Search This Blog

HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA - 3

 







    Simulizi : Hamunaptra - Mji Uliopotea

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mfalme wa Wahamsud akiwa katika kutahamaki Seido alikuwa ameshafika miguuni pake na kumshindilia upanga wa tumbo uliompelekea kutokwa na uhai. Seidon akampisha adondokee pembeni kisha akanyanyuka kwa haraka na kumkata kichwa, aliurudisha upanga wa Amata kwa kuurusha na kisha akauokota ule wa kwake, akaurudisha alani na kuingia kwenye kijichumba kimojawapo, mara giza likatawala ndani ya hekelu lile. Amata ga Imba alipoona giza hilo akajua kumekucha, akapiga mbinja kali na muda mfupi tu, farasi wale wawili walikuwa tayari wamefika, Seidon akarukia juu ya mmoja wapo na Amata vilevile kisha wakapiga mbio kuelekea upande wa kusini. Nyuma yao jeshi lilikuwa likija kwa kasi na farasi.

    “Amatagaimba! Wanatufuata….” Seidon alipiga kelele huku akiwa katika kasi ya ajabu.



    “Usijali Seidon, piga mbioooo,” Amata alijibu, akainua mkono wake na kuibusu pete yake, “Shusha dhoruba ya jangwani ee pete ya ajabu,” Amata alisema maneno hayo huku pete ile ikiwaq jirani kabisa na kinywa chake. Mara radi moja kali ilipiga na mchanga uliochanganyika na vumbi ulitimka nyuma yao na kuwatenganisha kati yao. Seidon na Amata walisimama mbele na kugeuka nyuma ambako walishuhudia vumbi zito likiwazuia adui zao wasiweze kuwafikia.

    Amata ga Imba na Seidon, wakagonganisha viganja vyao na kupeana ishara ya mafanikio, kisha wakaendelea na safari kuelekea mji wa Hamunaptra, tayari kwa kazi ya kurudisha fuvu lile la Cleopas.

    “Seidon,” Amata amuita swahiba wake, “Sasa tunakabili mji wa Kush, hauna tabu kuuvuka, lakini sharti lake hutakiwi kuongea na mtu yeyote, na mji ule ni vizuri kuuvuka majira ya saa tano wakati jua linapokuwa linauendea utosi, lakini kuna kijiji kidogo ambacho lazima tukipite kijiji hiki ni jicho kubwa la malkia wa Soari, Sharhazad, pale patakuwa na ugumu wa kupita kwa vyovyote vile, kwa hiyo tujiimarishe kiroho na kiakili,” Amata alimaliza risala yake na kumuacha Seidon akiwa midomo wazi kwani yote haya hakuwa akiyaelewa tangu awali. Waliendelea mwendo mrefu kidogo na kufika sehemu moja tulivu yenye dimbwi la maji safi, dimbwi lililozungukwa na mitende na maua mazuri.



    “Tupumzike hapa Amata, nimechoka sana,” Seidon aliomba, Amata alisimama na kumtazama Seidon ambaye tayari alikuwa amekwishaikanyaga ardhi na kuyakimbilia maji yale.

    “Seidon!” Amata aliita, Seidon akageuka, “Subiri kwanza, unajua tupo wapi?” Amata aliuliza, “Jangwani, kwani vipi?” Seidon alijibu na kutupa swali, “Sasa wewe umeshawahi kuona jangwani kuna maji? Seidon hayo si maji,” Amata alimwambia Seidon huku akimvuta kumrudisha nyuma.



    Seidon hakulipinga hilo, alirudi nyuma na molja kwa moja akapanda farasi wake, akamtazama Amata, Amata alikuwa akiyaangali yale maji kwa makini sana.

    “Huo ni mji wa watu, tusiwaamshe twende tuendelee mbele,” baada ya kusema hayo Amata na Seidon waliendelea mbele zaidi na zaidi, wakipanda vilima na milima ya jangwani. Jua la asubuhi lilianza kuchomoza upande wa Mashariki na kuanza kuliangaza anga lote, Amata alimuongoza Seidon mpaka kwenye mji Fulani ulioonekana kukaliwa na watu wachache sana, wake kwa waume, hapakuonekana mtoto, waliusogelea mji huo na walipoufikia walipokelewa na wasichana warembo. Seidon aliwatazama wasichana hawa, walikuwa warembo wa kuvutia, kisura hata kiumbo.



    “Usiogope Seidon, hapa ni mahali salama sana, kula, kunywa, lakini usilale na mwanamke, ukifanya hivyo utakuwa umeharibu kila kitu,” Amata alimwambia Seidoni wakati akiingia ndani ya nyumba moja iliyoonekana kupambwa na maua mengi mazuri lakini bado ilhali iko jangwani.

    Ndani kulikaa mzee mmoja wa makamo aliyevalia vazi la ngozi ya ngamia, na kichwani mwake akiwa na kofia ya manyoya ya mbuni.

    “Unakaribishwa sana ewe shujaa wa msitu,” Yule mzee alitamka maneno hayo huku akiinamisha kichwa chake.

    “Nimekaribia, ee mfalme wa Kushi, nimekuja kwako mimi na mwenzangu, tunapita njia tunaenda huko waliko wafu, utujalie yale tunayohitaji pamoja na mema yako,” Amata akasema hayo huku akiinamisha kichwa chake kwa namna ile ile aliyofanya Yule mzee pale mwanzo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Shaka ondoa, siku zote, mwema hupata mema na mbaya hubaki na mabaya yake, kwa nini nikupe dhoruba ilhali shwari ninayo? Seidon kitukuu cha Vernad, mwana wa Velvesh, bahati yako sana hukumrudia Sherhazad, lakini roho ya babu yako Vernad iko ndani yako, usimuache huyu shujaa wa Msitu hata utakapotimiza lile ulilotumwa,” Yule mzee aliongea kwa utulivu sana, Seidon alishangaa kukuta Yule mzee akilijua jina lake vyema, kalijuaje yeye hakuwa na jibu. Amata ga Imba na Seidon, walikaribishwa kwenye zuria safi la ngozi ya ngamia, kisha wasichana warembo waliingia na kuwapa huduma zote wazitakazo, huku Seidon akipewa matibabu ya jeraha lake huku akikandwakandwa viungo vyake.



    Amata ga Imba na mwenzake Seidon walipewa ukarimu wa hali ya juu sana, huduma zote alizostahili kupata mwana wa Suiltan basi wao waliziopata pia. Seidon alihisi nguvu zimemrudia na mwili wote ulikuwa umekuwa katika hali yake ya kawaida.

    “Unajisikiaje sasa?” mwanadada\mrembo aliyepiga magoti mbele ya Seidon alimtupia swali lile, Seidon alijikuta anashindwa kujibu, alibabaika kwa swali hilo hasa alipomwangalia msichana yule mbichi ambaye alivaa nguo ndefu lakini iliyoanzia kiunoni kurudi chini huku juu alibaki hivohivo, chuchu zilizochongoka na kusimama zilimfanya Seidon apagawe, midomo ilimchezacheza, kabla hajasema kitu alikabidhiwa ua zuri la manukato safi, akalipokea na kulinusa, ua la yugiyugi, Seidon akaongea maneno yasiyoeleweka katika lugha ya kwao na lile ua likachanua mkononi mwake, akatikisa kichwa kuashiria kuwa kuna kitu amegundua. Katika mila za Wavelvesh, ua la yugiyugi lilimaanisha bahati, hivyo msichana huyu kumletea ua hilo Seidon ilikuwa ni kama bahati.



    “Unaitwa nani?” Seidon akamuuliza

    “Teboria,” akajibiwa.

    “Teboria, Teboria, Teboria!” Seidon alirudia kutamka jina hilo kwa mara kada kwa sauti ya chini, alihisi ameshawahi kulisikia sehemu lakini hakumbuki ni wapi.

    Teboria akaketi jirani na Seidon, Seidon akahisi harufu nzuri ya manukato kutoka kwa binti yule, akasogeza kinywa chake jirani na yule binti, yule binti naye akafanya hivyo, ndimi zo zikapishana kwa ufundi mkubwa sana, Seidon alihisi raha ya ajabu ambayo hakuwahi kuipata katika maisha yake, sauti za mahaba zikaanza kukijaza chumba kile. Seidon akachanganyikiwa, akaweka upanga wake pembeni na kutaka kumsaula yule binti, yule binti akajitoa kifuani mwa Seidon, Seidon alipomtazama usoni hakuwa Teboria, balisura ya msichana mwingine kabisa ambayo pia haikuwa ngeni usoni mwake.



    “Ni nani wewe?” Seidon alimuuliza yule msichana huku akiwa kajirushia upande wa pili wa kichumba hicho.

    “Ulinikimbia ee? Sasa nimekupata tena, na sintokuacha mpaka uitimize ile ahadi yangu, mimi ni Sherhazad, Malkia wa Soria, nimekuona tangu ukiwa Hamsud na nikafurahi kwa kuwa ulifanikiwa kuchukua lile fuvu, haya nikabidhi au la naitoa roho yako na fuvu nalichukua,” Sherhazad, sasa alichukua sura na umbo lake la kawaida. Chumba kikajaa manukato maradufu, Seidon akabaki anatetemeka mkononi akiwa ameshika ule mfuko mweusi ambao ndani yake kulikuwa na lile fuvu. Sherhazad alimfuata huku mikono yake ikiota kucha ndefu kupita kawaida, ilikuwa ni hali ya kuogofya, ulimi wake uligawanyika mara mbili, mara kichwa chake kikageuka na kuwa cha nyoka, Seidon alisimama na kuutwaa upanga wake, sasa Sherhazad akawa nyoka kamili, nyoka mkubwa, tuseme joka. Lile joka likaruka kumfata seidon pale aliposimama, Seidon akaepa na kuvurumisha ule upanga lakini akalikosa. Kishindo kile kikubwa cha lile joka kuangukia chini kiliwashtua wengi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Amata ga Imba akiwa amejilaza chini ya mtende, alisikia kishindo hicho na mara akasimama na kukimbilia kwenye kile kinyumba alimokuwa Seidon, alipofika hakuamini macho yake, Seidon alikuwa amevirigwa na lile joka, Amata ga Imba akaufuta upanga wake na kukata sehemu ya mkia wa lile joka, mara akasikia sauti ya mwanamke ikicheka kwa kebehi, Amata ga Imba alitazama huku na kule hakuona kitu wala mtu ila sauti hiyo iliendelea kumcheka kwa kebehi. Amata ga Imba akatulia pale alipo huku upanga wake ukiwa juu hewani ameushika mpini kwa mikono yake miwili, alipoushusha alikata katikati mwa lile joka, lile joka likapiga ukelele wa ajabu na kumuachia Seidon, kisha likajizungusha pale chini na badala yake akasimama msichana mrembo, Teboria.

    “Amatagaimba, majini haya, tuondoke,” Seidon, alikurupuka na kutoka nje, Amata akamfuata, Seidona alikuwa tayari juu ya farasi wake, “Seidon,” Amata aliita na kumuamuru ateremke kwenye farasi.



    “Nilikwambia nini Seidon?” Amata ga Imba alimuuliza kwa ukali, “Nilikwambia nini?” aliuliza kwa kelele, “Sikiliza Seidon nilishakwambia epukana sana na wanawake, hawa wataharibu mpango mzima, sio binadamu wale ni majini, sasa usirudie tena, Sherhazad keshajua unakoelekea na ameshakuona ukiwa na hilo fuvu sasa kazi ni nzito kufika Hamunaptra, na hii ni kwa sababu tu umekiuka masharti. Wewe mwenyewe ulinambia kuwa babu yako amekuonya hivyo hivyo juu ya wanawake, sasa kwa nini utaki kusikia? Kuwa mwangalifu,” alimaliza Amata ga Imba kisha akarudi na Seidon mpaka pale chini ya mtende.

    Wakiwa katika kuketi pale mara akaja mmoja wa masuria wa yule mzee aliyewakaribisha akawapa ishara ya kuwa wamfuate, nao wakafanya hivyo, wakaingia ndani na kuketi mbele yake.



    “Sikilizeni vijana, hapa pameshaingia matatizo, inabidi muondoke mara moja, tayari pepo zinataka hilo fuvu kwa nguvu zote, pepo la Soria, mwanamke hatari tayari limeshakuja hapa kwa nguvu zote kabisa. Naomba watu wangu wasidhurike, muondoke, muende na safari yenu, lakini kwa kuwasaidi ili mfike salama, sikilizeni, msipande farasi kwani hana uwezo wa kuvumili shida na dhoruba za jangwani, maana sasa mtakatisha jangwa kubwa lenye vikwazo vingi lakini hamna budi kuvuka ili mfike haraka huko muendako na hiyo ndiyo njia fupi, piteni katikati, usiku, miifuata nyota ya kilimia itawaongoza mpaka katika bonde la Sham, ambapo amtalivuka na kutokea karibu na mto Frati kutoka hapo nafikiri mnaijua njia,” yule mzee mwnyeji wao aliwaekeza na kisha kuwapatia ngamia, masurufu ya njiani na kuwaruhusu waende zao, mara tu Maghalibi ikifika ili waondoa nuksi katika kijiji chao.



    Safari ilianza jioni hiyo, Amata ga Imba akiwa mbele na Seidon akiwa nyuma yake, walilikata jangwa kwa taabu ya upepo na ghasia za vumbi lakini walivumilia ili lengo lao lipate kutimia. Usiku wa manane walijikuta wamefika mbali sana na mbele yao palionekana kitu kama korongo kubwa sana, mbala mwezi ilikuwa ikiwaongoza kwa mwanga wake mwanana, wakasimama kwa muda na kutazama mandari ile yakutisha kama si ya kuvutia, ‘Bonde la mauti’ Amata ga Imba alihisi sauti ikimnong’oneza, akageuka nyuma asione mtu, akaendelea kutazama kutazama lile korongo kubwa sana, kitu kama moshi kilikuwa kikifuka na kulijaza lile korongo, waliweza kuona vitu kama mawe si mawe ilimradi tu vilikuwepo vipo. “Seidon, hapa kuna kazi,” Amata ga Imba alimwambia Seidon, akageuka kumtazama akamuona ametulia kimya kama mtu anayetafakari kitu fulani. “Seidon, unawaza nini?” akamuuliza.



    “Amata ga Imba, tutafika hii safari kweli, maana naona vikwazo ni vingi sana, na ninaanza kukata tamaa,” Seidon alijibu.

    “Usikate tamaa, hakikisha unafika mwisho na unarudisha hilo fuvu kwa Kleopas uwaokoe watu wako,” Amata ga Imba alimueleza kwa upole.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapa ni wapi au niulize hiki ni nini?” Seidon aliuliza huku akioneshea mkono kwenye lile bonde, Amata ga Imba kwa kutumia upanga wake akaukandamiza chini mkono wa Seidon, “Usipanyoshee kidole mahali hapo, hapo ni bonde la mauti, mji wa wafu,” alimjibu. Seidon alionekana wazi kushikwa na woga wa hali ya juu sana katika hilo. Akajiinamia kichwa kwenye nundu ya ngamia, akatazama ule mfuko mweusi wenye fuvu la cleopas, akarudisha macho yake tena kwenye lile korongo, akamuuliza Amata ga Imba, “Tunavuka?”

    “Ndiyo hatuna budi kuvuka,” Amata ga Imba akaibusu pete yake na kuitazama kwa makini, kisha akshusha mkono, “Sikia, inabidi tufike paleeeeee kwenye ule mlima unaong’aa sana, tykifika pale tayari Klakos itaanza kuvuta harufu ya hilo fuvu, najua nguvu kutoka kwao zitatujia ilitukamilishe safari na wakati huohuo upinzani utaongezeka, haya twende,” Amata ga Imba alisema hayo na kumuamuru Seidoni kuendelea na safari.



    Amata ga Imba na mwenzake Seidon walipewa ukarimu wa hali ya juu sana, huduma zote alizostahili kupata mwana wa Suiltan basi wao waliziopata pia. Seidon alihisi nguvu zimemrudia na mwili wote ulikuwa umekuwa katika hali yake ya kawaida.

    “Unajisikiaje sasa?” mwanadada\mrembo aliyepiga magoti mbele ya Seidon alimtupia swali lile, Seidon alijikuta anashindwa kujibu, alibabaika kwa swali hilo hasa alipomwangalia msichana yule mbichi ambaye alivaa nguo ndefu lakini iliyoanzia kiunoni kurudi chini huku juu alibaki hivohivo, chuchu zilizochongoka na kusimama zilimfanya Seidon apagawe, midomo ilimchezacheza, kabla hajasema kitu alikabidhiwa ua zuri la manukato safi, akalipokea na kulinusa, ua la yugiyugi, Seidon akaongea maneno yasiyoeleweka katika lugha ya kwao na lile ua likachanua mkononi mwake, akatikisa kichwa kuashiria kuwa kuna kitu amegundua. Katika mila za Wavelvesh, ua la yugiyugi lilimaanisha bahati, hivyo msichana huyu kumletea ua hilo Seidon ilikuwa ni kama bahati.

    “Unaitwa nani?” Seidon akamuuliza

    “Teboria,” akajibiwa.

    “Teboria, Teboria, Teboria!” Seidon alirudia kutamka jina hilo kwa mara kada kwa sauti ya chini, alihisi ameshawahi kulisikia sehemu lakini hakumbuki ni wapi.



    Teboria akaketi jirani na Seidon, Seidon akahisi harufu nzuri ya manukato kutoka kwa binti yule, akasogeza kinywa chake jirani na yule binti, yule binti naye akafanya hivyo, ndimi zo zikapishana kwa ufundi mkubwa sana, Seidon alihisi raha ya ajabu ambayo hakuwahi kuipata katika maisha yake, sauti za mahaba zikaanza kukijaza chumba kile. Seidon akachanganyikiwa, akaweka upanga wake pembeni na kutaka kumsaula yule binti, yule binti akajitoa kifuani mwa Seidon, Seidon alipomtazama usoni hakuwa Teboria, balisura ya msichana mwingine kabisa ambayo pia haikuwa ngeni usoni mwake.

    “Ni nani wewe?” Seidon alimuuliza yule msichana huku akiwa kajirushia upande wa pili wa kichumba hicho.



    “Ulinikimbia ee? Sasa nimekupata tena, na sintokuacha mpaka uitimize ile ahadi yangu, mimi ni Sherhazad, Malkia wa Soria, nimekuona tangu ukiwa Hamsud na nikafurahi kwa kuwa ulifanikiwa kuchukua lile fuvu, haya nikabidhi au la naitoa roho yako na fuvu nalichukua,” Sherhazad, sasa alichukua sura na umbo lake la kawaida. Chumba kikajaa manukato maradufu, Seidon akabaki anatetemeka mkononi akiwa ameshika ule mfuko mweusi ambao ndani yake kulikuwa na lile fuvu. Sherhazad alimfuata huku mikono yake ikiota kucha ndefu kupita kawaida, ilikuwa ni hali ya kuogofya, ulimi wake uligawanyika mara mbili, mara kichwa chake kikageuka na kuwa cha nyoka, Seidon alisimama na kuutwaa upanga wake, sasa Sherhazad akawa nyoka kamili, nyoka mkubwa, tuseme joka. Lile joka likaruka kumfata seidon pale aliposimama, Seidon akaepa na kuvurumisha ule upanga lakini akalikosa. Kishindo kile kikubwa cha lile joka kuangukia chini kiliwashtua wengi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Amata ga Imba akiwa amejilaza chini ya mtende, alisikia kishindo hicho na mara akasimama na kukimbilia kwenye kile kinyumba alimokuwa Seidon, alipofika hakuamini macho yake, Seidon alikuwa amevirigwa na lile joka, Amata ga Imba akaufuta upanga wake na kukata sehemu ya mkia wa lile joka, mara akasikia sauti ya mwanamke ikicheka kwa kebehi, Amata ga Imba alitazama huku na kule hakuona kitu wala mtu ila sauti hiyo iliendelea kumcheka kwa kebehi. Amata ga Imba akatulia pale alipo huku upanga wake ukiwa juu hewani ameushika mpini kwa mikono yake miwili, alipoushusha alikata katikati mwa lile joka, lile joka likapiga ukelele wa ajabu na kumuachia Seidon, kisha likajizungusha pale chini na badala yake akasimama msichana mrembo, Teboria.

    “Amata ga imba, majini haya, tuondoke,” Seidon, alikurupuka na kutoka nje, Amata akamfuata, Seidona alikuwa tayari juu ya farasi wake, “Seidon,” Amata aliita na kumuamuru ateremke kwenye farasi.

    “Nilikwambia nini Seidon?” Amata ga Imba alimuuliza kwa ukali, “Nilikwambia nini?” aliuliza kwa kelele,



    “Sikiliza Seidon nilishakwambia epukana sana na wanawake, hawa wataharibu mpango mzima, sio binadamu wale ni majini, sasa usirudie tena, Sherhazad keshajua unakoelekea na ameshakuona ukiwa na hilo fuvu sasa kazi ni nzito kufika Hamunaptra, na hii ni kwa sababu tu umekiuka masharti. Wewe mwenyewe ulinambia kuwa babu yako amekuonya hivyo hivyo juu ya wanawake, sasa kwa nini utaki kusikia? Kuwa mwangalifu,” alimaliza Amata ga Imba kisha akarudi na Seidon mpaka pale chini ya mtende.

    Wakiwa katika kuketi pale mara akaja mmoja wa masuria wa yule mzee aliyewakaribisha akawapa ishara ya kuwa wamfuate, nao wakafanya hivyo, wakaingia ndani na kuketi mbele yake.



    “Sikilizeni vijana, hapa pameshaingia matatizo, inabidi muondoke mara moja, tayari pepo zinataka hilo fuvu kwa nguvu zote, pepo la Soria, mwanamke hatari tayari limeshakuja hapa kwa nguvu zote kabisa. Naomba watu wangu wasidhurike, muondoke, muende na safari yenu, lakini kwa kuwasaidi ili mfike salama, sikilizeni, msipande farasi kwani hana uwezo wa kuvumili shida na dhoruba za jangwani, maana sasa mtakatisha jangwa kubwa lenye vikwazo vingi lakini hamna budi kuvuka ili mfike haraka huko muendako na hiyo ndiyo njia fupi, piteni katikati, usiku, miifuata nyota ya kilimia itawaongoza mpaka katika bonde la Sham, ambapo amtalivuka na kutokea karibu na mto Frati kutoka hapo nafikiri mnaijua njia,” yule mzee mwnyeji wao aliwaekeza na kisha kuwapatia ngamia, masurufu ya njiani na kuwaruhusu waende zao, mara tu Maghalibi ikifika ili waondoa nuksi katika kijiji chao.

    Safari ilianza jioni hiyo, Amata ga Imba akiwa mbele na Seidon akiwa nyuma yake, walilikata jangwa kwa taabu ya upepo na ghasia za vumbi lakini walivumilia ili lengo lao lipate kutimia. Usiku wa manane walijikuta wamefika mbali sana na mbele yao palionekana kitu kama korongo kubwa sana, mbala mwezi ilikuwa ikiwaongoza kwa mwanga wake mwanana, wakasimama kwa muda na kutazama mandari ile yakutisha kama si ya kuvutia, ‘Bonde la mauti’ Amata ga Imba alihisi sauti ikimnong’oneza, akageuka nyuma asione mtu, akaendelea kutazama kutazama lile korongo kubwa sana, kitu kama moshi kilikuwa kikifuka na kulijaza lile korongo, waliweza kuona vitu kama mawe si mawe ilimradi tu vilikuwepo vipo. “Seidon, hapa kuna kazi,” Amata ga Imba alimwambia Seidon, akageuka kumtazama akamuona ametulia kimya kama mtu anayetafakari kitu fulani. “Seidon, unawaza nini?” akamuuliza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Amata ga Imba, tutafika hii safari kweli, maana naona vikwazo ni vingi sana, na ninaanza kukata tamaa,” Seidon alijibu.

    “Usikate tamaa, hakikisha unafika mwisho na unarudisha hilo fuvu kwa Kleopas uwaokoe watu wako,” Amata ga Imba alimueleza kwa upole.

    “Hapa ni wapi au niulize hiki ni nini?” Seidon aliuliza huku akioneshea mkono kwenye lile bonde, Amata ga Imba kwa kutumia upanga wake akaukandamiza chini mkono wa Seidon, “Usipanyoshee kidole mahali hapo, hapo ni bonde la mauti, mji wa wafu,” alimjibu. Seidon alionekana wazi kushikwa na woga wa hali ya juu sana katika hilo. Akajiinamia kichwa kwenye nundu ya ngamia, akatazama ule mfuko mweusi wenye fuvu la cleopas, akarudisha macho yake tena kwenye lile korongo, akamuuliza Amata ga Imba, “Tunavuka?”



    “Ndiyo hatuna budi kuvuka,” Amata ga Imba akaibusu pete yake na kuitazama kwa makini, kisha akshusha mkono, “Sikia, inabidi tufike paleeeeee kwenye ule mlima unaong’aa sana, tykifika pale tayari Klakos itaanza kuvuta harufu ya hilo fuvu, najua nguvu kutoka kwao zitatujia ilitukamilishe safari na wakati huohuo upinzani utaongezeka, haya twende,” Amata ga Imba alisema hayo na kumuamuru Seidoni kuendelea na safari.

    Walishuka katika bonde lile wakiwa na wale ngamia taratibu, ukimya ulitawala kila kona giza likazidi kuwa kubwa, wakazidi kutokonmea gizani mpaka wakafika mahali hawaonani. Amata ga Imba akasimama, akapapasa na kumgusa Seidon, akamshika mkono, kisha taratibu akazidi kwenda nae ndani zaidi ya korongo lile. Kelele za watu waliokuwa sokoni zilisikika kwa mbali, mwanga hafifu ukaanza kujitokeza kwenye lile giza, Seidon alikuwa akiogopa sana, “Usioneshe unaogopa, jikaze, huu ni mji wa wafu, hawa wote utakaowaona ni wafu, waliokufa zamani huko duniani,” Amatagaimba akamwambia Seidon, wakaendelea kwenda, Seidon alianza kuona watu wengi kwa mbali na baada ya mwendo mrefu kidogo walifika kwa watu wale na kuwapita taratibu lakini baadae wakajikuta wamezingirwa na watu kama kumi na tano hivi, wao wakiwa katikati, Seidon na Amatagaimba wakapeana migongo na kuwatazama watu wale kwa zamu.



    “Mnakwenda wapi?” mmoja wa wale watu ambaye alionekana ana rangi ya kijivu aliuliza, si Amatagaimba wala Seidon aliyejibu swali hilo, akaja mwingine wa kijani mwili wote mpaka mavazi aliyevaa, “Hamusikii? Au hamuelewi? Mbona hamjibu?” kabla hajamaliza kuuliza mwingine akapita katikati yao na kusimama uso kwa uso na Sedon, “Lete huo mzigo hapa haraka!” Amatagaimba alisikia sauti hiyo, akajua kuwa jamaa hao wamegundua kuwa wao wamebeba nini, akaeuka ghafla na kukaa upande wa Seidon tayari upanga wake ulikuwa umekwishaondoa kichwa cha Yule jamaa, vurugu ikazuka kati ya watu wale na akina Amatagaimba, mapigano makali yakazuka, kila walipowakata kata na panga zao wale watu walizidi kuwa wengi na makelele yao yalikuwa yakiwasumbua masikio ya Amatagaimba na Seidon.



    Amatagaimba na Seidon walipopata upenyo wakatimua mbio maana waliona wazi kuwadhibiti watu wale isingekuwa rahisi, nyuma yao bado kundi kubwa la watu lilikuwa likiwafuata kwa kasi wakiwa na silaha mbalimbali. Seidon na Amata walikaza mwendo kwa kukimbia wakifuata ujia mwembamba uliokuwa ukiongoza wasikokujua, baada yam bio za muda mrefu bila ya kusimama, wakafika eneo ambalo lilikuwa na miamba mingi sana wakasimama na kujificha, walikuwa wakihema sana, Seidon alijilaza chali chini katika vumbi, Amatagaimba akabaki kuchungulia kama hao jamaa wanakuja, hakuwaona. Akatoka katika lile jiwe na kujisjika kiuno, “Seidon! Hawapo,” akamwambia Seidon ambaye muda huo alikuwa amejilaza pale chini, akajinyanyua na kuketi, atulia kidogo na kuweka sawa ule mfuko wake ambao ndani yake kuna lile fuvu, alipoliufungua alibaki akishangaa, Amatagaimba akamtazama Seidon, “Vipi mbona umeduwaa?” akamuuliza Seidon.



    “Amatagaimba, njoo uone maajabu haya!” Seidon akamwambia Amatagaimba, akajongea karibu na ule mfuko, alipotazama ndani alishangaa kuona lile fuvu liking’aa katika yale matundu ya macho, “Seidon,” Amatagaimba akaita kwa kunong’ona, Seidon akamtazama Amatagaimba usoni, “Klakos wameshapata harufu ya fuvu la Cleopas, sasa wao ndio watatuongoza katika hisia kulifikisha mahali pake, lakini bado mitihani mingi inatukabili, hatuna budi kuivuka, hasa hasa Serhazad, inabidi tumzunguke” Amatagaimba aliongea. Seidon akaufunga vyema ule mfuko na wote wawili wakaanza kutembea polepole kuendelea na safari yao, wakafika njia panda, sehemu hiyo ilikuwa ni njia nne zilizotoka kwenye njia moja, wakasimama. Amatagaimba akaziangalia kwa makini zile njia, Seidon alibaki amesimama akiwa hajui la kufanya. Kati ya zile nne, walipoiangalia njia ya kwanza mbele kabisa wakaona kuna msitu mkubwa ukali mbali, njia ya pili kulikuwa na maji mengi sana kama bahari kubwa ing’azwavyo kwa jua la adhuhuri, njia ya tatu kulikuwa na jangwa kubwa ambalo ukiangalia tu utaona kitu kama mvuke wa moto unaowaka juu ya mchanga ule, upepo nao uliuyumbisha huku na kule, njia ya nne ilikuwa na milima mikali ya mawe yabisi ambayo ilikuwa ni ngumu kwa mwanadamu wa kawaida kuyakwea. “Tunafanyaje?” Seidon akamuuliza Amatagaimba. Amatagaimba hakuwa na la kujibu kwa wakati ule, alilitazama jua linalochomoza kwa mbali likipendezeshwa kwa miale yake murua, akamtazama Seidon alieonekana kukata tama katika hali hiyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Lete hilo fuvu ndilo litakalotuongoza njia,” akamwambia Seidon, akafanya hivyo, akatoa katika ule mfuko mweusi fuvu la Cleopas akamkabidhi Amatagaimba. Hatua chache katikati ya zile njia, Amatagaimba akalishika lile fuvu na kulitazamisha katika njia moja baada ya nyingine, njia ya tatu, njia ya jangwa, macho ya lile fuvu yakang’aa, wote wawili wakatazamana na kutabasamu. Seidon akalirudisha lile fuvu mfukoni, kisha wakaanza kutembea kuelekea ile njia ya tatu.

    Jua lilizidi kupanda juu, mwendo ukazidi kuwa mgumu, mchanga ukaishika miguu yao na kuifanya mizito kama iliyofungwa mawe. Wakiwa katikati ya jangwa lile, Seidon aligeuka nyuma na kuwaona watu wane wakija kwa kasi farasi, wakielekea ule upande ambao wao walikuwepo. Amatagaimba aliwatazama watu wale akiwa amesimama bila kufanya lolote, nao wakizidi kukaribi pale walipokuwepo.



    Amatagaimba alisikia mlio wa upanga ukifutwa kutoka katika ala yake, akamgeukia Seidon, akamuona ameushika upanga wa makali kuwili mkononi mwake. “Seidoni, yumkini watu hawa si wa shari, rudisha upanga wako mahali pake, tusije tukakosa Baraka za Klakos,” Amatagaimba alimwambia Seidon. Upanga ukarudishwa mahali pake na wote wawili wakasimama kwa heri. Wale watu wane wakawafikia Amatagaimba na Seidon, watu wale walikuwa wamevaa mavazi tofauti kwa rangi. Mmoja wao akashuka kutoka katika farasi, yeye alikuwa amevaa nguo nyeupe zinazometameta, sura yake haikuonekana sawasawa kutokana na kinyago alichovaa ambacho mbele badala ya sura kulionekana kama tundu kubwa jeusi. Akasogea na kumwasogelea Amatagaimba na Seidon, “Seidon, Amatagaimba,” aliwaita kwa kuwatazama kwa zamu kila mmoja kwa wakati wake, “Safari mnayokwenda ni ndefu sana ijapokuwa mmekaribia pale muendapo, sikilizeni kwa makini, sisi mnaotuona, tumetafuta hilo fuvu kwa karne na karne na hatukulipata ndio maana mwaona mvua hakuna, jua ni kali na kadhalika, ninyi wanadamu mnatutegemea sisi daima. Mimi ni Malaika wa Jua, huyo mwenye vazi la kijani ni Malaika wa Mvua, huyo mwenye vazi jekundu ni Malaika wa Vita na huyo mwingine mwenye vazi la kijivu ni Malaika wa ukame na shida, kila mmoja ana uwezo wa kuleta kile alichonacho na kukizuia.



    Tulipata maono kuwa ninyi mnalo hilo fuvu na mko mbioni kulirudisha kwa Cleopas, maamuzi mazuri sana, sasa twaomba tuwasindikize mpaka katika mlango wa piramidi ambalo Klakos ipo ndani yake hapo sisi tutasubiri nje na kuwatakia heri kwa hilo lililo jema kwa wanadamu.”

    Amatagaimba akamtazama Seidon na kumpa ishara ya kuwafuata, kufumba na kufumbua waliona farasi wao wakija pale walipo, wakashangaa kwa hilo, walipowafikia, wakawapanda na safari ikaanza, Amatagaimba na Seidon wakawa katikati na wale watu wakawa mbele wawili na nyuma wawili, safari ikaanza.

    Baada ya mwendo mrefu juani walifika eneo pana lenye uwazi mkubwa mno, hakuna kilichoonekana zaidi ya mchanga na upepo unaovuma ambao unafanya vumbi la kutisha, “Sisi ni pepo nne za dunia, hapa tulipo sasa ni katikati ya dunia, nguvu ya uvutano inatawala eneo hili tulilosimama,” alisema Yule wa kijani.



    “Nasikia vurugu kubwa huko katika dunia ya chini, ulimwengu unavutana na kuzimu, mbingu zimetulia,” akasema Yule mwenye guo jekundu. “Basi na tusisonge mbele, maana hapa tulipo ni mji wa wafu,” akamalizia Yule mwenye vazi la kijivu. Wakateremka kutoka juu ya farasi wao na kusimama chini, juu ya mchanga, wakakutanisha mikono yao pamoja na kufanya kitu kama mraba. Amatagaimba na Seidon hawakuelewa kinachofanyika, wale watu wakatulia kimywa wakiwa wameinamisha nyuso zao chini, mavazi yao yalikuwa yakipepezwa kwa upepo mkali uliofanya vumbi jingi. Mara tai mkubwa alipita kwa kasi katikati ya Seidon na Amatagaimba, kufumba na kufumbua Yule tai alikuwa amenyakuwa ule mfuko mweusi wa Seidon wenye fuvu, Amatagaimba bila kuchelea alichomoa mshale katika podo lake na kuuweka kwenye uta wake, akavuta huku akibana jicho moja na kumlenga Yule tai aliyekuwa akienda kasi sana, Amatagaimba alijuwa wazi kuwa kama tai Yule alitoka upande wa kusini basi lazima atarudi kusini aliufyatua uta wake na ule mshale ulichomoka kwa kasi ya ajabu, kila aliyeangalia kwa macho aliona mshale ule kuwa umepigwa upande tofauti. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Usimuuuueeeeee!!!!!!” Yule Malaika wa jua alipiga ukulele na mara ule upepo ukakatika ghafla na vumbi lote likatulia ardhini kama mwanzo. Wote nyuso zao zikuwa zikitazama kule juu kwa Yule tai, mshale ule kama ulivyotumwa, wakati Yule tai akijigeuza kurudi upande wa kusini alikutana nao na ukampiga shingoni, miguu yake ikaliachia lile fuvu likawa likidondoka kwa kasi kurudi ardhini, Seidon alikwea farasi na kupiga mbio kuelekea kule fuvu linakodondokea, Amatagaimba alimtazama Yule tai na badala yake hakumuona tai bali aliona taswira ya mwanamke ikija kasi kutoka juu kuja kwake, mbele ya mikono yake kulikuwa na donge kubwa la moto.



    “Tufaaaaaaannnnnnnnn” Yule Malaika wa rangi nyekundu, Malaika wa vita alipiga kelele na wengine wote wakalala chini katika mchanga, Amatagaimba aliuchomoa upanga wake na kuuweka barabara, Yule mwanamke akauzungusha ule moto na kuuwacha utangulie kabla ya yeye hajafika, Amatagaimba aliuepa kiufundi na kupiga upnga wake pigo la kifo lakini Yule mwanamke alipita na kutua akasimama chini. “Ni nani wewe mwanamke muovu?” Yule Malaika akauliza, “Sherhazad Malkia wa Soria,” Yule mwanamke alijtambulisha, kabla hajamaliza Yule Malaika wa vita akaizungusha mikono yake kwa namna ya ajabu na kutengeneza kitu kama moto uliokuwa ukiwaka mbele ya mkono yake na kuutuma kwa Sharhazad,



    lakini kwa nguvu ya kichawi, Sharhazad nae aliuzuia moto huo katikati, ukawa ukiwaka hewani, Amatagaimba aliona ile vita haiwezi alisimama kando, alipowatazama wale wengine aliona bado wamelala kifudifudi huku vumbi kubwa likitimka upya eneo hilo, mapigano yalikuwa makali mpaka ardhi ya eneo lile ilikuwa ikitetemeka, Seidon alisimama kando ya Amatagaimba akiwa na ule mfuko mkononi baada ya kuudaka salama, wakati mapigano hayo yakiendelea asrdhi ilizidi kutetemeka, radi kali zikapiga na kuchora michoro ya kutisha angani, mara kipande cha ardhi kikamegeka na kudidimia, pakabaki uwazi mkubwa sana, Yule mwenye vazi la kijivu akawatazama na kuwaamuru kuingia kwa ishara ya mkono. Hakuna aliyesita, Seidon na Amatagaimba waliingia kwa kasi kwenye lile shimo wakiacha vumbi likitimka huko nje kwa jinsi ardhi ile ilivyokuwa ikizidi kutetemeka, hofu iliwajaa mara giza nene likatawala mbele yao,



    Seidon alipogeuka nyuma hakuona mwanga wan je, ardhi imejifunga. Amatagaimba akapapasa ukutanai na kushika kitu kama mti kilichopachikwa katika kiango, akauchomo na kugundua kilikuwa ni kienge ambacho kingewasaidia kuona humo ndani, Amatagaimba akachukua kitu mfano wa kijiti katika pindo la vazi lake, akakisugua katika nywele zake kile kijiti kikashika moto, akawasha kile kienge na mwanga wakutosha ukatokea. Seidon alisikika akishusha pumzi ndefu, kisha wote wawili wakaongoza kwenye ujia mrefu ulioonekana ukielekea mbele zaidi. Huku wakisaidiwa na ule mwanga kutoka katika kile kienge walitembea kwa tahadhari kubwa, Seidon alikuwa mbele wakati Aamatagaimba alikuwa akifuata kwa nyuma.



    Mchakato wa miguu ya farasi anayekimbia kwa kasi ilisikika, kwa jinsi ilivyosikika hakuna aliyejua ni upande gani ilitokea, mbele au nyuma. Mara ghafla upande wa nyuma waliona moto mkubwa ukija, wakaanza kutimua mbio kuelekea mbele, walikimbia na kukimbia lakini bado farasi Yule wa moto alikuwa akija kasi na akizidi kuwakaribia, “Orion,” Seidon akamwambia Amatagaimba huku akikimbia. Amatagaimba akasimama na kugeuka nyuma huku tayari akiwa na upanga wake mkononi, Seidon alizidi kukimbia bila kutazama nyuma. Amatagaimba alipigwa kikumbo kikali kabla hajautumia upanga wake, kwani kasi ya Yule farasi alishindwa kabisa kuidhibiti kwa upanga wake huo.



    Baada ya kikumbo hicho kilichomfanya ajibamize vibaya ukutani, alijikuta anaishiwa na nguvu na upanga wake asiuone mkononi mwake, haraka akautoa uta wake na kuchukua mshale ambao aliupachika na kuuvuta kwa kulenga shabaha kwa Yule farasi wa moto, alipouachia mshale ule ulikwenda moja kwa moja ukimuelekea Yule farasi wa moto ambaye sasa alikuwa sambasamba na Seidon. Seidon alimshuhudia aliyekuwa juu ya farasi huyo, akianguka udongoni kwa kishindo na kusababisha mlipuko mkubwa uliotetemesha pango lote hilo, mara vumbi na mchanga vilionekana kutokea katika nafasi zilizomo kati ya jiwe na jiwe. Amatagaimba aijinyanyua haraka na kukimbilia kule ambako Seidon naye al;ikuwa ameanguka baada ya mlipuko ule kumsukuma. Akamshika mkono na kumvutia kando.



    Mchanga ulizidi kumwagika kutoka katika ile mipenyo na pango zima likawa linatetemeka, “Amatagaimba, tuondoke hapa si salama,” Seidon alimwambia Amatagaimba wakati huo yeye akiwa tayari ameanza kuondoka eneo lile, Amatagaimba naye akaanza kutimua mbio kumfuata Seidon, ule moto uliendelea kuwa mkubwa na ukaanza tena kuwafuata huku mbele yake ukitanguliwa na upepo mkali sana. Katika kimbia hiyo Seidon aliona katika ukuta kuna kitu kama kichwa cha farasi lakini kilichochongwa kawa kutumia jiwe kikiwa kimejitokeza katika moja ya mawe yale yaliyopangwa kwa ustadi kufanya lile pango kuonekana katika hali ile. Seidon alilishika kwa mikono miwili lile jiwe lenye umbo la kichwa cha farasi, akafanya kama anabembea, akitumia mikono yake na kuinyanyua miguu yake, uzito wake ulifanya lile jiwe kuinama na mara baadhi yam awe yakaaza kurudi kwa ndani na kutengenea uwazi mdogomdogo katika kuta hizo. Amatagaimba aliona mawe ya mbele yake yakifunguka na kufanya kitu kama mlango,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hakuuliza aliingia na kusimama ghafla kisha akageuka nyuma na kumchungulia Seidon ambae alikuwa tayari ameliachia lile jiwe na kukimbili kule aliko Amatagaimba wakati ule moto nao ulikuwa umemkaribia sana, kabla hajaufikia ule mlango tayari moto ulikuwa umemfikia, “Amataaaaaaaaaaaaaa!!!!!!” alipiga ukulele na kabla Amatagaimba hajafanya lolote mara ilipiga radi kali sana iliyofanya mistari ya mwanga wa kutisha ndani ya pango lile, na ghafla mvua kubwa ikaanza kunyesha, ajabu. Amatagaimba aliishuhudia mvua ile ikinyesha bila simile ikitoka tu juu ya pango lile ambalo lilikuwa limeezekwa kwa mawe kwa ufundi wa hali ya juu, akanyosha mkono wake na kuushika ule wa Seidon kisha akamvuta kule alikokuwa yeye, mara ile mvua ikaacha kunyesha ghafla, na ule moto ulikuwa umezimika wote, Amatagaimba alitazama na hakuona farasi wala mtu aliyekuwa na farasi, ‘Orion?!’ alijiuliza huku amejishika kifua, moyo ukimwenda mbio, akamtazama Seidon aliyekuwa kajilaza chini akitweta.



    “Tuondoke,” Seidon alimwambia Amatagaimba huku akinyanyuka na kifuata njia hiyo inayopita chini kwa chini, sasa hawakuwa na kile kienge cha moto kwa ajili ya kuwaangazia, giaza liliwafunika kama kawaida, Amatagaimba akakumbuka kitu, akaufungua ule mfuko uliofungwa mgongoni mwa Seidon, mfuko wenye fuvu, akalitoa na kukuta liking’aa katika macho yake na kufanya mwanga mkali na mweupe kama wa jua la mchana. Mara baada ya kulito na kupata mwanga huo alianza kusikia kama kelele za vikaragosi vikishangilia na kukimbia huku na huko, “Nini hicho?” Seidon aliuliza. Amatagaimba akatega sikio kusikiliza akainua mkono wake na kuitazama pete yake ya ajabu, ndani ya pete hiyo aliona viumbe vya ajabu vikikimbia huku na huko, vingine havikuwa na vichwa, vungine vina mguu mmoja, vingine vilikuwa na shepu isiyoelezeka kimaandishi labda kimichoro.



    Amatagaimba akashusha mkono wake chini, akamtazama Seidon, “Tupo kwenye roho chafu,” Amatagaimba alimwambia Seidon huku akimzuia kwa mkono wake maana Seidon alitaka kupita mbele yake, akamtazama Seidon na kumwambia, “Hapa lazima tupite kinyumenyume ili hizi roho chafu zisituone,” wakafanya hivyo, wakapita eneo lile kinyumenyume, bado waliendelea kusikia vishindo vya roho hizo zikimbia huku na huku huku zikipiga kelele kama za panya walionaswa katika mtego. Baada ya kuvuka eneo hilo wakajikuta wametokea eneo la wazi kisha kuna ngazi ndefu inayoshuka chini na huko chini kunafuko moshi kana kwamba kuna moto uliozimwa muda huohuo, wakasimama na kuangaza macho yao kule, “Hamunaptra,” Seidon aliongea kwa kunong’ona. Ni Amatagaimba tu aliyemsikia, kisha wote wawili wakaanza kutelemka zile ngazi kwenda kule chini, walipofika katikati ya waliikuta ile ngazi imeishia hapo na ule mji waliouona ukali mbali bado, wakasimama na kushangaa jambo hilo.



    Walipokuwa kule juu waliiona ile ngazi imejichoma katika ule moshi, kumbe ilikuwa imeshia pale. Amatagaimba akabaki kuduwaa hajui afanye nini, alipogeuka nyuma alikuta hakuna ile ngazi ila yeye kasimama juu ya nguzo ndefu ambayo juu yake kulikuwa na eneo dogo sana la nusu mita ya mraba, alishindwa afanya nini, alipomtazama Seidon naye alikuwa katika nguzo nyingine kama hiyo. Amatagaimba aliangali chini ilikoanzia nguzo ile hakuona kutokana na kitu kama moshi kutanda eneo hilo, alichokiona ni urefu mfupi wa nguzo kama mita moja hivi zaidi ya hapo ni moshi uliokuwa ukipita kutoka sehemu moja kwenda nyingine ambao haukuwqaruhusu kuona chini kabisa zilikoanzia nguzo zile. Sauti za farasi na watu zilisikika mbali sana kutoka chini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    §§§§§§



    “Aaaaaaaaaa ha ha ha ha ha ha ha ha …” ilikuwa sauti kali ya Sherhazad iliyosikika akiangua kicheko kikali ambacho kiliwatoa ndege kwenye matundu yao. Alivuta hatua chache kutoka kiti chake cha enzi kilichotengenezwa kwa dhahabu safi, akateremka vijingazi hivyo huku akifuatiwa na vazi lake refu lililokuwa likimetameta kwa jinsi lilivyoundwa, kwa maana halikushonwa.

    Chini katika sakafu ya jumba hilo la kifahari kulikuwa na wazee wanne waliolala kifudifudi kuonesha heshima kwa Malkia huyo wa Soria. “Inukeni enyi wazee wangu,” aliwaamsha nao wakaamka. Akawatazama mmoja mmoja kisha akaangalia kule kwenye dirisha lake la kichawi na kuwaona Amatagaimba na Seido wakiwa bado katika zile nguzo, akacheka tena cheko lake la ajabu.



    “Asanteni sana kwa kazi mliyoifanya ya kuwatega wale wajinga pale, sasa tunakwenda kuwamalizia palepale kwani hawana uwezo wa kukimbia,” aliposema hayo akatoa vazi lake alilojifunga shingoni na kuonesha jeraha lake kubwa, “Hapa ni upanga wa Amatagaimba umepita, lazima moyo wake niutafune nyama, twendeni,” Sharhazad akaamuru. “Sikiliza ee jirani sana na mwezi kwa sasa, hivyo mpaka yapite majua mawili,” alisema mmoja wa wale wazee, kisha mwingine naye akafungua kinywa chake akasema, “Tazama ee Malkia, Amatagaimba, shujaa wa msitu wa Solondo ana pete ya ajabu aliyopewa na Malkia Baghoza wa msitu wakati alipoweza kuurudisha utawala wake kwa kumuangamiza Kelume, akiwa na pete ile kamwe hatutaweza kumshinda, isipokuwa tunaweza kupotea sisi wote, na utwala wako ukaanguka vibaya,”



    Yule mzee aliposema hayo Malikia Sherhazad alikunja sura yake na alionekana wazi hasira kumjaa kichwani mwake, radi kali zilipiga na kupasua anga, wale wazee wakaanguka kifudifudi, “Si hivyo ee Malkia, bali tahadhari ni muhimu kuliko hatari,” walisema wote kwa sauti moja. “Ninyi mnajua wazi kuwa tukilipata lile fuvu, sisi ndiyo tutakuwa na sauti juu ya ulimwengu wote wa majini, wale pale wameshafika Hamunaptra na tukiwakosa wakiingia katika pyramid kubwa, chini ya ardhi basi hatutawaweza tena,” Sherhazad aliwaeleza wale wazee, “Na sasa nataka niiteketeze hiyo pete ya Baghoza kwa moto wa ajabu kabla hatujaenda pale,” akaongeza kusema huku mikono yake ikiwa imeshikishwa kiunoni. Akautoa mkono wa ke wa kushoto na kuongea lugha ya ajabu lugha isiyoeleweka, macho yake yakageuka na kuwa mekundu kama makaa ya moto, ulimi wake ulikuwa kama muale wa moto unaowaka kwa nguvu, Sherhazad alipandisha sauti na kuwa makelele mengi ndani ya jumba lile kisha akatema donge kubwa la moto lililopita katika lile dirisha la ajabu na kupotelea milimani. Wale wazee waliinuka na kutazama pambano hilo litakalotokea huko katika mji wa Hamunaptra.



    §§§§§



    AMATAGAIMBA akiwa pale juu ya nguzo bado alikuwa hajui la kufanya kwa kuwa hakuwa anajua urefu kwenda chini, kila alipoangalia bado ni mawingu au ukungu ulimnyima uhuru wa kuona chini. Akiwa katika kutazama hilo alisikia sauti ya Seidon ikimpa tahadhari kuwa kuna kitu kama jiwe kikimjia kwa kasi, Amatagaimba aligeuka na kuona ile dhahama inayokuja, akashindwa afanye nini, alishangaa badala ya jiwe sasa liligeuka kuwa donge la moto, Amatagaimba akafikiri haraka na kujiweka tayari kuukinga moto ule, ulipofika akaepa ukapita pembeni lakini alishangaa moto ule ulikuwa ukija mkononi mwake, akagundua baadae kuwa ni pete inayotafutwa, akainua mkono akaibusu na kisha akanyoosha ule mkono wenye pete na kuusukuma kwa kasi ule moto kurudi ulikotoka, kitendo kile kilimfanya kuyumba na kudondoka kutoka pale aliposimama, alijitahidi asidondoke lakini haikuwa hivyo, alidondoka ila katika kujikinga akatanguliza mguu mmoja cha kushangaza hakudondoka badala yake mguu ule ulikanyaga ardhi umbali wa nusu mita tu kutoka pale aliposimama.

    “Shiiit,” alitoa sauti hiyo na kumwambia Seidon ashuke kutoka pale alipo kuwa hakuna shimo eneo lile, Seidon akaruka na kutua chini kisha wakatimua mbio kushuka poromoko lile kuelekea chini, wakaingia kwenye pango kubwa. Amatagaimba alipogeuka nyuma hakuona ule moto, wakendelea kusonga mbele na walipoibuka upande wa pili, waliona mapyramid mengi sana yaliyojipanga katika mtindo mzuri.



    “Sasa tupo Hamunaptra, inabidi tutafute pyramid la kale kuliko yote, humo ndimo tutapata Clakos,” Amatagaimba alisema hayo huku akiwa kasimama akiangalia yale mapiramidi, Seidon alikuwa nyuma yake tu nae akiuangalia mji huo. Akikumbuka jinsi alivyofika kwa mara ya kwanza kwa shida kuchukua fuvu lile. Wote wawili wakaendelea kutembea kwa kupita njia zinazowaficha ili watu wenye nia mbaya wasiwaone na kuwadhuru, lakini bado watu walikuwa wakiwakodolea macho kila hatua wanayopiga. Baada ya mwendo kidogo walikutana na mzee mmoja wa makamo, aliyevaa guo refu na kufunika kichwa chake, alionekana uso tu, uso wake ulikuwa ni kama wa kijivu hivi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia, Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja naye. Mbele kidogo wakaingia kwenye piramidi moja dogo lakini lililoonekana kumegekamegeka vipande, lilionekana ni la kale kuliko yote. Wakaingia ndani, chumba kilikuwa na giza lakini mishumaa ilijitahidi kulishinda giza hilo, Seidon akiwa na mfuko wake barabara mkononi mwake na upanga wa Vernadi kiunoni mwake, alikuwa akifuata kwa makini kila apitapo mzee Yule, Amatagaimba naye vivyo hivyo, yeye alikuwa nyuma kabisa akiwaacha Seidon katikati na Yule mzee mbele yao.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog