Search This Blog

VITA VYA MAPENZI - 5

 







    Simulizi : Vita Vya Mapenzi

    Sehemu Ya Tano (5)





    Akamweleza kila kitu nukta kwa nukta jinsi mkasa mzima ulivyokuwa mpaka kuhisishwa kwa mumewe katika saga lile la mauaji ya Mwandishi wa habariCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Suhail ameuwa? NOO! Haiwezekani..” aliongea kwa kasi mpaka akapaliwa na mate, akashusha pumzi na kuzipandisha tena kama mzani, Akaendelea “..Mbona amekuja hapa hana dalili yoyote ya kukabiliwa na kesi?.. Mmesema yuko wapi kwa sasa?”

    “Tumemwacha Polisi kwa sasa, ila hakuna haja ya kupaniki Mama yangu maana suala lake linashughulikiwa vizuri tu” alijibu Mama Sharifa

    “Hapana mama, hapa kuna jambo tu si bure!.. Wamekuwa wakimfutafuta sana itakuwa wamembambikia kesi tu” Kikapita kimya cha muda kidogo kila mmoja akiwa amezama katika tafakuri kivyake, ndipo tena Sharifa akaibuka na swala jingine lililozuwa mjadala mpya

    “Ni huyo aliyeuawa ni nani? Mmeshamjuwa?”

    “Aliyeuawa ni yule mwandishi wa habari aliyemchafua kwenye magazeti… Msigwa,” Alijibu Kilingo Mkude

    “NANI? Umesema?!..” Sharifa alizidi kuchanganyikiwa maana alimjua vyema Msigwa na alikuwa akijuwa kila kinachoendelea baina yao, na japo aliondokea kumchukia sana kijana yule lakini kwa hili la kuuawa lilimshituwa sana ukizingatia anayehusishwa kuuwa ni mumewe kipenzi, jasho lilimtoka “Msigwa ameuawa? Oooh.. Mungu wangu!” Sharifa aliendelea kuuliza huku macho yakimtembea huku na kule kama saa mbovu!

    Huku nako Mzee Kusekwa aliposikia jina la Msigwa hapohapo Kengere ya hatari ikagonga kichwani mwake, alilikumbuka vizuri jina hilo na punde taswira ya kijana Msigwa akimdhihirikia, akashindwa kujizuwia akaropokaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mmesema nani, Msigwa?.. Msigwa ameuawa? Sitaki kuamini..”

    “Kwani mnamjuwa huyo Msigwa?” Aliuliza kwa hofu Mzee Fungameza lakini hakujibiwa zaidi ya kuishia kuwasikia wenzie wakilalama tu, Mama Suhail naye akamkumbuka kijana yule waliyemlea kwa upendo kipindi kile akiwa Shule ya Sekondari Milambo mkoani Tabora, Walimtambuwa Msigwa kuwa ni rafiki kipenzi wa Suhail tangu walipokuwa shule na hata baada ya kuhitimu sasa iweje tena Suhail amwue mwenzie? Habari zile za magazetini walizisoma lakini hawakujua kua ni Msigwa aliyekua akiziandika kumchafua Suhail japo walitambua kuwa kwa sasa Msigwa ni Mwandishi wa habari

    “Kumbe Msigwa ndiye aliyekuwa akimchafuwa Suhail magazetini! Kwanini hasa?” Mzee Kusekwa alijiuliza mwenyewe kwa Sauti! Hakika ilikuwa ni habari mpya na mbaya kwao. Mzee Kusekwa akamgeukia Mzee Fungameza na kuanza kumpa historia ya Suhail na Msigwa tangu walipokuwa shuleni, ilikuwa ni historia yenye kumbukumbu tamu iliyoingiwa na shubiri. Baada ya majadiliano yahapa na pale Mzee Kusekwa akamuuliza Kilingo kama itawezekana waende kwa Msigwa ambapo bila shaka wataonana na wazazi wa marehemu ambao yeye alikuwa akiwasiliana nao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kutumiana zawadi tangu walipounganishwa na urafiki wa vijana wao

    “Walikuja hao wazazi wake, lakini tayari wameshachukua maiti na kwenda kuzika kwao huko Iringa” Jibu la Kilingo likakata hamu ya Mzee Kusekwa

    “Kama umesema una mawasiliano nao hebu wapigie simu labda utawapata,” alipendekeza Mama Sharifa lakini simu ilipopigwa majibu ni kuwa haikuwa ikipatikana.. wakatazamana!

    Mjadala ukaanza upya mle Wodini kuhusu mtungo wa matatizo yanayoendelea, hapakuwa na suluhu la matatizo hayo zaidi ya kila mmoja kutoa mawazo yanaoonekana kuchagizwa na Mchoko wa akili, Ndipo Mzee Fungameza akatoa rai kuwa waree kwanza nyumbani wakapumzike ili wavute akili mpya, wakaafikiana! Sharifa naye akagoma tena kuendelea kubaki pale Hospitalini.. Wakaondoka naye mpaka Ilala, nyumbani kwa Suhail na Sharifa

    *****

    Huko Kituo cha Polisi nako Inspekta Kenjah alikuwa amezungukwa na vijana wake wa kazi akiwapa mpango mkakati wa kukabiliana na kesi iliyo mbele yao ambapo alipanga vikosi kazi; Cha kwanza kikapangiwa kuweka ulinzi kule Hopitalini alipolazwa yule Mhariri aliyepigwa Risasi, kikosi hiki kilikuwa chini ya Koplo Marando. Cha pili kikapangiwa kuzifuatilia zile gari zinazotumiwa na akina ‘Meno ya dhahabu’ ili wafahamike nyenendo zao, kikosi hiki kikawa chini ya Sajent Malumbo. Na kikosi cha mwisho kilikuwa ni kikosi maalum kinachozuru eneo lolote muda wowote, hiki kilikuwa chini ya Inpektah Kenjah.

    Baada ya kuhakikisha wamejipanga vya kutosha wakaahidiana kuwa wakapumzike maana usiku ulikwishaingia, ili kesho yake ndipo kazi ianze!

    *****

    Giza likatanda na kufunika anga, Usiku ukaingia!

    Kila mmoja alikuwa nyumbani kwake amepumzika, lakini si kwa Mzee Sufian Bin Shamhurish wala Komando Takadir Al-harabi ambao wao walikuwa wakiendelea kuwindana kwa ustadi wa hali ya juu lakini hakuna aliyefanikiwa kumnasa mwenzie.

    Wakiwa katika hali hiyo ndipo tena Miale ya Pete(Khatam Budha) ikamjia waziwazi Komando Takadir Al-harabi, akaachana na kumwinda hasimu wake na sasa akaanza kuifuta miale ile, ilikuwa ikitokea kulekule katika kituo cha Polisi.. Akaifuata mpaka kituoni,

    Alipofika pale Kituoni kwa kutumia uwezo wake wa kijini akamwona sasa Suhail akiwa amejilaza ndani kabisa ya Selo, akajibadili kidogo tu kisha akaingia mpaka pale Kaunta, akawapita wale Askari wakiwa na majukumu yao bila ya wao kumwona akaingia mpaka kule alipolala Suhail.. alipoingia tu akajirejesha katika lile umbile lake la mwanzo kabisa ambalo Suhail alipata kuliona walipokuwa wakipambana kule Yemeni..

    Ghafla Suhail akashituka kutoka usingizini na kukutana uso kwa macho na Komandoo Takadir, Suhail akahamanika maana haraka alimng’amua Komando yule.. Jicho likamtoka kama Sorokoto kabanwa na mlango.. akataka kupiga kelele lakini kabla hajafanya hivyo Takadir akamuwahi kumsemesha

    “Bwana Suhail, usithubutu kufanya ujanja wowote ule nitakuangamiza hata maiti yako isionekane..” Komando Takadir alikuwa akiongea Kiswahili fasaha kama Mkwere wa Bagamoyo, Suhail akasimama na kurudi nyuma ili awe mbali na Takadiri lakini haikufaa kitu maana ukuta ulimpokea na kumzuwia.. Takadir akamsogelea mpaka karibu yake ksha akaendelea

    “..Leo nitaondoka na kimoja kati ya viwili au ikibidi vyote.. kama si Pete(Khatam Budha) basi roho yako! naomba uchaguwe moja”

    “Wewe ni nani, Na unataka Pete gani? Mbona sikumbuki kupewa pete na wewe!” Suhail alijibu huku Mdomo ukimtetemeka kama mtoto aliyekamatwa akilamba sukari, Jibu hilo lilitosha kuzichokoza hasira za Takadiri, Kelbu moja alilotandikwa Suhail lilimrusha mithili ya mtu aliyepigwa shoti ya umeme, kabla hajapumua akafuatwa tena akapigigwa ngumi kama kumi mfululizo mpaka akawa anaona nyotanyota tu, kisha akainuliwa akiwa anatweta.. Miale ya Pete ilikuwa ikionesha kuwa iko maeneo hayohayo lakini Takadir hakuiona, akamwangalia Suhail kidoleni hakuona kitu

    Kaiweka wapi Pete huyu? Alijiuliza Takadir! hakupata majibu.

    “Utanionesha Pete au hautanionesha?”

    “Mimi sina Pete utaniuwa bure kaka” Hapohapo akapokea kichapo kingine cha haja mpaka akatapakaa damu mwili mzima.. Suhail akawa hatamaniki! Sasa maumivu yakamtia ujasiri wa ajabu akajikuta anainuka kwa hasira na kumrukia Tajadir ili amshambulie lakini ilikuwa ni sawa na ‘Kukitoa kinu juani’ hakitanenepa wala kukushukuru, na hata ungekiacha juani kisingeungua.. Kazi bure! Akapokea kichapa kingine cha nguvu mpaka akaishiwa nguvu akaanza kupiga kelele sasa! Kelele hizo zilikuwa ni za maumivu yaliyochanganyika na kukata tamaa! Cha ajabu hekaheka zote hizo hazikumuamsha mtu yoyote mle ndani ya Selo wala hazikusikika kwa maaskari wa zamu usiku ule..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Komandoo Takadir akaendelea kumtesa sana Suhail ili aoneshe Pete ilipo.. Lakini ghafla katika hali ambayo hata Takadir hakuitegemea Suhail akatoa ukulele wa nguvu ukawafikia mpaka wale maaskari kule Kaunta.. kwa kasi na haraka Maaskari wakaukimbilia mlango na kuufungua.. kabla hawajafika ndani tayari Takadir alishafanya tukio jingine baya, alimpiga Suhail na miale kutoka katika macho yake, miale yenye nguvu kama umeme! Suhail hakuelewa kilichotokea zaidi ya kuhisi akirushwa na kitu kama Shoti ya umeme kilichombwaga chini na kumwacha akiwa hana fahamu!

    Askari walipoingia ndani walishangazwa na hali ile ya ajabu, walimkuta Suhail akiwa ametapakaa damu lakini akiwa hana jeraha hata moja.. wakajaribu kumuinua ndipo wakagundua kuwa amepoteza fahamu haraka wakamtoa nje ili kumpatia huduma ya kwanza.. mpaka kufikia hatua hiyo hapakuwa na mahabusu hata mmoja aliyeshituka kutoka usingizini

    “Humu kuna jambo limefanyika!” Aliongea Askari mmoja aliyekuwa akimpepea Suhail

    “Bila shaka!.. haiwezekani mtu aumizwe halafu wenzie wawe wamelala tu”

    “Kwani huyu kijana ana kesi gani humu?” Aliuliza tena Yule Askari anaempepea Suhail

    “Kwani we hujamjua huyo? Huyo nd’o ukisikia Suhail Yule tajiri anaehusishwa na mauaji ya Msigwa.. Tena ngoja nimpigie simu Insp Kenja ndiye anayeshughulikia kesi yao” Baada ya majadiliano ya hapa na pale akapigiwa simu Insp Leonard Kenjah, akaahidi kuwasili kituoni muda si mrefu sana!

    Alipofika akamkuta Suhail ameshazinduka lakini hali yake si nzuri, anaonekana kupewa matesomakali sana lakini hakuwa na jeraha hata moja mwilini

    “Suhail,” Aliita Kenjah huku akimshika kichwa Suhail

    “Afande,” Aliitika kwa sauti hafifu iliyobeba maumivu makali

    “Imekuwaje tena hivi,” Alisaili Insp Kenjah.. ikamchukuwa Suhail muda mrefu sana kabla hajaanza kuwaelezea juu ya mtu aliyemtokea ghafla na kumwadhibu vilivyo.. ilikuwa ni kama simulizi za watoto vile maana hakuna hata mmoja aliyeielewa.. kuamini kuwa kuna mtu aliingia na kumtesa vile bila sababu halafu ukizingatia mlango ulikuwa umefungwa ilikuwa ni Ndoto.. kibaya zaidi hata Mahabusu wenzie hawakusikia chochote. Inspekta akaagiza Daktari aitwe kuchunguza hali ya Suhail, na hata alipowasili daktari na kufanya uchunguzi wake majibu yalikuwa ni ya kushangaza sana! Suhail hakukutwa na tatizo lolote!



    Mapambazuko, siku mpya ikaanza! Habari zilizotawala kituoni ni tukio la jana yake usiku dhidi ya Suhail!

    Insp Kenjah alikuwa ofisini kwake akisubiri taarifa kutoka katika vikosi vyake ambavyo vilikuwa tayari katika majukumu yao, Muda huo familia nzima ya Suhail iliwasili kituoni kuendeleza jitihada zao za kumwekea dhamana kijana wao! Safari hii zoezi halikuwa gumu kwani Insp hakuona sababu ya kuendelea kukaa na mtu asiyeonesha dalili ya kuhusika na mauaji yale ukizingatia na hekaheka ya jana yake usiku akaona asije kuwafia mikononi mwao, Akampa dhamana!

    Hali ya Suhail iliwashangaza sana wazazi wake, Mkewe na hata wafanyakazi wake kwa jinsi alivyodhoofika! Wote wakaamini kuwa aliteswa sana na askari licha ya yeye mwenyewe kukana hilo.. walidhani pengine amekatazwa kusema ukweli! Baada ya kupewa dhamana na kufanya makabidhiano ya vitu vyake ikiwemo Pete(Khatam Budha) Wakamchukuwa mpaka nyumbani ambapo aliwaeleza kisa kizima cha kutokewa na Yule mtu! japo alificha kumfahamu, ilikuwa ni kisa kilichozidisha Hofu na mashaka! Sharifa amepona kimiujiza na Sasa Suhail anaumwa kimazingaombwe, Kazi ipo!

    Japo aliivaa Pete yake lakini haikumfanya Apone, hali yake ilikuwa mbaya tu japokuwa kidogo aliingiwa na nguvu mwilini.

    *****

    Simu ya Insp Kenjah iliita, akaitoa na Kuiangalia kabla hajaipokea.

    “Hallow”

    “Yes Boss.. Tuko Ilala Boma nje ya Hotel ya Shree Godha, tunamwona Joram Ndege anaingia ndani ya ile gari tuliyokuwa tukiishuku.. na sasa natafuta mwelekeo wa kutoka barabarani.. amevaa suti nyeusi na mkononi ana brifkesi” Ilikuwa ni sauti ya Sajent malumbo akitoa taarifa

    “Good news, Endeleeni kumfuatilia kwa uangalifu mkubwa.. akigundua tu kuwa anafuatiliwa mjuwe kesho tutayapigia mizinga majeneza yenu kabla ya kwenda kuwazika, Ni mtu hatari huyo..”

    “Ok Boss” Simu ikakatwa.. Damu ikamchemka sasa Insp Kenjah akainuka na kuketi tena asijielewe anataka kufanya nini.. Dakika chache akapokea tena simu

    “Ongea Sajenti,” Alinguruma Insp

    “Ameshika barabara ya Uhuru, anaelekea Buguruni.. ndani ya gari wako wawili tu yeye na dereva wake,”

    “Nimekupata.. kama nilivyokueleza,” Alijibu Kenjah na kukata simu kisha akampigia Koplo Malando

    “Nipe habari za hospitali”

    “Kila kitu kinaendelea vizuri Afande, hakuna mpya!” Simu ikakatwa. Insp akarejea kuketi

    Dakika kama arobaini baadeye Insp akapokea tena simu ya Sajini Malumbo “Tuko Banana, Gongo la Mboto. Kwenye hii barabara inayochepuka kwenda kitunda mkono wa kushoto kuna Jengo moja kubwa la ghorofa moja limepakwa rangi ya njano kwa mbele ndipo gari ya akina Joram Ndege imeegeshwa.. na sasa namwona anateremka na kuanza kuelekea ndani”

    “Kuna gari yoyote nyingine imeegeshwa hapo?”

    “Ndiyo, zipo kama tatu hivi kuna Landcruiser G8, Prado, na Rangerover”

    “Nakili namba za gari hizo haraka kisha nitumie kwa meseji.. usifanye mchezo wowote wa kitoto! Subiri hapohapo mpaka atakapotoka halafu uhakikishe unawaona watakaoingia ndani ya hizo gari zingine na ukishawaona jitahidi unijuze ni akina nani hao kabla hawajakuuawa, Sawa?” Ilikuwa ni ishara tosha kwa Sajent Malumbo kuwa akicheza tu atauawa na si vinginevyo!

    “Sawa Boss” Simu ikakatwaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****

    Nyumbani kwa Suhail aliwasili Dokta wake na kuanza kumpa matibabu japo naye hakuuona ugonjwa wala athari ya mtu aliyeteswa.. Mzee Fungameza kwakuwa ni Muumini mzuri wa dini ya kikristo ambaye pia ni Mzee wa kanisa huko kanisani kwao Tabora akaanza kuporomosha maombi huku akisaidiwa na mkewe, Mzee Kusekwa naye kwa imani ya Dini yake ya Kiislam akawa anafanya dua kwa mwanaye.. Badala ya kuimarika hali ikazidi kuwa mbaya

    Sharifa yeye hakukaukiwa machozi mashavuni mwake!

    *****

    Joram Ndege aliposhuka aliingia ndani ya Jengo lile na kupotelea kwenye Korido moja ndefu iliyosheheni vyumba vingi kulia na kushoto, kila chumba kikiwa na watumishi wakiendelea na majukumu yao taofautitofauti.. Korido ile ilimchukuwa moja kwa moja mpaka katika chumba kimoja kilicho kwenye kona, alipofika hakugonga mlango wala kubonyeza kitufe chochote Mlango ukafunguka wenyewe, bila shaka alikuwa akionekana kwenye camera maalum

    Alipoingia akapokelewa na sura za vigogo na waheshimiwa kadhaa wakiwa na sura zilizomakinika hasa na jambo Fulani, akaketi bila ya kusalimia

    “Nadhani tumekamilika?” Alifanya tashtiti Bwana Ibrahim Basha Bin Mende ambaye alikuwa ameketi katikati ya jopo lile haram akiwa kama mwenyekiti wao, Jina lake halisi ni Ibrahim Basha hilo la bin Mende alibandikwa tu kutokana na tabia zinazosemwa kuwa alipata kuwa nazo.. ni tabia chafu japo mwenyewe amekuwa akijitetea kuwa ni wabaya wake kisiasa nd’o wanamchafua.. Yeye ni mtu mwenye ushawishi mkubwa sana ndani na nje ya serikali. Upande wke wa kulia waliketi watu watano;

    Mhe Hamid Humud(Naibu waziri wa nishati na madini), Mhe Abdiroush Warriya(Naibu Waziri wa fedha), Bwana Moris Kungurume(Mfanyabiashara wa madini), na Bwana Charles Bikoraimana(Mfanyabiashara wa masuala ya usafiri wa majini). Upande wa kushoto Pia kulikuwa na vibopa watano; Kamanda Katinda Kuya(Mkuu wa polisi kanda maalum), Joram Ndege(Muuwaji wa kutumainiwa), Bi Kapemba Kitivo(Mkuu wa mkoa wa Musoma), John Patrick Massawe(Kiongozi wa chama cha upinzani), Msimbe Abrahams(Mbunge wa mkoa wa Manyara) na Adams Gosh(Muwakilishi wan chi ya Ugiriki ambayo ndiyo unaofadhili mpango ule). Baada ya kufunguliwa kikao kile aliendelea kuongea Mwenyekiti Ibrahim Basha Bin Mende

    “Mnaweza kushangaa Mhe 5051-10s na Mhe 42&2c hawajawasili.. imebidi tuwazuie kufika huku mara kwa mara maana kufuatia hili vuguvugu linaloendelea bila shaka watakuwa katika uangalizi mkali wa wana usalama hivyo si vyema kuwaalika huku kwa sasa.. ila wao kama Raisi wetu mtarajiwa na waziri mkuu wake watakuwa wakipewa taarifa za kila kinachoendelea kupitia mitandao yetu ya siri..” Akasita kidogo na kuwatulizia macho vigoo walio mbele yake kisha akaendelea ”Kifo cha Yule Mshenzi Msigwa kimesababisha baadhi ya mambo yetu kusita kwa muda maana kuna uchunguzi mkali wa chini kwa chini unaendeshwa na Inpekta Leonard Kenja pamoja na vijana wake.. nimekuwa nikiyapata mawasiliano yake kwa kina kupitia mtambo wetu wa Divier japo upelelezi wao unaonesha kutogundua lolote kuhusu sisi ila kuna dalili zote kuwa maji yanaweza kuzidi unga muda wowote”

    “Kivipi?” Alisaili kwa wahka Mhe Mlenda

    “Kuna tetesi kuwa IGP Succa amekuwa akimdodosa sana Mhe 5051 kuhusu haya matukio ya watu kuonekana wametma meseji sehemu waklati hawakufanya hivyo.. cha kujiuliza kwanini ang’ang’anie kumuuliza yeye wakti kuna wahusika wa masuala ya mawasiliano? Pia kuna habari za kutekwa kwa Yule Sekretari wa kule alipokuwa akifayia kazi Msigwa.. inasemekana Msigwa alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi ama ndo alikuwa katika mchakato huo na Yule binti hivyo inawezekana amemwambia mengi kuhusiana na sisi kabla ya kuuawa kwake lakini cha ajabu binti Yule ametekwa na sisi hatukuhusika na tukio lilesasa bila shaka ni mbinu tu imetumika na maadui zetu kumtowesha ili awape chochote akijuacho kutoka kwa Msigwa..Sasa tulichoamua ni kuwamaliza wote wanaoonesh dalili ya kutaka kung’amua chochote katika mpango wetu huu..”

    Akatulia tena kidogo kuruhusu maneno yake yaingie vichwani mwa wana mkakati kisha akaendelea “ Kwanza kabisa inatakiwa tuwajue waliomteka halafu pili Yule Mhariri Bwana Bucha naye anatakiwa akamaliziwe huko hospitali maana sote tunafahamu kuwa walikuwa wakimgombania huyo Lilian hivyo kama Msigwa alivujisha habari zetu kwa mwanamke Yule bila shaka mwanamke huyo naye alivujisha kwa huyo Bucha..”

    “Kuhusu Bucha.. nitaiendea roho yake huko hosptali baada ya kikao hiki,” alidakia Joram Ndege

    “Kuhusu huyo aliyeteka baada ya kikao hiki nitaenda kwa IGP bila shaka atanitapikia ukweli wote,” akadakia Kamanda Kuya

    “Good..huko kote mimi sina shaka napo ila ninataka kukazia jambo moja tu kuwa tujiepushe na matumizi yasiyo ya lazima ya mtambo wa Divier maana nd’o umeleta yote haya.. tujaribu kuyaheshimu makubaliano yetu juu ya mtambo ule na ikiwezekana kwa kuwa si mkubwa sana hata humu uhamishwe tu maana hata siku likitokea la kutokea tusijegundulika hila zetu mapema..” aliongea kwa Utulivu Mhe Humud

    “Yeah, hilo kweli ni la msingi sana.. na kuanzia tulipomaliza kadhia ile ya Msigwa kwa sasa mtambo ule haufanyi kazi nyingine yoyote zaidi ya udukuzi wa mawasiliano.. kwa mfano kila siku kasoro juzi na jana nimekuwa nikipata habari zote za huyo Kenjah na mbwa wake..” Baada ya hapo ukafuatiwa mjadala mwingine ambapo Msemaji mkuu alikuwa Mr Adams ambaye alikuwa akawasilisha majibu ya maombi ya fedha na silaha kutoka kwa Black Scopion kwenda nchini kwaoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya nusu saa ya kikao wakapangiana majukumu kisha kikao kikaahirishwa na kila mmoja akatoka.



    Simu ya Inspekta Kenjah aliita, alikuwa Sajenti Malumbo akipiga kutoa taarifa, Kenjah alikuwa akiisubiri kwa hamu simu hiyo maana zile namba za magari alizotumiwa kwa meseji kama alivyoagiza hazikuwa na majibu ya haraka maana hazikuwa za serikali wala watu binafsi

    “Hallow.. lete habari Sajent”

    “Naona wanatoka sasa ndani”

    “Umemjuwa hata mmoja?”

    “Ndio” Sajent Malumbo aliwajua wale mawaziri, mfanyabiashara mmoja pamoja na Kamanda wa Polisi, akamwambia Inpekta

    “Hii sasa ni hatari, naomba muendelee kumfuatilia Joram Ndege. Hao wengine achaneni nao”

    “Ok Boss”

    *****



    WAKATI Inspekta Kenjah akiinua simu yake kumwarifu IGP juu ya taarifa ile ya kushitusha tayari Joram Ndege alikwishaingia ndani ya gari aliyofika nayo pale na kuanza kuondoka. Sajenti Malumbo naye kama alivyoagizwa akawa nyuma yake akimfuatilia kimyakimya huku akitoa taarifa hatua kwa hatua.

    Baada ya ghasia za foleni na shtighali za hapa na pale hatimaye msafara ulikomea nje ya hospitali ya taifa Muhimbili, Joram Ndege alitoa mguu mmoja baada ya mwingine ndani ya gari ikifuatiwa na kiwiliwili chake kilichojazia misuli minene, huku nako nako Sajenti Malumbo akitoa simu yake maalum na kumpigia Inspekta Kenjah

    “Bila shaka sasa amedhamiria vita..” alijibu Inpekta kisha akakata simu, na kumpigia Koplo Malando aliyekuwa Doria hapo hospitalini kwa muda mrefu

    “Meno ya dhahabu ameshaingia hapo, hakikisheni haingii kwenye wodi aliyolazwa Bucha.. nami nafika hapo sasa hivi siko mbali sana,” Aliongea Inspekta

    “Nimemwona tangu anaingia.. amevaa suti nyeusi ila ameipita tu Wodi aliyomo Bucha, hapa namwona anakwenda kule Wodi za Mbele kabisa.. Namwona kuna wodi ameingia sasa hivi” Alijibu Koplo na kuendelea tena “..Kuna nesi pia namwona anaingia humohumo alimoingia Joram”

    “Huyo ni mjanja zaidi ya sungura itakuwa napoteza malengo tu.. kuweni makini sana, mfuate haraka na kwa hadhari ya hali ya juu, Kama atataka kufa kabla hajakamatwa muue tu.” Simu ikakatwa

    Haraka Koplo Malando akawahimiza vijana aliokuwa nao pale wakaweka silaha zao tayari tayari kisha yeye akajitosa.. akaenda mpaka usawa wa ile wodi alimoingia Ndege, alipofika hakupoteza muda akausukuma mlango…

    Patupu!

    Chumba kilikuwa kimya hapakuwa na mtu mwingine zaidi ya mgonjwa aliyelala kitandani akiwa amejifunika Shuka. Koplo akaanza kupepesa macho yake chumba kizima..

    Kimya!

    Akapeleka mkono wake kiunoni kuiangalia silaha yake, akaikuta ikimsubiri yeye tu, akaiacha na kuendelea kukikagua chumba. Akafungua makabati yaliyokuwamo mle ndani lakini hakukuta mtu, akachungulia chini ya uvungu wa kitanda nako Hola! Akapiga hatua kadhaa mbele na kumsogelea yule mgonjwa aliyefunikwa shuka.. hapo sasa ndipo Moyo wake ulipopiga almanusura ya kuchana kifua chake.. Hakuwa mgonjwa Kamwe!

    Ulikuwa ni mwili tu uliotengana na roho, ni mwili wa Yule nesi aliyeingia mle Wodi akifuatana na Joram Ndege! Loo salale,

    Sasa kwanini amemuua huyu dada asiye na hatia? Na amejificha wapi sasa? Alijiuliza Koplo bila majibu. Akataka kutoa simu yake ampigie Inspekta lakini akahofia kuusumbua utulivu wa chumba kile cha wagonjwa

    *****

    Askari kanzu watatu walikuwa mbele kidogo ya Wodi aliyolazwa Bucha, japo walijifanya kuwa bize na mambo yao lakini macho yakiwawaka kwa kuhakikisha usalama wa eneo lile.. walifanikiwa kuulinda usalama lakini si kuizuia shari ya Joram Ndege.

    Ndani sasa ya Wodi Bwana Kareem Bucha alikuwa amelala kitandani huku akiwa hajarejewa na fahamu, hali yake ilikua tiamajitiamaji, Mbele ya kitanda chake palikuwa na mrembo mmoja amesimama na kujaribu kumfunika vizuri mgonjwa, bila shaka mrembo alikuwa ni Nesi kwa muonekano wa mavazi yake

    Nesi huyo aliyekuwa akiendelea kumfunika na kumwangalia mgonjwa wake alikuwa akikabiliwa na hatari bila ya kujijua! Usawa wa kichwa chake kwa juu kidogo, dari ya chumba kile cha Wodi ilifunuliwa taratibu kwa kipande kidogo cha ‘Singibodi’ kuwekwa pembeni kasha mwanaume mwenye meno ya dhahabu akawa akichungulia kwa chini kama popo. Alikuwa ni Joram Ndege katika ubora wake!

    Alichokifanya ilikuwa ni mchezo mdogo tu, kumvunja shingo Yule nesi aliyejipendekeza kwake kule wodi ya mbele kisha akanyakia dari na kuanza kutembea juu kwa juu mpaka huki katika wodi aliyopo Bucha akidhamiria kushuka kuumaliza mchezo!

    Kwa mtu wa kawaida ilikuwa ni kazi ngumu kushuka tokea kule juu wakati ndani kuna mtu usiyetaka ashuhudie ukiichukua roho ya mgonjwa wake hivihivi ila si kwa Joram Ndege, angeweza hata kuzinyakua roho zao wote wawili ila tu akaamua kufanya subra mpaka nesi Yule atakapotoka, Haikuwa hivyo! Nesi hakutoka..

    Kwa joram Subra ni kitu adhim hivyo alikienzi daima! ikapita dakika ya kwanza, ya pili, ya tatu.. wakati mishale ya sekunde na dakika ikiendelea kukimbia ndani ya saa yake, Moyo nao uliendelea kukimbia ndani ya kifua chake akitambua kua muda si mrefu hospitali nzima itakuwa katika uangalizi kufuatia kifo cha yue nesi, Hakuiona tena haja ya subra ile!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akachungulia chini, akajiridhisha juu ya ukaaji wa Yule Nesi, akamalizia kuifunua vizuri sehemu ya dari iliyosalia kisha kama umeme akajitoma ndani! Lilikuwa ni tukio la ghafla ambalo kwa nesi wa kawaida angetoka mbio lakini si kwa dada Yule Mrembo mwenye umbo lililokatika mithili ya namba nane na weusi wa kung’aa watoto wa mjini huuita ‘Blaki byuti’

    Lengo la Joram sasa likabadilika toka kwenye kuchukua roho moja ya Buchan a kuwa roho mbili pamoja nay a nesi huyu!, kilichotekea Joram Ndege alibaki kinywa wazi. Alipokea mapigo ya judo mfululizo kutoka kwa Yule Nesi, dakika mbili uso wake ukawa hautamaniki! Alijaribu kujiinua kutokea kule sakafuni alikuangukia baada ya kupata dozi ya nguvu lakini kabla hajakaa sawa tayari Nesi alikwishawasili eneo lake na na kumshindilia maketeke ya mbavuni mpaka akaguna! Ilikuwa ni kimyakimya.

    Nesi naye akafanya uzembe kumwacha Joram ainuke japo alikuwa ameshalegea kwa kichapo cha nusu dakika tu, Ndipo Macho ya Joram yakakutana na Nesi Yule.. akamtambua, akaachia tabasamu ambalo lilibadilika ghafla baada ya kumwona mrembo Yule aliyevalia sare za manesi akimjia kwa kasi ya kumshambulia, akajiweka sawa na kulikwepa pigo jingine kutoka kwa dada Yule mwenye wepesi wa miguu kisha akaachia Pigo kali la ngumi lililokita katika mbavu za Nesi mpaka akatoa muungurumo mithili ya vyura wa majarubani.. Nesi akaanguka chini kama kifurushi na kabla hajatahamaki akafuatwa hapo chini na kunyanyuliwa mzobemzobe na kabla hajajua afanye nini akapokea ngumi nyingi za uso, Damu ikakutana na vipodozi alivyojiremba vikasambaa hovyohovyo usoni na kuwa mfano wa Upinde wa mvua!

    Kiza kitanda usoni mwake huku nyotanyota zikiyadhihaki macho yake!

    Bila kuchelewa Joram akamkata Ngwara Nesi yule na kumsindikiza na Teke la kichwa mpaka chini, lakini kwa wepesi wa ajabu Nesi akaruka tena juu mithili ya mtu aliyekalia kaa la moto, aliposimama tu hakutaka kufanya urafiki na muda, akaingiza mguu wake katikati ya miguu ya Joram aliyekuwa ameshitushwa na wepesi wa dada Yule na kumtandika teke kali katika Korodani zake! Yowe la uchungu likamtoka Joram. Yowe hilo ndilo lililowashitua wale maaskari waliokuwa wanaendelea na Lindo pale Hospitalini, Wakaivamia Wodi ile silaha zao zikiwa mikononi.. walipojaribu kuufungua mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, Wakauvunja!

    Walipoingia tu wakakutana na hali ile ya Sintofahamu, Wekundu wa damu ukiwa umetapakaa katika nguo nyeupe za nesi yule aliyekuwa amekunja ngumi akimwangalia Joram ambaye alikuwa ameyabana mapaja yake huku uso akiwa ameukunja kwa maumivu kiasi cha kufanya meno yake ya rangi ya dhahabu kuonekana waziwazi.. Kilichowashangaza zaidi ni namna watu wale walivyoingia mle Wodini maana si Nesi wala huyo mwanaume wote hawakuingilia mlangoni hivyo hakuna mlinzi hata mmoja aliyeufahamu uwepo wao! Sasa kabla hawajajua cha kufanya Joram alikwishafanya jambo. Risasi mbili kutoka ndani ya Bastola yake aliyoitoa kibindoni zilipenya katika mbavu za askari kanzu mmoja kati ya wale walioingia mle wodini, alipomgeukia askari mwingine ili naye amtende kama mwenzie alikuwa amechelewa maana teke kali kutoka kwa yule Nesi aliyekuwa akipambana naye na kuisambaratisha Bastola yake na hapo sasa ikawa ni vurugu na patashika ya nguo kuchanika

    Joram akapata upenyo na kutoka Wodini kwa kasi akifuatiwa na wale askari pamoja na Yule Nesi asiyejulikana, Kasi aliyotokana nayo Joram ilimchukulia kama nusu dakika tu kulifikia gari lake na kujitoma ndani, Muda huo Koplo Salum alikuwa akitoka kule wodini akifuatiwa na msururu wa madaktari aliowaita kuangalia maafa yale yaliyomkumba mtumishi wao ndipo sasa akaona ile vurumai ikitokea kule Wodini, Akajitahidi kukimbilia lile gari huku akitoa Bastola yake na kuanza kuirushia risasi lakini haikufaa kitu, gari ile ilikuwa hairuhusu risasi kupenya ndani yake, na hata hakupata fursa ya kuisogelea gari ile kwani dereva wa Joram Ndege aliyaelewa majukumu yake,

    Gari liliacha vumbi tu!



    Haraka baadhi ya madaktari wakakimbilia kule Wodini kumwangalia mgonjwa, Alikuwa akiendelea na utaaban wake wa mwanzo wala hakuumizwa zaidi ila chini kwenye sakafu alikuwa amelalia dimbwi la damu askari kanzu mmoja

    Wakiwa bado wanashangaa kule nje, Yule Nesi naye akiwa ametapakaa damu waliishia kumwona tu akijitoma ndani ya gari nyingine iliyokuwa imeegesha pembeni na kutoweka kwa kasi ileile, Koplo Salum alimtupia macho yule nesi haraka,

    ‘Ama!’ alikumbwa na mshangao wa haja, hakuamini alichokiona, alimtambua vilivyo nesi yule

    Amefuata nini huku?

    Anahusikaje na mchezo huu?

    Maswali yalibarizi kichwani mwake, ghafla akakatizwa na kelele za matairi ya gari yaliyotaabishwa na dereva wa Inspekta Kenjah aliyekuwa amefunga breki karibu ya miguu yake!

    Akashuka Inspekta Kenjah na kukutana na Saluti za kumwaga kutoka kwa askari waliotapakaa eneo lile

    “Nipe Ripoti ‘corporal’..” Aliongea kwa wahka Insp

    “Hali mbaya Mkuu..” aliongea Koplo Salum Mrando, halafu akaanza kutiririsha mkasa mzima ulivyokuwa

    “Nilikutahadharisha mapema Koplo.., sasa mlijuwaje kuwa ameingia huko Wodini?”

    “Kelele alizopiga huyo mtu mwenye meno ya dhahabu bila shaka kwa kibano alichopokea toka kwa yule Nesi ndizo zilizotufanya sisi tugundue kule ndani kuna mtafaruku, tulipoingia ndo tukapambana na hali ile ya hatari mpaka Afande Lau akapigwa risasi” alijibu mmoja wa wale askari waliokuwa wakilinda pale hospitali, majibu yake yalimshitua sana Inspekta, Si tu kwa kusikia kuwa askari wake amejeruhiwa kwa risasi ya Joram lakini pia kusikia eti Joram alipiga kelele ya maumivu kwa kupewa kichapo na nesi tu, tena Mrembo!

    “Yaani Joram Ndege apigwe na nesi mpaka atoe yowe?”

    “Joram?” alishtuka Yule Askari kusikia hilo jina ambalo amekuwa akilisikia tu kama hadithi, Insp hakujibu chochote zaidi ya kuongeza swaliCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Huyo nesi naye alipitia wapi mpaka akaingia Wodini?”

    “Hakuna aliyemwona Afande,” alijibu mmoja kati ya wale askari walionusurika huku akitetemeka kwa hofu

    “Daktari.. mnamjua huyo nesi?” Alisaili tena Kenjah huku akimgeukia daktari aliyekuwa ubavuni mwake, lakini tofauti na matarajio yake swali lake likajibiwa na Koplo Salum Marando

    “Hawezi kumjua hata chembe..” Ukimya ukatawala kwa sekunde kadhaa, kundi zima likamgeulkia Koplo Salum, akaendelea “Yule ni Lillian Ufoo..”

    “WHAAT..” Alimaka Inspekta “..Lilly?!, it can’t be.. Yule Sekre.. si alitek..” kila alilotaka kulisema lilishia njiani, alimjua Lillian kuwa ni msichana dhaifu tu aliyetekwa na watu wasiofahamika sasa iweje tena awe nesi ambaye ana ujasiri wa kupambana na jitu kama lile!

    “Ndiye huyo afande” Alijibu Koplo Salum, na muda huohuo simu ya Inpekta ikaita, akaitoa na kupokea. Maelezo aliyopewa yalionesha ni muhimu sana kiasi cha kusahau kila kilichotukia pale hospitalini, akatoa amri

    “Koplo Salum na watu wako tuondokeni haraka.”

    *****

    Katika Hoteli ya Shree Godha iliyopo Ilala Boma aliingia mtu mmoja aliyeonekana nadhifu kwa mavazi yake aghali yaliyomkaa vyema mauongoni, Kanzu nyeupe pee, Kofia ya mkono, makubazi, na saa ya rangi ya almasi huku mkononi akiwa ameshika Tasbihi na kijibegi kidogo

    “Karibu Ustadh Hussein,” Aliongea kwa sura yenye bashasha mhudumu aliyekuwa mapokezi baada ya mtu huyo kuwasili mapokezi

    “Shukrani habibi.. Nija’alie hali ya maungo yako?” Alijibu Sheikh Yule ambaye ni kweli jina lake ni Hussein, Ustadh Hussein Chaullah.. mwanzo alidhamiria kuficha jina lake lakini alipoona amejulikana ikabidi tu atulie, ni kama hakutegemea umaarufu wake kuwa katika kiwango kile..

    Japo ni Kiongozi mkubwa wa dini huko Tabora lakini kupitia huduma za kitabibu na Elimu kubwa anayoitoa kupitia katika vipindi kadhaa vya luninga hasa siku ya ijumaa vimemfanya awe maarufu nchi nzima mpaka huku katika hoteli za vichochoroni

    “Mimi sijambo Sheikh, kumbe upo Dar? Jana tu nilikuona kwenye Televisheni ukitoa darasa ukiwa Tabora..”

    “Ooh! Ni kweli nimeingia leo na ndege.. Sasa mimi sina jambo kubwa sana ila nimekuja hapa kwa maelekezo tu kuna Bwana mmoja ni mpangaji wenu hapa anaitwa Joram ameniambia nifike hapa hotelini kuonana naye”

    “Joram? Amekwambia namba ya chumba chake?”

    “Hapana hakuwahi kufanya hivyo, ila yupo hapa hotelini kwa muda mrefu kidogo.. ni mteja wenu wa kudumu”

    “Ooh itakua Yule mwenye meno ya dhahabu maana ndiye mteja wetu pekee aliyepanga hapa kwa takribani miezi miwili sasa”

    “Naam, Masha’allah ndiye huyo yakhe! Ni kweli ana meno ya rangi ya dhabu.

    Mhudumu akacheka kidogo na kuongea tena

    “Kama ndiye huyo meno ya dhahabu yuko chumba namba thelathini na nne japo hapa hajaandika hilo jina la Joram...”

    “Ameandika jina gani?” Alihoji Sheikh Chaullah huku hamaniko likichukua nafasi ya tabasamu lake lililotamalaki tangu awasili pale Hotelini, alijua sasa ameshayakoroga

    “Yaani Sheikh wangu nawe bwana hata jina la mtu unayemtafuta hulijui! Sasa asingekuwa na hayo meno ya dhahabu ungempataje?..” aliongea kwa utani kidogo mhudumu yule na kuongezea “..Hapa ameandika A-bashir”

    “Ooh umeona sasa Nd’o huyohuyo sheikh wangu maana ni kama miezi miwili iliyopita tu amebadili dini akachagua jina hilo sasa sikutaraji kuwa angelitumia mpaka kwenye masuala ya kawaida kama haya,” Ustadh akasema uongo japo sidhani kama alipata dhambi kutokana na uwongo ule uliokuwa na dhamira Fulani ndani ya nafsi yake

    “Ooh kumbe amesilimu? Haya sawa Sheikh Nenda ukajaribu kumwangalia maana hua anaondoka na fungo yake… Pitia hapa moja kwa moja halafu utakata kona mkono wako wa kushoto, utaona vyumba.. chumba chake ni namba 34”

    Baada ya ruhusa ile Sheikh Chaullah hakutaka kumpa tena nafasi mhudumu Yule ya kuzidi kumdodosa, akaanza kutembea kwa haraka kuelekea kule alikoelekezwa.

    Haikuwa mbali sana, akawasili katika korido ndefu iliyopangika vizuri kwa mfuatano wa vyumba, akakiona chumba namba Thelathini na nne, akasogea na kuusukuma mlango, Ulifungwa!

    Haraka akaangaza huku na kule, alipoona hakuna mtu akaingiza mkono kwenye mfuko wa kanzu yake akatoa Funguo ‘Malaya’ kama tano hivi, ya kwanza ikagoma, ya pili ikagoma pia, ya tatu ikatii kiu yake,

    Mlango ukaachama, akajitosa ndani!

    Hapakuwa na makolokolo yoyote ndani ya chumba kile kilichotandikwa va kupangwa vizuri zaidi ya Begi lilioachwa wazi sehemu kubwa ya zipu ya kati na kufanya nguo kuchungulia nje, Akaingiza mkono ndani ya Begi hilo na kulipekuwa, hakupata alichotaka! akafungua ndani ya kabati hapakuwa na kitu, akaenda chini ya uvungu wa kitanda akainama na kuchungulia hakukuta kitu, akainuka na kuangaza huko na kule kwa haraka kama Muha aliyeachwa na Treni ya kwenda Dar! ndipo wazo likamjia akainua Godoro nako hakuna kitu! Akaliendea Kochi dogo la sofa na kulitikisa akasikia vitu vikigongana, akalipekenyua Waooh akakutana na vitu alivyovikusudia, ilikuwa ni Laptop na Flash, akavitoa! pia kulikuwapo na Bastola nayo akaichukuwa japo hakuwa na haja nayo. Akarejesha kila kitu kama kilivyokuwa! Akaikunja kanzu yake pamoja na Msuli aliouvaa kwa ndani, akaweka Flash na ile Bastola katika mifuko ya Kaptula yake ya Jinzi aliyoivaa kwa ndani kisha akajirejesha katika hali yake ya unadhifu.. Laptop akaiweka katika kile kijibegi chake alichoingia nacho. Haraka akatoka na kukifunga chumba na kuondoka zakeCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipokata tu kona ya kwanza akakutana uso kwa macho na Joram Ndege akiingia ndani, wakapishana bila ya salamu kila mmoja akiwa anajiamini vilivyo! Hisia za hatari zikafukuta kichwani mwa Joram akapeleka mkono wake kiunoni na kuipapasa silaha yake kisha akamgeukia Ustadh yule aliyepishana naye bahati mbaya ama nzuri hakumwona tena, alikwishakata kona na kutoka kwa kasi mpaka pale Kaunta ambapo alimkukuta Yule Mhudumu amezungukwa na wateja wengi hivyo ikawa ni ponepone kutokana na mtungo wa maswali,

    Akatoka zake kimyakimya kwa mwendo wa ki-sheikh, mwendo wa kichamungu, tar’tib mwendo wa maringo!

    Kitokeo cha hapo Ustadh akaenda mpaka mbele kidogo tu akaangaza huku na kule na kujiridhisha juu ya hali ya usalama kisha akaiendea teksi iliyokuwa imeegesha pembeni kama inayomsubiri yeye, akaingia ndani na hapohapo dereva akaondoa gari.. wakaenda mpaka mbele kidogo kasha wakasimama, haikuchukua dakika mbili akawasogelea kijana mchafu wa mwili na nguo, akiwa amevalia nguo zake chakavu na mgongoni akiwa amening’iniza mfuko wake mkubwa sandarusi uliosheni chupa za maji na juisi anazopita kuokota mjini

    Kijana huyo anayeonekana kama aliyekolea na kutopea katika matumizi ya dawa za kulevya alipoifikia tu teksi ile mlango ukafunguliwa na kitendo bila kuchelewa ustadh Chaullah akatoa lile begi lake alilolitumia kuhifadhia ile Laptop aliyoichukuwa chumbani mwa Joram na kumkabidhi muuza makopo huyo! Mbali na Laptop pia ndani ya begi kulikuwa na ile Flash pamoja na Bastola alizoziweka humo baada ya kuingia ndani ya teksi ile. Kijana muokota makopo akalipokea begi lile na kulisweka ndani ya mfuko wake mchafu wa sandarusi na kuondoka zake

    Hakuna aliyeelewa tukio lile la aina yake!

    Ni kama vile ustadh alichanganyikiwa au amerogwa maana kukabidhi vitu hatari kama vile kwa mtu wa ajabu kama yule, vitu ambavyo yeye mwenyewe kuvipata kwake kulihatarisha maisha yake, Hasha!

    Baada ya makabidhiano yale Ustadh na dereva wake wakarejea mpaka sehemu Fulani wakaegesha gari yao!



    Nje ya Hoteli hiyo palikuwa na Msururu mkubwa wa Askari kanzu, wengine wakiwa ndani ya magari, wengine wakiwa miongoni mwa wale wateja waliopitwa na Sheikh Chaullah pale mapokezi, na wengine wakiwa katika mitindo yao tofauti ambayo isingekuwa rahisi kuwagundua! Lakini Joram Ndege alikwishagunduwa kuwa anafuatiliwa hivyo haraka alidhamiria kuvichukuwa vile vitu muhimu kwake ambavyo kwa muda ule vilikuwa vikimilikiwa na Ustadh Chaullah

    Inspekta Kenjah alikuwa ni miongoni mwa Wana usalama wale waliotanda nje ya Hoteli ile ambapo aliwasili kufuatia taarifa aliyopokea kutoka kwa Sajenti Malumbo aliyekuwa nje ya hospitali na kumshuhudia Joram akitoweka, akamfuatilia mpaka alipoona kuwa uelekeo wake ni wa kurejea huku hotelini alikokuwa mwanzo!

    Baada ya utulivu wa muda ndipo Insp akaamua kushuka ndani ya gari na kuelekea ndani ya hotel ile akifuatana na kijana wake mmoja mpaka mapokezi ambapo alikuta idadi ya watu kidogo ikiwa imetulia

    “Habari yako kijana?” Inspekta alimsalimu mhudumu

    “Salama bwana mkubwa, unahitaji vyumba?”

    “Kwani kwa unene huu nilionao naweza kuhitaji vyumba vingapi kwa ajili ya kulala,” Alidhihaki Inspekta baada ya kuambiwa kama angehitaji vyumba

    “Samahani sikuwa na nia mbaya, nina maana unahitaji chumba?”

    “Kwani hapa mnauza na Simenti?..” Kenjah aliendelea kujibu kifedhuli tu kiasi cha kumfanya mhudumu aishiwe cha kusema “..Namuhitaji mteja wako aitwaye Joram Ndege, yupo chumba namba ngapi?”

    “Nani? Joram? We nani? Mbona mnanichanganya kila anayeingia humu anamtaka Joram mtu.. mwenyewe wala hatumii jina hilo, hebu mpigie simu mwenyewe,” Alijibu kwa hasira mhudumu Yule aliyeudhiwa na majibu ya Kenjah, na hicho ndicho alichokikusudia Inspekta Kenjah, Kumuudhi kijana Yule ili aropoke chochote chenye manufaa, hakutaka kufanya haraka kumfuta ndani Joram maana hukujua ni chumba gani yupo japo amemwona akiingia mle hotelini, akabaki akijiliza sasa

    Kila anayekuja anamtaka Joram?

    Nani mwingine amekuja kumtaka Joram?

    Anatumia jina gani linguine?

    “Hatuna muda wa kupoteza,” Aliongea Inspekta huku akimwangalia mmoja kati ya askari alioongozana nao mle ndani, akampa ishara na Yule askari akaielewa. Akatoa Bastola akaiweka juu ya meza ya kaunta, kisha kitambulisho chake cha kazi na kumwonesha mhudumu

    “Sisi ni maofisa wa jeshi la Polisi, tunahitaji kujua Joram ana muda gani tangu apange humu na huwa anawalipa kwa njia gani? Pia tunahitaji kujua anatumia jina gani awapo hapa hotelini na ni nani mwingine aliyekuja kumuulizia, halafu mwisho utuambie umejuaje kua huyo aliyeandikisha hilo jina pia ndiye Joram tunayemuhitaji sisi!” Alifoka Askari Yule na kumfanya mhudumu atetemeke kama anayetaka kuchinjwa.. akautapika ukweli wote ulivyo! kilichomsisimua Insp Kenjah ni pale aliposikia kuwa kuna Sheikh alikuja kumtafuta Joram, na kwamba Sheikh huyo alimsilimisha na kumbandika jina la Al-bashir

    Joram asilimu?

    Inspekta akatoa simu yake na kumpigia Sajent malumbo “Hallow,” alipokea Sajenti Malumbo

    “Hakikisha mnaweka ulinzi wa kutosha nyuma yah ii hoteli, asiingie wala kuondoka mtu, sawa?”

    “Sawa mkuu.. tayari nipo huku nyuma muda mrefu hakuna mtu yeyote zaidi ya Mzee mmoja tu aliyekuwa akipiga deki vibaraza vya hoteli hii.. naye kaishaondoka huku, nadhani ni mtumishi wa hapa”

    “Good” Inspekta akakata simu na kuwaamuru vijana wake wamfuate kule walipoelekezwa kilipo chumba cha Joram

    *****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yule mzee aliyekuwa akideki kule nyuma aliondoka na beseni lake alilokuwa akilitumia kufanyia usafi, alipofika mbeleakajimwagia maji kidogo sehemu ya kichwa chake kilichosheheni mvi kisha akavuka barabara na kwenda upande wa pili badala ya kuingia huko hotelini mwao. Ni kama aliyekuwa akihofia kitu maana hata mwendo wake ulibadilika ukawa wa kasi na kuondea ile ladha ya utu uzima wake, kama haitoshi akakaza mwendo na kuamua kukimbia tu huku akigeuka nyuma kama kuna mtu anayemwona!

    Kwa pembele kidogo ikatokea teksi kama inayotaka kuvuka barabara, ilikuwa ni teksi pekee iliyojipendekeza kwa mzee huyu na kumfanya ajisikie mwenye bahati kama aliyeokota machungwa kwenye shamba la mafenesi, ama bahati ya mtende kustawi jangwani.

    “Ondoa gari haraka kwa mwendo wa kasi,” Aliongea mzee Yule baada ua kuingia ndani ya gari

    “Mzee pesa iko?”

    “Uliza jingine.”

    Dereva akafanya kama alivyoambiwa, japo mwendo ulikuwa wa kasi na hapakuwa na dalili zozote za kufuatwa lakini Mzee hakutulia, kila mara alikuwa akigeuka nyuma kuhakiki usalama wake. Hawakufika mbali sana wakapokelewa na foleni ndefu ya magari katika barabara hii ya uhuru!

    *****

    Insp Kenjah na askari wake hawakuwa na haja ya kuvunja mlango wa Joram maana ulikuwa wazi! Wakaingia wote kwa tahadhari na kuanza kukipekua.. Hapakuwa na mtu zaidi ya begi tupu!

    Kaenda wapi?

    Si ameingia huku nikimwona mwenyewe?

    jambo moja tu likamtia jakamoyo Inspekta, Sehemu ya juu ya chumba hicho kwenye dali ilikuwa wazi! Akakumbuka lile tukio la kule hospitalini baada ya Joram kupita juu kwa juu na kutokezea wodini.. Ghafla akasikia ukulele wa haja ukitokea vyumba vya mbele, ilikuwa ni sauti kali ya kike ikionesha kila dalili ya hamaniko. Haraka Inspekta na vijana wake pamoja na Yule muhudumu aliyekuwa nyuma muda wote wakatoka chumbani kwa Joram na kuifuata kelele ile. Walipotoka wakakutana na Msichana ambaye ni muhudumu wa usafi vyumbani akiendelea kupiga kelele huku macho yake yakiwa yamekodolea ndani ya chumba kimoja kilichokuwa wazi..

    Walipoingia walikutana na mwili wa mwanamke aliyekuwa ni mpangaji wa chumba hicho ukiwa hauna uhai, baada ya kuusogelea wakabaini kuwa amenyongwa kwa kutumia taulo, Salam walizoachiwa ilikuwa ni viatu na zile suti walizomuona Joram ndege akiwa amezivaa! Alipopepesa tena macho akakuta dirisha limevunjwa.. Hmadi! Hisia za hatari zikachemka kichwani mwa Inspekta Kenjah, akajiridhisha kuwa Joram alipita juu kwa juu kwenye dari mpaka ndani ya chumba hiki na baada ya mauaji akatoweka.

    Sasa kama amevua nguo zake, Je ametoka kama alivozaliwa? Haiwezekani!

    Machale yakamcheza, akakumbuka kuwa aliambiwa kuwa kuna mzee alikuwa akifanya usafi huko nyuma, akaona lililo bora na kumkamata huyo mzee ili aseme kama kuna mtu alimwona akitokea dirashani!

    “Ni mzee gani alikuwa akifanya usafi huko nje ya hoteli?” Insp alimuuliza Yule Mhudumu wa kaunta

    “Mzee?”

    “Jibu swali kijana.”

    “Hakuna mzee katika hoteli yetu, wahudumu wote ni vijana.. na wanaohusika na usafi ni wasichana tu.”

    Jibu likawa hadhir kabisa kuwa Yule mzee ni mtata! Haraka Insp na watu wake wakatoka nje ya hotel na kwenda kujumuika na afande Malumbo ambaye baada maswali kadhaa ilionekana kuwa mzee Yule aweza kuwa Joram! Haikuwachukua muda kuamini hivyo baada ya muuza vitumbua mmoja kuwaeleza kuwa amemwona huyo mzee akiingia ndani ya teksi na kuondoka kwa kasi akielekea mjini..

    Hawakupoteza muda nao wakaingia kwenye magari yao na kuanza kufukuzia!

    *****

    Mzee akamuamuru tena dereva wake akate kona ya kulia waingie mtaa wa Kilwa ambao utawachukuwa mpka kariakoo.. Dereva bila ajizi akatii amri, wakauvamia mtaa wa Kilwa na kuzidi kutokomea. Wakiwa wanaendelea na safari ndipo ghafla kikaibuka kizaazaa cha mwaka.. Ni wakati Yule mzee alipogeuka nyuma ili kuhakiki zaidi kuwa hakuna anayewafuata, Macho yake yakafumaniana na mtu aliyekuwa ameketi siti ya nyuma katika teksi hiyohiyo aliyopanda yeye. Yawezekana ni mteja au shanta lakini mbona mara zote alizokuwa akigeuka tangu wanaondoka hakumwona? Haiwezekani!

    Au ameingia ghafla huku gari ikiwa katika kasi yake?

    Haiwezekani!

    Au alikuwa amelala kwenye siti? Inawezekana!

    Kabla hajajuani lipi jibu sahihi la kioja hicho, ndipo ubongo wake ulimkubusha kuwa mtu huyo ameshapata kumwona mara kadhaa!

    Wapi vile? Kwenye Luninga.. na mara ya mwisho ni siku hiyohiyo muda mfupi tu aliopita, katika korido ya hoteli ya Shree Goza, tena akiwa amevalia mavazi hayohayo!

    Ni Ustadh Hussein Chaullah!

    Ama!

    Ustadh hakuwa na shaka kuwa sasa anatazamana na Joram Ndege, Mwuaji wa kokodiwa licha ya Nywele na ndevu bandia alizojipachika ili aonekane Mzee! Ustadh aliamini tu kuwa atakapokurupushwa na maaskari atatafuta gari ya kumkimbiza popote atakapo hivyo akaegesha kwa ajili ya kumpa huduma hiyo muhimu sana!

    Wakati Joram akiwa anatafuta kujua ni kipi kinaendelea mpaka Ustadh yule akaenda kule Hotelini na hatimaye sasa ameibukia ndani ya gari aliyoikodisha ndipo alipotolewa mawazo yake rasmi. Ngumi iliyojaa sugu ngumu zitokanazo na mazoezi makali ayafanyayo Ustadh Chaullah ilituwa katika kimpuma cha Joram Ndege na kumsababishia si tu maumivu makali bali pia alipata ugeni wa nyotanyota zilizoambatana na giza usoni mwake, Akaangukia karibu ya kioo cha mbele! Hapohapo Ustadh akamvagaa tena na kuporomoshea ngumi nyingi, mfululizo kwa mikono yake yoteyote.. ingekuwa ni uwanjani tungemfananisha na Lionel Messi!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Joram hakuwa mtu legelege kihivyo, mafunzo yake magumu ambayo ni sawa na ukatili aliyoyapata kwa maharamia waliokubuhu hayakumwacha mnyonge kiasi hicho! Alijibinua kidogo tu katika siti aliyokuwa ameketi, akawa kama aliyekalia mgongo, akaufyatua mguu wake kama risasi ukarudi kwa nyuma na kwenda kumtandika Ustadh Chaullah aliyekuwa anataka kumuinamia ili amshushie kipondo kingine, Teke hilo lilitosha kabisa si tu kumgaragaza Ustadh katika siti ya nyuma bali pia kumtoa ‘Mchuzi’ mdomoni baada ya kuchanika! Hapohapo Joram akamtaza dereva aliyekuwa hawezi kujihami kutokana na mwendo kasi, alipojiridhisha hilo akamwachia pigo takatifu la ngumi iliyotuwa sawa bin sawia ubavuni.. Dereva akayumba na kuuachia usukani kwa maumivu, gari ikahama njia na kwenda kulivaa Jiwe la msingi la chama fulani cha siasa.. Ikawa ni ajali baridi, gari ikiumia kiasi, huku abiria wote kwa wakati huo wakiumilia maumivu ya dozi walizopeana wenyewe

    Haraka Joram akashuka akashuka ndani ya gari huku akimwangalia dereva kwa hadhari, alipofika nje akalakiwa tena ngumi nzito kutoka kwa Ustadh ambaye alikwisha shuka haraka kabla yake! Wapita njia wachache waliohudhuria eneo lile walishuhudia sinema ya Bure kati ya Joram aliyekuwa katika mwonekano wake wa kizee na ustadh Chaullah akiwa ameikunja kanzu yake usawa wa kiuononi.. Mzee na Ustadh!

    Zilipigwa ngumi mujarab! Ngumi za kifundi, hakuna mjinga kati yao katika fani ya ngumi.. Ustadh alimjua vyema Joram hivyo alikuwa na hadhari kubwa katika mpambano ule, lakini Joram alijidanganya kuwa anapambana na Sheikh Fulani tu aliyejawa na hasira ya kukosa ubwabwa wa harusini, na hilo ndo likawa kosa kubwa! Ustadh alikuwa akizungusha mateke yake kama feni za pangaboi, mateke yalimzuzua akili Joram akawa kama aliyechanganyikiwa, mra kadhaa naye Ustadh alipokea ngumi za haja kutoka kwa Joram

    Wakiwa wanaendelea kuwindana kuwindana kama majogoo yaliyobaki taaban baada ya kupigana muda mrefu bila ya kutokea mwamuzi ndipo Joram alipofikia ukipigwa na kitu kizito kichwani na kumpotezea mwelekeo, alikuwa ni Yule Dereva amempiga na ubao mrefu alioupitia chini baada ya kuteremka kutoka ndani ya gari, kabla Joram hajajiweka sawa Ustadh akamnyakia usawa wa mabega na kichwa mithili ya Nyani aliyerushiwa ndizi, na hapo ndipo Ustadh alipofanya hitima kwa kuachia pigo la judo usawa wa kisogo na kumwangusha Joram mpaka chini akiwa hana fahamu

    Wapambe waliojitokeza walijikuta wakishangilia tukio lile kama wako sinema vile bila hata ya kudadisi kuwa chanzo cha ugomvi ule ni nini! Haraka Ustadh akatowa Pingu na kumfunga Joram, na kama haitoshi akatoa dubwasha Fulani hivi na kumwekea mdomoni. Muda wote huo Joram alikuwa ulimwengu mwingine kabisa, ulimwengu wa kutofahamu lolote linalotukia.. Naam, sasa angefahamu nini wakati hizo fahamu zenyewe kazipoteza hapohapo!

    Ustadh akatoa simu na kubofya namba Fulani, Simu ya Insp Kenjah upande wapili akiwa karibu ya mataa ya Karume ikaita

    “Hallow,” Alipokea ile simu Insp japo alijawa na hofu kubwa, si tu kwakuwa ni namba mpya iliyompigia, bali amepigiwa katika namba ile maalum aliyopewa na IGP

    Nani mwingine mwenye namba hii?

    “Inspektah Kenjah, hakuna haja ya kutwawilisha muda njoo haraka hapa mtaa wa Kilwa jirani na msikiti wa Waburushi..”

    “Kuna nini huko na wewe ni nani?” alifoka Inspekta

    “Huna haja ya kunijua, nimekusaidia kukukamatia mjanja wako… Joram Ndege”

    “Whaat?!.. Eti Jora..” alimaka Insp lakini simu ilikwishakatwa, alipojaribu kuipigia tena simu ile iliita mara moja tu,ikakatwa na kuzimwa kabisa. Hakika Insp alihamanika, akawaarifa vijana wake kuwa wasogeze magari pembeni na kutafuta uelekeo wa eneo aliloarifiwa afike.. Moyoni alizidi kuzongwa na hofu akiamini kuwa huyo aliyempigia huenda akawa ni mtu muhimu mpaka akaipata namba ile ya siri, ama wanaweza kuwa ni wale wahalifu wameinyaka na kutaka kumlengesha huko kwenye Domo la mauti! Akatamani ampigia IGP amuulize kama alimpa mtu mwingine namba ile lakini akajionea aibu, akawaamuru askari wake kwa mara nyingine na kuelekea Eneo la tukio

    Alipofika eneo husika alilakiwa na kundi la watu likiwa limeuzunguka mwili wa uliolala chini ukiwa hauna fahamu, Mwili wa Inspekta ulizizima baada ya kumwona Joram akiwa ameadhibiwa vilivyo, alipojaribu kuongea na mashuhuda waliobahatika kuuona mchezo ule, wakasimulia ‘Ei to Zedi’

    “Huyo aliyempiga yuko wapi?” alisaili Inspekta

    “Aliingia kwenye gari yeye na dereva wake wakatoweka!”

    *****

    Ustadh Hussein na Dereva wake wakiwa ndani ya teksi yao iliyoharibika kidogo sehemu ya mbele kwa ile ajali baridi walikuwa njiani wakianza safari nyingine, Safari ya Bagamoyo kwa mwalimu wake na Ustadh Chaullah. Mwalimu aliyediriki kumpa sehemu kubwa ya elimu yake ambayo inamsaidia kuitumikia jamii yake ki dini na kiusalama!

    Si mwingine ni mwalimu Atrash Bin Jamadu

    *****



    Ilala, Dar Es Salaam.

    Kama kawaida ya Jiji la Dar es Salaam, wekundu wa jua la asubuhi unapochomoza tu pilikapilika huanza, hakuna kupumzika, kila mmoja anaukimbiza ‘mwenge’ kuusaka mkate wake wa kila siku. Mitaa mingi huchangamka, kelele za muziki, pilikapilika za vyombo vya usafiri, mpishano wa waungwana na washenzi humfanya hata yule mwenye mawazo na changamoto lukuki za kimaisha naye kufurahi kidogo kiasi cha kuyasahau matatizo yake, Lakini si kwa familia hii ya Suhail Kusekwa ambaye u-taaban wake umewanyong’onyeza wote, hakuna mwenye Furaha, raha, wala amani.

    Ni kweli maradhi ni jambo la kawaida tu na laweza kumkumba yeyote, lakini sasa lau kuwe na japo Bima ya matumaini! Suhail anaumwa yu hoi taabani, Ugonjwa haujulikani, hauonekani, hautambuliki. Vipimo vyote vimehusishwa lakini wapi! Hali inazidi kuwa mbaya tu. Kama ungepita karibu na nyumba hii ya kifahari pengine ungehisi wenyewe wamehama kwa jinsi ukimya ulivyotanda! La hasha! palikuwa na watu wengi tu ila kila mmoja kajiinamia kivyake.. Mzee Kusekwa na Fungameza waliketi zao barazani kila mmoja kwenye kochi lake, hakuna aliyemsemesha mwenziye kwa muda mrefu tangu walipomaliza kupata Stiftahi waliyoandaliwa! Mzee Kusekwa alijifanya kumakinika na gazeti alilokuwa amelishika mkononi kama vile anayesoma jambo muhimu, masikini ya Mungu hakujua kwamba hata hilo gazeti lenyewe aliligeuza chini juu juu chini! Mzee Fungameza yeye alijifanya kuangalia Tv lakini lau kama ungelipita mbele ya Tv hiyo wala asingekuona maana ki mwili ni kama yupo pale ila ki fikra alisafiri maili nyingi sana

    Kama tu wanaume wazima wameshakata tamaa ya kuuguza kwa haraka kiasi hicho Je hao akina mama huko? Wao ndio kabisa, hakuna hata aliyepata kifungua kinywa kati yao zaidi ya kutoka kwenda msalani kwa zamu na kurejea vyumbani mwao.. Walikuja Dar kumuuguza Sharifa mara wakakutana na kisanga cha Suhail kuwekwa rumande, hawajakaa sawa nao wakawekwa ndani, walipotolewa wanakutana na Sharifa eti amepona ghafla kwa miale ya Pete kutoka kwa mtu asiyemjua, na mara sasa Suhail nd’o amegeuka kuwa mgonjwa, hakika walijichokea wazee wa watu!

    Nyumba ikiwa katika hali hiyo ya utulivu ndipo ikasikika kengere maalum ikigongwa kule getini, bila shaka pana mgeni, hakuna aliyejishughulisha nayo kwakuwa Dada wa kazi yuko huko uwani akiendelea na kazi hivyo angemfunguliaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Baba.. kuna Mgeni wenu hapa,” Aliongea msaidizi Yule wa kazi baada ya kuwasili pale barazani

    “Mkaribishe ndani,” alijibu mzee Kusekwa, kisha msaidizi Yule akatoka nje na kumruhusu mgeni aingie. Macho ya Mzee Kusekwa na Fungameza kwa pamoja yakajikuta yakitazamana na bwana huyu aliyeingia, Mzee Kusekwa alipatwa na mshangao baada ya kumwona mtu Yule akiingia, hakuwa na madhara yoyote bali hakumtegemea uwepo wake hasa katika mji huu wa ugenini kwao, wanafahamiana, na wote ni wakazi wa mjini Tabora. Alikuwa ni Ustadh Hussein Chaullah!

    “Sheikh Chaullah! Ni wewe?”

    “Ni mimi Mzee wangu.. Assalamu alaykum,” Alisalimia Ustadh huku akimpa mkono Mzee Kusekwa aliyekua amesimama kumpokea

    “Waaleyka Salaam, hata sijui nikuulize za Tabora ama za Dar.. haya karibu kwanza uketi.” Hakujibu kitu Ustadh, akamsogelea Mzee Fungameza naye akamsabahi na kurejea kwenye kochi moja lilokuwa likitazamana na Luninga iliyokuwa ikionesha mpira,

    “Haya habarini za hapa?”

    “Salama tu karibu sana”

    “Ahsante sana.. mimi nimekuja Dar majuzi ila pana mambo yakawa yamenishughulisha, na hata nilipoyamaliza nikaenda Bagamoyo jana na kulala hukohuko mpaka asubuhi hii nd’o nikaianza safari ya kurejea tena Dar”

    “Ooh, Pole sana kwa mihangaiko Sheikh.. Sisi tuna muda kiasi hapa mjini, Maradhi nd’o yametuleta huku! Mdogo wako hali yake mahamum”

    “Nilisikia khabari hizi lakini sikuzitilia ma’anani sana nikidhani ni maradhi ya kawaida tu.. ila huko Bagamoyo nilipokwenda ndiko kuna bwana mmoja anafahamiana na Suhail akanipasha kiufasaha.. Poleni sana ila tu mkumbuke Maradhi ni mtihani mkubwa nd’o maana Mungu akatuasa kuwa tukakujaribuni kwa njaa, maradhi na vifo.. hatuna budi kulishinda jaribu hili kwa matokeo yoyote ambayo Mola atatukadiria..”

    “Ni kweli kabisa,” alijibu Mzee Kusekwa kisha ukimya ukachukua nafasi kabla ya Mzee Kusekwa kumtambulisha Ustadh kwa Mzee Fungameza

    “Bwana Fungameza.. huyu ni Kiongozi wetu wa dini kutoka Tabora sijui kama umepata kumwona? Ni Imam na Ustadh wetu, pia huwa ni tabibu mzuri tu wa maradhi ya ajabuajabu kama haya ya Kijana.”

    “Namfahamu ila zaidi kwa kumwona kwenye ma televisheni tu.. Ni Shehe Hussein Chaullah kama sijakosema”

    “Naam, ndiye yeye wala hujakosea! Au kwakuwa umenisikia nikimtaja wakati akiingia?” alitania kidogo Mzee Kusekwa, wakacheka kidogo kiasi cha kuihuisha upya baraza iliyokuwa kama imekufa..

    “Sasa tuongee mawilimawili, hapa umepajuaje? Au ulishawahi kufika?” alihoji Mzee Kusekwa

    “Hapana sikuwahi kupajua hapa ila nilianzia kule ofisini kwake.. ndipo nikaelekezwa mpaka namba ya nyumba” Baada ya mazungumzo ya hapa na pale, Ustadh akaomba kuonana na Suhail, Mzee Kusekwa akamchukuwa mgeni mpaka katika mlango wa chumba alichomo Suhail kisha akagonga huku akiita

    “Sharifa!.. Sharifa”

    “Abee baba.”

    “Haya kuna Mgeni anataka kumwona mgonjwa.”

    “Sawa, aingie tu.” Ustadh akaingia mpaka chumbani na kumkuta Suhail akiwa amelala kitandani, Mashuka gubigubi! Sharifa aliketi pembeni yake. Kilikuwa ni chumba chenye hadhi ya kumlaki yoyote mwenye ukwasi wa kutosha, kila kilichomo mle ndani kilikuwa kizuri, imara, na chenye thamani kasoro afya ya Suhail tu ndio haikuwa imara japo kidogo.. Hakika alitingwa kijana wa watu, hakuwa hata na uwezo wa kuinuka kumpokea mgeni, alichoweza kufanya ni kujifunua shuka na kuinua jicho tu na kumtazama.. Baada ya salam, Sharifa akawapisha

    “Pole sana.. Mungu ataku’afu tu.”

    “Ahsante sana ustadhi, nashukuru umekuja kuniona, imenifariji sana!”

    “Usijali sisi ni kama ndugu kabisa yatupasa kufarijiana.. ila tu mimi si mkaaji sana, nina machache yamenileta hapa kufuatia hali yako..” aliongea Ustadh kwa utulivu na sauti ya chini

    “..haina ubishi kuwa hali yako si nzuri hata chembe, na inahitajika lifanyike jambo ili kujikomboa wewe na familia yako.. nina salamu zako kutoka Bagamoyo..”

    Kusikia jina bagamoyo, moyo wa Suhail ukapiga sarakasi, hakuwa tena na hamu japo ya kulisikia jina la mji ule, Ustadh aliliona hamaniko hilo lakini halikumzuia kuendelea kuongea “..Salamu kutoka Kwa Mzee Atrashi, kwanza anakupa pole kwa kila kilichokukumba, kama asingelikuwa hali ya afya yake kuwa na mgogoro basi bila shaka angelikuja mwenyewe” Aliposikia jina la mzee yule akajikuta ameingiwa na nguvu, akahisi kama mkombozi amewasili, akajiinua kutoka pale kitandani na kuketi.



    “..Mzee anasema alikukanya kuhusu Tamaa na Uongo.. mbona hujajirekebisha? Kwanini umeendelea kumdanganya mkeo Sharifa kwa kila jambo? Na kwanini mpaka leo licha ya matatizo kukufika shingoni bado hujawaeleza ukweli wazazi wako? Au unasubiri mpaka hawa maharamia wakuangamize ibaki siri sirini?..” Akaweka kituo kidogo Sheikh Chaullah ili kuyapa nafasi maneno yake yamwingie vizuri mkusudiwa, ila akakumbuka kitu akaamua kukisema kabla hajaendelea na

    “Nikutoe hofu, usiogope kuongea na mimi kuhusu matatizo yako.. najua kila kitu kuhusu wewe, najua khabari za Mzee Shamhurish, khabari za Khatam Budha, Khabari za Sharifa na Shekhia na nyinginezo! Mimi nimehitimu elimu yangu kwa Mzee Atrash na ndiye kijana pekee aliyenipa sehemu kubwa ya taaluma zake kuliko kijana mwingine yeyote hivyo ananiamini! Tangu siku ulipowasili kwake alikujua kuwa ni kijana wa Tabora ndipo akanipa habari hizi.”

    “Sheikh mimi sina usemi, hali yangu ni mbaya sana! Hapa ni siri yangu tu jinsi ninavyoumwa.. na sina hakika kama nitazidisha japo siku mbili nikiwa hai, nitakuwa nimeshakufa tu! Kilichoniponza bila shaka unakifahamu… mbaya zaidi Pete(Khatam Budha) niliyokuwa nikiitegemea imeshindwa kunitibu kamwe!” aliongea Suhail kwa sauti ya chini na ya kutaabika sana

    “Khatam Budha haijashindwa kukutibu bali wewe haujaipa chakula chake kama ulivyoelekezwa na Mzee Shamhurish”

    “Chakula chake? kipi hicho?”

    “Aaah Suhail.. we haukukubaliana na Mzee wako kuwa utakuwa unainywesha damu pete yako kila mwezi?”

    “Oooh nakumbuka Sheikh wangu.. na nimeshafanya hivyo bila mafanikio.. nimeshachinja mbuzi kama mara tatu lakini kila nikiiweka pete kwenye bakuli lenye damu hakuna lolote zaidi ya damu kuganda tu, sijui nd’o kusema imegoma kunywa au nini sijui!” Jibu hilo la Suhail almanusura limpasue mbavu Ustadh kwa kicheko alichokibana

    “Sikia Suhail, usiwe mjinga kiasi hicho.. Mzee Shamhurish alikudanganya tu kuwa utakuwa unatoa kafara ya damu ili usiogope dhamana hiyo, ila ulichopaswa kutoa ni kafara ya damu ya mwanaadamu ya mtu na si mnyama, na endapo utachelewa kutoa kafara hiyo kwa wakati basi itakulazimu kutoa kafara ya damu ya mtu wako wa karibu tu.. kama ni Mama, Baba, Mke, Mtoto ama nduguzo! na kwakuwa wewe umeshachelewa yakupasa kumtoa mmoja kati ya wanafamilia wako ama damu yako wewe itumike kuilisha pete.”

    “No! I can’t, kamwe siwezi.. Kuwauwa watu wangu?! No”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hiyo ni juu yako sasa ila mimi nilitaka tu kukutoa ukungu wa macho… kilichonileta hapa ni kazi niliyopewa na Mzee Atrash ya kujaribu kukuokoa kama Mungu atapenda aponyoke, ila tu kabla sijaanza kufanya hicho tulichokusudia kukifanya kuna mambo inabidi kwanza uyatekeleze.” Suhail akashusha pumzi, akajiweka sawa, na kuzidi kulengesha masikio yake ili kumsikiliza bwana huyu aliyeibuka kama mzimu

    “Kwanza naomba uitishe kikao cha familia nzima uwaeleze kila kilicho nyuma ya pazia, Eleza kila kitu kituo kwa kituo hakuna haja ya kuficha tena janga hili.. hiyo itakuwa ni hatua ya kwanza maana kwa kufanya hivyo ina maana utakuwa umekataa kuwa mfuasi na mtumwa wa majini. baada ya hapo tutafanya jambo linguine la msingi zaidi”

    Ilikuwa ni mtihani mgumu sana kwa Suhail, tena mgumu kwelikweli!

    Kukaa na wazazi wake, wakwe pamoja na mkewe kuwaeleza kuwa Eti alimsaliti Sharifa tangu alipokuwa chuoni kisa tama ya pesa, awaleze siri ya utajiri wake kuwa alipewa na Mzee Shamhurish huku akishinikizwa kumwoa binti yake ambaye baadaye aligundua kuwa ndiye Yule mwanamke wake wa huko chuoni, awaeleze kuwa hatimaye alikubali na kufunga ndoa na huyo binti mwenye asili ya kijini, kisha awaelezee hatua kwa hatua jinsi alivyokuwa akimlaghai Sharifa kuwa yeye ni mbovu ili tu asikutane naye kimwili kwa kukidhi matakwa ya Shekhia, aelezee nguvu kubwa aliyonayo na matukio aliyowahi kuyafanya kwa kutumia Pete ile ya ajabu aliyopewa, aelezee siri ya kuumwa kwake jinsi alivyochapwa na Yule Komando wa kijini, na kama haitoshi aelezee alivyofanikiwa kumlaghai Sharifa mpaka akakubali kuwa anakutana kimwili na Msigwa ambacho ndicho kilikuwa chanzo cha uhasama wao! na mengine yote ayaseme kinagaubaga

    Ilikuwa ngumu! Tena ngumu hasa ila kwakuwa alisikia kuwa baada ya kumaliza kusema ukweli kuna jambo litafanyaka huenda likamwokoa, akakubali Kishingo upande! akawaomba wazazi na mkewe wakutane mara moja kuna jambo anataka kuzungumza na familia

    Kwa nidhamu za wazee wa kitabora haikuwa rahisi kuingia chumbani kwa watoto wao, ikabidi sasa Suhail yeye nd’o ajisimikize atoke pale barazani na kuikuta familia nzima ikiwa imejawa na wahka wa kutaka kujuwa ni jambo gani jipya alilokuja nalo Ustadh yule kiasi cha kumfanya mgonjwa adiriki kuongea na familia nzima!

    Mzee Kusekwa na Mzee Fungameza waliketi katika kochi moja la kukaliwa na watu wawili huku wakitazamana na akina Mama Suhail, Mama Sharifa, na Sharifa mwenyewe walioketi katika kochi moja la kukaliwa na watu watu watatu

    Suhail na Ustadh Chaullah wao nao waliketi juu ya kochi moja la kukaliwa na watu wawili,

    Safu ikawa imekamilika!

    Kabla ya kuanza mjadala Ustadh akaomba achinjiwe kuku kisha damu iwekwe ndani ya Bakuli na kuletwa pale, pia akaagiza kuwe na bakuli lingine litakalokuwa na maziwa ndani yake. yote yawekwe hapo barazani.. zoezi hilo likafanyika, hakuna aliyestaajabu sana kwakuwa walimfahamu Ustadh Yule kuwa ni tabibu pia hivyo wakaamini kuwa kazi imeanza. Baada ya zoezi hilo kufana ndipo sasa tena Ustadh akafungua kikao kwa kuelezea mukhtasar wa kilichowajumuisha pale

    *****

    Mbezi, Dar es Salaam

    Katika nyumba nyingine ya Suhail inayokaliwa na Bi mkubwa, Shekhia bint Shamhurish iliyoko mbezi hali haikuwa shwari! Ni Baada ya msako mkali wa Komandoo Takadir Al-Harab kuzaa matunda kwa kugundua kuwa Mzee Sufian bin Shamhurish alijificha ndani ya nyumba ile ndipo akafanya ambushi ama uvamizi wa kushitukiza na kuwakuta wote wawili, mtu na mwanaye!

    Kama kawaida yake akaanza kutembeza ‘Mfueni’ wa nguvu, ilikuwa ni vita ya majini wenye uwezo mkubwa hivyo kwa mwanaadamu wa kawaida kukaa karibu na kuruhusu harusi ya kifo kunukia.. Shekhia ni mwanaadamu ambaye ana asili ya ujini kwa maana alichanganya damu hivyo hakuwa na ujanja wowote zaidi ya kukimbia tu na kuwaacha vidume wale japo alijuwa fika kuwa sasa mwisho wa Baba yake umewadia kwa jinsi alivykuwa akimsikia Baba yake huyo akielezea uwezo wa Takadir ambaye kwa mara ya kwanza amemshuhudia akipiga mapigo yasiyomithilika



    Wakati huko Mbezi kukifukuta na Ilala kukitokota, huko Ikulu ya Nchi mambo yalikuwa yameiva. Ndani ya chumba ha Siri walikutana kwa dharura Mhe Waziri Mkuu(Bw Khalid Bitebo), Mhe Waziri wa Ulinzi(Bw Lucas Shija), IGP(Cathbert Succa), Mkuu wa Majeshi na Mkurugenzi wa Usalama wa taifa(Bw Abdulrahman Mlenda)

    “Jamani tumekutana hapa kwa dharura tukiwa kama wapambanaji wakuu wa hili jambo.. tunahitaji kupeana mipango madhubuti ya kulimaliza jambo hili haraka na hatimaye watuhumiwa kumezwa na sheria… Hii vita ni kubwa sana ila kama tutatumia akili na maarifa tutaimaliza kama tunanawa vile.. sasa kabla sijatowa mwelekeo, hebu tupeane taarifa yoyote mpya kwa mwenye nayo,” Aliongea Mhe Waziri mkuu huku akiwatembezea macho wenzie

    “Iko hivi kuna vitu kidogo hatukupeana taarifa sasa vinanitatiza katika mapambano haya.. kuna watu wanaonekana kuhusika bila sisi kuwafahamu, kitu ambacho kinaweza kupelekea kuhatarisha usalama wao na wetu pia..” aliongea IGP Succa na kuendelea “..Kuna yule Sheikh kijana wa Tabora, Ustadhi Chaullah anapambana kusaidia jambo hili bila ya kufahamika yuko upadne gani, mimi nimemgundua baada ya kupoteza muda wangu mwingi kumfuatilia.. haya kuna Yule binti Sekretari aliyetekwa kule TuwaKadbra Production, Lillian Ufoo, ameonekana akiwa huru tena akipambana na maadui kitu ambacho kinazidi kutuacha na maswali bila ya majibu yake.. bila shaka ni vijana wetu, kama ni hivyo vije twafichana? Sote humu ni wanausalama kutoka katika vitengo vyetu tofautitofauti.”

    “Nikukate kauli IGP..” Alidakia Bwana Mlenda “..Ili kuokoa nguvu na muda.. hao wote uliowataja ni viajana wangu kutoka katika Idara ya Usalama wa taifa na ilibidi tuwatumie kuingilia jambo hili kutokana na uwezo wao na taswira zao katika jamii, Kupitia kwa Ufoo akiwa pale ofisini kwao kama Sekretari ndipo tuliweza kung’amua kuwa kuna mtambo unaoitwa Divier na unafanya kazi chini ya mtandao wa wasaka uraisi, na ndipo tukagundua kuhusika kwa marehemu Msigwa, na ni Ufoo huyuhuyo aliyebidi kutumika kuimarisha ulinzi pale hospitali baada ya kuona vijana wetu wa jeshi la Polisi wakipwaya na hatimaye tumeona alichokifanya ka muokoa mgonjwa na mengineyo kibao.. Yule Ustadh Chaullah ni kweli kabisa kuwa ni kiongozi wa dini wenye maarifa sana lakini kama mjuavyo idara yetu iko kila mahala hivyo naye ni Shushushu wetu mbobevu mwenye taaluma kubwa ya upelelezi na makabiliano kama mlivyoona alichomtenda Yule mshenzi Joram, na tuliamua kumtumia Ustadh kwakuwa kwa jinsi taswira yake katika jamii ilivyo isingekuwa rahisi kugundulika na kweli amelifanya hilo..” Kikapita kimya cha muda mfupi huku kila mmoja akitikisa kichwa kumwelewa Mkurugenzi

    “Ok, good kuhusu vilivyomo ndani ya Laptop hakuna jipya sana zaidi ya mipango yao tu ya kuikwaa Nchi.. pia tumegundua kuwa Mtambo wao huo wa Divier uko kule Gongo la mboto kwenye lile jengo lao, Mtambo huo pamoja na Joram ndege ni bidhaa aghali kuliko zote wanazomiliki watu hawa, bahati nzuri tayari bidhaa moja iitwayo Joram Ndege tunayo mikononi mwetu, Pia tumepata listi ndefu ya kundi lao wote wanaohusika ikiwa ni pamoja na wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa isipokuwa watu wawili tu ambao ndio vinara wao bado hatujawafahamu maana majina yao wanayoyataja wanatumia sana alama za kijasusi.. Sasa labda IGP atujuze kama wamembana huyo Joram na amecheuwa ukweli wowote?” Alihitimisha Bw Mlenda, Jopo zima likamgeukia IGP Succa ambaye aliwakatisha tama

    “Hakuna lolote alilokubali kusema, ameshateswa sana bila mafaniko.. yuko tayari kufa kuliko kusema lililo moyoni mwake”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ok, sio kesi sana! iko hivi katika maelezo tuliyoyagundua katika ile Flash ya Joram ni kwamba Riport za mipango yao yote ya siri iko ndani ya Laptop za Viongozi wao wawili wanaondaliwa kuwa Raisi na Waziri Mkuu wake, Kiongozi wa kwanza wanamwita 5O51-10S na mwingine ni 42&2c”

    “Tutawajuaje hao watu wanaotumia majina ya mficho?” Alihoji waziri mkuu na hapohapo akajibiwa tena na Bw Mlenda

    “Huenda tukawajua leo hii hii, tunachohitaji kukifanya ni kuitisha kikao cha dharura kitakachowajumuisha hao washukiwa wote.. na hapo ndipo tutakapo wakamata kwa upelelezi wa mwisho,”

    “Ikitokea tumeshindwa kuwapata kati yao hauoni tutakuwa tueyaanika mambo haya mapema sana kiasi cha kudhoofisha mpango kazi wetu?” Alidakia Waziri wa Ulinzi

    “Kwa mpango ulivyo tutawakama wote.”

    “Unapendekeza kikao kiwe wapi na saa ngapi? na tuwaalike akina nani?” Waziri Mkuu alimhoji mkurugenzi wa usala wa taifa aliyemjibu kwa mkato tu

    “Nusu saa kutoka sasa tukutanie ofisini kwa waziri wa ulinzi ili tusiwashitue watuhumiwa, tunawahitaji watu wachache tu; Mhe Sostenes Miti(Waziri wa Fedha), Mhe Shamsuddin Kisima(Waziri mambo ya nje), Mhe Fortunatus Mwita(Waziri wa nishati na madini) na Mhe Katinda Kuya(Kamanda wa Polisi, kanda maalum)” Akamaliza Bw Mlenda na kuungwa mkono na wajumbe.. taarifa ikaungwa mkono, Kikao kikaahirishwa!

    *****



    “Wazazi wangu kwanza naomba mtuwie radhi kwa kuwaitisheni kikao hapa, hatukuwa na namna yoyote kwakweli zaidi ya kufanya hivi..” Aliongea Ustadh Chaullah kwa utulivu ikiwa ni sehemu ya utangulizi wake katika kulituliza baraza huku macho ya wanafamilia yakimtazama yeye “..Sote twafahamu hali ngumu anayoipitia Suhail katika kipindi hiki, ni hali ngumu kweli na si maskhara, hatuna budi sote kwa pamoja kushirikiana ki mwili na ki akili ili kuhakikisha jambo hili linamalizika, hakika litamalizika tu kwa kudra zake Mola!.. Kubwa zaidi ni kwamba katika yote yaliyotukia ama yanayoendelea kutukia bila shaka pana jambo ndani yake, na hilo jambo kutokana na uzito wake ikiwa ni katika kulipatia ufumbuzi imebidi Suhail leo aliweke hadhir, jambo ni habari ndefu, ya kusisimua na kuumiza ila siku zote ukweli humweka mtu huru hivyo hana budi kulidadavua mbele yenu mwanzo mpaka mwisho..” Kimya kiliendelea kunawiri huku kila mmoja akitamani Ustadh amalize kuongea ili sasa wasikie hicho anachotaka kukiweka hadharani Suhail, lakini alichokikusudia Ustadh ni kuhakikisha kuwa anawaandaa kisaikolojia ili watakapopata mkasa ule wa ajabu waweze kuhimili “Kutokana na uzito wa mkasa wenyewe na ukizingatia kwamba anayetaka kuusimulia kwa sasa hali yake ni ta’abani hivyo sisi yatupasa kumsikiliza kwa umakini na kumliwaza kwa kilichomkumba. Sasa nisiwachoshe sana maana sisi masheikh ni watu wa majukwaa naweza kujikuta naongea mpaka muda unatuishia hapa!.. Karibu bwana Suhail” Alihitimisha Ustadh Chaullah na sasa ikawa ni zamu ya Suhail, Baraza nzima ilitulia huku macho ya wasikilizaji yakihamia kwa Suhail sasa! Ilichukua kama nusu dakika kabla ya Suhail kuanza kusema chochote, ni kama aliyekuwa anatafuta pa kuanzia

    “Awali ya yote Wazazi wangu pamoja na mke wangu nawaombeni radhi sana kwa haya nayokusudia kuwaelezeni, ni kadhia mbaya na ngumu kuelezeka ila kwa uzito wake sina budi kuyaweka hadharani kwenu kama wanafamilia, narudia tena kuwa nawaombeni mnisamehe sana.” Sauti ya Suhail ilikuwa imejawa na kitetemeshi mithili ya mtu aliyejawa na dukuduku ama hasira kali moyoni, baada ya kushusha pumzi sasa akaanza kutiririsha mkasa mzima hatua kwa hatua kuanza alivyokutana na Shekhia Chuoni na kujikuta akijiingiza katika mahusiano naye kutokana na hitajio lake la pesa kutoka kwa dada yule, akaelezea jinsi alivyoamuwa kuachana naye na kurejea Tbr baada ya kumaliza masomo yake ambapo akiwa ndani ya gari ndipo akakumbwa na ile ajali iliyomkutanisha rasmi na Mzee Shamhurish.

    Ilikuwa ni habari yenye kusisimua masiko ya msikilizaji yeyote, ni kama Simulizi iliyosukwa kiufundi kwa kuyapanga matukio katika mtiririko wa taharuki ya hali ya juu kiasi cha kumfanya msikilizaji atamani kujuwa kitakachojiri baada ya tukio lililopo hewani muda ule!

    Suhail akazidi kutirisha mkasa, na safari hii alikwishafika katika maajabu ya Mzee Shamhurish kuanzia alivyomkabidhi pete, pesa, na hata alipomtokea usingizini.. Simulizi ikaanza kuwa chungu sasa huku hofu ikijikita katika mioyo ya wasikilizaji, kila tukio lilipoanza kusimuliwa lilionesha kuwa ni zito kuliko lililotangulia.. Akaelezea hatua kwa hatua jinsi alivyofanikiwa kukutana na Mzee Atrash ambaye alimpa mkasa mzima wa akina Shekhia, mkasa uliomfanya Sharifa achanganyikiwe kuona kumbe anashea mume na jinni mtu… akajikuta akimshika mama yake kwa nguvu akiwa amejawa na woga vibaya! Alipoanza kuhadithia sasa jinsi alivyofungishwa ndoa na Shekhia na alivyoanza kumfanyia hila Sharifa ili asimuoe tena uzalendo ukamshinda Sharifa baada ya kububujikwa na machozi akaanza sasa kulia kwa Sauti

    “Sharifa, Unafanya nini Sasa? Nilitoa tahadhari gani wakati tunaanza?” alikemea Ustadh Chaullah, Suhail akanyamaza kidogo wakati Sharifa anamalizia kujifuta machozi kwa msaada wa kanga ya mama yake ndipo akaendelea tena kuelezea maisha yake yalivyokuwa alipolazimika kumwoa Sharifa lakini kwa kumlaghai kuwa yeye alikuwa mbovu hivyo kutokukutana naye kabisa, kitu kilichozua mgogoro mkubwa baina yao kiasi cha kuhatarisha ndoa yao

    Aliposimulia kuhusu Matukio aliyowahi kuyafanya kwa hisani ya ile Pete ya ajabu, na alipomalizia kwa tukio lile la kumlaghai Sharifa akubali kuwa akikutana kimwili na msigwa ili aweze kupata utulivu, Mzee Kusekwa alikuwa akitetemeka ndani kwa ndani mithili ya mwanafunzi wa shule ya msingi aliyenyeshewa na mvua kubwa, Mzee Fungameza yeye alikuwa akisali kimyakimya kumwomba Mungu tukio lile iwe ni kama yuko ndotoni tu,

    Haikuwezekana, ilikuwa ni tukio la kweli!

    Mama Suhail naye akashindwa kujizuia akaanza kulia, akamwambukiza kilio na Mama Sharifa, ikawa ni kilio cha haja! Wakabembelezwa na kutulia, Suhail akaendelea kuelezea mkasa wote huku akionesha kuelemewa na historia ya mkasa wake mwenyewe, akaanza kusimulia jinsi alivyojijengea uaduia kwa Msigwa na Shekhia kwa kufanya tendo lililopelekea ujauzito kwa Sharifa, akaelezea alivyopokea kichapo kutoka kwa Komandoo Takadir Al-harabi..

    Akiwa katikati ya simulizi yake, mara Pete yake ikabidili rangi na kuwa Nyekundu, akashituka na kuitupia macho, kila mmoja akamfuatishakuangalia kidoleni mwake na kushuhudia rangi ile iliyowaogopesha vilivyo! Maana alikwishawaeleza jinsiPete yake inavyobadilisha rangi kutokana na matukio kadhaa. Akiwa hajajua afanye nini ghafla king’ora cha getini kikalia, akasikika Yule msaidizi wakazi akiufungua, hawakutana mgeni kwa wakati ule wakihofia kuvurugiwa kikao, lakaini kabla hawajatanabahi Mgeni alikwishawasili mpaka pale barazani, Mgeni alikuwa akitweta sana kama aliyekimbizwa kwa umbali mrefu sana, Suhail alipomwona tu mgeni yule akajikuta amesimama kutoka pale kwenye kochi alipokuwa ameketi, akataka kukimbia, lakini hakufanya hivyo! Halikadhalika Sharifa naye alibutwaika kumwona dada Yule aliyevamia kikao chao, kwa woga akaanza kupiga kelele.. Mtungo wa maswali ukawavaa waliosalia, hawakuelewa iweje Suhail na Sharifa wamwogope mtu Yule ilihali haoneshi hatari yoyote zaidi ya kuonesha mchoko na dhiki zinaozohitajia msaada.. Mzee Kusekwa akavuta kumbukumbu na kuing’amua taswira ya dada Yule aliyepata kumwona siku Fulani kule hospitali alikolazwa Sharifa wakati anaugua, Naam ndiye yeye msichana aliyewapita bila salamu kiasi cha kuwaachia mjadala juu yake, alikuwa ni Shekhia bint Sufian

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Suhail naomba unisamehe mume wangu, niko chini ya miguu yako.. maji yameshamwagika huko, Baba atauawa muda wowote kuanzia sasa.. Ala’ala jitahidi tumsaidie,” Aliongea Shekhia huku akimsogelea Suhail pale aliposimama na kumpigia magoti

    “Huyu naye nani we Suhail?” Alihoji Mzee Kusekwa

    “Jamani huyu ndiye Shekhia.” Suhail alijibu huku akiwa hajui afanye nini? Aliposikia kuwa Mzee Sufian bin Shamhurish amevamiwa na adui ndipo alipopata jibu la ile rangi ya hatari iliyodhiri katika Pete yake maana hakupata kuiangalia kitaalam ili kujuwa kinachotukia muda ule

    “Ndiye yeye huyu! Ndiye huyuhuyu jamani.. huyu ndiye aliyenitokea kule hospitali na kunimulika na miale ya pete yake,” Aliongea huku akilia Sharifa, alipotaja tukio hilo kila mmoja sasa akaingiwa na hofu! Hakuna aliyeendelea kukalia kochi, wote walisimama. Ustadh akamshika mkono Shekhia na kumwinua pale chini alipokuwa amepiga magoti kisha akamkalisha kwenye kochi alilokuwa ameketi yeye na Suhail, halafu akawataka wote waketi pia, Wakatii!

    “We’ nd’o Shekhia?” alisaili Ustadh

    “Ndiye mimi,” Shekhia alijibu huku akiendelea kutiririsha machozi

    “Ni kweli wewe ndiye uliyomtokea hospitali Sharifa?”

    “Ni kweli.”

    “Ilikuwaje mpaka ukafanya jambo lile? kuwa mkweli tafadhali.. na usijaribu kuficha kitu.” Kauli ya Ustadh ukamfanya Sharifa apatwe na kigagasiko cha mdomo, hakuweza kujibu chochote mpaka alipoisikia kaluli ya mumewe, Suhail “..Shekhia waeleze kila kitu” Ndipo sasa Shekhia kwa hofu na mashaka akaanza kuelezea kila kitu, kunza alivyomsababishia Sharifa ugonjwa ule wa kiharausi na mpaka alipomfuata kwa mara ile kule hospitali akiwa na dhamira mbaya, akaelezea jinsi alivyoingiwa na hofu na huruma kiasi cha kuamua kumponya badala ya kumdhuru.

    Muda wote huo Pete iliendelea kung’aa kwa wekundu ikiashiria hali ya hatari! Kufuatia hali hiyo ikabidi Ustadh akamtishe Shekhia

    “Vua haraka hiyo pete yako, muda wa kafara umefika” Ustadh alimwamuru Suhail akiamini kuwa sauti yake itafiwafikia walengwa, baada ya kuivua akamwambia aitumbukize ndani ya bakuli mojawapo kati ya yale mabakuli mawili ambapo moja lilikuwa na damu iliyokwishaanza kuganda, na linguine lenye maziwa ndani yake kisha akayatenganisha; Moja akaliweka kwenye kona ya moja ya pale barazani na linguine akaliweka juu ya meza kubwa ya chakula, Ustadh akamsogelea Suhail sikioni na kumnong’oneza jambo kwa muda wa dakika kama tano hivi, Suhail akaonekana kuafiki huku akiwa ni aliyejawa na hofu kubwa huku wengine wakiwa mashuhudawa matukio yale ya kustaajabisha

    Wakarejea na kuketi kisha tena Ustadh akamtaka Shekhia aelezee ilikuwaje akamtokea Sharifa na kummwachia ile miale inayosadikiwa kumponya, Shekhia akaweka wazi kila kitu mpaka jinsi alivyomsababishia ule ugonjwa wa kiharusi na baadaye kwenda hospitali kummalizia lakini akajikuta anamwonea huruma na kuamua kumponya badala ya kummaliza, watu wote wakabaki midomo wazi!

    Wakati hayo yakiendelea ghafla hali ikabadilika, ukasika upepo mkali ukivuma huko nje, vumbi la haja likitimka, milango ikijibamiza, Cha ajabu upepo ule ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kufanya uingie mpaka mle barazani.. ilikuwa ni kimbunga kikubwa kilichofuatiwa na harufu kali ya marashi iliyotanda kwa takribani dakika tano!

    Mara tena mlango uliokuwa umejifunga ukafunguka kwa namna ya ajabu sana, ni kama vile hicho kimbunga huko nje kiliupiga kwa nguvu, ulipofunguka tu ghafla wakaingia kwa kasi wanaume wawili kama vile wamesukumwa kwa kasi ya umeme, ama waliokuwa wakigombania nafasi ya kuingia humo ndani, wakaangukia katikati ya baraza ile, japo walionekana kuwa hoi bin Taaban wakaanza kupigana vibaya sana huku cheche za moto zikidhihiri kutoka katika miili yao kama ilivyo cheche za moto utokanao na kuchomelewa vyuma!

    Hali ya Baraza ikachafuka tena, Suhail, Shekhia na Ustadh Chaullah walielewa kilichokuwa kikitendeka, waliwatambua wanaume wale wawili kuwa ni Mzee Sufian bin Shamhurish na Komandoo Takadar Al-harab.. Vilio na kelele za woga zikazizima kutoka kwa wanafamilia waliokuwa wametaharuki huku kila mmoja akijaribu kutaka kutoka nje, Haraka Ustadh akaukimbilia mlango na kuufunga kwa funguo kisha kuiweka funguo kwenye mfuko wa kanzu yake,

    Hakuna mtu kutoka!

    Vidume wale wakachakazana sana mpaka wakaishiwa nguvu, ikawa sasa hawana hata uwezo wa kusogeleana zaidi ya kutazamana kama majogoo tu! Lakini hali ya Mzee Sufian nd’o ilikuwa mbaya zaidi kuloko Takadir… Ghafla Komandoo Takadir akageuza macho yake na kuliangalia Bakuli lile lenye damu likiwa katika pembe ya nyumba ile, Akaangua kicheko cha nguvu na kusema “Suhail wewe ni mjinga sana, unatoa kafara ya damu ya mbuzi badala ya damu ya Mama au Baba yako.. Tazama sasa hatimaye leo unashuhudia kifo cha Sufian na kisha utashuhudia kifo chako mwenyewe kabla ya mimi kurejea budha leo hii nikiwa na Pete yao” Mzee Kusekwa na Mkewe wakatazamana kusikia damu yao nd’o ilipaswa kutumika kama kafara ya Pete ile ya ajabu, Familia nzima ikatazamana huku kila mmoja akiwa amebarizi kivyake kwa hofu na mashaka, ndipo tena wakamshuhudia komandoo akilisogelea Bakuli ili aichukuwe Pete, Suhail akiwa aliyejawa na woga akajikuta akikimbilia pembeni kumpisha Komandoo aliyekuwa akijongea kwa shida na tabu kutokana na mchoko wa mpambanoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “NOOO SUHAIL, USIMRUHUSU ACHUKUWE PETE,” Alilalama Mzee Sufian akiwa hajiwezi kwa N’de wala Sikio, Suhail alimtupia jicho tu na kumpotezea kama hakumsikia,

    Wakati sasa Komandoo Takadir amelifika bakuli lenye damu, aliachia tabasamu na kuingiza mkono wake ndani ya bakuli hilo, Suhail naye alikuwa amesimama jirani na meza ambayo juu yake kuna lile bakuli la maziwa, akaingiza mkono wake ndani ya bakuli lile huku akimtupia jicho Ustadh Chaullah aliyempiga ukope akimuashiria kufanya jambo fulani

    Ghafla tabasamu la Takadir likayeyuka na nafasi yake kuchukuliwa na simanzi iliyochanganyika na hofu, akamgeukia Suhail na kumkuta akimalizia kuivaa Pete yake.. Kumbe pete haikuwa kwenye lile bakuli la damu kama ambavyo Takadar alidhani na badala yake iliwekwa kwenye bakuli la maziwa ikiwa ni hila na mpango kabambe uliosukwa na Ustadh Chaullah! Kuna siri kubwa ndani ya maziwa, Siri ya kiafya na kitabibu, hivyo siri hiyo ilipotumika kitaalam ilimfanya hata Takadir na ukomandoo wake wa kijini aamini kuwa ndani ya bakuli lenye damu ndipo ilipo Pete.. Sasa kabla Komandoo hajafanya lolote tayari Suhail alikwisha kibenjua kile kidubwasha cha maangamizi kilicho nyuma ya Pete ile na kumwelekezea Takadir palepale alipo, Ikatoka miale ya ajabu, miale ya moto iliyochanganyika rangi nyekundu, kijani, na nyeusi.. Ulisikika ukulele mkali kutoka kwa Komando Takadir mpaka hofu ikamjaa kila mmoja aliyekuwa akishuhudia tukio lile

    Komandoo Takadr Al-Harabi alipatwa na maumivu yaliyochanganyika na ghadhabu zilizomtuma kumsogelea Suhail na kumuangamiza, lakini alikwishachelewa, hakupata nafasi ya kusogea japo hatua tatu, akateketea mpaka akabaki jivu tu.. Huo nd’o ukawa mwisho wake! hakuna aliyeamini.

    Suhail akamkimbia Ustadh na kumkumbatia kwa faraja!

    Wakati zoezi hilo linakamilika ndipo sasa Macho ya Mzee Sufian yakagongana na yale ya Fungameza aliyekuwa akimtazama muda mrefu

    “Bwana Fungameza!” Aliita kwa mshangao wa hali ya juu Mzee Sufiani na kuacha taharuki ya aina yake,

    “Sufiani? Ni wewe ama naota?” Mzee Fungameza alihoji akiwa haamini

    “Ndiye mimi kaka, najuta kwa yote niliyokufanyia.. nisamehe sana.”

    “Amaa kweli Malipo ni duniani akhera yaenda hesabu tu.. Leo umedhalilika mbele yangu, Yule mtu uliyenikarahisha, ukanidhalilisha na kuniahidi kuwa hakuna atakayekuweza wewe! hatimaye umewezekana… Haya Amanda yuko wapi?”

    “Ni mkasa mrefu sana uliotokea kaka, ila kwa kifupi ni bora hata ningekuachia tu Amanda wako maana kuwa naye ndiko kulikonishusha kabisa hadhi yangu mpaka leo kuwa hivi.. na hatimaye naye akauawa kinyama na kiumbe huyo mshenzi aliyeteketea hapo sasa hivi.. ila nilibahatika kupata naye mtoto mmoja ambaye ndiye huyo Shekhia.”

    “Khaaa! Amanda amekufa?.. Na huyu binti naye ni mtoto mwingine wa Amanda? Hii sasa ni aibu ya mwaka! Fedheha.. ila nilimkanya Amanda kuwa asipapatike na fedha za mtu asiyemjuwa lakini akanipuuza, hakujuwa kama anakikimbilia kifo, laity angejua anajiingiza katika mahusiano na Jini pengine angenisikiliza.. sasa maji yameshamwagika! Wanasema asiyesikia la mkuu, huvunjika guu!”

    Kikapita kimya cha muda mfupi kabla ya Ustadh Chaullah kutupa swali

    “Kwani mnajuana ninyi?” Ustadh alivunja hamu ya kila mmoja ya kutaka kujuwa endapo wanafahamiana vipi,

    “..Ndio, tena sana tu! Enzi za uhai wa ujana wangu nilipata kuishi na mwanamke fulani aliyeitwa Amanda.. nilijidanganya kuwa tunapendana kumbe nilipenda peke yangu.. Nilijidanganya hivyo kwa jinsi mwanamke yule mrembo wa kipindi kile alivyowakataa wanaume wengi na kuangukia mikononi mwangu na hatimaye tukaishi pamoja na tujaaliwa mtoto wa kike ambaye ndiye huyu Sharifa.”

    “Mungu wangu! Ina maana Shekhia na Sharifa ni ndugu? tena wa mama mmoja!” Aliropoka Suhail bila ya kutegemea, mara akaishiwa nguvu na kujikuta anaporomoka juu ya kochi kama kiroba…

    Aibu iliyoje kwa kila Baba, Mama, Kaka, Dada, nk kushuhudia ndugu wawili wa mama mmoja kuwa ni wake wa mwanaume mmoja! halafu mnakuja kugundua hilo mkiwa nyote mu wajawazito!

    Kilio kikazuka upya, kilio cha maumivu na fedheha!

    Ustadh akawatuliza na kumtaka Mzee Fungameza aendelee kutoa kumbukumbu zake za muhimu



    Ndani ya ofisi ya waziri wa ulinzi walisheheni vigogo wa Nchi hii, Alikuwepo Mhe waziri mkuu mwenyewe, Waziri wa fedha, IGP, Waziri wa ulinzi, Waziri wa nishati na madini, Kamanda wa Polisi kanda maalum, Naibu waziri wa fedha, Waziri wa mabo ya Nje, na Mkurugenzi wa usalama wa taifa. Pia walikuwepo maofisa wawili vijana wa Usalama wa taifa! Wote waliketi kwa kuizunguka meza moja ndefu iliyo katikati yao huku kila mmoja akiweka amekumbatia vitendea kazi vyao.. mwenye simu, mwenye laptop, nk

    “Awali ya yote poleni kwa majukumu, na kwa usumbufu wa kuwaiteni ghafla japo yote ni katika majukumu ya kulijenga taifa..” Alianza kufungua kikaorasmi Mhe Waziri Mkuu “..Kikubwa kilichotujumisha hapa ni kuhusu usalama wa Nchi yetu, kufuatia uchaguzi mkuu ambao uko jirani kabisa kumezuka vikundi na mitandao ya wasaka uraisi ambao hufanya hila chafu na ikibidi hata hudiriki kuuwa ili tu kujiweka katika mstari mzuri wa ushindi.. Sasa kufuatia hali hiyo mambo yamekuwa makubwa inabidi sisi tulioitana humu, ambao tunaaminiana, tushirikiane kuwang’amua na kuwashughulikia wauuzi hawa wachache..” Wakati waziri mkuu akiendelea kutiririka, Mkurugenzi wa Usalama wa taifa Bwana Mlenda alikuwa akiwatembezea macho waheshimiwa wote ikiwa ni katika mbinu zake za kumgundua mhalifu

    “…Kuna mtandao mmoja mkubwa unajiita Black Scopion umefikia hatua ya kuwashirikisha mpaka wauaji wa kukodisha kutoka nje na mitambo haramu ya Divier kwa ajili ya kufanikisha azma yao.. tumefanikiwa kumkamata muuwaji wao aitwaye Joram Ndege..” Neno Joram Ndege lilipokelewa kwa hofu na mashaka karibu na kila mmoja wao japo kwa namna tofauti.. haraka Mkurugenzi wa usalama wa taifa Bwana Mlenda alishakibaini kitu kutoka kwa Mhe Sostenes Mitti(Waziri wa fedha)“… Ila kwa bahati mbaya pamoja na kumtesa sana awataje wenziwe hakukubali mpaka akatufia mikononi,” Alidanganya hapo Mhe Waziri Mkuu kama alivyoelekezwa na Bwana Mlenda ambaye muda huo sasa alikisoma kitu kingine katika macho ya Mhe Fortunatus Mwita(Waziri wa Nishati na Madini)..”

    “Katika Laptop yake tumefanikiwa tu kujua hilo jina la kikundi chao na malengo yao ya kuukwaa uongozi kwa njia haram, tukagundua jinsi walivyomuuwa Yule mwanahabari baada ya kutofautiana naye, tukagundua kuhusu huo mtambo wenye kubumba meseji na kung’amua mawasiliano ya watu wengine kupitia simu zao.. zaidi ya hapo mambo mengine yote yaliandikwa kwa mtindo wa kijasusi sana, kitu kilichozidi kututilia ugumu wa kuwajua wahusika na eneo ulipohifadhiwa mtambo huo.. mathalani hao viongozi wao wanajiita 5051-10s na 42&2c na kwamba siri zote zimo katika Laptop zao..Sasa hii kama taarifa tumeona tuwashirikishe nyote kutokana na umuhimu wenu ili kila mmoja atowe maoni yake.” Alihitimisha Mhe Waziri Mkuu na kuwatazama wajumbe wa kikao kwa macho ya kuhitaji kusikia chochote kutoka kwao

    “Hili si jambo dogo.. ni jambo zito na bay asana hivyo si la kukurupuka, yatupasa tupate muda wa kutosha kila mmoja alichunguze ili tutakaporejea hapa kwa mara ya pili tuwe na pa kuanzia…” Aliongea Mhe Mitti, na kudakiwa na IGP “Mimi sikubaliani sana na Mhe Mitti japo ameongea kitu cha maana sana kuwa tunahitaji muda, ila inabidi kwa kupitia ushauri na maoni yetu hapo huenda ikawa ni mwanzo mzuri wa kuwajua hao mabazazi”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naogopa kuongea mengi kwa kuwa hata humu hatujafahamiana huenda ukakuta hao wahusika hata humu yumo mmoja wao hivyo naomba kushauri kitu hapa.. tuhakikishiane kuwa humu hakuna hata mmoja wao ndipo tuendelee,” Aliongea bwana Mlenda huku akipepesa macho yake kwa wajumbe alioanza kuwashitukia

    “Tutahakikishiana vipi sasa? Kwa kutamka tu? Hiyo itakuwa Ngumu mtu kujitaja” Alijibu waziri mkuu na kuzua mjadala mpana mle ofisini

    Mjadala ulichukuwa muda mrefu kidogo kabla ya Suluhu kupita kwamba.. kama yupo mwenye uwezo wa kung’amua majina yale ya mficho asaidie kabla hawajapambana.. Ndipo kijana mmoja kati ya wale wawili wa usalama wa taifa waliohudhuria akapita mbele na kuomba kutoa utaalum na uzoefu wake katika majina hayo ya mficho.. akaruhusiwa! Akavuta kijiubao kidogo kilichokuwa pembeni, akachukua na kalamu maalum ya kuandikia akaanza kuyanyambua majina yale

    *****

    “…Basi Sharifa akiwa bado mdogo ndipo huyu Sufian alipoibuka na kunipokonya mwanamke Yule niliyemjali na kumthamini, Pesa za Sufiani zikamhadaa Amanda, nilijaribu kupambana na Sufian nikiamini kuwa nitamshinda lakini kumbe nilikuwa natwanga maji kwenye kinu.. nikakumbana na madhila mazito mpaka nikanyoosha mikono, na sikuwaona tena mpaka leo hii..” Aliendelea kuongea Mzee Fungameza, huku mara kwa mara akitulia kidogo kupisha dukuduku lililomkaba kooni lipite maana angeendelea kuongea angevujisha machozi, kitu ambacho hakutaka kukiruhusu mbele ya wanawake, Akaendelea “…Kilichoniuma mimi ni jinsi nilivyopoteza muda wangu kwa Amanda.. Amanda aliingia Nchini kama mfanyabiashara lakini kiukweli hakuwa na dhamira ya biashara bali alikuja kumtafuta nduguye aliyezaliwa naye pacha! Nduguye huyo alipata kuniambia jina lake aliitwa Nadege Ndatabaye, kama ambavyo yeye aliitwa Amanda Ndatabaye.. tukiwa bado tuko katika jitihada za kumsaka huyo nduguye ndipo akapata ujauzito, ikamlazimu kusitisha kwanza biashara zake mpaka alipojifungua akiwa chini yangu kwa kila jambo, ndipo sasa alipoibuka huyu Suf..” Kabla Mzee Fungameza hajamaliza kuongea ikasikika sauti kali ya kilio, kilio cha uchungu na kutaabika.. alikuwa ni Mama Suhail akilia na kugaagaa sakafuni huku nguo zikimtoka maungoni, Mama Sharifa akajitahi kumzuia huku akimfunika nguo zake..

    “Mama nini tena sasa?” Alihoji Ustadh Chaullah

    “Inaniuma, inaniuma mie jamani! leo tumekumbwa na aibu ya mwaka.. sijui kwanini Mungu ameamua kutushushia mkasa huu..” aliongea huku akilia Mama Suhail, akaendelea “..Mimi ndiye Nadege Ndatabaye, na ni kweli nina pacha wangu aitwaye Amanda Ndatabaye niliyepotezana naye huko Rwanda tukiwa wadogo sana baada ya wazazi wetu kuuawa kikatili, na kupelekea mimi kuchukuliwa na mzee mmoja wa kitanzania na kuja kunilea huku wakati Amanda alibaki kule Rwanda akilelewa na Mwanakijiji mwenzetu wa kule.. kadri tulivyokuwa tunakuwa kiUmri tukawa tunatumiana salamu kabla ya kupotezana kabisa kufuatia kifo cha huyu mzee aliyekuwa akinilea huku Tanzania, Mzee Yule ndiye alikuwa kiuanganishi chetu kama daraja kufuatia safari zake za mara kwa mara katika nchi hizi mbili..” Mama Suhail akaendelea kulia na kusaga meno huku akibwabwaja maneno “Kumbe masikini ndugu yangu alikuja kunitafuta, pengine angenipata ningemzuwia kujiingiza katika tama hizi” Ilikuwa ni habari mpya iliyozua mshikemshike mwingine, Kumbe Amanda ambaye ni Mama yao na Shekhia na Sharifa pia ni Pacha wa Mama Suhail, hivyo Suhail ni ndugu yao kabisa na akina Shekhia.. Mzee Kusekwa aliikumbuka historia hiyo kutoka kwa mkewe kwakuwa mara kadhaa wamekuwa wakijadiliana kuhusu utaratibu wa kumtafuta huyo Amanda

    Hakika ilikuwa ni siku ya fadhaa!

    Safari hii ilikuwa ngumu sana kunyamazisha kelele za vilio kutoka kwa akina mama hawa pamoja na watoto wao.. Shekhia naye akaanza kulia huku akimsogelea Sharifa na kumpigia magoti amsamehe kwa kila kilichotokea. Wakati hayo yakiendelea kuwachoma moyoni likazuka jingine jipya, Mzee Sufian aliyekuwa akipambana na roho yake, ilimshinda na kumponyoka, Akaaga dunia! kilio kikubwa kikaibuka kwa Shekhia, huku hofu ikiwavaa waliosalia.. ikawa sasa kila mmoja analia na lake! Ustadh akamwinua Suhail na kumuamuru afanye jambo, bila ajizi akainuka na kuliendea lile bakuli lenye yale maziwa yaliyowekewa Pete pale mwanzo, akalichukuwa na kuumwagia maziwa mwili wa hayati Sufian bin Shamhuri ambao ulikwisha tokwa roho, Mwili ule ukaanza kuyeyuka mithili ya ujiuji Fulani.. na baada ya muda ukakauka na kuwa jivu kama ilivyokuwa kwa Takadir Al-harab

    “Hivyo ndivyo majini wanavyotoweka ama kufa, hatuwezi kuwazika kama tufanyianavyo sisi.. hivyo huo ndio mwisho wao.. hakuna maiti tutakayoendelea kuwa nayo humu ndani kisheria.. Poleni kwa yote yaliyowakuwa.. hivi ndivyo kadari ya Mungu ilivyotukia,” Aliongea na kuendelea “..Kila mmoja ameshajuwa kilichojiri kuanzia mwanzo mpaka sasa, huu ndio mwisho wa mkasa huu.. sasa ninyi kama wanafamilia ni jukumu lenu kukaa pamoja na kutafakari juu ya kadhia hii, hakika pana mafunzo makubwa sana kwa wenye kutafakari.. cha msingi machungu na dhoruba zilizotukumba kwenye mkasa huu zituimarishe na zisitubomoe, situfanye tuwe majasiri na wapambanaji wakubwa wa changamoto za namna hii katika jamii zetu…”

    “Naomba niwaage wapendwa wangu,” Suhail alidakia wakati Ustadh Chaullah akiendelea na mazungumzo, familia nzima ikamsogelea kwa hofu na mashaka

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Majina ya mficho huwa ni mchezo mdogo sana na wa kipuuzi tu, na wa kisanii hivyo haihitaji akili nyingi sana kuufumbua japo umakini unahitajika.. kwa mfano, wapo ambao hutumia namba za idadi ya herufi za majina yao ili kuficha majina yao, wengine hutumia namba za kisanii ambazo husimama badala ya herufi na kuleta maana ya majina yao, na wapo ambao hutumia tarakimu za majina yao kinyumenyume nk.. sasa kwa hapo tutaziangalia hizi namba ambazo zitatusaidia kupata njia ya kutupelekea kuyajua majina husika kama si kuyafahamu moja kwa moja..” Ukumbi mzima wa ofisi ulikuwa kimya kama kwamba hakuna watu, jasho ziliwafumka waheshimiwa licha ya kiyoyozi mwanana kilichokuwa kikiwapuliza, kijana akaendelea “..Nitaanza na huyu 5051-10s.. hiyo tano ya mwanzo ni namba ambayo kimuundo inaweza kufanana na herusi “S”, hiyo Sifuri nayo inafanana na herufi “O”, tano ya pili nayo ni kama ile “S” ya mwanzo, wakati hiyo moja inafanana na herufi “I”, hiyo kumi unaweza kuitamakwa kizungu ukaiita “TEN” Hivyo ukizijumlisha herufi hizo herufi zenye kufanana na hizo namba utapata kitu ‘SOSITEN’ na Ukiongeza na hiyo herufi ndogo ya “s” ambayo hutamkika “es” utapata kitu kama “SOSITENES” ambalo ni jina la mtu..” Ukumbi mzima ukamgeukia Mhe Sostenes Mitti(Waziri wa fedha) Hofu na mshawasha vikazizima, kisha kijana wa usalama akaendelea

    “… nikija katika hilo jina mficho la pili ambalo ni 42&2c.. unaweza kucheza na namba na matamshi tu kisanii.. mfano hiyo “4” kwa kizungu inaitwa ‘four’ japo inatamkwa “FO”, hiyo mbili inaitwa ‘two’ japo inatamkika “TU” hiyo nane mkunjo ni alama inayomaanisha ‘And’ ambayo kwa Kiswahili hutamkwa “NA” Kisha inafuatiwa “2” ambayo hutamkwa “TU” halafu inakuja “c” ambayo kwa Kiswahili hutamkika “si” ukizijumlisha herufi hizo utapata kitu kama “FOTUNATUSI” Ukumbi mzima ukamgeukia Mhe Fortunatus Mwita ambaye moyo wake ulishindwa kuhimili mapigo yake na kujikuta akiishiwa nguvu na kuanguka chini akiwa amepoteza fahamu.. wakiwa wamekumbwa na taharuki ile ndipo Mhe Sostenes Mitti aliona kuwa maji yameshazidi unga, liwalo na liwe! Akainama kama anaefunga kamba za viatu vyake na hapohapo akainuka akiwa na Bastola mkononi ikiwa tayari katika hali ya hatari ya kuruhusu risasi kuuingia mwili wa kaidi yeyote mle ofisini, akili ilikwishambadlika na kuwa kama ya mnyama, Ukumbi mzima ukazizima kwa hofu

    “Mhe Mitti, unataka kufanya nini sasa? yaani pamoja na yote maovu mliyoyatenda kwenye taifa hili kupitia wadhfa mliopewa kwa kuaminiwa bado tena unataka kutuuwa?” Mhe Waziri mkuu aliongea kwa sauti isiyo na hofu wala woga

    “Shut up, Niambie nani msafi humu kati yenu? kila mmoja ana yake aliyoyafanya kwa njia yake katika kujihakikishia anaulinda ugali wake.. Nani asiyetaka madaraka humu? na nani asiyetaka mali humu? Sasa nasema hivi atakayenisogelea hatua moja tu ataikuta roho yake ikimsubiri kuzimu mara baada ya kuufukia mzoga wake..” sauti ya Mhe Mitti ilikwishabadilika na kuwa kama ya mwuaji mkongwe. Wakiwa bado kila mmoja amesimama kivyake ndipo uliposikika mlio wa risasi iliyofyatuliwa, wote wakasambaa wakiruka huku na kule, Suti zikavurugika, vitambi vikawachomoza nje ya mashati yao yaliyochomoka.. Kimya kitandana! hapakuwa na sauti nyingine yeyote zaidi ya ile ya Mhe Mitti akilia kwa uchungu, kumbe ni yeye ndiye aiyepigwa ile risasi begani! na ghafla mpigaji wa risasi ile akaonekana akiteremka kutoa juu ya Paa la ofisi hiyo, Alikuwa ni Mwanadada Lillian Ufoo!

    Haraka Mhe Sostenes Mitti na Fortunatus Mwita wakafungwa pingu, na katika hali ya kushangaza Mkurugenzi wa usalama wa taifa akaamuru na Kamanda Katinda Kuya naye afungwe Pingu, ndipo sasa zikachukuliwa Laptop zao na kuanza kufunguliwa, haikuwa rahisi kuzifungua kwa jinsi zilivyofungwa kwa namba za siri nyingi lakini hapakuwa na mchezo ambao ungemsumbua Ufoo, alitulia kama dakika mbili tu na kuweka wazi kila kitu, Taarifa zote za kiharamia zikitaja majina ya washiri, kazi na sehemu wanazofanyia mambo yao zilionekana.. Wakati huo IGP alipokea taarifa kutoka kwa Inspekta Kenjah kuwa tayari wamefanikiwa kuvamia lile jengo la Black Scopion kule Gongo la mboto ambapo wameupata mtambo wa Divier pamoja na watumishi kadhaa, Pia wameshawakamata maofisa wao akiwemo Chanzi na Rwehumbiza

    ****

    “…Nimeumia sana na nimeteseka sana, siwezi tena kuendelea kuishi, inaniuma sana lakini sina budi kufa kwa amani… kabati kwangu kuna nyaraka za muhimu sana nilizoandika kuhusiana na mirathi.. mali zangu zote zikiwemo pesa na makampuni yangu mvigawanye kama nilivyoandika mwenyewe, wala msiviogope kwani kuanzia kesho hapatakuwa tena na himaya iitwayo budha kwani watateketea na kuangamia kwa kuiokosa Pete hii, Pete hii itayeyuka na kusambaa kabisa isibakie hata chembe muda utakapofika hiyo kesho wakati huo himaya ya budha nayo yote itakuwa ikiteketea na kupotea kabisa.. Naomba muishi na Shekhia kwa amani na upendo, msimtenge wa kumnyanyapaa.. huyo si jini kamili bali ana asili hiyo tu hivyo hana madhara yoyote…” Suhail alikuwa akiongea kwa unyonge kiasi cha kuwafanya sasa mpaka wanaume nao kutokwa machozi “..Mungu akijaalia Shekhia na Sharifa mkajifungua naomba kama watoto watakuwa wa kiume basi mmoja aitwe Noordin ikiwa na maana ya Mwanga wa ajabu na mwingine Aldin ikimaanisha Taa ya ajabu.. na kama watakuwa ni wa kike basi kila mmoja amchagulie jina lolote mtoto wake..” Kimya kikapita kila mmoja akimsikiliza Suhail ambaye alitulia kimya, alikuwa amemaliza kusema na amemaliza dakika yake ya mwisho kuwepo duniani,

    Roho ikaachana na mwili, Suhail Kusekwa akafariki dunia

    Kilipita kimya kama cha dakika tano, kila mmoja akiwa haamini anachokiona, ndipo sasa kilio kilipozizima mle ndani, hakuna aliyejizuia hata wanaume pia!, Sharifa alilia mpaka akapoteza fahamu, Mama Suhail naye alikuwa nusu mwehu kwa jinsi alivyo changanyikiwa. Majirani wakajaa ndani na kuanza pilikapilika za msiba mkubwa!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****

    Siku iliyofuata utaratibu wa kusafirisha maiti ya Suhail kuelekea Tabora ulifanyika na familia pamoja na jamaa wa karibu wakajumuika kwenda kumuhifadhi kipenzi chao, Suhail Kusekwa.

    Ulikuwa ni msiba mkubwa uliokusanya mamia ya vijana na wazee, Msiba ambao mbali ya Simanzi na huzuni, pia uliacha funzo kubwa sana kwa jamii..

    Hatimaye Suhail akazikwa katika makaburi ya Rufita, mkoani Tabora.

    Upande wa mtandao wa Black Scopion nako mambo yaliwiva ambapo baada upelelezi kukamilika, Watuhumiwa wakafikishwa mahakani.. na hukumu kutolewa kila mmoja na yake.. Joram Ndege, Sostenes Mitti, Fortunatus Mwita na Ibrahim Basha bin Mende wakahukumiwa adhabu ya kifo kwani wao walishiriki katika mauaji kadhaa kikamilifu, waliosalia wote akiwemo Kamanda katinda Kuya, Chanzi, Rwehumbiza, na wale wafanyabiashara, pamoja na viongozi wote walioshiriki wakahukumiwa Vifungo vya maisha na kazi ngumu gerezani.



    TAMATI

0 comments:

Post a Comment

Blog