Search This Blog

HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA - 4

 







    Simulizi : Hamunaptra - Mji Uliopotea

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Joto kali lilitawala katika piramidi lile, joto lililotokana na wingi wa mishumaa iliyojazwa katika vitu kama ngazi nyingi zilizozunguka katika piramidi hilo. Baada ya mwendo kidogo, Yule mzee akawanyooshea mkono kuwapa ishara ya kusimama, nao wakatii na kusimama. Hakuna kilichoendelea kati yao isipokuwa joto lililowafanya kulowa kama wamepita kwenye mvua.

    “Joto kali, kwa nini msizime mishumaa hii?” Seidon akauliza. Yule mzee akatulia bila kujibu kisha akageuka kumtazama.

    “Dunia yenu haiwezi kuwapa uhai ninyi bila mishumaa hii, endapo itazimika piramidi hili litajifunga nikimaanisha pande nne za piramidi hili ndizo pepo nne za dunia, hapa ndipo penye majira ya mwaka, panapogawa miezi, siku na miaka, ndipo panapofanya jua liwake, mvua inyeshe, hapa ndipo penye kila kitu, ukitaka kwenda mwaka 2000 unaweza, ukitaka kuona yatakayotokea kesho na miaka mia nne ijayo hapa ndio mahali pake, kwa kifupi niwaambie kuwa hapa ndipo katikati ya dunia, kitu chochote chenye madini ya chuma hakiwezi kuanguka chini wala kutoka mahali kilipo,”



    Yule mzee akamjibu Seidon, kwa Seidon na Amatagaimbailikuwa kama simulizi ya kusadikika hakuna aliyeamini ukweli wa maneno hayo, wakatazamana kwa mara nyingine tena na kisha kila mmoja akacheka peke yake moyoni. Amatagaimba akaushika upanga wake na kujaribu kuuchomoa kutoka katika ala yake lakini upanga ule uling’ang’ania katika ala, haukutoka, Amatagaimba alijaribu tena na tena lakini hali ilikuwa ileile, akamwambia Seidon ajaribu naye kuutoa wa kwake lakini hakuna aliyeweza.

    “Ina maana hamuniamini ninachowaambia?” Yule mzee aliuliza, “Sikieni ninyi wanadamu, katika dunia ya sasa huu sio mwaka mnaouishi, sasa mnaishi katika dunia ya kale, kama hamtakuwa na imani basi mjue safari yenu hamtofika kwa maana ili mfike Hamunaptra, mji wa wafu, mji uliopotea ambao upo chini kabisa ya ardhi lazima mvuke daraja la pepo, daraja ambalo lazima ufunge milango yako yote ya fahamu ndipo uweze kuvuka ukishindwa utatumbukia katika shimo kubwa ambalo kwenu duniani mnaliita kuzimu huku linaitwa bonde la uvuli wa mauti,” maneno hayo ya Yule mzee yaliwafanya Amatagaimba na Seidon kuingiwa na hofu kuu.



    “Mbona hatuendelei mbele?” Amatagaimba akauliza.

    “Ha ha ha ha haaaa!!!!” sauti ya kicheko cha kutisha kutoka kwa Yule mzee ikatawala mle ndani na kufanya mwangwi wa kutisha, “Hatuwezi kupita hapa sasa kwa sababu dunia hivi sasa inapishana na sayari ya Venus kwa upande huu wa Mashariki, hivyo kuna tetemeko kubwa la ardhi hatuwezi kuvuka,” Yule mzee aliwaeleza. Baada ya dakika chache waliona kitu kama vumbi kikipukutika kutoka katika kona za piramidi hilo, Amatagaimba akataka kufumba macho ili kuepuka vumbi hilo lakini alikatazwa na Yule mzee, akaambiwa kuwa ndani ya piramidi hilo hutakiwi kufumba macho hata mara moja. Ikabidi wote watulie hivyohivyo mpaka dhoruba ya tetemeko na vumbi ilipopita.

    “Sasa tunaweza kwenda, kulikabili daraja la pepo, tukifika eneo linaloitwa milima mitano itabidi kufanya ibada ya kufunga milango ya fahamu ili kuvuka daraja hilo, hapo hapahitaji utani hata kidogo,” Yule mzee aliwaasa kisha wakaendelea na safari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Giza lilikuwa nene, kati yao kulikuwa na wadudu wengi wa vimulimuli ambao walifanya nuru ya kupendeza, walitembea polepole wakimfuata Yule mzee aliyekuwa akiwaongoza njia. Mbele kidogo wakasikia sauti kama ya maji yanayopita mbali katika maporomoko makubwa. Amatagaimba akasimama na kugeuka huku na kule, ndani ya mlio huo wa maji alikuwa akisikia mlio wa farasi na mvumo kama upepo mkali. Yule mzee nae akasimama, akaonesha ishara tena ya mkono kisha wote wakasimama.



    “Orion!” Yule mzee akasema kwa sauti ya taratibu, Amatagaimba akaushika upanga wake tayari kwa pambano lakini hali ilikuwa ni ileile, upanga haukutoka katika ala yake. Amatagaimba hakuwa na ujanja, Seidon naye alijaribu lakini haikuwezekana, “Tupo katikati ya usumaku wa dunia, hakuna kitu cha chuma kinachoweza kufanya lolote hapa,” Yule mzee aliwaambia. Kisha akawapa ishara ya kuondoka na kuongeza mwendo.



    §§§§§



    ORION alijua wazi kuwa hapo katika daraja la pepo ndipo pa kuweza kutimiza azma yake kwani alielewa wazi kuwa hakuna silaha ya chuma itakayotumika. Orion alipiga mbio na farasi wake kulikabili lile daraja.

    “Ongeza mwendo Orion anatukaribia,” Yule mzee aliwahimiza akina Seidon ambao walikuwa wakitembea kwa tahadhari kwani giza lilikuwa nene mno. Amatagaimba akajipapasa na kujikuta akiwa na kamba kiunoni mwake, akafikiri jinsi ambavyo ataitumia kamba hiyo kuwa silaha dhidi ya Orion mwindaji mashuhuri wa enzi na enzi mwenye shabaha isiyokosa hata mara moja.

    Seidon na Amatagaimba walikuwa wakionekana wazi kwa macho ya ajabu ya mwindaji huyo aliyepewa kazi maalum na wachawi wa Misri kuhakikisha analipata fuvu la Cleopas. Akainua uta wake mkubwa wenye nguvu alioamini kuwa kwa kasi ambayo mshale huo utachomoka katika uta wake lazima utapasua nguvu za usumaku na kumfikia Seidon ambaye alikuwa nyuma tu ya Yule mzee.



    Akauvuta kwa nguvu zake zote huku misuli ya mikono yake mikakamavu ikiwa imedinda na kufanya nyama ya mikono hiyo kuwa ngumu ajabu.

    Ilikuwa bado hatua chache sana Amatagaimba na Seidon kumaliza ule ukanda wa usumaku wa dunia, ila Yule mzee tayari alikuwa amepita eneo lile. Mshale wa Orion ukaja kwa kasi ya ajabu mvumo wake ukawastua wote, ulikuwa ni kama mruzi upigwao. Kutahamaki Yule mzee alipigwa kichwani na ule mshale wa Orion, mshale wa kichawi, ukamtawanya kichwa chote na kisha kiwiliwili chake kubaki kimesimama vilevile. Seidon aliuona mshale ule ukimjia usoni, akatamani kupiga kelele lakini akajikuta akishindwa, akashangaa mshale ule ukisimama sentimeta chache kutoka usoni kwake, ukaganda kama igandavyo barafu ndanin ya jokofu, Seidon akashusha pumzi ndefu na kujaribu kuushika ule mshale.



    “Acha!,” Amatagaimba akamwambia Seidon, “Mshale huo umenasa katika nguvu za usumaku,” Seidon akaelewa kwa nini, akakumbuka Yule mzee alivyowaambia kuwa hakuna kitu cha chuma kinachoweza kufanya lolote katika eneo lile. Wakavuka na kufika eneo la pili eneo la milima mitano. Mbalamwezi ya kung’aa iling’aza eneo hilo lote na vilima vile vilionekana wazi umbali mfupi tu mbele yao, lakini hawakujua ni wapi watapita, Yule mzee tayari alikuwa hana kichwa na aliganda palepale kama nguzo. Mbele ya milima ile kulikuwa na giza linguine nene lisilo hata na vimulimuli, katikati ya giza hilo kulikuwa na kitu kama ujia mdogo uliokuwa uking’aa sana, daraja la pepo. Wawili hao wakatulia kwanza na kutafakari, wakiwa kimya kabisa, mara wakasikia mvuma mkali wa mbawa za ndege mkubwa.

    “Pelargonis,” Amatagaimba akaongea taratibu.

    “Umesemaje?” Seidon akauliza, kabla Amatagaiba hajajibu alijikuta kapigwa na ubawa mkubwa wenye nguvu wa ndege huyo na kuanguka mbali, Yule ndege akataka kunyakuwa ule mfuko wa Seidon, lakini Seidon naye hakukubali, mara hii alipoufuta upanga wake ukatoka ndani ya ala, akaushika kwa mikono yake miwili na kuanza kupambana na ndege huyo mkubwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Amatagaimba alijaribu kuinuka, na alipofanikiwa tayari idadi ya ndege wale iliongezeka na kumfanya Seidon kuelemea nao. Amatagaimba akautoa uta wake mgongoni na kuchukua mshale katika podo lake, shabaha yake haikuwa haba, kila mshale mmoja ulikuwa ukiangusha ndege mmoja. Yule ndege aliyeonekana kama ndio mama yao akaona wenzake wanavyopukutika, akamuacha Seidon akipambana na wengine yeye akamjia Amatagaimba, shabaha yam shale wa Amatagaima ilikielekea kichwa cha ndege Yule, lakini hakuamini kilichotokea, Yule ndege akaudaka mshale ule kwa midomo yake mirefu na kuuvunja. Amatagaimba akatoa kamba iliyokuwa kiunoni mwake na kuanza kumkabili ndege huyo wa kutisha. Aliizungusha ile kamba kwa ustadi mkubwa na alipoiachia Yule ndege alishuka chini zaidi na ile kamba ikapita juu, Amatagaimba alijirusha upande mwingine na shambulizi la ndege huyo likakosa lengo.



    Seidon kwa kutumia upanga wake aliweza kukata ndege wengi sana lakini alikuwa amechoka sana nab ado pambano lilikuwa likiendelea. Amatagaimba akiwa chini alikuwa hana ujanja mwingine Yule ndege alikuwa akija tena huku kapanua domo lake tayari kumdonyoa, akili ilikuja mara moja, kulikuwa na jiwe pembeni akaliinua na kulirusha, likatua sawia ndani ya domo la ndege huyo, likamkwama kooni, akaanguka na kujirusharusha huku nakule, Amatagaimba akachukua nafasi hiyo akauchomoa upanga wake na kumkata kichwa. Alipohakikisha kiumbe huyo amekwisha, ndipo alipomtazama Seidoni aliyekuwa bado akipambana na ndege hao. Kwa kutumia upinde na mshale wake aliweza kuwapiga ndege wote na kumkamata mmoja kwa kutumia ile kamba. Walimfunga barabara, alikuwa ndege mkubwa sana na wa kutisha ambaye hakuwahi kuishi wakati wetu huu, wote wawili walitweta wakiwa na kiu cha ajabu lakini hawakuwa na hata tone la maji.



    “Amatagaimba, tutavukaje daraja la pepo ilhali aliyekuwa akituongoza amekufa?” Seidon akauliza.

    “Swali gumu Seidon, tazama daraja lilivyo refu, na halina ukingo katika pande zake,” Amatagaimba alionesha mashaka katika hilo.

    “Na hapa si salama kwetu, itakuwaje kama Orion atatukuta hapa?” Seidon akauliza. Amatagaimba hakujibu neno, akainua mkono wake na na kuigonga kwa kwenzi mara tatu ile pete yake. Mara mbele yake pakatokea moshi mikubwa mno, Amatagaimba akatulia akiutazama na katikati yake alionekana Bagoza, bibi jinni wa Solondo, akiwa kazungukwa na upepo mkali uliochanganyika na ndimi za moto.



    “Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba, nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana, nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la Hamunaptra, ukishafika katika mlango huo, ingia bila woga, ijapokuwa Hamunaptra ni mji wa wafu, usiogope ndani yake kuna mji mkubwa sana ambao katikati ya mji huo kuna Clakos chini ya ardhi. Sasa shikeni njia mpita Mashariki kuzunguka milima mitano, baada ya majua mawili tu mtakuwa mmefika Hamunaptra, yeyote mtakayekutana naye njiani msiongee naye wala msimpa mkono, katikati ya njia mtapata shida kwa maana lazima mpitie mji mmoja katikati yake lakini mtavuka tu,” Baghoza alimueleza Amatagaimba.



    “Ewe baghoza malkia wa majinni, tunamhofia Orion na Sharhazad, je tutafika?” Amatagaimba aliuliza kwa mashaka huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.

    Baghoza akaizungusha fimbo yake katika pepo zote nne, kisha akamgeukia Amatagaimba.

    “Orion haonekani, Sharhazad haweze kuwashambulia hapa kwani nayeye hawezi kuvuka daraja la pepo, nendeni msichelewe, jua la tatu litapatwa na mwezi, huo ni wakati mbaya sana kwetu, je vipi kuhusu ninyi?” mara ule upepo ukaongezeka, vumbi likatimka na baghoza akatoweka mbele ya Amatagaimba. Aamatagaimba akaitazama pete yake, kisha akainuka kutoka pale alipokuwa amepiga magoti.

    “Amatagaimba umekiona kimbunga cha ajabu?” Seidon akauliza.

    “Je wewe uliniona wakati wa kimbunga hicho?” Amatagaimba akamwuliza Sedon.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana,” Seidon akijibu kwa woga.

    “Hakikuwa kimbunga, ila mimi nilikuwa ndani yake, Seidon, sasa twende hatua ya mwisho ya safari yetu,” Amatagaimba alipokuwa akisema hayo, mara matone ya mvua yakaanza kuwatonesha, Seidon aliachama kinywa chake na kuruhusu matone kadhaa yaingie ndani yake, kiu yake ikakatika na nguvu zikamrejea tena. Kisha wote wawili wakashika njia kuielekea milima mitano, Seidon alikuwa mbele na mfuko wake mweusi wenye fuvu ndani yake, Amatagaimba alikuwa nyuma yake, hakuna aliyeongea kila mmoja alikuwa akifikiri juu ya safari hiyo ya hatari.

    Jua lilipokuwa likizama Amatagaimba alikuwa amechoka bila kificho.

    “Tupumzike hapa na tupate chakula,” Amatagaimba akamwambia Seidon, wakaingia katika moja ya mapango yam awe yaliyokuwa eneo hilo na kuketi wakiangazwa kwa mbala mwezi. Seidon akafanya moto wa kuota maana baridi ilikuwa kali, wakatafuna masurufu waliyokuwa wamebeba, na wote wakapata usingizi.



    §§§§§



    Usiku wa manane, Amatagaimba na Seidon wakiwa wamelala katika pango hilo. Orion akiwa juu ya farasi wake mkubwa alivuta harufu na kuhisi kuna wageni pande hizo. Akamuongoza farasi wake kuelekea milima mitano ambako alipata hisia juu ya watu hao.

    Upepo uliendelea kuvuma na kuufanya ule moto waliokuwa amekoka Seidon kuongezeka na kufanya joto kali ndani ya pango lile. Orion alifika na kusimama mbali, kila alipojaribu kuvuta harufu ile aliyoisikia mwanzo hakuipata badala yake joto kali la moto lilipenya pua zake na kumuumiza mapafu yake, akarudi nyuma zaidi na kusimama, hakuna ujanja.



    KATIKA MJI WA SORIA



    NDANI ya kasri kubwa la Shrhazad, kulikuwa na watu walewale, wazee wa kichawi waliojaribu kuisitisha safari ya Amatagaimba na Seidon wakashindwa. Sasa walikuwa wakisubiri muda ufike ili kupambana upya.



    “Sikilizeni enyi wachawi wa Soria, Seidon na mwenzake wapo katika mapango ya Oregon, jirani kabisa na mji mtukufu wa Hamunaptra, lazima watavuka nchi ya Sharidan katika kijito cha Usoil, sasa na tuwasubiri pale kijitoni, mara hii tusikubali kabisa kulikosa lile fuvu maana ile ni neema ya Clakos, tukilipata tutaitawala dunia yote na itakuwa chini ya neno letu,” Sharhazad aliwaambia wachawi wake huku akitoka katika dirisha lake la ajabu. Akakiendea kiti chake cha enzi, kiti kilichotengenezwa kwa dhahabu safi na kung’azwa kwa moto mkali wa kuyeyushia chuma, vazi lake refu jeupe lenye mkia mrefu lilimfanya Malkia huyu kuonekana mkubwa kupita kiasi lakini alikuwa na mwili mdogo isipokuwa alikuwa na nguvu sana dhidi ya maadui wake, kila tawala iloimuogopa Sharhazad kwani alikuwa na uwezo wa kukugeuza chochote anachokitaka na usimzuie. Akakei juu ya kiti chake, na wale wazee wachawi wakainama mpaka chini kumpa heshima yake, kisha wakainuka na kuketi kwa kutumia magoti yao ilhali miguu yuao wameikunja kwa nyuma.



    “Tufanyeje tuwaangamize wale watu?” akauliza Sherhazad.

    “Mtukufu malkia, pete ya Amatagaimba ndiyo pekee inayotukwamisha kukamilisha ulilotutuma, ni lazima kwanza tuikamate pete ile kisha kazi inayobaki ni ndogo sana, kumbuka wakifika tu kwenye mstari wa Ikweta kamwe hatutawaweza tena kwani pale tayari Clakos itaona fuvu lake na nguvu za ajabu zitakuwa juu yao, tutafanya nini ee Malkia?” mchawi mmoja kati ya wale waliokuwepo pale akajibu huku akitetemeka kwa woga.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwa nini u muoga sana wewe? Kwa nini unaonesha kukata tama wakati tama yenyewe imeijaza mioyo yetu sote, nitakupeleka kwenye ulimwengu wa wadudu watambaao kwa jinsi zao mara moja endapo utaonesha udhaifu wako tena,” maneno makali ya Sharhazad yaliyokuwa yakimtoka kinywani huku yakisindikizwa kwa radi kali yaliwafanya wazee wote wainame tena kumpa heshima Malikia.



    “Ee malkia wa Soari uishi milele!!!” wote walisema maneno hayo.

    “Fusha mafusho, ili majinni yote yakusanyike,” Sharhazad akatamka. Mchawi mmoja wapo akachuku kitu kama kibuyu kikubwa, akatia ubani mwingi na vitu vingine kama amdalasini, akasema maneno ya ajabu katika lugha ya kicawai lugha yao wanayoielewa wao wenyewe, mara moshi mzito ukaanza kutoka kwenye kile kibuyu, harufu izuri ya udi, ubani na manukato ya ajabu yalilijaza lila kasri zima. Sauti za watu wengi zikaanza kusikika kama watu wanaobadilishana mawazo ya jambo Fulani.

    Kishindo cha kofi kali kikasikika, ukimya mkuu ukatawala, Sherhazad sasa likuwa kabadilika sura yake na kuwa Joka kubwa lenye vichwa vitatu, likiwa pale juu ya kiti, likanyoosha shingo yake huku na kule. Kisha likafungua kinywa chake na kuanza kuanza kunena kwa lugha yao.



    “Umefika wakati wa kuitawala dunia na pepo zake zote nne, viumbe yabisi na viumbe hewa vyote view chini ya mamlaka ya Soria, nyote mnajua kwa karne nyingi tumekuwa tukilitafuta fuvu la Cleopas ili kupata neema za Clakos zenye wingi wa mamlaka juu na chini ya mbingu, viumbe wawili wanalirudisha fuvu hilo kwa Cleopas, na wamebakisha jua moja tu kufikia lango la Hamunaptra, nimewaita ili sasa sisi sote tuweze kufanya kila hila tulipate fuvu hilo kabla hawajaingia nalo ndani ya Hamunaptra, mimi na wengine wachache tutawasubiri katika kijito cha Usoil, lakini nataka ninyi mutangulie mbele kufanya hila ya kuwazubaisha,” Sharhazad aliongea na viumbe wake kwa sauti ambayo wewe mwanadamu wa kawaida ungesiki milio ya ajabu ajabu tu ikimtoka nyoka huyo.



    “Ewe malkia mtukufu, sote tuko hapa kulinda na kuhakikisha utawala wako wenye nguvu hauanguki, yumkini hawa ni nani? Viumbe dhaifu vya dunia ya kesho hata vituzuie sisi ambao tuna nguvu, mamlaka na enzi kuikamilisha kazi yetu? Tunakuahidi kutekeleza na kuitawala dunia, kwa kuwa wale ni nyama na mifupa tutawapiga kwa magonjwa nao hawatakuwa na uwezo tena,” mmoja wale waliokuja pale aliongea.



    “Aaaaaah! Wewe bado ni mchanga sana kati ya wachanga, kumbuka katika mbingu hii magonjwa hayana nafasi, sisi tunaweza kuwapiga kwa magonjwa wakiwa kwao duniani, lakini katika ulimwengu huu wa jinni ya jinnu hakuna hewa inayotembea hivyo magonjwa hayawezi, lakini tumieni sura na maumbo yenu ya kuazima ili kuwatia udhaifu wale,” Sharhazad akatoa maelekezo kwa viumbe wake, kisha kwa kupitia dirisha lake la ajabu akawaonesha Amatagaimba na Seidon mahali walipo. Lakini jambo moja liliwashtua wote waliomo katika kasri lile. Walimuona Orion akiwa kasimama juu ya farasi wake mweupe, farasi anayeweza kuchomoa mbawa na kuruka kama ndege wa kawaida ‘pegasus’. Sherhazad alijawa na hofu.



    “Na huyu ni kikwazo kingine,” akawaambia.

    “Ewe Malikia mtukufu wa Soria, Orion ametumwa na wachawi wa Misri ili apate fuvu lile na kuwapeleka kisha wao watampa maji ya uzima ambayo kwayo kamwe hatoweza kufika katika miisho ya maisha yake,” mwingine akasema na kumwambia Sharhazad, akahamaki kwa jibu hilo.

    “Na tumuweke katika jalada la maangamizi kabla ya jua la mashariki ijayo,” Sharhazad akawaagiza na kisha moshi ule wa mafusho ukakatika ghafla, kasri likabaki tupu, kitini alikuwa yuleyule mwanamke mrembo, Sharhazadi, sasa katika umbo lake zuri la kibinadamu lakini alikuwa amelowa jasho mwili mzima.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    §§§§§



    “Seidon,” Amatagaimba alimwamsha Seidon, kisha wakajiandaa kwa safari, mbalamwezi ilikuwa ikitoa mwanga wake murua na kufanya vilele vya milima ile mitano kuonekana kama mtu aliyevaa kanzu nyeupe. Walipohakikisha kila kitu kipo salama wakaanza safari ya kumaliza ngwe hiyo. Wakiwa njiani, nyuma yao walisikia kwato za farasi akimbiaye, kabl;a hajatahamaki mfuko wa seidon ambao ndani yake kulikuwa na lile fuvu, ukanyakuliwa na Orion kisha Yule farasi akafungua mbawa zake na kuanza kuiacha ardhi, Amatagaimba alimshuhudia Seidon naye akinyanyuliwa kwani mfuko huo ulifungwa barabara kiunoni mwake.



    Amatagaimba akauchomoa uta wake na kuuweka mshale wake utani, akavuta huku akibana meno kwa hasira na uchungu, akauachia uta huo nao ukasafiri kwa kasi. Amatagaimba akashuhudia farasi Yule akidondoka tena ardhini pamoja na Orion aliyekuwa juu yake. Vumbi kubwa likatimka, lile fuvu ilikachomoka kutoka kwenye ule mfuko, Amatagaimba na upanga mkononi akafika eneo lile, alipiga upanga lakini Orion akaupangua kwa wake, akauvuta na kupiga pigo linguine, Orion akaupangua kwa ustadi zaidi. Mara pigo la upanga la Orion liliikosa shingo ya Amatagaimba padogo sana, akaepa na kudondoka chale katika mchanga. Oriona akawa anakuja kwa kasi na upanga wake wa makalikuwili uliokuwa uking’aa sana mkononi mwake, akaruka kwa nguvu zake na kuelekea kutua juu ya Amatagaimba. Kwa haraka akauvhomoa upanga wake na kuukinga ncha yake ikatazama juu. Amatagaimba aliliona jitu la kutisha lililoachama domo lake ambalo lilikuwa likitoka joka kubwa, Amatagaimba akajawa na woga lakini hakuondoka, alifumba macho na kutulia. Upanga wa Amatagaimba ukapita katikati ya kifua kikavu kisicho na damu cha Orion, akalitupia pembeni jitu hilo, kisha akasimama na kuuchomoa upanga wa Orion mikononi mwake akakata shingo yake, Orion akaanza kuyeyuka na kupukutika kama kuwa vumbi.



    Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya vumbi. Seidon aliinama na kuokota fuvu hilo kisha akalitia katika mfuko ule na kujifunga tena vizuri kabisa. akamsaidia na Amatagaimba kutembea kwa maana misuli ya mguu wake ilishtuka katika anguko lile. Orion hakuonekana tena, lakini hakuna aliyeamini kuwa kiumbe huyo kaisha waliona ni muujiza au kiini macho tu.

    Wakiwa njiani kwa mwendo wa taratibu, mara kimbunga kikali kiwatokea mbele yao, vumbi na upepo wa kisulisuli ukawatenganisha wawili hawa, Seidon alikuwa mbele na Amatagaimba alikuwa nyuma, katikati yao palikuwa na vumbu jingi na upepo mkali.



    “Tupatie hilo fuvu, haraka!” sauti kali ya kike ilimwambia Seidon.

    “Hilo haliwezekani,” Seidon alikataa huku akiufuta upanga wake na kuukamata kwa nguvu kwa mikono yake miwili. Sauti kali ya muungurumo kama wa radi ikatawala pande zote. Seidon akiwa tayari kajiandaa kwa lolote, mara kwa mbali aliona vumbi jingine likitimka lakini hili lilikuwa dogo tu, kutoka katika vumbi lile alimuona mtu aliyepanda farasi akija kwa kasi sana upande wake. Mara utulivu mkubwa ukatawala eneo lile, akageuka nyuma.

    “Amatagaimbaaaaa!!!!!” aliita bna kuita, lakini hakumuona Amatagaimba wala hakusikia sauti ya kuitika kwake. Walikuwa wametenganishwa katika njia ya kutatanisha. Seidon aliushusha upanga wake na kuupachika alani mwake. Msichana mrembo mwenye nywele ndefu kichwani mwake alisimama mbele ya Seidon akiwa juu ya farasi. Akamtazama Seidon kisha akateremka juu ya farasi huyo, alipotua chini katika ardhi, Seidon alihisi kama ardhi ikitikisika hivi, kisha ikatulia. Yule msichana akatabasamu, alijua kosa alilolifanya ambalo lingemgharimu baadae.



    “Ewe kiumbe wa dunia? Ni wapi uendako hata udiriki kuvuka katika nchi hii isiyo yako?” Yule msichana akmuuliza.

    “Ni nani wewe, hata kuniuliza swali kama hilo?” Seidon akajibu kwa swali.

    “Sikiliza, hapa ulipo si sehemu salama kwako, nakuhurumia kwani hatari inayokukabili ni kubwa, panda kwenye farasi nikuvushe kisha nikuache uende zako,” yule msichana akamwambia Seidon bila kumjibu swali lake. Seidon akatulia kimya, akainama chini kisha akainua uso wake.

    “Hapana, nitakwenda mwenyewe ninakotaka kwenda ama la jitambulishe kwangu kwanza hapo nitatimiza matakwa yako,” Seidon alimwambia Yule msichana.

    “Mimi ni Zamaradi, kutoka mlima wa tatu kati ya mitano uionayo, nchi inayoishiwa na wasichana tu ambao wote ni bikra kwa kuwa hakuna mwanaume kwetu, napenda nikukaribishe kwetu ili uishi nasi japo kwa kipindi kifupi kisha nitakuonesha njia fupi ya kufika utakako,” Yule msichana alijitambulisha kwa Seidon kuwa yeye ni Zamaradi. Yule msichana akamsogelea Seidon jirani kabisa, harufu ya manukato aliyojipulizia yaliziburudisha pua za Seidon hata kuanza kujisahau.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwani wewe unajua ninakokwenda?” Seidon akmuuliza.

    “Sisi, ndiyo tunaotawala mawazo yote ya binadamu, naliiona nafsi yako tangu ikianza safari ya kuja huku, yuko wapi mwenzi wako? Tazama upepo mbaya umemchukua na hutomuona tena, yuko wapi Orion? Adui aliyewazuia njia, usikifikiri ni ninyi mliyempoteza bali ni jeshi kubwa lililokuzunguka nyuma yako, ambalo ndilo limemchukua rafiki yako wa safari, hapa limetulia kwa kuwa linaniogopa mimi, nikikuacha tu nawe utakuwa katika hali mbaya,” Zamaradi alimwambia Seidon, akageuka nyuma hakuona mtu.

    “Mbona sioni chochote?” Seidon akamuuliza Zamaradi.

    “Macho yenye damu hayawezi kuona kilichopo katika giza nene,” Zamaradi akajibu akamshika mkono Seidon na kukitazama kiganja chake, “Ooooh Hamunaptra, una safari ngumu sana kufika hamunaptra, nitakuonesha njia fupi zaidi,” akasema na kumuachia mkono wake.



    Seidon alihisi kama anapigwa kwa shoti ya umeme, aliona vimulimuli vya radi kali vikipita mbele yake pale aliposhikwa mkono na Zamaradi.



    ‘…mshikane mkono na kiumbe chochote…’



    Seidon alirudiwa na maneno hayo, na hapohapo akaona kosa alilolifanya. Zamaradi akamchukua na kumpandisha katika farasi wake kisha kupiga mbio pamoja nae.

    Walipokuwa njiani Zamaradi akaingiwa na kitu kingine, yeye aliagizwa na Sherhazad akafanye hila ya kumpata Seidon baada ya kusaidiwa kutengenishwa watu hao, Zamaradi katika uwepo wake hakuwahi kuona mwanaume wa kibinaadamu, na sehemu anayoishi ni wanawake tupu, ulimwengu wa chini, akatamani kuonja mapenzi ya binadamu, akapiga mbio na kupita karibu na kabisa na miamba mikubwa sana ambayo haikuwa mbali na lango la Hamunaptra, pembezoni tu mwa Ikweta. Akasimamisha farasi wake.



    “Na tupumzike hapa!” akamwambia Seidon huku akitangulia kwa hatua zake za ajabu mpaka ndani ya jiwe kubwa akaketi, “Keti hapa karibu nami,” akamwambia Seidon. Zamaradi alimtazama Seidon kwa jicho la uchu, akaanza kumshikashika shingoni, Seidon akaanza kuhisi raha ya ajabu ambayo hajawahi kuihisi maishani mwake, akatulia akiiruhusu mikono ya Zamaradi ifanye inachotaka.



    Sheria au utaratibu wan chi ya Soria iliyopo katika ulimwengu wa chini, kunakoishi wanawake wengi ni kuwa hutakiwi kufanya mapenzi na mwanadamu ijpokuwa kwao ilikuwa ni kitu cha kifahari sana kama ukifanikiwa hilo. Wengi wao walipokujwa kwenye matembezi yao ya kificho walikuja duniani na kuwakwaza wanaume wengi kwa kuwapa utajiri mwingi lakini kwa sharti moja tu la kufanya nae mapenzi, na walikuwa na mapenzi mazito nay a dhati kuliko wanawake wa dunia hii, walikuwa na utamu usioelezeka katika kufanya mapezni walijua kumridhisha mwanaume kwa kila hali, watakufanya ukojoe kadiri unavyotaka na usijisikie kuchoka, sharti lao kwako ni moja tu, usimwambie mtu kama wao si binadamu na wala usiwe tena na mapenzi na binadamu wa kike, ukitimiza hayo watakupa kila kitu, wivu kwao ulikuwa ni ugonjwa. Lakini hawakutakiwa kufanya mapenzi na mwanadamu katika ardhi yao, hilo ndilo lilikuwa baya zaidi na hata hivyo hakuna mwanadamu aliyekanyaga ardhi yao bila idhini.

    Zamaradi alitamani kuonja kile alichokisikia kwa wengine waliowahi kufanya hivyo, kutokana na umri wake na ubikira wake alisahau kabisa sharti moja la kutofanya mapenzi katika ardhi ile kwani unaitia najisi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akamfanyia maandalizi Seidon, maandalizi ya nguvu, Seidon alishangaa kwa raha inayoufunika mwili wake, sasa nay eye akatamani ale tunda hilo la ajabu, akamkumbatia kwa nguvu Zamaradi, lakini akashangaa vazi lake likitoweka na kubaki kama alivyo, Seidon akiwa katika shughuli nzito alihisi kama anapaa kwa jinsi alivyokolezwa na Zamaradi, naye Zamaradi hakuamini anachokipata kwani aliona raha isiyo kifani. Miguno na milio vya mahaba ikatawala, sauti ya Zamaradi ikazidi ile ya Seidoni, ikaanza kuwa sauti ya kutisha sana, sauti kama ya mnyama mkali mwenye uchu wa nyama, Seidon alipomtazama lo, alikuwa amekumbatia mnyama mbaya wa kutisha, mwenye meno makali na marefu, ulimi kama nyika uliogawanyika vipande viwili, miguu ya ng’ombe yenye manyonya yaliyosimama kama miba ya nungunungu, pembe mb I zenye ncha kali. Seidon aliogopa lakini alijikuta hawezi kubanduka kwa Yule mnyama, aliendelea kufanya mapenzi, raha ya penzi hakupotea, iliongezeka mara dufu.



    Mara tetemeko la ardhi likaanza kuitikisa ardhi ile, likazidi na kuzidi, vipande vya mawe vikaanza kuwaangukia Seidon na mnyama Zamaradi, mara donge la moto likaja kutoka kusikojulikana, likavamia ndani ya pango lile, Zamaradi akatoa yowe kali la kutisha lililozidisha lile tetemeko, Seidon akaanguka kutoka kwa Yule mnyama na kutua chini kwa nguvu, fahamu zikamjia akatafuta huku na kule fuvu hakuliona lilikoelekea, akahisi kuchanganyikiwa, mara kwenye ule moto akatokea farasi mkubwa wa moto na juu yake kulikuwa na malaika wa moto, mwili wake ulitangenezwa kwa ndimi za moto, mikononi mwake alishika upanga wa moto. Sauti ya Zamaradi bado ilikuwa ikisikika kwa nguvu na ilikuwa ya kutisha kuliko mwanzo.



    §§§§§



    “Zamaradi umeniuzi, umekiuka masharti ya kazi niliyokutuma, adhabu yako unaijua, nitaiteketeza roho yako na kuitupa katika dimbwi la tope la ukaidi, huko utaishi milele kwa mateso na dhiki,” ilikuwa sauti ya Sherhazad ikimwambia Zamarad. Zamarad alimtazama Sherhazad kwa woga, akamwangukia na kumuomba msamaha lakini hakukuwa na kitu kama hicho, Zamaradi alikwishajua mwisho wake umefika, kwa kuwa alijua pia ambacho Seidon atafanyiwa na wenzake pindi akichukuliwa na malaika wa moto, akajaribu kuona cha kumsaidi kabla hajatupwa katika dimbwi hilo ambalo hukiingia hutoki tena kwani roho yako inageuka kama uji na kukutana na roho zingine za kale katika shida na dhiki kuu.

    Wakati hayo yakiendelea, Zamarad alimuona kiumbe mwingine akimkabidhi fuvu lile Sherhazad alilolichukua kwa Seidon.



    §§§§§



    Mwaka 2010

    Katika mapiramidi



    Amatagaimba alianguka vibaya katika shimo kubwa lenye giza nene, akabwagika mchangani. Ilikuwa ngumu kwake hata kusimama baada ya shambulizi hilo alilolipata kwa ghafla kutoka kwa kiumbe ambacho hakukiona kwa macho, ila alikuwa akihisi tu mara anabebwa na mara anabwagwa chini, akatumbikizwa kwenye shimo refu na kujikuta huko. Alijaribu kujinyanyua lakini ilishindikana.

    Alibaki pale chini akihema kwa nguvu na mhemo wake ulikuwa ukisafiri ndani ya shimo hilo kubwa, hakuwa na jinsi, macho yake yalipotulia akaona muali mwembamba wa nuru ya mwanga, akatambaa kama mtoto kuuelekea mwanga huo, Amatagaimba hakujua ni wapi alipo, aliendelea kutambaa huku akihema kwa nguvu, kiu nayo ilikuwa ni sehemu nyingine ya mateso yake.

    Amatagaimba akafika katika ule muali wa mwanga, mara tu alipoufikia mkono wake ulikutana na ule mwanga ile pete yake ikang’aa na kufanya nuru katika shimo zima. Amatagiamba akasimama kwa miguu yake, akatzama huku na kule asipajue alipo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Niko wapi?” aliongea kwa sauti ya chini lakini ilionekana kusikika kila mahali, michoro iliyokuwa katika kuta za shimo lile ilianza kufungua vinywa vyao na kucheka kwa sauti kali iliyosababisha kuta zile kutikisika. Amatagaimba katika kona moja ya kuta za shimo lile aliona kama kitu kilichojikunja au mtu, hakujua hasa ni nini anachoiona. Akaufuta upanga wake na kujikongoka taratibu mpaka kwenye ile kona, macho yake hayakumuongopea, alikuwa mtu, mwanamke, akamshtua, na Yule mtu akageuka kumtazama ijapokuwa alikuwa na woga machoni pake. Amatagaimba akarudisha upanga wake na kumpa mkono, akamwinua.

    “Wewe ni nani?” Amatagaimba akauliza.

    “Anna, naitwa Anna, Anna Davis,” akajitambulisha kwa sauti ya kukwamakwama.

    “We umeingiaje huku?” Amatagaimba akauliza tena mara hii kwa mshangao zaidi.

    “Nilikuwa na wenzangu, tulikuja ah, sijui hata kufanya nini, mimi nika, nika, ah, sikumbuki, kwani wewe ni nani?” Anna alijibu lakini alionekana kupoteza kumbukumbu. Amatagaimba alimtazama binti huyu aliyekuwa kachafuka mwili mzima kwa vumbi, nywele zote zilikuwa hazitamaniki jinsi zilivyo timtim. Alimuona wazi kuwa hawezi hata kusimama sawasaw kwa jinsi alivyochoka. Amatagaimba akamsaidia kunyanyuka.



    “Nina kiu,” akamwambia Amatagaimba. Eneo hilo lote hakukuwa na maji Amatagaimba akapapasa kibuyu chake na kugundua kuwa hanacho, akajishika kiunoi lakini hakukata tama, kw akutumia pete yake ya ajabu aliiomba imletee maji, mara wakasikia radi kubwa ikipiga na sauti kama sauti ya maji ilisikika upande wa chini. Amatagaimba akamshika mkono Anna na kuondoka nae eneo lile, walielekea upande wa kaskazini nahuko wakakuta ngazi ndefu zikielekea chini, wakateremka nazo na huko walikuta maji yaliyokuwa yakitembea, maji yam to ambayo hayakuonekana yatokako wala yaendako. Anna aliyavamia na kunywa kwa pupa mpaka akapaliwa, mara akataka aoge kabisa, lakini Amatagaimba akamzuia kuwa hapo si mahala pake. Kila mtu aliporidhika wakapita kandokando yam to ule na kutokea upande mwingine ambako kulikuwa na ngazi nyingi zikipanda kuelekea juu, wakazikwea taratibu, Anna akiwa mbele na Amatagaimba akiwa nyuma. Baada ya kupanda ngazi kadhaa hawakusikia tena ule mto wa maji kama mwanzo. Ila walianza kusikia kelele za popo wengi waliokuwa ndani humo. Amatagaimba akamwambia Anna asimame, naye akasimama kisha yeye akaenda mbele na kutazama popo wale kwa makini sana, hawakuwa wakitikisika lakini walikuwa wakipiga kelele kama wanaoongea jambo Fulani. Amatagaimba akamgeukia Anna akamtazama kifuani, alikuwa amevaa kidani cha jiwe Tanzanite na hereni zake.



    “Vua kidani, na hizo hereni pia,” Amatagaimba akamwambia Anna, naye akafanya hivyo bila kujua kwa nini anaambiwa hivyo.

    Kisha wakaendelea kwenda mbele wakivuka lile eneo lenye popo wengi. Anna alijitahidi kumfuata Amatagaimba kila anakonkwenda, wakapita ndani ya mapango mengi mengine ya kutisha sana, walikutana na viumbe vya ajabu ajabu kila wapitapo, kwingine waligeuza njia, kwingine walijitahidi kupita hivyo. Ilikuwa ni kazi ngumu kuona njia ya kutokea nje.

    “Tutatokaje humu Amatagaimba?” Anna akauliza huku akihema sana.

    “Humu ndani hatutoki kwa kutumia njia za kawaida kama huko duniani…” Amatagaimba alianza kueleza.

    “Sijakuelewa unasemaje?” Anna akauliza kwa mshangao.

    “Nimesema, humu ndani hatutoki kama huko duniani, unajua sasa hivi upo miaka mingi nyuma! Mimi nilikotoka ni miaka 1200 iliyopita, na nilipotea kimiujiza kama wewe, hivi wewe sasa kama ulitoka duniani mwa elfu mbili na kitu basi sasa upo mwaka elfu moja na kitu, hivyo kutoka humu ni kupata miaka iliyobaki,” Amatagaimba alieleza lakini Anna hakuelewa kabisa somo hilo, “Ili kutoka humu inabidi ukumbuke mwaka uliotoka duniani halafu tupate dira ya kutuonesha uelekeo, na dira hiyo ipo kwenye mnyama hatari, mnyama ambaye ndiye anayeshika pande nne za dunia,” Amatagaimba alimuelea Anna vitu vya ajabu ambavyo kwake vilionekana kama havina maana.



    “Kwani wewe umetoka wapi?” Anna akauliza.

    “Mimi nimetoka duniani miaka mingi sana, nikaingia ulimwengu huu wa chini ya dunia tangu nikiwa katika msitu wa Solondo nilipotoka sikuweza kurudi kwani njia yangu ya kurudi imekuwa ngumu mno,” Amatagaimba akaeleza.

    “Msitu wa Solondo!!!” Anna akashangaa kwa kusikia jina hilo.

    “Ndiyo vipi unaufahamu?” Amatagaimba akauliza huku akimtazama binti huyu usoni.

    “Siufahamu, na wala sijawahi kuuona kwa macho, ila nimeusoma kwenye kitabu cha riwaya kikibebwa kwa jina hilo, simulizi ya zamani sana hata mimi sikuwa nimezaliwa,” Anna akaeleza. Amatagaimba alimtazama mwanamke huyu mrefu, mwenye umbo shupavu.



    “Ni nini kitabu hicho kimeeleza?” Amatagaimba akauliza huku akiwa amemshika mabegani Anna, wakitazamana uso kwa uso.

    “Sasa ndiyo naelewa,” Anna akajibu na kuitoa mikono ya Amata kwa ghafla mabegani mwake, ‘Mzimu?!’ akajiuliza, Anna akaanza kutimua mbio.

    “Anna!” Amatagaimba akaita, mara kuta zikaanza kutikisika, Amatagaimba akaanza kutimua mbio kumfuata Anna, akamfikia, kila alipojaribu kumshika mkono, Anna alijitoa katika mikono ya Amatagaimba na kutimua tena mbio, Amatagaimba hakumuacha, naye alimkimbiza, wakiwa katika kukimbizana kwenye ngazi hizo, mara lile jengo likaanza kutetemeka kana kwamba kuna kitu kizito kikipita juu yake. Amatagaimba akasimama na kutazama huku na kule wakati Anna aliingia kwenye mlango mmoja ulioonekana wazi. Alipoingia tu mlango ukajifunga, Anna akabaki ndani, hana ujanja, aliuendea mlango na kuanza kuupigapiga huku akilia na kuita.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Amatagaimbaaaaaaaa!!!!! Nisaidie,” aliita kwa nguvu zote.



    Haikuwa rahisi kwa Amatagaimba kuingia, mlango mkubwa wa jiwe ulikuwa umejikita, Amatagaimba, akajisjika kiuno hakujua la kufanya, akatazama huku na kule bado hakuweza kujua la kufanya. Mtikisiko ulikuwa ukiendelea, Amatagaimba ikambidi atoke eneo lile na kwenda upande mwingine, mbele kidogo tu dude la ajabu likatua mbele yake, shetani si shetani, jinni si jinni, lilikuwa ni kiumbe kikubwa kilichosimama kwa miguu miwili yenye kwato, mikono miwili yenye vidole vitatu kila mmoja, alikuwa mkubwa mara tano ya binadamu, na alionekana kuwa na uzito mkubwa, midomo yake ilikuwa kama ya bata na macho yenye kung’aa sana, katika tumbo lake kulikuwa na kitu kama goroli kubwa lililokuwa likitoa mionzi mbalimbali. Amatagaimba akarudi nyuma taratibu, akiweka nafasi kati yake na mnyama yule, huku akiangalia kile kitu mfano wa goroli.



    Mara moja aligundua kuwa kitu kile ndicho hasa anachokitafuta ili kuweza kutoka nje ya shimo lile kubwa, kwani kinaweza kukuelekeza njia ya kutokea kutokana na nguvu yake iliyoshika pande nne za dunia. Lile limnyama likawa linamfuata polepole, lakini alichoshangaa halikuwa na nia ya kumdhuru. Amatagaimba akajikuta akiugonga ukuta nyuma yake, ikambidi kusimama, lile limnyama likamfuata mpaka pale, na kumuinamia, nyuso zao zikakutana, lile limyama likamtazama Amatagaimba, halikumfanya chochote. Mara kelele za Anna zikawa zina sikika kwa mbali, lile limnyama likageuka kuangalia kule zinakotokea kelele, kisha likamwangalia Amatagaimba, akatoa ukelele mkali ambao uloifanya vumbi litimke mle ndani, Amatagaimba akaanguka chini kwa woga. Lile limnyama likaanza kuvuta hatua kuelekea kule aliko Anna, Amatagaimba hakujua nini cha kufanya akatulia kusubiri aone. Kwenye ule ukuta kulikuwa na masanamu ya ya vichwa vya samba kuzunguka kote, lile limnyama likashika kichwa kimojawapo na kukikandamiza chini, mala lile lango la jiwe pale kwenye tundu alipoingia Anna likafunguka, Anna akatoka kwa kasi na kumkumbatia Amatagaimba aliyekuwa tayari amesimama wima akiangalia tukio lile.



    “Anna,” Amatagaimba alipiga kelele huku akiwa amemdaka. Kisha wote wakageuka na kumtazama yule mnyama. Yule mnyama akaanza kuwasogelea tena tarataibu mpaka pale waliposimama, likawainamia na kunyanyua mkono wake mpka kwenye shingo ya Anna na kuushika mkufu wake wenye kito safi cha Tanzanite ya buluu, akaukata na kukitazama kwa makini kile kito, akatikisa kichwa, akatenganisha kito na mkufu, akachukua kito tu, kisha akamtazama Anna ambaye alikuwa ametulia tuli, kabla hajafanya lolote, Amatagaimba akamvua Anna heleni zake nazo zilikuwa na kito hichohicho akampa yule mnyama, yule mnyama akanguruma na kutikisa kichwa chake kisha akageuka kuondoka kwa hatua zake nzitonzito za kutisha. Amatagaimba na Anna walikuwa wamesimama, baada ya hatua kama tano hivi alikuwa amefikia ukuta ule mkubwa, akasimama na kugeuka nyuma akawaona Anna na Amatagaimba wakiwa palepale, akaunguruma na kuwapa ishara wamfuate, wakafanya hivyo.



    Wakasimama palepale aliposimama, radi moja kubwa ikapiga kwa nguvu ndani mwote mkajaa mwanga, akamuonesha Amatagaimba jiwe kubwa lililojitokeza kama pande la tofari, Anna akapanda kisha yule mnyama akatikisa sanamu linguine na mawe ya mtindo ule yakatokeza mengi na kuyfanya ngazi kwenda upande wa juu, Anna na Amata wakazukwea kuelekekea juu ya shimo lile, akawapa ishara ya kuwa waondoke wakati yeye amekandamiza lile sanamu kwa mkono wake. Amatagaimba na Anna wakakwea kwa kukimbia kuelekea juu, zilikuwa ngazi nyingi ambazo unatakiwa uzipande kwa uangalifu sana. Muda si mrefu walijikuta wanatoikea mahala pendine kabisa. Anna alipotoka kwenye zile ngazi akaangukia kwenye mchanga mwororo ambao ulikuwa kama mchanga wa jangwani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tumepona Amatagaimba,” Anna akamwambia Amatagaimba ambaye alikuwa akijvuta pale mchanagani nae akiwa hoi.

    “Uhhhh!!!! Bado, kazi sijamaliza,” Amatagaimba akamwambia Anna, “Rafiki yangu sijui yuko wapi,” akajisemea.

    “Rafiki?! Rafiki gani?” Anna akauliza.

    “Ha, we unafikiri huku nimekuja peke yangu? Niko na mwenzangu, na tuko na kazi maalumu nab ado hatujaimaliza, sasa yapata nimtafute popote alipo ili tukamilishe misheni hiyo,” Amatagaimba alisema.

    “Nyanyuka twende zetu hatutakiwi kulala hapa, tuko hatarini sana,” Amatagaimba akamwambia Anna na kisha wote wakaanza safari ya kutembea kwenye mchanga kuelekea wasikokujua.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog