Search This Blog

VAMPIRE NUSRATY - 3

 



    Simulizi  : Vampire Nusraty

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Tulipoishia

    “Sikia nikwambie kitu wewe Zombie sijui vampire siwezi kufunga ndoa nawe hata iweje?

    Akanyanyuka na kusema

    “oky kwakuwa nakupenda siwezi kukufanyia kibaya chochote kile ila jiandae kumzika Mama yako",

    Akafanya kitendo cha kama kugosha kidole hivi ghafla nikasikia

    Mama akipiga mayowe ndani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mamaweee,,,,,"nakufaa....."

    Nikamwambia kwa sauti

    “please Nusraty achaaa,,,,,,"

    Songa nayo

    Sasa

    Nilijikuta natoka mbio kwenda ndani huku nikimuacha

    Nusraty akicheka tu, nikaingia chumbani kwa Mama na kumkuta amelala chini

    Akiwa anaugulia maumivu ya tumbo

    “uwiiiiii...nakufa!!!...

    Naomba maji"

    Nikaona itakuwa si vyema kumpa maji nikaenda chumbani kwangu haraka sana nikachukuwa msahafu

    Nikaja nao na kuanza kumsomea

    Surat Yasin....nilisoma kwa sauti kubwa huku jasho likinivuja

    Kama haitoshi nikasoma Ayatur kursiyu.....

    Baada kusoma kwa muda Mama akaacha kuugulia maumivu ya tumbo

    Akanyanyuka kama mzimu

    vile akaniangalia kisha akatoka nnje.

    Sikutaka kujiuliza sana

    nami nikamfata kufika sebureni nikamuona anaangalia Tv wakati hata haijawashwa

    nikabaki kumshangaa tu.

    Ndipo akaniambia.

    “Hafidhi naomba maji ya kunywa"

    Unajuwa mpaka hapo nikabaki njia panda yani nilimuona Mama kama kapoteza network kazaa hivi.

    Nikaenda kumtekea maji ya kunywa nikayasomea kwanza kisha nikampa akanywa yote. na kusema

    “Alhamdulillahi

    Hafidhi mwanangu sifikilii kama juwa la kesho nitaweza kuliona maana roho yangu nahisi ipo juu ya koromeo!"

    Mpaka hapo sikuweza kufikilia Mama anamaanisha nini.

    Nikajuwa atakuwa kaona kitu

    Maana macho yake kaikazia Tv wakati haiwaki ajabu hii.

    Baba aliporudi Mama akaenda kumkumbatia mumewe huku akilia na kusema

    “Mume wangu mie ndio nakufa hivyo tafadhali waangalie watoto wetu yani Hafidhi na Dada ake Fatuma

    pindi Fatuma akirudi boarding mwambie Mama yake nimeenda mbaali...tena mbali sana!"

    Baba nae akashangaa akajaribu kumuuliza mkewe kwani anamaanisha nini kutamka maneno yale.

    Akachukulia utani tu.

    Maana Mama akamuandalia chakula mumewe na maji ya kuoga kisha akaaga anaenda kulala ilibidi nikae na Baba pale sebureni akaniuliza

    “Hafidhi umemsikia Mama yako anavyosema?"

    Nikaitikia

    “ndio Baba nimeweza kumsikia

    na hata sijui anamaanisha nini"

    Hatimae nikaenda kulala pasipo kumwambia Baba kuhusu

    Nusraty,,,,,,

    Nilihofia sana usiku niliota ndoto ya kutisha sana yani nilimuona Mama akiwa ananyonywa damu na

    Nusraty kwenye shingo yake kisha akamchinja.

    Nikaja kustuka na kusikia hodi, yani Baba ananimsha twende msikitini

    Hakika mwili wangu ulikuwa mzito sana kunyanyuka kitandani,

    Nikamlaani Shetani aache kunijalibu.

    Nikatoka na Baba kwenda kusali,

    Msikitini kulikuwa na imamu mpya anaekwenda kwa jina la Shekhe

    Milongo, basi baada swala akasimama kutowa mawaidha kidogo kwa kusema

    Ndugu zangu waislamu

    hakika nyie ni Umma uliobora kuliko umma zote zilizopita....

    unajuwa kwanini nasema hivyo, kwa sababu katika zama hizi kila mmoja anajisifia kuzaliwa haliyakuwa ni Muislamu,,

    Sasa tuje katika huo uislamu anaojivunia.

    Leo hii ukimuuliza mtu yeyote nini maana ya dini atakujibu dini ni imani basi, sasa kama dini ni imani hakuna haja ya kufanya ibada,,,

    Mawaidha ya Shekhe huyu sikuweza kushika hata moja wala sikuweza kujuwa analenga kipi nikawa kimya namsikiliza tu,,,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akasema

    “hapa ndipo tunapata Muislamu jina yani kwakuwa anaitwa Selemani Abdallah au Zainabu khatibu Baba muislamu na mama muislamu

    Anajiona yupo katika umma bora kabisa

    Unakuta zama hizi kijana wakiume tena muislamu kabisa kichwani kanyoa sijui kiduku au kibwezi tena kavaa hereni kabisa suruali imemshuka na kuonyesha nguo yake ya ndani ionekane nnje, vijana wengine wanasuka kabisa basi amelaaniwa kila Mwanaume mwenye kujifananisha na Mwanamke na Amelaaniwa Mwanamke mwenye kujifanisha na Mwanaume

    Wewe

    huna tauro mpaka uvae

    Kanga ya mkeo msuri huna mpaka uvae kitenge cha mkeo,

    Kila Mwanamke mwenye kuweka dawa kwenye kichwa chake ajiandae siku hiyo...unataka kushindana na uumbaji wake Allah (s.w.t)

    Kuna maneno yalianza kunigusa ni kweli dunia kwa sasa imebadirika kila kitu tunaiga kwa Wazungu mpaka Wanawake weusi wanapotea.

    Nikatoka msikitini nikarudi nyumbani Ajabu nikakuta mlango haujafunguliwa wakati siku

    zote Mama sie tukitoka tu nae

    Anaamka nikirudi namkuta anafanya usafi kama kuku tayari washafunguliwa kwenye banda lao

    Sikutaka kujipa mashaka sana nikaenda kuwafungulia kuku

    kisha nikachukuwa ufagio na

    Kuanza kufagia

    kuna Mama mmoja muuza mchicha akaja.

    “vipi Hafidhi hujambo"

    Nikamjibu

    “sijambo Assalamu alaykum?"

    Akasema huku akiguna

    “Mmh mwenzangu mie hata siwezi kuitikia hiyo salamu niamkie tu"

    Nikamwambia

    “kuamkia kwetu sio salamu yani salamu iliyobora kwetu ni Assalamu alaykum,"

    “haya bwana vipi Mama yako bado ajaamka au?"

    Nikaweka ufagio pembeni huku nikimjibu

    “subiri nikamwite,

    Nikaingia ndani nikabisha hodi kwanza chumbani kwa wazazi wangu nikaita huku nikigonga...hodi!!!,,hodi!!!,,,

    Niligonga kama mara tatu sikuitikiwa kwa muislamu wa kweli hodi mwisho

    Mara tatu tu kama hujaitikiwa ondoka

    ajabu mie nikawa nina

    Wasiwasi moyoni

    Nikausukuma mlango huku

    nikisema yaa Allah nisamehe mimi kwa kuingia chumbani kwa wazazi wangu pasipo lidhaa yao.

    Baada ya kuingia nikamkuta Mama amelala nikamshika begani huku nikimtikisa kwa kumwita

    “Mama,,,"mama!!!,,

    Ajabu akawa kimyaa nilishangaa hata mapigo ya moyo hayapigi nikainamisha kichwa changu niweze kusikilizia

    Nikajikuta natoka nnje mbio huku nikiita

    “Mama,,,Subira!!!,,,njoo umuone Mama yangu,,,,,

    Yule Mama muuza mchicha akaniuliza

    Kwa mshangao

    “unasemaje akaingia ndani haraka kwakuwa chumba alikuwa anakifahamu akaingia tu

    Baada kumwita kwa kumtikisa akampima mwishoe akaangua kilio.

    Mama yangu alikuwa tayari

    Ametangulia mbele ya Haqi

    Nililia sana watu wakajazana Baba akapigiwa simu hakuweza kuamini

    Baada kufika nyumbani

    maana hata kutembea hakuweza na kujikuta akilala chini kwa huzuni

    “Mama Hafidhi kumbe ulikuwa Sirius kutamka vile",,,,,

    Kwanini mke wangu umeamua kuniacha mapema hivi,,,,"

    Umeniachia watoto,,,,

    Hakika Baba alilia kama mtoto mdogo ndugu zake na marafiki wakajitahidi kumbembeleza,

    Nikakunja ndita baada kumuonaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hasina nikapanga kuuwa tu.

    Kama Nusraty kaniulia Mama yangu subiri nimuuwe mdogo wake kama vita wacha ianzee...



    Nilimuangalia Hasina kwa hasira sana hakika nikatamani kwenda kumrukia niweze hata kuivunja shingo yake.

    Kilichonitia majozi zaidi pindi nilipomuona Dada yangu Fatuma anavyo lia,

    Tena kwa uchungu sana.....

    “iiiiiihiiihaaa....jamani",,,,,Mama yangu miee!!!...umeniacha na nani...

    eee...mamaaa!!!

    Nilijikuta mliaji naenda kumbembeleza mliaji mwenzangu maana ndugu na jamaa walishindwa kumtuliza Dada apunguze kulia.

    Nikamshika huku nikimpa maneno ya faraja,,wakati mie mwenye naitaji kupewa faraja pia

    “Fatuma Dada yangu punguza kulia sana hakika vilio vyetu tunazidi kumtesa Mama yetu usilie

    kumbuka njia yetu ni moja. Ewe Dada yangu

    Tuwe na moyo wa subira tusimkufuru Allah (s.w.t) kwani kazi yake

    haina makosa,

    Kwa sauti yakilio akanimbia

    “ni kweli Kaka yangu kwa hiko ukisemacho Mama ametuacha hivi tutabaki na nani sie?"

    Akaangua kilio kwa sauti zaidi mwishoe akaregea mwili

    Fatuma Dada yangu akapoteza fahamu.

    Nikajiwekea kisasi moyoni mwangu

    Hasina nitamnyonga tu,

    Hatimae kesho yake baada swalati Adhuhuri tukaenda kuupumzisha mwili wa Mama yangu mpendwa katika makaburi ya Manzese,

    Ndugu wakalala matanga

    japokuwa nilikuwa nimefiwa

    sikukosa hata kipindi kimoja

    Cha swala,

    Nikiwa narudi msikitini baada swala ya saa mbili usiku nikakutana na

    Nusraty..akiwa kajitanda ushungi

    yani kapendeza utasema Malkia gani

    Kidume nikakunja ndita na

    kukaza uso tukabaki kutizamana tu.

    Akaniambia

    “Hafidhi kwanza pole sana kwa kufiwa na Mama yako, nafahamu ni jinsi gani unahasira nami kwa kusababisha kifo cha Mama yako kwa kifupi tu

    Sio Mimi niliyeuwa!"

    Nikamkatisha huku nikimuonyeshea kidole

    “Shatapu mjinga mkubwa wewe usinione Mimi kama mtoto mdogo ukaona wa kunidanganya kwa pipi wakati wewe mwenyewe ulisema nijiandae kumzika Mama yangu, eti sijausika,

    Subiri na uwone show itakavyokuwa,,,,,"

    Nikampushi na kuondoka zangu

    Nilipopiga hatua kadhaa tu akaniita

    “Hafidhi"

    Nikageuka kwanza nikastuka,

    Khaa yupo na Mama nikarudi mbio kuja kumkumbatia Mama yangu ni kweli alikuwa Mama

    Akanikumbatia wote kwa pamoja tukaanza kulia.

    Mama kwa sauti ya majozi akaniambia

    “Hafidhi mwanangu naomba unisikilize kwa umakini sana, kwanza tambua kitu kimoja Mama yako sijafa bado nipo hai ila kwenye mateso makubwa sana hakuna mtu wakuja kuniokoa zaidi yako.

    Please mwanangu kubali kufunga ndoa na Nusraty

    Tafadhali nakuomba"......

    Nikajikuta natoka mikononi kwa

    Mama nikamshika

    Nusraty shingoni kwa kumkaba huku nikimwambia

    Namtaka Mama yangu....

    nilimkaba kisawa sawa huku Mama akinisihi nimuache

    Ajabu Mama akaenda chini kama mzigo. Puhuu

    Nikajikuta nastuka dahaa kumbe ilikuwa ni ndoto tu,,,,kudadeki

    Nikajikuta nipo kwenye mkeka nimelala huku waliokuwepo kwenye matanga kila mmoja akikoroma kimpango wake...." nikajinyanyua kwenda chooni

    Ajabu nikamuona Mama kwanza nikafikicha macho nikijuwa itakuwa ndoto juu ya ndoto,

    Maana Nusraty ananijalibu tu

    aone je imani yangu ikoje

    Mama akanyoosha mikono katika ishara ya kuniita

    Kama vile nimfate basi nikapiga hatua kumfata ajabu.

    Nikashikwa mkono kwa nyuma

    Nikageuka kumtizama aliyenishika ni

    Nusraty jamani...

    Akanitizama kwa kunikazia macho yake makali yenye kuwaka waka kama umeta hivi

    Kwa sauti yenye kuunguruma akaniuliza

    “Hafidhi kumbuka kile alichokuwambia mama yako

    wewe ndio muokozi wake, baada kusema vile akapotea kuangalia hata Mama hayupo dahaa

    Nikajuwa nitashituka tu kumbe walaa..

    Kesho yake Asubuhi nikaanza kumtega

    Hasina kwakuwa ilikuwa siku ya

    Ijumaa nikatega kwenye kinjia flani

    NikitegemeaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hasina atapita tu maana ndio njia yake

    mfukoni nina kisu changu.

    Kidogo hivi akipita tu

    Nimchinje ilikuwa saa nne Asubuhi hatimae ikatimia saa sita mchana muadhini akadhini...."

    Mawaidha yakaanza

    Nikatulia kimyaa kusikilia

    maana niliweza kuyasikia vyema.

    “ndugu zangu Waislamu khutuba yangu ya leo itahusu Madhambi makubwa kabisa ambayo kamwe Allah (s.w.t) hatoweza kukusamehe kamwe mpaka unaingia kaburini na kesho

    Kiama

    Kwanza kabisa kuuwa kwa

    kukusudia hii dhambi moja wapo hata kama utajenga misikiti billion.

    hata kama utaswali kila sekunde hakika wewe ni wamotoni tu,

    hii dhambi ya kuuwa kwa

    kukusudia inaendana kabisa na dhambi ya kujiuwa maana utakuwa umeizurumu nafsi yako,

    ewe ndugu yangu iyepuke dhambi hii

    kwanini uuwe wakati Allah amekataza, kwanini ujiuwe wakati unajuwa kabisa umejiangamiza?"

    Hakika ya Allah ndio mjuzi wa yote.

    Ametakasika kila jinsi ya sifa njema anastahiki,

    Dhambi ya pili na nikubwa mno ni Shirki yani kwenda kwa waganga sijui kutaka utajili au mtoto kivyovyote vile itakuwa ni shirki hakuna Apasae kuabudiwa wala kuombwa

    Zaidi ya Mwenyezi mungu hivi jiulize kitu kimoja unaenda kwa mganga kutaka utajili kwani yeye hautaki huo utajili au?.....

    Unataka mtoto wakati yeye mwenyewe analia usiku na mchana kutaka mtoto

    Siku Allah akakuruzuku kupata

    Mtoto utaanza kumpa sifa kedekede yule mganga...yani unasahau kabisa aliyekuumba ni nani,,,

    Hakika nikajikuta nasitisha Zoezi langu la kutaka kuuwa,

    Sijui huyu shekhe aliambiwa kama

    Hafidhi leo anataka kutenda

    kitendo hiki au vipi?"

    Baada kuswali nikatoka zangu

    msikitini

    nikamuona Hasina akiwa na wasichana wenzie.

    Nae akaniona akaja mbio na kunisalimia huku akinipa kiganja cha mkono kwa kukiweka kwenye kanga,

    Siku zote Waislamu haturuhusiwi kushikana nyama kwa nyama yani baina ya Mwanaume na Mwanamke.

    Asiekuwa halali yako,

    “Assalamu alaykum warahamatullah wabarakatur ewe Hafidhi?"

    Kiroho safi nikaitikia wakati huo kisu changu kipo kibindoni

    Asingekuwa Shekhe leo

    Wallahi ningemchinja,

    “Waleykum ssalamu warahamatullahi wabarakatur yaa ukhty"......

    Akaniambia

    “Kwanza pole sana kwa msiba Hafidhi nikuulize kitu?"

    Nikaitikia

    “Asante sana nishapoa ndio niulize!"

    Akaniambia kama sitojali twende tukakae sehemu,

    Basi tukatafuta sehemu nzuri yenye utulivu akanitizama ukimya wa kama dakika mbili hivi ukatanda

    kisha akavunja ukimya kwa kusema

    “Wacha nikupe historian ya Nusraty,

    Nikamtizama na kumuuliza

    “Nini!?"



    Nilikuwa na shahuku ya kutaka kuifahamu hiyo historia ya maisha ya

    Nusraty, basi

    Hasina akaanza kunisimulia,

    “kwanza kabisa Dada tokea akiwa mdogo alikuwa na wadudu kichwani.

    Nikamkatisha kwa kumuuliza

    “alikuwa na wadudu kichwani kivipi na hao wadudu ni wepi?"

    Hasina akanitizama kisha akanijibu na kuendelea kusimulia

    “Binafsi ninapozungumzia wadudu ni Mashetani, ndio alikuwa anaishi nao kichwani kwake

    Hakika walimtesa sanaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    yani walikuja saa yeyote ile na kuanza kupandisha iwe kwenye daladala au shuleni popote pale

    Kwa siku alikuwa anapandisha zaidi ya mara tatu au mbili

    Kila siku zilivyozidi kwenda Dada akazidi kukonda basi Mama

    Akampeleka kwa Shekhe huko bagamoyo akachanjwa mgongoni

    Kisha akapakwa dawa

    yule Shekhe akamsomea pale

    Huku akimpiga piga kichwani na usinga sijui mkia wa ng'ombe au mbuzi,

    Hapo nikamkatisha tena kwa

    Kumwambia

    “please huyo sio Shekhe ni mshilikina anaechafua hadhi za Mashekhe wetu tambua kitu kimoja

    Unapoenda kwa Shekhe kusomewa kwanza ukikuta sijui vitambaa vyeusi vyekundu na nyeupe

    tena ana kibuyu na pembe ya mbuzi au ng'ombe tambua huyo sio

    Shekhe hata kama anaswali swala tano au Anafundisha madrasa huyo

    Hafai kabisa mbele ya macho ya jamii

    Shekhe wa kweli anakusomea au kukuandikia thafarani basi!"

    Hasina akatabasamu na kusema

    “basi sawa tuseme ni mganga baada kufanya matibabu yule Mganga akasema Jini makata anataka Pete ya Almasi huku Maimuna akitaka Pete ya dhahabu,

    Baba akauza kiwanja chake kimoja ili aweze kumnunulia Nusraty hizo pete

    Baada kuveshwa na kufanyiwa

    Tambiko kwa kuchinjiwa mbuzi kama kafara kila kitu kikatulia akawa apandishi tena akaanza kunenepa

    Mpaka siku aliyokufa,

    kifo chake kilikuwa cha utata sana

    Yani aligongwa na nyoka akiwa jikoni anapika akapiga kelele ghafla akawa kimya,

    Hata tulipofika tulimkuta Dada tayari ameshakufa,,,,

    Hasina akaanza kulia nikaitaji kumshika nimbembeleze nikasita

    kwa sababu pindi Mwanaume na Mwanamke

    Wanapojitenga kwa kukaa peke yao wawili tu basi watatu yake ni Sheitwani, kwakuwa alizidi kulia hakika kama alijitonesha kidonda ambacho kilikuwa kishapona na kubaki kovu tu.

    Nikamshika kichwani kisha akajiegemeza kifuani kwangu. Nikamsihi asiendelee kulia, baada kumbembeleza kwa muda kidogo,

    Hasina akanyamaza na kunyanyuka ili aende nyumbani kwao. Nikaona si vyema kumuacha mtoto wa kike kama yule aende nyumbani kwa peke yake. Japokuwa ilikuwa mchana wa saa 8 na nusu,

    Nikamsindikiza huku nikimpa maneno ya kumfariji, ajabu

    Hasina mwendo wake haukuwa wa kawaida alikuwa anayumba yumba huku akinesa

    Tulipofika karibu na nyumbani kwao akadondoka chini.

    Nikawai kumdaka haraka sana nikapaza sauti kuita msaada

    Ndipo wakaja Wazazi wake, hawakuuliza kitu zaidi ya Kaka yake kumbeba na kuingia nae ndani, nikataka kuingia na mie nikazuiwa na Baba yake

    Hasina akaniambia

    “kijana tunashukuru sana kwa msaada wako wee nenda nyumbani tu",,,,,,

    Kisha akafunga mlango na kuniacha na maswali kibao kichwani.

    Hatimae siku hiyo Usiku ukaingia nikiwa nimekaa Mimi pamoja na Baba

    Ajabu Baba akaniuliza swali,

    “hivi Hafidhi mwanangu kwanini unakuwa na roho ya kinyama namna hiyo?"

    Nilishangaa sana kutokana na lile swali nikauliza,

    “Baba unamaanisha nini kuniuliza hivyo?

    “Najuwa hujui lakini unajuwa kabisa baada kumuuwa Mama yako unataka kuniuwa na Mimi sio yani mtoto mshenzi kabisa haufai!",,,,,,

    Nikajikuta nainuka pale nilipokaa nikabwata kwa sauti kubwa nikavunja adabu ya kutowatolea sauti kubwa Wazazi wetu hakika ni dhambi kubwa sana leo hii si ajabu kumuona Binti akimwambia Mzazi wake

    Eti unabahati umetangulia vinginevyo ningekuzaa...(Astaghafilullah)..

    Yani wewe ungemzaa Baba yako au Mama yako kumbuka ni laana kubwa hiyo...

    yani unapandisha sauti kumsuta Mama yako kisa fitina za mkeo au Mumeo ni ujinga huu tena ni laana kubwa kabisa....

    Sasa mie maneno ya Baba kusema nimemuuwa mkewe eti bado yeye nikajikuta napayuka tu.

    “wee Mzee shika adabu yako usiniletee bange zako hapa,,,,"

    Akaniuliza huku na yeye akiwa kanyanyuka.....

    “Eti Hafidhi mimi nishike nini,,,,leo hii mie navuta bange sio?....kwa hasira Baba akanipiga zinga la kofi ajabu sikuweza kusikia maumivu yeyote Yale zaidi ya Baba kuanza kulia huku akiwa kaushikilia ule mkono alionipiga kofi,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hii mkono wangu,,,,,ayaaa,,,uwiiiiiiiiii

    ....Baba akadondoka chini huku akitapatapa nikaita kwa sauti huku nikimshika

    “Baba!!!baba,,,,,,"

    Nikamuona Dada na ndugu wengine ambao walikuja kwenye msiba wa Mama walikuwa bado hawajaondoka wakaja mbiombio na kuuliza

    Kunanini kimetokea kumbe nyumbani alikuja mganga maana nae akatoka ndani ajabu

    Aliponiona mimi tu akatoka mbio ajabu huku tunguri zake akizitupa ndugu baada kuona vile nao

    Wakanihofia.



    ITAENDEEA

0 comments:

Post a Comment

Blog