Search This Blog

HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA - 2

 







    Simulizi : Hamunaptra - Mji Uliopotea

    Sehemu Ya Pili (2)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ndipo walipojikuta usiku mmoja wamevamiwa na wapiganaji walio juu ya farasi, wenye mijeledi na majambia, kijiji kizima walipigwa na wengine kuchomwa moto, ilikuwa hali ya kutisha sana. Waajemi walifanikiwa kulichukuwa fuvu lile na kutokomea nalo.



    Warelvesh waliapa kulirejesha fuvu hilo mikononi mwao wakati Wahamsud walilimezea mate, achana na Sherhazad ambaye yeye kama mwanamke asingeweza kulishika fuvu hilo. Tukio likawa historia, watu wakafa na wengine wakazaliwa, historia ikawa ni simulizi ya kuvutia, simulizi ikawa riwaya tamu unayoisoma sasa.



    Rejea … Sasa



    Upepo si upepo wala si mvumo wake, mara kwa mara Anna Davis alikuwa akisikia kitu hiko kikimsumbua, aligeukageuka mara kushoto na mara kulia, mara alizunguka kama pia, ilikuwa ngumu kwake kufuatia maelekezo yatolewayo na mtaalamu huyo.

    “We una nini? Mbona hutulii?” mwenzake alimuuliza

    “Hata sijui mwenzangu, naona kama vitu vinanipita hapa mara vinanizungukazunguka. Yaani mwili wote unanisisimka”

    “Acha uoga wewe, mbona wenzako hatuvioni!” alijibiwa na mwanafunzi mwenzake, kisha wote wakaendelea kusikiliza maelekezo.



    Kitu kama nyoka kilipita katikati ya wanafunzi wale na Anna lakini cha kushangaza wenzake hawakukiona ila yeye alishuhudia mchanga ukitimka mbele yake na mara nyuma yake, sauti kama mruzi mkali ulipenya masikio yake na kumfanya apige kelele. Muelezaji alinyamaza kwanza na kumwangalia Anna, ilionekana wazi hakufurahishwa na kitendo cha Anna.

    “Msichana! Hutakiwi kupiga kelele ukiwa humu ndani, utaamsha waliolala” yule mzee alimkazia macho Anna na kumueleza hayo.

    Macho ya Anna hayakuwa matulivu hata kidogo, kila alipoangalia michoro ya watu iliyochorwa katika kuta zile au wanyama yeye aliona kama zikimwambia kitu Fulani, aliona kama ni viumbe hai. Hali hii ilimfanya aogope sana, muda wote hakuwa na amani kabisa. Alitembea kwa hadhari kubwa huku akigeukageuka nyuma, maana alihisi kama kuna vitu vinamfuata na alipogeuka vilitulia. Katika moja ya kugeukageuka ndipo alipojigonga kwenye kigingi kikubwa cha jiwe, alianguka chali na kukosa pa kujishikia, bahati mbaya au nzuri mikono yake iligonga tofali mojawapo lililoshikia ukuta ule imara, mara juu yake aliona kukifunguka na kitu kama sanduku likianguka kuelekea alipo yeye, Anna alipiga kelele huku akiwa kafumba macho, hana la kujitetea.



    Wanafunzi wenzake walishtushwa kwa kelele za mwenzao walipogeuka nyuma walishuhudia vumbi zito likitimka na kuweka kama ukuta kati yao na Anna, kwa mbali walianza kusikia kama watu wanaoswali, sauti nyinginyingi zilisikika humo ndani ya piramidi

    “Tuondokeni haraka! Tutoke nje, nifuataeni mimi” yule mzee aliongea kwa kelele, wanafunzi wale walianza kukimbia kumfuata. Kipenzi cha Anna, alishindwa kumuacha shoga yake, alisimama na kugeuka nyuma huku akiwa amejishika mkono kujiziba mdomo.

    “Annaaaaaa!!!!!” aliita kwa nguvu na kelele ile ililijaza piramidi lote, kabla hajatahamaki jiwe kubwa lilianguka na kumponda kichwani, alianguka na kuumia vibaya, hakuweza kujinasua kwani tofali lile ni kama kilo mia mbili, alipoteza maisha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Msisimame, twendeni!” yule mzee alizidi kuwahasa viajana wale ambao sasa walikuwa wakikimbia na kupoteana wengine wakitamani kubaki kuwasaidia wenzao. Piramidi lote lilianza kutikisika na kuta zake kuanza kuchezacheza kwa mtindo ule ule, vumbi likazidi kujaa ndani mle kiasi kwamba ilikuwa ngumu kuona njia hasa zile za kupanda juu. Wanafunzi wale walipata shida kujiokoa lakini kwa maelekezo ya yule mzee walifanikiwa kutoka nje na kuliona jua waliloliaca likichomoza sasa lipo katyikati ya utosi.

    “Nyie, yule mwenzenu ana matatizo gani?” yule mzee aliongea kwa ukali

    “Matatizo kivipi?” kiongozi wa msafara alijibu kwa kuuliza.

    “Hii hali yote kaisababisha yeye, unapoingia mle ndani hutakiwi kugusagusa vitu”

    Vilio vilitawala kati ya wanafunzi waliobaki wakiwaomboleza wenzao waliosadikiwa kufa shimoni, hali ilikuwa tete.



    ***

    Amata ga Imba, akiwa amelewa sana na pombe yake nyingine mkononi alisimama ghafla, akashuka kutoka katika farasi wake na kutua chini taratibu, aliliweka guo lake vizuri mwilini na kurudishia pama lake kichwani. Alifikicha macho yake kutazama kilichopo mbele yake; ‘huyu mtu au kitu gani?’, alijiuliza huku akijongea kwa hatua za taratibu mpaka pale, alichuchumaa na kuinua kichwa cha majeruhi yule taratibu, akaweka mkono wake kifuani kwa mtu yule, akagundua kuwa bado uhai upo kwa mbali sana, mtu yule hakuwa na fahamu. Akamnyanyua na kumlaza juu ya farasi wake, kwa pembeni alimuona farasi mweupe aliyelala nyasini, akampigia mruzi na farasi yule akainuka kutoka pale, kisha akaondoka na mtu yule pamoja na farasi wake mpaka katika kijiji alichokuwa akiishi.

    Siku zote alikuwa akimpa tiba mtu huyu asiyemjua kwa muda wa takribani wiki moja mtu yule aliamka kutoka katika usingizi mzito, alikuwa akihema kwa nguvu na haraka haraka

    “Likowapi, likowapi? Nipe, nipe haraka” Seidon aliamka na kupiga kelele za maweweseko. Amata alimtuliza na kumlaza taratibu pale katika tandiko lake.



    “Tulia, tulia, usijitikise sana” Amata alimbembeleza Seidon ambaye alitii na kujilaza tandikoni.

    “Hapa nipo wapi?” aliuliza

    “Hapa ni kijiji cha Mshariki, kijiji cha wema kisicho na wabaya” Amata alimjibu Seidon kwa upole, akamtazama usoni na kuendelea “naitwa Amata ga Imba, nilikukuta porini karibu na jangwa la Sheba nikakubeba na kukuleta huku” akajikohoza kidogo kuweka koo lake vyema “pole sana! Hakika ungekufa lakini Mungu mkubwa nilikuwhi. Wewe ni nani?”

    “Mimi ni Seidon kutoka Relvesh, nilikuwa safarini nikitokea Hamunaptra kupitia Mesopotamia, Wakalban walikuwa wakinikimbiza wakiwa kundi, walitaka nilichonacho, lakini nikiwa katika kasi kubwa niliona kitu kama kamba mbele yangu ambayo ilimnasa farasi wangu miguuni na mi kuanguka vibaya. Wahamsud walinifanyia hivyo na kuchuku fuvu la Cleopas wakatokomea nalo” Seidon alitokwa machozi na kamasi jembamba akendelea “Babu wa babu zangu Vernad alikuwa na mpango wa kulipata fuvu hilo kwa ajili ya kusaidia kijiji chetu cha Relvesh dhidi ya laana tulizonazo...



    Rejea Vernad…



    Vernad alitembea taratibu mpaka kwenye kilima kidogo, na alipofika juu yake alitazama chini na kuona mji mkongwe, gofu la mkji uliofunikwa kwa mchanga upande wa juu. Bia kuchelewa alitimua mbio kulielekea gofu lile, punde tu alikuwa mbele ya mlango mkubwa, bila kusita aliingia ndani, hakupiga hata hatua tano alijihisi kakabwa kwa nyuma, alihangaika kujinasua lakini ilikuwa vigumu, aliishika mikono ya kiumbe huyo sawia na kuinama hata kumdondosha kiumbe yule kwa mbele, kitendo bila kuchelewa aliuchomoa upanga wake na na kumshindilia kifuani, kiumbe yule alitoa sauti ya maumivu kama sauti ya nguruwe lakini hakutoka damu, Vernad aliuchomoa upanga wake na kumkata vipande vipande kisha akaingia mlango wa pili na kuchukua ngazi kuelekea chini ya gofu hilo, alijikuta kwenye ujia mrefu uendao asikokujua, kwa kasi ya ajabu alikimbia kuelekea ujia ule uendako akiwa na upanga wake mkononi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Njiani alikutana mtu mmoja mbele yake ambaye alikuwa kafunga njia, Vernad bila kupunguza mwendo alijirusha na miguu yake kutangulia kifuani kwa mtu yule huku upanga ukifuata na kudidimia katika koromeo la mtu yule ambaye hakupata hata nukta ya kujitetea. Vernad alitua chini na kuuchomoa upanga wake, kabla hajaanza kuondo alipigwa ngwala moja na kujibwaga chini, wakati anapoanguka alijishika kwenye tofali moja wapo lililotokeza katika ukuta huo mara ardhi ikainamana na kufunguka Vernad alitumbukia katika shimo refu, alishuhudia radi kali zilizopiga huku na huku shimoni mle. Huku akiwa kajiziba masikio kutokana na upepo mkali uliyoyasumbua, upanga wake ukiwa haupo mikononi mwake, alijikuta akitua chini taratibu bila maumivu yoyote, alisimama wima na kushangaa eneo lile pana, uwanda mkubwa usio mawaa yoyote. Alijiuliza yuko wapi hakupata jibu, mbele yake aliona majengo mengi sana na watu wakiwa katika kazi nyingi, kazi mbalimbali. Aliinua mguu kuwafuata watu wale lakini nyuma yake alihisi kama anafuatwa alisimama na kugeuka, lo! Umati wa watu ulikuwa nyuma yake, alijaribu kuwahesabu harakaharaka lakini alishindwa kwa uwingi wao.



    Watu wengi walionyamaza kimya hakuna aliyetikisika walimtolea macho Vernad mpaka akaogopa, aliporudi nyuma walimfuata alipojaribu kuwasemesha sauti haikutoka, walibaki kumtolea macho tu, watu waliovaa nguo kuukuu zinazoonekana kuoza, macho mekundu kwa meusi, wengine walikuwa na mkono mmoja wengine walikuwa hawana masikio ilimradi waliogopesha, wafu, lakini mikononi mwao walikuwa na visu, mapanga, miundu na kadhalika. Vernad alijuwa wazi kuwa hapo hakuna msalie mtume, alianza kutimua mbio na watu wale wakaanza kumfuata, Vernad aliwaacha mbali kwa mbio zake lakini hakujua ni wapi anakoelekea, alipokuwa akiyapita yale majengo watu wengine walitoka katika yale majengo na kuanza kumfukuza, Vernad hakuchoka, aliongeza mwendo lakini ghafla alihisi kamba ikimfunga shingoni na kuanguka chini, haraka bila kuchelewa alijiinua na alipojaribu kuitoa kamba ile shingoni hakuweza kwani ilimfunga barabara, alihisi miale ya jua ikimchoma machoni kwa kubadilishana alijikinga kwa mkono wake wa kulia na kujaribu kuangalia, aliona kama kiumbe Fulani pale katikati ya mionzi ile. Mara miale ile ilianza kupungua nguvu,



    Vernad alishusha mkono wake na kumuona mtu aliyevalia joo jeupe, kiunoni akiwa na upanga mkubwa, mkono wake wa kushoto kashika ngao na kulia ana kamba ambayo ndiyo hiyo upande wa pili imemfunga Vernad, mgongoni alikuwa na uta mkubwa na podo lililojaa mishale.

    ‘Orion’ Vernad alijiwazia, akasimama kwa miguu yake na kuinamisha kichwa kutoa heshima kwa kiumbe huyo, aliponamisha kichwa Orion aliufuta upanga wake na kukata shingo ya Vernad. Vernad hakuwa na kichwa tena, alibaki kiwiliwili tu, alianguka chini na roho yake ikauacha mwili.



    seidon



    …Hakufanikiwa kwa sababu Orion alimdhibiti na kumuua. Sasa mimi nilitumwa kuikamilisha kazi hiyo iliyoahirishwa vizazi na vizazi” Seidon alimaliza kumuelezea kisa hicho Amata ambaye alibaki mdomo wazi maana alijaribu kufikiri hatari aliyoikabili Vernad na sasa Seidon.



    “Wewe umemshinda vipi Orion?” Amata alimuuliza Seidon

    “Amata! Ni simulizi ndefu sana…” akashusha pumzi ndefu na kuendelea “Mimi nimepambana na Orion uso kwa uso, sikumshinda kwani yule ni kiumbe mwenye akili hata upiganaji wake hauna makosa shida yake niliisoma ni moja tu, si mjanja na wala si mwepesi, nilifanikiwa kulipata fuvu alipolificha na hapo ndipo kazi ngumu ilikuwa, Amata!...



    …Sherhazad alimwangalia Seidon akipotea na farasi wake kwa kasi, akiwa pale katika dirisha lake la ajabu alitabasamu na kutikisa kichwa ‘wanaume wajinga sana! Ukilala nao kitandani tu watakupa kila kitu, ngoja alete hilo fuvu hakika kaburi lake litakuwa hapa hapa Soria’ alijisemea moyoni huku akitoka katika dirisha lake ambalo kwalo huweza kuona mambo yote yanayoendelea duniani na kusoma mawazo ya kila mtu anayemtaka.



    Seidoni alipiga mbio bila kuchoka na farasi wake alitii yote aliyoambiwa na bwana wake, punde si punde alijikuta mbele ya jingo la ajabu, jingo kubwa lililoonesha kila dalili ya kutoishi mtu, alijitoma ndani akiwa na farasi wake huyo, ndani humo alipita kwenye njia ndefu iliyokuwa haionekeni mwisho wake, kwa kasi ileile alipita na farsi wake, akiwa katika kukimbia huko akasikia farasi mwingine nyuma yake akipiga kelele alipogeuka aliona akifuatwa kwa kasi na mtu aliyekuwa juu ya farasi aliyeoneaka si muda angemfikia. Seidon aliongeza kasi lakini bado alijikuta umbali uleule na farasi yule wa nyuma. Hakuwa na jinsi kwa maana aligundua kuwa huyu wa nyuma yake angeweza kumdhuru muda wowote ukizingatia alikuwa karibu sana na yeye, alimkwepesha farasi wake upande na kusimama, yule wa nyuma alipitiliza na tayari upanga wa Seidon ulishapita katika ubavu wa mtu huyo, kwa kishindo alianguka chini, Seidon aliteremka na kumfuata pale alipo, damu ilikuwa ikitoka mdomoni, Seidon akapiga goti moja na kumtazama



    “Wewe ni nani?” alimuuliza

    “Mimi kiumbe wa Mashariki ya mbali” alijibu kwa taabu

    “Kwa nini unanifuata?”

    “Pepo zimenituma nikufuate nihakikishe hufiki uendako, na ukifika usifanikiwe lengo lako, na ukifanikiwe usitoke humu na ukitoka usifike mwisho wa safari yako…” kabla hajamaliza kuongea alikoroma na kukata roho. Seidon alipanda farasi wake na kuanza safari yake kwa mbio zilezile, lakini kamba iliyorushwa kwa ustadi iliifunga shingo ya Seidon na kuanguka vibaya, vumbi lilitimka mahali pale na lilipotulia hakukuwa na mtu zaidi ya farasi mweupe wa Seidon.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Orion alisimama kuangakli huku na huku hakumuona Seidon, kazidiwa ujanja. Aliiangalia kamba yake ambayo sasa ilionekana imemfunga farasi wa Seidon na sio Seidon mwenyewe. Orion alitereka kutoka katika farasi yule na kutua chini, kishindo cvhake cha kutua chini kiliwafanya popo kutimka na ardhi kutikisika kwa muda, kwa hatua fupi fupi alimuwendea farasi wa Seidon na kumuangalia kwa makini. Orion ambaye daima sura yake haionekani kwa kuwa alikuwa akiifuanika kwa kinyago maalum huwa hashuki kwenye farasi, yeye hupigana akiwa juu ya farasi wake, lakini akikuona wewe ni mjanja zaidi yake hapo ndipo atashuka ili akukabili vizuri. Alimtazama yule farasi lakini hakuelewa kilichotokea, aliichukua kamba yake na kupanda farasi wake kisha kuondoka kuelekea uelekeo ule ule aliokuwa akielekea Seidon.



    Seidon aliliachia jiwe alilokuwa amelidandia juu ya pango lile na kutua chini bila kufanya kishindo, ‘amenikosa’, alijiwazia kisha akapanda farasi wake na kuelekea kulekule alikoelekea Orion, baada ya mwendo wa kama dakika kumi katika pango lile alijikuta anafika njia panda, nji tatu zilikutana hapo, Seidon alifikiri ni ipi hasa anayopaswa kupita, kwenye njia moja alisikia mvumo wa maji kama mto upitao kasi lakini hakuyaona maji yenyewe, njia ya pili ambayo ilikuwa katikati alisikia mvumo wa moto uwakao mithili ya moto uchomao msitu na njia ya tatu alisikia kama watu wakinoa mapanga. Seidon alitulia kimya akitafakari la kufanya, aligeuka na farasi wake tayari kwa kurudi akijua kuwa labda kuna njia nyingine lakini sivyo, alipogeuka alikutana na ukuta, hakuiona njia aliyojia, alitafakari na kuona kuwa hana ujanja zaidi ya kuchagua moja, alimgeuza tena farasi katika uelekeo wa kuendelea na safari na moja kwa moja moyo wake ulimtuma kupita njia ya moto, hakuwa na muda wa kufikiri alijitoma ndani ya ujia huo na kuendelea kupiga mbio, kadiri alivyouwa akienda alihisi sauti ile ya moto ikizidi kuwa karibu zaidi,kila alipotaka kupunguza mwendo alisikia sauti ikimwambia aendelee kwa kasi.



    Seidon aligundua kuwa amepata kampan alipoona kuna farasi wawili na juu yake Malaika wa moto wenye upanga makali kuwili wakiwa katika kasi ileile, mmoja kushoto na mwingine kulia, Seidon alishindwa kujua afanyeje, akiongeza kasi nao walifanya vivyohivyo, mbele yake alishuhudia moto mkubwa sana ambao ulimtisha nafsi yake, afanye nini. Aliamua, kama kufa wacha afe kwani tayari alikuwa kwenye mikono ya mauti, kwa mkono wake wa kulia aliufuta upanga wake na kwa pigo moja alimchoma yule Malaika wa moto wa upande wa kushoto lakini hakuhisi kama kachoma kitu alipogeuka kwa yule wa upande wa kulia alikutana uso kwa uso na joka kubwa lililoachama kinywa chake, Seidon bila kuogopa wala kufikiri alipiga pigo moja kwa upanga wake na kulichoma joka lile, alipouvuta upanga kuuchomoa alihisi kama damu ikimrukia usoni alichelewa kujikinga, alijikuta akipoteza uelekeo na kuanguka vibaya, alijiinua haraka na kusimama kidete, joka lile lilitema ndimi za moto, Seidon alijitupa chini na kujiviringa kuelekea kuelekea kule joka lile lilipo, alifanya pigo la upanga na kulikata joka lile kipande, kisha aliposimama alijikuta akipaishwa juu kwa ngwala maridadi iliyopigwa kwa mkia wa joka lile, alijigonga vibaya na lianguka kama mzigo, alijtahidi kunyayuka lakini alipoangalia alijikuta chini ya upanga wa moto, Malaika wa moto alisimama juu yake akiwa kamnyoshea upanga.



    Seidon alitulia tuli, akijua sasa siku yake imefika, Malaika yule aliushusha upanga wake kwa kasi kwa nia ya kumkata Seidon, lakini kwa ustadi Seidon alipangua pigo lile kwa upanga wake na kumfanya Malaika yule apoteze shabaha ile, Seidon alinyanyuka kwa mtindo wa sarakasi na kusimama wima ardhini, alirusha teke kwa kujizungusha na kumtandika Malaika yule kichwani na kumfanya kuyumba kiasi lakini akajiweka sawa na kujibu shambulizi, aliuvuta upanga wake na kufanya pigo lingine ambalo almanusura liondoe kichwa cha Seidon endapo Seidon asingeinama. Seidon sasa alikuwa akitazamana na sehemu ya tumbo ya Malaika yule, bila kuchelewa aliuzungusha upanga wake na kukata tumbo hilo lakini alichokishuhudia ni kurushwa kwa nguvu na kutumbukia katika moto mkubwa uliokuwa ukizidi kusogea eneo hilo.



    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Anna Davis alitazama huku na huku, aliona sanduku kubwa kushoto kwake lililomkosakosa kumbonda na kumfanya aanguke tu kwa kishindo kile. Akiwa anatweta kwa nguvu alishindwa kujua ni nini hasa anatakiwa kufanya, alipotaka kupiga kelele za msaada alijikuta hana sauti ya kufanya hivyo, alipojiinua pale chini aligundua kuwa hakuwa peke yake bali pembeani yake kulikuwa na miili iliyokauka yaani iliyokufa miaka mingi nyuma, Anna aliogopa sana akaanza kutetemeka, taratibu aliinuka ili asisikiwe na miili hiyo. Alipoketi vizuri alitazama wapi pa kuelekea aliona ngazi ndefu zikishuka chini na pale alipo palikuwa na uwanda mkubwa kiasi uliozungukwa na kuta nene zenye michoro mbalimbali.



    Sauti za watu wakisali katika lugha isiyoeleweka zilisikika, Anna alitazama vyema na kuona viumbe kama watu wapatao kama ishirini hivi wakiwa wamezunguka kitu kama kitanda na katikati yake kulikuwa kumelazwa mwili wa binadamu ambao Anna aliutambua vyema, mwili wa rafiki yake kipezi Nesta. Anna alibaki kakodoa macho akiangalia tukio lile lilivyoendelea kule chini, wale viumbe walipiga magoti wakisali na mmoja aliyeonekana kama kiongozi wao alisimama upande wa miguu wa ule mwili akiwa na kisu kikubwa mkononi mwake, alikuwa akimwagia unga Fulani juu ya mwili ule kuanzia miguuni kuelekea kichwani huku akisema maneno kwa kurudiarudia na alipofika kichwani alijaza unga ule usoni mwa mwili ule na kukiinua kisu chake tayari kwa kukata shingo.



    Anna alipiga kelele za nguvu mara kuta zote zilianza kutikisika, na wale viumbe walionekana kukatisha ibada yao, walisimama na kutawanyika wakipandisha ngazi kuelekea juu alipokuwapo Anna, Anna alipogeuka akimbie alitandikwa kofi moja la nguvu lililompepesua na kumuangusha chini kwa haraka alinyanyuka na kusimama wima, mbele yake kulikuwa na ukuta na katika ukuta huo kulichorwa picha ya skeleton ya binadamu, hakujua ni nani aliyemchapa kofi lile, aliendelea kushangaa na hapo ndipo alipoushuhudia mchoro ule ukipata uhai, ukajitikisa na kujibandua pale kwenye ukuta na kukanyaga chini, kwa mwendo wa kustaajabisha ulianza kutembea kumuelekea Anna pale alipo.



    Hamna la kufanya Anna kwa kujihami aliuchomoa mwenge uliokuwa umepachikwa katika moja ya kuta zilizopo hapo na kumtishia kiumbe huyo aliyeonekana kusimama kwa kuogopa. Anna alisikia vishindo vya wale viumbe wengine wakipanda ngazi zile kwa kasi akaona sasa hapo si pa kukaa tena lakini hakujua ni wapi hasa aelekee. Alitazama huku na huku akaona viumbe wale wanazidi kukaribia pale alipo, alijaribu kukimbia, lakini alipogeuka tu alipigwa kofi lingine la kisogoni lililomfanya ayumbe na kujigonga katika ukuta, aligeuka na kukabiliana na skeletoni ile ambayo ilikuwa ikitembea kuelekea alipo msichana huyu, Anna hakuwa na silaha zaidi ya mwenge ule uwakao aliurusha kumtupia kiumbe yule ambaye kabla hata hajafikiwa na moto ule alijizungusha na kugeuka mchanga uliotimka na kufanya vumbi jingi ndani mle. Anna aligeuka kukimbia lakini mbele yake wale viumbe waliotoka kule ibadani walikwishamfikia, walimzunguka.



    Kutokana na urefu wa Anna aliweza kuwaona vizuri jinsi walivyo wafupi wenye macho ya kutisha na midomo iliyokuwa ikimwagika udenda mweusi mzito kila mara, Anna alichota mchanga na kuwamwagia kitendo kilichowafanya watawanyike, Anna aliokota tena ule mwenge uwakao na kuanza kukabiliana nao, aliushika kwa mikono miwili na kuuzungusha kwa kasi kitendo kilichofanya kuwapiga viumbe kama watatu kwa mfululizo na kuviangusha chini lakini bado vilikuwa vikija tena, alifanya tena kama mwanzo na kushuhudia kimojawapo kikilipuka kwa moto ule na kingine kikadaka mlipuko ule, Anna hakuona haja ya kuchelewa alipita katikati yao na kutimua mbio, bila kugeuka nyuma akiwa katika kasi hiyo mara mbele yake aliona ardhi ikifunguka na kwa kuwa alikuwa akikimbia alishindwa kusimama ghafla, alijaribu lakini alishindwa alijikuta akimezwa na shimo lile, akitumbukia ndani ya shimo hilo ambalo kwalo hakuona mwisho wake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alijibwaga kwenye lindi la mchanga, mahali asipopajua, aliketi akiegemea ukuta mkubwa nyuma yake, miguu yake aliikutanisha na tumbo lake na kujikunyata akitweta bila kujua la kufanya.



    ***



    Seidon alidondoka katika mandhari tulivu, udongo laini ulifanya vumbi sawa na la saruji lililomfanya seidon kupiga chafya kadhaa, alitazama huku na kule na taratibu kuvuta hatua, mbele yake kulikuwa na mlango mkubwa na ndani yake aliona mwanga mkubwa uliojaza chumba hicho, Seidon kwa mwendo wa tahadhari alinyata na alipoukaribia mlango ule alisikia mlio wa kwato za farasi ukija upande wake alipogeuka alikutana na kamba nene inayoikaribia shingo yake aliinama na kamba hiyo ikamkosa, alipojiinua aliiona ncha ya mkuki ikimlenga kifuani akaepa, na mkuki ule ukajichomeka mchangani. Orion alikuwa amefika eneo hilo, Seidon akauwahi mkuki ule lakini kabla hajaushika aliona ukiwaka moto, akaamua kuuacha, kabla hajageuka alijikuta akikanyagwa na miguu ya mbele ya farasi wa Orion ambaye alikuwa amejinyanyua na kusimama kwa miguu miwili.



    Seidon alidondoka mchangani na kutambaa kama mtoto, alitulia kidogo ili kumvuta Orion, Orion alisogea pale akiwa juu ya farasi wake, alimwangalia Seidon akiwa pale chini, Seidon alitulia kimya. Mara ghafla aligeuka na na kusimama bila kuchelewa aliuvuta upanga wa Orion kutoka kiunoni mwake na kuuzungusha kwa ustadi kitendo kilichosababisha farasi wa Orion kukatika miguu ya mbele kwa makali ya upanga ule. Orion alianguka chini na alipojiinua hakumuona Seidon. Seidon aliingia ndani ya chumba kile, mwanga uliojaa humo ndani ulimfanya kufinyafinya macho maana alishindwa kuuvumilia, kwa tabu aliliona fuvu la Cleopas limewekwa mahali na ndilo hasa lililokuwa likifanya mwanga ule, Seidon alilikimbilia na akajifungua kitamba chake cha kiuno ambacho kilikuwa na mfuko na kufunika fuvu lile, mara giza nene likatawala chumba kile.



    Seidon alimuona Orion kwa mbali akiwa anaingia kwenye ule mlango, Seidon akajibana kimya kabisa, Orion aliingia mpaka ndani kabisa ya chumba kile lakini alimpita Seidon bila kumuona. Kwa mwendo wa taratibu Seidon aliulekea mlango, alihakikisha hafanyi kelele yoyote ili asimgutushe Orion, alifanikiwa kutoka nje na akapiga mbinja kali ya mtindo wake mara farasi wake akafika eneo lile, bila kuchelewa Seidon akapanda farasi na kuanza kutimua mbio, aliamua kupuuzia maagizo yote ya Sherhazad malkia wa Soria, na kuondoka kwa kupitia lango la maghalibi.



    ***



    Mishumaa mikubwa yapata arobaini na saba ilikuwa imewashwa na kufanya mwanga wenye joto la kipekee ndani ya kasri la Sharhazad, malikia wa Soria, akiwa kwenye dirisha lake la ajabu, aliweza kuona ulimwengu wote isipokuwa upande wa nyuma yake, aliona kila kitu alichokifanya Seidon na jinsi alivyomgeuka, akasikitika na kusema, “Seidon ameamua kutugeuka, sasa ntamuonesha mimi ni nani,” Sherhazad alitoka kwenye dirisha lake la ajabu na kuketi kwenye kiti cha enzi akapiga makofi matatu na mara wazee wane wakaingia na vikorokoro vyao vya kichawi. Walipofika mbele yake wakaanguka kifudifudi na kutoa salamu hiyo ya heshima, Malkia wa Soria akawatazama na kuwaamuru wainuke, wakafanya hivyo, “Niwewaita, kuna kazi ngumu inatukabili mbele yetu, Cleopas, nataka fuvu la Cleopas, yule kijana niliyempa uwezo na maagizo ametugeuka, sasa nataka mumshughulikie na lile fuvu tulipate hapa haraka,” akasimama kutoka katika kiti chake na kujishika kiuno huku akiziruhusu nywele zake kumwagika sakafuni, akavuta hatua tano mpaka kwa mmoja wa wale wazee, akamshika bega na klumwambia, “Nataka kimbunga upande wa Maghalibi,”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vumbi kubwa lilitimka, upepo wa kisulisuli ulinyanyua kila kitu, Seidon alipambana na upepo huo ambao ulitaka kumfanya farasi wake ashindwe kuendelea, lakini kadiri ya ujasiri wa Seidon alimuendesha farasi yule kwa ustadi kiasi kwamba upepo ule haukumsumbua.

    Sherhazad akiwa kwenye dirisha lake la ajabu, alikasirika kwa kuona Seidon hapati shida na kimbunga kile, alisonya sonyo refu na kimbunga kile kikakatika ghafla, akageuka kumtazama mzee mwingine, “Mvua ya mawe” aliamuru tena. Mara anga likatanda wingu nene na mvua kubwa ya mawe ikaanguka, Seidon akiwa katika mwendo kasi aliiona mvua ile ikinyesha kumzunguka lakini alipo yeye hapakuwa na chochote, radi nazo zilijitahidi kupiga lakini wapi Seidon aliendelea kupiga mbio.

    “Inaonekana Seidon kawa jeuri sasa, nampa pigo la mwisho, na hasara iwe kwetu sote. Wape akili waamke, Wahamsud na Wakalban”

    Ndipo Seidon alipohisi anakimbizwa na watu wengi wenye farasi.



    ****



    Amata alimtazama Seidon kwa huruma sana, akampa kikoto cha maji ya kunywa, Seidon akayanywa na kidogo akaonekana kupata nguvu.

    “Seidon” Amata aliita. Seidon aliinua kichwa kuashiria itiko. Amata akanyanyuka kutoka pale alipokaa na kuelekea kwenye ukingo wa korongo kubwa sana, akageuka na kutazama pale alipomuacha Seidon, akafungua kinywa chake na kumueleza Seidon,

    “Ninyi wote hamjui mnachopaswa kutenda, kulileta hilo fuvu la Cleopas kwenye ardhi yako ni kuongeza mikosi.”

    Seidon aligutuka, akamkazia macho Amata,

    “Amata, we wa wapi? Inaonekana hujui lolote juu ya fuvu hilo” Seidon alimueleza Amata huku akimtolea macho. Amata akacheka kidogo, akaitazama pete yake iliyokuwa iking’aa kwa rangi tofauti tofauti, akaushusha mkono wake.



    “Seidon, fuvu la Cleopas linatakiwa lirudi kwa Cleopas. Kwa hiyo mwenye kupata baraka za Klakos ni yule atakayerudisha lile fuvu pale” Amata alimeza mate aliinua kibuyu chake cha maji na kugugumia mafunda kadhaa, akamuendea Seidon na alipomfikia akachuchumaa mbele yake, akamuuliza.

    “Sikia, Unaijua Klakos ni nini?” Amata alimtupia swali Seidon, na Seidon alionesha ishara ya kwamba hajui.

    “Vizuri sana, na wote hamjui, wote kabisa hamjui siri ya fuvu la Cleopas, sasa sikiliza, Cleopas na wenzake sita ndio walikuwa wakiiendesha dunia ya chini, dunia ya wafu, dunia ya waliolala, wao daima wamejipanga kwa mtindo huu, kushoto wapo watatu Aminus, Petrius na Segidus na kulia wapo watatu Sagitarius, Hesmepitus na Sectogamus, Cleopas yupo mbele katikati yao, ukiwaweka wote hivo ndio ule mkao wao unaitwa Klakos sasa waingereza miaka ile waling’oa fuvu la Cleopas ndiyo wakaleta ukame duniani maana chemchem, mito, mimea vyote si vinaota kutoka chini ni baraka za Klakos. Laana aliowapa ndio ile vita ya dunia huko Ulaya na matatizo mengine” Amata alimwangalia Seidon ambaye alionekana kukodoa macho tu.



    “Umenielewa?” alimuuliza Seidon ambaye alibaki midomo wazi, “Sasa unatakiwa uchukue lile fuvu ulirudishe kule kwa Cleopas kwenye mji uliopotea, mji wa wafu, Hamunaptra, mji ulio chini ardhini”.

    Seidon alishusha pumzi ndefu na kujiweka vizuri baada ya kusikia habari hiyo mpya.

    Aligeuka pembeni na kuutazama upanga wake, upanga wa Vernad, akauinua na kuubusu

    “Sikulijua hilo, na hakuna aliyewahi kuniambia” Seidon alimueleza Amata, aliuinua mkono wake na kuuweka begani kwa Amata “Wewe unatoka wapi?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mimi natoka Bara la Giza, nchi isiyo na mwanga, Amata ga imba, shujaa wa msitu wa Solondo,” Amata alijitambulisha kwa ubabe huku akijipigapiga kifuani. Seidon alimtazama kwa makini kijana huyu mweusi aliyejiamini kuliko vile alivyo.

    “Amata, nakualika katika hili, ufuatane nami tukakamilishe kazi hii, tuondoe laana katika jamii na baraka za Klakos zitumwagikie kama umande wa asubuhi” Seidon alimtupia ombi Amata kwa lugha ya kushawishi.



    “Hamna shaka, ombi lako limefika panapostahili, bega kwa bega tutakamilisha hilo, mimi nitakusindikiza kwa jua na mvua, kwa baridi na joto, kwa shida na raha,” walipeana mikono ya ushindi, kisha Amata akamuacha Seidon aendelee kupumzika.



    Baada ya majua 14



    Mazoezi makali yalikuwa yakiendelea kati ya Amata na Seidon katika misitu ya Progos, mazoezi ya kutumia panga, mishale yote yalichukua nafasi ili kumuweka fiti Seidon.

    Walipokuwa wameketi wakiota moto, Amata akamwambia,

    “Naona sasa tupo vizuri, twaweza kwenda” Amata alimwambia Seidon

    “Yah! Kumbuka tunaanzia kwa Wahamsud ambao ndiyo sasa wanalo fuvu hilo” Seidon alimkumbusha Amata.

    “Nakumbuka, Wahamsud tunawavamia usiku wa manane kupitia milima ya Ararat, tukiteremka ule mlima kwa chini utaona kijiji chao pale wewe utaenda kuliichukua hilo fuvu na mimi nitakulinda, inabidi tuhakikishe usiku uohuo tuwe tumeikamilisha kazi hiyo, maana wakitukamata tutakuwa nyama ya mbwa” Amata alimueleza Seidon huku wakiwa njiani kurudi kijijini.



    Mchana walijiweka sawa na jioni yake kuondoka kijijini kwao kwa dhumuni la kukikabili kijiji cha Wahamsud. Amata aliufutika upanga wake vizuri, aliiweka sawa pete yake ya ajabu aliyoipata kwa bibi kizee wa Msitu wa Solondo, kwa ujumla Amata alikamilika. Seidon, mpiga mbio, alikuwa tayari juu ya farasi wake, akiwa na upanga wa Vernad kiunoni na sasa alidhamilia kuupata upanga wa Orion iwe isiwe.

    Safari ikaanza wawili hawa wakaingia safarini, safari ilikuwa ngumu sana, kwa maana ilikuwa ni kupanda na kushuka milima yenye mchanga mwingi, mara kwa mara walikutana na dhoruba za jangwani zilizowapa taabu lakini walivumilia, safari yote hiyo hakuna hata aliyeongea na mwenzake kila mmoja alikuwa akiitafakari safari hiyo ngumu.

    Jua lilipokuwa maghalibi waliukabiri mlima mkubwa uliojaa mawe na miiba, kwa tabu walipanda mlima huo wakiwa juu ya farasi wao na baada ya muda tu walifanikiwa kufika kwenye tambarare iliyojazwa na uoto wa mkakati na mimea mingine yenye kustahimili shida, kando ya jiwe kubwa kulikuwa na mti wa mtende uliomea vizuri.



    “Seidon, tuketi hapa, tusubiri muda ufike ili tuweze kuwashukia Wahamsud,” Amata alimwambia Seidon.

    “Kwani haiwezekani kuwavamia sasa?” aliuliza

    “Hapana, Wahamsud wanategemea nguvu ya nyota inayoitwa LEO, inabidi tusubiri hapa kwa masaa kama mawili, nyota ile ikifika maghalibi tayari hawana nguvu, tutafanya kazi yetu kwa urahisi ambao hautautegemea, na tukishalipata fuvu ni safari ya moja kwa moja Hamunaptra kupitia upande wa kusini kandokando ya bahari nyekundu mapaka kaskazini mwa Kushi, tusipite kwa yule mchawi Sherhazad atatusumbua sana kwa kuwa bado ana chuki na wewe.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waliketi chini ya mtende huku Amata ga Imba akiendele kuburudika na kibuyu chake cha pombe.

    “Amata, huoni kwamba pombe unayokunywa inaweza kuharibu mipango yetu?” Seidon aliuliza baada ya kuchoka kuvumilia kwa kuwa wao kwao pombe ni mwiko kabisa kwani wamelelewa na falsafa inayosema pombe hulowesha roho.

    “Hapana, hii inasaidia sana kwa kuwa kuna baadhi ya nguvu za kishetani ambao hazitaki pombe, sasa mimi na wewe hatujui tukienda huko tunaenda kukutana na nini,” lilikuwa jibu la Amata ga Imba.



    Ilipotimu usiku wa manane, sauti ya Mbweha wa jangwani ikasikika, Amatagaimba aliinuka kutoka pale chini ya mtende, mbala mwezi ilikuwa iking’aa sana, Amata alisimama na kuangaza macho yake huku na kule, akamwamsha Seidon.

    “Kijana, amka, saa imefika inapaswa tutende lile tulilolikusudia,” Amatagaimba alimuamsha Seidon. Seidon alisimama na kujinyoosha, akachukua gudulia lake la maji na kugugumia mafunda kadhaa, kisha akalitua na kulirudisha kiunoni.



    “Na hii mbalamwezi huoni kama itatuharibia?” Seidon aliuliza.

    “Usiwe na shaka, Seidon, nitaifunika kwa nguvu za ajabu, na wingu litasimama juu yake mpaka tutakapomaliza kazi yetu,” Amatagaimba, alimtazama farasi wake na kumshikashika kichwani, “Seidon, tunaingia katika mji bila farasi, kwa mwendo wa miguu yetu,” Amata alizungumza huku akiweka podo lake mgongoni na kuukamata vyema uta wake, kwa mwendo wa taratibu walianza kuushuka mlima ule huku Seidon akishuhudia wingu zito likianza kuifunika ile mbalamwezi taratibu na kutengeneza kivuli kizito. Haikuwachukua muda walifika katika kilima kingine kidogo tu, walipokwea mpaka juu waliweza kuona mji wa Wahamsud ukiwa kimya ni mioto tu ya hapa na pale iliyokuwa ikiendelea kuwaka. Amata ga Imba alitulia akiangalia kwenye zile nyumba za Wahamsud, Seidon hakuthubutu kumuuliza anaangalia nini bali aliendelea kumtazama.



    “Seidon, hapa kazi ni ndogo tu, unaiona nyumba ileeeeeeee,” Amata alimuonesha Seidon nyumba iliyopo katikati ya zingine, iliyokuwa ikiwaka taa hafifu, “Pale ndipo penye fuvu la Cleopas, ulinzi uliopo pale ni mkali sana usione pametulia, sasa jiweke tayari tunaenda na lolote linaweza kutokea, mimi nitalinda nje wakati wewe utaingia ndani kulichukua hilo fuvu,” Amata alitoa maelekezo na kisha akauchukiua uta wake na kuuweka sawa, akachomoa mshale na kuutunga vyema kisha akauvuta kwa nguvu sote, “Seidon, washa moto hapo mbele, nataka niwapelekee kizaizai,” Seidon akawasha moto kwenye ncha yam shale wa Amatagaimba iliyokuwa imefungwa kwa kitambaa kizito chenye mafuta mazito ya mimea, kiliposhika moto sawia, Amata aliutazma mshale wake ulikuwa tayari kwa shambulizi, “Nakuagiza, katika jina la Amatagaimba, shujaa wa msitu wa Solondo, alieukonga moyo wa Baghoza na kuushusha utawala wa Kerume kwa mshale huu, mshale wa urithi wa mzee Nkhunulaindo, uende ukaanzishe kile tunachokikusudia,” akaunuia mshale wake aliokuwa amekwishauvuta kwa nguvu zote, akauachia nao ukaondoka kwa kasi ya ajabu, mvumo wake ulitikisa miti michache iliyo jirani na mle ulimopita, wakasimama juu ya kilima kile wakiuangali ukienda ulikotumwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Juu ya paa la nyumba ya mtawala wa Hamsud, mshale wa ule ulitua na kuwasha moto paa lile lililojengwa kwa aina Fulani ya mimea iliyoshika moto ule kwa kasi.

    “Twende sasa!” Amatagaimba akamwambia Seidon kisha wote wawili wakashuka wakikimbia upande ule kuliko na ile nyumba lilikohifadhiwa lile fuvu, Seidon, mpiga mbio alikuwa mbele na upanga wake mkononi, upanga wa Vernad mwana wa Velvesh. Watu walitoka kwenye nyumba zao na kujilinda huku wengine wakienda kusaidia kwa mfalme.

    “Tumevamiwa!!!” sauti ilitoka kwa mtu mmoja mwenye tambo kubwa aliyekuwa juu ya paa la nyumba mojawapo lililoonekana lilijengwa kama ngome ya kuweza kuwaona adui wanapokuja kutokea pande za milima Ararat.



    “Tumevamiwaaaaaa!” Yule mtu aliendelea kutoa hamasa kwa wengine, milio ya panga zilizofutwa kutoka katika ala zake ilisikika kila upande, Yule mtu kule juu alichukua baragumu na kupuliza, ikiwa ni ishara ya kuruhusu mapigano ya damu, kabla hajatua lile baragumu lake, mshale mmoja wa Amatagaimba ulipenya kifuani na kumdondosha kutoka juu mpaka chini, Amatagaimba alitua ardhini kutoka juu ya nyumba moja wapo na kuufuta upanga wake, hakujali ni wangapi wamemzunguka na silaha gani lakini ustadi wake wa kuuzungusha ule upanga uliweza kuwapunguza nguvu adui kwa kuwakata vibaya, ijapokuwa walionekana ni wengi lakini walionekana kana kwamba hawana nguvu za kufanya mapigano hayo ya kushtukiza.



    Seidon, alipambana na upinzani mkali kuweza kulifikia lango la ile nyumba, huku nje tayari akiwa ameshaua askari kadhaa, aliupiga teke mlango na ukafunguka bila kipingamizi, aliingia ndani na kutazama huku na huku, mara akasikia sauti ya kicheko nyumma yake, alipogeuka aligongana macho na mfalme wa Hamsud aliyevalia guo lake jeusi, mkononi akiwa na upanga wa makali kuwili, Seidon alisimama kimapigano na upanga wake mkononi.

    “Umekuja mwenyewe sio, sasa kama siku ile nilikuacha hai leo lazima nikikate kichwa chako kwa upanga huu, upanga wa Hamsud, wenye mapigo ya ajabu,” Yule mfalme aliongea kwa jazba huku akimfuata Seidon kwa kasi.



    “Hakika, nimekuja kuitaka roho yako na kulichukua fuvu la Cleopas ambalo si mali yako, amin nakuambia upanga huo mkononi mwako leo hii utakuwa mikononi mwangu,” kabla Seidon ahajamaliza kusema, ilisikika kelele ya panga mbili zilizogongana na kutoa cheche, ilikuwa ni pigo la kifo lililotoka katika mikoni ya Yule mfalme, lilikuwa likikielekea kichwa cha Seidon ambaye tayari nay eye Alisha inua upanga wake na kuuzuia ule wa Yule mfalme, kisha wote wawili wakashusha mikono yao chini na zile panga bado zikawa zimesigana katakati yao, wakisukumana na kutazamana kwa gadhabu. Seidon alijisogeza pembeni kwa ghafla na kumpiga pigo la kiwiko Yule mfalme, lakini kabla hajafanya lolote, upanga wa mfalme ulipita katika tumbo la Seidon na kuchana upande wa vazi lake, Seidona akaruka sarakasia kutua upande wa pili alijishika tumbo kwa maumivu, lakini bado alikuwa katika mapambano, mapigo kadhaa ya mapanga yaliifunikiza nyumba ile huku Seidon akionekana kuzidiwa maarifa na Yule mfalme, hakuna mtu aliyeingia katika pambano hilo.

    Amata ga Imba alikuwa nje akiimarisha ulinzi kwa kupambana na askari wale ambao walijiziuka naye wakisahau kuwa ndani ya hekalu lao kuna mwingine anayepambana na mfalme wao. Amata ga Imba aliangusha wengi awezavyo huku akiwakwepa kwa ustadi wa hali ya juu, akijaribu kuvuta muda ili Seidoni afanikishe lile alilotumwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Amata ga Imba alipoona Seidon hana dalili za kutoka alifanya kila hila za kimapigano na kukimbilia upande, mwingine ambao alikuwa jirani kabisa na lile hekalu la Wahamsud, mara akajikuta amezingirwa na askari wenye uchu wa kuitoa roho yake, aliishika pete yake na kuifanya anachojua yeye, mwanga mkali ukatoka kwenye pete ile na kuwaumiza mcho wale askari hata wasiweze kuona tena. Amata aliukaribia mlango wa hekalu na kuona jinsi pambano lile lilivyokuwa likiendelea lakini Seidon hakuonekana na upanga mkononi, “Seidoooooonnnnn!” Amata aliita na kumrushia upanga wake, Seidon alijrusha kwa ustadi na kuudaka ule upanga, alijiviringisha kwa ufundi kumuelekea Yule mfalme ambaye alishidwa kujua amshambulie nani.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog