Search This Blog

VITA VYA MAPENZI - 1

 





    IMEANDIKWA NA : MAUNDU MWINGIZI



    *********************************************************************************



    Simulizi : Vita Vya Mapenzi

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kelele za Shangwe na mbinja vilisikika kutoka kwa makondakta na wapiga debe kadhaa waliokuwa nje ya lango la kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar Es Salaam, wote wakimshangilia dereva wa basi la NBC Classic kwa umahiri wake na utundu alioutumia mpaka kuwa wa kwanza kutoa gari kabla ya madereva wengine wote kwa asubuhi ile.

    Kutokana na wingi wa mabasi katika Stendi ile, yote yakiwania nafasi ya kuwahi kutoka ilihitaji dereva hodari na mweledi ili kuwapiku wenziwe, na hicho ndicho alichokifanya dereva yule mwenye ndevu nyingi mashavuni. Sasa kwa nini asipongezwe?

    Abiria wake nao walikuwa wakimpa heko kimyakimya.

    Safari hii ilikuwa inaelekea mikoa ya Morogoro, Dodoma, na hatimaye Tabora ambako ndipo hasa alipokuwa akielekea kijana mmoja mrefu wa wastani, maji ya kunde, na mwenye mwili wa wastani aliyekuwa ameketi mwanzoni kabisa ‘Seat No. 10’.

    Sura ya kijana yule haihitaji ‘Degree’ hata moja ya saikolojia kutambua kuwa alikuwa na furaha kubwa moyoni. Japokuwa abiria wengi walionekana kuwa na nyuso zenye bashasha hasa baada ya dereva kuzikonga nyoyo zao kwa kuwahi kulitoa basi mapema na kuianza safari, lakini kwa kijana huyu palikuwa na vingi vilivyomfanya mara kwa mara aachie tabasamu bila kuhofia kutazamwa na abiria wenzie. Mbali ya kuwa alikuwa amefanya vizuri sana katika masomo yake aliyohitimu katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam lakini pia alikuwa na hamu ya kwenda kuonana na wazazi wake, nduguze na marafiki ambao kwa muda mrefu sana hakuwa ameonana nao. Lakini kubwa zaidi lilikuwa ni Sharifa. Mwanamke aliyempenda kwa dhati, aliyewekeana nae ahadi ya kufunga pingu za maisha na wazazi nao wakaridhia.

    Hakika safari ilikuwa na maana kubwa sana kwa kijana huyu.

    Wakati mawazo yakiendelea kutalii kichwani mwa kijana huyu, mara kwa mara alikuwa akikatizwa na mzee mmoja mwenye asili ya ki-asia ambaye alikuwa akimuangalia sana mpaka kijana akawa anaingiwa hofu. Si kwamba mzee huyu alikuwa akimfananisha bali macho ya yule mzee yalionesha kitu cha ziada ambacho kiliifanya ile hofu ya yule kijana ifunikwe na hamu ya kutaka kukijua kitu hicho. Mara kadhaa kijana alijaribu kumkazia macho yule mzee aliyekuwa ameketi jirani yake kabisa katika ‘Seat No11’, lakini kila walipokutanisha macho, mzee yule alijibaraguza na kuangalia pembeni kana kwamba hakuwa akimuangalia tangu mwanzo. Kijana alipoona kero ya kuangaliwa kama sanamu inamzidia akaingiza mkono katika kijibegi chake kidogo cha rangi nyeusi alichokuwa amekipakata miguuni kwake, akatoa miwani myeusi na kuibandika usoni ili asiendelee kupata bughudha ya kuangaliana na mzee yule. Hakuishia hapo. Akatoa ‘Ipad’ yake akaiunganisha na waya maalumu wa visikilizio na kuvipachika masikioni visikilizio vile na kuanza kupata muziki uliombembeleza na hatimaye kumsahaulisha habari za mzee yule.

    Safari iliendelea kwa raha mustarehe, kila mmoja akifanya yake. Wapo waliokuwa wakiangalia TV maalum iliyofungwa ndani ya basi hilo, wapo waliokuwa wakisoma vitabu na magazeti, na wengine wakiwa wanauchapa usingizi tu. Hakika kila abiria alikuwa hana wasiwasi na safari yake. Dereva alionekana kuijua vyema kazi yake maana si tu mbwembwe za kutoa gari pale getini Ubungo bali hata barabarani aliyajua vizuri majukumu yake, ndani ya masaa kadhaa gari lilikuwa likiiacha morogoro, matairi yake yakizunguka kwa kasi huku yakiendelea kusuguana na lami. Wakati safari ikiendelea namna ile, kijana wa kiti namba kumi alijisahau kabisa kuwa alikuwa safarini pamoja na jumuiya ya wasafiri wengine, akili yake ikiwa imechotwa kabisa na muziki aliokuwa akiusikiliza kutoka kwenye iPad yake, na akiwa katikati ya dunia yake ile ya pekee akitumbuizwa na muziki mororo huku akiwa amaefumba macho kwa raha zilizomzonga, alishtushwa na mkono laini uliomshika huku ukimtikisa bega lake la kulia. Alikurupuka kutoka kwenye ulimwengu ule wa raha na kutumbia macho, akikutana macho kwa macho na mwanadada mnyange akiwa amemchanulia tabasamu la kumcheka. Baada ya kujipikicha macho na kujikumbusha kuwa pale alikuwa ndani ya basi, aliweza kumtambua kuwa yule dada alikuwa ni mhudumu wa ndani ya lile basi kutokana na sare maalum alizokuwa amevalia, lakini kilichomshangaza ni kitendo cha baadhi ya abiria waliokuwa jirani yake kuwa wakicheka huku wakimuangalia yeye. Alibaki akijiuliza ni lipi alilolifanya ambalo liliwafurahisha namna ile lakini hakupata jibu. Aligonganisha tena macho na yule mzee wa ki-asia, na kuona kuwa yule mzee alikuwa akiendelea kumuangalia tu. Hacheki wala hanuni, jambo ambalo lilizidi kumtisha. Alimgeukia tena yule mhudumu wa basi na kuonaakiinama na kusogeza kreti la soda, ndipo alipojua kuwa ulikuwa ni muda wa kupata vinywaji.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unatumia soda gani Pharell?” Msichana alimuuliza huku bado akiwa anatabasamu, na kijana alishtuka kusikia anatajwa kwa jina lisilo lake, lakini haraka akakumbuka kuwa kabla hajapitiwa na usingizi alikuwa akisikiliza wimbo wa Pharrell William, msanii kutoka marekani hivyo akatambua kuwa kwa kuwa ‘Earphone’ zake zilikuwa masikioni muda wote huku sauti ikiwa juu sana bila shaka alikuwa akiimba kwa sauti ya juu kwa kuufuatisha wimbo ule, ndio maana alionekana kituko kwa abiria wenzie.

    Oh, shiit!

    Haraka akachomoa vile visikilizio kutoka masikioni na kumjibu yule mhudumu kwa tahayari kidogo.

    “Eeem, Nipatie Fanta,tafadhali.”

    “Fanta gani?”

    “Fanta ukwaju,”

    Jibu hilo liliwafanya abiria wenzake waangue vicheko kwa mara nyingine tena huku wakimuangalia kwa uelewa mpya yule kijana , kwani pale kila mmoja akawa ameshaelewa kuwa kijana alikuwa mtundu sana.

    “Mnh jamani kuna fanta ya ukwaju kweli duniani?”

    “Basi kama hakuna nifungulie yoyote ile uipendayo wewe dada’angu” Mhudumu akamchagulia Fanta Orange na kumkabidhi huku akiunganisha na tabasamu pana. Wakati mhudumu anaifungua soda ile ndipo kijana aliposhtushwa na sauti ya yule mzee wa ki-asia, ambaye naye sasa alikuwa akitabasamu.“Suhail we’ ni mtundu sana, halafu leo unaonekana una furaha sana eeh?”

    Heh!

    Kijana alishangaa upeo wa kushangaa. Lile swali lilimuacha hoi, kwani kwa hakika alikuwa anaitwa Suhail.

    Mnh, mzee! Um…umejuaje kama nina furaha…? Na jina langu…umelijuaje mzee?”

    “Nimekusikia ukiimba muda mrefu tena kwa sauti ukisema ‘Because am happy’,” Mzee alimjibu huku akizidi kutabasamu na kumfanya Suhail sasa athibitishe mawazo yake kuwa ni kweli alikuwa akiuimba kwa sauti ule wimbo wa Pharrel William,‘Happy’. Lakini pia akaona kuwa yule mzee hakumjibu swali lake la pili.

    “Duh, okay…na jina langu? Umelijuaje?” Akakumbushia. Mzee akazidisha upana wa tabasamu lake tulivu, kisha akampigapiga begani Suhail kwa namna ya kumpoza au kumuondoa hofu.

    “Manta khouf’ ‘young man’,” Alimwambia kwa upole, akimaanisha kuwa “usiwe na hofu kijana”, kisha hapo hapo sura yake ikabadilika mithili ya mtu aliona au aliyekumbuka kitu kibaya sana. Mzee akakunja uso na kubaki akiangalia mbele kwa dereva, akimuacha Suhail akiwa amepigwa butwaa.

    Safari iliaendelea kushika kasi, lakini hofu iliyokwisha ingia moyoni mwake, ilikuwa imeshika kasi zaidi. Soda haikunyweka tena, wakati mtungo wa maswali yasiyo na majibu ukijirefusha kichwani mwake.

    Huyu mzee ni nani?

    Amenijuaje mimi?

    Mbona sina kumbukumbuku ya kupata kumuona popote pale duniani?

    Na kwa nini tangu mwanzo wa safari ananiangalia sana? Na kikubwa zaidi, kwa nini baada ya kuongea name maneno machache tu akaebadilika ghafla kama aliyeona kitu kibaya?’

    Maswali yalizidi kumtesa Suhail. Alitamani amhoji zaidi yule mzee lakini sura mpya ya mzee ilimhakikishia kuwa asingejibiwa hata swali moja. Mzee hakuwa na mpango naye tena, na badala yake alionekana kumakinika na kitu ambacho Suhail hakukiona wala kukijua..

    Taratibu Suhail akaiweka vema usoni miwani yake na kujilaza kitini. Muda mfupi baadaye, akapitiwa na usingizi mzito.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Walipokuwa wanakaribia kuingia Dodoma, wakiwa katika mapori ya mwisho mwisho kabisa ambako hapakuwa hata na dalili ya makazi ya watu, kwenye kona ya mlima Kisera likatokea Lori kubwa likiwa na shehena ya magogo makubwa likija kwa kasi ya ajabu. Licha ya dereva wa Lori hilo kuliona lile basi aliendelea kuendesha kwa kasi ileile, na dereva wa basi akafanya jitihada ya kupeleka gari lake pembeni lakini Lori likamshinda nguvu derava na kupamiana uso kwa uso na basi lile.

    Ilikuwa ni ajali mbaya kupata kutokea. Basi lilisambazwa vibaya na kupinduliwa hovyohovyo huku baadhi ya magogo yaliyochomoka kwenye lile Lori yakilifuata kwa juu na kuzidi kulipondaponda. Lile Lori lilianguka na kupindukia kwenye mashamba ya mahindi yaliyokuwa kando ya barabara, japo mashamba yale yalikuwa hayajalimwa kwa muda mrefu sana.

    Suhail alishituka kutoka usingizini wakati ajali ikitokea na hakujua kilichotokea mara moja, ila baada ya muda mfupi akaelewa kuwa walikuwa wamepatwa na ajali. Tena ajali mbaya kabisa. Alijiona akiwa ametapakaa damu mwilini mwake, japo hakujua damu ile ilikuwa ikimtoka sehemu gani. Alijaribu kujikaza na kujiinua, lakini alihisi kuishiwa nguvu. Sauti za vilio vya maumivu na hamaniko za watoto, akina mama na hata za akina baba zilitawala ndani ya basi lile. Aliona miili ya baadhi ya abiria wenzake ikiwa tayari imeshaachana na roho zao, ikiwa imezagaa hovyo ndani ya basi lile. Wahka ukamshika. Woga ukamgubika.Alijikakamua na kujilazimisha kuinuka kiubavu-ubavu, akaketi.Na ndipo alipoweza kuona vizuri matokeo ya ajali ile. Hakika ilikuwa ni ajali kubwa na ya kutisha sana.

    Baada ya muda mfupi wa taharuki ile abiria wachache walionusurika wakawa wameshainuka na kutoka nje ya basi huku wakisaidiana kuwatoa majeruhi wenzao na kupeanaa huduma ya kwanza kwa kadiri walivyoweza katika mazingira yake.

    Kwa shida Suhaili akajilazimisha kuinuka ili atoke nje ya basi ajiangalie hali yake na ikibidi aungane na abiria wenzake kwenye kutoa msaada kwa wenzao, na katika kufanya hivyo ghafla macho yake yakaangukia kwayule mhudumu aliyekuwa akisambaza vinywaji ndani ya basi akiwa amelalachali, chuma kikiwa kimemtumbua vibaya tumboni, macho yakiwa yamemkodoka bila kuona. Alikuwa amepoteza maisha. Suhail akafuta machozi yaliyoanza kumtoka bila ya kutaka, akageuza uso wake upande mwingine kuikwepa taswira ile.

    Hamaadi!

    Akakutana macho kwa macho na yule mzee wa ki-asia aliyekuwa akimuangalia sana hapo awali, akiwa amelala juu ya dimbwi la damu, akionekana kuwa hai lakini hoi bin taabani. Alimsogelea haraka na kujaribu kumuinua ili amkokotee nje, lakini yule mzee akakataa, akawa anamtazama Suhail si kwa jicho lile la mwanzo kabla ya ajali bali sasa kwa jicho la kukata tamaa.

    “Wacha…nikus…saidie mzee wangu! Ajali hii!” Suhail alimwambia kwa taabu.

    “Amaa kweli aheri ya mrama kuliko kuzama!” Aliongea kwa taabu sana yule mzee , na Suhail akamshangaa.

    “Unamaanisha nini mzee?”

    “Bora chombo kiende mrama lakini kifike salama, kuliko kiende salama halafu kikaishia kuzama!” Mzee alimjibu kwa taabu. Maneno yale yalimuacha hoi Suhail.

    “Bado sijakuelewa mzee…hebu tutoke nje ya hili basi kwanza…linaweza kushika moto hapa!”

    “Tulimsifia sana dereva wetu kuwa ni bingwa, basi likaenda vema, tukajiona tumekabidhi roho zetu sehemu salama, kumbe haikuwa! Tukamsahau mpaka Mola wetu…na sasa tumeishia kuzama tu mwanangu…mi ndio basi tena!” Mzee alizidi kuongea kwa taabu kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyapata. Alionekana wazi kuwa amepoteza tamaa ya kupona.

    “Mzee lakini hayo sio muda wake huu! Nadhani tungeangalia hali yako kwanza kwa sasa!” Suhail alimsisitiza.

    “Wala usihangaike mwanangu, utapoteza muda bure. Afya yangu si muhimu tena, ninakufa tu mimi. Nimeumizwa sana, na nilijua tu kuwa leo ni lazima watanimalizia kwenye ajali hii. Hata wewe pia nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kukukinga, bila ya hivyo nawe ungekuwa maiti saa nyingi tu.”

    Nini??

    Sura ikambadilika Suhail. Alimtazama yule mzee mwenye wingi wa kauli tata, kama anayemtazama jini.i

    “Mzee kwa nini unasema hivyo? We’ ni nani kwani? Ulijuaje kama leo itatokea ajali hii? Na ni akina nani hao hasa wanaotaka kukumaliza?” Alimvurumishia maswali kwa wahka mkubwa.

    Badala ya kumjibu yule mzee aliliachia tabasamu la dhaifu, la huzuni, la kukata tama. Tabasamu la kumuonesha Suhail kuwa alikuwa hajui chochote kinachoendelea. Walibaki wakitazamana kwa takriban dakika mbili hivi, kisha yule mzee akashtuka na kukaza macho kuelekea chini, upande wa pili wa viti alivyokuwa amelalia baada kutupwa tupwa huku na kule wakati wa ajali, kisha akawa anamuonesha Suhail kwa kidole chake usawa wa kule alipokuwa anatazama., Haraka Suhail akapeleka macho kule alipokuwa anaelekezwa. Hapakuwa na kitu chochote zaidi ya mifuko na mabegi yaliyosambaa hovyo kutokana na kuanguka kwa lile basi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Lete hilo begi kubwa jekundu…ni la kwangu usiogope.” Mzee alimtuma, na Suhail akashangaa kuona badala ya kujali afya na usalama wake kwanza, mzee alikuwa anataka begi, lakini hakubisha kijana wa watu. Akajikongoja mpaka lilipokuwa lile begi lile na kumsogezea kwa shida yule mzee., Mzee akainuka kwa tabu sana, kisha akafungua zipu kubwa ya katikati kwenye begi lile, na ndipo Suhail alipopigwa na butwaa, huku akishindwa kuamini iwapo alichokuwa akikiona ndani ya begi lile kilikuwa ni chenyewe, ama anaota. Akili yake ilijaribu kufanya kazi mara kumi kidogo, lakini bado hakupata jibu la kile alichokuwa akikiona..

    Mzee aliliona hamaniko la Suhail lakini hakujali. Bila shaka alijua tu kuwa kijana angeshtuka, kwani lile begi jekundu lilikuwa limesheni pesa mpaka juu, tena zikiwa ni dola mia-mia tu za kimarekani.

    Lah!

    “Usichanganyikiwe kijana. Mimi nakufa, hilo halina pingamizi,ila nimekutunuku.Pesa zote hizi nakupa wewe na mali zingine ambazo utazijua muda ukifika.”

    Ama!

    Baada ya maneno hayo mafupi, ambayo kwa hakika Suhail alikuwa kama kwamba anayasikia kutokea mbali sana na pale walipokuwa, mzee akavua pete yake kubwa yenye kito cha rangi ya njano aliyokuwa ameivaa kwenye kidole chake cha kati na kumshika mkono Suhail, akamvisha ile pete.

    Eh!

    Suhail akajihisi akiingiwa ganzi mwili mzima. Haya mambo yalikuwa mazito sana kwake kuyabeba.

    “Ah, sasa…hii pete nayo ni ya nini, mzee?”

    “Hiyo pete inaitwa ‘khatam budha’.Itakufaa sana maishani… itakulinda na kukuongoza. Hiyo ni silaha na siri ya mali zote hizi unazoanza kuzimiliki sasa. Sina muda mrefu sana wa kuendelea kuishi hapa duniani kijana, hivyo nisikilize kwa makini sana...” Mzee aliongea kwa taabu, kisha akabaki akitweta. Halafu akashusha pumzi nzito, akameza funda kubwa la mate, na kabla hajaendelea akajaribu kuchungulia nje ya basi ambako tayari wasamaria wema walishaanza kuwasili eneo la tukio. Alipofuata uelekeo wa macho ya yule mzee, Suhail akaona kuwa baadhi ya waandishi wa habari pia walikuwa wamefika, wakionekana kuwahoji abiria walionusurika kule nje.Sasa mle ndani ya basi watu hai walibaki wao wawili tu, baada ya wenzao kutolewa nje.

    “…Pesa zote hizo nakupa wewe, ni za kwako... lakini kwa sharti moja tu, ambalo si gumu sana. Unapaswa umuoe binti yangu na uishi naye kwa wema, amani na upendo. Ukawe mlinzi na kiongozi wake…Sitaki kamwe mwanagu aolewe na majini!”

    Heeeh!

    “Majini...?” Suhail alimaka kwa mshangao, na kabla hajajibiwa akaendelea,“ ...ki…kivipi mzee? Mbona sikuelewi? Kwani wewe ni nani hasa?”

    “Mimi naitwa Mzee Shamhurish.Fanya hima umpate mwanangu!, Anaishi Bagamoyo…anaitwa Shekhia!”

    “Whaat? Nani?” Swali la hamaki kutoka kwa Suhail ni kama lilihitimisha safari ya mwisho ya Mzee Shamhurish duniani, mikono ya yule mzee ilianguka, macho yakajifumba nusu, pumzi zikakata, roho yake ikatengana na mwili.

    “Nooo! Hupaswi kufa kwa sasa mzee! Amka! Amka, please unijibu japo kidogo tu aaaah! Nnoo!” Suhail alikuwa anauongelesha mwili wa Mzee Shamhurish kama mwendawazimu huku akimwagikwa machozi bila kujijua., Kilichomshtua kuliko vyote ni jina la Shekhia, jina ambalo alilijua na alimjua vema huyo msichana aliyeitwa Shekhia S. Sufian. Ni msichana mrembo aliyekutana naye huko chuoni alipokuwa anasoma. Wakafahamiana na kuwa marafiki. Mengi yakapitikana baina yao, na wakaishia kuwa maadui wakubwa.

    Suhail alizidi kupagawa. Hakuwa na hamu tena na zile pesa alizokabidhiwa, na alipoiangalia ile pete ndiyo hofu ilipozidi kumvaa.

    “Ni kweli Shekhia alipata kuniambia kuwa kwao ni Bagamoyo. Je ndiye yeye aliyekusudiwa na mzee huyu? Kama ndiye basi NIMEKWISHA!”



    *****



    Wakati ajali hiyo iliyowaangamaza abiria wengi ikitokea, upande wa Pili huko Tabora Mchumba wake na Suhail aitwae Sharifa alikuwa akiendelea na usafi wa nyumba huku mama yake akiwa jikoni akiungurumisha chakula, Sharifa alikuwa ni msichana mchapakazi sana licha ya kua ameajiriwa lakini siku za jumamosi na jumapili badala ya kupumzika tu yeye hupendelea kujishughulisha na majukumu ya pale nyumbani ili kuwasaidia wazazi wake hasa mama yake, lakini pia siku hiyo alikuwa na hamu kubwa na hamasa ya kufanya shughuli zote za nyumbani kutokana na furaha kubwa ya kumpokea mchumba wake ambaye hajaonana nae yapata mwaka mmoja tangu alipokwenda Dar kumtembelea, kama ungempasua Sharifa katikati ya moyo wake basi si ajabu ungekuta jina la Suhail limeandikwa kwa wino wa dhahabu kwa jinsi alivyompenda, aliona kama masaa hayaendi vile, alitamani muda ufike haraka akampokee kipenzi cha moyo wake..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    .kama ungempasua Sharifa katikati ya moyo wake basi si ajabu ungekuta jina la Suhail limeandikwa kwa wino wa dhahabu kwa jinsi alivyompenda, aliona kama masaa hayaendi vile, alitamani muda ufike haraka akampokee kipenzi cha moyo wake..

    Wakati Sharifa akiwa anaendelea kufagiafagia ‘seating room’ pale nyumbani kwao ndipo ghafla ladha ya furaha iliyotanabahi ndani ya moyo wake ilipogeuka shubiri baada ya kutupa macho katika kioo cha televisheni iliyokua ikiripoti tukio la ajali mbaya inayohusisha Lori na Basi la Nbs alilokua amepanda mchumba wake. Aliisogelea kwa kasi Tv kama vile alievutwa na sumaku, kisha macho na masiko yake vikashirikiana kupata habari ile mbaya

    “…AJALI HIYO MBAYA INAYOHUSISHA LORI LILILOKUA LIMEBEBA MAGOGO NA BASI LA NBS CLASSIC LILILOKUA NA ABIRIA YAMEGONGANA USO KWA USO KATIKA KONA YA MLIMA KISERA NJE KIDOGO YA MJI WA DODOMA NA KUSABABISHA VIFO VINGI NA MAJERUHI, UOKOZI UNAENDELEA ENEO HILO BAADA YA WASAMARIA WEMA KUWASILI…” Wakati taarifa hiyo ikiendelea kusomwa Macho ya Sharifa yalikuwa yakiwaangalia baadhi ya majeruhi waliokuwa wakihojiwa lakini hakupata kumuona Suhail, alituliza macho yake katika kioo cha luninga yao lakini hakumuona kamwe ndipo uzalendo ukamshinda ukaangua kilio cha hali ya juu, ndipo sauti yake ikavuma mpaka jikoni alipokuwa ameketi mama yake, masikini ya Mungu Bi mkubwa Yule akautupa mwiko wa mboga na kutoka mbio kuelekea kule sebuleni ilipokua ikitokea sauti ya Sharifa, Hakika Mama huyu alimpenda sana binti yake, alimpenda kama binti yake wa kumzaa mwenyewe mpaka majirani wote walikuwa wakijua kua ni mwanae wa kuzaana pia humuita ‘Mama Sharifa’, lakini ukweli wa mambo ni kwamba Sharifa hakuwa mtoto wa kuzaliwa na Bi mkubwa Yule kwani Wakati mama huyu naolewa na Mzee Fungameza alimkuta Sharifa akiwa ameshazaliwa japo alikuwa ni mdogo sana, mtoto wa miaka kama minne tu hivi hivyo akamlea mwenyewe tangu hapo mpaka nae akajaaliwa kupata mtoto wake aitwae Florida, Malezi hayakua magumu kwa Bi mkubwa huyu dhidi ya Sharifa isipokua sehemu moja tu, Sharifa tangu akiwa na umri huo mdogo aling’ang’ania kufuata dini ya mama yake mzazi ambaye alikuwa ni muislamu, japokuwa mama yake huyo alitoweka katika mazingira anayoyajua Mzee Fungameza peke yake, hivyo japo Mzee Fungameza alikuwa ni Mkristo tena ni mzee wa kanisa alijikuta akilazimika kumuacha mtoto huyo afuate dini ya mama yake.

    Baada ya mama Sharifa kuwasili sebuleni pale alikuta taarifa ile kwenye Tv ikimalizikia wakati huo Sharifa akigaagaa kwa kilio pale sakafuni

    “We mtoto una nini lakini?”

    “Mamaa! Mamaa! Uwiiii Suhail jamani mama,” Sharifa alikuwa akilia kwa kuomboleza kiasi cha kumtia hofu zaidi mama yake

    “Suhail amefanyaje sasa?”

    “Amepata ajali na itakua amekufa tu” Sharifa alikuwa akilia kwa uchungu sana. Wakati huo mama yake nae alikuwa kama amepigwa ‘shoti’ ya umeme kusikia habari hizo maana nae alikuwa akijua kua Suhail yuko safarani akielekea huko Tabora na hapakuwa na siri yoyote kua watoto wao walikuwa ni wachumba

    “We nani amekuambia habari hizi?” Sharifa hakumjibu mama yake bali alimuashiria kwa kidole chake kua ameona kwenye Tv, haraka mama Yule akaiangalia Tv ambayo ilikuwa ikionesha kipindi cha maisha ya wanyama, Alikwishai chelewa habari ile, akajaribu kushika ‘remote’ na kubadili ‘channel’ kadhaa kama angeweza kuiona habari hiyo lakini haikuwa hivyo ikabidi tu sasa mama Yule ajikaze ili apate nguvu ya kumbembeleza binti yake

    “Sikia mwanangu wewe ni msichana msomi na muelewa sana sasa kwanini unapenda kuongozwa na hisia? Wakati mwingine hisia hua si uhalisia wa jambo, huwezijua mwenzio yupo katika hali gani kwa sasa, cha msingi ni kuzidi kumuomba bawana Mungu wetu amuokoe”

    “Lakini mama Maiti ni nyingi sana na majeruhi ni wachache lakini Suhail hayumo kabisa katika majeruhi hao waliokuwa wakihojiwa, itakua amefariki tu mama,” Sharifa alijibu huku akiendelea kulia kwa uchungu

    “Hebu nyamaza kwanza ili tuelewanae, kutokuhojiwa kwake haimaanishi ndio amekufa na inawezekana waliohojiwa si wote na ndio maana hata katika maiti zilizooneshwa yeye hujamuona, lakini Je umeshampigia simu kujua kama atapokea au Laa?” Sharifa hakujibu swali la mama yake harakaharaka akaikimbilia simu yake iliyokua juu ya meza ndogo ya kunyooshea nguo, akaichukua na haraka akaipiga namba ya Suhail lakini simu iliita bila kupokelewa, alijaribu kupiga takribani mara tatu lakini simu iliita tu huku majibu yakiwa ni yaleyale, sasa hofu ndio ikazidi kupiga kambi moyoni mwake. Ikabidi sasa mama Sharifa nae achukue simu yake ili ampigie mumewe Mzee Fungameza ampashe habari hizo.

    Simu ya Mzee Fungameza iliita kwa muda mrefu sana na hatimaye mwishoni ndipo akapokea

    “Hallow.”

    “Baba Sharifa uko wapi?,” aliuliza mama sharifa bila hata ya kusalimia

    “Niko njiani naelekea kwa Bwana Kusekwa nina shida nae kidogo, vipi kwani?” Mzee Fungameza hakutaka kumueleza mkewe kua anaenda kwa Mzee Kusekwa kufuatilia habari za ajali hiyo ambazo tayari zimeshazagaa maeneo kadhaa ya mji, na imetapakaa habari kua Suhail amefariki katika ajali hiyo, alichelea kumueleza mkewe akihofia habari kumfikia Binti yake kwa wakati huo

    “Una shida nae gani au ndo hiyo habari ya ajali?” Swali hilo likazidi kummaliza nguvu mzee Fungameza akajua sasa mambo yako wazi, akakaa kimya kama sekunde kadhaa kisha akajibu

    “Ndio, lakini alaala jitahidi sana Sharifa asijue habari hizi kwa sasa, ni hatari”

    “Ajue mara ngapi?”

    “Khaa Kwanini umemuambia wewe??”

    “Yeye ndo kaniambia mimi”

    “Afanaaleki..hii sasa hatari..” Kikapita kimya cha muda mfupi kisha Mzee Fungameza akaendelea “..Nitakupigia baadae” kisha akakata simu



    *****

    Mtaa wa Rufita mkoani Tabora Nje ya nyumba ya Mzee Kusekwa ambaye ni baba yake mzazi na Suhail walikuwa wamejumuika majirani wawili watatu kwa ajili ya kumfariji jirani yao kutokana na habari hizo za ajali, ndipo punde Mzee Fungameza nae akawasili nyumbani hapo akiwa na Pikipiki yake ndogo, na baada ya kuipaki pembeni chini ya Mwembe ulio pembezoni mwa nyumba ya mzee kesekwa akaanza kujongea eneo walilokua wameketi akina Mzee Kusekwa na jirani zake

    “Karibu bwana Fungameza..”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ahsante sana, habarini za hapa” Wakaitikia salamu wote kwa pamoja huku wakimkaribisha, baada ya kuketi hapakuwa na mazungumzo mengine zaidi ya Mzee Fungameza kuufungua mjadala

    “Poleni na hekaheka jamani”

    “Aah hatujapoa bwana mkubwa”

    “Mimi nilikuwa huko maeneo ya Gongoni kwa bwana Kondela ndipo niliposikia habari hizi za ajali, na kwakua tayari nilikuwa nafahamu kua kijana nae alikuwa anakuja leo na basi ikabidi nifuatile ndipo nikaambiwa kua amepanda Basi hilohilo, aisee mwili wangu wote ukazizima kwa hofu”

    “Ndio hivyo bwana, ajali ni mbaya sana na waliotoka ni wachache lakini cha ajabu kila tukifuatilia hatupati habari za uhakika maana hata simu yake haipokelewi”

    “Mnh, kwahiyo mkipiga simu yake inaita tu?”

    “Ndio inaita tu bila majibu yoyote” Baada ya majibizano hayo mafupi kila mmoja alionekana kuzama katika tafakuri ya kina kisha Mzee Fungameza akaibuka tena

    “Hebu jaribu tena kumpigia inawezekana mazingira ya ajali yakawa yamembana sana hata ashindwe kujishughulisha na simu.” Kwa shingo upande Mzee Kusekwa akatoa simu yake na kuipiga tena namba ya Suhail, safari hii ikawa kama bahati hivi maana baada ya kuita kama mara tatu tu, kwani mara ya nne ikapokelewa, japo ni bora hata isingepokelewa tu maana hilo jibula mkato walilojibiwa liliwakata ‘maini’ kabisa

    “Hallow, jamani tunaomba msubiri kwanza tunaendelea na uokoaji hatuwezi kuelewana kwa sasa” Maneno hayo yaliweza kusikika na kila mmoja aliyekuwa pale maana Mzee Kusekwa alikuwa ameweka ‘loud speaker’ katika simu yake. Majibu hayo yaliwamaliza nguvu wote, kila mmoja akaamini kua sasa inawezekana Suhail ameshapoteza maisha ndo maana hata simu yake inapokelewa na mtu mwingine, wote waliangaliana, hofu ikazidi. Majibu kutoka katika Simu hiyo sasa yakapelekea kufunguliwa mjadala mpya

    “Mimi nashauri jamani tungeji pigapiga mifukoni ikiwezekana kesho Mzee Kusekwa na mtu mmoja waende huko Dodoma kuitambua miili..” alitoa rai Bwana Kituka, mmoja wa wale majirani waliokwenda kujumuika pamoja na Mzee Kusekwa, wazo lake likapita kwa asilimia zote na sasa ikabakia suala la pesa tu maana hali ya uchumi ya Mzee Kusekwa hakuna asieifahamu, ‘Dhooful-haal’

    “Jamani mimi nakwenda kwangu mara moja nitarejea baade ila mimi ninajitolea kwenda na bwana Kusekwa mpaka huko Dodoma,” Alisema Mzee Fungameza huku akiinuka kwa ajili ya kuondoka, akamshika mkono Mzee Kusekwa na kutoka nae faragha kama vile anaehitaji kusindikizwa, walipofika pembeni Mzee Fungameza akatoa pesa takribani Tsh laki moja akamkabidhi mzee Kusekwa

    “Hizi za nini Baba Sharifa?,” aliuliza Mzee Kusekwa

    “Najua tayari tatizo lipo mbele yetu hivyo haipendezi sana kuchangiwachangiwa pesa na majirani labda mpaka itakapo bidi sana, sasa hizo ni pesa za nauli utakata Tiketi mbili za Basi ili kesho tuianze safari japo nao kama watakuchangia itakua ni ziada.”

    “Nakushukuru sana Mzee mwenzangu, hakika umenifaa hasa, sina cha kukulipa ila Mungu anajua mbadala wa kukupatia”

    “Usijali bwana Fungameza, hili letu sote, sasa tutawasiliana baadae” Wakaagana wazee wale marafiki, Mzee Fungameza akaondoka huku Mzee Kusekwa akirejea kwa wezee wenzie akiwa ‘mzito’ mfukoni



    *****



    Baada ya Suhail kuhangaika huku na kule ndani ya Basi akijaribu kupingana na ukweli kwamba Mzee Shamhurishi ameshakata roho, ghafla alipatwa na ujasiri akalifunga vizuri begi jekundu lenye pesa akalivaa mgongoni kisha akachukua begi lake dogo jeusi akalibeba mkononi na kuanza kutoka nje ya Basi.



    Alipofika nje alikuta idadi ya watu ikizidi kuongezeka japo sio kubwa sana, wakati huo palikuwa na mitambo ya televisheni iliyofungwa huku wanahabari wachache waliowahi kufika eneo lile wakiendelea kuwahoji baadhi ya raia wema waliowahi kufika eneo la ajali. Wakati Suhail akiwa ameshasimama nje kuna akina mama kama wawili na vijana kama watatu hivi walionusurika kwenye ajali hiyo walikuwa wakimuangalia kwa mshangao tangu anashuka kwenye basi, wakamsogelea mpaka pale alipo

    “Kaka vipi?,” alianza mama mmoja mnene hivi kuuliza swali

    “Safi tu mama’angu,”

    “Kumbe ulikuwemo ndani ya Basi muda wote?”

    “Ndio, nyie wakati mnazitoa maiti nilikuwa nawaangalia tu lakini nilikuwa kama nilieishiwa nguvu sana, na hata sikujua nimeumia wapi mpaka sasa kwani wakati ajali inatokea mimi nilikuwa usingizini” wale abiria wakaangaliana kwa mshangao kisha mmoja akamtupia tena swali Suhail

    “Mbona hatukukuona kabisa, na tulihakikisha hakuna aliebaki mule ndani?”

    “Nadhani hamkuangalia kwa makini ila nilikuwepo humuhumo, mimi niliwaoneni”

    “Mnh, yaani ndio wote tusikuone? Haya tuachane na hayo, mbona mizigo mkononi?,” Kijana mwingine alimuhoji suhail huku akimsontea kwenye lile begi lake dogo jeusi, Suhail alijua tu angekutana na maswali ya aina hiyo lakini akajikaza na kujitetea

    “Jamani mimi inabidi tu niondoke maeneo haya haraka vinginevyo nitapatwa na matatizo makubwa” Abiria wale walizidi kumuangalia Suhail kwa tahadhari maana walimuona mtata sana kila nukta ilivyokua ikisonga mbele

    “Hapana kaka, haupaswi kuondoka, tena ukiwa na begi hilo, kiusalama si kitu chema maana hatuwezi kuamini kama begi hilo na vilivyomo ni mali yako”



    “Jamani iko hivi, mimi nilikuwa nawahi Dodoma kuripoti kazini ambako niliondoka tangu majuzi bila ya ruhusa maalum sasa kama nitagundulika nilikuwa safari na nimepata ajali hii nitafukuzwa kazi hivyo nawaombeni sana mnielewe ndugu zangu, sina nia mbaya” Suhail alijaribu kuwashawishi abiria wenzie wamuelewe, japo nao kiasi walikuwa wanashawishika lakini kiasi hawaamini ila baada majadiliano ya muda mrefu wakakubaliana kua wamkague Suhail katika hilo begi lake wajiridhishe kisha wamuache awahi kwenda kazini. Suhail akawa anatetemeka akihofia pesa nyingi kama zile alizonazo katika Begi jekundu zitaonekana hakuna atakaeruhusu aondoke hivihivi lakini sasa cha ajabu kila abiria pale alikuwa akiliangalia Begi lile dogo jeusi tu, na hakuna hata mmoja aliejishughulisha kuangalia lile begi kubwa Jekundu lililokua mgongoni, Suhail nae aliligundua jambo hilo japo lilimpa faraja lakini lilizidi kumuacha na maswali mengi kichwaniCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Hawalioni hili begi au nini hasa?, kama wanaliona kwanini hawalitilii shaka! Na kama hawalioni je ni kwanini?’ Maswali mengi yalipita kichwani lakini hakupata majibu mpaka alipomaliza kukaguliwa katika begi lake jeusi na hatimaye akaruhusiwa na kuanza kuondoka eneo lile akiwa na mabegi yake yote mawili mpaka barabarani ambapo ilikuwa ni hatua ndefu kidogo tokea pale lilipokwama Basi lao.



    Alipofika barabarani alikuta vijana wawili wakiwa wamepaki Bodaboda zao pembeni wakitaka nao kujongea kule lilipoangukia ajali lakini walipomuona Suhail akielekea usawa wao kila mmoja alianza kumuhoji kama angehitaji usafiri, Akamsogelea kijana mmoja akaongea nae na baada ya makubaliano alipanda kwenye Bodaboda yake na safari ya kuelekea Dodoma mjini ikaanza haraka. Safari haikuwa ndefu sana kwa mwendo wa Pikipiki, takriban dakika 45 zilitosha kuwasili mjini na walipofika wakaenda mpaka katika moja maarufu lipo karibu na Stendi ya mabasi, Lilikuwa ni jingo la ghorofa na lenye nakshi ya na mapambo megine ua kuvutia, kwa juu ya Jengo hilo kuna bango kubwa liliosomeka ‘SEFLAVA LODGE’, baada ya kumalizana na dereva wake aliingia ndani kwa ajili ya kuchukua Chumba apumzike na kuweza kupanga sasa nini cha kufanya. Naam akapokelewa na wahudumu mahiri waliokuwa tayari kupokea wageni. Baada ya kuandikishiana na wahudumu kwenye kitabu maalum cha kumbukumbu za wageni akapelekwa mpaka ghorofa ya pili, chumba No112 akakabidhiwa chumba na kuachwa hapo. Kilikuwa ni chumba kizuri sana, ‘Self contained room’, palikuwa na huduma zote muhimu ndani, Baada ya kujibwaga kitandani ili japo uatafute usingizi ikashindikana, hakuwa na usingizi hata chembe, mawazo na fikra zikarudi kwa Mzee Shamhurish, aliyakumbuka maneno yote ya mzee Yule kabla hajakata roho, moyo ulipiga tikitaka kila alipokumbuka jina la Shekhia, Jina hilo lilimtesa sana moyoni akapiga moyo konde akalisogelea begi Jekundu lenye pesa akalifungua tena, hakuwamini alichokiona, mikono ilimtetemeka, Dola Miamia za kimarekani zilisheni ndani ya Begi, japo alishaziona tangu mwanzo lakini pesa nyingi kama zile hakuwahi kua na urafiki nazo. Baada ya muda mrefu wa tafakuri aliona sasa ni muda muafaka kuwapigia simu wazazi wake ili awajuze kuhusu ajali hiyo lakini kila alipoitafuta simu yake hakuiona, alijipekua kila kona lakini hakuipata simu ndipo alipokumbuka kua huenda aliiacha ndani ya Basi, Akawa hana namna tena zaidi ya kuomba msaada wa kuazimwa simu, akauendea mkonga wa simu uliokua mule chumbani katika meza ndefu ya mbao,akaunyanyua na kuwapigia mwahudumu akimuomba mmoja wao aende chumbani kwake. Muda mfupi tu mlango wa Chumbani kwake ukagongwa, akainuka kivivu na kuufungua akaingia dada mmoja mrembo akiwa amevalia sare maalum zenye nembo ya ‘Seflava Lodge’

    “Karibu mrembo.”

    “Ahsante, naweza kukusaidia!”

    “Nina shida na mambo mawili, kwanza nataka chakula, Niletee Chipis kuku na juisi, Pili ninahitaji uniazime simu yako niweze kupiga kidogo maana kumbe simu yangu nimeisahau huko nilipotoka”

    “Ok, haina shida, huyo mtu wako anatumia mtandao gani?”

    “Anatumia Voda”

    “Sasa mimi ninatumia tiGo, na sijajiunga kupiga mitandao yote”

    “Duh kumbe dada unatumia tiGo?,” aliuliza Suhail huku Swali lake lakimfanya Yule mhudumu acheke kwa sauti kisha akajibu

    “Kwani kuna ubaya jamani?”

    “Hakuna ubaya, hata mimi ninatumiaga hiyo”

    “Hiyo nini?”

    “tiGo, Ok kuhusu vocha usiwe na tabu nitanunua tu, kwani jumla ya chakula pamoja juisi ni shilingi ngapi?”

    “Itakua ni Shilingi elfu nane tu”

    “Ok, poa” Suhail akatoa noti moja ya Shilingi elfu kumi akamkabidhi mhudumu ili akanunue chakula kisha akampa maelekezo kua chenji itakayobaki ndio anunulie vocha, Dada Yule akaipokea na kuondoka zake mule Chumbani.



    Wakati ametoka mhudumu Yule ndipo macho ya Suhail yakapiga katika televisheni ya mule chumbani iliyokua sasa ikiendelea kutoa taarifa ya ajali hiyo huku ikionesha baadhi ya miili ya marehemu, macho ya Suhail yaliendelea kuangalia kwa makini kama ataweza kuuona mwili wa Mzee Shamhurish lakini aliambulia patupu, hakuweza kumona kamwe mpaka taarifa ile ikamalizika na ‘program’ zingine zikaendelea. Akili ya Suhail sasa ikazidi kuzunguka na hofu ikatuama moyoni mwake,akiwa bado ameduwaa asijue la kufanya mara mlango wa chumbani kwake ukagongwa kwa nje na baada ya kuruhusu akaingia tena Yule mhudumu akiwa na chakula mkononi pamoja na simu ikiwa tayari ameshaiongezea salio, lakini kutokana na mfadhaiko wa muda mfupi alioupata Suhail hapakuwa tena mazungumzo marefu na mhudumu Yule kama awali

    “Haya kaka karibu chakula, na simu hiyo hapo nitairudia wakati nakuja kuondoa vyombo”

    “Ok ahsante dada yangu” Mhudumu akatoka nje na kumuacha Suhail akiwa katika lindi la mawazo, alijikaza kiume akachukua chakula na kuanza kula taratibu huku akiumiza kichwa juu ya Shekhia, haraka akakumbuka kitu, akaacha kwanza kula, akachukua simu na kutaka kumpigia Shekhia ili ajiridhishe kama ndie yeye anaekusudiwa ama ni Shekhia mwingine lakini akakumbuka kua namba ya simu ya Shekhia imepotea pamoja na simu yake kule kwenye ajali. Akashusha pumzi na kuendelea kula kabla hajakumbuka suala la muhimu zaidi nalo ni kumpigia simu Baba yake mzazi Mzee Kusekwa ili kisha ampigie na Sharifa, kipenzi cha roho yake. Kwa hao zoezi halikuwa gumu kwani namba zao alizikariri kichwani hivyo akaona malizie chakula ndipo awasiliane nao



    *****

    Hali ya mzee Kusekwa haikuwa nzuri kabisa, mawazo yalimzidia kiasi cha kumfanya awe anasema peke yake, ndani ya muda mfupi tangu apokee taarifa ya ajali hiyo mwili wake umesawajika vibaya na kunyong’onyea vilivyo. Ilikuwa majira ya Alasiri sasa wakati mzee huyo akitokea mjini maeneo ya stendi ya zamani ya mabasi mkoani hapo ambapo ndipo zilipo ofisi za Air bus alipokuwa amekwenda kukata tiketi kwa ajili ya safari ya kwenda Dodoma kujaribu kutambua miili ya marehemu pamoja na kuwaangalia majeruhi kama watampata Suhail. Siku hiyo mzee Kusekwa aliiendesha baiskeli yake kimazoea tu maana kimwili alikuwa juu ya baiskel lakini kiakili alikwishawasili Dodoma, magari na watembea kwa miguu alipishana nao ki mungumungu tu na hatimaye akawa amewasili nyumbani kwa Mzee Fungameza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipofika akapitiliza moja kwa moja mpaka ndani kwa kua hakuwa mgeni sana katika nyumba hiyo, Nyumba ilikuwa kimya, akapitiliza moja kwa moja mpaka barazani ambapo alipokelewa vizuri tu na Mzee Fungameza aliyekuwa amekiti kwenye kochi lake la sofa

    “Ohoo, karibu bwana Kusekwa,”

    “Ahsante nimekwisha karibia, vipi za mida?”

    “Aah nzuri tu, karibu uketi”

    “Ahsante sana” Wakati wazee wale wakiendelea kupokeana huku wakijuliana hali Sharifa alikuwa chumbani kwake akiendelea kulia kwa uchungu lakini aliposikia sauti ya baba yake na Suhail imeingia ndani kwao ikabidi sasa ajikaze ili apate kusikia taarifa alizokuja nazo mzee Yule, Hakika Sharifa alimpenda sana Suhail na hakuwa na sababu tena ya kuisha bila ya kijana Yule, sasa akasogea katika upenyo wa mlango wa chumbani kwake akategesha sikio ili kuibia mazungumzo ya wazee kule barazani

    “Sasa bwana mimi si mkaaji sana”

    “Ndio..”

    “Nimepita tu kukufahamisha kwamba ndo nimetoka kukata ticket, nimepata Air Bus, muda wa kuwasili stendi ni saa kumi na moja na nusu alfajir na safari itaanza saa kumi na mbili kamili”

    “Ooh, ok hakuna matata bwana mkubwa tuombe uzima tu Mungu atuamshe vema” wakati wanaendelea na mazungumzo yao ndipo Simu ya Mzee Kusekwa ikaita, alipoitoa mfukoni ili kuangalia nani mpigaji hakuweza kumfahamu kwakua ilikuwa ni namba mpya, akabonyeza kitufe cha kupokelea kisha akailengesha spika ya simu hiyo katika sikio lake la kushoto

    “Hallow”

    “Shikamoo Baba”

    “Marahaba, nani wewe?”

    “Aah baba yaani huijui sauti ya mwanao?”



    “Mnh, wewe ni Su.. we ni nani” Mzee alipata hamaniko ghafla, akataka kutamka jina la Suhail lakini akasita, wakati huo Mzee Fungameza nae akawa kama amepatwa na hisia fulani hivi. Alimsogelea mzee mwenzie ili ajue anaongea na nani. Huko chumbani nako Sharifa akawa anahesabu tu mapigo ya moyo wake wakati Mzee kusekwa anaongea na simu.



    “Ndio mie Suhail” Sauti ya Suhail ilipenya sawasawa katika siko la baba yake.



    “Wee! Suhail?”



    “Ndio baba, vipi kwani?” maneno yale yakamfanya Mzee Kusekwa aishiwe na nguvu akajikuta amepigwa butwaa tu. Ikabidi haraka Mzee Fungameza ainyakue simu ile na kuiweka sikioni wakati huo tayari Sharifa alishatoka barazani pale huku akifuatiwa na mama yake ambae nae kumbe alikuwa akiyasikilizia mazungumzo chumbani kwake.



    “Suhail?!” Mzee kusekwa nae aliuliza kwa mshangao, na sauti kutoka upande wa pili wa simu ikathibitisha swali lake.



    “Naam ndio mimi, naongea na nani tena?”



    “Mimi Mzee Fungameza, hujambo lakini wewe na uko wapi?”



    “Mimi sijambo mzee Shikamoo..”



    “Marahaba.. Enhee?”



    “Mimi nipo Dodoma, mbona ghafla naongea na wewe? Baba imekuaje hapo?”



    “Baba yako amejikuta tu ameishiwa nguvu hapa, vipi uko hospitali au wapi?” swali lile likamfanya sasa Suhail apate picha halisi kuwa tayari nyumbani kwao wote walikua wanazo habari za ajali ile.



    “Mimi nimesalimika mzee namshukuru Mungu, wakati huu nipo Dodoma mjini. Nimeumia kiasi tu maeneo baadhi ya mwili, poleni nanyi kwa hekaheka za taarifa hii ya ajali.”

    Sharifa akajikuta anashindwa kujizuia na haraka akatoka hadi pale barazani. Alitamani hata ainyakue ile simu amsikie mchumba wake. Ghafla, mama Sharifa nae akatoka chumbani kwake alikokuwa amejifungia. Kumbe, naye alikua akiyasikilizia maongezi hukohuko chumbani. Sebule ikajaa furaha ghafla. Sharifa na mama yake walikumbatiana huku wakirukaruka. Mzee Kusekwa, kama mtu aliyetoka usingizini, aliunga tena katika chereko hizo. Kisha, akaichukua simu yake na kuzungumza tena na Suhail.



    Mazungumzo yalikuwa marefu sana. Suhail akawaelezea jinsi ajali ilivyotokea hatua kwa hatua japo aliwaficha kuhusu mkasa wa Mzee Shamhurish. Wazee wale wlipomhitajikuwa kesho yake tu awe Tabora, aliwakatalia. Aliwadanganyakuwa kutokana na maumivu kidogo ya mwili anakusudia kurejea Dar es Salaam kesho yake kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Aliwaahidi kurejea Tabora baada ya hayo.



    Haikuwa kazi rahisi kuwashawishi wazee wale. Alikazia msimamo wake. Alihitaji sana kupata fursa ya kuwasili Dar. Alihitaji kujipanga juu ya namna ya kufanya na pesa. Aliamini hakuwa salama kwenda nazo kwao. Wazee wake walilazimika kumwelewa japo kwa shingo upande. Walipomaliza mazungumzo, alikata simu.



    Amani ilirejea ndani ya nyumba ya Mzee Fungameza. Kila mmoja alikuwa akijisemea lake lililokuwa moyoni. Ghafla simu ya Sharifa ikaita. Alipoiangalia akaona namba mpya inampigia. Mawazo yake yalimpeleka kwa Suhail. Alikimbilia chumbani kwake. Alitaka kuzungumza na simu hiyo kwa uhuru mkubwa. Alijihisi kama anaota. Hata hivyo alikuwa furahani. Furaha yake haikuwa na kifani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipoipokea simu, alikutana na sauti ya Suhail. Sauti impayo raha moyoni mwake. Sauti imjazayo mahaba. Baada ya salamu, maongezi marefu yalishika hatamu. Pengine, isingekuwa hivi vifurushi vya kujiunga katika mitandao ya simu, maongezi yao yasingenoga kiasi hiki.



    Maongezi yale yalikatizwa na muhudumu wa kule hotelini alipopanga Suhail aliyeingia kwa ajili ya kutoa vyombo na kuchukua simu yake. Suhail aliagana na mchumba wake kwenye simu na akimuahidi kuwa kesho yake atakapofika Dar atarudisha namba yake iliyopotea kisha wataongea kwa kirefu zaidi.



    Simu ikakatwa



    *****

    Ilipotimu saa saba mchana, Suahil alikwishawasili Dar. Alikwenda moja kwa moja hadi Ilala Bungoni akiwa na mabegi yake. Alichukuwa chumba katika hoteli moja kubwa na ya kisasa. Hakuwa na tatizo na pesa za kumuwezesha kukaa katika hoteli ya hadhi hiyo. Alipoingia hotelini kwake, alijitahidi kujisahaulisha kadhia ya Mzee Shamhurish.



    Baadaye, Suhail aliamua kwenda kuzihifadhi pesa zile benki. Kwa kuwa alikuwa na akaunti katika benki mbili za NBC na NMB, aliamua kuzitawanya pesa hizo katika akaunti zake zote. Pia, alibakiwa na kiasi kingine kikubwa cha pesa. Alianza kupanga mikakati ya miradi. Aliamini kwa kuanzisha miradi haraka itamsaidia kuzidhibiti pesa hizo kutopotea. Suhail alikuwa na elimu nzuri tu tena katika masuala ya fedha na biashara.



    Waswahili wanasema pesa hupasua mwamba. Wiki moja baade Suhail alifanya mambo makubwa kuliko wengi waliomfahamu wangeweza kuamini. Alinunua nyumba kubwa za kisasa katika maeneo ya Mbezi na Ilala. Ndani aliweka kila kitu cha kifahari. Pia alikuwa katika hatua za mwisho za kufungua kampuni yake kubwa ya masuala ya Bima na nyingine ya upakiaji na upakuaji mizigo bandarini. Pesa ipo Elimu ipo Mungu ampe nini Suhail!! Tayari alikwishapata Ofisi za kukodi maeneo ya Kariakoo na Posta, na alishaanza kutafuta wafanyakazi wa kuwaajiri katika kampuni zake baadhi wakiwa ni marafiki zake aliosoma nao chuoni lakini ili kuficha siri ya pesa hizo wengi aliwadanganya kua kuna mzee mmoja tajiri sana kutoka Yemeni ndio amemkabidhi mali zake amsimamie.

    Maisha yalikuwa matamu japo kila siku alikuwa akipata taabu kutokana na usumbufu anaopata kutoka kwa wazazi wake pamoja na mchumba wake huko Tabora, alikua akihitajika aende haraka japo akafanyiwe hata tambiko na dua za wazazi kutokana na kusalimika katika ajali.



    Wiki moja tena mbele akiwa tayari ameshafungua kampuni zake na shughuli za utendaji zikiendelea sasa akawa anapanga tu kwenda nyumbani kwao Tabora ili pamoja na mambo mengine akabadilishe hali ya maisha ya familia yake. Suala lake la kumuoa Sharifa lilikua likipita kichwani mwake lakini kila alipokumbuka kauli ya marehemu Mzee Shamhurish kuwa amuoe binti yake aliishiwa nguvu kabisa.



    Kila akikumbuka historia yake na Sharifa tangu walipokuwa shuleni alijihisi dhalimu mkubwa endapo hatotekeleza ndoto yao ya kufunga ndoa. Lakini Kila alipokumbuka kuhusu Shekhia hakika Jasho lilimtoka.



    *****



    JUMAPILI moja tulivu Suhail akiwa nyumbani kwake Mbezi amejilaza kitandani huku akiperuziperuzi katika kompyuta mpakato yake ndipo ghafla aliposhtushwa na sauti ya mtu aliyekuwa akimwita kutoka nje ya chumba hicho. Sauti hiyo ilikuwa ikitokea sebuleni. Aliingiwa na hofu kuitikia kwani mule ndani hakuwa akiishi na mtu yoyote zaidi ya mlinzi tu ambae naye yupo getini huko na asingeweza kuingia ndani kwa kuwa mlango ulikua umefungwa. Akabaki anajiuliza huyu mtu kaingiaje ndani tena huku akimuita kwa jina lake kabisa!.

    Wakati akiwa katika tafakuri iliyogubikwa na hofu mara ghafla hali ya hewa ikabadilika, Chumba chote kikawa kinanukia utuli mzuri kwa kiwango cha juu sana, yaani kama ni ‘Perfume’ basi huyo mtu aliejipulizia inaonekana alimaliza chupa ya lita kumi. Ilikuwa ni harufu kali mpaka sasa akaanza kuhisi maumivu ya kichwa. Akiwa bado hajaelewa kinachoendelea mara ghafla akaona mlango wa chumbani kwake ukifunguliwa taratibu. Moyo wake ukapiga chogo chemba! Akatamani akimbie akaufunge mlango lakini alikuwa ameshachelewa. Aliinuka haraka na kuketi papohapo kitandani. Macho yake yaliganda mlangoni ili kumtazama mtu aliyekuwa akiufungua mlango huo.



    Jambo la ajabu, mlango huo ulifunguka hadi mwisho. Hakuonekana mtu aliyekuwa akiufungua. Akiwa bado hajui cha kufanya ndipo ghafla akashtushwa tena na sauti kali ya mtu akicheka kwa nguvu nyuma ya kitanda alichokuwa ameketi. Akageuka haraka huku akiwa ametaharuki. Hakuamini alichokiona. Mapigo ya moyo yakabadilika. Akawa anahema juujuu mithili ya mtu aliyekimbizwa kwa muda mrefu. Macho yake yalikuwa yakitazamana na Mzee wa makamo aliyekuwa amesimama huku ameegamia dirisha kubwa la mbao lililofunikwa na pazia ya rangi ya samli, alihisi kumtambua Mzee yule lakini kumbukumbu zilikataa kumjia, akatuliza macho yake kwa sekunde kadhaa ndipo sasa fikra zake zikasalimu amri, akamkumbuka Mzee yule aliekutana nae kwenye basi siku aliyopata ajali, alikuwa ni Mzee Shamhurish. Suhail akakurupuka pale kitandani kwa kasi japo akiwa hajui hata anataka kufanyaje, ndipo mzee Shamhurishi akamtuliza kwa sauti yake ileile

    “Tulia Suhail, unataka kufanya nini sasa? Ulidhani nitaingilia mlangoni? Huwa hatwendi hivyo..”



    “We ni nani na unafanya nini humu ndani?” Suhail alijikuta akiuliza swali la kipuuzi huku akitetemeka, japo alimkumbuka vema mzee Shamhurish ambae kwake yeye aliamini kua mzee yule ni marehemu lakini alijichetua akili kujifanya hajamfahamu. Mzee Shamhurish akacheka tena kabla hajaendelea kuongea kwa ile sauti yake ya utulivu.



    “We ni mtu mzima Suhail haupaswi kujifanya punguwani, ina maana umenisahau mimi? Mimi ni Mzee Shamhurish, haya umeshanikumbuka?,”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana sijakukumbuka, Mzee Shamhurish ninayemkumbuka mimi alikwisha fariki katika ajali ya basi, sasa wewe ni Shamhurish yupi?.”



    “Kumbe una kumbukumbu, sasa nisikilize mwanangu, zingatia sana maelekezo niliyokupa kule kwenye basi kuwa unapaswa kumuoa Shekhia haraka iwezekanavyo sitarajii kukuona ukiendelea kula raha tu kabla haujatekeleza agizo hili, fanya hima uende Bagamoyo unasubiriwa huko kwa ajili ya ndoa. Pili tafadhali ile pete niliyokupa usiwe unaivua na kuiacha mbali kwani ile ndiyo siri ya mafanikio na ulinzi wako wewe na mkeo mtarajiwa najua kwua tangu ulipoivua wakati unaoga bafuni hukuivaa tena na ukaitelekeza hukohuko.”



    “Mzee mimi sitaweza kumuoa huyo binti yako, kwani nami nina mchumba tayari,”

    Jibu hilo la Suhail likamfanya mzee yule mwenye asili ya Kiasia kua kama mbogo aliyejeruhiwa kwa jinsi alivyopandwa na ghadhabu. Mzee akamsogelea Suhail mpaka pale kitandani alipokua ameketi, akachukua bilauri ya juisi iliyokuwa juu ya meza ya kioo na kummwagia yote usoni na maeneo ya kifuani kisha kitendo bila kuchelewa Mzee Shamhurish akamzaba Suhail kibao cha uso. Maumivu makali yakamfanya Suhail apige kelele kali na ya uchungu

    “Yalaaaaaaaaaaaaaa!”



    Kelele hiyo ndiyo iliyomtoa usingizini na kumfanya agundue kumbe alikua anaota tu, akainuka haraka pale kitandani akatazama huku na kule huku akitweta kama labda angemuona Mzee Shamhurish lakini hakuona kitu, akashusha pumzi kidogo, akainamia tendegu la kitanda ili apate kutuliza munkari lakini ghafla mapigo yake ya moyo yakabadilika na kupanda juu tena, hakuamini alichokiona. Alikuwa ametapakaa juisi usoni na mwilini hasa maeneo yale yale ya kifuani alipomwagiwa na mzee Shamhurish ndotoni, sasa akabaki anajiuliza kama ilikua ni ndoto tu sasa imekuaje tena ajikute amelowana juisi wakati hakua na juisi yoyote pale kitandani. Taharuki ikaongezeka, akaanza kuvuta picha ya maongezi yake na Mzee Shamhurish alipokua ndotoni. Akakumbuka kuhusu maelekezo aliyopewa kuhusu pete na wakati huo shavu lake la kulia likichonyota kwa maumivu ya kibao alichopigwa usingizini.



    ‘Yaani kofi nimepigwa usingizini lakini maumivu mpaka uraiani! Hii sasa kali’, akajiangalia kidoleni wakati anafikiria kichapo alichopokea kutoka kwa Mzee Shamhurish na kugundua kuwa ni kweli hakuwa na pete ile na akakumbuka kuwa aliiacha kweli bafuni kama alivyoambiwa na Mzee Shamhurish, ‘Hii ndoto ni ya aina gani? Huyu mzee atakua amenitokea kiukweli, sasa nimekwisha Suhail mie. Mawazo ya hofu yalizidi kutalii ndani ya kichwa chake. Akaondoka haraka mpaka bafuni akaikuta pete yake palepale alipoiacha, akaichukua na kurudi mpaka sebuleni. Akaketi juu ya sofa akijaribu kujituliza kidogo

    ‘Sasa ni muda wa kumtafuta Shekhia bila ya kujali ndie yule nimjuae mimi au ni Shekhia mwingine vinginevyo nitauawa bure.” Mawazo yaliendelea kutembea kichwani na baada ya mawazo mengi kichwani aliamua kuwa kesho yake atakwenda Bagamoyo kumtafuta Shekhia. Akiwa anamalizia kupitisha wazo lake hilo simu yake ya kiganjani ikaita. Akaingiza mkono katika mfuko wake wa suruali akaitoa, alipoangalia jina la mpigaji akamtambua, Mzee Kusekwa.



    “Hallow, Shikamoo Baba,” Aliamkia Suhail baada kupokea simu.



    “Hakuna cha Shikamoo hapa, hivi we mtoto huna wazazi? Au ulijizaa mwenyewe?”



    “Kwanini Baba?”



    “Kwanini Baba,” Mzee kusekwa nae alijibu kama alivyoulizwa japo yeye aliibana sauti na kuitolea puani kuonesha keji kwa mwanae kasha akaendelea “..We ni Mpumbavu wa akili ama? Unauliza swali gani hilo? Kwanini hautaki kuja kwenu wakati unajua fika kwamba kila mtu alikuwa akuusubiria ujio wako kutokana na ajali uliyoipata, sasa unatutukanisha sisi kwa majirani kwa ujinga wako”



    “Lakini Baba..”



    “Hakuna cha lakini hapa, sasa nasema hivi kama mimi ni baba yako..” Kabla Mzee Kusekwa hajamalizia kusema alichokuwa amekikusudia simu yake ikakatika na kumuacha Suhail akiwa amekumbwa na fadhaa kubwa sana, akawa ameishika simu yake asijue cha kufanya, alitamani kumpigia mzee wake lakini alihofia majibu ambayo angekutana nayo, akiwa bado hajai afanye nini, Simu yake ikaita tena, Suhail akashtuka tena, akavuta pumzi akitafuta cha kujibu lakini alipoiangalia simu yake hakua Baba yake tena, Safari hii alikua ni Mchumba waker, Sharifa Fungameza. Alijua tu hapakuwa na jingine zaidi ya lawama mpya, Aliishia kuitazama simu mpaka ilipokatika, akaimalizia kuizima kabisa ili asipate bughdha ikamuharibia safari yake ya kesho!



    *****



    Upepo mwanana uvumao kutokea usawa wa bahari uliendelea kuvuma karibu kila pembe ya mji wa Bagamoyo, mji wenye karibu kila aina ya vivutio vya kitalii, Mji huu kihistoria ulikaliwa sana kwa kiasi kikubwa na wegeni wa kiarabu ambao walifika pwani ya Afrika mashariki kwa minajili ya kuendesha Biashara ya utumwa hivyo mila nyingi na tamaduni za hapo Bagamoyo zilirandana kwa karibu na maisha yao kila siku katika wilaya hiyo iliyo katika mkoa wa Pwani. Watu wengi kutoka katika mataifa tofautitofauti wakimemo Waarabu na Wazungu hufika mahala hapo kwa ajili ya kufanya utalii, wenyeji nao kutoka ndani ya Tanzania aghalabu hufika mahala hapo kufanya kile kiitwacho utalii wa ndani. Lakini hali ilikuwa tofauti kwa Suhail Kusekwa ambaye nae aliwasili siku hiyo katika mji huo wa kihistoria kwa ajili ya kazi moja tu, kazi ya hiari iliyo ya lazima, nayo ni kumtafuta Shekhia mtoto wa mzee Shamhurish, japokuwa hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika Bagamoyo lakini hakuwa na hamu hata kidogo ya kutalii kwani akili yake ilikuwa imeshavurugwa na ndoto ya ajabu aliyoiota jana yake, Ndoto yenye dalili zote za kuashiria ujumbe wa kweli uliomfikia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Swali kubwa lililojenga kambi kichwani mwake ni Je wapi atampata Shekhia, na Je ni Shekhia Yule anaemjua yeye? Hakuwa na pakuanzia ukizingatia hakuwahi kufika Bagamoyo kabla ya siku hiyo,



    Baada ya kuwasili katika stendi ya mabasi ya hapo Bagamoyo akitokea jijini Dar es Salaam, alianza kutoka nje ya stendi hiyo taratibu kama vile ni mwenyeji. Wakati akiendelea kutembea akielekea nje ya lango la kuingilia stendi hapo alikumbana na ghasia za hapa na pale kutoka kwa baadhi ya madereva wa Bodaboda kila mmoja akijitafutia riziki, Suhail hakushughulika nao akaendelea kutembea mpaka alipofika nje kabisa akawa anaendelea kuangalia mandhari ya Bagamoyo ambayo amekua akiyasikia tu na kuyasoma kwenye vitabu. Alipomaliza kuyaridhisha macho yake ndipo sasa akamuita kijana mmoja dereva wa bodaboda aliyekuwa amepaki upande wa pili wa barabara, na ndani ya dakika moja kijana Yule akawa ameshafunga breki mbele ya Suhail

    “Mambo vipi afisa?,” alisalimia kijana Yule kwa ucheshi

    “Poa kaka, Eee bana nataka unipeleke sokoni mara moja.”

    “Hakuna noma ka’Mkubwa, ni sokoni palepale au?”

    “Yeah ni hapo hapo sokoni” Akajibu Suhail huku akikaa katika pikipiki ile, nae dereva bila ajizi akapeleka kidole chake katika ‘stata’ na kuibofya, akatia ‘gia’ na safari ikaanza. Wakiwa njiani Suhail alikuwa akiangalia mazingira mazuri ya mji ule mpaka akajikuta anasahau shida zake, alijaribu kua anamuuliza maswali kijana Yule aliembeba ili azidi kuyafahamu mazingira ya mji ule lakini hakupata nafasi ya kengine itamrahisishia safari yake na kazi ya kumsaka Shekhia



    “Kaka wewe ndie wa magomeni?,” aliuliza Suhail huku akimuangalia kijana Yule anaemuuzia mikufu

    “Ndio mkubwa”

    “Na mimi ni wa Ilala nadhani tuko karibukaribu” Jibu hilo la Suhail likawafanya vijana wale wote waangue kicheko kabla ya Yule kijana hajamfahamisha tena Suhail

    “Iko hivi kaka hapa Bagamoyo pia kuna pahala panaitwa Magomeni wanapotoka watoto wa Kiswahili, hatuna maana ya magomeni hiyo ya Dar” Suhail ikabidi nae acheke tu, akajua kua amejichanganya, akaachana nao vijana wale baada ya kununua vidani viwili, akatoka mpaka nje ya soko akiwa sasa amepata mwanga kidogo akamuita tena dereva mwinginewa bodaboda akamtaka ampeleke sehemu inayoitwa Magomeni, haikua mbali sana kutokea pale sokoni, ni mwendo kama wa kilometa mbili tu akawa ameshafika, akateremka na kumlipa mwenye bodaboda kisha akaanza kutembea kwa miguu taratibu huku akitafutauelekeo. Baada ya mwendo wa muda mrefu akiendelea kutembea tu akatokea kwenye nyumba moja akawakuta wasichana kama watatu hivi wameketi katika kibaraza cha nyumba hiyo huku mmoja akimsuka mwenzie na mwingine aliekua amejifunga kilemba cha njano akiwapigisha stori tu wenzie, akawasogelea na kuwasalimu

    “Wapendwa Asalamu alaykum”

    “Waalyakum salaam,” wakaitika wote kwa pamoja kabla ya Yule msichana anaemsuka mwenzie kumkaribisha

    “Karibu kaka”

    “Haya nimeshakaribia, jamani mimi shida yangu maji ya kunywa tu”

    “Wala usijali kaka yangu labda kama una jingine” dada yule msusi akamuagiza Yule mwenzao aingie ndani akamchotee maji Suhail, wakati anainuka Yule msichana kuendea maji ndipo Suhail akachombeza neon hapohapo

    “Pia naomba niwaulize jamani”

    “Uliza tu kaka”

    “Mimi natokea Dar, hapa Bagamoyo si mwenyeji sana, namtafuta msichana mmoja anaitwa Shekhia” aliongea kwa umakini sana Suhail huku akiwatazama wale wasichana wanaosukana nywele lakini alishangazwa na hali ya wale wasichana baada ya kuwatamkia kile kitu maana waliacha kusukana kisha wakamuangalia kwa pamoja kabla ya msusi kutupa swali

    “Shekhia yupi huyo?”

    “Mtoto wa mzee Shamhurish”

    “Mzee Shamhurish? Huyo hatumjui”

    “Sasa mbona kama mlishtuka sana kusikia namuulizia Shekhia?”

    “Tulidhani unamuongelea Shekhia Sufiani” jibu la msusi likamlipua moyo Suhail, akamkumbuka Shekhia S. Sufiani aliesoma nae chuoni

    “Inaweza ikawa nd’o huyo, kwani huyo yeye ni wa wapi?” wasichana wale wakatazamana tena kisha kwa pamoja wakaangua kicheko wakati huo Yule mwenye kilembo cha njano akiwa ameshatoka na gilasi yake ya maji mkononi na kumkabidhi Suhail, wakati Suhail anakunya maji akamsikia Yule msusi akimuambia yule msichana alieendea maji ndani

    “Haya shosti kuna ugeni hapo”

    “Upi huo?”

    “Huyo mkaka anamuulizia Shekhia”

    “Shekhia?” Swali la dada mwenye kilembo cha njano japo lilielekezwa kwa msusi lakini haraka Suhail akamalizia funda la maji na kujibu

    “Ndio Shekhia, jamani hebu niwekeni wazi kwani ana nini dada yule?” Swali la Suhail halikua na maana zaidi ya kuwazidishia siku za kuishi akina dada wale kwa kuwafanya wazidi kucheka, Suhail akabaki njia panda, ikabidi sasa nae aketi pale kibarazani na kuanza kuwadadisi wasichana wale. Baada ya muda mrefu wa udadisi ndipi dada mwenye kilemba cha njano akaanza kufunguka

    “Ni simulizi ndefu sana iliyotokea hapa Bagamoyo, Shekhia alikua ni rafiki yangu zamani sana tulipokua shule ya msingi kwakua tulikua majirani na tulisoma shule moja, tukiwa bado wadogo kikatokea kioja cha mwaka kilichopelekea kifo cha maajabu cha mama yake mzazi, tangu hapo Baba yake akamkataza tena Shekhia kutokatoka nje kuja kucheza, ikawa tunakutania shuleni tu na baadae Shekhia kahamishwa shule na kupelekwa Dar japo kila wiki akawa anakuja pale kwao lakini akawa hachezi na sisi tena..” Kabla dada hajaendelea Suhail akamkatisha kwa swali

    “Samahani kidogo, naona kama umeruka kitu, hicho kifo cha mama yake kilikua ni cha aina gani? Na wakati huo mlikua mkiishi wapi na akina Shekhia?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tulikua tukiishi huko Mlingotini kama umewahi kupasikia.. siku moja Kilitokea kimbunga kikali kilichokua kama kilichotumwa vile, kikapita nyumba zote mpaka kwa akina Shekhia, kilipofika uani kwao kikamvaa mama yake na Shekhia akiwa anapika uani kwao kwao, cha ajabu waliokua jirani na nyumba hiyo wanadai ndani ya vumbi lile la kimbunga waliwaona watu kama watatu hivi, na kabla kimbunga hakijasambaa watu wale wakambeba mama Shekhia na kutoweka nae wao pamoja na kimbunga kile..” Msichana yule akaweka kituo kidogo ili kuyapa uhuru mapafu yake kuvuta hewa mwanana itokeayo baharini, hakika habari ile ilikua ni ya ajabu na kutisha, Suhail alikua akizidi kuzizima ndani kwa ndani kwa uoga, alishaelewa kua Shekhia anaeongelewa hapo ni yule binti aliekutana nae kule chuoni lakini pia yawezekana ndie akawa mtoto wa Mzee Shamhurish, msichana mwenye kilemba cha njano akaendelea kusimulia huku wale wenzie wakiendelea kusukana nywele “..Basi bwana, nusu saa baada ya kimbunga kupotea watu wakiwa wamefurika uani kwa akina Shekhia wakishangaa muujiza huo ndipo tena ghafla ukadondoka mwili wa mama Shekhia ukiwa umeshaachana na roho yake ukitokea angani, watu wakatawanyika kila mmoja na njia yake. Patashika ya nguo kuchanika, Ilikua ni tukio la ajabu sana japo kwa hapa bagamoyo matukio kama hayo ya kustaajabisha ni sehemu ya maisha yetu. Baadae wazee wakasogea tena pale, wakamstiri mama yule ili wamsubiri mumewe arudi lakini haikua hivyo, ilichukua kama siku mbili bila ya mumewe ambae ni baba yake na Shekhia kurejea hivyo viongozi wakaamua kwenda kumzika tu yule mama huku wakimchukua Shekhia kipindi hicho akiwa mdogo sana. Mwezi mmoja Baadae ndipo yule Mzee alirejea, alipofika akapewa taarifa za tukio lile lakini cha ajabu hakuonekana kushtushwa sana na habari zile, ni kama vile aliekua akijua kila kilichotokea, alichokifanya akaenda kwa majirani tu kutoa shukrani zake kwa waliomsitiri mkewe, Akamchukua mwanae, na Baada ya muda hali ikatulia na kisa kikaanza kusahaulika. Ndipo hapo sasa Shekhia akapotelea Dar hatukujua tena Shekhia huko Dar anakaa kwa nani maana hata hapa hatukuwahi kuwajua ndugu zao kwa kua walikua wakiishi peke yao tu. Ila mpaka hivi tunaongea nadhani Shekhia yupo hapahapa Bagamoyo maana hua anaonekana mara mojamoja sana inasemekana amemaliza chuo ndo karejea. Sasa Baada ya tukio lile la ajabu hata huyo Baba yake nae akawa haonekani kabisa. ila kama ukitaka kujua habari hizo kwa kirefu yupo babu yangu mimi kama ulishwawahi kumsikia Mzee Atrash Jamadu, yule ni kiboko anajua uganga wa kila aina, na yeye ndie anaejua siri kubwa ya akina Shekhia ila hua hasemi hovyohovyo, Nasikia ni watu wa hatari sana” maneno ya msichana yule yalimmaliza nguvu Suhail, akawa kama aliepigwa bomu la kutoa jasho mwilini, akiwa bado ameshangaa akatupiwa neno na yule msusi ambae aliekua kimya muda wote

    “Upo hapo mkaka?, hii ndo bwagamoyo yakhee karibu sana, kama ulidhani umeopoa chombo basi umeopolewa” kisha kicheko cha kishangingi kikaunguruma

    “Unaweza kunipeleka kwa huyo babu yako?,” aliuliza Suhail huku akimuangalia dada mwenye kilemba cha njano

    “Ukafanye nini sasa?”

    “Si umesema yeye ndio anajua mambo mengi zaidi?”

    “Tena zaidi ya mengi lakini mimi siwezi kwenda huko saa hizi, kwanza ni mbali na pili ndio nimetoka huko sasa hivi nimekuja huku kwa rafiki yangu kusuka, labda nikusaidie kukuelekeza tu uende mwenyewe”

    “Kwani ulisema ni wapi vile?:

    “Panaitwa mlingotini, ni nyuma kidogo kabla haujafika huku Bagamoyo mjini, laity ungejua ungeshukia kulekule”

    “Sikia dada naomba tu twende wote nitalipia Tax mpaka huko kwenu kisha itakurejesha tena mpaka hapa, na pesa ya Msusi nitakulipia”

    “Mnh, kaka kwani we una jambo gani na Shekhia mpaka umekua makini kiasi hicho?”

    “Aaah kawaida tu, kwakua tumeshakua marafiki nitakueleza tu muda ukiwadia, ila kwa sasa naomba ukubali twende tukamuone mzee” ilikua ni kama bahati ya mtende kwa Suhail kukutana na wasichana hawa waliompa maneno yaliyommaliza kabisa maana pamoja na uzito wa maneno ya msichana yule ameambiwa kua Mzee Atrash Jamadu ndio anajua Siri kubwa,



    ‘Ni siri gani hiyo?’



    Ikabidi sasa Suhail atumie nguvu kubwa ya ushawishi pamoja na kutumia pesa ndipo dada yule akakubali kurudi huko Mlingotini kwa ajili ya kumpeleka Suhail, hawakua na sababu ya kuendelea kupoteza muda tena, wakainuka na kuwaaga wenzao kisha wakaanza kuondoka na kuelekea barabarani, walipofika tu haraka wakasimamisha Tax, wakapatana bei, na safari ikaanza huku Suhail akiwa kama mwendawazimu kwa habari alizozipata kuhusu Shekhia



    *****

    DAKIKA zipatazo ishirini na tano kwa mwendo wa teksi zilitosha kabisa kuwafikisha Mlingotini lakini kutokana na Miundombinu ya barabara kua si nzuri sana hivyo ikawalazimu washukie barabara kuu na kuanza kuanza kutembea kwa miguu kuelekea nyumbani kwa Mzee Atrash ambapo hapakua mbali sana kutokea barabarani hapo, Ndani ya dakika tano wakawa wanatazamana na Nyumba ya ‘Msumbiji type’ mali ya Mzee Atrash. Nyumba hiyo hiyo iliyojengeka kizamani ilipigwa ‘Lipu’ kwa upande wa mbele na kushoto, lakini upande wa kulia matofari ya kuchoma yalionekana waziwazi. Miti mirefu ya Minazi, Mitende, mipapai, Migomba, nk iliyoonekana kupandwa kiustadi kuzunguuka nyumba hiyo iliupendezesha muonekano wa eneo hilo huku kijani kibichi cha miti midogomidogo kama vile Mikomamanga, mipera, michungwa nk kikitawala mazingira hayo na kuyafanya yajenge taswira kua ni nyumba ya Mswahili pwani haswa!



    Waliingia ndani ya nyumba hiyo Suhail na Mwenyeji wake mwenye Kilemba cha njano kwa kupitia mlango wa Mbele huku wakifuatana mmoja mbele na mwingine nyuma kama watoto wa Bata, ilikuwa ni Korido Ndefu iliyotenganisha vyumba vinne vya upande wa kulia na vitatu vya kushoto. Waliendelea kutembea katika korido ile ndefu wakielekea mwisho kabisa ambapo kabla ya Mlango wa kutokea uani palikuwa na ‘Seating Room’ upande wa kushoto iliyokua imepambwa vizuri tu kwa mitindo ya kisasa licha ya kwamba kwa nje nyumba ilionekana ni ya kizamani sana. Walipofika hapo ‘Seating Room’ walipokelewa na akina mama wawili waliokuwa eneo hilo, Mmoja akiwa amekalia kibao cha mbuzi huku akiendelea kukuna nazi na mwingine akiwa ameketi katika zulia lililotandikwa chini akiwa anajipaka hina katika vidole vyake vya miguuni, Baada ya salamu Suhail akakaribishwa aketi juu ya Kochi na baada ya kuketi ndipo Sasa Dada mwenye Kilemba cha njano akaanza kutoa utambulisho mfupi kwa mgeni na wenyeji

    “Kaka Suhail karibu sana nyumbani, jisikie huru,” aliongea kwa utulivu dada yule

    “Ahsante sana nimeshakaribia.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nikutambulishe sasa kidogo, huyo anaekuna nazi ni mama yangu mzazi, na huyo mwingine hapo ni mama yangu mdogo, wote ni watoto wa Mzee Atrash..”

    “Ooh, nashukuru sana kuwafahamu,” alijibu Suhail kabla ya dada mwenye kilemba cha njano kuendelea kutoa utambulisho kwa upande wa pili

    “Jamani huyu anaitwa Suhail, ametokea Dar es Salaam, ni mgeni wa Babu”

    “Haya karibu mwaya, jisikie uko nyumbani,” alijibu Bi mkubwa aliyekuwa akikuna nazi kisha sauti nyingine ya yule aliyekuwa akipaka hina nayo ikasikika ikimkaribisha Suhail, hakika nyumba hii ilitawaliwa na ustaarabu na ucheshi wa hali ya juu.

    “Ahsanteni sana Mama”

    “Ila sasa ufanye Subra Mzee anaswali ndani akimaliza utaingia kumuona, leo tangu asubuhi yuko ‘busy’ na wageni tu, akitoka huyu anaingia yule”

    “Haina tatizo mama, Nashukuru” Baada ya maelekezo hayo sasa Ikabidi Dada mwenye Kilemba cha njano aondoke zake ili awahi kwa msusi wake kule Bagamoyo mjini, na kwakua tayari alikwishapewa ujira wake na Suhail alipokuwa ndani ya gari hivyo hakuwa na la ziada, akaaga na kuondoka..

    Baada ya dakika kama Kumi na tano hivi Suhail akiendelea kuwaza na kuwazua juu ya mambo yanayoendelea kumkumba, akakatizwa mawazo na Sauti kavu ya kukwaruza iliyotokea chumbani

    “Kama kuna mgeni aingie” Sauti ile iliwafanya wale akina mama waliokuwa wakiendelea na shughuli zao wamgeukie Suhail kwa pamoja kisha yule anaekuna Nazi akamfanyia kwa ishara Suhail kua aingie ndani akaonane na Mzee Atrash, akainuka na kujongea taratibu akielekea katika chumba cha kwanza kabisa upande wa kulia ilipotokea sauti ile, Badala ya kufurahia kuonana na mtu atakae mpa Ukweli wa mambo asiyoyajua badala yake Mwili wa Suhail ulizizima kwa hofu na woga, vinyweleo vikajitutumia katika ngozi yake, ubaridi ukabarizi karibu kila kona ya maungo yake

    Akabisha hodi na kukaribishwa, akaingia.. Kilikuwa ni chumba kikubwa tu kilichosheni makabati makubwa ya vitabu, na Makochi mawili ya sofa ambayo hayakuonekana vizuri rangi yake kutokana na hali ya giza iliyomo ndani mule iliyosababishwa na madirisha kufunikwa na mapazia makubwa kila pembe



    “Karibu tafadhali bwana,” Sauti ile kavu kutoka kwa Mzee yule ilitoka kwa kukwaruza ikimkaribisha Suhail. Mzee yule aliyekuwa ameketi katika Mkeka mdogo alionekana kua na umri mkubwa sana, licha ya Mvi zilizoonekana kujaa kichwani mbali ya kua Kibaraghashia alichokuwa amekimaa kilizima nusu ya sehemu kichwa chake lakini hata maungo yake yalikuwa yamechakaa kwa uzee wake



    “Ahsante sana Mzee wangu,” alijibu Suhail huku akiketi chini jirani na Mzee Yule



    “Haya nini hali zenu nyumbani huko utokeako?”



    “Aaah huko tunamshukuru Mungu hatujambo, sijui ninyi hapa”



    “Nasi hatujambo kadri ya hali, Karibu..” Salamu zilijichukulia dakika kadhaa kabla ya Suhail kuanza kujielezea



    “Mzee mimi natokea Dar es Salaam, naitwa Suhail nimekuja hapa kwa ajili ya kuhitaji kujua jambo moja kubwa,..”



    “Naam, lipi hilo?.”



    “Kuhusu watu wawili, Shekhia na Mzee Sufiani.”



    “Unataka kujua nini kuhusu wao na kwanini unahitaji kujua?”



    “Nataka kujua kuhusu maisha yao kwa ujumla, Kuna Biashara tunahitaji kufanya nao hivyo nimeambiwa niwafuatile kwanza niwajue ndipo mambo mengine yatafuata,” Aliongea Suhail kwa kudanganya ili apate kujua habari nyeti bila ya kumfanya Mzee huyo ashituke



    “Hua siongelei habari za mtu hovyohovyo tu, wala hua sitoi habari nyeti kwa mtu asiekua makini, kwa mtu muongo, kwa mtu msaliti na kwa mtu mwenye tamaa..” Akakohoa kidogo Mzee Atrash lakini kabla hajaendelea akawahiwa na Suhail



    “Sijakuelewa Mzee”



    “Utanielewa tu, Athari za Mtu Muongo, Msaliti, na Mwenye tamaa huzijui?”



    “Nazijua,” alijibu Suhail huku akiwa anamuangalia usoni Mzee yule ambaye yeye hakuwa akimuangalia kabisa zaidi ya kuendelea kukiinamia kitabu chake kama vile yale ayasemayo anayatoa katika kitabu kile



    “Vizuri, sasa mtu wa aina hiyo hua hana muamana, Ila pamoja na hayo, acha nikusaidie.. Nitakusimulia ila hua natoza pesa nyingi kwa huduma nazotoa hapa..”



    ”Nitalipa tu Mzee, haina tatizo”



    ”Hapana, kwako wewe sitakutoza hata Senti tano, nitakuhudumia bure tu.. nina sababu ya kufanya hivyo” Akakohoa tena Mzee yule ambaye bila shaka kifua kilikuwa kikimsumbua, Sasa Suhail akaingia rasmi katika uwanja wa tafakuri za hofu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Miaka takribani Ishirini na tisa iliyopita katika eneo hili la Mlingotini alitujia mgeni, namwita Mgeni kwakua hakuwa katika jamii yetu, akanunua nyumba kubwa eneo la mbele kidogo hapo, akaikarabati vizuri sana nyumba ile na akawa anaishi hapo. Taratibu tukaanza kuzoeana nae na tukaishi nae kwa Amani na ujirani mwema, japokuwa alikuwa ni mtu wa kusafiri mara kwa mara lakini mara chache alizorejea alitutembelea majirani zake kutujulia hali, hiyo haikuwa ajabu kwani huo ndio haswa utamaduni wa Waungwana wa Bagamoyo, Bwana yule mwenye asili ya asia alietambulika kwa Jina la Sufian au Mzee Sufiani kama ambavyo vijana wengi walivyomwita kwa heshima. ilisemekana ni mfanya biashara mkubwa wa Mafuta na Madini na kwamba huzungukia mikoa na nchi kadhaa kwa ajili ya kutekeleza biashara zake hizo. Lakini katika kipindi chote alichokuwa akiishi ndani ya jengo lake hilo hatukuwahi kumjua mke wala mtoto wake zaidi ya vijana wawili wa kiarabu waliotambulika kama watumishi wake..” Mzee alisita kidogo kuendelea akakohoa kwa nguvu sana mpaka akawa kama anaeishiwa nguvu lakini baada ya sekunde kadhaa akatulia kidogo, akameza funda la mate, kisha akaendelea



    “..Muda si muda ikafika siku moja bwana yule akaja na mwanamke mmoja hivi hakika alikuwa mzuri sana lakini hakuwa na asili ya asia kama yeye Sufiani, mwanamke yule alikuwa ni mweusi tu kama mimi na wewe kitu ambacho kiliwastaajabisha wengi pale Mzee Sufiani alipotutambulisha kua yule ni mkewe, si unajua tena hatukuzoea kuona wenzetu weupe wakioa kwetu sisi weusi, basi hatukua na jinsi zaidi ya kukubaliana nae tu.. hawakuja’aliwa na mtoto kwa wakati huo, waliishi wawili tu ndani ya jengo lao lilikuwa na uzio mkubwa sana na imara japo kwa sasa naona kama uzio wenyewe umeanza kupoteza mvuto wake, hawakua wakitembelewa na wageni mara kwa mara hivyo kuacha maswali kwa majirani wenzao kufuatia upweke wao huo.. mwaka mmoja baadae wakajaaliwa kupata mtoto baada ya Bi mkubwa yule Kushika ujauzito ambao ulimsumbua sana kiasi cha kukaa nao tumbo kwa miezi kumi na tano badala ya tisa iliyozoeleka, ilikuwa ni gumzo mtaani hatimaye Mungu akaleta neema akajifungua mtoto wa kike waliemwita Shekhia Bint Sufian, Maisha yakaendelea..” Suhail alikuwa akiisikiliza kwa makini habari ile iliyoiteka akili yake na kuiacha na maswali ambayo alitegemea angeuliza mwishoni ili kukidhi adabu za mazungumzo, hakujua kua asingepata nafasi hiyo tena. Mzee Atrash akaendelea



    “..Siku moja likatokea balaa la kile kimbunga kilichoibuka ghafla na kumsomba Bi mkubwa yule, kikampeleka juu na muda mfupi baadae kikamuachia na kumdondosha chini akiwa hana uhai, Japo majirani waliumizwa na kifo cha mwanamwama yule mzuri wa umbo na Sura lakini kwa wajuvi wa mambo tuliona ni sawa tu acha afe kidhalili kwakua alistahiki kifo hicho cha kinyama.. sina haja ya kuelezea hapo kwa kirefu kwakua Tayari Sauda kaishakueleza mlipokutana nae huko Bagamoyo mjini, kwa kifupi tu ni kwamba baada ya Sintofahamu ile kubwa tulizika bila ya Mzee Sufiani kuhudhuria, na kwakua Shekhia alikuwa mdogo sana na hapo nyumbani kwao hawakua na mtu mwingine hivyo iakabidi sasa achukuliwe na baadhi ya majirani mpaka baba yake aliporejea baadae sana..” Maelezo ya Mzee Atrash yalizidi kumchanganya kichwa Suhail si tu kwa kusikia kua kifo kile kilimstahiki mama yake Shekhia bali pia alijiuliza Mzee huyu amejuaje kua amekwishaongea na yule dada mwenye Kilemba cha njano ambaye bila shaka ndie Sauda mwenyewe! wakati Sauda hakupata nafasi ya kuonana na Babu yake huyo tangu walipofika mpaka alipoondoka kurudi kule kwa Msusi!! Sasa alianza kupata picha ya kwanini Mzee yule alimpiga mafumbo kuhusu mambo ya ‘uongo’, aliamini kua mzee yule anajua vitu vingi sana.

    Mzee Atrash alikiinamia tena kitabu chake na kuiperuzi mistari kadhaa kabla ya kuendelea kuongea kwa kuanza kutoa historia mpya iliyoonekana kama ni tofauti na mada iliyopo mezani

    “Miaka kadhaa iliyopita Bi Mkubwa mmoja aliingia nchini Tanzania akitokea Rwanda, alikuwa akijihusisha na biashara za nguo hasa hasa vitenge hivyo uwepo wake wa mara kwa mara hapa Tanzania ukamfanya nae awe ni kama raia wa hapa, hakika alikuwa ni Mzuri wa Sura na Umbo, vitu vilivyowafanya wanaume wengi kumuhitajia. Katika harakati zake za Kazi akakutana na Bwana mmoja Mtanzania wakapendana na kuamua kuishi pamoja kama mume na mke japokuwa walikuwa na tofauti kubwa mbili, tofauti ya utaifa na Dini zao, Bwana yule alijiona ana bahati sana ya kumpata mwanamke yule aliyekuwa akiwasumbua wanaume wengi kwa uzuri wake, Wakawa wanaishi kama mume na mke huku wakipanga mipango itakayowawezesha kufunga ndoa. Siku ya Siku mwanamke yule akakutana na mwanaume mwingine aliemtaka kimapenzi, Mwanamke yule akakubali bila ya kujali tayari ana mtu wake na amekwisha panga nae kufunga ndoa, kilichomzuzua zaidi mwanamke yule mpaka akamkubali mwanaume yule mpya ni Pesa alizokuwa nazo mwanaume yule ambaye nae hakuwa mtanzania, alikuwa ni mwanaume mwenye asili ya ‘Weupe’. Hatimaye mwanamke yule akamkana na kumtenda vibaya mwanaume aliyekuwa tayari ameanza nae maisha kisha akakimbilia kwa tajiri huyu aliemuhadaa kwa kile alichokuwa nacho.

    Vikaibuka vita vikubwa baina ya Wanaume wale wawil, ‘Vita vya Mapenzi’..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ilikuwa ni mpambano wa kumsaka nani mwamba zaidi, zilitumika hila na mbinu za kila aina lakini Kutokana na nguvu za ziada za mwanaume yule mweupe hatimaye aliishinda ile vita.. Mtanzania wa watu akasalimu amri, lakini kibaya zaidi Mwanamke yule alipomkimbia mwanaume wake wa mwanzo alimuacha na kitu kilichozidi kumpa simanzi na mawazo mwanaume yule..Japo kilikuwa ni kitu adhimu”



    Mzee Atrash alisita kidogo kabla hajakitaja kitu hicho adhimu, mara akamtupia swali Suhail “..Umeshamjua huyo mwanamke na huyo Mwanaume?” Lilikuwa ni swali ambalo Mzee Atrash alijua vema kuwa Suhail asingekuwa na jibu ila alimuuliza ili kumzindua kutoka katika lindi la mawazo na hofu



    “Hapana, sijawajua,” alijibu Suhail na kumfanya Mzee yule alievalia kanzu ya rangi ya Udhurungi aendelee kuongea



    “Huyo mwanaume Mweupe ndie Mzee Sufiani, na huyo Mwanamke mfanya biashara kutoka Rwanda ni Mama Shekhia aliefariki kwa kusombwa na kimbunga.. Usaliti na Tamaa vikamponza mama yule..”

    ‘Usaliti na tamaa vilimponza vipi mama huyo? Kwani kifo chake kilisababishwa na Kimbunga au na Tamaa?’ Swali lilipita kichwani mwa Suhail, Kama vile Mzee Atrash aliyaona mawazo ya Suhail akaanza kutiririsha historia nyingine iliyoanza kuyaangunisha matukio yote na kumpa jibu Suhail, Jibu lililozidi kumnyima raha badala ya faraja



    “Miaka ya nyuma kidogo palikuwa ni Himaya huko chini ya bahari zikiendesha utawala wao, Himaya moja kubwa sana ikiitwa Budha, himaya hiyo ilikuwa na utajiri na ulinzi mkali kuliko zote.. utawala wao ulikuwa ukiwaniwa kwa udi na uvumba kama iwavyo huku duniani kwetu ifikapo kipindi cha mchakato wa Uchaguzi, sasa ilipoanza kukaribia kipindi chao cha uchaguzi kila kikundi kikawa kinamuandaa Jini alieonekana kuwa na uwezo wa kuukwaa uongozi wa juu wa Himaya ya Budha, Sasa Kiongozi anaemaliza muda wake nae akawa anamuandaa jinni aliemtaka yeye ili aje amuachie madaraka hayo ili aje afiche maovu yote aliyokuwa akiyafanya kipindi cha utawala wake, wakati huo Wana Himaya wengine wa Budha Jini nao walikuwa wamemuandaa Jini mwingine aje ashike madaraka hayo, Jini huyo Aliitwa Sufian Ibn Shamhurish..”



    Moyo wa Suhail ukapiga tikitaka ndani ya kifua chake, mapigo ya moyo yakaanza kukimbia mara dufu, licha ya hali ya upepo wa pwani uliotawala eneo la Mlingotini lakini Suhail alikuwa akifuka Jasho, hakutaka kuwamini anachokisikia kwamba Mzee Sufian ambaye ni Baba yake na Shekhia ndie Mzee Shamhurish aliyekutana nae kwenye basi na ukweli mgumu kuukubali ni kwamba ni Jini. Hamu ilimwisha, Hamaniko hilo ni dhahiri Mzee Atrash aliliona hivyo akakaa Kimya kidogo kabla ya kuendelea kuongea “..Katika Himaya hiyo ya Budha Mzee Sufian Shamhurish alikuwa ni Mkuu wa kitengo cha Ulinzi na Utajiri na alikishika kitengo hicho kwa umakini wa hali ya juu kiasi cha kufanya baadhi majini wenzie wamteue yeye ashike nafasi ya juu ya utawala huo. Hapo sasa ikawa ni vita ya ushindani baina ya makundi mawili hasimu ikawa ni mshikemshike almanusura ya kuuwana, Katika hali hiyo ya kutafutana ndipo wanaompinga Bwana Sufian Wakaamua kumuundia kashfa kubwa itakayopelekea kumnyima sifa za kuwa mgombea wa nafasi hiyo ya juu kabisa katika Himaya yao, katika kumtafutia Kashfa wakawa wanafuatilia kama Bwana Sufian ameshawahi kupatwa na kashfa ya kujihusisha na Uzinzi, hawakubahatika kuipata kashfa hiyo kwa kuwa licha ya bwana Sufiani kuwa hajawahi kuoa lakini hajawahi kupatwa na tuhuma za uzinzi katika Himaya yao, Sasa katika kuendelea kumfuatilia ndipo wakagundua kuwa bwana Sufiani hua anakuja sana Duniani ndipo wakaanza kumfuatilia na kugundua kuwa alikuwa akijihusisha na Mwanamke mmoja ambaye amempora mwanaadamu kwa kutumia nguvu zake za kipesa. Hapo sasa wakakusanya ushahidi wa kutosha, na kwa kuwa ni kinyume kabisa na Sheria zao kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kiumbe kisicho cha jamii yao wakamtia hatiani, na wakajiridhisha kwamba hakuwa amemuoa mwanamke huyo hivyo akawa amepoteza sifa za kuwa Kiongozi wao. Bwana Sufiani hakukubali kushindwa kapambana kujisafisha kwa muda mrefu sana bila mafaniko, ndipo akaamua kutoroka na kundi la wafuasi wanaomuunga mkono, akatorokea Dunia na kuja kuishi Bagamoyo ambapo baada ya kununua nyumba yake akamleta mwanamke yule niliekutajia mwanzo na hatimaye Kumzaa Shekhia”

    ‘Kwahiyo Shekhia ni Jini Mtu?,’ alijiuliza Suhail, hakujibiwa chochote kwakuwa alijiuliza ndani ya fikra zake mwenyeweCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Majini katika himaya ya Budha wakaanza kufanya msako mkali wa kumtafuta Sufian, walimtafuta karibu kila kona bila ya mafanikio, lakini baadae wakagundu kuwa yuko Duniani ndipo wakamfuata, Kikubwa kilichowafanya wahangaike kumtafuta ni kwamba bwana Sufiani alitorokana kitu adhimu sana kwa mustakabali wa Himaya yao, kitu ambacho ni kama Roho ya himaya yao, kitu ambacho kinayabeba na kuyaongoza maisha ya Himaya yao kiulinzi na kiuchumi. Kitu hicho kilikuwa ni Pete Kubwa isiyokuwa na Rangi, Iliitwa ‘Khatam Budha’ Pete hiyo alikuwa akiimiliki bwana Sufiani kwaku Kitengo cha Ulinzi na Fedha kilikuwa chini yake yeye hivyo akapata fursa ya kutokomea nayo duniani, sasa Wanahimaya wa Budha wakaingiwa na hofu kuwa hawana Ulinzi tena wala hawawezi kupata mali kubwakubwa za baharini na nchi kkwakuwa Zana yao hapo nayo tena ndipo msako ukabidi kupamba moto, lakini iliwapasa kuwa makini sana katika kumsaka kwakuwa walijua fika kuwa Pete ile ni Silaha, na kwa yeyote atakaingia vibaya kwa Sufian ataangamizwa. Na kweli mara kwa mara walipokaribia kumtia nguvuni aliwagundua na kuwateketeza vibaya, akawapunguza kasi na idadi hivyo akawa anajiongeza tu makosa ya mauaji ya kwenda kujibu huko Budha kama atakamatwa..” Suhail alipigwa na mshtuko wa ajabu sana kusikia habari za Pete ile amabayo bila shaka nd’o hiyo aliyonayo mkononi, alipoiangalia akashangazwa kuona ina kito cha rangi nyeupe wakati alipokabidhiwa ilikuwa na kito cha Rangi ya Njano, akiwa bado anajiuliza maswali Mzee Atrash alianza tena kukohoa kwa nguvu baada ya kuwa muda mrefu ameongea bila tabu, akachukuwa maji kidogo ya kunywa, akapiga mafunda kadhaa, akapata nguvu mpya, akamuangalia Suhail alivyokuwa akijiangalia kidoleni alipoihifadhi Pete yake kabla ya kuendelea “..Ndipo wale majini wakaona kwakuwa Bwana Sufian amempenda sana yule mwanamke wa kibanaadam hivyo wakaamua kumchanganya kwa kumuua mwanamke yule ili iwe rahisi kwao kumpata yeye, Na kweli wakatimiza lengo lao la kumuua mama yule Msaliti mwenye tamaa kisha wakaanza kumuwinda na Shekhia japo kwa Shekhia hawakuwa na lengo la kumuua kwakuwa Shekhia ni katika jamii yao, ni binti ya Jini mwenzao hivyo wakawa wanataka wamchukue ili wampeleke katika himaya yao ya Budha ili akikuwa aolewe hukohuko ili mwisho wa siku bwana Sufian atapatikana kiurahisi, haraka bwana Sufian akazigundua hila zao, akamuhamisha mwanae kutoka Bagamayo na kumpeleka Dar es Salaam ambako alikulia huko na kuendelea na masomo yake huko akiwa katika ulinzi wa hali ya juu. Tatizo kubwa lililokuwa likimgharimu bwana Sufian Shamhurish mpaka akawa mara kwa mara anajulikana alipo hata kama atajificha wapi ni Nuru kali itokanayo na Pete ile, hakika ile Pete ilikuwa na Nuru kali sana kiasi kwamba popote atakapojificha ataonekana tu, Nuru ya majini ilikuwa ikizidiwa ukali na Nuru ya Pete hiyo hivyo miale ya Pete ile ilikuwa ikionekana japo kwa mbali na kusababisha awe ni kiumbe wa kuhamahama na kukimbiakimbia tu. Ndipo sasa wazo likamjia kichwani kwamba Binaadam hua ana Nuru kali zaidi kuliko majini, na hata kuliko ile Pete hivyo ikawa ni lazima apate mwaadamu wa kumvisha pete ile kwakuwa akifanya hivyo itawafanya maadui zake wasiione tena Nuru ile na kumfanya yeye asijulikane alipo mpaka siku iatakapowadia yeye kurejea kule Budha kwenda kufanya mapinduzi makubwa nay a ghafla, lakini mwanadamu atakaekabidhiwa atakuwa akifanya kazi zote za kiulinzi na kiuchumi kwa maelekezo yake yeye... Sifa za mwanaadamu huyo huyo atatakiwa kuwa mwanaume, mwenye Nidhamu, na awe na Nyota ya ‘Shamsi’, nyota yenye nuru ya jua. Kumpata mtu huyo ikawa ni kisanga kilichomhukuwa miaka kadhaa bila mafaniko.. Ndipo siku ya siku mwanae akampa taarifa kuwa amepata mchumba anependana nae kwa dhati ikabidi Mzee Sufiani ajiridhishe kwa kumfuatilia mchumba wa mwanae ndipo akamkuta kijana mmoja aliemvutia sana, alipomchunguza akagundua kuwa ana sifa za mwanadamu aliepaswa kuvishwa Pete ya ‘Khatam Budha’..na kwakuwa atakuwa ni mkwe hivyo atakuwa muadilifu na ataitumikia mamlaka yake kwa kila nukta”



    “Mzee wangu NIMEKWISHA,” Sauti ya Suhail alimkatisha mzee Atrash aliekua akiendelea kuongea, ikabidi sasa Mzee Yule anyamaze kidogo kuacha maneno yake yamuingie Suhail, na alipoona sasa kijana ametulia kimya ndipo akaendelea

    “..Pete hiyo inaweza kuleta utajiri mkubwa kama itaamrishwa kufanya hivyo, Pete hiyo inaweza kuleta maafa makubwa kwa maadui wa kijini na kibinaadamu kama itaamrishwa kufanya hivyo, na Pete hiyo ni ulinzi dhidi ya hila za kijini au kibinaadm kama itaamrishwa ikulinde.. Inahitajika elimu ndogo sana ya kuitawala na kuiamrisha Pete hiyo lakini taaluma ya matumiz sahihi ya Pete hiyo Mzee Sufian atamfundisha kijana aliemkabidhi ili aitumie vema kumlinda, japo najua kua hawezi kutoa taaluma zote za kiusalamia akihofia siku moja kugeukwa maana anawajua vema wanaadam..”

    “Mzee yaani naona kama nachanganyikiwa kabisa, akili yangu kama haifanyi kazi sawasawa, naomba unisaidie Mzee.. lakini sasa mbona Mzee Shamhurish alifariki katika Basi?”

    “Nikusaidie nini wakati ulisema unataka tu kufanya nao Biashara?, Shamhurish hakufariki kama unavyodhani wewe bali ilikua ni njia ya kuondokea huku Tanzania na kutokomea Yemen sasa Baada ya kumpata mtu wa kumpa pete yake tena mtu mwenye ni Mkwewe hivyo alipaswa aonekane hayupo tena katika Nchi hii kwa kufa au vinginevyo, hivyo hiyo ilikua ni kiini macho tu..” Akashusha pumzi Mzee Atrash kisha akaanza kuhitimisha mazungumzo yake “..Kilichokuponza wewe ni Tamaa ya pesa za Shekhia kama ilivyomponza mama Shekhia kutamani pesa za Mzee Sufian Shamhurish, Pia kilichokuponza tena wewe ni Usaliti uliomfanyia Sharifa licha ya kwamba alikupenda, akakuamini, na kukutahamini kwa hali na mali kama ambavyo Mama Shekhia alivyomsaliti yule Mwanaume aliempenda, akamjali na kumthamini.. Vita vya Mapenzi vilivyotimka kipindi kile cha Nyuma sasa historia itajirudia kwako.. Na kinachoendelea kukuponza wewe ni Uongo kama huu uliokuja kunidanganya mimi hapa kua mnataka kufanya Biashara na akina Shekhia, haya sasa kaendeleeni na Biashara yenu ila ujue hii ndio Bagamoyo, pwani ya wajuvi wa mambo, haupaswi kuja ukavamia mji kwa mbinu za uwongo. Haya mimi nimemamaliza yangu naomba sasa kwa heshma na ta’adhima utoke nje waingie na wengine,” Alihitimisha Mzee Atrash na kumuacha Suhail akibubujikwa na machozi huku akiwa haamini kinachomtokea

    “Mzee wangu naomba unisaidie, naomba unifae sina pa kukimbilie mie,” Suhail alikua akikongea na kulia kwa wakati mmoja kiasi cha kufanya sieleweke viozuri anaongea nini, lakini Mzee Atrash alisimama katika maamuzi yake akamuamuru Suhail atoke nje tena bila ya malipo, ila akamuambia anamkaribisha siku nyingine akiwa amejirekebisha tabia zake..

    ‘Afua mbili, Kufa na Kupona’ Suhail alijisemea kimoyomoyo, akainuka kishingo upande na kutoka nje ya nyumba hiyo huku akifuta machozi ili asigundulike na akina mama wale. Akatoka akiwa Kichwa chini mikono nyuma,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****

    Maneno ya Mzee Atrash yalimzidia uzito kichwani bwana mdogo Suhail, akawa kama aliyechanganyikiwa kabisa, akatoka mule ndani bila ya kujielewa, yaani njia nzima akawa anjisemea peke yake tu, kichwa chake mwenyewe lakini alihisi kikimzidia uzito kutembea nacho. Alipofika nje akawa anatoka na kile kinjia ambacho ni mfano wa barabara ndogo ili akaikute barabara kubwa asubiri gari la kurejea Dar es Salaam hakukumbuka tena kilichompeleka Bagamoyo ni kumtafuta Shekhia na kutafuta habari za Shekhia pengine angelizingatia hilo angesalimika lakini sasa amekua adui wa maamuzi yake mwenyewe, hakuona thamani ya kuendelea kuishi japo pia hakufikiria kuupoteza uhai, kila alipotembea hatua kadhaa aliiangalia Pete yake, hakua na kuifanya zaidi ya kutikisa kichwa na kuendelea kutembea kuelekea barabarani..

    Dakika chache akawa amefika Barabarani, akawa anaangalia huku na kule kama ataona kituo maalum ambacho magari husimama kwa pale Mlingotini yakitokea Bagamoyo mjini kwenda Dar, ndipo ghafla alipatwa na mshtuko wa mwaka, moyo wake ukapiga tikitaka ndani ya kifua chake baada ya kushtushwa na Sauti nzuri nzuri iliomsemesha ikitokea kwa nyuma yake pale alipokua amesimama, ni sauti aliyoifahamu sana, na alipogeuka alithibitisha hisia zake kua alikua akitazamana uso kwa uso na Shekhia S. Sufian au Shekhia bint Shamhurish, nguvu zikamwisha kaanguka mpaka chini kama kiroba cha uchafu, akaanza kuhisi hali ya kupoteza fahamu lakini aliipigani nafsi yake kiume, akajikaza mpaka akasimama wakati Shekhia akimsogelea kwa furaha isiyo kifani,

    “Suhail yaani mpenzi wako ulieyekua ukilala nae leo unamuogopa kamahujawahi hata kugusana nae?!, acha utoto wewe,” aliongea Shekhia huku akilizidisha lile tabasamu lake pana lililokua likiwachanganya vijana wengi kule chuoni. Lakini kwa sasa Suhail hakuliona wala hakuhitaji kuliona. alipoinuka tu akaanza kutimua mbio kama mwendawazimu, Shekhia alijaribu kumuita kwa furaha ili ampunguze hofu aliyonayo lakini haikuwezekana, Suhail alikimbia umbali mrefu mpaka akawa hamuoni vizuri tena Shekhia, na hapo akaona haina haja ya kusubiri gari kubwa akasimamisha Tax iliyokua ikitokea kulia mwa barabara ambako ndiko njia ya kwenda Dar es salaam akaisimamisha na kuingia haraka huku akitweta akafunga mlango na kumuamuru dereva ageuze gari waelekee Dar es Salaam. Dereva hakubisha alitii amri akaanza kuendesha lakini hakugeuza gari yake kwa maana ya kuupata uelekea wa kurejea ambako Suhail alipataka

    “We vipi mbona haunielewi, nimekwambia naenda Dar, sasa unaelekea huku wapi? Mimi siendi huko Bagamoyo,” alikaripia Suhail lakini kijana yule hakujibu wala hakujihangaisha japo kumtazama Suhail, aliendelea kuendesha gari yake mpaka hatua kadhaa ndipo akakata kona mkono wa kulia ikiwa ni njia kama ya pili hivi au ya tatu kutokea kwenye ile njia ndogo inayokwenda moja kwa moja mpaka Mzee Atrash, Sasa Suhail alipoona hamuelewi dereva yule akaamua kufungua mlango ili ashuke haraka kwa kua gari ilipunguza mwendo pale kwenye kona, alipojaribu kufungua mlango haikuwezekana, Mlango ulikua umepigwa “Lock” na dereva, hakika Suhail alitamani hata amvae tu kijana yule lakini hakua na nguvu kabisa akabaki tu anamuangalia dereva yule ambae aliendesha gari yake kwa umakini mpaka katika nyumba moja hivi ndefu kwenda juu, ni kama ghorofa moja lakini ilikua ni chakavu sana kiasi cha kumfanya mpita njia ambae ni mgeni kuamini kua mule ndani hapakaliwi na watu na labda pengine ni Gofu tu la kuhifadhia taka. Lakini cha ajabu jingo hilo lilikua limo ndani ya uzio ambao ulionekana kusafishwa kwa kupaliliwa majani yaliokua yakiota pale na kufanya hisia kichwani mwa Suhail kua mule ndani kuna watu wanaishi,

    Naam kulikua na watu wakiishi!

    Dereva kasogeza gari mpaka getini ambapo bila ya kupiga honi mlango ukafunguliwa na kijana mmoja bila shaka ni mwenye asili ya kiarabu kutokana na nywele zake za singa na rangi yake ya ngozi. Gari ikaingizwa mpaka ndani kisha ikapakiwa upande wa kulia ambapo palikua na sehemu maalum ya maegesho ya magari, kijana yule aliefungua geti akasogea mpaka pale katika gari kisha dereva akatoa ‘lock’ ya milango na kumuamuru Suhail ateremke nae akatii bila shuruti, Maswali mengi yakawa yanapita kichwani mwa Suhail bila kuyapatia majibu, alijiuliza au labda ametekwa na majambazi kutokana na habari zilizoanza kuzagaa mjini kua yeye ni mfanya biashara tajiri sana kwa sasa, lakini hakutaka kuamini hivyo kutokana na kwanza huku Bagamoyo hakua akijulikana na mtu yeyote, Pili muonekano wa vijana wenyewe, hasa huyu aliefungua geti alikua akionekana kujawa na furaha isiyoeleweka ni ya nini. Akateremka kwenye gari ile akifuatiwa na dereva wake

    “Karibu sana kaka, tulishaanza kuingiwa na hofu tukadhani hauji tena,” alisema kijana yule alieonekana kama mwarabu vile huku akimpa mkono Suhail, japo Suhail hakuupokea mkono ule wala hakuijibu salamu zaidi ya kuanza kulalama tu

    “Ninyi ni akina nani? Na mmenileta humu kufanyaje?.”

    “Khaa! Kwani we leo ulikuja Bagamoyo kufanyaje yakhee?,” aliuliza kijana yule huku akitabasamu kwa furaha na kumfanya Suhail azidi kuhamaki huku akiamini kua huenda sasa ameuvaa mkondo wa Mzee Shamuhurish

    “Usiniulize swali juu ya swali, nimekuulizeni ninyi mmenileta humukufanya nini?,” aliongeaSuhail kwa jazba huku akiendelea kuyatilii mazingira ya mule ndani kama itawezekana kujaribu kuponyoka lakini alisalimu amri kua hakua na ujanja tena maana uzio ulikua imara madhubuti

    “Nadhani ulikubaliana na Mzee kua leo utakua hapa kwa shughuli maalum, nadhani ndo umekuja hivyo hatuna haja ya kupoteza muda twendeni tu ndani” kijanayule alimalizia kauli yake na kumshika mkono Suhail kisha akaanza kuondoka nae na kuelekea ndani, Suhaila alikua kama aliyemwagiwa maji au kama vile mtuhumiwa anaekwenda kunyongwa kwa jinsi alivyoishiwa mbinu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatua chache wakawa wameingia ndani ya jengo lile chakavu kwa nje lakini kwanda ilikua ni mfano wa ikulu ndogo kwa jinsi lilivyopendeza na kupambwa kiustadi sana, pia palikua na ngazi ambazo ziliashiria kua juu kuna ghorofa inaendelea lakini hawakuelekea huko bali waliendelea kutembea katika sebule ndefu ambayo iliwapeleka mpaka sehemu flani ambapo palikua na ngazi zikiashira kua zinaelekea chini zaidi ‘Underground’. Muda wote huo hapakua na mazungumzo yoyote kati ya Suhail wala kijana yule wa Kiarabu, yule dereva yeye aliishia pale kwenye ngazi za kupandia juu. Hapakua na haja ya kuelekezana chochote wote wakaanza kwenda chini huku Suhail akiwa ameshikwa mkono, Hofu ikazidi kumuingia.

    Safari ikaendelea!



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog