Search This Blog

HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE



    *********************************************************************************



    Simulizi : Hamunaptra - Mji Uliopotea

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Riwaya ya kufikirika, itakayokupa taharuki, tafadhali soma kwa makini ikiwezekana rudia mara kadhaa ili upate uhusiano wa mtukio yaliyoitengeneza riwaya hii kali, tamu, haijawahi tokea katika kare hii



    CHAPISHO LA 1



    I



    Seidon alipita kwa kasi na farasi wake mweupe, mwendo aliokuwa akienda ulikuwa si wa kawaida hata kidogo, kwa kuwa farasi huyo alimjua vyema bwana wake, alitii kila amrisho apewalo. Kila alipogeuka nyuma, Seidon alishuhudia vumbi likitimka katika jangwa lile umbali mfupi kutoka yeye alipo, aliongeza mwendo, na farasi wake alitii.



    Njia ilikuwa na mchanga mwingi, jua kali la utosi lilimfanya Seidon alowe kwa jasho, akiwa mkono mmoja kashika lijamu ya farasi wake, mkono mwingine ulikuwa umeshika mfuko mweusi, hakukubali kuachia hata kimoja wapo kati ya vyote. Alimaliza kijangwa kile kwa tabu na kuuanza msitu mdogo lakini wenye miti mingi na mirefu, vichaka vilivyofungamana, aliangalia nyuma kwa mara nyingine, bado aliona vumbi lile na sasa halikuwa mbali sana na hapo, moyo ulimdunda kwa kasi, kiu ilimshika koo na kuipoza kwa jasho lililokuwa likitiririka usoni mwake. Mara ghafla alijikuta akipaa juu na kujibwaga chini kama mzigo, mfuko mweusi ulimtoka mikononi na kuangukia pembeni, farasi wake alikuwa akijaribu kuinuka kutoka pale alipoanguka.



    “Ha ha ha ha aaaaaa, mbio za sakafuni huishia ukingoni!” sauti ilisikika kutoka katika kichaka cha jirani. Seidon alishtuka na kujaribu kunyanyuka lakini alishindwa, kumbe alipoanguka aliteguka mgongo, alibaki kugugumia tu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwanaume mrefu aliibuka kutoka kichakani akiwa amevaa nguo nyeusi na kichwani kajifunga kitambaa cheusi, kiunoni mwake alikuwa na jisu kubwa, aliuokota mfuko ule na kuuchungulia ndani, kisha akatikisa kichwa kuashiria kuwa kilichomo humo ndani ndicho hasa akitakacho. Akapiga mbinja kali, na mara katika vichaka vile waliibuka watu takribani kumi na tano wenye mavazi ya kufanana na wote wameweka majisu makubwa viunoni mwao, wakakaribia eneo lile ambalo Seidon ameangukia, wakamzunguka. Yule mkubwa wao akasogea jirani na Seidon, akamwinamia kama anataka kumwambia kitu. Akamtazama, Seidon alikuwa nusu mfu.



    Yule kiongozi wao akatwaa upanga wake na kumchoma kidogo shingoni, Seidon aliinua kichwa kumtazama.

    “Hata nikikukata kichwa nitapoteza nguvu zangu tu. Hao wanaokuja ndiyo watakaokuua.” Yule kiongozi alirudisha upanga wake alani na kuwatazama vijana wake “Ale!” alito amri na mara farasi kwa idadi yao walitoka porini na kufika eneo lile, wakapanda na kutokomea zao porini.



    888



    “Shit!!!” aling’aka kwa hasira Bw. Kalban. Alimwangalia Seidon pale chini akiwa hajitambui. Alijishika nywele zake ndefu na kuzitimuatimua huku akizungukazunguka bila mpangilio, aliona wazi kuwa wamewahiwa kwa kila hali.

    “Kichwa kiko wapi?” alimuuliza Seidon kwa hasira huku akimnyooshea upanga wake mkali.



    Seidon kwa shida aliinua mkono kumuonesha jamaa walipoelekea. Bw. Kalban aliwageukia wafuasi wake ambao bado walikuwa juu ya farasi zao,

    “Wahamsud, wametuwahi!” aliwaambia vijana wake, ambao wote walionekana kugadhibika kwa hilo, wakifikiri jinsi walivyo mkimbiza kutoka mbali sana na wasipate wanachotaka.

    “Hatuwezi kukata tamaa, lazima tukipate kile kichwa, twendeni tuwafuate” Bw Kalban na wafuasi wake walipotelea porini kuwafuata waamsud na kumuacha Seidon palepale akiwa hajiwezi kwa lolote.



    “Ha ha ha ha ha !!!” Bw. Hamsud alicheka akiwa kashika fuvu la kichwa mikononi mwake akiligeuzageuza “Mmmmh! Hapa ndiyo kila kitu, neema zote za ‘Klakos’ ziwe juu yetu” alipomaliza kusema hayo wale wafuasi wake wakapiga magoti na kuinamisha vichwa vyao, kwa pamoja wakaitikia



    “Amin, viwe kwetu sote”

    Kisha kwa pamoja walielekea kwenye jingo la kale, hamamu la Kipersia lililojengwa miaka zaidi ya mia tano nyuma na kuingia, ndani humo kulijawa na giza nene lakini walipoingia tu lile fuvu likang’aa na kufanya mwanga ndani ya lile hamamu, mwanga wake ulikuwa ni zaidi ya wa mchana unaoujua wewe. Wakiwa ndani ya mavazi meusi, walizivuta kofia zao zilizounganishwa na maguo yao meusi ambazo daima huning’inia kwa mgongoni, wakajifunika na kukaa kwa kutumi amagoti katika mtindo maalumu.



    Bw. Hamsud akiwa na fuvu lile alitembea taratibu huku akisemasema maneno Fulani kwa sauti ya chinichini, mara akafika sehemu ya mbele kabisa, ambapo palikuwa na kitu kama sanamu ya mtu lakini hakikuwa na kichwa, akainua lile fuvu na kukipachika kile kichwa juu yake. Radi kali ilipiga na kulikata anga lote, vishindo vya kutisha vikaendelea kusikika, wafuasi Wahamsud ndani ya lile hamamu walilala kifudifudi wakisema maneno Fulani Fulani.

    Wingu zito lilifunika anga lote na mvua yenye upepo ikaanza kunyesha kwa fujo.

    “Shusha mema yako ee Klakos,” walirudiarudia maneno yale wakiwa bado katika hamamu lile.



    Wahamsud, walikuwa ni jamii ya watu iliyoishi huko pembezoni mwa mto Ganges, jamii ya wakulima iliyokuwa na roho mbaya ya ubinafsi, kijiji chao kilikuwa ni kijiji chenye kila uhai, ardhi yenye rutuba, mazao na uoto wenye afya. Lakini daima walipenda kunyenyekewa na majirani zao, walipenda kuonekana wao ni Miungu watoto , walizuia maji yam to Ganges yasiende kwa wengine, daima alipora mali za majirani zao na kujilimbikizia wao, walikuwa hata wakipita maeneo mengine, wakiona wanawake wazuri huwateka na kuwapeleka kijini kwao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara hii walipata habari juu ya fuvu la Klakos, Mungu wa zamani wa Wahabesiani, kihistoria iliaminika Mungu huyo aliishi miaka zaidi ya mamilioni yaliyopita huko Hamunaptra, India.



    Ilisemekana kuwa Klakos aliweza kukupa kila utakacho, mvua, jua, mali, mazao, kuishi muda mrefu, kushinda vita na kila utakacho. Tamaa ilimjaa Bw Hamsud, kiongozi wa jamii hiyo, aliwaita vijana wake wakakamavu na kuwapa habari hiyo, na kuamua kufunga safari kwenda Hamunaptra kutafuta fuvu hilo kwa hali yoyote ile, wakafanya hivyo. Safari yao haikuwa rahisi kama walivyofikiria, ilikuwa ngumu sana ukizingatia wao hawakuwahi kuishi jangwani, ilibidi wakatishe jangwa kubwa ili kufika huko. Kama walitegemea wafike na kulichukua fuvu hilo na kuondoka basi haiakuwa hivyo, walikuta jamii nyingi za watu wakitafuta kitu hicho hicho, achana na wale ambao wamekuja huko kujifunza ‘study tour’ kutoka nchi mbalimbali za ulimwengu. Kulikuwa na mchanganyiko wa watu wengi eneo hilo.



    888

    Warelvesh, walikuwa wakiishi kwa shida sana katika jangwa kubwa la Persia, wao walikuwa ni wafanyabiashara lakini mara nyingi walikuwa wakiporwa biashara zao na Wahamsud kila waendapo kupeleka bidhaa zao sehemu mbalimbali za ulimwengu.

    Wakawa masikini, mji wao haukuwa na rutuba sana ya ardhi, walitegemea vitu vingi kutoka nje ya mji wao kwa kununua au kubadilishana. Walikuwa wema, wakarimu, hata wasafiri wakipita hapo ilikuwa lazima wasimame na kupata japo chakula au kinywaji.

    Walisikia habari fuvu lile wakiwa katika misafara ya biashara katika nchi za bara Hindi.



    Miaka 1200 iliyopita



    Siku moja wakiwa katikati ya mji wa Jamunah, mtu mmoja aliyeonekana kama kichaa alikuwa akipayuka huku na huko habari juu ya fuvu hilo. Watu walimsikiliza na kumpuuzia. Vernad alisimamisha farasi wake mweusi mwenye manyoya mengi ya kuvutia mbele ya kichaa huyo, alimtazama kwa tuo, juu mpaka chini, watu walikuwa wakimfukuza kila apitapo na kelele zake. Vernad alimsikiliza kwa makini sana mtu huyo mwenye nywele ndefu na nguo chafu. Alipoona watu watamshtukia kwa jinsi alivyomwangalia kichaa yule alimuamuru farasi wake kusonga mbele, baada ya umbali mfupi alisimama na kushuka kwenye mgahawa mmoja ili kupata kahawa.



    “Huyu mtu mbona ana kelele sana?” alimuuliza mmoja wa wahudumu wa mgahawa huo huku taratibu akinywa kahawa yake na kashata zilizotengenezwa kwa karanga.

    “Ah huyo ni kichaa tu hana lolote, kila siku yeye ni kelele hizo hizo, amechanganyikiwa” alijibiwa.

    “Mh!” Vernad aliguna na kumkazia macho mhudumu yule, kisha akaendelea “Fuvu! Fuvu gani anazungumzia?”

    “Aaah habari za zamani hizo kaka!”

    “Za zamani?! Kivipi?”

    “Huyu jamaa wanasema ni mchunguzi wa mambo ya kale, sasa amechanganyikiwa na mambo mengi ya ajabu aliyokuwa akiyaona wakati huo. Hakuna anayejua kuhusu hilo fuvu, yeye anakazania ‘ukilipata linakupa kila kitu’”

    Vernad alipotelea katika mawazo mazito, moyoni mwake hakuona chembe ya uongo hata kidogo katika kelele zile za kichaa.



    Alitafakari kwa kina na akaona hakuna la kufanya lazima juu chini ampate kichaa yule ili apate ukweli wa habari hiyo na ikibidi ahakikishe fuvu hilo analitia mkononi. Aliinua kichwa chake na kumtazama yule mhudumu, hakumuona, moyo ulienda mbio au alikuwa anaongea na Jini? Hakupata jibu. Aliuvuta mkoba wake na kutoa dinari kadhaa na kuziweka mezani pale, moyoni aliazimia wazi kuwa lazima alale katika mji huo wa Hampusta na kuhakikisha usiku huo ampate kichaa yule. Alitoka nje ya mgahawa ule na kushangaa kukutana na giza lililotanda nje, watu wakikimbia kimbia huku na huko, alitazama vizuri angani na kuona ni kundi kubwa la nzige likipita na kuzuia mwanga wa jua kuifikia dunia. Alipiga hatua chache na kuchukua farasi wake kisha kurejea kule alikomuona kichaa yule.



    Alikodi chumba kwenye nyumba ya kulala wageni katikati ya mji ule. Baada ya kujipumzisha jioni ile alitoka na kutembeatembea mitaani, hakuchukua muda mrefu sana mbele yake alikuta jumba kubwa la kifahari lenye kila nakshi za kisultani, liliyapendeza macho yake hata kumfanya asimame kuliangalia. Akiwa katika kulishangaa jumba hilo ndipo alipohisi kama kuna mtu nyuma yake, akageuka taratibu huku mkono wake ukiwa umeshika mpini wa jambia lake tayari kwa shambulizi la aina yoyote ile.

    “Ha ha ha ha ha!!!!” kicheko cha kutisha kilizifanya nywele zake kusimama, hakuelewa aliyetazamana na ye ni binadamu au ni nani. Katika mtu huyo mara aliona sura ya yule kichaa mara kwa mchanganyiko iligeuka na kuwa ya nyoka, mara ya kobe. Vernad alirudi nyuma hatua kadhaa sasa jmabia lake likiwa mkononi.



    “Unanitafuta! Umenipata, haya sema shida yako” Vernad alisikia sauti kama kumi na tano zikitoka katika kinywa cha mtu yule. Alishindwa afanyeje, aliendelea kurudi nyuma lakini bado alimuona mtu yule bado akiwa umbali ule ule kutoka kwake, aliamua kutimua mbio. Kelele nyingi zilimfuatia nyuma yake kana kwamba kuna watu walikuwa wakimfukuza. Aliongeza mwendo kukimbia, hamad! Alijikwaa na kuanguka chini, alipojigeuza kutazama juu kwa mtindo wa ‘chali’,radi kali ilimpiga usoni hata kuhisi kuwa amepoteza nuru ya kuona.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kaupepo katamu kalimpitia Vernad, alijaribu kuamka pale alipokuwa lakini ilikuwa ni vigumu kwake. Alilala tena kwa utaratibu katika vumbi lile, kwa haraka haraka hakujuwa ni wapi alipo, jangwa kubwa lilimzunguka na jua kali lilimchoma uso, alichokiona sehemu hiyo ni misafara ya ngamia kutoka eneo moja kwenda lingine. Alifanikiwa kunyanyuka baada ya kukusanya nguvu nyingi sana, aliinuka na kujipukuta vumbi lilioujaza mwili wake na kumfanya awe kama kinyago. Aliyaficha macho yake kwa viganja vya mikono yake ili kupambana na nuru kali ya jua iliyomlenga moja kwa moja machoni kwake.

    Kutoka mbali aliona farasi aliyekuwa akielekea pale alipo kwa kasi sana, Vernad alitulia kuona kitachoendelea. Punde si punde farasi yule alisimama mbele yake na mtu aliyekuwa kapanda juu yake aliteremka na kuuvuta mkoba wake toka mgongoni, akatoa kibuyu cha maji na kumpa Vernad aliyekuwa amekaushwa kwa jua kali lenye hasira.



    “Asante bwana! Bila shaka wewe ni mtu wa Mungu” Vernad alimshukuru yule mtu.

    “Ha ha ha ha ha !!!” yule mtu alitoa cheko lililomfanya Vernad akumbuke yaliyompata usiku ule.

    “Umejuaje niko hapana nahitaji maji?”

    “Nimekuona tangu mbali sana, na lengo lako la kusaidia watu wako, Warelvesh. Vernad! Naitwa Ismokum, mimi ni mtu kutoka kuzimu, nilishakufa miaka mingi nyuma na sasa naishi katika hii dunia ya chini, mji wa Hamunaptra.” Alikohoa kidogo, huku akishuka kutoka katika farasi wake na kusimama chini katika ardhi yenye mchanga mwingi. Alimsaidia Vernad kunyanyuka na pamoja wakasogea pembani palipokuwa na jabali kubwa wakakaa hapo.



    “Sijaelewa! Umesema wewe ni mtu uliekwishakufa?”

    “Ndiyo, bila shaka, mimi nilishakufa miaka mingi ambayo hata babu yako alikuwa hajazaliwa.”

    “Hamunaptra ni kitu gani?” Vernad aliendelea kwa maswali.

    “Huo ni mji wanaokaa watu waliokufa zamani, mji wa wafu, mji uliopotea. Mji ambao sasa upo chini ya ardhi, mji usio na shida wenye kila kitu utakacho isipokuwa mapenzi.” Yule mtu alimjibu Vernad.

    Vernad alimkazia macho mtu yule mwenye manywele na mandevu marefu sana, midomo myekundu kama aliyekula nyama mbichi, macho yake ambayo yalikuwa yameangalia kilamoja upande wake, hakika alikuwa marehemu jinsi alivyoonekana.

    “Na hapa nimefikaje?”



    “Jana usiku ulikuwa ukinifatilia mimi, na nilijua unachotaka kwangu, sasa usihofu, umepata. Fuvu la Cleopas! Kulipata si kazi ndogo, kwanza Cleopas mwenyewe analitafuta pepo zote nne za dunia” Vernad, alistuka kidogo ‘analitafuta?’

    “Ndiyo, analitafuta!” yule mtu alimwambia Vernad, ambaye alistuka kwa mara ya pili, ‘kajuaje kama nimejiuliza analitafuta?’. Vernad alijua kuwa, haswa kujiingiza katika kutafuta kitu usichokijua ni hatari lakini afanye nini? Kwa ajili ya watu wake. Yule mtu alivuta hatua chache mbele na kumpita kwa karibu Vernad, alipompita aligeuka kumwangalia, hakuwa mtu yule, sura yake ilionekana kama iliyooza ikibubujika mabonge ya damu, meusi, mdomoni, puani na machoni. Vernad alitetemeka kwa woga, hakujua kama akimbie au abakie pale pale.



    “Ukilipata fuvu hilo ulirudishe kwenye mji wa Hamunaptra na ulipachike kwenye shingo ya Cleopas na hapo Clakos atakupa utakacho. Ukikaidi litakuteketeza wewe na jamaa yako yote”. Upepo wa ghafla ulipita kati yao na vumbi la jangwa likawatenganisha, lilipotulia Vernad hakuona mtu wala kitu mbele yake. Sauti zilifikia masikioni, sauti za ajabu zikijirudiarudi ndani yake zikitamka jina Hamunaptra, Hamunaptra, Vernad aligeuka huku na huku, akisumbuliwa na sauti zile lakini hakuona aliyeongea wala hakujua zimetoka wapi, aliziba masikio lakini bado aliendelea kuzisikia kwa nguvu sana.



    1850

    Sehemu Fulani huko India

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jua liliwaka kwelikweli, vibarua walifanya kazi ngumu ya kuvunja mawe na kusogeza hapa na pale, kukusanya vyuma ili kutandika reli mpya kwa manufaa ya koloni la Uingereza. Askari wa Kiingereza walisimama kando wakipuliza moshi wa kiko na cigar, huku mijeledi ikiwa viunoni mwao, hutakiwi kusema umechoka wala unaumwa, utafanya kazi mpaka pumzi yako iishe.

    Haikuwa rahisi hata kidogo, mataruma mazito yalivutiwa hapo na kazi ya kuunganisha njia ya reli iliendelea chini ya engineer wa kiingereza aliyejawa na dharau na nyodo kupita kiasi.



    Ili kupata mawe yanayotakiwa hasa katika kazi hiyo iliwabidi kupasua majabali makubwa na miamba ya kutisha, vibarua wengi walipoteza maisha kwa kupigwa na mawe hayo yaliyoruka huku na huko. Baada ya kupasua mawe hayo an kuyamaliza sasa walianza kuchimba kuelekea chini. Hakukuwa na mashine kama hizi tulizo nazo wao walichimba kwa dhana duni lakini zilikuwa bora kwa wakati huo.



    Prakesh Minto, kibarua aliyeipenda kazi yake aliinua juu sururu yake na kuitelemsha ili kupiga jiwe lililoonekana kujitokeza katika shimo hilo, kabla sururu ile haijatua alijikuta ikimtoka mikononi na kuruka pembeni, kisha alisikia sauti zikiongea maneno yasiyoeleweka. Prakesh alichanganyikiwa na kuanza kukimbia hovyo. Waingereza wale waliokuwa hapo katika kusimamaia shughuli ile walimuona Prakesh kama aliyeruykwa na akili, walimpiga risasi na kumuua.



    Kisha wakasogea eneo lile, kijana mwingine alikuwa akichimba lufuata kitu kama ukuta. Walipoona ukuta ule hauna dalili ya kufika mwisho ndipo walipoomba wataalamu kutoka Uingereza kuja kutoa msaada katika hili.

    Baada ya Miezi kadhaa ya kuchimba na kusafisha eneo lile walijikuta mbele ya mji mkubwa, mji wa kale ambao kwa wakati huo ulikuwa umesha zama ardhini kwa karne na karne, hata waenyeji walikuwa wakiishi hapo miaka hiyo hawakulijua hilo. Kuta zenye nguvu, nguzo kubwa, milango iliyotengenezwa kwa mbao ngumu ambazo zilidumu hapo bila kuliwa na nondo.



    Paul Smith, aliivua kofia yake aina ya pama na mkono mmoja alikuwa kajishika kiuno. Mtaalam huyo wa mambo ya kale, alijivunia sana ugunduzi wake, aliendelea kupiga mluzi akiimba moja ya nyimbo za kwao. Baada ya kuhakikisha kuwa eneo lote liko safi, waliadhimia sasa kuingia ndani ya mji huu kujionea kilichopo, mioyoni mwao waliamini kuwa sasa utajiri upo jirani. Walijaribu kuvunja mlango lakini hata hawajathubutu mlango ulifunguka wenyewe na kiza kinene kiliwa karibisha.



    888



    Vernad aliitoa mikono yake masikioni, nyuma yake alikuwa amesimama mtu mmoja wa makamo aliyeva kanzu la hariri, kichwani kajiviriga kilemba cha rangi ya hudhurungi. Vernad alimtazama mtu huyu kwa woga hakujua kama ni yule aliyeondoka kwanza au huyu ni mwingine, aliendelea kumtazama huku kasimama kidete mono wake wa kulia ukiwa tayari umeshika mpini wa jambia lake.



    “Ha! ha! ha! ha! ha! Vernad, karibu sana Hamunaptra. Huku hatutumii silaha kwa kuwa wote tunaoishi hapa ni wafu, huu ni mji wa wafu, wafu siku zote hawafi tena” yule mtu alimaliza kauli yake na kuelekea upande wa maghalibi wa jangwa lile, naye Vernad alimfuata uko huko.

    “Wewe ni nani?” Vernad alimuuliza mtu yule huku akimfuata nyuma kwa kukimbia maana mwendo aliyekuwa akitembea haukuwa wa kawaida.



    “Mimi ni Maghalibi” alimjibu Vernad ambaye sasa alikuwa amesimama akimtazama mtu yule akitokomea vumbini na kadiri alivyokuwa akienda aligeuka kuwa vumbi. Vernad alisikia sauti za watu wakimpita huku na huko lakini hakuweza kuona mtu yoyote, alihisi kama yuko sokoni lakini bado hakuona chochote zaidi ya mchanga mwingi uliyojaa katika eneo laote hilo. Kwa namna moja au nyingine Vernand alikuwa anahangaika hakujua yuko wapi, anakwenda wapi na anatoka wapi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    II

    Miezi michache nyuma…



    “Seidon!” sauti ya kizee iliita

    “Naam!” Seidon aliitikia huku akikurupuka kutoka alipolala na kumuwahi babu yake ambaye alikuwa mzee sana na katika uzee huo daima alipenda kukaa na mjukuu wake, Seidon.



    “Seidon!” yule babu aliita tena, sekunde chache za ukimya zikapita kati yao, “Umeshakuwa kijana sasa! Watu wetu wanaishi kwa shida sana, hatuna maji, hatuna mvua, ardhi imepoteza rutuba kabisa, hii ni laana kwetu. Inabidi ukatafute fuvu la Cleopas”, Seidon alistuka kidogo aliposikia hilo, babu yake akampigapiga mgongoni kwa upole “Usiogope, siri ya fuvu la Cleopas na baraka za Klakos, ziko na sisi watu wa Relvelsh, chukua farasi wangu, piga mbio kuelekea Maghalibi mapaka Hamputra, pita kijia kidogo cha kuelekea katika mpaka wa Pakistan na India, ingia kwenye mapango ya Dosh na utatokea Mesopotamia, funga safari mpaka kwenye mapiramid ya Misri kwa njia ya chini, nenda kalete fuvu la Cleopas”.



    Seidon aliangalia chini, hofu kuu ilimjaa moyoni akijaribu kupima ugumu wa safari hiyo na umbali wa njia lakini hofu ilimuondoka mara tu alipokumbuka kuwa farasi wa babu yake alikuwa na mbio za ajabu.

    “Sogea hapa Seidon,” babu yake alimwita Seidon na kuichukua mikono yake na kuipachika mapajani kama ishara ya kula kiapo.

    “lazima uwe muaminifu, babu wa babu zako Vernad alifanikiwa kulipata fuvu hilo kutoka katika mikono ya Wamisri baada ya kupambana kiume na shujaa Orion, na sasa lipo katika mikono ya Waajemi baada ya kuja na kutunyang’anya apa hapa kwetu, ukiwa njiani usitamani mwanamke wala kulala nae, la, utapata nuksi ambayo kazi niliyokupa itakushinda” Babu yake alimaliza wosia na seidon akatoka na kuketi chini.



    “Babu nitahakikisha nafanikisha hilo kwa uaminifu.” Alijibu kwa utii.

    “Chukua upanga wa Vernad hapo juu, na roho yake ikuangazie katika mapito yako.”





    Jioni hiyo Seidon alichukua farasi wa babu yake, farasi mweupe, na kujifutika upanga wa Vernad kiunoni, kisha kutokomea kuelekea jua linapozama. Safari ilikuwa nyepesi sana mwanzoni, farasi alipiga mbiyo za kutosha zilizofanya Seidon kuifurahia safari hiyo, alipita miji mbalimbali, majangwa na mapori akiutafuta mji wa Hamputra. Usiku mnene sana alifika Hamputra, mji mtulivu kila mtu alikuwa amejifungia ndani na kuota ndoto zake. Ni kiumbe mmoja tu, Seidon alikuwa nje akipita taratibu katika barabara ya mawe iliyopita katikati ya mji huo, mwendo mfupi mbele akasimama, akatoa kibegi chake na kufungua kishapo akaketi chini ya mti na kula chakula chake taratibu akishushia na maji. Kwa mbali aliona mtu akielekea upande ule alioketi yeye, alimwangalia kwa makini sana, hakuamini macho yake, akayafikicha, maana aliona labda kasinzia. Msichana mrembo wa sura, mwenye rangi mororo ya kuvutia alikaribia eneo lile aliloketi Seidon, mwendo wake wa kunesa ulianza kuusumbua moyo wa Seidon, shujaa wa Relvesh ‘njiani usitamani mwanamke wala kulala nae’, kauli hii ya babu yake ilimkosesha raha kila alipoikumbuka. Aliendelea kumkodolea macho kiumbe yule ambaye sasa alikuwa kasimama umbali wa kurusha jiwe tu, alimtazama kuanzia macho mapaka miguu na kuridhika na uzuri wake, Seidon akajikuta hali yake inakuwa mbaya, mate ya utu uzima yakamtoka. Msichana yule alimsogelea Seidon na kumshika mkono akamuinua.



    “Ewe mpiga mbio, mpanda farasi hodari, kwa nini wateseka hapa ilhali nyumba na wenyeji wa kukukarimu tupo?! Ondoa kongwa lako, njoo upumzike mahali salama” msichana yule alitumia lugha laini na nyepesi kumshawishi Seidon kwa hila hiyo. Seidon alisahau wosia wa babu yake aliinuka taratibu na kumfuata msichana yule. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Seidon alijikuta katika ukumbi mkubwa wenye harufu nzuri za kuvutia, udi uliozungushwa kila kona ya nyumba hiyo uliijaza kwa moshi, zuria lenye manyoya safi ya sufu, nakshi za kiajemi, matunda ya kila aina yalijaa mezani. Kwa hatua za kujivuta Seidon alitembea juu ya zuria lile akitanguliwa na msichana yule ambaye sasa alikuwa amezifungua nywele zake na urefu wake ulifika kiunoni, akiwa anatembea huku anawasha udi ambao ulikuwa bado kuwashwa, alikuwa akiongea maneno kwa lugha ya Kiajemi, Seidon hakuelewa chochote katika hayo.

    “Unaitwa nani?” Seidon alivunja ukimya kwake baada ya kupaliwa na ule moshi wa udi



    “Sherhazad binti Sahib” alijibu yule msichana.

    “Nyumba hii yote unaishi peke yako?”

    “Ooooh, mpiga mbio, niambie kwanza unaitwa nani.” Badala ya kumpa jibu lake; alimgeukia na kumshika mabegani kabla ya kumuuliza swali hilo.

    “Sei…”

    “Seidon!” yule msichana alimalizia jina hilo kala Seidon hajamaliza. Seidon alijiuliza imekuwa hata akajua jina lake na kulimalizia, “Umejuaje, hata ukamalizia jina langu?”

    “Bwana wangu, Seidon!” Sherhazad alipiga magoti na kubusu kiganja cha Seidon, kisha akainua uso wake kumwangalia Seidon usoni ambapo Seidon, mono mmoja ukiwa kiunoni na mwingine umeshikwa na Sherhazad, “Nilikuona tangu ukitoka Relvesh kupitia njia ya maghalibi, watu wangu walikusindikiza kwa sababu tunajua nini unatakiwa kufanya.”



    Seidon, alitafakari kwa sekunde kadhaa, akakumbuka kuwa alivyokuwa akija hakuona mtu yeyote kumfuata. Aliinua uso wake kutoka kwa Sherhazad na macho yake moja kwa moja yakaangukia ukutani, picha kubwa ya mtu aliyepanda farasi akiwa ameuvuta uta wake kana kwamba analenga mtu au kitu iliupamba ukuta huo na kuyavutia macho ya Seidon.

    “Mimi ni Malkia wa Soria, nilikuwa nakusubiri hapa muda mrefu, nilijua kuwa siku moja utapita tu. Sikiliza, Seidon, nitakupa kila utakacho hata nusu ya tawala yangu iwe chini yako ukinitimizia jambo moja tu.”

    “Jambo gani, Sherhazad?” Seidon aliuliza kwa shauku

    “Nijibu kwanza kama utafanya hivyo nami nitakwambia ni jambo gani.”

    Seidon alitafakari, hakupata jibu ‘majaribu’, alijiwazia, “Naahidi, ee Malkia uliyetukuka kutoka Soria”

    Sherhazad, Malkia wa Soria alitembea taratibu akimuacha nyuma Seidon, moja kwa moja akaelekea kunako ile picha kubwa “Huyu anaitwa Orion, muindaji maarufu kutoka Misri, shabaha yake haina makosa, pigo lake halina huruma. Daima huonekana wazi majira ya mwisho wa mwaka, usiku wa giza nene, usio na mawingu. Kamwe huwezi kupambana nae, kwa maana wengi hata sasa wanasubiri, kwa kuwa wanashindwa kupambana nae. Wewe u peke yako, wenzako wapo jeshi lakini Orion amewadhibiti.



    Bwana wangu, utakapolipata fuvu la Cleopas, niletee hapa nami nitakutimizia ahadi yangu kwani kwa Muungwana ahadi ni deni”, Sherhazad aligeuka na kumtazama Seidon. Seidon alitikisa kichwa kama ishara ya kutokubaliana na Sherhazad, alikumbuka wosia wa babu yake kuwa asitamani wala kulala na mwanamke katika safari yake hiyo. Sherhazad alimsogelea Seidon na kumuwekea mikono yake mabegani, sasa walikuwa wakitazamana, Seidon aliangali chini kwa aibu, Sherhazad akamvutia kwake na kukutanisha kifua chake na cha Seidon, Seidon alihisi kitu ambacho hakuwahi kukihisi kabla katika maisha yake, chuchu zilizochongoka za Sherhazad zilizojaa sawa sawa japo zilifunikwa kwa nguo ya hariri zilimchoma Seidon hata akaishiwa nguvu, alihisi kama ganzi kuanzia kifuani kwake mpaka katika nyayo za miguu yake. Sherhazad alimuweka kichwa chake vizuri na kukutanisha midomo yake na ya Seidon, ulimi wa moto wa Sherhazad ulipenya kinywani mwa Seidon ukazungukazunguka ndani humo na kumpa Seidon ladha ya ajabu, alisahau kila kitu, alisahau kama ana safari ngumu inayomkabili mbele yake, alijikuta mikono yake ikikikamata kwa nguvu kiuno chembamba cha Sherhazad, ikikivuta karibu na chake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Subiri kidogo, mbona una haraka?” Sherhazad, alimwambia Seidon huku akijitoa katika himaya yake, akamuoneshea ishara ya kidole ya kumkatalia jambo hilo, huku akirudi nyuma. Seidon alibaki kumtazama, midomo yake bado ikiwa wazi kiasi, Punjabi alilovaa lilikuwa limetuna kwa mbele chini kidogo ya kitovu likiashiria shughuli, alivuta hatua chache kumfuata Sherhazad ambaye bado alikuwa akirudi kinyumenyume “Timiza nililokuomba utapata vyote” alimwambia Seidon.

    “Nitakutimizia, nitakuletea fuvu hilo siku kama hii na muda kama huu” Seidon alimjibu Sherhazad.

    “Nenda, kakamilishe kazi yako kisha urudi hapa na fuvu, nami nitakutimizia niliyokuahidi hapa hapa” Sherhazad sasa aliongea kwa amri kidogo. Seidon aliinamisha kichwa kama ishara ya heshima kwa msichana huyu ambaye sasa alikuwa ameketi juu ya kiti chake cha enzi, kiti kikubwa kilichowekwa nakshi za dhahabu na kufanya urembo mzuri wa kihindu na kiajemi.

    “Sawa Malkia mtukufu wa Soria” Seidon alivaa kofia yake na kuuweka upanga wake vizuri kiunoni, alirudi kinyumenyume kama hatua saba na kuinamisha kichwa chake tena, akageuka na kuondoka.

    “Seidon!” Sherhazad aliita, Seidon akasimama na kugeuka mzima mzima

    “Malkia!” aliitika

    “Ukikamilisha kazi yako huko Hamunaptra, rudi kwa kupitia njia ya kusini na si Mashariki kama ilivyo kawaida” Sherhazad alimwambia Seidon huku mkononi akiwa na zabibu kadhaa na kurushia kinywani.



    Mwaka 2010

    Chuo Kikuu cha Dar es salaam.



    Wanafunzi wa mwaka wa tatu katika kitengo cha mambo ya kale (ALCHEOLOGY) walikuwa kwenye lecture, katika ukumbi wa Nkurumah. Utulivu ulitawala ukumbini humo, mkufunzi professor Masati alikuwa akieleza juu ya chunguzi zilizowahi kufanya na mchunguzi maarufu wa Kiingereza Bw Paul Smith hasa ile ya Hamunaptra ambayo ilivuta masikio ya watu wengi duniani.

    Maelezo yake kwa vijana hawa yalikuwa ya kina sana kwa akili yao, yaliwagusa kwa namna moja au nyingine hata wakavutiwa siku moja wafanye study tour huko. Wazo ambalo lilikubaliwa na wengi.

    Hata lilipofika mezani kwa Pof. Mkandala, halikuwa na ubishi, liliandikiwa na kupelekwa wizara husika, siku si nyingi lilipitishwa na mipango ya safari hiyo ilianza.

    ***



    Wanafunzi ishirini na wakufunzi watatu walikuwamo katika msafara ndani ya ndege kubwa ya Egypt Air, kuelekea Misri kisha kuchukua usafiri wa merikebu kupitia mto Nile mpaka mji wa Gosheni ambapo kwa usafiri wa ngamia wangefika Hamunaptra kwa mwendo wa masaa 6 jangwani.



    Anna Davis, alikuwa miongoni mwa wanafunzi hao, kila wakati alishtukashtuka hasa alipokumbuka kuwa wanakoelekea ndiko kunakosemekana kuwa kuna makaburi mengi ya kale yenye miujiza ya kutisha, makaburi ya mafarao wa Misri. Hata hamu ya kula ilimwishia kabisa katika safari hiyo.

    Baada ya kukaa ndegeni kama masaa matano hivi, sauti nyororo ya msichana iliyoongea kwa lugha ya kiingereza na kiarabu iliwaashiria kuwa sasa wanapita juu ya anga ambalo chini yake kuna mapiramidi makubwa, mji wa Giza, ambayo duniani kote yanapatikana hapo tu na kuwa historia ya nchi ya Misri ilikuwa hapo katika mapiramidi hayo.

    Anna aliangalia kwa makini majumba yale makubwa yaliyojengwa miaka na miaka yakiwa yamejipanga katika safu za kupendeza.



    Punde si punde walikuwa katika ardhi ya Hosni Mubaraka, ardhi ya Misri, jiji la Cairo, jua liliwachoma kweli kweli lakini uvumilivu ulishika hatamu. Hamu ya kufika kujionea Hamunaptra ilikuwa imezidi mioyoni mwa vijana hawa, walionekana kuchangamka sana. Siku hiyo walipumzika Cairo na kesho yake walianza safari kuelekea mji wa Giza kupitia mto Nile.



    “Hapa si Hamunaptra, lakini hamuwezi kuielewa historia ya Hamunaptra bila kupita hapa Giza” sauti ya kitetemeshi ya mmoja wa wazee waliokuwa wakifanya kazi ya kuongoza na kutembeza watalii katika hayo mapyiramid, alisafisha koo kidogo kwa kujikooza na kuendelea “Na lazima mjue kwamba Hamunaptra ni mji uliopotea miaka mingi iliyopita, ni mji wenye historia kubwa sana duniani, mji huu kiuhalisia upo India na si Misri, ila hapa Giza, kuna piramidi kubwa sana ambalo ndani yake, chini kabisa kuna pango kubwa sana, ukipita ndani yake utatokea Mesopotamia halafu linaendelea kutokea India katika eneo ambalo huo mji ulikuwa umefukiwa na mchaga kwa miaka mingi sana.” Walivuta hatua chache kidogo na kuanza kuyaona kwa karibu na hata kuyashika kwa mikono yao huku wakiuliza maswali mengi.



    Hamunaptra



    Hamunaptra (Mji wa wafu), uligundulika huko India mnamo mwaka 1850, wakati mainjiania wa kiingereza walipokuwa katika kujenga njia ya reli ndipo walipougundua. Mwaka wa 1920 ndipo wataalamu walipofanya kazi ngumu ya uchunguzi, chini ya ardhi walikuta mji mkubwa sana na wenye mambo mengi, ilisemekana kuwa kulikuwa viumbe walioishi huko miaka ya 1900-1700 kabla ya Kristu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mji uliotulia ardhini, ulijulikana hivyo kwa kuwa ulionekana huko, wachunguzi wengi waliojaribu kupita pango hilo walipoteza maisha, wengine kuwa vipofu na wengine walipatwa na hali za ajabu ajabu. Lakini ilisemekana kuwa miaka hii maajabu hayo hayakuwapo tena hivyo wengi waliingia ndani humo na kujionea yaliyokuwamo.



    Karne kadhaa nyuma…



    Wachawi kutoka Misri waliingia ndani ya piramidi hilo kubwa, lengo lao lilikuwa ni kwenda kuchukua fuvu la Cleopas. Walishuka mpaka chini kabisa ya piramidi hilo mpaka kwenye mdomo wa pango kubwa lililopo huko. Huku wakifanya matambiko kwa lugha zao za kichawi, walipita katika pango hilo na katikati yake wakaingia sehemu Fulani na kukuta chumba cha wastani kilichonakshiwa kwa maandishi ya kimisri na kihindu, michoro mbalimbali ilizunguka kuta zake zote. Walisimama bila kutikisika na kutazama mbele kabisa ya chumba hicho cha chini. Mbele hapo kulikuwa na kitu kama jukwaa lenye ngazi ngazi na juu yake kulikuwa na skeleton ya kiumbe Fulani aliyekaa kwa kukunja miguu yake, pembeni kulikuwa na skeletoni zingine nne lakini zilikuwa na maumbo madogo kuliko ile ya katikati, zilionekana kuwa zimemuinamia kama ishara ya heshima kwake. Lakini ile skeleton kubwa haikuwa na kichwa! Cleopas.



    “Wamechukua…” kiongozi wa wale wachawi aliwaeleza wenzake kwa lugha yao ya kichawi. Wengine walibaki midomo wazi. Walipanga kuingia kuchukua kichwa cha Cleopas ili kufanikishia mambo yao ya kichawi lakini hawakulikuta, walijiuliza nani mwenye nguvu za kulichukuwa fuvu hilo, hawakupata jibu kwa kuwa wao walijiona kuwa ndiyo wachawi bora duniani. Walibaki wameduwaa, hata wao walishangaa siku hiyo wakiingia kiulaini sana tofauti na karne za nyuma, walishawahi kufanya jaribio hilo mara kadhaa kizazi hata kizazi lakini hawakufanikiwa kufika hapo.



    Siku chache baadae …



    Wachawi na waganguzi wote wa Misri walikutana kwenye vikao vyao lengo ni kutaka kujua nani kachukua fuvu lile. Baada ya kikao kirefu, na kutumia mbinu zote za kichawi waligundua kuwa fuvu lile limechukuliwa na Waingereza miaka mingi nyuma.

    “Haiwezekani!” Kiongozi wao alisema

    “Watu wa Maghalibi hawawezi kutuzidi maarifa” mwingine aliongeza

    “Haina haja kulumbana, tuangalie tunafanya nini kurejesha fuvu lile mahali pake”



    Baada ya majadiliano marefu walifikia muafaka wa jinsi gani ya kurejesha fuvu lile. Walikubaliana kumtafuta muindaji maarufu wa Misri Orion, ambaye alikuwa ni shujaa katika mambo mengi, mpiga shabaha maarufu duniani mpaka sasa. Baada ya mapigano makali huko kusini mwa London alifanikiwa kulipata fuvu hilo akisaidiwa na uchawi wa Kimisri. Alipolirejesha fuvu hilo liliwekwa ndani ya piramidi kubwa kabisa huko katika mji wa Giza.

    Watu wa makabila ya kiajemi waliijua habari hiyo, hapo ndipo ilipoanza vurugu ya kila kundi kufanya mbinu ya kulipata fuvu hilo. Tatizo lililowakabili ni ubinafsi, kila mmoja alitaka alipate ili ajinufaishe yeye na watu wake. Lakini Klakos ilitaka fuvu lile lilirejeshwe kwa Cleopas na huyo atakayelirejesha ndiye atakayepata neema za Klakos, yeye na watu wake.

    Kazi haikuwa ndogo kwani Orion alidhibiti pande zote nne za dunia watu wasiweze kulipata fuvu hilo, kila aliyejaribu alitoka kapa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vernad alipokutana na Orion, haikuwa kazi ndogo kwake kufanikiwa kulipata fuvu hilo, mapigano yaliyoandamwa na nguvu za nyingi yalitawala katika mji wa chini ya ardhi. Si kwamba Orion alishinda bali alizidiwa maarifa na Vernad wa Relvesh. Wahamsud walifuatilia mapigano hayo toka mbali, wakitaraji kwa kwa vyovyote lazima mmoja ashindwe, hawakuamini waliposhuhudia Vernad akimshinda ujanja Orion na kutoroka na fuvu hilo. Relvesh ilijawa na furaha sana kwa kumpokea shujaa wao huyo akiwa na mkoba mweusi mkononi uliowekwa fuvu hilo la ajabu, walilihifadhi vizuri, wakiwa na nia njema tu ya kulitumia kwa manufaa yao. Lakini hawakujua kuwa pembeni yao kuna wanaowaangalia kwa jicho la husuda.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog