Search This Blog

PENZI LANGU - 5

 





    Simulizi : Penzi Langu

    Sehemu Ya Tano (5)



    mpenzi wake Happy waliyefahamiana kupitia mtandao wa facebook alipojifunua shuka na kumweleza dada huyo kwamba alitaka kumwambia jambo. Je , alitaka kumweleza nini? Tuwe pamoja mdau wangu. . . Kulipokucha sikusubiri nikamuomba anieleze , akiwa ametulia aliniambia kuna jambo ataniambia lakini iwe siri yangu kwani hakupenda watu wengine walifahamu . Nilipomhakikisha kwamba nisingemweleza mtu alinikumbatia akanibusu na kusema alikuwa akinipenda mno ndiyo maana aliamua kuniambia siri hiyo . Alinieleza kwamba alipokuwa na umri wa miaka saba wakati akiwa darasa la kwanza alikumbwa na jini ambaye alikuwa akimtokea mara kwa mara usiku na kuzungumza naye . Nikiwa nimepigwa butwaa , aliniambia nisihofu kwani jini wake hakuwa mbaya na alikuwa akifurahishwa sana akifanya aliyokuwa akimuagiza. Alisema alifanikiwa mambo mengi sana kupitia jini huyo hasa baada ya kufuata aliyokuwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akimweleza , mfano kujifunika shuka jeupe alipoanza kuweweseka na kuishiwa nguvu. Mpenzi wangu aliongeza kuwa , jini huyo alimweleza afanye hivyo pale alipohitaji kuzungumza naye mambo mbalimbali yahuyo maisha kama wafanyavyo binadamu wa kawaida wanapokutana . Ingawa niliogopa lakini sikuwa na jinsi kwa sababu nilikuwa nimempenda kwa dhati mpenzi wangu huyo ambaye mpaka muda ule hakuniambia kama hakuwa Mkristo . Nilipomuuliza jini huyo alikuwa na faida gani kwake, alicheka na kuniambia zilikuwa nyingi na moja wapo ni kuwa na akili nyingi jambo nililokubaliana naye kwani ndivyo alivyokuwa. Aliongeza kuwa , ukiacha kuwa na akili nyingi , wachawi walikuwa hawawezi kumfikia kwa sababu alipewa ulinzi na jini wake akishirikiana na nduguze . Nilipomuuliza nduguze aliwafahamu vipi , aliniambia dada wa jini wake alikuwa akimtembelea mara kwa mara usiku na kwamba alikuwa akimpenda . Nikiwa namsikiliza kwa makini , alinieleza kuwa usiku jini wake alimpa maelezo yaliyonihusu lakini alimwambia atamtuma dada yake aje azungumze nami . Alipotoa kauli hiyo nilishtuka na kumuuliza atakuja kuzungumza na mimi kivipi, mpenzi wangu alicheka na kunieleza nisiwe na wasiwasi kwani majini wake walimpenda na kwamba siku atakayokuja itabidi nijifunike shuka kama alivyokuwa anafanya yeye. Nilimuuliza nikijifunika shuka ndiyo itakuwaje , akaniambia nisiwe na haraka mara nitakapojifunika ndipo nitakapojua kila kitu, moyo ukapiga paa ! Kwa ujumla mambo aliyonieleza mpenzi wangu yalikuwa mageni kabisa na ya kustaajabisha , nikamwambia nisingeweza kukabiliana nayo . Mpenzi wangu aliniondoa shaka kwa kuniambia kwamba, nisiogope chochote kwa sababu yeye tangu alipokumbwa na majini ulipita muda mrefu hakuwahi kupata tatizo wala kukwama kimaisha zaidi ya kutegemea kuwa na maisha mazuri kwa msaada wa viumbe hao. Alinieleza jinsi majini hayo yatakavyorahisisha maisha yetu na kuwa na mafanikio makubwa , aliponiambia hivyo alinivuta kisha aliulaza mgongo wangu juu ya kifua chake na kunisifia nilikuwa mzuri . Waswahili wana msemo usemao kila shetani na mbuyu wake ndivyo ilivyokuwa kwa mpenzi wangu ambaye nimekuambia alikuwa na akili nyingi sana . Alipogundua mambo aliyonieleza kuhusu ma jini wake , yalinichanganya , si nikiwa nimelala kifuani kwake akaanza kuzichezea embe zangu bolibo, alipohakikisha nimelegea kama mlenda, hakuniacha. Tulipomaliza kufanyiana fujo aliniita na kuniuliza kama nilikuwa nampenda, nilimwambia hatatokea mwanaume nitakayempenda kama yeye. Alifurahi sana akawa ananishika vizuri maeneo tofauti ya mwili wangu na kuniambia yote aliyonieleza yasiniogopeshe kwani majini hawakuwa viumbe wabaya kama inavyovumishwa na watu hivyo nisihofu na niwe tayari kuzungumza na dada wa jini wake . Aliponiambia hivyo , licha ya awali kuogopa nilimwambia nilikuwa tayari kisha nilimuuliza atafika lini akanieleza siku yoyote ila nijiandae. Nilipomuuliza nijiandae vipi , alicheka na kusema majini walikuwa wakipenda harufu nzuri ya manukato hivyo nilipaswa nianze kujipulizia kila siku usiku nitakapokuwa nalala kwake. Baada ya kuniambia hivyo nilikubaliana naye kwani hata yeye kabla ya kulala alikuwa akipenda sana kujipulizia manukato. Siku moja nilipomuuliza sababu ya kufanya hivyo , alinidanganya kwamba alikuwa akipenda harufu yake. Kutokana na harufu nzuri ya manukato hayo , nami nilikuwa naipenda lakini sikufahamu kama yalihusiana na majini . Tukiwa tunaendelea na stori , aliniambia ataninunulia manukato hayo ili nianze kuyatumia kama maandalizi ya kuzungumza na dada wa jini wake ambaye kibinadamu alikuwa wifi yangu . Kufuatia kunieleza hivyo , nilimwambia asijali akiniletea manukato hayo nitakuwa najipulizia kabla sijalala kama alivyokuwa anafanya yeye. Baada ya kuzungumza hayo nilimuomba twende kanisani akaniambia kuna sehemu alitaka kwenda , ukweli ni kwamba alinipiga chenga kwa sababu hakuwa Mkrito . Nilipombana twende kanisani baada ya kutoka huko ndipo aende safari yake, alikataa na kunieleza isingewezekana na kuahidi kwenda Jumapili iliyofuata .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kutokana na kusisitiza hivyo , niliamua kuachana naye nilijiandaa kisha nilikwenda kanisani na kumuacha mpenzi wangu pale nyumbani. Baada ya kutoka kusali, tulipata chakula na kama kawaida yetu tuliingia chumbani ambako tulipiga stori hadi jioni ambapo mpenzi wangu alinisindikiza hadi hosteli . Jumamosi iliyofuata jioni kama kawaida yetu , tulikutana na mpenzi wangu kwake Tabata , jambo la kwanza alinipatia manukato aliyoahidi kuninunulia . Nilipojipulizia , yalikuwa na harufu nzuri ambayo d wangu aliniambia yalikuwa yanapendwa sana na majini wake , nikamshukuru kwa kujali bila kujua nini kingetokea baadaye. Kwa kuwa sikujiandaa kupika , ilipofika saa moja tulioga na kwenda kwenye ile baa ambayo tulikuwa tunapenda kula tukaagiza chipsi na mishikaki, tulipomaliza kula tulirudi nyumbani. Kabla hatujalala mpenzi wangu aliniambia kulikuwa na uwezekano mkubwa wa dada wa jini wake kufika pale usiku ule kwa lengo la kuzungumza nami, nikaogopa . Aliendelea kunieleza kwamba nisiwe na wasiwasi kwani nitamzoea na kufurahia ujio wake, nilimuuliza kama nami nitakuwa naweweseka na kuishiwa nguvu kama ilivyokuwa ikimtokea , akaniambia hapana . Baada ya kupiga stori hadi saa nne tulipitiwa na usingizi hadi mpenzi wangu aliponiamsha saa nane kasoro na kuniambia mgeni wangu aliwasili hivyo nijiandae kuzungumza naye . Alichokifanya alichukuwa ile chupa iliyokuwa na manukato , akaniambia nijipulizie kwenye nguo yangu ya kulalia ikiwa ni pamoja na ile ya ndani, nikafanya hivyo . “ D hakika unanukia vizuri sana, hivyo ndivyo majini wanavyopenda na mgeni wako atafurahi sana, ” Happy anasema mpenzi wake alimwambia. Kwa kuwa sikumuona nilimuuliza alikuwa wapi, akaniambia nisingeweza kumuona isipokuwa nilale ndipo nitakutana naye , kwa kuwa alinitoa wasiwasi nilijilaza kitandani akachukuwa shuka lingine jeupe na kunifunika gubigubi. Alipofanya hivyo , nilijikuta nipo katika hali ambayo haikuwa ya kawaida kisha nilisikia upepo ukivuma nje nikapatwa na usingizi wa ajabu . Nikiwa katika hali hiyo , niliota ndoto nimeketi kwenye sebule ya jumba la kifahari iliyokuwa na vito vya thamani karibu kila sehemu . Jumba hilo ambalo katika maisha yangu sikuwahi kuingia lilinukia manukato mazuri lakini cha ajabu pamoja na kuwa na vito vya thamani halikuwa na viti isipokuwa zulia zuri la manyoa . Zulia hilo lilikuwa na rangi mchanganyiko na pembeni kulikuwa na meza iliyokuwa ikimeremeta, juu ya meza hiyo palikuwa na runinga na redio kubwa. Nikiwa natupia macho vitu vya thamani vilivyokuwa kwenye ile nyumba, niliona mlango mkubwa wa chumbani ukifunguliwa na dada mmoja wa Kiarabu ambaye alikuwa akitabasamu akaniita jina na kuniambia alifurahia sana ujio wangu pale . Ingawa ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana naye , nami nilimchangamkia na kumshukuru kwa kunikaribisha , aliponifikia alinipa mkono na kunisabahi kwa kusema ; “ Asalaam alaykhum ?” Ingawa sikuwa Muarabu, niliitikia kwa kusema : “ Alaykhum salamu . ” Yule dada alifurahi kisha aliketi mbele yangu na kujitambulisha kwamba alikuwa akiitwa Zaria bin Nassor , aliniacha hoi aliponitajia jina langu, la baba na la ukoo wetu. Nilipomuuliza alinifahamu vipi ? Alicheka na kuniambia jamii yao ilikuwa na uwezo mkubwa wa ufahamu kuliko binadamu, kwa kuwa naye alikuwa binadamu nilimuuliza kwa nini alisema vile. Dada huyo aliniambia yeye hakuwa binadamu wa kawaida isipokuwa jini Zaria bin Nassor aishiye chini ya bahari na huko ndiko uliko ukoo wake . Licha ya kuniambia hivyo , sikuwa na shaka , nilimuuliza pale tulikuwa wapi, dada huyo ambaye muda mwingi alikuwa akiachia tabasamu aliniambia nilikuwa katika nyumba yake iliyopo duniani. Alipoeleza hivyo , nilimuuliza na huko kwao ujijini alikuwa na nyumba nzuri kama ile , akacheka na kuniambia nisiwe na haraka ya kutaka kujua kila kitu siku moja . Dada huyo aliniuliza kama nilikuwa na njaa , ingawa sikula nilimwambia nilishiba akasema nisijivunge nimwambie kwani mle ndani mlikuwa na chakula cha kila aina. Nilisisitiza kwamba nilishiba , alinishukuru na kuniambia kilichomfanya ahitaji kuzungumza nami ni juu ya ndugu zake akiwemo kaka yake mkubwa kutonipenda. Kwa kuwa sikuielewa kauli yake, nilimwambia mbona sikuwafahamu hao ndugu zake na kwa nini walidai walikuwa hawanipendi wakati nilikuwa siwafahamu , yule dada akacheka . Baada ya kucheka aliniambia kwamba, kama alivyonieleza kuwa , wao walikuwa na ufahamu mkubwa wa mambo kuliko binadamu hivyo niamini aliyoyasema .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kufuatia swali langu, yule dada wa Kiarabu alicheka na kuniambia wao walikuwa na ufahamu mkubwa wa mambo kuliko binadamu hivyo niamini aliyoyasema . Jini huyo aliniambia kwa upande wake alikuwa akinipenda sana ndiyo maana alinifuata ili anieleze sababu za ndugu zake kunichukia . Aliniambia kwamba chuki ya ndugu zake dhidi yangu ilikuwa ni uchafu yaani nilikuwa mchafu na sikustahili kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu wao, yaani mpenzi wangu. “ Kwa kuwa nilikuwa nazingatia sana suala la usafi wa mwili na mavazi na nilijipenda sana , nilimweleza mbona nilikuwa msafi na kuongeza kuwa walikuwa wakimsema mtu mwingine. Yule dada alicheka na kunifahamisha kwamba mimi ndiye nilikuwa mchafu na lengo la kuniita pale lilikuwa kunifundisha usafi ambao waliuhitaji wao kwani jamii yao haikupenda uchafu hasa kwa mwanamke. Nilishangazwa na kauli yake, nilimuuliza ni usafi wa namna gani aliokuwa akiuzungumzia maana kama kuoga nilifanya hivyo asubuhi na jioni , nilifua nguo na nilikata nywele za sehemu muhimu zilipoanza kujitokeza. Yule dada alicheka tena na kuniita kwa jina langu, nilipoitika aliniambia kwamba kwa kuwa muda ulikuwa umekwisha tungeonana siku nyingine akaomba anisindikize kwa vile muda ule alihitaji kurudi kwao ujijini . Tuliinuka na kutoka mle ndani kupitia mlango mkubwa wa sebuleni uliokuwa unang’ aa sana, tulipofika nje aliniongoza hadi kwenye geti kubwa lakini ile natakakutoka tu nikashtuka na kujikuta nipo kitandani , nimejifunika shuka gubigubi. Huku mapigo ya moyo yakinienda kasi na jasho likinitiririka, nilijifunua lile shuka , macho yangu yakagongana na ya mpenzi wangu ambaye ilionekana alikuwa akinisubiri . “ Vipi d?” aliniuliza . Kufuatia kuniuliza hivyo , kutokana na jambo lililonitokea muda mfupi uliopita nilibaki nimeduwaa nikimwangalia , akaniita tena . Nilipoitika aliniuliza kama nilikutana na mgeni wangu, nilimwambia nilikutana naye na kumsimulia kila alichoniambia kuhusu kuwa msafi . Nilimweleza jinsi nilivyoshangaa kufuatia yule dada wa Kiarabu kuniambia sikuwa msafi wakati nilikuwa naoga na kufua nguo . Mpenzi wangu alinieleza kuwa huenda ni kweli sikufikia kiwango cha usafi walichokihitaji ndiyo maana alisema hivyo , mpenzi wangu akaniuliza nilipewa maagizo gani kuhusu usafi? Nilimfahamisha kwamba dada wa jini wake alinieleza muda ulikwisha na kuniahidi kuja tena siku nyingine , akasema sawa na kusisitiza kujipulizia yale manukato aliyoninunulia asubuhi , mchana na wakati wa kulala. Nakumbuka wiki niliyotokewa na yule dada wa Kiarabu tulikuwa tumeanza mitihani kwa ajili ya mapumziko ya wiki mbili , kutokana na ubize huo sikwenda Tabata kwa mpenzi wangu ambaye tulikuwa tunawasiliana kwa simu. Jumamosi iliyofuata nilikwenda Kimara nyumbani kwa baba mdogo ambako sikuwahi kwenda tangu nilipohamia hosteli , usiku nikiwa na Joyce tulizungumza mengi kuhusu wapenzi wetu . Hata hivyo , kila nilipotaka kumweleza stori ya mpenzi wangu kutokewa na jini na jinsi nilivyokuwa nikumfunika shuka alipoanza kuweweseka na kuishiwa ngumu na nilivyotokewa na yule jini wa Kiarabu nikawa nasikia sauti ikinipa onyo. “ Happy usimwambie mtu yeyote kuhusu majini wangu utakuwa umefanya kosa kubwa sana, ” nilisikia sauti ikiniambia hivyo . Kutokana na sauti hiyo , sikuthubutu kufanya hivyo , siku iliyofuata tulikwenda kanisani na jioni nilirudi hosteli kujiandaa na mitihani siku iliyofuata. Tulipomaliza mitihani kesho yake ambayo ilikuwa Jumamosi tulikutana na mpenzi wangu nyumbani kwake Tabata tukaagana kwani Jumatatu iliyofuata nilitarajia kuondoka kwenda Musoma. Kwa kuwa baba alikuwa akinipenda sana , nilipomweleza nilitarajia kurudi nyumbani aliahidi kutumia fedha ili nikakate tiketi ya ndege hadi Mwanza . Jioni ya siku hiyo baba mdogo aliporejea kutoka kazini alinikabidhi tiketi ya ndege na Jumatatu alfajiri niliondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza , mishale ya mchana nilikuwa nipo Musoma. Wazazi na ndugu zangu walifurahi kuniona , tulizungumza mengi kisha nikaanza rasmi likizo yangu ya wiki mbili, licha ya kuwasiliana kila siku na mpenzi wangu lakini sikuwahi kuota ndoto wala kutokewa na yule jini wa Kiarabu aliyeahidi kunitembelea siku nyingine . Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana mpenzi wangu, licha ya kutokewa na vijana wa Musoma niliwakataa wakaishia kusema tangu nilipojiunga na chuo kikuu jijini Dar nilikuwa naringa. Binafsi niliishia kuwaangalia tu kwani sikuwa na mpango wa kumsaliti mpenzi wangu niliyekuwa nampenda sana, siku moja nikiwa nakwenda sokoni nilisikia mtu akiniita nilipogeuka nilimuona yule kijana aliyenisaliti na rafiki yangu .



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Awali sikutaka kusimama lakini nilipoona ananiita na kuniomba nimsubiri , nilisimama ili kusikia alichotaka kuniambia , aliponifikia alinisabahi na kunisifia kwamba nilikuwa nimependeza. Kufuatia kunieleza hivyo , alinikumbusha lile tukio la kumfumania na rafiki yangu , nikamjibu kwamba mimi kupendeza au kutopendeza hakumhusu nikaamua kuondoka . Yule kijana alinifuata na kuniambia anajua bado nilikuwa nina hasira za tukio alilonifanyia na kuniomba msamaha na kusema alitambua kosa lake hivyo aliomba kama sitajali turudishe uhusiano wetu. Kumkata kauli nilimwambia sikuwa na mpango huo na kwamba nilikuwa nina mpenzi wangu niliyekuwa nampenda sana nikamweleza akaendelee na rafiki yangu , yule kijana aliishia kunitazama na kusema sawa . Nilipoona anazidi kunichefua, niliondoka na kuelekea sokoni nikiamini asingerudia kunisumbua, wakati narudi nikamkuta amesimama nje ya saluni moja akinisubiri . Nilipofika hapo aliniita na kuniomba msamaha kwa yaliyotokea kitambo badala yake tugange yajayo, nilimsonya na kumwambia hakuwa na akili timamu nikaendelea na safari . Yule kijana ambaye nilijua alikuwa akinitamani kwa sababu nilikuwa nimenawiri hivyo alihitaji kunichezea tu aliamua kunifuata huku akiniomba nimpe tena nafasi katika moyo wangu. Kwa kuwa alikuwa kanitibua , nilimtukana matusi ya nguoni na kumweleza anikome na sikuhitaji hata kumuona , nikakaza mwendo kurudi nyumbani. Baada ya kutembea umbali wa mita kama thelathini, niligeuka nyuma kuona kama alikuwa akinifuata lakini sikumuona, moyoni nikajisemea kwamba; “ nimekukomesha mjinga wewe!” Nilipofika nyumbani niliingia jikoni na kuanza mapishi bila kufikiria kama yule mpenzi wangu zilipendwa nilikuwa nimemkera na alipanga kunikomesha. Siku moja ya Ijumaa zikiwa zimebaki siku tano kumaliza likizo ili nirudi shuleni , nikiwa nyumbani alikuja kijana mmoja ambaye tulikuwa tunaelewana sana . Baada ya salamu tulipiga stori kisha aliniaga na kuniomba nimsindikize , tukiwa tumetoka nje ya geti letu alinifahamisha kwamba yule mpenzi wangu wa zamani alipanga kunifanyizia hivyo nichukue tahadhari. Nilimshukuru kwa taarifa hiyo na kumuuliza alijuaje akaniambia siku alipokuwa akipanga njama hizo na marafiki zake aliwasikia bila wao kujua ndiyo maana alifika kuniambia . Baada ya maongezi tuliagana lakini nilishindwa kumwambia mama wala baba kuhusu mpango huo kuhofia kujiwa juu kwa sababu walinikataza kabisa nisijihusishe na masuala ya wanaume. Kwa vile nilijua kama ningetulia nyumbani wasingeweza kunipata , nilipanga kutotoka au popote nilipotarajia kwenda ningeongozana na ndugu zangu . Kama nilivyopanga, nilimaliza likizo yangu salama lakini kabla sijaondoka wazazi wangu waliniketisha chini na kuniasa nisijihusishe na masuala ya mapenzi mpaka nitakapohitimu masomo yangu na kuolewa . Licha ya kuwa na mpenzi wangu tuliyefahamiana kupitia facebook ambaye alikuwa na majini , niliwaambia wasiwe na shaka kwa hilo. Kesho yake nilikwenda Mwanza na alasiri niliondoka kwa ndege nikafika Dar na kupokelewa na Joyce, Diana na mama , mpenzi wangu alishindwa kuja kuwahofia ndugu zangu . Baada ya kufika Kimara , nikiwa na Joyce chumbani kwetu , d wangu alinipigia simu na kunieleza jinsi alivyonimisi na kuahidi kunipa penzi shatashata tutakapoonana. Maneno yake yalinisisimua nikawa nina hamu ya kukutana naye , nikamwambia kesho yake jioni anifuate hosteli ili nikalale kwake . Siku hiyo tulipiga stori kibao na Joyce , kulipokucha niliwafahamisha baba na mama mdogo kwamba alasiri ningeenda hosteli kujiandaa kwa ajili ya kuanza masomo . Wazazi wangu hawakuwa na neno ambapo baba mdogo aliniambia kama asingekuwa na safari ya Dodoma angenipeleka kwa gari lake , alinipatia shilingi 20, 000 na kuniambia nitafute usafiri nitakaoupenda , nikamshukuru. Kwa kuwa sikuwa na mizigo, Joyce aliniambia muda wa kuondoka ukifika atampigia simu dereva wa Bajaj aliyekuwa akifahamiana naye ili anipeleke kwa shilingi 7, 000.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kweli muda huo ulipofika , alimpigia simu mwendesha Bajaj ambaye aliwasili tukaondoka kuelekea hosteli , njiani nilimpigia simu mpenzi wangu nikamweleza tulipokuwa. Kufuatia yeye kuwa Ubungo na gari la kaka yake, alituambia anatufuata hivyo tukifika Kimara Bucha tushuke , nikamwambia sawa . Tulipofika Bucha tulishuka tukamlipa yule dereva wa Bajaj shilingi 2, 000 akaendelea na hamsini zake, hatukukaa muda mrefu mpenzi wangu aliwasili . Baada ya kuteremka garini , tulikumbatiana na baada ya salamu alipakiza mabegi yangu kwenye buti akaondoa gari kuelekea Tabata alikokuwa amepanga . “ D mtanisamehe , tunakwenda kwanza Tabata halafu jioni nitakupeleka hosteli kisha nitamrudisha Kimara shemeji yangu wa ukweli ,” d wangu alitueleza . Tuliendelea kupiga stori hadi tulipofika Tabata , tulipoingia ndani, Joyce aliyekuwa anapenda sana filamu za Kibongo akawasha runinga na kuanza kuangalia DVD ya filamu ya marehemu Kanumba . Wakati Joyce anatazama filamu hiyo , mimi na mpenzi wangu tulizama chumbani ambako alinikumbatia, akaanza kunishika sehemu zote zenye shoti ya umeme na kunieleza kwamba alinimisi sana. Wakati akinigusa maeneo hayo ‘ matamu ’ tulikuwa na manyoa a . k . a nguo ndipo laazizi wangu akafungua vifungo vya blauzi niliyokuwa nimevaa na kukutana live na embe bolibo zangu za kuchoma. Kutokana na mushawasha aliokuwa nao, aliziminyaminya kwa ustadi wa hali ya juu kisha aliibugia moja na kuanza kuifyonza kama embe, mtoto wa kike nikapagawa si kidogo. Kwa kuwa nami nilikuwa nimemmisi sana, sikumuangusha , nilijibu mashambulizi kwa kumchezea mkuu wake wa kaya akawa anahema huku akiniambia kwa sauti nzito ya kiume kwamba alifurahi sana. Baada ya kupagawishana vya kutosha alimalizia kuninyonyoa manyoa yangu nami nikamnyonyoa yake tukabaki weupe pee , kilichofuatia alinibeba na kunitupia kwenye uwanja wa fundi seremala . Kutokana na kuwa na hamu ya kula nanasi langu alilolimisi sana, hakuwa na kipingamizi alinifuata na kunipiga mabusu ya uhakika yaliyokwenda sambamba na kula mua a . k . a denda , nikawa hoi bin taaban . Alipoona nimeishiwa nguvu namwangalia kwa macho yaliyolegea mithili ya mwanamke aliyekula kungu, alinikamata nami nikamkamata vizuri kisha tukapeana mkomboti wa nguvu. Tulipomaliza kunyweshana dafu la kwanza nikakumbuka sebuleni tulimuacha Joyce, nikajifunga kanga na kwenda kumuona , Joyce aliyejua kilichokuwa kikiendelea kule chumbani aliponiona aliachia tabasamu na kusema ; “ Haya mama kwa raha zetu !” Nilimwambia aache tu maana nilimmisi sana d wangu naye alinimisi na kwamba muda ule kwa kiasi flani nilikuwa mwepesi , Joyce akacheka. Kufuatia mimi na mpenzi wangu kupashana joto, Joyce aliamua kumpigia simu mpenzi wake wa Segerea ambaye alimwambia alikuwa maeneo ya Tabata Aroma anakula kwenye baa flani. Joyce alipoambiwa hivyo , aliniaga kwamba anamfuata na kwamba asingerudi na kwamba tungeonana wikiendi , lakini kabla hajaondoka nilimshauri amuage d wangu . D , wangu alitoka , wakaagana na Joyce akampatia shilingi elfu kumi kisha tukarudi chumbani kuendelea na yetu bila kujua kama miezi michache baadaye penzi letu lingesambaratishwa na jini . Licha ya nyumbani kwa baba mdogo kujua nilikwenda hosteli , kutokana na kummisi sana d wangu , niliamua kulala Tabata kwa nia ya kukatana kiu ya mapenzi na mpenzi wangu . Mishale ya saa nane usiku , tukiwa tumepitiwa na usingizi , nilishituka na kuanza kuweweseka na kuishiwa nguvu kama ilivyokuwa ikimtokea mpenzi wangu , nikajua jini wake alinijia. Kutokana na hali hiyo , d wangu aliniambia nisiogope akachukuwa lile shuka jeupe akanifunika , nikajikuta nimekaa kwenye ile nyumba ya kifahari aliyoishi dada wa jini aliyekuwa akimtokea mpenzi wangu. Nikiwa nashangaa samani na vitu vingine vya dhahabu vilivyokuwepo pale sebuleni ambapo hapakuwa na masofa zaidi ya meza maalum ya kuwekea runinga , yule dada wa Kiarabu alifungua mlango akaja kunikumbatia . Alinisalimia kwa Kiarabu na kuniambia alifurahi kuniona , akaniuliza nilipenda kula au kunywa nini nikamwambia nilishiba , akanitania kwamba kama niliona aibu shauri yangu . Dada huyo wa Kiarabu aliniambia hakupenda tupoteze muda mwingi kwa sababu nilitakiwa kurudi nyumbani mapema, akaniuliza nilikumbuka aliishia wapi kunieleza kuhusu suala la kuufanyia usafi mwili wangu ?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Baada ya kumwambia  nilisahau, yule jini ambaye ni dada wa jini wa mpenzi wangu alicheka na kusema:“Nilijua utaniambia hivyo ila usijali nitakueleza kuanzia mwanzo hadi mwisho, kikubwa unachotakiwa kukifanya ni kuzingatia nitakayokueleza kwa sababu yatakuwa na faida kubwa sana kwako.”Baada ya kuniambia hivyo, alinifahamisha kwamba wao majini wanapenda sana usafi ndiyo maana aliamua kuja kunifundisha namna ya kuwa msafi kwa sababu kaka zake walichukizwa na jambo hilo.Alisema walichukizwa na kitendo cha mtu wao yaani mpenzi wangu kutembea na mimi ambaye nilikuwa sijui kuoga na kufanya mambo mengine waliyokuwa wakiyapenda.Aliongeza kuwa, baada ya mwanamke kuoga kama wanavyotaka wao, anatakiwa kujifukiza udi huku akiwa amejifunika shuka au blanketi unaomfanya anukie vizuri.Mwarabu huyo alisema tangu siku hiyo nilitakiwa kubadili utaratibu wa kuufanyia usafi mwili wangu, alisema nilitakiwa kuoga zaidi ya mara tatu, kujifukiza udi ambao nitakuwa nauchoma kwenye chetezo na kujipulizia manukato ambayo sitapenda kuyaweka wazi wanayoyapenda.Aliongeza kuwa, siku nitakazokuwa natumikiasiku zangu za hedhi, nitatakiwa kuoga zaidi ya mara nne ili niwe msafi maradufu tofauti na zamani ambapo nilikuwa naoga mara mbili.Nilipomuuliza nitawezaje kufanya hivyo ninapokuwa mbali na nyumbani, akaniambia hata wao wanalielewa hilo, nifanye hivyo ninapokuwa nyumbani.Hakuishia kwenye manukato tu, alinielekeza mafuta ambayo jamii ya majini inayapenda watu wao wajipake ambayo pia sitayaainisha kwa majina.Upande wa mavazi alisema hawana tatizo sana isipokuwa aliniambia kama nitakuwa navaa nguo nyeupe, pinki na nyekundu hasa wakati natumikia siku zangu za hedhi siyo vibaya.Alinielekeza mambo mengi na kusisitiza kuyafuata ambapo aliongeza kuwa kwenda kinyume wangechukizwa na adhabu yake ilikuwa kifo au maradhi yasiyotibika.Sijui nilikuwa nimefungwa na nini, nilikubali kufanya yote aliyonielekeza bila kujua kama mpenzi wangu hakunieleza ukweli kuhusu dini yake nikiamini baada ya masomo yetu tungefunga pingu za maisha kanisani.Baada ya kunielekeza masuala ya usafi, aliniambia muda wa kurudi nyumbani uliwadia na kuahidi kuja kunitembea wakati mwingine, tuliinuka tukawa tunatoka kwenye lile jumba lake la kifahari.Alipofungua mlango mkubwa wa kutokea nje ile nataka kuteremka ngazi nilikashtuka na kujikuta nimefunikwa shuka huku mapigo ya moyo yakinienda kwa kasi.Nilipojifunua nilimuona mpenzi wangu akiwa ameketi pembeni yangu, macho yetu yalipogongana aliachia tabasamu lililomfanya apendeze mara dufu, akaniuliza nilijisikiaje?Nilimwambia mapigo ya moyo yalikwenda kasi, akacheka tena na kuniuliza bado tu nilikuwa sijamzoea mgeni wangu? Nikamwambia nilimzoea ila sikujua sababu ya mapigo ya moyo kunienda mbio.Kama ambavyo nilielezea huko nyuma kwamba mpenzi wangu alikuwa ana akili sana, kuniondoa katika hali hiyo aliniinamia akanibusu midomoni na mashavuni kisha akakivamia kifua changu na kuanza kuzichezea embe bolibo zangu, akili ikanihama mtoto wa kike.Aliendelea kunipagawisha nami nikajikuta najibu mashambulizi, kilichofuatia ilikuwa ni patashika nguo kuchanika, hakika d wangu aliyaweza mambo.Tukiwa tumemaliza kuburudishana, kwa sautinyororo mpenzi wangu aliniuliza mgeni wangu aliniambia nini, nilimsimulia kila kitu, akasema nilikuwa mwanamke mwenye bahatihapa duniani kufundishwa usafi na jini.Alisema, kwa kuwa alikuwa akinipenda na kwamba nilikuwa mke wake mtarajiwa, angekuwa ananinunulia manukato, udi na mafuta ambayo niliagizwa kuyatumia.Nilimshukuru, tukalala hadi asubuhi ambapo tulioga pamoja kisha niliandaa chai tukanywatukaendelea na maongezi hadi alasiri ambapo d wangu alinipeleka hosteli.Tangu siku hiyo nikaanza kuoga mara nne kwa siku, siku ambazo nilikuwa kwa mpenzi wangu nilipooga nilijifukiza udi na kujipulizia manukato niliyoelekezwa.Mpenzi wangu alikuwa anafurahi sana jinsi nilivyokuwa ninanukia, jambo lingine ni kwamba sikuwahi kutokewa tena na yule dada wa Kiarabu zaidi ni mpenzi wangu ambaye alikuwa hamalizi wiki bila kutokewa na jini wake.Kama ilivyokuwa kawaida, alipopatwa na hali ya kuweweseka na kuishiwa nguvu nilimfunika kwa shuka ambapo alizungumza na jini wake kisha kunifahamisha.Mfano kuna wakati alipotokewa na jini wake alikatazwa kwenda sehemu ambazo zilikuwa za hatari, wakati mwingine aliambiwa twende tukakae ufukweni



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ungana nami katika sehemu hii ya mwisho.Kwa ujumla tulilifurahia penzi letu na sikutegemea kama ingetokea simu tungeachana na kubaki na mateso ya moyo ambayo yamenifanya niogope kuingia kwenye uhusiano mpya mpaka leo.Baada ya kukaa kwa muda mrefu na mpenzi wangu huku tukiendelea na masomo, ulifika wakati wa kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ndipo penzi letu lilipotenganishwa.Kama ambavyo nilikueleza kuwa, tangu nilipofahamiana na mpenzi wangu ambaye facebook alitumia jina la Kikristo niliamini dini zetu zilifanana na tungefunga pingu za maisha kumbe haikuwa hivyo.Ikiwa imebaki siku mbili Waislam kuanza kufunga, nilikwenda Tabata kwa mpenzi wangu, siku hiyo hakuwa na furaha kama ilivyokuwa kawaida yake.Nilipomuuliza sababu aliniambia anasikitika kuniambia kuanzia muda ule aliamua kuachana nami kwani kama tungeendelea kulikuwa na hatari kubwa mbele yetu, sikumuelewa kwa kweli.Nilipomuuliza sababu alisema ameamua tu ndipo nilimuomba aniambie sababu akasemaataniambia usiku lakini hadi tunakwenda kulala hakuniambia.Usiku nikiwa nimelala, nilianza kuweweseka na kuishiwa nguvu akanifunika shuka, ghafla nilijikuta nipo ndani ya nyumba nimezungukwa na majini warefu wa Kiarabu  watatu.Mmoja wa jini huyo aliniambia kwa kifupi kwamba kuanzia siku hiyo niachane na mtu wao ambaye alikuwa akijiandaa na mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kwamba nikikaidi wataniua.Jini huyo aliongeza kuwa, asingekuwa dada yao aliyekuwa akinitetea wangekuwa wangenisambaratisha muda mrefu hivyo wakanipa onyo kwamba kuanzia siku hiyo niachane na mtu wao.“Wewe binadamu nafikiri umetusikia na kutuelewa sawa?” Yule jini aliniuliza.Kwa hofu niliyokuwa nayo huku nikilia nilimjibu kwamba niliwaelewa na ningefanya kama walivyoniamuru, akaniambia kama nilikuwa nayapenda maisha yangu nizingatie walichonieleza, akasonya kisha wakatoweka.Kutokana na amri niliyopewa, nilipozinduka kutoka usingizini nikiwa sipo sawa nilimuuliza d wangu kwa nini hakuniweka wazi kuhusu dini yake, akaniambia hakuwa najinsi na kwa usalama wangu nifuate nilichoambiwa na majini wake.Nilianza kulia na kwa hasira niliondoka Tabata usiku uleule ambapo mpenzi wangu alinisindikiza, nilipofika hosteli niliendelea kulia lakini haikusaidia kwani jini lilikatisha penzi letu tamu wakati nilikuwa nampenda sana d wangu.Mpenzi wangu ambaye hakuwa na namna ya kuokoa penzi letu, alinikumbatia na kunipa pole na kusema alikuwa akinipenda lakini asingeweza kwenda kinyume na uamuzi wa jini wake.Aliniomba msamaha kwa kunificha dini yake na kunieleza kwamba alijua nilivyoumizwa na kilichokea lakini hakuwa na cha kufanya zaidi ya kuzingatia alichoagizwa.Nililia sana na kuanza kujiuliza inakuwaje kila nikiwa kwenye uhusiano na mwanaume mwisho huwa na mamivu, nilikumbuka tukio la kusalitiwa na mpenzi wangu wa kwanza.Mpenzi wangu aliniambia alikuwa kanizoea na kwamba hata nisahau na atakuwa akinisaidia kila nafasi itakapomruhusu, nikamwambia tukiachana sitahitaji msaada wala kuwasiliana naye.Aliniuliza kwa nini, nilimwambia aelewe hivyo, kumuonesha sikumtania nilimwambia afute namba yangu ya simu nami nafuta yake,nikafanya hivyo huku akiniangalia.Licha ya kunibembeleza sana tuendelee kuwasiliana hata kama hatutakuwa wapenzi, nilikataa akaniambia hakubaliani na uamuzi wangu angenitafuta siku nyingine nikiwa nimetulia ilikuwekana sawa nilikataa, akaniaga na kuondoka.Tangu siku hiyo nilimchukia sana mpenzi wangu huyo niliyetokea kumpenda na kuamini angekuja kuwa mume wa maisha yangu, nikabaki nikijiuliza kwa nini nilikuwa napata matatizo katika uhusiano!Kwa ujumla nilipoteza furaha na muda mwingi nikawa mtu wa kuwaza, nilijilaumu kuanzisha uhusiano na kijana huyo kupitia mtandao wa kijamii wa facebook.Napenda kuwaasa watu wanaotumia mitandao ya kijamii hususan vijana kuwa makini hasa katika suala la kuanzisha uhusiano wa mapenzi na watu wasiofahamu vizuri.Kwa upande wangu najuta kwani kijana niliyefahamiana kupitia facebook alinificha mambo mengi ambayo nilikuja kuyagundua nilipoanzisha uhusiano naye wa kimapenzi, mwisho kujikuta penzi letu tamu likikatishwa ghafla na jini wake aliyeniambia nikiendelea kuwa naye angeniua.Kwa kweli tukio hilo bado linaniumiza na limenifanya niwe muoga wa kuanzisha uhusiano mpya licha ya kwamba chuoni kwetu vijana kibao wananitokea lakini nawakataa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog