Search This Blog

NYUMBA YETU,NYUMBA YA WACHAWI - 5

 







    Simulizi : Nyumba Yetu, Nyumba Ya Wachawi

    Sehemu Ya Tano (5)



    Maneno ya mjomba yalifanya hali ya Faluu kuzidi kubadirika na nguvu zilimuisha na kutokana na upepo kuzidi paa ya nyumba yao iliezuliwa na eneo lile lilikua na baridi sana na muda mfupi baadaye mvua ilianza kunyesha katika nyumba yao tu Na kumuongezea hofu Faluu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    (Huku akiwa anatetemeka Faluu aliongea)



    ‘’Mjomba sasa haya yote yanamaana gani? Kwa maana mimi sikukusudia kabisa ‘’Faluu aliongea huku akiwa ananyeshewa na mvua tena mvua ya mawe.



    ‘’Unasema hukukusudia,unamaana gani kusema hivyo?’’ Mjomba alimuuliza Faluu.



    ‘’Mimi nimetoka asubuhi hapa nikawa naenda zangu sokoni kama ulivyoniagiza nifanye,wakati nikiwa njiani nilikutana na dada mmoja hivi,huyo dada namkumbuka alishawahi kunifanyia mambo ya ajabu,kwa hiyo baada ya kumuona niliogopa sana nikawa narudi nyuma,kumbe nyuma yangu kulikuwa na shimo kubwa sana na huyu dada wa niliyekuwa namkimbia aliliona nilipogeuka nyuma yangu nilikutana na dada mmoja uso kwa uso kama huyu niliyemkimbia mbele yangu akanisaidia nisidondokee katika lile shimo,ghafla nageuka tena sikumuona niliogopa sana ikabidi nikimbie nirudi nyumbani,kwa hiyo ndio hicho kilinichonikuta’’ Faluu aliongea.



    ‘’A aah,sawa kumbe ndiyo hivyo,basi haina tabu,lakini hawa wakubwa watakula nini??’’ Mjomba aliongea.



    ‘’Heee! Wakubwa ?? wakubwa gani tena’’aliuliza Faluu..



     ‘’Aaah,samahani wewe haya kuhusu’’alijibu mjomba huku akiondoka



    ’Sasa mjomba mbona unaondoka’’aliongea Faluu huku akiwa anamshika mkono mjomba wake hasiondoke.



    ‘’Ndio kwani kuna nini?’’ Mjomba aliuliza.



    ‘’Naomba nikuulize kitu’’ Faluu aliongea



    ‘’Niulize tu usijali’’aliongea

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Swali langu la kwanza,hapa wakati tunaongea mara ya kwanza upepo ulikuja paa ikaezuliwa na mvua ikanyesha na mpaka sasa juu kuko wazi na vitu vyetu vimelowa tunaishije? Na swali la pili siku ya kwanza nilipouliza kuhusu ndugu zangu hapa uliniambia wamesafiri na muda si mrefu watarudi,mbona sikuelewi?’’Faluu aliuliza.



    (Mjomba alicheka )



    ‘’Kwanza kwa swala la mvua lisikupe shaka japo umelowa na vitu vimelowa,wakubwa walikuwa wamechukia,ila kwa kuwa umenieleza wewe mwenyewe utashuhudia kitakachojiri na kuhusu ndugu zako,sitapenda tena uniulize hilo swali katika kipindi chote tutakacho kuwa wote hapa nyumbani sawa’’ Mjomba aliongea na kuondoka.



    Wakati mjomba akiondoka,lile paa liliokuwa limeezuliwa na upepo lilirudi na katika nyumba ya akina Faluu na mazingira yote yakawa kawaida kama zamani,kipindi hicho Faluu alikuwa na mawazo hasa kuhusu lile swali alililomuuliza juu ya ndugu zake pale nyumbani na alipokuja kutazama juu alishangaa kuona paa ya nyumba yao na kila kitu kiko sawa.Hali ile ilimstahajabisha sana na kujikuta akichunguza chunguza ili ajue imerudi rudi vipi pamoja na mabadiriko ya mule ndani.Muda wa kulala ulifika,wakati akiwa katika usingizi mzito alianza kusikia sauti kama mtu akiunguruma,sauti hiyo ilimfanya kukosa usingizi na hivyo ikabidi aamke.Wakati akiwa ameamka alianza kuifata na  kuisikia vizuri ile sauti iliyokuwa ikiunguruma,Wakati akiwa ametoka katika chumba chake alishtuka baada ya kuona jitu kubwa sana likiwa ilinakula nyama huku likiwa limetapakaa damu,Faluu aliogopa sana nakushindwa kuvumilia na hivyo kujikuta akipiga kelele..



    ‘’Mama…mama…mama…’’



    Lile jitu liligeuka huku likiwa limebeba ile nyama kwa bahati mbaya kumbe ile nyama ilikuwa nyama ya mtu na wakati akigeuka aliona vizuri kichwa cha yule aliyekuwa analiwa,kumbe alikuwa ni mjomba wake Faluu,Faluu alivuta pumzi huku nguvu zikiwa zimemuishia..

    ‘’Haaaaaaaaa,kumbe ni mjomba wangu…’’ aliongea Faluu aliongea



    Baada ya zile kelele za Faluu na lile jitu la kutisha kumsikia,lilianza kumfuata Faluu huku Faluu alijikuta akishindwa kukimbia kutokana na namna alivyokuwa.Lile jitu liliendelea kumsogelea mpaka lilimkaribia ,ghafla likiwa linataka kumbeba alitokea mama yake Faluu nakupambana na lile jitu na baada ya kulishinda lilikimbia na kumuacha Faluu na mama yake pale huku mule ndani kukiwa kumetapakaa damu iliyotokana na kifo cha mjomba wake Faluu.Faluu na mama yake walijaa na simanzi sana.



    ‘’Sasa mama ni aina gani ya maisha ambayo mimi naishi katika hii nyumba? Na nitaendelea kuishi hapa mpaka lini mama yangu?’’ Faluu alimuuliza mama yake.



    ‘’Naujua ugumu unaopitia mwanangu,lakini hii ndio njia yako ya ushindi na ndiyo sehemu pekee itakayo kufanya wewe kuwa huru”mama aliongea.



    ‘’Ndio  sehemu pekee itakayo nifanya mimi kuwa huru? Uhuru gani huo wakati mimi Napata shida? Kwanza ona hadi mjomba wangu kafariki?”aliongea Faluu huku akiwa analia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Mambo yote unayoyazungumza huko sahihi,lakini pia inabidi uwemwangarifu na mvumilivu maana ndivyo mafanikio yanavyohitaji na pia naomba usijifananishe wewe na mjomba wako sawa, maana kati yenu hamtembei katika njia moja’’mama aliongea.



    ‘’Kwani mama,embu naomba uniambie,kwanini mjomba amefanyiwa kitu hiki kibaya na kwa namna hii? Mtu analiwa kama ndege?’’ Faluu alimuuliza mama yake..



    ‘’Inaonekana mjomba wako hakuwaandalia hawa viumbe chakula chao,kwa hiyo limeamua kumla yeye mwenyewe’’ mama aliongea



    ‘’Daaah,inamaana mimi ndio chanzo cha haya?maisha gani haya sasa jamani!! Hapana “Faluu alijikuta akifikiria



    ‘’Mbona unashangaa sasa?”mama aliongea



    ‘’Hamna mama niko sawa tu”Faluu alijibu

    Waliongea kwa muda mrefu na baadaye walijikuta wote wakiangaliana,baada ya kusogea mbele ya eneo walilokuwepo walijikuta wakiwa wakipigwa na butwaa baada ya kuona vipande vya nyama nyama kama kichwa na miguu ya mjomba wake Faluu yaliyoachwa na lile jitu lililokuwa likimla,Walianza kukusanya kusanya vipande vile huku Faluu akiwa anajaribu kujizuia kulia wakati tukio lile likiendelea,ila kutokana na  simanzi aliyokuwa alijikuta akishindwa kujizuia kutoa sauti na hivyo akajikuta akipaza sauti yake..



    ‘’Mjoma wangu…ndio nini sasa mjomba”Alilia Faluu



    ‘’Shiiiiiiiiiiiiiiiiii,acha kutoa sauti bhana,hivi hujui kama saa hizi ni usiku’’Aliongea mama yake.



    Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Faluu maana japokuwa mama yake alikuwepo pale lakini alijikuta akihukosa uwepo wa mjomba wake pale nyumbani..

    Kumbe kutokana na sauti ile aliyoitoa Faluu majirani wa karibu walimsikia na hivyo kuwafanya wasogee karibu ili wajue kinachoendeleaa,walipofika pale nje walianza kugonga kwa nguvu,huku Faluu na mama yake walibaki wanaangaliana..



    ‘’Embu nenda kawaone’’Mama aliongea.



    ‘’Mmmh,Sawa mama’’alijibu Faluu na baadaye alielekea Mlangoni kwaajili ya kuwaona hao watu waliokuwa wanagonga mlango.Alipofika mlangoni alijikuta akipigwa na butwaa baada ya kuwaona wale watu aliowakuta pale mlangoni kwa maana walikuwa ni wazee sana na hivyo kujikuta akitaka akukimbia lakini alipojaribu kufunga mlango ili akimbilie ndani,mlango ulikuwa  mgumu kufunga na hivyo wale waliingia ndani..



    ‘’Kulikoni mbona unataka kufunga mlango,halafu kama unawasiwasi sana ?”Bibi mmoja alimuuliza.



    ‘’Aaah,hamna…..!’’Faluu alijibu huku akijilazimisha kutabasamu..



    ‘’Hamna nini?wakati unaonekana kama macho yako yapo juu juu?” bibi mwingine aliongea kwa makazo sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Muda huo ambao walikua wakijibizana ilikuwa saa kumi(10) alfajiri,



    ‘’Enhee!embu tuambie kulikoni mbona tumesikia sauti kama unalalamika?kulikoni ndugu yetu na mjomba wako yuko wapi?”Faluu aliulizwa..

    Baada ya Faluu kusikia hivyo,alijikuta akishindwa kujibu chochote na badala yake alijikuta machozi yakimtoka huku akishindwa kujizuia..



    ‘’M..mmh…mmh,haaaaaa’’Faluu alikua akiunguruma tu bila kuwa na jibu.



    Kutokana na hali aliyokuwa akionesha Faluu wale wazee walijikuta wakimtolea macho na kujikuta wakishindwa kumuelewa kile anachokimaanisha na hivyo kupelekea kukimbilia ndani kwa kasi ili wakajue nini kinampelekea Faluu kuwa katika hali ile.Walipofika mule ndani na kuiona ile hali ya mazingira walijikuta wakifurahi na kupeana pongezi..



    ‘’Safi sana!kumbe ndiyo haya yanayoendelea”aliongea mtu mmoja.



      ‘’Ndio hata mimi ndio nakumbuka,binafsi nilikua nasubiri kwa hamu sana swala hili,sasa tunafanyaje?”mzee mmoja alikuwa akiwauliza wenzie na katika kipindi hicho Faluu alikuwa akiwatazama tu..



    ‘’Huyu mototo tunaondoka naye leo,hatumuachi!!”alijibu mzee na muda huo walianza kuondoka naye huku Faluu akigoma…



    Baada ya hapo waliondoka naye huku wakivutana,maana Faluu hakuwa tayari kutoka pale nyumbani,hivyo alijikuta akimuita mama yake..



    ‘’Mama!,mama yangu..! mama huko wapi sasa mama yangu?”Faluu aliita huku akiwa analia

    Baada ya wale watu kumsikia analia huku anamwita mama yake,walianza kumcheka hadi wengine alikuwa wananguka chini kwa kukosa nguvu kutokana  vicheko vyao..



    ‘’Muone huyu motto,mpuuzi kweli,eti mama..mama…mama yangu huko’’aliongea mmoja kwa kejeli huku akiibana pua yake.



    ‘’Hata mimi namshangaa sana huyu kijana,inamaana hajui kama mama yake alishafariki kweli?et wewe kijana au unauita mzimu?hahahahhah’’aliongea na mwishoni alicheka sana.



    Kipindi chote hicho walikuwa wakitoka nje ya hiyo nyumba kutokana na ukubwa wa uzio wa nyumba hiyo,walichukua muda sana kutoka nje huku wakiendelea na maneno yao ya kashfa.Wakati wakiendelea na maneno yao,katikati yao alikuwepo kijana mmoja ambaye alikuwa ametulia na hakuwa anaongea kitu chochote wakati mengine yakiendeleaa.Wakati wakiwa wanaelekea getini ili watoke nje alijitokeza mbele yao na kuongea maneno..



    ‘’Embu muacheni kijana wa watu aende kwao,msimuumize kabisa’’aliongea huyo kijana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Wewe ni nani? Na unaongea kama nani? Wewe ni mfanyakazi tu hapa’’ mzee  mmoja aliuliza.



    ‘’Mimi ndio nasema muacheni huyo kijana wa watu aondoke tena sasa hivi kabla sijakasirika’’aliongea tena yule kijana .



    ‘’Hahahahhaha, eti tena sasa hivi kabla sijakasirika’’ aliongea mzee mwingine huku akiwa anamsogelea yule kijana. Wakati akiwa anamsogelea yule kijana,yule kijana alianza kucheka sauti Fulani ya kutisha na watu wote walishtuka na kubaki wakimtazama,huku wakijaribu kujihami.



    ‘’Wewe umekuaje?”mzee mmoja alimuuliza.



    Katika kipindi chote walichokuwa wakimuuliza, Yule kijana alikuwa akiendelea kucheka huku na ghafla katika mwili wa yule kijana alitokea mama yake Faluu na kuyaanzisha mashambulizi pale paleBaada ya kupambana sana,mama yake Faluu alifanikisha kumuua mzee mmoja pale na kwakuwa ndio kulikuwa kuna kucha ,wengine waliobaki walikimbia na kumuacha mwenzao akiwa amelala pale huku akiwa amekufa.Faluu alijikuta akitetemeka sana baada ya kuyaona yale    yaliyotendeka pale .



    ‘’Mama sasa hii nini mama yangu?” Faluu alimuuliza mama yake.



    ‘’Kwani wewe unaona nini?mbona unakuwa na maswali ya ajabu?”mama alimueleza mwanawe huku akiwa ametapakaa damu katika mwili wake.Baada ya yote alianza kumla yule mtu aliye fariki.Lile swala lilianza kumuogopesha Faluu.



    “Aaaah,mama sasa hiyo nini?si mtu huyo?mbona unafanya hivyo?acha bhana”Faluu alimwambia mama yake.Mama aligeuka na kumuangalia Faluu kwa macho Fulani ya kutisha,hali ambayo ilimpelekea Faluu kuogopa na kisha mama alicheka na katika mazingira yasiyotarajiwa alipotea na ule mwili wa marehemu.Ilikuwa ni siku ya historia kwa Faluu kwani hakuyategemea mambo yote yaliyotokea usiku kucha na hivyo kumpelekea kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu palepale.



    Alilala pale kwa muda mrefu sana na kwa kuwa pale ndani hakukuwa na mtu yeyote,ilikuwa ngumu sana kwa Faluu kupata msaada.Masaa yalizidi kwenda,wakati Faluu akiwa usingizini,alianza kuota akiwa mkubwa na pia yuko kwenye hiyo nyumba ya mjomba wake na watu wengi wakiwa wanamuabudu yeye, lakini wakati akiendelea na maisha hayo kwenye ndoto,siku moja alikuwa ametoka nyumbani yeye na mfanya kazi wake wakiwa wameenda kutafuta dawa katika msitu mmoja mkubwa sana,alikutana na bibi mmoja mzee sana akiwa hajiwezi,huyo bibi alianza kuomba msaada kutoka kwao..



    ‘’wajukuu zangu naomba mnisaidie bibi yenu’’Huyo bibi aliongea.



    Faluu alimuonea huruma na kutokea kuvutika kumsaidia yule bibi,Lakini lile swala la kutoa msaada yule mfanya kazi wake hakulihafiki kabisa.



    ‘’Sikia mzee,moyo wangu hauko tayali kabisa wewe kumsaidia hyo bibi,ni vyema ukamwacha tukaendelea na shughuli zetu’’Yule mfanya kazi aliongea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yale maneno ya mfanya kazi wake yalimuingia kidogo kichwani na hivyo kufanya wao waendelee na safari yao,lakini walipokuwa wakiondoka yule bibi alianza kulalamika huku akionesha kushindwa kufanya kitu chochote pale..



    ‘’eeeh,mweeeeh!nisaidieni jamani,nakufa…ooooh”alilalamika yule bibi huku akipiga kelele katika msitu ule.



    Baada ya yule bibi kulalamika sana,Faluu alishindwa kuivumilia ile sauti na hivyo akajikuta anarudi nyuma ili aende kumsaidia yule bibi,wakati akigeuka nyuma ili aende kumsaidia,yule mfanya kazi wake alimshika mkono na kumzuia asiende..



    ‘’Sikia mzee,tafadhali sana usiende kumsaidia yule bibi,acha tuendelee na kazi iliyotuleta huku muache huyo bibi aendeleee na biashara yake’’Mfanya kazi wake alimsihi sana Faluu asifanye vile,lakini ilikuwa ngumu sana kwa Faluu kuvumilia ile sauti ya yule bibi na hivyo ilibidi aende kumsaidia.



    Kwa bahati mbaya alipomsogelea karibu yake lilitumwa kombora mithili ya moto na kumuingia Tumboni na hapo hapo Faluu alijikuta akishtuka baada ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu,baada ya kufumbua macho tu,mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni mama yake..



    ‘’Mama nimeota ndoto hapa….’’ Aliongea Faluu huku akiwa anathema kwa nguvu sana,lakini kabla hajamalizia mama yake aliongeaa..

    ‘’Najua,lakini usipoangalia huruma yako itakupeleka pabayaa” Mama yake aliongea.





    Yale maneno yalimfanya Faluu habaki mdomo wazi huku akijikuta anakosa kitu cha kumueleza mama yake.Baada ya muda wa dakika kadhaa alitabasamu na kuongea maneno kwa mama yake..



    ‘’Mama naomba nikuulize kitu’’ Faluu aliongea.



     ‘’Wewe uliza tu’’ Mama alijibu.



    ‘’Kwanini umeniambia hivyo? Na umeijuaje ndoto yangu ?’’ Faluu alimuuliza mama yake.

     (Mama alicheka sana )



    ‘’Sikia mwanangu,kwanza nikueleze kitu hivi,mimi mama yako ninauwezo mkubwa sana saa hizi,ninaweza kukuona na kutambua kitu unachokifikiria wewe au mtu yeyote na pia nikikuona wewe naijua tabia yako kwasababu mimi ndiye niliyekuzaa,hivyo nakujua zaidi ya mtu yeyote anavyokujua,jaribu kubadirika kwa maisha unayoyaendea’’Mama aliongea.



    ‘’Nijaribu kubadirika? unamaanisha nini?” Faluu aliuliza.



    ‘’Mwanangu nikikuona wewe,nakuona mtu Fulani mkubwa sana katika maisha yako ya baadaye,lakini naona maisha Fulani magumu kwako na yenye maumivu usipo badirika, kwasababu

    ya mwenendo wa eneo hili na watu wake,unatakiwa usiwe na huruma sana na wakati mwingine ili uende vizuri jaribu kuangalia sana maisha yako kuliko kitu chochote kile katika dunia hii’’Mama

     alijibu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘’Mama yangu nahitaji sana kukuelewa lakini bado naona kama unazunguka tu, naomba uniambie tu mama yangu ili nikuelewe’’Faluu aliongea.



    ‘’Haya mwanangu,ndoto yako si umeifatilia ,yale ndiyo maisha halisi yanayokuja kwako na kile ulichofanyiwa ndicho kitakacho tokea kwenye maisha yako usipokuwa msikivu nakuangalia maisha yako,kwasababu siyo kila mtu anayekuja katika maisha yako anahitaji sana msaada wako,lakini wengine wanafanya hivyo ili wapate nafasi ya kuharibu maisha yako mwanangu,Siyo kila anayekuchekea anakufurahia,wengine wanakuwa wanakusanifu tu’’mama yake Faluu aliongea kwa ukubwa.



    ‘’Mama nimekuelewa sana,enhe! Neno la mwisho kwangu nini?’’Faluu alimuuliza mama yake.

    (Mama alitabasamu, kutokana na mwanaye kuelewa maneno yake)



    ‘’Vizuri  sana mwanangu, kitu cha wewe kufanya ni hivi,angalia sana na uwe makini mtu asiutambue udhaifu wako, kwa sababu udhaifu wako utakapo julikana watu wengine wanaweza kuutumia ili wakuangushe wewe hapo’’Aliongea mama na baadaye alipotea katika mazingira yale.



    ‘’Kwa hiyo…aaaah, sasa mbona unaondoka tena! Ila siyo mbaya asante kwa maneno yako mazuri mama yangu’’ Faluu aliongea huku sura yake ikitawaliwa na furaha.

    Wakati Faluu akiwa amaezubaa anayafikiria yale maneno amabyo mama yake limueleza Hali ya hewa ilibadirika na mawingu yalitanda katika kile kijiji na kijiji chote kilionekena kuwa na utulivu sana.



     ‘’Eeeh, hii hali vipi sasa mbona imekuwa ghafla sana’’ Faluu aliongea huku akionekana kustahajabika, Wakati akiwa katika mshangao huo,kwa mbali alisikia sauti kama mtu anaongea,hali ambayo ilimfanya kutega sikio na kusikiliza kwa makini ili ajue kinachoongelewa.



     ‘’Haya jamani leo kutakuwa na kikao pale nyumbani kwa mwenyekiti wetu wa kijiji, hivyo watu wote mnatakiwa kufika bila kukosa,tutaongelea mambo yote yaliyotokea katika kijiji chetu na matatizo yote yanayokikabili kijiji’’ Huyo mtu aliongea na baada ya ile sauti kusikika, ile hali ilipotea ..

    (Faluu alishtuka)



    ‘’Heeee! Hii hali vipi tena, halafu kwa huyu mwenyekiti ndiyo wapi?” Faluu alikuwa akijiuliza maswali tu.



    Masaa yalienda na ilipofika saa kumi na moja(11) jioni watu walianza kukusanyika katika eneo la tukio huku Faluu akiwa ametulia nyumbani kwao akitafakari kikao hicho na eneo ambalo hicho kikao kitafanyika.Baada ya watu kuwa wengi, watu wengine  walianza kujiuliza baadhi ya maswali..



    ‘’Mbona huyu mzee wa mtaa wa juu hapo hatumuoni? Au hata yule kijana wake’’ Mtu mmoja aliongea.



    ‘’Mzee wa hapo mtaa wa nyuma? Mzee nani huyo” Aliuliza mtu mwingine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Nazungumzia mzee Kachali’’ Yule mtu alijibu.



    ‘’Aaah,mzee Kachali! Kwani mzee Kachali anaishi na kijana pale nyumbani kwake saa hizi?”Yule mtu aliuliza.



    ‘’Ndio yupo’’ Yule mtu alijibu,



    ‘’Mmmh,sijawahi kusikia,wala kumuona labda atakuja’’huyo mtu aliongea huku akionekana kutoyaamini yale maneno.Baada ya mazungumzo yao kwa dakika kadhaa,waliachana nayo na kila mtu aliendelea na mambo yake huku wakisubilia kuona kitakachoendelea.

    Wakati huo Faluu alikuwa akiendelea kuyafikiria maisha maisha yake,hali iliyopo na hicho kikao,mawazo yake yalionekana kutokuwa na maamuzi sahihi juu ya nini afanye kwa wakati huo hususa ni kifo cha mjomba wake na mambo mengine. Kipindi hicho Faluu akiwa katika msongo wa mawazo aliisikia sauti ikimueleza…



    ‘’Fanya unayoweza lakini hakikisha haukosi kwenda katika hicho kikao sawa’’



    (Faluu alishtuka na kujikuta akigeuka geuka ili amuone huyo anayeongea)



    ‘’Kwanini unasema hivyo?’’ Faluu aliuliza.



    ‘’Hakikisha unaenda usikose maana huko ndiko kwenye ushindi wa maisha yako’’ hiyo sauti iliongea na wakati huo mama alijitokeza.



    ‘’Ndio ushindi wa maisha yangu? Na pia kwanini unapenda kupingana na mawazo yangu?’’ Faluu aliongea, huku akionekana kulaumu sana.



    ‘’Sikiliza mwanangu sina la ziada,ila kubwa kwa sasa ni hilo tu,wewe nenda eneo la kikao ni mtaa wa mbele hapo,simama uende sasa hivi’’ mama aliongea, huku akijivuta Faluu alisimama na bila kufanya chochote katika mwili wake,alianza safari ya kwenda kwenye kikao hicho,alipokaria katika mazingira yale,watu wote waligeuka kumshangaa huku wakimshangilia na kuongea..



    ‘’Huyu Ndiye…’’ watu waliokuwepo pale waliongea…Tukio lile la watu kumshangaa yeye,lilimfanya abaki akiwashangaa wale watu pia,  kwasababu hakuwaelewa nini wanamaanisha kuongea vile,hata yule mwenyekiti aliyekuwa anasimamia kikao kile alibaki akiwashangaa piaa.



    ‘’Jamani mbona kama siwaelewi mnachomaanisha kusema hivyo?’’Faluu aliwauliza.



    ‘’Ni kweli hata mimi mmeniacha njia panda,nini maana yenu,kuzungumza hivyo?’’Mwenyekiti aliongea.Walijikuta wakikaa dakika tano bila kusema chochote,muda kidogo alisimama kijana mmoja nakuongea.



    ‘’Samahani mwenyekiti,sisi tunataka huyu kijana ndiye awe kiongozi wa hiki kijiji chetu’’aliongea yule kijana.Faluu baada ya kusikia hivyo alijikuta akipigwa na butwaa na kutokana na mshtuko ule alianguka na kupoteza fahamu,watu hawakujali walimpa huduma ya kwanza na baada ya kupata nafuu na fahamu kurudi,aliongeaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘’Jamani samahani mimi siwezi kazi zenu’’Faluu aliongea.Watu walizidi kumsihi na kumtaka hakubali kulivaa jukumu hilo,baada mvutanao wa muda mrefu,alikubali na kuwa kiongozi,yaani mwenyekiti wa kijiji hicho na ndiye alivunja rekodi ya kiongozi mdogo kuliko wote waliowahi kuwa katika kijiji kile.





    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog