Search This Blog

MZIMU WA WAUFI - 4

 







    Simulizi : Mzimu Wa Waufi

    Sehemu Ya Nne (4)



    Makaburini hapakua mbali sana na nyumbani hivyo safari ya mwendo wa miguu tu ilitosha kuwafikisha katika viwanja hivyo vya makaburi ndani ya muda wa kama nusu saa hivi, na taratibu zote za mazishi zikafanyika na hatimae Kishindo akazikwa, ilikua ni huzuni na vilio kila kona, vijana kwa wazee walishindwa kuzificha huzuni zao na kuangua vilio hukohuko makaburini, hapakua na Jinsi tena maana neon la Mungu limetimia, Wafiwa na ahali zao wakarejea nyumbani baada ya kumalizia dua ya mwisho katika kaburi la Marehemu Kishindo

    *****



    MKOANI SHINYANGA, Kama ilivyo ada nje ya nyumba ya Mzee Kagomba hukusanyika watu wa rika tofauti kwa ajili si tu ya kununua kahawa bali pia kupashana habari zinazojiri ndani na nje ya mkoa wao, na kwa siku hiyo habari iliyochukua ‘Ukurasa wa mbele’ katika kijiwe hicho cha kahawa maarufu kama BBC ni taarifa za matukio yanayoendelea huko jijini Dar katika familia ya swahiba wao Mzee Kikoko, walikua wakizipata habari za matukio yote kupitia kwa wenzao kadhaa walioko huko, na kwakua Kikoko mwenyewe alishapata kuwaeleza kila kilichokua kikimsibu mwanae kupitia Ndoto ya ajabu,

    “Unajua tangu mwanzo sisi tulimuhadhari Bw Kikoko kua hiyo Ndoto ya mwanae si kitu chepesi kiasi hicho na tukamnasihi kua aende kwa Mzee Maguno huenda akasaidiwa ushauri na tafsiri ya Ndoto hiyo ya mwanae lakini Mjuaji Yule akatupuuza..” Mzee Kagomba alikua akizungumza na hadhira ile iliyojikusanya kuizunguka meza yake ndogo ya kahawa, Bahati nzuri siku hiyo mzee Maguno nae alikuwepo kijiweni hapo, akamuwahi kumdakia neno Mzee Kagomba

    “Kwangu asingeweza kuja kwakua mimi naijua vema kesi yao hiyo ya Mizimu ya Waufi”

    “Ni mizimu ya waufi au Dini ya waufi? Maana sisi tulisikia kua ni dini”

    “Hakuna dini ya hivyo hiyo ni mizimu ya huyo mkewe mkubwa, ila katu hawatomuweza Masu japo ni kijana wao wenyewe, mwenzao anasaidiwa na Mizimu kutoka Kigoma kwa babu yake mzaa baba na pia anasaidiwa na mizimu ya umamani kwake Tabora” Maneno haya yalionesha kuwaingia sana watu wote pale, ikawa kimya kimetanda mpaka Mzee Kagoma alipovugumiza swali kwa Mzee Maguno

    “Sasa mnatuchanganya, huko Tabora kwa mama yake gani wakati mama yake ni huyuhuyu Mama Masu wa hapo kwa hayati bwana Masanja, na inakuaje unasema kua hiyo mizimu ya Waufi ni ya mke mkubwa wa Kikoko wakati huyo mke mkubwa ndie mama yake mzazi na huyo Masu?” Mzee Kishindo akacheka kidogo, kisha akajiweka sawa katika kiti chake kirefu cha uvivu kilichofungwa kwa kitambaa cha rangi ya maziwa ili aanze kuwapa somo wadau wa BBC KAHAWA. Lakini kabla hajasema chochote aliwasili motto mkubwa wa Mzee Kangomba anaefanya kazi ofisi za Tanesco, anaitwa Abuu, alipofika akawasilimu

    “Wakubwa Shikamooni”

    “Marahaba..”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Jamani mna habari za mjini huko au mmekaa tu?” Swali hili liliwashtua wanywa kahawa wote na kufanya Mzee Kagoma amjibu manae huyo

    “Habari gani tena mwenzetu?”

    “Mzee Kasimba amefariki huko”

    “We motto!! Kasimba Amefariki?.. Innalillah..”

    “Kasimba ndo nani huyo?” aliuliza Mzee Maguno aliekua ameunika kidogo kwa mshituko kutoka pale katika kiti cha uvivu alichokua amejiegesha

    “Aaah yaani we humjui Kasimba? Sema tu mtu kidole unamjua ukimuona ni shemeji yake na Bwana Kikoko”

    “Aaah nimeshamjua si ni Yule bwana mrefu anapenda kunyoa kipara muda wote pia hua kama mgangamganga hivi?”

    “Naam huyo huyo, na huo uganga ni wa urithi kutoka kwa marehemu babu yao” Watu wote walisikitishwa na taarifa zile, ndipo sasa Mzee Maguno alipomgeukia tena aliezileta habari hizo ambae ni Abuu

    “Enhee, alikua anaumwa? Na amefariki saa ngapi?”

    “Sasa ninyi ndo mnajifanya eti BBC halafu hamna habari nyeti kama hizo, hamna u BBC wowote” Abuu alijibu kwa mzaha huku akimuangalia usoni mzee Maguno ambae alikua kama hamuoni vizuri kutoka na mwanga hafifu wa chemli ndogo iliyopo juu ya meza ya kuuzia kahawa

    “Embu acha upuuzi wako bana, hii ni BBC ndo maana hata wewe umetoka na habari zako huko na kuja kuripoti hapa kitu kikuu cha habari Shinyanga mjini” Watu wote wakacheka kwa pamoja kabla ya Abuu kuanza kuwapa habari zilizozidi kuwaacha vinywa wazi

    “Yule bwana amekufa ghafla, amekutwa katika vile vijumba vyake vya kufanyia mambo yao ya uganga mnaviita ‘Nzu’ Akiwa na jeraha dogo kifuani upande wa kushoto lililotengeneza tobo, Baadae imegundulika kua alinyofolewa moyo kwenye jeraha hilo, na pia amekutwa na alama za vidole na michubuko kama vile alikabwa sana kooni na kukwaruriwa kwa kucha maeneo ya Shingoni” watu walizidi kupigwa na mshangao huku wakimkodolea macho Abuu ili aendelee kuwapa habari,

    “Ebwana eeh, mbaona mauji ya kinyama sana!! Sasa kama hizo alama za kucha na vidole ni za muuaji basi lazima atapatikana kama hakuzitifuta kwa kitambaa, siku hizi teknolojia imekua sana” alisema kijana mmoja aliekua ameketi tu bila ya kinyaji maridhawa cha kahawa

    “Agundulike mara ngapi?” alijibu Abuu na kuwafanya watu wote wamgeukie kumsikiliza nae kwa maringo akajifanya kama hana hamu ya kuwapa habari hizo akaanza kuondoka kuelekea ndani kwao

    “We mtoto kuja hapa, na ukiondoka nitakutolea radhi” Aliongea Mzee Maguno kwa sauti kali lakini ya Mzaha ili kumfanya Abuu arudi, nae karejea

    “Mie siwezi kusimama hapa naongea tu hata kiti hamnipi, wala kahawa hamninunulii wakati nawapa habari nyeti ambazo pamoja na uBBC hamjazipata licha ya kua zimetokea tangu saa sita mchana”

    “Hee tangu saa sita? Kweli dunia sio kijiji tena, hebu kaa kiti hicho hapo kipo wazi”

    “Mninunulie na kahawa kwanza”

    “Hilo tu? Sema jingine, kama kahawa inalewesha basi leo utaema kushoto kasha utafukia kulia, utakunya TANI yako” Alijibu tena Mzee Magunokwa mshawasha wa hali ya juu, hakika zilikua ni habari tamu na za majonzi kwa upande wa pili,

    “Hizi habari bado ni siri, mie ninawadokeza tu kwakua nilizipata kutokea kwa chanzo changu cha habari ndani ya kitengo muhimu na nyeti sana, hivyo muwe makini kuzisemasema kwa sasa, mkikamatwa mie simo”

    “Tupe ufyetere huo kaka mkubwa” alijibu kijana mwininge aliekua ametulia akisikiliza kwa usongo

    “Baada ya maiti kufikishwa hapo katika Hospitali ya ‘Gavumenti’ vipimo vikafanyika ambapo walizichunguzo hizo alama za vidole mnaziita sijui fingaprint” Watu wote walikua kimya wakimsikiliza, akachukua kikombe kidogo cha kahawa alichokua tayari ameshamiminiwa na baba yake Mzee Kagomba ambae muda wote alikua kimya akisikiliza kisa hicho kipya

    “Alama za vidole zilizopo katika mwili wa marehemu zimegundulika kua na za mtu mmoja anaitwa Kishindo Rehani”

    “NINI?? Kishindo rehani huyu wa Dar?” aliliza kwa mshangao Mzee Kagomba

    “Huyo huyo aliekufa majuzi kwa kupigwa na Radi na kuzikwa juzi”

    “Mtoto acha maskhara tafadhali”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sio wewe tu, hata uongozi wa usalama na jopo la madaktari wote hawaamini kilichoonekana kwenye vipimo vyao wenyewe na ndomaana wameamua kuifanya siri kwanza”

    “Sasa nimepata majibu kamili, vita ya mizimu imeanza” alidakia tena mzee Maguno ambae ni gwiji wa Nujumi(Masuala ya Nyota) na Tafsiri za Ndoto, Kauli hiyo sasa ikawafanya watu wote pale wapate kiu ya kusikiliza hiyo vita, nae Mzee Maguno hakusubiri kuambiwa aendelee ‘kumwaga mchele’

    “Iko hivi siku yoyote ukikuta mtu ameuawa kisha ametobolewa sehemu ya kifuani wakaunyofoa Moyo wake ujue huyo mtu ni Mchawi au anahusishwa na Uchawi…” Akavuta kikombe chake cha kahawa kisha akaendelea “..Iko hivi wachawi wote duniani hua wana kitu mfano wa Fitra kinakua ndani ya moyo wa kila mmoja wao na hicho ndo uchawi wenyewe hasa, na kinamtambulisha kwa wachawi wenzie popote atakapokwenda hata kama ni nje ya nchi, pia kazi ya kijidubwasha hicho ni kumuamsha huyo mchawi kila ifikapo usiku wa manane kwa ajili ya kujumuika na wenzake katika shughuli zao za kichawi, ndomaana mchawi yoyote hata kama awe amechoka vipi ikifika muda wa kwenda kuwanga usiku lazima atashituka tu, sasa huyo Bw Kasimba anahusika kikamilifu katika hii kadhia ya huo mzmu wa Waufi akisaidiana na dada yake ambae ni mke wa Kikoko, sasa itakua nguvu ya Mizimu ya WASWEZI ya huko Tabora umamani kwa Masu na nguvu nyingine ya mzimu ya WALUWA kutoka Kigoma na Kongo kwenye asili ya

    ubabani kwa Masu imeanza kumsaidia mtumishi wan a kijana wao ndomaana katolewa moyo ila ngoja tuvute subra tutayasikia mengi tu..” Maneno hayo ya Mzee Maguno yaliwaogopesha wengi pale kijiweni na pia yalizidi kuacha maswali mengi hata kwa mtu mzima Kagomba pia ambae alishindwa kujizuia na kuendelea na maswali yake ya kidadisi na kichokonozi

    “Sasa kwani mama yake na Masu sio huyu tumjuaye sisi? Na ni yeye anaemroga Masu? Na kwanini sasa vipimo vioneshe kua muuaji alikua ni marehem Kishindo ambae sio Masu anaeteswa kama ni kweli” Baada ya swali hilo kila mmoja alimgeukia Mzee Maguno kusikia jibu ambalo bila shaka lilikua likimkwaza kila mmoja pale

    “.. Jibu ni jepesi sana, Ni hivi Ya Ngoswe mwachie Ngoswe, nay a Kaisari..??” alijibu kimkatao tu Mzee Maguno

    *****



    NDANI ya Nbs, Basi lifanyalo safari zake toka Dar es Salaam kwenda Shinyanga, seat za katikati walikua wameketi Sheikh Jabu na Mama Masu, na safari yao hii ilikua ni kuelekea Shinyanga msibani, tayari taarifa za kushtua za msiba huo ziliwafikia tangu jana yake hivyo ikabidi tu sasa wapange safari ya kurudi Shinyanga ili wajaribu kuwahi mazishi, ndani ya gari sura zao zilikua zimesawajika kwa matatizo makubwa yanayoendelea kujitokeza, Matatizo ambayo hakika ni mitihani mikubwa kwa familia yoyote ikikubwa, Raha na amani ilianza kufifia tangu ilipoanza ile Ndoto ya ajabu aliyokua akiiota Masu, Ndoto hiyo ikapelekea Mzee Kikoko akapigana na marehem Kishindo akimtuhumu kumfitinisha na mwanae, Ndipo Mzee Kikoko akacharazwa na mkia wa taa, Mara Kikoko akazidi kugombana na Mkwe wake kwa Masu akimtuhumu kumroga mwanae na kumtorosha pale nyumbani, Kesi ya Kikoko ikiwa tayari chini ya mikono ya Polisi mara Kishindo akafa kwa kupigwa na radi akiwa safarini,

    ikagundulika kwamba katika Safari hiyo iliyomtunukia kifo Mzee Kishindo kumbe alikua na Masu, Cha ajabu baada ya tukio hilo la ajali ya Radi ane akapotea ghafla huko msituni, mara msibani mke wa marehemu kapandisha majini akidai kua mumewe katekwa na Waufi, mara mtoto wa Masu anasema Yule Ng’ombe aliebebwa na Kimbunga ndie alikua baba yake, Basi ni songombingo kila kukicha, na sasa Bw Kasimba kaka yake na Mama Masu nae ameuawa kinyama sana kwa kunyofolewa moyo, mawazo yalionekana kumzidia mama Masu aliekua akitiririsha machozi mashavuni mwake kila nukta.. Maziko yalikua yamepangwa kufanyika siku hiyohiyo kutokana na hali ya mwili wa marehemu lakini ikabidi muda waupeleke mbele kidogo mpaka saa kumi alasiri ili kujaribu kuwavutia muda Mama Masu na Sheikh jabu ambao walikua wameshatoa taarifa kua wapo njiani wanakwenda,, Na kwa taarifa za kimawasiliano kutoka kwa Mzee Kikoko alieko hospitalini Dodoma na swahiba wake wa karibu sana Sheikh Jabu

    zilidhihirisha kua hali yake haikua mbaya sana hivyo aliahidi kua yeye angelihudhurua huko msibani keshokutwa baada ya kupata ruhusa pale Hospital kwahiyo akawa amemridhia Sheikh jabu akamuwakilishe huko msibani kwa Shemeji yakeCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****

    Koplo Sebastian Bangirana kutoka kituo cha polisi cha wilaya ya Shinyanga kilichopo jirani na mahakama alishawasili pale msibani kwa ajili ya mahojiano na wanafamilia kama mpelelezi wa kesi ile, aliingia pale msibani akiwa amevalia sare zake za kazi zilizomkaa vizuri maungoni ukijumlisha na ule mwili wake uliojengeka kimazoezi basi alionekana ni kamanda kwelikweli, alienda mpaka pale jamvi walipokaa wafiwa, akavua viatu kiustaarabu na utulivu kisha akajisogeza karibu nao, alipofika pale kila mtu alikua makini kumpokea afande huyo, akavua miwani yake ya macho halafu akawasalimia salam kwa lafudhi iliyodhihirisha kua hakua muumini wa dini husika

    “Saramaleku”

    “Waaleykum salam..” Walimuitikia wazee hao huku wakimkaribisha “Karibu sana Afande..”

    “Ok ahsanteni jamani, Poleni sana na matatizo”

    “Aaah bado hatujapoa, ila ndo kazi ya Mungu haina makosa”

    “Mimi ni Ofisa wa Polisi kutoka kituo cha kati, naitwa Sebastian Bangirana unaweza kuokoa nguvu na muda kwa kuniita ‘BANGI’..” Wazee wote waliangaliana halafu wakaachia tabasam hafifu kusikia mtu najiita Bangi japokua ilikua ni kifupi cha jina lake, baada ya utambulisho huo Sajent BANGI akaendelea

    “Naweza kumpata kiongozi wa familia kwa ajili ya mazungumzo kidogo?” Mzee Maguno na Mzee Kagomba nao walikua wamejilaza hapo jamvini wakisikiliza mazungumzo hayo

    “Kiongozi wa familia ndo huyo aliefariki, ila mimi nipo kwa niaba yake”

    “Ok hata wewe utanifaa tu, tunaweza kusogea pembeni kidogo kwa mazungumzo kiasi?”

    “Haina shaka Afande” alijibu Bwana huyo aliejitambulisha kua ni kwa niaba ya familia, wakainuka na kusogea mbele kidogo ya nyumba ili wawe huru kuzungumza kuhusiana na tukio hilo la mauaji, inaonekana Mzee Kagomba hakupenda jambo lile la Afande kutaka mazungumzo yake yawe faragha, bila shaka alitaka ‘kunyonya’ umbea wa kwenda kuuongea jioni maeneo ya ‘BBC’



    “Poleni sana kwa msiba mzito sana kwenu” alianza Afande Bangi baada ya kusogea pembeni

    “Ahsante Afande”

    “Umesema wewe ni nani hapa?”

    “Mimi ni Katembo Masanja, mdogowake na marehem Kasimba Masinja”

    “Ohh kumbe we ni mdogo wa marehem, mmh mbona majina yenu ni ya aina moja? Katembo. Kasima?” Swali la Inspekta Bangi lilimfanya Bw Katembo akaachia tabasamu la mbali kisha akajibu

    “Marehemu baba yetu alikua ni kiongozi mkubwa sana katika kabila lao, na pia alikua ni mganga mashuhuri sana hivyo maisha yake ikiwa pamoja na hili la kutoa majina kwa baadhi ya wanae lilijikita kiimani na kimila zaidi”

    “Safi sana wazee wetu walikua wakizienzi sana tamaduni zetu, sasa hebu niambie ilikuaje wakati marehemu anafariki?”

    “Mimi binafsi sikuwepo hapa nyumbani, mimi hua naishi sehemu nyingine huko nimepanga hivyo nilipigiwa simu na mama Salum kua kaka amefariki ndipo nikaja haraka nyumbani”

    “Huyo mama Salum ni nani?”

    “Ni Mke wa Marehemu”

    “Unamjua Mzee Kishindo?”

    “Sijawahi kumuona ila namfahamu tu kwa jina kwa kua ni rafiki wa Shemeji yetu, mume wa dada yetu, nae nilisikia kua amefariki kwa kupigwa na Radi na muda huo alikua na mtoto wa dada yetu huyo anaeitwa Masu ambae nae tangu tukio hilo alitoweka ghafla”

    “Huyo shemeji yako ndo Mzee Kikoko?”

    “Ndio huyo”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kikoko amekua Bidhaa adimu sana mikononi mwa Polisi”

    “Kwanini Afande?”

    “Ahh tuacheni nae, kwa ukaribu wako na marehemu Je kuna mtu yoyote alikua anadaina nae au alikua na ugomvi nae?”

    “Hapana sijawahi kusikia maana watu wengi walikua wakimuheshimu sana kutokana na uganga wake, amewasaidia wengi sana”

    “Kwahiyo Kikoko yuko wapi?”

    “Nasikia alikua anaumwa ila yuko njiani anakuja msibani” Baada ya mahojiano ya muda mfupi, Sajent Bangi alitaka kuonana na mke wa marehemu lakini ilishindikana kwa wakati ule maana hali ya mke huyo ilikua mbaya sana kutokana na kifo cha mumewe basi Sajent Bangi akamuaga Bw Katembo na kumuahidi kua takuja mazishini, ila akamsisitiza kua asimuambie Mzee Kikoko kua aliuliziwa na Polisi, kisha Sajent akaondoka zake

    *****



    Ndani ya chumba kidogo, walikuwemo watu kama watano hivi wamesimama huku wakiwa wameizunguka maiti iliyomo ndani ya Sanda, walikua wakijadili kuhusu utaratibu wa kumzika maiti huyu, kulikua na mabishano ya namna bora ya kuyafanya maziko hayo

    “Hapana, hiyo ni hatari zaidi, kwasasa hatuna muda wa kupoteza ni kumzika tu kama hajafa vizuri basi atamalizikia humu humu kaburini” alisema mzee mmoja wa makamo

    “Tutakua hatujafanya kitu, mie nadhani huyu kijana atakua ameshajifunza kua nguvu yetu ni kubwa kiasi gani na atakubali tu kujiunga na kutoa kafara ya mwanae mmoja” alijibu mmoja kati ya wale watu mule ndani

    “Acheni mawazo yasiyowezekana, huyu azikwe tu tena sasa hivi tumalize huu udhia vinginevyo tutazidiwa nguvu halafu tutaangamia wote, kaeni mkijua kua mizimu ya kwao huko Tabora imeanza mapambano nasi huku ikisaidiwa na mizmu ya Kigoma kwa Mzee Kikoko kwahiyo nguvu yao ni kubwa sana, hebu fikirieni kua wameweza kumuua Kiongozi mkubwa wa ‘Nzu’ ya Waufi bwana Kasimba, hivyo kama tutamkosa huyu kijana basi mjue Mizimu hiyo itatumalizia na sisi pia mkumbuke tuna deni la damu yakara kutoka kwa wakuu wetu wa Waufi, Mizimu inataka damu ya kafara hivyo tutaambiwa tumtoe mama yake mzazi ambae ni mtiifu kwa mzimu itakua ngumu sana,” alijibu kijana mmoja aliekua amejifunga kitambaa Chekundu kichwani, alikua ni kijana mrefu kiasi, ana sura ya kikatili sana inayosababishwa na Jicho lake bovu, huyu ni Hunudu



    Katikati ya Sanda hiyo alikua maevingirishwa na kufungwa kama Pipi kijana Masumbuko Kikoko tayari kwa ajili ya kwenda kuzikwa akiwa hai, japo alikua hai lakini alikua ni nusu mfu maana hakua na uwezo wa kusema lolote wala hata kutikisika mithili ya mtu aliechomwa sindano ya nusu kaputi, alichokua anaweza kufanya ni kufumbua macho na kusilia tu, bali vingine vyote havikua tena kwenye mamlaka yake, alijitahidi kuwajibu wale mabwana kutoka katika Mizimu ya Waufi lakini mdomo ulikua mzito kama mtu aliyechomwa sindano ya ganzi wakati wa kung’oa jino, alipojirabu kujitikisa japo kidogo ilikua ni zoezi gumu sana kwake ikabidi atulie tu aendelee kusikilia majadiliano ya kikatili sana dhidi yake, kilichomshtua zaidi pale aliposikia kua mama yake ni mtiifi sana kwa Mizimu yao hivyo hapaswi kuuawa zaidi yake yeye ndipo akaanza kukumbuka maneno ya Marehemu Kishindo kua mama yake alisaidiwa na Mizimu kuinyakua mimba ya mke mwenzie na kuiamishia kwake kwa njia ya

    nguvu za giza, akiwa anavuta picha aliwasikia watu wale waliosimama huku wakiwa wamemzunguka wakiafikiana kua akazikwe tu kufuatia Ushauri uliotolewa na Hunudu, Masu alipata uchungu sana kuona sasa anaenda kuzikwa akiwa hai, kajikaza na kutoa sauti kali ya kuashiria kua wasimuue lakini sauti haikutoka hata kidogo..

    “Kaburi mlichimbia wapi?” akauliza Hunudu

    “Hapo kwenye shamba la midizi”

    “Mna uhakika ni refu?”

    “Ndio, zaidi ya futi tisa”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Vizuri, haya mnyanyueni huko twende haraka haraka kabla hakujapambazuka” Masu alikua katika wakati mgumu akijaribu kuipigania nafsi yake bila ya uwezo wowote, akaona ananyanyuliwa juu kutokea pale chini alipokua amelazwa, GHAFLA Masu akajishangaa anapata nguvu na ujasiri wa ajabu akapiga KELELE Kali sana, akaijikua anafumbua macho na kujigundua kumbe alikua usingizini anaota, alijitikisa kichwa ili aone kama yuko sawa, taarifa kutoka katika ubongo wake ikazidi kumthibitishia kua alikua akiota tu, lakini kumbukumbu zake za mwisho anakumbuka alivyosombwa na Kimbunga kikali sana kikampeleka masafa marefu kwenda juu na hakujua mwisho wake, akainuka pale juu ya kitanda kidogo cha chuma, akasimama na kuanza kuangaza huku na kule ndipo akamuona Mzee mmoja akiwa amesimama karibu ya kitanda hicho, alijaribu kumuangalia vizuri na baadae sura ikaanza kumuijia japo hakuweza kwa haraka kutambua alimuona wapi mzee huyu

    “Pole sana Masu, hila za Hunudu sasa zinafikia tamati, hawezi kukuzika mshenzi huyo, Sisi tunapambana na waliomtuma, acha yeye ajidanganye tu” Maneno haya yalizidi kumpa maswali zaidi Masu kua hapa yupo wapi na huyu ni nani hasa, lakini baada ya Masu kumtazama Mzee huyu kwa utulivu alimkumbuka aliwahi kumuona siku moja Shinyanga, tena ilikua ni nyumbani kwa Kikoko, na alipozidi kuvuta fikra vizueri alipata jibu kua ni Babu yake na mke mdogo wa Kikoko ambae yeye anamuita Ma’mdogo japo kwa sasa ameshaanza kugundua kua ndie aliekua mama yake stahiki kabisa, pia Masu anajua kua mzee huyu hua anishi Kipalapala, Tabora, sasa hapa ni wapi? Na kama ni kipalapala amefikaje? Maswali hayo alikua akijuliza mwenyewe kichwani lakini cha ajabu Mzee huyu alianza kuyajibu utadhani alikua akiyaona yakipita kichwani mwake

    “Ni kweli mimi na Babu yake na mama yako mdogo ambae ndio mama yako hasa, na hapa ni Kipala pala Tabora, umeletwa kwa nguvu za mizimu ya WASWEZI iliyokuijia huko Dar ulipokua umegeuzwa Ng’ombe na Hunudu akawa amejiandaa kukuchinja, kile Kimbunga ilikua ni Waswezi na Walua wamekuijia, uje nyumbani kwenu uitambue asili yako na mizimu ya kwenu, pia ufanyiwe Tambiko la zindo kubwa kwa Mshenzi yoyote atakae jaribu kukusumbua tena, Kisha sasa ndo tutaanza kazi ya kuwamaliza hao Waufi”

    *****





    MUDA wa mazishi ukawadia, tayari nyumba ilikua imezungukwa na waombolezaji, wake kwa waume, lakini mpaka muda huo unatimu Basi lililowabeba Sheikh Jabu na na Mama Masu lilikua halijawasili Shinyanga mjini hivyo suala la kwenda kuzika likawa halina budi kutendeka bila ya kuwasubiri walioko njiani, Baada ya kukamilika kwa Ibada maalum ya dua kwa marehemu na swala ya MAITI sasa wanaume walikua wamelinyanyua Jeneza tayari kwenda makabuburini kuitimiza faradhi ya kuuhifadhi mwili, wakati kundi la wanaume likizidi kutokomea makaburini Tax ikasimama mbele ya nyumba ya marehemu kisha akashuka Sheikh Jabu huku akifuatiwa na kilio cha hamaki kutoka kwa Mama Masu ikabidi Ndugu waliobaki wasimame kusaidiana kuwapokea na kumtoa ndani ya Tax Mama Masu ambae hakua na nguvu kabisa, Kwa kuzingatia taratibu za misiba ya kiislam ni kwamba wanawake hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika hivyo hapo ndio ikawa mwisho wa mama Masu lakini Sheikh jabu akaongea na dereva wa Tax

    ile iliyowapeleka hapo nyumbani ili imuwahishe huko malaloni, cha ajabu Mama Masu alikua kama aliechanganyikiwa baada ya kukuta tayari maiti haipo tena, akawa analia sana huku nae aking’ang’ania nae aende makaburini, jambo hilo liliwashangaza wengi na kuacha maswali yasiyo na majibu juu ya taharuki hiyo ya bi mkubwa huyu,. Kina mama watu wazima ambao walikua wamesogea kuwapokea wakamzuia na kumuingiza ndani huku wakimuacha Sheikh Jabu akiingia ndani ya Tax tayari kwenda makaburini, kwakua Sheikh Jabu hakua mwenyeji sana wa Shinyanga hivyo ikabidi aondoke na kijana mmoja pale nyumbani ambae hakwenda makaburini ili awe kama muongazaji wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Haikuchukua muda mrefu kwa mbali Sheikh Jabu aliuona msafara wa watu wakiwa wamebeba jeneza, walipowakaribia akamuamuru dereva asimamishe gari, akamlipa pesa zake kisha yeye na kijana aliekwenda nae wakateremka na kuungana na wenzao kwenda mazikoni. Haikua kitambo kikubwa tokea pale walipowakuta mpaka yalipo makaburi hivyo waliwasili katika viwanja vya makaburi, na baada ya dua kadhaa za mwisho zoezi likaanza la kumuhifadhi mzee Kasimba, na hapo ndo ukawa mwisho wake wa safari hii ya Dunia

    *****



    Nje ya nyumba waliyomtoa marehemu kulikua kimya kabisa kwakua wanaume walikua bado hawajarudi kutokea makaburini, na wanawake wengi walikua wamekaa uani, Sebuleni walikua wameketi watu wawili waliokua katikati ya mazungumzo mazito, alikua ni dada wa marehemu ambae ni Mama Masu alieketi katika kochi dogo la kukaa mtu mmoja, huku upande wake wa kushoto alikua ameketi Koplo Bangi huku shingo yake akiwa ameilaza kiupande hivi ili apate kumuangalia vizuri bi Mkubwa aliekua akimsaili, wakiwa katikati ya Mazungumzo ndipo wanaume nao walikua wakirejea kutokea huko malaloni, ikabidi Inspekta asitishe kidogo mazungumzo kutokana na watu kuzidi kuwasili mahala pale,

    “Huyo Sheikh Jabu ndo yuko wapi hapo?” alisaili Koplo Bangi huku akimuelekea Mama Masu ambae muda huo alikua akijaribu kuinua kichwa chake huku akiangalie kwa nje ya nyumba ile kama atamuona anaetafutwa,

    “Huyo hapo alievaa kofia ya kufumwa kwa mkono”

    “Naona wenye kofia hizo kama watatu hapo.. ni yupi sasa hapo?”

    “Huyo mwenye ndevu kama nyekundu hivi,, hua anazipaka hina” Baada ya maelekezo hayo sasa Inspekta aliweza kumtambua vilivyo mtu mzima Yule na hapo hapo akamuagizia kijana amuite ndani, na baada ya kuwasili sebuleni pale alijumuika nao katika amzungumzo yale

    “Karibu sana Mzee..” alianza Koplo Bangi kumkaribisha sheikh jabu

    “Ahsante sana”

    “Poleni na msiba”

    “Aah kazi ya mola haina makosa”

    “Vipi mbona mlichelewa sana kuingia Shinyanga?” Koplo alitupia swali la kwanza la mtego

    “Nadhani tungewahi kufika kama kama isingekua hitilafu za lile basi njiani..”

    “Oooh poleni kumbe basi liliwapa tabu, na vipi Mzee Kikoko mmemuacha wapi?” Sasa swali hili lilimshtua kidogo Sheikh Jabu, hakutegea kuulizwa vile maana bila shaka kama huyu anae muuliza ni mwanafamilia pale au ni jirani wa karibu atakua anajua tu kua Kikoko anaumwa nab ado yuko Dodoma

    “Kwanza samahani, umeanza tu kunisaili bila ya kujitambulisha..”

    “Ooh bila ya samahani mzee, mimi naitwa Koplo Sebastian Bangilana, unaweza kuniita Koplo Bangi,”

    “Sasa kwani Bi Mkubwa hapo hajakueleza juu ya alipo mumewe mpaka ukanihoji mimi?”

    “Sio vibaya nikisikia pia kutoka kwako”

    “Mwenye Jukumu la kujibu wapi alipo Bwana Kikoko ni mkewe na si mimi”

    “Iko hivi Mzee, mimi hapa niko kazini na nimechagua kuhojiana nanyi mahala hapa kwa wema wangu tu kutokana na hali yenyewe ya msiba ila kwa sasa mlipaswa nyote muwe chni ya ulinzi huku mkinijibia maswali yangu katika viti vya mbao ofisini kwangu, hivyo naomba Ihsani yangu isiwe Nuksani, nitabadili mfumo wa mahojiano sasa hivi, umenieelewa?” Koplo Bangi alibadilika mara moja na kua kama pilipili, Macho ya Sheikh Jabu yakagongana nay a Mama Masu, kisha akarudi kumtazama tena Inspekta halafu akakohoa kidogo ndipo akaendelea

    “Kuna kitu sijakuelewa, yaani sisi tulipaswa kua chini ya ulinzi? Kwa kosa gani hasa?”

    “Kwa kumficha Mzee Kikoko ambae ni mtuhumiwa namba moja wa mauaji haya yote yanayoendelea”



    MWANAUME Mrefu aliejazia mwili wake kimazoezi alikua akirandaranda kwa kwenda mbele hatua kadhaa na kurudi nyuma huku kichwa chake akiwa amekiinamisha chini, mikono yake miwili akiwa ameipa hifadhi katika mifuko ya suruali yake ya kijivu, akiwa anendelea na zoezi hilo la hiari ndipo ghafla alisitisha zoezi lake hilo baada ya kumuona Dokta Nyango ambae ni mganga mkuu katika Hospitali hiyo ya Kitete ambapo mwanaume huyo alikua akirandaranda katika korido zake,

    “Habari yako..” Dk alimsabahi mwanaume huyo

    “Salama tu Dk, pole na majukumu”

    “Aah ahsante, najua u-mgeni wangu karibu ofisini”

    “Ahsante sana Dk” Baada ya salamu waliongozana mpaka katika Ofisi ya dokta huyo ambayo haikua mbali na hapo alipokua akitalii mwanaume huyo, kisha wakaingia ndani

    “Karibu uketi hapo..“

    “Ahsante.. Naitwa Sajent James Marumbo kutoka kituo cha polisi kati, tumepokea taarifa za wito wako hivyo ikanibidi nije haraka haraka” Sajenti Marumbo alianza kwa kujitambulisha baada ya kuketi huku akihangaika kuingiza mkono katika mfuko wa suruali yake ambako alitoa kitambulisho chake cha kazi kwa lengo la kumuonesha Dk

    “Oooh No, hakuna haja ya kitambulisho, ninakufahamu vizuri tu” Dk Nyango alivua miwani yake ya macho akaiweka juu ya meza yake kisha akaanza kujipikicha macho kabla hajainua tena uso wake na kumtulizia macho yake Sajent Marumbo kwa sekunde kadhaa kabla ya kumtupia swali la uchokonozi

    “Mlileta maiti hapa, Sio?”

    “Yeah”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mliitoa wapi maiti hiyo?”

    “Aahh tulikua na operesheni yetu maalum maeneo ya kipalala, kuna mtuhumiwa wa mauaji tulienda kumkamata, sasa tukiwa eneo la tukio ndipo tukamkuta huyo dada akiwa amelala katika Dimbwi la damu lililotokana na kupigwa na upanga kichwani, na bahati nzuri tukamkuta Mwanaume mmoja akiwa na Panga hilo mkononi na tulipomuhoji..” Kabla hajamalizia hadithi yake akatizwa na sauti ya utulivu kutoka kwa Tabibu huyu

    “Sina haja ya kufika huko kote. Nilitaka tu kufahamu mlijuaje kua amekufa wakati hamkua na mtaalamu yeyote huko”

    “Dk kuna vitu vingine vinaonekana hata kwa macho tu, Dada alikua amepoteza maisha” Wakati mtaalamu huyu wa upelelezi akibwabwaja maneno yake huku akitupa mikono yale huku na kule kama ishara ya kuonesha msisitizo kwa hicho anachokiongea lakini hiyo ilizidi kumfanya sasa huyu Mtaalmu wa Afya atikise kichwa chake kabla hajaaendelea kuzungumza

    ‘”Ok, Ok, nimekuelewa.. Sasa iko hivi naomba nikushauri kijana wangu jambo moja la msingi sana..” akaweka nukta ndogo ili aruhusu mwayo uliokua jirani na koromeo lake kisha akaendelea “..Ninyi ni wataalamu wa masuala ya upelelezi, walinzi wa raia na mali zake, sasa haipenzi kabisa kwa namna yoyote ile kuingilia taaluma zisizokua zenu..” Akaweka tena nukta ndogo huku akiupikicha uso wake katikati ya viganja vyake vipana vya mikono, Sajenti Marumbo akataka kuongea lakini hapohapo akakatishwa na Sauti ya Dokta iliyoendelea tena kutoa maelezo amabyo afande huyu alihisi kutokuyaelewa “..Mmemleta Yule dada hapa huku mkishinikiza kua awekwe mochwari, bila ya kujali taratibu za kitabibu zilizopo hapa, na hata pale mlipopewa taratibu zeti mlizidi kuelekeza kwa kukaripia wataalamu, Sasa iko hivi huyo dada wala hakupoteza maisha kama unavyosema bali alipoteza kitu kingine kabisa, Fahamu tu”

    “Ama!” Sajent Marumbo ambae alikua na uhakika kabisa kua dada Yule alikua amefariki alishituka wazi wazi huku akipepesa macho yake kwa kauli ile ya Dokta

    “Ndo hivyo, na mpaka sasa tunaendelea na jitihada zetu za kupambana na hali hiyo mbaya ya mgonjwa maana mpaka sasa hajarejewa na fahamu, sasa Je vipi kama tungemuweka kwenye barafu si ndo tungekua tumemmalizia kabisa?? Na Je vipi kama tutawashitaki kwa kutaka kummalizia mgonjwa aliekua mahututi kwa kuwashinikiza wataalamu wetu wamuhifadhi mochwari?” Sajent alizidi kupagaishwa na majibu haya maana kwa jinsi alivyomuona Yule dada pale kituoni wakati anafikishwa alikua ameshakufa, sasa ghafla vipimo vinadai kua Yule dada ni Mgonjwa tu, hakua na jinsi tena ya kuyakataa majibu ya Dokta, bali ni kuyapokea na kuomba radhi kwa niaba ya wenzake

    “Ok dokta nimekuelewa, naomba tu radhi kwa kilichotokea kwakua ni kutokujua kwetu lakini hapakua na nia mbaya yoyote, sasa Je tunaweza kwenda kumuona japo kidogo?”

    “Ooh yes, why not?(Kwanini ishindikane, tunaweza tu) ila tu muwe makini muda mwingine” waliinuka na kuongozana mpaka wodini ambako Nyamizi alikua amelazwa, hali yake haikua mbaya sana ukllinganisha na jinsi alivyokua hapo awali, japo hata kufikia muda huo alikua bado hajarejewa na fahamu zake..



    Baada ya Sajent kujiridhisha na hali hiyo ya mgonjwa akabidi kumuaga Dk na kisha akarejea mpaka kituoni ambako alifanya mazungumzo na mkuu wa kituo kwa kina juu ya tukio hilo na taratibu za kawaida zikaendelea kama kawaida huku wakisubiria hali ya mgonjwa itakavyokua, Lakini kutokana na kesi hiyo kua na mlolongo mrefu ambao umepelekea mpaka hata Masu kutokuwepo pale ikabidi sasa wampigie simu mpelezi wa kesi ya kule Shinyanga Koplo Bangirana ili nae wampe taarifa za mabadiliko ya habari za mwanzo kua dada aliekutwa amekatwa na Panga kichwani amefariki, na kwakua Sajenti Marumbo alipata kuwasiliana na Koplo Bangi mwanzoni mwa kesi hiyo hivyo alikua na kumbukumbu ya namba za Koplo Bangi hivyo ilikua ni kazi rahisi tu kumpata kwa namba yake binafsi

    *****



    TAARIFA za hali ya Nyamizi huko kitete zilizidi kumpa hamasa na matumaini Koplo Seba ya kujaribu kuifuatilia vizuri kesi hiyo, ikabidi sasa azidishe ukaribu na Sajent Marumbo kwa ajili ya kua anapata habari zote muhimu kutoka huko, akili yake alikua imeshagoma kuamini kua kina Masu ni wauaji kweli kutoka na utata unaoendelea kuigubika kesi hiyo, Lakini hakumuambia chochote mkuu wake wa kazi akihofia kuzidi kujichanganya kutokana na vitisho anavozidi kupewa, na kwakua jioni ilikua imeshaanza kutanda akaamua kuiacha kipolo kesi hiyo mpaka kesho yake ndipo ajue la kufanya

    *****



    USIKU WA MANANE,



    Usiku wenye kiza kinene,

    Chini ya Mbuyu mkubwa ulipo katika moja ya Shamba kubwa laukoo wa marehemu kasimba walikua wamekusanyika watu zaidi ya Hamsini hivi, wote wakiwa wamevaa nguo nyeupe vichwani wamejifunga vitambaa vyeusi kiasi kwamba kama ungetokea ghafla ungeweza kuwajua tu maana nguo nyeupe katika giza huonekana kiurahisi sana, wote walikua wamekaa chini huku wakionekana kua katika kina cha mazungumzo mazito, Kila aliekua akipata fursa ya kuongea alisimama juu na kuongea kwa hisia kali, Ulikua ni mkutano wa dharurawa wafuasi wa Mzimu wa Waufi..

    Aliekua akiongea wakati huo alikua ni Bazazi asiekua na huruma, kijana mwenye jicho moja, Hunudu!

    “Jamani binafsi nataka kusema jambo moja tu, naomba mniskilize vizuri..” akaweka kituo kidogo, akakohoa kisha akendelea “..Hii vita imeshakua kubwa sana japo mnaweza kudhani kama vile imekwisha Laa hasha iVita ndo kwanza inaanza, Japokua tumewatengenezea kesi ya mauaji lakini bado tunakibarua kigumu kulitimiza hilo, ukweli ni kwamba Yule Dada hakufa bali alipoteza tu fahamu na nilishindwa kummalizia kwa kua hali ilikwishavurugika pale..”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “NINI??” Hunudu alikatizwa na sauti ya mshangao iliyotokea usawa wa chini kwa hawa waliokaa ikionesha kushangazwa na taarifa ile ya Hunudu, huyu aliyeshangaa alikua ni Afande Ngulinzila, mfuasi mwingine wa Waufi Lakini alikatishwa kuongea na sauti kavu ya mzee mmoja alieonekana kua kama kiongozi wao pale

    “Kaa kimya binti,hujui taratibu zetu wewe? huu muda anongea mtu mwingine..” Baada ya Mzee Yule kumkaripia Afande Ngulinzila sasa Hunudu hakusubiri kuambiwe aendelee

    “Zimebaki siku saba tu za kuhakikisha Masu anajiunga na waufi au tunamuondoa duniani, vinginevyo zikipita siku saba kama hatujaitekeleza amri hiyo basi mkumbuke kua Mzimu unataka tumtoe kafara mama Masu mwenyewe kwakua ndie alieingia makubaliano na Mzimu tangu hajamzaa huyo Masu kua atatoa kafara ya Damu ya mjukuu wake atakaekujakumpata kwa Masu, japoyeyealidhani itakua mbali sana ila kwa mizimu hilo ni jambo la muda mfupi..” Hunudu akaweka kituo, akajikohoza kidogo halafu akaendelea

    “..Kesho inabidi sasa dada Joyce Ngulinzila kwakua Masu yuko mikononi mwako huko kituoni utafute nafasi ya faragha ili ukae nae umpe vitisho ili akubali kujiunga nasi na akubali kutoa kafara ya mwanae mmoja ili tumnusuru huyu Bi mkubwa, na hiyo itakua ni mara ya mwisho, wakati huo mimi nitasafiri kwa upepo mpaka tabora ili nikammalizie Yule dada ili tuzidi kuwaweka katika mazingira magumu ya kesi ya mauaji, watakapokua wakihangaika kupambana na kesi yao ndipo sisi tutakapozidi kuchanja mbuga kuwamaliza wote” Baada ya Hunudu kutoa ripoti yake akapigiwa makofi kisha akasimama Mzee mmoja hivi baada ya kupewa ruhusa, nae akaanza Kuwasalimia kwa ari zao za kimizimu

    “WAUFIIII..”

    “Mzimu wa watemi wa bahari” wakaitika wote kisha akaendelea kuongea

    “Jamani tatizo kubwa ni huyuhuyu mama Masu, sisi tulimshauri tangu mwanzo kua tummalize tu huyo Masu maana anataka kutuzidi nguvu lakini akakataa sasa leo tunasumbuana hapa kutaka kumuokoa kwa jambo alilojitakia, kwanini hasa? Kwani ni wangapi tulishawatoa kafara kwa kuzembea maelekezo ya Waufi? Mie nadhani tungeacha hii kesi aimalize mwenyewe na kama atashindwa ndani ya siku saba hizo zilizosalia basi awe asusa ya Mzimu” kauli ya Mzee huyu alipekea sauti ya kilio cha uchungu kutoka kwa Bi mkubwa mmoja aliekua ameinamisha sura yak echini muda wote wa majadaliano haya, na aliponyanyua uso wake akadhihirika kua ni Mama Masu, Baada ya Mzee huyo kuwasilisha hoja yake nae akaketi ndipo sasa kilio cha Mama Masu kikakatizwa na faraja kutoka kwa mwanamke mwenzake ambae ni Afande Ngulinzila aliesimama na kuanza kuongea kwa jazba kama ilivyo kawaida yake

    “Tumeitana hapa kwa ajili ya kutatua jambo la dharura, na hatupo hapa kwa ajili ya kulaumiana, hata hao mnaosema walitolewa kafara kwa makosa yao ilibidi kufanya hivyo baada ya kuwasaidia kwa muda mrefu sasa kwanini leo kwa Mama Masui we tofauti? Tangu tulipoanza kupambana na nguvu za Mzimu wa KASOMANGILA uliopo chini ya Waswezi tumekumbana na vikwazo vingi sana lakini hatujalalamika cha ajabu leo analalamika mtu ambae wala hajafanya lolote.. Mjinga mjinga tu na tumbo lake” Ghafla Ngulinzila alikatishwa na mkuu wao ambae ni Mwanamama mmoja hivi mweupe aliekua amejifunga kitambaa cheupe kilichokatiza juu ya kifua chake, akasimama na kumuamuru Joyce Ngulinzila aketi chini halafu akawasalimu salamu yao ya hamasa

    “WAUFIIII”

    “Mzimu wa watemi wa bahari”

    “Sasa naongea kama Kiongozi, Mimi ndo mtemi Kalovya, naomba sana msitutie aibu na fedheha mbele ya Mzimu, kumbukeni Mzimu wetu ni mzimu mkubwa sana, ni mzimu wa baharini, mzimu ambao matambiko yake ni ya baharini ndio maana wengi hushindwa kupambana nao, sasa itakua ni kituko eti tushindwe na wapuuzi wachache kutoka bara tu, hivyo sioni haja ya kuendelea kutupiana lawama hapa badala ya kupanga mipango ya kuwamaliza hawa waswezi, Hunudu ameongea vizuri sana kwa kutuonesha dira na mbinu ya kuwamaliza na hicho ndio kitu pekee kinachopelekea kila siku tumpe vyeo Hunudu, sasa hakuna malumbano tena zaidi ya kuutekeleza mpango kazi uliowasilishwa na Hunudu hapa, ila cha kuwasihi ni kua makini katika kila hatua maana tuna upinzani mkubwa, kumbukeni tayari tumeshampoteza kiongozi wetu wa mazindiko marehemu Kasimba aliuawa na Mizimu ya Kigoma huko kwao na marehemu Kishindo, Mizimu hiyo inatumia kivuli cha marehemu Kishindo kupambana na sisi huku wakishirikiana

    kwa karibu na Mzimu wa Waufi, na hilo ni kosa tulilolifanya baada ya kumsambaratisha Kishindo kwa Radi ilipaswa tuisambaze na nguvu yake ya asili ya mzimu ambayo ndio hicho kivuli chake. mizimu yote hii imeungana kumsaidia Masu, kumbukeni kua Masu ni wa Kigoma kwa upande wa Baba yake bwana Kikoko, sasa hapa tunapambana na nguvu za aina mbili tofauti, sio padogo hapo..”

    *****



    SIKU Iliyofuata ilikua ni Siku ya majuku mazito,

    Majukumu mazito kwa Afande Bangi wa kituocha Polisi cha Shinyanga kuanza kuifuatilia kesi hii kwa ukaribu zaidi,

    Majuku mazito kwa Afande Malumbo wa kituo cha Polisi Tabora kufuatilia kesi hiyo kwa kuanzia na kuifuatilia hali ya mgonjwa alie taabani hospitalini,

    Majuku mazito kwa Afande Ngulinzila aliepewa jukumula kumtisha Masu mpaka akubali kumtoa kafara mwanae na ajiunge na Waufi,

    Majukumu mazito kwa Hunudu kuhakikisha anasafiri kwa nguvu ya upepo na anafanikiwa kummaliza mgonjwa alie Mahututi huko katika Hospitali ya rufaa ya Kitete mkoani tabora..



    Wakati kila mmoja akiwa akiwa ameshaamka katika siku hiyo mpya akiwa tayari kutekeleza majukumu yake huku kituoni nako nyuma ya Nondo za Selo ndogo hapo kituoni walikua wameketi chini Sheikh Jabu na Masu wakiwa katikati ya Mazungumzo marefu sana, Masu alikua akimsimulia swahiba huyo wa baba yake kuhusu hali ile iliyojitokeza jana yake mule ofisini alipoingia yule askari wakike. Alielezea kwa ufasaha mkubwa jinsi alivyomkumbuka dada huyo siku ile alipomtokea akiwa na Masu, ilikua ni muda mfupi tu baada ya kuongea na marehemu Kishindo, suala hilo lilimtisha sana Sheikh Jabu kwani aliamini kua kumbe hawakua wakipambana na washabiki wa Waufi bali ni wafuasi hatari wa Mzimu huo, lakini kwa mtu mwenye hekma kama yeye hakupaswa kuonesha hofu yake mbele ya Masu, na badala yake alijifanya kua hajatishwa kabisa na matukio yanayoendeleaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimekuelewa sana mwanangu, ila nataka kukuambia jambo moja na ulishike sana, kaa ukijua hii ni vita ya Mizimu, vita ya nguvu za giza, wote wanapambana kwa ajili yako,kila mmoja anakuhitaji kwa maslahi ya mzimu wake, japo tunajua kuahawa Waufi ndo washenzi kabisa lakini uje kila muwamba ngoma huvutia kwake hivyo hata hao Waswezi wa huko Tabora nao hata kama wana mapungufu yao lakini watavutia kwao tu hivyo uwe makini sana..” Sheikh Jabu akavuta pumzi kidogo kisha akaendelea kutoa somo kwa mwanae “..katika vita hii utakaeumia ni wewe kwa kua huoni mbele, huna taaluma ya nguvu wanazozitumia wao, hakuna sehemu mbaya kama pale ulipogeuzwa Ng’ombe maana kama hao watu wa kwenu kipalapala wangechelewa kidogo tu saa hizi tungeshakula nyama yako zamani sana, pia ukae ukijua kwamba japo Mama yako aliiba mimba lakini nae alikuzaa kwa uchungu, pia alieibiwa mimba nae alipata tabu kubwa ya kuilea mimba yako kwa miezi ya awali hivyo hao wote ni mama zako..”

    Kabla Jabu hajaendelea Masu akamdakia

    “Mama zangu?? Yaani niwe na mama wawili?” Kabla Sheikh Jabu hajaendelea kuongea wakasikia sauti ya OC CID Ngulinzila akiingia kituoni kwa mikwara kama ilivyo kawaida yake, na baada ya kusalimiana na askari wake alisikika akitoa amri

    “Hebu nileteeni huyo Masumbuko Kikoko Ofisini kwangu, Haraka” Masu na Sheikh Jabu walitazamana baada ya kusikia kua sasa Masu anaitwa ndani na kabla hawajapeana cha kuongea tayari mlango palikua na sura kavu ya askari mmoja akliemwita Masu huku akifungua makufuli, ikawa Hakuna ujanja tena, ni kwenda tu kumsikiliza mfuasi huyu mahiri wa Waufi anaefanya kazi za serikali huku akichanganya na Waufi,



    Baada ya Mlango kufunguliwa Masu akawa ameshasogea mlangoni kwa ajili ya kutoka na kuelekea ofisini kwa Afande Ngulinzila ndipo ghafla ukasikika ukelele wa nguvu kutoka ofisini kwa OC CID, kelele za hamaniko na maumivu makali kutoka kwa apigae kelele hiyo, ilikua ni sauti ya Afande Ngulinzila, Askari wote walioisikia sauti ile walihamanika vilivyo, wote wakatoka mbio huku wakipamiana kuelekea ofisini kwa mkuu wao huyo, kwa kua hawakua mbali na ofisi hiyo hivyo haikuwachukua muda mrefu kuwasili ndani ya ofisi hiyo na kumkuta akiwa amelala chali juu ya Dimbwi la damu, ikawa ni kelele za hofu kutoka kwa baadhi ya askari wa kike walioshindwa kujizuia, Askari wakazidi kujaa ndani ya Ofisi hiyo kushuhudia tukio hilo la ajabu ambalo liligonga kichwa cha kila mmoja wao, ikabidi haraka baadhi ya askari watoke nje ya Ofisini hiyo ili kuangalia kama kuna dalili ya mtu aliefanya unyama huo!!

    *****



    Nje ya Ofisi ya muuguzi wa zamu katika Hospitali yaKitete mkoani Tabora alikua amesimama kijana mmoja akisubiri ruhusa ya kuingia ndani kuonana na muuguzi huyo, alisimama kwa muda karibu wa dakika mbili baada ya kugonga mlango ndipo akaruhusiwa kuingia, alipoingia ndani ya ofisi hiyo ndogo yenye kabati moja kubwa lililowekwa shuka nyeupe katika baadhi ya droo zilizozungukwa na vioo, pia kulikua baadhi ya mafaili yaliyojipanga ubavuni mwa meza hiyo, pia kulikua na meza ndogo ambayo juu yake kulikua na Trei ndogo iliyokua na Glove pamoja na mabomba ya sindano, katika kiti kilichokua kimetazamana na mlango wa kuingilia alikua ameketi muuguzi mmoja aliejitambulisha kupitia mavazi yake ya kitabibu, macho mawili ya muuguzi huyu yaligongana na jicho moja la kijana huyu alieingia ndani humu, Hunudu!

    “Karibu..”

    “Ahsante sana, habari za hapa?”

    “Nzuri tu, naweza kukusaidia..”

    “Oooh yeah, naitwa Hunudu nimekuja kumuangalia ndugu yangu”

    “Kaka huu si muda wa kuona wagonjwa, uje kwenye saa nane mchana”

    “Samahani Dokta, mimi nimetokea safari baada ya kupata habari za hali mbaya ya mgonjwa wangu, hivyo naomba tu unisaidie hata kwa dakika kumi nimuone tu”

    “Kaka huo sio utaratibu wa kazi, naomba uzingatie hilo,” Hunudu alibaki akimkodolea muuguzi huyo kwa jicho lake moja ndipo alipogundua kua dada huyu alikua akimaanisha akisemacho, akaona isiwe tabu, akaingiza mkono mfukoni kisha akatoa noti mbili nyekundu akamuwekea muuguzi yule juu meza, nae bila ajizi akazichukua na kuzisunda mfukoni kabla ya kumtupia macho yake bazazi huyu kutoka waufi

    “Mgonjwa wako anaitwa nani?”

    “Nyamizi Fundikira..”

    “Ohh yule aliepigwa panga kichwani?”

    “Ndio huyu huyo”

    “Ok nitakupeleka ila usikae muda mrefu maana wakitokea wakuu utaniletea kizaazaa, sawa?”

    “Haina shida dada, ni kama dakika kumi tu” Baada ya maridhiano hayo wakatoka ofisini huku wakielekea wodini kwa mtindo wa watoto wa bata

    *****



    Huku Shinyanga hali ilizidi kua tete kufuatia tukio hilo la kustaajabisha, Askari walikua wamechanganyikiwa kisawasawa, kila mmoja alikua akisema lake huku mwili wa Afande ukiwa badoumelala pale chini, muda huu sasa Afande Ngulinzila alikua kimya!!

    “Hakuna haja ya kuendelea kuduwaa hapa, tungemuwahisha kwanza hospitali” aliongea askari mmoja wa kike aliekua amesimama ndani kidogo kwa mlangoni

    “Hospitali kufanyaje? Afande hatunae tena, ameshakufa huyu, ametobolewa kifuani na inaonekana kama aliemtoboa alikua akinyofoa kitu ndani yake kama Moyo vile maana kuna nyamanyama nyekundu katika tundu” Kauli hiyo ilizidi kuzua taharuki ofisini pale na hapo ndipo sasa akili ya Koplo Bangi ilipogonga kengere baada ya kusikia kua huenda Afande Ngulinzila amenyofolewa moyo, akakumbuka tukiolilivyokua kwa marehemu Kasimba, wakati huo Koplo Bangi alikua amesimama katika mlango wa kuingilia ndani ya Ofisi hiyo, ikabidi sasa asogee ili aone hicho alichokisika cha kunyofolewa Moyo, aliposogea akashuhudia zaidi ya kilichompeleka, akashuhudia alama za kucha zilizokwaruza sehemu ya shingo ya afande huyu,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Taswira ya tukio la mauaji ya namna hiyo yaliyomkuta hayati Mzee Kasimba sasa yamemdhihirikia Afande Ngulinzila ambae amekua akionesha dalili ya kumtetea mama Masu ambae ni dada wa marehemu Kasimba’ Mawazo yalifanya utalii wa ndani katika kichwa cha Koplo Bangi

    *****



    Wakati Hunudu akiwa tayari ameshaingia ndani ya wodi kwa ajili ya kutekeleza azma yake ya kummaliza yule mgonjwa aliemkata na panga kichwani ndipo alipopokea ishara ya hatari ikimuarifu juu ya hali ya tukio la kuuawa mfuasi mwenzie wa Waufi ambae ni afande Ngulinzila, taarifa hiyo ya kiishara ilimfikia kwa nguvu zao za giza, Sasa tayari Hunudu alishahamaki kwa kiwango cha juu sana, akawa njia panda asijue cha kufanya, alitamani ammalize yule dada haraka lakini pia alihisi labda ajaribu kumuwahi Afande Ngulinzila labda angeweza kumnusuru, Ilimchukua kama dakika tano ndani ya wodi ile akiendelea kupambana na mawazo yake mwenyewe kabla hajapitisha maamuzi ya kuondoka ili akamuwahi afande Ngulinzila huku akitia nia ya kurudi tena pale wodini



    Haraka kwa mwendo wa upepo Hunudu alitoka hospitalini hapo bila ya kuaga huku akijaribu kuwahi Shinyanga kama atafanikiwa kuokoa uhai wa mfuasi mwenzie wa Waufi, alijaribu kupingana na taarifa zinazoendelea kupita kichwani mwake kua Ngulinzila ameshatokwa na uhai..

    *****



    Katika kituo cha polisi mkoani Shinyanga tayari maiti ya afande Ngulinzila ilikua imeshatolewa na kupelekwa hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa kifo hicho cha kutatanisha, hali ya simanzi, hofu na mashaka vilizidi kutamalaki katika mioyo na askari kadhaa waliokua pale kituoni, Gumzo la vuguvugu kufuatia tukio hilo la aina yake vilizidi kutiririka kutoka katika vinywa vya askari waliopo kituoni wakiungana na askari wengine waliozidi kuwasili kituoni hapo baada ya kutapakaa kwa taarifa za kifo cha afande Ngulinzila, Wahenga wanasema ‘Apatikane na mkasa hupatwa na vingi visa’ msemo huo ulidhihiri sasa maana kila mmoja alikua akisema yake anayoyajua, mazuri na mabaya ya Marehemu Ngulinzila huku wakiyanasibisha na tukio lenyewe lililotokea, hakuna aliekubali kutoa mtazamo wake ukizingatia askari hawa ni weledi wa upelelezi..



    Wakati hayo yakiendelea kufukuta hapo kituoni, katika ofisi ndogo ya upelelezi alikuwa ameketi peke yake Koplo Bangi akiwa ‘busy’ akipekua makaratasi katika mafaili kadhaa yaliyozagaa juu ya meza yake, wakati huo akiandika baadhi ya vitu katika faili lake maalum, Kazi kubwa iliyokua ikimmakinisha Koplo Bangi ni agizo maalum alilopewa na Mkuu wa kituo OCD Amosi Nkeli la kuandika maelezo ya kina juu ya kadhia iliyotokea kuanzia mwanzo wa kesi mpaka mwisho, Taarifa za utata wa kesi ya kina Masu ilizidi kumpa wakati mgumu Ocd Nkeli na tayari alikua ameshapata fununu na ‘udambudambu’ kuhusiana na Waufi, hivyo basi kwa kua Koplo Bangi alionekana kua na taarifa za kina hivyo akaachiwa aandae taarifa ya kiuchunguzi na kiuchokonozi ili aikabidhi kwa wakubwa wake wa kazi kwa ajili ya hatua endelevu..



    Baada ya takribani saa tatu na ushee tayari Koplo Bangi alikua ameshapanga mafaili yake vizuri ndipo akainuka kutoka kitini alipokua ameketi kisha moja kwa moja akatoka mpaka nje ya ofisi hiyo huku akielekea kaunta kwa ajili ya kuwachukua watuhumiwa wake kwa ajili ya mahojiano maalum, safari hii akiwa huru zaidi kuhoji atakalo kwa watuhumiwa hawa, sio tu kwa kua aliekua akimzuia amefariki bali kufuatia agiza maalum kutoka kwa mkuu wa kituo. Alipofika kaunta akaanza kutaniana na askari waliokua zamu pale

    “Haya sasa majukumu ya Afande Ngulinzila umeachiwa mzee wa kazi, bila shaka hata kifo kitakachofuatia ni cha kwako..” alidhihaki mmoja wa askari aliekuwa pale kaunta

    “Acha kuniombea dua baya hilo kaka, hii ishu sio ya kitoto bana”

    “Lakini afande Bangi hebu tupe ufyetere kidogo, kuna nini hasa hapa katikati”

    “Na wewe kwa udadisi mambo unajiweza!!..” Wote wakacheka kwa pamoja kisha Afande Bangi akamalizia kuongea

    “…Hebu nawaomba kwanza hao watuhumiwa halafu baadae tutaongea tu”

    “Lakini afande Ngulinzila si alikukemea wewe kujihusisha na kesi hii?”

    “Hah ha ha yake yamekwisha, hi indo dunia bhanaa” wakacheka tena kwa pamoja kisha afande alieklua zamu akawafungulia Akina Masu, Jabu, na mke wa mdogo wa Mzee Kikoko



    Walipotoka tu Koplo Bangi aliwachukua bila kupoteza muda na kuondoka nao wakielekea ofisini kwake huku nyuma waliacha gumzo likizidi kutia nanga, japo muda wote wa tukio la kifo cha ngulinzila watuhumiwa hawa walikua ndani tu lakini tayari walikwishajua kinachoendelea baada ya zogo la taharuki kua kubwa kufuatia kifo cha Ngulinzila, hivyo wote walikua kimya, wakielekea ofisini kwa Afande Bangi huku kila mmoja akiwaza yake, walipofika ofisini waliketi katika viti vitatu vilivyopangwa maalum kwa ajili yao huku kiti kingine cha nne kikiwa kitupu kikiangaliana na vile vya kwao huku wakifarakinishwa na meza iliyo katikati, na muda wa sekunde kadhaa baada ya wao kuketi ndipo Koplo Bangi nae akaketi katika kiti kile huku akiwatembezea macho yake kila mmoja wao kisha akaanza

    “Najua nyote mnajua kadhia inayoendelea kuighubika kesi yenu, na hicho ndicho kitu pekee kinachowafanya muendelee kukaa ndani muda wote huu..” Koplo Bangi akajikohoza kidogo kabla ya kuendelea

    “Sasa nataka tuyamalize humu ndani mimi na nanyi ila endapo tu mtanieleza kila kinachoendelea kwa ukweli na uhakika” Baada ya afande Bangi kuweka nukta ndogo akaangaliana na watuhumiwa wale halafu akaanza na MasuCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Masu kwakua wewe ni muhusika mkuu wa kesi hii, hebu nipe kila kitu ukijuacho kuanzia mgogoro wa baba yako na marehemu Mzee Kishindo na mpaka kifo cha kishindo kule porini ukiwa nae wewe na ikawaje mpaka ukatokomea porini huko kabla ya kukamatwa kule kipalapala Tabora… Nasisitiza ukweli utawale mahala hapa” Baada ya Koplo Bangi kumaliza kusema yake ndipo sasa ikawa zamu ya Masu ambae alianza kuielezea kadhia ile mwanzo mpaka mwisho huku Sheikh Jabu na mke wa Mzee Kikoko wakisikiliza kwa makini, wakati huo Koplo Bangi alikua akiandika baadhi ya vitu muhimu kutoka katika maelezo ya Masu kilichozidi kumshtua na kumpa udadisi zaidi koplo Bangi ni pale Masu alipoelezea alivyokua akimjua marehemu Ngulinzila na kumuhisisha na Waufi siku ile alipotokewa na Hunudu kwa mara ya kwanza..



    Kama ilivyo taaluma hii ya upelelezi kila unapotoa maelezo basi maswali huzalika zaidi, ndivyo ilivyokua kwa Koplo Bangi

    “Sasa Je unajuaje kama afande Ngulinzila alikua ni mfuasi wa Waufi? Je kama huyo Hunudu alipewa lifti tu kama ulivyopewa wewe?” lilikua ni swali la kipuuzi tu kuoka kwa afande huyu lakini lenye utafiti mkubwa ndani yake

    “Bila shaka walikua wakijuana kwa kua maongezi yetu yote yalikua yakua yakifanyikia ndani ya gari hiyo hiyo na wala dada huyo hakushtuka, pia zaidi ya hayo alikua akisapoti kinachosemwa na Hunudu huku akitabasamu mara zote, na ndo maana hata aliponiona hapa tulitazamana kwa dakika kadhaa kabla hajaendelea kukaripia” Baada ya majibu ya Masu sasa Koplo akamgeukia Mke wa Mzee Kikoko

    “Mama haya umesikia habari yote kutoka kwa Masu inawezekana kua ni mwanao kweli? Na je unaijua na kuikumbuka hii habari?”

    “Ni kweli naijua hili tukio, lilinitokea mimi mwenyewe, na kila alichokisema Masu kuhusu upande wangu ni kweli kabisa”

    “Mimi nataka unielezee wewe kwa maelezo yako” Mke wa Kikoko sasa alianza kuelezea hatua kwa hatua tangu kuibiwa ujauzito wake kishirikina, hatua zote za usuluhishi zilizopitiwa, mpaka kufikia hapo walipofikia, lakini alikataa kujua chochote kuhusiana na kifo cha marehemu Kishindo,

    “Sasa ilikuaje ukawa unataka kutoroka ukiwa tayari na begi lako mkononi kama hauhusiki?”

    “Mimi sikuwa nikikimbia, bali nilikua naelekea stendi kwa ajili ya kuangalia usafiri wa kwenda Dodoma kumuangalia mume wangu baada ya kuambiwa kua anaumwa na amelazwa huko” baada ya maelezo yake nae alikumbana na maswali ya papo kwa papo ambayo aliyajibu kwa kadri ya uwezo wake.. Baada ya kumaliza sasa koplo Bangi akamgeukia Sheikh Jabu ili amalizie Ngwe yake

    “Sheikh wewe ni swahiba wa karibu sana wa Mzee Kikoko na marehemu Mzee Kishindo, najua una mengi unayajua, hebu nahitaji hekma zako ambazo mwanzo ulizificha mpaka ukjikuta upo hapa leo hii” Swali lile lilikua kama la dhihaka kidogo kwa Sheikh Jabu lakini halikumfanya ashindwe kutumia hekma na fasaha yake katika uzungumzaji, alieleza mambo mengi sana japo yakiwa hayana tofauti sana na wenzie waliomaliza kuhojiwa punde, sema tu Jabu aliyaongea kwa balagha ya hali ya juu kiasi cha kuyafanya yazidi kueleweka na kumuingia vema afande Bangi

    “Sasa Mzee wangu hauoni kua huu ni utata? Yaani Ndoto tu ndo imezua yote haya? Tazama sasa Kishindo ameshakufa na kuzikwa lakini vipimo vinaonesha Marehemu Mzee Kasimba amekutwa na alama za mikono ya marehemu Kishindo, we haudhani kua huyu Masu anajua mahala alipo Kishindo?”

    “Hata mimi najua mahala alipo Kishindo” jabu alimkatisha Afande Bangi

    “Mnh.. yuko wapi?”

    “Kishindo yuko Kaburini sasa hivi, tumeshamzika! Kifo cha kishindo na kuendelea kuhusishwa na tukio la mauaji ya hayati Kasimba ndio litakua jibu la swali lako la kwanza”

    “Swali lipi?”

    “Umesahau ulichoniuliza? Umenuiliza hivi ‘Mzee hauoni kua huu ni utata?’, Naam huu ni Utata”



    Wakati Koplo Bangi akizidiwa na hasira ndani ya moyo wake zilizosambamba na udadisi uliomjaa kufuatia maelezo ya laini kutoka kwa Sheikh jabu ndipo ghafla mlango wake ukasukumwa kwa nguvu na hapo hapo akaingia Ocd Nkeli, mkuu wa kituo cha Polisi, akionekana ni mwenye taharuki kubwa. Kitendo bila kuchelewa Koplo Bangi akasimama na kutoa saluti kwa Bosi wake huyo kisha akampa kiti aketi huku akimuhoji

    “Mzee kuna usalama kweli?”

    “Hakuna usalama Koplo..” wote mule ndani wakawa wanamuangalia Mkuu huyo akiongea kwa hali ya hofu na wazo mengi kichwani, hakuna alieingiza neon mpaka alipoendelea mwenyewe kutiririka

    “Nimetokea hapo Hospitali ya mkoa kuonana na Dr Shamsi, amenipa majibu ya vipimo vya Mareh.. ahh Afande Ngulinzila”

    “Majibu gani hayo kayatoa?” Koplo Bangi alijaribu kuchombeza swali

    “Muuaji wa Mzee Kasimba ndie aliemuua Afande Ngulinzila…” akaweka nukta kidogo kuipa nafasi pumzi nzito iliyoambatana na mwayo kisha akaendelea

    “… Alama za vidole zilizoonekana katika mwili wa marehemu kasimba ndizo zilizoonekana tena maeneo ya kifuani na kooni mwa Afande Ngulinzila” hapo hapo Ocd Nkeli akaitupia juu ya meza ya Koplo Bangi bahasha ya kaki yenye nakala ya vipimo kutoka hospitali kasha akamalizia kwa kuhoji

    “Hawa ni akina nani?” huku akiwatazama Masu na wenzie

    “Si ndio wale watuhumiwa wa kesi hii”

    “Oooh sorry…” alijua amefanya kosa kuongea mambo nyeti kama yale mbele ya watuhumiwa, halafu akamalizia kusema

    “..Ok ingiza na taarifa za vipimo hivyo katika Report yako kabla hujaiwasilisha mezani kwangu” hapo hapo Mkuu AkatokaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kichwa cha Koplo Bangi sasa kikahama kwenye majibu yaliyomghadhibisha kutoka kwa Sheikh Jabu na sasa mawazo yakahamia kwenye taarifa mpya aliyoipokea kutoka kw mkuu wake wa kazi, sasa kazi ilikua ndio kwanza inaanza, akafunika mafaili kisha akanyanyuka kwenye kiti na kuwaamuru watuhumiwa wake wasimame na baada ya hapo akawarejesha tena selo ili aweze kuandika kwa utulivu taarifa yote baada ya kupata picha ya kila kinachoendelea kuzunguka ndani ya kichwa chake

    *****

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog