwenda kuanza kuishi kule,ndoto ile aliitafakari sana na kuanza kuiweka moyoni akijua huenda ikawa ni ujumbe wa kweli halafu akaudharau,alikumbuka mchana wakitoka shule kuwa walikuwa hawaelewani kati yao na wakina Ester waliokubali kuishi kule na gafla tu wakagairi kwenda kule na kuungana na wenzao kuamua kuishi kama mwanzo,jambo lile likampa mashaka Natasha na kuona hapa kati kuna jambo na laweza kuwa ndio kweli ndoto hiyo hiyo ikawa ninkama ujumbe kwake,alipata mashaka sana na kuona kuna haja ya kufanya kitu kabla ya jambo hili halijatokea kweli japo moyoni alishaanza kumchukia Sara na kuona ndio sababu ya mambo yote haya,alirudi kitandani na kuanza kuutafuta usingizi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Michael alibaki akicheka tu akiona jinsi anavyo watumia watakavyo,ni yeye ndiye aliye tengeneza ndoto ile na kuipandikiza kichwani mwa Natasha na kumfanya apate wasiwasi na ndoto ile,alifanya hivyo kusudi tu akijua kwa hasira atakazo kuwa nazo Natasha kwa kumpenda Denis lazima akayaongee maneno haya hadharani hali itakayo wafanya wanfunzi waluokuwa wakimjuwa Sara kwa jina la Sasha wataupata ukweli siku ya kesho,basi alipohakikisha ameshamlambisha sumu hiyo Natasha na yeye akarudi kitandani kupumzika.
Kesho yake Michael aliwasili shuleni huku akiwa na uhakika wa kufanya jambo lake alilo lipanga,alipanga siku hiyo kufanya jambo kubwa ambalo litamfikisha mahala pazuri yote ni kuhakikisha anammaliza Sara ambaye amemfanya akose kuitawala jamii ile kuwa Mfalme wao,hivyo alitaka kuhakikisha atatumia njama yeyote kumteketeza Sara,alijiaminh kwa kuona amempata Denis na kumtumia vile atakavyo.
Huku kwa Natasha akiwa darasani alionekana kuwa na wasiwasi,hii ni kutokana na ile ndoto aliyo ota jana usiku kuona Sara amemchoma kisu cha tumbo Denis na kumfanya adondoke chini huku damu zikimtiririka,alijuwa tu kwa vyovyote huenda ni kweli akafuata na yeye kwa sababu wamekataa kuwa pamoja na wenzao,hali ile ikamfanya akose hamu ya kuwa darasani akatoka moja kwa moja kuelekea darasa la akina Denis,alipokuwa akipita Michael alimuona akiwa zake darasani na kubaki kutabasamu tu akijua kinachoenda kutokea.Natasha alipofika na kuhakikisha hakuna mwalimu akaingia na moja kwa moja akamfuata Sara pale alipo akionesha kuja kwa shari,Sara alipoangalia tu Natasha akajua hakuja kwa wema,alipo tazama pembeni na kuona hakuna mwanafunzi anaye watazama akanyanyuka na kumshika mkono Natasha wakaongee nje lakini cha ajabu Natasha akaukataa mkono wa Sara na kubaki kuangaliana tu,jambo lile liliwafanya wakina Ester na Magreth wabaki kuangaliana wakijiuliza kumetokea nini.
"ina maana tulivyo kubaliana kumbe hamkuridhikaee?"alisema Natasha kwa sauti na kufanya darasa zima liwe kimya wakigeuka kumsikiliza anaye ongea,Sara alivyoona kuwa Natasha anaweza akaropoka mambo yote ikawa kesi kubwa kwa kufichua siri zao,na pale alipo ni mbele kila mwananzi alikuwa akitazama kusikia anayo yasema Natasha ikamfanya Sara ashindwe kuonesha uwezo wake mbele za watu,muda huo huo Denis alinynyuka na kusogea pale walipo simama."
"Natasha kwani vipi,nini kimeto kea"aliuliza Denis lengo ni kutaka Natasha aongee,jambo lile liliwafanya wakina Magreth watahaluki na kuona anaweza Natasha akaropoka mambo yao,Ester aliamua kutumia nguvu alizo nazo kumfumba mdomo Natasha asiongee,huku Michael naye akiwa anangojea tu kusiki Natasha anavyopayuka maneno lakini alishangaa kuona kimya,akaamua kutoka darasani na kwenda kuangalia kumetokea nini.Na kweli Natasha alijitahidi aongee lakini akajikuta anashindwa kusema kabisa na kuwafanya wanafunzi wamshangae wasijue nini kimemkuta,hata Sara mwenye alipoona hali ile ikamfanya atambue kuwa kuna nguvu zimetumika hapo na kubaki kutabasamu.Michael alifika darasa lile na kuishia nje dirishani akapata kuona tukio lile,cha ajabu alimuona Sara akiwa pale mbele amesimama na Natasha hvyo isingekuwa rahisi kwa yeye kutumia nguvu za kichawi pale mbele,akawa anajiuliza inawezekana vipi swala lile maana hakuna mtu mwenye nguvu zile zaidi yao waw wili,lakini alipopiga macho kwa wanafunzi alipata kumuona Ester akiwa anamtazama Natasha kwa macho makali hali iliyomfanya Michael asiamini anachokiona,na muda huo huo Natasha baada ya kutoielewa ile hali aliamua kugeuka na kuondoka zake huku moyoni akiwa na dukuduku kuhusu Sara kwa kuihisi ile ndoto kuwa yaweza kuwa kweli,Denis kuona vile naye akatoka kumfuata Natasha wakimuacha Sara akiwa pale amesimama.Hakuna mwanafunzi yeyote aliye elewa lolote linalo endekea wakaamua kuendelea na mambo yako,hata Ester baada ya kazi ile alirejesha macho yake ya awali huku akitabasamu akiangaliana na Sara baada ya kusaidiana kwa jambo hilo,lakini kwa yale yaliyo tokea Sara akapata kutambua jambo.Michael pale nje ndipo akapata kujua kuwa Ester naye ni miongoni mwa viumbe kama wao,alikasirika sana kuona Sara anapata nguvu ya msaada mwengine,akageuka na kurudi zake darasani
Muda huo Natasha alikuwa amesimamishwa na De nis.
"Natasha mbona umenyamaza hukuongea pale!"aliuliza Denis na kumfanya Natasha amtazame usoni.
"sikuweza kuongea,nilijitahidi lakini nimeshindwa Denis."alijibu Natasha na kumfanya Denis abaki kutafakari.
"Denis...lakini kwanini unanifanya nahangaika kwaajili yako,nakuwa na mashaka na maisha yako muda wote lakini wewe hata hujali kuhusu hili,nimepata kuota usiku wa kuamkia leo kuwa...wenzetu hawapo pamoja na sisi na kwa kuwa tumekataa basi watatuua."
"ati nini?"
"ndio hivyo Denis,na ndio maana nikaingia darasani kwenu na kumfuata Sara kumueleza ukweli wa kile wanachotaka kutufanyia lakini nashangaa kuona nashindwa kuongea,hii inanipa wasiwasi huenda ikawa kweli."alisema Natasha na kumfanya Denis atambue jambo,alimtazama Natasha kwa namna ya kipekee na taratibu akamsogelea pale aliposimama na kupeleka kinywa chake kwenye mdomo wa Natasha na kupeana radha ya mate yao kwa muda kisha akamuacha.
"usijali ha kita tokea kitu kwetu wakatudhuru,tutaishi huku huku duniani kwa amani"alisema Denis na kumfanya Natasha atabasamu,kwa busu aliloonjeshwa ndio kabisa akazidi kumuamini Denis na kuanza kujipa matumaini na kuwa naye kimahusiano.Basi waliagana na kurudi madarasani kila mtu na vipindi vikaendelea.Baadae Sara alikaa na wakina Magreth muda ambao wanafunzi walitoka kwenda kunywa chai,kwa mambo yaliyo tokea kila mmoja alikuwa na mawazo yake.
"yaani kama ndio kupenda kupiliza basi Natasha amekuwa chizi kabisa,na vile kafanya kusudi akijua huenda ukawa na mahusiano na Denis"alisema Magreth baada ya kujua kuwa Natasha amekuwa na wivu kwa Sara.
"ina maana hawatuamini tena,au wamejua kuwa tulienda kule maana kaingia tu na kumwambia sara kuwa tulivyokubaliana hatukuridhika!"alisema Ester.
"sikileni niwaambie kitu,Denis na Natasha sio wenzetu kwa sasa,na msikae mkapanga mambo yenu mkawashirikisha,wenzenu wametekwa zaidi tulikuwa tukimhisi mmoja kati yao lakini nimewatazama tu nikajua kuwa ni wote wanatumiwa na Michael,na anafanya hivi kusudi ili atuweke mbalimbali tusielewane,kwa hili sitakuwa na huruma hata kidogo nitaonesha umbo langu halisi la Sara"alisema Sara na kuwafanya wenzake wamuunge mkono kwa hilo kuonesha wako pamoja.
Michael alikuwa pembeni tu anawatazama bila kujua wameongea jambo gani,akaona kuwa wale ndio wanao msumbua,akapanga namna ya kuwadhibiti ili wasiharibu mpango wake.
Wakiwa pale wanaongea mambo yao Sara alipata wazo na kuona litafaa ikambidi awashirikishe na wenzake ambao waliona linafaa,muda huo huo Sara akatoka zake na kumfuata Natasha akionekana ametulia mahali,alimsalimia na kuanza kumuongelesha.
"nisamehe sana ndugu kwa yale yaliyo tokea,ila nimekuja nikueleze tu ukweli,NAMPENDA DENIS kupita maelezo japo nilikuwa namkatalia mara kibao akinitongoza,lakini nimeona kweli ana upendo wa dhati kwangu na leo nimepanga kumwambia ukweli huo na nahisi leo nitakuwa naye muda mwingi tukiongea mambo yetu"alisema Sara na muda ule ule kengele ya kuingia madarasani ikalia na kumfanya Sara amuage Natasha kumwambia wataongea vizuri,aliondoka huku akitabasamu tu akimuacha Natasha akimtazama kwa hasira na dharau,maneno yale yalimchefua sana kusikia leo Sara anamkubalia John,hata Michael kule alipo alipata kuyasikia maneno ya Sara kwakuwa anamtumia Natasha pia kwa mambo yake,alistaajabu kusikia hivyo na kubaki aki cheka tu mwenyewe maana hakuamini Sara yule aliyekuwa akishikiria msimamo wake leo amekubali mwenyewe.
Na kweli Sara alipofika darasani alielekea moja kwa moja kwa Denis aliyekuwa amekaa pekeake.
"mambo jembe"alisalimia Sara na kumfanya Denis atabasamu.
"poa tu vipi Sara"
"powa tu ila nimekuja nikuombe kama leo tukitoka ukiwa na nafasi tuonane mahali tuongee mambo yetu sish wawili,ukiwa tayari utanishtua basi"alisema Sara kwa sauti ya kushawishi na kumfanya Denis astaajabu kusikia maneno yale,hakutaka kukaa sana akageuka Sara na kwenda sehemu yake kukaa huku akitabasamu.
Kitendo kile kilimshangaza Michael kuona Sara amejirahisisha kiasi hicho,kwake ikawa ni furaha na kuona ni muda wa kukutana wawili hao ndio atakao utumia kummaliza Sara,huku napn mawazo ya Sara yalikuwa mbali na kuamini kuwa ndio njia pekee ya kumuanza kumtoa Denis kwenye mikono hatari ya Michael,na upande wa Natasha ile kauli ya Sara ili mtibua kabisa.
"siwezi kukubali kijinga kumuacha Denis,Sara anataka kumshawishi tu ampeleke kule ni kitu ambacho sitakubali kama Natasha,nitaliingilia swala hili siwezi kunyamaza"alisema Natasha akiwa kwenye dawati lake.
Basi muda wa kuondoka wanafunzi ulifika na kila mtu akaongoza njia kurudi makwao,,kama ilivyo ada Sara na wenzake waliongozana pamnja njiani huku wakiongea mambo mbalimbali,siku hiyo walishapanga kabisa kufanya jambo kwa Denis lengo ni kutaka kumuondoa utumwa ule kwa Michael bila yeye kujua,lakini jambo hilo ililchukua sura mpya kwa Natasha ambaye alikuwa akihisi vengine juu ya upendo wake kwa Denis.,sasa kitendo cha Sara kupanga kumweleza Denis kuhusu upendo wake kilimfanya Natasha ahisi wivu hali ya kuwa tayari Denis ameshaanza kuonesha uelekeo wa kuwa naye,akapanga kuhakikisha jambo alilopanga Sara lisitimie,nao wakina Ester walishaelewa jambo analofanya Sara hivyo wakamuacha huru kidogo kuwa karibu na Denis wakiwa njiani wanatembea jambo Natasha hakuliafiki na kuamua kuwa karibu nao asimpe nafasi kabisa Sara,Magreth na Ester wakabaki kutabasamu tu wakijua yote ni wivu wa mapenzi ndio unao msumbua Nata
sha hadi kufanya vile,walichokifanya ni kumsogelea huku wakiwa wanaenda na kuanza kumuongelesha mambo kadhaa wakimchanganya asielewe kinacho ongelewa,na kweli Sara wakaelekezana mahala pa kukutana baadae kawa walivyoahidiana.Hata walipofika kijijini kila mtu akaongoza njia yake ya kuelekea makwao,huku Michael akiwa na hamu ya kujua atakacho ongea Sara baada ya kukutana na Denis hapo baadae.Basi jioni muda ulipofika Denis alielekea eneo ambalo walipanga kukutana na Sara,kulikuwa na giza mahali hapo ambapo hakuna yeyote anayeweza kuwafahamu haraka,na kweli baada ya muda Sara aliwasili pale na kukaa mahali wakawa wanaongea.
"naaminh leo utaniambia maneno ya kunifanya nifurahi,haya nakusikiliza"alisema Denis akiwa anategemea jambo zuri kutoka kwa Sara.
"mh una harakaaa,"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"lazima niwe na haraka maana kusubiria kitu ambacho hukijua inakupa hamasa ya kujua kitu gani"
"ok sawa,nimekuta tukutane kuna jambo nataka
tulionge,.."alisema Sara na kumfanya Denis awe makini kumsikiliza. "maneno yako uliyokuwa unaniambia kila tukikutana najaribu kuyasahau lakini nashindwa,tangu siku ile nimekuwa nikiisikia sauti yako masikioni mwangu na kuanza kuingiwa gafla na kitu moyoni kuhusu wewe,sikuwahi kupenda mwanaume maishani mwangu na wala sikufikiria kabisa,lakini najikuta nashawishika gafla yani hata sielewi"alisema Sara akiwa mwingi wa aibu,moyoni Denis alijikuta akiona mwenye bahati kuona kweli amefanikiwa kumshawishi Sara,Michael kule alipo alijipigia makofi mwenyewe baada ya kuona sasa anaelekea kwenye mafanikio anayotaka.
"Sara,niamini mimi Denis kwa yale niliyokwambia,nakupenda sana na ndio maana sichoki kukueleza hisia zangu."alisema Denis akizidi kushindilia msumari,Sara alimtazama Denis kwa macho ya kushawishi.
"Denis,hutanisaliti kweli wewe?"
"siwezi,na sijui nitaanzia wapi kufanya hivyo maana hata moyo utanisuta kwa hicho kitendo,niamini kwa haya ninayo kwambia"alisema Denis huku akimtazama Sara aliyeonekana kuangalia chini,alinyanyua uso wake kumtazama Denis.
"naomba usiniumize Denis ukanifanya nijute kupenda mwanaume,wewe ndio mwanaume wangu wa kwanza maishani mwangu"
"usijali Sara,siwezi kukufanya uumie"alisema Denis na kumfanya Sara aachie atabasamu.
Ile ahadi aliyoisema Natasha kuhusu jambo la ukaribu wa Denis na Sara aliitekeleza,muda wote huo wakiwa wanaongea mambo hayo alikuwa pembeni tu ana wasikia na kubaki kuumia moyoni,hakika alimpenda kiukweli Denis lakini kwa yale aliyoongea Denis kumwambia Sara ni wazi kwamba hana mpango na Natasha,huku Natasha na Ester wakiwa nao wanatazama mambo yanavynenda,walimuona Natasha akiumia tu moyo,walimuonea huruma lakini wanajua nini wanafanya.
Huku stori zikawa zinaendelea baina ya Sara na Denis ambaye baada ya kuona tayari wamekuwa wapenzi akawa na uhuru wa kutaka kufany a kitu chochote kwa mpenzi wake huyo,alimgeukia na kujikuta akimkumbatia Sara ambaye alishangaa,jambo lile likamfanya Natasha azidi kuumia tu,muda huo huo Ester na Magreth wakawa wanamsogelea taratibu Natasha ambaye hakujua kinachoendelea.Wakiwa wamekumbatiana pale Sara ndio akapata nafasi ya kufanya kile alichokipanga,alipeleka mikono yake kuupapasa mgongo wa Denis na kumfanya azidi kumteka tu kimapenzi,taratibu akaanza kupandisha mikono yake hadi masikioni mwa Denis na kuanza kuyatekenya kwa vidole na kumfanya Denis ajisahau kabisa,haraka na kwa umakini Sara akauminya mshipa mmoja wa sikio na papo hapo Denis akapoteza fahamu,jambo lile lilimshtua sana Natasha na kuanza kuikumbuka ndoto ile aliyoota siku ile,kwa haraka akahisi huenda Sara amepanga kweli,akapata ujasiri na kushindwa kuvumilia akatoka pale alipojificha kutaka kumfuata Sara pale alipo lakini hakupiga hata hatua mbili akasikia kitu kikimgong a kichwani na kumfanya adondoke chini apoteze fahamu,walikuwa ni wakina Ester walifanya hivyo kwa makusudi.Kule kwa Michael alishangaa kuona kimya hasikii chochote kinacho endelea,alipata wasiwasi na kuona gafla tu hana analopata kwa Natasha na mwenzake Denis,alihisi tu kuwa ni Sara ndiye aliyefanya hivyo,alipata hasira za gafla kuona mambo yameharibika.
Kule Sara na wenzake wakawaweka mahala pamoja Denis na Natasha wakiwa hawajielewi.
"hatuna muda wa kupoteza tunapaswa kuondoka hapa haraka."alisema Sara na haraka wakawashikana mikono wenzao na wakapotea gafla eneo lile.
Walitokea chumbani kwa Sara wakiwa wamewashika mikono wenzao,wakawalaza kitandani na kubaki kumsikiliza Sara ambaye haraka alienda kufungua kabati lake na kutoa kichupa kidogo na kurudi pale kitandani.
"Ester utamshika Mage kichwa kwa mikono miwili na Magreth pia utafanya hivyo kwa Denis,hapa tunatoa vitu mwilini mwao kwahiyo
nguvu zenu zitatumika hapa kuwatuliza wenzetu."alisema Sara na wenzake wakamuelewa,wakafanya kama alivyosema.Sara akaafungua kile kichupa na kuanza kumimina mkononi mwake kukatoka kama mafuta hivi akaanza kuwapaka Denis na Natasha kwenye masikio yao,machoni na kwenye vidole vya miguu huku akitamka maneno fulani na muda mchache mosi mweusi kabisa ukawa unatoka masikioni alipowapaka dawa ile wenzake,gafla tu wakaanza kutetemeka kama wenye kuugua degedege,Ester na Mage wakawa na jukumu la kuwashika kisawa sawa hata ikabidi kutumia nguvu zao kuwatuliza wenzao.Hali ile ilimfanya Michael kule alipo atambue kuwa Sara amewachuku wenzake kujaribu kuwasaidia na kubaki akilalama mwenyewe na kulitupa lile beseni lililopo mbele yake akilitmiaga kama kufahamu wanachokifanya Natasha na Denis.Iliwachukuwa muda sana kuhakikisha wanawatoa kwenye utumwa dhidg ya Michael,hata mzee Junior alikuwa akisikia tu mambo yakiendele a na kuona jinsi gani mwanaye alivyokuwa na upendo na huruma kwa wenzake wakisaidiana kwenye shida kama hizo.Iliwachukua muda sana usiku ule kuwatoa wenza uchawi walio wekwa na baadae wakashuhudia wenzao wakitokwa na madonge ya damu kinywani kuonesha wamefanikiwa kutoa kile kilicho mwilini mwao na palepale wakatulia kabisa na kulala,Magreth na wenzake wakabaki kuangaliana huku majasho yakiwatiririka kwa kazi nzito,wakawafuta damu zile na kuwaweka safi kisha waka wafunika shuka wapumzike kidogo,nao walikaa chini kama mizigo wakishusha pumzi,wakawa wanaongea mambo yao wakipongezana kwa kazi nzito waliyoifanya,uzuri wake ilikuwa ni usiku wa Ijumaa hivyo hawakuwa na shaka ya kuwarudisha wenzao kwao,waliwaacha tu wapumzike pale mpaka asubuhi watawapeleka kwao kuwatetea kama kutakuwa na jambo kwa wazazi,nao taratibu wakaanza kujiwa na usingizi,walitandika mkeka pale chini na kulala.
Asubuh kulipokucha Natasha alikuwa wa kwanza kuamka na kuanza kujinyoosha mwili,alipotazama mahali alipo alishtuka hakupafahamu huku kichwani akiwa amefungwa bandeji kwa maumivu aliyopata muda ule alipopigwa na kuzimia,alipegeuka alishangaa kumuona Denis akiwa amelala pembeni yake,alishtuka na kuamza kujiuliza amefikaje pale na Denis,akaanza kukumbuka mara ya mwisho ilikuwaje kwani mpaka yeye kufika pale,akavua kumbukumbu na kufahamu mara ya mwisho alimuona Sara akimzimisha Denis wakiwa segemu fulani na ni yeye pekee aliyeshuhudia tukio lile na alipotaka kumfuata Sara alihisi kitu kama gongo likitua kichwani mwake na kushindwa kuelewa nini kiliendea,akabaki kumtazama tu Denis kutaka kumuamsha japo akawa anasita,kwakuwa hakuelewa hata yeye nini kimetokea akaamua kumuamsha tu.
"Denis...Denis.. Aamka"alisema Natasha kwa sauti ndogo huku akimtikisa Denis ambaye alifumbua macho taratibu akionesha kuwa bado na usingizi,alipopiga jicho akaona sura ya Natasha,alishtuka na kunyanyuka pale kitandani huku akimtazama Nata sha akiwa pale kitanda.
"hee wewe!heeeee umenifanya nini mimi!umenileta hapa kwa makubaliano gani?"aliuliza Denis akionesha hajui lolote.
"haa jamani,unaniuliza mimi tena wakati wewe ndio sijui umenileta hapa,nikuulize umenifanya nini!"alijibu Natasha ikawa ni kila mtu anamtupia mpira mwenzake na mwishowe wakatulia kila mtu akitafakari kivyake.
"ina maana Denis hukumbuki kilichotokea kabisa kabla ya kufika hapa,"aliuliza Natasha baada ya kuona hamuelewi Denis ambaye alikaa na kuanza kutafakari ya nyuma,ilimchukuwa muda sana na baadae akakubuka.
"nimekumbuka...mara ya mwisho nakumbuka tulikuwa tunakunywa chai na mikate,nilipomaliza kunywa chaiii....ah sikumbuki ikawaje,heeh kwani nini kimetokea Natasha?nilianguka au?"aliuliza Denis akionesha hana analojua kabisa,hata Natasha alistaajabu kusikia vile,siku anayo izungumzia Denis ni siku kama tano nyuma zimepita na ndio anapokumbuka.
"ina maana hajui kuwa tuna mpango wa kuishi huku wawili,hata ile siku alivyo ni... Eh huyu kaingiwa na nini mbona simuelewi?"alisemea moyoni Natasha akiwa hajapata jibu bado,wakiwa kwenye hali hiyo mlango ukafunguliwa na kuingia Sara,Magreth na Ester wakionesha kutabasamu.
"mmeamkaje wapendwa.?"walisalimia kwa pamoja na kuwafanya wakina Denis washangae.
Michael baada ya kujua kuwa tayari amewakosa wakina Denis na Natasha ambao alikuwa akiwatumia kiakili,akawaita watu wake kupanga namna nyengine baada ya kuona kila akifanya jambo mwenyewe anafeli hivyo akaongeza nguvu kwa watu wake.
"naona sasa hali inakuwa ngumu kwangu,nikategemea kupitia wenzao nitawamaliza kwa urahisi lakinh yule mtoto wa malaya amelizuia hili,amenizuia mara nyingi sana na naona ananizidi kidogo maarifa,NATANGAZA RASMI VITA baina yao,ni kuua tua yeyote aliye mbele yako wewe ua,ila kwa Sara kwa yeyete atakaye niletea kichwa chake nitampandisha kuwa mkubwa"alisema Michael kuwaambia watu wake ambao walipokea oda hiyo na kumhakikishia wanaifanya hiyo kazi,basi waliondoka zao na kwenda kuwapa taarifa na wenzao wengine ili waongeze nguvu.
Kule chumbani kwa Sara,baada ya kuwaeleza ukweli wote Denis na Natasha kuhusu kutumiwa akili na Michael,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ndio maana ikanilazimu nimlaghai Denis baada ya kunitongoza kwa siku za nyuma,nilijua tu sio yeye ndio maana nikajisahisisha kwake lengo langu ni kumsaidi kumtoa uchafu aliotupiwa na Michael,hata wewe Natasha mwenzako alipogundua kuwa unamfuata sana Denis akapata nafasi ya kukuteka na wewe akijua kwa chochote atakacho kifanya Denis na wewe lazima ukifanye,sisi ni kama ndugu Mage,Mimi au Ester hawezi akaona mmoja wetu anapotea halafu aangalie tu,ndio maana tumejitolea kuhakikisha tunawatoa kwenye matatizo haya"alisema Sara na kuwafanya wakina Denis waelewe ilivyokuwa,na muda kidogo wakakaa kimya wakitafakari namna mambo yanavyokuwa Denis alinyanyuka na kumtazama Sara.
"Sara,kama kuna uwezekano wa kukuomba samahani basi nisamehe tu maana hata siku moja sijawahi kufikiria kukutamani na kuwa wapenzi,wewe ni kama dada,ndugu kwangu ni vigumu kufanya hivyo,nisamehe sana Sara."alisema Denis baada ya kuambiwa mambo aliyoyafanya kwa Sara.
"hamna Jembe,wewe huna hata kosa na hukuwa wewe pale,hata mimi mwanzo nilishangaa kusikia unanitamkia maneno yale,lakini nilipokuja kupata na kujua ukweli nikakusamehe pale pale,ila ni mmoja tu ndio ameonesha kuwa kweli anaumia,Natasha,amekuwa akikuhusudu muda wote na kuonesha kweli ana upendo wa dhati na huenda siku mkakaa mkaambiana ukweli ila kwa sasa hebu tufanye hili kwanza kulituliza tuwe na amani"alisema Sara na kumfanya Denis ageuke kumtazama Natasha ambaye aliangalia chini kwa aibu,akageuka tena kumuangalia Sara.
"nimekubali,na ninaomba hata sasa twende kwenye falme nikapewe baraka za nguvu kama ze nu"alisema Denis na kuwafanya wakina Magreth watabasamu,Sara alitikisa kichwa kuashiria amekubaliana naye,wakamtazama na Natasha kujua naye ameamuaje,alimtazama Denis kwa aibu kisha akageuka kunuangalia Sara.
"mimi pia niko tayari"alisema Natasha na wote wakafurahia kuwa kitu kimoja.Basi waliongea mikakati yao na baadae wakawasindikiza wenzao makwao wakiwatetea walikuwa wakijisomea usiku wakachelewa hivyo ikawabidi walale kuhofia kukabwa usiku kama wangerudi,ikawa ni salama kwa wote na kila mmoja akarudi kwao wakipanga jioni kukutana tena kwenda kwenye falme kwaajili ya wenzao wapatiwe nguvu kama wao.
Na kweli jioni ilipofika walirudi tena kwa Sara na kuanza safari ya kuelekea kwenye falme,hata walipofika kule zilifuatwa taratibu kama za awali,walipelekwa kwenye chumba kile maalumu na kukaa kwenye viti Denis na Natasha huku Sara kama kawaida yake akawasogelea na kuwapa maneno ya kuwatia moyo na kuwatoa wasiwasi juu ya jamao lile,muda mfupi kazi ikaaza kwa wale wazee wakitoa nguvu kuwapatia wakina Denis oa mwenzake Natasha huku wakina Mage wakishuhudia tukio lile ambalo nao walipitia hivyo.Wakatoka mule chumbani wakiwaacha wazee wakiendelea na kazi yao,walikaa mahali wakibadilishana mawazo ya hapa na pale,baadae waliletwa wakina Denis wakiwa tayari washawekwa nguvu za ajabu,Sara na wenzake walitabasamu kuona sasa wote wapo na uwezo mmoja,waliwapokea na kukaa nao pamoja wakawa wanapeana moyo na kujuzana baadhi ya mambo.Muda huo walikuja wazee wawili na kumtaka Malkia Sara waongee nae,wakatoka pale na ku elekea kwenye mahala wakawa wanaongea mambo fulaki.
Basi Jumatatu iliwadia kama ilivyo dada wanafunzi wakiwa madarasani waliendea na masomo yao,Michael alikuwa tayari kasha wakabidhi kazi watu wake na kuhakikisha wanafanya kile walichokipanga kwa haraka,kwakuwa anafahamu baada ya Sara kuwatoa Denis na Natasha kwenye mikono yake ni wazi kwamba atakuwa amewapa nguvv zile kama zao hivyo itakuwa ni kazi ngumu kuwapata kwa urahisi,ni nguvu za ziada ndio zitatumika kufanikiwa kwa hilo,hivyo aliwaweka watu wake kila mahala ya njia ambazo kila mmoja wao wa kundi la akina Sara wanapita.Wakiwa hawana habari walikuwa na furaha tu wakiwa pamoja,wakiwa kwenye hali hiyo Sara alikumbuka muda ule alivyoitwa na wazee kule kwenye falme kuna maneno alipata kuambiwa yalimfanya atabasamu tu wakiwa nje ya darasa na wenzake akiwatazama wakiwa kwenye hali ya furaha.
"kuna kitu cha furaha napaswa niwaambie,"alisema Sara na kuwaf anya wenzake wamtazame kwa makini kumsikiliza.
"kuna jamao niliambiwa na wazee kule kuwa uwezo wa kuishi tena huku tukiwa hivi umewezekana na hii ni kutokana kupewa muda wa sisi kuhakikisha tunawapoteza wasuriati wote walio kuwa wanaenda kinyume na falme na kila mtu ana uwezo wa kupambana nao hivyo yatupasa kuwa kitu kimoja kuwamaliza wote ndio itakuwa tiketi yetu ya kuwa huru kuishi duniani na hata kwenye falme tukipenda hivyo muwe tu na amani huku duniani na kuhakikisha tunasaidiana kulimaliza hili jambo"alisema Sara kuwaambia wenzake ambao walilipokea jambo hilo na kuona ndio muda wao pekee wa kuitumia nafasi hiyo kuhakikisha wanawamaliza wasuriati,muda wa darasani ulipofika walirudi kuendelea kusoma,Michael kwake alikuwa kama haelewi kitu darasani na kujikuta akiyakumbuka matukio mengi ya nyuma aliyofanya kwa Sara lakini hafanikiwi,kikubwa hasa alimkumbuka sana baba yake na kuikumbuka siku ile ni yeye
ndiye alichoma kile kisu kwenye kioo na kujikuta akimuua baba yake badala ya Sara,alipata hasira sana na kuona ana kisasi kikubwa kwa Sara ambaye ndio amesababisha Michael amuue baba yake bila kupenda,akiwa kwenye kufikiria huko akapata kutambua kitu,akajikuta anajishangaa mwenyewe.
"sasa kwa nini sikufanya hivyo mapema ndio nakumbuka leo!lazima nilipe kwa hili,kama baba yangu amekufa na yeye lazima nimuue baba yake"alisema Michael baada ya kujua Sara anaishi na baba yake na amepanga kumuangamiza mzee Junior.Basi kwa hasira alizokuwa nazo akatoka darasani na kuelekea zake chooni ambako hakuna anaye muona,kisha akafanya uchawi wake na kupotea gafla pale.
Akiwa hana habari mzee Junior alikuwa anakunja nguo zake,gafla tu akaanza kuhisi hali ya utofauti ndani mara upepo mkali ukavuma na kufanya hata baadhi ya vitu kupeperuka kwa upepo ule mkaki,akatokea Michael akiwa kwenye sura ya utofauti sura ya kikatili. Mzee Junior alipomtazama kwa makini alistaajabu kumuona Michael akiwa vile.
"nadhani ushanifahamu na kutambua nikiwa hivi nini kinafuata,"alisema Michael guku mwili wake ukifuka moshi.
"sijakuelewa una maana gani?"
"unafahamu fhka mwana kile alichonifanyia siku za nyuma,kwa makusudi ameamua kutumia mikono yangu kusudi nimuue baba yangu,nimeumia sana tena sana na hiki nilichokipanga naona ndio sahihi kwangu kupoza machungu ya moyoni,lazima nikumalize na wewe nipate kutulia."alisema Michael kwa hasira.
"wewe si ndio ulitaka umuue Sara kwa kutumia mikono yako?sasa ulitaka aache ili umuue asijitetee,ndio maana akamuweka baba yakn ili uone uchungu wa kifo."alisema mzee Junior na kumfanya Michael azidi kukasirika.
"unaongea upumbavu gani,nimeumia kumpoteza mzazi wangu na siwezi kulikalia kimya hili."
"kwahiyo unataka uniume mimi sio?haya ukishaniua utamuacha Sara na wenzake kuwafuatilia kwa ubaya?"aliuliza mzee Junior kwa upole na kumfanya Michael abaki kumtazama tu,akajikuta akiangua kicheko cha hasira kisha akamsogelea mzee Junior.
"furaha yangu ni kuona naitwa mfalme kwenye jamii yetu,sasa nitawezaje kuwaacha watu ambao wapo kinyume na wanashindana na mimi?nakuua wewe atafuata mwanao Sara na wenzake wote,hapo ndipo nitatulia kuona kazi nimeimaliza."alisema Michael na muda huo huo akaandaa nguvu za kichawi kummaliza mzee Junior,akiwa anavuta nguvu zile kule shuleni Sara akiwa darasani akimsikiliza mwalimu Isack akiwa anafundisha somo lake ubaoni,alishangaa ubao unaonesha picha halisi inayoendelea kule nyumbani kwao,Ester,Denis na wenzao nao walipotazama ubaoni walishangaa kuona jambo lile na hakuna mwanafunzi mwengine zaidh yao waliyopata kuona vile,haraka bila kuaga Sara akatoka darasani mbio na kuwafanya wanafunzh washangae,hata wakina Mage na wenzake wote nao wakanyanyuka kuondoka zao haraka wakielekea kwen nye tukio husika,mwalimu Isack akabaki kuwatazama mlangoni wakikimbia kabisa kutoka kwenye eneo la shule,hata wanafunzi wa darasa hilo walishangaa kuona vile.
"wale vipi?wana nini"aliuliza Mwalimu na kuwafanya wanafunzi nao wabaki nao kushangaa,wakina Sara walipohakikisha wamefika mbali na shule kila mtu akapotea kimaajabu wakielekea nyumbani kwa akina Sara kuona kama wanaweza kumuwahi Michael asifanye kile alichokusudia.
Huku Michael alikuwa tayari kashaanda uchawi wake ammalize mzee Junior.
"kama unataka kuniua basi ungekubali tu umuache Sara na wenzake lakini kwakuwa umekata kwa tamaa zako za kutaka madaraka ambayo huusiki nayo,hufai kuwa kiongozi hata kidogo"alisema mzee Junior kwa kujiamini na kauli yake ikamfanya Michael azidi kukasirika,akanyanyua mkono wake na kuziachia nguvu za kichawi kuelea kwa mzee Junior lakini gafla tu akatokea Sara na kumtoa baba yake pale mahala pale na zile nguvu zikapiga mahali na kupasua baadhi ya vitu vilivyopo mule ndani,Michael alishangaa kumuona Sara akiwa pale tena kabadilika kwa hasira huku akiwa amemshika baba yake,muda huo huo wakatokea pia wakina Natasha,Ester na Denis wakiwa kwenye vazi lao la shule huku macho yao yakiwa makali hadi Michael akashangaa baada ya kuona amewekwa kati.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"yaani ulipofika huku ni kubaya tena sana,nisumbue,niumize mimi na wenzangu lakini sio mzazi wangu,kamwe sitakuacha mzima"alisema Sara kwa hasira na kunyoosha mikono yake miwili kumuelekezea upande wa Michael zikatoka miale ya mwanga wa aja ambao Michael akawa na kazi ya kuzuia naye kwa nguvu zake,nao wakina Ester walivyokuwa na hasira naye wakaziachia nguvu zao kwa pamoja kumtupia Michael ambaye aliona hali sio nzuri upande wake,akasema maneno fulani na punde tu akapotea kimaajabu eneo lile.Denis kwa jinsi alivyokuwa na hasira naye baada ya kufahamu alitumiwa sana na Michael kwa mambo yake akaona hawezi kumuacha kirahisi.
"wacha nimeuate mpumbavu huyu haweyi akatufanya sisi wajinga"alisema Denis na yeye akapotea kumfuata Michael,Natasha kuona vile naye akamfuata Denis wauwe pamoja jwenye hilo.Sara aligeuka kumtazama baba yake.
"nisamehe baba kwa kukuweka kwenye matatizo haya,ila nakuahidi LEO yatakwisha,amegusa sehemu ambayo sikutegemea kama angefanya hivyo."
"kuweni makini naye tu wanangu maana ana watu wanaomsapoti kwa haya"alisema mzee Junior kwa upole na kumfanya mwanaye aelewe,alimtazama Ester kwa macho ya ukali akimaanisha kweli amekasirika,wakageuka na kuondoka zao.
Mhchael moja kwa moja akaelekea kwenye mahala ambapo wasurati wenzakewalipata kuweka makazi yao baada ya kukimbia kule kwenye falme,alipofika tu akawakusanyakwa pamoja na kuanza kuwaeleza kilichotokea.
"muda wowote kuanzia sasa muwe tayari kwa kupambana na wakina Sara na wenzake,nilienda kumuua baba yake lakini wakawahi na kuanza kunishambulia kwa pamoja nikawatoka hivyo hawawezi kukaa kimya lazima waje"alisema Michael kuwaambia watu wake nao wakawa tayari kwa jambo lolote litakalo tokea,hawakukaa muda akatokea Denis mbele yao na kuwafanya wasuriati wamshangae,vidoleni akaanza kutokwa na makucha makubwa yenye kuwaka huku akianza kuwatazama wasuriati waliokuwa pale nao wakimuangalia na kuona kweli amekuja kishari,Denis akamtazama Michael akawa mbele ya wenzake.
"ndio mnakopanga upumbavu wenu huku kumbe,yani nyie hamtaki watu waishi kwa amani muda wote wawe na hofu juu yenu mmekuwa nani hasa nyie,sasa mlitutesa kipindi kile tukawa tunawahusudu kwa kuhofia mtatuua,lakini kwa sasa tutaongea jwa vitendo,hasa wewe....wewe....Michael wewe,kifo chako kitakuwa ni historia na sidhani kama kuna mtu atakuonea huruma."alisema Denis na muda huo huo akatokea Natasha pale na kushuhudia umati ule wa wasuriati,akafika na Ester pale na kus imama watatu pale mbele ya wasuriati.Michael alianza kucheka kwa sauti na kuwafanya wenzake nao waangue kicheko cha dharau kwa muda kisha Michael akasogea hatua mbili mbele.
"yani nyinyi kupata huo uwezo juzi tu ndio mmejiamini kuja kututunishia vifua,dah poleni.Michael hatishiwi hata siku moja na sio mtu wa kuogopa kiasi hicho,na wakuniumiza kichwa sio nyie ni huyo dada yenu aliye watuma"alisema Michael kwa kujiamini na gafla akatokea Sara akitua katikati ya wasuriati na wakina Denis,wote wakamshanga baada ya kumuona Sara,hata wakina Ester w
listaajabu kumuona Sara ameivaa ile bangili yake ya zamani ambayo ni muda sana aliitupa porini siku ile aliyofukuzwa shule,hakuongea lolote kwa haraka isiyo ya kawaida akamvuta mmoja wa wasuriati kiuchawi karibu yake na kumkamata shingoni akamnyanyua juu kabisa hata dakika haijaisha yule mtu akakauka na kuwa kama mtu alinasa kwenye umeme na kuwafanya watu wote washngae kuona vile,Sara akamtupa chini yule mtu kuwatazama wasuriati kana kwamba anatafuta mwengine,waliogopa kuona ile hali.
Kwa uwezo wa Sara aliokuwa nao alijikuta akiandamwa na wasuriati wengi sana kwa pamoja kutaka kummaliza lakini walijikuta wakishambuliwa kwa nguvu za Sara alizo nazo na kuwamaliza wasuriati wengi mahala pale ambao bado nao walikuwa wakija tu kwa kasi,Sara alitamka maneno fulani na likatokea jamvia kubwa likin'gaa kwa ukali mikononi mwake,hakuwa na huruma nao hata kidogo alichinja kila aliyesogea kwake huku akiwa na sura ya kikatili akikumbuka mambo waliyofanyiwa na hawa wasuriati wakiongozwa na Michael hasa kule mapangoni Amboni,lengo hasa walitaka wauliwe ili wazuie ndoto za Sara kuwa kiongozi wa jamii yao kama Malkia wao,hakika alizidi kumwaga damu za wasuriati bila kuona huruma.
Huku wakina Denis nao waliendelea kupambana na baadi ya wasuriati huku Michael akiwa amesimama tu anaangalia mambo yanavyoenda.Kadiri muda unavyoenda anashangaa wenzake wanaangamizwa tu na kufanya idadi kubwa ya wasuriati kupungua,hali ile ilimuogopesha Michael na kujikuta akiingia mwenyewe kupambana na moja kwa moja akamsogelea Sara aliyeoneka akìhema kwa kazi nzito.
"naona umejileta upotelee kabisa huku,haya sawa pia nakupa hongera kwa kuwaua watu wangu,na inakubidi ulipe kwa ulicho kifanya"alisema Michael na haraka akaanza kutumia uchawi wake kumtupia miale ya radi Sara aliyeweza kuizuia naye kwa kutumia nguvu zake,ika ni kasheshe ya kuzuia nguvu zile za Michael aliye onekana kupania kweli huku akiwa na sura ya kutisha ya hasira,hali ile alipata kuiona Ester na kuamua kusogea hadi pale na kuachia nguvu zake zote zilizokwenda kwa Michael na kumrusha mbali kidogo ikawa ni afadhari kwa Sara.Michael alipoa mka alimtaza alifanya vile,alimpiga jicho Ester baada ya kumjua ndio aliyemtupa vile,Sara kuna kitu alitaka kukifanya lakini kuna sauti inamkataza asifanye kwa sasa,aliwatazama wenzake na kuwaona wanavyoendelea kupambana na wasuriati kwa moyo mmoja,aligeuka na kumtazama Michael pale chini,taratibu akiwa na Ester wakaanza kumsogelea huku wakimtazama usoni kwa hasira,Michael aligeuka kuwatazama watu wake na kuona wanazidi kupungua,alichokiona bora kwao ni kuondoka eneo lile maana wana kila dalili za kushindwa,kwa yeye binafsi hawez kupambana na watu wawili wenye nguvu za ajabu ndio maana kila wakati anawatuma watu wake kufanya kazi hiyo,haraka alitoa ishara ya sauti kwa wenzake ambao nao walijuwa kuwa wanapaswa kufanya nini na muda huohuo wakapotea gafla wote waliobaki na kuwaacha wakina Sara na wenzake pale wakishangaa kuona hali ile,wakasogea na kukaa wote pamoja.
"Sara tusiwaache hawa kabisa tuwamalize" "alisema Ester akionesha kuwa na moto kweli wa kuendelea kupambana na viumbe wale.
"hapana wala haina haja Ester,kwa kazi tuliyofanya leo hapa inatosha kabisa kuwapunguza idadi yao,ni wachache tu waliobaki hivyo itakuwa rahisi sana kwetu kuwamaliza,turudini tu maana mmefanya kazi nzito sana leo"alisema Sara akiwapa sifa wenzake kwa kile kilicho tendeka,basi walimuelewa Malkia wao na kupanga wote warudi makwao kila mmoja.
Basi Sara alirudi kwao na kukaa na baba yake akimuandalia chakula cha jioni siku hiyo,walikaa mezani na kuongea mambo mengi sana huku akimuomba msamaha baba yake kwa kile kilichotokea mchana wa siku hiyo huku akimhakikishia haitajirudia tena.Mzee Junior alikuwa na kufahamu ni mitihani tu inayomtokea mwanaye katika harakati za uongozi wake na hivyo ikamfanya azidi kumuasa mwanaye kuwa makini na ajitambue.Huku kwa wenzake Sara kila mmoja alikaa na mzazi anayemlea kwa sasa na kuwaeleza hali waliyo nayo kwa sasa,jinsi walivyokubali kwa lolote hadi kuamua kuzipokea nguvu za ajabu wakiwa wameamua hata waambiwe wataishi kule kwenye falme ni sawa kwao,kila mmoja aliongea ukweli wa mambo yanavyoenda kwa sasa,Ester akiwa amekaa na bibi yake akimweleza mambo hayo na kumfanya bibi atoe chozi la huruma.
"kwanini lakini wanakuwa na roho ya tamaa na kikatili kama hiyo,halafu mtu mwenyewe ni kadogo tu mnasoma nae shule moja,si mumfichue kwa mwalimu ili wanafunzi na walimu wamjue afukuzwe?"aliongea bibi akiwa ameguswa kwa maneno aliyoambiwa na mjukuu wake.
"ah hapana bibi huwezi ukasema mambo haya kwa walimu,maana akijulikana hataweza kukaa kimya lazima atatutaja na sisi ikawa ni kesi zaidi,na kama hajasema basi ndio tungempa uhuru yeye akiwa uraiani afanye mambo anavyotaka maana tukiwa naye pale pale tunajua baadhi ya mambo anayofanya,kuwa na amani tu bibi yangu"alisema Ester na kumfariji bibi yake usiku ule, Basi walifanya maombi usiku ule kabla ya kulala ili mungu awaepushe na mitihani na shari za usiku,na bada ya zoezi hilo kila mmoja akaelekea zake kupumzika.Usiku ule kwa Michael hakuweza kabisa kupata usingizi hasa akifikiria hatma ya jambo analo lipigania,alikumbuka mwanzo wa jambo hili alikuwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wakimsapoti akiwemo baba yake mzazi,na wengi kati yao ameshawapoteza wakiwa wanapigania kuhakikisha yeye anakuwa Mfalme wa jamii yao nzima lakini mwishowe anakuja kuthaminiwa na kukabidhiwa uongozi mtu mwengine ambaye ni Malkia Sara.Alikumbuka jinsi alivyo karibia kuwa mfalme hadi kuvalishwa ile kofia ya kifalme,alipokumbuka hiyo kofia akayakumbuka maneno ya marehemu baba yake siku moja alimwambia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"fanya kila njia uwezavyo upate kuitwa Mfalme wa jamii yetu uongoze watu wa jamii hii kama Mfalme,ukiona umeshindwa kabisa na kuona huna uhakika wa kufanikiwa kupata nafasi hiyo haraka tafuta mbinu uichukuwe kofia ya kifalme ukae nayo duniani kwa siku tatu na zikipita siku hzo hawaja kujua kuwa ni wewe ndio mwenye kofia hiyo basi unaweza kujitokeza na ukapewa nafasi ya kuwa mume wa Malkia kupitia tamaduni na desturi ziliyopangwa,kwa maana hiyo wewe utakuwa kama Mfalme sasa na kama utataka kumuua huyo malkia utafanikiwa kwa urahisi maana utakuwa naye muda mwingi."yalikuwa ni maneno ya baba yake Michael ambaye naye aliwahi kuwa Mfalme kwa kuwa mume wa malkia Aznaty.Maneno yale yalimfanya Michael atabasamu na kujiona mwenye bahati ya kuwa mfalme kweli pindi atakapoipata kofia hiyo ya kifalme,akajikuta akicheka sana akiona ndio njia iliyobaki kwake maana amewapoteza wenzake wengi waliokuwa wakimsapoti huku akijijua kuwa hana uwezo mkubwa wa kupambana na kundi lote la Sara.Aliamua kufanya kazi hiyo ya kurudi tena kwenye Falme akaibe kofia ile ili akae nayo duniani kwa siku hizo zilizopangwa,.
Basi alijipanga kufanya kazi hiyo na taratibu akarudi kupumzika huku moyo wake walau ukifarijika kwa kile alichokifikiria,akasahau yote yaliyo tokea siku hiyo ikiwemo na kukimbia vita ile na wenzake wachache.
Asubuhi kama ilivyo ada wanafunzi waliendelea na masomo yao kama kawaida,Michael alikuwa naye darasani akipata mawili matatu akiwa hawa wasiwasi kabisa.Baadae Sara alikaa na wenzake wakiongea mambo yao,wakiwa kwenye hali hiyo alikuja mwanafunzi mmoja.
"Ester,Denis na wenzenu mnaitwa na mwalimu Isack ofisini"alisema yule mwanafunzi akageuka na kuondoka zake.Ester akabaki kutazamana na wenzake baada ya kujua wanachoitiwa,walinyanyuka na kuelekea ofisini walikoitwa na mwalimu. Walipofika tu mwalimu Isack aliwaamuru wapige magoti chini nao wakatii.
"haya mnieleze ilikuwaje jana mkatoka darasani bila ruhusa na kuanza kukimbia mkaondoka kabisa eneo la shule?"aliuliza mwalimu Isack huku akiwa amekamata bakora,wote wakabaki kuangalia na kujikuta wakiongea wenyewe kwa hisia kujadili jinsi ya kujitetea,Denis akapata wazo papo hapo.
"mwalimu kiukweli Sasha ana mapepo hivyo laiti tungemuacha dakika dakika kadhaa tu angeenda mbali hata kuingia maporini huko ikawa kesi."alisema Denis na kuwafanya wenzake waitikie huku Sara mwenyewe akiwa mwenye kuona aibu na kuangalia chini.
"ana mapepo?nyie mmejuaje?"aliuliza mwalimu.
"huyu ni rafiki yetu na ni jirani yangu mwalimu,wazazi wake walituambia kuwa ana mapepo hivyo yatupasa tuwe naye karibu ndio maana tumekuwa karibu naye kila siku kama tulivyo."alisema Ester na kumfanya kidogo mwalimu aamini kwakuwa Ester anajulikana kama mlokole na mwenye kauli za ukweli,akajikuta anawaamini kwa kile walichosema.
"matatizo kama haya mnapaswa kumweleza mwalimu mapema ili siku nyingine asiwafikirie vibaya,Sasha...pole sana mdogo wangu"alisema mwalimu Isack na kumfanya Sasha aipokee pole ile kisha wakaruhusiwa kurudi darasani.Walifurahi sana kuona wamejitetea bila kujulikana na kuanza kumtania Sara kuwa ana mapepo,baada ya muda waliingia madarasani na kuendelea na masomo.Basi muda uliena na muda wa kuondoka ulipofika wanafunzi walirudi makwao,Michael alibaki kuwatazama tu wakina Sara huku akiwa amepanga jambo lake.
Jioni ilipofika Michael alianza safari ya kuelekea kule kwenye falme lengo hasa ni kuichukua kofia ya kifalme apate kuondoka nayo.Ulinzi kila mahali ndani ya jengo la kifalme wakihakikisha usalama unakuwepo mahali hapo,Michael aliweza kuwasili na kukaa mahali akipanga namna ya kuingia huku akiwasoma walinzi mahala walipo,ikamchukua muda sana kujua wapi ataanzia na mwishoni ataishia wapi.Akiwa mahala pale aliona wasichana wakiongozana kuingia ndani ya falme wakiwa wamebeba vyungu vyenye maji na wengine wakiwa na maua,akapata kutambua kuwa ni wafanyakazi wanaingia kufanya usafi na kupandikiza maua kwenye sehemu zisizo ota majani,akaona ile ndio njia pekee ya yeye kuingia ndani,walipotea haraka na kutokea kwa msichana wa mwisho akamtia kabali huku akimfumba mdomo na kufanikiwa kumnyonga kwa mikono,papo hao akaamua kutumia uchawi wake kufanikisha zoezi lake,alimsogezea uso karibu yule msichana huku akisema maneno neno fulani ya kichaji na kujikuta akivaa sura ya yule msichana na umbile lake kama alivyo,alisimama na kujishika akaona kweli amebadilika na kuwa kama yule msichana,alinyanyua mapambo ambayo yalikiwa yameahikwa na yule msichana na taratibu akaingia zake ndani ya falme akijichanganya na wale wengine wakijulikana wanakwenda kufanya usafi na kupamba katika baadhi ya sehemu.Basi walipofika kazi zikaendelea kila sehemu huku Michael naye akiwa pamoja nao na hakua yeyote aliyemtambua.Mmoja wa viongozi wajuu kwenye falme ile aliwachukuwa wasichana watatu akowemo na Michael mwenye umbile la yule msichana na moja kwa moja wakapelekwa kwenye chumba ambacho Malkia na Mfalme mavazi yao ya heahima yanawekwa hapo pamoja na vitu mbali mbali vya siri,basi waliagizwa wafute vumbi pamoja na kusafisha sehemu zengine huku wakisimamiwa na mlinzi mlangoni akihakikisha kila kitu kinaenda sawa.Michael aliendelea kufuta futa vitu vya pale huku akipeleka macho huku na kule kutazama ni wapi kofia ya kifalme ilipowekwa,alizidi kupiga kazi huku akoendelea kuangaza huku na kule na kwa bahati akapata kuiona ikiwa juu ya nguo za kifalme zikiwa zimekunjwa vizuri na kiwekwa kwenye kiti,moyo ulimuenda mbio kuona ndio mida mzuri wa kukamilisha kilichomleta na kuanza kumuangalia mlinzi ambaye muda wote alikuwa makini anawatazama wakifanya kazi..
Alichokifanya Michael kwa yule mlinzi ni kudondosha upanga aliokuwa ameushika kwa kutumia uchawi wake na kumfanya mlinzi yule aache kuwatazama wale wasichana wanaofanya usafi na kuinama chini kutaka kuokota upanga wake,na muda huo huo Michael aliikamata kofia ile na kuificha kwenye gauni alilovaa.Mlinzi aliponyanyuka aliona wakiwa bize na kusafisha na kuwa na amani nao.Siku hiyo Denis naye alikuwa anakuja kwenye falme kujua mambo yanavyoenda kwakuwa tayari amekuwa na imani kwamba nayeye ni miongoni mwa viumbe wa jamii hiyo,basi alipofika akawa anatembea tembea kwenye jengo lili na mbele aliwashuhudia wasichana wakitoka ndani ya baada ya kufanya usafi kwa muda na kazi zengine,walipofika kwa Denis walimpa heshma yake kwa kuinama kidogo kwa kunyenyekea kisha wakapiga hatu kuondoka zao,alibaki akiwatazama wote alimuona mmoja kati yao akitembea tofauti na wenzake,alionekana kuwa na haraka ya kufika mbele zaidi,hakuwa anafahamu lolote Denis aliona ni hali ya kawaida tu hivyo ikamfanya asihisi lolote akageuka na kuendelea na safari,basi alizidi kulipitia jengo lile la kifalme huku akipata heshima yake kwa walinzi na watu wengine,akiwa kwenye pitapita hizo aliona mahali mguu wa mtu umetokeza,alishtuka kuona tukio lile na taratibu akasogea mahala pale na alifika alishaa kuona mwili wa msichana ukiwa pale chini,alimsogelea na kumshika akajua tayari ameshakafa,haraka alipiga kelele za kuwaita walinzi na mara moja wakafika na kushuhudia tukio lile,haraka wakambeba yule msichana na kuupeleka mwili wake mahala salama.Denis alibaki akiikumbuka sura ya msichana huyu alimuona kwenye kundi lile alilopishana nalo muda ule,sasa imekuwaje tena hata dakika tano hazitapita anamkuta amekufa!alijiuliza bila kupata jibu na haraka akaamua kuwasiliana wenzake wote juu ya jambo hilo lililo tokea gafla.Nao kusikia hivyo haraka wakaja ili kujua kwa undani zaidi,Sara aliwa wa kwanza kufika na kuanza kutaka kuonyeshwa pale mwanzo msichana yule alipokuta na Denis,akainama eneo lile kwa umakini huku wazee pamoja na wenzake wakimtazama tu anavyoendelea na jambo lake,alipomaliza hapo akarudi tena hadi uliko ule mwili wa yule msichana akaanza kuukagua na baadae akapata kujua kitu.
"kuna mtu amemkaba na kuamua kumuu kabisa"Sara na muda huo huo akatokea yule mlinzi aliyekuwa akisimamia usafi.
"Malkia.."aliita na kuenda chini kupga magoti."kuna wizi umetokea,kofia ya kifalme imepotea,alisema yule mlinzi na kuwafanya hata wazee washangae,wote wakatoka na kwenda kushuhudia kweli wanachoambiwa,na kweli walipofika waliona kweli hakukuwa na kofia ya Kifalme,wote wakabaki kuangaliana imekuwaje,wakawa wenye kujadili juu ya swala hilo kwa muda na baadae ikawabidi wazee wakae pembeni na malkia kuteta jambo.
"unafahamu fika umuhimu wa kitu hicho na ni wewe ndio mwenye dhamana nacho na ni wajibu wako kuitafuta kofia hiyo ukaipata,na kama haikupatikana ndani ya siku tatu na ikaja kuletwa na mtu wa kiume basi ndiye atakaye pewa dhamana ya kumuoa Malkia,na kama akiwa ni mwanamke basi atakuwa ndio mtu wako wa karibu hivyo yakupasa uelewe hilo"alisema mzee mmoja wakiwa faragha,maneno yale yakamtia mashaka Malkia Sara na kujikuta anashindwa kuongea lolote,ni jukumu lake kuhakikisha anairudisha kofia ya kifalme mapema kabla ya siku tatu ili apate kuwa Malkia la sivyo ikaletwa na mtu baki basi atakuwa na jukumu la kuolewa naye.
Huku Michael alikuwa anaxbeka sana baada ya kufanikisha jambo lake alilokuwa akilifikiria,alibaki ameishika tu ile kofia akiiangalia kwa furaha,taratibu akaivaa na kujihisi ndio anapiga kweli hatua ya kuwa Mfalme wa njia ya kumuoa Sara CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"kwisha jeuri yako weweee.....haya kiko wapi ulichokuwa unajigamba kwa kunitisha na ziada ya nguvu zako...mimi natumia akili na hii ndio njia yangu ya mwisho kuitumia na ndio naona ni nyepesi sana kuingia kwenye falme kwa heshma kama Mfalme...hahahahahh hahahhaha"ilikuwa ni furaha kwa Michael akiwa tayari kashajipa ushindi wa kuwa Mfalme huku kofia ikiwa kichwani mwake.
Usiku huo Sara na wenzake wakawa walirudi duniani na moja kwa moja wakawa wametulia cvumbani kwa Sara wanajadili jambo ambalo aliambiwa na wazee wale.
"Lakini huyu kiumbe anatutaka nini hasa sisi?yaani hachoki na tamaa zake sasa ameamua kuiba kofia ili aingie kwenye falme kwa njia hiyo"alosema Natasha akioneaha kuchukizwa na hilo,tayari walishaanza kumhisi ni Michael ndiye aliyefanya wizi huo.
"Hapa haina haja ya kumjadili yeye,kesho siku ya kwanza inakatika inatubidi kuanza kutafuta mahali anapoishi popote pale kujua wapi ameiweka kofia hiyo,maana tukimfuata kumweleza jambo hilo hata tukimuadhibu hawezi kusema mwenyewe yeye atataka siku tatu zipite apate tiketi ya kuingia kwenye Falme...hapa kesho ni kuanza msako wa kila sehemu tunayohisi Michael ameweka makazi yake tutafute kwa juhudo zote kabla ya hizo siku"alisema Denis na kuwafanya wenzake washushe pumzi maana zoezi hilo ni kubwa sana hadi kujua wapi ilipofichwa kofia ni jambo zito mana mtu mwenyewe aliyechukuwa kofia hiyo naye ana uwezo wa ajabu hivyo sio rahisi..Basi waliongea mengi na kupanga namna ya kuanza zoezi hilo,walimhakikishia Sara kusaidiana naye ili wafanikiwe kuipata kofia hiyo kabla ya siku hizo tatu.
Asubuhi kulipo pambazuka wanafunzi walielekea mashuleni kupata elimu bora,usafi ukawa ndio kifua mbele kuhakikisha nazingira ya shule yanakuwa mazuri.Basi baada ya kuweka mazingira hayo safi wanafunzi wakaingia madarasani tayari kwa vipindi kuanza,Natasha asubuhi hiyo hakutaka kulaza damu baada ya kuona jambo lile kwa vyovyoye aliyelifanya ni Michael akamfuata hadi darasani kwao kabla hata walimu hawakuanza kufundisha,akamsogekea moaka pale akipokaa na kubaki wakiangaliana sura zao.
"naomba unisikilize tena kwa makini we mvulana.... kulazimisha kitu ambacho hakiwezekani i sawa na kupoteza muda wajo tu bure,na kwa haya unayo yafanya siku ukiingia kwenye mikono ya watu unao wafanyia haya mauzi utajuta nakwambia,rudiaha ulicho kichukua haraka ili upate kuishi siku byingi kidogo maana naona kama umefanya hili ili uwahi kumuona baba yako aliye tangulia....nakusihi sana rudisha kofia uliyo chukuwa"alisema Natasha akioneaha kweli amechukizwa na kitendo kile.Michael alitabasamu tu baada ya kusikia maneno ya Natasha na kuona ni mikwara tu inayo endelea pale.
"aisee una maneno ya kutisha sanablaiti angekuwa mtu wa kawaida kaiwada sasa hivi angehaha kutaka kufanya hicho ulichosema"alisema Michael na kusimama sasa kumtazama Natasha vizuri."sikia wewe nkwambie...hicho kitu mnacho kitaka kwa sasa hakipo na hata mimi sijui kipo wapi...ila kinaweza kupatikana kwa baada ya siku kadhaa kupita na ninaimani tu kitapatika kwa siku hizo baadae,nitawasaidia kutafuta"alisema Michael kwa dharau sana na kuanza kutabasamu akakaa kwenye kiti chake akiendelea kupangaa madaftari yake,Natasha alimtazama kwa hasira sana kwa maneno aliyosema Michael,akayatazama madaftari ya Michael aluyokuwa anayapanga na kuyapiga shoti kwa uchawi na kumfanya Hata Michael mwenyewe ashangae baada ya kuyaachia madaftari yale haraka ba kumtazama Natasha,aligeuka na kuondoka zake huku Michael akimsindikiza kwa macho,alibaki kutabasamu tu akiacha wakasirike lakini jambo lake litimie.Basi baadae muda wa wanafunzi kwenda junywa chai wakina Sara walitumia muda huo kukaa pamoja na kupeana majukumu ya kuhakikisha wanapata kofia ile ya kufalme kabla ya siku zile tatu.
"hapa inabidi tugawane Magreth,Natasha na Denis mtaenda kule walipoweka makazi wasuriati tukawavamia siku ile,hakikisheni mnatafuta kila mahali na kama kuna mtu yeyote wao jaribuni hata kumbana huenda akasaidia kutuambia,mimi na Ester tutamfuatilia Michael mwenyewe hadi anapokaa tujue wapi alipoiweka...zoezi hili litaanza pindi tytakapotoka shule leo na naamini tutafanikiwa tu"aliaema Sara akiwapanga wenzake na wakaku baliana kufanya hivyo..Baadaye walipotoka shule kweli taratibu zikaanza kufanyika haraka,wakiwa njiani Sara alikuwa tu anamnyemelea kwa nyuma Michael bila kujua akitaka kujua wapi anapokaa kwa sasa huku wenzake wakielekea kule walipo wakuta wasuriati na kuwaangamiza,walipofuka kule hawakukuta mtu yeyote eneo lile zaidi ya mabaki ya nguo nguo tu na vitu vengine,basi wakaanza kusachi kila mahala kuitafuta kofia ile.
Huku kwa Sara alifanikiwa kupajua anapoishi Michael baada ya kumfuatilia muda wote,siku hiyo hakuweza kufanya chochote aligeuza na kuondoka zake.Michael alipofika tu chumbani kwake akafunua mkeka aliokuwa ameutandika na kuitazama sakafu ile pale chini na kutabasamu,akashuka chini na kuishika sakafu ile huku akisema maneno fulani na kuifanya sakafu ile iachie pande mbili akaingiza mkono na kuitoa kofia ile ya kifalme huku akitabasamu na kubaki kuitazamabkwa makini tu kofia ile ya dhahabu yenye kun'gaa."zimebaki siku mbili tu nipate kukuweka kichwani mwangu nikapatwa kuitwa jina jipya...."alisema Michael akiwa na matumaini mapaya ya kuwa Mfalme.
Basi usiku wa siku hiyo wakina Mage walikitana na Sara na kuweza kumweleza hali halisi.
"itakuwa kuna mahali ameificha maana kule hakuna mtu wala kofia hiyo na tumetafuta kweli yani..."alisema Denis.
"ngoja hapo kesho niangalie itakuwaje maana nishapajua mahala anapokaa yutaenda mimi na Ester kuangalia pindi yeye akiwa hayupo"alisema Sara na kuwafanya wenzake wapate tumaini kidogo kuhisi huenda kweli Michael atakuwa nayo kofia ile pale anapokaa,basi walirudi makwao baada ya kupanga mambo yao.
Asubuhi ya kesho yake shuleni masomo yaliendelea kama kawaida.Siku hiyo Sara na Ester walitega shule hawakuenda ili tu kukamilisha kazi yao.Alixhokifanya Denis kule shule ni kupita darasani kwa Michael kuhakikisha kama yupo au laa....na kwa bahati alimkuta yupo darasani tena ndani ya kipindi mwalimu akisomesha,basi akapita zake lakini Michael alipata kumuona Denis akiondoka zake japo kwa haraka hakuweza kutambua alifuata nini,akaelekeza akili yake kwenye kusoma.
Basi Denis alichokifanya ni kumsubiria mgonga kengele ya kipindi ili asogee kwenye kengele apate kuwaeleza wakina Sara kwamba Michael yupo darasani hi yo waendelee tu na kazi yao.Na kweli baada ya muda TimeKeeper alisogea kwenye kengere na haraka Denis akasogea mpaka pale karibu na kengele,yuke kijana alipogonga tu kengele na Denis akaongea na Sara kwa hisia kuwa waendelee tu,hali ile ilisaidia Michael asisikie kilichoendelea kwa kelele zile za kengele.Basi kweli wakina Sara waliweza kuelekea nyumbani anapokaa Michael na walipofika kwenye nyumba ile walifungua kwa nguvu zao na kuzama hadi ndani wakaanza kupitia kila chumba kukagua kuitafuta ile kofia,walisachi kila sehemu ya nyumba ile lakini wapi hadi wakachoka na kubaki kuangaliana tu wasijuwe wafanye nini na ndio siku ya pili hiyo imebaki siku moja tu ambayo ni ya kesho yake,wakifikitia ivyo wanajikuta wanaendelea kupekuwa tena na tena lakini wapi.
Muda uliyoyoma hadi saa ya mapumziko wanafunzi wakatoka na kwenda kupata chai na wengine wakiwa wametulia tu katika mazingira ya shule,sasa Michael wakati yupo anakunywa zake chai akapata kusikia wanafunzi wa kidato cha tatu wakiongea.
"yaani kwa mara ya kwanza ndio naona leo Ester ametega shule sijawahi kuona akikaa nyumbani na wala kusikia kuwa anaumwa yule mwanamke"alisikika mwanafunzi mmoja akiongea.
"si hata yule rafiki yake Sasha naye pia hakuja leo...maana ndio marafiki muda wote wanakuwa pamoja"aliongea mwanafunzi mwengine wakiwa wanapoga tu kama stori wakiendelea kunywa chai.Kauli ile ikamshitua kidogo Michael na kuhisi jambo,haraka akarudi hadi madarasani na kuwakuta wakina Denis,Natasha na Magreth wakiwa wanajadili jambo....hali ile ikamtia wasiwasi na kuona hawa kuna kitu wanakifikiria,alitazama huku na kule hakuna mwengine aliyemuona zaidi ya wale na pale pale akapotea gafla mbele yao na kufanya wakina Denis wahamaki na kujuwa kwa vyovyote atakuwa amejua,haraka wakawasiliana na wenzao waondoke haraka kule...
Huku kwa Sara na Ester mpaka muda ule walitumia kila njama lakini hawakuweza kufanikiwa,Sara akaona atafeli kuipata kofia ile,alichekecha akili yake haraka haraka na kuona bora afanye jambo ambao litakuwa ni hatari lakini lenye maana kwake...muda ule ndio wakapata kusikia sauti ya Denis masikioni mwao kwamba waondoke haraka Michael anakuja...basi haraka Ester akageuka na muda huohuo akaanza kupotea kimaajabu,Sara alikitazama kile chumba na kukaa kwa sekunde kidogo na muda huohuo Michael akatokea akiwa na sura ya hasira,sasa Sara alipomuona tu Michael ndio akataka kupotea kimiujiza hali ambayo Michael aliona na kumrushia uchawi Sara ukampata na kudondoka chini,japo aliumia lakini akajikaza na kupotea kimaajabu muda ule akamuacha Michael pale akishangaa,haraka akaenda hadi pale alipoficha ile kofia na kuitoa kwa uchawi wake akaikuta ipo salama tu...alitabasamu tu kuona kumbe walikuja kuitafuta lakini wakashindwa kuipata kwakuwa alificha sehemu ambayo asingeweza mtu yeyote kuiona.
"kwa kile nilichomfanya sidhani kama atakuwa na ujanja....ndio nimemteka kabisaaa pumbaaaavu"alisema Michael akiwa anamaanisha..ule uchawi aliyomtupia Sara ulikuwa na maana kubwa kwake..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na kweli Sara alipofika tu kwao alipasikia maumivu makali sana..akajitahidi kujitibu mwenyewe kwa kujishika mahala palipoumia na baada ya muda maumivu yakaanza kupotea taratibu.Basi kwa kile alichokifikiria mwanzo aliona ni sahihi wacha afanye vile alivyodhani,alipanda kitandani mchana ule na kupumzika zake bila wasiwasi.Wakina Denis waliporudi shule wakapitia kwa Ester kujua kilichotokea,walipata jibu kwamba hawakufanikiwa ikawa ni kazi kwao sasa,hadi kufika jioni bado walikuwa wakihangaika kutafuta lakini wapi,wakaamua kwenda kwa Sara kupata mawazo yake na cha ajabu walipofika wakamkuta yupo kitandani amelala kabisa hana wasi,walishangaa kuona vile maana imebaki siku moja lakini hana hata wasi, wakamuamsha.
"Yaani imebaki siku ya kesho tu tukikosa kofia ujue Michael anakuoa wewe na yeye anakuja kuwa Mfalme...wewe umelala saahizi una maana ganj?"alisema Ester na wote wakimtazama Sara ambaye aliwatazama tu wenzake..
"Ah KAMA IMESHINDIKANA BASI....ACHA IWE KAMA IMEPANGWA"alisema Sara na kuonesha kuwa siriasi na kile anachokisema,hakuna aliyeamini baada ya kusikia kauli ile ya Sara anayosema,walikosa nguvu kabbisa na kujikuta wote wakikaa chini ya sakafu wakimshangaa.
"u...unaaa....unasemaje....unasemaje Sara???"aliuliza Denis akiwa haamini kwa kile kilichoongelewa.
"Denis...mimi Sara nduo nimesema hivyo...kama imeagindikana kupata hiyo Kofia basi tungojee kitakachotokea.."alisema Sara kwa kujiamini.
"Hivi una kichaa wewe Saraee??ina maana unaona bora tu Michael awe Mfalme?ndio umeamua hivyo?"alisema Ester huku chozi likimdondoka kwa uchungu.
"Ester...mimi Sara Malkia wenu ndio nimeamua iwe hivyo."alisema Sara na kurudi kitandani akajifunika shuka na kuwaacha wenzake wabaki wameagikwa na butwaa kujiuliza nini kimemkuta Sara.
Michael akule alipo alikuwa anacheka tu...alikuwa akisikia yoye yanayoongelewa na maadui zake.
"hatimaye yeye mwenyewe amekubali... Michael naenda kuwa Mfalme...na ni lazima nikuue Sara niimiliki Falme pekeangu"alisema Michael akiwa ameishika kofia ya kifalme,uchawi aliomtupia Sara muda ule ulianza kumtoa akili Sara taratiibu na kujikuta akikubali kila anachokisema Michael,naye amekuwa kama katekwa na Michael kiakili.
Basi baadae Denis na wenzake wanaanza safari ya kurudi makwao huku wakiwa hawaamini yale yanayozungumzwa na Sara ambaye muda woye alikuwa kitandani tu amejilaza,Ester alikuwa wa mwisho kuondoka na kubaki kumtazama tu Sara,alijiuliza sana kipi kimemkuta mwenzao kwa muda mchache tu,na kama kwenda kule kwa Michael waliondoka wote wakiwa na akili ya kutafuta ile kofia ya kifalme lakini waluporudi ndio hali ya Sara inakuwa hivyo....akaanza kuoatwa na wasiwasi juu ya hilo hasa akikumbuka walipoambiwa waondoke haraka Michaela sije kuwakuta yeye ndio alikiwa wa kwanza kuondoka lakini Sara alibaki tena kwa makusudi kabisa,Ester akaona huenda kweli Michael amemtupia uchawi Sara,aligeuka na yeye akaondoka zake usiku ule.
Basi kesho yake asubuhi vipindi viliendelea kama kawaida madarasani kuhakikisha watoto wanapata elimu bora,muda wote Ester na wenzake walikuwa wakimtafakari Sara kwa kauli zake za jana ambazo zilowaacha midomo wazi,mwenyewe hakuwa na wasi kabisa na muda wote akaonekana ni mtu wa tabasamu tu usoni,haikupita hata dakika mbili Sara alinyanyuka na kutoka zake nje kwa furaha hali iloyowafanya wenzake wamshangae,Ester akanyanyuka na kumfuata nje kujua anaenda kufanya nini,Denis na Mage walibaki kumtazama tu Ester akitaka kujua nini kimemkuta mwenzao,taratibu akaanza kumfuatilia Sara na kumshuhudia akielekea kwenye madarasa ya kidato cha pili na kusimama,akageuka kuangalia darasa ni na kukutana na sura ya Michael ambaye alipomtazama Sara naye wakawa wanaangaliana.Sara aliachia tabasamu zito na kuzidi kumshawishi Michael kwa kujiamini na kujipongeza kwa kile alichokifanya hadi kumshika akili Sara kiulaini,basi Sara baada ya kumaliza kuonana na Michael aligeuka na kurudi zake darasani hali iliyomfanya hata Ester ashangae kuona mbio zote za Sara kutoka kule darasani kwao kumbe amekwenda kumuona Michael,hapo ndipo akajua kuwa kuna mchezo mchafu unaendelea,Sara alikiwa akipita pale pale alipo Ester ambaye alikujikuta akimkamata mkoni Sara.
"Hivi Sara wewe umerogwaeee!!! Umesahau kabisa kuwa leo ni siku ya mwisho ya kutafuta ile kofia na tusipoipata unampa nafasi kubwa Michael ya kuimiliki Flme wakati hastaili,uule ni adui kwetu na wewe unajua sasa inakuwaje unaamua iwe hivi?niambie Sara kama kuna jambo umefanyiwa nifanye mpanho wa kukusaidia urudi kama mwanzo tukamilishe hili Sara wangu!!"aliaema Ester na kumfanya Sara abaki kumtazama tu Ester,taratibu alimsogelea hadi pale aliposimama Ester na kumsogezea uso akioneaha kuwa siriasi.
"sijabadilika wala sijarogwa,Sara ndio yule yule wa sasa na hili nimeliamua mwenyewe kutoka moyoni wala hakuna atakaye nizuia,tena waambie na waki a Denis wasisumbuke kuitaguta hiyo kofia wakapoteza muda wao maana nimeshaamua iwe kama ilivyokuwa."alisrma Sara akionesha kudhamiria kweli,aligeuka na kuondoka zake darasani akamuacha Ester pale akiwa ana tafakari maneno ya Sara kuonesha kweli ameamua.Anampenda sana rafiki yake hivyo anavyoona anapata matatizo hata yeye anaumia,hakutaka kumpoteza Sara kwa namna kama hiyo akijua kuwa lazima atakuja kuolewa na Michael kama ndio mwenye kofia,aliondoka na kuelekea zake chooni baada ya kutafakari kwa kina na kuona afanye kitu,alipofika alitazama huku na kule hakuna mtu aliyemuona na papo hapo akapotea zake na kuelekea kwenye falme na moja kwa moja akawakusanya wazee na kuwaeleza hali halisi iliyokuwa ikiendelea kwa Malkia wao,hata wao walishangaa kusikia vile na kuanza kuwa na wasiwasi juu ya falme yao kama Michael ndio atakuja kuwa Mfalme basi ni wazi ndio falme inakwenda kuangamia,ikawa ni mada ya kujadili namna ya kufanya wakiwa sambamba na Ester.
Basi kule shuleni muda wa kuondoka ulipofika Mavreth alochukuwa begi la Ester baada ya kujua hayupo shuleni,akaongozana na wenzake lakini Sara walishangaa hayupo nao,wakawa wanamtafuta kubu na kule na gafla tu wakashikwa na butwaa na kuwafanya wote wabaki kushangaa tu wakimuona Michael akiwa sambamba na Sara wanatembea kuondoka zao,Magreth akajikuta akilibwaga begi la Ester kwa kushikwa na butwaa,hakuna aliyeamini jambo lile.
"Hapaaana.....hapana nakataa kabisa...Sara sio yule wa siku zote hapa kuna jambo limemkuta hawezi akafanya uchafu wa namna ile...mtu tumekuwa na uadui naye kwa muda wote leo hii Sara awe naye wanaongea vizuri vile...hamna kuna kitu Sara atakuwa kapewa."alisema Natasha akiwa haamini.
"Hata mimi sielewi hivi ni Sara kweli yule,Sara aliyekuwa anamchukia Michael leo hii wanatembea wote?"alisema Denis na kuwafanya wenzake wasiamini.
"siku zote yeye ndio tumekuwa tukimtegemea ili kuhakikisha Mixhael tunampindua..sasa leo hii yupo pamoja na adui yetu unategemea nini hapo kitatokea...byuuuu ni upumbavu huu"alisema Magreth akioneaha kuchukizwa na jambo lile,aliokota begi la Ester na kukamata njia yake akaondoka kwa hasira akiwaacha Denis na Natasha wakiangalia tu.
alisema Sara na kumfanya Michael atabasamu tu akijua yeye ndiyo aliyemtupia uchawi na kumfanya Sara apende zaidi,basi akasogezaa meza pembeni na kutoa mkeka aliyoutandika eneo lile kisha akaanza kunena maneno fulani ya kichawi yaliyofanya kutokea kofia ile ya kifalme ikiwa inan'gaa akampa Sara aishike.
"ni kweli mimi ndiyo niliichukuwa kofia hii na nliingia bila yeyote kujua na nkaiiba nkijua tu siku tatu zitapita hamtaipata kofia hii na nitakuwa na nafasi ya kuwa mumeo,na madam nawe umeridhia hili basi sina shaka kwa hili tena."alisema Michael na kumfanya Sara atabasamu tu.
"Natamani hata sasa twende tukamalize jambo hilo haraka Michael."alosema Sara kwa furaha akitamani ndoa hali iliyomfanya Michael atabasamu tu.
"usijali leo nitawaeleza waauriati wenzangu kuhusu hili maana leo ndio siku ya mwisho ya tatu hivyo jioni tutaenda kuipeleka kofia hii ili mambo mengine yaendelee."alisema Michael na Sara akakubali,wakawndelea kuongea mambo yao.
Basi kama ilivyopangwa Michael alienda kuwaeleza wasuriati wenzake jinsi alivyomteka kiurahisi Sara na kuwapa uhakikia wa hilo jambo,ikawa ni furaha kwa wasuriati na kuona ndio wanaingia kwenye falme rasmi wakimtumia Sara ili waitawale falme ile.Jioni ilipofika Sara aliongozana na Michael ambaye alikuwa ameahika kofia ile,wazee walishangaa kjmuona Michael twna akuongozana kabisa na Sara na kuamini yale waliyoambiwa na Ester ambaye naye aiku hiyo alikuwepo na wazee hao wakishuhudia mambo yanavyoenda,alikasirika sana kuona Michael ana kofia ile kaishika halafu Sara hana hata nguvu ya kumpokonya kuonrsha amekubali kuolewa.
"Hivi Sara ni upumbavu gani unaotuletea hapa?tunahangaika kwaajili yako wewe ndio kabisa hutaki kusaidiwa umeamua iwe hivyo si ndio?"alifoka sana Ester kwa hasira na kuwafanya hata wale wazee waangalie chini,alifanya kosa kubwa sana kumtusi Malkia mbele yao lakini Ester aliona kawaida kwa kuwa anajuana na Sara muda wote.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"unamuita Malkia mpumbavu?heee..eti wazee wangu Malkia anatukanwa?hii ni sawa kwa mila zetu?" alidakia Michael huku akiwatazama Wazee wale.
"Ester umenikosea sana...nikiwa huku ni kama Malkia unapaswa kuwa chini yangu...na kwa hili lazima upate adhabu baadae..ondoka hapa niskikuone"alisema Sara akioneaha kuchukizwa sana,Eater alishangaa kuona Sara amebadilika kabisa yaani hataki kushauriwa,alichukia na kuondoka zake kwa hasira huku Sara akimtazama tu akiishia.Basi walikaa na wazee na kuanza kuluongelea swala la mila na desturi zao baada ya Michael kuileta ile kofia ya kifalme,wazee walimsogeza Malkia pembeni na kumueleza kuhusu Michael lakini Sara hakutaka kusikia na kutumia Cheo chake kama Malkia kuwaamrisha iwe kama anavyotaka,hawakuwa na jinsi wale wazee japo mioyo yao haikutaka wakaipokea ile kofia kwa Michael na kumpa tu taarifa kuwa atamuoa Malkia na ndio atakuwa Mfalme wao,siku hiyo Eater alifuatwa na wafanyakazi wa Malkia na kuelezwa kuwa amepewa adhabu ya kuwa mhudumu wa Mfalme Michael siku ya harusi,alivyoambiwa vile alizidi kukasirika na kuona ni dharau kubwa sana,hakuwa na jinsi alibaki kuumia tu moyoni .Basi harakati za siku hiyo ya ndoa zikaandaliwa haraka na ndio siku ya Michael kuvalishwa kofia ya kifalme,na kweli siku yenyewe ilipowadia watu wengi sana walifurika hasa baada ya kusikia yuke kiongozi aliyetaka madaraka kwa nguvu Michael ndio anakuwa mume wa Malkia wao hivyo yeye ndio atakuwa Mfalme,kelele za watu zilisikika kwa chini chini wakiongelea kuhusu ndoa hiyo,Sara alikuwa kwenye kiti chake cha kimalkia huku Michael alikuwa kwenye vazi la kifalme akiwa kwenye kiti chake pembebu wakiwa wasuriati wenzake waluobaki,siku hiyo ilikuwa ni furaha kwao.Basi mzee mmoja mwenye hekima zake alinyanyuka na kuongelea machache kuhusu kumkabidhi ufalme Michael na ndoa ifungwe,basi baada ya kuongea machache akakaribishwa Mfalme mtarajiwa aongee na wananchi wake kidogo,Michael akasimama huku wasuriati wakimshangilia,akawa anaongea na watu machache akiwaahidi kuwa bora kwao na wasahau yaliyopita,wananchi walimuelewa na kumpigia makofi kwa wingi wakiwa na imani nae kwasasa,basi alipomaliza karudi kukaa na kukaribishwa Malkia naye aongee yake...naye aliongea machache wananchi wakampigia makofi.Michael aliongea na Sara jambo kidogo na Sara akaelewa,akawaambia wazee ili lifanyike haraka.Sara alisimama na kusogea mbele kuongea tena na wananchi huku wakina Denis,Natasha na Magreth wakiwa tu pembeni wanashuhudia tukio zima.
"Ili furaha na amani tuhakikishe kweli imerudi na kuungana na wenzetu wasuriati basi nimeandaa karamu ya kuunganisha pande hizi mbili kuwa sawa"alisema Sara na muda huo huo Ester akatokea akiwa ameshika sinia kubwa lenye chupa ya dhahabu iliyokuwa na kinywaji kikixhoandaliwa kwaajili ya kuunganisha pande hizo mbili kuwa pamoja,hata watu walishangaa kuona Ester amekuwa kama mhudumu jambo ambalo ni kama dharau...basi taratibu Ester akaanza kumimina kwenye vikombe kwa upole akitumikia adhabu yake,akampa Malkia kile kikombe,akamuwekea na Mfalme mtarajiwa Michael naye akapokea jwa daharau huku akimtazama Ester ambaye hakujali,akawamiminia na wasuriati wote wakapata.
"naomba kwa pamoja tufurahie kiny2aji himi kiwe kama kuoneaha umoja wetu"alisema Sara na kuanza kugongana vikombe kama kufurahia pamoja na kila mtu akanywa wakiongozwa na Malkia Sara na Michael huku watu wakipiga makofi na shangwe kwa kile kilichofanyika,wazee walikuwa wakitazama tu hawajashirikishwa kwenye ji ywaji na kuona Malkia amekaribisha vita.
"Basi kwa hili naamini kila mtu amekuwa shahidi wa hili,na muda mfupi tu nitawaonesha jambo nilili liandaa na hakuna hata mmoja wenu,hata Mfalme Michael hajui hili ila nitawaonesha sasa......"alisema Sara na kuwafanya watu wote wawe kimya kusubiria hilo jambo,haikupita dakika watu wawili wasuriati wakadondoka na kuanza kuatapatapa kama wanaumwa degedege huku damu zikiwatoka puani na mdomoni na papo hapo wakafa,sekunde chache mbele wakafuata wengine hali iliyowafanywa watu washangae hata wale wazee walistaajabu kuona vile.Michael alioagawa kuona vile na kujikuta akimgeukia Sara.
"umewafanya nini wenza ngu Sara um...."alishindwa kuendelea kuongea baada ya kuhisi kitu tumboni kinachoma.Ester alibaki ameshikilia lile sinia na kubaki kutabasamu..,alikumbuka usiku wa jana akiwa hapati usinfizi akifikiria kuhusu Michael anavyopata ufalme kirahisi gafla alijiwa na Sara na kumueleza ukweli kumbe siku zote hizo alikuwa akimuektia tu Michael kusudi aje mbele ya umati wa watu amfanyie kitu mbele zao nsio maana alijiweka karibu sana Michael akwaacha wenzake,akampa sumu na kumwambia aichanganye kwenye kiny2aji atakachokiandaa kesho,kinywaji chenyewe ndio hicho kinawamaliza wasuriati.Alimtazma tu Michael akiwa anashika tumbo lake..
Sara akimaogelea karibu na kumtazama.
"mimi ndio SARA....mtetezi wa wanyonge na mwenye kutaka haki muda wote,kabisa kwa akili zako ukafikiria Sara ake kuwa mkeo na uitawale Falme hii kirahisi uzidi kuleta mabalaa kwenye jamii yangu,hapana Michael hauwezi.....siku ile ulijuwa umenitulia uchawi ukadhani ndio umeniteka,nilienda kwa mama....Marehemu Aznaty kumlilia kwa maana napitia mateao mengi nisione mafanikio,na kweli kanisikiliza na kunipa nguvu mpya kwa kunipa sumu hii ninywe kisha siku ya leo nitakapokunywa tena nitapata kupona na kuwa sawa...sasa ninyi mmekunywa mara moja nadhani hiyo ya pili mtakunywa mkiwa kuzimu,mmetusumbua sana nyie wasuriati wacha leo iwe mwisho wa matatizo katika falme na jamii hii...naamini sasa watu wataisgi kwa amani mkiondoka nyie....Pole sana Michael."alisema Sara akiwa siriasi na kuwafanya hata wazee na wakina Denis washangae,hawakutegemea kabisa kama Sara alikuwa anacheza mchezo huo wa hatari bila kumsgirikisha mtu na mwisho we ndio kaja kumweleza rafiki yake wa pekee Ester na kusaidiana kufanikisha zoezi hilo,aliagiza Upanga mkali uletwe na mara moja akakabidhiwa mkononi mwake huku Michael akishuhudia upanga ule ukishikwa na Sara.
"Sara....nakuomba sana tena san....nisamehe Malkia....wewe ndio Malkia nakiri nimekosa na siwezi kurudia tena ni tamaa tu zilinijaa ahhhhhh"alisema Michael kwa huruma huku akisikia maumivu. makali sana tumboni,gafla tu damu zikaanza kumtoka mdomoni ile sumu iliyochanyanywa kwe ye kile kinywaji ni kali sana,alijitahidi kutamka maneno yake kuona kama anaweza kuootea kinaajabu lakini waoi,hakuna nguvu hizo tena kuona sasa ndio mwisho wake kweli.
"sidhani kama kuna mtu anakutamani hata kukusikiliza wewe..."alisema Sara na kuwageukia wananchi wake."eti jamani kuna anayempenda huyu mtu aendelee kuishi"aliuliza kwa sauti kubwa Sara.
"Auaweeeee"
"Afe huyo"
"Afeeee"
"Chinja shingo wote haooo"zikisikika kelele za watu wote wakioneaha hawapmpendi bora afe,Michael aliwatazama tu wale watu na kubaki kutabasamu tu hana ujanja,alinyanyua sura na kumtazma Sara.
"kweli nimeamini sipendwi,nimefanya mazambi sana,nastahili adhabu yeyote,niue tena kifo cha haraka nisipate tabu."alisema Michael mqenyewe akikiri kwa yale aliyoyasema.
Sara alinyanyua upanga wake mkali juu na kuanza kukumbuka matukio yote ya nyuma aliyofanya mtu huyu,ndiye aliyemsababisha Natasha kuonekana ana mashetani shuleni,ndiye aliyemuua mwalimu Eddy kwa ukatili pindi alipoenda bafuni,ni Michael ndiye aliyewachonganisha Natasha na Denis watamaniane lengo ni kuwaua lakini Sara aliwahi na kuwasaidia japo Denis alishakuwa tayari amekufa lakini alitumia uwezo wake kuurudisha uhai wake,Michael ndio aliyempa uchizi Ester na kumsingizia Sara kuwa mchawi akafukuzwa shule na ndio huyu aliye wasumbua kwenye mapanfo ya Amboni akitaka wafe kabisa na hapo walipo ndipo Sara siku ile alisulubiwa nusu auliwe na kisu na huyu Michael lakini Ester alimsaidia,matukio hayo tu yalimpandiaha hasira sana Sara na kuona Michael hapaswi kuishi,alivuta nguvu zake zote na kuushusha upanga ule moja kwa moja shingoni kwa Michael na kukitenganisha kichwa na mwili kivyake huku damu zikiruka na kuchafua nguo zake za umalkia,Denis na wenzake nao walisogea na kuwamalizia wasuriati walikari ua kukata roho na kukamilisha zoezi lao la kuteketeza jamii ya kisuriati yote,wazee walipiga goti wote na kuwafanya wananchi woote wapige goti chini kumpa heshima kubwa Malkia Sara kwa kile alichokifanya kwa kupoteza kabisa kizazi cha kikatili cha kisuriati,Ester,Denis,Natasha na Magrwth na walipoga goti chini ikiwa ni moja ya heahima mbele ya Malkia wao Sara,chozi lilimtoka akigeuka huku na kule kuona umati wa watu wengi sana wakimuunga mkono kwa kile kilichotendeka,alitupa upanga chini na kuanza kulia sana akikumbuka mateso na mitihani aliyopitia hadi leo kufika pale na qenzake salama,Falme ikawa na amani na furaha tangu suku hiyo huku wananchi wakizidi kumoenda Malkia wao kwa kuwajali na kuwasikiliza,aliwapa wenzake madaraka na vyeo kwenye baadhi ya sehemu ndani ya falme ile na kuwafanya nao waheahimike kama yeye.
Basi muda,siku na miezi ilienda na siku hiyo shule nyingi zilifungwa baada ya kupewa ripoti zao za mitihani waliyofanya wiki mbili nyuma kila mtu akataka kujua mwenzake amekuwa wangapi.
"mimi wa saba kati ya wanafunzi 56"alisema Natasha kufunua ripoti yake akwaoneaha wenzake wakaaminiCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"miye wa Tisa"alisema Magreth naye akafanya hivyo
"miye wa tatu"alisema Sara na kuonesha.
"Miye wa Tano"alisema Ester na kuonesha ripoti kwa wenzake...wakamtazama Denis wakimuona yupo kimya.
"Haya nawewe mwanaume wetu tuoneshe"alisema Magreth na wote wakamtazama Denis,taratibu akageuka na kuongoza njia kuondoka zake...
"Hata nyumbani siendi maana baba anajua tu nafasi yangu darasani....hapo kaanda mibakora yake na hanipati leo naenda kushinda kwenye falme hadi likizo iishe hiyooooo"alisema Denis na kuanza kukimbia na gafla akapotea kimaajabu kuonesha kweli ndio ameenda...wakina Sara walicheka sana kusikia hivyo kuona siku zote Denis ni mtu wa mwisho mwisho, basi waliahika mikono kwa furaha wakiyonayo na kukimbia nao wakaelekea nao kwenye falme baada ya shule kufungwa.
MWISHO WA SEASON 1
0 comments:
Post a Comment