Search This Blog

VITA VYA MAPENZI - 2

 







    Simulizi : Vita Vya Mapenzi

    Sehemu Ya Pili (2)



    Muda wote huo hapakuwa na mazungumzo yoyote kati ya Suhail wala kijana yule wa Kiarabu, yule dereva yeye aliishia pale kwenye ngazi za kupandia juu. Hapakuwa na haja ya kuelekezana chochote wote wakaanza kwenda chini huku Suhail akiwa ameshikwa mkono, Hofu ikazidi kumuingia.

    Safari ikaendelea!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safari ya kwenda chini ilikuwa ndefu kiasi chake maana kila alipohisi kuwa sasa wanafika cha ajabu ngazi ziliendelea tu kwenda chini zaidi, ilikuwa ni kama dakika tano za kuteremka chini ndipo walipowasili sehemu nyingine iliyokuwa ni Tambarare!, ilikuwa ni sehemu iliyosafishwa na kutengenezwa vizuri sana kukiwa kumepambwa kwa mapambo yenye kufanana na yale waliyoyakuta kule. Huku nakshi za milangoni zikiwa za rangi ya dhahabu, Ilikuwa ni kama nyumba ya kawaida tu ila iliyotengenezwa kwa uimara wa hali ya juu, hata hewa yake haikuonesha kuwa wapo sehemu ya chini ya ardhi, pia taa kubwa za umeme zilizo katika maumbo tofauti zilikuwa zikiwaka. Upande wa kulia tokea pale waliposimama akina Suhail palikuwa na Zulia kubwa jekundu huku kwa juu yake kukiwa na Sahani ya shaba, pia palikuwa na kabati kubwa la mbao upande wa kushoto tokea pale waliposimama, halafu kwa mbele yao palikuwa na Korido ndefu inayoonekana kuendelea kwenda ndani zaidi.. Korido ile ilitawaliwa na ukimya na hali ya giza kutokana kukosa taa, ilikuwa ni eneo la kuvutia sana lakini kwa Suhail ilikuwa ni eneo lenye kutisha sana.

    Wakiwa eneo lile walisimama kama dakika mbili hivi ndipo wakaanza kusikia sauti za nyayo za watu zikisogea eneo lile zikitokea kule kwenye Korido ndefu, wote wakageukia upande ule lakini kutokana na giza lile hawakuweza kuona kinachowasogelea, lakini haikuwachukuwa hata dakika moja sauti za nyayo zilizidi kujongea na hatimaye wenye nyayo wakawasili. Lilikuwa ni kundi la watu kama tisa hivi, wakiwa wamevaa kanzu nyeupe huku wamejitanda vilemba vya rangi ya kijani wote kwa pamoja, walikuwa ni watu wenye asili ya ki-asia, Macho yalimtoka Suhail asijue cha kufanya,

    Angefanya nini sasa!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Watu wale wakawasogelea akina Suhail wakawasalimu huku wakiwapa mikono na kuwakumbatia kwa furaha, bado lilikuwa ni tukio lisilo na majibu kwa Suahil, baada ya Salamu ile wote wakafuatana mpaka katika lile zuria jekundu kisha wakaketi kwa pamoja kwa kuizunguruka duara ile sinia. Haikuchukuwa dakika tano ghafla ukafunguka mlango usawa wa lile kabati kubwa lililokuwa upande wa kushoto, kwa harakaharaka usingeweza kutambua kuwa pale palikuwa na mlango kwa jinsi palivyonakshiwa kitaalamu, Baada ya mlango ule kufunguka wakasimama wote kuwashiria kuwa kuna mtu mzito anawasili eneo lile, ndipo sasa macho ya Suhail kwa mara ya tatu ukiachalia mbali mara ya kwanza kule kwenye ajali na mara ya pili kule usingizini, hapa akamuona Mzee Shamhurish akifika na kupokelewa kwa heshma na furaha na wale watu waliokuwa wamesimama, safari hii Mzee Shamhurish akiwa amevaa kanzu nyeupe huku amejifunika kichwani kwa kiremba chekundu kilichomfanya aonekane tofauti na vijana wengine wote mule ndani. Baada ya Salamu Mzee Shamhurish akaketi chini ndipo na wale wengine nao wakaketi

    “Haya bwana Suhail karibu sana Bagamoyo,” alivunja ukimya Mzee Shamhurish huku akimtazama Suhail usoni

    “Ahsante mzee,” alijibu Suhail kwa sauti iliyojaa kitetemeshi cha uoga

    “Kwanza kabisa jisikie huru, jisikie kama upo nyumbani, ondoa hofu na mashaka moyoni mwako. Sisi sote hapa tunafuraha ya kuwa na wewe mahala hapa, sisi ni wenzio hivyo hakuna haja ya kuogopana ili tumalize zoezi lililo mbele yetu.. Hiki ndicho haswa kilichokuleta Bagamoyo na si huko kwa Mzee Atrash, siku nyingine kuwa makini kijana” akajiweka sawa katika zuria lile bwana Sufian Ibn Shamhurish kabla hajaendelea kuzungumza

    “Na kama utakuwa makini sidhani kama yatatokea kama yale ya kule nyumbani kwako Mbezi..” kauli ile ikamfanya Suhail sasa athibitikiwe kichwani mwake kuwa lile tukio lililomkuta usingizini lilikuwa ni la kweli kama alivyoamini, hakuna na cha kuhoji zaidi ya kumsikiliza mzee yule “..Jamani hakuna muda wa kupoteza, huyu ndie bwana Suhail Kusekwa ambaye ni mchumba wa ndugu yenu Bi Shekhia, na leo ndio ile siku yao ya kufunga ndoa ili wakaishi maisha yao kama mume na mke, hovyo nadhani sasa tungeendelea na taratibu za kufunga ndoa hii maana leo nitahitajika kuondoka na kwenda yemen mara moja” Baada ya maneno ya Mzee Shamhurish yaliyouchoma moyo wa Suhail, akasimama mwarabu mmoja hivi mtu wa makamo akaanza kuzungumza

    “..Taratibu zetu ni fupi sana, na kwakuwa Suhail amekubali kuoa na Shekhia amekubali kuolewa hivyo hakuna kingine zaidi ya kuwafungisha ndoa, pia kwa Suhail kutakuwa na mkataba wa matumizi ya ‘Khatam Budha’ ambao atausaini kwa kuzingatia mashart na vigezo..” Baada ya msemaji kufika mwisho akainuka kijana mmoja akakabidhi nakala mbili za mkataba kwa Mzee Shamhurish ambaye nae akakabidhi nakala hizo kwa Suhail ili azipitie na kujiridhisha ndipo aweke saini, Suhail akazipokea nakala hizo akiwa hana ujanja wa kukataa hata kidogo kutekeleza kilicho mbele yake, akaanza kuipitia mikataba ile lakini akili haikuwa pale kabisa, aliweza kuvielewa baadhi ya vipengelea vilivyo ndani ya mkataba ule lakini baadhi hata hakuviona kwa jinsi alivyohamanika, hakuwa katika hali ya kawaida kabisa, kichwa kilishavurugika

    Baada ya kupitia kwa haraka na woga mara punde akawa amemaliza kupitia akazirejesha nakala zile kwa Mzee Shamhurish

    “Umesoma kwa makini?,” alihoji mzee Shamhurish

    “Ndio mzee.”

    “Una uhakika?”

    “Ndio” alipokiri tu akasogezewa kalamu ili aweke saini yake, akafanya hivyo katika mikataba yote miwili kisha akainua kichwa na kumuangalia Mzee Shamhurish alieonekana kuwa na furaha. Baada ya tukio lile akainuka tena Mzee yule alietoa maelekezo ya mkataba ule akaenda mpaka kwenye kabati akatoa bakuli kubwa, alipolitoa tu wote wakasimama, na Suhail nae akaamriwa asimamae kisha wakaongozana mpaka kwenye ile korido ndefu, wakaendelea kutembea kuelekea kule kwenye giza lakini hawakufika mbali wakasimama na kuufungua mlango uliokuwa upande wao wa kulia kisha wakaangia ndani. Kilikuwa ni chumba kama vilivyo vyumba vingine vya mitaani, tofauti yake na uzuri wake na vilivyomo, kilikuwa ni chumba chenye hadhi ya Nyota tano kama ingekuwa ni Hotelini, hapakuwa na vitu vingi sana zaidi ya kitanda kikubwa cha sita kwa sita chenye mtindo wa sofa, Kabati kubwa moja, na ‘Dresing table’ moja iliyochongwa kwa mtindo ambao si wakawaida, na baadhi ya vitu vingine vichache sana mule chumbani. Juu ya kitanda walikuwa wameketi wanawake watatu, wote wamejitanda vizuri kwa Shungi zao. Walipofika pale karibu ya kitanda wote wakasimama kwa heshima ndipo Suhail akamuona vizuri binti aliyekuwa ameketi katikati, alikuwa Shekhia akiwa ametulia kiungwana sana huku macho ameyainamisha chini, japo hakuwa amevaa mavazi yale aliyomuona nayo kule nje

    “Haya tuoneshe mkeo mtarajiwa hapo,” Sauti ya Mzee Shamhurish ilirindima chumbani huku akimuangalia Suhail, haraka Suhail akamsonta Shekhia kwa kidole chake, hapohapo Mzee Shamhurish akawaamuru wanawake wale akiwamo mwanae waketi, kisha yule Mzee alietoa maelekezo juu ya mkataba akarudi nyuma kama hatua tano hivi, kisha na wale wafuasi wengine wa Mzee Shamhurish nao wakarudi nyuma wote kwa pamoja kimyakimya, wale akina dada waliokuwa wameketi na Shekhia kitandani nao wakawafuata wenzao, Suahil alipoona vile nae akataka kurudi nyuma lakini akazuiliwa na Mzee Shamhurish, akabaki amesimama palepale hivyo pale karibu ya kitanda wakabaki wamesimama watu wawili, Suhail na Mzee Shamhurish wakati Shekhia akiwa ameketi kitandani,

    “Ni kitu gani hicho ndani ya bakuli,?” Mzee Shamhurish alimuuliza Suhai

    “Nadhani ni damu hii”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naam ni damu ya mbuzi, sasa vua Pete yako kisha uiweka humo ndani ya bakuli” Suhail akatii agizo lile, akaivua pete ile iitwayo “Khatam Budha’ kisha akaiweka ndani ya Bakuli kubwa lililo na damu. Alipoiweka tu akapigwa na butwaa, Damu ikaanza kupungua ndani ya bakuli, yaani bila shaka pete ilikuwa ikiinywa damu ile, macho ya Suhail yaliendelea kuliokodolea bakuli lile mpaka damu yote ikaisha na kubaki Pete tu ndani yake

    “Hivyo ndivyo utakavyokuwa ukifanya kila baada baada ya mwezi mmoja utapewa maelekezo vizuri, sasa Ichukue na uivae tena,” Mzee Shamhurish alimuelekeza Suhail wakati huo wale watu wengine wakiwa nyuma kabisa huko, alipomaliza kuivaa tu Mzee Shamhurish akahitimisha

    “Kuwanza sasa Shekhia ni Mkeo halali” kisha akampa mkono, hapo hapo wale watu wengine wakasogea wakiwa na furaha wakampa mikono Suhail, ilikuwa ni mikono ya pongezi kwa kufunga ndoa, Suhail hakuelewa hekma ya Kukabidhiwa mke baada ya Pete ile kunywa damu ya mbuzi lakini hakuwa na haja ya kuhoji chochote zaidi kupokea mikono ya pongezi, Kisha Mzee Shamhurish akaendelea kuongea

    “Tutakuwa na tafrija fupi kwa ajili ya furaha hii ya ndoa Saa tatu kutoka hivi sasa, baada ya hapa nitahitaji faragha na Suhail kwa ajili ya kumpa maelekezo ya kuitumia ‘Khatamu budha’ kisha nitaondoka na kurejea Yemen Lakini Suhail na Shekhia mtabaki hapa Bagamoyo kwa siku saba mfululizo, Kuwanzia sasa Suhail utakuwa ndie mmiliki wa Ngome hii yote ya Bagamoyo japo utaamua muishi wapi wewe na mkeo”

    Baada ya maneno hayo ya Mzee Shamhurish watu wote mule chumbani wakaanza kutoka nje kwa utaratibu maalum huku Mzee Shakhurish mwenyewe akiwa mbele yao na kuwaacha mume na mke wakiwa peke yao chumbani, wawili tu..

    *****



    Utendaji kazi katika kampuni ya Bright Future Distributor Ltd inayojijishughulisha na upakiaji na upakuwaji mizigo bandarani inayomilikiwa na Suhail ulikuwa ukilegalega kwa kiasi Fulani huku hofu na Sintofahamu vikatawala Bongo za wafanyakazi karibu wote, kwa jinsi walivyomuhusudu ‘Boss’ wao basi haikuwa suala rahisi wao kuendelea na majukumu yao wakati yapata siku ya tatu ‘Boss’ wao hajulikani alipo, kila alieulizwa hakujua ni wapi Boss wao alipokwenda, Simu zake hazipatikani kabisa. Meneja wa kampuni hiyo Bwana Frank Mkali kwa kushirikiana na na Meneja mwenzie wa kampuni nyingine ya Suhail iitwayo Deseret Insuarence Brokers inayojishughulisha na masuala ya Bima Bwana Kilingo Mkude waliamua tu sasa kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi baada ya kujiridhisha kuwa hali haikuwa sawa maana majibu ya walinzi katika nyumba za Suhail yalikuwa hadhir kuwa Suhail hakuwepo ndani kwa siku tatu mfululizo na hawana taarifa yoyote juu yake huku gari zake zote zikiwepo nyumbani tu, Mr Mkali na Mkude mbali ya kuwa watendaji wakuu katika kampuni za Suhail lakini pia hawa ni jamaa zake wa karibu sana, walisoma wote katika Chuo kikuu cha mlimani japo hawakuwa karibu sana bali walifahamiana hivyo kwa Suhail ilikuwa ni faraja sana kuwapa ajira nzuri jamaa zake wale akiamini kwa kujuana kwao watakuwa waaminifu na wachapakazi wazuri sana, Kwa vijana hawa ilikuwa ni maswali tu ndani ya vichwa vyao kuwa imekuwaje jamaa yao waliotoka nae Chuo amekuwa tajiri ndani ya muda mfupi na hatimaye kuwa muajiri wao? Lakini majibu yasiyo mazito kutoka kwa Suhail yalikuwa yakiwaliwaza kiasi kidogo. Suhail aliwaambia kuwa zile mali zote ni za Mzee mmoja wa ki-Yemeni lakini hataki kujulikana hivyo yeye kwakuwa alikuwa akijuana nae kitambo Mzee Yule akamtaka afungue miradi ile na kuisimamia kama yak wake.



    Baada ya kumaliza kutoa taarifa kituo cha Polisi kila mmoja akarejea katika kituo chake cha kazi kuendelea kuwajibika, Lakini Mr Mkude yeye hakuridhika kabisa akaendelea kuperuzi baadhi ya nyaraka za Suhail zilizomo ofisini mwake ili kama ataweza kupata namba za watu wake wa karibu, Na kweli alifanikiwa kuchukuwa namba kama tatu hivi..



    “Leo asubuhi alikuja hapa Mzee Fungameza kukusabahi lakini ule ujie wako Mnh,” Aliongea Mama Suhail akimpa taarifa mumewe Mzee Kusekwa

    “Najua tu anakuja kunitukana kikubwa, na sina hata cha kujitetea maana nitasema nini sasa,” alijibu Mzee Kusekwa kwa hasira, kikapita kimya cha muda kidogo kabla hajaendelea kuongea Mzee Kusekwa “..Mke wangu ukisikia aibu ndio hii, watu wanajiuliza iweje mtoto amepata ajali lakini hataki kurudi kwao?, mwishowe ataambiwa amewaibia abiria wenzie ndio kaamua kujificha kabisa”

    “Kwakweli huyu mtoto anatuvua nguo sasa, Mzee Fungameza anajua kuwa tulikuwa tunataraji kuwanza mazungumzo ya mipango ya kuwaozesha vijana hawa sasa anaona kimya tu, hapati majibu yoyote sasa hii kama si aibu kitu gani?.” Mjadala ulikuwa mkubwa, hakika wazee hawa walikuwa wamekwazwa sana na kitendo cha Suhail kutokurejea nyumbani tangu alipopata ajali

    “..Na kwambia labda sio mimi Kusekwa ila huyu mtoto atakoma na mimi, siku akitia mguu wake tu Tabora hii anakutana na Ndoa, huko Dar atarejea na mke asinichezee mimi,” Alibwata Mzee Kusekwa

    “Vema aje akiwa salama. Hivi siku ile uliposema umempigia mlikubaliana kitu gani?”

    “Enhee tena umenikumbusha, siku ile simu ilikatika kabla hatujamaliza mazungumzo, nae vile mshenzi hakunipigia tena bila shaka alijua tu kuwa hali ya hatari, sasa nikaweka vocha tena lakini nilipompigia hakupatikana tena, na mpaka kesho yake asubuhi nilimtafuta alikuwa bado hapatikani tu.”

    “Mimi nadhani ungemtafuta tena ili hata kama utakutana na Mzee mwenzio huko ujue unamjibu nini mapema.” Maneno ya Mama Suhail yakajibiwa kwa vitendo na Mzee Kusekwa ambaye harakaharaka alitoa simu yake ili ampigie mwanae, lakini akiwa ameishikilia simu yake akajikuta yeye ndio anapigiwa na namba mpya asioifahamu. Akabofya kitufe cha kijani katika nokia yake ya tochi akaweka simu sikioni na kuongea

    “Hallow”

    “Mzee Shikamoo,” Sauti iliyotoka upande wa pili wa simu ilimuamkia Mzee Kusekwa

    “Marahaba, nani mwenzangu?”

    “Mimi naitwa Kilingo Mkude ni mfanyakazi katika kampuni ya Suhail, namuulizia Mzee Kusekwa”

    “Mfanyakazi katika kampuni ya Suhail?”

    “Ndio, Kwani wewe sio baba yake na Suhail?”

    “Mimi ni baba yake ndio”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa Mzee mimi naulizia tu kama huyu bwana yupo huko?””

    “Huko wapi, mbona haueleweki wewe?”

    “Nina maana huko Tabora, huku Dar hayupo na hajaaga mtu tangu majuzi, simu zake hazipatikani, tumemtafuta kule kwenye nyumba yake ya mbezi hayupo, na hata kule Ilala mlinzi wake amesema hajamuona sasa tumepatwa hofu kidogo”

    “Khaa, Suhail ana kampuni na nyumba Dar?”

    “Mzee hivi wewe ni Baba yake Suhail kweli naona kama hatuelewani!”

    “Hebu ngoja kwanza, emesema Suhail haonekani?Ameenda wapi?”

    “Khaa sasa mzee mimi nakwambia kuwa hajaaga mtu halafu we unaniuliza ameenda wapi? !” Mkude akakata simu na kumuacha Mzee Kusekwa akiwa ameduwaa



    “Vipi mbona hivyo?,” alihoji Mama Suhail kufuatia majibizano yalikuwa yakiendelea kati ya mumewe na mtu asiemjua. Mzee Kusekwa akamuelezea mkewe kila kitu hakika mama Yule nae alibutwaika

    “Sasa haya majanga, Huyu mtoto ametoa wapi Kampuni jamani! Na ametowekaje ghafla! Isije ikawa huyo aliekupigia wewe ni muhalifu na ndie amemteka mwanagu jamani..” Mama Suhail alikuwa akihatahata kwa maneno

    “Hilo nalo neno, hata mimi najiuliza huyu Kijana ametoa wapi namba zangu?”

    “Au mume wangu ulisemezana nae maneno mabaya siku ile ulipoongea nae ndo maana akachukuwa uamuzi huo mbaya?”

    “Hiyo wala haihusiani kabisa, Unajua kuna..” Kabla Mzee Kusekwa hajamalizia kauli yake akakatizwa na mtu aliyekuwa ‘Akibisha’ hodi, ilikuwa ni sauti ya Mzee Fungameza, Ilikuwa ni ghafla bin Vuu, Mzee Kusekwa alitamani ajifiche katika mfuko wa suruali yake, akiwa bado ameishiwa maarifa tayari Mzee Fungameza akaingia ndani na kuwanza kuwasabahi

    “Wenyewe salama humu?”

    “Salama kiasi, karibu bwana mkubwa,” Alijibu Mzee Kusekwa na kumfanya Mzee Fungameza kubaki roho juu

    “Kunani tena jamani?”

    “Mnhuu, si huyu mwanao Suhail..”

    “Kafanya kipi tena?” Mzee Kusekwa akaanza kumsimulia Mzee mwenzie aliyekuwa ametulia juu ya kochi la kukereza huku akisikiliza kwa makini mpaka mwisho wa habari ile japo masuala ya Suhail kuwa anamiliki kampuni na ana nyumba Mbezi na Ilala hakuviweka wazi. ilikuwa ni habari inayoacha maswali mengi kuliko majibu. Baadhi yalikuwa yakiingia akilini na baadhi yakipita tu hewani

    “Haya sasa mapya, Hebu mpigie huyo Mtu ili atujuze habari kamili maana hii si ya kupuuzia kabisa,” hatimaye Mzee Fungameza alivunja ukimya..

    “Tatizo mimi sina namba yake.”

    “Jamani Baba Suhail si umetoka kuongea nae sasa hivi, sasa hauna vipi namba yake?,” aliuliza Mke wa Mzee Kusekwa aliyekuwa ameketi kwenye kigoda

    “Aaah mwenzangu nilishachanganyikiwa mie, hebu itafute humo umpigie,” Mzee Kusekwa alikuwa akiongea huku akimkabidhi simu Mzee Fungameza

    *****

    Katika Kasri la chini kwa chini la Mzee Sufiani bin Shamhurish ambalo kwa sasa linamilikiwa na mkwewe Suhail Kusekwa hali ilikuwa shwari kabisa, hapakuwa na ghasia wala rabsha za aina yoyote zaidi ya raha na burudani za fungate la maharusi wawili, tayari Mzee Sufiani alikwashaondoka na kuelekea zake Yemeni baada ya kuhakikisha amemfundisha Suhail namna ya matumizi ya ‘Khatam Budha’. Suhail alikuwa amejilaza juu ya kitanda cha kifalme, kitanda chenye nakshi za dhahabu na almasi huku akikandwakandwa na kusingwa mafuta na Mnyange Shekhia Bint Sufian, hofu ilikuwa imeanza kuyeyuka mithili ya theluji juani. Akiwa kitandani alikuwa akiitazama ile Pete ya Budha kwa umakini hakika alishangazwa sana na uwezo mkubwa wa pete ile japo aliyaamini maneno ya Mzee Atrash kuwa Mzee Sufian hatomfundisha kila kitu lakini kwa hayo machache tu aliyofundishwa alishangazwa sana, aliamini kuwa atakuwa salama na tajiri mkubwa sana, mambo mawili yatokanayo na Pete ile yalimnyima raha mara kwa mara, la kwanza ni kila alipokumbuka kauli yam zee Sufiani kuwa atawajibika mara moja itakapohitajika kwenda kupambana na kuwaangamiza majini wa Budha endapo wataonesha kugundua alipo mzee Sufiani hata kama itakuwa huko Yemeni Pete ile itampa taarifa maalum na itamchukuwa kwa upepo mpaka huko na kufanya mashambulizi, pili kila alipomfikiria Mchumba wake halali Sharifa alihisi kuzimia.



    Akiwa anaendelea kupata raha kutoka kwa mpenzi wake wa tangu chuoni na hatimaye sasa ni mkewe, Mke mwenye asili ya ujini, ndipo alipokumbuka kuwa hakuiwasha simu yake tangu mara ya mwisho alipoongea na Baba yake

    “Hebu niletee simu yangu iko kwenye Suruali,” Suhail alimwambia Shekhia

    “Simu ya nini tena jamani mume wangu,” alijibu binti Yule mtoto wa Jini kwa deko na maringo

    “Unajua tangu nilipokuja huku simu ile haikuwa hewani, sasa najua tangu nimeshasababisha usumbufu mkubwa kwa vijana wangu wa kazi na hata kwa wazee nyumbani” Shekhia akainuka kitandani kwa kujivuta sana kama mtu aliechoka, akaeiendea suruali ya mumewe iliyokuwa imetundikwa katika ‘Enga’ maalum kisha akaingiza mkono mfukoni na kuitoa simu, akaanza kurejea nayo pale kitandani huku akiiwasha na kumkabidhi Suhail ambaye alipokelewa na meseji nyingi sana utadhani ameizima kwa mwaka mzima. Zilikuwa ni meseji kutoka kwa baadhi ya matajiri anaofanya nao kazi kwa karibu sana, pia akakutana na meseji za Vodacom zikimtaarifu juu ya namba zilizokuwa zikimpigia muda wote alipokuwa amezima simu yake, aliitegemea hali hiyo lakini kilichomshtua zaidi ni simu kutoka kwa Kilingo Mkude na Frank Mkali wasimamizi wa kampuni zake, walionekana kumpigia zaidi ya mara kumi kwa kila mmoja.. ndipo haraka akabofya namba za Mr Mkude na kumpigia

    “Yes Boss,” Alipokea Mkude na kusikilizia kidogo

    “Niambie Mkude”

    “Shwari kaka, are you Okey?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ooo yeah, vipi nimeona mmenitafuta sana!”

    “Ndio kaka, si kawaida yako umetoweka ghafla tukajua umepatwa na matatizo maana tumeanda Mbezi haupo, Ilala nako haupo aisee tukachanganyikiwa kabisa ikabidi sasa tukaripoti Polisi tu,” Majibu yale hayakumfurahisha sana Suhail lakini kidogo ilimfariji kuona yuko na vijana wanaomjali sana hivyo hakuonesha tofauti yoyote, akauliza tena

    “Aisee nilipatwa na udhuru usiokwepeka kaka, haya niambie”

    “Kilichoniacha hoi sasa wakati tunaendelea kukutafuta ndipo nikapata wazo la kuperuzi kwenye ‘Diary’ yako ofisini nikaona namba imeandikwa Baba ikabidi haraka nimpigie il nijue kama uko huko!”

    “Umempigia baba?!,” Suhail alihoji kwa mshtuko kidogo

    “Ndio lakini kila napojitambulisha tukawa hatuelewani maana namwambia mimi ni mfanyakazi katika kampuni ya Suhail akawa anashangaa kusikia unamiliki kampuni, nilipomuambia kuwa tumekutafuta katika nyumba yako ya Mbezi na Ilala ndo kabisa akawa hanielewi lakini…” Kabla hajamaliza kuongea Suhail akamkatiza

    “KILINGOOOOOO.. Umeharibu kila kitu kaka, kwanini umempigia mzee aaakh”

    “Lakini kaka mimi nilipoo..” Kabla Mkude hajamaliza kuongea Suhail akakata simu halafua akafuatishia na tusi kali la nguoni mpaka Shekhia akaonesha mshtuko

    “Vipi mume wangu, kuna nini tena?,” Aliuliza Shekhia huku hiyo ‘Mume wangu’ akiitamkia kwa puani kama mwanamke wa Kitanga, hakika Pumu imepata Mkohozi

    “Yaani hawa wafanyakazi wangu wapumbavu sana, wamenipigia simu wakaona sipatikani, wakaenda kunitafuta kwangu waliponikosa tu wakaenda kutoa taarifa kituo cha polisi kisha kama haitoshi wamempigia simu baba..”

    “Lakini mume wangu ujue siku tatu mfululizo si haba lazima wapate hofu”

    “Hata kama , mimi si mtoto mdogo bana, sasa wameshiniletea taabu kwa Baba maana ameshajua kuwa ninamilikia Kampuni na nyumba kadhaa”

    “Aaah we nae vipi! Mali umiliki wewe halafu umuogope baba yako?Kwa utoto gani ulio nao?”

    “Hapana, unajua habari kama hizo ilipaswa nimwambie mimi mwenyewe na si..” hata hakulifikisha neno lake mwisho Simu yake ikawa inaita, Alikuwa ni Mzee Kusekwa, Tumbo lakimunguruma kwa hofu, akajikaza na kupokea

    “Hallow”

    “Suahil?!,” Alianza kwa kuita jina Mzee Kusekwa, ilikuwa ni sauti iliyjawa na hofu kubwa sana, kwakuwa Suhail alikuwa ameshajua kuwa Mzee wake alazima angekuwa katika hali hiyo baada ya kuwambiwa kuwa kijana wake ametoweka ghafla

    “Una matatizo gani?”

    “Niko salama tu baba, nilikuwa safari ya dharura Nairobi ndio nimerejea sasa hivi”

    “Nairobi kufanya nini we Mtoto?Hivi Suhail kwanini unataka kunitia jaka moyo we mototo?”

    “Baba kwani kuna nini?”Suhail alijifanya hajui kinachoendelea

    “Yaani pilipili yangu mwenyewe inanitoa kamasi sasa, umekuwa haueleweki kabisa, jangili si jangili, gaidi si gaidi, au umejiingiza katika makundi mabaya we mtoto? Sasa nasema hivi mimi kama baba yako, Kesho naomba uwe Tabora Laa sivyo mimi sio Baba yako utamtafuta aliekuzaa, umenielewa?..” Mzee Kusekwa alikuwa akiongea mpaka povu lilifurumia mdomoni, alipoona hajajibiwa akahoji tena “..Umenielewa wewe?!”

    “Ndio Baba. Lakini,” Suhail alijibu, na alipotaka kuongeza neno simu ikawa imeshakatwa, Akaishia kushusha pumzi kwa nguvu, Kimya kikatawala ndani ya Kasri la Bagamoyo.



    “Vipi imekuwa?” Shekhia alivunja ukimya

    “Jiandae tuondoke sasa hivi, maji yameshazidi unga”

    “Hee jamani Twende wapi sasa?”

    “Twende Dar es Salaam, inabidi kesho asubuhi niende Tabora baba anasema nisipoenda basi nitafute baba mwingine, hii sasa hatari”

    “Uende Tabora au twende Tabora”

    “Ukafanye nini?”

    “Ukanitambulishe kwa wakwe zangu”

    “Tafadhali usinikoroge kichwa, nadhani tulikwishaliongea hilo kuwa haliwezekani kutokana na hali ya nyumbani” Suhail alijitutumua na kujibu kiukali kidogo japo alijua kuwa nguvu za Shekhia hawezi kupambana nazo ila kwakuwa alijua kuwa anapendwa sana na jina mtu Yule hivyo aliitumia fursa hiyo ipasavyo, Shekhia akanywea, wakakubaliana na kuwanza maandalizi ya kurejea Bagamoyo na walikubaliana kufikia Mbezi ili isiwe rahisi kwa jamii inayomfahamu kumtilia shaka.



    Masaa mawili Baadae walikuwa Mbezi, mipango ya safari ikaratibiwa kwa haraka ili kesho yake awe Tabora,

    *****

    KIASI cha saa nne asubuhi ndege ya FastJet ilishusha matairi yake na hatimaye kushuka katika Uwanja wa Ndege mkoani Tabora ikiwa inatokea jijini Dar es Salaam. hapakuwa na pilikapilika ya watu uwanjani hapo kama ilivyozoeleka katika viwanja vikubwa vya ndege vilivyopo katika majiji kama vile Arusha, Mwanza, na Dar. Uwanja huu ulitawaliwa na mafungu ya watu wachache waliohudhuria uwanjani hapo bila shaka kuwapokea wageni wao. Suhail Kusekwa alikuwa ni miongoni mwa Abiria walioteremka katika Ndege ile ya wastani huku mkononi akiwa na Begi moja tu kubwa huku macho yake akiwa ameyaficha ndani ya miwani myeusi. Aliinua mkono wake wa kulia na kuwangalia majira kupitia saa yake ya mkononi huku Akiendelea kutoka uwanjani hapo baada ya kukamilisha taratibu zilizowekwa makhsusi kwa ajili ya usalama kisha akainua kichwa juu akiangalia dereva Teksi yoyote wa kumchukuwa mpaka kwao. hakuwa na haja ya kuwaangalia watu waliokuwa wakipokea ndugu zao kwaku alijua hakuna alikwenda kumpokea kwakuwa hakutoa taarifa ya ujio wake kwa mtu yoyote. Akaenda mpaka akatoka katika geti maalum la kutokea uwanjano hapo, akamuona kijana mmoja dereva wa teksi akiwa tayari ameshafungua mlango wa gari yake huku akimuoneshea kwa Ishara Suhail kuwa amefungua mlango ule kwa ajili yake, ni uchangamfu wa kibiashara tu!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Twende afisa tuwahi,” Aliongea dereva Yule huku akionesha shauku ya kumbeba mteja yule alieonekana ‘Matawi yaj uu’ kwa jinsi alivyo ‘Vunja kabati’ kwa vitu alivyonyuka, Miwani ghali usoni, Mkononi kuna saa aina ya Oxlux, Jinzi ya Deckies, na Shati kali la ‘draft draft’ na miguuni ameji’komelea’ raba kali za Reebok

    “Mambo vipi kaka?,” Alisalimia Suhail baada ya kuwa ameketi ndani ya Teksi ile na wakati huo dereva nae akiitoa gari barabarani kuianza safari

    “Poa mkubwa, Hongera kwa safari”

    “Hivi hua ni Hongera kwa safari au Pole kwa safari?” Suhail alihoji kwa hali ya mzaha, na majibu aliyopewa yalikuwa ya mzaha kama ambavyo alivyotania yeye

    “Aah Pole wanapewa wanaoshuka kwenye gari moshi huko kaka, ila we ulikuwa kwenye ‘Mwewe’ hata haujui kwanza umefikaje hapa” Kicheko kikafuata kabla ya Dereva kuwanza kuhoji muelekeo wa safari yao,

    “Tunaenda mtaa wa Rufita.”

    “Oooh kule kwa akina Mheshimiwa Rage”

    “No, kule inakuwa mbele sana, mimi naishia mwanzomwanzo tu”

    “Au pale karibu ya Berenja Hotel?”

    “Enhee Kwa mbele kidogo sasa kuna Kona inayoingia mtaa wa Usagara”

    “Nimekupata, hiyo kona inakuwa kulia wakati kushoto kuna nyumba moja kubwa ya zamani hua kuna bi mkubwa mmoja hivi hua anapika vitumbua pale”

    “Duuh kaka inaonesha we mwenyeji sana na mitaa ile? Umemjua mpaka Bit Rajab Kanyoro muuza vitumbua mashuhuri wa tangu dahar” Dereva Teksi akacheka kidogo kufuatia swali la Suhail

    “Si unajua tena kaka Kazi zetu zinatupasa kuyajua maeneo mengi zaidi ili kurahisisha utendaji kazi”

    “Ok vizuri, basi ni maeneo hayohayo ukishakatiza hiyo kona basi kwa mbele kidogo tu Nyumba yetu inatazamana na nyumba moja hivi ina Ofisi kubwa ya mafundi wa mageti ya kuchomelea na ya ‘Aluminiam’..”

    “Aaah kumbe hapo, nimekusoma mkuu, hapo kwenye hao mafundi ni kwao na jamaa mmoja hivi alwatan sana anaitwa Kijukuu cha Soud”

    “Eee bwana eeh hapohapo, aisee nimekuvulia kofia, we ni hatari” wakacheka tena kwa pamoja kisha Safari ikaendelea



    Ni mbali kiasi chake kutokea ulipo uwanja wa ndege mpaka mjini kati yalipo makazi ya watoto wa mjini, hivyo iliwagharimu kiasi cha dakika thelathini ama telathini na tano hivi mpaka upeo wa macho yao yalipoanza kushuhudia Soko, Shule nyingi, Bank, ofisi za mashirika makubwa, purukushani za waendesha baisekeli na waenda kwa miguu, ikawa ni ishara tosha kwao kwamba wameingia mjini Tabora. na kutokea mjini kwenda mtaa wa Rufita ni umbali kama wa dakika saba tu, sidhani kama ni haram ukisema kuwa Rufita ni mingoni mwa mitaa ya mjini.



    “Shilingi ngapi kaka?,” Suhail aliuliza bei baada ya kuwa gari imeegesha nje ya nyumba yao

    “Elfu Saba tu kaka” Suhail hakujibu akaingiza mkono mfukoni akatoa noti ya shilingi elfu kumi akampa dereva

    “Chenji utanunua soda kaka”

    “Oooh ahsante sana mtu wangu, Mungu akubariki,” Alijibu dereva na kumuacha Suhail akiteremka na begi lake mkononi kasha yeye akipiga msele na kuwacha vumbi hafifu wakati anaondoka



    Mlango wa barabarani ulikuwa wazi lakini sebuleni hapakuwa na watu hivyo Suhail akaingia moja kwa moja na kwenda kupigia hodi angali sebuleni kabisa,

    “Hodi wenyewe”

    “Karibuu,” Mama Suhail aliitikia akiwa uani na wanawe na mumewe wakipata zao Chai na viazi vitamu vya kuchemsha almaarufu kama ‘Vinumbu’ au ‘Ndombolo ya Solo’ na asali kwa pembeni. Suhail akapitiliza mpaka uani, alipofika tu akakutanisha macho yake na wanafamilia, hakuna alieamini kumuona kijana Yule, wadogo zake watatu mmoja akiwa wa kike kwa shangwe na kelele za furaha, wakaacha sinia la viazi likishangaa tu wakamkimbilia kaka yao na kumrukia kama Simba achezavyo na wanawe, Mama mtu nae uzalendo ukashinda nae akatoka mbio huku akijifunga khanga yake vizuri na kwenda kumlaki kijana wake alieondoka kitambo. Mzee Kusekwa nae akawa amesimama tu huku akiwa hana hata kumbukumbu ya alipozipotezea hasira zake alizolala nazo usiku kucha, akajikuta tu sasa nae ‘Akiganyala’ kama dume la nyani taratibu akaenda kupokea Begi la mwanae na kulipeleka ndani huku mkononi akiwa na gilasi ya maziwa mgando almaarufu kama Mtindi au ‘Mbobhoto’ kwa pale Tabora



    “Haya jamani habari za masiku tele?” aliuliza Suhail baada ya kuketi katika kigoda huku akitembeza macho yake kwa kila mmoja pale uani kwao, alipozaliwa na kukulia

    “Yaani hata siamini jamani, haya kwanza ni Basi gani ulilopanda la kukufikisha Tabora saa hizi?”

    “Mama bana, nimekuja na Ndege” Jibu la Suhail likawafanya wazazi wake waangaliane kwa macho ya kuulizana

    “We Suhail pesa ya kupanda Ndege umetoa wapi we mtoto ?” Safari hii swali lilitoka kwa Mzee Kusekwa

    “Baba dunia imebadilika sasa hivi, hakuna cha ajabu tena, hata wewe utapanda tu tuombe uzima, hebi nipeni maji ya kunawa kwanza nipate chai mie” Haraka wadogo zake wakamsogezea maji akanawa na akaanza kujipatia ‘Vinumbu’ vyake taratibu

    “Duh jamani Tabora yetu haibadiliki kabisa, nilitegemea kuwa nitakuta hali ime’change’ hata kidogo lakini wapi,” Suhail alivunja ukimya

    “Yaani huu mkoa sijui ni nini hasa, nasikia eti wanasema kuna Sharifu sijui alioachiaga laana zamani sana” Majibu ya Mzee kusekwa yalisababisha kicheko kikanguruma pale uani kabla ya Suhail kujibu tena

    “Aah baba hizo ni imani tu lakini kama watapatikana viongozi wenye dhamira safi hakika patabadilika tu”

    “Sio viongozi tu, yatupasa wanachi sote tuwe na nia ndio mabadiliko yatakuja” Basi ikawa ni habari za hapa na pale mpaka zoezi la kupata chai likakamilika, ndipo wakahamia sasa Sebuleni kwa ajili ya mazungumzo, wakati huo wadogo zake Suhail wakiondoa vyombo walivyovitumia kupatia kifungua kinywa chao na kuviosha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Haya kwanza pole kwa mkasa wa ajali” Alianza kuongea Mama Suhail huku akimuangalia mwanae wa kwanza kwa furaha

    “Aisee ahsante, ilikuwa ni balaa” Kimya kikatanda kidogo kabla ya Mzee Kusekwa nae kuongeza neno

    “Enhee haya hebu tuambie ilikuwaje siku hiyo ya ajali maana leo tunaongea huku tunacheka pengine saa hizi tungekuwa tunaongea mengine kabisa” Suhail akaanza kuwahadithia jinsi safari ilivyokuwa mpaka walipopata ajali na ilivyokuwa mpaka akaokoa na kuwamua kurejea kwanza Dar, katika simulizi yake hiyo alificha mambo mengi sana ikiwemo kuhusu Mzee Shamhurish, pia aliunda habari ya uongo kuwa alipata lift ya kurjra Dar hivyo akaona ni bora atumie fursa hiyo ili kujiepusha na mshikemshike pindi wanausalama watakapo wasili eneo lile, Habari ilikuwa ni nzuri nay a kusikitisha ukizingatia ajali iliondoka na roho za watu, wakati simulizi ikiwa inafikia tamati Mzee Kusekwa akamuita mwanae wa kike ambaye ni Mdogo wake na Suhail akampa kazi ya kukamata Jogoo mmoja bandani kwake kwa ajili ya Takrima kwa mgeni,

    “Haya ikawaje tena mwenzetu ukang’ang’ania Dar mpaka tunataka kutoleana radhi?” Suhail akatoa historia ndefu ya uongo “Unajua ile ajali iliniathiri sana kwa ndani lakini mwanzo sikujielewa, sasa nilipofika Dar baada ya kufanya vipimo ndipo nikajibaini kuwa sikuwa sawa sana ndipo nikaanza kupatiwa matibabu

    “Pesa ya matibabu ulitoa wapi?,” alisaili Mzee Kusekwa

    “Ndio nakuja huko baba, usiwe na haraka. Wakati nilipohitimu tu masomo nilibahatika kukutana na Mzee mmjoa hivi ana asili ya kiasia akawa anatafuta kijana mmoja muaminifu aliesoma fani ya biashara kwa ajili ya kumsimamia kazi zake kwakuwa yeye mara nyingi anakuwa nje ya Nchi, ndipo kuna mwalimu mmoja akanipendekeza mimi, nikawa nimefahamiana na Mzee Yule na tukaingia mkataba mzuri tu wa kazi na kwakuwa hakutaka kuwandika jina lake kwenye makampuni yake hivyo akaniambia kuwa makampuni yote anayofungua yatakuwa kwa jina langu hivyo watu wengi wanajua makampuni yale ni yangu na mpaka vijana walioajiriwa wananijua mimi kuwa mmiliki wa makampuni hayo hivyo wote wananiita Boss..”

    “Alhamdulillah mwanangu na wewe sasa umekuwa Boss, Mungu ashukuriwe jamani, hata siamini.. Sasa na wadogo zako hawa wakimaliza tu Shule uwapachike huko..” Aliongea Bi Mkubwa yule kwa furaha sana lakini alikatishwa na mume wake aliyekuwa na hoja nyingi kichwani mwake

    “Wee Mama Suhail acha kupenda sana hela we mwanamke zitakuja kukutokea puani, unamjua huyo mtu anaempa tu mwanao mali kiajabuajabu mpaka unashabikia tu? Badala uhoji umekalia tu ulimbukeni” Alibwata Mzee Kusekwa huku akimuangalia mkewe kwa wahka, akageuza macho yake mpaka kwa Suhail akataka kuhoji juu ya hizo nyumba inazosemekana nazo ni za kwake lakini akajua tu jibu litakuwa kama la kwenye umiliki wa kampuni kuwa ameziandikisha kwa jina lake lakini si za kwake akajua ameshafilisiwa hoja akatulia na kuwanza tena

    “Suhail mwanangu nisikilize kwa makini sana.. umekuja Tabora leo umetukuta wazazi wako wote, Una Baba hapa na Mama pale lakini hofu yangu usije ukaondoka ukiwa na Mama tu badala ya wote wawili, kitu ambacho ni hatari sana katika maisha yako yote yaliyosalia..”

    “Kwanini unasema hivyo baba, kufa ni mipango ya Mungu tu naweza kuwanza hata mimi ninyi mkabaki”

    “Sina maana hiyo mwanagu..” Alijibu kwa utulivu Mzee Kusekwa kisha akamuangalia mkewe na punde akayarejesha macho yake kwa Suhail na kuendelea “Kukosa kwako baba si mpaka afe tu hata atakapokuwambia kuwa hana motto wa aina yako, usingekuja leo nisingebadili kiapo changu nilichokuwapia kwenye simu kuwa sitakuwa baba yako tena.. Nashukuru Mungu umekuja na sasa nakupa kiapo kingine mwanangu unisikilize kwa makini sana..” Kabla hajamalizia kuongea akakatishwa tena na mkewe

    “Lakini mume wangu mbona unaendekeza sana tabia ya viapo kwa watoto? Si vizuri ujue”

    “Umemaliza?!” alihoji Mzee Kusekwa huku akimtumbulia macho mkewe kana kwamba ameongea pumba, alipoona hajajibiwa akaendelea “..Nitaendelea kuwa baba yako endapo utaondoka hapa Tabora na kurejea Dar ukiwa ni mume wa Sharifa, kinyume na hapo mimi sitakuwa baba yako” Maneno yale yaliwafanya familia nzima iliyokuwa imejumuika pale Sebuleni ibutwaike,

    “Lakini baba kwanini imekuwa ghafla hivyo? Hili suala linahitaji muda na pesa pia”

    “Muda wa nini tena? Tangu ulipokuwa shuleni sisi kama familia na wewe ukiwemo tulikubaliana kuwa tutasubiri umalizapo tu masomo utarejea kufunga ndoa, Je muda wote huo unaona hautoshi? Kama haukutosha muda huo basi hakuna muda utakaotosha kamwe, pili hilo la kuhusu Pesa usilirejee tena mbele yangu maana mimi ni mtu mzima sipendi kufanywa Juha.. Pesa gani unazohitaji tena zaidi ya hizi ulizozitaja mwnyewe hapa!..” Kimya kikatanda huku mawazo sasa yakikishambulia kichwa cha Suhail, hakuwa na hamu hata chembe ya kuchokoza vita na Shekhia wala baba yake Mzee Sufian Bin Shamhurish kwa hicho anachotaka kukifanya Mzee Kusekwa, kila mmoja sebuleni pale alizama katika tafakuri kivyake “..Sijui kama unakumbuka kipindi kile unasoma Sekondari ya Isevya jinsi ilivyotaka kuwa songombingo hapa baada ya Mzee Fungameza kuwambiwa na wale waalimu wenu kuwa unajihusisha kimapenzi na binti yake, lakini tulikaa na bwana Yule tukayaongea na kuyamaliza kiutu uzima, usidhani amesahau na hata ulipopatwa na ajali tulishirikiana nae kwa karibu kama mwanafamilia.. Mlipohitimu shule na kuwa watu wazima wenyewe mkaridhia kuwa wachumba na kuwahidiana kufunga ndoa mbele yetu sasa leo unataka kusuasua wakati kila sababu ya kulitekeleza hilo ipo! Narudia tena kuwa mimi kama Baba yako nasema hivi Tabora utaondoka na mke” Alihitimisha Mzee Yule mwenye msimamo wa aina yake, kimya kikatanda tena huku upepo ukipiga kwa mbali kupitia madirishani, Ikawa ni zamu tena ya Mama Suhail kuvunja ukimya “Ila katika hilo hata mimi sina kipingamizi, Suala la ndoa halikwepeki kwa sasa japo hua sipendi hiyo tabia yako bwana wewe ya kuwapizaapiza watoto..” Aliongea kwa ustadi na utulivu Mama Suhail na kumfanya sasa Suhail ahisi kuwa hana mtetezi katika hilo, alijaribu kadri ya uwezo wake kujitetea bila mafaniko mpaka mjadala ukafungwa

    “Leo jioni nitaenda kuongea na Bwana Fungameza juu ya utekelezaji wa hili jambo lakini kabla sijaonana nae nahitaji wewe uonane nae, tena ikiwezekana sasa hivi uende nyumbani kwake.. hakuna kazi ngumu utakayoenda kuifanya huko zaidi ya kuonesha heshma na kumjali kwa kwenda kumsabahi kabla yeye hajazisikia habari mjini huko kuwa umekuja”

    Hilo likapita bila kupingwa, mazungumzo mapya yakachukuwa nafasi japo akilini mwa Suhail hakuwepo kabisa pale alimfikiria Shekhia, akamuwazia Sharifa kila mmoja kwa vitimbi vyake kasha akajisemea kimoyomoyo



    ‘Amaa kweli hivi ndivyo vita vya mapenzi alivyoniasa mzee Atrash’



    Akatoka nyumbani kwao akiwaacha mama na ndugu zake wakimuandalia chakula japo hakuwa tena na hamu ya chakula chao, alipofika nje ikambidi sasa aingie nyumba kadhaa kwa majirani wao wa karibu kwa ajili ya kuwasabahi, na kutokana na mkasa wa ajali uliovuma kila kona akajikuta anapoteza muda mrefu wa mazungumzo katika kila nyumba aliyoingia, hata kufikia saa sita akawa ndio tena amerejea barabarani akielekea mjini akachuke usafiri wa kumfikisha Chemchem kwa Mzee Fungameza, Baba yake na Sharifa japo hakuwa amemtaarifa hata Sharifa kuwa amewasili, alitembea kwa miguu katika mtaa wa rufita mpaka alipofika mwanzoni kabisa mwa mtaa ule ambapo unakutana na Barabara kubwa inayokatisha mbele ya Soko Kuu la Tabora, sasa kabla hajafika huko mbele ikambidi asimame kidogo nje ya hotel ya Berenja kwa pembeni kidogo kuna Mkungu mkubwa ambapo kila siku iendayo kwa Mungu hukusanyika watu wa rika zote kwa ajili ya kupiga soga huku wakinogeshwa na michezo mbalimbali ikiwemo Bao, Draft, Rudo, Dhunna, Keram, na Pool table, kila mchezo ulijizolea washabiki wengi sana kutoka karibu kila pembe ya mkoa wa Tabora, Eneo hilo la mkunguni pia lilibarikiwa mvuto wa kibiashara bila shaka kutokana na idadi ile ya watu hivyo huduma kama Chakula, vinyaji, kahawa, Studio za muziki, Vinyozi, matunda nk vilishamiri sana. Sasa kutokana na umaarufu wa Suhail pamoja na baba yake basi ajali ile iliyopata kumkuta Suhail ilijadiliwa vilivyo kila mmoja akiwa ni gwiji wa kusimulia, basi alipowasili pale kijana Yule akapokelewa kwa Shangwe ya aina yake huku kila mmoja akitaka kumsikia Suhail mwenyewe, ikamchukuwa karibu nusu saa nzima kuiongelea ajali ile huku akijibu maswali kadhaa kutoka kwa wazee na vijana wenzie, akajitahidi kuyafupisha mazungumzo ili sasa awahi kwa Mzee Fungameza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyumba ya Mzee Fungameza ilikua katika hali yake ya ukimya, hapakua na bughdha ndani ya nyumba ile bila shaka ni kutokana na ukweli kwamba hakuna watoto wadogo wala idadi kubwa ya watu wazima zaidi ya Mzee Fungameza, Mama Sharifa, Sharifa mwenyewe na mdogo wake Sharifa ambae mara nyingi hua shuleni huko. Suhail akapitiliza mpaka ndani, alipofungua mlango tu akakutana ana kwa ana na Sharifa ambae hakika uzalendo ulimshinda akavibwaga vyombo alivyokua akipatia chakula akatimua mbio kumkimbia mchumba wake akamrukia na kumkumbatia huku akicheka na kubwabwaja maneno mengi na matamu yasiyomithilika, Suhail nae akajikuta katika hali ya furaha kiasi cha kumsahau kwa muda Shekhia,

    “Yaani hata siamini Suhail, halafu kwanini umekuja bila taarifa we mwanaume?”

    “Nilitaka kuku Surprise mpenzi wangu,” Alijibu Suhail huku akifuatishia tabasamu lake pana, kisha kabla Sharifa hajaongeza jambo lolote Suhail akamtoa maungoni mwake alipokua amemganda kama Ruba

    “Mbona unanitoa?”

    “Baba yupo?”

    “Ndio yumo kule ndani kabisa”

    “Sasa akitokea ghafla hapa?”

    “Hee jamani kwani hajui kama mwane nimeshapenda?” wakaangua kicheko cha pamoja kabla ya Suhail kuongezea

    “Tena umekufa umeoza.. Sasa potezea kwanza, acha nikamsalimie” Wakaachana na Suhail akaingia ndani moja kwa moja mpaka ‘Seating room’ huku akimuacha Sharifa akiwa hana tena hata haja ya kula



    “Owhoo, we bwana leo nd’o umeibuka kama nyota ya Jaa,’ Alitania Mzee Fungameza baada kumuona Suhail akiingia ndani, akaacha haraka kitabu pale juu sofa lake akasimama na kumsogelea Suhail, akampokea kwa furaha huku akimkumbatia na kumkaribisha baada ya kusalimiana

    “Karibu uketi.”

    “Ahsante sana, habarini za hapa tu”

    “Ah nzuri tu pole na misukosuko”

    “Tumeshapoa midhali nimerejea salama nashukuru Mungu” Baada ya Salamu michapo ikaendelea kwa muda mrefu mpaka na mama Sharifa aliekua amelala nae akaamka na kujumuika nao pale katika makochi. Baada ya maongezi ya muda mrefu Suhail akaaga ili aondoke japo alikumbana na vipingamizi vya hapa na pale akilazimishwa akae kwa ajili ya kupata chakula cha mchana alipambana nao mpaka wakamuelewa na kumuacha akiondoka, wakamtoa mpaka barabarani hivyo kumnyima fursa Sharifa kuongea lolote tena na Mchumba wake,



    Lakini hakikuharibika kitu, Simu zilitenda kazi!



    *****



    Suhail alirejea nyumbani kwao kwa ajili ya kupata chakula cha mchana, ilikua ni mahanjumati kwelikweli, Pilau lililokolea zabibu na Abdalasini, Mchuzi wa kuku uliungwa shatashata kwa nyanya za kuchuna.. Unaweza kujiuma ulimi aisee, Familia nzima ilijumuika pamoja kupata wasa’a mzuri wa chakula wakiwa pamoja. safari hii hapakua na mazungumzo mengi zaidi ya kuwapa salamu kutoka kwa Mzee Fungameza, wakati akiwa nyumbani kwao alikua akiwasiliana na mchumba wake Sharifa na wakakubaliana kua ifikapo saa kumi alaasiri wakutane katika hotel ya Saratoga iliyopo maeneo ya Bachu ambapo watachukua chumba ili wapate faragha tulivu ya kupiga stori zao huku Suhail akidhamiria kupasua ‘jipu’



    *****



    Mashariki mwa chumba Kochi moja aina ya sofa lenye uwezo wa kukaliwa na watu wawili liliegeshwa ukutani chini ya dirisha kubwa lililofunikwa upande mmoja kwa pazia pana. Laiti kama kochi hilo lingekua limekaliwa na mtu basi macho ya mtu huyo yangekua yakitazamana moja kwa moja na Kioo kikubwa cha Luninga aina ya Hitach iliyokua ikionesha tamthiliya ya kihindi kiasi cha kufanya nyimbo za malalamiko ya mahaba kutawala Chumba kile kilichopo Ghorofa ya tatu katika hotel ya Saratoga. Pembezoni mwa Luninga ile palikua na mlango mdogo unaoingia moja kwa moja mpaka maliwatoni, na kukiacha Kitanda kikubwa cha sita kwa sita kikiwa sentimeta kadhaa kutoka katika mlango huo, Juu ya Kitanda hicho walikua wamejilaza vijana wawili wapendanao huku kila mmoja akiwa na lake kichwani. Suhail kusekwa akiwa amevalia jinzi yake safi pamoja na fulana yake mchinjo alikua amejilaza chali kitandani hapo huku akitafakari namna bora ya kuanza kumaliza ‘Mzozo’ uliokua ukimsukasuka moyoni Wakati Msichana aliekua amemlalia kwa juu usawa wa kifuani huku amevalia Suruali yake laini na fulana nzito alikua akiiwazia ndoa tu aliyokua akiisubiri kwa hamu kitambo kirefu.. Hakika moyoni kwa mtu mbali, hakuna aliejua mwenzie anafikiria nini muda ule!

    “Leo nilipanga nikawasalimie jamaa zangu pale kijiweni kwao,” Suhail alivunja ukimya uliokua umetawala baada ya kua wameshasalimiana na kuoongea mambo mawili matatu tangu walipoachana mara ya mwisho na habari za ajali iliyomsibu mpaka aliporejea Dar na kuanza kazi

    “Hivi kumbe haujaenda tu?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Huo muda ningeupata saa ngapi sasa? Yaani kila napopita inanibidi nikae karibu nusu saa kuongea..Kuanzia nilipotoa mguu wangu nyumbani kwa Mzee Kusekwa nikaanza kukutana na watu tunaofahamiana, Rufita nzima nilikua nikisimama simama, na pale Mkunguni ndio nilikaa sana, mara Kwa Mzee Fungameza..”

    “Wee Sio Mzee Fungameza, sema Baba Mkwe’” Sharifa alimkatisha mchumba wake kwa utani, kikafuata kicheko kidogo kabla ya Sharifa kuendelea “Unadhani hata utapakumbuka hapo kijiweni kwenu?”

    “Kumekuwaje kwani?”

    “Wamepaboresha hadi raha, ukifika tu barabara ya ujiji pale kwenye Kona inayoungana na mtaa wa Heri, nyumba kama ya tatu tu hivi Utaona Bango Kubwa likinadi MIKINDA PROJECTS CAMP(MPC) na anuani zao pamoja na huduma zitolewazo ofisini hapo..”

    “Aisee wamekua na ofisi kabisa inayotoa na huduma? Safi sana”

    “Ndani kuna huduma za kifedha, huduma za Steshenari, malipo ya umeme nk, huku kwa nje kuna vijana wa bodaboda wameegesha pikipiki zao na biashara ndogondogo zikiendelea, Camp ile imekua sana yaani nd’o kioo cha vikundi vyote vya hapa mjini kwa sasa”

    “Safi sana, sasa wamejichanga wenyewe ama nani amewafadhili?”

    “Wao wenyewe tu lakini pia si unajua tena wanasiasa wakishaona kipindi cha uchaguzi kinaanza nao nd’o wanajifanya kuwajali na kuwawezesha vijana, sasa nasikia kuna Mheshimiwa mmoja anautaka ubunge nd’o kawawezesha lakini wengine wanasema kua ni wao wenyewe wamejichanga, nafikiri ukienda kwakua wewe ni jamaa zako watakupa ukweli wa mambo” Alijibu Sharifa kisha mazungumzo mengine yakashika kasi, Iliwachukua muda mrefu kuongea huku wakiliwazana kwa maneno matamu ambayo kwa kiasi kikubwa yalikua yakitoka kwa Sharifa huku Suhail akijikuta akiwa na mchombezaji tu mpaka giza la Magharibi likaanza kuingia..

    “Sharifa mpenzi wangu kuna jambo moja kubwa sana na la muhimu nahitaki kuongea na wewe leo.. nahitaji umakini wako na Subra kubwa katika hili..” Suhail alianzisha sasa mjadala alioukusudia na kumfanya Sharifa ajitengeneze vizuri katika kifua cha kijana Yule, kisha bila ya kujibu chochote akaendelea kusikiliza “Mimi na wewe tuna historia ndefu sana tangu tuliingia katika mahusiano yetu, tukapambana na vikwazo vingi kuanzia kwa baadhi ya wanafunzi wenzetu pale shule, kwa walimu, na hatimae kwa wazazi wetu.. Tukaishinda vita ile huku tukikubaliana kua yatupasa tuishinde vita ya pili ambayo ni kutokukutana kimwili mpaka siku ya ndoa yetu, hakika vita ile tuliishinda ingawaje ni sahihi zaidi endapo nitasema kwamba wewe ndie ulieishinda zaidi.. Sasa kuna vita ya mwisho yatupasa tuishinde pia..” Kufikia hapo Suhail akatulia kidogo ili kuruhusu maneno yale yapenye kichwani mwa Sharifa,

    “Una maana gani Suhail, usiniambie kua ulinisaliti huko Dar?” alibwata Sharifa kwa sauti ya juu huku akijiinua kutoka kifuani kwa Suhail ambae alimzuia na kumrejesha katika himaya yake kisha akaendelea

    “..Nasema wewe ndie ulieishinda ile vita kwasababu uliyatekeleza makubaliano yetu kwa lengo lilelile makhsusi ukiamini siku ya ndoa yetu tutafurahia kwa pamoja.. Tofauti na mimi nilieishinda vita hiyo kwa kushinikizwa zaidi na matakwa ya mwili wangu” Suhail akavuta pumzi huku akitafuta maneno mazuri ya kuyatumia kwa ushawishi alioupanga “…Mimi pia nimejizuia kama wewe japo mimi ni zaidi ya wewe.. Wakati wewe ukijua kua uvumilivu huo una mwisho wake ambao ni siku ya Ndoa yetu lakini kwangu mimi hali iko tofauti kwani nitaendelea kua katika hali hii ya kutokukutana na wewe na hata mwanamke mwingine kiasi cha maisha yangu yote yaliyobaki hapa duniani..”

    “We Suhail mbona sikuelewi wewe?” Sharifa alimkatisha Suhail kuendelea kuongea huku akijitoa kwa nguvu toka pale kifuani alipokua amejilaza, hali ya hatari ilishabisha hodi moyoni mwake

    “Sikukueleza hili tangu tulipokua shuleni pamoja, Mimi mwenzio ni Mbovu… siwezi kua Mume kwa mwanamke yoyote katika dunia hii, sipaswi kufunga ndoa kisheria..”

    “Whaaat?!” Alimaka mwanadada yule kwa sauti kali huku akiendelea kuongea kwa ghadhabu “Siamini kabisa.. siamini Suhail, yaani umeona mimi ni bwege kiasi hiki? Umeamua kuniacha kwa kwa ‘Style’ hii!!! Haiwezekani” Sharifa aliendelea kulalamika kwa sauti ya uchungu kiasi cha kuanza kutiririsha machozi usoni mwake, Suhail aliekua kimya muda wote wakati Sharifa akilalama alijiinua kitandani ili ambembeleze mchumba wake lakini aliambulia patupu, Sharifa alimsukumia kwa nguvu kitandani kisha akaendelea kulia kwa sauti “Suhail kwanini unataka kunifanyia hivi lakini? Nimekukosea nini we mwanaume? Kumbuka yote niliyoyafanya kwa ajili yako, kumbuka Isevya Sec tulipotokea, yaani leo umeamua kuniacha kwa sababu ya hivyo vijisenti vyako, nakwambia sikubali Suhail.. Sikubali”

    “Hebu tulia kwanza Sharifa tuongee mpenzi wangu, kumbuka mwanzo nilikuomba uwe na Subra na makini katika jambo hili, kumbuka hili ni suala zito kuliko hivi tunavyoliongelea, linahitaji uelewa, umakini, subra, na usiri mkubwa.. Sijawahi kumueleza yoyote hapa duniani zaidi yako kwakua nakupenda na kukuamini hivyo kunielewa kwako ni faraja kwangu..”

    “Hakuna cha Subra wala nini hapa.. tangu mwanzo nilishaanza kukushitukia kua unataka kunigeuka, Kama wewe ni Mbovu si kuna dawa kemkem zinatolewa kwanini ukimbilie tu kua eti hauwezi kuoa? Hila zako nimezibaini Suhail,” Sharifa aliendelea kujibu huku akilia kwa sauti na kumfanya Suhail ajisikie vibaya sana, hakika alihisi dhambi kubwa sana kwa kitendo kile alichodhamiria kukifanya lakini hakua na jinsi

    “..Sharifa mpaka hapa unapoona nimeamua kukueleza jambo hili usifikiri sijapita kwa wataalamu, nimepita kila kona lakini majibu nayopewa naambiwa kua sitaweza kupona ugonjwa huu, usifikiri mimi napenda fedheha hii, naomba unielewe mpenzi wangu.. na ninakuahidi kwamba katika mali hizi ninazozimiliki kwa sasa kuna sehemu kubwa ya mali hiyo nitakupatia wewe ili upate pa kuanzia katika maisha yako mapya na mtu utakaekua nae.. Nakupenda sana Sharifa lakini sijiwezi katika hili” Maongezi yalikua marefu sana lakini Sharifa hakukubaliana hata kidogo zaidi ya kuendelea kuongea kwa jazba na uchungu huku mara kadhaa akimsogelea Suhail pale kitandani na kumkwida kwa nguvu mpaka ile fulana yake ikawa kama iliyotafunwa na Ng’ombe



    “Oky, Ok Suhail, nimekuelewa, tena vizuri sana,” Sharifa alianza kuongea tena upya huku akijizuia kulia “Sina tena Mume aitwae Suhail, sina tena furaha na amani moyoni, sina tena thamani duniani, hivyo nitakuacha na pesa zako na wanawake zako uendelee nao kwa uhuru.. Mimi bora tu sasa Nife nikapumzike, siwezi kuendelea kuishi katika hali hii..” Maneno hayo ya Sharifa yalimshtua sana Suhail aliekua amejilaza kitandani, akainuka haraka ili ajue nini maana ya maneno yale.



    Loo salale!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakika Sharifa alikua akimaanisha akisemacho, Suhail aliishia kumshuhudia Sharifa akiwa ameshaparamia juu ya Dirisha kubwa la chumba kile kilichopo Ghorofa ya tatu katika hotel ya Saratoga iliyopo kata ya Gongoni kiasi cha kuvunja vioo vya dirisha hilo, Vioo hivyo vikamchana sehemu ya kichwa chake akawa ananing’inia tu juu huku anavuja damu kichwani

    “NOOO, Sharifa pleeeese usifanye hivyo’,” Suhail alihamanika na kuanza kupayuka hovyo

    “No Suhail, I can’t.. Lazima nife tu”

    “Usifanye hivyo Sharifa mpenzi wangu, Hebu fikiria hayo maamuzi unayotaka kuyachukua, wafikirie wazazi wako na unifikirie na mimi.. nakuomba tukae tuzungumze”

    “Hakuna mazungumzo Suhail, nitaiweka wapi Sura yangu mimi jamani, yaani kukupenda kote kule umeamua kunidhalilisha namna hii! siwezi nakuambia ni bora nife” Kila Suhail alipotaka kumsogelea ndivyo alivyojisogeza mpaka kwenye ncha ya dirisha hilo ikiwa na sehemu kidogo tu iliyobakia ili akijiachia tu atabadilika jina na kuitwa Marehemu.



    Wakati hayo yanaendelea Meneja wa Hotel hiyo akiwa katika ofisi yake iliyopo ndani ya hotel hiyo alishtushwa sana na tukio hilo aliloliona kupitia katika Kompyuta yake iliyounganishwa na Kamera nyingi zilizotegeshwa kila kona kwa nje ya hotel hiyo, na kwakua sasa Sharifa alikua ameshatokeza nje ya dirisha hivyo aliweza kuonekana kwenye kompyuta kupitia kamera zilizokua nje ya chumba hicho. haraka Meneja akamtumia taarifa mlinzi wake ambae akatokezea kwa chini ya chumba kile akawa anampigia kelele Sharifa arejee ndani, Hakika lilikua ni tukio la fedheha na kuogofya. Sasa wakati Sharifa amemgeukia yule mlinzi aliekua akipiga kelele akaona imeshakua dhahma hivyo akaona liwalo na liwe Bora ajirushe tu.. ndipo haraka Suhail akautumia mwanya huo akaruka kwa kasi ya ghafla kutokea pale alipokua amesimama kuelekea kule Dirishani alipokua anataka kujirusha Sharifa., Sharifa nae alikua kaishagundua kua anarukiwa basi hakua tena na sababu ya kujichelewesha, Akarijusha kwa nguvu ili aangukie nje aitoe roho yake mwenyewe. Mlinzi aliekua chini aliishia kupiga kelele kali za uwoga huku Suhail nae alipiga kelele za hamaniko na woga mkubwa..

    *****

    “Kwanini umeamua iwe haraka hivyo?,” Mzee Fungameza alimsaili Mzee Kusekwa aliekua amewasili nyumbani kwake kwa ajili ya mjadala wa Ndoa ya vijana wao Suhail na Sharifa

    “Sikuhitaji iwe haraka lakini kwa hali ya mazingira naona kama itakua ni busara tukifanya hivyo maana hawa ni vijana bila kuhimizwa basi lolote laweza kutukia.. na nimeona Suhail ameshapata kazi inayomfanya awe busy kiasi cha kua haeleweki hata alipo sasa hii chelewachelewa unaweza kukuta mwana si wako”

    “Ok sawa, sidhani kama ni vibaya ukizingatia kwamba ndoa za kiislam hua hazina haja ya kuchukua muda mrefu lakini itakua ni busara zaidi tukisema na walengwa wewnyewe ili nao tusikie wanataka hili suala liende kwa mtindo gani..”

    “Sawa, hakuna shida mimi leo nitaongea na Suhail japo nimeshafanya hivyo, sasa Kesho nitakuja kuongea nawe kujua umefikia wapi” Wakati wazee wanaendelea na mipango ya Ndoa ya vijana wao hawakua wakijua kua mambo yanaharibika huko Saratoga Hotel, Laiti wangelijua pengine wasingelikua pale muda huo wakijadili kitu chenye utata mkubwa sana..



    Bahati nzuri wakati sharifa anajirusha Suhail alikua ameshakamata sehemu ya kiunoni katika suruali aliyoivaa, hakumuachia.. akamng’ang’ania japo kutokana na uzito wa Sharifa aliekua akining’inia kule juu Dirishani Suhail nae akajikuta akizidiwa na kuvutwa yeye nje badala ya yeye kumvuta Sharifa, ikawa kititim sasa. Akaendelea kumzuia na kujizuia yeye ili wasianguke wote mpaka hatimae akafanikiwa kumvuta ndani kwa nguvu kupitia palepale dirishani, Kabla hajafanya lolote akiwa anatweta huku akimuangalia Mchumba wake kwa hasira na hofu ghafla akasikia mlango ukigongwa kwa nguvu sana, akauangalia mlango kwa mashaka makubwa akijua sasa mambo yameshaharibika, akataka kwenda kuufungua lakini akahofia kumuacha Sharifa peke yake pale chini akihofia kua asije akapata tena upenyo wa kujirusha kwa mara ya pili, akaamua kumnyanyua na kusogea nae mpaka mlangoni.. Akaufungua na kumruhusu aliegonga aingie, akaingia mwanaume mmoja akiwa ametaharuki vibaya, bila shaka alilishuhudia tukio lile

    “Vipi?,” Suhail alimsaili jamaa yule alieingia ndani

    “Vipi Kuhusu nini?” Jamaa yule alijibu kwa hasira zilizochanganywa na dharau kubwa, Suhail akajikuta ameishiwa cha kuongea kabla Yule jamaa hajaanza tena kuongea kwa kasi ya ajabu

    “We ni mpumbavu sana pamoja na huyu mwenzio, hivi unataka kuniletea dhahama hapa, kama mna matatizo yenu kwanini msiende kuuania huko maporini?”

    “Tafadhali bwana mkubwa usiniite mpumbavu, We unajua kilichotokea humu ndani mpaka unaanza kulalama tu? Acha dharau,” Suhail alibwata kwa ghadhabu

    “We unanijua vizuri mimi?, mimi ndie Meneja wa Hotel hii sasa ulitaka nije kukupongeza kwa upuuzi mlioufanya humu ndani?..” Jamaa Yule akasita kidogo, akamgeukia Sharifa pale chini akiwa analia na kutoka damu eneo la kichwani, Akaenda mpaka pale Kitandani akachukua shati la Suhail akalichanaa kipande kisha akamwambia Suhail asogee haraka wasaidizane kumfunga kichwani ili kuzuia damu isizidi kutoka, Wakamfunga na kumuinua pale Sakafuni akiwa bado analia tu, Kisha Mwanaume Yule akamtupia swali

    “Hivi wewe Sharifa una akili kweli wewe,” Aliuliza jamaa Yule aliejitambulisha kama meneja wa hotel, akamfanya Sharifa aache kulia kwa mshtuko wa kutajwa jina lake na mtu asiemfahamu “Hivi kwa nini unataka kujiua kwa upumbavu we mtoto? Nd’o kupenda sana ama nini? Baba yako ninasali nae kanisa moja, na ni Mzee wa kanisa anaehishimika sana sasa unataka kumtia aibu kubwa kiasi hiki, sasa mimi nampigia simu sasa hivi aje hapa” Kusikia vile Moyo wa Suihail ukapiga chogo chemba, akahamanika haswa, akajua sasa kua siri zote zitakua hadharani, akamsogelea jamaa Yule aliekua ameshatoa simu yake ya kiganjani kisha akamzuia

    “Tafadhali kaka usifanye hivyo, nipo chini ya miguu yako kaka, naomba tu tusaidiane”

    “Usaidiane na nani? Mimi sihitaji msaada wako wowote”

    “Sawa kaka, naomba unisaidie mimi, tuyaongee tu usipige simu tafadhali”

    “No, hivi we unadhani hili tukio ni dogo eeh? Mmeharibu mali pia mmejeruhiana humu ndani, je akifa huyu binti hapa?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kaka usijali kuhusu kila kilichoharibika nitakulipa gharama zote kisha kitokeo cha hapa nampeleka hospitali..” Baada ya maelezo yale Suhail akamsogelea jamaa Yule kasha akamnong’oneza neno akijaribu kumshawishi kua atampoza pesa kidogo mbali ya hizo za matengenezo ya dirisha ili tu asitoe habari ile, Jamaa akalainika kusikia pesa akamsogelea Sharifa, akamshika mkono ili sasa watoke waanze safari ya kwenda hospitali, ila akampa tahadhari Suhail kwamba akae na Sharifa wamalize tofauti zao ili Sharifa asije akafanya tena huo mchezo aliotaka kuufanya pale halafu ikaja kugundulika kua alishawahi kufanya hivyo pale Hotelini kitu ambacho kitamletea matatizo yeye kwa kulikali kimya jambo hilo zito, akaahidi angemueleza kila kitu Mzee Fungameza kawa wasingeyamaliza mambo hayo. Ikawa ni kitanzi kingine kwa Suhail, Baada ya majibizano ya muda kidogo Wakakubalina. Suhail akatoa pesa za kumuachia jamaa Yule kisha wakashuka ghorofani, wakaita Teksi na Safari ya kuelekea Hospitali ikaanza

    *****



    Majira ya saa mbili kasorobo usiku walikua kwakiendelea kupatiwa huduma nzuri tu pale Hospitali, hawakwenda katika Hospitali ya Kitete kwa kuhofia kuzalisha maswali na mwishowe huenda taratibu za kipolisi kuingia kati hivyo walikwenda mpaka Mtaa wa Ujiji katika Hospitali ya Dokta mkubwa sana anaekubalika pale mkoani, na kwakua pesa iliongea hivyo huduma ikaenda kwa kiwango kizuri, Suhail alipoona mambo si mabaya sana akamwambia Sharifa ampigie simu mama yake kumjuza kua amepatwa na matatizo, ikabidi amfundishe uongo wa harakaharaka kua aseme amekatwa na vioo vilivyodondoka kutoka katika gari moja kubwa lililopita karibu yake lakini hali yake si mbaya sana, Akafanya hivyo!



    Muda mfupi baade Mama Sharifa alifika Hospitalini hapo na kujumuika na wanawe, Baada ya huduma kukamilika Wakaondoka huku wakitakiwa tena kesho yake kwenda kupata sindano, Sharifa na mama yake wakaenda kwao Chemchem na kumuacha Suhail nae akirejea kwa Rufita akiwa na mawazo na mchoko usiosemekana, Hakika alijutia!

    *****



    SUHAIL aliporejea nyumbani kwao akawapa habari ya kilichomkuta Sharifa lakini hakuwaeleza kama tukio lilivyokua, Alidanganya na kulifanya tukio lile kuonekana ni dogo na la kawaida tu kuliko uhalisia wake ulivyo. Na kutokana na Msongamano wa mawazo kichwani mwake hakutaka kabisa kupoteza muda wa kuendelea kukaa pale sebuleni japo familia ilionekana kua na hamu nae sana. akawaaga ili aende zake chumbani kulala, hiyo ilikua ni baada ya kupata chakula cha usiku. Lakini baba yake hakumpa nafasi hiyo akamzuia kwa ajili ya kuanzisha majadiliano kuhusu Suala la Ndoa yake, safari hii majadiliano hayakua makubwa sana kwakua ilikua ni kama marejeo tu kwani mada walikwisha ijadili, Wakamalizana japo si kwa muafaka wa asilimia miamoja. Wakaingia kulala.



    SAA tisa usiku, hali ya ukimya ikiwa imetawala karibu maeneo mengi sana huku walio wengi wakiwa wanavuta shuka tu vitandani mwao, Suhail yeye alikua njiani akielekea Mbezi, Dar es Salaam. hakua na usafiri wowote zaidi ya Pete yake iliyomtoa pale Tabora kwa kasi ya ajabu baada ya kuiamrisha tu kufanya hivyo, Moja ya faida ya Pete ile ilianza kuonekana! Ndani ya dakika tano tu akawa amewasili Mbezi, Dar es Salaam huku wazazi wake wakijua yuko chumbani amelala

    *****



    “Shekhia mke wangu najua una uwezo wa kuona mbali, bila shaka umeona kila kilichojiri huko Tabora.. Hali ni mbaya Baba anataka kunitolea radhi kama sitaoa, Sharifa nae anataka kujiua...,” Suhail aliongea kwa hofu na kwa harakaharaka kama anaetaka kuwahi kuondoka

    “Kwa hiyo mimi nifanyaje?” Shekhia aliekua ameegama katika kabati kubwa alijibu katika mtindo wa Swali huku akitikisa mguu wake kwa dharau, inaonekana ni kweli aliona kila kilichojiri kule Tabora

    “Shekhia nakupenda mke wangu, ila ili mambo yaende sawa inabidi tu Nimuoe Sharifa”

    “Nini wewe? Nyang’au wewe” Shekhia alijibu kwa hasira kisha akamnyooshea mkono wake wa kushoto uliokua umevikwa pete katika kidole chake cha kushoto, ilikua ni Pete yenye nguvu za kijini japo haina uwezo mkubwa kama ile aliyonayo Suhail, alipomuelekezea tu ile Pete ikatoa miale mikali ya moto, yenye uwezo wa kuangamiza na hata kuua, hakika alipatwa na hasira kiasi cha kudhamiria kumdhuru Suhail, lakini kutokana na nguvu alizonazo Suhail kupitia katika Pete yake kubwa ya ‘Khatam Budha’ ikashindikana kudhurika

    “Unataka kufanya nini Shekhia? Yaani unataka kunidhuru mimi? We una akili kweli?” Suhail nae alimjia juu Shekhia kwa kitendo kile, ikawa sasa hakuna maelewano ndani kila mmoja alijiona anaweza kufanya lolote, ila kwakua Shekhia alitenda kosa kutaka kumdhuru mume wake ikabidi awe mpole kiasi na hapohapo Suhail akautumia mwanya huo kumshinikiza Shekhia kukubali Suala la yeye kumuoa Sharifa lakini hapo pakawa pachungu haswa, ikawachukua muda mrefu sana kulijadili suala hilo huku Suhail akitumia maneno aliyotolewa na baba yake kua kama fimbo wakati Shekhia nae akimkumbusha Suhail kua makubaliano yao siku walipofunga ndoa ni kwamba yeye atakua ndie Mke pekee wa Suhail. Patamu hapo!

    “Sasa mimi siwezi kukosa radhi ya mzazi wangu kwa ajili yako, sawa nakupenda ila na wazazi wangu nawaheshimu sana, siwezi kukhalif amri zao, nitakosa Baraka na radhi zao.. Maisha yangu yote yataharibika hapa duniani na kesho Mbinguni”

    “Hayo yote haukuona umuhimu wake tangu mwanzo ulipokubali kuoa kwa masharti mbele ya Mzee Sufiani? Na kwa taarifa yako nikimueleza Baba huu ujinga wako atakuangamiza hata kabla jua halijachomoza”

    “Najua hilo mke wangu nd’o maana nataka tuyaongee mimi na wewe kwakua tunapendana, sasa Baba yako akiniangamiza mimi hata wewe utakua umepoteza mume, si ndio?”

    “Yeah Kuliko kuchangia mwanaume ni bora tu nikupoteze” Majadiliano yalikua makubwa sana mpaka hatimae wakaanza kufikia maamuzi, Shekhia akakubali Suhail aoe lakini kwa sharti moja tu kwamba asikutane kimwili kamwe na Sharifa, hiyo nayo ikawa na mada mpya

    “Sasa itawezekanaje hiyo? Hakuna Ndoa bila Tendo, hauoni kua ni kujiletea matatizo makubwa zaidi,” alimaka SuhailCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Itawezekana tu kwakua tayari ameshajua kua wewe ni Mbovu hivyo hatokua tena na sababu ya kukusumbua, zaidi ya hapo sitokua na muafaka na wewe kwa jambo lolote tena, na ukae ukijua kua kama una mpango wa kufanya tofauti hakika jihesabu wewe ni Mfu mtarajiwa” Alhitimisha Shekhia kwa mkwara mzito. Suhail akabaki njia panda ila akawa hana budi kuafikiana na Shekhia akiamini japo kwa hatua hiyo ya awali, aliamini kwamba huo ni mwanzo mzuri na Mengine yatajipa ndani kwa ndani!



    Kwa kasi ileile Suhail akarejea Tabora, Usiku uleule

    *****

    Mpaka saa tatu asubuhi familia nzima ya Mzee Kusekwa walikwishaamka isipokua Suhail tu aliekua akikoroma kitandani kwake. Shughuli za usafi na maandalizi ya kifungua kinywa ilikua ikiendelea, na hata ilipokamilika waliendelea kumsubiria Suhail aamke ndipo waweze kupata kifungua kinywa hicho kwa pamoj, Hakika Suhail Alichoka sana na Pilika za mchana na usiku kucha, hakuamka mpaka alipoamshwa!



    Alipoamka kitu cha kwanza alichokifanya ni kumpigia simu Sharifa lakini simu haikupatikana, akatoka chumbani na kwenda bafuni kujiswafi mwili kisha akarejea kujumuika na familia kupata kifungua kinywa huku wakipiga stori za hapa na pale,

    “Jamani mimi nataka nitoke kidogo,” Suhail aliwaaga wazazi wake

    “Unaenda wapi?,” Mzee Kusekwa nae alisaili haraka

    “Naenda mara moja kwa jamaa zangu kule Minazi Mikinda, sijaonana nao tangu nimekuja” majibu ya Suhail yalikua ni ‘Funika kombe, mwanaharamu apite’ lakini lengo lake lilikua ni kwenda Hospitali kumuwahi Sharifa kwakua alijua kua angekwenda pale kwa ajili ya kupata sindano

    “Ooh, ngoja basi tufuatane tutakwenda kuachania mbele maana name naenda kwa Bwana Fungameza” Baada ya maelezo hayo Mzee Kusekwa aliinuka na kuingia chumbani kwake kujiandaa ili waweze kutoka

    *****



    Mkabala na Hospital kubwa ya Dr Nyango Bango kubwa lililosomeka ‘KWA MZEE ANDOGA’, Lilikua likiunadi mgahawa mkubwa wa kupatia chakula pamoja na vinywaji, watu wengi hujumuika maeneo yale kupata chakula safi. Kwa nyuma ya mgahawa huo palikua na Bustani kubwa iliyotengenezwa vizuri sana kwa ajili ya wateja kupata vinywaji huku wakiburudishwa na upepo mwanana utokanao na miti kadhaa iliyapandwa kuizunguka bustani hiyo huku harufu ya maua ikizipendezesha pua zao. Suhail na Sharifa walikua wameketi katika kona kabisa ya bustani ile baada ya kutoka kupata sindano, Sharifa hakua na furaha kabisa na hata Suhail nae alijilazimisha tu kua katika hali ya furaha lakini haikutoka moyoni

    “Sharifa nadhani jana ulifikia kuchukua maamuzi yale bila kutaka kunielewa lakini kama ungenisikiliza kwa kina wala tusingefikia kule kote”

    “Hauwezi kutaka kunifanyia unyama ule wewe Suhail, angalia sasa Wazee wameshaanza kujadili suala hili la Ndoa, na jana tu walikua wakijadiliana halafu wewe ulete mambo ya aibu kweli?”

    “Sawa, sasa wewe pamoja na hayo tuliyojadiliana unashauri tufanyaje?”

    “Hakuna cha kushauri chochote hapa, Ndoa kama kawaida halafu hayo mengine sijui ya ubovu yatajuliakana baadae, ila Ndoa ni lazima”



    “Na vipi kama nitaendelea kua mbovu ndani ya ndoa hata kama tutahangaika huku na kule, utaweza kuvumilia kweli?”

    “Ndio nitaweza, halafu kwanini ufikirie kutokupona tu? Nakwambia we utakua na Ajenda ya siri, sio bure” Mjadala ulichukua muda mrefu huku Suhail akionesha kukubali kishingo upande tu lakini ndani ya moyo wake alijua dhahir kua hayo ndio makubaliano yake na Shekhia. Baada ya kuhitimisha mjadala, Suhail akamchukulia Teksi Sharifa impeleke kwao japo haikua mbali sana tokea hapo walipokua

    *****



    “Nimetokea kwa Bwana Kusekwa, amesema amekwishaongea na binti yake na ameridhia kuliwahisha jambo hili, hivyo tumeazimia kua Ndoa hii Ifanyike wiki mbili zijazo,” Mzee Kusekwa alikua akiongea na mkewe Sebuleni kwao

    “Mimi sina tatizo ila kwa muda huo mlioafikiana naona kama hautatosha kufanya maandalizi yote.. yaani kuwaalika watu, kuandaa maakuli, Mahari, nk yote hayo yanahitaji pesa na muda..”

    “Hatuhitaji harusi kubwa sana bali ni ndogo tu ya kupendeza, gharama za kawaida hazitamshinda Suhail kulipa” Wakiwa katika mazungumzo ndipo na Suhail nae akarejea

    “Enhee bora umefika wakati muafaka, kuna jambo hapa linakuhusu,” Mzee Kusekwa alimdaka mwanae bila hata kusalimiana, akamsogezea kiti kisha akaanza kumpa maelezo aliyokua akimwambia mkewe, Suhail alikua kimya akimsikiliza baba yake na kwakua tayari alikwisha yamaliza na Shekhia sasa hakua na hofu sana zaidi ya kuafiki tu, na hata aina ya harusi kwamba itakua ni ndogo tu ilimfurahisha pia, hakutaka harusi ya Gumzo, Baada ya Baba yake kumaliza kuongea nae akaweka lake

    “Lakini Baba..”

    “Lakini nini wewe, mbona unataka kunikwaza tena” Mzee Kusekwa alimkatisha mwanae akihisi kua anataka kuweka kipingamizi, lakini akazuliwa na mkewe

    “Mwache basi nae atoe maoni yake, usimpelekepeke tu. Hebu sema Suhail”

    “Kwa kua mmeazimia zoezi hili lifanyike baada ya wiki mbili mimi nimeafiki ila siwezi kukaa huku siku zote hizo huku, kumbukeni nimewaambia kua mimi kwa sasa nimeajiriwa, ninasimamia Biashara za watu” Suala lile likawa zito sana japo Mzee Kusekwa hakuafiki kabisa akiamini kua Suhail akiondoka tu pengine angeibuka na kisingizio kikubwa cha kutokuja tena siku hiyo ya Harusi, ikawa ni malumbano mule ndani lakini kwa uzito wa hoja aliyoitoa Suhail ikawa hakuna budi kuikubali tu.

    *****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku mbili baadae Suhail aliondoka na kurejea Dar kuangalia miradi yake na kuwaacha watu wa nyumbani kwao wakianza pilikapilika za maandalizi ya harusi ikiwa ni pamoja na kuwaalika majirani zao, pia Suhail aliacha amekwishalipa mahari na akawaachia wazazi wake pesa za matumizi muhimu. Kwa upande wa Mzee Fungameza hapakua na maandalizi makubwa, Ukizingatia tofauti ya kiimani baina yake na binti yake hivyo hakua na uwelewa mkubwa wa harusi za dini nyingine zinavyokua hivyo mambo mengi alimruhusu Mzee Kusekwa ayasimamie.



    Siku ziliyoyoma kuelea katika Ndoa ambayo kwa Suhail aliamini ni ndogo sana lakini huko Tabora ilipokelewa kwa Shangwe ya hali ya juu, marafiki zake wengi kwa jinsi wanavyompenda waliisubiri kwa hamu huku jamaa na majirani wa pande zote mbili kwa Mzee Kusekwa na Fungameza nao wakiipokea kwa aina yake kutokana na ukweli kwamba wazee hawa ni wacheshi na wanakubalika sana kila mmoja kwa namna yake na kwakua wao pia hujitolea sana kushiriki katika Shughuli za wenzao hivyo fadhila ilikua ikilipwa sasa.



    Harusi ilipangwa kufanyika siku ya Ijumaa saa tatu asubuhi, Sharifa aliendelea kutawa huku akiisubiri siku hiyo kwa hamu. Na Suhail nae aliendelea na shughuli zake huko jijini Dar es Salaam huku akiahidi kua angewasili Tabora kwa usafiri wa Ndege siku moja kabla ya harusi, yaani siku ya Alkhamisi

    *****

    Siku ya alkhamisi ikiwa imesalia siku moja kufika siku ya harusi Suhail alikua ameshajiandaa kwa safari ya kuelekea Tabora, ilikua ni saa tisa alasiri akiwa na mabegi yake mikononi alikua akiagana na mkewe wa mwanzo Bi Shekhia Bint Sufian. Hapakua na mazungumzo mengi kwani masuala walikwisha zungumza na wakakubaliana kwamba Shekhia atabaki pale Mbezi na Sharifa ataenda kukaa Ilala. Lakini gubu la Shekhia lilafanya mjadala uanze kumea upya

    “Usije ukafikiri mimi ni mpumbavu kukubali ufunge ndoa na huyo Sharifa, nimeamua tu kukunusuru na matatizo ya kwenu huko Sasa wewe ujitie tu hamnazo hakyamungu utajuta kunifahamu,” Shekhia alikua akiongea na Suhail kwa mkwara mzito

    “Usijali mke wangu, nakupenda sana kuliko hata unavyojipenda wewe mwenyewe, huyu namuoa tu kwa kuwaridhisha wazazi” Suhail alijibu kwa utulivu na ulaghai mkubwa huku akiwa tayari amekwishapendeza kwa ajili ya safari, na mabegi yake yakiwa miguuni pake

    “Ila nakusisitiza tena kua ‘Tendo’ ni marufuku, usithubutu..”

    ‘Itawezekania wapi,’ Suhail alijibu kimoyomoyo huku akijua kua anaiingia hatari kubwa sana, Sasa wakiwa katikati ya Mazungumzo ndipo ghafla Pete ya Suhail ikawasha mwanga mwekundu huku ikimtetemesha kidoleni kwa nguvu mfano wa simu iliyowekewa huduma ya ‘Vibration’, hali ile iliwashitua sana, mara Pete ile ikaanza kupiga mbinja kwa sauti kali, Wakaangaliana huku kila mmoja akitetemeka hasa kuona hali ile ya hatari, ilikua ni taarifa ya wito kutoka kwa Mzee Sufiani Shamhurish akihitajia msaada wa ‘Khatam Budha’, bila Shaka amevamiwa na amezidiwa nguvu na Maadui zake kutoka katika himaya ya Budha. Shekhia akaanza kulia kwa sauti huku akitetemeka kwa woga, Suhail nae akawa hajui afanyeje. Haraka akayatupa chini mabegi yake aliyokua ameyaweka tayari kwa ajili ya kutoka kuelekea ‘Airpot’ Kisha akaitumbulia macho pete ile mpaka nae macho yake yakaanza kubadilika yakawa kama ya Paka aliejeruhiwa, akaona mambo yote yanayojiri kwa Mzee Shamhurish, ilikua ni hali ya hatari Baba mkwe wake alikua anashambuliwa vibaya katika Jengo moja kubwa sana lilotawaliwa na ukimya katika mji mmoja huko Yemeni. Aliwashuhudia Wanaume watatu wenye asili ya ki-asia wakiwa wamemuangusha chini Mzee Sufiani huku wawili wakihitaji kumuua lakini mmoja wao alikua akikataa wasifanye hivyo mpaka Mzee Sufiani atakapowaeleza mahali ilipo Pete yao(Khatam Budha), Wakaanza kumpa kibano cha hatari jinni mwenzao. Suhail alioogopa sana ukizingatia tangu akabidhiwe Pete ile hakawahi kupambana na jinni yoyote Yule hivyo ile ilikua ni mpambano wake wa kwanza, Hofu ilimvaa kiasi cha kuanza kusahau namna ya matumizi katika mashambulizi. Akajipa moyo kisha haraka akaiamuru Pete ile ikamchukua kwa kasi na kumpeleka Eneo la tukio huku akimuacha Shekhia akitokwa tu na machozi

    *****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati Suhail akiwa njiani kuelekea Yemeni kumnusuru Baba Mkwe wake hali ilikua ya kipekee huko Tabora ambapo ilikua imesalia siku moja tu tu kufika siku ya Ndoa. Shamrashamra na maandalizi ya Ndoa vilizidi kupamba moto, Ilikua ni Ndoa ndogo tu lakini ya kipekee, Ndoa ambayo kwa Suhail aliamini ni ndogo sana lakini huko Tabora ilipokelewa kwa Shangwe ya hali ya juu, marafiki zake wengi kwa jinsi wanavyompenda waliisubiri kwa hamu huku jamaa na majirani wa pande zote mbili kwa Mzee Kusekwa na Fungameza nao wakiipokea kwa aina yake kutokana na ukweli kwamba wazee hawa ni wacheshi na wanakubalika sana kila mmoja kwa namna yake na kwakua wao pia hujitolea sana kushiriki katika Shughuli za wenzao hivyo fadhila ilikua ikilipwa sasa.



    Lakini hofu ilianza kutanda baada ya kuona muda ukizidi kuyoyoma na hakuna taarifa zozote za Suhail kuwasili mkoani, Wazazi na majirani walianza kuulizana juu ya ukimya wa Bwana Harusi mtarajiwa, mbaya zaidi Simu yake kila ilipopigwa iliita bila kupokelewa.



    Muda ukazidi kupotea, Giza likapiga hodi kuashiria siku inakwish hatimae matumaini ya kumuona Suhail yakafifia, Hofu ikazizima.

    *****



    Maandishi makubwa yaliyofifia na kupoteza ile rangi yake ya asili yaliyosomeka

    ‘AL- JAMHURIYYAH AL-YAMANIYYAH.

    MAT’ HAF’ yalilinadi jengo moja kubwa na chakavu lililokua likionesha kila dalili ya kuhamwa na kutelekezwa kwa kipindi kirefu. Kama ambavyo maandishi hayo yanavyojieleza kua hilo ni Jumba la Makumbusho lililo chini ya Jamhuri ya Yemen. Jumba hilo lililopo katika kisiwa cha Socotra Nchini Yemen lilihamwa miaka mingi iliyopita na Shughuli zake kuhamishiwa katika Jengo jingine lililopo katika mji mku wa SANA’A Nchini humo. Kutokana na hali ya Upweke ya Jumba hilo la zamani la makumbusho ikiwa ni pamoja na kukosa ulinzi wala usimamizi hivyo uovu mwingi umekua ni sehemu ya maisha ya ndani ya Jumba hilo pweke ambalo si vibaya kama utaliita ‘Pagara’ kwa jinsi lilivyoharibika na kuachilizwa huku miti mingi ikiota kwa nje ikilizunguuka jumba hilo.



    Mzee Sufian Shamhurish nae hatimae akawa ni miongoni mwa wahanga waliowahi kufanyiwa unyama na Udhalimu mkubwa ndani ya Jumba hilo, Alikua akiteswa vikali humo ndani alipoingizwa msobemsobe baada ya kukamatwa ghafla kwa kushtikizwa alipokua akitembeatembea maeneo aliyokua akiishi, waliomkamata ni Makomandoo watatu wa Kijini kutoka katika Himaya ya Budha ambapo waliagizwa kufanya msako mkali na kuhakikisha wanamtia nguvuni Mzee Sufiani kisha Wamnyang’anye Pete yao(Khatam Budha) kabla ya Kumfikisha Budha akiwa hai au akiwa Maiti. Mzee Sufian hakua na ujanja tena kwani Nguvu zake pekee za kijini hazikua na uwezo wa kufua dafu kwa Makomandoo wale watatu wa Kijini waliokua wakimporomoshea Kipigo na mateso ya nguvu ili aseme ilipo Pete(Khatam Budha) hivyo tegemeo lake Pekee ni Silaha takatifu iliyopo kidoleni kwa Mkwewe, Suhail Kusekwa.



    Ndani ya muda wa takribani dakika kumi na tano Suhail alikwishawasili katika Jumba lile la zamani la makumbusho, Alipowasili tu akaingia moja kwa moja mpaka ndani kabisa huku hofu yake ya kibinaadamu ikianza kumezwa na ujasiri wa Kijini kutoka katika Pete ile aliyoivaa, alitembea kwa haraka kila kona akimsaka Mzee Sufiani na Maadui wake lakini hakuona chochote, alipoona kimya kimezidi kutanda akaanza kupatwa tena na hofu kua isije ikawa wamekwisha muuwa, akaenda mpaka Sehemu moja ambapo kuna makabati mengi makubwa yaliokua yakitumika kuhifadhia vitabu vya kale ili sasa aitumie Pete yake imuoneshe ni wapi walipo viumbe aliokua akiwatafuta, Hilo kwake lilikua ni kosa kubwa kwani Majini wale hatari walipomsikia anaingia mule ndani haraka walijificha ili wapate kumjua anaeingia, na hapo katika Kabati alilosimama ndipo alipokua amejificha Takadir Al-harabi ambae ndie Mkuu wa Opesheni ile ya Kijini, Komandoo huyo alikua akimuangalia vizuri Suhail lakini hakujua ni nani hasa Yule kijana, Mwishowe aliamini kua kijana Yule ni Binaadamu tu wa kawaida na pengine mule ndani yumo kama Msimamizi tu wa Jumba lile lakini hali aliyoingia nayo mule ndani ndio ilizidisha hofu kwa Takadir Al-harabi maana alikua kama anaetafuuta kitu, Ndipo sasa akaamua kutoka ndani ya kabati lile akiamini hatoonekana na macho ya Mwanaadam wa kawaida. Hilo likawa kosa lake la kwanza kwani alipotoa pua yake tu alikutana na Pigo takatifu kutoka kwa Suhail aliemuona sawia, kabla hajakaa sawa tena Suhail akamuwahi akamrukia matekea mfululizo kama mwendawazimu, mapigo yaliyokua yakimtoka Suhail ni ya kiwango cha hali ya juu kiasi cha kumstaajabisha mpaka yeye mwenyewe maana alijielewa fika hakua na taaluma wala mazoezi ya mapigo yale, akajua kua ana nguvu ya ziada ndani yake.. Baada ya kichapo kumuelemea Komando Takadir ndipo sasa kua hakua akipambana na Mwanaadamu wa kawaida hivyo nae akajiweka sawa Kisha akaruka juu kwa mtindo wa ajabu sana na kumtandika Suhail teke kali la kifuani lililomrusha kwa kasi akaenda kujibamiza katika Mlango mdogo wa Chumba kilichokua zamani kikitumika kama Ofisi ya Utawala, Mlango wa chumba hicho ukasambaratika akaingia nao mpaka ndani ambapo alikutana na Majini wengine wawili waliokua wamemdhibiti Jini mwenzao ambae ni Mzee Sufian, Majini wale hawakulaza Damu wakampokea Suhail kwa kichapo cha haja mpaka Suhail akajihisi kufakufa tu,Wakati majini wale wawili waliokua wamejificha mule chumbani wakiendelea kumshushia kichapo ghafla Suhail akashangazwa na tukio lililotokea ambapo Mzee Sufiani alieonekana kuishiwa kabisa nguvu aliruka sarakasi akatua juu ya Meza moja chakavu mpaka ikasambaratika kisha bila kuchelewa akamrukia mmoja kati ya majini wale akamtandika mateke ya kwenye mbavu mfululizo mpaka zikasikika sauti za mbavu zikivunjika, hapohapo Suhail nae akamrukia Yule mwingine aakampelekea ngumi za nguvu kisha akamshika kichwa na kumvunja Shingo yake. Ilikua ni mapambano ya kuangamizana, Suhail alipopepesa macho yake akakutana na Ishara aliyopewa na Mzee Sufian, akamuelewa vema, akaibenjua Pete yake haraka ikatoa miale mikali ya moto wa ajabu ambayo aliielekeza kwa majini wale wawili, Wakaungua na kuteketea kabisa. Harakaharaka Suhail akatoka Nje ya chumba kile ili amuangalie Yule Jini wa mwanzo aliempiga lile teke lililompeleka mpaka kule chumbani lakini hakumuona, akabofya Sehemu ya nyuma ya Pete ile ili apate kumuona Jini Yule lakini hakumuona kamwe katika Eneo lile.. Akasonya kwa sauti kali kisha akaanza kurejea kule chumbani huku akiingalia ile Pete iliyokua ikimpa nguvu za ajabu, Akatabasamu!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Vipi,” Aliuliza Mzee Sufiani walipokutana na Suhail mlangoni

    “Aah Yule mwanaharamu ametoweka”

    “Hiyo ni hatari Suhail”

    “Kivipi Mzee?”

    “Ukisikia Takadir Al-harabi ndio Yule, ndie Komando mkuu wa msako wao huu.. Sasa kama amekukariri vizuri atakusumbua Yule” Maneno hayo yalipeleka ubaridi wa woga moyoni mwa Suhail, lakini Mzee Sufian akawa anampa moyo kua anayo silaha kubwa sana ya Khatam Budha



    Haraka Suhail na Mzee Sufian wakaondoka eneo lile kwa kasi ya upepo wakielekea Bagamoyo kupata mapumziko mafupi maana kwa kiasi Fulani Mzee Sufiani alikua amejeruhiwa. Iliwatumia kama Dakika chache tu kuwasili Bagamoyo ambapo Mzee Sufiani alipatiwa huduma za haraka na muhimu kutoka kwa wale vijana wakiarabu wanaolinda Nyumba hilo ambao nao ni majini, Suhail aliendelea kukaa pale mpaka usiku ndipo akamuaga Mzee Sufian kua anakwenda nyumbani kwake Mbezi, wakaagana kisha akaondoka usiku uleule

    *****

    Alipowasili alimkuta Shekhia akiwa katika hofu na mawazo makali kwani hakujua hatma ya Baba yake, Uwezo wake wa kijini wa kuona na kufanya jambo loloto haukua mkubwa, mara nyingi alikua akiweza kuona ama kupambana na binaadam wa kawaida tena walio katika umbali wa kawaida kama huu wa ndani ya Nchi, hakua na uwezo wa kuona mbali sana wala wa kupambana na majini Hivyo Suhail alipoingia ndio akaanza kupata sasa Simulizi tu ya kilichojiri, wakaongea mengi na hatimae wakalala wakiwa wameazimia kua kesho yake Suhail ataondoka saa kumi na mbili kwa Ndege akielekea Tabora kisha Shekhia ataelekea Bagamoyo kuonana na Baba yake

    *****



    Saa kumi na mbili asubuhi Suhail alikua ‘Airport’ akijiandaa kwa safari yake ya Tabora huku Shekhia nae akiwa njiani akielekea Bagamoyo..



    Saa mbili asubuhi Suhail alikua katika uwanja wa ndege wa mkoani Tabora ambapo alichukua Taksi mpaka Nyumbani kwao..



    Nyumba ya Mzee Kusekwa ilikua imefurika watu waliokua katika vikundi vidogovidogo vya majadiliano, Kilichowakusanya pale ni harusi ambayo kwao iligeuka Ndoto tu maana Baba harusi hakuonekana wala hakua akipokea simu, baadhi walifurahi kuona familia zikidhalilika, na baadhi walilaani sana kitendo kile cha Suhail. Mzee Kusekwa alikua ndani tu muda wote akiugulia kimyakimya maana hakua na cha kuwaambia waalikwa huko nje. Hakika fedheha ilimvaa.



    Macho ya Waalikwa wale waliokua katika majadiliano huku baadhi yao wakianza kuondoka yalipiga ndani ya Teksi iliyopaki nje ya Nyumba ya Mzee Kusekwea na Kumshuhudia Suhail akiteremka na mabegi yake kutoka katika Teksi hiyo, ilikua kama maigizo lakini ndio hali halisi hiyo kwamba Baba harusi aliedhaniwa kuingia ‘Mitini’ sasa amerejea..



    Kelele za shangwe, Nderemo na vifijo zilitawala katika eneo lile huku akina mama nao wakitoka uani kuangalia kilichojiri na kumkuta Suhail akiwa anawasili, Kelele hizo zikamtoa nje Mzee Kusekwa aliekua chumbani amejawa na Fadhaa kubwa, nae alipigwa na Butwaa tu.. Shamrashamra zikaanza upya, Suhail akaingia ndani na kupokelewa na Ndugu na jamaa

    “Suhail,” Mzee Kusekwa aliita kwa mshangao kama asieamini kile anachokiona

    “Naam Baba” Baada ya Suhail kuitikia wito ule ukimya ukatanda bila ya Mzee Kusekwa kusema chochote mpaka ikambidi Suhail aanze kujisemesha mwenyewe

    “Poleni kwa usumbufu jamani, cha kushukuru Mungu nimewahi kufika,” Alijiongelesha Suhail lakini si baba yake wala ndugu yake yoyote aliejishughulisha kumjibu, akajikuta anaedelea tu kubwabwaja “..Nilipatwa na safari ya dharura nilikua nchini China kikazi nimewasili Tanzania leo saa kumi usiku sikutaka hata kwenda kwangu nikasubiri ndege ya kwanza kuja nayo Tabora”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kutokana na hali ya kimazingira kua si rafiki tena hivyo hapakua na haja ya kuzalisha mjadala wowote. Mzee Kusekwa akatoka nje haraka ili kuwatuliza na kuwatangazia waalikwa wote kua punde msafara wa kuelekea Kuoa utaanza. Dakika kumi na tano tu zilitosha kwa Bwana harusi mtarajiwa kujiandaa kisha safari ikaanza, msafara mkubwa wa magari na pikipiki ulifuatana huku mavuvuzela yakifanya kazi yake njia nzima, hakika vijana walimuitika kijana mwenzao.

    Walipowasili Chemchem kwa Mzee Fungameza nako wakapata mapokezi makubwa na ya kuvutia sana huku umati wa wahudhuriaji ukiogezeka mara dufu tofauti na awali asubuhi walipohudhuria kwa mara ya kwanza kabla hawajaanza kutawanyika baada ya kusikia uvumi kua baba Harusi ameingia mitini, Bila shaka waliongezeka kuja kujionea tukio hilo lilitaka kuwakatisha tamaa mwanzo. Shamrashara, nderemo na vifijo viliwatawala katika uwanja wa Mzee Fungameza wakati ndoa ikifungwa, Hatimae Suhail akatwaa ‘Jiko’, tukio hilo likafuatiwa na Sherehe fupi lakini nzuri vilivyo, watu wakala, wakanywa na kusaza.



    Baada ya Ndoa na hafla fupi kukamilika sasa msafara ukaingia barabarani kuelekea nyumbani kwao na Suhail ambapo nako waliandaa Sherehe nzuri ya kumpongeza kijana wao kwa kupata mke. Sherehe ikahitimishwa kwa siku tatu za Fungate iliyoandaliwa na kufanyikia katika Hotel kubwa ya ‘FrankMan Palace Ord’ ambapo baada ya kukamilika kwa fungate hiyo Suhail na Sharifa wakaondoka mkoai Tabora na kuelekea Jijini Dar kuanza maisha mapya ya Ndoa

    *****



    Maisha hayakua mabaya kwa Suhail, Sughuli zake ziliendelea vizuri pasi na kizuizi chochote, kampuni zake mbili ya Upakuaji na upakiaji mizigo bandarini pamoja na ile ya masuala ya Bima zilikua zikimuingizia pesa nyingi na kumuingiza katika orodha ya vijana wadogo waliotwaa ukwasi mkubwa kwa muda mfupi, Pia aliongeza kampuni zingine kubwa kama tatu ikiwemo ya Uchimbaji madini huko Geita,



    Hakika maana ya Maisha kwa uhalisia wake wa kuishi kwa raha mustarehe ilijionesha kwa Suhail,



    Kuoa kwake hakukua na matatizo yoyote kwa Mzee Sufiani ambae alipewa taarifa na Shekhia mwenyewe kwa kuelezwa makubaliano aliyoyafikia na Suhail kuhusu atakavyokua akiishi na Sharifa. Nyumba ya mbezi aliishi Shekhia na Nyumba ya Ilala aliishi Sharifa japo Sharifa hakuelewa chochote katika siri hiyo ya ndani kabisa ya Suhail.



    Kutokana na usiri mzito wa Ndoa yaSuhail na Shekhia ikabidi sasa Mke atakaekua akitambuliwa na jamii atakua ni Sharifa. Hakuna aliejua kua Suhail amefunga ndoa na Sharifa zaidi ya rafiki zake Shekhia wawili tu aliomaliza nao chuo, Nancy Kileo na Mwacheni Faraji.



    Maisha yakasonga mbele



    MIEZI MITATU BAADAE



    Hali ya raha na amani vikaanza kua ni msamiati wa kichina kwa Suhail, Shubiri ikatumbukia katika bwawa la raha alilokua amebweteka akiogelea, Suhail na Sharifa wakawa mithili ya Chui nap aka kwa jinsi walivyoanza kuishi kwa uadui huku kila mmoja wao akimuona mwenzie kua ndie tatizo. Nyumba ikawa haikaliki, chakula hakiliki, hakuna jambo wala Cheko. Hii yote ni baada ya Sharifa kutambulisha msimamo wake mpya kwa Suhail kua anaitaka haki yake ya Ndoa japo aliamini kua mumewe ni ‘Mbovu’, alichotaka yeye ni kuanza kutembea kwa wataalamu kutafuta tiba ya tatizo hilo la mumewe kitu ambacho Suhail alikipinga na kukikwepa sana kwani aliamini kua kwa kufanya hivyo ni kujihatarishia maisha yake kwani endapo wataanza kutembea kwa matabibu mwishowe mkewe huyo ataangukia mpaka kwa waganga wa kienyeji ambao kama atapatikana mjuzi kama Mzee Atrash basi mambo yote yatawekwa hadharani na itakua balaa.

    “..Nakwambia hivi Suhail mimi ni mwanamke makini ninaejitambua, nimeshakugundua kua wewe una hila unaiendeleza kisirisiri nd’o maana unakwepa hatua za kujitibu, sasa kwa taarifa yako nimeshakuchoka mwanaume wewe na nimedhamiria kabisa kutafura njia mbadala ikiwemo kuwaeleza wazazi juu ya tatizo hili,” Sharifa alikua akiongea kwa ghadhabu huku akimuangalia Suhail aliekua amevaa fulana nyeupe huku akiwa amejilaza kitandani baada ya kutoka kuoga, Suhail aliogopa sana kusikia mkwara ule mzito kutoka kwa mkewe, ulikua ni mkwara uliomuingia sana na hakutaka jambo lile lifikie huko hivyo sasa ikampata kazi ya ziada ya kumbembeleza a kumsihi mkewe asithubutu kufanya hivyo

    “Mke wangu leo umefikia hatua hii ya kutaka kunidhalilisha na kunifedhehesha kwa wazazi kwa kutoa siri zetu za ndani?! Hebu jitafakari upya we ni mke bora kweli..” Kabla Suhail hajaendelea kuitafuta huruma ya Sharifa akakatishwa tena na mkewe huyo aliekua amefura kwa hasira

    “NO Suhail, hii sio siri tena, hili ni tatizo, tea kubwa hasa ambalo kama mimi na wewe tumeshindwa kuelewana kulitatua ni lazima sasa wazazi wasimame katika nafasi yao’

    “Aliesema mimi na wewe tumeshindwana ni nani? Tatizo we unadhani mimi nimebweteka tu, Hapana nimeshahangaika vya kutosha mpaka nikachoka.. Na hapa ninajiandaa wiki ijayo niende Nigeria nimeambiwa kuna mtaalamu mwingine wa Tiba hizi”

    “We usiichezee mimi hauendi popote nimeshakutilia shaka, utatumia dawa za hapahapa Tanzania mpaka tukihakikisha umenyoosha mikono ndipo tutafungua miguu kwenda mbele zaidi, na kila Tabibu tutakaempata ni lazima na mimi niende pamoja nawe kujihakikishia.. Na tunaanza sasa” Mbinu ya Suhail ya kutaka kusingizia kua ataenda kutibiwa Nje ili aonekana anafanya jitahada saa ikagonga ukuta kwa kukutana na masharti imara kutoka kwa mwanamke mwenye msimamo, Masharti hayo yakamshinda Suhail kuyatekeleza hivyo kuzidisha minyukano baina yao.

    Maisha ya hofu, huzuni na mashaka yaliendelea kumtesa Suhail akawa kama mwehu sasa maana ilifikia hatua akawa anaongea peke yake barabarani, hata kazini kwake huko Wafanyakazi wake waliomzoea kupita kiasi waligundua kua hali ya Boss wao haikua sawa wakati mwingine alizidiwa na mawazo mpaka hufikia kutiririsha machozi kama aliefiwa. Nyumba haikaliki tena, zaidi ya Salamu hakuna kingine isipokua ni malumbano kila kukicha, Hali hiyo ilimnyima Suhail amani kabisa japo ilimuonngezea umakini mkubwa hasa awapo na mkewe kitandani maana wakati mwingine alijikuta akitaka kuzidiwa kwa vitimbi na mitego ya mwanamke Yule mzuri wa Sura na Umbo, alihofia kuuingia mtego ambao ungeyagharimu maisha yake

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara kadhaa ambazo Suhail alikwenda kulala kwa Shekhia ndipo walau alipata utulivu wa nafsi japo napo alizidi kupewa Msisitizo wa tahadhari endapo atadiriki kuvunja makubaliano kwa kukutana kimwili na Sharifa mkewe halali, Vioja!

    Ikawa sasa kila anapokimbilia kuna vitisho na vimbwanga vyake. Kadri siku zilivyozidi kuyoyoma ndivyo ghadhabu za Sharifa zilivyozidi kuchagiza maamuzi magumu ndani ya kichwa chake, akaamua sasa kuanza kupitapita kwa Wataalamu kutafuta dawa, kila dawa alizopatiwa alimuwekea Suhail katika chakula kisirisiri na alijiapiza kupambana mpaka pumzi yake ya mwisho na kwamba endapo atashindwa basi lazima awashirikishe wazazi wao wote wa pande mbili.



    ***Vita ni Vita...!



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog