Search This Blog

MZIMU WA WAUFI - 3

 







    Simulizi : Mzimu Wa Waufi

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Familia zilijaribu kukaa na kufanya suluhu ili kwakua mambo haya yanautata mkubwa waweze kuiyamaliza, ilikua ni suala gumu sana lakini hatimae waliridhiana kishingo upande huku kila mmoja akibaki na lake moyoni, inasemekana wakati Bi Kapemba alipokwenda Shinyanga Mizimu ya kwao iliinyakua kichwawi mimba ya Bi Mwajabu na kuihamishia kwake kisha wakampa sharti kua ni lazima atoe kafara ya damu haraka iwezekanavyo Laa sivyo watamchukua Masu wao na Pia walimtaka Bi kapemba kuwa Masu akifikisha miaka kumi ampeleke ili akaingizwe rasmi kwenye Ukoo wao chini ya Mizimu ya Waufi kwakua hakua damu yao lakini hakufanya hivyo….



    *****



    Masu alikua amemtolea macho Mzee Kishindo aliekua akimpa mkasa mzima wa kuzaliwa kwake, ilikua ni stori ya ajabu na kustaajabisha sana

    “Kwahiyo hakuna Dini ya Waufi mwanagu hiyo ni mizimu ya Waufi na kila wanachokufanyia ni kiini macho tu, hata Yule mchungaji na huyo sheikh wote si WAUFI bali unapokua unaongea na mtu yeyote anaonesha kutaka kukusaidia anakuja huyo hunudu na kujivisha umbile la huyo mtu kisha anajifanya nae ni Waufi”

    “Mbona kwako wewe hua hatokei?”

    “Nitakupa siri ya mizimu ya kwetu mimi”

    “Sasa Baba nae aliamuaje?”

    “Kikoko aliyakubali matokeo tu na anajua kila kitu sema anajaribu kujisahaulisha wakati wewe unaangamia” Masu akawa analia baada ya kuusikia Mkasa wake ule, Ikabidi sasa Mzee Kishindo akamkataze kulia

    “Nilikuambia uwe na kifua, sasa unalia nini?”

    “Mzee Kishindo mie nitakufa tu, sasa nitafanyaje mimi? Yaani kumbe Mama Masu hakua mama yangu halali??!”

    “Hauwezi kufa japo huu mpambano ni mkali, unachotakiwa kufanya kwenda kwao na mama yako wa damu Bi Mwajabu Huko kipalapala tabora ili ukafanyiwe tambiko la kwenu, tambiko la Waswezi Laa sivyo utapotea kijana, ukiwa tayari nitakusindikiza”

    “Kwahiyo tanafanyaje Mzee wangu?”

    “Nitakusaidia, andaa nauli nitakupeleka mpaka Tabora kwenu, kwa mama yako”



    Wakiwa katikati ya maongezi mazito ghafla walisikia sauti ya pikipiki ikija maeneo ya pale kwa Mzee Kishindo kisha mlio ukazima na baada ya muda kidogo mlango ukagongwa



    Ngo! Ngo! Ngo!



    Kabla hawajafanya lolote mlango ukafunguliwa akaingia Mzee Kikoko akiwa na Sheikh Jabu, baada ya Sheikh Jabu kugonganisha Macho na Mzee Kishindo hapo hapo Kikoko akamgeukia Sheikh Jabu

    “Si nilikuambia kua huyu mshenzi ndie anaeleta fitna kwenye familia yangu?!!!”



    ******



    MZEE Kikoko hakusubiri kugongewa kengere kama ishara ya kupata kibali cha kumvaa Mzee Kishindo na kuanza kumtembezea kichapo, ilikua ni kitendo cha kunusa na kutoa chafya, balaa kubwa kati ya wazee hawa ikaanza, tayari Kikoko alikua ameshasogelea na ameshamkunja shati Mzee Kishindo,

    “Tafadhali Bw Kikoko niachie, hapa ni nyumbani kwangu utajiletea dhahma kubwa” alibwata Mzee Kishindo

    “Sikuachii nataka nikuadabishe kidogo maana nilishakukanya kwa maneno ukaweka Nta masikioni” bada ya maneno yale hapo hapo Kikoko akamrukia kichwa mzee mwenzie, akamrushia ngumi, mara akamza ba kelbu la uso, Hakika Kikoko ni mzee mtata mwenye kila chembe ya ukorofi na shari, wakati huo kichapo kinaendelea Masu alikua ameshafika mlangoni kwa ajili ya kukimbia lile varangati lilikua likiendelea kuzizima mule ndani..

    “Kikoko acha tafadhali” Sheikh Jabu alikua akijaribu kumuhami Mzee Kishindo asiendelee kupokea kichapo kutoka kwa Alwatani Kikoko ambae alikua ameshamgaragaza chini Mzee Kishindo, Kikoko aliendelea kumvugumizia makonde ya nguvu Mzee Kishindo, hakika ilikua ni hali ya hatari sana, baada ya purukushani kubwa pale chini hatimae Mzee Kishindo alifanikiwa kuinuka na kuponyoka kutoka katika mikono ya Kikoko, akatoka mbio akielekea Chumbani kwakeCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nitakuua mimi, unaleta ubwege wako hapa..” Kikoko aliendelea kutamba pale sebuleni kabla Kishindo hajatoka chumbani kwake kwa kasi ya ajabu, Alionekana kama Ng’ombe aliechanganyikiwa, hakika alikua amepandwa na ghadhabu, Mkononi akiwa ameshika kitu cha hatari sana, kitu chenye madhara, Naam ilikua ni mkia wa taa, Mkia wa taa ni hatari sana kwa mwenye kuujua hata ikiwa katika ugomvi mkubwa kiasi gani mtu akiutoa tu ule kila mwenye kuujua atakimbia kabisa, Ukichapwa na mkia ule kwanza utapata maumivu makali yasiyo ya kawaida na pia baada ya siku kadhaa utajishanga ukiugua tu hovyo

    “Kishindo achaa tafadhali hiyo ni hatari” alipayuka Sheikh Jabu” Lakini Kishindo hakusikia ‘La Imam wala la mnadi swala’ Alikua amekasirika haswa! dakika chache tu akawa kaishamkaribia Mzee Kikoko na hapo hapo alianza kumcharaza kwa nguvu zote Mzee Kikoko, alimtandika mwilini hovyo hovyo, Kikoko alikua ameshahamaki hivyo kila alipojaribu kutaka kujihami ilikua ni sawa na kazi bure maana tayari Kishindo alikua ameshamtaiti vilivyo, Kipigo kilipozidi Kikoko Akaamua kutoka nduki kali lakini kutokana na Simenti laini iliyopo sebulaeni kwa Mzee Kishindo akaanguka chini ndipo sasa Mzee Kishindo akapata upenyo mzuri wa kumuadhibu Alwatan, Kikoko akawa anagaa gaa pale chini huku akipiga kelele lakini Kishindo hakua na hata chembe ya huruma aliendelea kutoa kiminyo utadhani anaua Nyoka,



    Wakati hayo yakiendelea tayari Masu alishatoweka mule ndani, pia Sheikh Jabu alikua amekimbilia upande wa pili wa sebuleni akihofia kukaa karibu maana alijua bila shaka Mzee Kishindo atamgeukia na yeye na kumuadhibu pia, na kwa jinsi alivyoijua sumu iliyomo kwenye mkia wa taa hakutaka dhahma ile imkumbe,



    Ghafla Kikoko akapata upenyo akachomoka na kutoka mbio mpaka nje ya nyumba ile, nae Sheikh Jabu akafuata mbio mpaka nje, Mzee Kikoko alikua kavimba mwili kwa kichapo cha mkia wa Taa

    “Kama mwanaume kwanini ukimbilie mkia wa Taa?” Alipayuka kwa sauti Mzee Kikoko huku akiwa anatweta

    “Pole Swahib wangu ila nilikukanya wewe, kua tukifika usifanye fujo hata kama tutamkuta Masu”

    “Yule asingekua na ule mkia ningemdhibiti tu mimi ni mtoto wa mjini, we hukuona nilivyomuanzishia mpaka akahuma, halafu ananishambulia na silaha na wewe umekaa tu pembeni na kanzu yako mchinjo hiyo kama mtoto anaesubiri kutahiriwa..”

    “Hilo ndo tatizo lako Bw Kikoko”

    “Na hakyamungu usingekua swahiba wangu leo ningekutandika na wewe maana huna maana”

    Baada ya malumbano na majibizano ya muda mrefu yale, Sheikh Jabu na Kikoko wakapanda pikipiki yao aina ya ‘Bata vuz’ kisha wakaondoka kwa kasi kuelekea nyumbani



    *****



    Nje ya Ofisi ya Birimuye Holding Ltd alikua amesimama Masumbuko Kikoko akiongea na kijana mmoja mfanyakazi mwenzie pale ofisini aliezoeleka kwa jina Shamsi, lengo la Masu ni kwenda kuongea na Boss wake Mr Kitale aweze kupatiwa kiasi kidogo cha fedha kwa kama mkopo ili akitumie haraka kwenda Tabora akisindikizwa na Mzee Kishindo ili akafanyiwe Tambiko na Zindiko kutoka katika Mizimu ya damu ya mama yake huko Kipalapala, Mizmu ya WASWEZI, Lakini Masu alishangazwa na taarifa alizopewa na Shamsi..

    “Mbona sikuelewi Shamsi?” Alishangaa Masu

    “Ndio hivyo Kaka, unajua mimi nimekulia uswahilini kama wewe, hayo mambo ya kishirikina ninayaelewa vema lakini hapa Ofisini kuna watoto wa Kishua tu hawayaelewi kabisa, wanachoamini wao kua wewe umechanganyikiwa hivyo wameamua kukusimamisha kazi kwa muda usiojulikana mpaka Boss atakapojiridhisha kua sasa umepona, na pia kama utaonekana hapo ofisini kwa kipindi hiki utaitiwa askari’

    “Shamsi mbona nazidi kuchanganyikiwa ndugu yangu, sasa nitakimbilia wapi mie hapa nilikua nimekuja kuomba kukopa pesa kwa ajili ya nauli”

    “Nauli ya kwenda wapi tena?”

    “Si nimekudokeza kuhusu hilo suala la kwenda kufanyiwa tambiko huko Tabora”

    “Sasa na wewe huna hata akiba nyumbani? Kwani inatakiwa kiasi gani?”

    “Sio kama sikua na akiba, nilikua nayo kidogo lakini sasa nasikia Mzee Kikoko kamnyang’anya mke wangu kila kitu muhimu ikwemo na kadi za Benki na kwakua nitaenda na Mzee Kishindo hivyo nahitaji kama Tsh laki tatu tu zingenitosha kabisa” Masu alikua akitikisa kichwa kwa uchungu huku akiwa ameinamisha paji lake la uso chini kwa huzuni, kasha akamtupia swali Masu

    “Sasa mwanzo uliniambia kua Mzee wako amewavamia pale kwa huyo Mzee Kishindo halafu akawaanzishia vurugu sasa huoni kua huyo mzee hatokua tena na nia ya kukusaidia?”

    “Hayo nitaenda kuyajua hukohuko lakin kwanza niwe na pesa mkononi ili hata kama nitamshawishi na kumuomba radhi basi kazi itafanyika si unajua tena mkono mtupu haulambwi, Kwani humo ofisini yumo nani?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Aaah wamo tu kina Leylah, Hindu, nadhani na Yule dada mtata kutoka tabora”

    “Ritha..??”

    “Yeah Ritha, ila hao wote ndo wale wale wanamjaza Sumu Boss na kama wakikuona tu watampigia simu sasa hapo itakua shida kwako” Kikapita kimya cha muda mrefu kidogo kila mmoja akionakana kuzama katika dimbwi la mawazo, ndipo tena Shamsi akavunja ukimya

    “Sikia ndugu yangu, mimi na wewe tumetoka mbali sana siwezi kukuacha ukiangamia, nitakuusaidia mpaka pumzi yangu ya mwisho”

    “Nitashukuru kaka.. nifae ndugu yangu”

    “Nitakupa hiyo pesa na utakapo rudi utanirejeshea, sawa?”

    “Sawa kaka yaani nikirudi tu nitafanya mpango wa kukulipa”

    “Ok usijali, ila sasa kwakua baba yako anaonekana kutaka kuvuruga kila kitu kwako sasa mie ninakushauru uje ulale kwangu na usimuambie mtu yoyote kua uko kwangu, au we unaonaje?”

    “Yeah ni wazo zuri tu ila sasa kwakua umenipa uhakika acha sasa nikaongee kwanza na Mzee Kishindo”

    “Poa, take care”

    “Ok” Baada ya makubaliano hayo sasa Masu alipata nguvu hivyo akaanza tena kupuyanga kuelekea nyumbani kwa Mzee Kishindo huku kichwani akiwaza itakuaje kama atamkuta bado Mzee wake yuko kule



    *****



    Haikuchukua muda mrefu tayari Sheikh Jabu alikua ameshafunga breki za pikipiki yake mbele nyumba yake akiwa amembeba Mzee Kishindo, wakateremka na kuingia ndani, walipofika tu ndani wakakutana Mama Salman(Mke wa Sheikh Jabu) pale uani akiwa amefura kwa hasira

    “Haya wenzetu mmeanza lini ubondia huko?” Mke wa Sheikh Jabu aliwauliza kwa kejeli

    “Ubondia gani?” akajibu haraka haraka Sheikh Jabu

    “Hamjui eeh”

    “Hebu we fanya shughuli zako achana na mambo yasiyokuhusu..”

    “Hayanihusu eeh.. ok sasa mtaenda kumtafuta Mama Masu kila kituo cha Polisi mpaka mtakapo mpata”

    “Hee Mama Masu kakamatwa? Na nani? Na kwa nini?”

    “Heheee, mie si hayanihusu haya kaeni na ujuaji wenu..” Baada ya kashda zile haraka Bi mkubwa Yule akachepuka zake ndani akiwaacha wazee wale wakitazamana bila ya majibu, Mzee Kikoko alipepesa macho huku na kule lakini hakumuona Mkewe, alizidi kuhamanika, ikabidi wamfuate kwa utaratibu huko huko sebuleni

    “Mama Salma hebu kua makini kidogo mke wangu, imekuaje tena?”

    “Wamekuja hapa maaskari utadhani kuna mtu ameua, wanamtaka Kikoko, wanadai alimpiga mkwewe na kumjeruhi vibaya na mbaya zaidi kaingia ndani kachukua pesa pamoja na kadi za benki walipomkosa ndo wamemchukua Mama Masu ili akaisaidie Polisi mpaka Kikoko atakapopatikana”

    “Mungu wangu” Kikoko alijisemea huku akishusha pumzi nzito” Sheikh Jabu akamgeukia swahiba yake Kikoko

    “Sasa na wewe kwanini umechukua hivyo vitu?”

    “Jabu, vile vitu ni mali ya mwanangu sasa kulikua na ubaya gani mimi kuvichukua?”

    “Sasa ukizushiwa umeiba vitu vingine vingi au pesa nyingi uatakatalia wapi na kweli uliingia chumbani?” Kikoko alibakia ameduwaa asijue cha kufanya



    *****



    Baada ya muda mrefu wa kutembea hatimae Masu alikua nje ya nyumba ya Mzee Kishindo, nyumba ilikua kimya, hapakua na dalili hata ya mtu ndani. Akasogea mpaka mlango halafu akategesha sikio lake mlangoni ili asikie kama kuna dalili za watu kule ndani, GHAFLA

    “Toka hapo we mwanaharamu, naona sasa mnataka kuniulia mume wangu Toka kabisa kabla sijafika hapo” ilikua ni sauti ya mke wa mzee Kishindo ikitokea chumbani, Kumbe muda wote huo Bi mkubwa Yule alikua akimuangalia kupitia dirisha la mbele ya nyumba hiyo, Masu alihamanika akajua sasa tayari bwawa limeshaingia ruba, akajifanya kama hajaelewa alichoambiwa, akabaki amesimama kama mtoto ya yatima.

    “Nakwambia TOKAA Hausikii wewe mpaka nije nikumwagie maji ya moto hapo?”

    “Mama ungenisikiliza japo kidogo tu”

    “Sina hata hamu ya kuyaona hayo magwambala yako hapo” Masu akabaki kimya akiwa amehuzunika, maswali kibao yakizunguuka kichwani mwake, alijiuliza kama mke tu amekasirika vile Je Huyo Kishindi mwenyewe yuko katika hali gani?, wakati anaendelea kufikiria ghafla akasikia sauti ikitokea kwa ndani zaidi, ilikua ni chumba cha uani, ni sauti ya Mzee Kishindo mwenyewe

    “Mwache aingie kama ni Masu”

    “Ili aje alete sekeseke lake humu au sio?, ukiumizwa au ukipelekwa Polisi atakaehangaika ni nani”

    “Hapana huyo hana kosa lolote anahitaji kusaidiwa tu” Mke wa Kikoko akasonya kwa sauti mpaka kule nje akasikika , Masu kimoyo moyo alikua akimshukuru Mungu alianza kupata matumaini mapya kutoka kwa Mzee Kishindo ambae ndie aliekua kimbilio lake kwa muda ule, ghafla mlango ukafunguliwa akakutanisha macho na mke wa Mzee Kishindo akiwa amenuna vibaya



    “Shikamoo mama”

    “Hivi kwanini ninyi hamna huruma? Mpaka mumuue huyu mwanaume?” kabla Masu hajajibu lolote akasikika tena Mzee Kishindo

    “We hausikii? Nimekuambia umuache huyo aingie” Yule mama akarudi ndani huku akiwa na jazba, Masu akaingia sebule na hapo hapo akakutana na Mzee Kishindo akitokea chumbani kwake, akamkaribisha kwa furaha tu kitu ambacho Masu hakukitegemea, alijiuliza mara mbili mbili juu ya ukarimu wa mzee Yule licha ya tabu anazomsababishia, Masu akenda mpka katika makochi akaketi kisha Mzee Kishindo nae akafuata, akaketiCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Masu uko salama mwanangu?”

    “Niko salama mzee wangu, ila kwanza naomba kwa yote yaliyotokea unisamehe mimi, usinichoke mzee wangu tafadhali”

    “Ahhh Masu achana na hayo, Yule baba yako kaishachanganyikiwa, sasa chamsingi tulishaongea mengi na sasa inatakiwa ufanye kila uwezalo tuanze utekelezaji wa mpango huu haraka iwezekanavyo” Masu akashusha pumzi, akafurahia kusikia kua mzee Yule hajabadili maamuzi hata kidogo, Basi kwa kua Masu alikua na uhakika wa kupata pesa akaongea mambo mengi na Mzee Kishindo wakakubaliana kua kesho yake asubuhi wakapande Basi waelekee Tabora, baada ya makubaliano hayo wakaagana na Masu akatoka na kuondoka zake



    *****



    Usiku majira ya saa mbili Masu alikua nyumbani kwa Shamsi wakijadiliana juu ya tatizo lake huku wakipeana ushauri wa hapa na pale

    “…Zaidi ya yote Mungu ndie mjuzi ya yote atakusimamia,”

    “Amiin, nashukuru sana kaka kwa ushirikiano wako”

    “Sasa utachukua hiko ki begi kidogo maana hauna haja ya kwenda na nguo nyingi pia utachukua na nguo zangu kidogo tu” Baada ya mazungumzo yao, Shamsi akaingia chumbani halafu punde akatoka na bahasha ya kaki, alipofika pale seating room akaifungua na kutuoa pesa kisha akampa Masu ahesabu, Masu akahesabu na kuthibitisha Tsh Laki tatu taslim

    “Nashukuru sana Shamsi, sina cha kukulipa ila Mungu ndie anajua cha kukulipa kwa wema wako”

    “Ahh usijali kaka, sisi sasa hivi ni ndugu, sasa we ingia tu chumba hicho ukajipumzishe ili asubuhi usipate tena tabu ya usingizi”

    “Ok poa, Mungu akipenda kesho” Masu akainuka akimuacha Shamsi akimuangalia kwa jicho la huruma sana, akingia chumbani kwa ajili ya kulala!!



    Japo usingizi ulikua wa Mang’amng’am kutokana na kiwewe cha safari pia na hofu ya kutokewa na Hunudu, lakini hatimae akalala….



    ****



    Ndani ya Basi la NBS kutoka Dar es Salaam kwenda Tabora, seat namber tisa na kumi walikua wameketi Mzee Kishindo na Masumbuko, walibahatika kupata seat zilizokaribu karibu hiyo ikawa ni nzuri kwao wakaweza kupata wasaa wa kupanga kila hatua wanayopaswa kiuifanya, hakika Kishindo alikua amejitoa kumsaidia Masu..

    “Mama yako huko nimeacha tumenuniana, alikua hataki niondoke”

    “Nik kweli unajua wanawake wana roho ndogo sana pia usikute anahofia kama Kikoko atatokea pale ghafla itakua shida”

    “Hawezi kufanya lolote tena kwanza anatafutwa na Askari huko”

    “Bora tu wameweke ndani ili sisi tukamilishe zoezi letu”

    “.. haya ila sasa inabidi tuwe makini kwa kila nukta maana hii ni vita ya mizimu”

    “Ni kweli mzee ila mimi naomba Mungu tu tufike salama kwani sidhani kama umakini wetu utaweza kuzuia nguvu zao kama watatuvamia hapa hao waufi”

    “Ondoa shaka, kwanza kaa ukijua hauko peke yako, ile mizimu ya kwenu huko Tabora iko pamoja na wewe ndo maana kila walipokua wakikuijia usiku kwa njia ya ndoto kila walipotaka kukulazimisha kutoa kafara ulikua unashtuka usingizini, sasa ile na nguvu ya Waswezi ilikua inakuokoa”

    “Kwa hiyo kumbe hiyo Mizimu inanitambua nayo?”

    “Ndio, we ni damu yao kabisa hawaezi kukutelekeza, pia hata ule ujasiri wa kutoa siri zao unadhani uliupata wapi?”

    “Mmmh”

    “Ndio hivyo, hebu lete huo mfuko wangu hapo chini nikuoneshe kitu” Masu akautoa mfuko na kumkabidhi mzee Kishindo ambae alifungua na kutoa kitu falani hivi kama mkia wa Ng’ombe

    “Unajua hii kitu?”

    “Hapana, ni nini hasa?”

    “huu unaitwa USINGE, nilipewa na wazee wa kwetu kigoma, kazi yake ni kupambana na nguvu za kichawi na ki mzimu kama zinazokusumbua wewe, hivyo kama litatokea tatizo kubwa tutatumia huo kutatua”

    Safari ilikua ndefu sana, kutoka Dar kwenda Tabora ni hatua ndefu tena kama kipindi hiki cha mvua nyingi barabara nyingi hua mbovu sana, Hatimae Basi likafika porini sehemu na Konda akanadi

    “Haya Abiria tuna dakika tano tu za ‘kuchimba dawa’..” haraka abiria wakaanza kuteremka na kwenda kwenye vichaka kwenda ‘Kuchimba dawa’, Mzee Kishindo nae akashuka lakini Masu hakushuka akaendelea kukaa pale pale kwenye seat yake, na kabla ya dakika zile kuisha mvua ikawa inaanza kunyesha kwa mbali, musa si mrefu abiria wote wakawa ndani ya Basi kuendelea na safari lakini Madsu akashtuka kuona gari inaanza kuondoka bila ya kumuona Mzee Kishindo

    “We Konda hebu zuia mzee wangu hajapanda” Masu alimwambia Konda

    “Sasa nae amekula nini? Tangu muda ule aah, Oyaa Suka zuia kuna mtu hajapanda” Dereva akazuia lakini mzee Kishindo hakuonekana, waliposubiri kwa takribani dakika kadhaa bila kumuona ikabidi Masu ateremke ili afuate kule kichakani akaangalie kuna nini? Wakati hua Masu anateremka ile mvua ilikua ikiendelea kwa mbaali, Masu aliingia mpaka kichakani lakini hakumuona mzee Kishindo

    “Mzee Kishindo!!!, MZEE KISHINDOOO!!” Masu alikua akiita kwa sauti lakini hakujibiwa na mtu, ghafla mvua ikaanza kuongeza kasi na dakika chache tu mbele ikarindima mvua ya adabu, ilikua ni mvua kubwa sana kiasi kwamba hata mbelea hauoni, ikabidi sasa Masu ajaribu kukimbia tu kurudi kwenye kule alipoliacha Basi, lakini kila alipozidi kuongeza kasi alizidi kuhisi kupoteza muelekeo maana hakuliona Basi wala hata dalili ya BasiCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hivi wameniacha au?” alijisemea peke yake Masu “Huu sio uungwana, sasa watatuachaje porini peke yetu? Halafu na mifuko yetu imo humohumo dah” Masu aliendelea kuulaumu upepo maana hakukua na mtu aliemsikiliza, Mvua alikua kubwa mithili ya enzi zile za Elnino, takribani nusu saa ilinyesha mvua kubwa ya mawe iliyofanya hali ya pale porini kuwa ya kutisha na kuogofya sana



    Baada ya nusu saa ya kunyesha mvua ya kishindo sasa hali ikaanza kua shwari, mvua ilianza kupungua na hatimae kukatika kabisa, ilipokatika sasa Masu akiwa almelowana chepechepe akaanza kuangaza huku na kule kama atamuona mzee Kishindo lakini hakumuona ila kilichomshangaza zaidi hakuliona Basi walilokua wamepanda haikuchukua muda mrefu akasikia sauti ikimuita kwa kasi

    “Masuuuuuu, njoooo” Masu akageuka haraka aliifahamu vema ile sauti, ilikua ni ya Mzee Kishindo, sauti ile ilikua ikitokea kwenye kichaka kikubwa tu upande wa mashariki mwa pori lile, Masu akakimbia mpaka maeneo yale na punde akamuona Mzee Kishindo akiwa amekaa chini, cha ajabu licha ya Mvua kubwa iliyonyesha lakini mzee Kishindo hakua amelowana hata kidogo

    “Mzee vipi? Ulikua wapi?”

    “Lete haraka ule USINGE wangu, tumeshavamiwa na Waufi “

    “heee, Mzee usinge umo kwenye Basi na Basi lenyewe hata silioni itakua limeshaondoka”

    “Kwanini sasa ulishuka jamani? Tumekwisha sasa”

    “Sasa ningefanyaje maana uliposhuka wewe kwenye Basi ukachelewa kurudi ndo maana ikabidi nishuke kukuangalia”

    “Halafu mbona umelowana hivyo?”

    “Mzee inamaana wewe hukuiona mvua hii yote? Mvua kubwa yam awe mpaka mie nikawa sioni mbele”

    “Mvua gani? Mbona mie sijalowana?” Masu alipigwa na butwaa, akaendelea kumuhoji Mzee Kishindo

    “Kwani imekuaje mpaka ukasema kua Waufi wameshatuvamia?”

    “Wakati nikiwa najisaidia hapo kichakani ametokea kijana mmoja mweupe kiasi ana Jicho bovu…” Kabla Mzee Kishindo hajamaliziakuongoa wakasikia mlio mkali sana kama wa Simba aliyejeruhiwa na ghafla akatokezea mnyama mmoja mweusi, mnyama wa ajabu haelewekua ni aina gani ya mnyama, akaanza kuja kwa kasi ya ajabu usawa ule waliokua wamesimama Masu na Mzee Kishindo

    “TOBAA.. Masu kimbiaa” Mzee Kishindo alipayuko kwa hofu, wakatimua mbio za hatari, wao mbele yule mnyama nyuma, walikimbia kwa muda mrefu na kwa umbali mrefu mpaka wakabaki hio bin taaban bila ya kujua hatima yao ni nini na ghafla walipogeuka nyuma hawakumuona tena yule myama,



    *****



    “Khaa!! amepotelea wapi?” aliuliza Masu

    “Mungu wangu hii sasa ni hatari kabisa”

    “Sasa tutafanyaje hapa Mzee?”

    “Tusubiri kufa tu, maana Usinge nao umeutelekeza kwenye Basi” wakiwa wamesimama wako hoi kwa zile mbio za bila kutarajia ndipo tena mvua ikaanza kunyesha ikabidi sasa wakimbile kwenye mti mkubwa uliokua pembeni ili wajisitiri, walipofika tu chini ya mti ule yaani kitendo bila kuchelewa Ikapiga RADI kubwa na yanguvu ikamrarua hapo hapo mzee Kishindo, akakauka na kua mweusi kama mkaaPia Radiu hiyo ikaunguza na ule mtiwaliokua wamesimama ukawa sasa unawaka moto tu! ilikua ni Radi ya hatari kisha mvua ikazidi kuchukua kasi yake, hakika Masu alikua amechanganyikiwa kisawasawa , akaanza kulia huku akiukimbia mwili wa Mzee Kishindo uliokauka kama vile ulio chomwa kwenye tanuri la mkaa, wakati masu akiwa ametaharuki ndipo tena alipomuona Yule mnyama mkali asieleweka akija tena kwa kasi inaonekana kama aliekua amewapoteza machoni pake akina Masu na Mzee Kishindo ambae tayari bila shaka ameaga dunia kwa Radi ya ajabu iliyomtandika vilivyo, Yule Mnyama

    alionekana ana ghadhabu ya hali ya juu..



    Masu akaanza kukimbia kwa kasi ya nguvu, sasa yule mnyama alikua amedhamiria kabisa kummaliza Masu, na sasa alikua akizidi kumkaribia, Masu alikua ameulenga mti mmoja mkubwa ili akifika ajaribu kukwea japo hakua na uwezo mkubwa wa kukwea miti, ila alijipa moyo kua angeweza tu bila ya kujali hata kama Mnyama huyo nae anaweza kukwea mti pia. Mnyama Yule alikua anakimbia kwa kasi kubwa kiasi sasa cha kumkaribia Masu, sasa Masu akajua kua mwisho wake umefika akaanza kulia kwa sauti kubwa sana lakini haikusaidia kitu, ilipobakia hatua kadhaa mnyama Yule amkamate Masu Masu akaongeza Speed kwa nguvu zake zote, Laa Haula!! Kumbe mbele kulikua na Shimo kubwa sana Masu hakulitambua hilo masikini! akatumbukia, lilikua ni Shimo refu kupita kiasi, Masu aliendelea kwenda chini bila kufika mwisho huku akijipigiza hovyo pembeni mwa shimo hilo bila ya kufika mwisho, hakujua kama lilikua ni Korongo au ni shimo la aina gani maana aliendelea kwenda chni bila ya kujua

    atafikia wapi na muda gani.. hatimae alianza kusikia kizunguzungu kutoka na na kasi kubwa iliyokua ikimpeleka chini na hapo ndipo sasa akaanza kujua kua halikua shimo la kawaida bali itakua ni nguvu tu ya Waufi maana sasa ilichukua takribani masaa matatu akiwa anaenda tu bila kufika mwisho wa shimo hilo na hajui yataongezeka masaa mangapi kabla ya kufika chini, Pumzi ikawa inamuishia kutokana na upepo mkali aliokua akikutana nao wakati anazidi kwenda chini

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    DAR ES SALAAM



    Nyumbani kwa Mzee Kishindo kilio kilikua kimetawala, watu wengi walikua wamejumuika, wake kwa waume, ndugu na majirani wote walikua wakilia kwa uchungu mkubwa, ni baada ya kupokea taarifa kuwa Mzee Kishindo amefariki kule Porini aliposhuka kujisaidia akapigwa na Radi kali, taarifa hizo zililetwa na Polisi baada ya kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo…

    “Jamani samahani, kwani ilikuaje?” aliuliza mzee Jfari jirani yake na Bw Kishindo, alimtupia swali hilo Sheikh Jabu aliekua tayari ameshawasili hapo msibani

    “Kwa maelezo tuliyoyapata kutoka kwa mkwewe ni kwamba Kishindo na Masumbuko yule kijana wa Mzee Kikoko walikua safarini wakielekea Tabora lakini masaa mawili yaliopita amepokea simu kutoka Polisi kua mumewe amefariki kwa kupigwa na Radi ndipo akanipigia mimi haraka nikaenda Mochwari kuutambua mwili”

    “Duh jamani mbona kama siamini vile!! Kishindo huyu huyu nilikua nae jana hapa?”

    “Ndio huyo hivyo hakuna cha ajabu hapo, kwa Mungu ni madogo hayo, ila mwili umeharibika hivyo tunasubiri tu Ruhusa ya daktari tukauchukue mwili tuje tuusitiri, cha ajabu huyo Masu aliekua nae hajulikani alipo, wanadai amepotelea hukohuko Porini, yaani hizi taarifa zinachanganya sana”

    “Hajulikani? Kivipi?”

    “Inasemekana kua Mzee Kishindo alishuka kweny Basi kwenda kujisaidia lakini akachelewa sana kurudi ndani ya Basi hivyo sasa Masu akaenda kumuangalia lakini nae hakurudi wakati huo mvua kubwa ikawa inanyesha, na kabla ya mvua kukatika ndo ikapiga Radi kubwa, mvua ilipotulia ikabidi abiria washuke kwa ajili ya kujaribu kuwatafuta, ndipo walipomkuta Mzee Kishindo akiwa amefariki kwa KUPIGWA NA Radi hiyo mpaka kakauka, Lakini Masu hawakumpata kabisa”

    “Mmh, haya sasa Maajabu’



    Masu aliendelea kwenda chini na hatimae akajikuta ameanguka kama mzigo au kifurushi, Naam Maajbu na mauzauza yameanza tena kwa Masu, kajikuta ameangukia katikati ya Zizi la Ng’ombe, cha Ajabu na yeye ni Ng’ombe pia, japo ameumia kwa jinsi alivyoanguka vibaya lakini sasa anastaajabu kujiona katika hali ile, akaanza kuhata hata, inaonekana hata wale Ngo’ombe wenzie wameshangaa kumuona pale bila shaka hawamjui kabisa, kulikua na Ng’ombe wakubwa sana, wana pembe mpaka zimejikunja kwa juu ya vichwa vyao, Masu akaanza kulia kwa woga lakini haikua sauti yake ile ya mwanzo, ilikua ni sauti mujaribu ya Ng’ombe, Ghafla akaanza kupokea kichapo cha haja kutoka kwa Ngo’ombe wenzie, Masu akawa anavuja damu kichwani baada ya kuchomwa na pembe la mmoja kati ya wale Ng’ombe waliokua waimuadhibu,,



    Masu akiendelea kujaribu kujinusuru na kichapo kutoka kwa Ngo’ombe wenzie ndipo akawaona watu watatu wakija mpaka pale kwenye zizi, akawa anasikiliza mazungumzo yao, anatamani kuwajibu lakini kila akitaka kuwasemesha sauti inatoka kama ya Ng’ombe wengine tu, hali hiyo ilimtia sana uchungu sasa ikabidi tu atulie asubiri hatma yake, huku mazungumzo ya wale mabwana yakiendelea

    “Mzee Songoro sisi ni ndugu zako na tumepatwa na msiba hivyo tunataka Ng’ombe kwa ajili ya pale msibani hivyo tufanyie tahfuf kidogo” aliongea mmoja kati ya wale vijana wawili

    “Ni kweli, hata mimi na marehem Kishindo tulikua na ujamaa pia ila hiyo be nimewatajia ni ya chini kabisa kwakua tu nawafahamu na nimeangalia uzito wa jambo lenyewe” Masu alizidi kushangaa kusikia zile taarifa kua hawa jamaa wamekuja kununua Ngo’ombe kwa ajili ya kwenda kuandaa chakula msibani kwa Mzee Kishindo, alianza kulia baada ya kuamni sasa kua Kishindo amekufa, laiki alizidi kushangaa kua yaani pamoja na kuzama kwenye lile shimo kule kumbe ametokezea tena sehemu uliko msiba, hakika alijua kua amepatikana



    Baada ya makubaliano ya muda mrefu sana hatimae wakaafikiana bei, wakalipana pesa, kisha Mzee Songoro akaingia zizini na kumkamata Masu(Ambae kwa sasa kawa Ngo’ombe) halafu akaanza kumfunga kamba, na baada ya muda ikaja gari na kumbeba Ng’ombe huyo na kumchukua mpaka msibani, Walipokua njiani Masu alishangaa kuiona mitaa ya jiji la Dar es Salaam, akajua kua kumbe amerudishwa kule kule mjini na sasa anakwenda kuchinjwa, Roho ilimuuma lakini hakua na ujanja tena na Baada ya muda akawa amefikishwa nyumbani kwa Mzee Kishindo, akateremshwa kwenye gari na akafungwa kwenye mti kwa kamba ngumu ya manila, Hali ya pale nyumbani ilithibitisha kua Kishindo hayupo tena duniani watu walikua wakilia kwa uchungu sana, Masu alimuona Sheikh Jabu, pamoja na vijana kadhaa kutoka kule dukani wanakokwenda kupiga stori, nao walikua katika majonzi na simanzi ya hali ya juu, kilichomuuma zaidi aliwaona kwa pembeni wanawe wadogo wale mapacha wakiwa wamesimama pale uani japo

    hakumuona mkewe yaani Masu alipatwa na uchungu wa aina yake aisee



    “Sasa jamani tugawane majukumu hapa haraka haraka kwakua wenzetu wameenda kufuatilia mwili, sasa sisi tungeanza majukumu mengine ya kupanga mazingira wakati wengine mkamchinje kabisa huyo Ng’ombe na mumchune kabisa” alikua ni Sheikh Jabu akijaribu kugawa majukumu pale msibani

    “Sawa ila hapa hakuna mtaalam wa kuchnja Ng’ombe, Labda mumuite Mzee Kikoko ndio hua anachinja Ng’ombe” alijibu kijana mmoja pale msibani lakini alikatishwa na Jabu

    “Mzee Kikoko hayupo ameenda kule ilipotokea hii kadhia, si mnajua mwanae kapotea ghafla huko ndio ameenda Polisi kujaribu kumtafuta”

    “Aaah sasa nani ataweza kuchinja?”

    “Ngoja nijaribu kuuliza hapo nje kwa hao waliokaa kwenye jamvi kama kuna mtu wa kuchinja” Sheikh Jabu akatoka, Masu alikua akiyasikia mazungumzo yote yale, alikua akilia kwa uchungu lakini haikusaidia kitu, alionekana kua ni Ng’ombe tu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya Muda Sheikh Jabu alirudi akiwa na kijana mmoja amevaa kofia ya kibaraghashia, bila shaka ndie Mchinjaji mwenyewe maana tayari ailiakua na kisu kikubwa mkononi, Masu alivyoinua macho AFANALEKI!! Alikua ni Hunudu Bin Waufi, Hunudu alisogea mpaka pale kwa Ng’ombe kisha akawaita wale vijana

    “Njooni basi mumfungue kamba halafu mje tusaidiane kumshika tumalize harakaharaka” Masu alikua akilia kwa uchungu kila alipojaribu kujitetea kwa Hunudu hakuweza kusikika kwa kua sauti iliyokua ikitokani ni ya Ng’ombe. Wakati vijana wale wakija Hunudu akamsogelea Yule Masu halafu akamuambia kwa manenoya chinichini

    “Kiburi na ujuaji ndivyo vinavyokuua leo, mwenzio kaisha kufa na kabla ya kwenda kumzika kwanza Ndugu, jamaa na marafiki watakula wewe nyama yako ndio tukamfukie huyo mwenzio, Pole Masu” Hunudu masikini akawa analia, cha ajabu mtoto wa Masu wa kike akawa nae amesogea pale halafu kama akaropoka

    “Huyu Ng’ombe mbona analia mpaka anatoa machozi kama mtu?”

    “Hebu toka hapa, kacheze huko” alifoka Hunudu

    *****

    *****



    SEHEMU YA TISA



    UMATI wa watu ulifurika nje ya nyumba ya hayati mzee Kishindo, wanaume walikaa mbele nyumba hiyo kama ilivyo desturi ya misiba mingi ya kiislam, na wanawake walikaa uani, Sura za waombolezaji zilisawajika vilivyo kutokana na vilio vilivyotawala muda mrefu tangu kupatikana kwa taarifa za msiba huo, Msiba huu uliwagusa wengi, wake kwa waume, na hii ni kutokana na tabia njema alizokua nazo mzee huyu, Mzee Kishindo alikua ni msemaji, mchangamfu, na mcheshi sana, alikua na moyo wa upendo, wengi amewasaidia pale mtaani si kwa pesa basi hata kwa ushauri wake wenye busara, Wengi walihuzunika sana na kubaki na maswali kichwani juu ya utata ulio kigubika kifo cha mpendwa wao, Kifo chenye utata, Kifo cha kutisha, Kifo cha kuhuzunisha..



    Vijana wengi walikua wamekaa katika vikundi vidogo vidogo wakijaribu kupeana mkasa mzima ulivyokua maana kama ilivyo desturi ya jamii nyingi ‘Apatwae na mkasa hupatwa na visa’, Tayari habari zilishajulikana kua marehemu alikua akienda Tabora kwa ajili ya kumpeleka Masu kufanyiwa matambiko kwenye Mizimu ya mama yake (japo hilo nalo liliwaumiza vichwa wengi tu kwakua mama yake Masumbuko wamjuao wao ni mwenyeji na mzawa wa hapohapo Shinyanga) kutokana na kusumbuliwa sana na mizimu, pia walikua wameshapata taarifa za tukio la kifo hicho kule Porini, pia habari kwamba Masu ametoweka kabisa hukohuko porini zilizidi kuwaacha vinywa wazi. Kila mtu alikua akisema lake, kila mtu alikua ni msimuliaji, hakika msiba huu ulizigusa hisia za wengi

    *****



    Pembezoni mwa nyumba ya Mzee Kishindo walikua wamesogea vijana kadhaa wakimfunga kamba Yule Ng’ombe kwa ajili ya kumchinja, hakuna aliejua kua Ngo’ombe Yule hakua Ngo’ombe wa kawaida bali ni binaadamu, tena wengine ni swahiba wao wa karibu, ila kutokana na kiini macho kilichofanywa na Mzimu wa Waufi alionekana kama ni Ng’ombe tu kumbe ni Masumbuko, Baaada ya kumfunga kamba vizuri Hunudu akajongea na kisu chake kikali kwa ajili ya kumaliza zoezi la kumchinja Masu/Ng’ombe lakini kutokana na nguvu za mnyama huyu ikabidi na vijana hawa waendelee kumshika ili achinjwe vizuri, wakati zoezi hili la kinyama na kuhuzunisha likiendelea Mtoto Fani, mtoto wa Masu aliekwenda msibani hapo na mama yake alionekana kuvutiwa na tukio lile kila mara alisogea japo alifukuzwa akacheze pembeni lakini aliendelea kung’ang’ania kukaa eneo lile, na kabla hajachinjwa Masu mwanae huyu akalopoka

    “Kwanini mnamchinja Baba yangu?” Swali hili kutoka kwa mtoto huyu liliwashangaza wale vijana wakajikuta wanamuangalia wote kwa pamoja kila mmoja akiwa kama ameshangazwa na swali lile

    “Baba yako yuko wapi?” aliuliza kijana mmoja akiwa katika hali kama ya mzaha maana aliamini kua yale maneno yalikua ni ya kitoto tu, ndipo mtoto akaendelea

    “Basa si huyo mmemfunga kamba” baada ya jibu hilo, Masu alijisikia uchungu kupita kiasi kuona mwanae amemjua, Masu akashindwa kujizuia kaanza kulia kwa sauti akiamini labda angesikilizwa lakini sauti iliyotoka kinywani mwake ilikua ni mlio tu kama wa Ng’ombe wengine, Masu alihuzunika sana. Haraka Hunudu akamfukuza Yule mtoto

    “Hebu nenda ukacheze huko pembeni”

    “Namtaka baba yangu” Fani alipojibu tu kua anamtaka baba yake hapohapo akajipenyeza na kumng’angania Yule Ngo’ombe asichinjwe

    “Hebu mtoeni huyu mtoto jamani tufanye kazi” Hunudu aliwaambia wale viajana waliokua wamemshika Yule Ng’ombe lakini vijana hawa walionekana kama kutomsikiliza sana Hunudu, tukio lile japo lilifanywa na mtoto mdogo lakini lilizivuta hisia za vijana wale, ndipo mmoja kati ya vijana wale akauliza

    “Kwani huyu ni mtoto wa nani??”

    “Ni mtoto wa Masu” alijibu kijana mwingine

    “Mmh jamani hapa kuna kitu”

    “Kuna kitu gani sasa? Yaani mambo ya watoto ndio yatukwamishe hebu acheni ujuha nyie” Hunudu alijikuta anashindwa kuzificha hisia zake na kuanza kuongea kwa ghadhabu



    Wakati hayo yakiendelea, upande wa mbele ya nyumba uliingia msafara wa gari kama kama tatu hivi zikiwa zimeandamana huku zimewasha taa, kila mtu akageuka kuangalia, ilikua ni Maiti ya Mzee Kishindo ikiingia ndani kutokea Hospitali ilikofikishwa kwa ajili ya taratibu za kitabibu, watu wote walisimama kuupokea mwili huo, ikabidi sasa hata zoezi hili la kuchinja Ngo’ombe/Masu lisitishwe kidogo kwa muda ili vijana hawa wakaungane na wenzao kwenda kuupeleka mwili ndani , vijana wakajumuika pamoja na vijana wenzao waliokwenda kuuchukua mwili hospitali, wakafika pale kwenye zile gari, wakaupokea mwili wa hayati Bw Kishindo ukiwa umelazwa juu ya Machela huku umefunikwa na shuka za hospital, wakaushusha kwenye gari, wakaubeba vizuri kwa pamoja kisha wakaanza kuingia nao ndani, Wanawake walikua wamejaa pale sebuleni, wote wakasimama kuonesha ishara ya utii na nidham wakati maiti inaingizwa ndani, wanaume waliokua wameubeba mwili ule wakakatiza mpaka upande wa

    kushoto ndipo kilipokua chumba cha marehemu wakaingia na mwili mpaka mule ndani. Chumba kilikua tayari kimeshasafishwa na vitu vyote vilikua vimeshatolewa nje, kulikua na kabati moja tu kubwa liligeuzwa ukutani, na kitanda cha kamba kwa ajili ya kuoshea maiti



    Wakati wanaume wakiendelea kuuweka mwili vizuru kule chumbani, huku Sebuleni sasa wanawake wakaanza kulia kwa sauti huku wakiomboleza kwa maneno yaliyozidisha hisia kali za kuondokewa na mtu muhimu sana, Mke wa hayati Kishindo nae alishindwa kabisa kujizuia, alikua analia kwa sauti mpaka anaishiwa nguvu kabisa, kina mama wenzie wakawa wanajaribu kumbembeleza huku wakimpepea nakanga zaokutokana na joto la mule ndani ambalo lilimfanya atokwe na jasho sana, Ghafla Mama huyo akapandisha majini kichwani, akawa sasa ana nguvu za ajabu, nguvu zinazowazidia wanawake wenzie, alikua akitaka wamuachie, aingie chumbaniCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Niachieniiii, nasema niachieni, Mume wa kiti wangu hajafa kabisa, Waufu manataka kumchukua Kishindo, nasema tutapambana mpaka mwisho” Maneno hayo ya Bi mkubwa Yule yalizidisha taharuki mule sebuleni, ikawa ni mkanyagano tu, wengine waoga wakaanza kutoka uani kabisa, lakinikina mama majasiri waliendelea kumzuia huku wakiomba msaada kwa wanaume maana sasa alianza kuwazidi nguvu,

    “Tulia basi kwanza utueleze tatizo ni nini” aliongea bi mkubwa mmoja aliekua amejitahidi kumzuia mjane wa mzee Kishindo

    “Huyo ndani sio Kishindo, ni mzoga tu huo, utoeni njeeee, nakuja kusaidia mume wa kiti, Kiti wangu hawezi kudhalilishwa mbele yangu” Watu walihamaki kusikia maneno haya, sasa Msiba ukazidi kunoga kwa taarifa za ajabu kila abaada ya muda mfupi, Wanaume wakaja mpaka pale sebuleni kusaidiana na kina mama ili kumtuliza mke wa Kishindo, pia ikabidi waingie ndani mashehe wataalamu wa masuala ya majini, wakaanza kumsomea dua mbalimbali ili atulie lakini wapi ikasindikana, Dua ziliendelea kwa muda mrefu bila kukata tamaa mpaka hatimae Mama yule akatulia sasa, Bila shaka jinni lilikua limeruka, Sebule nzima ikawa kimya, Bi mkubwa huyo akaanza kupepesa macho huku na huko alionesha kua ahakua akijua chochote kilichokuakikiendelea pale, akajikuta tu anauliza

    “Kuna nini?”

    “Hakuna tatizo shemeji, Presha ilitaka kukuzidia” Sheikh Jabu kwa hekma sana, baada ya Bi Mkubwa kutulia, watu wakatoka nje ili kuendelea na majukumu mengine pale msibani huku hofu ikizidi kutawala zaidi



    Nje ya nyumba kila mtu alikua ameingiwa na baridi ya uoga na hofu, vikazuka vikundi vya majadiliano

    “Hiki kifo kina utata wa hali ya juu sana kila kitu kama sinema vile” Mzee mmoja jirani wa karibu wa marehemu, aitwae Kabango alikua akiongea na wanaume wenzie nje ya nyumba ya Kishindo

    “Mie hata huyo ng’ombe nimeshamtilia mashaka, hata mkimchinja mie sitokula” alijibu mmoja katika wale vijana waliokua wanajiandaa kwenda kumchinja Ngo’ombe

    “Kwanini tena?”

    “Sisi tunaona ni Ng’ombe halafu mtoto anamuona baba yake, halafu baba yake mwenyewe nasikia ndio aliepotelea huko porini”



    “Mbona sijakuelewa kijana, hebu nieleweshe kwa kituo..” wakati stori zikizidi kutamalaki wakakatizwa na Sheikh Jabu aliesogea pale na kuongea harakaharaka huku akijiandaa kuondoka

    “Sasa Bw Kabango mimi ninaondoka sasa hivi naenda Kituo cha polisi kumtoa Mama Masu mke wa Bw Kikoko si unajua yuko ndani?”

    “Hapana sina habari, amefanya nini tena?”

    “Kuna matatizo yaliotokea sasa askari wakawa wanamtafuta mumewe hivyo walivyomkosa ndo wakamkamata yeye, hivyo naenda kumtoa huko”

    “Mhh haya sawa Kaka yangu, kwahiyo Kikoko yuko wapi?”

    “Kikoko alikua ameenda huko ilipotoke ajail hii ya radi, maana mwanae nae ametoweka hukohuko, lakini taarifa mbaya zaidi nilizozipata ni kwamba hali ya Bw Kikoko imekua mbaya, na hivi sasa amepumzishwa katika hospitali moja pale Dodoma Sijajua ni Presha au ni nini! hivyo nikashamtoa mkewe tu huenda nikaondoka nikamuangile huko Dodoma hata maziko nadhani sitashiriki”

    “Sasa Sheikh Jabu wewe ndio kinara hapa utakapoondoka itakuaje?”

    “Hakuna kitakachoharibika, utabaki wewe kwa niaba yangu” Hapo hapo Sheikh Jabu akaondoka akiwa anaonekana kuzidiwa na majukumu kichwani, kapanda pikipiki yake na kisha akaondoka..



    Hunudu alikua amesimama karibu na Ng’ombe/Masu kwa ajili ya kutekeleza zoezi la uchinjaji, hakika Hunudu alikua amemshupalia hasa kijana mwenzake, na kama alikua ametumwa na hao waufi basi alieetendea haki mizimu yao, vijana walisogea kushirikiana kumshika Yule Nng’ombe, Masu/Ng’ombe alilia kwa sauti kubwa ya uchungu ambayo iliotoka kama ilivyo kwa Ng’ombe wengine wanaokua machinjioni, Hunudu akasogea na kisu chake kisha akamshika kichwa na kuibinua shingo kwa juu, Koromeo likawa liko mbele likisubiri kisu

    Wakati Hunudu ndo ananyanyua kisu achinje ghafla kikazuka kimbunga kikubwa sana, Kimbuka kilichoambatana na upepo mkali kupita kiasi, vumbi likatinga vilivyo eneo lile, watu wakainuka na kujificha sura zao kuhofia mchanga kuwaingia machoni, wengine walijigeuzia kwenye kuta za nyumba ili kuupisha upepo huo mkali upite, Kimbuka hiki hakikua cha kawaida kabisa maana kilichukua muda mrefu eneo moja tu pale pale msibani, mpaka baada ya dakika kama tano kimbunga kikaisha na kutoweka kabisa, vumbi likapungua, watu wakawa wanajifuta mchanga machoni, Vijana waliokua wameinama kumshika Ngo’ombe nao walikua wamesambaratika kwa Kimbunga kile kilichoacha gumzo pale msibani, baada ya hali kutulia watu wakarudi kukaa kwenye majamvi na wachinjaji nao wakarudi kuchinja, Hunudu alionekana kubadilika sura yake kwa jazba, ni kama vile ameshagundua kua hali haikua ya kawaida kabisa, Vijana wakasogea na kumshika Ng’ombe tena kwa mara nyingine ili achinjwe, sasa awamu hii

    hata kabla Hunudu hajainama na kisu chake Kikazuka tena Kimbunga kikali kuliko kile cha awali, watu wakataharuki tena, kama ilivyo kawaida ya Vimbunga hua vinazunguka kwa mtindo wa duara huku kikihama sehemu moja kwenda nyingine, basi Kimbunga hiki kikahama na kusogea mpaka kule anapotaka kuchinjwa Ng’ombe/Masu kikazunguka eneo lile mpaka wachinjaji wakasambaana kisha Kikafuatiwa na Tetemeko kubwa sana la ardhi, baada ya sekunde kadhaa kimbunga kikasambaa kwa kuelekea juu!!!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    TOBAA!!



    Kimbunga kikampita Ng’ombe na kupeperuka nae juu ya anga, baadhi ya watu waliokua wamefumbua macho yao walishuhudia tukio lilela ajabu na la kuogofya sana, wakajaribu kuoneshana juu kabisa jinsi Kimbunga kinavyoondoka na Ng’ombe mzima, watu wakaanza kukimbia kwa woga, hakuna alieamini tukio lile la kustaajabisha, na baada ya sekunde chache hali ikatulia na upepo ukapoa na kurudi kama ilivyokua mwanzo, Kina mama wengi walitoka uani mpaka barabarani kuja kushuhudia kilichotokea kufuatia kelele zilizokua zikiendelea huku Barabarani

    “Imetokea nini?” Aliuliza Bi mkbwa mmoja wa makamo hivi

    “Tangu nizaliwe mpaka natoka mvi zote hizi sijawahi kushuhudia muujiza kama huu” alijibu mzee Kabango huku akiwa bado anaangalia juu ambako Kimbunga kimepotelea huko

    “Nini hasa kimetokea sasa?”

    “Ng’ombe amebebwa na kimbunga kimemchukua na kupotelea nae juu”

    “Maajabu haya jamani” kila mtu alieshuhudia tukio lile alikua akiwasimulia vijana wenzie alichokiona

    “Hapa kuna kitu tu sio bure, haiwezekani kila tukianza tu kumchinja Yule Ng’ombe kinazuka kimbunga, mara kimeibuka na kumpitia kabisa ng’ombe” alisema mmoja kati ya wale viajana waliokua wameinama kwa ajili ya kumshika vizuri Yule ng’ombe

    “Halafu jamani si mnakumbuka Yule mtoto aliekua analia anasema tusimchinje baba yake, sasa ndo naanza kupata picha kamili”

    “Halafu baba yake na huyo mtoto ni Masu huyu aliekua na marehemu huko porini na amepotea hukohuko”

    “Jamani hapana, hili sio jambo la kufumbia macho”



    Judith, mke wa Masu alikuwepo pale nje akisikiliza mkasa mzima hivyo akawa analia kwa uchungu mkubwa baada ya kuanza kupata picha kuwa inawezekana ni Mume wake huyo aliekua anataka kuchinjwa

    “Kwani huyo Ng’ombe mlimnunua wapi?”

    “Mimi hata sijui alinunuliwa wapi, itakua ni machinjioni tu” Watu walizidi kumiminika pale msibani, wengine walikua wanatokea maeneo ya mbali sana, nao walifika kufuatia kusambaa kwa taarifa hiyo ya ajabu kua Ng’ombe amebebwa na Kimbunga, Wazee wenye hekma walijitahidi kuwatuliza watu na kujaribu kuwafanya walichukulie lile jambo ni la kawaida tu ukizingatia pale ni msibani na hata maiti angali hajahifadhiwa bado, japo ilikua ngumu kueleweka ila kwa kiwango kidogo walijitahidi kuituliza hali ile na watu wakarudi kwenye utulivu uliokuwepo, japo stori zilizoendelea kutawala ni hizo tu

    *****



    Nje ya kituo cha Polisi cha Msimbazi alikua amesimama Sheikh Jabu akiwa amefanikiwa kumuwekea dhamana mke wa Mzee Kikoko, na sasa alikua akimpa habari zote za Mkasa wa Masu na kifo cha Mzee Kishindo, Japo mama huyu hakuonesha kushtuka kabisa kutokana na habari hizo, zaidi mama huyu alikua akiulizia hali ya mumewe tu

    “Kwahiyo huko Ddodoma unaenda na nani?”

    “Ninaenda peke yangu, we nakuchukulia bodaboda uende nyumbani ukaoge halafu uwahi msibani”

    “Hapana mimi sitakwenda huko msibani kabisa”

    “Shemeji kwanini usiende, hivi hauoni utaleta picha mbaya sana kwa jamii?”

    “Hapana Sheikh Jabu, kumbuka kwamba ni majuzi tu marehemu aligombana na mume wangu nasikia mpaka wakapigana na mikia ya taa, halafu Mzee Kishindo ameng’ang’ania kumlaghai Masu, na sasa amefariki katika mazingira ya utata hivyo naweza kufika pale nikaonekana mimi ndio muhusika”

    “Kwanini ujishuku kua umehusika, Shemeji jaribu kujifikiria mara mbili” Baada ya majibizano hayo wakaagana Sheikh Jabu akaenda kutafuta gari ya kumpeleka Dodoma kumuangalia swahiba wake na huku mke wa Kikoko akachukua bodaboda iliyompeleka moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Sheikh Jabu ambako ndiko alikofikia

    *****





    AKIWA njiani kuelekea stand ya mabasi ya UBUNGO kwa ajili ya kuangalia kama ataweza kupata usafiri wa gari ndogo inayokwenda Dodoma, simu yake ikaita, kwakua alikua barabarani na anaendesha pikipiki hivyo hakujishughulisha kuipokea wala kuingalia, lakini mtetemesho aliouweka kwenye simu yake hiyo wakati wa muito ulimtoa katika umakini wa uendeshaji akajikuta anakosa utulivu kabisa, na kwakuhofia kusababisha ajali ikabidi apaki pembezoni mwa barabara ili aiangalia simu yake apate kumtambua huyo anaempigia simu, alipoitoa simu yake na kuiangalia ilikua ni namba mpya, akabonyezo kitufe cha kupokelea kishaakai lengesha spika ya simu hiyo katikati ya sikio lake la kushoto

    “Hallo..”

    “Sheikh Jabu?...” ilikua sauti ngeni kidogo kwake, hakuweza kuitambua vema

    “Naam, ni mimi, we nani?”

    “Mzee Kabango hapa naongea”

    “Ndio Bwana mkubwa, kuna usalama?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hakuna usalama, uko wapi sasa hivi?”

    “Mie niko njiani naelekea Stand ya mkoa, mbona unanitisha?”

    “Fanya hima urudi kaka, mambo yameharibika huku”

    “Bwana Kabango, nilikuambia tangu mwanzo kua jukumu la hapo nyumbani ni la kwako sasa mimi nije kufanya nini tena! Hapa najitahidi kumuwahi Bwana Kikoko hali yake ni mbaya huko”

    “Najua hilo, lakini mpaka nimekupigia ujue maji ya yametufika shingoni, Chondechonde fanya hima uje kila mtu anakusubiri wewe hapa” Simu ikakatwa ghafla na kumuacha Sheikh Jabu akibaki njiapanda asiejua pa kwenda, Hali ya Kikoko ilizidi kumtia hofu, huku msibani nako kuna umuhimu sana, alitafakari kwa kina mwishowe akaamua kurudi tu kule msibani ili akapate taarifa ya kilichotokea

    *****



    Huko msibani watu sasa walikua wametulia kidogo, utulivu ulirudi katika hali yake, na sasa watu wote waiofurika kuja kuangalia ule muujiza wa Ng’ombe kubebwa na Kimbunga walianza kusambaa na kuifanya idadi ile ya mwanzo ya wafiwa kurudi kama ilivyokua awali, Hunudu alitoweka katika mazingira ya ajabu sana kiasi cha kuacha maswali kwa watu wengi pale msibani maana kila walipomuangaza hawakumuona tena, na hata hivyo hakuna aliekua akimjua pale msibani. Pikipiki ya Sheikh Jabu iliingia pale msibani na haraka haraka akaigesha chini ya uga uliosukwa vizuri kwa nyasi kisha akajongea mpaka pale kwenye Jamvi kubwa la rangi ya kijivu, Baada ya kuwasalimu aliketi chini na kumfanya sasa Mzee Kabango aliekua amejilaza kama mtu aliekimbia kilometa kadhaa ainuke na kuketi huku wakiwa wametazamana

    “Naam bwana mkubwa nimetika wito..” Baada ya Sheikh Jabu kufungua mazungumzo mzee Kabango alikohoa kidogo nae akaanza kushusha mtiririko wa kisa kizima kilivyokua mpaka mwisho, Kisa hiki kilimuacha mdomo wazi Sheikh Jabu, licha ya ujasiri ambao hua ndio vazi lake kuu lakini kwa hili aliingiwa na baridi ya hofu, watu kadhaa walijisogeza karibu pale kujaribu kuchangia mada

    “Huyo aliyekua mchinjaji yuko wapi?”

    “Ametoweka tu na hakuna aliemuona wakati anaondoka”

    “Mnajua kweli huyo?”

    “Hapana ila cha ajabu wakati tunataja wajih wake kuna Binti mmoja alishutuka sana akasema kua anahisi kumjua huyo mtu”

    “Ni nani huyo binti?”

    “Wanamuita Mama Zani..”

    “Mmh Judith? Mke wa Masu?, Amemjuaje?”

    “Anadai kua mumewe alikua akisumbuliwa sana kwenye Ndoto ya ajabu, na katika sifa za huyo mtu aliekua akimuota kila siku ndo huyo kijana mwenye Jicho bovu, sasa ukijumlisha na utata wa hili tukio la leo ndo kabisa ameamini” Kisa hiki hakika kilizidi kuacha maswali mengi yasiyo na majibu, Lakini kwa Hekma na Busara ikabidi Sheikh Jabu awatulize watu pale msibani kwa kuwanasihi kwa maneno ya busara sana mpaka wakatulia, akawaomba kwanza washirikiane kulimaliza suala la mazishi halafu hayo mengine yatapata muda wa kutosha wa kuyajadili, watu walimuelewa na sasa Shughuli za kuandaa mazishi zikaendelea kama kawaida, Ikabidi sasa bila ya kupenda Sheikh Jabu asisafiri tena na badala yake abaki pale nyumbani ili kukabiliana na matatizo yatakayojitokeza



    Ilipotimu saa tisa alasiri watu walikusanyika nje ya nyumba ya Mzee Kishindo kwa ajili ya kufanya Ibada ya visomo maalum kama dua ya mwisho kwa marehemu wao, hakika watu walikua wengi kuliko kawaida, bila shaka wapo waliohudhuria kutokana na uvumi tu uliojitokeza wakati wa tukio lile, Naam Dua zilifanyika kwa ukimya na utulivu mkubwa tofauti na misiba mingine, Hatimae Mwili wa marehemu ukawekwa ndani ya Jeneza tayari kwa ajili ya kuswaliwa kisha kwenda malaloni kumuhifadhi.. Ikafanyika Sala ya Maiti iliyoongozwa na Sheikh Jabu mwenyewe, mbali ya ukaribu wake na marehemu pia Sheikh jabu alikua ni msomi mzuri tu na mjuvi wa masuala dini, Baada ya kumaliza swala hapakua na cha ziada tena maana hata chakula hakukuandaliwa tena tangu Ngo’mbe apotee ghafla, hivyo wanaume wakanyanyua Jeneza na kuliweka katikati ya mabega na shingo zao kama ilivyo kanuni na taratibu za ubebaji wa Jeneza, na safari ya mwisho ya hayati Kishindo ikawa inakaribia kufikia tamati

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Makaburini hapakua mbali sana na nyumbani hivyo safari ya mwendo wa miguu tu ilitosha kuwafikisha katika viwanja hivyo vya makaburi ndani ya muda wa kama nusu saa hivi, na taratibu zote za mazishi zikafanyika na hatimae Kishindo akazikwa, ilikua ni huzuni na vilio kila kona, vijana kwa wazee walishindwa kuzificha huzuni zao na kuangua vilio hukohuko makaburini, hapakua na Jinsi tena maana neon la Mungu limetimia, Wafiwa na ahali zao wakarejea nyumbani baada ya kumalizia dua ya mwisho katika kaburi la Marehemu Kishindo



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog