Search This Blog

VITA VYA MAPENZI - 4

 







    Simulizi : Vita Vya Mapenzi

    Sehemu Ya Nne (4)



    Akajikaza na kubadilisha mada kama kinyonga

    “Sungura, nd’o jina tunalolitumia mimi na yeye kutambuana, just tell him Sungura namuhitaji” Dada yule hakujibu kitu zaidi ya kuinua mkonga wa simu na kumpigia Boss wake, ilichukua dakika kadhaa za majibizano kabla ya dada yule kurejesha mkongo wake mahala pake

    “Haya ingia kaka, katiza hapo kulia kisha nenda moja kwa moja chumba cha pili kutoka mwisho, mkono wako wa kulia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ubarikiwe,” Alijibu Suahil na kupotelea kule alipoelekezwa,



    Alipofika katika mlango alioelekezwa akagonga na kuingia kabla hajajibiwa

    *****

    Vijana wawili ndani ya gari aina ya Mark II, Mmoja aliebandika miwani myeusi ya jua akiwa nyuma ya usukani huku mwingine mwenye Meno ya rangi ya dhahabu bila shaka yaliharibika kutokana na maji akiwa pembeni, wote waliendelea kubaki ndani ya gari yao karibu ya Mti mmoja mrefu nje kidogo ya Jengo la TuwaKadra kwa muda mrefu sana,



    Hawakua wakiongea chochote zaidi ya kuangalia saa zao mara kwa mara huku yule Abiria mwenye umbile lililojazia kimazoezi na meno yake ya rangi ya dhahabu akiendelea kutoa report kupitia simu yake ya kiganjani.



    ‘Meno ya dhahabu’ alionekana mwenye Usongo wa kutekeleza jambo Fulani ambalo bila shaka alikuwa akisubiri maelekezo kutoka katika simu yake. Usingeweza kulibashiri jambo alilokua akilisubiri pale kwa harakaharaka maana ilikuwa ni kama fumbo. Suhail alipoingia ndani ya ofisi ile kijana yule yeye alikuwa akiwasiliana na simu yake tu huku akiiweka sawa silaha yake, Aliendelea kupokea maelekezo kutoka upande wa pili wa simu yake

    *****



    “Karibu bwana Kusekwa” Alikaribisha Mkurugenzi mwenyewe aliyekuwa ametuna katika kiti chake kilichokaa katikatika ya meza yake kubwa huku kushoto kwake akiwa ameketi mtu mwingine na kulia pia wote wakiwa wameegesha vikwiko vyao juu ya meza hiyo. Suhail akaenda moja kwa moja na kuketi kwenye kiti kimoja ambacho hakikua na mtu



    “Sina muda mrefu wa kupoteza hapa, ila nimekuja kukupasha habari kwamb..” Suhail alikuwa akiongea kwa jazba lakini kabla hajafika mbali akakatishwa na Mkurugenzi Mr Kassa ambaye mbali ya utaalamu wake katika masuala ya kiutawala lakini pia hekma zilizotamalaki ndani Bongo lake zilifanya kazi mara kumi mbele, alijua kua Suhail ana jazba juu ya kilichoandikwa na magazeti yake hivyo alihitaji kutulizwa kwa nidhamu ya hali ya juu

    “Mr Kusekwa, tafadhali mdogo wangu najua uko katika wakati mgumu kufuatia kadhia hii iliyokumba, ni kitu kibaya sana ambacho hata mimi nisingependa kinitokee lakini nakuhisi hebu punguza kwanza jazba ili tuongee kwa kina”

    “Nipunguze jazba ili tuongee kwa kina wakati ninyi mmeshakunja mamilioni ya noti na kuzisweka mifukoni mwenu kufuatia habari za kizandiki mlizonichafua, mnajua ni kwa kiasi gani mmenisababishia usumbufu kwa familia yangu, jamaa zangu na jamii kwa ujumla? Mnajua mmenipoteza wateja wangapi katika biashara zangu kutokana na kunichafua huko? Mnaweza kulipa fidia zangu ninyi? Au mnataka tu kuniharibiaibada zangu zote nilizowahi kuzifanya maana ninaweza kuwapoteza nyote kwa mkupuo kuanzia alieandika, aliehariri, aliechapa, na mwenye gazeti mwenyewe..au hichi kijikampuni uchwara kinawazuzua eeh? Mna pesa ya kuchuana na mimi hata kwa wiki moja tu? Mnaweza kusiama na mimi mahakami ninyi?”

    “Noo Mr Kusekwa, Cool down please, hatuhitaji kufika huko, punguza ghadhabu kwanza na unisikilize, utuonapo humu ndani tulikuwa na kikao kikubwa sana kilichosababishwa na habari ile, Msigwa amekua akitusababishia hasara kubwa katika kampuni hii kwa kuandika madudu yake yasiyo na tija wala ushahidi, mara kadhaa tumepelekwa mahakamani na kuambulia kulipa mamilioni ya shilingi, mara kadhaa tumeletewa barua za kukemewa na Serekali, hata yeye mwenyewe mara nyingi tu amekoswakoswa kuuawa kwa ajili ya ujinga wake huo sasa kwa hili tumeona imetosha sasa, nadhani maamuzi tutakayoyafanya dhidi yake punde tu kutoka sasa maana tuko tunamsubiri yeye tu hapa hata wewe utaamini kua hatukupendezwa na mambo haya” Mr Kassa alikuwa akiongea kwa upole na unyenyekevu mkubwa, alijua kabisa kua Suhail au Mr Kusekwa kama ambavyo anapenda kumuita kwa jina lake la mwisho ku ni kajana mdogo mwenye utajiri mkubwa, anaweza kutokana na ujana wake kuamua kufanya baya lolote dhidi yake na kampuni yake

    “Mr Kassa we ni mtu mzima na ninakuheshimu sana kupitia uelewa wako naona uona kupitia kwenye maandiko yako mengi sana, hivyo usinifanye nikakushusha chini kabisa. Huyo Msigwa hata awe ameandika uovu ninyi si mna wahariri katika magazeti yenu? Sasa ilikuwaje nao wakaidhinisha jambo lile?”

    “Suhail mdogo wangu, kuna mengi yamejificha hapa ila nakuahidi utayafurahia matokea ya maamuzi yangu, Mhariri aliehusika nae naugulia huko na maamuzi niliyoyapitisha juu yake, cha msingi nakuomba tu sifanye jambo, makosa ni yangu mimi mwenye kampuni, najua huu si muda muafa wa kukuomba radhi lakini mimi nitakutafuta kabla ya magazeti yangu kuomba radhi hadharani, nakuomba sana” Suhail alimuangalia Mtu mzima yule akiongea kiungwana kupita kiasi mpaka nae akalegea kidogo japo hakutaka kuonekana kama amelegeza uzi, akainuka na kuondoka kwa kasi bila ya kuaga.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nje ya jengo hilo la TuwaKadabra Suhail aliingia ndani ya gari yake kwa ajili ya kuondoka ndipo macho yake yakaiona gari ya Msigwa ikiiwasili eneo lile. Hakutaka kufanya haraka kuondoka, akatulia kidogo mpaka gari ilipofika usawa wa gari kisha akona kioo cha Pembeni kikifunguliwa taratibu huku ile gari nayo ikiendlea kujongea taratibu vilevile, baada ya kioo kifunguka akamuona Msigwa aliyekuwa akiendesha gari ile akitoa mkono wake nje ya Kioo kile, kisha akamuoneshea kidole chake cha kati ikiwa ni isahara mbaya ya Tusi, baada ya hapo mkono ukarejeshwa ndani na kioo kikafungwa.



    Hasira zilichemka vilivyo ndani ya kichwa cha Suhail, akatoa haraka Pistol yake ili amalize mzozo tu, akaikoki huku jasho likimfumka mwilini.. Wakati tukio lile linatokea katika uga wa kampuni ya TuwaKadabra wale vijana ndani ya Gari walikuwa wakijitahidi sana kufuatilia kila kinachoendelea huku ‘Meno ya Dhahabu’ akiendelea kupokea maelekezo kutoka kwenye simu yake, Kupitia katika darubini yake maalum Meno ya dhahabu alikuwa akimuangalia vizuri sana Suhail akiwa ndani ya gari yake, kisha akawa anajaribu kumuangalia Msigwa tena bila mafanikio.



    Suhail akufanya lolote baada ya kujitafakari kwa kina, akaikumbuka kauli ya Mzee Atrash kua ‘Vita vya Mapenzi’ vitaibuka. Akashusha pumzi halafu akajisemea kimoyomoyo ‘Siku zako zinahesabika Msigwa’ akairejesha silaha yake kiunoni kisha akawasha gari yake na kuacha vumbi katika eneo lile, Wakati Msigwa anaingia Ofisini huku nako Macho ya dhahabu na Dereva wake wakawasha gari na kutokomea zao

    *****



    Baada ya Msigwa kuingia ndani ya Ofisi ya Mkurugenzi hakuhitaji miwani ya lenzi kuona jinsi Boss wake huyo alivyofura kwa hasira ukizingatia ni mara kadhaa sasa amekua akikatazwa kuleta habari zenye utata na ushahidi wa kuungaunga, hapakuwa na maelezo mengi alipoketi zaidi ya kauli chache za mkurugenzi kabla ya kukabidhiwa barua yake ua kuachishwa kazi

    “Mara zote ulizotuletea matatizo kwa habari zako za ajabuajabu tulikusamaehe, tumelipishwa faini mara nyingi kwa ajili yako, barua za Kuonywa tumeshapewa mara mbili na laity kama Suhail atatupeleka mahakamani kwa awamu hii ni lazima tutafungiwa na gazeti lenyewe, umekua mzigo kanjaja, wewe ni mfano wa Waandishi makanjanja, Barua yako hiyo hapo juu kuanzia leo wewe si mfanyakazi wetu tena, kama kuna stahiki zako zozote basi zimeelezwa katika Barua hiyo kwa nukuu ya ndani ya mkataba wako.” Alihitimisha Mkurugenzi na kumuacha Msigwa akiwa haamini kinachotokea, siku zote alidhani yeye ni muhimu sana kwa habari anazoandika lakini hatimaye siku hiyo alifikia kikomo, alilia na kusaga meno akiomba radhi kwa Boss wake lakini haikuwezekana tena. Kichwani mwake aliumizwa zaidi kila alipofikiria mkataba alioingia na Black Scopion ambao lazima autekeleze akiwa ni Mwandishi wa gazeti lile,



    Hakika alihamanika.



    Akavuta picha kichwani akaamini kua Suhail ndie amemchomea utambi mpaka kafukuzwa akamgeukia Bwana mmoja aliyekuwa ameketi pembeni yake, Ni Mr Karim Bucha, Mhariri wa gazeti la HAKI aliyekuwa safarini kwa dharura ndipo Msigwa na Mhariri wa gazeti la Mdadisi(Mr Mbelwa) wakatumia fursa hiyo kuandika na kuihariri wao wenyewe na hatimaye kuiingiza kiwandani kuichapa, Hasira zikazidi kumchemka Msigwa.. Macho ya Mr Buchan a Msigwa yalidhihirisha kua wana lao jingine mbali ya kadhia ile inayoendelea,



    Nini tatizo lao?



    Ni Lilian Ufoo ‘Secretary’.



    Akachukua Bahasha yake ya kaki iliyobeba barua yake iliyomtoa machozi na kutoka nayo nje ya Ofisi ile akiwa si mwandishi tena katika magazeti yanayomilikiwa na Kampuni ile



    Suhail alikwishawasili Ofisini kwake, safari hii akiwa na vijana wake wa kazi ambao licha ya kua marafiki zake aliotoka nao shuleni pia amewaajiri kama Mameneja katika kampuni zake mbili tofauti, Ni Kilingo Mkude na Frank G Mkali, alikuwa akiwasimulia habari zilivyokua mpaka yeye kuandikwa vibaya na Msigwa, alitoa Stori za uongo na kweli ili kujisafisha, akawaelezea mpaka alivyovamia ofisi za TuwaKadabra na kuwatetemesha vilivyo, akiwa katikati ya Mazungumzo akakatishwa na mwito wa Meseji katika simu yake, alipoangalia jina ilikuwa ni Msigwa



    ‘Umefanikiwa kunifukuzisha kazi, ila haujafanikiwa kudhalilika kabla ya kifo chako.. Mimi ni mwandishi alwatan nitatumia hata magazeti ya jamaa zangu kumalizia Skendo yako ya mwisho kua ‘Jogoo hapandi mtungi’ kisha nitakupa salamu kwa marehemu Babu yangu ili akupokee kwa salama huko kuzimu uniache nile zangu raha na Mwanamwali Shar..’ Hivyo ndivyo ujumbe kutoka kwa Msigwa kwenda kwa Suhail ulivyosomeka.



    ‘Anastahiki kifo huyu Shetani,’ Alijisemea peke yake Suhail huku akifuta jasho,



    “Guys, kaendeleeni na kazi tutaongea baadae,” Suhail aliwaambia jamaa zake waliokuwa mbele yake, nao bila ajizi wakajitokea zao, Suhail alikuwa katika majuto ya hali ya juu, kila alipogusa paliteleza, hakika Msigwa alimchachafya, alitamani hata tu atumie ‘Khatam Budha’ kumteketeza lakini alihofia kua Mzee Sufian angeweza kupata ‘Report’ ya tukio lile hivyo angejikuta yeye mwenyewe anayaweka hadharani majanga yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Baada ya Tafakuri ya kina alijiridhisha kua Msigwa anataka Mtoto kwa hali yoyote kwakua hana kizazi(Kama ni kweli Maneno ya Specyoza), Pia kwa sasa hana tena ajira hivyo anahatahata kama kichaa. Njia pekee ni kumtafuta na kufanya nae makubaliano ikiwezekana ampe fungu la pesa aweze kufunga kinywa chake, ama kama atakataa basi atakua ameweka signature katika mkataba wa kifo chake..Kazi ya kumtafuta Msigwa ikaanza harakaharaka kabla hajaitoa skendo ya mwisho. Hakupokea simu, hakujulikana anapatikana wapi, wala anashinda wapi..



    Siku kadhaa zikapita huku maisha yakiendelea, ilikuwa ni wakati wa Suhail sasa kwenda kulala kwa Shekhia baada ya siku nyingi za kua kwa Sharifa, lakini kila alipofikiria jinsi alivyoondoka bila ya kuaga siku alipopigiwa simu kua Sharifa amekwenda Tabora pia ukijumlisha na tukio lake la ‘Kuzabinayoo’ na Sharifa Loohsalale hakutamani hata kuonana na mkewe huyo mwenye asili ya kijini. Japo alikumbuka kua alimwacha mkewe huyo akiwa Mgonjwa kule Bagamoyo lakini alijua akifika tu vita itaanza upya nap engine itamgharimu sana, akaamua kuongeza muda wa kulala kwa Sharifa



    Akiwa nyumbani kwake siku moja Suhail alipokea simu kutoka kwa Msigwa, ilikuwa ni nafasi pekee aliyokuwa akiitafuta kwa hamu japo alijua atakumbana na matusi mazito kutoka kwa kijana Yule aliyetokwa na utu lakini akajiakaza na kumuwahi kabla hajatukana

    “Hallow”



    “Suhail nisikilize kwa makini sana..”



    “No, Msigwa kwanini lakini kila siku mimi na wewe tunaongeza uadui? Hebu..”



    “Uadui umeutaka wewe sasa Iko hivi..”



    “Hapana Msigwa, hebu nisikilize ndugu yangu yatupasa tuyazungumze haya na tuyamalize kiume bila ya kuumizana”



    “Kiume huku umeshanifukuzisha kazi? Nd’o kiume gani hiyo?”



    “Ondoa shaka kuhusu kazi cha msingi ni maridhiano yetu tu, kama shida yako ni pesa nitakulipa na kama shida ni kazi mimi ninaweza hata kufungua Magazeti yangu nikakuachia wewe ukawa ndie msimamizi wangu, ya nini kugombana kwa kiwango hiki tulichofikia? Kumbuka Milambo Sec tulikokua kama mapacha Msigwa” Ikawa ni kukatana tu maneno, hakuna aliefikisha mpaka mwisho sentensi yake, Suhail alitumia lugha laini mpaka akafanikiwa kuziteka hisia za Msigwa ambaye baada ya kusikia habari za pesa akalainika.



    Wakaanza kuongea kwa kusikilizana sasa na hatimaye wakakubaliana kua wakutane kesho yake wafanye mazungumzo ya ki-utu uzima,



    Wapi?



    BreakPoint-Kijitonyama, Mkabala na Crdb Bank

    *****



    Siku ya Miadi ikawadia na muda ukatimia. Wakati Msigwa akitokea Magomeni Suhail yeye alikuwa akitokea ilala huku kila mmoja akiwa nyuma ya usukani wa gari yake akielekea eneo la miadi. Suhail aliyekuwa wa pili kuwasili pale Break Point akifuatiwa na Msigwa, wakati wakwanza wao alikuwa ni ‘Meno ya dhahabu’ aliendelea kuwasiliana na simu yake kila nukta inayotokea huku akijiweka tayaritayari kwa lolote. Hakuna aliemuona ‘Meno ya dhahabu tangu alipowasili eneo lile nusu saa kabla ya mahasimu wale kuwasili eneo lile.



    Wakati vidume hao wanaochuana wakiwa wanawasili huko upande mwingine Shekhia Binti Sufian alikuwa anakaribia kuingia jijini Dar Es salaam akitokea Bagamoyo huku dhamira ndani ya kichwa chake kwenda kumuangamiza Sharifa, hakuwa na chembe ya huruma moyoni, aliumizwa sana na kila kitendo kilichofanywa na Suhail na Sharifa

    *****



    Wakati Msigwa anashuka katika Gari yake pale sehemu ya nje ya kuegeshea magari akakutana hapohapo na Suhail aliyekuwa anaongea na simu muda mrefu, baada ya kuonana wakasogeleana ili wasabahiane kabla hawajaingia ndani kutafuta nafasi tulivu kwa mazungumzo yao, Hapo sasa lilitokea tukio lililowashangaza wengi mpaka wao wenyewe..



    Ilikuwa ni kitendo kidogo tu cha yule ‘Meno ya Dhahabu’ kutoa kauli yake katika simu iliyokua hewani muda wote, aliposema tu ‘NOW’ palepale zilimiminika risasi kama Mvua eneo lile walipokuwa wakipeana mikono Suhail na Msigwa zikitokea upande wa pili wa barabara, ilikuwa ni kizaaza, watu walitaharuki na kusambaa hovyo, Risasi zilikuwa zimesambaza gari moja iliyokua ikioshwa pembezoni mwa Suhail na Msigwa, vioo vilisikika vikisalimu amri.. Kitendo cha Suhail na Msigwa kuachiana mikono na kulala chini kufuatia hali ile ya hatari nd’o ikawa ponepone yao kwani hakuna Risasi hata moja iliyowapata, kila mmoja akashika njia yake

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akiwa anaushuhudia mchezo wote kupitia katika vioo vyake vya giza vya gari yake ‘Meno ya dhahabu’ alikuwa akimlalalamikia mtu kupitia simu yake huku akimtolea matusi ya nguoni, bila shaka alikuwa akiongea na mpigaji wa Risasi zile. Ndani ya sekunde chache gari ya Meno ya dhahabu iliondoka eneo lile wakifuatiwa na magari kadhaa ya wateja waliokuwa katika Bar ile, wakiwemo Suhail na Msigwa kila mmoja na gari yake huku akishika njia yake.



    Haikujulikana mlengwa alikuwa nani!



    Wakati Suhail anawasili ofisini kwake huku akiamini kua amenusurika kuuawa na watu waliokuwa wametegwa na Msigwa, huko upande mwingine nako Msigwa alikuwa ameshawasili katika kituo cha Polisi akitoa maelezo kua amekoswakoswa kuuawa kwa kupigwa risasi na watu anaodhani wametumwa na Suhail.



    Uadui ukachipua tena kama uyoga wa ‘Kanswerere’,



    Ilipotimu mchana wa siku hiyohiyo Suhail akapokea wito maalum kutoka katika kituo cha Polisi chaKijitonyama kua anahitajika kwenda kutoa maelezo ya tuhuma za kuandaa mpango wa tukio lile la Risasi linalohisiwa kua ilikuwa ni mpango wa kumuua rafiki yake, Msigwa. Hakika alichanganyikiwa kijana wa watu, alikuwa ni kama alielaaniwa na wazazi maana kila uchwao matukio yanajipanga tu, Sasa kufuatia tukio hilo la msigwa kumuwahi Polisi ndio akaamini kua Msigwa ndie aliechezesha mchezo ule hatari. akakubali kua angewasili Kituoni nusu baadaye ili nae ajipange kwa lolote litakalotokea huko..



    Maajabu ya pili ni pale alipoamua kuziperuzi meseji alizokuwa akitumiwa na Msigwa ili iwe kama ushahidi kwamba Msigwa ndie aliyekuwa akimtishia kumuua hakuziona kamwe, alitafuta karibu robo saa nzima hapakuwa na meseji yoyote kutoka kwa Msigwa ndani ya Simu yake..hakujua zimeyayushwa na nini hasa,



    Akainuka akiwa mpole kabisa, Safari ya kituoni ikaanza bila ya ushahidi wa kujitetea itakapolazimu kufanya hivyo

    *****



    Ndani ya chumba kidogo cha kipelezi kilichopo ndani ya Jengo la Polisi Kijitonyama, walikuwa wameketi watu watatu, Suhail na Msigwa pamoja na mpelelezi wa kesi yao Inspekta Leonard Kenjah. Ilikuwa ni mtanange wa nguvu katika kutoa maelezo kila mmoja alipopata nafasi ya kujieleza alimtuhumu mwenzie kwa tukio lile japo hakuna aliesema waziwazi kiini cha kuhisiana vile, walijitahidi kuficha uhalisia wa mgogoro wao lakini kwa Weledi ya Inspekta Kenjah alianza kupata picha kua watu wale walikuwa wana uhasama mkubwa sana. Wakati mjadala ule ukiendelea Simu ya Suhail alikuwa ikiita mara kwa mara, hakuweza kupokea kutoka na mvutano mkali katika majadiliano



    ”Iko hivi ndugu zangu, sote ni watu wazima hapa tusifanyane watoto. Kaeni mkijua tukio lile si dogo kama mnavyodhani, naweza kuwashikilia nyote mkasota rumande mpaka upelelezi utakapokamilika endapo mtaendelea kuzua malumbano yasiyo na tija humu ndani..” Wakati Ispekta Kenja akiendelea kuongea, Simu ya Suhail ikawa kero kwa jinsi inavyoita mara kwa mara

    “Hebu pokea uwaambie wakuache kwanza mtaongea baadae, au ikiwezekana uizime kabisa,” Aliagiza Inspekta Kenjah



    Alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Kilingo Mkude, Meneja wake

    ”Hallow”



    ”Kaka uko wapi?,” Kilingo aliuliza kwa sauti ya taharuki na hamaniko



    ”Nina dharura kidogo Mkude, unaweza kunipigia baadae tafadhali?!”



    ”No Suhail, Shemeji hali yake ni mbaya sana”



    ”Nani?”



    ”Sharifa”



    ”Sharifa m-ke wa-ngu?, amepatwa na nini? Na umepata wapi hizi habari?,” Aliuliza Suhail kwa sauti iliyoingiwa na kigugumizi



    ”Sharifa amepatwa na Kiharusi, amepooza upande mzima wa kulia, wanasema wanakupigia simu haupokei ndipo wakabahatisha kunipigia mimi wakanipata, hapa nipo kwako tunatafuta usafiri wa kwenda Hospital”



    ”Oooh my God, ‘Shekhia kazini’,” Alibwabwaja maneno Suhail mbele ya Inspekta Kenjah na Msigwa, Simu ikamdondoka na kuanguka chini bila ya kujijua

    ”Kuna nini tena Mr Kusekwa?,” Alisaili kwa wahka Inspekta Kenjah

    ”Mke wangu amepatwa na ‘Stroke’, yuko mahututi”

    ”Whaat?!” Msigwa nae akashituka kwa nguvu kama vile asieamini anachoambiwa, lakini mshituko wake huo ulizimwa na jicho kali alilotupiwa na Suhail,

    “Ooh very sorry, unaweza kuondoka kwa sasa then tutakapokuhitaji utarejea, Oky?” Inspekta Kenjah alitoa ruhusa ile kisha Suhail aliinuka baada ya kupewa ruhusa ile akaanza kuondoka bila hata ya kuaga, huku nyuma yake akifuatiwa na na Inspekta na Msigwa mwenyewe,

    wakatoka wote mpaka nje kabisa ambapo Suhail aliingia ndani ya gari yake na kuondoka kwa kasi akiwaacha wenzie pale nje wakiwa wamejianika mbele ya ‘Target’ ya ‘Meno ya dhabu’ aliyekuwa umbali wa kilometa chache kutoka upande wa pili wa Barabara



    Hakufika hata umbali mrefu akasikia Risasi zikirindima kule usawa wa kituo cha Polisi, Kwa jinsi alivyokua ameshitushwa na habari za kuuguliwa ghafla na mkewe wala hakujishughulisha na Risasi zile, alichukulia tu kama kasikia sauti ya pancha kwenye tairi la baiskeli.



    Japo siku hiyo kulikuwa na foleni za mara kwa mara lakini hatimaye akawasili nyumbani kwake ambapo alipokelewa na majirani tu, Si mkewe wala rafiki yake bwana Kilingo aliowakuta, akaingia kwa kasi ndani ili apate kuonana na dada mmoja aliempangisha sehemu ya uwani ya nyumba yake, nae hakuwepo

    ”Wamekwenda hospitali,” Aliongea mtoto Fulani aliyekuwa akichezacheza pale nyumbani, Suhail akamuangalia na kumpuuza. Akatoa simu yake na kumpigia Kilingo, Simu ikaita bila kupokelea, akapiga tena.. safari hii ikapokelewa na sauti ya kike

    ”Hallow”

    ”Mpe mwenye simu tadhali”

    ”Yuko anaongea na Dokta, mimi ni Zulfa”



    Zulfa ni mpangaji wake na Suhail, alichomaanisha ni kwamba Kilingo asingeweza kuongea na simu kwa muda ule ndio mana amempokelea

    ”Mko Hospitali gani?”

    ”TMJ” akakata simu na kuingia harakaharaka kwenye gari na kuianza safari mpya ya kuelekea Hospitali

    *****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Katika viti maalum walikuwa wameketi watu kadhaa kila mmoja akiwa na lake lililomsibu yeye au nduguye hapo Hospitalini, Suhail alikwishawasili lakini hakupata fursa ya kuonana na Mkewe, akawa anapewa hali ilivyokua na Zulfa aliekuwepo nyumbani wakati Sharifa anaanguka na kupooza, Kilingo alikuwa kwa pembeni akimliwaza rafiki yake na Boss wake.



    Suhail alichokijua ni kua Shekhia amekwishafanya yake hivyo nae sasa akawa hana jinsi, akaamua tu kutumia Pete yake ya Kijini(Khatam Budha) kumponya mkewe kwanza kisha mengine yatafuata, japo alijua fika endapo ataitumia pete ile atafanikiwa lakini taarifa itakwenda kwa Mzee Sufiani ambaye itamlazimu kufuatilia kila kitu, na hapo sasa huenda akawa nd’o ameyakoroga mambo, Hakujali!



    Akiwa anaendelea kumsubiri Dokta awaruhusu kuingia ghafla wakapata ugeni wa watu watatu

    Inspekta Kenjah akiwa katika mavazi yake nadhifu ya kiraia, na askari wengine wawili wakiwa wamevalia sare zao zilizoyakamata maungo yao kutokana na mazoezi wayafanyayo

    “Mr Kusekwa, Pole kwa usumbufu tunakuhitaji kituo cha Polisi sasa hivi,” Aliongea Inspekta huku akitweta

    “Aah Afande, si tulikuwa sote huko ukaniruhusu kutokana na hali ya mke wangu?”

    “Yeah sure, ila kuna dharura kubwa zaidi”

    “Naweza kuja hata baade lakini, hata mara ile niliyokuja sikuijiwa hivi” Mazungumzo yalikuwa ya kutatanisha sana mpaka wagonjwa na wauguzi wengine wakaingiwa hofu,



    “Samahani kwa kuwaingilia, kama kuna jambo zito nadhani Inspekta ungeliacha wazi ili atambue kabla hajaondoka,” alidakia Kilingo

    “We unaongea kama nani Bwa’mdogo,” Ispekta Kenjah alimaka

    “Tafadhali usiniite bwa’mdogo, naomba uinawirishe heshima yako.. we unanijua mimi? Au huu wembamba wangu unakudanganya? Kama huyu ni mtuhumiwa anapaswa kujua anachokamatiwa” Malumbano yakachukua muda mrefu sana, kilingo alionekana kujiamini sana,

    “Suhail imekuaje tena?,” Aliuliza dada mmoja aliyekuwa amewasili muda mfupi nae akiwa ameleta mgonjwa wake hospitalini hapo, Macho ya Suhail yalipogongana nay a dada Yule hamaniko likadhihiri waziwazi usoni mwake, alikuwa ni Nancy Kileo, Msichana ambaye mbali ya kua rafiki yake wa tangu chuoni pia ni Shemeji yake kwa Shekhia. Suhail hakujibu kitu akameza fundo la mate kisha akaanza kuondoka na askari wale waliokuja kumkamata kwa kosa ambalo hakuwa akilijua



    “Eti kaka imekuaje?,” Kileo alimuuliza Kilingo aliyekuwa amesimama kwa hasira akimuangalia Suhail anavyoondoka



    “Aah, hawa askari njaa zao zitawamaliza, mtu ana matatizo halafu mnamng’ang’ania utadhani ameua bana”



    “Mnh, haya makubwa sasa ngoja nimpigie simu mkewe,” alijibu dada Yule



    “Mkewe nd’o huyo aliemleta hapa, amelazwa huko ndani”



    “Khaa, Shekhia amelazwa?”



    “Shekhia?Nd’o nani huyo?”



    “Si nd’o mkewe jamani?”



    “Mke wake anaitwa Sharifa, au dada utakua umemfananisha nini?”



    “No siwezi kumfananisha Suhail mimi, nimesoma nao wote yeye na mkewe hapo Udsm,”



    Maneno yale yaliwaacha midomo wazi Kilongo na Zulfa ambao wao humfahamu Sharifa tu, sasa wakati hayo yakiendelea bahati mbaya ama nzuri Nancy akaitwa na nduguze kule kwa Dokta walikomuingiza mgonjwa wake hivyo ikabidi aondoke bila ya kupata ufumbuzi

    *****



    Mpaka wanawasili kituoni Suhail hakuwa ameelewa chochote zaidi ya kumuona Inspekta Kenjah akiwa amebadilika sana tofauti na awali

    “Kuna nini Afande, just tell me,” Aliuliza Suhail wakiwa wanaanza kuteremka kwenye gari iliyowatoa kule TMJ na kuwafikisha pale Kituoni,

    “Msigwa amepigwa Risasi muda mfupi baada yaw ewe kuondoka”

    “Whaat?!, Ooh my God,” Suhail alilalama kwa nguvu lakini hakuna aliemjali mpaka walipofika nyuma ya Kaunta,



    “Umeshapata habari?,” Aliuliza afande mmoja aliyekuwa amesimama pale karibu ya meza ya mapokezi huku akimtazama usoni Inspekta Kenjah,

    “Habari gani Afande?”

    “Mtu wako aliepigwa Risasi..”

    “No, amefanyaje?” alisaili Inspekta kwa wahka

    “Amefariki dunia hatua chache kabla hajaingizwa katika geti la Muhimbili”



    Nguvu zilimwisha Inspekta Kenjah, akamgeukia Suhail aliyekuwa amelainika vilivyo kufuatia habari ile

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mr Kusekwa, No way out, inabidi uandike maelezo yako kabla haujaingizwa lockup kwa usalama wako na msaada kwetu pia”

    “Lakini Afande mimi nashikiliwa kwa lipi sasa? Wakati tukio linatokea mimi sikuwepo kabisa hapa na umenikuta kweli nilipokutaarifa kua nakwenda.. Sihusiki chochote mimi jamani” Alipomaliza kubwabwaja maneno yake, akaambulia kumwona kwa mbali Inspekta Kenja akiwa natokomea ofisini kwake akiwa ameshatoa maelekezo ya nini cha kufuatwa, alitamani apate japo dakika moja awahi kumponyesha Sharifa kwa nguvu ya Pete yake lakini haikuwezekana kwa muda ule. Aliiona dunia chungu, kila kitu ni kama kimemuelemea sasa.



    ‘Sharifa amepigwa Kiharusi bila shaka na Shekhia, Msigwa kanichafua kwenye vyombo vya habari na hatimaye nae ameuawa bila shaka na watu wasiojulikana. Msala wote kaniachia mimi, Chambilecho cha mzee Atrash Hivi ni vita vya mapenzi’ Alijisemea kimoyomoyo wakati alipokuwa amemaliza kutoa maelezo yake na kuambiwa avue vitu vyote visivyohitajika kuingia navyo ‘Lupango’.



    “We hiyo Pete unaenda nayo wapi?,” Afande wa zamu pale kaunta alimuwahi Suhail alipokuwa akitaka kuingia ndani,

    “Ooh hii haina shida Afande”

    “Usitufundishe kazi bwana mkubwa. Vua hiyo takataka yako iweke pamoja na vitu vyako hapo” Suhail alihisi kuishiwa nguvu, hakupaswa kuiacha ile Pete mbali na kidole chake kwa muda mrefu, nae hakujua atakaa ‘Ndani’ kwa muda gani. Alijaribu kuleta upinzani bila mafanikio, akaivua Pete yake(Khatam Budha) na kuswekwa Ndani.



    Huo ukawa ni Mwanzo wa Sekeseke!

    *****



    Hekaheka za Hospitalini zilisimamiwa na Kilingo Mkude huku vurumai za Polisi zilisimamiwa na Frank Mkali, wote wakiwa ni marafiki na wafanyakazi katika Kampuni za Suhail. Bahati nzuri wakati Suhail alipokuwa Hospitali aliwasiliana na wazazi wao wote huko Tabora hivyo nao walikuwa wakiratibu mpango wa Usafiri kesho yake asubuhi, hakika waliumizwa sana na Taarifa zile.



    Hatimaye siku ikamalizika na Suhail akalalia sakafu ya Polisi akiwa ni mshukiwa wa Mauaji yale.. Hali ya Sharifa ilizidi kua mbaya kadri muda ulivyozidi kusonga mbele, Habari zikazagaa kila kona huku baadhi ya Magazeti na vyombo vingine vya habari vikiripoti kwa mbwembwe habari ile ya Mauaji.

    *****



    Mzee Kusekwa, Mzee Fungameza pamoja na wake zao waliwasili katika Hospitali ya TMJ wakiwa na mwenyeji wao Mr Mkude aliekwenda kuwapokea Airport wakati wanawasili, hawakutaka hata kupitia Nyumbani zaidi ya kwenda moja kwa moja kumuona Mgonjwa, Vihoro vyao viliongezeka maradufu baada Kilingo kuwaeleza habari ile nyingine mbaya kua Suhail nae anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na Mauaji ya Mwandishi mashuhuri wa magazetini Bwana Msigwa.



    Bahati ilikuwa yao walipofika tu Wodini wakaruhusiwa kwenda kumwona Mgonjwa wao aliyekuwa amepooza mwili wake upande wa Kulia, Wazazi wa kike uzalendo ukawashinda wakaanza kulia, huku waume zao wakijikaza kisabuni tu lakini nao Simanzi zilishambulia mioyo yao ndani kwa ndani.

    “Jamani habari zenu,” Alisalimia Nancy Kileo punde baada ya kuwasili katika chumba alicholazwa Sharifa

    “Nzuri kiasi dada, za tangu jana?”

    “Hivyohivyo nasi hatujambo, wakubwa Shikamoni” Wakaitikia wazee wa watu kutoka Tabora

    “Enhee vipi Suhail aliachiliwa jana?”

    “Hapana, mpaka sasa yuko ndani ila kuna watu wanaendelea kufuatilia mpango wa kumwekea dhamana”

    “Na mkewe ameshawasili? Maana tangu jana nampigia simu yake haipatikani”

    “Mnh, Dada Mkewe si ndie huyu hapo kitandani, nadhani tangu jana nilikwishakwambia” Mr Mkude alijibu akiwa ameanza kukasirika kuona dada Yule anang’ang’ania jambo moja tangu jana yake

    “Jamani mbona sielewielewi? Mke wa Suhail Kusekwa nimjuaye mimi ni Shekhia Sufian na wote nimesoma nao Chuo Kikuu, au ana wake wangapi?”



    Swali la Nancy halikupatiwa majibu zaidi ya kuzua hali ya Sintofahamu Wodini pale, Si Kilingo, wala Wazazi alieweza kutegua kitendawili kile. Ikawa sasa ni maswali lukuki kwa Nancy kutoka kwa Mzee Kusekwa, hakuna walichoelewana zaidi ya kuchanganyana tu. Hatimaye waliamua kuyaacha hayo kwanza na kutazama yaliyopo

    *****



    ”..Ngoma ikivuma sana mwishowe hupasuka tu..”

    ”Sasa inahusiana nini na mada yetu?”

    ”Si huyo Msigwa wenu, amevuma sana mpaka akapitiliza, huo ndio ukisikia umaarufu kunuka! Yaani unajizolea umaarufu kwa kutumiwa na watu ambao ukishauawa kama vile wao wataishia tu kusema Bwana alitoa na bwana ametwaa..”

    ”Kweli binaadamu hatuna wema, kila siku tunawalalamikia vigogo na wanasiasa wanaotumia vibaya rasilimali za nchi na wanatuangamiza sisi katika kujipandisha kwa juu Sasa kijana wa watu ameitumia taaluma yake ya habari kutusemea na kutupazia sauti sisi tusio na sauti mpaka imemgharimu maisha yake halafu leo badala tumuenzi kwa hilo tunakalia unafiki tu na uzandiki..”

    ”Hakuna chochote alichokuwa akitusemea zaidi ya kutumiwa na haohao wanasiasa na vigogo kuwachafua wengine, kwani unadhani hatujui kua alikuwa kambi ya Mhe Fulani? Acha afe tu bwana hii nd’o Bongo ukijitia hamnazo unakufa wewe”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ”Hivi asingekua Msigwa kuandika makala zake nani leo hii angejua kuhusu sakata la Waziri wa Nishati na Madini kusaini mikataba mibovu na kandamizi kwa taifa letu ili kuwefurahisha mabwana zake wa ulaya anaotarajia watamuwezesha katika mbio zake za kuuwania urasi?. Nani leo hii angegundua kuhusu matajiri wengi nchini kujihusisha na vitendo viovu katika utajiri wao?”

    ”..Hivi we unaongea nini wewe?Au haufuatilii habari? Hiyo sio ishu tena mjini, yule Waziri alikanusha habari ile na akawashitaki mahakamani wamiliki wa Gazeti la Mdadisi, Msigwa akashindwa kutoa ushahidi wa habari ile kampuni ikatakiwa kumlipa Mhe Waziri fidia na kumtaka radhi hadharani, na walikwishafanya hivyo, we uko Dunia gani?”

    Malumbano ya vijana wawili katika mgahawa wa chakula ulio mkabala na Jengo la ofisi za Tuwa Kadabra Productions kufuatia kuuawa kwa mwandishi wa habari Bw Msigwa yaliziteka hisia za wengi waliokuwa wakijipatia maakuli

    ”Na kwa taarifa yako hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa kampuni yao kushitakiwa na kulipishwa fidia kufuatia habari za kizushi zilizoandikwa na Msigwa, unakumba ile kesi ya yule Muhindi ambaye Msigwa alimuandika kua ni muuza madawa ya kulevya anaetumiwa na Waziri wa Madini kufadhili harakati zake za uchaguzi mkuu? Napo waliburuzwa mahakamani na wakalipa fidia, isingekua mkono wa Mwanasiasa fulanifualani hakyamungu Msigwa angefungwa kipindi kile”



    ”Hata mimi inaniingia kichwani hiyo, kwahiyo inawezekana Msigwa alikuwa akitumiwa na wanasiasa eeh?,” Aliuliza bwana mmoja aliyekuwa akiufuatilia kwa karibu sana mjadala ule huku akijipatia supu ya Ng’ombe, bwana yule alikuwa amevaa kofia ‘kapelo’ iliyotanda sehemu kubwa ya sura yake kiasi cha kufanya asionekana kiurahisi

    ”..yule safari hii kapamia kwa watoto wa mjini, nasikia ile habari aliyomwandika yule kijana anaemiliki Mgodo huko Geita ndio imeleta yote hayo, maana nasikia kabla ya kuuawa alikoswakoswa Risasi maeneo ya Break point pande za K-Nyama.. mwishowe amejaa” alidakia kijana mwingine aliyekuwa amesimama kwa ajili ya kutoka zake ndani ya mgahawa ule baada ya kumalizia chakula chake

    ”Duh kumbe yule bwa’mdogo Suhail ni noma eeh?,” Alisaili yule bwana alievaa kapelo nyekundu, lakini kabla hajajibiwa na mtu aliemkusudia, akasikia sauti ya dada mmoja aliyekuwa ameketi katika kiti muda mrefu, inaonesha ni mhudumu wa mgahawani pale kwa jinsi alivyovaa kikazi zaidi

    ”Kilichomponza Msigwa ni Mapenzi tu hakuna kingine, alijiingiza kwenye vita vya mapenzi na Boss wake”

    ”We nae kauze supu huko huna ulijualo, yule Mzee Kassa mtu mzima hawezi kujiingiza kugombea mwanamke na yule chokoraa”

    ”Kama hautaki sikulazimishi, mimi nd’o nawahudumia chakula kila siku karibu watumishi wote wa kampuni yao hivyo nazisikia fununu zao, na Sio Boss huyo sasa naesemea mimi”

    ”Kumbe Boss gani sasa?”

    ”Nd’o ungetulia ukaelekezwa sasa kuliko kujifanya mjuaji, Msigwa alikuwa akigombea mwanamke na Mhariri wa gazeti lao anaitwa Bucha, na mwanamke mwenye ni yule Sekretari anaitwa Lilly..” majadala ulikuwa mkubwa sana kila mmoja akijifanya kuilewa vema kesi ile bila mafanikio, ikawa sasa ni fujo tu. Bwana mwenye kapelo nyekundu akainuka na kutoka nje ya mgahawa ule hakuona haja ya kuendelea na mjadala ule ulioharibika tayari kwa kuvamiwa na wajuaji. Alipofika nje akaivua kofia yake ili apate kulitazama vema jengo la ofisi aliyokuwa akifanyia kazi Msigwa, akaishika mkononi kofia yake kisha akaliendea jingo lile na kingia mpaka ndani kabisa



    ”Habari yako mrembo?”

    ”Nzuri, karibu”

    ”Ahsante, Naitwa Inspekta Kenjah natokea kituo cha Polisi kijitonyama, nahitaji kuonana na Mista Kassa” baada ya maelezo yale, Lilly akanyanyua mkonga wa simu na kumpigia Boss wake kumuarifu juu ya ujio ule, baada ya muda akaurejesha mkonga ule wa Simu mahala pake, akamruhusu afisa yule wa jeshi la Polisi aingie

    *****



    “Karibu sana Inspekta,” Bwana Rasheed Kassa alimkaribisha Inspekta Kenjah licha ya kua Inspekta alikuwa hajajitambulisha mwenyewe, hilohalikumpa tabu Inspekta

    “Ahsante sana Mr Kassa” Baada ya salamu za hapa na pale Inspekta akaianza kazi iliyompeleka pale

    “Poleni tu na Msiba”

    “M_si_ba.. Ooh kazi ya Mola haina makosa bwana, bado hatujapoa,’ Alijibu Kassa huku akisuasua kama ambaye hakuwa akijua chochote kuhusu msiba ule au kama hakutegemea kupewa pole ile

    “Kazi ya Mungu? Hapana bwana Mungu hafanyi kazi ya kinyama kama ile. Mie nadhani ni kazi ya Shetani alielaaniwa tu iliyotekelezwa na wafuasi wake wa hapa duniani”

    “No ni kazi ya Mungu pia, hakifanyiki chochote hata jani kudondoka kutoka mtini isipokua kwa idhini yake maulana”

    Jibu hilo la lilimfanya Inspekta Kenja ashushe pumzi , akavuta sekunde kadhaa mbele bila ya kusema chochote akiwa anatafuta swali lingine litakalomsaidia kumsoma Bwana mkubwa yule jinsi alivyoupokea msiba ule

    “Sasa mbona nyote mko kazini licha ya msiba huu mzito sana?”

    “Kama ambavyo wewe uko kazini kaka licha kua ulikuwepo wakati wa tukio, lakini yote kwa yote kifo ni ahadi hakuna kigeni hapo, na kwakua maiti bado iko mikononi mwenu wanausalama ndio maana tuko hapa ila ikiwa tayari tutajumuika mazikoni” alijibu Bwana Kassa

    “Ila jamani kwa mfanyakazi wenu mahari kama yule mlipaswa nanyi kuonesha kuguswa na jambo hili”

    “No, Msigwa hakuwa mfanyakazi wetu.. Siku kadhaa zilizopita aliacha kazi rasmi hapa”

    “Mnh jamani si ni majuzi tu hapa aliandika habari kwenye gazeti lenu kuhusu yule kijana tajiritajiri? Anyway tuachane na hayo..aliacha mwenye kwa hiari yake au mlimfukuza?”

    “Ile nd’o ilikuwa habari yake ya mwisho kuandika katika gazeti hili, tulimuachisha kazi siku chache baada ya habari ile”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwanini mlimuachisha kazi?”

    “Aah, hayo ni masuala binafsi ndugu, sidhani kama itakua ni hekma kuyabwaga hapa tena”

    “Unajua siku chache kabla ya ninyi kumfukuza kazi akakoswakoswa kupigwa Risasi, hatimaye akauawa kabisa hauoni kua tuna haja ya kujua kila kitu kuhusiana na ninyi?”

    “Ooh yeah, Ok, hakuna kikubwa sana zaidi ya yeye kutoka nje ya makubaliano yetu yaliyo ndani ya mkataba wake, hakuwa muadilifu na hakuwa makini hivyo habari zake mara kwa mara zikatutia hasara na kutogombanisha na watu..na mara kadhaa tulipokea barua za onyo kuhusu tatizo hilo ambalo kimsingi lilikuwa likitoka kwake kila mara”

    “Ok vizuri, lakini kwanini hamkumfukuza kazi siku zote alipokuwa akifanya makosa hayo makaja kumfukuza kipindi hiki alichomuandika swahiba wako Suhail?,” Inspekta alisaili kimtego

    “Tulikuwa tukimpa barua za Onyo mara zote hizo, lakini mara hii iakawa hatuna jinsi tena zaidi ya kumuachisha kazi tu.. maana hata huyo kijana uliyenizushia kua swahiba wangu alikuja na kutukana sana hapa akiahidi kutuburuza kortini”

    “Unaweza kunipa ‘copy’ za barua hizo zote pamoja na hiyo ya mara ya mwisho ya kumfukuza”

    “Ndio, inawezekana” Mkurugenzi akainuka na kwenda nje ya ofisi ile ambapo baada ya dakika kadhaa akarejea na Barua zake tatu na kumkabidhi Inspekta



    “Naweza kuongea na bwana Karim Bucha tafadhali?,” alisaili Inspekta Kenjah wakati akiendelea kuperuziperuzi barua zile

    “Bila shaka yuko njiani anakuja, niliwasiliana nae akiwa ndio anaondoka Kariakoo ilipo ofiosi yetu Ndogo”

    Wakiwa katika ya mahojiano mara ghafla ukasikika mlio wa Bunduki ukifuatiwa na kelele za watu nje huko usawa wa Geti la Jengo lile, Macho ya Inspekta yakakutana na ya Bwana Kassa halafu bila ya kusemezana chochote wote wakainuka na kuanza kutoka nje kufuatilia kilichojiri kila mmoja akiwa na hofu yako ukizingatia tukio la mauaji ya Bunduki bado liko vichwani mwao. Wakatoka mpaka nje kabisa ambapo walianza kuwaona watu kadhaa wakikimbilia karibu na Geti la kuingilia katika Jengo lile.



    Haraka Inspekta akatoka mpaka pale akakuta mwanaume mmoja Shombeshombe wa kiarabu akiwa amelalia dimbwi la damu, hakutaka kumsogelea akasimama kando kidogo ili ajipe muda wa kuangaza kama ataona dalili za muuaji, lakini akaambulia patupu. Wakati huo Bwana Kassa alikwishafika pale lakini alionekana kushitushwa na tukio lile kuliko kawaida akaivua miwani yake akiwa haamini na kumsogelea bwana yule aliepigwa Risasi

    “Vipi umemjua?,” Inspekta Kenja alimuuliza Kassa lakini Bwana Kassa alimgeukia kwa jicho la mshangao kisha nae akajibu kwa mtindo wa swali

    “Sasa Insp ulikuwa ukimuuliza mtu usiemjua?” Jibu hilo lilimfanya Inspekta Kenjah akagundua kua yule alikuwa ndie Karim Bucha, wakati huo tayari watu walishaanza kujaa eneo lile huku Lilian Ufoo akionekana kutaharuki kwa kilio cha uchungu kila alipojaribu kumuangalia Karim Bucha akiwa anatapatapa pale chini risasi ikiwa imepiga kifuani kwake usawa wa kulia



    ‘Huyu nd’o alikuwa mtu mzuri kwa ushahidi, nae kadunguliwa, hivi nani anaendesha matukio haya na kwa lengo gani hasa?” Alijiuliza mwenyewe Inspekta Kenjah, bila ya kujipa majibu akawaamuru wale watu wasaidizane kumnyanyua Mr Bucha na kumpakia kwenye gari kwa ajili ya kumuwahisha hospital. Zoezi hilo likafanikiwa kwa asilimia mia!



    Baada ya kukamilisha taratubu zote akamuacha Mgonjwa hospitalini akiwa chini ya uangalizi wa Madaktari na wanausalama kadhaa kaianza safari mpya ya kuelekea Ofisini kwake alikokua akimuwahi Kopro Salum Marando aliyekuwa amemuarifu kwa njia ya simu kua amekamilisha uchunguzi wa awali aliomuagiza uafanye maeneo kadhaa

    *****



    Watu wengi walikuwa wamekusanyika katika fukwe za Shoab, au ‘Shoab beach’ kama ilivyozoeleka kutamkwa na wakazi wengi wa kisiwa hicho cha Socotra Nchini Yemen, kusanyiko hilo la watu halikuwa na jipya zaidi ya burudani tu zifanyikazo hapo kila siku ila zaidi siku za mapumziko ya mwisho wa wiki, wapo waliojitokeza kuogelea na kuchezea maji na wenzi wao, wapo waliokuwa wakichezea mchanga mweupe mithili ya maziwa, na wapo walioamua kukaa pembeni wakipata upepo sanjari na kuburudishwa na upepo mwanana huku ndege kadhaa waliojitulizania katika miti pembezoni na fukwe hizo wakiendekea kunung’unika kwa sauti zao.



    Kijana mmoja wa rika la kati aliyekuwa amevaa bukta nyepesi huku akiwa kidali wazi alikuwa akiogelea kwa furaha na msichana Fulani mrembo wa hali ya juu, umbile lake lililoonekana waziwazi kupitia kijiguo chake cha ndani alichobakia nacho wakati anaogelea, hakika lau kama angekua amevaa suruali pengine ungehisi amevicha bastola, hakika msichana Yule aliyazuzua macho ya wanaume wengi hasa wale waroho wa mali za watu. Haikuhitaji msaada wa mpiga ramli kutoka bumbwini ili kuthibitisha wawili wale walikuwa wapenzi, na Kwa jinsi walivyokua wakicheza pamoja usingetilia shaka kua walikuwa wakipendana sana japo hilo halikuwa kweli. Hawakua na mapenzi ya kweli kwanza hata ungepewa historia yao ungecheka, tangu wajuane hawakua hata na siku tatu ambapo siku yao ya kwanza ilikuwa juzi yake walipokutana katikati ya kisiwa hicho katika moja ya hafla ya mfanyabiashara Fulani maarufu wa mafuta, hapo ndipo wakapendana na kuahidiana kua wakutane siku ile katika fukwe za Shoab, japo muda wa kua katika mapenzi si tatizo sana kama mtakua mmependana kwa dhati lakini hawa walikuwa na zaidi ya hilo. Kila mmoja alikuwa na lake la ziada kichwani. Lugha waliyokuwa wakitumia ni kiarabu kama walivyo wao wenyewe ni waarabu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakiwa wanaendelea kuogelea kuna hisia za ajabu zilimkumba mwanadada Yule mrembo mpaka hamu ya kuendelea kuogelea ikamwisha akatamani kuondoka hapohapo lakini mazingira ya kumuacha mpenzi wake yule hayakua mazuri

    “Mpenzi naomba nikapumzike kidogo nahisi kuchoka,” Alijisemesha mrembo yule wa kiwango cha Lundenga

    “Ooh usijali twende tu tukapumzike wote”

    “No, we endelea kuogelea niwe nakuangalia napenda sana jinsi unavyoogelea,” Alijibu huku tabasamu pana likichanua usoni mwake kama Uwaridi, na kijana yule aliejengeka vizuri mwili wake kimazoezi kwa kupenda sifa hajambo, akakubali na kumuacha mpenzi wake akienda pembeni kupumzika wakati yeye akiwa anaendelea kupiga maji.



    Ilikuwa ni kitendo bila ya kuchelewa Mrembo yule akapotea katika mazingira ya kutatanisha, alitoweka katika mazingira ambayo mwanadamu wa kawaida asingeweza kutoweka vile, yeye aliweza kwakua hakuwa mwanadamu wa kawaida. Yule alikuwa ni Komandoo Takadiri Al-harabi alijibadili na kua katika umbile lile la kike ili aweze kuishi vizuri katika kisiwa kile akiendelea na msako wake aliotumwa na kiongozi wa himaya ya Budha kuutekeleza hapa duniani..



    Watu waliendelea kuogelea kwa furaha, hakuna Mwanadamu yoyote aliyeweza kuling’amua tukio lile katika hali ya kawaida lakini Si kwa kijana yule aliyekuwa akicheza nae katika maji, yeye haraka alihisi hali ya tofauti kwani nae hakuwa Mwanaadamu wa kawaida, Yule alikuwa Mzee Sufiani Bin Shamhurish aliyekuwa katika umbile lile la kijana ili asiweze kugundulika haraka na Takadiri Al-harabi ambaye alikwishamuona mara ya kwanza akiwa katika lile umbile lake la kiutu uzima, lengo lake safari hii ni kumuwahi na kumuangamiza komando yule



    Cha kuchekesha na kustaajabisha Si Mzee Sufian wala Takadiri aliegundua kua alikuwa akiogelea na hasimu wake, hakika ile ilikuwa ni miamba ya kuotea mbali. Kila mmoja alijibadilisha kiukweli kiasi cha kutomfanya mwenzie ahisi kitu tangu walipokutana kwa mara ya kwanza, hakuna aliyekuwa na mapenzi na mwenzie kwani kila mmoja alikuwa kazini ila ule utowekaji wa kipekee ulitosha kabisa kwa Mzee Sufiani akiwa katika umbile la ujana kuhisi hali ya hatari, akatoka haraka na kuanza kumfuatilia Msichana yule



    Kilichomuondoa haraka Takadiri Al-harabi ni Nuru na miale ya Pete(Khatam Budha) iliyokua ikimjia kwa mbali sana huku ikitaka kufifia, miale ile ilikuwa ikitokea katika kituo cha Polisi Kijitonyama alikohifadhiwa Suhail, kama ambavyo Suhail alielekezwa kua atakapoivua kwa muda mrefu Pete ile basi Nuru yake ni kali itaweza kuwafikia wale majini waliokuwa wakiisaka kwa udi na uvumba



    Japo haikumdhihirikia waziwazi Komando Takadiri kua Nuru ile inatokea wapi lakini alianza kuifatilia kwa ustadi wa hali ya juu, huku nae kwa nyuma akifuatiliwa na Mzee Sufiani Bin Shamhurish



    Katika chumba cha kipelelezi ambacho ndio ofisi ya Inspekta Kenjah, walikuwa wameketi huku wakitazamana, Alikuwa ni Inspekta Kenjah mwenyewe na Kopro Salum Marando alieleta taarifa ya uchunguzi mfupi alioupeleleza, hali aliyokuwa nayo yule Kopro ilimtisha sana Inpekta maana kijana alionekana kujawa na wahka wa hali ya juu

    “Enhee Ongea ‘corporal’..” alianza mjadala Inspekta Kenjah

    “Afande hali inatisha kiasi…” akakohoa kidogo na kuendelea “..Nimeenda kuonana na mkurugenzi wa ile Bar ya Break down baada ya kujitambulisha kua nimetoka kwako akanipokea vizuri sana na kunipa ushirikiana hatua kwa hatua..”

    “Enhee matokeo ua ushirikiano wake..”

    “Kabla ya akina Suhail na marehem Msigwa kuwasili pale Bar, Camera zilikuwa zikionesha magari kadhaa yaliyoanza kuwasili pale, magari hayo yalikuwa mengi tu ila kuna magari mawili japokuwa yalikuwa yameegeshwa tofautitofauti tangu yalipowasili hakushuka mtu yeyote na hatimaye tuligundua kua mpigaji wa zile Risasi alikuwa ameketi ndani ya moja ya gari hizo”

    “Duh, gari gani hiyo?,” alisaili Inspekta Kenjah kwa wahka

    “ilikuwa ni Prado ya rangi ya buluu, namba zake za usajili nimeziandika kwenye Report hapo juu, na hata baada ya tukio lile ile Prado ikatoweka hapohapo huku ikifuatiwa kwa kasi ileile na gari ile nyingine ambayo nayo tulichukua namba zake sa usajili, hii ilikuwa ni Bmw zile Old model”

    “Kazi nzuri kopro,” aliongea Inspekta Kenja huku akimpa mkono kijana wake kwa kazi nzito lakini akakatishwa na maneno ya kijana yule

    “Zaidi ya hilo Afande… Nimezifuatilia gari zile na nimefanikiwa kupata moja”

    “Ipi hiyo?”

    “Ile Bmw, alishuka kijana mmoja bila shaka anaeelekea kwenye utu uzima, japo anaonekana ni Bishoo tu lakini anaonekana ni mtu wa kazi yule”

    “Kwanini unamuita Bishoo?”

    “Japo alikuwa amevaa suti ya kawaida tu lakini kwa mtu wa umri wake asingepaswa kubandika meno ya dhahabu ndani ya kinywa chake”

    “Nini? Meno ya dhahabu?,” alisaili kwa hofu Inspekta, Kopro Salum Marando hakujibu akafungua begi lake dogo na kutoa kamera yake aliyotumia kumpigia ile picha, haraka Inspekta akachukua ile Camera na kuiangalia picha ile, hakutaka hata kumalizia akaiweka juu ya meza Camera ile huku akishusha pumzi

    “Tumevamiwa Kopro..”

    “Kwanini afande?”

    “Huyu ni muuaji hatari kutoka Uganda na hua anatumiwa na Mtandao mkubwa sana, anaitwa Joram Ndege, ni hatari huyo mtu..na sasa nimeanza kupata picha ya zile meseji ambazo Suhail alikuwa akilalamika kua zilikuwa zikienda kwa mkewe bila ya yeye kuzituma”

    “Sasa anahusiana nini na hizo meseji?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kuna taarifa nilipata kuambiwa kua Mtandao ule una mtambo maalum wa kunasa mawasiliano ya simu hizi za kawaida pia wanaweza kuandika wao meseji wakiwa hukohuko walipo kasha wakaituma kwenye namba yoyote waitakayo na wakaamua iingie kwa jina gani ulilolisevu wewe katika simu yako.. Sasa tukio hilo la Suhail ni la pili kutokea na tuligundua kua kuna uwezo huo kufuatia ile kesi iliyokua kule Msimbazi kuhusiana na yule mwanamke aliyekuwa akilalamika kua kuna meseji za aina ile zilionesha akiwa anawasaliana na namba ambazo hakuwasiliana nazo kamwe..” Kabla Inspekta hajaendelea akadakiwa na Kopro Salum

    “.. Ooh nimeikumbuka hiyo kesi, sikia sasa Afande, unajua kua mume wa huyo dada aliyekuwa akilalamika alikuwa ndie huyo mwandishi wa habari alieuawa..Msigwa”

    “Kweli eeh?”

    “Hakika Afande”



    Kikapita kimya cha haja huku kila mmoja akitafakari juu ya kadhia ile kabla ya Kopro kuuliza swali hewani

    “Sasa inamaana Msigwa anahusika na mtandao huo?”

    “Inawezekana maana jamaa hua wanatumia sana vyombo vya habari, sasa kwa mtu mpenda pesa kama Msigwa itakua walikuwa wakimtumia sasa labda wakatofautiana jambo au pengine alivujisha siri zao”

    “Kama ni mshirika wao ikawaje tena meseji hizo za kubumba zikakutwa kwenye simu ya mkewe mpaka wakaachana”

    “Hapo ndipo tutakapoanzia upelelezi”

    *****



    Wakati matukio hayo yakiendelea huko mjini, hali ilikuwa imechemka upande wa pili huko Bagamoyo ambapo Shekhia alikuwa anamalizia kutoa kafara ya damu kwa pete yake ili baada ya hapo sasa arejee tena Dar Es Salaam kuja kumaliza mchezo alioucheza nusu.



    “NO, nadhani itakuwa busara kama upelelezi utaanzia kwa Sajenti Rwehumbiza,” alidakia Koplo Marando akimtaja askari mwenzie nd’o achunguzwe



    “Rwehumbiza? Kwa lipi hasa?” Alimaka Insp Kenjah



    “..Risasi moja aliyopigwa Msigwa haikutosha kuing’oa roho yake hata ikabidi apigwe risasi ya pili bila shaka na mkondo uleule wa wauaji.”



    “Mbona sikuelewi Koplo!.. unataka kuniambia Marehemu Msigwa alipigwa Risasi nyingine tofauti na ile ya mwanzo?..”



    “Afande, kama utathibitisha kuwa Msigwa alipigwa Risasi moja tu ulipokuwa naye basi akina Rwehumbiza ndio watakaopaswa kutujibu kuwa Risasi ya pili ilitokea wapi?”



    “Kivipi?”



    “..Iko hivi Afande, baada ya tukio lile la risasi wakati wewe ulipokuwa unaondoka haraka kujaribu kufuatilia muelekeo ulipotokea risasi ile mimi na Afande Chanzi tulikamilisha haraka sana taratibu zote kisha tukawa tunataka kumuwahisha hospitali yule bwana aliye kwenye jokofu muda huu… lakini ghafla akawasili Sajenti Rwehumbiza na kuniamuru kuwa nibaki pale kituoni wakati yeye na Afande Chanzi wakiingia ndani ya gari wakijitwisha jukumu la kumpeleka mgonjwa hospitali.. Majibu niliyatarajia tu kuwa Mgonjwa angefia nje ya hospitali.. na ndivyo ilivyokuwa” Inpekta Kenjah alibaki mdomo wazi asimwelewe vyema kijana wake huyu anayeongea kwa mbwembwe na kujiamini

    “Risasi mbili? No, alipigwa risasi moja tu mbele yangu...” alisema Inspekta Kenjah na kuongezea “..Kwanini wewe ulihisi kuwa angefia nje ya hospitali?”



    “Mtindo alioutumia Sajent Rwehumbiza kunipokonya jukumu lile la kwenda hospitali japo ni mkubwa wangu tena huku akitaka kushirikiana na Afande Chanzi ndio lilinipa udadisi zaidi maana huyu Chanzi si mtu mzuri sana… kama utakumbuka amekuwa akihusishwa na matukio kadhaa ya kutumiwa na wanasiasa, na hilo ndilo jambo lililomfanya akahimishiwa huku kituoni kwetu akitokea kule Msimbazi. Sasa baada ya kupata habari za kifo cha Msigwa niliwahi haraka Hospitalini nikaonana na daktari ndipo akanionesha vipimo vya uchunguzi wa mwili wa marehemu vinavyoonesha kuwa marehemu alipigwa risasi mbili.. moja kulia na nyingine kushoto mwa kifua chake..”



    “E bwana eeh, hakika kuna mchezo mchafu hapa! Rwehumbiza na Chanzi wamehusika kummalizia Msigwa.. Kwanini hasa?!.. Wametumwa tu, na aliyewatuma hatujamjua, Lazima tumjue..” Kikapita kimya cha muda mfupi kabla ya Insp Kenjah kuendelea “..yatupasa kuwa makini sana katika hili lakini ni lazima tuwabaini na kuwatia chini ya chini ya uvungu wa Sheria” kikapita tena kimya cha muda mrefu huku kila mmoja akiwazua yake moyoni



    “Sikiliza Koplo hii kazi iliyo mbele yetu ni kubwa kuliko inavyoonekana, kila kinachotokea sasa kinazidi kunithibitishia kua kuna mtandao mkubwa wa Mauaji ndani ya Nchi yetu, Joram Ndege ‘Meno ya dhahabu’ ni kiashiria tosha kua kuna kazi maalum inaendelea humu Nchini hivyo sasa tunaingia kazini, kufa na kupona, Mimi na wewe..”



    “Sawa Afande, ila ninashauri tu kua ili kazi hii iwe rahisi hawa akina Rwehumbiza tutawachunguza kimyakimya bila kusema nao jambo lolote wakati tukiwa tunaendelea na upelelezi wa kawaida kwa Suhail, Bucha, Kassa, Lillian, na watakaohitajika.”



    “Yeah, hilo jambo la msingi.. hata mimi ninafikiria kwenda kuongea na CP Kibila ili afahamu hatua kwa hatua lakini nahofia kuchanganya samaki mbichi na mchicha maana kama tayari kuna harufu ya wakubwa kuhusika hatuwezi kumjua mwema ni nani kwa sasa.”

    Walijadili mengi mwishowe wakakubaliana namna ya kuanza, kwa hatua hiyo wakaafikiana kuwa Insp Kenjah aende akafanye uchunguzi ofisini kwa Suhail wakati huo Koplo Marando yeye atakwenda kufanya uchunguzi wake nyumbani kwa marehemu Msigwa, lakini kabla hawajatawanyika ikaingia simu kwa Inspekta Kenjah



    “Hallow,” alipokea Leonard Kenjah kisha akawa akiisikiliza sauti itokeayo upande wa pili wa simu yake. Kadri alivyokuwa akisikiliza ndivyo alivyozidi kuonekana kuchanganywa na taarifa alizokuwa akipatiwa,

    “Tukio lina muda gani?,” alisikika tena Kenjah akimsaili mtu aliyekuwa akisema nae na kuongezea tena “..Mmejaribu kunakili namba za gari hiyo?”

    Maongezi yaliashiria kua kuna tatizo limeibuka huko itokeako sauti ya upande wa pili wa simu. Koplo Marando alikua akimshangaa tu mkuu wake akiongea kwa wahka japo hakutambua sana kinachojiri ndani ya simu ile



    “Tuondoke haraka Koplo, mambo yameshaharibika huko,” aliongea Inspekta Kenjah baada ya kukata simu yake



    “Kuna nini Afande?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Lillian..”



    “Yupi?”



    “Yule binti tuliepanga kumuhoji kuhusu Msigwa na Bucha.. ametekwa na maharamia waliomvamia wakati akitoka ofisini kwake, wametoweka naye kusikojulikana.”



    “Hakuna waliemjua hata mmoja mmoja kati ya hao watekaji?”



    “Hata namba ya gari ilikua ni ya kichina achilia mbali wao watekaji..”



    “Aisee hii kali, nani amekupigia wewe?” Koplo Marando aliendelea kumuuliza Inpektah Kenjah wakati wakiwa wameshatoka nje ya ofisi kwa ajili ya kuanza msafara wao



    “Kanipigia yule Mkurugenzi wa pale, Bwana Kassa, dah tumepoteza shahidi mwingine huyo.”



    “Hapa kuna hila ya kupoteza ushahidi wa kadhia hii.”



    “Hakika.”



    Miale/Nuru iliyokuawa ikimea kutokea katika Pete(Khatam Budha) ilimfanya Komando Takadir Al-harab azidi kusogea mpaka jijini Dar es Salaam akiwa vilevile katika Umbile la yule Msichana mrembo alilotoka nalo kule katika fukwe za Socotra japo hakugundua kwa haraka kuwa Nuru ile inatokea katika kaunta ya kituo cha Polisi Kijitonyama ilikohifadhiwa na wana usalama baada ya kumvua Suhail. Hakuweza kulijua hilo kwa haraka kwa kuwa Nuru ile ilikuwa ikimea na kufifia ndani ya muda mfupi kwa sababu japo haikuwa kidoleni mwa Suhail lakini haikuwa mbali sana kutokea pale kaunta mpaka kule Selo alikohifadhiwa.

    Naye Mzee Sufian Bin Shamhurish akiwa katika umbile lile la kijana wa kule ufukoni aliendelea kumfuatilia kwa karibu Msichana yule ambaye bado hakuwa amemgundua kuwa ni Takadir Alharabi japo tayari alikwishahisi kuwa hakuwa Mwanaadam, na alishagundua kwamba ni kiumbe kutoka kule katika Himaya yao ya Budha. Aliligundua hilo baada ya kuona uelekeo wa Msichana yule ukisogea maeneo ya kule kituoni ambako ilikwisha mdhihirikia kuwa Suhail aliwekwa mule.

    Alitamani kusogea kituoni kuinyakua Pete ile na kutoweka nayo lakini alihofia kumpa Msichana yule nafasi ya kumuhisi uwepo wake mahala pale.. akatulia!

    Siku nzima ikawa ni mawindo yasiyo na tija kwa pande zote.. Komandoo Takadir akiiwinda Pete, Mzee Sufian akimwinda msichana/Takadir.

    Ilipofika Usiku sasa Mzee Sufian Bin Shamhurish kama walivyo majini wengine akaondoka kwa upepo mkali mpaka Bagamoyo ambako alimkuta Shekhia akijiandaa kwenda Dar es Salaam kufanya tukio alilodhamiria, Muda huu sasa Mzee Sufian akiwa amejirejesha katika umbile lake la ki-utu uzima ambalo ndilo nembo yake awapo duniani



    “Unakwenda wapi?,” Mzee Sufian alimuhoji Shekhia baada ya Salamu punde tu alipowasili nyumbani kwake



    “Nakwenda Dar.”



    “Kufanya nini?”



    “Nakwenda nyumbani kwangu.”



    “unajua wewe ni mpumbavu kwa kiasi kikubwa sana! Unadhani una akili sana kuliko mimi!.. Kila ulichokifanya kipo kiganjani mwangu, umefanya makosa makubwa sana ambayo huenda yakaitaifisha roho yangu na yako pia katika mikono ya baradhuli Takadiri.”



    “Makosa gani baba?” Aliuliza kwa mshangao Shekhia baada ya kusikia habari hizo mbaya maana japo hamjui kabisa huyo Takadiri lakini mara kwa mara hupewa habari zake za uwezo wake



    “haujui eeh? Suhail na Sharifa wako wapi? Nani sababu ya yote hayo?”

    Shekhia aliinamisha kichwa chini kwa hofu, akajikohoza kidogo kabla hajajibu kwa uwoga na kwa sauti ya kulalamika



    “Baba naomba unisamehe tu ila Suhail ndie kanifanyia kitu kibaya sana.. Na kwa kitendo alichokifanya maana yake amenigeuka mimi na wewe pia, amevunja masharti yako.”



    “Hata kama..” alidakia Mzee Sufian na kuendelea “..ulipaswa kuwa mstahamilivu tu kwa kuwa unafahamu fika kua kuna kazi yetu muhimu sana anaitekeleza. Sasa mpaka hivi tunaongea hapa ninawindwa vibaya na Adui ambaye huu ndio ulikua muda wa kumuangamiza lakini silaha haipo, Suhail yuko chini ya Polisi, na mbaya kuliko zote na Khatam Budha nayo iko chini ya mikono ya Polisi pia.. Takadiri kaishasogea eneo la kituoni na tusipokuwa makini tutaangamia sote”



    Mjadala ulikuwa si wenye tija sana zaidi ya lawama tu, Shekhia hakuwa na uwezo mkubwa wa kijini wa kuweza kumsaidia baba yake. Akaruhisiwa aondoke naye Akaondoka na kurejea Dar huku akimuacha Baba yake akiwa kulekule Bagamoyo akijaribu kuwapanga wale wafuasi wake wote kwa ajili ya mpambano.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kichwani, Shekhia aliendelea kwa kiasi kikubwa kutawaliwa na dhamira yake ileile ya kwenda TMJ Hospital kumalizia kazi aliyomtenda Sharifa.

    Wakati Mzee Sufian akiendelea kupanga watu wakehuko Bagamoyo ndipo ghafla lilitukia jambo ambalo hakulitegea maishani mwake, Ilikuwa ni kipigo cha ghafla na kushitukiza, kipigo cha kitaalam ambacho kilikua kikiacha maumivu makali na majeraha kwa Mzee Sufian na wafuasi wake tena ndani ya nyumba yake bila ya kumwona mpigaji.. Mvamizi huyo alikuwa akipiga mapigo ya kuangamiza na kuteketeza, hakika alidhamiria ubaya maana ndani ya muda mfupi alikua amewalaza chini wafuasi watano wa Mzee Sufian wakiwa wameshasalitiana na Roho zao.

    Mzee Sufian alichanganyikiwa vibaya akawa amehamaki sasa,alipojipanga naye kitaalam ndipo alipomuona kwa tabu sana mvamizi wake! Komando Takadir Al-harabi akiwa katika umbile lilelile la kike. Mwili wa Sufian ulizizima kwa hofu na uwoga kila alipokumbuka kuwa kumbe kule ‘Beach’ hakuwa na msichana wa kawaida. japo aliduwazwa na maswali lukuki kichwani mwake kua aliwezaje kukaa muda wote ule akikumbatiana na Adui yule bila ya kumjuwa, hakupata jibu lakini alifarijika kidogo kwakuwa aligundua kuwa Takadir asingegundua kuwa ni yeye aliyekuwa naye kule ufukweni kwa kua hakuwa katika umbile lile la ujana muda ule wakiwa wanatazamana.

    Mpambano ukaanza upya!

    Ilikuwa ni piga nikupige. Ngangari kwa ngunguri, jino kwa jino..

    Hakuna aliekuwa na Silaha yoyote nzito zaidi ya uwezo wa kila mmoja wao hivyo ikawa ni mtindo wa kuzichapa ‘Kavukavu’

    Mzee Sufian alijitahidi kupambana lakini hakuwa akipambana na Jinni wa kiwango chake bali alikuwa akipambana na Komandoo wa Kijini hivyo mara zote alielemewa yeye na wafuasi wake.

    Hali ilikuwa tete kwa upande wa Mzee Sufian ambapo wafuasi wake walizidi kuteketea licha ya kuwa alikwisha wapigia kelele ya kuwatahadharisha kua wanapambana na Takadir! Ndani ya dakika takribani kumi za mapambano aliwabakiza watu wawili tu, Mzee Sufian na kijana wake wa mwisho huku wengine wote wakiwa tayari wameshafungasha virago vyao kuelekea kuzimu. Ilikua ni maafa ya kutisha na kuumiza kwa Mzee Sufian Bin Shamhurish kupoteza kambi yake nzima, nyumba nzima ilitapakaa damu.. Takadir aliyafanya hayo kwakuwa hakuwa na jinsi tena japo hakupaswa kuwaangamiza majini wenzie lakini kwakuwa juhudi za kuipata Pete ile huku akiwa peke yake baada ya wenzie wote kuangamizwa na Mzee Sufian iligonga mwamba hivyo naye akaona hakuna namna zaidi ya kuwaangamiza wenzie walioasi na kumuunga mkono Mzee Sufian.

    Kikubwa zaidi ni muda! Muda wa kuwepo huku katika uso wa Dunia, kwa mujibu wa kanuni zao ni kwamba muda wa kiongozi wao mkuu kua madarakani unakwisha na zilibaki siku chache sana umalizike kabisa lakini hakuna kiongozi atakaekabidhiwa Himaya/Nchi bila ya ‘Khatam Budha’ ambayo kwa sasa inamilikiwa na Mzee Sufian. na endapo kama muda utaisha wa kiongozi aliyopo madarakani kabla ya khatam Budha kupatikana basi maafa na majanga yatakayowakumba hayatamithilika, Himaya nzima na waliyomo itaangamia na kuteketea na hapatakuwa tena na utawala huo

    Baada ya kichapo kuzidi kipimo Mzee Sufian akatoweka kimaajabu huku akimtelekeza yule kijana wake pekee aliyebaki hai aendelee kupambana na Jabari lile kutoka himaya ya Budha, japo roho ilimuuma akijuwa kabisa kijana wake yule asingedumu hata dakika tano tu kwa Takadiri angekuwa maiti,

    Na hivyo ndivyo ilivyokuwa!

    Baada ya kutoa kichapo kile cha nguvu kilichombakiza Mzee Sufiani na binti yake Shekhia wakiwa hai huku wenzao wote wakiwa wameteketezwa na Komando yule wa Kijini, sasa ile Miale kutoka katika Pete(Khatam Budha) ikaanza kumjia waziwazi Komandoo Takadir Al harabi, akaiona kwa uwazi kabisa inakotokea, Kituo cha Polisi Kijito nyama. Hakua na haja ya kukaa tena Bagamoyo akaanza kuondoka kufuata uelekeo wa miale ile

    *****



    Inspekta Kenjah na Koplo Mrando waliwasili katika ofisi ya Tuwa Kadabra kule Ilala, walilakiwa na hali ya taharuki na sintofahamu kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni na wananchi nje ya kampuni walioshuhudia tukio lile la aina yake.



    “Enhee Ilikuwaje kaka?” Inspekta Kenjah alimsaili kijana mmoja fundi baiskeli alieushuhudia ‘mkanda’ mzima wa tukio



    “..Unajua ilikuwa ni kama mchezo wa kuigiza, kuna gari ilikuja na kuegesha hapo karibu ya geti, sasa nikawa naishangaa kwanini haiingii ndani muda wote? Sasa wakati sijapata jibu ndipo nikamwona Yule Binti akitoka nje ya geti..”



    “Enhee ikawaje?” Koplo Marando alitamani kumuwahisha Yule Shuhuda atoe maelezo haraka haraka kwa jinsi alivyokuwa akitamani kujua ilivyokua, Yule Shuhuda akaendelea kutiririsha tukio lilivyokuwa “..Sasa ghafla Yule dreva wa gari ile akashusha kioo, nadhani alimsalimia binti Yule maana kama vile binti Yyle alisita kidogo.. hapohapo akashuka kijana mmoja amevaa suti nyeusi alipofika tu akamdaka kwa nguvu yule binti na kuanza kumuingiza ndani ya gari, Yule dada akawa anapiga kelele za kuhitajia msaada lakini hazikufaa kitu mpaka alipoingizwa ndani ya gari na kutokomea naye.”



    “Sasa muda huo wewe ulichukua hatua gani?,” Alisaili Kenjah



    “Nilisaidia kupiga kelele huku nikiikimbilia ile gari, wakatoka hao akina dada wa hapo Mgahawani wanapouza chakula nao wakanisaidia kupiga kelele lakini hazikufaa kitu maana walikuwa wameshatoweka.”



    “Hamkuweza hata kunakili namba za gari?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nilitaka kufanya hivyo lakini nikagundua kua gari ile ilikuwa na namba zisizoeleweka kirahisi… ni kama herufi za kichina tu.”

    Ilikuwa ni utata juu ya utata, Walijaribu kuwasaili watu wengine wawili watatu bila ya kupata cha maana..



    Wakamchukua Bwana Kassa na na huyo fundi baiskeli wakaondoka nao na kuelekea kituoni kwao kuwachukua maelezo kwa utulivu zaidi.



    Nje ya hospitali ya TMJ Walikuwa wamesimama akina Mzee Kusekwa na Fungemeza pamoja na wake zao wakimsubiri Kilingo Mkude alierudi wodini kuchukuwa funguo ya gari aliyoisahau juu ya kitanda ili sasa waelekee kituo cha Polisi kumuangalia Suhail, hii ikiwa ni mara yao ya pili kwenda kituoni bila mafanikio ya kumwekea dhamana kijana wao wala hata kuonana nae, hapakuwa na sababu za msingi sana zaidi ya kuambiwa kuwa warejee tena siku nyingine kwani mpelelezi wa kesi hiyo ametoka.

    Wakiwa wanaendelea kujadiliana mawili matatu mara wakapishana na Binti mmoja aliekua akiingia mule Wodini kwa kasi, ni Binti tu kama walivyo mabinti wengine machoni mwa wazee wale, alikuwa amevalia hijabu lake zuri jeusi na mtandio wa Njano. Mavazi yalimtafsiri kuwa ni msataarabu na muungwana lakini kitendo cha kuwapita bila hata salamu wazee wale ambao bila shaka ni wa umri wa sawa na wazazi wake yeye ilitilia shaka uungwana wake, lakini labda hiyo ndio hali ya jijini tofauti na huko mikoani watokeapo, au pengine amepokea taarifa za mgonjwa wake pale. Hakuna mwenye jibu zaidi yake mwenyewe! Wakaachana naye.



    Alikuwa ni Shekhia Bint Sufian, Mchoko wa safari yake ya mwendo kasi akitokea Bagamoyo ulizidisha kiu yake ya kummalizia Sharifa Mle Wodini..

    Wakati huo Kilingo naye akiwa na Funguo yake ya gari mkononi alipishana na dada Yule akielekea kulekule alipokuwa akitokea yeye lakini hakujali kwa kuwa watu wengi huingia Hopitalini hapo kuangalia wagonjwa wao.. akatoka mpaka nje na kuungana na wazazi, wakajongea katika gari yao na kuianza safari ya kituo cha Polisi huku wakimwachia Uhuru Shekhia wa kutenda lolote alitakalo kwa mgonjwa wao, hawakulitambua hilo

    *****



    Inpektah Kenjah na kijana wake machachari Koplo Salum Marando walikua wameketi ndani ya Ofisi yao, muda huo wakitazamana na Suhail akiwa mchovu kabisa. Ilikuwa ni muda mfupi baada ya kumaliza mahojiano na Bw Kassa pamoja na yule fundi baiskeli alieshuhudia tukio la utekaji nyara



    “Mara yako ya mwisho kuonana na Joram Ndege ilikua lini?,” Inspektah Kenjah alimtupia Suhail swali la mtego ili apate kujuwa namna atakavyopokea kwa mshituko swali hilo



    “Joram Ndege nd’o nani tena?”



    “Naomba uwe ‘serious’ Bwana Suhail, usilazimishe kazi hii iwe ndefu.. ina maana wewe haumjui Joram Ndege?”



    “Yeah simjui nd’o maana nikakuuliza.. labda naweza kumfahamu kwa sura au kwa jina linguine.”



    “Yule jamaa yenu mwenye meno ya dhahabu, ilikua lini ile ulipowasiliana nae?”

    “Mnh, Afande mbona sikuelewi? Sina mtu wa jina hilo katika kumbukumbu zangu.”



    “Ok, hautaki kusema Eeh, haya tuendelee na mengine.. ulikuwa na ugomvi gani mwingine mkubwa zaidi na marehemu Msigwa?” Inspekta aliendelea kusaili kwa udadisi



    “Sikuwa na ugomvi naye.. ila huenda yeye alikuwa na ugomvi na mimi, labda m’ngemuuliza mwenyewe”



    “Khaa! Tumuulize mtu aliekufa?” Sasa Insp alibadilika na kuuva ‘Uso wa Dagaa.’



    “Ooh! Samahani Afande nilipitiwa tu.. unajua ni kama haijaniingia kichwani kuwa Msigwa amefariki” Insp akamwangalia kwa makini na udadisi mkubwa sana Suhail wakati alipokuwa akijitetea



    “Kati yako wewe na marehemu Msigwa ni yupi aliyemtambulisha mwenzie kwa Joram Ndege?” Koplo Salum nae alitupia swali ambalo tayari Suhail alikwishalijibu, alikuwa na maana yake ya kulirejea tena



    “Nimeshajibu swali hilo.”



    “Jibu tena.”



    “Simfahamu huyo Joram Ndege.” Maswali yalilenga zaidi kufahamu kuhusina na mgogoro wa Suhail na Msigwa pia maafisa hawa wa Polisi walitaka kuhakikisha kama kuna dalili zozote za Suhail kumfahamu ‘Meno ya Dhahabu’ lakini haikuwa kazi rahisi maana Suhail alionesha kutoelewa chochote

    Wakiwa katikati ya majadiliano mara mlango wa ofisi ukagongwa, baada ya Inspekta kuamuru aliegonga mlango aingie, wakaingia wazee wawili.

    Si Inspekta Kenjah wala Koplo Salum aliefahamiana na wazee wale, Suhail aliyekuwa kaupa kisogo mlango wala hakujishughulisha kugeuka kwa minajili ya kuwatambuwa walioingia mle ndani!

    Kabla hakajisemwa chochote Punde mlango ukafunguliwa tena akaingia mtu mwingine, huyu sasa ndiye aliemfanya Inspekta Kenjah afungue kinywa chakeCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Umefwata nini huku wewe?..” alibwata Inspekta na kabla hajajibiwa akaendelea tena “..We si ulijifanya una ‘Mdomo’ sana eeh!!”

    Ndipo Suhail akageuka ili amtambue anayekemewa ndipo macho yake yakakutana na watu watatu aliowafahamu vilivyo,

    Mzee Kusekwa na Mzee Fungameza wakiwa mbele huku wakifuatiwa na Kilingo Mkude. Akashusha pumzi!

    Hakujua kwanini Kilingo anakaripiwa na Afande Yule lakini muda huohuo ikamjia picha ya siku alipokuja kukamatwa pale Hospitalini yalitokea majibizano kati ya Kilingo na Insp Kenjah

    “TOKA NJE KIJANA, PUMBAAVU” Alibwata Inspekta huku matuta yakijitengeneza katika paji la uso wake, Kilingo hakubisha akajitokea zake nje, macho ya Insp yakahamia kwa wazee wale wawili waliokuwa wamesimama bila ya kujua malumbano yale ni ya nini

    “Enhee, na ninyi niwasaidie nini hapa?”

    “Samahani bwana Afande, sisi ni wazazi wake na huyo Suhail.. tulipofika hapo nje tukaelekezwa tuje huku ndani tuongee na afande anaehusika na kesi yake.. sasa kama kuna kosa tulilolifanya utuwie radhi mwanangu,” Mzee Kusekwa aliongea kwa sauti ya upole yenye kutia huruma mpaka Insp Kenjah akajikuta anapoa nafsi

    “No, hakuna kosa mlilofanya wazee ila kosa alilifanya huyo kijana kwa kutokujua matumizi sahihi ya mdomo wake aongeapo na watu.. na kosa la pili wamelifanya hao waliowaelekeza mje huku ndani wakati wanafahamu kua huu ni muda wa majukumu ya dharura..”

    “Sasa Wazee mnaweza kusubiri kwanza nje hapo kidogo ili tumalize kazi kidogo?!” Koplo Salum aliingilia kati lakini alikatishwa na Kenjah

    “No, labda wamemletea chakula kijana wao, Eti?”

    “Hapana, hatujaleta chochote zaidi ya kuja kufuatilia utaratibu wa kumwekea dhamana kijana na ikiwezekana kuzungumza naye machache”

    “Tunasikitika kuwa yote hayawezekani kwa sasa, si dhamana wala kuongea nae chochote.. kesi ya mauaji ni kubwa sana wazee” Baada ya majadiliano ya muda wazeewale wakaamriwa waondoke warejee kesho yake.. Lakini kabla hawajatoka ndipo Suhail akasema jambo

    “..Sasa Afande kama imethibitika siwezi kupata dhamana kwa sasa, basi nilikuwa nina ombi moja tu..”

    “..Lipi hilo?”

    “..Katika vile vitu vyangu nilivyoandikisha pale kaunta naomba niwakabidhi hawa wazazi wangu waende navyo nyumbani”

    Suhail aliongea kwa utulivu kama vile mtu asiyekuwa na mashaka yoyote huku dhamira ya kuvihitajia vile vitu vyake ikiwa ni Pete(Khatam Budha).

    Ombi hilo halikuwa gumu sana kwa Inspekta Kenjah ukizingatia hakuwahi kukwazana na Suhail tangu alipomweka chini ya ulinzi, Akamuamuru Koplo Marando akavilete vitu hivyo..

    Ilikua ni ‘Wallet’, mkanda wa Suruali, Pesa, na Pete. Baada ya Koplo Marando kuvileta vitu vile akamkabidhi Insp Kenjah ambaye naye akavikabidhi kwa wale wazee waliokuwa wamesimama kwa unyonge muda wote tangu walipoingia mle ofisini.. Wakavipokea na kuanza kuondoka zao

    “Hey! Embu ngojeni kwanza.. Leteni hiyo Pete,” Insp Kenjah aliwawahi wale wazee kabla hawajaondoka. Mapigo ya moyo yakambadilika Suhail, hofu ikamvaa upya hakujua ni kwanini Pete inataka kuzuiliwa.. Wazee wakarejea, Inpekta akaichu

    “..Nakumbuka kwenye Maelezo Suhail uliandikisha kua una Pete ya rangi ya Kijani, sasa mbona hii ni Nyekundu?” Suhail macho yakamtoka Pima, ni kweli aliandikisha vile kwa kua muda ule rangi ya Pete ilikua ni ya Kijani lakini alitambua kua Pete ile hujibadili rangi mara kwa mara kutokana na sababu za msingi, hilo halikumpa hofu kwa kua anaifahamu vema Pete ile, lakini hofu yake kubwa zaidi ni pale aliposikia kua Pete ile ilikua imebadilika na kua Nyekundu rangi ambayo huashiria hatari mara zote itokeapo.. hakujua ni hatari ipi iliyosababisha mpaka Pete ile kujibadili na kua Nyekundu

    “Itakuwa aliyeandika alikosea tu ila nd’o hiyohiyo,” Suhail alijibu kwa kujitetea

    “Hapana, hua hatwendi hivyo.. isije ikawa umepewa kitu cha mtu mwingine halafu ikaja kuleta shida baadaye, ngoja nimuangalie aliyekuandika maelezo siku ile” Insp Kenjah akatoka Nje ya Ofisi ile akiwa na ile Pete Mkononi

    Alipofika Kaunta akazungumza na wale askari wa pale mapokezi mpaka alipojiridhisha kuwa ile ni Pete ya Suhail ndipo akaanza kurejea ndani.

    Wakati huo Macho ya Binti mmoja mwenye asili ya Kiarabu aliyekuwa ameketi katika Benchi pembeni ya Meza ya kaunta yalikuwa yakimwangalia Insp Kenjah kwa udadisi na Mashaka kuanzia alipofika pale Kaunta na mpaka alipoanza kurejea ofisini kwake, macho ya Binti yule aliyejitanda mtandio mfupi wa Pinki yalipiga ghafla mkononi mwa Insp alipokua ameishika ile Pete(Khatam Budha), ilikuwa ni Pete aliyokua akiitafuta kwa udi na uvumba binti Yule, na sasa ameiona kwa mara ya kwanza ikiwa mkononi mwa Insp Yule wa jeshi la Polisi, akatamani amvamie palepale lakini akaamua kumwacha kwanza atoweke mbele ya macho ya wale askari wenzie..

    Mrembo yule hakua mwingine bali ni Komandoo Takadir Al-Harabi katika lile umbile la Binti wa Ufukweni, Aliwasili kituoni pale muda mfupi tu akivutwa na Nuru ya Pete ile

    Insp alipoingia tu Ofisini kwake ndipo Takadir nae akainuka na kuanza kumfuata kule ofisini mwake alikoingia..

    “Nadhani itaku ni yako bwana Suhail, maana hakuna mtuhumiwa yoyote alieacha Pete pale zaidi yako.. hebu ihakikishe mwenyewe,” Insp Kenjah aliongea huku akikabidhi ile Pete kwa Suhail baada ya kuingia mle ofisini kwake. Hilo likawa ni kosa kubwa kwa Kenjah lakini ni fursa adhim kwa Suhail..



    Alipoipokea tu akaivaa hapohapo kidoleni kama vile anaeijaribisha kisha akakibenjua kitufe kidogo sana kilichopo kwa upande wa nyuma wa Kile kito cha Rangi nyekundu. hapo hapo akaanza kuona taswira za ajabu zikijidhihirisha machoni mwake, Mshituko na mshangao vikamvaa, akakaza macho yake katika Pete ile iliyokuwa ikimwarifu matukio lukuki ya hatari!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakuna mwingine yoyote ndani ya ofisi ile aliyeelewa kuwa kijana Yule ameona nini maana alikuwa kama aliyepigwa na Butwaa la kawaida tu. Miongoni mwa Matukio yaliojidhihirisha machoni mwake baada ya kuivaa Pete ile, alimwona Shekhia akiwa amesimama katika Wodi aliyolazwa Sharifa huku akionekana kua na dakika chache tu za kutekeleza azma yake ya kummalizia mwenzie, Mara akaziona maiti zikiwa zimetapakaa kule nyumbani Bagamoyo, mara akamwona Msichana aliyekua anakaribia kuingia mle ofisini akiwa na kila dalili za hatari lakini hakumjuwa.

    Hakutaka kuendelea kuangalia taswira zingine kutoka katika Pete ile, hapohapo akasimama kisha akajiulizisha

    “Samahani Afande ni nani alieniandikisha maelezo yangu siku ile?” alipoona anachelewa kujibiwa akaendelea tena “..Embu nisubirini kidogo” akaanza kuondoka mle ofisini na kutoka nje, wale Maaskari walikuwa kama waliopigwa Shoti ya umeme maana walijikuta wakimwacha mtuhumiwa akitoka nje ya Ofisi yao bila idhini yao. Sasa alipotoka ndipo wao wakawa kama waliozinduka usingizini, wakaanza nao kumfuata.

    Wakwanza kutoka ofisini mle alikuwa ni Insp Kenjah akifuatiwa na Koplo Marando, Uso kwa Uso wakakutana na Takadir Al-Harabi bado akiwa katika umbile la kike

    “We unataka nini huku?” Koplo Marando alimsaili yule dada/Takadir aliyekuwa akipepesuka baada ya kusukumwa kwa ghadhabu na Insp Kenjah aliyekuwa akijaribu kumuwahi Suhail

    “Nilikuwa nina shida na huyo Afande,” Alijibu kwa upole na nidhamu yule Msichana/Takadir

    “Hakuna mtu uliyemuona akitoka humu ndani sasa hivi?” Koplo Salum alimtupia swali Dada Yule

    “Hapana, sijamwona mtu yoyote.. kwani kuna nini Afande?” Takadir alijiulizisha huku akitupa macho yake katika mkono wa Insp Kenjah bila kuiona Pete aliyoikusudia.. japo ni kweli hakumwona mtu yoyote akitoka mle Ofisini ila akahisi kua kuna jambo zito maana ghafla ile miale ya Pete hakuiona tena.. akatumia uwezo wake wa kijini lakini hakuambulia chochote..

    Wale maaskari wakaenda mpaka upande wa pili wa ile Korido inayokwenda mpaka katika ofisi ile waliyokuwemo wakawakuta akina Mama wawili wameketi pamoja katika Benchi

    “..Eti huyu kijana aliyetoka kule ofisini amepita hapa?” Leonard Kenjah aliwauliza kwa wahka akina mama wale

    “Kijana gani?.. hakuna kijana aliyepita hapa”

    “Ninyi mnafanya nini hapa?”

    “Hao ni wake zetu baba..” Sauti ilijitokeza nyuma ya Inspekta, ilikua ni sauti ya Mzee Fungameza

    “Anhaa kumbe mnafahamiana, Hapa kuna mchezo mmetuchezea.. haiwezekani mtu ametoka sasa hivi na ninyi mpo hapahapa halafu mseme hamjamwona.. mnaficha ukweli eeh?” alibwata Kenjah huku akiwa amewatolea macho wazee wale

    “Hakuna lolote tuliloliona hapa baba yangu..”

    “Hakuna kitu kama hicho.. naomba nyote mtulie hapohapo, asiondoke mtu” Insp alitoa amri ile kisha akaanza kuelekea kule Kaunta, akakutana na Koplo Marando nae akitokea kulekule

    “Vipi huko?”

    “Nao wanadai hawajamwona mtu yoyote kule, itakua amejificha hukuhuku” wakarudi masikini ya Mungu vijana wale maofisa wa Jeshi la Polisi mpaka kule walipokua mwanzo, wakapekua kila kona bila mafanikio.

    Wakarejea walipowaacha wale wazee wakawakuta wote wakiwa palepale isipokuwa mtu mmoja tu, yule dada wa kiarabu aliejitanda mtandio, Naye alitoweka katika mazingira ambayo hakuna jicho lililomdiriki

    “Yule dada wa Kiarabu yuko wapi?” Inpekta Kenjah aliuliza huku akiwatazama kwa ghadhabu akina Mzee Fungameza na wake zao

    “Dada wa kiarabu Yupi tena huyo?”

    “Nyie ,mnataka kutuchezea akili sio? Kila mtu mnajifanya hamjamwona eeh?”

    “Jamani hakuna mtu tuliyemwona sisi,, kwanza wakati ninyi mnatoka mle ofisini sisi tulikuwa wa mwisho kutoka.. na tulipotoka tukaja moja kwa moja mpaka pale mlipokua mkiwahoji hao mama zenu sasa huyo mwarabu sisi tumemwonea wapi jamani?”

    Ilikua ni kizaazaa, Wakiwa bado katika hali ile ya Sintofahamu mara ghafla simu ya Inpektah Kenjah ikaita, alipoangalia simu yake ilikuwa ni namba ya Inpekta Jenerali wa Polisi, IGP Cathbet Charles Suca. akaonesha kwa kidole ishara ya kuwataka wawe watulivu wakati akipokea simu ile..

    “Jambo Afande..” alianza Inp Kenjah

    “Uko wapi Inpekta?” alisaili IGP

    “Niko ofisini mkuu..”

    “Wewe nd’o unayo kesi ya yule Mwandishi wa habari aliyeuliwa?”

    “Ndiyo Mkuu”

    “Nataka kukiona kichwa chako hapa ofisini kwangu sasa hivi” Kabla Kenjah hajajibu simu ilikuwa imeshakatwa.

    Bila ya kupoteza muda Inpekta Kenjah akatoa maelekezo huku akiondoka “Koplo nimeitwa na mkuu.. IGP, Sasa hakuna cha ziada kwa sasa naomba uwaweke ‘lockup’ hao wazee wote mpaka nitakaporejea.. na wakiendelea kuleta ujanjaujanja wataozea jela mpka watakaposema Suhail ametorokea wapi pamoja na yule dada wa kiarabu..” Kusikia hivyo Mama Suhail akaanza kuangua kilio cha nguvu japo hakikusaidia kitu, masikini mama wa watu Polisi aliizowea kuisikia kwa jirani tu!

    Inspekta Kenjah akaondoka akielekea kwa IGP huku Koplo Marando akiwasweka ndani akina Mzee Kusekwa na wake zao

    *****

    SHEKHIA Bint Sufian alisimama karibu kabisa na kitanda alicholazwa Sharifa, Dhamira yake ikiwa ni mbaya moyoni mwake. Macho ya Sharifa yalikuwa yakimtazama ila kwa ule muonekano tu alitambuwa kuwa dada Yule hakuja kwa wema kabisa, alitamani hata ainuke ili ajihami endapo litatokea la kutokea lakini hiyo ilikuwa ni ndoto ya mchana! viungo vyake vyote vya upande wa kulia vilishamsaliti kitambo,

    Hakuweza kufanya lolote!

    Shekhia alilitambua hilo hivyo hakujihangaisha kumfikiria mara mbili hasimu wake Yule aliye taaban kitandani, akanyanyua mkono wake akaupeleka mpaka kinywani kisha akaibusu Pete yake kwa sura iliyojaa hasira, kiburi na dharau. Usingeweza kulitoafautisha hilo busu lake na ‘Msonyo’ tu kutoka kwa shetani mwingine yeyote.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kilichokua kikifuatia ni kumaliza N’gwe ya mwisho kwa kutoa Pigo takatifu, lakini akawa anasita, nafsi ikawa inamsuta, alijisikia vibaya sana kutekeleza jambo lile baya kabisa, Kumwua mtu asiye na hatia.. akajikuta anatiririsha machozi ya uchungu mashavuni mwake bila ya kujitambua.

    Hali ile ikawa inazidi kumshangaza Sharifa, hakujua ni kipi kinachomliza Mwanadada yule aliesimama kisharishari mbele yake

    “Pole sana Sharifa.. Sio kosa lako,” hatimae Alisema Shekhia huku akifuta machozi yake kabla ya kuugeukia mlango na kuanza kutoka mle Wodini akiwa hajatekeleza azma yake,

    Alipofika Mlangoni kabla hajatoka nje ya Wodi ile akageuka tena na kumuangalia Sharifa akiwa kule kitandani amelala vilevile, akamuangalia tena kwa Uchungu, hasira na huruma kwa wakati mmoja mpaka yeye mwenyewe akawa anajishangaa.. akafikiri mara kadhaa kisha akaamua kumrudia tena mpaka pale kitandani..

    Safari hii akiwa na dhamira ngumu!

    Alipofika hakutaka kupoteza tena muda, alimuangalia kwa mara ya mwisho kabla hajazungusha Kito cha Pete yake iliyokua kidoleni.. alipokibenjua tu ‘kito’ kile cha Pete ikatoka miale hafifu ya rangi ya kijani, akaielekezea kwa Sharifa kwa sekunde kadhaa kasha alipoona amefanya alichotaka akaondoka harakaharaka na kutoka kabisa Wodini..

    Alipofika nje ya Wodi ile akakata kona ya kushoto na kutokomea.. Wakati huohuo Kona ya kulia Suhail nd’o alikuwa akiingia hospitalini hapo baada ya kuletwa kwa kasi ya Upepo kutokea kule Polisi mpaka pale Hospitalini baada ya kuiamuru Pete(Khatam Budha) kufanya vile huku kukiwa hakuna hata mmoja aliemuona.. ilikua ni mchezo wa kawaida sana kutoka katika Pete ile

    Alipofika tu akapitiliza mpaka Wodini bila hata ya kuanzia kwa Dokta kupata maelekezo, kwa kuwa alikwishaifahamu Wodi aliyomo mkewe hivyo hilo halikua tatizo kwake..

    Hakuamini alichokiona baada ya kuingia mle Wodini, Hofu ilimvaa, woga ukamkumba akahisi kama anayeota vile. Mapigo ya moyo yakaongeza ‘Mdundo’

    Akiwa amesimama mlangoni huku amepigwa bumbuwazi macho yake yalikuwa yakimtazama Sharifa aliyekuwa amesimama jirani ya kitanda chake! kilichomstaajabisha zaidi si kumuona mkewe bali kumkuta akiwa katika hali ile, akiwa amesimama huku akionesha kua haumwi chochote kile.. Laiti kama Isingekua uwezo wa Pete yake ile iliyokuwa ikimuonesha hali ya mkewe huyo kabla hajawasili pale Hospitalini basi asingeamini kama alikuwa mahututi muda mfupi uliopita.. alitaraji kukutana na mzoga tu hasa alipomuona Shekhia akiwa mle Wodini akionesha kila dalili ya Nia ovu

    Sharifa nae kwa upande wake alikua akistaajabu juu ya tukio lililomtokea baada ya yule Mwanadada kummulika kwa Mwanga wa kijani kutokea katika Pete yake na hapohapo akashangaa amepona kabisa, viungo vyake vyote vikarejewa na uhai uliotoweka.. kila mara alijaribu kujikagua na kugundua kuwa alikuwa amepona kabisa, Bukheri wa A’fya!



    Alichokifanya Shekhia ilikuwa ni kitu kidogo tu, Kubadili maamuzi ya kudhuru na kuamua kumponya mwenzie baada ya kuingiwa na huruma ambayo hata yeye mwenyewe hakujuwa imetokea wapi.

    Suhail akamkimbilia mkewe na kumkumbatia kwa Nguvu akiwa haamini kabisa kama amemkuta mkewe huyo akiwa salama, wakati huo Sharifa alikua akitokwa na machozi ya furaha yaliyochanganyika na hofu..

    “Mke wangu..”

    “Mume wangu..”

    “Mbona sielewi?”

    “Hata mimi sielewi mume wangu.. najishangaa tu”

    Wakakumbatiana tena kwa nguvu kisha wakasogea pale kitandani na kuketi, ndipo sasa Sharifa akaanza kumsimulia Suhail tukio zima lilivyokua kuanzia alipowasili yule dada mpaka alipotoa mwanga wa ajabu katika Pete yake na jinsi alivyojishangaa kupata nguvu na kuinuka pale kitandani.. ilikuwa ni stori ya aina yake kwa wote kati yao kila mmoja kwa namna yake. Suhail hakuamini kabisa na wala hakutaka kuamini kua Shekhia amemwacha Sharifa bila ya madhara yoyote.. Sharifa naye alijawa na kiu ya kumjua mtu Yule lakini hakupata nafasi hiyo tena

    “Kwahiyo unasema haukumjua kabisa mwanamke huyo wala haukupata kumwona mahala popote?,” Suhail alimuuliza Sharifa huku akimshikashika nywele zake kwa kumliwaza na kumfariji

    “Nakwambia sijawahi kumuona kamwe.. na sijui tu kuna nini kinachoendelea”

    “Ukimuona tena unaweza kumtambua?”

    “Bila shaka.. maana nimemuangalia kwa muda mrefu sana akiwa mbele yangu”

    Wakaongea mengi sana mtu na mumewe mpaka wakaafikiana kua wamwite daktari aje ajionee hali ile ili ikiwezekana waondoke zao.. Madaktari nao hali ile ya mshangao ikawakumba, hawakuamini kuwa Msichana Yule amepona ghafla na kimiujiza, wakaanza kuitana wote na kumfanya Sharifa kuwa ni kivutio cha kitalii kwa macho na Bongo zao.. japo madaktari walijiridhisha kuwa Sharifa amepona lakini walikataa kumpa ruhusa kwa haraka namna ile, wakamsihi Suhail amwache mkewe huyo aendelee kuwa katika uangalizi wao mpaka kesho yake ndipo wangemruhusu kwa kuwa hali ile hua inaweza kujirudia ghafla.. Suhail na mkewe wakakubali kwa Tabu! Baada ya hapo sasa Suhail akaondoka Wodini hapo akimwambia mkewe kua angerejea baadaye kidogo. Sharifa hakuwa akijua lolote kuhusu kesi ya mauaji inayomuhusisha mumewe kwa kuwa hakuambiwa chochote kutokana na hali yake ya kiafya kua mbaya sana hivyo alikubali na kumwacha mumewe akiondoka

    *****

    Ndani ya Ofisi ya IGP Suca utulivu ulitawala, Kelele pekee zilizokuwa zikisikika ni za Feni tu iliyokuwa ikizunguka taratibu! Tayari Inpekta Kenjah alikuwa ameshawasili na kumkuta IGP ambaye baada ya Salamu zao za kijeshi walianza mazungumzo ambapo IGP alimtaka kwanza Leonard Kenjah kumpa taarifa nzima ya mwenendo kesi ile anayoipeleleza;

    Kenjah alieleza kwa kirefu na kwa ufasaha wa hali ya juu kwa kadri anavyoielewa kesi ile mpaka hisia zake juu ya baadhi ya maofisa wa jeshi la PolisiCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa nisikilize kijana wangu,” Aliongea IGP kwa utulivu sana baada ya Kenjah kumaliza kuwasilisha.. Akaitengeneza vizuri miwani yake usoni kisha akaendelea “..Kwanza hongera kwa hatua nzuri uliyofikia na moyo wako wa kujituma katika kulilinda taifa lako ila ujue kuwa hiyo kesi ni ngumu sana, ngumu kuliko ugumu wenyewe! Ngumu kuliko mnavyoichukulia! ninyi mnadhani mnapeleleza kwa Siri kumbe kuna watu wako Pembeni wanawafuatilia kwa kila nukta bila ya ninyi kugundua.. Msipokua makini mtajikuta mnavikwa taji la miba badala ya lile la maua..” IGP akatulia kidogo na kuendelea “Kuna vita ya kisiasa inaendelea Nchini kwetu, kambi kadhaa za wasaka uraisi zimeshajidhihirishwa waziwazi huku kila kambi ikiwa imejipanga vilivyo ima kwa kuuwa ama kuteketeza.. Kifo cha yule mwandishi wa habari ni matokeo ya minyukano hiyo baada ya Mwandishi huyo kukwaruzana na hao wenzie na kuamuwa kutoa siri zao.. Najua utajiuliza maswali mengi sana lakini nitakuelewesha yaliyo muhimu tu kwako kwa sasa” IGP Alituliza macho yake yaliyokua yamejificha ndani ya miwani yake kabla ya kuendelea tena

    “..Kuna kesi kadhaa kuhusu mchezo wanaofanyiwa baadhi ya watu kupitia simu zao, wanaonekana kutuma meseji kwa jamaa zao huku ukweli wakiwa hawajatuma wao.. Ndoa zimevunjika kwa mchezo huo, watu wameuawa na wengine kufungwa kwa ushahidi wa Meseji ambazo hawakuziandika, sasa hiyo ni moja ya kazi za moja ya kambi kubwa ya wasaka uraisi iitwayo ‘Black Scopion’ Hawa huzitengeneza meseji hizi kwa hila za kimtandao kupitia katika mtambo wao maalum uitwao ‘DIVIER’ na kisha kuzituma kwa mtu wamtakaye lakini huko watakapozituma wanaamua wao zioneshe zimetoka kwa nani.. bila shaka umepata kusikia hiyo kesi!!”

    “Naam,” alijibu Kenjah huku akitikisa kichwa chake chini juu kuashiria kuafikiana na hicho anachoelezwa

    “..Sasa basi hicho ndicho kinachofanywa halafu huyo Mwandishi aliyeuawa akawa anatumika kuwachafua baadhi ya viongozi huku akijivunia meseji hizo za kisanii kama ushahidi endapo atakaemchafua atahitaji kwenda Mahakamani.. na watu wengi walikua wakiogopa kumshitaki kwakuwa walijuwa kuwa kuna meseji zao zimekua zikionekana katika simu za watu wao ijapokuwa hawakuzituma wao.. Kambi hiyo ya Black Scopion inayojihusisha na Mchezo huo mchafu inaongozwa na Joram Ndege ambae anajipambanua kua ni raia wa Kenya huku ukweli wa mambo yeye ni Raia wa Uganda.. Sasa kilichotokea ni kwamba kwakua huyo Msigwa alikuwa akiwatumikia vilivyo hao Black Scopion ikafika siku naye aliwataka wamsaidie kutuma meseji hizo kwenye simu ya mkewe huku zikionesha kua zimetoka kwa Yule kijana waliemsingizia kua ana mahusiano nae, Lengo likiwa ni kutafuta sababu ya kuachana na mkewe huyo kwakuwa inasemekana hazai.. na muda huo akawa ana mpango wa kumuoa mfanyakazi mwenzie aitwae Lilian ambae pia ni ‘Secretary’ wa Boss wake japo alikuwa akikumbana na upinzani mkali kwa mfanyakazi mwenzie aliyesemekana kua naye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na huyo Lilian..”

    Insp Kenjah alikuwa ametulia kwa umakini mkubwa akisikiliza kesi ile ngumu kuliko.. alijilaumu kujitwisha mzigo wa kesi ile lakini hakua na jinsi ya kujitua tena..

    “..Alifanikwa zoezi lile marehemu Msigwa japo walikosea kidogo katika utekelezaji ambapo walituma meseji zile huku simu ya Yule mkewe ikiwa Morogoro, aliisahau kwa kaka yake alipokwenda kumjulia hali.. na hapo ndipo tuliposhangaa na kuanza upelelezi wa kina ambapo tukabaini mambo mengi sana. nakushirikisha haya ukiwa ni mtumishi muaminifu” IGP alikuwa akiongea kwa umakini sana kama ilivyo kawaida yake huku Kenjah naye akimsikiliza kwa umakini vilevile

    “Mgogoro kati ya Msigwa na hao Black Scopion uliibuka baada ya Msigwa kutaka tena kutumia mtambo wa Divier kutuma meseji za uchonganishi kwenye namba za mke na wazazi wa huyo mfanyabiashara mnaemshikilia.. anaitwa nani vile?”

    “Suhail Kusekwa”

    “..Yeah, huyohuyo.. nasikia walikuwa ni marafiki wakubwa sana kabla ya kukwazana na kua maadui huku sababu za kimapenzi zikionekana dhahiri.. Sasa Joram Ndege akamkataza Msigwa kuutumia mtambo ule kwa migogoro yake binafsi.. Msigwa akachukia kukatazwa japokuwa anajua kabisa kuwa Mtambo ule ni kwa kazi maalum tu! Hapo sasa nd’o akatishia sasa kutoa siri, ikabidi wamtulize kwa kumkubalia Ombi lake hilo huku nao wakimtaka atekeleze moja ya mpango wao wa kumchafua mmoja wa mahasimu wao kisiasa. Kilichotokea Msigwa akamchafua huyo Suhail kabla ya kumchafua mtu aliye elekezwa, matokeo yake akafukuzwa kazi hivyo kushindwa kutekeleza makubaliana yao akiwa pale Gazetini.. sasa hakuwa na sababu tena ya kuendelea kuishi kwa usalama wa kambi ya ‘Black Scopion’ ndipo ukapangwa mpango kabambe wa mummaliza na ilikusudiwa ifanyike katika mazingira ambayo atakuwepo yeye na Suhail ili kesi iwe ya Suhail huku wao wapate kujifichia katika hicho’kichaka’..” IGP akavua miwani yake na kuiweka juu ya meza, akapikicha macho yake halafu akaifumbata mikono yake kifuani, akawa anajizungusha katika kiti chake huku akimuangalia usoni Inspekta Kenjah kwa utulivu

    “Nakuelewa Afande,” Kenjah alijibu kabla hajaulizwa kitu, alijishitukia kuona amekaa kimya muda mrefu bila ya kuchangialolote



    “Nataka unielewe kweli si maskhara.. Mtambo huo wa Divier mbali ya kubumba meseji hizo haram pia unaweza kunyaka mawasiliano ya simu hizi za kawaida.. na ndio maana hata upelelezi wako wote unaojidanganya kuwa ni wa siri wenzio wanaoupata kwa kila hatua.. hivyo kuanzia sasa nitakupa simu tatu zenye namba maalum ambazo utazitumia wewe na vijana wawili tu katika kuwasiliana muda wote wa kuipeleleza kesi hii! kila hatua utakuwa ukiwasiliana na mimi kwa namba yangu ya siri kama hiyo nitakayokupa.. haupaswi kumpa mtu yoyote namba hizo.. Mpelelezi wetu aliyezikusanya habari zote hizi amemaliza kazi yake mpaka hapo alipofikia, mazingira hayamruhusu tena kuipeleleza kesi hii hivyo sasa Joho hilo unalivaa wewe.. tunahitaji kujua ni wapi ulipo huo mtambo wao wa Divier, tunahitaji kujua ni Mwanasiasa yupi aliewaleta na kuwafadhili wauaji na wadanganyifu wote walio ndani ya Kambi hiyo inayojiita Black Scopion maana mpaka sasa hatujajua ni kambi ipi kati ya hawa Wasaka uraisi inayohusika moja kwa moja, tunahitaki kumkamata Joram Ndege akiwa hai au ikibidi akiwa maiti kabla hajaendelea kuteketeza Raia wetu, tunahitaji kujua Yule Binti aliyetekwa..Lillian amepelekwa wapi?, pia hakikisha Yule kijana Mhariri aliepigwa Risasi anakuwa salama ili huenda akatusaidia upelelezi wetu kwa namna moja ama nyingine maana bila shaka sasa hivi wanamwinda wammalizie.. na kuhusu huyo Suhail hatuna umuhimu nae sana japo si vibaya kama utaendelea kumchunguza kujua alikuwa akigombea nini hasa na Msigwa mpaka akatuma zile meseji kwa watu wake..” Baada ya hapo IGP akavuta droo ya meza yake, akatoa Simu tatu na kuzikabidhi kwa Inspekta Kenjah

    “Moja ya kwako, hizo mbili za utakaoshirikiana nao.. Je utahitaji nikupatie na utakaokuwa ukitumia nao hizo simu”

    “Ninae mmoja Afande, anafaa sana, Ni Koplo Malando.. nitaomba mmoja unipatie wewe,” Aliongea kwa Kujiamini Insp Kenjah huku lengo lake likiwa lina maana kubwa kwamba ni lazima mpelelezi mmoja atoke kwa IGP kwakuwa ni lazima atakuwa na uwelewa mkubwa wa kesi hii hivyo kumrahisishia yeye kupata ‘Data’ zote lakini pia alichokuwa amekilengea ni endapo Mpango uta’fail’ basi n huyo mmoja ambaye ni chaguo la IGP naye atakuwemo hivyo kuzidhibiti hasira za Bosi wao huyo. IGP hakubisha, akakubali ombi lile na kumtoa mmoja wa Wapelelezi waliopo pale Ofisini kwake ili kushirikiana na akina Kenja katika sarakasi zile walizokua wakizianza, aliitwa Sajenti Malumbo.

    *****

    Suhail alipotoka pale Hospitalini akaamua sasa kurejea kituoni ambako kupitia Pete yake aliwaona wazazi wake wakiwa ‘Nyuma ya Nondo’

    Akaondoka kwa kasi ileile ya ajabu mpaka Kituoni Kijitonyama, Alipofika akaingilia kwa nyuma ya Jengo lile la Polisi, akakata kona ya kulia na kutokezea mbele ya Kaunta ya kituo hicho.. hakutaka kushangaa akihofia kuonekana kabla yeye mwenyewe hajajikabidhi, akaenda mpaka ndani ambapo akapitiliza mpaka kule zilipo ofisi za wapelelezi, akagonga mlango kisha baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti ikimtaka aingie ndani.. alipoingia tu akakutana uso kwa uso na Koplo Salum ambaye alishituka mithili ya aliyeona mzimu lakini akajikaza kiaskariCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Suhail..” aliita kwa wahka Koplo Malando

    “Yes Afande”

    “Ulikua wapi muda wote.. tangu ulipotoka?”

    “Nilikua hapo nje Afande.. Si niliwaomba jamani mningojee kidogo? Au mlidhani nitakimbia? Siwezi kufanya hivyo”

    Hali ile ilimshangaza sana Koplo Malando, ikabidi ampigie simu Insp Kenjah kumpasha habari ile, naye Inspekta hakuamini ila kwakuwa alikuwa njiani akielekea kituoni hapo akatuliza munkari na kukaza mwendo.

    Dakika Ishirini baadae ndani ya Chumba cha upelelezi walikuwamo Inpekta Kenjah, Koplo Marando na Suhail mwenyewe! mjadala ulikua mkubwa sana kuhusu mahala alikokuwa Suhail, maelezo ya Suhail hayakuwaingia akilini kabisa kuwa alitoka nje kabisa ya jengo lile,

    Alipoulizwa kama alionana na wale akina mama waliokua wameketi pale nje ya Ofisi ambao ni wazazi wake alikiri kuwaona lakini alidai aliwapita wakiwa wamejiinamia hivyo hawakumtambua,

    Alipohojiwa juu ya kilichomtoa nje kwa haraka kiasi vile, hata yeye mwenyewe hakukitambua! labda ni majini au mashetani yalimpanda kichwani.. hilo ndilo liliku jibu lake!

    Kwa Insp Kenjah hiyo haikuwa kesi sana, akamuamuru Koplo Marando awatoe wale wazee waliokuwa wakimshikia nafasi Suhail ili sasa mwenye nafasi arejeshwe ndani.. Japo kichwani mwa Insp Kenjah Suhail hakuwemo tena kwa maana ya kumuhusisha moja kwa moja na kadhia ile ya mauaji kutokana na maelezo aliyoyapata kwa IGP, na kutokana na hata Suhail mwenyewe anavyoonekana kujiamini na kujipambanua kutokuhusika kwake na Kesi ile.. alishaanza kufikiria hata kumpa dhamana lakini hakuona haja ya kumwacha harakaharaka

    Wazee wakatolewa kisha Suhail akarejeshwa ndani!

    Ilikuwa ni hali ya Sintofahamu inayoendelea kuwakumba wazee wale, walizidi tu kuchanganyikiwa maana kila muda matukio ya ajabu yalikuwa yanawadhihirikia. Kuanzia kuhusishwa na mauji kwa kijana wao Suhail, Kuugua kwa Sharifa, mara taarifa za kua Suhail ana mke mwingine tofauti na Sharifa, mara kutoroka na kurejea kwa Suhail pale kituoni.. hakika walilewa bila ya kunywa

    Wakaondoka wazee watu, safari hii hawakutaka hata kukumbushia vile vitu ambavyo Suhail mwanzo aliwataka waende navyo nyumbani.. vitu vile pamoja na Pete(Khatam Budha) viliendelea kubaki palepale kituoni.

    Bahati nzuri Kilingo nae alikuwa amewasili tena kituoni baada ya kuondoka na gari muda mrefu uliopita, aliyelekea Ofisini kwao alikohitajika kwa dharura punde baada ya kufukuzwa na Insp Kenjah, akawachukua wazee na kuianza tena safari ya kurejea Hospitalini kumwangalia Mgonjwa wao waliemuacha akiwa kitandani

    *****

    Mawindo yakaendelea..

    Mzee Sufian anamwinda Komando Takadir wakati nae(Takadiri) anawawinda Mzee Sufian, Suhail, na Shekhia huku akiwa amedhamiria kupambana na kila mmoja kwa mtindo wake tofauti.. wakati huo Silaha hatari ya Khatam Budha ikiwa Kituoni Polisi..

    Muda huohuo Joram Ndege(Meno ya Dhahabu) naye anawawinda wabaya wake ambao kwa namna moja ama nyingine wanatishia usalama wa kambi yao ya Black Scopion kwa kutoa siri zao ama kwa kuwachunguza mambo yao..

    Huku nako Insp Kenjah, Koplo Marando na Sajent Bangi wakiwawinda kila watakaohisiwa kuhusika na kadhia hiyo inayoendelea, kuanzia na Joram Ndege mwenyewe, Sajent Rwehumbiza, na afande Chanzi

    Ulikuwa ni Mchezo mtamu

    *****



    Mzee Kusekwa na Fungameza wakaingia ndani ya gari wakifuatiwa na wake zao kisha safari ya kuelekea hospitali ikaanza huku Kilingo Mkude akiwa nyuma ya usukuni. Safari ilielemewa na foleni ndefu ya magari iliyotanda barabarani lakini mpaka wanaingia Hospitalini hakuna aliyegundua kuwa kulikuwa na foleni kubwa kutokana na mlundikano wa mawazo vichwani mwao. Wakateremka garini baada ya kuegesha katika eneo maalum hapo hospitalini kisha wakaongozana mpaka Wodini.

    Ule mfadhaiko uliomkumba Suhail baada ya kumwona mkewe Sharifa akiwa mzima kabisa sasa ulihamia kwa wazee hawa pamoja na Kilingo, hakuna aliyeamini utendaji kazi wa macho yake pindi walipomwona Sharifa akiwa Bukheri wa Afya ndani ya wodi.. ilikuwa ni furaha na hofu vilivyowakumba kwa wakati mmoja maana mgonjwa mliyemwacha akiwa taabani kumkuta katika hali ile ilikuwa si jambo dogo japo hilo halikuwafanya wamkimbie au wamwogope mtoto wao bali lilizidi kuwapa hamasa ya kumsogelea kwa kasi wakistaajabishwa na hali ile.

    Baada ya kuketi, hawakupata muda wa kusalimiana, ikawa ni maswali juu ya maswali.. Sharifa akaanza kuwaelezea mkasa mzima ulivyokuwa, ilikuwa ni mkasa wa ajabu na vioja! Mkasa uliowastaajabisha wote mle Wodini

    Hali ya mshangao ikazidi pale Sharifa alipowaeleza kuwa Suhail aliwasili Hospitalini pale muda uliopita na ameahidi kurejea tena baadaye

    “Unasema?! Suhail alikuwa hapa?” Aliuliza kwa mshangao Mama Suhail, na si yeye tu pekee aliyekumbwa na mshangao huo bali wote walibutwaika! kila walipojaribu kuyapanga matukio hayakuwaingia akilini, kubwa zaidi ni muda ambao Suhail alitoweka na kurejea kule kituoni usingetosha kwake kuja mpaka huku Hospitali na kurejea tena, na hata kama angeweza kwanini afanye vile hasa? Hakuna mwenye majibu!

    “Ndiyo alikuwa hapa na nimekaa naye sana hapa”

    “Ama!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mbona siwaelewi kwani kuna nini kinachoendelea?” Hatimaye Sharifa aliingiwa na hofu kufuatia hali wanayoonekana nayo wazazi wake ikabidi sasa awasaili kwa umakini zaidi, Wakajaribu kumlaghai kwa kuuficha ukweli lakini nyuso zao zilizotahayari zilionesha dhahir bin Shahir kuwa hali haikuwa shwari hata chembe.. Sharifa alilisoma hilo ndipo akawakazania wamweleze tu kila kitu bila kumficha, hatimae Mzee Fungameza akampasulia jipu ‘Pwaa!’



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog