Search This Blog

VITA VYA MAPENZI - 3

 







    Simulizi : Vita Vya Mapenzi

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ikawa sasa kila anapokimbilia kuna vitisho na vimbwanga vyake. Kadri siku zilivyozidi kuyoyoma ndivyo ghadhabu za Sharifa zilivyozidi kuchagiza maamuzi magumu ndani ya kichwa chake, akaamua sasa kuanza kupitapita kwa Wataalamu kutafuta dawa, kila dawa alizopatiwa alimuwekea Suhail katika chakula kisirisiri na alijiapiza kupambana mpaka pumzi yake ya mwisho na kwamba endapo atashindwa basi lazima awashirikishe wazazi wao wote wa pande mbili

    *****



    Nyumba ikazidi kua chungu, mke amepamba moto, ndani hakuna kusikilizana, mizozo na mitafaruku kila kukicha. Hata raha ya maisha haionekani tena, Ladha ya chakula kwa Suhail ikawa ni msamiati wa kichina. Kila siku alikua akitafuta namna ya kupambana na tatizo lililo mbele yake, wakati mwingine alifikia hatua ya kutaka hata kuua au kujiua mwenyewe ili mradi tu aondokane na tatizo hilo, siku moja likamjia wazo kichwani mwake na baada ya kulichekecha akalipitisha na kulipa nguvu ya kisheria ndani ya halmashauri ya kichwa chake. Wazo lake hilo lilionekana kua ndio suluhu ya tatizo lake lakini ili alitimilize alilihitaji mtu mwingine tofauti na yeye alitekeleza kwa umakini na usiri mkubwa ikiwezekana hata kwa kumlipa pesa, aliamini kua sasa atapunguza kama si kumaliza kabisa tatizo lake endapo atalifanikisha zoezi lile kwa kadri ya kichwa chake kilivyopitisha azimio hilo, lakini sasa huyo mtu makini kumpata ikawa ni shida, alijaribu kuwafikiria watu kadhaa lakini hakuna alieonekana kukidhi vigezo vyake, alihangaika kwa siku kadhaa bila kupata mtu mwenye sifa alizozihitaji. ndipo siku moja akiwa analifikiria jambo hilohilo kengere ya ukumbusho ikagonga kichwani mwake, akamkumbuka rafiki yake wa karibu aitwae Msigwa. Hakika Msigwa alikidhi vigezo vyote kwa fikra zake yeye Aliamini kua atakua ndio funguo ya tatizo lake kama ataelewa somo na kukubali kumsaidia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Suhail na Msigwa ni marafiki wa siku nyingi walioshibana haswa, walikutana kwa mara ya kwanza walipokua wakijiunga kidato cha kwanza katika shule ya ‘MILAMBO HIGH SCHOOL’ iliyopo mkoani Tabora ambapo Msigwa alikua akitokea mkoani Iringa na Suhail akiwa ni kijana wa mkoa huohuo wa Tabora aliebahatika kuchaguliwa kujiunga na shule hiyo akitokea shule ya Sekondari Isevya ya hapohapo mkoani Tabora, Kwa kiasi kikubwa urafiki wao ulitokana na kupangiwa bweni moja lililokua likiitwa ‘RUGAMBWA’ na pia wakawa katika chumba kimoja kilichopo juu ghorofani. Kwa Msigwa ilikua ni bahati zaidi kumpata rafiki ambae ni mwenyeji wa mkoa huo wa Tabora ambao kwake yeye ulikua ni mkoa mgeni sana ikiwa ndo mara yake ya kwanza kufika hivyo alikua na uhakika wa kupata huduma za muhimu na msaada wowote endapo utahitajika kufanywa na watu wa nyumbani kwao. Na kweli Suhail akaenda kumtambulisha nyumbani kwao kwa Mzee Kusekwa pamoja na mkewe waishio mtaa wa Rufita ikiwa ni hapohapo katika manispaa ya Tabora, hakika nao walimpokea kijana yule kwa mahaba kama mtoto wao wa kumzaa hivyo mara kadhaa hasa katika siku za mwisho wa wiki viajana hawa marafiki wakawa wanakwenda nyumbani kwao kutembea na kubadili ladha ya ugali maharage wanaoufakamia huko shuleni kila siku japo hata hali ya uchumi ya Baba yake Suhail haikua nzuri lakini walau Mchicha na kisamvu kiliwaliza sana vijana hawa, wakati mwingine hata Suhail asipoenda nyumbani kwao lakini Msigwa aliweza kwenda peke yake na kushinda huko kama kijana wa pale tu. Hata siku moja ulipotokea Mgomo mkubwa sana shuleni hapo kutokana na wanafunzi kupinga huduma mbovu za chakula na ufundishaji wanazopewa, wakasusia kulala mabwenini na kutokula chakula cha shule hapo kwa takribani siku tatu mfululizo na walipoona hakuna hatua za makusudi za kuwasikiliza wakafanya ghasia kubwa sambamba na uharibifi wa mali za shulehali iliyopelekea mkuu wa Shule hiyo kutangaza kuifunga shule hiyo mpaka watakapotangaziwa vinginevyo hivyo wanafunzi wakatakiwa kuondoka shuleni hapo ndani ya masaa arobaini na nane kitu ambacho kilikua kigumu ukizingatia wengi wa wanafunzi wanatokea mikoa ya mbali na hawana pesa za haraka haraka lakini kwakua tayari hali ilikua ni ya hatari hivyo serikali ikasaidia kupeleka askari wa kutosha kuwadhibiti watakaokaidi agizo hilo la shule, ilikua hali mbaya sana kwani baadhi ya vijana waliuza vitu vyao vya thamani huku wengine wakikimbilia kuomba msaada katika nyumba za ibada ili wapate ahueni ya maisha na nanuli za kuwapeleka makwao. Lakini kwa Msigwa licha ya kua anatokea mbali sana lakini hakupata tabu yeye na Suhail walikimbilia nyumbani kwao mtaa wa Rufita ambapo waliishi vizuri tu wakisubiria tangazo la kufunguliwa kwa Shule, familia ya akina Msigwa huko Iringa ilipopata habari ile walitaka kuchanganyikiwa lakini baadae Mzee Kusekwa akawasiliana nao na kuwatuliza kua kijana wao yupo salama na anapata huduma zote nyumbani hapo. Hiyo ikawa ni hatua nyingine ya muhimu kati ya familia mbili za vijana wale, Wazazi wakawa marafiki kama walivyo watoto wao. Na hata Shule ilipofunguliwa vijana wakaendelea na masomo, na wakati wa Likizo ukifika Mzee kusekwa akawa anafungasha zawadi kadhaa anampa Msigwa apeleke huko Iringa kwa Wazazi wake ambao nao walimfungashia mara tu aliporejea masomoni Tabora, Ikawa ni kama udugu sasa

    *****



    Kupitia historia hiyo fupi Suhail na Msigwa walikua wameshibana sana kama ndugu wa damu, lakini baada ya kumaliza masomo yao ikawabidi kusambaana kila mmoja akiendelea na hatu nyingine mbele ambapo Suhail alijiunga na Chuo kikuu cha Dar es salaam wakati msigwa alipata chuo huko jijini Mwanza ambapo alikua akisomea uandishi wa habari. Baada ya miaka takribani minne ndipo tena Suhail na Msigwa wakakutana Jijini Dar es Salaam ambapo Suhail alikua akifanya biashara zake na Msigwa akiwa ameajiriwa na Kampuni moja kubwa ipatikanayo Ilala, jijini Dar es Salaam iitwayo TuwaKadabra Production, ni kampuni mashuhuri inayozalisha magazeti kadhaa ya kila wiki, inajishughulisha na uchapaji na usambazaji wa vitabu, pia inamiliki kipindi maarufu cha luninga katika vituo kadhaa vya luninga nchini.



    Kwa muda mfupi ambao Msigwa amekua akiandika habari katika magazeti ya ‘Mdadisi’ na ‘Haki’ yote yakiwa chini ya kampuni hiyo ya TuwaKadabra Production amejizolea umaarufu mkubwa sana kutokana na habari anazoziandika katika magazeti hayo, ni habari za kipelelezi na kichokonozi kuhusiana na watu mashuhuri nchini katika Nyanja za Siasa, michezo, na muziki. Mbali ya umaarufu huo aliojizolea lakini pia Msigwa alikumbana na matatizo kadhaa ikiwemo kutishiwa na mara kadhaa kukoswakoswa kuuwawa na baadhi ya vigogo wa serikalini kwa tuhuma kadhaa alizowaandika, na wengine walidiriki kumfikisha mahakamani wakidai anawachafua lakini huko kwenye mikono ya Sheria aliwabwaga vibaya kutokana na ushahidi wa matukio ayaandikayo, Hakika alikua na kipaji na mtandao mkubwa uliokua ukimpa habari nzitonzito za watu kibao, lakini hakujali kutishiwa aliendelea kutekeleza wajibu wake kwa umakini, umahiri, na Usiri mkubwa.



    Umakini, Umahiri, na Usiri ndivyo hasa vigezo vya Suhail kwa mtu amtakae hivyo akalipigia mstari jibu lililopita kichwani mwake kua Msigwa ataumaliza mzozo, japo hawakua karibu sana kama zamani kutokana kila mmoja kubanwa na majukumu yake lakini walikua wakitembeleana mara moja moja na kutambulishana kwa wake zao na bahati nzuri au mbaya kila mmoja alikua ana mke tu na hawakua wamejaaliwa kupata watoto kila mmoja kwa sababu zake.



    Akiwa katika gari yake aina ya ‘Land Cruiser’ akielekea kwa Msigwa maeneo ya magomeni alikua anaomba Mungu afike haraka ili afanye mazungumzo na rafiki yake huyo wa siku nyingi katika kulitafutia ufumbuzi tatizo lake na familia kwa ujumla. sasa alipofika maeneo ya Magomeni mapipa ikiwa si mbali sana na huko anapoelekea ndipo alipomuona mwanamke mmoja kupitia katika vioo ya pembeni vya gari yake akiwa amesimama sambamba na Abiria wengine waliokua kituoni hapo kusubiri daladala. Alikua ni mwanamke ambae alihisi kumfahamu, lakini kumfahamu kwake tu haikua jambo kubwa bali hali aliyomuona nayo mwanamke Yule ilikua si ya kawaida sana kama alivyofikiri, akasogeza gari yake pembeni kabisa ya barabara kisha akashusha vioo vyeusi vya gari yake akachungulia nje ya gari ili amuhakiki mtu aliehisi kumfahamu, Hakika alikua ndie yeye lakini hakua sawa kabisa, alikua amevaa rafurafu tu huku akiwa na mabegi kama mawili hivi, pia alionekana kua kama anaelia hivi ikabidi haraka Suhail apaki gari Ashuke kwenye gari, akafunga vizuri milango pamoja na vioo kisha akaanza kurudi nyuma alipompita dada Yule



    “Specyoza, mbona uko hivyo? Kuna usalama kweli?,” aliuliza Suhail kwa mshangao kutokana na hali aiyomuoa nayo mwanamke yule aliemfahamu vizuri kua ni mke wa rafiki yake kipenzi, Bwana Msigwa. Swali hilo la Suhail ni kama lililotumbua mfuko wa machozi ndani ya macho ya Specyoza maana sasa alishindwa kujizuia akawa analia waziwazi na kuruhusu mifereji ya machozi kutalii mashavuni mwake. Hali hiyo ilimfanya Suhail ajisikie simanzi sana bila ya kujua tatizo la shemeji yake huyo japo kutokana na dalili zinazotafsiriwa na mabegi aliyoyabeba Specyoza ni dhahiri amegombana na Msigwa. sasa kutokana na mazingira yale ambayo hayakua mazuri kuongea jambo lolote kutokana na macho ya Abiria wengi kuwashambulia wao tu na kuwafanya kama vituko pale, ikabidi Suhail ambembeleze sana shemeji yake waondoke mahala pale wakaingie kwenye gari yake, Specyoza alikubali baada ya kubembelezwa kwa muda kidogo wakaondoka na kuifuta gari ilipokua imeegeshwa, Huku nyuma waliwaacha abiria wengi wakiwashangaa, wengine wakionekana kuguswa sana na hali ya mwanamke yule na wengine wakisikika kucheka na kurusha maneno ya kebehi. walipofika wakajitoma ndani ya gari kisha Suhail akaondoa gari taratibu bila ya kuongea chochote na Specyoza mpaka walipofika mbele kidogo ambapo wakaegesha gari pembeni mjadala ukaanza

    “Haya kunani tena Shemeji yangu, imekuaje tena hivi?,” aliuliza Suhail huku akimgeukia Shemeji yake alieketi siti ya nyuma, lakini Specyoza alionekana kuzidiwa na hasira na uchungu maana kila alipojaribu kutaka kuongea ndivyo alivyozidi kulia kwa uchungu na sauti ya ‘kwikwi’, ikabidi Suhail ambembeleze sana ndipo akatulia kidogo na kuanza kuelezea mkasa uliomkumbaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “..Rafiki yako kanifukuza, na kaniambia kuanzia leo mimi na yeye basi, hanitaki tena, wala hataki kuniona maishani mwake…” alishindwa kumalizia maneno yake akaanza kulia tena, akatoa kitambaa cha laini na kujifuta machozi kabla ya kuendelea kuongea “..Yaani Msigwa nimemsomesha chuo kwa pesa zangu mimi kipindi hicho nafanya kazi mgodini mpaka amemaliza chuo, akawa hana muelekeo wa kupata kazi na bahati mbaya kipindi hicho mimi nilikua nimeachishwa kazi huko Mgodini baada ya kuchukua pesa za ofisi ambazo nilimtumia yeye amalizie kulipa ada chuoni, Akaenda kwao Iringa na mimi nikaja Dar kwa Shangazi yangu ambapo baada ya muda nikapata kazi katika ofisi ya tiGo haikuchukua muda nikamchukua akaja hapa Dar nikawa naishi nae na kumuhudumia kwa kila kitu japo sikua tena na kipato kikubwa kama awali, Akaniambia kua tufunge Ndoa ilinikamkubalia bila kujali hakua na pesa wakati huo, tukafunga ndoa japo ndugu zangu walipinga kwakua hatukua tumejipanga kimaisha lakini mimi niliwapuuza.. Kaka yangu mimi akamtafutia hiyo kazi ambayo imempa pesa na umaarufu anaoutumia kuninyanyasa leo hii..” Kabla Specyoza hajaendelea kulalama ikabidi Suhail amkatize kwa kumtupia swali

    “Pole sana Shemeji, Najua unaumia lakini tusifike huko mbali, Sasa kisa cha yote haya ni nini?”

    “..Ni hadithi ndefu sana shemeji yangu, kama ujuavyo mimi na msigwa tangu tumefunga ndoa ni karibu mwaka wa pili sasa hatujabahatika kupata mtoto hivyo hilo limekua ni tatizo kubwa sana, Ndugu zake na Msigwa hasahasa dada zake wamekua hawataki hata kuniona na wanamshinikiza Msigwa aniache, mwanzo Msigwa alikua ana msimamo na alikua upande wangu katika kunitetea lakini sasa amebadilika na hali imekua mbaya zaidi maana nae sasa hanitaki waziwazi, kila kukicha ananizushia mambo ya ajabuajabu ili apate sababu ya kuniacha, nimezigundua njama zake muda sasa..” alisita kidogo, akatoa leso yake laini akajifuta machozi kisha akaendelea “..Wiki iliyopita Msigwa alikua amepanga safari ya kuelekea Dodoma kikazi, ghafla name nikapokea taarifa kua kaka yetu mkubwa anaumwa huko kwake Morogoro hivyo ikanilazimu name kuondoka. Tukapanga kuondoka kwa pamoja siku ya jumamosi, na kweli ilipowadia siku hiyo tukapanda basi moja wote tukaondoka, Nilimbembeleza sana mume wangu tushuke wote hapo Morogoro ili nae akamuone Shejemeji yake lakini aligoma akidai kua anawahi jambo la muhimu sana huko Dodoma, sikua na pingamizi zaidi ya kumuacha aende tu nikamwambia kua kama hali haingelikua mbaya sana ningelirejea Dar kesho yake siku ya jumapili, Nilipofika Morogoro nikashuka na kumuacha yeye akiendelea na safari ya Dodoma, hapo Stand Morogoro nilipokelewa na watoto wa kaka yangu huyo ambae alikua mgonjwa, tukaondoka mpaka nyumbani ambapo nilikuta hali ya mgonjwa ikiwa si mbaya sana hivyo nikaendelea kukaa pale huku hali ya Mgonjwa ikiendelea kuimarika. Nilikaa pale Morogoro kwa siku kama tatu hivi ambazo ni hiyo Jumamosi niliyofika, Jumapili, na jumatatu, Kisha jumanne Nikarejea Dar lakini nilipofika nyumbani nikagundua kua simu yangu ambayo hua naweka line ya tiGo imepotea, nikaiangalia katika mifuko yangu yote bila mafanikio, ikabidi nimpigie simu kaka aniangalizie kule kama nimeiacha kwake, bahati nzuri akanijibu kua ameiona niliisahau juu ya Radio ya chumbani Nililaani kuisahau simu yangu lakini kumbe ilikua ni bora nilivyoisahau tu huo..” Alishusha pumzi zake Specyoza au Specy kama ambavyo rafiki zake walivyopenda kumfupisha jina lake, kisha akaendelea “..Mpaka kufikia siku hiyo niliporejea Dar Msigwa hakua amerudi Dar hivyo nikawa peke yangu tu nyumbani, nilikua nikiwasiliana nae mara chache sana, haikunishangaza kwani hali ya maisha yetu sasa yalikua ni ya aina hiyo mpya ya kisirani muda wote, kutokana na ukimya wake huo sikuona haja ya kumfahamisha kuhusu simu niliyoisahau kule Morogoro kwa kua nilijua hua hanipigii mara kwa mara katika namba ile japo anaifahamu na anayo kwenye simu yake. Hiyo namba ya tiGo nilipewa ofisini hivyo huitumia mara kwa mara kuwasiliana na wafanyakazi wenzangu wa kule kazini kwangu, hata hivyo nikajua endapo angepiga katika namba ile angekuta haipatikani kwani nilipowasiliana na kaka nilimwambia aizime tu ili asipatwe na bughudha ya kupokea simu. Sasa jana Ijumaa kaka alinitumia simu yangu kwenye Basi hivyo kwenye majira ya saa kumi alaasiri nikaenda ubungo kuichukua, nikaipata na kurejea nyumbani nilipofika nikakuta Msigwa nae ndo amerejea kutokea Dodoma, nikamsogelea pale katika kochi alipokua ameketi ili nimpokee ghafla nikashangaa napokelewa kwa kipigo cha mbwa mwizi. alinipiga makofi, ngumi, mateke, nk. Nikamuuliza nimemkosea kitu gani mpaka ananipiga kiasi kile? Hakunijibu kitu akauchukua mkoba wangu akamwaga chini vitu vyote kisha akaichukua ile simu yangu ya tiGo niliyotoka kuichukua stendi. Simu ilikua imezimwa kwakua sikukumbuka kuiwasha tangu nilivyoipokea, akaiwasha yeye na kuiwekea ‘Security code’ punde ikawaka na zikaingia meseji kama nne hivi, alionesha kushtuka kidogo kama vile hakutegemea kuona zile meseji zikiingia muda ule, akazisoma kisha hapohapo akanirukia na kuanza kunipiga huku akinitukana kua mimi ni Malaya na hanitaki tena, akaniambia kwamba alipokua safari alipigwa simu na rafiki yake siku ya Jumatano, saa sita mchana kua nimeonekana naingia Guest na kijana mmoja ambae ninafanya nae kazi pale tiGo anaitwa Msonjo, nilishangaa sana na sikutegemea kusikia habari hizo, huyo Msonjo ni kijana mmoja ambae hua ninaheshimiananae sana pale ofisini sasa leo naambiwa amkua bwana wangu tena Sikuamini, akanionesha hizo meseji zilizokua katika simu yangu ya tigo hapo sasa ndo nikachoka kabisa, zilikua ni meseji za kweli zikionesha Msonjo na mimi tunawasiliana mambo ya mapenzi, nilishangaa zaidi nikamwambia Msigwa kua hicho kitu sikufanya na ninakishangaa hasa kwani hizo meseji zinaonesha nilikua nikiwasiliana na huyo Msonjo siku ya Jumanne ili kesho yake tukutane Guest sikuziandika mimi, na hata simu yangu haikua hewani tangu siku hiyo ya jumanne mpaka hiyo jana siku ya ijumaa, nikamuelezea jinsi nilivyoisahau hiyo simu kwa Kaka na mpaka alipoizima, Cha ajabu alionesha kushtuka aliposikia maneno yangu hayo mpaka mimi nikamshangaa lakini ghafla akaendelea kunipiga huku akinishutumu.. mwisho akaniambia nifunge kila kitu changu niondoke Laa sivyo ataniua, Hakika nilichanganyikiwa sana nikampigia simu kaka huku nalia na kumueleza mkasa mzima ulivyokua, hata yeye alishangaa sana akaniambia kutakua kuna jambo tu hapo limejificha, hakuamini nilichomwambia kwakua simu inayonasibishwa na tukio hilo alikua nayo yeye.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akampigia simu Msigwa wakaongea kidogo tu lakini hawakuelewana ghafla wakaanza kujibizana vibaya na kutoleana maneno machafu, sikufichi shemeji Nililia usiku kucha kama mwendawazimu lakini haikufaa kitu, rafiki yako aliendelea kusimamia maamuzi yake, Sikuondoka nikalala hapohapo nyumbani mpaka asubuhi ya leo ambapo wakaja dada zake, nao wakanitokomeza kwa maneno machafu kua ninajaza tu choo cha kaka yao nimekalia umalaya ndo maana nashindwa kuzaa, Msigwa akaniambia ameniacha rasmi, akanifungashia mabegi yangu akaniambia niondoke.. Nikampigia simu kaka akaniambia niondoke niende nyumbani kwa Shangazi hapo Ilala ila yeye yupo njiani anakuja Dar karibia afike” alipofikia hapo tena Specy akashindwa kujizuia akaanza kulia tena kwa uchungu huku akiingiza mkono katika pochi yake, akatoa Simu yake hiyo iliyoleta majanga ya ajabu na kuifungua katika sehemu ya meseji. akamuonesha Suhail zile meseji zinazoonesha kua alikua akiwasiliana na Msonjo..



    Meseji ya kwanza ilikua ni ya Specy akimtumia Msonjo siku ya jumanne saa tisa mchana, ilisema hivi;

    ‘Sasa mpenzi fanya basi kesho tuonane tukale raha zetu, nimeli-Miss penzi lako tamu na la nguvu ulilonipa ile w’End.’



    Meseji ya pili ilikua ni ya Msonjo akimjibu Specy, ilisema hivi;

    ‘Mnh tusije tukakamatwa bure, kwani huyo bwege wako hayupo?’



    Meseji ya tatu ilikua ni ya Specy ikionesha amejibu hivi;

    ‘Wala usijali Honey, yule Pimbi hayupo amesafiri tangu jumamosi amekwenda Dodoma hivyo tutakua huru na kufanya tutakavyo, hata ukitaka uje kwangu poa tu’



    Meseji ya mwisho ilikua ni ya Msonjo akijibu hivi;

    ‘Mnh kwako hapana, basi poa kesho saa tano tukutane Ilala pale Paradise Lodge’



    Suhail alisoma meseji zile tata na kubaki mdomo wazi asijue aseme nini, kila alichokifikiria kilimgomea kichwani, mkasa ulikua ni waajabu na kushangaza

    “Au baada ya kaka yako kuizima simu kuna mtu aliiwasha tena ndo akawa anajibizana na huyo kijana?,” Aliuliza Suhail

    “Hapana, simu yangu hua ina ‘Security code’ hivyo baada ya kaka kuizima isingewezekana tena mtu mwingine yoyote kuiwasha, hata kaka mwenyewe asingeweza tena, na kaka anasema alipoizima aliifungia ndani ya kabati yake na ndo maana hata yeye amekalipinga suala hilo, Pia nilimpigia simu mtu wa tiGo aliyopo kwenye ‘systerm’ aniangalizie kama namba yangu iliwashwa saa ngapi tangu ilipozimwa siku ya jumanne, akaniambia haikuwashwa mpaka kufikia hiyo jana jioni ambapo alieiwasha alikua ni Msigwa” Suhail alichoka kabisa akajikuta ameyasahau mpaka yaliyokua yakimpeleka huko kwa Msigwa, akakohoa kidogo kisha akamwambia Specy kua inabidi waende kuongea na Msigwa ili wayamalize mambo hayo, japo Specy aligoma kabisa lakini Suhail alimbembeleza mpaka akakubali, na hivi alikua akiipenda Ndoa yake akakubali kishingo upande



    Suhail akawasha gari na kuanza kuondoka eneo hilo huku kichwa chake kikiwa kimevurugwa kabisa na mkasa ule

    ****

    Dakika kama kumi na tano tu akawa ameshawasili nyumbani kwa Msigwa akiwa yuko na Specyoza katika Gari yake, lengo lake likiwa ni kutafuta Suluhu baina ya Wanandoa hawa kwani pamoja na kwamba hakupenda waachane kwa tukio lenye utata kama lile lakini pia hata shida yake yeye iliyokua ikimpeleka kwa Msigwa ingependeza zaidi kama Msigwa angeitekeleza akiwa katika Ndoa yake. Specy alitaka kugoma kushuka ndani ya Gari lakini Suhail akambembeleza mpaka akakubali, wakashuka wote na kuanza kuelekea kule katika mlango mkubwa wa kuingilia ndani, hapohapo Msigwa akatoka huku akifuatiwa na dada yake, Msigwa hakua yule aliezoeleka siku zote, alikua ni kama Sheikh alielishwa nguruwe, hasira zilionekana kumjaa usoni, alipofika tu akawazua kwa mbali Suhail na Specy

    “Kaka Suhail nakuheshimu sana ndugu yangu sitaki tuachane vibaya, naomba usiingie ndani mwangu na huyu mzoga, mwanamke Malaya mchafu sijapata kuona,” aliongea Msigwa mpaka povu likafurumia mdomoni

    “Kaka tafadhali Shusha jazba kidogo tuongee, kumbuka mimi ni ndugu yako na nina haki ya kuongea na wewe katika kuwekana sawa, haupaswi kutoa maneno mach..” Kabla Suhail hajamalizia akakatizwa na dada yake na Msigwa aliekua ameshatoka nae nje na kusimama pale uani

    “Kaka Suhail hebu haya mambo ungeyaacha kama yalivyo, Laiti ungeujua uchafu aliokua akiufanya huyu mbwa kwa kaka yetu sidhani kama hata ungekubali kuipakia hiyo najisi katika gari lako, Mtoe nje, Mtoe bana anatuletea kichefuchefu” Wakati dada yule akiendelea kutoa maneno ya kinyama na kishenzi huku akisaidiana na Msigwa mwenyewe, muda huo palikua na gari nyingine imewasili na kuegesha jirani na ilipokua imeegeshwa gari ya Suhail, mlango wa Gari hiyo aina ya Rangerover iliyokua imejaa vumbi ukafunguliwa akashuka Mwanaume mmoja asiefanana sana na gari ile kwa jinsi alivyokua amevaa. alikua amevaa kaptura ya jinzi, shati la draftidrafti, na miguuni amevaa Kandambili huku mkononi akiirusharusha funguo ya gari. Mtu huyu hakua Mzee wala kijana sana, alikua ni mtu wa rika la kati, kichwani kwa mbali alikua kama ana mchirizi wa Mvi uliokua ukianza kuukaribisha utu uzima, Ni bonge mwenye mwili uliojaziajazia ‘nyama uzembe’. Suhail hakumjua kwa haraka kua ni nani lakini alihisi kua Msigwa na Specyoza walimjua maana walishtuka sana kumuona. Mtu yule alikwenda kwa kasi mpaka pale uani ambapo Ngonjera ya maneno machafu na ya kebehi yalikua yakiendelea

    “Wewe nilikuambia uende wapi?,” aliuliza mtu yule huku akimtazama Specy kwa hasira kidogo

    “Kwa Shangazi”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa bado uko hapa unafanya nini? Au unaona raha unavyodhalilishwa na kuadhiriwa kama usiekua na kwenu?”

    “Hapana kaka, nilikua nimekwishaondoka ndipo nikakutana na huyu hapa kaka hua ni rafiki wa karibu sana na Msigwa, nikamsimulia ilivyokua nd’o akaniambia turudi mpaka hapa aje aongee na Msigwa” Hapo ndipo Suhail akapata picha kua huyo mtu ndie kaka yake na Specy aliekua njiani anatokea Morogoro, aligundua hivyo kwakua Specy alikwisha mdokeza kua kaka yake wa Morogoro amemuambia aende kwa Shangazi yake na yeye yuko njiani anakuja Dar

    “Aje aongee nini na mtu aliedhamiria kukufukuza?” Swali la bwana mkubwa yule safari hii halikupata nafasi ya kujibiwa na Specy kwani tayari Msigwa alitiririsha maneno

    “Bwana Shemeji kwahiyo wewe unafurahia umalaya anaoufanya mdogo wako? Au na wewe unahusika? Au ulitaka nimuache tu hapa aendelee kufanya ukahaba wake ili mwishowe aje aniue kwa magonjwa Kisa ulinisaidia kupata kazi.”

    “Msigwa unasema mimi nahusika na huu upuuzi wako? Sikiliza nikuambie kijana mimi kwanza sio shemeji yako tena kwakua umesema umeshamuacha mdogo wangu pili ukae ukijua mpango wako haramu ulioufanya umekosea njia nitaugundua tu, simu ya Specy haijahusika kufanya uovu wowote, hilo nina uhakika nalo asilimia zote kwakua nilikua nayo mimi, nimetafakari mara mbili na nimeshapata jibu kua hapa kuna mchezo unachezwa na nitaujua tu, Mimi ni Mtoto wa mjinikuliko wewe Bwa’mdogo nitakufuatilia mpaka mwisho na nitatekeleza wajibu wangu juu yako. Wewe si ni mchafuzi katika vyombo vya habari eeeh! Haya Sasa kanichafue na mimi, umemdhalilisha Specy na umeidhalilisha familia nzima kwa huu mchezo wa ajabu uliotokea.. tutaoneshana, Specy twende tuondoke,” alimaliza kuongea bwana mkubwa yule akamchukua Specy na kuondoka nae, ikabidi Suhail akawafungulie mlango wa gari yake ili Specy atoe mabegi, walipomaliza tu Specy na kaka yake wakaingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi ya ajabu.. Lilikua ni tukio la aina yake.



    Suhail akarejea mpaka pale waliposimama Msigwa na dada yake wakiwa kimya, Kilichomshangaza zaidi Suhail ni ile hali ya kutahayari iliyoonekana katika sura ya Msigwa, yaani ni kama vile anaejutia jambo Fulani lakini anajizuia kuionesha hali hiyo waziwazi,

    “Kaka mimi nikuache kwanza upumzishe kichwa, nilikua nina shida kubwa iliyonileta kwako lakini kwa hali hii nimejikuta nimeambulia kazi ya ziada ambayo sikuifikiria kabisa,” aliongea Suhail baada ya kumsogelea Msigwa

    “Oooh, No usijali kaka ni mambo ya kawaida tu, sidhani kama kuna haja ya kuchanganywa na ushenzi wa mtu mmoja. Kama ni jambo zito tukae tu tuongee,” alijibu Msigwa na kuzidi kuacha maswali mengi kichwani mwa Suhail

    ‘Hivi kweli umemfumania mkeo unaweza kua katika hali ya kawaida kama hii, unataka tuongee tu kilichoonileta! Mnh’ Mawazo yaliyokua katika mtindo maswali yalipita kichwani mwa Suhail huku akimuangalia Msigwa



    Suhail hakuweza kuongea Mengi, akamuaga rafiki yake na kumuahidi kua angerejea tena siku nyingine kwa ajili ya mazungumzo yaliyompeleka pale, Baada ya hapo akaondoka zake na kurejea nyumbani kwake kupambana na Mchaka mchaka wa mkewe Sharifa..



    *****

    IKAPITA karibu mwezi mzima bila ya Suhail kuonana na Msigwa huku Suhail akiwa ameshakata shauri kua hapaswi tena kumtaka msaada jamaa yake huyo kwakua kwa sasa hana mke tena, aliamini kua zoezi lake lingetekelezeka vizuri endapo Msigwa angeendelea kua ni Mume wa Mtu, wakawa sasa wanapowasiliana wanajadiliana mambo mengine tu ikiwemo tatizo la Ndoa ya Msigwa, hapakua na jipya Msigwa alijiamini kufuatia ushahidi wa Meseji alioufumania katika simu ya mkewe hivyo aliendelea kuuamini msimamo wake. Lakini sasa kutokana na ukweli kwamba haikua kazi rahisi kumpata mtu mwingine mwenye vigezo alivyovikusudia, akajikuta sasa anaanza kurejesha maamuzi ya kuongea na Msigwa japo aliiona harufu ya hatari ikimnyemelea lakini akapiga moyo konde akaamua kufanya kile alichodhani ni maamuzi ya kiume. Akaamua kumtafuta Msigwa ili sasa amfikishie ya moyoni, Hakua na haja ya kurefusha muda kwakua alikua Kariakoo katika moja ya ofisi zake akaiona haja ya kwenda haraka Magomeni kwa jamaa yake, akaingia ndani ya gari yake ndogo aina ya ‘Solano vheik’ na safari ya kwenda Magomeni ikaanza.. japo ilimchukua muda mrefu njiani kutokana na msongamano wa magari barabarani lakini hatimae aliwasili. Bahati haikua yake kwani hakumkuta jamaa yake, wadogo zake wakamwambia kua aliondoka muda mrefu sana hivyo nae akaamua tu kuondoka, lakini kabla hajaondoka akatoa simu ili ampigie ajue ni wapi alipo ili kama kuna uwezekano aweze kumfuata, Hakutaka kulaza damu!



    Simu ikaita kwa muda mrefu mpaka ikatakata bila ya kupokelewa, akajikuta anasonya peke yake ndani ya gari kama aliechanganyikiwa. Akawasha gari na kuweka ‘Gear’ ili aondoke ndipo sasa Simu yake ikaaita, akaitoa haraka na kuangalia ni nani aliekua akimpigia, alipomjua tu haraka akabonyeza kitufe cha kupokelea kisha akaweka simu sikioni na kuongea

    “Hallow..”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Niambie kaka, kwema?” ilikua ni sauti iliyojibu kutokea upande wa pili wa simu yake

    “Kwema mzee, we nae hautulii kwako,” Alitania Suhail na kumfanya Msigwa nae acheke kwa sauti baada ya kuelewa kua rafiki yake alikua amewasili nyumbani kwake na hakumkuta nd’o maana anamtania kwa maneno yale

    “Yaani we acha kaka utadhani miguu ilirambwa na Mbwa, haya niambie wapi hiyo?”

    “Mimi nd’o natoka kwako hapa, nilikua nimekuja kwa ajili ya yale mazungumzo yetu, kama vipi niambe ulipo nikufuate”

    “Mimi nd’o natoka Lamada Hotel, Ilala hapa”

    “Basi usondoke nisubiri hapohapo nakuja sasa hivi,” Alijibu Suhail na kukata simu, haraka akaingiza gari barabarani kwa kasi ili amuwahi Lamada



    *****



    Meza nzuri ya duara iliyokerezwa vizuri kwa ubao imara wa mninga ilikua Imebeba vinywaji ghali huku ikiwa imevitenganisha viti viwili, Kimoja akiwa amekikalia Suhail na Kingine Msigwa huku wakitazamana baada kumaliza kusalimiana na kujuzana habari na mitikasi ya mjini, ilikua ni katika bustani ya maua iliyopo katika Hotel hiyo ya Lamada

    “Kaka nimekuita ili niongee na wewe jambo moja la muhimu sana, jambo ambalo kwa muda mrefu sasa limekua likiyatesa maisha yangu na kunifanya nisione furaha ya maisha haya,” Suhail aliongea kwa utulivu mkubwa huku akimuangalia Msigwa usoni, Msigwa hakujibu chochote ikiwa ni ishara kwamba anaendelea kusikiliza kitu kilichomuamuru Suhail aendelee kuongea

    “Kinachonitesa ni Siri nzito iliyokua moyoni mwangu, Siri ambayo niliamini kua sikupaswa kumwambia mtu yoyote nikihofia kua endapo itavuja nitapata tabu maana waswahili wanasema ‘Siri ni ya watu watatu endapo wawili kati yao wamefariki’ sasa kutokana na hali kua ngumu ikabidi niitoe Siri hiyo kwa mke wangu kipindi hicho tukiwa hatujafunga ndoa, haikusaidia kitu zaidi ya kuongeza matatizo ambayo sasa yananilazimu niitoe tena hiyo siri kwako wewe kama ndugu yangu na rafiki yangu wa karibu nikiamini kua wewe ndio msaada wangu wa pekee uliebaki.. Sasa kaka utaweza kuitunza siri yangu? Na je utaweza kunisaidia kweli?” Swali la Suhail lilimfanya Msigwa ashushe pumzi nzito sana kabla hajajibu

    “Nina uwezo mkubwa sana wa kukaa na siri, hilo sina shaka nalo lakini hili la kukusaidia naogopa kulijibu haraka kwakua sijajua ni msaada wa aina gani uutakao, pia sijui kama utakua ndani ya uwezo wangu au Laa, ila ukweli utabaki palepale kua ni jukumu langu kukusaidia kama mtu wangu tuliotoka mbali sana”

    “Sidhani kamamimi ninaweza kukuleta Mswada ambao najua hauwezi kuutekeleza, bila shaka unaweza kama utadhamiria”

    “Haya tuendelee kaka, Lete maneno”

    “Iko hivi kaka, We ni rafiki yangu wa kitambo tangu shule, tumeongea na kufanya mambo mengi kwa pamoja lako likiwa langu na langu likiwa lako. Je katika kipindi chote hicho ulishawahi kusikia kua nina mahusiano na msichana yoyote?”

    “Ndio, ni Sharifa lakini uliniambia kua mlikubaliana kua msikutane kimwili mpaka mtakapooana”

    “Sawa, sasa ile ilikua ni mbinu yangu tu ya uwongo kwa Sharifa lakini ukweli ni kwamba nilimkatalia tusifanye chochote kwakua nilikua nikijielewa hali yangu”

    “Hali? Hali gani hiyo?”

    “Kaka naomba unisitiri kwa hili, naumia moyoni kukueleza kua mimi ni Mbovu, siwezi kukutana na mwanamke na nimeshahangaika kwa wataalam kibao bila mafanikio”

    “Eee bana eeh, pole sana kaka usikate tama unaweza kuja kupata mtaalamu na ukapona tu, sasa uliwezaje kuoa na kuishi na mkeo mpaka leo katika hali hiyo?,” aliuliza Msigwa kwa Fadhaa kubwa iliyomkumba

    “Hilo sasa ndilo tatizo lililofanya nikutafute wewe kama jamaa yangu unifae na kunistiri aibu yangu hii..”

    “Mnh, kivipi?”

    “Mke wangu nilimueleza mapema hali yangu kabla sijamuoa akanikatalia katakata kuniamini, akataka mpaka kujiua akiamini kua nimepata mafanikio ndo nataka kumuacha kisanii, nilijaribu sana kumuelewesha akagoma, akaniambia nilazima tu tufunge ndoa kisha hayo mengine yataelewekea ndani ya Ndoa. Ilikua ngumu sana kumkubalia lakini mwishowe tukakubaliana kua tutafunga ndoa lakini wakati huo tutakua tunatafuta wataalamu, tukafanya hivyo baada ya Ndoa bila mafanikio sasa Mke wangu kawa kama mbogo aliejeruhisha, nyumba haikaliki, kelele ndo kelele, ugomvi kila siku mpaka sasa nimechoka mwishowe nikapitisha uamuzi wa kulitatua tatizo hili ila mtu pekee wa kulimaliza ni wewe?

    “Kivipi sasa nilimalize mimi”

    “Nahitaji ili mke wangu awe mtulivu ni lazima awe na mwanaume mwingine atakaekua anakidhi haja zake, Mwanaume huyo atatakiwa awe Muungwana, Msiri, Mstaarabu na makini katika kila nukta. Na kamwe sitakua na wivu wala usumbufu kwake kwakua mimi siwezi kutekeleza jambo hilo mwenyewe.. Mtu huyo mwenye sifa tajwa ni wewe kaka” Maneno hayo ya mwisho ya Suhail yalimshtua na kumshangaza sana Msigwa, hakika hakutegemea kabisa kukutana na jambo lile

    “Suhail unasema?!,” Aliuliza Msigwa kwa Mshangao akiwa haamini alichokisikia

    “Nadhani umenisikia vizuri kaka, naomba usiniangushe katika hali tafadhali” Msigwa alikaa kimya kwa Sekunde kadhaa kisha akaibukaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nisikilize kwa Makini Suhail, wewe ni rafiki yangu kama ndugu tu, nakupenda kama unipendavyo wewe lakini kwa hilo hapana, No! Siwezi kufanya huo upuuzi kamwe, hebu jaribu kujifikiria mara mbili yule ni mkeo iweje upange mipango hiyo ya ajabu kaka? Siwezi kukufanyia ushenzi na ukatili kiasi hicho.. haujafikiaubaya kiasi cha mimikukudhalilisha kwa kutembea na mkeo”

    “Msigwa mbona unataka kupoteza uelewa ambao huo uko nao? Hakuna mke bila ya tendo kaka, pia ukumbuke ule sio kwamba ni ushenzi au ukatili utakaokua umenifanyia bali ni msaada mkubwa kwangu, utamfanya yule mwanamke atulie na kunipa heshma yangu katika jamii vinginevyo yakizidi ataweza hata kwenda kuwaambia wazazi wake na wangu kitu ambacho sitaki kamwe wakijue, nakuomba kaka nipo chini ya miguu yako unifae ndugu yangu”

    “Hivi Suhail hata watu watakapojua si itakua aibu kubwa zaidi? Kwako, kwangu na kwa Sharifa mwenyewe!!.. na kwanini uogope wazazi kujua wakati wanaweza kua msaada kwa tatizo hili? Hata huyo Sharifa akijua kua nimekubali kufanya huo ujinga si atanishusha kabisa!,” aliongea kwa msisitizo Msigwa



    “Sikiliza Msigwa katika vitu vilivyosababisha nikupendekeze wewe ni Usiri wako sasa nitashangaa utakaponiambia kua watu watajua, watajuaje sasa? Wakati mtakua huru wawili tu na nitawaacha muwe huru zaidi katika ile nyumba yangu ya Mbezi ambako hakuna waswahili kabisa, Pia Ondoa hofu kuhusu Sharifa nimekwishaongea nae kwa kina na akaridhia kabisa, na nilipokupendekeza wewe akawa hana pingamizi kwa kua ana kuamini kwa utulivu na umakini wako, hivyo kila kitu kipo tayari kaka,” Alidanganya Suhail lakini moyoni alijua kabisa kua hakua ameongea chochote na Mkewe

    “Sikia kaka, kumbuka ni masiku kadhaa tu yaliyopita nimeachana na mke wangu, na ninatuhumiwa sana kwa kumuacha japokua ushahidi wa meseji ulionekana katika simu yake mwenyewe kua anafanya uchafu sasa hauoni kama ikija kuvuja nitaonekana nilimuacha mke wangu ili nipate kutimiza mambo haya?”



    Ilichukua muda mrefu sana marafiki hawa wakiendelea kuwekeana hoja juu ya hoja lakini Msigwa aliendelea kukataa kabisa ikabidi sasa Suhail atumie nguvu ya pesa zake akimuahidi Msigwa kwamba atakua akimlipa pesa kama shukrani kwa kazi hiyo, na kwakua Msigwa anapenda sana pesa kiasi cha kujiongezea maadui maishani mwake akaanza kulegea japo hakuonesha kwa haraka hali ile

    “Sasa kaka, naomba uende uniache nifikirie kwa kina jambo hili kwakua ni zito sana na ukizingatia umenishtukiza mno, kisha tutakaa tena siku nyingine tuzungumze zaidi,” Alimaliza mjadala kwa mtindo huo bwana Msigwa

    “Ok poa kaka, ila nakusihi naomba usiniagushe wangu”

    “Usijali kaka tutalipanga na kulifikisha mpaka mwisho”



    Wakafikia muafaka na kupanga siku ya kuongea tena jambo hilo, Moyoni alianza kufurahi kuona Msigwa ameshalegea..



    Lakini laiti kama angejua kinachojiri asingethubutu!!

    *****



    Siku hiyo alirudi mapema zaidi nyumbani tofauti na kawaida yake, mara nyingi hujichelewesha kurudi nyumbani mapema akihofia kukwazana na mkewe, Lengo kuu la kurudi mapema nyumbani ni kuongea na mkewe juu ya mpango wake alioubuni na ambao tayari ameshamdokeza muhusika namba mbili ambae ni Msigwa, na sasa ilikua ni zamu ya muhusika namba moja ambae ni Sharifa. Siku hiyo nyumba ilikua kimya kama vile hakuna mtu alipofika getini akafunguliwa Mlango na Mlinzi akaingiza gari na kuiegesha sehemu yake kisha akaingia ndani akiwa na Shauku ya kuanzisha mazungumzo na mkewe japo bila shaka aliuona ugumu wa kuiwasilisha hoja yake. Alipofika ndani alipokelewa na Msaidizi wao wa kazi za ndani aliekua akinyoosha nguo zake, baada ya kupokelewa mizigo akaenda moja kwa moja mpaka ilipo ‘Seating room’ yake akamkuta Mkewe ameketi sofani akiangalia ‘Movie’ hizi za Kibongo, Akamsalimia

    “Haujambo mamaa?”

    “Sijambo,” alijibu Sharifa huku akiendelea kuangalia zake Tamthilia, Suhail akapitiliza zake chumbani akiwa hajua aanzie wapi.



    Dakika ishirini baadae akatoka mpaka pale barazani akiwa amevaa fulana nyepesi ya rangi nyeupe na Bukta yake akamuita mkewe kisha akarejea chumbani akifutiwa na mkewe,

    “Mke wangu nimekuita ili tujadili mustakabal wa Ndoa yetu, naona hali hii ya ugomvi na migogoro kila siku haifai kabisa hivyo nadhani tujadili suala la muhimu, tujikite zaidi katika kutafuta ufumbuzi na si mizozo ya kila siku,” Alianza kuongea Suhail baada ya kuwa wameshaingia chumbani na kuketi juu ya kitanda

    “Ufumbuzi ndo kitu ninachokililia kila siku, lakini mwenzangu haujali”

    “Mke wangu yatupasa kutafuta njia sahihi zinazowezekana kwa sasa, na si hizi ambazo zinaonesha kushindwa kufanya kazi kabisa”

    “Zimeshindwaje kufanya kazi? Hautaki kwenda kwa wataalam kutafuta tiba, hautaki kuwashirikisha wakubwa watusaidie, sasa utajuaje kama jitihada zimeshindwa kuzaa matunda?”

    “Mimi sihitaji tugombane mke wangu, nahitaji amani ya nafsi na familia nzima hivyo naomba na wewe uwe na dhamira kama yangu”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Haya embu sema wewe unatakaje?”

    “Hilo ndilo la msingi sasa..” Aliongea Suhail huku akijiweka sawa pale kitandani, huku akiyapanga maneno kabla hajayatoa kinywani “..Mke wangu mimi katika pitapita zangu huko kwa wataalam wa afya nikitafuta tiba ya matatizo yangu haya japo we unaona kama vile sijishughulishi, ndipo nikawa natafuta na suluhu ya amani ya ndoa yetu sasa huko nikashauriwa vitu vigumu kuingia kichwani, nikabishana na ukweli huo sana lakini baada ya kutulia na kutafakari kwa kina nikaona kuna haja ya kulifanyia kazi suala hilo..”

    “Mnh, haya sema tusikie”

    “Mke wangu hizi hasira na mitafakuru ya mara kwa mara ni matokeo ya kimwili zaidi ambayo yanahitaji kutulizwa, inabidi bila kumung’unya maneno tutafute mtu utakaekua ukishiriki nae tendo kisirisiri wakati mimi pia naendelea kuhangaika huko na kule, na katika hilo mimi sitakua na kipingamizi kabisa ili tu amani itawale humu ndani, na pia katika kurahisisha zoezi hilo linalotakiwa kufanywa kwa usiri na umakini mkubwa nimeamua kumuomba Msigwa kama mtu wangu wa karibu anaeweza kuitunza habari hi indie uwe unashiriki nae, na Pia..” Kabla hajaendelea akakatizwa na sauti kali ya Sharifa

    “Shut up Suhail, hivi una akili timamu kweli wewe? Umekua mpumbavu kiasi hicho? Yaani unadiriki kuniambia ushetani wako huo mimi, nakwambia hivi naondoka humu ndani, siwezi kukaa na ibilisi kama wewe..” Sharifa alikua akiongea kwa hasira na hisia kali mpaka akaanza kuvujisha machozi. Suhail akajikuta anaingi hofu sasa na kujuta hata kwanini alikua akifungua mambo yote yale kwa mkupuo, lakini alijikaza kiume akaanza tena kumtuliza

    “Tafadhali mke wangu, naomba unielewe sina nia mbaya kabisa, yote hii nafanya kutafuta Suluhu la kudumu katika ndoa yetu, hata mimi nilipoambiwa kwa mara ya kwanza nilishtushwa sana lakini nilipotuliza kichwa niliona umuhimu wa Suala hili na mpaka nimepata ujasiri wa kukuambia hapa” Suhail aliendeleza ushawishi kwa mkewe bila matunda, Mke akawa amepamba moto huku akilia lakini Suhail alijivika ujasiri akaendelea kumtuliza mkewe huku akimuaminisha kua ana nia njema kabisa,



    Baada ya muda mrefu wa majadiliano mwishowe akafanikiwa kumtuliza mkewe kutoka hali ya taharuki aliyokua nayo lakini hakufanikiwa kupitisha ushawishi wake. Wakaacha na mazungumzo hayo wakaenda kula na kisha wakarejea chumbani kwa ajili ya kulala kila mmoja kichwani akipiganisha mawazo yake mwenye

    *****

    Siku iliyofuata kama kawaida waliamka mapema kila mmoja akiyawahi majukumu yake, Suhail alijihisi mwepesi sana siku hiyo kwa kitendo cha jana yake kutoa la moyoni aliloamini litafanikiwa tu, wakati huo Sharifa akimfikiria na Suahil kwa kumuonea huruma akiamini kua mumewe maji yamemfika Shingoni ndo maana anatafuta suluhu gumu namna ile, Ni kweli maji yalimfika Shingoni lakini si kwa jinsi alivyofikiri yeye.. Maisha yakaendelea



    Kwa Suhail ilikua ni faraja kubwa kwake kwani tangu alivyowasilisha hoja hiyo kwa mkewe imesaidia kumfanya mkewe awe kimya kwa takribani wiki nzima bila ya kuongelea tatizo lake tofauti na ilivyokua awali, lakini Kwa Sharifa hali ilikua ngumu kichwani mwake alijikuta akihofia kuanzisha mada yoyote kuhusiana na tatizo la mumewe akijua kua endapo ataanzisha mada hiyo atasababisha muswada wa ‘kutembea’ na Msigwa utarejeshwa tena meza. Suhail aliendelea kupumua kidogo huku akiendelea na kazi zake japo kidogo kwa utulivu.. Maisha ya Suhail yalikua ni ya kusaifiri mara kadhaa japo safari zingine hazikua nzito sana zaidi ya kwenda kulala kwa Shekhia huko ambako alitimiza haki zote za ndoa kama Mume huku akimuacha masikini ya Mungu Sharifa akiendelea ‘Kudoda’ ndani



    Wiki mbili baade Sharifa akalianzisha tena ndani, ilikua usiku walipokua wakilala sasa ikawa amelianzisha balaa mwenyewe Suhail akaendelea kukazia msimamo wake, Mzozo mkubwa ukaibuka tena haikua kazi rahisi kufanikisha wazo lile lakini Mwanaume hakukata tamaa,

    “Hivi mume wangu kwanini u mpumbavu kiasi hiki? Hebu fikiria nimejitunza bila ya kuguswa na mwanaume yoyote kwa ajili yako kama tulivyokubaliana halafu leo unadiriki kuruhusu mwanaume mwingine aje atengeneze historia katika mwili wangu wakati wewe upo! Inashindikana nini kuhangaika kwa wataalamu kutafuta tiba?” hakika Maneno yale yalimchoma moyoni Suhail, akatamani aghairi maamuzi, ukisikia kuchanganyikiwa ndo huku sasa, Lakini kila alipofikiria viapo alivyopewa na Mzee Shamhurish, na kila akimfikiria Shekhia aliishiwa kabisa nguvu, Akawa hana jinzi zaidi ya kuendelea na msimamo wake ulele. Suhail alikua na uwezo wa kujenga hoja na kushawishi, alimpiga maneno mkewe kwa kumhadaa mpaka masikini ya Mungu binti wa watu akaingia mkengu kwa shingo upande, akaona kama ni kweli mpaka matabibu wamemshauri mumewe afanye hivyo nae akaona hakuna jinsi sasa akakubali!, akakubali kua atakua mara moja moja akilala na Msigwa lakini wakakubaliana kua Suhail nae awe anaendelea kutafuta tiba kwa kushirikiana na mkewe huyo, Suhail akakubali harakaharaka hakutaka kumuudhi tena mkewe asije akaghairi bure, alijua tu kua hayo ni maneno ya mpito lakini aliamini kua Sharifa atakapokua akitoka na Msigwa mwishowe atasahau kabisa habari ya Suhail hivyo kumfanya yeye awe na amani na mtiifu kwa Shekhia, aliogopa sana kumuudhi Shekhia akiamini kua atakua yuko hatiatini, aliijua vema nguvu ya Mzee Sufian Shamhurish, Jini Muasi. Baada ya maridhiano siku ikawa njema, na usiku ukawa mwanana,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Wakalala Doro!’



    *****

    ‘Kaka vipi?’

    ‘Poa Suhail’

    ‘Naona kimya kabisa’

    ‘Pilika ndugu yangu’

    ‘Nilikuacha muda mrefu kidogo, ili upate kufikiria kwa kina jambo letu lile’

    ‘Yeah’

    ‘Umefikia wapi Mzee?’

    ‘Iko hivi Suhail, nimetafakari sana juu ya jambo hili nimeona ni makosa makubwa na dhambi kubwa sana lakini kwaku wewe ni wangu sina jinsi kufanya kwa lengo la kukuokoa wewe’

    ‘Sijui hata nikushukuru vipi Msigwa’

    ‘Hapana kaka wala usijali, mimi na wewe damdam ila nikusisitize jambo moja tu Suhail’

    ‘Ndio kaka..’

    ‘Iko hivi nadhani unajua jinsi ambavyo mimi nimekua target kwa wanasiasa na vigogo mbalimbali kwa kufichua maovu yao magazetini, sasa hili suala linahitaji umakini na usiri wa hali ya juu sana’

    ‘Hilo ondoa shaka kaka, tutalimudu, sisi sote wasomi’ Hayo yalikua ni majibizano kwa njia ya Ujumbe mfupi wa maandishi katika simu zao za mkoni, Msigwa alikubali kuifanya kazi aliyoombwa.. Suhail akawa ameshinda. Ikaanza sasa mipango ya jinsi watakavyokua wanakutana, wakakubaliana itakua kule Mbezi, na itakua mara mojamoja sana ili kuepuka macho ya watu, pia wakakubaliana kua siku ambazo Msigwa atakua anekwenda kulala kule itambidi Suhail awe analala katika ile nyumba yake ya ilala au ya kule Kinondoni, Wakaafikiana na Zoezi likaanza kutekelezwa wiki hiyo hiyo



    Maisha yakaendelea huku Suhail akiwa ni mume jina tu kwa Sharifa huku jukumu lake la msingi kama mume likaendelea kutekelezwa kisawasawa na Msigwa ambaye ni rafiki yake kipenzi. Kwa Msigwa ilikuwa ni bahati ya mtende kujipatia raha za bure kutoka kwa Sharifa huku akiitumia fursa hiyo kutumia rasilimali za Suhail ikiwemo nyumba, magari, na pesa kila alipohitaji. Yote hii ni kwa ajili ya kutekeleza kazi ya siri anayomfanyia rafiki yake japo hali hiyo ilikuwa ikimuumiza sana Sharifa, hakika hakuridhia kufanyiwa jambo hilo ila hakuwa na jinsi kufuatia ushawishi aliokumbana nao kwa mumewe ambaye yeye alikuwa akijipongeza na kujiona shujaa baada ya kuhakikisha mpango wake umefanikiwa hasa ukizingatia hali ya amani ilianza kuchpua upya tena kwa kiasi kikubwa ndani ya nyumba yake tofauti na ilivyokua mwanzo.



    Sharifa alijiapiza kua ni lazima apambane na hali ile ya mumewe mpaka apone hata ikibidi kulitekeleza hilo kisirisiri kwakua hakuwa akipata ushirikiano wake. Mara kadhaa ambazo alilala na mumewe alimuandalia chakula na kumuwekea dawa kadhaa alizokuwa akizipata kwa wataalamu alioanza kuwazungukia kimyakimya huku nae akijitahidi kufanya hila na mitego ya hapa na paleili ‘kumuamsha’ mumewe.



    Siku moja Msigwa akiwa na takriban wiki mbili tu tangu asafiri na kuelekea Arusha kikazi, kama ada Suhail aliwasili nyumbani kwa Sharifa ambapo baada ya chakula na maji ya kuoga wakaingia chumbani kulala, Sharifa aliamini kua dawa zake anazopewa na wataalam wake zimeshaanza kufanya kazi hivyo ikawa sasa ni zamu yake kuonesha makeke mpaka mumewe ‘atingishike’, Mbwembwe na Mitego yake ilianzia kwenye Khanga yake moja iliyokua imeyang’ang’ania maungo yake kutokana na unyevu wa maji yaliyosalia mwili baada ya kuoga ilianza kumfadhaisha Suhail, hakika maumbile ya Sharifa yalikuwa na uwezo wa kumuita mwanaume yoyote aliekamilika kama Suhail, japo yeye alijifanya kua ‘Hafai’, hivyo aliendelea kujizuia lakini macho yake yaligoma kuacha kutazama mirindimo ile. Siku ilikuwa ngumu sana kwa Suhail ambaye mabadiliko ya kimwili yalianza kujidhihirisha, Mfadhaiko ukamvaa japo alijitahidi kujibana. hatimaye Sharifa akaigundua hali ya Mumewe akaamua kumfuata palepale kitandani alipokuwa amejilaza mumewe huyo wakati yeye akiwa katika ‘Dresing table’, alipofika hakuuliza kitu zaidi ya kuushambulia na kuutalii mwili wa Suhail kwa hila na mitego mpaka jasho likamtoka kijana wa watu. Suhail alijaribu kutoa upingamizi lakini viganja laini vya mwanadada mnyange vilizishinda hila zake, akaendelea kutalii karibu sehemu zote za mwili wa mumewe mithili ya motto anaekwagungua vocha taratibu. Mwanga hafifu chumbani mule na sauti ya radio kwa mbali iliyochanganyika na sauti laini ya mahaba kutoka kwa Sharifa vilizidisha hali ya mazingira kuimeza hofu ya Suhail, Akili ikaruka kabisa asijue anafanya nini, akawa anahema kama aliekimbia maili kadhaa, hatimaye akaona liwalo na liwe akajiachia kabisa na kumpa Uhuru Sharifa, Uhuru ambao ulimshtua sana Sharifa baada ya kuiona waziwazi hali ya mwanaume Yule kua iko sawa bin sawia. Sharifa alichanganyikiwa kwa furaha, hakuwamini anachokiona, ilikuwa ni kama bahati ya Mtende, yaani Mumewe aliehangaika kwa miaka yote kusaka dawa kila kona hatimaye hali imeimarika, alijipongeza kwa ushujaa wake wa kutafuta dawa na kumpa mumewe kisirisiri japo hakujua kua mumewe hakuwa ‘mbovu’ kamwe. hakuwa tena na haja ya kuongeza ghasia pale kunako uwanja wa fundi seremala badala yake bila kurefusha muda akaliwahisha zoezi alilolikosa kwa mumewe huyo tangu alipoolewa, Suhail nae bila ajizi akiwa hajitambui akalivunja Sharti alilopewa na Shekhia pamoja na Mzee Sufian Bin Shamhurish, Tendo likafanyika, Hilo likawa kosa kubwa litakayoyagharimu sehemu kubwa ya maisha yake!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Furaha kubwa iliyoendelea kutamalaki moyoni mwa Sharifa ilikatishwa ghafla na hali aliyoonekana nayo Suhail, ilikuwa ni hali ya ajabu kwa mwanaume aliepona tatizo kama lake, kwani hakuonesha furaha hata chembe zaidi ya dalili zote za huzuni kiasi cha kumuachia maswali mengi sana Sharifa,

    “Hivi una matatizo gani wewe,” Sharifa alimuhoji Suhail kwa ghadhabu lakini Suhail hakujibu kitu, mawazo yake yalikuwa yamesafiri umbali mrefu yakimuona Mzee Sufian na Shekhia jinsi watakavyomteketeza, hakika nguvu zilimwisha, alitamani hata angelikua anajua namna ya kuitumia Pete ile katika kumuangamiza Shekhia na Mze Sufiani ili aondoe udhia lakini hakuweza kamwe

    “Wewe si ninakusemesha?.,” Sharifa alibwata tena na kumtoa Suhail katika lindi la mawazo na huzuni

    “Ooh usijali mke wangu, yaani hata siamini kilichotokea”

    “Huamini nini sasa?”

    “Kama nimepona..” Suhail alijitahidi kuzificha hisia zake zilizokua tayari zimeshamdhihirikia Sharifa, Mjadala ukaanza upya lakini Suhail akajitahidi kumrejesha Sharifa katika hali yake ya kawaida ili asiigundue hali yake ya hofu, Akamvuta na kumlaza kifuani pake huku akimpa maneno matamu, Sharifa akautumia tena mwanya huo Kumuamsha upya mumewe, Nae ‘Akaamka’ tena, Hakika kitanda kilisulubiwa ipasavyo siku hiyo



    Ulikuwa ni usiku wa neema kwa Sharifa ila wa majuto kwa Suhail. Hatimaye wakalala na siku ikapita

    *****



    Siku iliyofuata Suhail aliingiwa na hofu kubwa akijua kua amefanya kosa kubwa na zito sana, aliamini kua bila shaka Shekhia ameona kila kitu, sasa kila akiifikiria adhabu yake kama si kifo kabisa akili ilimpea. Siku hiyo kazi hazikuenda kabisa mpaka wafanyakazi wake waliigundua hali ya Boss wao. Lakini hali ilikuwa tofauti kwa Sharifa huko nyumbani kwake ambapo kila mara alikuwa ametabasamu kwa zoezi la jana yake usiku, aliamini kua sasa muda wa kuijenga familia yake na mwanaume aliempenda umewadia, hakutamani tena japo kulisikia jina ‘Msigwa’ na akadhamiria kua usiku wa siku hiyo atamueleza mumewe kua hahitaji tena kuonana na Msigwa midhali yeye ameshapona tatizo lake



    “Mume wangu kuna jambo zuri nataka kukueleza,” Aliongea sharifa huku akimuangalia Suhail wakiwa juu ya meza wakipata chakula cha usiku baada ya Suhail kurejea kutoka kazini

    “Jambo gani hilo?” Suhail alijibu kwa mashaka tele huku kichwani akiwa na mpango wake kabambe

    “Kwakua wewe umepona mimi nadhani sina haja tena ya kukutana na Yule mshenzi”

    “Mshenzi?”

    “Ndio, huyo Msigwa wako”

    “Hapana, haupaswi kufanya hivyo kwa sasa inaweza kua na athari kubwa, ni lazima twende hatua kwa hatua kabla hatujafikia uamuzi wowote” Suhail alijibu huku kichwani akiwa amedhamiria kuanzisha tena utata wa kutokumruhusu Sharifa japo kumshika tu ili asipate fursa ya kulirejea tukio la jana yake akiamini huenda akapata ahueni kwa Sharifa kwani alipanga kusingizia kua ilijitokeza hali ya ajabu sana akashindwa kujizuia

    “Hivi we mwanaume ni hayawani au? Inakuaje hauna akili kiasi hiki, yaani unashindwa kuwa na wivu kwa mkeo, kwahiyo wewe unataka niendelee kutumiwa na mtu mwingine wakati wewe upo?”

    “Sina maana mbaya mke wangu, ila mwenzio nafikiria mbali zaidi, sasa Je vipi kama itakua hali hii imejitokeza kwa mshtuko wa siku moja tu halafu ikagoma kujirudia hauoni tutakua tumefanya kosa kubwa kumzuia Msigwa?”

    “Acha upumbavu wewe, sio mjinga nakwambia hivi ukileta mchezo katika hili tutaachana vibaya, umekwishapona wewe na leo tutaendelea na mchezo kama kawaida” Maneno ya Sharifa yalimzidisha hofu Suhail, akawa hajitambui kabisa, nyumba akaiona chungu, akatamani hata kukimbia lakini haikuwezekana hivyo akaona silaha ya pekee ni kuzidisha malumbano na mgogoro ili apatie sababu ya kutokusogeleana na Sharifa, na akafanikiwa katika hilo vita ikawa kubwa hatimaye wakalala Dolo



    Maisha yakaendelea, hali ya amani ikatoweka tena nyumbani kwa Suhail na Sharifa, wakawa kama chui na paka, kila mmoja akimkasirikia mwenzie, Suhail aliendelea kujifanya kua ile hali yake ya ubovu imemrejea tena lakini cha ajabu hakutaka kumpa nafasi Sharifa japo ya kumgusa tu akijua kua ‘Atashituka’. Hali hiyo ya sintofahamu ikachukua takriban wiki tatu na ‘Ushee’ mpaka Msigwa aliporejea tena Dar es Salaam, Suhail akafurahi akiamini kua Msigwa ataendelea kutimiza zoezi lake kama kawaida ili Sharifa apate utulivu na asighasi tena, lakini ikashindikana, Sharifa akaendelea kua na Msimamo wa kukataa kuonana na Msigwa.



    Siku moja Suhail akiwa kazini kwake ameketi, mawazo yalikuwa yamemzidia kiasi kwamba kama angetokea mwendawazimu mmoja akamshtua kwa ghafla basi angeweza hata kumuua kwa Mshituko, Hofu ya Suhail ilizidi kuongezeka kwani tangu afanye tendo lile na Sharifa hakupata kuwasiliana na Shekhia alikuwa akijuliza ni wapi ataanzia, wala hakwenda kule Mbezi nyumbani kwa Shekhia. Sasa kimya kimezidi akaamua kama mwanaume kujikaza na kumpigia simu yake haikupatikana, akapatwa na hofu. akaamua tu kwenda Mbezi sasa kumuangalia lakini nako hakumkuta, akatamani kuitumia ile Pete yake ili imuoneshe uelekeo aliopo mkewe lakini alihofia kufanya hivyo kwani angemshitua Mzee Sufiani, maana kila anapoitumikisha Pete ile Mzee Yule hupata taarifa na kumfuatilia kila nukta, akaamua tu kutulia japo hakuwa sawa kabisa kichwani kwani na hali ya Sharifa haikuwa nzuri, asubuhi hiyo alipoondoka nyumbani alimwacha Sharifa akielekea hospitali, alikuwa akiumwa!.

    Sasa akiwa katika lindi la mawazo ndipo simu yake iliyokua ikiita ikamtoa katika hali ile ya tafakuri, akaiangalia na kuona jina la Msigwa, Akashituka kidogo, akajikaza na kuipokea

    “Hallow kaka”

    “Suhail,” Aliita Msigwa kama anataka kupata hakika anaongea na Muhusika

    “Ndio mimi mkuu, vipi salama?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hakuna cha salama hapa, sasa nisikilioze kwa makini sana..” Msigwa alionekana kuchukizwa na jambo kubwa sana maana si kawaida yake kuongea na Suhail katika hali ile “..Iko hivi kama ulikuwa ukidhani mimi ni mtoto sana basi badilisha fikira zake, mimi ni mtu mzima tena timamu, mchezo mnaojaribu kuupanga wewe na mkeo nimeuelewa sasa nitakudhalilisha na kukuangamiza na utajiri wako huo wa haramu” Suhail alishangazwa na maneno yale ya rafiki yake lakini hakujua kinachoendelea ikabidi aendelee kumtuliza kwanza ili amuhoji vizuri

    “Sasa kaka ungepunguza kwanza wahka ili tusemezane vizuri kwani tatizo nini hasa?”

    “Unajifanya hulijui tatizo? We si ulikuja kwangu kichwa chini mikono nyuma ukilalamika nikusitiri ili kukulindia ndoa yako, kumbe ulikuwa unataka kunitumia tu nguvu zangu ili baadae ukishapata unachotaka unibwage sio, nakwambia hivi mimi nina mtandao mkubwa nitakupoteza wewe na huyo kahaba wako,” Msigwa alimalizia kulalama kisha akakata simu na kumuacha Suhail akiwa kama aliechangnyikiwa. Kiti kilikuwa kichungu, akasimama, akasogea mpaka mlangoni lakini hakutoka nje akarejea tena alipokuwa ameketi lakini kabla hajaketi tena simu yake ikaita, akajua ni Msigwa tu huyo, akaipoteza kwa dakika kadhaa huku akijipanga cha kujibu, alipoiangalia simu akakutana na namba ya mkewe, Sharifa

    “Sema,” Suhail alipokea simu kwa hasira

    “Mume wangu, nina good news”

    “Enheeee nini?”

    “Nimetoka hospital kupima, Nimepata ujauzito yaani hata siamini mimi jamani,” Sharifa alijibu kwa furaha huku akisahau kua wana mgogoro na mumewe huyo

    “Nini?”

    “Mimba..”

    “Mbona sikuelewi wewe, mimba ya nani?”

    “We hayawani nini? Swali gani sasa hilo? Mimba yako wewe, na nimeshampigia huyo Msigwa nimemueleza kila kitu kua umepona na umenipa ujauzito” Suhail alishituka, macho yakamtoka, jasho likawa linamtiririka makwapani, Sasa akap[ata picha ya kila aliliosemewa vibaya na Msigwa, hasira ikazidi kuvilia ndani kwa ndani, akafoka kwenye simu

    “Hivi wewe una akili kweli? Kwanini umeamua kufanya ujinga huo, hauoni sasa umekaribisha vita hii? Msigwa amenipigia simu kanitukana sana, anachojua yeye kua mimba ni yake, na ni yake kweli”

    “Acha ujinga wako wewe, ni mimba yake iliingia kwa Rimoti? Mimba imeingia akiwa safari, siku niliolala na wewe..tena tafadhali uishie hapohapo”

    “Kwa jinsi ulivyonikera leo, omba Mungu nisifike hapo nyumbani, Laa sivyo nitakupiga mpaka ulazwe”

    “Kibao kimoja tu utakachokikutanisha na mwili wangu kitatosha kabisa kuniruhusu niwapigie simu kwenu Tabora nimueleze baba yako kila kitu, hatua kwa hatua, Njoo unipige nipo nyumbani” Majibu ya Msimamo kutoka kwa Sharifa yalimmaliza nguvu Suhail, akakata simu.



    Akainama chini huku akimfikiria Msigwa mzee wa uchafuzi kwenye magazeti hakika aliishiwa nguvu, akamfikiria Shekhia na wivu wake tumbo likamkata ghafla, na alipomfikiria jemedari mkuu Mzee Sufiani, Hakika alijuta majuto ya Nasuha. Akajiapiza kutorudi kwake siku hiyo!

    *****

    BAADA ya tafakuri nzito na ya kina mle Ofisini hatimaye Suhail aliamua kuondoka, akatoka na kuwapita wafanyakazi wake bila hata kuwaaga akaenda mpaka alipoegesha gari yake na kuiondoa kwa kasi huku nia na dhamira yake ni kwenda moja kwa moja Bagamoyo kumuangalia Shekhia ili pamoja na mambo mengine akatengeneze mazingira ya kumtaka radhi. Akiwa nyuma ya usukani wa Rangerover yake nyekundu aliamua kumtaarifu mkewe(Sharifa) kua amepata safari ya dharura ya kikazi mkoani Morogoro hivyo hatorejea nyumbani siku hiyo, Alidanganya! Ujumbe wake haukujibiwa.



    Akiwa njiani simu yake ilipiga mbinja mara kadhaa ikiashiria kuna Meseji zinaingia lakini hakujishughulisha kuziangalia si tu kwakua alikuwa akiendesha bali alijua ni Sharifa huyo analeta upingamizi. Alipofika mbali sana akakumbwa na kihoro cha kutaka kujua amejibiwa nini na Sharifa, akaichukua simu yake na kuperuzi, akakutana na meseji karibu tano, zote zikiwa ni kutoka kwa Msigwa, Ni meseji chafu za vitisho. Hakuijibu hata meseji moja akabaki kufuta machozi tu, Uadui umeingia sasa, Vita vya mapenzi alivyodhani vitakua kwa Sharifa na Shekhia pekee sasa vinaanza na yeye na Msigwa. Akaendelea na Safari huku mara kadhaa akitaka kusababisha ajali kutokana na msongamano wa mawazo katika kichwa chake, hatimaye akawasili Bagamoyo, na moja kwa moja akaenda mpaka katika Jumba la Mzee Sufiani na kuingiza gari ndani ya geti baada ya kufunguliwa na yule kijana Mlinzi wa getini. Lilikuwa ni jingo kubwa lililochini ya dhamana yake yeye tangu alipokabidhiwa usimamizi wa Jengo hilo, japo alikwishazoea mazingira yale lakini ukimya wa siku ile ulimtisha kiasi cha vinyweleo vyake kutuna na kuzidi kumsisimua kila mara, akaenda mpaka ndani na kuanza kuteremka chini kabisa yalipo makazi yao ya siri wawapo pale. Alipofika kule chini karibu na Chumba chao akamkuta kijana mmoja wa kiarabu amabe hua ni mtumishi wa Mzee Sufian awapo pale, alishangaa kumkuta kule chini kijana yule kwani hapaswi kua pale na badala yake hua kule juu kabisa kwa ajili ya usalama, akamsogelea

    ”We mbona upo hapa saa hizi?,” Suhail alimsaili kijana yule bila hata ya kumsalimu

    ”Nilikuja kusaidia shughuli za usafi kidogo kaka”

    ”Lakini jukumu la kufanya usafi huku si lako, yule binti anaehusika na kazi hizi yuko wapi?”

    ”Nani?”

    ”Hajra, kwani wewe haujui kua Hajra ndo mwenye kazi hizi za huku chini?”

    ”Nafahamu, Hajra tangu majuzi anakua zaidi chumbani huko kwa Shekhia anamuhudumia maana hali haikuwa nzuri sana”

    ”Kwani Mzee Sufiani yuko wapi?”

    ”Aliondoka siku moja kabla hali ya Shekhia haijabadilika”

    ’Inamaana Shekhia anaumwa?, kwanini Mzee hakuniaga kama anaondoka!!’ Suhail alikuwa akijiuliza mwenyewe kichwani mwake, haraka akamuacha kijana yule kisha akaenda mpaka katika mlango wa chumba chake na kuingia ndani. Alipofika chumbani macho yake yakapiga moja kwa moja katika kitanda chao ambapo Shekhia alikuwa amelala huku Hajra akiwa ameketi pembeni yake, akajongea mpaka pale kisha akasalimu

    ”Vipi Salama?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ”Kiasi tu, habari za huko?”Alijibu Hajra na kumtupia swali Suhail aliyekuwa amemkdolea macho Shekhia pale kitandani

    ”Imekuaje tena huyu?”

    ”Nadhani alipatwa na mshtuko wa jambo ambalo hakulipenda sasa ukizingatia na hali yake hi indo akazidiwa ghafla, ila kwa sasa anaendelea vizuri”

    ”Hali yake? Hali gain?”

    ”Ujauzito” Mshtuko usiomithilika ulimkumba Suhail kusikia Shekhia ni mjazito, akavuta picha huko Dar nako Sharifa ni mjazito hakika alichanganyikiwa, akamuangalia Shekhia pale kitandani, kasha akarejesha macho yake kwa Hajra, akajikaza na kuizuia ile hali yake ya hofu na taharuki iliyokwishajionesha waziwazi isiendelee kumpa faida Hajra, maana ni suala la kustaajabisha kuonekana hajui habari za ujauzito wa Mkewe japo ni kweli hakuwambiwa, akajiuliza Kwanini Shekhia hakumueleza hali yake hiyo hakupata jibu la harakaharaka, akairejea kauli ya Hajra kua Shekhia alipatwa na mshtuko wa jambo lililompelekea kuzidiwa hapo tena hakuhitaji mnajibu wa kumueleza kua Shekhia likwishajua kila alichokifanya na Sharifa, akashusha pumzi kwa nguvu, Hisia kali za kufakufa zikawa zinamnyevuanyevua kichwani mwake

    ”Ok, hebu tupishe kidogo tafadhali” Suhail alimtaka Hajra atoke nje, nae bila ajizi akatoka na kumuacha mtu na Mkewe, wawili tu!



    Suhail akajisogeza karibu zaidi na Shekhia aliyekuwa amelala, akainua mkono wake na kupeleka kiganja chake katika paji la uso wa Shekhia ili amuamshe lakini hakubahatika kutimiza azma yake ile, Ghafla mkono wake ulipigwa kikumbo kikali na mikono ya Shekhia, kumbe hakuwa amelala, alijifanya kulala kumbe alikuwa akifuatilia kila kitu. Akawa anamuangalia sasa mumewe kwa macho ya ghadhabu mpaka Suhail alipovunja ukimya

    ”Shekhia unaendeleaje Mke wangu?”

    ”Nani mkeo? Tena ushike adabu yako tafadhali, mimi sio mkeo tena, Mkeo ni Sharifa”

    ”Shekhia naomba unisamehe sana mke wangu, sikudhamiria kabisa kutenda jambo lile wala kukhalifu amri ya Mzee. Najutia sana upuuzi ule na tangu siku ile ninamgombeza kila siku yuke Shetani sitaki hata aniguse,” Suhail aliendelea kubwabwaja huku akiitafuta huruma ya Shekhia iliyoonekana kutoweka kabisa, hakuwa na haja ya kuficha chochote aliamini kua Shakhia amekwishajua kila kitu, muda wote huo Shekhia alikuwa akimuangalia tu jinsi mumewe huyo anavyoweweseka na maneno yaliyozidi kumpandisha hasira, Suhail akaendelea kuongea huku akiipeleka mikono yake katika tumbo la Shekhia “..Mke wangu nimefurahi sana kusikia u-mjamzito, naomba unisamehe tumalize tatizo hili ili tupate fursa ya kuulea ujauzito huu na hatimaye mtoto wetu mtarajiwa kwa upendo..” Akiwa anakaribia kuligusa tumbo la Shekhia akashangaa tena anaambulia kusukumwa na Shekhia ambaye sasa alikuwa amejiinua kutoka pale Kitandani na kuketi huku akitweta kwa hasira

    ”Uulee ujauzito wa nani?..Si ninakuuliza wewe? Na huo wa Sharifa unamuachia nani?, nakwambia hivi umevunja masharti uliyokubali mwenyewe na sasa ujihesabu kua wewe ni m’fu unaetembea, kabla sijamueleza Baba kila kitu nitakuacha kwa uionje joto ya jiwe kutoka kwa Msigwa” Ikawa sasa nipe nikupe, Shekhia anamshambulia Suhail vilivyo, hakuna maelewano lakini Suhail anajitahidi kua mdogo kama ‘Pilton’ akawa anaendelea kutafuta huruma ya mkewe huyo..



    Usiku ukaingia huku Suhail akiendelea kubembeleza bila mafaniko, giza likatanda kila mmoja akalala

    *****



    *****

    Siku ya pili ikaanza Suhail akiwa Bagamoyo akiendelea kumbembeleza Shekhia bila mafaniko, siku hiyo nayo ikaisha. Hakuwasiliana na Sharifa kabisa zaidi ya wafanya biashara wenzie, wafanyakazi wake, Meseji kali kutoka kwa Msigwa. Siku ya tatu ilipowadia akiwa bado angali Bagamoyo, mara simu yake ikaita, alipoangalia jina alikuwa ni Mzee Kusekwa, Baba yake Mzazi. Akaishike simu yake na baada ya kubofya kitufe cha kupokelea akaiweka sikioni

    ”Hallow, Shikamoo”

    ”Hiyo Shikamoo kama ni chakula kula wewe unenepe” Majibu ya Mzee Kusekwa yakazichemsha hisia za hatari kichwani mwa Suhail, akajua tu vyovyote iwavyo mambo yamekwisha haribika

    ”Baba kuna nini tena mbona sikuelewi?”

    ”Utanielewa tu mwendawazimu wewe, hivi kwanini we mtoto unataka kuniua kabla ya muda wangu? Haya madudu uyafanyayo unataka nieleweke vipi mimi kwa Mzee mwenzangu”

    ”Madudu gani baba?” Hakika Suhail alizidi kuchanganyikiwa hakujua kilichojiri japo alishaanza kupata taswira kwamba lazima Sharifa amewapigia simu tu

    ”Sikiliza sasa nikuambie, huna utakachoficha tena, Sharifa amekuja hapa tangu jana usiku, matusi na ghasia zako zote katueleza na ushahidi wa meseji zako za juzi zote zipo hapa”

    ”Mnh, meseji zangu za matusi? Mimi sijamtukana Sharifa hata mara moja”

    ”Sasa unataka kubisha nini wakati ushahidi uko hapa, sasa nisikilize Sharifa yupo hapa amekuja baada yaw ewe kumfukuza, naomba kesho uwe Tabora, vinginevyo ukatafute baba mwingine” Simu ikakatwa



    Suhail akaivugumiza simu yake juu ya kitanda, alipogeuka upande wa pili akakutanisha macho na Shekhia alieachia tabasamu la kebehi na dhihaka,

    ’Ni meseji gani niliyomtumia Sharifa mimi? Au ni huyu Shekhia alinivizia nikiwa nimelala?’Maswali yalipita kichwani mwa Suhail, raha yote ilimtoka.Mara wazo likamjia, akaiendea simu yake na kumpigia Sharifa

    ”Ongea,” Alipokea kwa dharau sana mwanamke yule alieonekana kua mtiifu sana kwa mumewe katika kipindi chote walichoishi pamoja

    ”We Sharifa umekua na dharau kiasi hiki?”

    ”Ongea harakaharaka kabla sijakata simu yako mie”

    ”Sharifa mke wangu kwanini umechukua uamuzi mbaya kiasi hicho, yaani umeamua kunidhalilisha na kunifedhehesha kwetu kwa wazazi wangu?”

    ”Umejidhalilisha na kujifedhehesha mwenyewe, usingeyataka hayo usingenitumia meseji chafu kama zile tena huku ukinibababisha kunifukuza kama nisie na kwetu”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ”Khaa mbona siwaelewi jamani, mimi nimekutumia meseji lini wewe?”

    ”Unajitoa akili sio? Yaani leo haujui ulinitumia meseji gani, au ulikuwa unaota wakati unaandika?”

    ”..Hebu niambie ni lini meseji hiyo imeingia katika simu yako” Sharifa akamtajia siku na saa iliyoingia meseji ile, hapo ndipo Suhail alitahayari, muda uliotajwa ndio yeye alikuwa akiendesha gari kuelekea bagamoyo, simu yake alikuwa nayo mwenyewe hakumpa mtu na hakuwandika meseji yoyote, akamuomba Sharifa amtumie hiyo meseji aione. Dakika mbili baada ya kukata simu ikaingia Meseji kwenye simu yake kutoka kwa Sharifa ikiwa ni meseji inayosemekana kua yeye aliituma huko kwa Sharifa, mapigo ya moyo yalimbadilika, akachanganyikiwa sana. Ujumbe ule ulisomeka hivi;

    ’NIKIFIKA HAPO NYUMBANI NISIKUKUTE MBWA WEWE, MIMI SIWEZI KULALA NA SHETANI MCHAFU KAMA WEWE. HIYO MIMBA IPELEKE KWA MWENYE NAYO AKAKUSAIDIE KUILEA, SITAKI KUKUKUTA KWANGU, UKIKAIDI NITAITOA ROHO YAKO NA HUYO MTOTO TUMBONI KWA MKONO WANGU KAMA ULIKUWA HAUJUI MIMI NI ZAIDI YA MAFIA’ Ni meseji ambayo Suhail hakuiandika kamwe, sasa imefikaje kwenye simu ya Sharifa ikionesha kua imetoka kwenye simu ya Suhail? Ikawa ni kitendawili. Baada ya tafakuri nzito Suhail akazirejesha fahamu zake nyuma kabisa, akamkumbuka Specyoza aliyekuwa mke wa Msigwa siku alipokuwa akimlalamikia kuhusu mchezo kama huo aliofanyiwa, akamkumbuka kaka yake na Specyoza alivyokua amekasirika mapaka akamuambia Msigwa kua ule ni mchezo aliouratibu yeye mwenyewe, hakika ulikuwa ni mchezo wa ajabu sana! Akaanza sasa kupata picha kua bila shaka ule ni mchezo unaofanywa na Msigwa, lakini anawezaje kuandika meseji za namna ile kama kweli ni yeye, hakuna jibu alilopata. Akatoa haraka simu yake na kumpigia Specyoza ili apate kujua kua walipata ufumbuzi gani katika lile tatizo lao, alipoiweka simu sikioni alikumbana na ujumbe usemao ‘Namba ya simu ya mteja unaempigia haipatikani kwa sasa tafadhali jaribu tena baadae’



    Suhail akainuka akiwa amechanganyikiwa, akaenda mpaka sehemu aliyokuwa ametundika nguo zake, akazichukua na kuzivaa, akaweka kila kitu chake sawia kisha alianza kutoka ndani na kuanza kuelekea juu ili atoke kabisa katika jumba lile bila hata ya kumuaga wala kumsemesha Shekhia. akiwa amedhamiria kuelekea Dar kutafuta ufumbuzi wa Meseji ile kabla hajaenda Tabora alikohitajika na Baba yake

    *****



    Kwa kawaida siku ya Ijumaa hutawaliwa na hekaheka na pilikapilika za watu mitaani, barabarani, na makazini. wengi wakiwa wanapambana kutafuta chochote kitu kwa kua mwisho wa wiki unaanza hivyo shughuli za kupelekea mkono kwenda kinywani hudorora kwa siku mbili mbele mpaka itakapoanza tena siku nyingine iitwayo Jumatatu.

    wengine hua katika maandalizi ya kuitekeleza ibada tukufu ya sala kwa mujibu wa imani yao, Lakini hali ni tofauti katika ofisi ya Bright Future Distributors Ltd inayomilikiwa na Suhail Kusekwa. Ambapo kila mmoja alikuwa katika hali ya huzuni na Simanzi kubwa, hakuna alieonekana kua na raha hata kidogo labda kama alikuepo yoyote aliehitimu mafunzo ya Unafiki kwa kiwango cha juu kiasi cha kuweza kuzificha hisia zake za furaha moyoni halafu kwa nje akauvaa utulivu wenye hisia za simanzi.



    Kubwa lililowakera wachapakazi hawa ni habari mbaya iliyoibuka kuhusu Boss wao, habari iliyopata kutwaa katika ukurasa wa mbele kabisa wa gazeti maarufu nchini, Gazeti la Mdadisi linalomilikiwa na Kampuni ya TuwaKadabra Productions. Habari hiyo si tu imewashitua wafanyakazi hao bali imewashitua watu wengi mtaani ambao kwa namna moja ama nyingine wamekua wakimfahamu ama kumfuatilia kwa karibu kutokana na utajiri wake Bwana Suhail Kusekwa. Habari hiyo inamtaja Suhail Kusekwa kua ni miongoni mwa matajiri vijana wanaoshutumiwa kuhusika na uuzaji wa madawa ya kulevya,



    Mwandishi wa makala hiyo Bwana Msigwa alienda mbali zaidi akaelezea kua baadhi ya wananchi wanamfahamu Kusekwa kua ni Kijana anaemiliki ukwasi huo kwa njia za kishirikina. Hakika habari ile iliwanyima hamu ya kufanya kazi watumishi wale kiasi kila mmoja akawa anaidurusi habari ile zaidi ya mara moja kujihakikishia, Watafanyaje sasa kazi kwa ari wakati Boss anaewalipa pesa nyingi kuliko kampuni yoyote jijini Dar inayojishughulisha na Biashara za aina yao Anadhalilishwa?. Wapo walioamini kua Msigwa ni rafiki wa karibu sana kwa Suhail Sasa ‘Kipi kilichomsibu mpaka akamwandika vibaya kiasi kile swahiba wake huyo wa siku nyingi’, Hapakuwa na mwenye jawabu



    “Amaa kweli Msigwa hana urafiki na mtu,” Alisema kijana mmoja muuza magazeti maofisini aliyekuwa amepazoea sana kuuza magazeti pale Ofisini



    Ujio wa ghafla wa Suhail katika ofisi yake uliwamakinisha sana wafanyakazi wake waliokuwa wanaendelea na Shughuli zao kwa kusuasua, aliwasalimu kwa haraka huku akielekea ofisini kwake na kuacha Mjadala wa chini kwa chini ukirindima, wakadhani huenda ameshazipata habari zake kwenye Mdadisi Kumbe mwenzao ana yake mengine kabisa. Kilingo Mkude, Meneja wa kampuni hiyo akamfwata Suhail ofisini kwake ili akamkabidhi Tiketi yake ya Ndege ya kuelekea mkoani Tabora ambayo alikwenda kumkatia jana yake usiku baada ya kupewa maagizo hayo, Aliingia huku Mkononi akiwa ameshika Gazeti la Mdadisi



    “Vipi hali Mkuu.” Alianzisha mazungumzo Mkude baada ya kuingia katika ofisi ile ya kisasa kabisa na kuketi

    “Aah kiasi nzuri, vipi umeshaandaa Report ya wiki?”

    “Ooh yes, ila sijaimalizia nadhani nitaimalizia jioni”

    “Ok poa, nitakuja kuipitia nitakaporejea kutoka Tabora”

    “Kuna usalama kweli huko kaka? Maana naona harakaharaka sana, halafu mbona umesema hali kiasi nzuri?”

    “Usalama upo japo sio sana kuna mambo tu kidogo ya kifamilia yalileta tabu, kuna Meseji za ajabuajabu zinaonekana kua zimetoka kwangu kwenda kwa Shemeji yako wakati mimi sijazituma kabisa, sasa naona muda hautoshi nilitaka nipitie Voda hapo wajaribu kuniangalizia huu utata kwenye mtandao, Lakini sio Issue sana vipi Tiketi yangu unayo hapo?”

    “Yeah ninayo, Mnh hayo sasa makubwa Meseji zinatoka kwako halafu haujaziandika wewe!!..nilidhani ni haya ya Magazetini,” Alijisemesha Mkude ili kupata hali halisi kama Boss wake anazo habari zile

    “Magazetini? Yepi hayo?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwani we hujapata habari zozote za magazetini?”

    “Sijanunua gazeti lolote leo, yaani hapa Nd’o natokea Bagamoyo” Mkude hakujibu kitu zaidi ya kulibwaga gazeti la Mdadisi juu ya meza ya kifahari ya Suhail Kusekwa ambaye kwa hofu na mashaka alianza kuliperuzi gazeti lile huku kila nukta moja mbele alizidi kuonekana kua mwekundu, bila shaka ni kwa ghadhabu zilizokua zikimpanda kichwani, akasimama kutoka katika kiti mkono mmoja ukiwa umeshikilia gazeti wakati mkono wa pili ukiwa umeshika kichwa kwa kihoro, hakuwamini akisomacho Gazetini. Ghafla akalitupia kwa Nguvu Gezeti lile juu ya Meza huku akibwabwaja kwa Sauti

    “NOO, Big No! yaani Msigwa ameamua kufikia hatua hii, this is too much”

    “Kwani kuna nini kinachoendelea Boss?” Swali la Kilingo lilimgutusha kua hakuwa peke yake pale ndani wakati anaropoka maneno yale

    “Ooh Kilingo huyu jamaa amefikia kileleni sasa, sina budi kumrejesha kwa muumba wake tu bora nikafungwe maisha, nitamuua kwa mkono wangu mwenyewe” baada ya maneno yale ya hamaki na jazba Suhail akapenyeza mkono wake mgongoni kwa ndani ya shati lake alilochomekea nadhifu kabisa akaitoa Bastola yake kwa ajili ya kujiandaa kulitekeleza azimio lililotuama kichwani mwake, azimio la kumuondosha Msigwa katika uso wa Dunia, Tukio lile likamuogopesha sana Kilingo, akamuwahi Suhail na kumzuia huku akimsihi kwa maneno ya Hekma kua asithubutu kuifanya jambo lile litakayoyagharimu maisha yake, maisha ya familia yake, na jamiii inayomzunguka. Ilichukua muda mrefu sana kwa Kilingo kumtuliza Bosswake mpaka akarejea kwenye hali ya kawaida japo kwa kiwango kidogo

    “..Cha msingi kaka wewe nenda kwanza Tabora ukayamalize hayo ya kifamilia kisha utakaporejea sasa tuanze kufanya utaratibu wa kisheria kwa kadhia hii ya kuchafuliwa kwako,” Alisema Kilingo Mkude wakati akiendelea kumliwaza Suhail, Suhail alitafakari kwa kina pale Ofisini na kukubaliana na Kilingo, na kwakua muda ulikuwa unayoyoma hivyo wakaondoka wote wawili wakielekea Airport ili wakati Suahil naondoka na Ndege, Kilingo arejee na Gari

    *****



    Masaa kadhaa katika anga yalihitimika bila ya ghasia yoyote mpaka Ndege ilipotua katika uwanja huo uliopo mkoani Tabora, bila ya kupoteza muda Suhail akachukua Teksi imepeleke nyumbani kwao ili sasa akapambane na utata mpya kutoka kwa Mzee Kusekwa na kwa Sharifa, njia nzima ilikuwa chungu kwake, ukijumlisha na habari ya gazetini ndio kabisa alichanganyikiwa, Zaidi ya salamu na maelekezo ya safari hakuongea chchote na dereva wa Teksi. Akiwa katika lindi la mawazo mara ghafla akapokea Meseji kwenye simu yake, ni ujumbe uliozidi kutonesha kidonda katika moyo wake, ilikuwa ni meseji ambayo hakuwahi kuifikiria kama itaweza kutoka kwa Mkewe, ilikuwa ni kutoka kwa Sharifa.



    Meseji ile ilisomeka hivi;

    ‘Nimekuvumilia sana mwanaume Suruali wewe sasa nimechoka, Sijui kwanini unamsumbua Rijali wa watu Msigwa, amejitahidi kukusitiri sana Sasa ameweka mamba unaanza kuweweseka. Ulitaka afanyaje? Na mwache ajilie raha zake We si ulishindwa, na kama utaendelea kumsumbua nitapasua jipu. Kama mvuvi vua, usichezee mashua Babu eeeh’



    Suhail alipikicha macho hakuwamini anachokisoma, akarukaruka kwenye siti yake akitamani awahi kufika nyumbani kwao, akajipigapiga kichwani kwa hasira// akajiweka sawa kwenye kiti, akaipitia upya meseji ile, hakika ilikuwa ni kutoka kwa Sharifa, alitamani kulia lakini machozi yalikuwa safari ya mbali sana.



    Safari yake ikazidi kuingia shubiri.



    Baada ya muda aliwasili nyumbani kwao ambapo alipokelewa na familia nzima kwa furaha kabisa isipokua baba yake tu Mzee Kusekwa ndio hakuwepo nyumbani

    “Haya pole na safari,” Alisema Mama Suhail baada ya kumpokea kijana wake



    “Ah ahsante Mama, habari za hapa nzuri tu, za huko?”



    “Huko salama, mbona wengine siwaoni?,” Alisaili Suhail huku akipepesa macho yake huku na kule



    “Baba yako amondoka asubuhi tu kwenda kufuatilia biashara zake huko vijijini atarudi usiku kabisa, na Mkeo yuko ndani huko amejilaza”



    “Jamani baba nae, haya mambo yake ya kuuza hizo nyanya zake si nilishamkataza!” Suhail aliendelea kujibu kwa utulivu huku akijitahidi kuzificha hisia zake kali zilizokua zikiendelea kuchemka ndani ya kichwa chake, alitamani hata amuwahi Sharifa hukohuko Chumbani akammalize tu lakini alichelea kuvuruga mambo

    “Mwenzangu we, Mjasiri haachi asili” Baada ya mazungumzo mengine ya hapa na pale Suhail aliinuka na kwenda katika Chumba alichokirimiwa mkewe, Akaingia chumbani kwa hasira huku akilifikiria lile neno la karne ‘Kama mvuvi vua usichezee mashua’



    “Mke wangu Sharifa, mwanamke niliekupenda nikakuheshimu, hivi kweli leo umeamua kua mwiba wa samaki katika koromeo langu? I can’t take this, I can’t” Suhail likua akilalama huku akifanya mfereji wa machozi katika mashavu yake, Sharifa aliyekuwa ameketi kitandani baada ya kuamsha na Suhail nae alikuwa amekodoa macho yake akimsikiliza Suhail, lakini kabla Suhail ahajaendelea nae akadakia

    “Suhail tafadhali usinifanye mie mtoto, unanitukana na kunidhalilisha kama si mkeo halafu unataka kunigeuzia mimi kibao. Mara ngapi umeniudhi na kunikera hasa lakini sikufikia kufanya maamuzi magumu lakini ulipoona nakuwekea kauzibe ukaamua kunitumia meseji zako chafu” Suhail alianza kujitetea kwa mkewe kua hakutuma kabisa zile meseji lakini hilo halikumuingia kabisa Sharifa, ikachukua muda mrefu wa majibizano ya kimyakimya mle chumbani kabla ya Suhail kurukia kwenye suala la piliCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “..Haya sasa kwahiyo nd’o ukaamua kuja kunichafua na kuniadhiri kwa Baba?”

    “We utakua umeanza kuchanganyikiwa! Nimekuchafua nini? Kwani uongo kua wewe U-Mgonjwa?..” akaweka nukta kidogo ili apate kushusha pumzi na kuendelea “..Lakini pamoja na hayo yote sijamueleza chchote baba kuhusiana na ugonjwa wako zaidi ya kumuonesha hii meseji yako ya kukataa mimba na kunifukuza nyumbani tena kwa kunitishia kuniua” Kusikia kua Baba yake ahajapewa habari yoyote kuhusiana na aibu yake ile ya uongo na kweli Suhail akashusha pumzi,

    “Lakini si ni wewe mwenyewe umenithibitishia hilo?”

    “Lipi?”

    “Kua mimba ni ya Rijali Msigwa..”

    “Naomba usinikoroge tafadhali, mwanaume uliekosa haya wewe unatafuta kunisingizia ili nami nionekane mbaya sio? Wapi na lini mimi nakaongea upuuzi huo?”



    Suhail akastaajabu ya Musa..yaani Sharifa anayakana maneno yake mwenyewe, akafungua simu yake na kutoa meseji iliyotoka kwa Sharifa, akamkabidhi Sharifa aisome. Ilikuwa ni ajabu hasa pale Sharifa nae alipong’aka kua haitambui meseji ile, alijitetea mpaka nae akaanza kulia huku akiwa hajui lolote,



    Baada ya mabishano ya muda mrefu Suhail alituliza kichwa akaamini kua zile meseji ni Mchezo mchafu anaofanyiwa, kwa mara nyingine tena akalikumbuka tukio la Specyoza, aliyekuwa Mke wa Msigwa jinsi nae alivyokua akilalamika kua hakuwandika meseji zilikutwa katika simu yake aliyoisahau Morogoro.



    Wakaongea kwa Muda mrefu sana hatimaye wakaridhiana kua wasiyakuze mambo yale, wayamalize wenyewe ili Mzee Kusekwa atakaporejea na kuitisha baraza la usuluhishi yaishe kwa salama. Kiasi Suhail alipata faraja kuona Sharifa hakuwahi kusema jambo lolote baya kwa Mzee Kusekwa, pia kuona Sharifa ameaminikua zile meseji zina hila ndani yake.. Wakakubaliana kua Sharifa asiseme chochote kwa kwa Mzee Kusekwa, na Suhail nae asiioneshe ile Meseji ya ajabu. Ila sharti gumu kuliko yote ni pale Sharifa aliposisitiza kua kama Suhail anataka yaishe ni lazima usiku ‘Walicheze Sebene’.



    Taswira ya Shekhia akiwa amekasirika ikamjia usoni Suhail, hamu yote ikamwisha tena!



    Siku ikaanza kuingia gizani bila Mzee Kusekwa kurejea, Suhail na Sharifa wakawa wamejumuika na familia kwa furaha kana kwamba hawakua na ugomvi mpaka Mama Suhail akabaki na alama ya kuuliza, Hatimaye usiku ukaingia, wote wakaingia kulala,



    Suhail na Sharifa nao chumbani kwao baada ya patashika ya hapa na pale hatimaye wakakisulubu kitanda kisawasawa, Kwa mara nyingine tena Suhail akavunja shart la Shekhia.



    Asubuhi na mapema wadogo zake Suhail walikwisha amka, na kwakua ilikuwa ni siku ya Jumamosi hivyo hawakwenda Shuleni, wote wakawa wanamsubiri kaka yao kwa hamu aamke wapate kuzungumza nae, hakika walimpenda kaka yao ila kutokana na umri wao au pengine kutokushirikishwa kwao katika masuala makubwa ya kifamilia hakuweza kujua kua ujioule ulitokana na matatizo ya kifamilia kwa kaka yao.



    Suhail aliamka kwenye saa tatu, akatoka nje akimwacha Sharifa nae anajizoazoa pale kitandani, Alipofika nje alikutana na Mzee Kusekwa akipiga mswaki upenuni na mwa kibada cha kufugia kuku, akasogea na kumsabahi, baada ya kujuliana hali, akaondoka na kwenda Bafuni kujiswafi mwili. Akarejea sebuleni kupata kifungua kinywa pamoja na wadogo zake waliokuwa wakimsubiri kwa hamu, haikuchukua muda mrefu Mzee Kusekwa akawaita Suhail na mkewe pamoja na Mama Suhail kule sebuleni kwa ajili ya baraza,



    “Haya we bwana nataka unijuze juu ya huo u-mbwa uliombatiza huyu binti mdogo, pili uniambie huyo mwenye ujauzito wake ni nani hasa kabla sijaendelea na mada,” Mzee kusekwa alianza kushambulia baraza baada ya kufungua kikao chao rasmi, Mzee alinguruma kama Simba kiasi cha kuwatetemesha wote pale barazani, Suhail wa watu hakutaka makuu kwanza akaanza kwa kuwataka radhi kwa usumbu uliotokana na tukio lile, lakini akatumia muda mrefu kumueleza baba yake huyo juu ya mchezo unaofanywa na mtu aliejifanya kutokumtambua kua ndie anaetuma meseji zile za kichonganishi na kwamba tukio hilo amepanga kwenda kuli-report Polisi kwa ajili ya tahadhari, akaenda mbali zaidi na kumueleza baba yake kua hata yeye pia alipokea meseji za ajabu kutoka kwa Sharifa lakini alipochunguza alijiridhisha japo inaonekana ni namba ya Sharifa ila hakutuma yeye asilani. Japo ilikuwa ni stori ya kushangaza lakini Mzee Kusekwa ilibidi aelewe tu na kuridhia baada ya kusikia kua wameshayaongea na kuyamaliza kama Mke na Mume, akawapa tu nasaha zake kisha akahamia kwenye jambo la pili lililomshangaza Suhail, ni kuhusu tuhuma za gazetini

    “Haya mwenzangu umekua maarufu sasa mpaka unaandikwa magazetini, kuna siku ulituletea habari za kusadikika hapa kuhusu hizo mali unazosimamia, Mama yako akashangilia hapa ila mimi haikuniingia akilini hata chembe sasa leo umeshaanza kuchunguzwa na wakubwaga hadharani, Kumbe hivi vijisenti vyako ni vichafu?” Maneno hayo ya Mzee Kusekwa yalikuwa kama Msumari wa moto ndani ya moyo wa Suhail, alijihisi kutetemeka kwa ghadhabu na hamaki, hakika sasa hili ni balaa hakutegemea kama Baba yake huyo angepata kusoma Gazeti lile la Udaku

    “Baba ingekua vizuri ukaniuliza badala ya kunituhumu, kumbuka kashfa hizo hata mimi zinaniumiza sana kama binaadamu na nahitaji faraja kutoka kwenu mkiwa kama familia yangu, hakuna ukweli wowote juu ya jambo hilo zaidi ya mchezo wa kuchafuana tu hasa ukishakuwa maarufu ama ukawa unamiliki kiasi kikubwa cha fedha ambacho kitapelekea Ushindani wa kibishara na matajiri wakongwe.. Na hicho ndicho kilichotokea, nadhani huo ni muendelezo tu wa huyu mtu anaetuma meseji mbaya hata kwa mke wangu ili kunivuruga kabisa kisaikolojia.. Sasa mimi na madawa ya kulevya wapi na wapi?”

    “Madawa ya Kulevya,” Alimaka Mzee Kusekwa kusikia habari za madawa ya kulevya

    “Ndio baba, si nd’o hizo habari nilizochafuliwa katika gazeti la Mdadisi”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Khaa, kumbe na gazeti la mdadisi limekutaja? Tena kwa habari ya kuuza madawa? Mwanangu hebu mche mola wako yaani jamii inapambana kuwanusuru vijana kutokana na madawa hayo halafu wewe umeyavamia, Sikua na khabari hizo maana mimi hua sisomi magazeti yenu ya Udaku..” Mzee Kusekwa akapatwa na mfadhaiko mpya, akainuka mpaka pembeni ya Sebule ilipo kabati kubwa ya vyombo, akachukua mfuko wake akatoa gazeti moja kisha akarejea nalo pale barazani, akaendelea kuongea

    “Mimi hua sisomi magazeti ya udaku, Hili hapa ndilo gazeti nililokua nikilitaja mimi tena ni la leo, linakutaja mwanangu wewe kua pesa zako zote uliwaibia wahanga wenzio kwenye ajali ya Basi kule jirani na Dodoma, kwanini wewe tu? Mbona tumeshawaona matajiri wengi tu, akina S.S Ally, akina Abdul Thabit, akina Ndamutahi wote hawakukumbwa na kashfa hizi! Iweje wewe ambaye mali yenyewe unasema unaisimamia tu?” Suhail hakuwamini kabisa habari ile mpya na ya kusisimua, alipoliangalia vizuri lilikuwa ni gazeti la HAKI linalomilikwa na kampuni ileile ya TuwaKadabra Productions, akashusha Pumzi kisha akajisemea kimoyomoyo ‘Msigwa Kazini’ kashukuru Mungu tu kua katika makala ile inayomtaja yeye kwa uovu mwingine hapakuwa na jina la mwandishi wake, zaidi ilisomeka ‘Na Mwandishi wetu’ Alijua kama jina la Msigwa lingewekwa kama lilivyowekwa kule kwenye gazeti la Mdadisi bila shaka Mzee Kusekwa angemkumbuka Msigwa kwa kua alipata kumlea miaka kadhaa iliyopita walipokuwa Milambo High School.



    Ikampata tena Suhail kazi ya kuwaeleza wazazi wake habari ile kwa ufasaha, huku akiyanasibisha magazeti yale kua ni zao la kampuni moja ambayo inamtengenezea chuki baada ya uvumi kuzagaa kua nae anataka kuanzisha magazeti yake mapya chini ya kampuni anazosimamia, yalikuwa ni maelezo marefu ambayo kiasi yalimuingia Mzee Kusekwa na mkewe, na kiasi yaligoma, japo Sharifa alielewa kila kitu kua ‘Msigwa yu kazini’



    Mzee Kusekwa hatimaye alikubali tu ki-shingo upande, akatoa tena nasaha zake kwa vijana wake hao, kisha akatoka na kwenda zake mjini huku akiwa ameshaambiwa kua kesho yake, siku ya jumapili Suhail na Sharifa wangerejea Dar, Hamu yote ya kwenda kuwatembelea jamaa ilimwisha Suhail, akabaki ndani tu kama anayetawa.



    Magazeti mawili yameshamchafua,

    nae anazidi kuvunja makubaliano na Shekhia,

    *****



    Masaa matatu yaliwatosha kuwasili jijini Dar Es Salaam wakitokea mkoani Tabora kwa usafiri wa Ndege huku Sharifa akishindwa kabisa kuizuia furaha yake, aliamini kua sasa amezikata ngebe za Suhail hakujua kama mwenzie yuko katika lindi la matatizo. Baada ya kuwasili nyumbani kwao Ilala iliwabidi kupumzika kidogo japo hawakua wamechoka na lolote ndani ya masaa kadhaa waliokuwa hewani, ila tu mazoea hujenga tabia.



    Kuna msemo wa Wahenga usemao;

    ‘Akumulikae mchana usiku atakuunguza ’ Naam sasa kama mtu mchana kweupe ambako kuna mwanga yeye anakumulika unadhani usiku kwenye giza atakufanya nini? Atakuunguza tu.



    Sasa nini cha kufanya!.. Wahenga hawakutuacha hivihivi, ndipo wakatupa suluhu kwa kutuasa kua ‘Akunyweshae kijiko cha mkojo, ukimpatia nafasi Mnyweshe pipa zima’.

    Sasa Msigwa anammulika Suhail mchana kweupe je ikifika usiku atamfanyaje? Suhail akashituka kwakua ameshanyweshwa kijiko cha Mkojo hivyo nae anaisaka nafasi ya kumnywesha adui yake huyo Pipa zima,

    Hapakuwa na kitu kingine ndani ya akili yake zaidi ya kumuangamiza Msigwa tena kwa mkono wake mwenyewe maana pamoja na ukwasi wake hakuwa akijuana na kikundi chochote cha maharamia ambao wanaweza kumfanyia kazi ile.



    Ambacho Suhail hakukitambua mapema ni kwamba wakati yeye anapanga mkakati wake huo Msigwa nae alikuwa akipanga yake, bila shaka na Mungu nae alikuwa anapanga yake.



    Suhail akamuaga mkewe kua anakwenda mara moja kazini kwake, japo kichwani alipanga kuelekea moja kwa moja Ilala Sharifu Shamba ilipo Ofisi ya TuwaKadabra ili pamoja na mambo mengine akapige mkwara mzito wa kulifikisha gazeti hilo mahakami kwa kumchafua na kumsababishia ghasia na hasara pia katika Shughuli zake kufuatia habari ile. Akatoka na kuivagaa barabara!

    ****



    “Haujambo mrembo?,” alisalimia Suhail akiwa amelaza viwiko vya mikono yake katika meza moja nzuri na ndefu iliyopo ndani ya Jengo kubwa na la kisasa, Mali ya Kampuni ya TuwaKadabra. Alikuwa akimsabahi mrembo mmoja aitwae Lilian Ufoo kama ambavyo kibao maalum kilichokua pale juu ya meza ile kilivyomnadi jina pamoja na kazi yake kua ni Secretary wa Mr Rasheed Kassa ambaye mbali ya kua Mkurugenzi wa kampuni ile pia ni Mwandishi mashuhuri wa vitabu vya Riwaya na vya masuala ya Utawala

    “..Naweza kukusaidia kitu tafadhali”



    “Ndio Lilly..nahitaji kuonana na Mr Kassa”



    “Ooh alisema atakua na kikao cha muhimu sijui kama ataruhusu, ngoja nimuulize kama bado hajaanza kikao, nimwambie nani anamuhitaji?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mwambie naitwa Sungura?,” alidanganya Suhail ili apate nafasi ya kuingia ndani kwa haraka maana alijua endapo atajulikana kua ni yeye(Suhail) huenda angecheleweshwa kama si kukwamishwa kabisa kuonana na na Mkurugenzi kutokana na habari ambayo tayari imesharuka magazetini na kuzua utata kila kona,



    “Sungura nd’o Kiswahili cha Suhail?,” Alisaili dada yule na kumfanya Suhail apatwe na hamaniko kidogo katika Sura yake, ambacho alitaka kukisahau ni kwamba utajiri wake wa ghafla ulizidi kumpa umaarufu, ukijumlisha na hizo skendo za magazetini nd’o kabisa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog