Search This Blog

NYUMBA YETU,NYUMBA YA WACHAWI - 2

 







    Simulizi : Nyumba Yetu, Nyumba Ya Wachawi

    Sehemu Ya Pili (2)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Mmh! Enhe! Ndio ikawaje?’’aliongea mwenyekiti.



    ‘’Baada ya kuingia porini kufika sehemu nikakutana na watu,wale watu sura zao zilikua ngeni sana katika macho yangu,tulipishana huku mimi nikiwa namtafuta Faluu,baada ya kumuita kwa muda mrefu nilisikia sauti yake ikiitika,lakini cha ajabu wakati nikifuatilia kule sauti ilikokua ikitokea nageuka nyuma nikakutana uso kwa uso na wale watu’’



    “weeeeeee’’ watu walijibu



    “enhe!! Ikawaje?’’aliongea Mwenyekiti



    ‘’wakaniambia Sikiliza wewe!leo umepona ila onyo kwako,uliyoyaona huku usimueleze mtu yeyote,tena sikiliza!Usimueleze mtu yeyote!!, sina mengi ila ni matumaini yangu umenielewa,huwasirudii mara mbili,sasa ukitaka kuona kitu gani nitafanya katika maisha yako,wewe fanya hivyo, na baadae yule mkubwa wao akanipulizia upepo nikajikuta natokea hapa nyumbani’’



    Watu baada ya kusikia hivyo walishangaa na wengine walianza kulia, kwa maana mambo yale yalikua ni mapya kwao…



    ‘’Unaweza ukalikumbuka hilo pori ulilokuwepo?’’mwenyekiti alimuuliza Elly



    ‘’Ndio nalikumbuka sana’’Elly alijibu



    ‘’Basi jamani akina baba wote naomba mjiandae tuingie msituni’’aliongea Mwenyekiti………





    Baada ya maneno mazuri kutoka kwa M/kiti,wanakijiji waliokuwepo katika eneo lile walitawanyika ili wakajiandae na kazi iliyokuwepo mbele yao kama Mwenyekiti alivyowaeleza.Kulitokea na minong’ono ya hapa na pale kutoka kwa wanakijiji wale huku kila mmoja wengine wakielekea katika eneo la msiba na wengine wakielekea majumbani kwao.Kwa namna moja ilikua ni udhuni sana kwa namna moja kutokana na tukio ambalo lilikua limemtokea kwa  Faluu.



    ‘’Sasa ,hivi tutakuta yule motto ni mzima kweli??,mbona kama mimi nakuwa na wasiwasi sana?’’ Mama mmoja alikua akimuuliza mwenzie,huku wakiwa wanaelekea katika msiba.



    ‘’Hata mimi Napata shida kidogo katika hili jambo,lakini kuna msemo unasema

    (Hakuna kitu kinachopotea katika haki,huenda akakutwa ni mzima’’ yule mama mwingine alijibu



    (Huku akivuta pumzi kwa nguvu,yule mama aliongea)



    ‘’Aaaaaaah,labda bwana,lakini Mungu atamsaidia’’



    Waliendelea na maongezi yao na baada ya muda walifika msibani na taratibu nyingine ziliendelea pale katika msiba.



    Baada ya Elly kubaki pale nyumbani kwao,alijikuta akipokea maswali mengi sana kutoka kwa watu waliokuwepo eneo la nyumba yao,wakitaka kujua zaidi nini na nini kiliendelea pale na namna alivyoathirika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Kijana pole sana kwa hili’’ aliongea mzee mmoja pale.



    ‘’Asante sana Mzee Koo,nimesha poa’’ Elly alijibu.



    ‘’Mmmh, embu naomba unieleze hasa,juu ya mazingira husika ya tukio hili lililokusibu’’



    ‘’Mzee wangu sijui hata niseme nini,lakini zaidi ya yote ,ndivyo ilivyokua.Zaidi ya yote naomba tu tujiandae,tukajaribu kumuona huyu rafiki yangu Faluu,ili tupate na nafasi ya kumzika mama yake,lakini ni tatizo,maana sijui hata hari yangu itakuaje baada ya kusema kitu hiki..’’alisema Elly



    Wakati akiwa pale watu walitawanyika na wakakubaliana waende kujiandaa kabla ya kuaanza safari ya kwenda porini kumtafuta Faluu.Wakati Elly akiwa ametulia nyumbani kwao katika chumba chake akisubiri watu wakusanyike ili wakaendelee na majukumu yao,Kabla muda waliokubaliana haujafika,Alianza kuhisi hali tofauti katika chumba kile na kuanza kusikia milio ya ajabu



    ‘’Huuuu…! Huuuuuu!’’ kama upepo na wakati mwingine alisikia kama kuna mtu anamwita,hali ile ilimfanya aogope sana na kupelekea kushindwa kujizuia kukaa ndani,ndipo alipoamua kutoka nje ili akatafute msaada kwa watu.Wakati akiwa anataka kufungua mlango ilia toke,alikuta mlango haufunguki…ile hali ilimshangaza sana.



    (Huku akitetemeka,alianza kupiga kelele)



    ‘’Mama…..!mama..!mama…!,jamani nisaidieni,Nakufa” Elly alianza kupiga kelele.



    Wakati huo Elly akiwa ndani,watu walianza kukusanyika pale katika nyumba yao na zaidi ya 75% ya watu waliokuwa wanatakiwa kwenda katika shughuli ile walikua wamefika ,hivyo walikua wanamsubiri Elly tu maana ndiye kiongozi wa sehemu waliokua wanataka kwenda.



    ‘’Jamani,mbona hatumuoni Elly,eti..mama Elly,Elly yuko wapi??’’ Mzee mmoja aliuliza.



    Lile swali lilimshtua sana mama yake Elly nakuanza kumtazama huku na huku,huku akianza kua na wasiwasi.

    ‘’Mmmmh,sijui alikua hapa hapa,ila muda Fulani aliniambia anaingia ndani ili apumzike wakati anasubiri mkusanyike,toka hapo sijamuona ,embu jaribu kumuona humo chumbani kwake’’ mama yake Elly aliongea..



    Kutokana na kauli ya mama yake Elly,ilipelekea wanakijiji waliokuwepo pale kuanza kua na wasiwasi na hivyo kupelekea kua na minong’ono ya hapa na pale kutokana na tukio lile.Mmoja alijitokeza na kwenda kumuona katika chumba chake.Wakati yule mtu anaenda Elly alikua akipiga kelele,lakini sauti ya ajabu ilimueleza Elly…



    ‘’Wewe si unajifanya mjanja,sasa nataka nikuoneshe,maana naona kuna mtu anakuja kukuona’’



    Ghafla walipotea katika chumba kile na Elly kujikuta akiwa katika pori zito lililompelekea kuogopa sana…

    (Kwa sauti ya upole huku akitetemeka,Elly aliongea)



    ‘’Samahani,umenileta wapi huku,mbona mimisipaelewi,halafu pia tumekujakuja tu,naomba nirudishe nyumbani’’

    Lile jitu lilicheka sana tena kwa mguvu huku ardhi ikitetemeka na baadae liliongeaa



    ‘’Elly rafiki yangu wewe unajifanya mjanja sana,uliambiwa na mkubwa wangu kua ulichokiona kule usiseme sehemu yoyote,lakini kwa vile wewe unaakili kutushinda ukasema,sasa mimi nimekuja kukuua leo,hilo tu ndio jukumu langu,hahahahhahahahah’’liliongea na baadae lilicheka sana…



    Maneno yale yalimfanya Elly aone kama hakuna maisha tena kwa upande wake,hivyo alijikuta nguvu zikimuishia..



    ‘’Naomba….,niko chini ya miguu yako,yaokoe maisha yangu,sitafanya tena hayo mambo,nisamehe tadhali’’aliongea Elly huku machozi yakimtoka kama maji na macho yake yakiwa mekundu sana.



    Wakati akiongea lilelijitu lilikua limetulia likimsikiliza huku likiwa limeinamisha kichwa chake chini,baada ya Elly kumaliza kuongea liliinua macho yake huku  yakiwa yatoa moto na vidole vyake vikiwa vimetoa kucha ndefu sana na kila alipokua akiongea mdomoni mwake mlikua mnatoa moto huku akiwa anamsogelea Elly..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya Elly kumtazama na kuona muonekano wake mpya,alishtuka sana na kujikuta macho yake yanapoteza uwezo wakuona mbele kutokana na ule moto.Wakati lile lijitu likitaka kumuua Elly ghaflaulitokea Mwanga mkali sana katika eneo lile………



    Baada ya mwanga ule kutokea,lile jitu lilipotea ghafla katika eneo lile na katikati ya ule mwanga alimtokea mtu mweupe mwenye mavazi meupe ,Elly alibaki akimshangaa tu,



    (Akiwa anashangaa,Elly alimuuliza)



    ‘’Mbona mnanitesa sana na wewe ni nani?? ‘’Elly aliuliza



    ‘’Pole saana kijana,nimefatilia sana  namna unavyoteseka na naomba uamini kua mtu mnayetaka kumtafuta nimzima kabisa na muda si mrefu utamuona,lakini swala ambalo napenda sana umfikishie ni hili,naomba umwambie kua katika maisha yake atateseka sana,lakini lazima awe na matumaini ya kufika kule anakotakiwa kufika’’aliongea yule mtu pale na baadae alipotea.



    Baada ya kumaliza kuongea na kupotea,ilikua kama saa 9 usiku na ghafla alimuona Faluu mbele ya macho yake,Alishangaa sana  …

    .

    ‘’Daah,rafiki yangu Faluu ni wewe??ulikua wapi ndugu yangu na unaendeleaje??’’ Yalikua ni maswali mfululizo ambayo Elly alikua akimuuliza Faluu.



    Katika kipindi chote hicho,Faluu alikua hamjibu kitu chochote na zaidi ya yote alikua akimtazama tu.Wakati akimtazama ulipita upepo katika eneo lile na dakika chache walijikuta wakiwa nje ya nyumba ya akina Elly,Elly aliona kama miujiza ujiza ikimtokea,maana mara yuko hapa,mara hayupo…..



    ‘’Mbona kama maisha haya mimi siyaelewi?,nini maana yake??’’alikua akijiuliza pasipo kua na majibu. Wakati wakiwa nje alikua akitoka mtu mmoja akienda kwake huku wakiwa wamekata tama juu ya kila kitu kilichokua kikiendelea juu ya kumtafuta Faluu na Elly..



    (Alishtuka sana kuwaona pale)



    ‘’Jamani! Jamani! Jamani! Faluu na Elly hawapa nje”aliongea huku akikimbilia ndani,watu wote walishtuka na kujikuta wakishindwa kujibu chochote…na mwisho wa siku watu wote walikimbilia nje ili wakawaone vijana hawa maana akili zao zilikua zimechoka na kushindwa kuamua chochote kwa namna mambo yalivyowakabili.



    Baada ya kufika nje walipatwa na mshangao sana,watu wakulia walilia,wakufurahi walifurahi,kila mtu alikua na hisia zake kwa kipindi kile,ilikua ni shangwe iliyochanganyikana na huzuni kutoka na mambo yaliyowakabili,wengi wao walimfata Faluu ili walau awaambie kitu chochote..



    ‘’Faluu baba embu ongea,nini kimekukuta?’’aliuliza mama mmoja huku akitokwa machozi..



    Faluu hakua na cha kujibu na zaidi machozi yalikua yakimtoka tu pale,kutokana na hali ile,Elly alijibu..



    ‘’Mimi naomba mumuache Faluu,maana ninaamini hawezi kujibu chochote,hata mimi nimemkuta katika mazingira hayohayo’’aliongea Elly..



    ‘’Kwani umemkuta wapi??na kwanini umeenda peke yako??’’



    (Huku akitabasamu kwa hudhuni,Elly alijibu)



    ‘’Wewe acha tu,ni historia ndefu,kwamaana sijui hata niseme nini hapa’’



    ‘’Kwanini unasema hivyo kijana??’’aliuliza mzee mmoja.



    ‘’Mimi ninachoweza kukumbuka ni kwamba,mimi nilikua nimelala ndani kwangu nikiwa nasubiri muda ufike kama tulivyokubaliana,lakini kilichonikuta nashindwa hata kuelezea,lakini zaidi ya yote nashukuru sasa Faluu rafiki yangu huyu hapa tu’’Aliongea Elly huku machozi yakiwa yanamtoka.



    Kutokana na hali ile,ilipelekea watu waliokuwepo pale wawe na uzuni saana na baadae walichukuliwa na kupelekwa ndani na kusubiri utaratibu mwingine wa nini kiendelee.Kipindi hicho Faluu alikua mtazamaji tu.Ilipofika asubuhi kama ya saa kumi na mbili alifajiri,Faluu alisikia sauti kwa mbali ya watu wakilia,Sauti ile ilimfanya ashtuke sana na kutoka nje,ndipo alipoona watu wakilia na  ghafla kumbukumbu zake zilirudi..Akajikuta mawazo yakimjia..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Baada ya mambo yote ya msiba kuisha hakikisha unaenda kwa mjomba wako,hayo ndiyo maneno ya mwiso nilioachiwa na mama yako”



    ‘’Inamaana ni kweli mama yangu amefariki?? Inawezekana vipi?? Na kwanini aseme mimi niende kijiji cha pili?? Nini tatizo??’’ yalikua ni mawazo yalioambatana na maswali mengi huku machozi yakimtoka.



    Mwisho wa siku alianza kupiga kelele na kutoka mle ndani akikimbia huku akielekea kwao ilikujua nini kinaendelea juu ya taarifa alizosikia kuhusu mama yake,watu walishtuka kutokana na kelele zile na kuanza  kumfatilia kujua wapi anaelekea,pia kwasababu Elly alikua amebaki mle ndani walianza kumuuliza kama kuna chochote kamueleza..



    ‘’Vipi mbona ndugu yako ameshtuka na kuondoka ghafla hivi??kuna nini kinaendelea?’’Elly aliulizwa.



    ‘’Kwa kweli nashindwa jibu kamili la kutoa hapa,ila nililoona ni kwamba alisimama dirishani nakuwaona watu waliokua wakilia na baada ya dakika chache ndio hilo lilotokea likatokea’’aliongea Elly



    Baada ya hapo waliacha kumuuliza maswali na badala yake walianza kumfatilia ilikujua wapi ameelekea,Baada ya Faluu kufika kwao huzuni iliongezeka zaidi baada ya kukuta nyumba yao yote imeteketea kwa moto,alilia sana..



    ‘’Mama hivi ni kweli umeondoka mama yangu na hii ndio njia uliyoondokea??, inawezekana vipi mama yangu? Maana nakumbuka hata uliponiamsha na kunitaka niwahi shambani na ukaniambia natakiwa nikazane maana maisha ya kufanikiwa yanataka mapambano,kumbe ndio ulikua unaniaga,hapana mama yangu  ‘’ alilia sana Faluu na kujikuta akiwa akigaa gaa chini..



    Kilio kile cha Faluu ni kama kilikua kikiamsha tena hisia za watu waliokuwepo katika eneo lile na hasa kutokana na hali ya kuondokewa na mama na nyumba nzima na kila kitu ndani kuteketea.Jioni yake walishughulikia maswala ya mazishi kwa maana ule mwili ulikua umekaa muda mrefu na hivyo kupelekea kuanza kuharibika.



    Baada ya mazishi Faluu alikua hana sehemu ya kwenda,hivyo mama yake alimchukua na kumtaka aende kukaa kwake na watu wengine walijitolea kumsaidia vitu vingine.Siku mbili baadae akiwa amekaa nje ya nyumba yao,alijikuta mawazo yakimjia..



    ‘’ ’Baada ya mambo yote ya msiba kuisha hakikisha unaenda kwa mjomba wako,hayo ndiyo maneno ya mwiso nilioachiwa na mama yako’’

    Maneno yale yalimshtua tena sana…………………………





    Mawazo yale yalimfanya kua na wakati mgumu sana,maana hakujua ni maamuzi gani ambayo angechukua kwa kipindi hicho.Wakati akiwa amekaa pekee akiyatafakari maisha yake kwa ujumla,Alijikuta akisimama na kuelekea ndani asijue nini anaenda kufanya ndani,Alipokaribia mlangoni alikutana na Elly..



    ‘’Rafiki yangu vipi mbona sikuelewi?nimekutafuta tuje kunywa chai sijakuona na pia nikiangalia sura yako naona kama huko mbali sana?sikiliza hiki si kipindi cha kuwa mbali hivyo kimawazo,kwa maaana utakuwa unakaribisha vitu vinginee ambavyo kimsingi vitakuletea matatizo sana katika afya yako,kua makini sana na maisha yako yanayokuja basi na vitu vingine’’ aliongea Elly kwa uchungu sana.



    Yale maneno yalimfanya Faluu atulie pale,lakini hakuwa na jibu la kumueleza Elly kwa wakati ule na badala yake aliondoka tu na kuingia ndani .Hali ile ilimpa wakati mgumu sana Elly na akaona haitakuwa nzuri kama hatashindwa kumueleza mama yake juu ya kila kitu kinachoendelea kwa rafiki yake…



    ‘’Mama mimi nimekuja kukueleza kitu kimoja hapa’’ aliongea Elly



    ‘’Kitu gani hicho mwanangu ?’’aliuliza mama yake Elly.



    ‘’Unajua Ulipotuandalia chai muda Faluu hakuwepo ndani na nilijaribu kumtafuta sikumuona kabisa,mimi nikanywa hivyohivyo,lakini wakati natoka ndani saa hizi nimekutana nae mlangoni hapo,lakini nilivyomuona tu nikajua namna anavyohisi,Faluu hayuko sawa kabisa mama yangu na tukichelewa  tutampoteza’’ aliongea Elly kwa msisitizo zaidi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

       ‘’Sasa tutafanyaje mwanangu?’’aliuliza mama yake.



    ‘’Daah!!mimi sijui hata tunafanyaje,lakini kikubwa naona ipo haja ya kumkalisha chini na kumshauri,maana bila hivyo sijui hata itakuaje’’ alijibu Elly



    ‘’Kweli mwanangu,maana hatuna jinsi’’ aliongea mama yake Elly.



    Wakati wakiongea kule,Faluu alikua ndani akiwa ametulia mwenyewe huku akiwa na msongo sana wa mawazo na hasa mawazo yake yalikua juu ya nini msaada wa maisha yake.



    ‘’Nitafanya kitu  gani juu ya maisha yangu ya baadae?? Na nani atakae nisaidia kulifanikisha swala hili??,Mungu wangu mbona kama hauko na mimi?nisaidie Mungu wangu maana sijui ni kwanini mama yangu kafariki katika mazingira haya’’ Faluu alikua akifikiria sana.



    Wakati akiwa katika mawazo yale,Ghafla aliona hali ya chumba kile alichokuwepo ikibadirika na kulitokea na upepo mkali sana na baada na muda mfupi kulikua shwari kabisa,kitendo ambacho kilimfanya awe na wasiwasi zaidi.



    ‘’Mmmh,haya mambo gani tena humu,jamani mbona kama mnanifuatilia??mama yangu mumembeba na mimi tena??nimewafanyia kitu gani? Haya njooni mnichukue basi ili mfurahi’’ Faluu aliongea kwa uchungu sana.Sauti ile ilisikika nje walikokuwepo Elly na mama yake,sauti ambayo iliwafanya washtuke na kutaka kufatilia ili wajue nini kinaendelea..



    ‘’Wwe Elly embu ingia ndani uangalie nini kinaendelea,mbona mwenzio anaongea hivyo,wahi bhnaa’’ aliongea mama yake Elly.



    ‘’Kweli mama,ngoja nimuangalie’’ alijibu Ellyn a baadae alikimbia kuingia ndani alikokuwepo  Faluu ili akathibitishe ajue nini kinaendelea.



    Alipofika alimkuta Faluu akiendelea kuongea yale maneno na cha ajabu,Elly alianza kuangalia huku na kule ili ajue ni nani atakua akiongea nae..



    ‘’Faluu ndugu yangu,wewe ni ndugu yangu sasa,naomba utambue hauitaji kunificha kitu chochote sasa hivi,embu niambie,unaongea na nani?? Na mbona unakua katika hali hiyo??punguza mawazo kaka ‘’ aliongea Elly



    Katika kipindi chote hicho Faluu hakuwahi kuongea kitu chochote kilichokua kikimsibu,Lakini baada ya kusikia maneno kutoka kwa rafiki yake Elly ilibidi aongee kitu…



    ‘’Ni kweli ndugu yangu unayoyazungumza,lakini kuna wakati nafikiria najiona kama niko peke yangu na sina msaada kabisa maisha yangu’’ aliongea Faluu huku akilia.



    ‘’Kwanini unasema hivyo?’’ Elly aliuliza.



    ‘’Kwasababu siku ile wakati niko shambani,kuna sauti niliisikia katika masikio yangu ikinieleza kua,baada ya mazishi ya mama nilitakiwa nihame hapa,niende kijiji cha jirani,ndivyo alivyoniambia’’aliongea Faluu.



    Maneno yale yalimshtua sana Elly na kujikuta yakimkumbusha siku alipomuona Faluu porini …



    ‘’Aisee,rafiki yangu pole saana,najua namna unavyoumia,lakini pia kuna maelekezo nilipewa kwamba ;Pole saana kijana,nimefatilia sana  namna unavyoteseka na naomba uamini kua mtu mnayetaka kumtafuta nimzima kabisa na muda si mrefu utamuona,lakini swala ambalo napenda sana umfikishie ni hili,naomba umwambie kua katika maisha yake atateseka sana,lakini lazima awe na matumaini ya kufika kule anakotakiwa kufika’’aliongea yule mtu pale na baadae alipotea…



    (Kwa mshtuko mkubwa sana ,Faluu aliongea)



    ‘’Nitateseka?? Sasa ndio maisha gani? Na pia ni mtu gani huyo aliyekueleza maneno hayo’’



    ‘’Aisee,rafiki yangu pole saana,najua namna unavyoumia,lakini pia kuna maelekezo nilipewa kwamba ;Pole saana kijana,nimefatilia sana  namna unavyoteseka na naomba uamini kua mtu mnayetaka kumtafuta nimzima kabisa na muda si mrefu utamuona,lakini swala ambalo napenda sana umfikishie ni hili,naomba umwambie kua katika maisha yake atateseka sana,lakini lazima awe na matumaini ya kufika kule anakotakiwa kufika’’aliongea yule mtu pale na baadae alipotea…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    (Kwa mshtuko mkubwa sana ,Faluu aliongea)



    ‘’Nitateseka?? Sasa ndio maisha gani? Na pia ni mtu gani huyo aliyekueleza maneno hayo’’Aliongea Faluu



    ‘’Unatakiwa utulie kwanza na upunguze wasiwasi sawa,ila kiukweli mtu huyu si mfahamu na namna alivyotokea pale nilipokua katika msitu ule sijui hata nikueleze nini,embu tuanze maisha mapya sawa ndugu yangu’’Aliongea Elly.



    ‘’Sawa rafiki yangu,nimekuelewa sana,lakini nitahitaji sana msaada wako’’Aliongea Faluu



    Baada ya kukubaliana pale,Elly alimchukua na kumpeleka moja kwa moja kwa mama yake,ili na mama naye aongeze maneno yake,maana waswahili wanasema,maneno ya mtu mzima ni dawa kutokana na hekima iliyopo ndani yake. Mama alipomuona alifurahi sana ..



    ‘’Karibu mwanangu,jisikie nyumbani ‘’aliongea mama



    ‘’Asante sana mama yangu’’alijibu Faluu



    ‘’Mama nimemleta Faluu kwako na nimemweleza kila kitu,kikubwa nataka kushirikiana naye’’aliongea Elly.



    ‘’Sawa mwanangu,lakini napenda kuongea neno moja kwako mwanangu,Maisha yetu binadamu,yana mambo mengi,hususa ni furaha ,amani na wakati mwingine maumivu,hayo ndiyo maisha yetu wanadamu,kikubwa katika ni uvumilivu na kujua kua hayo yote ni maisha sawa mwanangu,tutakua wote hapa usijali,Nakupenda sana mwanangu’’mama yake Elly aliongea.



    Maneno yale yalimfariji na kumfurahisha sana Faluu na kujiona kama maisha ameyashinda tayali.Faluu alianza maisha yake kwa moyo na akajikuta akiwa na furaha sana na siku zilizidi kwenda.Baada ya miezi kadhaa Faluu alianza akijishughulisha na biashara ndogondogo ya kuuza nyanya akiwa na rafiki yaake Elly ambaye ndiye aliyemchukulia kama ndugu,kwa maana akuwa na ndugu mwingine tofauti na familia aliyokua akiishi kwa kipindi hicho.



    Biashara yao ilizidi kukua siku hadi siku na alizidi sana kuyapenda maisha yale aliyokuwepo.Lakini siku moja akiwa amekaa sokoni anaendelea na biashara yake,Elly alikua ametoka kidogo ameenda kufatilia mzigo mwingine,Faluu alijikuta mawazo mabaya yakimjia katika kichwa chake,yalikua ni mawazo juu ya maisha yake yaliyopita na zaidi ya yote ilikua ni kumbukumbu juu ya mama yake na wakati huo huo akiwa katika mawazo hayo alijikuta yale maneno aliyoambiwa kipindi akiwa shambani siku mama yake anafariki yanamjia…



    ‘’Baada ya mambo yote ya msiba kuisha hakikisha unaenda kwa mjomba wako,hayo ndiyo maneno ya mwisho nilioachiwa na mama yako’’ Maneno haya yalifanya hali yake kubadirika na kua na majonzi sana.



    Wateja walipokua wakifika kutaka huduma walishangaa sana,maana hawakumzoea akiwa katika hali ile,wengine walijaribu kumuuliza..



    ‘’Faluu kaka mbona kama unaonekana hauko salama leo,kulikoni ndugu yangu’’ aliuliza dada mmoja..



    Lakini cha ajabu siku hiyo Faluu akuwa na maneno mengi zaidi ya kutoa huduma tu kwa wateja na kuendelea na hali yake.Ilikua nikipindi kigumu sana kwa Faluu na kulikua na swali ambalo lilikua likimsumbua zaidi…..



    ‘’Kwanini mama yangu alinitaka niondoke hapa baada ya kumaliza mazishi??, hivi inawezekana kweli?? Na kwanini??’’ lakini kwa upande wake alikua akikosa majibu maalumu yakujijibu..



    Baada ya muda Elly alifika na kujikuta akipigwa na butwaa baada ya kuona hali ile kwa Faluu,maana ile hali muda mrefu sasa kuiona kwa rafiki yake,



    ‘’Ndugu yangu vipi?, mbona hivyo kaka’’aliuliza Elly



    ‘’Samahani kaka naomba nikuache,nikapumzike kidogo nyumbani,siko salama sana,nakuomba’’hayo ndiyo maneno aliyoongea Faluu na baadae aliondoka na kuelekea nyumbani.



    Elly alibaki njia panda pale,maana Faluu hakumfungua kujua nini ni nini kwake na wakati mwingine alifikiria kama yeye ndiye sababu ya hali aliyokua nayo Faluu..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Mmmh,kwanini hali hii ghafla??kulikoni??lakini labda’’alifikiria na baadae aliamua kuachana nayo na kuendelea na biashara pale sokoni…



    Baada ya Faluu kufika nyumbani,alipitiliza hadi katika chumba wanacholala na kupumzisha mawazo yake kidogo,lakini pia wakti akiwa ndani amelala,yale maneno yalimjia tena na kusumbua akili yake,alijikuta akishindwa kuvumilia..



    ‘’Jamani nitaisha hivi mpaka lini ??,basi ngoja nifanye mnavyotaka basi’’yalikua ni mawazo yake Faluu na baadae aliamka na kuanza kukusanya nguo na baadae aliondoka bila kutoa taarifa na kuelekea katika kile kijiji alichoambia aelekee baada ya mazishi ya mama kama maagizo  kutoka kwa mama yake ………………..





    Faluu aliondoka na kuelekea katika kile kijiji alichoelekezwa na ile sauti aliyoisikia shambani.Wakati akiwa njiani alikua na mawazo mengi sana na hasa alikua akitafuta sababu ya kwanini aende kwa mjomba wake katika hicho kijiji.Alipokua amefika katika mti mmoja mkubwa  uliokuwepo pembezoni mwa njia aliyopita,upepo mkali sana ulianza kuvuma ghafla tu,hali ambayo ilimfanya aingiwe na hofu..



    (Huku mapigo yake ya moyo yakiwa yamebadirika,mawazo yalimjia)



    ‘’Mmh! Hii nini sasa na kwanini hivi,mbona nateseka saana??’’ alikua akiwaza huku machozi yakimtoka,hali ile ilimuumiza sana..

    Baada ya Elly kukaa muda mrefu sokoni bila majibu yoyote ya rafiki yake,alianza kujisikia vibaya na kujikuta akiingiwa na hofu sana na kwa vile alikua amezoea kua naye sokoni alijkuta akikosa amani na hivyo akaamua kufunga ili aende akamjulie hali yake nyumbani.Alipofika nyumbani alimkuta mama jikoni akiwa anapika,mama alipomuona alibaki akimshangaa tu kitendo ambacho kilimpa wasiwasi Elly..



    ‘’Mama mbona unaniangalia sana kulikoni’’ Elly aliuliza.



    ‘’Nakushangaa wewe hapo,’’ mama alijibu.



    ‘’Unanishangaa?? Nini tena??’’ Elly aliuliza



    ‘’Sasa mbona huko peke yako? Rafiki yako yuko wapi?’’ mama aliuliza



    Swali lile lilimshtua sana Ellyn a kumfanya hautupe ule mfuko aliokua amebeba…



    ‘’Peke yangu?mbona Faluu amekuja huku muda mrefu sana,maana muda Fulani ametoka sokoni akiwa analalamika hajisikii vizuri,mimi nikamwambia aje apumzike,kwani wewe hujamuona?’’ Elly aliongea huku akiwa na amepagawa.



    Kutokana na majibu yale ya Elly hata mama yalimshtua sana..



    ‘’Hapana sijamuona huku nyumbani’’ mama alijibu na baada ya Elly kusikia hivyo alikimbia na kwenda kumuona ndani kwao kama hata mkuta.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipofika ndani,alijikuta nguvu zikimuisha maana alichokiona hakufikiria kama atakutana nacho..



    ‘’Mama….mama..mama’’aliita Elly



    ‘’Nini mwanangu??’’alijibu mama



    ‘’Njoo uone,Faluu ameondoka,maana hata nguo zake hazipo,sasa atakua ameenda wapi?’’ Elly aliongea



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog