Search This Blog

VAMPIRE NUSRATY - 2

 







    Simulizi : Vampire Nusraty

    Sehemu Ya Pili (2)



    TulipoishiaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huku mfuko wa mchele na mafuta

    Nimevitupa huko

    Chezea mbwa kichaa.

    Baada kukimbia umbali mrefu kidogo

    nikasimama nikiwa nahema.

    Adhana nayo inalia nikaenda msikitini

    Nikiwa na mawazo

    Kibao sijui nitamjibu nini Mama kuhusu mchele kingine

    Nusraty kama atang'atwa na yule mbwa nitaonekana zinga la boya

    yani kidume nimeshindwa kumtetea binti ninayempenda

    Ajabu nikamkuta Baba nae anatia Udhu.

    SONGA NAYO

    SASA

    Sikutaka kuongea nae chochote kile nikaingia chooni kwanza kujisaidia

    kisha nikatia. Udhu na kwenda kuswali

    Alhamdulillahi niliweza kuwai

    Swala ya jamaa,,,,,,

    Baada kumaliza shekhe akasimama na kutusalimia,

    “Assalam alaykum ndugu zangu Waislamu?"

    Wote tukaitikia japokuwa salamu yake haikufika mwisho na huu ndio ujinga wa zama hizi kuikatisha salamu.

    Sijui uvivu wa kuitamka au hii Warahamatullah haina haja au vipi,

    Baada kuitikia akaleta kizungu kwa kusema

    (In the name of Allah, the most Gracious, the Most Merciful)

    Ndugu zangu waislamu nimesimama hapa mbele yenu kwa ajili ya kuwahusia nafsi zenu pamoja na nafsi yangu juu ya kumcha Allah (s.w.t)

    Binafsi sio muongeaji sana leo nitazungumzia japo kwa uchache kuhusu dalili za kiama kama alivyosema Mtume wetu Muhammad (s.a.w)

    Alitoa dalili nne.

    Ya kwanza kabisa itafikia kipindi watu Wajinga watakuwa wengi zaidi yani utakuta mtu anafanya mambo ya kijinga atajiona yuko sahihi kwa kile anacho kitenda kwa hiyo kukisiri kwa ujinga

    Jambo la pili ni kukisiri kwa unywaji wa pombe na sio ajabu leo hii wanywaji wapombe wamekuwa wengi kupita kiasi utakuta mtu anajifanya Muumini kumbe cha pombe,

    Jambo la tatu Zinaa itaongezeka yani watu watafanya zinaa kama ni halali vile. Embu fikilia katika kipindi hiki ukikuta Watoto kumi wanacheza basi Watoto tisa wote ni watoto wa Zinaa,,,,,,hakika kuna chakujibu siku ya siku,,,

    Jambo la nne Amesema itafikia kipindi Wanawake watakuwa wengi kuliko Wanaume. Je dalili hizo hatuzioni",,,,,,

    Bila shaka dalili zote ziko wazi japokuwa Mtume (s.a.w)

    Alizitamka karne hiyo,,,,,,"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Binafsi maneno ya yule Shekhe yalinigusa sana Maana kila kitu ni ukweli mtupu utakuta Muislamu anaishi na kimada ndani ikifika Ijumaa anapiga kanzu kubwa na barakashia yake

    Anakuja msikitini Yaa Allah tusamehe sisi waja wako,

    Tukatoka msikitini nikiwa na Baba kila mmoja yuko kimya hakuna kuongea chochote,

    Kwanza niliona ajabu Baba kuanza kuswali ikabidi nivunje ukimya kwa kumchokoza

    “Hakika nyumba yetu Allah kaipa baraka,"

    Akasimama na kuniuliza

    “unamaana gani kusema hivyo?"

    Nikamjibu,

    “Kwanza nafarijika kukuona Baba yangu leo hii tutakuwa tukienda msikitini wote tena nitatembea kifua mbele maana pale kwenye mbuyu nilikuwa naogopa kupita, peke yangu!"

    Baba akacheka na kusema

    “Ha!ha!ha! Hafidhi mwanangu si unajiita Commando sasa utaogopaje kupita pale kwenye mbuyu?"

    “Unajuwa nini baba Mimi Commando wa kupambana vita huko Vietnam sio na mazombie!"

    Tukajikuta tushafika nyumbani, baba akaingia ndani mie nikasita kuingia baada kukumbuka

    Mchele na mafuta dahaa, muda mwingine mama anakuwa mtata kwa vitu kama hivi kuna kipindi alinipiga na mwiko wa kichwani. Kisa nilimwaga chumvi, nikawa najizungusha zungusha tu pale nnje

    Gafla Mama akatoka akiwa na ndoo ya maji akaniambia

    “Vipi mbona uingii ndani Baba yako anakungojea mkale,

    Wakati anaanza kuongea mwili ukaanza kunitetemeka ila alipotamka Baba ananingojea nikale sikutaka kuinua mdomo wangu kuongea chochote.

    Nikaingia ndani na kukaa kwenye mkeka ndio Waislamu wa kweli inavyotakiwa kingine Muislamu ni haramu kula kwa kijiko nikanawa na nikasoma duwa la kuanza kula maana ukisoma duwa hakika Shetani hukimbia mbali sana

    Tukiwa tunakula mama akaingia na kusema,

    “Unajuwa leo mwanangu Hafidhi umenifanya nicheke sana kwanza nimekuagiza mchele ukawai kuniletea ukaweka mkaa kwenye jiko ukawasha ukachambua mchele ukauosha,

    Hivi ukuchelewa msikitini kweli?"

    Nikajikuta nauliza

    (What!?)

    Maneno ya Mama nikaona kama utani sijui vipi maana nakumbuka alivyo niagiza sikurudi nyumbani inakuwaje atamke maneno kama yale.

    “Sasa unauliza (what!)

    ili iweje.

    Hakika hata hamu yakula sikuwa nayo tena nikajikuta nanawa na kuingia chumbani kwangu, nikaweza kumsikia Baba akisema

    “Sasa ndio nini hiki umeona kabisa mtoto anakula hapa. Unaanza kumwambia maneno kama hayo!"

    “Kwani mume wangu kumsifia mwanangu kwa kile alichonisaidia leo vibaya au?"

    “Sio vibaya ungemsubiria amalize kula ndio uanze kumpa sifa hizo unajuwa Muislamu atakiwi kula huku anaongea bwana",,,,,,,

    Hakika nilijawa na uoga sana nilijiuliza hivi Mama yuko series kwa kile alicho kisema au?......

    Sasa kama ni kweli nilirudi kuja kumpa mchele,,,,,dahaaa.

    Hatimae usingizi ukanichukuwa nikaja kustuka baada Kusikia Baba ananigongea huku Aswalatur khairu mina nnaumi ikisikika yani

    Swala ni bora kuliko usingizi. Nikaenda nikatoka nikiwa na Baba kwenda kuswali,

    Muda wa kutoka Baba akaunganisha kuelekea kazini mie nikashika njia kurudi nyumbani ajabu kufika pale

    Mbuyuni nikakutana na

    Nusraty akiwa kabeba kidumu kile cha mafuta na kimfuko cha mchele,

    Aliponiona akaanza kucheka yani alicheka mpaka namie nikajikuta nacheka tu.

    “Ha!ha!ha!ha!

    Hahahahaha tehe,,tehe,,

    Nikajishika tumbo na kumwambia

    “Embu Nusraty acha ujinga wako bwana mwenzio tumbo linaniuma huko,"

    Akapunguza kucheka na kusema

    “Unajuwa Hafidhi kuanzia jana ile nimeamini wewe muoga yani sijawai kuona mtu muoga kama wewe,

    kumbe yule Mbwa alikuwa anamkimbiza paka maana paka alipita karibu yetu,

    Ajabu kidume ukatimua mbio balaa ukaviacha vitu vyako pale nikaona nikuokotee nilitaka kuja kwenu nikasita ndio nikaenda kuvihifadhi nyumbani embu shika niwahi kuondoka mie,

    Nusraty akanikabizi mchele na mafuta ya kula

    Hapo nikapata picha kumbe

    Mama alikuwa ananitania tu,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikafika nyumbani na vile vitu nikamkuta Mama anafagia nikamtolea salamu,

    Baada kuitikia akaniuliza

    “Vipi tena Asubuhi yote hii upo na mizigo?"

    Ikabidi nimwambie ukweli Mama

    Kwanza akacheka na kusema

    “Hafidhi usinione Mimi mwehu kumbuka kabisa jana nilikuagiza Mchele na mafuta ukarudi, embu subiri nimwite Mama mjumbe maana nae alikuwepo. Akapaza sauti kumwita Mama mjumbe akaitikia

    Si akaja.

    “Ehee bibi wewe kwanza samahani kwa kutokukusalimia hivi ile jana tukiwa tumekaa pale. Bwana huyu alikuja akiwa kabeba nini?"

    Mama mjumbe akajibu huku akionyesha

    “Si hivyo vitu alivyo vishika akaweka mkaa kwenye jiko akawasha moto huku akisema ingekuwa sio muda wa kwenda msikitini Angepika yeye!"

    Mama akacheka na kusema



    “Haya na huyo sema muongo sijui nini,

    Hivi mwanangu huo uwongo ndio unaanza kujifunza au?"

    Mama mjumbe nae akauliza

    “kwani anasemaje maana sielewi umeniita tu na kuniuliza?"

    Mama akamjibu,

    “mwenzangu mbona makubwa si madogo Hafidhi anadai hivi ile jana nilipomuagiza mchele kumbe hakuleta,

    Mchele na mafuta alivitupa huko,

    Baada kukimbizwa na

    mbwa ,,,,,"

    Mama mjumbe akacheka huku akisema

    “ha!ha!ha!

    Hafidhi bwana ulijuwa leo April 1au,

    Ukaona uje kumdanganya Mama yako

    ina maana kama si wewe yule kumbe nani?"

    Nikaona kumbe hawa lao moja tu, nikaingia zangu ndani.

    Hakika kichwa kiliniuma si mchezo mpaka nikahisi kama kuna mtu anagonga nyundo kwenye kichwa

    changu.

    Nilijiuliza Mara mbilimbili

    “hivi huyu Mama na shogaake

    wamepanga kunichezea mchezo sio?"

    Hatimae siku ikapita,

    nilimeza panadol kupunguza maumivu

    Kesho yake Asubuhi baada kutoka kuswali swalat subuhi niliweza kusikia vilio vya watu vikitokea nyumbani kwa Mama mjumbe nikaweza kufahamu bila shaka kuna msiba umetokea

    Je kafariki nani?

    ikanibidi niende kutaka kufahamu.

    Ni nani aliye tutoka,,,"

    Nilistuka sana baada kutambua aliyefariki ni Mama mjumbe dahaa

    Inna lillahi wainna ilahi rajiun,

    Hakika kwake tutarejea,

    basi ilikuwa vilio vimetawala msibani pale kuanzia watoto wake na ndugu zake wengine

    Hakika ilikuwa simanzi, kubwa sana yani kifo chake kilikuwa cha ghafla mno.

    Maana hakuumwa wala nini, wenye roho nyepesi wakafikia hatua ya kumkufuru Allah (s.w.t)

    Kwa kusema eti kifo chake kimetokana na imani za kishirikina

    Ewe mwanaadamu kumbuka hili kuru nafsi zaaikatul lmauti,

    Pindi mke na mume wanapokutana kimwili Basi Allah huweza kujaalia kiumbe kwa tone la manii lenye mchanganyiko na tone la damu kisha ikawa pande la nyama,

    Kila kifo kimeandikwa angali kiumbe kikiwa bado tumboni embu soma kisa hiki kwa makini sana

    Kulikuwa na mfalme mmoja hivi katika nchi ya Misri huyu mfalme alikuwa akiyamini sana mizimu yake,

    Ikatokea mke wa mfalme kushika ujauzito, hakika mfalme alifurahi sana maana hakuwai kuwa na mtoto na ukicheki umri ushaenda sana,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Usiku mmoja akiwa amelala

    Mzimu wake ukamjia na kumwambia

    “Hakika mkeo atajifungua mtoto wakiume ila tayari ameshaandikiwa kifo chake atakufa kutokana na pembe la ng'ombe.

    Mfalme akastuka kutoka usingizini, huku kijasho kikimvuja. Akaifikilia ile ndoto hakuweza kupata majibu

    Akaipuuzia ajabu ile ndoto ikaweza kujirudia zaidi ya Mara tatu

    Mfalme akaona ahaa subiri aende kwa Mizimu yake, basi akapewa majibu ni kweli

    Akatoa Amri ng'ombe wote kwenye inchi ile wachinjwe.

    Wananchi wakatekeleza Amri ya

    Mfalme ng'ombe wote wakachinjwa siku za mke wa mfalme kujifungua zikafika akaweza kujifungua salama mtoto wa kiume,

    Hakika ilikuwa furaha kubwa sana.

    Mfalme akaanda bonge la tafrija kwenye 40 ya mwanae.

    Siku zikazidi kusonga mtoto akatimiza umri wa miaka Saba binafsi mfalme hakuwa na wasiwasi wowote ule maana kwenye mji wake hakuna tena ng'ombe mtoto akatimiza miaka nane

    Basi siku moja sijui tuseme miujiza au vipi kuna Ng'ombe mkubwa mwenye mapembe sijui katokea wapi......

    Akavamia kwenye kijiji kile watu wakapaza sauti kwa kupiga kelele

    “jamani,,,,,ng'ombee,,,,,ng'ombee

    Mfalme akiwa ndani kwake akastuka yani moyo wake ukafanya pahaa....!

    Akatoka nnje mbiombio huku akiita jina la mwanae Yasri,,,,

    Cha kushukuru walinzi wa mfalme wakaweza kumuuwa yule ng'ombe basi akachinjwa watu wakapewa nyama kichwa kikaenda kufungiwa store

    Mfalme akafurahi sana

    Na kusema kwisha kazi

    Baada kupita siku kama tatu hivi,

    Siku hiyo Yasri alikuwa akicheza mpira na watoto wenzie Basi Yasri akapiga shuti ule mpira ukaingia kwenye chumba kimoja hivi, watoto wote wakaenda kutaka kufungua mlango ila ulikuwa umefunga,

    Dahaa ikabidi wabebane mmoja aweze kupenya kwenye lile tundu Ambalo umepitia mpira Yasri akajitolea kupita basi

    baada kufika kule juu

    akachungulia ndani akaweza kuuwona mpira akatanguliza miguu ghafla bin vuu Yasri akateleza na kujikuta akidondokea ndani mule, kumbe ilikuwa ndio store kilichohifadhiwa kichwa cha ng'ombe.

    Yasri akatua juu ya pembe na kujikuta akitobolewa tumboni akafa hapohapo,

    Mfalme akapata habari

    Hakika akajikuta anadondosha chozi na kusema

    “Hakika alipangaro Mwenyezi Mungu huwezi kuliepuka

    (Inna ajala llah)

    Hakika ajali ya Mwenyezi Mungu

    (Idhaajaa) pindi inapokuja

    (laa yuakharu) haicheleweshi.

    Sasa nashangaa leo hii mtu akifa utasikia sijui karogwa kachukuliwa msukule,

    Na mambo mingine mengi tu watu watasema, basi kesho

    yake tulienda kumzika

    Mama mjumbe niliweza kuona mambo mengi sana ya ajabu kama vile mtu kupita juu ya kaburi hakika Amesema Mtume (s.a.w) ni bora kwenu nyinyi kukanyaga au kukalia kaa la moto au msumari kuliko kukanyaga kaburi au kukalia

    Basi leo hii si ajabu

    kumuona mtu akiwa anakanyaga kaburi na kukalia sehemu iliyo jengewa.

    Baada ya kutoka makaburini tukarudi hadi msibani tuweze kupata chochote kitu,

    Niliweza kumuona Nusraty ajabu wengi walikuwa wakimwita kwa jina

    la Hasina,

    nilijaribu kumtizama kwa jicho la kiwizi wizi kumbe mwenzangu hakutokea hata kushituka nami.

    Nikamuona anaondoka nikapiga moyo konde kwa kumkimbilia huku nikimwita

    Hasina".....Hasina!!!

    Akageuka kunitizama kisha akaitikia

    “Abee"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakika sauti yake haina tofauti na Nusraty,

    Nikamfikia na kumpa salamu

    Akaitikia nikamuomba kuzungumza nae kitu,

    Akaniambia nisijali nizungumze tu,

    “Unajuwa Hasina mpaka sasa sikuelewi kabisa yani Usiku unajiita Nusraty mchana unaitwa Hasina hivi kwa nini unafanya hivi?"

    Akanitizama kisha akajibu

    “unajuwa wewe kaka sikuelewi kabisa unamaanisha nini kuniuliza hivyo kumbuka siku ile ulikuja nyumbani ukanikuta naosha vyombo Mama alikwambiaje, sasa kama unataka kuamini Mimi sio

    Nusraty twende nyumbani nikakuonyeshe picha nilizopiga

    na Nusraty maana ni

    Dada yangu!"

    Sikutaka kukataa nikaongozana nae mpaka kwao

    Akaingia ndani na kutoka na Albaamu

    Hakika nilistuka sana baada kukuta picha za mapacha wawili waliofanana kila kitu mmoja kapigwa arama ya (X)

    Dahaa tena alikuwa

    Nusraty

    “umemuona huyu ndio

    Dada yangu Nusraty amefariki miaka minne iliyopita kwa kugongwa na nyoka!"

    Nilitoa macho pima kama fundi saa kapoteza nati kijasho nacho kikinivuja kumbe Nusraty ni Vampire a.k.a

    Jini dahaaa,,



    Nilihisi mapigo ya moyo yakipanda na kushuka.

    Hasina akaniuliza

    “Kwani kaka vipi mbona sikuelewi"

    Nikajikuta naondoka pasipo kuaga huku Hasina akiniita na kunikimbilia,

    “wee kaka",,,,,kaka!!!

    Mbona unaondoka tu pasipo kuongea chochote"

    Baada kunifikia akasimama mbele yangu. Hakika nilimuona

    Nusraty kama kuna kamchezo flani hivi ananichezea nikapaza sauti tena

    kwa ukali kabisa kumwambia anipishe.

    Hasina hakubisha akapisha njia,

    Nikaondoka zangu,

    Huku nikiwa najiuliza maswali ya hapa na pale nikaona suruhisho pekee niende kwa Shekhe Yusuf nikajiuliza

    “sijui atakuwa bado yupo msibani au vipi?

    Nikaona bora niende nyumbani kwake nilipofika kwake Alhamdulillah nikamkuta ndio anajiandaa kuchinja kuku. Nae aliponiona akasema

    “Vizuri sana kijana wangu umekuja maana nilikuwa najiandaa kumchinja huyu kuku tatizo mkono wangu unaganzi, embu nichinjie kwanza!"

    Nikachukuwa kisu na yule kuku nikamchinja

    Sauda binti wa shekhe akaleta maji nikanawa kisha nikaenda kukaa kwenye Mkeka

    Nikimngojea Shekhe Yusuf atoke ndani

    Basi akatoka akiwa kabeba Msahafu na tasbihi mkononi.

    Akaja kukaa kwenye mkeka huku akisema

    “Astaqhafilullah",,,,,,

    Haya niambie kijana wangu leo unaitaji kujifunza tafasiri ya sura gani?"

    Nilichelewa kujibu nikamtizama kwanza kisha nikatamka haliyakuwa ni mwenye majonzi tele moyoni mwangu

    “Ewe shakhe wangu hakika kijana wako nimekumbwa na mtihani mzito sana, sijui kama mtihani huu nitafeli au nitafahuru"......

    Shekhe Yusuf akanitizama kwa muda akaniuliza

    “Hafidhi kijana wangu mbona unaniacha njia panda embu niweke wazi ni mtihani gani huo?"

    Sikutaka kumficha kitu nilimueleza kila kitu mwanzo mwisho.

    Akaniambia....

    “hakika Hafidhi umeingia mikononi mwa kiumbe hatari sana kile ambacho ulikuwa unakiogopa leo hii ndio umekisogerea na itakuwa ngumu sana kukuacha,,,,,"

    Dahaa maneno ya Shekhe yakazidi kunitia uoga

    Maana alizidi kusemaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ni kweli kulikuwa na mabinti mapacha mmoja anaitwa Nusraty mwingine ni Hasina huyo Nusraty ameshafariki muda tu na kwenye mazishi yake Mimi ndio niliye yasimamia.

    Kingine kijana wangu huyo atakuwa ni Jini aliyetokea kukupenda,

    kwakuwa hili swala umelifikisha kwangu basi usijali nitalifanyia kazi haraka iwezekanavyo, ninacho kuomba ni kitu kimoja tu, ukikutana

    Nae usimuonyeshe

    ishara yeyote ile kama umemtambua yeye ni nani

    maana ukifanya hivyo ataweza kukudhuru!"

    Basi nikaitikia kwa kile alicho niambia Shekhe Yusuf

    Nikaondoka pale nikiwa natabasamu maana swala zima nimelifikisha sehemu usika

    Zikapita siku kama nne hivi pasipo kuonana na Nusraty.

    Basi siku hiyo nikaenda msikitini kuswali ajabu mpaka Adhana inapigwa Shekhe Yusuf hakuja ukafika muda wa kukimu swala hakuonekana

    Na sio kawaida yake.

    Maana siku zote anakuwa wa kwanza au wapili kuja msikitini.

    Basi tukasali na kutawanyika kwenda majumbani kwetu,

    Ilipofika saa tatu Asubuhi nikiwa nakunywa chai

    Ghafla Mama akaingia ndani huku akisema

    Inna lillahi wainna ilahi rajiun,"

    Sikuweza kujuwa kuna jambo gani limetokea mpaka Mama katamka vile,

    Akaniambia

    “Hafidhi mwanangu kuna msiba"

    Nikauliza

    “wa nani tena Mama?"

    Akanijibu

    “wa Shekhe wako Yusuf amekutwa amefariki ghafla kitandani kwake!"

    Nilistuka vibaya mno nikatamka

    Inna lillahi wainna ilahi rajiun,

    Dahaa mchozi ukanitoka basi tukaenda msibani

    Taratibu zikafanyika tukaweza kumzika Shekhe wetu

    Imamu wetu aliyetutoka ghafla huku akiwa katika hali ya kunipigania Mimi

    Hafidhi nikabaki mnyonge nisijuwe nini cha kufanya,

    Maana ndio hivyo tena mtetezi ameshapotea,,,,

    Yani ikawa kupita usiku pale mbuyuni sipiti tena

    Nikawa nazunguka umbali mrefu ili niweze kwenda kusali

    Basi sikuhiyo nilikuwa nimekaa kibarazani huku nikicheza game la nyoka kwenye simu ya Mama ghafla akaja mtu na kunipora nilitaka kupaza sauti kuita mwizi,,,

    kumcheki mtu mwenyewe kumbe ni

    Nusraty,,,,dahaa

    Mwili ukaanza kunitetemeka

    Wakati mwenzangu anacheka tu.

    “ha!ha!ha!ha! Hafidhi bwana ulijuwa mwizi au?"

    Nikashindwa kumjibu kitu akaweza kutambua ule uwoga wangu

    Basi akatumia mkono wake kunishika sehemu ya moyo kisha akasema

    “Hafidhi mbona mapigo yako ya moyo yanaenda mbio hivyo nini tatizo?"

    Nikabaki kimyaa huku nikipiga mahesabu ya kukimbia

    Kumbe mwenzangu keshanisoma kitambo tu akaja kunishika kabisa kwa kuupitisha mkono wake begani kwangu kwa sauti ya chini yenye kusikika vizuri kwangu

    Akaniambia

    “Binafsi natambua ushaweza kujuwa mimi ni nani sasa basi tambua kitu kimoja kwa upande wangu nimetokea kukupenda naitaji kufunga ndoa nawe utake usitake ndoa itafungwa tu

    Na kila atakaye ingilia kutaka kuzuia penzi letu Mimi nawe

    Basi mauti yatamkuta kama Mama mjumbe na huyo Shekhe!"

    Nilistuka nikatoa macho kodo

    huku mdomo ukinicheza cheza nikamuuliza

    “Hivi wewe ndio umewauwa?"

    Akaitikia ndio,

    “Kwanza Shekhe ilikuwa ni kazi ngumu sana kumuondoa hapa duniani ila kupitia mkewe nikaweza kuifanya kazi hiyo,,,,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikautoa mkono wake begani kwangu kwa hasira nikamwambia

    “Sikia nikwambie kitu wewe Zombie sijui vampire siwezi kufunga ndoa nawe hata iweje?

    Akanyanyuka na kusema

    “oky kwakuwa nakupenda siwezi kukufanyia kibaya chochote kile ila jiandae kumzika Mama yako",

    Akafanya kitendo cha kama kugosha kidole hivi ghafla nikasikia

    Mama akipiga mayowe ndani.

    “Mamaweee,,,,,"nakufaa....."

    Nikamwambia kwa sauti

    “please Nusraty achaaa,,,,,,"



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog