Search This Blog

KISIWA CHA MAJINI - 1

 







    IMEANDIKWA NA : RAIS WA IRAMBA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Kisiwa Cha Majini

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ilikuwa mida ya jioni hivi nilikuwa nimebaki nyumbani peke yangu, mama yangu na baba yangu walikuwa wameenda kwenye msiba wa babu yangu maeneo ya kiomboi. Mdogo wangu Subira yeye alikuwa ameenda kwa Mama mdogo kwenda kuongea kwani Shule walikuwa wameshafunga. Hivyo nyumbani nilikuwa nimebaki peke yangu. Kwa kweli nyumba Yetu ilikuwa kubwa sana mimi nilikuwa muoga sana hivyo kulala peke yangu kwenye hiyo nyumba ilikuwa nikitu ambacho kilikuwa hakiwezekani kabsa. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nilichoamua muda ule ule niliondoka Na kuelekea kwa Rafiki yangu Mdete kwenda kumuomba ili Tuje kulala nyumbani wote. Kutoka nyumbani Sabasaba singida Hadi kwa kina Mdete unyankindi ilikuwa ni mbali kiasi hivyo niliamua kuchukua boda boda ili niwahi kufika. Nilipofika kwa mdete kwa kweli haikuwa bahati yangu kwani mama yake na mdete aliniambiakuwa Mdete alikuwa ametumwa Kijini kwao ndurungu kwa babu yake kwani kuna mzigo alimtuma kwenda kuchukua. Nilimuuliza mama yake na Mdete kuna uwezekano wa Mdete kurudi. Jibu la mama yake Mdete kuniambia kuwa mdete atarudi kesho na siyo leo ndio lilinifanya nikaaga haraka na kuondoka. Tayari hapo nilikuwa nimeshapanga Safari ya kwenda hadi Misuna kwenda Kumuangalia rafiki yangu Mwingine Juma ili nikalale naye. Nilikuwa nafanya vile kwani nilikuwa naujua udhaifu wangu kuwa nilikuwa muoga sana nisingeweza kulala nyumba kubwa kama ile peke yangu. Nilipofika kwa juma kwa kweli bahati ilikuwa imelalia upande wangu kwani nilimkuta Juma yupo. Nilimsalimia mama yake na juma kisha tulitoka pembeni na juma ili tutete pembeni. "Wewe kapopo hicho sahau mkubwa siwezi hata Siku moja kwenda kulala kwenu. Hivi kama nikikupitia tu nyumbani kwenu kwenda shuleni mzee wako huwa anafoka hivi akifikilia namvizia Subira je akinikuta nimelala humo si itakuwa kuuana sasa"Aliongea juma baada ya kumuelezea shida yangu. Nilimuelezea Juma kuwa baba yangu mama yangu pamoja na Subira wote walikuwa hawapo lakini juma alionekana kuwa mgumu hakutaka kabsa kwenda kulala kwetu. Ilikuwa kama utani utani lakini juma alikataa katakata. Kwa kweli sikuwa na jinsi niliamua kuondoka pale na kuelekea nyumbani kwani tayari ilikuwa muda wa saa moja hivi na giza ilishaanza kutanda. Nilipofika nyumba hivyo hivyo huku nikiwa nimeoogopa nilingia Hadi ndani niliwasha taa na kwenda hadi kwenye sofa na kukaa.nilipokaa kwenye lile sofa nilihisi kama Kichwa changu kinaanza kuongezeka Ukubwa huku nywele nazo nikianza kuona zinasisimka. Ile hali kwa kweli nilijua siyo hali ya kawaida maana mimi kama kichwa kikisisimka tu huwa inamaanisha kuna kitu cha hatari ambacho siyo cha kawaida kinaweza kunitokea. Niliamua kutoka pale ndani kwa kasi ya Ajabu na kuelekea flamingo bar. Huko nilipanga kwenda kutafuta hata mlevi yeyote ili tukasizi naye maana mimi kulala peke yangu nilikuwa siwezi kabsa.nilipofika Flamingo bar niliangaza lakini sikuona mlevi yeyote ambaye nilikuwa namfahamu. Kwa kweli nilizidi kuchoka, nilichoamua sasa ni kunywa pombe kwa Wingi sana ili nilewe nikifika home nijitupie tu kitandani na kulala. Nilipiga pombe aina ya safari kama nne hivi mfululizo hapo ndio niliona kichwa kinaanza kuyumba. Nilichofanya nilichukua na zingine mbili nilianza kuondoka moja kwapani alafu nyingine naifanyia unyambusi. Kwa kweli nilikuwa nimelewa mbaya hadi nilianza kudondoka. Uzuri nilishakaribia na nyumbani hata ile bar haikuwa far sana na home. Nilipofika nyumbani nilifungua mlango na kuingia hadi ndani. Ile nimeingia tu cha ajabu nilihisi tena kichwa kinasisimka ingawa bado nilikuwa nimelewa mbaya. Nilijivuta hadi chumbani kwangu kitandani na kwenda kukaa. Ile nimekaa nilibaki nikiwa nashangaa pombe yote niliyokunywa inayeyuka kichwani kwa kasi ya ajabu na kubaki kama vile sijanywa kabsa. Yani hata dalili ya kuhisi kama nilikuwa nimelewa ilikuwa hakuna. Muda huo kichwa kilikuwa kinasisimka mbaya. Nilichukua ile bia Moja iliyobaki na kuinywa kwa kasi yote cha ajabu nilikuwa nimekunywa kama maji tu kwani hakuna ambacho kilibadilisha mwili wangu zaidi ya tumbo kujaa. Nikiwa nipo pale nikishangaa ghafla nilianza kusikia harufu kali sana ya perfume. Kwa kweli nilishawahi kujisikia harufu nzuri sana za perfume kama One southand and nine, siliver, mrs juck na zingine kibao lakini sikwahi kuona perfume ambayo ilikuwa kali na inaharufu nzuri kama ile. Nikiwa nashangaa ile harufu ilikuwa inatokea wapi ghafla nilianza kusikia kama mtu akiwa anatembea sebureni. Ile hali kwa kweli ilizidi kunishangaza kweli. Niliamua kujikaza na kuamka nilienda nilifungua mlango na kuchungulia sebureni ili nione ni nani yule ambayo alikuwa anatembea. Cha ajabu nilipofungua mlango sikuweza kumuona mtu. Ile hali kwa kweli ilizidi kunitisha nilirudi chumbani kwangu nikafunga mlango kwa komea vizuri na kujitupia kitandani na kuanza kutafuta usingizi wa kulazimisha. Nikiwa nipo kitandani huku macho yakiwa mlangoni nilishangaa mlango wa chumbani kwangu unaanza kufunguka taratibu. Ile hali kwa kweli ilinishitua sana na kuanza kurudi ukutani. Kitendo cha mlango kufunguliwa wakati nilikuwa nimefunga alafu yule ambaye alikuwa anafungua alikuwahaonekani kiliniogopesha sana. Ule mlango ulipofunguka wote kwa kweli nipatwa na Mshituko wa kutisha sana Nilipomuona mtu wa ajabu sana akiwa anatoka chumbani kwangu akielekea sebureni na tayari alikuwa amekaribia mlangoni. Yule mtu mwili wake wote ulikuwa hauonekani. Kwanza alikuwa ni mrefu sana ila kichwa kilikuwa hakionekani wala kiuono, yani alikuwa anaonekana sehemu za kutoka kiuononi kwenda chini na kutoka shingoni kwenda hadi kwenye tumbo. Kiuno na kichwa vilikuwa havionekani. "Hahaha hahahaha hahahaha hahahaha hahahah kikikikkki kiiiiiiiiii huhuhuhu huuhuu"Kilikuwa ni kicheko kikali sana kilisikika kutoka pale chumbani kwangu. Kwa kweli kile kicheko kilikuwa kikali sana hadi masikio yaliziba.

    ********************************************************************************************** CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Kwa kweli kile kicheko kilikuwa kinatisha sana na kilikuwa kikali na kinaumiza masikio mbaya. Tangia nizaliwe sikuwahi kuona Mtu akiwa anacheka namna ile. Muda huo tayari mwili wangu ulikuwa umeshaloa jasho. Wakati nikiwa nashangaa kile kicheko kilikuwa kinatokea wapi Ghafla upepo ulianza kuvuma kwa kasi ya ajabu mle ndani. kwa kweli ule upepo ulikuwa mkali sana kila kitu kilikuwa kinapeperushwa mle ndani. Jikoni kulitawala kelele za vyombo tu jinsi vilivyokuwa vinapeperushwa. Tv zilianguka chini na meza yani vitu vyote vilikuwa vinapeperushwa. chupa ya bia ambayo ilikuwa imebaki nayo ilianguka chini. Yani ule upepo ulikuwa mkali sana hata kitanda ambacho nilikuwa nimelalia kilinyanyuliwa upande mmoja. Nilijikaza pale kitandani na kuamka ili kwenda kufunga mlango. Nilipofika nilishika mlango ili nifunge cha ajabu hata sentimita moja sikuweza kusogeza. Ule upepo ulivuma kwa kasi ya ajabu kwa muda kama wa dakika kumi ndio ghafla ulikata na kubaki kukiwa kimya kabsa. Cha ajabu upepo tu ulipoacha tu kuvuma vitu vyote nilishangaa kuona vipo kwenye sehemu husika kama kawaida. Tv ambayo ilikuwa imeanguka chini ilikuwa ipo vile vile kama ilivyokuwa mwanzo, pazia ambazo zilipeperushwa na upepo hadi zilichomoka nazo zilirudi kama ilivyokuwa. Yani vitu vyote vilivyo peperushwa na upepo vilirudi kama ilivyokuwa Mwanzo. Kwa kweli ile hali iliniogopesha sana kwani ilikuwa kitu kigeni sana kwangu. Nikiwa kwenye ile hali ya mshangao nilisikia kama mtu akiwa anatembea chumbani kwangu. Niligeuka haraka haraka kila sehemu ya chumba changu kuangalia kama nitamuona yule mtu ambaye alikuwa anatembea lakini cha ajabu sikumuona mtu. Kile kishindo cha mtu akitembea kiliendelea kusikika akitembea. Nikiwa nashangaa huyu mtu yuko wapi mbona anatembea humu humu chumbani. Ghafla niliona nyao za mtu kama vile anatembea anakuja kwenye kitanda ambacho nilikuwepo. Zile nyao zilikuwa na damu flani hivi yani ilionekana kama yule mtu ambaye alikuwa anatembea kwenye nyayo zake za miguu alikuwa anatokwa na Damu. Ile hali kwa kweli ilinifanya nianze kutetemeka mbaya Muda huo nilitamani kukimbia lakini nilihisi miguu yangu ikiwa mizito mbaya. joto ndani lilikuwa kinatisha mbaya utafikilia juu ya bati kuna mtu alikuwa amekoka moto. Nikiwa nipo sijui la kufanya nilibaki nikishangaa nilipoona mkono wa mtu tu ukichukua chupa ile ya bia moja iliyobaki na kuanza kumwaga bia chini. Cha ajabu kila bia ilipokuwa inafika chini ilikuwa inabadilika na kuwa damu. "Hahahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha kumbe na wewe muoga"Kilikuwa ni kicheko tena cha kutisha ambacho kilitokea nyuma yangu kwenye kona ambayo nilikuwa nimejibanza. Ghafla niliruka sehemu nyingine na kuangalia ni nani yule ambaye alikuwa anacheka nyuma yangu lakini sikumuona mtu wa aina yeyote. Ile hali kwa kweli ilizidi kuiogopesha kwani vitimbwi ambavyo niliviona kwa muda mchache vilinichosha ile mbaya. "Hivi wewe kijana unataka kuniambia sehemu ni hihi tu mbona umenibana sana sogea huko bhana. Mbona sehemu pana sana lakini umejibana kwangu"Ilikuwa tena sauti ya mtu ikisikika kutoka nyuma yangu. Ile nimegeuka kuangalia kwa kweli nilijikuta naruka kwenye kitanda na kutua chini kisha niliondoka kwa kasi ya ajabu na kwenda hadi kwenye chumba cha wazazi wangu. Kwani nilipokuwa nimegeuka nyuma nilimuona mtu wa ajabu sana. Kwanza kichwa chake pamoja na uso wake ulionekana kama umeoza alafu meno yalikuwa yametokezea zaidi kuushinda mdomo. Yule mtu alikuwa amevaa nguo nyeupe zote kuanzia juu hadi chini kiufupi yule mtu alikuwa anatisha mbaya. Nilipofika chumbani niliingia moja kwa moja hadi kwenye uvungu wa kitanda nikajibanza na kutulia kimya. Cha ajabu ambacho hadi sasa nikifikilia huwa sipati jibu nilipoingia kwenye uvungu wa kitanda na kujibanza nilikuja kushituka nimelala juu ya kitanda. Kwa kweli nilibaki nimetulia hivyo hivyo wala sikutingishika. Ghafla nilianza kuhisi usingizi ukinijia hatimae nililala sikujua kile ambacho kiliendelea. Nilipolala nilianza kuota nimelala na mwanamke mzuri sana. Yule mwanamka alinifuata na kuanza kunishika shika. Kwa kweli jinsi alivyokuwa mzuri yule mwanamke nilijikuta na mimi nikianza kumshika shika. Nilipokuja kushituka cha ajabu nilishangaa nilipokuta nipo juu kwenye mti wa mbuyu alafu nilikuwa napapasa tawi la mbuyu ambalo nilikuwa nimelalia





    Kwa kweli nilipojikuta nimelala juu ya Mti wa mbuyu nilibaki nikiwa nashangaa tu. Sikuamini kama kweli nipo kwenye tawi la mbuyu au nilikuwa ninaota. Ilibidi nipeleke mkono kwenye macho yangu nikafikicha ili nihakikishe kile nilichokiona ni Kweli au naota. Hata nilipofikicha macho yangu ukweli uliendelea kubaki pale pale nilikuwa nimelala juu ya mbuyu. Kwa kweli niliogopa Sana ile hali kwani ninachokumbuka nilikuwa nimelala chumbani kwenye kitanda cha wazazi wangu sasa huku nimefikaje. Niliaza kushuka kwenye huo mbuyu huku nikiwa napiga kelele za kuomba Msaada sikujali hata kama ilikuwa ni usiku. Nilipoangalia kwa chini nilimkuta mtu akiwa kama Anaswali hivi huku akiwa amevaa nguo zote nyeupe. Mimi wala sikutaka kumfatilia sana yule mtu, bado niliendelea kupiga Kelele ya kuomba Msaada huku nikiwa naendelea kuhangaika kushuka kwenye huo mbuyu. "Wewe kijana hebu jiheshimu bhana utatupigiaje kelele watu wengine wamelala sasa hivi na wengine wanaswali. Hebu acha huo upumbavu wako"Nilisikia mtu akiwa ananiongelesha kwa Nyuma yangu. Niligeuka kwa haraka kuangalia yule alikuwa nani ambaye alikuwa ananisemesha kwenye ule mbuyu usiku kama ule. Nilipogeuka kuangalia nilijikuta mwenyewe najirusha kwenda chini nilipomuona Mtu wa ajabu sana akiwa kwenye ule mbuyu. Yule mtu hakuwa tofauti sana na yule ambayo nilikuwa nimemuona ndani. cha ajabu nilipojirusha kwenda chini nilishitukia mtu amenidaka."Kuwa makini wewe siyo kila sehemu ni ya kuruka tu. Utakuja kufa unafikili kama nisingekuwa naswali hapa nani angekudaka"Aliniambia yule mtu ambaye alikuwa amenidaka kisha alinitupa chini. Huyu mtu aliyenidaka nilipomuangalia yeye alikuwa ni Mwanamke flani mweupe ambaye alikuwa mzuri sana. Kilichokuwa kinanishangaza ule muda ilikuwa ni usiku ambae sikujua ni saa ngapi ila yule mtu alionekana vizuri tu hadi nilimtambua kuwa alikuwa wa kike. Baada ya yule mtu kunitupa niliamka haraka haraka huku nikiwa natetemeka na kuanza kukimbia. Mwendo ambae nilikuwa nakimbia ilikuwa wa hatari sana na ilikuwa usiku sikujali hata hii sehemu ilikuwa na miiba na nilikuwa nakimbia huku nikiwa sioni nilikuwa nakimbia naelekea wapi. Kiujumla nilikuwa nakimbia ilimladi niende mbele tu. Nilikimbia Kwa muda kama wa nusu saa ndio nilikuja kutokea kwenye barabara ambayo kwa haraka haraka nilijua ilikuwa ni barabara kutoka manyoni kwenda singida town. Niliendelea kukimbia huku nikiwa nimefuata barabara huku nikimuomba Mungu hataCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Gari tu iweze kutokea nipande. Maombi yangu nahisi mungu aliyaelewa kwani haikupita hata muda mrefu niliona kama Gari ilikuwa inakuja. Ilibidi nisimame kabsa barabarani ili kuja kuisimamisha nipande. Ile gari ilipofika karibu kabsa na mimi nilishangaa inapotea sikuona imeelekea wapi nilikuja kushitukia imeshapita na ilikuwa inasikika kwa nyuma yangu. Niligeuka kuangalia kweli niliona taa zile inakwenda. Kwa kweli yale yalikuwa ni maajabu sana ambayo sikuwahi kutegemea kuyaona. Nikiwa nipo nimesimama nawaza jinsi lile Gari lilivyopotea kisha kutokea kwa mbele yangu nilisikia mlio wa gari tena. Kama Kawaida nilikaza moyo wangu nikasimama barabarani na kuanza kusimamisha. Bahati muda huo ilikuwa imelalia upande wangu kwani ile gari iliponifikia ilisimama kisha nilienda kupanda na gari iliondoka. Ile Gari ilikuwa ni Coster flani hivi. Nilipopanda kwenye ile Gari kama wasiwasi flani ulianza kuniingia kwani watu ambaye walikuwepo kwenye ile Coster wote walikuwa kama Waarabu hivi harafu walikuwa na sura nzuri sana. Nilijiuliza maswali Mengi sana kuhusu ile gari iweje gari wawe waarabu watupu. Lakini nilijipa moyo huenda walikuwa wamekodi. Safari iliendelea kwa Muda kama wa nusu saa hivi bado nilikuwa sijapita hata sehemu moja ambayo nilihisi huenda nilikuwa naifahamu. "Konda naomba nishushe kwenye huo Msikiti wa jini Maimuna"Alikuwa ni abilia mmoja akiwa anamwambia yule Konda. Yale maneno kwa kweli yalinishitua sana. Kwani nimewahi sana kusafiri kutoka singida manyoni, singida dom singida Dar lakini hakuna hata kituo kimoja ambacho kilikuwa kinajulikana kwa jina la Jini maimuna. Ile hali kwa kweli ilinishitua sana. Kweli ile Gari ilifika sehemu moja ambaye kulikuwa na Msikiti hivi ilisimama. Nilipochunguza ule msikiti kwa kweli kwangu ilikuwa ni Mgeni kabsa. Kitukilichozidi kuniogopesha na kunitia wasiwasi ni ile harufu ya perfume ambayo nilikuwa naisikia ndani kwangu ilianza kusikika tulipofika kwenye huo msikiti. Yule mtu aliposhuka Gari iliendelea na safari. Lakini ghafla gari ilisimama tena "Konda nimesau mkoba wangu samahani kidogo"Aliongea yule mtu kisha kilichonishangaza hadi sasa hivi nikiwaza hadi kichwa kinasisimka. Yule mtu alipopanda mlangoni mwa gari wala hakuenda kwenye siti ya gari kwenda kuchukua begi aliachama tu na ulitokea ulimi mrefu ulienda hadi Kwenye siti ukachukua Mzigo kisha alishuka tena na gari iliendelea na safari. Kwa kweli ile hali ilinifanya niogope ile mbaya. Moja kwa moja nilianza kuhisi hii gari ambayo nimepanda siyo yenyewe hata kidogo. "Hizi siti za gari wamezibana sana bhana yani mtu hadi miguu inakufa ganzi"Aliongea mzee mmoja wa kiarabu wa makamo ambaye tulikuwa tumekaa siti moja kisha alitoa miguu yake na kuweka juu ya siti. Kwa kweli nilishituka sana nilipoona ile miguu ya yule mzee ilikuwa kama ya punda hivi.



    Kwa kweli nilishituka sana nilipoona ile Miguu ipo kama ya Punda. Mapigo yangu ya Moyo yalianza kwenda mbio na kugundua nilikuwa katika mazingira ya hatari sana. "Unajua jini unaweza kulitambua kwenye miguu yake. Majini mengi yakiwa kwenye ujini wake huwa na miguu yenye kwato kama ya punda, ng'ombe au farasi"Nilikumbuka Moja ya Maneno ambayo watu huwa wanasimulia nilijua moja kwa moja nimepanda gari la majini. "Haa! Wewe kijana mbona unanishangaa hivi na Umekodolea miguu yangu macho inamaana huijui au"Aliongea yule mtu ambayo tulikuwa nayo huku akiisogeza kabsa miguu yake karibu na kwangu. Kwa kweli Nilitoka nduki pale kwenye kiti cha Gari maana si nilikaa kiti cha pembeni. Nilipochomoka kwenye kile kiti nilianza kukimbia kwenda kwenye mlango wa gari huku nikipiga kelele za kutaja jina la Mama yangu badala ya Mungu wangu kwani yeye ndio mwenye uwezo wa kuniokoa na siyo mama. Wakati nikiwa nakimbia huku nikiwa napiga Kelele cha ajabu ghafla nilishangaa nikiona nipo Sebureni Chumbani kwangu huku nikiwa nakimbia. nilienda kupalamia Sturi ambayo ilikuwepo Njiani na kuanguka nayo hadi chini. "Kijana polepole bhana utakuja kuniua tatizo nini. Hebu amka bhana wengine wazee utakuja kuniua"Nilisikia kama mtu ananisemesha pale chini sehemu ambayo nilikuwa nimeangukia. Nilipoangalia kweli nilikuta nimemwangukia Mzee flani hivi ambaye alikuwa amevaa nguo zote nyeupe. Niliamka pale kwa kasi hata maumivu ambayo nilikuwa nimeyapata ya kupamia Sturi nilikuwa siyaoni. Nilipoamka moja kwa moja nilienda hadi kitandani kwangu nikajitupia na kujibanza kwenye ukuta. Kitu ambacho kilianza kunishangaza baada ya kujitupia tu Kitandani nilianza kusikia usingizi wa Ajabu sana ukinijia. Sikumaliza hata dakika mbili tayari nilikuwa nimeshalala. Baada ya usingizi kunipitia kwa kweli nilianza kuota kuna mwanamke mzuri sana ambaye alijitambulisha kwa jina la maimuna amekuja anataka mimi nimuoe. Huyo Mwanamke alinieleza kuwa ni jini na anahitaji nimuoe na tunaenda kuishi chini ya bahari. Nilikuja kushituka Kama mtu akiwa ananiita hivi huku akiwa ananitingisha. Niliposhituka na kutoa shuka ambayo nilijigubika nilishangaa namuona alikuwa rafiki yangu Mdete. "Kapopo vipi yani jombaa hadi sasa hivi bado umelala. Kweli mtoto wa bosi siku zote lazima uwe boss tu yani mwana bado umechili. Vipi nilisikia Jana ulikuja kuniulizia Nyumbani"Aliongea Mdete. Mimi bado niliendelea kushangaa tu maana tayari ilikuwa saa nne hivi asubuhi. Ghafla matukio ambayo yalinitokea Usiku yalianza kunijia. Kwa kweli nilikuwa nimechoka kichizi. Niliamka nikamuelezea Mdete kila kitu ambacho kilinitokea sikuacha hata kimoja. "Daah jamaa yangu muombe mungu iwe kweli basi. Maana ukiwa na uhusiano na jini tayari Hata mimi rafiki yako mdete nitakuwa nime wine. Bhana kama hujui majini ukibahatika kuwa na uhusiano nao jua umeshakuwa tajari moja kwa moja. Kwa nini mimi huwa sipati bahati kama hizi yani nayatamani sana haya majini. Bahati hii mchizi wangu kapopo usiiache tena mimi nazidi kukuombea kwa mungu yawe ya kweli"Aliongea rafiki yangu Mdete na kuniacha Mdomo wazi nikiwa namshangaa. Sikutaka Kuongea sana maana mambo ambayo niliyashuhudia yalikuwa siyo ya kawaida sana. Tulipika chai na Mdete tukanywa kisha tuliamua kutoka ili tukatembee Tembee kidogo Maeneo ya Msufini. Wakati tukiwa tunaendelea na safari yetu nilipofika Maeneo ya jengo la T.R.A Nilimuona Mwanamke ambaye alikuwa anafanana kwa kila kitu na Mwanamke ambaye nilikuwa nimemwota kwenye ndoto. Yule mwanamke alikuwa vile vile, kuanzia mavazi, msuko wa nywele, sura hata tembea yake. Kwa kweli ile hali ilinishangaza sana kwani haikuwa kawaida kumuona Mtu ambaye ulimuota ndotoni akiwa anafanana namna hiyo. Nilichoamua nilipanga kumfuata huyo mtu alafu nikamwite jina lake maana yule wa ndotoni alikuwa amejitambulisha kwa jina la maimuna. nilimfuata tule Binti hadi nilimfikia kisha nilimuita jina lake. "Kapopo nini bhana nina haraka kwani wewe unashida gani. Kama unashida nitakutafuta ila sasa hivi ninawahi sehemu"Alinijibu yule mwanamke bila hata kugeuka kuangalia ni nani ambaye amemwita. Kwa kweli ile hali ilinishangaza Sana kwani mtu kumuita alafu ataje jina langu bila kugeuka kuniangalia kilinishitua Sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Kwa kweli hakuna Siku niliyopata Pressure kama ile. Nilibaki nikiwa nimesimama tu kwenda mbele kumfatilia yule binti niliashindwa wala kurudi nyuma nilishindwa nilibaki nimesimama huku nikimwangalia yule binti kwa macho. Nilijiuliza maswali mengi sana kuhusu yule binti lakini sikupata jibu. Kitendo cha yule Mwanamke kufanana kwa kila kitu na yule binti ambaye nilimuota kwenye ndoto kisha nilipoenda kumuita aliitika huku akitaja jina langu bila hata Kuniangalia kwa kweli kiliniacha wakati mgumu mbaya. "Wewe kapopo twende bhana, nilishakwambia hao Mabinti siyo Saizi yako waachie watu wenye migodi yao ya Madini. Unaona umepewa Jibu moja tu alafu umebaki umekanda kama umedondokewa na barafu"Nilimsikia rafiki yangu Mdete akiongea Huku akicheka. Kitendo cha Mdete kuongea Ndicho ambacho kilinishitua na kugeuka kuendelea na safari. "Unajua Mdete unavyomaanisha Siyo kabsa, huyu binti siyo kwamba amenipa jibu moja nikashindwa kuendelea lahashaa. Unakumbuka kuwa nilikwambia kuna Mwanamke wa kijini anaitwa Maimuna nilimuota kwenye ndoto kuwa anahitaji nimuoe. Sasa yule Mwanamke ambaye nilimfuata alikuwa anafanana vile vile na Maimuna yani kuanzia kila kitu hadi tembea yake. Kwa kweli nilipoona wanafanana vile vile niliamua kumfuata ili nimwite jina lake nihakikishe anaweza akawa Mwenye. Nilipomwita hilo jina cha ajabu alinijibu bila kugeuka kuniangalia huku akiwa ametaja jina langu"Nilimwelezea Mdete uhalisia wa mambo hadi Mdete naye alibaki akiwa anashangaa tu. "Hayo unayo yaongea ni kweli baba au unajioshea tu kwangu"Aliniambia Mdete huku akisimama kuacha kuendelea na Safari. Kwa kweli yale maneno ya Mdete yalizidi kunishangaza. Mimi nilikuwa namwambia vitu ambavyo vilikuwa vinanitisha alafu yeye analeta utani at najioshea. "Mdete kwenye haya mambo hebu tuache utani bhana, Ninachokwambia ni kweli yule ambaye tumekutana ndio Jini maimuna ambaye nilimuota Usiku kwenye ndoto"Nilimwambia Mdete huku nikiendelea kutembea maana Mawazo ya mdete niliona ni hasi yote yanaweza kuniunguza tu. "Kapopo kama kweli huyu ndio mtoto ambaye umemuota kwenye ndoto usiku hata kama jini nakushauri oa. Kwa kweli tangia nizaliwe sijawahi kuona binti mzuri kama huyu. Hivi wewe umeshawahi kuonja penzi la watoto wa kiarabu acha uboya wewe. Tuulize sisi tukusimulie, Watoto wa kiarabu kama Huyu uliyekutana nao wanamapenzi ambayo yana Masters kabsa. Kwanza nywele zao tu jinsi zilivyomwagika Mgongoni hata Mwenyewe utapenda weupe sasa wa mwili wake acha utani oa wewe fala. Sijui kwa nini hizi bahati mnapata nyinyi makenge. Kwanza achana na Mapenzi ukioa Jini moja kwa moja utakuwa Tajiri maana majini huwa matajiri kichizi au Hupendu uje kunipa hata Noah moja na mimi rafiki yako"Aliongea Mdete huku akiwa siliasi mbaya. kwa kweli nilibaki nikiwa Namshangaa tu Mdete kwa nini alikuwa anayapenda hivi majini. Sikutaka sana kuendelea kuongea na Mdete maana nilijua maneno ambayo anaongea mdete hakuna hata moja ambalo linijua nitalifanyia kazi. Tuliondoka pale na kuendelea na Mishe zetu. Tulienda Msufini tulicheza Pool table hadi kwenye Muda wa saa tisa ndio tuliondoka hadi kwa kina Mdete na kwenda kula. Yani hiyo siku nyumba nilikuwanimeizira kichizi sikutaka hata kurudi nyumbani. Muda wa saa moja tulirudi hadi nyumbani kwetu tukiwa na Mdete tulifungulia kuku kisha tuliondoka kuelekea tena kwa Mdete maana nilipanga kwenda kulala huko. Tulipofika kwa kina Mdete tulikula chakula cha usiku na kuelekea ghetoni kwa Mdete ili kwenda kulala. "Daah kweli majini noma wewe ambaye dini kwako imekimbiaga, unamiaka hujawahi kwenda Msikitini leo unaomba Kabla ya kulala leo noma. Mimi naomba hayo majini yaje alafu uyaambie mimi nataka yanichukue maana wewe unalinga sana"Aliniambia mdete alipoona naomba. Aliyoongea Mdete nikweli wakati wa kulala nilikuwa mtu wa kulala tu bila kuomba ila muda ule nilikuwa naomba. Yale maneno ya Mdete yalinikumbusha pia maneno ya shehe aliyosema watu humkumbuka mungu wakati wa shida tu. Baada ya kuomba nilijitupia kitandani na kulala. Muda wa usiku wakati nikiwa usingizini nilikuwa nasikia kama watu wanapiga kelele. Nilipokuja kushituka kwa kweli nilibaki nikiwa nashangaa nilipojikuta nimelala chumbani kwangu nyumbani huku watu ambaye walikuwa wamevalia nguo nyeupe walikuwa wanazunguka huku wakipiga zikiri huku Ubani nao ulikuwa unanukia kichizi.





     Nilipokuja kushituka na kujikuta nimelala chumbani kwangu huku Pembeni watu wakiwa wananizunguka huku wakipiga zikiri kwa kweli niliogopa sana. Ile hali ilinifanya nikaogopa Sana huku nikivuta kumbukumbu kali. Nilichokumbuka Nilikuwa nimelala na rafiki yangu Salumu unyankindi Sasa iweje nijikute nimelala Chumbani kwangu. Niliamua kuamsha kichwa na kufikicha macho ili Kuamini haye ambayo nilikuwa nayaona ni kweli naota. Nata nilipoamsha macho na kufikisha kichwa ukweli uliendelea kubaki pale pale nilikuwa nimelala Chumbani Kwangu Sabasaba. Nilipoamsha Kichwa ile harufu kali ya Perfume ambayo nilikuwa naisikia chumbani kwangu Jana ilitanda Kwenye pua yangu. Kwa kweli Uvumilivu ulinishinda niliamka kwa Kasi ya ajabu huku nikipiga kelele za Kumuita mama badala ya Mungu. Cha ajabu nilipopiga Kelele za kumuita mama nilijishangaa nikiwa kwenye gheto la Mdete huku nikiwa napiga kelele. "Kapopo nini bhana unatupigia kelele usiku huu, watu tumelala na nilikuwa naota Ndoto nimependwa na jini wewe unanikatisha. Hivi unataka uwe unaota wewe tu umependwa na jini siyo"Aliongea Mdete huku akijitengeneza na kuendelea kuuchapa Usingizi. Kwa kweli yale maneno ya mdete yalizidi kunishangaza. Nilishindwa kuelewa kwa nini Mdete alikuwa anapenda Namna hii majini. "Mdete siyo kwamba nakupigia kelele bure. Unajua nilipokuwa nimelala niliposhituka nilijikuta nimelala chumbani kwangu huku watu wakiwa wanazunguka huku wakipiga zikiri. Niliamsha shingo nikafikicha macho ili nihakikishe ni kweli. Hata nilipofikicha macho ukweli uliendelea kubaki palepale nilikuwa chumbani kwangu. Mbaya zaidi na hiyo perfume ya yule jini Maimuna ilitanda chumbani kwangu. Nilipojaribu kupiga kelele za kuomba Msaada cha ajabu nilijikuta nipo kitandani kwako"Nilimwambia Mdete huku nikipiga kelele. "Mungu wangu kwanini wewe kapopo umepiga kelele sasa, kwa nini ndoto kama Hizi nisiote mimi. Au Mungu unaubaguzi nini basi Mungu nisaidie na Mimi nipendwe na Jini maana Naona unawapa bahati watu ambae hawataki. Tena Hayo majini ya Zikiri mimi nayapenda kichizi kwani hayana mashariti hata makubwa. Yakikupenda utasikia yanakuambia Muoe Maimuna alafu uhakikishe usitembee na mwanamke yeyote nje ya ndoa. Sasa mimi Mdete mtoto wa Mzee Kibindi nipate mtoto Mzuri wa kijini kama Maimuna alafu nianze kutembea na wabongo labda niwe chizi"Aliongea Mdete huku akiwa Amenyoosha Mikono yake juu kama Inshara ya kumuomba Mungu Amsaidie. Kwa kweli katika siku ambazo nilimshangaa Mdete ilikuwa ni siku hiyo. Niliwaza Mdete ameingiwa na kitu gani hadi amekuwa hivi lakini sikupata jibu. Nikiwa nashangaa Ile hali Ghafla Mlango wa Chumbani Kwetu ulifunguliwa na Upepo mkali ulianza kuvuma ile mbaya. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Ule upepo ulikuwa hauna tofauti na Ule ambao ulikuwa unavuma Siku ile nyumbani Kwetu kwani hata kitanda chetu kilikuwa kimenyanyuliwa upande vile vile. Ule upepo ulivuma kwa Muda kama wa dakika tano kisha ulikata ghafla. Ulipokata Ule upepo nilianza kusikia Joto kali sana na ule mlango ulikuwa umejifunga tena. Yani lile joto lilikuwa linatisha utazani tulikuwa tumekoka moto mkali juu ya bati. Tukiwa tunaendelea kushangaa yale mambo ambayo yalikuwa yanatokea ghafla Mlango ulifunguka wa chumba ambacho tulikuwa tumelala. Ule mlango ulipofunguka kwa kweli nilibaki nikiwa nashangaa nilipoona Bonge la bahari inaonekana huku kukiwa na maandishi ambayo yalikuwa yanasomeka hivi. "KARIBU KAPOPO KWENYE ULIMWENGU WA PILI WA DUNIA YANI ULIMWENGU WA MAJINI* Kwa kweli nilipoona yale maandishi nilijikuta woga unaongezeka kwa hali ya juu hadi mikojo ilikaribia kunitoka. Nilipomwangalia Mdete cha ajabu nilimkuta anatetemeka ile mbaya huku tayari Suruali yake ilikuwa imeshaloa mkojo. Kwa kweli nilibaki nikiwa nashangaa huyu Mdete ambaye muda wote alikuwa anaomba kutokewa na jini. Leo hii ameona maji tu na upepo kidogo mikojo imeanza kumtoka je akikutana na matukio ambayo yalikuwa yananipata mimi si angekuwa anazungukwa na nzi kabsa. Wakati nikiwa Namshangaa Mdete nilishangaa yale maandishi yanaanza kupotea moja moja. Yalipoisha tu yale maandishi nilishangaa Kumuona Maimuna Mwanamke ambaye nilimuota ndotoni kisha tulikutana tazara aliibuka kwenye yale maji. Alipoibuka tu alianza kuja sehemu ambayo tulikuwa tupo huku Perfume ambazo zilikuwa zinanukia Chumbani kwangu zilitanda mbaya.





    Kwa kweli nilipomuona Maimuna akiwa anakuja kwenye kile chumba ndio nilizidi kutetemeka ile mbaya. Kwanza bado sikuelewa kwa nini ile nyumba kwa muda ule ilikuwa inaonekana iko karibu na bahari kubwa namna ile. Wakati mkoa Mzima wa Singida hakuna bahari hata yakusingizia.Wakati nikiwa natafakari yale Mambo nilimuona Rafiki yangu Mdee akiamka Kwenye kitanda na kuanza kukimbia kwenye ule mlango ambae ulikuwa umefunguliwa huku akiwa anapiga Kelele za kuomba Msaada. Alipofika kwenye mlango tu wa kutokea kwenye chumba Ambacho tulikuwa tumelala. Cha ajabu alianza kuyumba huku Damu zikiwa zinamtoka mdomoni Puani na Masikioni kisha alienda Mzima mzima hadi chini. Kwa kweli ile hali ndio ilizidi kunichanganya kichwa changu. Taratibu mikojo ilianza kunitoka huku kasi ya Jasho ikiongezeka Mwilini kwangu utafikilia nacheza mpira wa miguu saa nane mchana Dsm. "Uliniita Kwenye Jengo la T.R.A nikakwambia kuwa nipo busy kuwa tutaonana Siku nyingine. Sasa ndio nimekuja Kukuchukua tukaongee zaidi"Aliongea Maimuna huku akiwa ananisogelea kwenye kile kitanda ambacho nilikuwepo. Kwa kweli yani pale nilikuwa nimeogopa mbaya. Ingawa mtu ambaye alikuwa ananisemesha alikuwa mzuri wa kupindukia ila mimi nilikuwa namuogopa mbaya. Nilisogea ukutani kabsa mwa kitanda na kujibanza kabsa huku Mdomoni nikitaja Jina La Mungu kama takataka ili Anisaidie. Nikiwa nimejibanza ukutani Ghafla nilimuona Maimuna anapotea kisha alitokea tena juu ya kitanda changu. Alinisogelea kabsa hadi sehemu ambayo nilikuwepo akanishika huku akinisihi kama nataka kuwa Salama niamke. Sikutaka kuwa mbishi maana umri wangu kweli nilikuwa nataka kuendelea kuwa mzima. Niliamka tu taratibu ili Kumsikiliza Maimuna alikuwa anataka kunifanyaje. "Sasa kapopo kuna sehemu nakupeleka. Huko kila kitu ambacho utakuwa unaulizwa utatakiwa kukubali. Kiufupi tu mimi nimetokea kukupenda Sana hivyo nahitaji unioe ili niwe kama Mke wako. Naimani ukinioa Utakuja kuishi maisha ya furaha Sana huku huku duniani"Aliongea Maimuna huku akiwa ananivuta kuelekea sehemu ambayo alikuwa amesimama. "Hapana mimi bado nasoma nasema mimi siwezi, naomba unisamehe dada yangu" Nilimwambia Maimuna huku nikiwa natetemeka. "Hilo nalitambua ila utaenda kutoa Sababu za kunipinga huko huko. Kama watakuelewa basi nitakuacha"Aliongea maimuna na kuzidi kunishangaza kwani sikuelewa ni wapi anataka kunipeleka. Maimuna aliponivuta hadi alipohakikisha nipo Karibu na yeye alinisogeza na kunilaza kwenye kifua chake kama mama anataka kumnyonyesha mtoto wake. Aliponiliza tu kwenye kifua chake nilimuona ananyanyua mkono wake na kuelekeza juu. Ile amenyanyua Niliona nyumba kwa juu inaachanuka na kuwa wazi. Kwa kweli ile hali ilizidi kunishangaza ile mbaya. Wakati nikiwa naendelea kushangaa taratibu niliona tunaanza kupaa kuelekea juu huku maimuna akiwa amenikumbatia



     Kwa kweli ile style ambayo tulikuwa tumetoka nayo mle ndani hadi mimiilikuwa inanigopesha sana. Ile chumba ambayo nilikuwanimelala na Mdete ilikuwa imepigwa Gymsung board kabsa. Sasa kitendo cha Maimuna kunyoosha Mkono wake tu kisha ile Gymsang kuachanuka ikaacha Uwazi kisha tulipaa kuelekea juu kwa kweli kilinishanga ile mbaya. Wakati nikiwa Juu hewani nilishindwa nifanyaje kwani Kufurutuka nilikuwa lazima nianguke. nilifikilia kwa makini nifanye nini niliamuabora nifurutuke tu hata nikianguka poa tu kuliko kuondondoka na yule jini. Wakati nikiwa nawaza hivyo nilishangaa kuona Upepo ukinipulizia kwenye Macho yangu. Ule upepo uliponipulizia nilianza kuhisi mwili wangu kama Unapoteza nguvu kwa kasi ya ajabu huku macho yangu naye yakipoteza uwezo wa kuendelea kuona. Hatimae sikumaliza hata dakika mbili tayari usingizi Mzito ulikuwa Umenipitia Sikujua Kile ambacho kilikuwa kinaendelea. Nilipokuja Kushituka nilijikuta Nipo kwenye ukumbi flani hivi mzuri huku nikiwa nimekaa kwenye kiti kizuri ile mbaya. Kwa mbele yangu kulikuwa na watu wa ajabu sana na wao walikuwa wamekaa kwenye viti. Wale watu kwa kweli walikuwa wa ajabu sana kwanza miguu yake ilikuwa inafanana na Kwato za Punda huku Wakiwa na Masikio makubwa kama ya Farasi. Macho yao yalikuwa kama ya binadamu lakini akikuangalia yalikuwa mekundu kama kama Kaa la moto. Nilipogeuka kwe ye mkono wangu wa kushoto na kulia niliona kuwa pale mbele Sikuwa peke yangu bali kulikuwa na Watu wengine ambae walikuwa na Sura za kutisha na wao walikuwa mbele na walikuwa wamekalia vitu vizuri kuliko hata changu. "Baba huyu ndio Mwanaume ambayenitafunga naye ndoa. Hivyo amekuja hapa yupo tayari kukusikilizi wewe kwa mahari ambayo atakwambia"Nilisikia kama mtu akiwa anaongea kwa Nyuma yetu. Ile sauti kwangu ilikuwa siyo ngeni sana kwangu. Moja kwa moja nilijua alikuwa Maimuna. Nilipogeuka kuangalia kweli nilimuona Maimuna akiwa kwenye vazi zuri ile mbaya.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kweli lile Vazi jeusi aina ya Hijabu ambaye alikuwa amevaa Maimuna lilimfanya apendeze sana. Maimuna alikuwa ni moja ya wanawake wazuri sana sura yake nyeupe ndio iliyofanya kwenye ile hijabu kuonekana kuwa alikuwa mwanamke wa mzuri wa kupindukia. Kwa kweli yale maneno ya Maimuna ndio Yalizidi kunichanganya. Maimuna mimi hata Siku moja sijawahi kukaa na yeye tukazungumza kuwa tutaoana. Achilia mbali kuoana hata kukaa tu nikamtongoza au yeye akanitongoza ilikuwa hakuna. Nilitamani kuongea ili kupinga kile ambacho alikiongea Maimuna lakini nilishangaa mdomo wangu ukiwa mzito mbaya. Kila nilipokuwa Najitaidi kunyanyua Mdomo ili kuongea nilikuwa nashindwa na mdomo wangu ulikuwa unatetemeka. Ile hali kwa kweli ilizidi kunishangaza zaidi. Muda huo sikuwa na jinsi tena nilimwacha tu Maimuna kuongea yale maneno yote ambaye alikuwa anayataka. "Mwanangu kwa kweli umechagua Mwanaume mzuri sana kama wewe. Nazani atakuwa mwanaume mcha mungu, mwanaume mwenye heshima. Ndio maana mimi nilikushauri ukitaka mtu wa kukuoa kamtafute binadamu mwenye tabia nzuri akuoe. Nahitaji kupata wajukuu wenye sifa za Mchanganyiko mimi. Nusu awe binadamu alafu nusu awe jini hii itakuwa safi sana"Aliongea mtu mmoja hivi ambaye alikuwa na sura ya kutisha kimyama. Kwa maneno ambayo alikuwa anaongea yule mtu moja kwa moja nilijua anaweza akawa ndio baba yake na Maimuna. "Sasa kapopo wewe ni kijana wangu na napenda sana uwe miongoni mwa watoto wangu. Mwanangu kama alivyosema kuwa amekuchagua wewe ili uje umuoe. Je wewe upo tayari kufunga pingu za maisha na Mwangu Maimuna binti Hijirafu"Aliongea tena baba yake na Maimuna. Kitu ambacho kiliendelea kunishangaza pale yule mzee wakati akiwa anaongea ghafla alibadilika ile sura yake ya kutisha nakuwa na Sura ya kawaida ya ubinadamu. Kwa kweli hata yule mzee alikuwa na Sura nzuri kwani alikuwa Mwarabu ambaye alivaa kanzu nyeupe huku kichwani akiwa amevaa kofia. Cha ajabu watu wote mle walikuwa hawana sura tena za kutisha wote walikuwa na sura za kibinadamu tu alafu walikuwa na sura nzuri sana. Kwa kweli mimi nilibaki nikiwa nashangaa tu kwani yale mambo ambayo yalikuwa yanatokea mle yalikuwa mageni sana kwangu. "Kapopo nakuuliza upo tayari kumuoa Mwanagu Maimuna bint Hijirafu"Aliongea tena Yule mzee kwa sauti kidogo hali iliyonifanya nikumbuke kama nilikuwa nimeulizwa swali. "Hapana siwezi kukubali kumuoa Maimuna mimi bado nasoma na siwezi kabsa kumuoa Mwanamke huyu maana bado mwanafunzi"Niliongea kwa sauti ya juu. Ila kwa kweli nilibaki nikiwa nashangaa yale maneno ambayo yalikuwa yanatoka mdomoni kwangu na kusikika yalikuwa tofati kabsa kwani yale maneno ambayo niliyaongea yalisika hivi. "Ndio nipo Tayari kumuoa kwani mimi ni mwanafunzi. Hivyo wakati nikiwa naendelea na masomo naomba iwe kama siri watu wasigundue"Yalikuwa ndio maneno ambayo yalikuwa yanasikika kutoka mdomoni kwangu wakati naongea tofauti na niliyokuwa nafikilia kuyasema. Yale maneno yaliposikika nilishangaa watu wakipiga kelele za vigelegele kwa hali ya juu sana. "Nashukuru sana Mwanangu kapopo kwa majibu mazuri namna hiyo. Nashukuru sana kwa kukubali kumuoa mwanangu Maimuna binti hijirafu. kwa kweli kwa upande Wangu Mzee Hijirafu sina neno la kuongeza kabsa. Ila unajua Pindi unapoa lazima mtu unatakiwa utoe mahali. Ila mimi kapopo sihitaji mahali Kubwa sana Kwako. Yani mimi nahitaji mahali ndogo Sana kwako ili umuoe mwangu. Hivyo kapopo utamtoa Kafala mzazi wako mmoja. Wewe ndio utachagua atakuwa mama yako au baba yako"Aliongea Mzee Hijirafu na kukaa



    *****---*****--------**** Kwa kweli yale maneno ya Mzee Hijirafu yalinifanya nichanganyikiwe mbaya maana aliongea vitu ambavyo sikumuelewa kabsa. Kitendo cha Kuniambia Nimtoe baba yangu au Mama yangu Kafala ili niweze Kumuoa Maimuna ilikuwa ni kitu ambacho kilinichanganya sana. "Kwa hiyo Sasa hivi watu Mnatawanyika tulikuwa na kikao cha kumtambulisha tu. Siku ya harusi ikifika tutapeana taarifa" Alisimama mtu Mmoja na kuongea haya maneno na wale watu waliokuwepo pale walisimama na kuanza kutoka. Wakati wakiwa wanatoka watu wengine walikuja na kunipa mkono kama inshara ya kunipogeza au kusalimiana. Kwa kweli ingawa sikutaka kuwapa Mkono lakini nilishangaa kila ambaye alikuwa anakuja kunipa mkono nilijikuta mkono wangu wenyewe ukiongoza kufanya hilo zoezi. Baada ya karibia watu wote kutoka kwenye ule ukumbi na kubaki wachache tu. Maimuna alinisogelea hadi sehemu ambayo nilikuwepo huku akiwa anatabasamu na kunikumbatia Usoni. Aliponikumbatia Usoni kwa muda kama wa Sekunde kumi kisha alitoa mikono yake nilishangaa kuona nikiwa sehemu nyingine tofauti na ile ambayo nilikuwepo ya kwanza. "Kapopo naomba unisikilize kwa makini tena tega sikio kabsa usije kuharibu kila kitu. Unajua ninakupenda sana hadi nimembembeleza baba yangu kukupunguzia mahali ya ndoa hadi kuwa yale. Sasa ninachotaka mimi ukubali tu kwa moyo wako kutoa hiyo mahali unioe. Maana hata kama ukikataa lazima tu mzazi wako mmoja lazima umtoe kafala. Si unakumbuka wakati unaulizwa upo tayari kunioa mimi. Ulijibu maneno tofauti na yale ambayo ulikuwa na lengo ya kusema. Ulikuwa hutaki kuwapa watu mikono lakini uliwapa bila wewe kupenda. Pia kama ikitokea ukatae kumtoa mzazi wako kama Mahari ya kunioa mimi basi mimi kwa lazima nitawatoa wote wawili kama Adhabu"Aliongea Maimuna na kwenda kukaa kwenye kitanda. Kwa kweli yale maneno ya Maimuna yalinifanya CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/nichanganyikiwe sana. Sikuafiki kabisa kumtoa mzazi wangu yeyote kafala kumuoa mtu ambaye nilikuwa sijamchagua. Sawa maimuna alikuwa mzuri lakini sikutaka kumuoa kupitia damu moja ya mzazi wangu. "Maimuna naomba usinifanyie hivyo tafadhari, niambie mahali nyingine yeyote ila hata pesa kiasi gani nikatafute ili nisimue mzazi wangu. Maimuna wazee wangu nawapenda sana sasa kwa nini niwafanyie kitu cha kinyama kama hicho wewe unachoniambia"Nilimwambia maimuna. "Hahaha hahaha hahaha kapopo hebu acha utani wako bhana. Sisi ndio tunataka kukupa wewe pesa, mzee wangu anapesa hadi anajiogopa ndio maana hana haja ya kuwaambia mtoe mahali pesa. Yeye ndio anahaja ya kukupa wewe pesa. Nakuomba chagua mtu mmoja yupi utamtoa kama mahali unioe mimi na hilo nakupa Siku mbili tu uwe umenipa majibu. Ukijifanya Mjanja na siku hizo zipite basi wote nawatoa kafala"Aliongea tena Maimuna huku akiwa ananicheka. Kwa kweli sikuwa na jinsi niliamua kutulia tu huku nikiwa natafakari nimwambie nini Maimuna ili aweze kunielewa. Nilifikilia mambo mazuri ambayo amenifanyia baba yangu licha ya kuwa mchango mkubwa wa mimi kuiona Dunia yalikuwa ni mengi sana. Nilifikilia pia mambo ambayo alinifanyia mama yangu licha ya kunileta duniani kwa kweli yalikuwa mengi sana. Niliwaza hadi nilijikuta naanza kulia tu kwani hadi muda ule sikuona ni yupi kati ya mama yangu na baba yangu nimtoe kafala kama mahari ya kumuoa Maimuna. Wakati nikiwa kwenye ile nyumba kupitia madirisha ya chumba kile nilibaini kama ile nyumba ilikuwa imezungukwa na maji ya bahari. "Maimuna nataka nirudi nyumbabi kwanza, nahitaji kwenda kumuona baba yangu na mama yangu. Hili ombi ambalo umenipa kwa kweli naona kama halitawezekana. Hebu nipe kwanza muda alafu na wewe uwe unafikilia ni kitu gani kingine ambacho utaniambia nikupe ila siyo wazazi wangu"Nilimwambia maimuna. " Hahahah hahaha hahaha inamaana kama hilo ombi halitawezekana basi umekubali kuwatoa wazazi wako wawili kafala. Hiyo ni lazima kapopo yani siyo ombi kunioa utanioa na mahali itakuwa mzazi wako mmoja kama wewe utakubali kumtoa, au wazazi wako wote wawili kama wewe hutakubali kuwatoa. Mimi nakurudisha kwenu unafikili nakubana sana, najua kabsa kama maisha huku utayaweza ingawa huku ndio kuna raha kupita hata dunia. Hata pindi utakapo nioa ndio nafanya mambo ili tukaishi tu Duniani. Hivyo kama unataka Kurudi kwenu nenda tu pitia kwenye hicho kioo hapo kikubwa"Aliongea maimuna huku akiwa ananionyesha kile kioo. Niliangalia ile sehemu ambayo alikuwa ananionyesha nilikutana na kio ambacho kilikuwa kikubwa sana. Huku nikiwa natetemeka nilianza kutembea kukifuata kile kioo. Nilipo kikaribia nilishangaa kinanivuta kwa nguvu. Ile hali ilinifanya nipige kelele ya kuomba msaada cha ajabu nilishangaa nikiwa napiga kelele nipo kitandani kwangu huku nikiwa narusha rusha miguu. "Mwanangu nini mbona unapiga kelele kuna nini"Nilimsikia mama yangu akiongea. Nilipoangaza macho vizuri nilikuta ndani mle kuna baba yangu na ndugu zangu wengine wengi zaidi.



     "Mwanangu pole sana, unaweza kuniambia kitu gani kimekupata Mwangu. Yani tangia turudi kutoka Msibani tumekukuta umelala chumbani kwako wala hujitambui. Sasa hivi tulikuwa Tunajiandaa kukupeleka Hospitalini mwanangu"Aliongea mama yangu huku machozi yakiwa yanamtoka. "Mama mbona Sikuwepo hapa kitandani, mimi sikuwepo hapa kitandani mama"Nilimwambia mama yangu huku nikiwa nashangaa maana nilikuwa najua nilikuwa kwa Maimuna. Hivyo kitendo cha Mama yangu kuniambia Kuwa nilikuwa nimelala kitandani kwangu kilinishitua kidogo maana Sikuweza kuelewa niligawanika au vipi. "Mwanangu hebu acha utani wako bwana. Hukuwepo ulienda wapi sasa mbona sisi tumekukuta umelala hapa kitandani hujitambui. Haya nimekubali wewe hukuwepo ulikuwa wapi"Aliniuliza mama yangu huku na yeye akianza kunishangaa. Kwa kweli Swali ambalo aliniuliza mama yangu majibu yake yalikuwa magumu sana kumwambia nilikuwa sehemu gani. Nilipokumbuka moja ya maneno ya Maimuna na baba Yake Hijirafu hadi nilijikuta Machozi yanaanza kunitoka na kuanza kulia na kushindwa kujizuia. "Malaria yatakuwa yamempanda, unajua Mtoto malaria yakimpanda huwa hajielewi kabsa hata hapa huenda amechanganyikiwa ndio maana anasema hakuwepo. Hivyo mama Amina hebu jiandae Tumkimbize Hospitalini ngoja na mimi nitoe pikipiki "Aliongea Mzee wangu huku akiamka kuelekea nje. Kwa kweli nilibaki nikiwa nashangaa huku nikiwa najiuliza maswali mengi sana ambayo ilikuwa vigumu kupata majibu. Ninachojua nilikuwa kwa jini Maimuna leo na mama yangu anasema nilikuwa nimelala kitandani kwangu. Sasa bora hata mama angenikuta kwa kina Mdete nimelala hapo ningeamini nilikuwa naota kwani usiku ule nilikuwa nimelala kwa mdete. Nilijaribu kuvuta taswira kwa kina ili kupata jibu sahihi haya mambo ya kuhisi nilikuwa kwa Maimuna ilikuwa ni kweli au nilikuwa naota. Nilivuta taswira kwa umakini wa juu kumbukumbu zangu ziliendelea kubaki pale pale kuwa nilikuwa nimelala kwa Kina Mdete baadae maimuna alikuja kunichukua na kunipeleka sehemu ambayo nilikuwa sipajui. "Hicho ambacho unakiwaza kichwani mwako kipo sahihi kabsa. Hukuwa unaota kapopo wala hiyo haikuwa ndoto. Ukweli ulikuwa kwangu na unatakiwa uje unipe jibu langu ni nani kati ya baba yako na mama yako umeamua kumtoa kafala"Nilisikia sauti kama ya maimuna ikisika pale kwenye chumba ambacho nilikuwepo huku ikifuatiwa na harufu nzuri ya perfume yake. Niligeuka kuangalia sehemu ambayo ilikuwa inatokea ile Sauti lakini cha Ajabu sikumuona mtu. Baada ya baba yangu kutoa pikipiki alikuja kunichukua na kunipeleka Hospitali na mama yangu alibaki tu nyumbani baada ya kuniona nikiwa na nguvu tu kabsa. Tulipofika hospitalini nilipimwa lakini hakuna ugonjwa wowote ulijitokeza. Baba yangu hakuelewa kabsa yale majibu. Ilibidi akafanya mapango wa kupiwa magonjwa yote kupitia mkoja hadi kinyesi changu. Hata walipo nipima walinikuta nipo safi kabsa. Kwa kweli yale majibu ya dactari yalionyesha Kumchanganya sana mzee wangu. "Dactari ni kweli unauhakika kijana wangu ni mzima kabsa. Yani huwezi amini dactari huyu kijana tumemkuta nyumbani amelala huku akikoroma tu. Ukimwamsha haamki na mwili wote ulikuwa umelegea sasa kuniambia kuwa mzima wa afya hana tatizo lolote nahisi maajabu kidogo"Aliongea mzee wangu kisha akanishika mkono tukaanza kuondoka. Tulipotoka Hospitalini tulipanda kwenye pikipiki na kuanza kurudi nyumbani. "Hivi baba kwa mfano wewe umetokea kupendwa na mwanamke flani. Bahati mbaya huyo mwanamke ambaye anakupenda akawa jini. Baadae akasema kuwa anataka umuoe na mahali iwe kumtoa kafala mzazi wako mmoja wewe utamtoa nani. Ukikataa kumtoa yeye anakwambia atawatoa wote wewe ungefanyaje baba yangu, ungemchagua nani kumtoa kafala"Nilimuuliza swali baba yangu kimtego ili nijue atanijibuje. Lile swali kwa kweli lilimfanya mzee wangu hadi alisimamisha pikipiki na kuanza kuniuliza nasemaje.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********************************** Kitendo cha baba yangu kusimamisha pikipiki na kuanza kuniuliza nasemaje. Nilibaini kama lile Swali ambalo nimemuuliza halijamuingia akilini. "Mwanangu inamaana kuna jini umempata unataka umuoe alafu umeambiwa mahali utoe mzazi mmoja. Maana kwa hali ya kawaida mtu hawezi kumuuliza mzazi wake swali zito kama hili lazima kutakuwa na kitu. Nakuomba kama ulikuwa na mpango huo basi nitoe mimi. Tafadhari mke wangu Mwache ili anilelee Mwanangu Amina bado mdogo sana. Hiki kizazi ambacho tunakizaa cha hatari sana mtoto anakuwa bado mdogo anamawazo mabaya zidi ya wazazi wake. Mbona sisi hatujakutoa kafala ili tuwe matajiri"Aliongea Mzee wangu kwa jaziba kidogo kisha aliwasha pikipiki tukaendelea na safari ya kurudi nyumbani. "Baba siyo kwamba nimesema kuwa nahitaji kumtoa mzazi wangu mmoja kafala ili nioe jini. Yani hii ilikuwa ni ndoto ambayo nilikuwa naota. Sasa hii ndoto mimi nimehisi kama bangua bongo flani hivi ndio maana nimejaribu kukupa swali na wewe ili nijue kama Ungelikuwa wewe ungefanyaje"Nilimwambia Mzee wangu ili kuweza kumshushia hasira kidogo. "Basi mwanangu kama ni ndoto au hata kama ingekuwa kweli mtu wa kumtoa ni baba. Ingawa baba naye anamajukumu mengi ya kuitunza familia lakini unatakiwa kumtoa baba yako ili mama aendelee kuilea familia"Alinijibu tena mzee wangu. Sikutaka tena Kumuuliza tena swali Baba yangu hadi tulifika nyumbani. Kwa kweli ndugu zangu walipoambiwa kama nimeenda kupimwa alafu nimekutwa sina Homa walibaki wakiwa wanashangaa huku wakiwa wanajiuliza nimekumbwa na nini. Kuna tatizo gani ambalo lilinipelekea mimi kuwa vile. "Tusiwe na wasiwasi sana haya ni mabadiliko tu ya mwili ambayo muda mwingine yanaweza kumpata mtu. Unajua hii inatokana na nini huenda kijana alikuwa amefanya kazi nyingi bila kupumzika. Hivyo pindi anapolala anaweza kulala kama style hii tuliyomkuta nayo. Ingawa huwa nadra sana jambo kama hili kumpata mtu"Aliongea mjomba wangu ambaye alikuwa ni mwalimu wa sekondari. Kupitia yale maelezo kidogo ya mjomba wangu ambayo mimi nilihisi ya uongo ili kuwashushia mawazo ndugu na wazazi wangu waliokuwepo kweli walielewa na kutawanyika kwenda kuendelea na majukumu yao ya kazi. Baba mwenyewe alichukua pikipiki yake na kuondoka kuelekea Msufini kwenye kibanda chake cha ndizi. Nyumbani alikuwa amebaki mama tu kwani hata mdogo wangu Amina bado alikuwa yupo mwanza kwani shule walikuwa wamefunga. "Mama kuna swali flani mwalimu alitupa kama chemsha bongo yani swali hili halina jibu kamili. Ila idadi kubwa ya watu watakavyo egemea na point zilizoshiba hilo ndio litakuwa jibu. Swali lenyewe ni kama La debate. Mfano tuchukulie mama wewe ungekuwa mwanaume. Akatokea jini Mwanamke akakupenda na akataka umuoe. Mahali akakwambia umtoe kafala mzazi wako mmoja yani baba yako au mama yako. Pia akakwambia kama utakataa kumtoa basi yeye atawachukua wote wawili. Je ingekuwa wewe ungefanyaje? Ungemtoa mmoja wapo ambaye atakuwa ni nani au ungeeacha jini awachukue wote"Nilimuuliza tena mama swali kama lile ili niweze kupata jibu la kufanyia maamuzi yangu kama jini maimuna atakuja kunichukua tena. Maana nilishindwa kufanya maamuzi kwani wazazi wangu wote nilikuwa nawapenda sana. "Mwanangu kwanza unatakiwa kuelewa ni heri nusu shali kuliko shali kamili. Unajua unapokosa mzazi mmoja sizani kama mtu atakuita yatima. Sasa nataka unisikilize kwa makini majibu yangu ambayo nitayatoa. Hapo mtu wa kumtoa ni mama. Unajua kwa sababu gani nimesema hivyo. Mama huwa na Jukumu la kubeba mimba ya mtoto wake hadi anamzaa. Akisha mzaa anamlea hadi anafikisha miaka mitano hilo sasa litabaki jukumu la mzazi wa kiume kama kusomesha watoto na kuilisha familia. Hivyo tuchukulie familia yetu hakuna mtoto mwenye miaka chini ya saba hapa. Hivyo mwenye majukumu ya kutunza familia hapa ni baba yako. Baba yako ndio anatakiwa kuwaza familia yangu leo ile nini, watoto wangu watapataje elimu. Hivyo kama itakuja kutokea kitu kama hicho wewe mtoe mama kafala"Aliongea mama yangu. Kwa kweli yale maneno ya mama yangu yaliniumiza zaidi hadi machozi yalianza kunitoka. Kwa jinsi ambavyo nilikuwa nampenda mama yangu jibu lile alilonipa liliniumiza zaidi. Sikutaka kuendelea kukaa pale kwa mama maana angegundua kama nalia kuna kitu angelikishitukia. Kwa kweli majibu ambayo niliyapata Pande zote mbili yalikuwa ya utata sana. Usiku baada ya chakula nilienda hadi chumbani kwangu kwenda kulala. Nilipoingia tu chumbani kwangu nilishangaa kumkuta Maimuna akiwa kwenye kitanda changu. Ile hali kwa kweli ilinishitua Sana kwani nilijua mambo ndio yanataka kuanza. "Kapopo mimi nimekuja kwa kitu kimoja tu hapa,nimefuata mahali yangu baba kanituma. Hivyo niambie yupi awe mahali kati ya baba yako au mama yako au wote wawili. Maana unaweza ukawa unanipenda zaidi ukaona mahali ya mzazi mmoja utakuwa unanionea ukaamua kutoa wote wawili. Niambie yupi unamtoa ili nimchukue"Aliniuliza Maimuna huku akiwa anatabasamu.

    Kwa kweli yale maneno ya maimuna yalizidi kunichanganya mbaya. Nilishindwa nimwambie nini kwani sikuwa tayari hata kidogo kuweza kumtoa hata mzazi wangu mmoja kafala. "Maimuna mimi sipo tayari kumtoa hata mzazi wangu mmoja kafala. Tafadhali nakuomba nitoe mimi mwenyewe na siyo wazazi wangu"Nilimwambia Maimuna huku nikiwa nimepiga magoti ili aweze kunielewa kile kitu ambacho nilikuwa namwambia. Muda ule mimi Maimuna wala sikuwa namuogopa kama Mwanzo muda ule Maimuna kwangu nilikuwa namuona kama wa kawaida tu.



    "KAPOPO HEBU ACHA KUJIDANGANYA UJINGA, UNATAKIWA KUJUA KILA KITU AMBACHO JINI HUITAJI BINADAMU AFANYE JIBU HUWA NDIO. MIMI NAZANI KUKATAA KWAKO KUMTOA MZAZI WAKO UNAMAANA KUWA UMEKUBALI NIWATOE WOTE WAWILI. UNATAKIWA UJUE KUWA HATA UONGEE UKARIBIE KUFA SWALA LITABAKI PALE PALE MIMI KUMTOA MZAZI WAKO MMOJA AU WOTE ILI IWE KAMA MAHALI YA KUNIOA MIMI"Aliongea Maimuna huku akiwa ananisogelea kabsa hadi alinifikia sehemu ambayo nilikuwa nimesimama. Aliponifikia alinipulizia kama upepo flani hivi kwenye uso wangu. Kitendo cha Kunipulizia ule upepo Nilianza kuona kama naishiwa nguvu hivi huku macho yangu nayo yalikuwa yanapoteza kwa kasi ya ajabu nguvu za kuendelea kuona. Sikumaliza hata muda wa dakika moja tangu Maimuna anipulizie ule upepo tayari usingizi ulikuwa umenipitia na nilikuwa nimelala sikujua kile ambacho kilikuwa kimeendelea.



    Nilipokuja kushituka nilijikuta nimelala kwenye chumba flani hivi ambacho kilikuwa kigeni kwenye macho yangu. Kile chumba kwa kweli kilikuwa kizuri sana tangia nizaliwe sikuwahi kuona chumba kizuri kama kile. Nimeshawi kuangalia picha mbali za waigizaji hapa tanzania na nje ya nchi lakini sikuwahi kuona chumba ambacho kilikuwa kizuri kama kile. Kitanda ambacho nilikuwa nimekilalia nilipokitazama hadi Nilianza kuogopa. Kwenye ukuta wa kile chumba kuliku kumetanda picha mbali mbali za Maimuna akiwa amepiga na mimi. Nilijiuliza hizi picha nilipiga wapi na Maimuna lakini sikupata jibu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wakati Nikiwa naendelea kushangaa kile chumba huku Nikiwa najiuliza nipo wapi, Mlango ulifunguliwa kisha nilimuona Maimuna akiingia kwenye kile chumba. Nilipomwangalia Maimuna mkononi alikuwa na kisu ambayo sikujua alikuwa anakuja nayo kwa kazi gani.



    "Hiki ndicho chumba chako ambacho utakuwa unafikia pindi utakapokuwa unatoka duniani na kuja huku. Ila nimekuleta huku kwa jambo moja tu nataka umtoe mzazi wako mmoja ili iwe kama mahali ya kunioa mimi. Najua utakuwa mgumu sana na utajifanya unajua ila ukinibabaisha mimi nawauwa wote"Aliongea Maimuna kisha alienda sehemu moja hivi ukutani ambako kulikuwa na kitu kama kioo hivi na kuanza kukipapasa. Alikipapasa kama muda wa dakika mbili cha ajabu nilishangaa kile kioo kikianza kutoa miale mikali sana na Ngurumo zilizokuwa zinatisha sana. Baadae miale ilipokata nilishangaa kuwaona wazazi wangu wakiwa wanaonekana kwenye kile kioo.



    ******************************************** Kwa kweli kile kitend cha kuwaona Mama yangu na baba yangu wakiwa kwenye kioo ukutani kwa Maimuna kiliniumiza sana. Maimuna alipoona Wazazi wangu walionekana alianza kutembea kuja kwenye kitanda ambacho nilikuwa nimelalia. Aliponifikia aliniangalia kwa macho makali kisha alinikabidhi ile kisu. "Haya nimekupa hiyo kisu ili ukafanye kitu kimoja tu kwenye zile picha. Kachole alama ya X kwa mzazi wako ambae unataka afe. Kama hautafanya hivyo nitakuonyesha mwenyewe wote nawaua"Aliongea Maimuna pindi tu aliponikabidhi ile kisu. Kwa kweli yale maneno ya Maimuna yalizidi kunichanganya ile mbaya. Nilishindwa yupi kati ya baba yangu na mama yangu nikamuwekee alama ya x. Kila mzazi kwangu alikuwa muhimu sana na nilikuwa nampenda kupita maelezo. nilikumbuka Maneno ya baba na mama kila mmoja alivyokuwa amenijibu nimtoe yeye hadi nilikuta machozi yanaanza kunitoka. "Maimuna tafadhari kwa nini usinitoe tu mimi Kafala badala ya wazazi wangu. Niue tu mimi Maimuna ili hata huo mpango wa ndoa ufe kuliko kuwauwa wazazi wangu. Maimuna mzee wangu kanilea tangia nikiwa mtoto hadi nimefika hapa. Mama yangu kahangaika na mimi miezi tisa tumboni na kunizaa. Aliponizaa alihangaika kunilea huku akishika mikojo na mavi yangu leo nije kumlipa kafala kwa kweli haiwezekani. Tafadhari naomba uniue mimi waacha wazazi wangu Maimuna"Nilimwambia maimuna. "Naona kile ambacho nimekwambia hutaki kunielewa. Sasa utaenda kuwazika wazazi wako wote wawili. Maana mimi nakupenda sana hadi mimekupa uchague mzazi wa kumtoa kafala wewe unajifanya unawapenda zaidi. Sasa ngoja nikuonyeshe kama thamani yangu ni kubwa sana unatakiwa unitolee mahari wazazi wako wawili"Aliongea Maimuna na kuniondolea ile kisu ambayo alinipa. Aliponiondolea ile kisu alianza kutembea kuelekea kwenye kile kioo ambacho walikuwa wanaonekana wazazi wangu. Kwa kweli muda ule mwili wote nilikuwa natetemeka baridi. Cha ajabu wakati nikiwa naona baridi kali huku nikiwa natetemeka kwa woga. Mwili wangu wote ulikuwa umeloa jasho. "Kama ikija kutokea kitu kama hicho naomba uje unitoe mimi. Tafadhari umwache mke wangu alee familia"Nilikumbuka maneno machache ya baba yangu aliyeniambia huku nikiwa nimechanganyikiwa mbaya. "Mwanangu mwenye majukumu ya kulea familia huwa ni baba. Kazi ya mama huwa kumlea mtoto hadi anapofikisha miaka mitano. Kwenye familia yetu hakuna hata mtu mmoja ambaye yupo chini ya miaka mitano. Hivyo kitu kama hicho kikitokea naomba unitoe mimi mama yako. Kwani baba yako atakuwa na Majukumu ya kuwasomesha na kuilisha familia kwa Ujumla"Nilikumbuka pia maneno ambayo alishawahi kuniambia mama yangu ndio nilizidi kuchanganyikiwa Maimuna tayari alikuwa ameshafika kwenye kile kioo ambacho walikuwa wanaonekana wazazi wangu. Aliniambia anahesabu mara tatu kama sitakuwa nimebadilisha uamuzi wa kukubali mzazi wangu mmjoa amtoe kafala basi anawatoa wote. "Naomba nipe hicho kisu usiwauwe wote wazazi wangu lete nitamua mmoja wao. Ila hata kama nikimtoa mzazi wangu kafala Sipo tayari kukuoa wewe. Naomba nikimaliza kazi yangu nitarudi duniani nikaendelee na Shule pia sitaki uhusiano wa aina yeyote na wewe"Nilimwambia Maimuna huku nikiwa naamka kitandani kwenda kuchukua kisu kumtoa mmoja kafala kati ya baba yangu au mama yangu. Hadi muda naamka kitandani na kwenda kuchukua kisu kwa Maimuna Bado nilikuwa sijajua ni nani natakiwa kumtoa kafala. "Yani wewe kijana unanichekesha sana. Hata hivyo ulivyoongea kama hutaki tena kunioa mimi nitakupa Conditional mbili. Unieo hivyo hivyo huku ukiwa na uhuru wa kuishi duniani na huku. Au nikuue na kukutoa kule Duniani alafu uje unieo kwa nguvu na kuwa mtu wa huku tu kutokuiona dunia tena"Aliongea Maimuna na kunifanya hadi nishituke. Maana yale maneno mengine ambayo aliyaongea ndio yaliniogopesha zaidi. Nilisogea hadi kwenye kioo ambacho zilionekana sura za wazazi wangu na kuanza kuhesabu huku machozi yakiwa yananitoka. Nilishashindwa yupi nimtoe kafala hivyo nilianza kuhesabu sehemu ambayo itaishia kumi ndio ambayo nitamtoa kafala. Nilihesabu hadi nilifikisha kumi na sehemu ambayo ilifika kumi ilikuwa kwa baba yangu. "Baba naomba unisamehe sana mwanao, siyo makusudio yangu nimelazimishwa tu.kwa kweli nilikuwa nakupenda kuliko maelezo ila Sina jinsi. Naomba huko uendako usije ukanichukie mimi mwanao"Niliongea yale maneno huku machozi yakiwa yananitoka. Nilipomaliza yale maneno nilifumba macho yangu kisha niliweka x kwenye picha ambayo alikuwepo baba yangu. Nilipofumbua macho nilikuta Damu zikiwa zimetapakaa kwenye mikono yangu na kioo kizima kimeenea damu. Muda kama wa Sekunde tatu hivi nilishangaa kioo kinakuwa kisafi kisha nilimuona baba yangu akiwa anamtingisha mama yangu huku akiwa anamwita. Ile hali mimi ndio iliyozidi kunichanganya sana. "Kapopo mimi ni mzuri ati na unatakiwa ukitoe kitu ambacho unakipenda sana ati. Hivyo kati ya baba yako na mama yako umeonekana unampenda sana mama yako. Hivyo ulipokuwa unachoma zile picha niliweka kinyume chake. Yani picha ambayo alikuwa anaonekana baba yako alikuwa mama yako. Na picha ambayo alionekana mama yako alikuwa baba yako. Nenda ukamzike mama yako huku ukiwa unajiandaa na harusi yangu na wewe nakupenda sana"Aliongea Maimuna huku akiwa anatabasamu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kweli yale Maneno ya Maimuna yaliniuma sana hasa aliponiambia kuwa ambaye amekufa hakuwa baba yangu bali ni mama yangu. Nilishindwa hata Nifanyaje nilibaki nikiwa nalia huku nikiwa nakumbuka mambo mengi ambaye amewahi kunifanyia mama yangu. "Nenda kwenye Msiba hutakiwi kunililia hapa. Hivi faida ambayo utaipata baada ya mama yako kufa unaifahamu. Ipo siku utakuja kuniomba msamaha wewe taila. Unalia kwa kitu ambacho hakipo kabsa. Hivi uliambiwa kama mama yako atakuja kuishi uzima wa milele hapa Duniani. Mama yako angelikufa tu muda wowote si bora hivi anakufa na wewe unapata faida"Aliongea Maimuna kiukali kidogo kisha alianza kusogelea Mlango ili atoke. "Faida gani ambayo nitapata wewe Maimuna. Hata kama kifo cha mama yangu kitasababisha nipate ndege lakini sitaona faida kutokuwa na mama yangu hata siku moja. Sawa kufa kwabinadamu ni kawaida kwani kila binadamu aliumbwa kwa Udongo na atarudi kwa Udongo ila siyo mimi ndio kisababishi cha kutoa Roho ya mtu. Mwenye mamlaka ya kutoa Roho ya mtu ni Israel tu na wala siyo mwingine"Nilimwambia maimuna huku nikiwa nalia maana huzuni ambayo nilikuwa nao ulikuwa hauzungumziwi. "Kwani wewe hapo ndio umechukua roho ya mama yako Si kachukua israel. Wewe hapo ni kisababishi tu ili mama yako afe kama vile visababishi vingine kama mtu kuugua Malaria, mtu kugongwa na gari, kuumwa na tumbo"Aliongea Maimuna na kupotea kwa Kasi ya ajabu. Alipopotea Maimuna sikuwa hata na haja ya kuendelea kuwepo kwenye kile chumba. Maana nilihisi chumba kile ni kidogo sana kwa pressure ambayo nilikuwa nayo kuhusu kifo cha mama yangu. Sasa nilianza kupiga akili nitawezaje kutoka hapa ili nirudi Duniani ingawa Maimuna ameshaondoka yeye ndio alitakiwa kunisaidia. Nikiwa nipo pale natafakari nilikumbuka kuwa kwa mara ya kwanza nilipoletwa huku nilirudi kupitia kwenye kioo kikubwa ambacho kilikuwa kwenye ukuta. Nilichofanya niliamka na kuanza kuangalia kwenye ukuta wa nyumba ambae ulizungushiwa mapazia kuangalia kama nitaona kioo ili niondoke pale. Wakati nikiwa nazunguka kile chumba kutazama sehemu ambayo nitakiona kile kioo nilishangaa nilipofika sehemu flani nilikuwa kama navutwa hivi kuelekea kwenye ule ukuta. Nilibaini pale huenda ndio kutakuwa na kioo. Hivyo mdogo mdogo nilianza kusogea ile sehemu ili kwenda kuangalia kuna kioo. Kabla hata sijafikia ule ukuta nilishangaa navutwa kwa kasi ya ajabu kuelekea kwenye ule ukata. Nilipotaka kujikaza ili nisiende niliashangaa nikiwa nipo kwenye kitanda changu huku nikiwa narusha rusha miguu yangu. Kwa kweli kile kitendo kiliniacha nikiwa nashangaa ile style ambayo nilikuwa narudi kutoka ulimwengu wa majini na kuja Duniani kwa kweli ilikuwa ya aina yake. Niliamka pale kitandani na kuanza kuelekea sebureni. Nilipofungua tu mlango wa chumba nilishangaa kelele za watu wakiwa wanalia huku wakitaja jina la mama yangu. Vile vilio vya watu wale vilinifanya na mimi machozi yaanze kunitoka taratibu. Nilijikaza nikajongea na kwenda hadi chumbani ambako alikuwa amelazwa mama yangu. Nilienda kumfunukua na Kumwangalia kwa mara ya Mwisho kabla ya kutokuonana milele. Mama yangu nilimkuta akiwa amefumba macho huku akiwa kama amelala hivi. Wakati nikiwa naendelea kumwangalia mama yangu nilibaki nikiwa nashangaa nilipomuona akifumbua macho yake na kuniangalia. "Nashukuru kwa kufanya vile kama nilivyokuambia. Hii itafanya muishi maisha yenu bila mateso kwa sababu baba yenu yupo atawasomesha na kuwalisha. Kama ungelimtoa baba yako kafala unafikili ingekuwaje kama siyo mali zote zingegombewa na Ndugu. Mwanangu huna haja ya kujilaumu wakati hicho kitu kilikuwa nje ya uwezo wako. Ninachokuomba Mdogo wako amina naomba Umpende sana na uwe naye bega kwa bega"Aliongea mama yangu kisha alifumba macho na kutulia kimya. Kwa kweli kile kitendo kiliniogopesha sana na kubaki nikiwa natetemeka tu. Mama yangu alikuwa tayari ameshakufa leo nilipoenda mimi afumbue macho na kuanza kuongea ilikuwa ni kitu ambacho hakipo kabsa kwenye fikra zangu za akili. "Jamani mfunukueni mama yangu shuka, mama yangu hajafa sasa hivi alikuwa anaongea na mimi. Tafadhari mama si amka sasa amka mama yangu"Niliongea kwa Sauti ya juu huku nikiwa namtingisha mama yangu. Ile hali kwa kweli iliwashangaza Watu na kuja kunishika. "Jamani mtoeni Nje huyo unajua anaisumbua maiti bure. Mtu anapokufa haitaji buguza ya aina yeyote bali ni kumwimbia na kumsomea uradi na dua mbalimbali ili kule aendako adhabu za kaburini zipungue. Huyo kachanganyikiwa kwa kifo cha mama yake hivyo mtoeni nje"Aliongea Mzee yusuph Imamu wa msikiti. "Lazima Mjomba wangu achanganyikiwe, Dada yangu hata saa moja haijapita nilikuwa naongea na kucheka naye leo hii niambiwe amekufa. Nasema tutachinjana humu nitamchinja mtu. Huu uchawi mimi nimeuchoka kama nitakubaini umemua dada yangu lazima na wewe uzikwe leo leo"Aliongea mjomba wangu na yeye huku akiwa analia. Nilishikwa pale na watu huku nikiwa natolewa nje. Nilipofikishwa Sebureni nilimuona Mzee wangu na yeye macho yake yakiwa mekundu. "Kapopo ile ndoto yako ambaye ulikuwa unaiota mbona umeenda kinyume mwanangu. Mimi nitabaki na nani sasa mwangu, nilikuambia wewe nitoe mimi mwanangu lakini hukutaka kufanya hivyo sasa umefanya nini"Aliongea mzee wangu kwa shida kisha alianguka chini kama Mzigo na fahamu zilikatika.



    Kwa kweli kitendo cha baba yangu kuanguka kisha kukata moto kilinichanganya sana. Haraka haraka Tulimbeba mzee na kumkimbiza Hospitali ili kuweza kwenda kufanyiwa hudumu kuokoa Maisha yake. Kila nilipokuwa nakumbuka jinsi mama yangu alipofumbua macho na kuongea na mimi ndio nilizidi kuchanganyikiwa zaidi. Kwa kweli nilijiona Mkosaji mkubwa mbele za Mungu lakini sikuwa na jinsi tayari kile kitu kilishafanyika. Upande mwingine nilitokea kujipa matumaini kwani hata kama nisingefanya hivyo wazazi wangu wote wangekufa nisingebakiza hata mmoja. Muda ule tayari ilikuwa Saa tisa usiku tulifanikiwa kuwakuta Madactari ingawa ilikuwa usiku kwani Kwenye Hosptali ya Mkoa madactari huwa wanaenda kwa Shift. Tulipomfikisha moja kwa moja Mzee wangu aliingizwa kwenye chumba cha Wagonjwa maututi na kuanza kufanyiwa Huduma. Mimi na mjomba wangu na watu wengine tuliokuwa nao ilibidi kukaa nje ya chumba kwenye viti ili kuweza kusubilia. Tulikaa kwa Muda kama Wa saa moja ndio Dactari kutoka kwenye chumba ambacho aliingizwa mzee wangu alitoka. "Plesha tu ilipanda kidogo, hii inatokana na mtu kuona kitu cha kutisha au kuambiwa kitu ambacho hakutarajia kama kweli kingetokea sasa hivi hali yake siyo mbaya Sana hivyo Subilieni muda Wa Saa moja mnaweza kwenda kumuona na Kesho Asubuhi nazani mnaweza mkaruhusiwa ili msiendelee kuongeza Gharama"Aliongea Yule dactari. Kwa kweli niliposikia Kama mzee wangu alikuwa CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/amesharudiwa na fahamu nilimshukuru sana Mungu kwani yeye ndio ambaye nilikuwa nimebaki naye. **** **** **** Kesho yake mida ya saa mbili mzee wangu tayari alikuwa amesharuhusiwa hospitalini. Wote tuliongozana na kwenda hadi nyumbani. Ilibidi watu walizuiwa kulia maana kama wangeendelea kulia nazani Wangesababisha mzee wangu kuweza kupoteza fahamu tena. Pia idadi kubwa ya watu kama mama yangu mdogo mama mjomba walikuwa wanapoteza sana fahamu. Hivyo waliamua kuimba nyimbo tu za kuweza kumuombea marehemu na siyo kulia. Kwa kweli sikuwahi kupatwa na huzuni na sizani kama nitakuja kupatwa na Huzuni kama kifo Cha mama yangu. Muda wa saa tano Asubuhi tayari Maiti ilikuwa imeshaoshwa na kusaliwa hivyo tulibeba na kuelekea Makaburini. Tulipofika Makaburini mama yangu alizikwa. "Pumzika salama mke wangu na mimi ipo siku nitakuja kukufuata tu. Nazani hakuna ambaye ataishi maisha ya milele hapa dunia. Wote hapa ni wapitaji tu"Aliongea mzee wangu kwa huzuni huku akiwa anashika shika kaburi la mama. Kwa kweli muda ule nilikuwa nimelia hadi nilikuwa nimechoka nilishamlaumu maimuna hadi nilishachoka. Baada ya mazishi watu wote tulianza kurudi nyumbani. Tulipofika nyumbani Nilikuta kuna Gari moja nzuri sana ilikuwepo nyumbani. Nilianza kujiuliza ile gari ni nani ambaye alikuwa amekuja nayo lakini bado sikupata majibu. Nilipokaribia hadi nyumbani nilishangaa Kumuona maimuna na yeye akiwa kwenye mchanganyiko wa watu huku akiwa analia na watu wakiwa wanambembeleza. Kwenye ile Gari watu walikuwa wanashusha mchele na mafuta nilipowaulizia nani kaja cha ajabu walinionyesha Maimuna. Kwa kweli nilitamani kuwazuia kushusha ile mizigo lakini kila ambacho nilikuwa napanga kukisema Mdomo wangu nilikuwa nauona mzito na kushindwa hata kuongea neno lolote. "Kwa kweli huyu mama anaonekana alikuwa kipenzi cha watu. Umemuona yule Dada mwarabu, yule dada ndio kaleta hivi vitu vyote pia katoa milioni moja kuendeshea huu Msiba. Pia tayari kuna watu wametumwa wakachukue Ng'ombe sabasaba kanunua ili waje wachinje kwa ajili ya Msiba. Kweli mtu ukishakufa unasaminiwa mbaya"Aliongea kijana Mmoja akimwambia mwenzake. Kwa kweli nilibaki nikiwa nashangaa tu maana ile pesa ambayo alitoa Maimuna ilikuwa kubwa sana na ukifikilia yeye ndio ambaye alimuua Mama yangu. Niliamua kumfuata Maimuna kulekule ambako alikuwepo ili kwenda kumuuliza kwa nini anajifanya kujitolea huku yeye ndio ambaye amemua mama yangu. Cha ajabu wakati nikiwa nawaza kwenda kufanya hivyo nilishangaa maimuna Anatokezea karibu kabsa na sehemu ambayo nilikuwepo. "Huna haja ya kulia kwa mtu ambaye bado mzima. Furaha ambaye utakuja kuipata kwenye maisha yako hutakuja kunisahau kamwe. Ipo siku utakuja kuniomba Msamaha kwa haya ambayo unanifanyia. Nafanya hivi vyote kwa Sababu nakupenda kapopo. Mama yako tayari ameshakufa hivyo haina budi kuendelea kunichukia mimi"aliongea Maimuna na Kuja kunishika kichwani. Kwa kweli yale maneno ya maimuna kwangu yalikuwa kama mafumbo flani hivi ambayo bado sikuyaelewa maana yake. Kwanza mwanzo ameniambia haina haja ya kulia kwa mtu ambaye bado mzima pia mwishoni akaniambia kuwa mama yako tayari amekufa hivyo haina haja ya kumlaumu yeye. Hayo maneno kwangu kwa kweli nilishindwa kuyaelewa yalikuwa na maana gani. Kitu kingine ambacho kilianza kunishangaza baada tu ya maimuna kunishika kichwani kwa kweli mawazo yote juu ya kifo cha mama yangu yaliyeyuka mbaya. Sikuwa nawaza tena kuhusu kifo cha mama yangu nilianza kuona hali ya kawaida tu. Niliondoka pale na kwenda kumuangalia Maimuna kwenda kumuomba msamaha kwa maneno mabaya ambayo nilikuwa namwambia. Muda ule nilishangaa naanza kumpenda Maimuna kwa kasi ya ajabu. Wakati nikiwa naingia ndani hivi cha ajabu nilimuona Rafiki yangu Mdete yule ambaye alianguka kwenye chumba chake na damu zilitapakaa alipotaka kumkimbia Maimuna. Kwa kweli nilibaki nikiwa nashangaa kumbe mdete alikuwa bado mzima. Niliamua kumuita ili tutete pembeni kidogo nijue aliwezaje kupona maana mimi nilimwacha kwenye hali mbaya na nilijua tayari alikuwa ameshakufa. Nilipomwita mdete alipogeuka na kuona mimi ndio namwita nilishangaa kumuona anatoka nduki na kuanza kukimbia.





     Kwa kweli kitendo Cha Mdete kuniona na kuanza kunikimbilia kilinishangaza sana. Bado sikuelewa ni kitu gani ambacho kilimfanya Mdete alipoona anikimbie. Nilichoamua na mimi ni kumfatilia Mdete hadi nimkamate ili niweze kumuhoji kitu gani kinamfanya anikimbie. Nilitoka pale kwenye zizi bila kukimbia. Nilipohakikisha nimetoka kwenye uzio wa nyumba na mimi ilibidi nianzishe mbio ili niweze kumkata Mdete. Uzuri mdete alipokuwa anakimbia bahati mbaya alijikwaa na kuanguka. Hivyo ilinisaidia mimi nimfikie ile sehemu ambayo alikuwepo. "Kapopo usiniguse nakuomba uniache hivi hivi nilivyo"Aliongea Mdete huku akionekana kutetemeka kabsa. Kwa kweli yale maneno ya Mdete yalizidi kunishangaza kwa nini alikuwa ananiogopa hivi. Wakati mimi nilikuwa rafiki yake na tulikuwa tunashinda wote. Siku moja ilikuwa ngumu sana sisi kuweza kupitisha bila kuonana. "Mdete kuna tatizo gani ndugu yangu mbona unanikimbia. Tafadhari hebu jaribu kunieleza vizuri ndugu yangu kuna tatizo gani linakufanya unanikimbia"Nilimwambia Mdete huku nikijaribu kuongea maneno ya upole ambayo yangemshawishi aweze kuniambia kile ambacho kilimfanya akimbie. "Ndugu yangu wewe ondoka tu wewe kuwa rafiki yangu nazani nitakuwa naweka undugu na kifo. Kwa kweli sasa hivi itabidi uishi kipeke yako zaidi. Ile siku ndugu yangu mimi nilichezea kichapo sana mle ndani. Sawa sikuweza kuumia lakini kipigo ambacho nilikipata ilikuwa siyo cha kawaida. Sasa mbaya zaidi mtu ambaye alikuwa ananitandika nilikuwa simwoni. Wewe naye nilipotaka kukuamsha nilishangaa sikuoni. Mimi nahisi kama siyo wewe mchawi ulikuwa unanitandika basi ni yale majini yako. Maana mwanzoni nilikuwa naota unaniamsha nilipoamka ndio nilianza kuchezea kichapo"Aliongea Mdete. Kwa kweli yale maneno ya Mdete yalizidi kunishangaza zaidi. Kwanza kitendo cha kuniambia yeye hakuumia ila alichezea kichapo cha kutosha mimi bado sikuelewa vizuri. Ambacho nilikuwa naamini mimi nilikuwa najua lazima Mdete alikuwa ameshakufa. Maana wakati Maimuna alipokuwa anakuja kwenye chumba ambacho tulikuwa tumelala. Mdete aliamka na kuufuata mlango ili afungue akimbie lakini nilishangaa anaanguka chini na damu kwenye sakafu zilisambaa. Ndio maana mdete aliponiambia yeye wala hakuumia nilibaki nikiwa namshangaa tu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Niliongea mambo mengi sana na mdete hali mdete alifikia kunielewa. "Sasa wewe mdete si ulikuwa unayapenda majini sasa inakuaje. Binadamu mwenzako tu ambaye nilikuwa nashida na wewe kila siku nimekuwa na uhusiano na jini tu wewe unanikimbia. Je ukionana kabsa na jini lenyewe utafanyaje"Nilimwambia mdete baada ya kuelewa kuwa kumbe hata yale mambo aliyokuwa anayafanya usiku siku ile maimuna alipokuwa amekuja kunichukua yeye kwake ilikuwa kama ndoto. "Kuanzia sasa mimi na majini yakuna, ile ndoto ambayo nilikuwa nimeiota kwa kweli haikuwa ya mchezo. Tena sasa hivi bora niwe chapombe na kula nguruwe kwa sana ili hayo majini yaniogope kama Ukoma"Aliongea Mdete. Baada ya kuongea mambo mengi na Mdete mimi niliondoka na kuelekea nyumbani ila kwenye maongezi yangu sikumwambia mdete kuwa kifo cha mama yangu kilikuwa kinahusiana na yale majini. Ingawa aliniulizia chanzo cha kifo cha mama yangu kama kinamahusiano na majini maana kilikuwa cha ghafla mimi nilimwambia sijui

    Mimi nilimwelezea tu kuwa sijui chanzo cha kifo cha mama yangu wala Maimuna hajahusika na kitu chochote kuhusu kifo cha mama yangu. Baada ya kuagana na Mdete niliondoka na kwenda hadi nyumbani. Nilipofika nyumbani nilikuta ile gari imeshaondoka pale nyumbani. Ile hali ilikuwa inamaanisha kuwa Maimuna hakuwa pale tena nyumbani. Kwa kweli kitu ambacho kilikuwa kinanishangaza kwa Muda ule nilikuwa na hamu sana ya kumuona Maimuna na tayari moyo wangu ulikuwa umeonekana kuvutiwa sana kwake. Muda ule hata huzuni na mawazo kuhusu kifo cha mama yangu ilikuwa hakuna kabsa. Yani muda ule ilikuwa kawaida sana kama nilikuwa sijafiwa na mama yangu. Niliingia hadi ndani kwa mzee wangu. Cha ajabu mzee wangu aliponiona na yeye alifurahi sana na kubaki akiwa anacheka tu. Ile hali kwa upande wangu ilinishangaza sana. Kwani nilichotegemea kama mzee wangu angeniona angeanza kulia na kunilaumu kama mwanzo. Sasa kitendo cha mzee wangu kuniona na kuanza kucheka kilizidi kunichanganya. Niliwaza kichwani kitu gani mzee wangu ambacho amekipata au amekiona kutoka kwangu ambacho kimemfanya hadi kuwa na furaha namna hii. "Mwanangu kwa kweli endelea kuwa na tabia hii hii. Kuna binti flani hapa kasema mlikuwa mnasoma shule moja ya Kindai ingawa yeye alikuwa amekuzidi darasa. Ameniambia alikuwa rafiki yako sana na alitokea kuvutiwa sana na tabia zako. Ila yeye hakumaliza hata kidato cha nne pale alipofika kidato cha tatu aliweza kuhamishiwa Saud Arabia. Sasa aliposikia kama umefiwa na mama yako huwezi amini ametoka Saud arabia hadi huku kuja kwenye msiba wa mama yako. Kwa kweli huyu binti mungu ambariki sana. Kwani katoa gunia moja ya mchele kwa ajili ya arobaini ya mama yako, mafuta ndoo tano kubwa, sukari kilo mia moja unga wa ngano kilo mia na sembe kilo mia mbili. Achana na hayo makorokocho ambayo ametusaidia pia Ametoa kiasi cha pesa cha shilingi milion mbili kama pole yetu kwa kufiwa na mama Amina"Aliongea mzee wangu. Kwa kweli mimi yale maneno sikuyashangaa sana zaidi ya kumsifia tu Maimuna na kumwambia mzee kweli alikuwa ni rafiki yangu. "Mwanangu kwa kweli hiyo bahati naomba usije kuiacha kabsa kwani pia ameniambia kuwa kama Mungu akipenda anaweza kuwa mmoja katika familia yetu kupitia wewe. Sasa yale maneno mimi nilipoyapima nilijua moja kwa moja kuwa yule binti anataka umuoe. Sasa kama bahati hiyo itatokea naomba usije ukaiacha mwanangu. Tena mimi nataka nitimize yale maneno ya mama yako ambayo aliniambia kabla ya kufa. Mama yako aliniambia kuwa nihakikishe nakusomesha hadi unapata kazi yako pia nihakikishe unaoa msichana mwenye tabia nzuri. Hivyo haya mwanangu mimi lazima niyafanye ili hata mama yako kule alipo basi aishi kwa furaha"Aliongea mzee wangu. Kwa kweli mimi muda ule nilikuwa namsikiliza tu mzee wangu sikutaka kumpinga kwa kitu chochote. Pia sikutaka kumueleza kabsa kama Maimuna ni jini. Maana nakumbuka maimuna aliniambia kuwa hataki mtu yeyote duniani zaidi ya mdete kusikia kuwa mimi nilikuwa na uhusiano na Jini. Kwa kweli baada tu ya mazishi ya mama yangu ndani pale hasa upande wa baba yangu na ndugu zangu ilikuwa ni kicheko tu kulikuwa hakuna kabsa huzuni tena. Nilishindwa kuelewa maimuna amewafanyia kitu gani hawa watu hadi kufikia kusahau msiba mkubwa namna hii uliotokea kwa ghafla na kubaki wakiwa wanacheka tu. Tayari ndugu walishatoa shukrani kwa watu na kuwaelezea kuwa haina haja ya matanga hivyo wasubilie hadi siku ya kumaliza kilio yani Arobain. Muda wa saa tatu Usiku baada ya chakula cha Usiku niliondoka na kwenda kitandani kwangu kwenda kujipumzisha. Nilipofika tu chumbani nilikutana na aina nyingine kabsa ya perfume. Kwa kweli perfume ya siku ile ilikuwa ni kiboko yake. Ile perfume ilikuwa inanukia vizuri ile mbaya hadi nilibaki nikihangaisha pua yangu kuweza kunusa ile perfume. Kwa dalili ile ya perfume niligundua lazima Maimuna alishakuja na hakuwa mbali kabsa na hii nyumba. Wakati nikiwa nawaza yale mimi sikuwa na wasiwasi kabsa maana tayari maimuna nilishamzoe na nilikuwa namuona mtu wa kawaida kabsa. Nilienda hadi kitandani kwangu nikajitupia na kutulia kusubilia ujio wa jini Maimuna maana nilijua lazima aje. Nilipojitupia tu kitandani ghafla upepo mkali ulianza kuvuma kwenye chumba changu. Cha ajabu ule upepo ulikuwa unavuma mbaya lakini haukuweza kunyanyua hata kitu chochote. Ule upepo ulivuma kwa dakika kama mbili hivi kisha nilishangaa kumuona maimuna akitokezea kwenye chumba changu. Kwa kweli nilijikuta mwenyewe nikitabasamu nilipomuona Maimuna. Kwani Maimuna alikuwa amependeza mbaya kwa lile vazi lake jeupe ambalo alikuwa amevaa. Baada ya kutokezea Maimuna alinisogelea na kunipiga Busu kisha alinikumbatia na kushangaa tuanza kupaaa kuelekea juu. Baada ya kupaa kwa mita kama mia moja hivi kutoka chini usingizi mzito ulinipitia na sikujua kile ambacho kilikuwa kimeendelea. Nilipokuja kushituka nilijikuta nimekaa kwenye kiti kizuri sana mbele ya ukumbi ambaye ulikuwa mzuri sikuwahi kuona. Kwa kweli nilishawahi kuona kumbi mbali mbali nzuri lakini sikuwahi kuona ukumbi mzuri kama ule. Niliangalia upande wangu wa Kushoto nilishangaa kumuona mdete naye alikuwa amekaa pembeni yangu huku akiwa ametinga bonge la suti. Kwa kweli ile hali ilinishitua sana, niliangalia mkono wangu wa kulia nilishangaa kumuona Maimuna akiwa amevalia vazi zuri nyeusi huku pembeni na yeye akiwa na mpambe wake. Mbele yangu nilipoangalia nilikutana na watu wengi sana ambao walikuwa na nyuso za furaha. Nikiwa naendelea kushangaa ile hali ndio nilipigwa na Butwaa nilipomuona mama yangu akiwa na baba yangu wamekaa kwenye viti huku wakiwa wananiangalia mimi na kutabasamu.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kweli ile hali iliniogopesha na kunishangaza sana. Nilichokuwa nakijua mimi mama yangu alikuwa ameshakufa hivyo kumuona akiwa yupo pale mzima huku wamekaa na baba yangu wanacheka ilikuwa kitu ambacho kilikuwa kigeni sana. Niligeuka na Kumwangalia mdete na yeye nilishangaa akiniangalia na kutabasamu tu huku akiwa na furaha mbaya. Nilishindwa kuelewa huyu mdete amewezaje naye kuja huku. Ni nani ambaye amemleta hadi huku. "Baada ya wageni wote wetu kufika ambao tulikuwa tunawasubilia basi ni vizuri tuendelee na sherehe"Aliongea mtu mmoja ambaye alikuwa na Sura nzuri pamoja na sauti ya kuvutia. Moja kwa moja yule mtu nilijua alikuwa ni Mtangazaji pale. Mambo ambayo nilikuwa nayaona pale ya kupiga Vigelele nilijua moja kwa moja ilikuwa ndoa yangu na Maimuna. "Kabla kabsa hatujaanza Ratiba yetu rasmi ningependa niwatambulishe wageni wote muhimu katika hii sherehe. Nikianza na mkono wangu wa kushoto. Huku wamekaa wazazi wa Mwanaume kapopo naomba wasimame na wapunge mikono"Aliongea yule Mc. Wazazi wangu wote wawili wakiwa na Furaha walisimama na kupunga mikono huku vigelele vikipigwa mbaya. Kwa kweli wazazi wangu walikuwa na furaha sana hadi mimi nilikuwa nashangaa. "Maimuna mimi kuna kitu kinanisumbua Sana akili yangu. Hapa mimi naona kama giza tu sielewi kitu chochote. Nahisi wewe unanipenda sana na mimi sasa hivi nakupenda kuliko hata unavyoelewa. Ila naomba nikuulize swali moja na naomba unijibu vizuri ili nielewe tafadhari naomba nipe maelezo ili kichwani kwangu kuwe kweupe Kabsa. Swali la kwanza nataka nielewe hapa kitu gani kinaendelea, swali la pili nataka nielewe mdete baba yangu na watu wengine wengi tu wamefikaje huku. Cha tatu ambacho ndio kimenichanganya zaidi nataka nielewe mama yangu amekufa au bado yupo mzima maana nashangaa namuona yule pale"Nilimwambia Maimuna lengo nipate Jibu sahihi maana nilikuwa natatizwa tu. "Hahahaha kapopo bhana umesema unaniuliza swali moja umeniuliza matatu. Jamani kapopo mbona unanishangaza sana, inamaana unataka kuniambia hujui ambacho kinaendelea hapa, Kinachoendelea hapa mimi na wewe tunafunga ndoa. Nazani swali lako la kwanza nimemaliza. Swali la kuhusu ndugu zako wamefikaje hapa naomba unisikilize kwa makini. Hawa ndugu zako wote wamefika hapa bila wao kujielewa. Yani haya ambayo yanafanyika hapa pindi watakaposhituka itakuwa kama walikuwa wanaota tu. Ndoa yangu na wewe ni lazima ndugu zako na wazazi wako wote wafike. Ndio maana tumewaleta huku bila wao kujielewa na watakuwa kama wapo kwenye ndoto ili kuweza kufanikisha kile kitu ambacho tunataka kukifinya. Nataka harusi yetu iwe na baraka pande zote mbili hasa kwa wazazi wangu na wazazi wako. Kuhusu mama yako kufa ni kweli amekufa na hapa tumemleta kama kimvuli ili kuweza kuhudhuria ndoa yetu"Aliniambia Maimuna. Kwa kweli yale maneno ya Maimuna yalinishangaza sana. Kitendo cha kuambiwa kama ndugu zangu wote walikuja kushuhudia harusi yetu kama watakuwa wanaota ilikuwa ni maajabu mengine. Hapo niliamini kumbe baadhi ya ndoto ambazo watu huwa wanaota zingine huwa ni kweli na huwa wanafanyiwa na majini. Pia kitu kingine ambacho kiliendelea kunishangaza ni kile kitendo cha Maimuna kuniambia kweli mama yangu alikuwa ameshakufa ila pale alikuja kama Kimvuli tu bado nilikuwa sijaelewa kabsa. Swali jingine ambalo lilikuwa linanisumbua kama kweli mama yangu alikuwa amekuja kama kimvuli je kile kimvuli kilikuwa kimetokea wapi. ****** ******* ******* **** Sikuwa na jinsi wala kuuliza Maswali mengi. Niliacha pale na kusikiliza kipi ambacho kilikuwa kinaendelea. Ndoa ilifungishwa pale na mimi nilikuwa nakubali kwa kila kitu ambacho nilikuwa naambiwa. Baada ya ndoa yetu kufungwa huku watu wakiwa na furaha ya Aina yake ilifuatia muda sasa wa kutoa zawadi. Kwa kweli hapo ndio niliona kulikuwa na utofauti mkubwa sana. Mimi kwa upande wangu nilikuwa nafahamu na nilikuwa naona zawadi watu walikuwa wanatoa kama vyombo pesa lakini pale ilikuwa tofauti. Watu ambao walikuwa wanatakiwa kutoa zawadi walikuwa wametoka upande wa maimuna tu na walikuwa watatu tu walikuwa wamechagulia. "Kwa kweli mimi ninafuraha Sana kuhusu hii ndoa, furaha ambayo ninao kwa kweli sijawahi ona. Nimepata mwanangu wa pili wa kiume ambaye ni Binadamu. Hiki ndio kitu ambacho nilikuwa nakililia sana ndio maana nilimwambia mwanangu aweze kuolewa na binadamu. Ili kuwadhihirishia kuwa leo ninafuraha nitawapa wanangu gari moja pia nitawajengea nyumba ya kuishi nzuri"Aliongea baba yake na Maimuna na watu wote walishangilia. Kitu ambacho kiliendelea kunishangaza yale maneno ambayo aliongea baba yake na Maimuna hadi mama yangu nilimuona akiwa anashangilia. Mama yake na Maimuna naye alitoa zawadi na zawadi ya Mwisho ilikuwa imetoka kwa mjomba wake na maimuna. Zawadi zote ambazo zilikuwa zimetolewa zilikuwa za thamani sana ambayeCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ binadamu wachache hutoa kwa watoto wake. Baada ya ndoa watu walipewa chakula na kuanza kula. Kwa kweli kile chakula kilikuwa cha aina yake na kilikuwa kizuri na kimepikwa kwa Utalamu wa hali ya juu. Watu walikula chakula na vinywaji hadi waliacha. Baada ya chakula mimi na Maimuna tuliondoka na kwenda hadi chumba ambacho niliambiwa na Maimuna nitakuwa nafikia. Nilipofika kwenye kile chumba nilijitupia kwenye kitanda. Nilipojitupia kwenye kitanda tu ile nataka kugeuka nikishuhudia na yeye maimuna jinsi ambavyo atajitupia kitandani nilibaki nikiwa nashangaa nilipojiona nipo chumbani kwangu. "Mwananguuuu, mwanangu mamamaaaaaaa nakufa"Zilikuwa ni kelele ambazo zilikuwa zinatoka chumbani kwa baba yangu. Niliondoka nduki na kwenda hadi kwa baba yangu kwenda kuangalia nini kimemkuta hadi anapiga kelele usiku ule wote. "Mwanangu nimeona ndoto mbaya sana. Mwanangu nimeota at mnafunga ndoa na yule binti ambaye alikuja kutoa pole hapa. Yule binti ambaye alijitambulisha kama maimuna na rafiki yake. Sasa mbaya zaidi kwenye hiyo ndoa at Hadi mama yangu alikuwa yupo"Aliongea baba yangu huku akiwa anatetemeka





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog