Search This Blog

666 NYAYO ZA KUZIMU - 1

 





    IMEANDIKWA NA : STEVIE BYBLOVE FERICIOUS





    *********************************************************************************



    Simulizi : 666 Nyayo Za Kuzimu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Upepo ulivuma mno,miti na majani ilionekana kuinama kutokana na kushndwa kupambana na pepo



    ile kali,giza lilikua kali sana kwa kuwa mwezi ulikua umefunikwa gubigubi na wingu zito jeusi



    lisiloonyesha hata



    kama mvua itanyesha.utulivu wa hali ya juu ulitawala,hakuna kilichosikika zaidi ya milio ya kiuoga



    ya mbwa na vijidudu vidogo vidogo vya usiku,kila kibatari kilichowashwa ilhali na moto ilizimika



    kutokana na kutokua



    stahimilivu na hali iliyokuwepo,hakukuwa na mtu yeyote alieonekana yu nje akifanya jambo



    lolote,na ni kutokana na hali ya ajabu ya ghafla iliyotawala katika lile eneo.Kwa mbaali angani



    ilionekana nyota ndogo



    ikichomoza,ghafla sauti ya kuamuru ilisikika kutoka kwenye kijumba cha msonge ikisema..



    "sukuma,jitahidi Vero sukuma!...enhee..tena...tena!!..ewaaah!...umepata mtoto wa kiume Vero!"

    sauti ya mama Marinda mkunga wa jadi Maarufu kijijini iliskika..iliyoambatana na tendo na



    kumsaidia bibie



    Veronica kupata mtoto wake wa kwanza kabisa,upepo ulitulia ghafla,hali iliyomfanya Mama Utopi



    kupumzika na zoezi la kukikinga kibatari kisizimwe na upepo ili shughuli ile ya Ukunga iliyokua



    inafanyika ipate kuisha



    salmini,alikiweka kile kibatari chini na kusogea karibu zaidi ili apate kumshuhudia mtoto aliyeingzwa



    ulimwenguni..



    "mbona hata halii?"



    akauliza mama Utopi kwa shauku kubwa ya kufahamu,

    "mie mwenyewe sijui,kwani miaka yangu yote ishirini ya ukunga sijawah kukutana na hili jambo la

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mtoto kutolia ingali anaonyesha yu mzima kwa kuchezesha mikono na miguu yake.....

    Na isitoshe...ni wa baridi mno! Zaidi hata ya maji ya asubuhi ya mtoni!"



    alisema kwa msisitizo mama Marinda huku akimtolea macho mama Utopi aliesimama,Vero



    hakuchangia chochote kwani hakuwah kukumbana na lile swala kokote pale,hivyo aliishia



    kuwatazama mama Utopi na



    Mama marinda wakiwa wanajibizana.Mama marinda aliemshkilia mtoto alianza kuingiwa na



    hofu,alimtazama yule mtoto kwa macho yakinifu hakupata jibu,alionekana ni mtulivu



    mno,hakuonyesha dalili ya kucheka wala



    kulia,Mama Marinda akaanza kuhisi mapigo yake ya moyo yanaenda mbio,jasho lililojaa uoga



    taratiibu lilishuka...



    Mama Marinda alianza kuhisi mapigo ya moyo yanaenda mbio kuliko kawaida,mikono yake



    iliyomshka mtoto ilianza kutetemeka,alitoa macho kwa mshangao na ghafla aliropoka..

    "mama Utopi embu mchukue huyu mtoto,haraka!!"

    naye mama Utopi bila kujivunga aliinama na kumtwaa mtoto akiwa na kiulizo kichwani..

    "kwani vipi jamani?"

    aliuliza Vero baada ya kuiona ile hali linayoendelea pale,

    Mama Marinda alikua kimya akionekana kubanwa na mawazo hali iliyompa nafasi mama Utopi



    kunena..

    "mwanao ni wa tofauti Vero?"

    "kivipi?"

    "kwanza halii,pili ni wa baridi mno!"

    "mmmh...haitokua ni kwasababu ya hali ya hewa?"

    "sidhani,mana hata hali yenyewe imebadilika tu baada ya wewe kusikia uchungu,na sasa hivi



    umeshajifungua huoni kama hali imetulia?"

    alisema Mama Utopi huku akimtazama Vero alieonekana anafikiria jambo kutokana na kauli



    aliyoambiwa,aliona Vero anapata shida kuongea na ni kutokana na kutoka kujifungua na hali ilikua



    inaonyesha dhahiri ya kwamba kachoka,hakutaka muongelesha tena na alimsihi apumzike kwa



    muda,mama Utopi alimtazama vizuri mtoto aliyembeba huku mikono yake ikistahimili baridi



    lililoonekana kuanza kumzidia,allivua khanga yake na kubakia na gauni tu lililochoka la rangi



    nyekundu lenye maua maua kisha ile khanga akamfunikia tena mtoto ili kujikinga na mikono yake



    vilevile na kumkinga mtoto na hali ya hewa.Mama Utopi,mmama mwembamba mwenye uweupe wa



    mbali na kichwani akiwa kasuka vibutu vibutu vilivyoonekana kufumuka fumuka alimgeuzia shingo



    mama Marinda,alimuona bado butwaa ya mawazo imemshika...na yupo tu pale kifikra,alimstua..

    "we mama Marinda!"

    "Abee!..."

    kwa kukurupuka aliitika,

    "vipi wewe?"

    "mmmh...embu njoo nje tuongee kidogo"

    alijibu Mama Marinda huku akitoka nje ya ile nyumba ya msonge akifuatiwa na Mama Utopi baada



    ya kumkabidh Vero mwanae,

    walisogea kidogo mbali na ile nyumba hali iliyoashiria ya kwamba maongezi yao ni ya siri.

    Mama Marinda aliangalia kushoto na kulia kama kuna mtu,akatengenezea khanga yake rangi ya

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kijani na manjano yenye nyota nyekundu,akakuna kichwa chake kilicho na mvi zilizotosha



    kujionyesha kisha kwa msisitizo akasema..

    "hivi unayakumbuka maneno ya yule mganga?"...



    "unayakumbuka maneno ya mganga?"

    "maneno yapi tena?"

    "si yale ya kizazi cha nyoka...

    Hukumbuki?"

    alizidi kusisitiza mama Marinda,

    "aahaaa!..nishakumbuka,enhe?"

    "sasa wewe huoni kama inahusiana na haya?"

    "yapi?"

    "nawe!..he! Si haya ya huyu mtoto!...

    Hukumbuki mganga alituambia kwamba,kwanza siku akizaliwa hali ya hewa itabadilika na kua ya



    kutisha naa....."

    "ndioo!..pia nakumbuka alituambia kwamba nyota ndogo itachomoza!"

    (haraka wakanyanyua nyuso zao na kutazama angani)

    "haa!...si unaiona!"

    kwa tahamaki alisema mama Marinda huku akinyooshea kidole nyota ile,

    "ndio mama Marinda,naiona!"

    alijibu kwa mshangao mama Utopi,

    "sasa tunafanyaje?"

    sura yenye wasi wasi ya mama Marinda ilitamka,

    "mmh...mi nadhani hapa si pa kukaa tena,mana yule mtoto ni hatari sana!...si unakumbuka alituambia



    kwamba akifungua macho yake wote wasio na imani thabiti juu yake watapata majanga..!!"

    "ndio!...tuondoke haraka iwezekanavyo tumuache atajijua yeye na mumewe!!"

    aling'aka mama Marinda,walishikana mikono na kuanza kukimbia haraka wakipita katikati ya msitu



    mzito ilipo njia nyembamba ya kuelekea kwao,milio ya mbwa na wadudu ilizidi kuwatisha na



    kuwafanya waangalie nyuma kila mara kwa hofu,mama Marinda alianza kuchoka kukimbia,uzee na



    mwili wake ulikua ni kikwazo tosha kwake kuendelea na safari,ilibidi wapumzike



    kidogo.....wakusanye nguvu kisha wamalizie safari yao iliyobakia kidogo kuikamilisha,walilaumu



    nafsi zao kwa tamaa ya pesa ya mzee Ndolanga mume wa Vero iliyowafanya waingie kwenye



    matatizo yote hayo,kwani kama wangelijua wasingejisumbua na kujihusisha na ile shughuli,katikati



    ya mapumziko yao mafupi walisikia sauti na vishindo vya watu vinakuja,haraka walijificha,punde si



    punde walishuhudia wazee watatu waliojifunika gubi gubi wanaotumia msaada wa fimbo



    kutembea,wakiwa wanajongea bila uoga huku wakionekana kufurahia jambo...

    Ghafla wale wazee walisimama,mmoja wao akasema..

    "nasikia harufu ya binadamu hapa.."

    huku akipepesa pepesa macho yake mekundu,

    mwingine akadakia..

    "naisikia hata mimi pia!.."

    macho ya wakina Mama Marinda yalitoka na mioyo ilipiga mbio mithili ya mkizi



    baharini,walishikana kwa uoga,waliwaona wale wazee wakiwa wanarudi kuelekea upande wao huku



    wakiwa wanatazama tazama wakitafuta kitu!

    * * * *

    "mama Marinda tukimbie!.."

    alinong'oneza mama Utopi,

    "mie siwezi tena,miguu inaniuma!"

    "jitahidi jamani,huoni wanazidi kuja!..

    Na wanasikia harufu yetu!!"

    alizidi kusisitiza mama Utopi huku wakiwa bado wamejificha na wale wazee wapo hatua kumi tu toka



    walipo...

    "tupige tu ukunga watu waje watusaidie"

    "usiku wote mzito huu nani atajitoa nje ya nyumba yake?...

    Twende mam

    a Marinda...twendeee!!"

    alimshka mkono na kuanza kukimbia,alikua mbele ya mwenzake na aliutumia mkono wa kushoto



    kumkokotea...

    Wale wazee hawakuonekana wakikimbia,walisimama tuli huku macho yao yakiwa yanawatizama



    wakina mama Marinda wanaokimbia,hawakufika umbali mrefu,mkono wa mama Marinda



    ulimponyoka mama Utopi,kama gunia la ulezi alidondoka chini!!.

    "mama Marinda...amka twendee!..amkaa!!...

    "siwezi!...siwezi!!..miguu yangu imefungwa na majani mama Utopi!..siwezi kuitoa!!...

    Mama Utopi nisaidieee navutwaa!"

    mama Utopi alijitahidi kumpa mkono mama Marinda lakini hakufanikiwa,Mama Marinda alivutwa



    haraka kwa kasi ya ajabu,sauti yake ya kuomba msaada ilizidi kupotelea msituni,na mwishowe

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    haikuskika kabisa.Mama Utopi hakua na cha kufanya,aligeuka na kuanza kukimbia kwa kasi



    zaidi....machozi yakimtoka na moyo ukidunda kwa nguvu kutokana na uoga na hofu nzito



    iliyomshika,aliona umbali wa kufika nyumbani umeongezeka,na kila akijitahidi kuongeza kasi ilikua



    kama ni kazi bure,mapafu yalimbana...na alihisi kama hapati pumzi,ilimbidi asimame kidogo apate



    kuhema,hakua na amani kabisa,alikua anatizama kila pande kuthibitisha usalama wake,machozi



    yalizidi kumtoka alipofikiria mwenzake aliekua nae muda si mrefu hayupo tena,ilikua ni kama



    mchezo wa kuigiza alipomshuhudia mwenzie akivutwa na majani na kupotelea kabisa,alitupia macho



    upande wa kulia,aliona mwanga wa taa umbali wa kama hatua ishirini na tano toka alipo,akili yake



    ilimuambia kwamba pale ni kwa mama kadogo,haraka bila kupoteza muda aliamza kukimbia



    akielekea upande huo.

    Alifungua kwa pupa geti la makuti la ile nyumba,aliingia ndani na kuanza kupepesa pepesa macho



    aone wapi atapata msaada,ghafla alisikia sauti kali iliyompasua wake moyo..

    "wow! Wow!..wow!"

    alistuka mno kuona mbwa watatu wakimfuata,alianza kurudi nyuma kwa tahadhari huku



    akiwaangalia mbwa wanaomsogelea,kwa nguvu aliropoka kuomba msaada..

    "mama Kadogoo!!..mama Kadogoo!"

    sauti hiyo ilimstua mama Kadogo aliekua ndani amelala na mumewe,na zaidi aliogopeshwa na sauti



    kali za mbwa zilizofika vizuri masikioni mwake,alimuamsha haraka mumewe,ilikua kidogo kazi nzito



    kwani alikua ametekwa vilivyo na usingizh mzito,ila kwa bugudha za kutosha alizozifanya



    zilifanikisha kuondoa mang'amung'amu ya mumewe,

    "nini mama Kadogo?"

    "nimesikia sauti nje ya mwanamke inaniita..na huskii mbwa wanavyobweka kwa nguvu??"

    aliuliza mama Kadogo,

    bila kuchelewa baba Kadogo alichukua panga lake chini ya kitanda kisha akatoka nje kwa



    kasi,alipofika nje alishuhudia mbwa wake wakiwa wanamparua parua mmama ambaye alikua bado



    hajamfahamu ni nani,aliwaamrisha mbwa wake waache lile tendo na haraka walitii amri,alimsogelea



    yule mtu na kugundua ya kwamba ni mama Utopi,aliloa damu kutokana na majeraha makubwa



    aliyosabishiwa na wale wanyama,alikua anagugumia kwa maumivu na huku akitetemeka.



    "mama Marinda tukimbie!.."

    alinong'oneza mama Utopi,

    "mie siwezi tena,miguu inaniuma!"

    "jitahidi jamani,huoni wanazidi kuja!..

    Na wanasikia harufu yetu!!"



    alizidi kusisitiza mama Utopi huku wakiwa bado wamejificha na wale wazee wapo hatua kumi tu toka



    walipo...

    "tupige tu ukunga watu waje watusaidie"

    "usiku wote mzito huu nani atajitoa nje ya nyumba yake?...

    Twende mama Marinda...twendeee!!"



    alimshka mkono na kuanza kukimbia,alikua mbele ya mwenzake na aliutumia mkono wa kushoto



    kumkokotea...

    Wale wazee hawakuonekana wakikimbia,walisimama tuli huku macho yao yakiwa yanawatizama



    wakina mama Marinda wanaokimbia,hawakufika umbali mrefu,mkono wa mama Marinda



    ulimponyoka mama Utopi,kama gunia la ulezi alidondoka chini!!.

    "mama Marinda...amka twendee!..amkaa!!...

    "siwezi!...siwezi!!..miguu yangu imefungwa na majani mama Utopi!..siwezi kuitoa!!...

    Mama Utopi nisaidieee navutwaa!"



    mama Utopi alijitahidi kumpa mkono mama Marinda lakini hakufanikiwa,Mama Marinda alivutwa



    haraka kwa kasi ya ajabu,sauti yake ya kuomba msaada ilizidi kupotelea msituni,na mwishowe



    haikuskika kabisa.Mama Utopi hakua na cha kufanya,aligeuka



    na kuanza kukimbia kwa kasi zaidi....machozi yakimtoka na moyo ukidunda kwa nguvu kutokana na



    uoga na hofu nzito iliyomshika,aliona umbali wa kufika nyumbani umeongezeka,na kila akijitahidi



    kuongeza kasi ilikua kama ni kazi bure,mapafu yalimbana...na alihisi kama hapati pumzi,ilimbidi



    asimame kidogo apate kuhema,hakua na amani kabisa,alikua anatizama kila

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    pande kuthibitisha usalama wake,machozi yalizidi kumtoka alipofikiria mwenzake aliekua nae muda



    si mrefu hayupo tena,ilikua ni kama mchezo wa kuigiza alipomshuhudia mwenzie akivutwa na majani



    na kupotelea kabisa,alitupia macho upande wa kulia,aliona mwanga wa taa umbali wa kama hatua



    ishirini na tano toka alipo,akili yake ilimuambia kwamba pale ni kwa mama kadogo,haraka bila



    kupoteza muda aliamza kukimbia akielekea upande huo.



    Alifungua kwa pupa geti la makuti la ile nyumba,aliingia ndani na kuanza kupepesa pepesa macho



    aone wapi atapata msaada,ghafla alisikia sauti kali iliyompasua wake moyo..

    "wow! Wow!..wow!"

    alistuka mno kuona mbwa watatu wakimfuata,alianza kurudi nyuma kwa tahadhari huku



    akiwaangalia mbwa wanaomsogelea,kwa nguvu aliropoka kuomba msaada..

    "mama Kadogoo!!..mama Kadogoo!"



    sauti hiyo ilimstua mama Kadogo aliekua ndani amelala na mumewe,na zaidi aliogopeshwa na sauti



    kali za mbwa zilizofika vizuri masikioni mwake,alimuamsha haraka mumewe,ilikua kidogo kazi nzito



    kwani alikua ametekwa vilivyo na usingizh mzito,ila kwa bugudha za kutosha alizozifanya



    zilifanikisha kuondoa mang'amung'amu ya mumewe,

    "nini mama Kadogo?"

    "nimesikia sauti nje ya mwanamke inaniita..na huskii mbwa wanavyobweka kwa nguvu??"

    aliuliza mama Kadogo,



    bila kuchelewa baba Kadogo alichukua panga lake chini ya kitanda kisha akatoka nje kwa



    kasi,alipofika nje alishuhudia mbwa wake wakiwa wanamparua parua mmama ambaye alikua bado



    hajamfahamu ni nani,aliwaamrisha mbwa wake waache lile tendo na haraka walitii amri,alimsogelea



    yule mtu na kugundua ya kwamba ni mama Utopi,aliloa damu kutokana na majeraha makubwa



    aliyosabishiwa na wale wanyama,alikua anagugumia kwa maumivu na huku akitetemeka.



    "mnasema nini??"

    "sisi ni mamajusi wa kishetani!..na tumekuja kumlaki mfalme wetu!!.."

    "m..m..mfa..mfalme...yu..yu..yupi!"

    aliuliza Vero huku akitetemeka,

    "mfalme Chernobog,Mungu mweusi!"



    Vero macho yalizidi kumtoka,hofu ilichochea ndani yake,alimuangalia yule mtoto aliembeba



    akamuona anatabasamu!...aliporudisha macho juu,aliona wale wazee watatu tayari washaingia,alisk

    ia moyo umepasuka ghafla....hakuvuta tena pumzi,mwishowe akapoteza fahamu.Neno



    CHERNOBOG lina asili ya urusi,ni



    mchanganyiko wa majina mawili,cherno ikimaanisha 'nyeusi' na bog imaanishayo 'mungu',kwahiyo



    kwa pamoja huza neno 'mungu mweusi' kama anavyoitwa mtoto yule na wale wazee.



    Mtoto alichukuliwa kutoka kwenye mikono ya Vero aliepoteza fahamu,kila mzee alimbusu kwenye



    paji la uso na kuongea maneno fulani yaliyozid kulitunza tabasamu la yule mtoto.

    Ghafla alifungua macho yake,hayakua ya binadamu wa kawaida na hata alipopanua mdomo



    wake,hakua na ulimi wa binadamu



    wa kawaida,vyote vilikua ni viungo vya nyoka,tabasamu lenye afya lilichomoza kwenye kila sura ya



    wale wazee,kwa pamoja wakasema..

    "baruch haba chernobog..

    Ooh baruch haba"



    lugha ya kiebrania(Hebrew) ikimaanisha 'karibu mungu mweusi,ooh karibu!'

    ..Vero bado fahamu hazikumrudia,hivyo hakupata kushuhudia kilichokua kinajiri,alijiona yu ndani ya



    giza nene akipepesa macho huku na kule kuutafuta mwanga,akiwa katika harakati hizo mara ghafla



    alihisi mkono umemgusa begani,haraka aligeuza yake shingo kwa hofu kuangalia ni nani,hakuona



    kitu,jasho likawa linamtiririka,mwili nao ukawa unatetemeka ilihali na nywele kichwani zikawa



    zinasisimka,

    "wewe nanii???"



    sauti iliyoshiba uoga ya Vero iliskika,hakuna sauti yoyote ya kimajibu iliyorudi masikioni mwake



    zaidi tu ya mwangwi uliomjuza ya kwamba yu ndani ya jengo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliunyanyua mguu wake na kuanza kusogea mbele akiutafuta mlango huku akipata taarifa finyu



    kuhusu anapokanyaga kutokana na macho yake kushindwa kupambana na giza lile kali,kila alipozidi



    kusogea mbele alizidi kusisimka na kuhisi hatari zaidi,mguu wake wa kulia ulio mbele ulikanyaga kitu



    chenye ncha kali,alipiga yowe ya maumivu uliojibiwa na mwangwi mkali uliorudi masikion



    mwake,nafsi yake ilizidi kushiba hofu kwani alipoangalia kilichomchoma ni nini,hakupata



    kukiona!..bali tu alishuhudia mguu wake ukimimina damu,hapo ndipo alipoisikia sauti,nzito ya



    msisitizo na yenye kuogopesha!..

    "tazama nao huo ndio utawala unaokuja!..

    Utawala wa kiza!...kiza!..kiza na giza!!

    Utawala wa nyama na damu!!



    UTAWALA WA CHERNOBOG!!!...

    Ha! Ha! Ha! Ha! Ha!........."



    Vero alipiga makelele ya kiuoga na ghafla alijikuta ameamka toka kwenye usingizi ule



    mzito!....alipotazama pembeni hakuona kitu zaidi ya kusikia sauti za nyimbo zikitokea



    nje,alijinyanyua kwa tabu kutokana maumivu aliyokua bado anayo,alijisogeza mpaka mlangoni na



    kuanza kuchungulia,macho yake yalishuhudia wazee karibia ishirini wakiwa wamevaa mavazi meupe



    na mekundu wakicheza na kuimba huku wakimrusha rusha yule mtoto juu juu!!..



    Baada ya dakika tano lile zoezi lilikoma,sauti ya mzee mmoja aliyekua ameshikilia fimbo yenye



    alama ya msalaba ikasema..



    "wana wa utawala wa kiza huu ni wakati wetu!!"

    "amen!"

    wakaitikia wale wengine huku wakiinamisha vichwa vyao,

    "na tupo hapa kumlaki mfalme atakaetuöngoza mpaka pale tutakapoikamata dunia!!"

    "ameen!"

    "na kuanzia leo jua halitochomoza,na ni ishara ya kutokua na mipaka kwenye maamuzi!"

    "Ameen!"

    "ila sadaka ya mtu mmoja haitoshi kabisa kumpokea mfalme wetu,hivyo basi inahtajika nyingine ya



    ziada!!.."

    "ameen!"

    "na nendeni mashariki na magharibi,kaskazini na kusini..MKAITWAE!!!!...."



    Wale watu walitawanyika huku na huko kwenda kutafuta sadaka kwa ajili ya mapokezi ya mungu



    wao CHERNOBOG yani 'mungu mweusi',macho yao mekundu,miili yao ya kijivu iliyofunikwa na



    mavazi meupe na mekundu ilizidi kuchanja mbuga pande zote nane za dunia kwa ajili ya kuifanisha



    tafrija yao.



    Baba Kadogo alizidi kutembea kuelekea mbele,alibakisha umbali usio mrefu sana kukamili

    sha safari yake aliyodhamiria,ghafla panga lilimponyoka,akainama akaliokota akaendelea na



    safari,baada ya hatua mbili tatu panga likamponyoka tena!



    Moyo ukaguma,akapata wasiwasi kuhusu ile hali,ila hakujali sana,aliinamisha tena mgongo wake



    akaliokota,mara ghafla akahisi upepo umempita kwa haraka!

    Mwili wake wote ukasisimka!



    Ujasiri wake ukaanza kupata mashaka,moyo wake nao taratibu ukaanza kuchanganyia mbio,alihisi



    joto limepanda,kijasho chembamba kilimshuka,alimeza mate kisha akaendelea kutembea,haukupita



    tena muda mrefu panga likamponyoka kwa mara ya tatu!



    Milio ya hatari ikaanza kuita kichwani mwake,nafsi yake ikamtonya ya kwamba hayuko salama,bila



    kuuliza mara mbilimbili wala kupoteza muda wa ziada aliinama na kuliokota ganga kisha akaanza



    kukimbia!!



    Hakuruhusu miguu yake isimame wala kupunguza kasi,alikimbia kadiri ya uwezo wake huku akihema



    juu juu kwa pupa kuitafuta oksjeni,tahamaki alisikia vishindo kwa nyuma vinakuja kwa kasi!

    ...Baba Kadogo alieanza kuloa uoga na kujuta kwanini hakusikia ile kauli ya mkewe alizidi kuongeza



    mwendo!



    Alikimbia kupita uwezo wa miguu yake,mwishowe kama kiroba cha viazi alidondoka puh!!...panga

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kule!



    Kabla ya kujikusanya na kuinuka,tayari alishazungukwa na watu watatu waliopendezeshwa na



    mavazi meupe na mekundu!!

    Sauti kali ya maumivu ya baba Kadogo iliskika kwa nguvu kutoka msituni

    "aaaaaahhh!!!!!!"

    kisha tena kukawa kimya,

    idadi ikawa ni watu wawili waliokwenda kwa ajili ya sadaka tayari!

    * * * * * * * *



    mama kadogo alihisi moyo wake umelipuka ghafla!

    Alikosa amani,moja kwa moja alihisi kuna jambo baya limechukua nafasi,alitoka kwenye dirisha



    alipokua anachungulia na kumsubiria mumewe,kiuchovu na kimawazo akaelekea kwenye kiti alipo



    mama Utopi ambaye bado fahamu hazikumrudia,alikaa kihuzuni huku akishika tama,



    "jamani mume wangu,sijui yupo salama huko?..mbona mapigo yangu ya moyo yanaenda mbio



    hivi?....eh mungu saidia!"

    "koh!-koh!"

    ghafla kikohozi cha mama Utopi kikaskika!

    Haraka mama Kadogo aligeuza yake shingo na kumtazama,

    "mama Utopi!"

    "ab..bee!"

    "vipi mama unajiskiaje?"



    "......mmm,mikono inaniuma na miguu pia..inavuta sana!"

    alisema mama Utopi huku sura yake ikiakisi maumivu aliyokua nayo,

    "usihofu mama,itapoa tu kwani dawa iliyoekwa kwenye hizo bandeji ni kiboko.."

    "ahsanteni jamani...ahsanteni sana"



    alisema mama Utopi huku akikunja kunja sura kutokana na miale ya maumivu kumpitia,

    "haina shida mama,ila samahani sana kwa wale mbwa wetu waliokujeruhi.."

    "wala usihofu mwanangu.."

    "hivi mama ilikuaje kwani?"

    "mh...mama Kadogo,tumekwisha!!"

    "tumekwisha? Kivipi yani...sijaelewa!"



    "kile kizazi cha nyoka alichotuambia mzee Otongo yule mganga..kimewadia!!"

    "eh? Umekionea wapi??"

    "mtoto va Vero!..mtoto wa Vero ndie yule....

    (kabla hajamalizia alikatishwa na hodi toka mlangoni)

    "ngo! Ngo! Ngo!"

    "nanii?"



    aliuliza mama Kadogo huku macho yakiwatoka kwa uoga,

    "mimi Baba Kadogo!"

    sauti toka nje iliskika,



    mama kadogo alifikiria kidogo,kisha akataka kuinuka ila mama Utopi alimzuia haraka!

    Kisha akamuuliza,

    "una uhakika huyo ni Baba Kadogo??"

    swali lililomstua mama kadogo na kumfanya aanze kutia shaka,

    * * * * * * *

    "mh..lakini ni sauti yake hiyo ninayoisikia?"

    "haijalishi mama Kadogo...inabidi uwe makini,embu nenda kachungulie pale dirishani kuhakiki"

    "nenda basi wewe"

    "ah..ah si mume wako? Nenda wewe!"

    walisakiziana kwa uoga,

    "lakini mama utopi...mi...mi..naogopa! Au tumuamshe Kadogo aje atusaidie?"

    "atusaidie nini? Kwani tunajifungua hapa?...

    Jiamini mtoto wa kike,tupo wawili humu we nenda tu,mie ningeenda sema miguu inanivuta kweli!"

    alitamka mama Utopi kwa ujasiri huku akifichama hisia zake za uoga,

    mama Kadogo alinyanyuka na taratibu alianza kujongea kuelekea kwenye dirisha,alitizama tizama



    nyuma kila mara kumuangalia mama Utopi ambaye alikua anampa ishara za kujiamini na kuzidi



    kusogea,aliunyanyua mguu wake wa kulia kumalizia umbali uliobakia wa kulifikia dirisha,ghafla



    alishtushwa na hodi ya mara ya pili iliyotoa sauti kali na kuutikisa mlango!

    "ngo!! Ngo!! Ngo!! Ngo!!"

    aliyatoa macho na haraka aliyageuzia kwa mama Utopi alieonesha kwamba naye kashtushwa!

    Alishindwa kuizuia miguu yake,alikimbia haraka kurudi alipotoka kuungana na mwenzie alieonekana



    naye kujawa na uoga uliomeza ule ujasiri wake wa kuigiza,

    "umesikia hiyo??...mh,sasa hivi nenda wewe!"

    "mimi?...kwa we ulifika?!"

    "mie sijafika ndio ila nilikaribia karibia!"

    "sasa kwani sie tulikubaliana kukaribia karibia ama kufika pale dirishani?"

    aliuliza mama Utopi kwa sauti ya chini,

    "ngo!!! Ngo!!! Ngo!!! Mama kadogo fungua!!!"

    sauti tena ya kuamuru iliskika toka nje ikiambatana na mlio wa nguvu wa mlango,kwa mara hii sauti

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    haikua tena ya Baba kadogo iliyokua mwanzoni,ilikua ni sauti nzito ya kutisha!

    "mama Utopi hiyo si sauti ya mume wangu!!"

    kwa mshangao uliojaa uoga alibwatuka mama Kadogo,

    haraka waliinuka wakakimbilia chumbani na kuacha sebule tupu,waliingia chumba cha kwanza



    kabisa kilichokua karibu yao ambacho ni chumba cha Kadogo mtoto wa pekee wa mama Kadogo,hali



    ya kuingia kwa kukurupushana ilimfanya Kadogo astuke toka kwe usingizi,alipigwa na butwaa na



    kile kitendo cha kuona mama yake anajaribu kuingia chini ya uvungu wa kitanda chake,na



    alipogeuza shingo upande wa kushoto alishuhudia mama wa rafiki yake kipenzi mama Utopi akiwa



    anafanya jitihada za kuchungulia dirishani,

    "mama kuna nini?"

    aliuliza kadogo,hakuna aliyejibu swali lake kila mtu alionekana yu bize kufanya kile kilichoonekana



    kumleta lile eneo,mama Kadogo baada ya kushindwa kuingia uvunguni alikua amesimama akipepesa



    pepesa macho yake kushoto kulia juu na chini kuona ni wapi ambapo anaweza kujishkiza na kusahau



    kabisa ya kwamba mwanae bado anamuangalia kimshangao na anasubiri jibu la swali lake



    alilouliza,wakati hilo zoezi linachukua nafasi sauti ya mama Utopi aliekua anachungulia dirishani



    ilipata kuskika,

    "mama kadogo,mbwa wako wote wamekufa!!"

    "wamekufa? Nani kawaua?"

    "sasa mie ntajuaje na wote tupo ndani?

    Alafu nilivyochungulia upande wa mlangoni sijaona mtu!"

    "we! Ujaona mtu?..sasa ile sauti iliyokua inabisha hodi ni ya nani?"

    "hapo sasa!!..au kazunguka kwa nyuma?"

    "mh mungu wangu!..mie hata sielewi,yani hapa haja zote zimenibana!"

    "mie naona bora ya wewe,mwenzio hapa miguu inatetemeka na moyo unanienda mbio kweli!"

    "mama kwani kuna nini??"

    Kadogo alilirudia swali kwa msisitizo baada ya kuona maongezi yaliyokua pale hayaelewi,

    Mama kadogo alitazamana na mama Utopi kwa muda kidogo,kisha akajibu

    "lala tu baba wala usiogope.."

    "mama silali mpaka uniambie kuna nini

    mbona mnaonekana mnaogopa?"

    "haina shida mwanangu,hakuna chochote baba eenh...wala usiogope we lala tu"

    "kweli Kadogo wala usihofu hakuna kitu"

    alidakia mama Utopi huku akililazimisha tabasamu kumjazisha Kadogo ujinga,

    mama Kadogo alisita kumwambia ukweli mwanae kwa hofu kua unaweza kulirudisha tatizo ambalo



    huwa linamsumbua la mshtuko wa moyo,hivyo alijitahidi kuuzika ukweli kwa uso wa bandia na



    maelezo yasiyo sahihi ili aepushe jambo lingine kutokea,

    wakiwa katika maongezi mafupi ya kuubadilisha ukweli katika macho na masikio ya Kadogo,ghafla



    walishtushwa na sauti toka nje zilizokua zinaimba!

    "nao ni utawala wa giiiiza!

    Nao ni utawala wa kiiiiza!

    Wasio amini kuwaumiza!

    Na watakaoungama kuwahimiza!

    Sita! Sita! Sita!

    (sauti nyingine ikidakia)

    kwenye paji la uso!

    Sita! Sita! Sita!

    Kwa maisha!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sita! Sita! Sita!

    Tunawasilisha!

    Sita! Sita! Sita!

    Tunawakilisha!!"

    kisha sauti ikatulia kwa muda kidogo,sauti nyingine ya mtu mmoja ikaskika..

    "kama wataka jiunga na ulimwengu,

    kama wataka kuishi tangu na tangu,

    toka nje upewe alama ya maisha!

    Toka nje na yote yatakwisha!

    Ila ukibaki humo ndani utakua ni wa sadaka!!"



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog