Simulizi : 666 Nyayo Za Kuzimu
Sehemu Ya Pili (2)
Mama Utopi baada ya kusikia hayo alidondoka chini kama mzigo,akapoteza fahamu!
Kazi ilibakia kwa mama Kadogo ambaye tayari aliishalowesha khanga yake kwa mkojo,masikini mwanae nae alikua anachungulia dirishani akiyatoa macho yake kwa kutoamini,watu waliokua pale nje na mavazi yao meupe na mekundu walioonekana hawana muda wa kupoteza,wapo serious na wanasubiri ujio wao,aligeuza macho yake kwa mama yake akauliza,
"mama hawa wakina nani?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hakujibiwa kama alivyotarajia,mama yake alikua amezubaa na mdomo ulikua mzito kuufungua,macho yalikua yamemtoka na kichwani alikua anajaribu kujiuliza kwamba yupo ndotoni ama ni kweli?
Alishtuliwa na sauti ya mwanae Kadogo iliyouliza tena kwa mara ya pili ikiambatana na tendo la kumsukuma sukuma ili kumrudisha kwenye fahamu,
"mama hawa watu ni wakina nani?"
"njoo...njoo! Sogea haraka!!!"
alielekeza mama Kadogo,alimvuta mwanae baada ya kumkaribia kisha akamueka mgongoni,kabla ya kujitoa ndani ya chumba alimuangalia mama Utopi aliyezirai,kwa uchungu akasema
"inanibidi nifanye hivi,samahani sana"
kisha haraka alitoka ndani ya nyumba kwa kupitia mlango wa nyuma,
alikimbia sana kadiri ya uwezo unavyomruhusu kutokana na mzigo wa mtoto aliokua nao mgongoni,alikatiza mashambani kama hana akili nzuri,alikimbia na alikimbia maskini kuokoa maisha yake na ya mwanae mwenye umri wa miaka saba tu,kila alipokimbia bado aliona haitoshi hivyo alizidi kuendeleza zoezi,baada ya muda wa dakika arobaini na tano alichoka na alikua anahema kama mbwa,alimshusha mwanae na wakaanza kutembea haraka haraka wakielekea mbele wasikokufahamu kutokana na giza kali lililotawala machoni mwao,
"mama tunaelekea wapi?"
"sijui,ila twende tu"
"mama mi naogopa...ni giza sana!"
"nisikie mwanangu,hatuna la kufanya zaidi ya hili tulifanyalo sasa kama tungependa kuishi zaidi,tusogee tu mbele kwa mbele tutajua cha kufanya hukohuko"
"mama...kwani yupo wapi baba?"
"sijui yupo wapi!"
"hatujamuacha nyumbani?"
"hayupo nyumbani,aliondoka na hajarudi mpaka sasa hivi"
alijibu kiuchungu mama Kadogo,
"he! Mama ile nini?"
"wapi??"
kiuoga haraka aliuliza,
"kile kinachowaka!"
"mh nadhani ule ni moto,ila...ni nani atakua kauwasha?"
aliuliza mama Kadogo huku wakiwa wamesimama na mwanae kibutwaa,
baada ya muda kidogo walimuona mzee mmoja akitokea na kuni alizozishika mkononi kisha akazirushia kwenye ule moto,kumbukumbu za mama Kadogo zilimwambia kwamba yule ni mzee Otongo mganga wa jadi wa pale kijijini kwao na ndie yule aliyekua anawaonya juu ya ujio wa kizazi cha nyoka ambacho sasa hivi ndicho kinachoanza utawala,bila kupoteza muda alimshika mwanae mkono na kuanza kumswaga kuelekea lile eneo,
"mzee!.."
aliita mama Kadogo na kumfanya mzee Otongo ataharuki kwa kutokutegemea,
"we nani?"
"mie mama kadogo!"
"mama Kadogo? Umefikaje huku?"
"mzee tumekimbia nyumbani,lile jeshi la 666 lilituvamia!"
"yote mmeyataka nyie!!!"
"mzeee!"
"hakuna cha mzee,yote mmesababisha nyie wenyewe!...ni mara ngapi nilikua nawaambia kwamba Vero auwawe?"
"mzee sasa mimi ningewezaje?"
"unataka kuniambia kwamba kijiji chote cha Igesambo kingeshindwa kufanya hilo jambo?
Mume wako ni shujaa,na anajulikana kijiji kizima,kwanini hakufanya hivyo kuokoa maisha yetu??"
"lakini mzee wangu sidhani kama huu ni muda wa kuzozana na kulumbana,inabidi tutafute suluhisho la haya.."
"suluhisho gani unavyodhani? Kwanza una uhakika hata wa kuiona baadae hapo ulipo??!"
alifoka mzee Otongo huku mate yakirukaruka toka mdomoni,
"kwahiyo mzee Otongo tusubirie tufe tu hivihivi?"
"sina matumaini tena,mke wangu wameshambeba,watoto wangu pia watatu washachukuliwa,na Kilembo yule msaidizi wangu tayari ashapigwa chapa kwenye paji lake la uso,amekua mfuasi wao!"
"kwahiyo mzee wangu hakuna cha kufanya kabisa?"
aliuliza tena mama Kadogo kwa sura ya udadisi,
"sijui yani,sijui! Tegemeo letu lipo tu sehemu moja mama Kadogo,sehemu moja tu!"
"sehemu ipi hiyo tena mzee Otongo??.."
aliuliza,
Mzee Otongo alionekana anafikiria jambo,kisha alifungua kinywa chake kwa mjazo akasema
"kila saa naangalia angani,kila mara nanyanyua nyuso yangu kuielekeza juu kutizama na kuchunguza kama kuna tumaini lolote litakalochipukia,tumaini letu ni kuchomoza kwa nyota nyingine angani,nyota itakayoamsha matumaini yetu yaliyokufa,nyota itakayozima uoga wetu na kuangaza amani yetu.."
ghafla sauti ya kitu kilicho kwenye mwendo iligota kwenye masikio yao,walitoa macho kwa uoga,mapigo ya moyo yakaanza kuchochea kasi hasa ya Mtoto Kadogo mwenye matatizo ya moyo,walitizamana kwa macho ya viulizo na midomo iliyogoma kufunguka,joto likatotesha nguo zao,haraka wakainuka na kukimbia kwenda kujificha!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kadogo alikua anahema juu juu na kwa nguvu hali iliyomfanya mzee Otongo amzibe mdomo,ubavu wa mzee yule uliegemeana na wa mama Kadogo aliyekua anatetemeka hivyo mtetemo wote ule uliokua unampitia mama Kadogo alikua anausikia,walitoa macho na kufumba kabisa midomo yao ili wasiskike,huku wakishuhudia watu wale walio idadi ya watu watano wakiwa wanapepesa macho yao kutafuta watu kwa ajili ya sadaka zaidi,mzee Otongo alinong'oneza..
"mama Kadogo tuondoke hapa si salama"
"mh tukiondoka si watatuskia?"
"hapo walipo wananusa harufu yetu na ndo mana unaona wamekazania hili eneo"
"kwahiyo?"
"tuondoke taratibu kabla hawajatugumia"
alizidi kutia msisitizo mzee Otongo,
baada ya muda si mrefu walinyanyuka taratibu toka kwenye kibanda kilichokongoroka walipokua wamejificha,walianza kunyata kama watu wanaohesabiwa hatua,pole pole huku macho ya tahadhari yakiwa yanawatizama wale watu mara kwa mara,mioyo yao ilikua inadunda kwa kasi hasa Kadogo ambaye ana matatizo,alitoka jasho mno ikiwa ni moja ya viashiria ya kuanza kuzidiwa,damu ilikua inazunguka kwa kasi mwilini na mama yake aliligundua hilo,alianza kuhisi mkono wa mwanae alioushika unapoteza nguvu na hakua na jinsi zaidi ya kumnyanyua na kumweka mgongoni,waliendeleza zoezi la kunyata kunyata na kunyata mpaka pale mzee Otongo alipotoa ishara,
"tukimbie mama Kadogo!"
na mbio zikaanza kama za farasi,mzee Otongo alitangulia sana mbele na kumuacha mama Kadogo nyuma hali iliyomfanya aamue kumsaidia mama Kadogo mtoto anaeonekana kumchosha ili wakimbie zaidi,mkono wa mama Kadogo ulishikwa na mzee Otongo kinguvu hasa ili usiponyoke,walijitahidi sana kukimbia huku wakipambana na hali ile ya baridi la usiku na visiki na mawe mbalimbali yaliyoonekana kuwaumiza miguu yao,hawakujali hilo ila walilenga tu kusogea mbele na kuokoa roho zao.Mgongo wa mzee Otongo ulionekana kuhimili mzigo wa mtoto Kadogo ila mama Kadogo ambaye alitoka kukimbia kabla ya kukutana na mzee Otongo alionekana hana nguvu tena ya kuendelea na zoezi lile,alisimama huku akishika kiuno,akasema..
"mzee....uuh!...uuh..siwezi tena!...nimechoka!"
"mama Kadogo jitahidi,hatujawaacha mbali sana wanaweza wakatufikia!"
"mzee Otongo....uuuh..uuh!..nimechoka sana aisee..!"
huku akiinama,
"mama Kadogo!!"
"abee...mzee Otongo"
kiuchovu aliitika
"embu angalia ile!!"
"nini tena??"
mama Kadogo aliuliza,
"ile angani! Ni nyota nyingine ama macho yangu!!?"
haraka mama Kadogo aliyarusha macho yake angani kutizama alichoelekezwa,
"ndio!! ...eh!..ndiooo jamani! Ni nyota nyingine mzee Otongo...ni nyota nyingine!!!"
"ha! Mama Kadogo kuna mmama ana uchungu wa kujifungua sasa hivi tunavyoongea!! Na ndie atazaa mtoto atakaetuokoa,mama Kadogo tumaini li hai!..huree!!"
"sasa huyo mmama yupo wapi??"
"kijiji cha pili toka ilipo Igesambo,na inabidi tumuwah kabla huyo mama hajadhuriwa na Jeshi la 666 kwani wakiiona tu ile nyota watamtafuta kwa udi na uvumba ili wamtokomeze!!...haraka inuka mama Kadogo,haraka tumuwahi mtoto anekuja!"
haraka mama Kadogo alieanza kupata nyuso yenye mwanga wa matumaini aliinuka na wakaanza kutembea harakaharaka kwa dhumuni la kukusanya nguvu ya kukimbia hapo mbele,kushoto kulia kushoto kulia miguu yao ilipiga maksai wakitafuta kijiji cha pili toka kilipo Igesambo,kijiji cha Utowele,kijiji cha wavuvi na wakulima kama imaanishavyo jina lake,kukifikia kijiji cha Utowele inabidi wavuke mto mkubwa Inguvai,wapite safu ya milima Iramba kisha ndipo watakapokanyaga ardhi ile ya mwanga,ardhi ya tabasamu,ardhi ya mapinduzi na ardhi ya ukombozi,baada ya safari yao kutimiza nusu saa walianza kusikia maporomoko ya maji yaliyowajulisha ya kwamba wapo karibu na mto,mto Inguvai usiopungukiwa na maji misimu yote ya mwaka kutokana na kutokea kwenye safu ya milima Iramba ipokeayo mvua za kutosha zipendeshazo msitu kwa umbijani,
ilihitaji uangalifu mkubwa sana kuvuka mto ule hasa muda ule wa usiku,maji yake yana nguvu mno na yanatosha kabisa kumpeleka mtu mzima hata mnyama yeyote endapo akitumbukizwa.
Walivyowasili kwenye kingo za ule mto mzee Otongo alimshusha chini kadogo,kisha aligeuza sura yake na kumtazama mama Kadogo akisema
"inatubidi tusali mama Kadogo,mungu awe nasi na atushike mkono,atuongoze kuuvuka mto huu,na pia atuongoze tuivuke milima ile...na hata kama mmoja asipofanikiwa isiwe mwisho wa mapambano.umenisikia mama kadogo?"
"Inatubidi tusali mama Kadogo,mungu awe nasi na atushike mkono,atuongoze kuuvuka huu mto,na pia milima ile....na hata mmoja wetu asipofanikiwa isiwe mwisho wa mapambano yetu.umenisikia mama Kadogo?"
sura yenye msisitizo isiyotania ya mzee Otongo iliyatamka yale maneno.
"sawa mzee Otongo,inatubidi tupigane mpaka tone la mwisho la damu yetu,inabidi tufe tukijaribu"
alieleza mama Kadogo huku chozi likimlengalenga.
Aliyatupia macho ya huruma kwa mwanae,akachuchumaa akambusu kwenye paji la uso kisha aliinuka na kusema
"sasa tunaweza kuvuka.."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akamueka mwanae mgongoni,akaanza kusogelea maji ya mtoni taratibu huku akitanguliwa na mzee Otongo.
Mto Inguvai hauna daraja la kumuwezesha mtu kuvuka kwa urahisi,ni utashi wa mtu tu ndio unaotakiwa ili aweze kurukia mawe yaliyokuwepo pale kwa ajili ya kuikuta ng'ambo,ilimuwia vigumu sana mama Kadogo kurukia yale mawe kwani ukiachana na lile
giza la ule muda bado alikua na mtoto mgongoni,walisogea hatua mbili tatu huku moyo wa kila mtu ukidunda kwa uoga na tumbo la kila mtu likisokota kwa uoga pia,mawe waliyokua wanayakanyaga yalikua yameshika utelezi hivyo ilihitaji uangalifu mkubwa na bado miguu yao iliyo peku ilikua inapitiwapitiwa na maji kitu kilichoashiria ya kwamba maji ni mengi kiasi cha kukaribia
kufunika yale mawe yatumiwayo kama kivushio,hakukua na muda wa kutosha wa kuangalia nyuma,kila mtu aliyatoa macho kwa kiasi kikubwa ili yapambane hata kidogo na lile giza lililopo ili apaone pa kuutuliza mguu wake,walizidi kusogea na mwendo wao wa kinyonga na ilibakia kama mawe matano tu ili waweze kupita kile kizuizi,ghafla sauti kubwa ya mlio wa pembe la ng'ombe iliskika!!
Haraka kwa uoga mama Kadogo aligeuka nyuma kabla sauti ya mzee Otongo kufika masikioni mwake ya kwamba hatakiwi kugeuka!!
Mguu wake wa kulia ulio mbele uliteleza na kumfanya aifungue mikono yake kwa ajili ya tahadhari ya anapodondokea na kumuacha Kadogo aliekua kambeba mgongoni akidondoka kwa urahisi!!!
Mikono yake miwili ilishikilia mawe kwa nguvu na kumfanya abakie salama kwa kutopelekwa na maji ila mwanae Kadogo ambaye kamwili kake hakakutosha uzito kushindana na ile nguvu ya yale maji alibebwa kama kikaratasi akimuacha mamaye akilia kwa uchungu bila msaada wowote!!
Mzee Otongo ilimbidi arudi nyuma kitaratibu,alishika mikono ya mama Kadogo iliyoanza kuzidiwa nguvu na kuanza kumvuta kwa lengo la kumuondoa kwenye yale maji yenye kasi kubwa!!
"mama Kadogo jitaahiiidiiiiiiii!!!!.."
"mzee Otongo niache tu nife! Mwanangu jamani!!!!!"
"mama Kadogo hatuna muda wa kupotezaaa!!!!..
Tafadhali jitahidi utoke kwenye hayo maji nguvu inaniishiaaa!!!!!"
"mwanangu Kadogo jamaniii!!!"
"mama Kadogooo!!!...tafadhali nadhani unakumbuka nilivyokuambia kabla hatujavuka..tafadhali jitahidi utoke,tafadhali nguvu zinaniiiishaa!!!"
kwa nguvu aliropoka huku akikunja sura!
* * * *
upande wa pili wa shilingi jeshi la 666 lilikusanyika,ile mbiu ya pembe la ng'ombe iliyopigwa ilikua ni ishara ya kwamba wanaitwa,walisimama kwa utulivu na usikivu,na tahamaki ndani ya jeshi hilo mama Utopi alikuwepo!!..na si tu huyo hata mama
Marinda na Vero!!...walishapigwa chapa,hivyo walishakua chini ya utawala wa Chernobog!!
Mzee mmoja asie mfupi wala mrefu yani saizi ya kati alisimama mbele yao,mkononi alishika fimbo yenye alama ya nyota nyekundu na kimavazi alinawirishwa kwa rangi nyeusi na nyeupe,macho mekundu na lips zake pana ziliönyesha ana kabiliwa na jambo,bugudha na hasira zilionekana kumteka!!
Kabla ya kufungua mdomo na kunena jeshi la 666 liliinamisha vichwa na kudhihirisha ya kwamba alie mbele ni mkubwa wao,
"ni nyota ndio iliyotuita!
Ni kwasababu ya nyota tupo hapa!!
Nyota nyingine imechomoza angani,nyota itishiayo nyota ya CHERÖBOG!!!..nyota imaanishayo ya kwamba kuna mtoto anazaliwa,nyota imaanishayo hatari kwa utawala wa giza,nyota itakayoamsha tena Jua lililopotea,nyota itishiayo makazi ya KUZIMU duniani!!!
Hakikisheni huyo mtoto haponi! HAKIKISHENI MNAMTOKOMEZA KABLA JUA HALIJACHOZA TENA!!! HAKIKISHENI
MNAMMALIZA HARAKA IWEZEKANAVYO!!!"
"Ameen!!"
Walikimbia kwa kasi ya ajabu,hasira na dhamira ya kweli ikitawala vichwa vyao,kila mmoja kwenye paji lake la uso alikua na alama ya 666 ikiashiria na kuthibitisha ya kwamba anamilikiwa na utawala wa giza,utawala wa wapinga mwanga,utawala wa nyama na damu,utawala wa mungu mweusi,utawala wa CHERNOBOG,macho yao mekundu na pua inusayo harufu ya binadamu,miili yao ya baridi na yenye rangi ya kijivu bila kusahau masikio yao yaliyosimama yalikua ni sare zao mbali na nguo zao nyekundu na nyeupe,walitumwa wakamuangamize mtoto aliezaliwa,walitumwa wakamtokomeze haraka iwezekanavyo kabla ya jua kuchomoza kwani ni hatarishi kwa utawala wao na ni hatarishi kwa malengo yao,baada ya muda wa dakika arobaini na tano walishawasili kwenye kingo za mto Inguvai!!!
Je wakina mama Kadogo wako wapi?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa mbaali juu ya safu ya milima Iramba mzee Otongo na mama Kadogo walionekana wakizidi kukwea,walizidi kupanda milima kwa lengo la kwenda upande wa pili kumuwahi mtoto aliezaliwa kabla ya kuchukuliwa au kuwahiwa na jeshi la 666,miili yao ilikua imechoka kutokana na zoezi lile gumu lakini hawakujiruhusu wapumzike kwani walifahamu ya kwamba jeshi la 666 li njiani na tayari watakua na taarifa juu ya uzao ule,wote walikua wanahema kama mbwa hasa mama Kadogo ambaye bado uchungu wa kupotelewa na mwanae ulikua umemtawala moyoni,alishindwa kuzuia machozi yasimtoke lakini pia hakutaka aruhusu miguu yake isimame,alimuita mzee Otongo alie mbele yake kisha akampa mkono wake wa kulia,akasema
"nahisi kichomi!"
..mzee Otongo akamvuta na kumkumbatia kwa nguvu kisha akamnong'oneza..
"imebakia umbali wa kama nusu saa kufika kijiji cha Utowele,imebakia huo umbali tu ili tulikute tumaini letu,imebakia tu umbali huo kwa ajili ya maisha yetu.hapa nilipo nina kiu na miguu inanivuta mno,lakini unanihitaji ili tuendelee,na mimi pia nakuhitaji ili niendelee,tafadhali jitahidi tukamilishe tulichokianzisha"
yale maneno yalimpa motisha kubwa mama Kadogo,alishusha pumzi ndefu kisha wakaanza tena kutembea kuelekea mbele kwa mbele.
Wafuasi wa jeshi la 666 bila kujiuliza mara mbilimbili walijitosa ndani ya mto Inguvai,mto wenye maji yenye kasi na nguvu ya hatari,lakini cha kushangaza walipiga mbizi mithili ya samaki na hakuna hata mmoja wao alieonekana kuzidiwa!!..hata mama Utopi mama Marinda na Vero waliopigwa chapa tayari walionekana kumudu yale maji!!
Mikono yao ilikua na nguvu ya ajabu na pia nyuso zao zilionekana kupambwa na alama ya moto ya tarakimu 666!
Baada ya kufika upande wa pili wa mto,pua zao zilianza kuvuta harufu ya binadamu na haraka bila kupoteza muda walianza kuifatilia kwa mwendo wa kasi,huku macho yao yalioakisi mwezi yakionekana kung'ara mithili ya paka!!
Umbali waliopo wao ulikua ni kama kilomita moja kamili tokea walipo wakina mama Kadogo,ila kwa ile kasi waliyokua nayo ilikua ni hatarishi na hivyo uwezekano wa kuwafikia ulikua ni mkubwa ukizingatia matatizo ya vichomi na miguu inavyowapa mtihani mama Kadogo na mzee Otongo.
Jeshi lile la 666 halikua na utofauti wowote na wanyama,hawakua na huruma hata kidogo kutokana na mioyo yao kubadilishwa na kua ya kishetani,maumbo yao pia hayakua ya binadamu wa kawaida,kuanzia kwenye vidole na kucha mpaka kwenye unywele,walikua na nguvu mno na ni kutokana na giza lililopo na ndio mana walipopewa maagizo waliambiwa wayatekeleze kabla ya jua kuchomoza kwani ndio utakua ukomo wa nguvu zao za ajabu!
Walizidi kujongea kwa kasi bila kuonyesha dalili yoyote ya kuchoka huku wakiwa wamepangana kimstari!...mara ghafla mwenzao alie mbele alisimama kisha akageuza shingo na kuwaambia wenzake
"nimeona watu kule juu!!!"
Mungu wangu wale walikua wakina mama Kadogo!!
Jeshi la 666 liliongeza kasi huku macho yao yakieka msisitizo kwa wale watu kwa mbali waliowaona,mzee Otongo alihisi watu wanakuja kwani alisikia vishindo vikubwa na sauti za watu ambao hazikuleta maana masikioni mwake,aligeuka na kumshika
mkono mama Kadogo na kuanza kukimbia nae kwa kasi!!.
"mama Kadogo kimbia wanakuja!!!"
kwa tahamaki alitamka huku akimvuta mama Kadogo alietia kidogo uvivu,mzee Otongo alijitahidi kumburuta mama Kadogo alieonekana kama mzigo kwa nguvu zake zote na hakutaka kabisa kumuachia,mama Kadogo hakutamka neno lolote kitu
kilichoonyesha ya kwamba alishakata tamaa hata ya kuishi!!..hata kasi yake ya kukimbia ilikua ni ile ya kukosa matumaini kabisa!
Jeshi! Jeshi! Jeshi la 666 lilizidi kuwakaribia wakina mama Kadogo na huku mbele yao akionekana mama Utopi ndie aongozae msafara!
Kanzu yake aliyovalishwa yenye rangi nyeupe nusu na nyekundu haikutosha kumzuia kukimbia kwa kasi mithili ya simba alieona swala,aliruka viunzi na visiki,aliruka mashimo na vizingiti lengo kichwani likiwa moja tu,la kumuangamiza mtoto aliezaliwa na kuua wote wale waonekanao vikwazo kwao,
kimbia! Kimbia! Kimbia!
Alizidi kusema mzee Otongo kwa sauti iliyokaribia na kulia huku bado aliekua anamvuta akiwa kimya na mzito kama furushi la dhambi!
Hayawi hayawi yakawa! Mama Kadogo alipigwa na gongo mgongoni na kudondoka kama mzigo chini!!
Alilia kilio cha maumivu kilichokwangua hadi sakafu ya moyo wa mzee Otongo aliegeuka na kushuhudia jeshi! Jeshi! Jeshi la 666 likiwa tayari karibu nae lishawadia,
alipigwa kofi moja kali lililomrusha mbali mithili ya mtu aliepigwa na shoti ya umeme!
Hata kabla ya kufungua macho yake alisikia mgongo wake ukiita kwa mlio wa nguvu uliosababishwa na kupigwa na gongo!
Aaaaaaahhh!! Alilia mzee Otongo kwa uchungu wa maumivu ambao haukusaidia hata kidogo kumuokoa na kipigo alichokua anakipokea toka kwa jeshi! Jeshi! Jeshi la 666,alipigwa kipigo cha mbwa mwizi!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipigwa kila eneo na alichanwa chanwa mgongoni na makucha ya wale watu walio na mioyo ya wanyama!
Hakuwahi kuhisi maumivu kama yale toka azaliwe na mama yake Lenaka miaka arobaini na mbili iliyopita ndani ya kijiji cha Igesambo! Macho yake yalianza kupoteza muelekeo na yakaanza kuelekea juu kisha yakafumba kabisa!
Upande wa nyuma hatua kama tano mama Kadogo alikua bado anashushiwa kipigo na wanawake wenzake wakina mama Marinda,Vero na mama Utopi waliokua wanyama tayari chini ya CHERNOBOG!!
Hawakua na fikra za huruma hata kidogo! Hawakua na mioyo ya kibinadamu! Hawakumjua tena mama Kadogo na akili yao haikua tena ya binadamu hivyo walitumia kila zana ikiwemo mikono yao iliyo na kucha mithili ya simba kumjaza alama za kutosha mmama yule alieonekana yu kimya!!
Kabla ya wao kuridhika na lile zoezi ghafla jua lilianza kuchomoza,anga likaanza kuwa la kahawia na giza likaanza kupotea!!
Walipigwa na butwaa na kuwehuka huku wakitoa sauti za ajabu na wakikimbia huku na huko bila mpangilio kurudi kule walipotokea,walichanganyikiwa baada ya kuona ile hali na zile chapa zao zilizo juu ya mapaji yao ya uso zilianza kufuka moshi uliodhihirisha ya kwamba wanaungua!!!
Hae hae lile eneo lilikua! Lakini bado mama Kadogo na mzee Otongo walikua kimya huku miili yao ikivuja damu!!
Kabla ya wao kuridhika na lile zoezi ghafla jua lilianza kuchomoza,anga likaanza kua la kahawia na giza likaanza kupotea!!
Walipigwa na butwaa na kuwehuka huku wakitoa sauti za kupayuka na wakikimbia huku na huko bila mpangilio kurudi kule walipotokea,walichanganyikiwa baada ya kuona ile hali na zile chapa zao zilizo juu ya mapaji yao ya uso zilianza kufuka moshi uliodhihirisha ya kwamba wanaungua!
Hae hae lile eneo lilikua!
Lakini bado mzee Otongo na mama Kadogo walikua kimya huku miili yao ikivuja damu!
Kuchomoza kwa jua kulithibitisha kushindwa kwa CHERNOBOG (Mungu mweusi),lengo la kumuangamiza mtoto aliezaliwa ilibidi lifanyike haraka na kwa ufanisi mkubwa kabla ya jua kuchomoza kwani nguvu zake zina mipaka,zina mipaka? Ndio zina mipaka,wakati wa usiku huwa ni kali na za kutisha zaidi na ndio mana walitaka watekeleze ule mpango kabla ya jua kuchomoza ili kuhakikisha ya kwamba jua halitokutana tena na uso wa dunia,hivyo utawala utakua wao daima na milele!
Masaa yalizidi kusonga huku miili ya mzee Otongo na mama Kadogo ikianza kuzongwa zongwa na Inzi waliofuata majeraha makubwa waliosababishiwa na jeshi! Jeshi! Jeshi la 666,saa nne asubuhi isiyotambulika madakika yake watu watatu waliokua katika shughuli za uwindaji toka kijiji cha jirani Utowele waliiona miili ile miwili iliyolala kama mizoga,walishtushwa na lile jambo! Na moja kwa moja walidhani ya kwamba watakua wamedhuriwa na wanyama wakali wa msituni kwani safu ya milima Iramba ina wanyama wakali kama chui na simba ambao ni mara chache kuonekana mida ya asubuhi na mchana,mapigo ya moyo ya mzee Otongo yalisikika kwa mbali sana! Vile vile na ya mama Kadogo kitu kilichoashiria ya kwamba hawana muda mrefu maisha yao yatarudi yalipotokea,yani mavumbini.
Wale watu watatu,mmoja akiwa ni mzee wa makamo na wengine wawili wakiwa vijana,waliibeba ile miili na kuelekea kijijini kwao,ilibidi wasitishe lile zoezi la uwindaji kwa sababu za kibinadamu,je watapona? Hilo lilikua ni swali lililokita kichwani mwa wale watu walioonyesha roho za utu.
Baada ya mwendo wa robo saa waliingia kijiji cha Utowele,kijiji walichokua wanakitafuta wakina mama Kadogo kabla ya kukumbwa na la kuwakumba,kijiji chenye wakulima na wafugaji kwa kiasi kikubwa,kila mtu alishangazwa na ile hali! Na pia walibumbazwa na lile tendo! Hawa mbona wametuletea mizoga? Hilo ndilo swali lililokuja kichwani kwa kila alieshuhudia lile tukio,haraka taarifa zilienea! Kila mtu alieona alimtaarifu na mwenzie,mwisho wa siku kijiji kizima!
We baba Madhifa mbona umetuletea mizoga kijijini kwetu??? Maswali yalirushiwa kwao,kila walipotaka kujibu walikumbana na lingine! Na hali ilikua mbaya zaidi baada ya kusema kuwa wameiokota msituni,wanakijiji walicharuka! Waliwataka wakina baba Madhifa na wanae wawili wairudishe ile miili kwani wanaweza wakaleta laana kwenye kijiji chao,hakuna alietaka kuwasikiliza kwa maelezo zaidi na ukizingatia wakina baba Madhifa ni jamii ndogo ya wawindaji kwenye kijiji cha Utowele kilichojazwa kwa kiasi kikubwa na wafugaji na wavuvi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tokaaa!!! Peleka mizoga yako huko!!!!!
Hatutaki maiti tusizozijua kijijini kwetuuu!!..we una okota okota tu!!
Maneno ya kebehi na kashfa yalirushwa kwao yaliyochanganyikana na dharau kutokana na hadhi yao ndogo ndani ya kijiji cha Utowele,waligeuka na kuanza kurudi msituni walipotokea baada ya kuona zoezi lao lilioambatana na utu limepingwa vikali na wanakijiji wenzao,ghafla kabla ya kutokomea,sauti ilisikika toka kwa mmoja wa wanakijiji aliyeonekana ni mkubwa kiumri akitokezea toka kwenye mlango wa nyumba ndogo ya udongo iliyojaa moshi ndani kutokana na shughuli ya upikaji dawa aliyokua anaifanya,
"suubiiiiiirrrriiiinii!!"
huku akiambatanisha na zoezi la kupunga mkono!
"waleteni hao watu!!"
"sio watu,ni miili ile! Wamekufa!"
sauti ya mmoja wa wanakijiji iliskika ikipinga,
"nyamaza!! Nani kakuambia wamekufa??"
aliuliza yule mzee na kufanya kidogo ukimya utawale huku macho ya wanakijiji yakionesha kujawa na hofu,
baada ya muda mfupi baba Madhifa alikua ashafika kwenye eneo la tukio na wanae wawili waliowabeba wakina mzee Otongo na mama Kadogo,waliiweka ile miili chini kama walivyoelekezwa,yule mzee akaanza kuikagua!
Ilichukua kama dakika kumi yule mzee akiitizama na kuipekua ile miili huku wanakijiji wakiwa wamemzingira,aliinua macho yake na kutoa amri ya ile miili kuingizwa ndani,wale vijana wa baba Madhifa walitekeleza hilo jambo haraka,waliingiza ile miili ya
mzee Otongo na mama Kadogo ndani ya kale kajumba kadogo cha udongo cha yule mzee alieonekana kuheshimiwa na kusikilizwa na wanakijiji,bila ya kujivunga yule mzee nae aliingia ndani na kuwaacha nje wanakijiji waliokua na shauku kubwa ya kutaka jua kinachoendelea,baadhi yao walianza onekana wakijiondoa kwenye lile eneo taratibu na kwenda kuendelea na
shughuli zao zingine huku bado midomo yao ikiteta lile tukio lililoonekana kuchota hisia zao kwa kiasi kikubwa,wakati hayo yote yanachukua nafasi kuna baadhi ya wanakijiji walikua hawana habari kabisa kuhusu lile tukio!!...labda kutokana na kubanwa na
hali husika,umbali wa nyumba kumi na tano toka pale pa yule mzee kulikua na nyumba moja tulivu ya udongo iliyopakwa chokaa iliyofanya ionekane ni ya kipekee kidogo tofauti na nyumba zingine,madirisha yake makubwa yapitishayo hewa na sauti bado
hayakutosha kuwajuza watu walio ndani juu ya kinachoendelea kwa nje,nyuso zao zilijawa na tabasamu na huku wakionekana
kutowaza kabisa yanayojiri ulimwengu mwingine,
"enhe..sasa nimpe jina gani?"
lilikua swali alilouliza mdada mmoja aliemshika mtoto akijulikana kama Julina huku akitabasamu
"mmh mie mwenyewe sijui,we si ndo mama bwana! Mie kazi yangu ya ukunga nshaimaliza"
alijibu mama Halima,mmama mwenye rangi ya maji ya kunde,mkunga maarufu kijijini aliebakia baada ya kifo cha mama Ramla miaka miwili iliyopita,
"au tumsubirie baba yake?"
"utakavyoona wewe ni sahihi..."
"ujue nini mama,mimi ni kama mwanao,sina utofauti na mwanao Halima,sijui hata nikushukuru vipi kwa kweli,namsubiria tu mume wangu arudi ndipo tutakapojua cha kufanya"
"wala usihofu mwanangu,ujue hii kazi ya ukunga ni kama karama kwangu,si ajira!! Kwahiyo naifanya kwa ajili tu ya kuwasaidia
wanizungukao kwani baada ya mwanangu Halima kufariki,kila mtoto nizalishae ni kama mtoto wangu"
"pole sana mama,kifo cha Halima kiliniachia pia pengo kubwa,kama unavyojua,alikua ni rafiki yangu mkubwa! Yeye ndo kwa kiasi kikubwa alinishawishi niole na Kitanzi"
"tuachane na hayo mwanangu nisije nikatonesha donda lililoanza kupona,ila mumeo Kitanzi yupo wapi saa hizi?"
"mmmh...hata sifahamu kwa kweli,aliahidi kuwa atakuwepo hapa usiku wa jana,lakini mpaka saa hizi sijamtia kwenye zangu mboni"
nyuso zao zilificha matabasamu yalionawiri hapo kabla,mawazo yakaonekana kuwashika hatamu,Julina alianza kupata hofu,mama Halima akaligundua hilo..
"sikiliza mwanangu,ujue sisi binadamu tunapanga na mungu pia anapanga,hivyo huwezi jua,tuombe tu uzima!"
"mmh kweli mama.."
kidogo maongezi yaliingiliwa na kilio cha mtoto,mtoto alieonekana hana muda mrefu ulimwenguni,haraka Julina alitoa titi lake la kushoto na kumyamazisha nalo,uso wa Mama Halima ulionekana unaficha jambo,na hata macho yake yalikua yanasadifu ya kwamba ana kitu ndani ya mtima chamsumbua..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"mama vipi??..mbona hivyo tena!"
"mmh,kuna kitu kinanitatiza kusema kweli,jana usiku wakati tupo katija zile shughuli za kufungulishana nilisikia kelele!!"
"kelele??...si kelele zangu hizo ama?"
"hapana!...mara ya kwanza ilikua ni kelele ya kike,na mara ya pili ilikua ya kiume!!!"
"wee!..mie mbona sikuzisikia??"
"usingeweza kuzisikia,uchungu uliokua nao usingekuruhusu ufanye hilo.."
"mama una uhakika na hilo jambo??"
aliuliza Julina kwa umakini huku akimtikisatikisa mwanae kitaratibu,
"asilimia zote!...na ubaya ni kwamba kila ninapotulizana,zile sauti hunirudia masikioni!!!!!"
kwa msisitizo alinena Mama Halima huku akiyatoa macho,hofu ikaanza kumrudi Julina tena!!...huyo atakua sio mume wangu kweli?? Alijiuliza moyoni,kabla hajapata majibu,hodi ikaskika!
"ngo!-ngo!-ngo!"
"nani??"
aliuliza mama Halima,
"wageni!!"
sauti ilijibu toka nje,
"wakina nani?"
"wageni!!"
ilirudia tena!
Ilimbidi mama Halima ainuke na kwenda kuchungulia dirishani kabla ya kufungua,he!! Alishuhudi mabibi wawili wageni machoni wakiwa mlangoni!!..aligeuza shingo yake na kumtizama Julina kwa tahadhari,
"unawajua hawa watu?"
aliuliza,
"wakina nani?"
"njoo uwaone!"
alielekeza kwa sauti ya chini iliyokamatwa na kauoga,
Julina aliwatazama wale mabibi kupitia pale dirishani kisha akamjibu mama Halima kwa kunong'oneza,
"mmh mh,siwajui!!!"
Cha kushangaza walivyorudisha tena nyuso zao dirishani kutizama nje...hawakuona kitu!!!!..Pah!!!..tik-tak!!! Tik-tak!!! Tik-tak!!! Tik-tak!!..mioyo yao ilianza kwenda kasi ya ajabu!!! Bumbuwazi lilikamata midomo yao bara-bara! Macho yaliwatoka mithili ya kwamba wamemshuhudia shetani akionja pepo!!!..walitupiana macho ya uogo wakiulizana wameenda wapi??? Swali lililopasua hisia zao mithili ya shoka kali lililotoka kiwandani kwenye gogo bua lililochoka!
Mungu wangu..watafanyaje sasa?? Hilo lilikua ni swali la pili rejea lililokita vichwani mwao kama hitimisho!!!
Hapakukalika tena!!..nyumba ilizidi kuwa ndogo kwao!
* + * + *
koh-koh! Sauti ya kikohozi cha maumivu kiligona sikioni mwa mzee Patili,aligeuka haraka na kuangalia kilipotokea akagundua ya kwamba chatoka kwa mzee Otongo aliekua amelala chini chali,alitabasamu kwa mbali,jitihada za dawa yake aliyompaka zilionekana kuvuta kheri,hakutaka kupumbazwa na hilo jambo,aligeuka na kuendelea na shughuli yake ya kumpaka dawa mama Kadogo taratibu akimalizia miguuni baada ya mikononi na usoni akijitahidi kuyaziba majeraha na dawa ile ya unga yenye rangi ya kahawia,mchanganyiko wa miti mbalimbali iliyosagwa.
Chumba kilitawaliwa na moshi kwa kiasi kikubwa,lakini hilo halikuonekana kumkwaza mzee Patili,kwani tangu na tangu,enzi na enzi amekua katika yale mazingira ambayo hasa huchangiwa na shughuli zake za upikaji dawa,mvi ziligoma kabisa kuja kichwani japokua umri uliruhusu hilo,uso wake ulio na makunyanzi ndio uliothibitisha ya kwamba kala chumvi,mzee Patili alikua ni zahanati tosha pale kijijini,akiheshimika na kusikilizwa kama marehemu baba yake aliemrithisha hizo kazi.Baada ya kumaliza ile shughuli ya upakaji dawa,alishusha pumzi ndefu kisha akajituliza kwenye kigoda chake chenye ufa kwa mbali uliodhihirisha ya kwamba ni cha muda mrefu,haraka akili yake ilimtumbukiza kwenye lindi la mawazo,lindi la mawazo mazito juu ya ndoto aliyoota usiku wa kuamkia hiyo alfajiri,ndoto ile ilionekana kumkosesha amani na hata raha vilevile na kila alipotaka kuitafutia ufumbuzi hakupata kitu!!!
Alitizama juu ya dari kimawazo huku kichwa kikiegemea mkono akijaribu kuitumikisha akili yake iliyojaa uzoefu wa maisha kumpa majibu,
ghafla!!!!
"mzee patili funguaaa!!!"
sauti za kile zilisikika toka nje,
"niniii???..nyie wakina nani!!!"
kwa tahamaki aliuliza,
"Julina na mama Halima!!!..tafadhali tufungulie haraka!!"
alijibiwa,alijinyanyua toka kwenye kile kigoda haraka na kuelekea mlangoni,akaufungua mlango na haraka kwa papara waliingizana wakina mama Halima!!
"nyie vipi???"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
aliuliza mzee Patili,hakujibiwa,akauliza kwa mara ya pili kwa sauti ya msisitizo!
"nyie kuna nini?? We mama Halima vipi na huyu Mzazi tena!!!"
huku wakihema kwa pupa wakajibu,
"kuna wabibi wawili!!"
"wamefanya nini?"
"wa..wa..walikua wanagonga..mm..mlang..mlango.."
"halafu haraka wakapotea!!!"
Julina akamalizia sentensi huku akiwa kamkumbatia mwanae na mikono itetemekayo!,
"wakapotea!!! Wakaelekea wapi??"
"hatujuuii!!!!"
julina alidakia,
"he! Mzee Patili hawa waliolala hapa chini wakina nani???"
aliuliza mama Halima baada ya kuiona ile miili ya mama Kadogo na mzee Otongo pale chini,Julina pia mwenye damu iliyotawaliwa na uoga nae alistuka baada ya kuona hilo,akatahamaki
"mungu wangu!!!! Mzee Patili hawa wakina tena???"
"msijali kuhusu hao watu,waliletwa hapa na baba Madhifa,waliokotwa toka porini,embu punguzeni uoga na presha enh...tulieni embu,tulieni kisha mnielezee kilichojiri"
aliwatuliza mzee Patili.
Mzunguko wa damu wa Julina uliongeza kasi kutokana na uoga! Alikua anahema kwa kasi,mama Halima vilevile!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzee Patili ilimbidi anyamaze huku akiwashuhudia wale wakina mama kwa jicho la kutafakuri hali ile iliyowatokea,moshi uliokuwemo mule ndani ulianza kumuathiri mtoto,akaanza kupaliwa na kikohozi hali iliyomfanya mzee Patili kumshauri atoke nje,kiuoga alijibu
"nani?? Mie!! Ah-ah sitoki nje! Wale wabibi watanifata!!!"
mzee Patili aliamua kumaliza zogo,alimnyakua mtoto toka kwenye mikono ya mama yake Julina kisha akatoka nae nje,hali ya kushangaza Julina nae kwa uoga akatoka nje!!!!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment