Search This Blog

NYUMBA YETU,NYUMBA YA WACHAWI - 3

 







    Simulizi : Nyumba Yetu, Nyumba Ya Wachawi

    Sehemu Ya Tatu (3)





    ‘’Mmmh sidhani’’ mama alijibu.Elly alikua na wakati mgumu sana,alijitahidi sana kutoka huku na kule kuuliza kama watu watakua wamemuona,lakini hakufanikisha.Lakini baadaye baada ya kurudi huku akili yake ikiwa imetulia aliiona karatasi ikiwa imeanguka chini,Karatasi ile ilimshtua na hivyo akaamua kuikota ili ajue ina nini.Alipoishika alikutana na maneno haya…



    ‘’Rafiki yangu najua utakua na wakati mgumu baada ya kusoma haya kama mimi nilivyo na wakati huo,Lakini sasa sina jinsi maana inabidi yafanyike ili maisha yaendelee,Rafiki yako nimeondoka naomba usiwe na wasiwasi kwa maana niko salama,naamini siku moja tutaonana.MAISHA MEMA  Wako Faluu’’CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Maneno yale yalimuumiza na kumfanya apige kelele mpaka mama alisikia na kuja haraka ili ajue kulikoni..,lakini mama alipofika Elly alimpa ile karatasi ilia some mwenyewe.Maneno yale yalimsikitisha sana na aliona namna mwanaye alivyokua akiumia..



    ‘’Mwanangu najua namna unavyoumia,lakini tambua kitu kimoja tu;Milima haikutani,ila binadamu tunakutana,usivunjike moyo sawa’’aliongea mama na baadaye aliondoka kwenda kuendelea na shughuli nyingine.



    Wakati Faluu akiwa anatembea huku alikua na mawazo ambayo yaliambatana na huzuni ghafla aliisikia sauti ya mtu akicheka na alipogeuka alikutana uso kwa uso na mjomba wake.



    ‘’Mpwa wangu karibu sana’’aliongea mjomba huku akiwa amejaa tabasamu zito katika uso wake.



    ‘’Asante sana mjomba wangu,lakini umejuaje kama mimi nakuja? Au huu ulikua mpango wako?? Na kwanini haujakuja katika mazishi ya mama?’’ Faluu alijikuta akiuliza maswali mengi sana na mfululizo.



    ‘’Aaah, acha wasiwasi  mjomba nilijua tu nan i maagizo aliyoniachia mama yako,twende nyumbani ukapumzike’’aliongea mjomba.



    ‘’Sasa hadi siku ya leo umejua kama mimi nakuja! Unanipa wasiwasi mjomba wangu’’aliongea Faluu.



    Wakati wakiwa wanajibizana Faluu na mjomba wake huku wakiwa wanatembea,Faluu alikua akijaribu kuchunguza pembezoni mwa njia,ghafla aliona kama kuna watu wamekaa pembezoni mwa njia hiyo wakiwa wamejificha na mbaya zaidi alimfananisha mtu mmoja aliyekua miongoni mwa watu waliomkamata siku ile,kitu ambacho kilimshtua sana na akajikuta akishindwa kujizuia na mwishowe ilibidi amuulize mjomba..



    ‘’Mjomba mbona kama naona kuna watu wamejificha pembezoni mwa njia hii?? Ni wakina nani?’’ Faluu aliuliza.



    Swali lile lilimfanya mjomba ashtuke saana na akajikuta akishindwa kujibu na badala yake alio

    ‘’Aaah!...aah.. mimi sijui,….mimi sijaja nao,kwanza wako wapi?’’aliongea mjomba.



    Majibu ya kubabaisha ya mjomba yalimfanya Faluu kuwa na wasiwasi na kua makini sana wakati mjomba anaongea,kutokana na wasiwasi wa mjomba alijikuta akipiga kipenga na bila kupoteza muda walitokea watu wengi na waajabu katika eneo



    ‘’Mjomba hii nayo nini?’’aliuliza Faluu,

    Mjomba aliishia kumtazama tu na bila kupoteza muda walipotea ghafla katika eneo lile





    Baada ya kupotea katika eneo lile,walijikuta wakitokea nyumbani kwa mjoma wake. Faluu alijikuta akijishangaa tu baada ya kutokea pale huku asijue nini afanye kwa wakati ule.Kwa upande wa mjomba alijikuta naye akishangaa,lakini lengo lake ilikua nikujitoa ili Faluu hasijue kitu chochote.



    ‘’Mjomba nini kinaendelea? Mbona mimi sielewi mjomba wangu?’’ Faluu aliuliza.



    (Huku akisita,mjomba aliongea)



    ‘’Aaah..aah..! hata mimi sielewi mjomba wangu,lakini usijali sawa’’Mjomba aliongea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya maneno yale Faluu aliishia kuguna tu na baadae alitoka nje..,Wakati akitoka nje Mjomba wake alishtuka na ghafla aliongea..



    ‘’Faluu unaenda wapi huko? Njoo nikuoneshe chumba chako huku’’ aliongea mjomba



    ‘’Hamna mjomba nilikua nataka niangalie tu huku’’ alijibu Faluu.



    ‘’Hapana usiende huko,njoo kwanza huku’’ aliongea mjomba na baadae Faluu ilibidi amsikilize mjomba na hivyo alirudi na kumfata mjomba wake.



    Mjomba alienda kumuonesha chumba chake na sehemu mbali mbali katika ile nyumba,ilikua ni nyumba kubwa sana iliyokua nan a vyumba vingi,lakini mazingira ya nyumba ile yalimshtua sana na kumfanya kua na maswali mengi..



    ‘’Mjomba mbona kama kuko kimya,wengine wako wapi?’’ Faluu aliuliza



    (Mjomba alishtuka)



    ‘’Mmmh!!.., hamna mjomba wangu,hapa nipo pekee yangu wengine wamesafiri kidogo” Mjomba aliongea..



    Baada ya kupewa maelezo yale Faluu alikubali na baadae aliingia ndani kwake kupumzika,wakati akiingia ndani kupumzika ilikua ni saa tisa usiku.Alimuacha mjomba wake akiwa amekaa Sebuleni ,Wakati akiwa amelala ndani alianza kuota kama nyumba inaungua na katikati ya moto ule alimuona mama yake akiwa anaungua katika ule moto huku akitaja jina la Faluu..



    ‘’Faluu…!Faluu mwanangu …Mwanangu haya ndiyo maisha ya mama yako,kikubwa tulia mwanangu ili uyafikie mafanikio’’aliongea mama katika ndoto na baadae aliteteketea kabisa katika ule moto.



    (Faluu alishtuka)



    ‘’MA…MA….MAMA!! MAMA..!!’’ Aliongea Faluu na ghafla mapigo ya moyo yalibadirika na Jasho lilianza akajikuta akimkumbuka sana mama yake



    (Huku machozi yakimtoka aliongea)



    ‘’Mama inakuaje unaondoka na kuniacha mimi katika mazingira kama haya mama,embu angalia sasa mwanao ninavyoishi mama yangu..hiiihiii, Nakukumbuka sana mama,sijui hata niseme nini mama …’’Aliongea Faluu huku machozi yakimtoka na kutokana na ndoto ile alijikuta usingizi na uchovu ukimuisha nakumfanya aamke na kusongwa na mawazo sana katika akili yake.



    Asubuhi ilipofika Mjomba waliamka wote na mjomba alimfata katika chumba chake kumjulia hali.

    ‘’Faluu mjomba salama’’ Mjomba wake Faluu aliongea



    ‘’Mimi mzima mjomba,shikamoo’’ alijibu Faluu.



    ‘’Marahaba,lakini mbona kama leo hujalala wewe’’aliongea mjomba



    ‘’Hamna mjomba…. Mmh….,niko salama lakini’’alijibu Faluu na mjomba alibaki kumtazama tu.

    Baada ya muda mjomba alimuita tena ili ampe maagizo,



    ‘’Sasa mjomba Faluu,mimi nataka nitoke,lakini si unajua tupo wawili tu humu ndani,utaangalia pesa nimeacha pale juu ya kabati kama shilingi 2000,utaenda kununua mboga na utapika’’ aliongea mjomba.



    (Faluu hakulipenda lile swala)



    ‘’ Mmh,sawa mjomba nitafanya hivyo,ila sijui mazingira ya huko unakonunua’’alijibu Faluu



    ‘’Mbona kama unaguna au haujaridhika? ” mjomba aliuliza.



    ‘’Aaah,hamna mjomba niko sawa’’ alijibu Faluu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Basi  sawa,ila kuhusu maelekezo ya eneo la soko,kuna mtu atakuja kukuelekeza sawa’’ alijibu mjomba Na kisha akaondoka..



    ‘’Kuna mtu atakuja kunielekeza?mtu gani huyo?’’ Faluu alijiuliza, Wakati akiwa anajiuliza alisikia sauti ya mtu akitembea mule ndani na wakati akigeuka alishtuka kwa maana alikua ni mtu mmoja mfupi sana,baada ya kumuona mwili wake ulisisimka sana…



    ‘’Na wewe nani?’’Faluu aliuliza



    (Huku akicheka,yule mtu alijibu)



    ‘’Hahahahahhaha, unauliza mimi nani?, mimi ndiye natakiwa nikuulize wewe,ila kwa kua huu si muda wa maswali na majibu tuyaache maswali,nimeagizwa nikusindikize sokoni ukanunue mboga’’yule mtu aliongea.



    Wakati yule mtu akiongea,sauti yake ilipelekea mtikisiko mkubwa sana wa ile nyumba na kumfanya Faluu kuishiwa maswali na badala yake ndiye alikua wa kwanza kutangulia mbele kutokana na uwoga aliokua nao..

    “Twende sasa mbona unabaki nyuma?”aliongea Faluu





    Baada ya yule mtu kusikia hivyo alitoka na baade waliambatana wote kwenda sokoni kununua hizo mboga,walipokua barabarani watu waliomuona Faluu walikua wakimshangaa na kuulizana maswali ya kwanini yule kijana kafatana na yule mtu..



    ‘’ Jamani yule kijana ni nani? Na mbona kafatana na yule mfanyakazi wa yule mzee Kachali? Au ndio mfanyakazi mpya nini? Na mbona anamtumikisha kijana mdogo hivyo” mama mmoja alijikuta akiwauliza wenziye maswali mengi  yaliyokosa majibu kwa masikitiko maakubwa.



    ‘’Mmmh! Na wewe unatuuliza maswali hayo wakati unajua kila kitu bhana,sisi tuko wote hapa halafu unatuuliza’’alijibu mama mmoja,Wenziye walimcheka sana yule mama ,kutokana na maswali yake,

    (Kwa aibu yule mama alijibu)



    ‘’Jamani ndio mmeamua kuanzisha mjadala hapo,mimi nimeongea tu,kama maswali yangu yamewakela naomba mnisamehe’’ Yule mama alijibu na baadaye aliondoka katika eneo lile huku wale wakina mama wenzie wakiendelea kucheka.



    ‘’Watu wengine bhana,sasa sisi kucheka ndio tumemfukuza?,maswali gani haya anatuuliza sisi,kwanini asimuulize mumewake?’’mama mmoja aliongea pale..



    (Wenzake kwa pamoja walimjibu)



    ‘’Acha naye huyo’’na baadaye waliendelea na maongezi yao.



    Baada ya pale Faluu alienda na yule Mtu aliyepewa amsindikize mpaka katika bucha ya Nyama ili kwanza ajue mahali atakapotakiwa kupata huduma hiyo nan i huduma gani,



    ‘’Haya kijana mahali penyewe ndio hapa’’aliongea yule mtu.



    ‘’Mbona kama hii ni Bucha?’’Faluu aliuliza



    ‘’Ndiyo ni Bucha na ndio sehemu tunayonunua vitu vyetu’’alijibu.Baada ya kuangalia angalia,mazingira ya ile Bucha yalimfanya Faluu kupata wasi wasi kidogo na hivyo kumfanya kushindwa kuelewa..



    ‘’Mmmh,ndiyo Bucha yenu?kwa maana hiyo ndiyo sehemu mnayonunulia mboga zenu’’Faluu aliuliza .

    “Ndiyo bhana aah!’’yule mtu alikasirika.



    ‘’Oyaa! Tunaomba mboga zetu,tupatie za shilingi 3000’’ yule mtu aliongea..



    ‘’Mboga zetu?? Mbona sikuelewi?’’Aliongea Faluu na alijikuta yale maneno yakizidi kumchanganya na kumuacha yule mtu afanye vile anavyotaka ,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Haya bhana,basi fanya hivyo’’aliongea Faluu.Baaada ya kuongea vile,yule mtu alipima nyama. Wakati akipima ile nyama,Faluu alishtuka sana Baada ya kuiona ile nyama katika ule mzani kwa namna ilivyokua ikionekana..



    ‘’Mmmh!nyama gani hii,mbona kama haileweki?’’ alikua akiifikiria huku macho yote akiyaelekeza mahali ilipokuwepo.



    ‘’Wewe kijana mbona unaona sana? Kuna tatizo?’’ yule muuza nyama aliuliza.



    ‘’Aaah,hamna tatizo,ila naomba kujua,ni nyama gani hii?maana sijawahi kuiona’’ Faluu aliuliza pale.



    ‘’Mbona unakua na haraka hivyo utajua tu’’Yule muuza nyama alimjibu,Baada ya pale Faluu hakua na maswali tena,mwisho wa siku yule muuzaji aliitoa ile nyama na Faluu alitoa hela huku na kupokea ile nyama na baadaye walirudi nyumbani.Ile nyama ilikua mchanganyiko wa steki na mifupa mifupa.Walipofika nyumbani yule mtu aliyepewa amuelekeze,alimpa maelezo pale juu ya nini anatakiwa aweke wakati anapika ile nyama.



    ‘’Wewe!! Sikia hiyo nyama hatuweki viungo vyovyote,nisikie wewe,usiweke nyanya wala kitunguu chochote,huwa tunakula hivyo hivyo’’aliongea yule mtu huku akitokwa na udenda kutokana na uchu aliokua nao.



    ‘’Mbona kama mimi siwaelewi?? Embu nipe maelezo yakutosha ili mimi nikuelewe,sikuelewi kabisa’’Faluu aliongea huku kichwa chake kikionekana kujaa maji.



    ‘’Sikia hakuna maelezo mengine zaidi ya hayo,chemsha hiyo nyama na usiweke kiungo chochote,hiyo huwa tunakula hivyo hivyo na hayo ndiyo maelekezo yangu ninayoweza kukupa zaidi ya hapo mimi sijui’’ alijibu yule mtu.



    ‘’Bado mimi sijakuelewa hapa kabisa’’aliongea Faluu



    ‘’Utajua mwenyewe,ila kikubwa fanya hivyo ,mengine utakuja kumuuliza mjomba wako sawa’’ aliongea yule na kuondoka.Wakati anaondoka ulitokea upepo kidogo na pasipo kutarajia yule mtu aliingia katika korido moja  na ghafla kulikua kimya katika eneo lile.



    ‘’Mmmh,mbona kama mimi sielewi?,hivi usalama upo humu ndani kweli? Haya mambo vipi?’’



    aljiuliza Faluu na baadaye aliona apike kama jinsi alivyopata maelekezo kutoka kwa mwenyeji wake.

    Baada ya hapo,Faluu alianza kupika ile nyama huku akiitafakari sana na wakati huo alikua na njaa sana kutokana na safari na pia likua hajaweka kitu chochote katika tumbo lake,hivyo masaa yalizidi kusonga.Ilipofika saa 6 mchana,baada ya njaa kuzidi aliamua kupakua ile nyama bila kujali ni nyama gani ilikupoza njaa yake,alipotaka tu kuiweka mdomoni,aliisikia sauti ya mtu ikimueleza..



    ‘’Wewe hiyo nyama huwa hatuli kizembe hivyo,embu acha!’’Alishtuka na kuanguka chini na mara alipogeuka nyuma alimuona yule mtu aliyekua akimuelekeza …Jambo lile lilimstahajabisha sana.



    Baada ya hapo,Faluu alianza kupika ile nyama huku akiitafakari sana na wakati huo alikua na njaa sana kutokana na safari na pia likua hajaweka kitu chochote katika tumbo lake,hivyo masaa yalizidi kusonga.Ilipofika saa 6 mchana,baada ya njaa kuzidi aliamua kupakua ile nyama bila kujali ni nyama gani ilikupoza njaa yake,alipotaka tu kuiweka mdomoni,aliisikia sauti ya mtu ikimueleza..



    ‘’Wewe hiyo nyama huwa hatuli kizembe hivyo,embu acha!’’Alishtuka na kuanguka chini na mara alipogeuka nyuma alimuona yule mtu aliyekua akimuelekeza …Jambo lile lilimstahajabisha sana.



    ‘’Kwani wewe ulikua wapi?’’Faluu alimuuliza



    ‘’Acha maswali yako ya kejeli,kwani wewe haukuniona?mbona nilikua hapa hapa’’Yule mtu aliongea huku akicheka.Swala lile lilimpa shida sana



    ‘’Ulikua hapa hapa ?kwani mimi ningekuona ningekuuliza?’’aliongea Faluu.



    ‘’Basi ndio hivyo’’alijibu yule mtu..



    Wakati wakijibishana alitokea mjomba wake Faluu (Kachali)..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Vipi mbona mnabishana?kulikoni?’’ aliuliza Mjomba.



    ‘’Aaah,hamna mjomba tunaongea tu hapa’’ Faluu alijibu.



    ‘’Halafu mjomba mimi nahisi njaa sana,naoma nifanye utaratibu’’aliongea Faluu



    (Mjomba alicheka sana)



    ‘’Hahahahah,mjomba hapa sisi huwatunakula maramoja tu tena usiku,kwa hiyo subiri sawa’’mjomba alijibu.Majiu yale yalimshtua sana Faluu..



    ‘’Nisubiri hadi usiku?sawa’’alijiongelea Faluu na baadae alitulia tuli.Masaa yalizidi kusonga ilipofika saa mbili usiku walianza kuandaa chakula na kupeleka katika chumba kimoja kilichokua ndani ya hiyo nyumba,jambo lile lilimfanya Faluu azidi kujiuliza maswali juu ya mazingira halisi ya ile nyumba,



    ‘’Mjomba na hiki chumba vipi?’’aliuliza Faluu



    ‘’Humu ndani ndio tunakolia chakula’’alijibu Mjomba.



    ‘’Mbona giza sana?tunafanyaje’’aliongea Faluu..



    ‘’Hamna kukosawa tu  na mbona ndani kukosafi’’aliongea mjomba..Wakati Faluu akiwa nje alianza kusikia sauti za watu wakiongea ongea mule ndani,sauti zile zilimuogopesha sana na kumfanya kua na hofu,aliogopa sana na kujikuta akisita kuingia mule ndani…



    (Mjomba aligeuka nyuma na kumuangalia)



    ‘’Mbona unasita?embu ingia ndani’’ Aliongea Mjomba na baadae alirudi na kumshika mkono na kuingia ndani.Faluu aliishia kuguna tu na walipoingia ndani kulikua kimya tu na hakukua na mtu yoyote zaidi ya mjomba na yule mtu aliyekua akimuelekeza namna ya kupika ile nyama.



    Faluu alibaki kushangaa mazingira ya mule,kwa maana yalikua yametapakaa na michoro ya ajabu ajabu yenye kutisha ambayo ilimfaya Faluu ashindwe kuvumilia..



    ‘’Mjomba mbona kama mimi sielewi humu ndani kwa jinsi mlivyo? Embu naomba uniambie basi mjomba wangu’’ aliongea Faluu



    Kabla mjomba hajajibu kitu chochote juu ya swali alilouliza Faluu,yule mtu aliyekua karibu alisimama na kuongea..



    ‘’Sikia Faluu huu sio muda wakumuuliza mkuu maswali,embu leta chakula tule hapa hayo maswali baadae’’ aliongea huyo mtu huku akiwa ametoaa macho yake. Mambo yale yalizidi sana kumchanganya Faluu na baada ya mambo yale mjomba wake Faluu alicheka sana na kwa sauti ya kuunguruma aliongea..



    ‘’Embu nenda ukalete mara moja kama ulivyoelekezwa kule ‘’ aliongea mjomba, maneno yale yaliyokua yakiongelewa yalimfanya Faluu ashindwe cha kufanya maana hakujua wanachomaanisha…Ama kweli kila jambo na mtu wake



    ‘’Mbona mnanichanganya sasa eti mjomba na wewe baba,sikilizeni sasa!! Mimi siwaelewi kabisa ‘’ Aliongea Faluu kwa ujasiri mkubwa sana.



    Walibaki wakimtolea macho tu wasijue nini cha kumueleza Faluu kwa muda ule na wakati huo masaa yalizidi kusonga na ilipofika saa 7 usiku,ghafla Mjomba alianza kucheka kwa sauti tofauti tofauti za kutisha sana,ambazo zilimfanya Faluu kuanza kua muoga na muda muda huohuo kulitokea upepo mkali sana mle na alipogeuka nyuma  hakumuona yule mtu mwingine,alijikuta mwili mzima ukitetemeka na kujikuta akishindwa kuongea,ndipo alipojivuta mpaka pale alipokuwepo mjomba wake akiwa anatembelea magoti maana hakuwa na nguvu za kutembea kutokana na miguu yake kuishiwa nguvu.Alimshika bega mjomba wake na mara mjomba alipogeuka doooh!! Sura yake yote ilikua imejaa vidonda hali ile ilimshtua na kujikuta akipata nguvu na kusimama  na kukimbilia mlangoni na alipofika mlangoni kufungua mlango ili atoke nje,mlango haukufunguka ndipo akajikuta akiongea maneno haya kwa ghadhabu..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Sasa mambo gani haya,mbona unafanya vitu kama mtoto mdogo mjomba wangu?’’aliongea Faluu na hakuna mtu yeyote aliyemjibu na muda mfupi baadae alianza kuona watu waajabu wakitokea katika pembe za kile chumba…



    Baada ya Faluu kuona vitu vile alianza kurudi nyuma na ghafla alijikuta akimgonga mjomba wake,alipogeuka na kumuona alikutana na kundi kubwa sana la watu wenye maumbile na sura tofauti tofauti,nguvu zilimuisha na pale pale alipoteza fahamu.



    ‘’Hii nyama tena bado laini kabisa’’aliongea kiumbe mmoja.



    (Mjomba wake alishtuka kusikia vile)



    ‘’Hapana huyu mwanangu sikumleta huku kwaajili ya kazi hiyo’’ aliongea mjomba wake Faluu



    ‘’Unamsaidia sio” waliongea wale viumbe huku wakionekana kukasirika



    ‘’Hapana mimi simsaidii,lakini mnasahau kama nyie ndiyo mlio muua mama yake ?huyu pwa wangu nimemleta kwaajili ya kazi nyingine kabisa tulieni’’aliongea Mjomba wake Faluu na kwa vile ndiye aliyekua kiongozi wote walimsikiliza na baada ya pale walikula zile nyama na ilipofika saa 11 alfajiri walipotea katika mazingira yale.



    Faluu alikaa muda mrefu sana akiwa amepoteza fahamu,hasa ni kutokana na njaa iliyosababishwa na kukaa muda mrefu bila kula.Ilipofika saa 4 asubuhi  Faluu alishtuka na alijikuta akiwa katika kile chumba ,Moyo wake ulizidi kuingiwa na hofu bila kujua hatima ya matatizo yake.



    ‘’Mungu wangu haya yanayotokea kwenye maisha yangu ni kitu gani?mbona mimi sielewi jamani? Et Mungu nijibu basi” Faluu alikua akijiongelea.



      Alikua akijiongelea huku machozi yakimtoka na wakati mgumu sana Katika kipindi hicho,baada ya muda wa dakika kadhaa alikuja mjomba wake huku akiwa anatabasamu..



    ‘’Aaaah, mjomba umeamka,daah pole sana’’ aliongea mjomba wake.Wakati mjomba akiongea Faluu alikua akimtazama huku sura yake ikionekana kua na hasira sana..



    ‘’Samahani mjomba,hivi unaweza kuniruhusu nikuulize swali?’’ Faluu aliongea



    ‘’Hahahah,usiogope mpwa wangu wewe uliza tu’’ Mjomba alijibu huku akiwa anacheka.Kicheko cha mjomba kilimpa hasira sana Faluu,maana alijiona kama mjomba anamdharau,ila kwake aliona muda ule siyo sahihi kuonesha anachofikiria.



    ‘’Hivi mjomba maana halisi ya wewe kuniambia niingie mule ndani nini hasa na mbona unanifanyia mambo ya ajabu? Na wale watu waajabu walikua akina nani?’’Faluu aliuliza maswali huku akionekana kua na mambo mengi sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati mjomba akitaka kumjibu ghafla alitokea yule mtu ambaye jana alikua anamuelekeza kupika na kutengeneza ile nyama,Faluu alishtuka sana na kujikuta akijiuliza maswali mengi sana katika ufahamu wake..



    ‘’Hivi huyu mtu ni nani? Na ,mbona ninapokua naongea na mjomba wangu na kumuuliza maswali anapotaka tu kunijibu anatokea na kunuiletea ubabe,ngoja nimuone atakachoniambia leo’’ Faluu alikua akifikiria.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog