Search This Blog

VAMPIRE NUSRATY - 1

 





    IMEANDIKWA NA : HAFIDHI J IKRAM



    *********************************************************************************



    Simulizi : Vampire Nusraty

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yapata majira ya saa mbili usiku nikiwa naelekea msikitini kuswali,

    Ghafla moyo wangu ukaingiwa na hofu sana baada kufika sehemu yenye. Mbuyu mkubwa sana hakika sehemu hiyo inatisha na kuogopesha yani ukipita utahisi kama tumbo linacheza.

    Nikapita mbiombio

    Mpaka msikitini nikiwa nahema nikatia udhu kisha nikaswali

    Nikasikiliza mawaidha kutoka kwa, kwa Shekhe Yusuf ndio imamu wetu wa msikiti,

    Sasa ukafika muda wa waumini kutawanyika kurudi majumbani kwao.

    Nikatamani niongozane na watu hata wawili

    au mmoja ili niweze kukatiza eneo lile kwa Amani, ajabu hakuna hata mtu mmoja

    anaepita maeneo yale nikabaki kuwaza na kuwazua tu.

    ghafla nikaguswa begani na Shekhe Yusuf akaniuliza,

    “Hafidhi vipi mbona waumini wote washaenda majumbani kwao wewe mpaka saa hizi inakwenda saa nne upo tu hapa?"

    Nikamtizama Shekhe wangu usoni kisha nikamjibu.

    “Hakika moyo wangu umejawa na hofu sana naogopa kwenda nyumbani peke yangu sababu ya ule Mbuyu pale",,,,,

    Shekhe Yusuf akatabasamu na kusema

    “Hafidhi kumbuka kile ambacho unafundishwa na Walimu wako hutakiwi kuwa na hofu na kitu chochote kile zaidi ya Allah (s.w.t)

    Usiogope Majini wala Mashetani hakika wao ni viumbe dhaifu sana mbele yako, nenda nyumbani. Kijana!"

    Basi nikatoka msikitini nikiwa na nguvu mpya kabisa

    Nikapiga hatua kuelekea nyumbani.

    Hatimae nikafika eneo lile la mbuyuni Kidume nikakaza uso nikapita huku nimekunja ngumi

    Ajabu nikaweza kumuona mtu akiwa kajiinamia huku akilia tena kaegemea ule Mbuyu,

    Nilistuka sana,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikatamani nitoke mbio ila nafsi ikaniambia usikimbie...."

    Nikajiuliza maswali pasipo kupata jibu

    “hivi huyu ni nani,,,,,anafanya nini hapa usiku wote huu?

    Kidume nikapiga moyo konde niende kumuuliza nikaangalia kulia na

    Kushoto hakuna mtu hakika kulikuwa kimyaa sauti ya kwikwi kutoka kwa yule binti ilisikika tu

    Nikamsogerea,,,,,

    Japokuwa hofu ilinitawala nikajikaza kiume nikamgusa begani huku

    nikimuuliza,

    “Wewe nani?"

    Yule binti akastuka na kutaka kama kukimbia hivi hata mie nilistuka.

    Akaniangalia usoni na kujifuta machozi kwa kutumia viganja vyake vya mkono,

    Nikamuuliza tena kwa sauti ya upole zaidi

    “Wewe nani mbona upo peke yako sehemu hatari kama hii je huogopi?"

    Akatingisha kichwa kwa sauti ya kwikwi akanijibu,

    “Hapana kaka yangu siwezi kuogopa kitu chochote kile hakika maisha yangu hayana thamani tena,

    Dahaa sauti ya huyu binti ikanimaliza kabisa, yani sauti nyembamba utafikili kinanda au Ndege aina ya Chiliku,

    Nikampa mkono

    Japokuwa ni haramu kushikana mikono na Mwanamke asiekuwa halali yako Hafidhi nikajikuta nasahau hilo

    Binti nae akanishika.

    Nikamsaidia kunyanyuka pale chini,

    Binti akayumba kidogo kisha

    nikamwambia,

    “Naomba tuondoke haraka sana eneo hili maana sio eneo salama kwa sie kuwepo hapa!"

    Binti akatikisa kichwa kukubaliana nami basi tukaondoka

    Niliweza kumthaminisha baada kukatiza sehemu zenye mwanga wa taa hakika binti ameumbika si mchezo

    Muda wote tulikuwa kimya huku tukipiga hatua za kutembea.

    Nikavunja ukimya kwa kumuuliza,

    “Samahani Dada yangu kwanza unaitwa nani unaishi wapi?"

    Dahaa binti akatabasamu na kunijibu jamanii sauti sasa

    yenye kumtoa nyoka pangoni akajibu,

    “Naitwa Nusraty Nassoro naishi hapo mtaa wa pili tu kwa Mzee Cheche!"

    Nikadakia

    “ohoo hakika unajina zuri sana kama ulivyo wewe mwenyewe mimi naitwa

    Hafidhi j ikram naishi kwenye ile nyumba yenye chuping nyekundu,"

    Akasema.

    “ohoo kumbe tumepishana mitaa tu wewe si upo karibu na yule Mzee ndevu za bati?"

    Nikaitikia,

    “Ehee huyo ndevu za bati ni mjomba Angu,"

    Nusraty hakika nilitamani kumsikia akiongea kila sekunde au kila dakika mtoto anasauti tamu

    isiyokwisha hamu kila muda anatabasamu dahaa,,,,,,,"



    Japokuwa ilikuwa Usiku tena gizani niliweza kumsaminisha Nusraty kwa jinsi alivyoumbika,

    Nikamuuliza swali ambalo alichelewa kujibu.

    “hivi Nusraty binti mrembo kama wewe ni kitu gani kilichokusibu mpaka ukafikia hatua ya kwenda kukaa peke yako sehemu ya hatari kama ile?"

    Ukimya wake ukanifanya niongee zaidi

    “Unajuwa ile sehemu ni mbaya sana kwanza kuna Majini Wachawi na

    Mashetani pia,

    Nusraty akacheka na kusema

    “ha!ha!ha!ha!

    Hafidhi bwana embu wacha kunichekesha kwani wewe unaogopa Jini au Shetani?"

    Nikamjibu

    “Wee tena kama itatokea siku nikaonana na Jini ana kwa ana nahisi nitakufa hapohapo",,,,,,,,

    Nusraty akazidi kucheka hakika nilipenda aendelee kucheka tu,

    Akaniuliza

    “Kwani majini ndio viumbe gani na Shetani kiumbe gani?"

    Nikamjibu kwa vile nilivyo fahamishwa madrasa.

    “Binafsi Allah aliumba viumbe vyote sijui wanyama mimea mirima bahari wadudu ndege majini kila kiumbe, akaweza kukaa karne kwa karne ndipo tukaumbwa sisi Binaadamu

    Kwa jambo moja tu kumuabudu yeye,

    Binafsi Shetani hakuumbwa jina laCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shetani ni kama laana aliyopewa Ibirisi baada kukataa kumsujudia Baba yetu Adam (a.s)

    Kumbuka hata binaadamu anaweza kuwa Shetani kutokana na matendo yake hayampendezi Allah (s.w.t)

    Baada kumwambia vile

    Nusraty akasema

    “Hapo nimekuelewa nashukuru sana kwa mawaidha yako wacha nirudi nyumbani!"

    Nikapeana nae mikono ishara ya kuagana.

    Nikarudi zangu nyumbani nikiwa nina furaha ajabu

    Kila hatua ninayopiga nakenua meno tu, baada kufika nyumbani

    nikamkuta Baba amekaa kibarazani akisoma gaazeti.

    Unajuwa muda mwingine kuna vitu vinachekesha sana

    Siku zote Baba kusoma gaazeti mpaka usiku tu.

    Nikampita kimya kimya kumbe mwenzangu keshaniona tokea nakuja

    Akanistua kwa kuniita

    “Wee kenge blue kuja hapa!"

    Nikageuka na kwenda kumsikiliza Baba nini anataka kuniambia,

    “Hivi hapa ulipopita umeona gogo au?"

    Sikuweza kujuwa nimjibu nini

    Nikabaki kimya ni kweli tokea Asubuhi Baba sikuonana nae

    Akaniambia

    “Kama umeona gogo haya nenda zako

    Mtoto mpumbavu sana wewe

    Kisa cha kumuweka roho

    juu mama yako ndio nini kila muda anakuulizia wewe tu, ehee ulikuwa wapi muda wote huu?"

    Nikamjibu

    “unajuwa Baba mimi nashangaa sana kwani Mama hajui kama mwanae nilienda msikitini au?"

    “Sasa hilo swali kamuulize Mama yako yupo sebureni hapo binafsi mie

    hataa sina haja na wewe!!!

    Nikaingia zangu ndani nikamkuta Mama anaangalia TV.

    Nikamsalimia japokuwa muda wote nipo nae hapa nyumbani tofauti na Baba akitoka saa kumi na moja alfajili akirudi usiku saa tatu,

    Assalamu alaykum",,,,,,,,

    “Waaleykum ssalam yaa ibnaiyaa

    vipi tena Hafidhi yani huko msikitini mpaka saa hizi msikiti gani huo na kulikuwa na nini?"

    Mama aliuliza maswali mfurulizo,

    Nikamjibu

    “Unajuwa Mama mie kupita pale mbuyuni naogopa kwahiyo nikawa navizia mtu yeyote Apite uelekeo ule ndio namie nipite,,,,,,"

    “Mmh inamaana Mwanaume mzima unaogopa kupita pale kwenye mbuyu

    Wakati Dada yako kila siku anapita tena aogopi chochote kile",,,,,

    “Mama bwana wee unasema tu hujui chochote kile

    Kwanza njaa inaniuma mie!"

    Binafsi Mama ananipenda sana kupita watoto wake wote maana kwetu tumezaliwa watoto wanne

    Nikiwa wakiume peke yangu binafsi mpaka hapo ushanipata nina madada wangapi,

    Mama akaniambia chakula kipo kabatini.

    Nikaenda kabatini kuchukuwa hotpot

    Nikajisevia.

    Baada kula nikaenda kuoga pamoja na kutia udhu,

    Siku zote Muislamu wa kweli lazima alale akiwa katia Udhu.

    Maana huwezi kutambua kama kesho utaweza kuamka

    Jikabizi kwa mola wako haliyakuwa ukiwa msafi

    Nikasoma (Ayatur kursiyu) mara tatu

    (Surat Yasin) nilisoma mpaka aya ya tano kisha nikamalizia sura kadhaa kwenye juzuu Amma, nikalala haliyakuwa tayari

    Nimejikabizisha kwa Allah (s.w.t)

    Hakika yeye ndio muweza wa yote.

    Kesho yake Asubuhi baada kutoka kuswali swalat Subuhi

    Laiti ningekuwa naenda msikitiniCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alfajir peke yangu nisingeenda ningeswalia ndani kizuri zaidi naongozana na Babu mmoja hivi,

    Baada kumaliza kufua nguo zangu nikaitaji kwenda nyumbani kwa kina Nusraty.

    Binti niliyekutana nae jana usiku,

    Nikamuaga Mama natoka kidogo akaniambia

    “haya Baba kumbuka uwahi kurudi huko uendako"

    Nikatoka moja kwa moja mpaka nyumbani kwa kina Nusraty

    Nikamkuta Nusraty akiosha vyombo

    Nikampa hi ajabu hakunichangamkia

    Akaniangalia kwa jicho kali kisha akasonya na kuendelea kuosha vyombo,

    “Assalam alaykum

    Yaa Ukhty.....Nusraty?"

    Si akaniuliza,

    “Hivi wewe kaka chizi au maana unamsalimia sijui Nusraty huyo Nusraty yuko wapi hapa?"

    Nikabaki kuduwaa na kumjibu

    “Nusraty si wewe hapo kwani ukumbuki kama Jana nilikuona ukiwa unalia pale mbuyuni!!!

    Kabla sijaongea zaidi akatokea Mama mmoja kutoka ndani ya nyumba ile

    Huku akiita

    “Wee Hasina",,,,,,,

    Yule binti akaitikia

    “Abee Mama!"

    Nikabaki kujiuliza mara mbilimbili ina maana huyu sio Nusraty au

    ile Jana kanidanganya jina au?

    Yule binti akamwambia Mama yake

    “Mama eti huyu mkaka ananiita Mimi Nusraty,,,,

    Nikaweza kumuona yule Mama akiwa kama kastuka hivi kisha akasema

    “Hasina mwanangu inawezekana kakufananisha na Dada yako Nusraty..."

    Maana mmefanana sana!"

    “Lakini Mama mbona Dada kafariki muda tu yapata miaka minne sasa,

    Ile kauli aliyoitoa Hasina ikanifanya nishituke kumbe

    Nusraty ni marehemu sasa mbona Jana nimemuona,



    Niliondoka pale nikiwa najiuliza maswali chungu mzima,

    maswali ambayo yalikosa majibu.

    “au nimekosea nyumba nini,,,

    itakuwa Nusraty aishi pale sasa kama aishi pale mbona Hasina kasema Nusraty kafa tokea miaka minne iliyopita?" Dahaa

    binafsi ni kweli sie wageni maeneo haya ya Msasani baada Baba kununua nyumba miaka miwili iliyopita. tukapisha na tumehamia miezi sita tu iliyopita maana

    Baada Baba kuinunua hii nyumba tukapisha matengenezo kama ujuavyo kuna mafundi ujenzi uchwala yani

    Kuweka gipsam wiki mbili hiyo Niru miezi mitatu yani

    Utakuta fundi ujenzi kwa siku kapiga tofari ishilini tu.

    yani chumba kimoja tu kinaweza kuchukuwa miezi hata miwili uvivu tu wakazi

    Mara leo waje kesho wasije matokeo yake Baba akatumia gharama kubwa sana kuwalipa wao kwa kazi ndogo tu.

    Wakati kuna kipindi niliona mafundi flani hivi wakijenga nyumba

    Kwanza msingi wakachimba siku hiyohiyo na kuanza kujenga ikawa bandika bandika tofari tu, kufika jioni kitu kipo juu.

    sasa hawa ndio mafundi sio mafundi uchwara tofari hili limeingia ndani hili limetoka nnje.

    Nikajikuta nafika nyumbani, nikamkuta Mama anapika

    kama kawaida yangu nikitoka namuaga nikirudi namsalimia

    “Assalam alaykum yaa Ummy?".....

    neno ummy ni Mama yangu.

    kwa wasionielewa,

    Akaitikia na kuniuliza huku akitabasamu

    “Waaleykum ssalam yaa Ibnaiya..."

    Vipi mbona umerudi mapema hivyo?"

    “Mmh Mama wee acha tu sijui hata nikwambie nini unielewe binafsi tuyaache tu!"

    Nikaingia chumbani kwangu na kujibwaga kitandani, kichwa kilikuwa kizito kutokana na mawazo yaliyonisonga,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nikaota ndoto nipo na Nusraty tumekaa sehemu moja hivi sijui mrimani city au wapi tukila zetu chostick

    nikaja kustuka baada Mama kuja kuniamsha kwa kuniambia

    “Hafidhi mwanangu muda wa kwenda msikitini tayari nenda kwanza msikitini ukirudi ule maana chakula tayari,

    Nikanyanyuka toka kitandani nikaenda kwanza kuoga kisha nikashika njia kwenda msikitini binafsi napenda kuswali kuliko kitu chochote kile nilipofika pale Mbuyuni nikasimama nikaangalia ile sehemu ya jana niliyoweza kumuona

    Nusraty, nikatikisa kichwa kwa masikitiko nikaenda kuswali.

    Nakumbuka ilikuwa usiku kama saa moja hivi kigizagiza kishaingia Mama akaniagiza niende kununua mchele na mafuta ya kula. Nikatoka zangu mpaka dukani

    Baada kupimiwa kila kitu nikatoka nirudi nyumbani

    Ajabu nikasikia naitwa

    “Wee Hafidhi"

    Nikageuka kumuangalia huyo anayeniita ni nani kwanza nikastuka baada kuweza kumuona Nusraty kwa mwendo wa madoido akanisogerea na kunisalimia

    “Assalam alaykum yaa Akhy?".....

    Nikaitikia kwa bashasha kubwa maana moyo wangu ulikuwa umejawa na furaha kwa kuweza kumuona binti ninayempenda.

    “Waaleykum ssalam yaa ukhty....."

    Vipi mbona leo Asubuhi nimekuja kwenu nikakukuta unaosha vyombo ukanikana kama unijui!"

    “ahaa...unajuwa nini baby ahaa Hafidhi mpaka nakwita baby tena"

    Nikamkatisha kwa kumwambia

    “Sio mbaya ukiniita baby maana mie bado mtoto si unaona nimeagizwa mchele huu,,,,,"

    Basi Nusraty akacheeka na kusema

    “Basi ile Asubuhi ulivyokuja nyumbani nimekuchezea bonge la movie kwanza nikajifanya sikujui siitwi Nusraty ukaondoka bila hata kuaga!"

    Nikamuuliza,

    “kwanini umenitendea kitu kama kile?

    Akajibu huku tukisogea pembeni,

    “unajuwa ulipokuwa unakuja nilikuona basi nikaingia ndani kuongea kitu na Shangazi yani yule aliyetoka sio Mama yangu ni Shangazi maana ningekuchangamkia pale nahisi Baba angenivunja miguu. Maana hapendi kuniona naongea na Wavulana.

    Nikacheka kwanza.

    “Ha!ha!ha!ha! hakika wewe na shangazi yako mnafaa kuwa Maector wa movie maana dahaa,

    Ghafla tukasikia sauti ya mbwa akibweka kucheki anakuja mbio upande wetu basi kila

    Mmoja akatimua mbio nikashika njia yangu

    Nusraty nae yake nilitimua mbio si mchezo swali linakuja kwangu kama kweli unampenda utamlinda

    Sikuweza kumkumbuka Nusraty nilikimbia kimpango wangu

    Huku mfuko wa mchele na mafuta

    Nimevitupa huko

    Chezea mbwa kichaa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada kukimbia umbali mrefu kidogo

    nikasimama nikiwa nahema.

    Adhana nayo inalia nikaenda msikitini

    Nikiwa na mawazo

    Kibao sijui nitamjibu nini Mama kuhusu mchele kingine

    Nusraty kama atang'atwa na yule mbwa nitaonekana zinga la boya

    yani kidume nimeshindwa kumtetea binti ninayempenda

    Ajabu nikamkuta Baba nae anatia Udhu.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog