Simulizi : Kijijini Kwa Bibi
Sehemu Ya Tatu (3)
ILIPOISHIA...
______________
Mara ghafla panya akatokea
kichakani, alikuwa kama anakimbizwa na kitu.
akawa anaelekea kwenye miguu ya Omary, katika
jitihada za kumkwepa, Omary akajikuta anamkanyaga yule Panya,
damu ikaenea katika viatu vya Omari, mganga aliliona lile tukio,
akajikuta anasema kwa sauti iliyokata tamaa
"tumekwisha...".
Na wakati huo huo mzimu ukachomoka kutoka katika mwili wa maiti na
huku ukifoka kwa hasira kiasi kwamba ndege na wadudu walioloala
maeneo Yale ya makaburini waliamka na kukimbia hovyo..............
___________
ENDELEA
___________
"Hapa sijui kama tutapona" Mganga alitamka maneno hayo, huku akiwa
kama anajitayarisha na pambano jingine.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzimu ulipiga kelele zilizowatisha watu wore pale, kisha ulirudi
kwa kasi ndani ya mwili wa Kayoza, kisha Kayoza
akanyanyuka taratibu, alikuwa tayari
keshabadilika, alikuwa anaogepesha ukimtazama msoni, macho yalikuwa
meupe yasiyo na mboni na meno ya mbele pembeni yalikuwa marefu kama
ya mnyama simba.
Kayoza akawatazama wote, alafu akawa
anamfuata Omari, Omari kuona hivyo, mkojo
ukaanza kumtoka na hata kukimbia akawa anashindwa ila alibaki
ametoa macho huku machozi yakimtoka ingalikuwa halii.
Kayoza alipomfikia Omary
akamuangalia kisha akaachane nae, sasa akawa
anafuata mganga ambaye muda wote alikuwa bado anafanya mambo yake
ya kiganga kwa ajili ya kujaribu kuutuliza mzimu wa Kayoza.
Mganga baada ya kuona mzimu unamfuata, maamuzi aliyoyachukua ni
kutoka tu
mbio, akasababisha na watu walikuwepo katika
hilo eneo nao watoke mbio
mganga hakufika hata mbali, Kayoza akamkamata,
"Wewe ni nani mpaka utake kunitoa katika nyumba yangu?" Mzimu
ulimuuliza mganga huku ukiwa umemkaba katika shingo na kusababisha
kucha zake ndefu zipenye kwenye shingo ya mganga,
"Mi...mii..nimeagi..zwa tu na ndugu za...ko" Mganga aliongea kwa
tabu huku damu zikimchuruzika shingoni.
Ila pamoja na utetezi wake ule mzimu ulimbeba juu na kung'ata
shingoni kisha aakaanza kumnyonya damu, alipomaliza akamtupa
pembeni.
Kisha mzimu ukatoka mbio na kuwakuta wasaidizi wa mganga wakiwa
wanakimbia na wale
wasaidizi wake pia wakanyonywa damu.
Kisha Kayoza akamfuata sajenti Minja, ambae yeye alikimbia ila
mwisho akaamua asimame tu maana aliona hata kama akikimbia ni
lazima tu akamatwe.
Mzimu akamkamata mkono Sajenti Minja alafu akawa anamvutia
kichakani sehemu ambayo kulikuwa na miti mingi, alipofika katika
eneo lenye miti,
"Usipate kichwa kwa kuwa niliahidi kutoidhuru damu yenu, wewe ndiyo
utasababisha nivunje ahadi yangu" Mzimu uliongea huku
Ukikata fimbo, na kisha ukaanza kumtandika Sajenti Minja,
alimtandika
kisawa sawa, mpaka sajenti Minja akawa analia kama mtoto.
Mzimu uliporidhika na bakora alizozipata Sajenti Minja ukamuachia
na Sajenti Minja akatoka mbio kama mwendawazimu na kuishika ile
njia waliyokuja nayo ambayo ilikuwa inaelekea nyumbani kwa Mganga.
Mzimu ulipomuachia Kayoza, Kayoza akadondoka chini kama kifurushi
na akapoteza fahamu.
Omary yeye baada ya kuachwa na mzimu wala hakukimbia, alikuwa
anaangalia tu unyama unaofanywa na mzimu na hata wakati Kayoza
anaanguka na kupoteza fahamu Omary aliona na akaamini tayari mzimu
umemuachia rafiki yake, Maamuzi aliyoyachukua Omary ni kwenda kumpa
msaada Kayoza, alipofika, akambeba Kayoza kisha akawa kwenda
walipoacha gari lao ambapo ni nyumbani kwa Mganga.
Walifanikiwa kufika salama nyumbani kwa mganga na wakamkuta Sajenti
Minja anaangaika kufungua mlango wa gari ili aingie,
"Vipi huyo tayari au bado?" Sajenti Minja alimuuliza Omary baada ya
kumuona anakuja na Kayoza,
"Tayari amerudi katika hali yake" Omary alijibu huku akifungua
mlango wa gari na kumuingiza Kayoza,
"Aisee hii siwezi kuisahau" Sajenti Minja aliongea huku akiwasha
gari na kuiondoa kwa kasi.
"Hii ilikuwa hatari, ila wewe hajakudhuru" Omary aliongea huku
akijua fika Sajenti Minja alipewa bakora zisizo kuwa na idadi,
"Usiseme hivyo wewe, dah yaani nimefanywa mtoto Leo, tena mtoto wa
shule" Sajenti Minja aliongea kwa huzuni,
"Umefanywaje kwani mjomba?," Omary aliuliza huku akimcheka
kimoyomoyo,
"Hata kuhadithia siwezi, ni kitendo cha aibu sana" Sajenti Minja
aliongea,
"Si uniambie tu mjomba" Omary alikazania huku akiendelea kumcheka
moyoni,
"Nitakuambia tukifika bwana" Sajenti Minja alijibu huku akiongeza
mwendo wa gari.
*****************
Katika hospitali ya mkoa kulikuwa na kasheshe
kubwa sana, kuna watu waliambiwa ndugu yao
amefariki, ila walipoenda monchwari hawakuikuta
maiti ya ndugu yao, walipowafata madaktari
wakawathibitishia kuhusu kifo cha ndugu yao, na
hata babu wa monchwari alithibisha kupokea maiti
ya huyo ndugu yao, sasa cha ajabu maiti ikawa
haionekani
Polisi walipofika pale hospitali, wakamchukua
babu wa mochwari huku wakiwa na uhakika kuwa
huyu mzee anahusika kwa namna moja au nyingine
katika upotevu wa ile maiti.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Babu akachukuliwa hadi kituoni, walipomfikisha
wakaanza kumuhoji,
"Mzee kuwa mkweli, tuambie huo mwili umeupeleka wapi?" Askari
alimuuliza Babu wa monchwari,
"Yaani hata mimi sielewi, ule mwili kweli niliupokea ila hata
ulivyopotea mimi sijui" Babu alijibu kwa kujiamini,
"Kwani walinzi mpo wangapi pale monchwari" Askari aliuliza,
"Tupo wawili" Babu alijibu,
"Umesema wewe ndiye uliupokea mwili, he wakati mwili unapotea
ilikuwa zamu ya nani kulinda?" Askari akaendelea kuuliza,
"Yaani huo mwili niliupokea Jana saa mbili usiku, na imeonekana
haupo Leo saa kumi na mbili alfajiri" Babu alijibu,
"Ilikuwa zamu ya nani?" Askari aliuliza,
"Zamu yangu" Babu alijibu,
"Babu acha kutuchanganya, inaonesha wewe unajua kila kitu kuhusu
kupotea kwa huo mwili" Askari aliongea huku akitabasamu ili
asimtishe Babu,
"Unadhani nakutania mjukuu wangu?, kweli mimi sijui kitu,
inawezekana mile chumba cha monchwari kina wachawi, si unajua
wachawi wanazipenda sana maiti" Babu alijitetea na kumfanya askari
acheke,
"Babu sema kweli usiogope, hata kama umeusika hatuwezi kukufunga,
maana utakuwa kama shahidi, na si unajua shaidi hafungwi?" Askari
alimlainisha Babu huku akiendelea kucheka,
"Kweli hamuwezi kunifunga?" Babu aliuliza huku akimuangalia Askari,
"Kama utamtaja muhusika hautofungwa mzee, ila ukishikiria msimamo
wako wa kuficha ndio utakaokuingiza matatizoni" Askari alimwambia
babu wa monchwari,
"Kusema ukweli aliyeuchukua ule mwili namjua kwa sura ila jina
simjui" Babu aliamua kusema ukweli,
"Anakaa Wapi?" Askari aliuliza,
"Sijui ila nikimuona tu sura yake namjua hata kama nikitoka kulala"
Babu aliendelea kukazania maneno yake,
"Kulikuwa na makubaliano yoyote kati yenu mpaka auchukue huo
mwili?" Askari aliuliza,
"Hapana aisee" Babu alikataa,
"Sasa alichukuaje na wakati wewe mlinzi ulikuwepo?" Askari
aliendelea kumbana kwa maswali,
"Alikuja na bunduki akanitishia, kisha akaingia ndani na kubeba
maiti" Babu wa monchwari aliamua kusema uongo,
"Sasa kwa nini tokea mwanzo hukusema hivyo?" Askari aliuliza huku
akimuangalia usoni,
"Nilikuwa siamini kama mtaniamini" Babu alijibu,
"Sawa babu, itabidi urudi ndani" Askari aliongea huku akisimama,
"Ndani tens kufanya mini?" Babu aliuliza kwa kuamaki,
"Utatoka tu babu, ila kwa sasa mtuhumiwa bado unahesabika ni wewe
mpaka apatikane huyo mwingine unaedai alikuvamia na bunduki" Askari
aliongea na kubonyeza kitufe kilichopo mlangoni na mlango
ukafunguka wakaingia Askari wengine wawili,
"Mpelekeni selo" Askari aliwaamrisha wenzake ambayo walimshika babu
huku na huku na kutoka nae nje.
wanamtoa katika chumba cha mahojiano, ili
wampeleke rumande.
****************
Mida ya saa tano asubuhi, ndio sajenti Minja
alikurupuka, akaangalia simu yake, akukuta
missed call 12 za mkubwa wake wa polisi,
akawaamsha wakina Kayoza, kisha wakaenda
kujiswafi, wakatengeneza chai wakanywa.
Sajenti Minja akawarudisha wakina Kayoza kwa
mama Kayoza, kisha yeye akawa anaelekea
kituoni,
alipofika, akapaki gari lake kisha akawa anaenda
katika ofisi ya mkubwa wake, katika kolido ya
ofisi akapishana na askari watatu waliokuwa
wamemfunga pingu mzee mmoja ambae sura
yake haikuwa ngeni kwake yeye Sajenti Minja, ikabidi
ageuke amwangalie tena, na yule mzee nae
akageuka kumuangalia sajenti Minja, ndipo
sajenti Minja akamkumbuka, ni yule mzee mochwari na hapo pia ndipo
yule mzee monchari akamkumbuka kuwa yule wanaepishana nae ndiye
aliyemuuzia maiti na kumsababishia madhira Yale, Babu wa Monchwari
akasimama huku akiwa bado amemgeuzia shingo Sajenti Minja ....
...yule babu wa mochwari akasimama, "vipi we mzee, songa mbele"
askari mmoja akaongea kwa hasira.
"taratibu wanangu, nimemuona mtu kama aliekuja kununua ile maiti"
yule babu akaongea kwa matumaini huku shingo yake akiitoa kwa
Sajenti Minja na kuwageukia wale maaskari,
"yuko wapi?" askari mwenye hasira akauliza.
Yule babu akageukia ile sehemu aliyokuwepo sajenti Minja ili
awaoneshe maaskari,
"kha!," yule babu akajikuta anashtuka kwa mshangao baada ya
kutomuona tens Sajenti Minja,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"vipi babu?, tuoneshe haraka, unatuchelewesha" yule askari mwenye
hasira akauliza huku amemtolea macho babu,
"alikuwepo pale" yule babu akasema huku akionesha lile eneo
alilokuwepo Sajenti Minja.
"kwa hiyo hayupo?", yule askari mwenye hasira akahoji.
"alikuwepo pale", Babu akajitetea.
"hujanijibu bado, kwa hiyo hayupo" yule askari aliuliza tena huku
akiwa na shauku ya kufanya kitu.
"ndio mwanangu" Babu akajibu kwa upole.
Bila kutegemea, babu alipigwa mtama mmoja mkali sana, akaangukia
makalio.
"unatuchelewesha majumbani kwetu, hatujalala na wake zetu tokea
juzi usiku" askari mwenye hasira aliongea huku akimnyanyua babu
babu baada ya kumpiga mtama.
Sajenti Minja akacheka tu baada ya kushuhudia ule mtama aliopigwa
babu kisha akaishia kujiuliza ni kwanini babu amekamatwa, akajiona
mkosaji kwa kukimbia kwa maana yeye angeweza kuwa msaada wa babu,
pia akaona alichokifanya kinaweza kubwa sahihi zaidi kwa kuwa
huenda Babu atakuwa amekamatwa kutokana na kesi ile ya kuiba maiti,
yaani inawezekana kabisa ndugu wa marehemu wamegundua kuwa
wameibiwa, na mwisho akajisemea itabidi achunguze ni kitu
kilichofanya mpaka yule babu awe katika mikono ya polisi.
"Vipi mbona una mawazo hivyo?" Askari mmoja aliyekuwa anatoka
msalani alimuuliza Sajenti Minja aliyekuwa amezama katika bahari ya
tafakuri,
"Ah, si unajua tena mawazo ni kawaida kwa binadamu" Sajenti Minja
alijibu baada kushtuka kutoka katika lindi la mawazo,
"Wewe ni mgeni kituoni hapa? Maana sura yako sijawahi kuiona" Yule
askari alimuuliza Sajenti Minja,
"Kabisa, inaelekea kila mtu anaefanya kazi hapa umemkariri?"
Sajenti Minja aliuliza,
"Yaani wote, sisi ndio wakongwe wa hapa" Yule askari alijibu huku
akitabasamu,
"Sawa bwana, mimi ndio nawasili muda huu kuja kuripoti kwa mara ya
kwanza" Sajenti Minja aliongea huku nae akitabasamu,
"Bila shaka wewe ndiye Joel Minja?" Yule Askari aliuliza,
"Haswaa, umenijuaje?" Sajenti Minja aliuliza,
"Tuliambiwa Leo kuna ugeni wa askari mpelelezi kutoka Dodoma" Yule
askari aliongea,
"Basi ndio huyo" Sajenti Minja aliongea,
"Umeshafika ofisini kwa mkuu?" Yule Askari aliuliza,
"Bado, yaani hapa ndo mahala pa kwanza kufika" sajenti Minja
aliongea na wote wakacheka,
"Sasa ofisi ya mkuu unaijua?" Yule askari alimuuliza,
"Nitaijulia Wapi mimi?" Sajenti Minja alijibu,
"Sasa ungefikaje" Yule askari aliuliza,
"Ningefika tu, ila kwa kuwa nimekutana na wewe, mambo yatakuwa
sawa" Sajenti Minja aliongea,
"Twende nikupeleke" Yule askari akaongea huku akitangulia mbele
Wakatoka katika eneo la chooni, akawa anaelekea katika ofisi ya
mkubwa wake, walipofika yule askari aliyempeleka hakutaka kuingia,
aliishia mlangoni na kuondoka zake na kumuacha Sajenti Minja
mlangoni.
Sajenti Minja akapiga hodi kisha akaingia, aliporudishia mlango,
akampa heshima yake mkuu wa polisi,
"kaa hapo sajenti" Mkuu wa polisi wa shinyanga alimuelekeza sajenti
Minja sehemu ya kukaa.
sajenti Minja akasogeza kiti, kisha akakaa.
"habari yako Minja" Mkuu wa polisi akamsalimia.
"nzuri tu, shikamoo mkuu" sajenti Minja akajibu.
"Marhaba, Leo ndio siku ya kwanza kuwasili kituoni hapa" Mkuu wake
alimuuliza huku akiwa jibu analo kabisa,
"Naam mkuu" Sajenti Minja alijibu kikakamavu,
"Vizuri sana, na kilichokuleta huku nadhani unakijua" Mkuu wake
aliuliza tena,
"Ndio mkuu" Sajenti Minja alijibu,
"Tukupatie Askari wa huku ili msaidiane au wewe una pendekezo
Gani?" Mkuu wake alimuuliza,
"Naimani peke yangu nina uwezo wa kufanikisha" Sajenti Minja
alijibu,
"Kwanini hutaki msaada?" Mkuu wake aliendelea kumbana,
"Kwa sababu hata niliyofikia katika upelelezi wa hii kesi ni hatua
nzuri, sasa ukinipa mtu wa kusaidiana nae itakuwa kama tunaanza
upya kwa kuwa atakuja na mipango, mbinu na mawazo tofauti kuhusu
hii hii kesi" Sajenti Minja alijibu,,
"Lakini kumbuka umoja ni nguvu" Mkuu wake aliongea huku
akitabasamu,
" hilo nalijua mkuu, nitapohitaji msaada nitakwambia" Sajenti Minja
aliongea,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kesi unayoifuatilia umeishia nayo wapi?" Mkuu wake aliuliza,
"Kwa kweli hata niliyopiga ni ndogo sana, bado nahitaji mwanga
zaidi ili hata nijue wa kumtia hatiani" Sajenti Minja aliongea,
"Sawa, basi hapa nna habari ambazo zinaweza kukupa mwanga kidogo"
Mkuu wake aliongea na kumfanya Sajenti Minja atege masikio vyema,
"Habari zipi hizo mkuu?" Sajenti Minja aliuliza,
"leo asubuhi wasamalia wema walitoa taharifa za kuwepo watu wanne
ambayo walikuwa wana alama ya kung'atwa shingoni na kitu kama
mnyama mwenye meno makali, tulipoenda tuliweza kukuta watatu
waliokuwa wamenyonywa damu makaburini, ila habari nzuri mmoja wapo
amekutwa yuko hai, lakini hali yake sio nzuri, ni wa leo au wakesho
muda wowote anaweza kufa", Mkuu wa Polisi aliongea huku akiangalia
baadhi ya makabrasha yaliyopo mezani kwake,
Sajenti Minja alivyosikia habari ya watu kukutwa wakiwa wamekufa
kwa kunyonywa damu eneo la makaburini, moja kwa moja akajua kuwa ni
yule mganga na wasaidizi wake, ila habari ya mmoja kuwa hai ndio
hakuipenda,
"ndio, nakusikia mkuu" sajenti Minja akajibu baada ya ukimya wa
muda mfupi,
"Sasa kwa fikra zangu za haraka haraka haya mauaji nayafananisha na
yanayofanywa na mtu unaemtafuta kwa maana hata wale watu waliokutwa
wamekufa katika geti la mchungaji walikuwa hivyo hivyo na hizo
alama shingoni" Mkuu wake alitoa maelezo,
"Nadhani kwa kuwa huyu mmoja yupo hai basi anaweza kutusaidia
tukapata mwanga kidogo" Sajenti Minja aliongea huku moyoni akiwaza
hata huyo mtu afe,
"Sasa hivi yupo sehemu ya wagonjwa mahututi amepumzishwa, jioni
tutaenda kuongea nae" Mkuu wake aliongea,
"Litakuwa jambo jema sana" Sajenti Minja aliongea,
"sasa ni hivi tutatoka mimi na wewe hadi katika ofisi za akari
wengine ili nikutambulishe, alafu jioni ndio tutaenda hadi
hospitali ili tuchukuwe maelezo ya huyo aliebakia, maana anaweza
kutupa pa kuelekea" mkuu wa polisi alimalizia kuongea huku
akisimama,
"sawa mkuu" sajenti Minja akajibu.
Walitoka nje ya ofisi ya mkuu na kisha muda huo sajenti Minja
akaanza kutembezwa katika ofisi za askari wa ngazi mbalimbali ili
atambulishwe kwa wenzake hao, na kisha pia alizungushwa katika
mazingira yote ya eneo like la Polish kwa ajili ya kupata kuyaona
ili hata akitoka nje ajue duka linapatikana wapi? vyoo vinapatikana
wapi na mambo mengine yanayolizunguka eneo lile.
Baada ya Mkuu wake kuridhika aliamua na kumpeleka katika ofisi
ambayo Sajenti Minja ataitumia muda wote ambao atakuwepo pale na
kisha wakaagana huku wakikumbushiana kuwa jioni ni lazima waende
hospitali kumuona huyo mtu aliyebakia ya wenzie kunyonywa damu,
Sajenti Minja hakupenda kabisa hyo safari ila hakuwa na la kufanya,
ilibidi atimize matakwa ya kazi yake.
************************
Jioni ilifika haraka sana kwa upande wa Sajenti Minja, alitamani
hata isifike kabisa.
Mkubwa wake alimpitia na wakatoka eneo la kituoni.
Baada ya kutoka kituo cha polisi, sajenti Minja na mkuu wake
wakafunga safari hadi hospitali, njia nzima sajenti Minja alikuwa
anatetemeka, alijua fika kuwa anaenda kuumbuka mbele ya mkuu wake,
"vipi Minja, mbona unatetemeka sana?" mkuu wa polisi akauliza.
"leo nimeamka na homa, kwa hiyo sijisikii vema kabisa" sajenti
Minja alidanganya.
"itakuwa malaria, tukifika itabidi upime kabisa" mkuu wa polisi
alimshauri Sajenti Minja.
Gari ilipofika, sajenti Minja na Mkuu wa polisi wakatelemka kisha
wakawa wanaelekea sehemu ilipo wodi za wagonjwa mahututi, walitumia
dakika mbili mpaka kufika katika chumba ambacho alilazwa yule
msaidizi wa Mganga ambae alikuwa amenusurika na kifo, ila chumba
kilikuwa kitupu,
"Eh, mbona hayupo, ameshakufa nini?" Mkuu wa polisi aliuliza huku
akitoa macho kuangaza bila mafanikio. Kwa upande wa Sajenti Minja
hiyo habari ilikuwa nzuri, alijikuta anatabasamu waziwazi mbele ya
Mkuu wake,
"Mbona unacheka, unafurahia kumpoteza shahidi?" Mkuu wake
alimuuliza kwa mshangao,
"Hapana mkuu, nacheka unavyopeleka imani yako katika kifo wakati
hata hujaenda kuuliza kwanza kwa madaktari" Sajenti Minja
alijitetea kwa njia ya uongo,
"Kweli bwana, ebu twende tukaulize" Mkuu wake aliongea huku
akielekea upande zilizopo ofisi za madaktari na huku Sajenti Minja
akiendelea kuomba wakifika waambiwe yule bwana amekufa.
Baada ya sekunde kadhaa walitokea sehemu zilipo ofisi za madaktari,
ila kwa bahati nzuri hata kabla hawajaingia ndani, walikutana na
Daktari ambae ndiye anayesimamia matibabu ya msaidizi wa Mganga,
"Ooohoo kamanda umeshawasili?" Daktari aliongea huku akimpa mkono
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mkuu wa polisi,
"Vipi kuna wema kweli? mbona mgonjwa wetu hayupo kule katika wodi
aliyokuwepo asubuhi?" Mkuu aliuliza huku akionesha wasiwasi,
"Wema upo, tens mkubwa sana" Daktari alijibu huku akicheka,
"Hapo kidogo umenipa nguvu, haya niambie huo wema" Mkuu aliongea
huku akiwa bado yupo makini kumsikiliza Daktari,
"Mgonjwa wako amepata nafuu na hata kuongea anaongea" Daktari
alitoa habari zilizokuwa nzuri kwa Mkuu wa polisi ila hizo hizo
habari zilikuwa mbaya sana kwa Sajenti Minja,
"Mmempeleka wapi sasa?" Mkuu wa Polisi aliuliza,
" yuko katika wodu ileee" Daktari aliongea huku akiwaelekeza kwa
kidole katika wodi ambayo amehamishiwa msaidizi wa Mganga.
Sajeni Minja na Mkuu wa Polisi baada ya kumshukuru Daktari wakawa
wanaelekea kwenye wodi aliyokuwamo yule msaidizi wa mganga huku
Sajenti Minja mapigo yake ya moyo yakiongezeka kasi.
wakaingia ndani ya wodi, kisha wakawa wanaelekea kwenye kitanda cha
yule msaidizi wa mganga, hapo Sajenti Minja moyo ulikuwa unamkimbia
ajabu, akatamani hata sura yake ibadilike au akatamani hata yule
msaidizi wa Mganga awe amepoteza kumbukumbu zake, lakini haikuwa
hivyo.
Walipofika katika kitanda cha yule msaidizi wa mganga, wakakuta
kalala huku kawapa mgongo, yule mkuu wa polisi akamshika bega kwa
lengo la kumuasha, yule msaidizi wa Mganga akageuza sura na macho
yake yakagongana na macho ya Sajenti Minja........
.. "umekuja kuniona mheshimiwa?," yule msaidizi aliongea kwa
tabasamu huku akimuangalia sajenti Minja.
"ndi...ndio, unaendeleaje?" sajenti Minja akamuuliza huku
akitetemeka, kiasi kwamba mkuu wa polisi akaliona hilo.
"nashukuru mungu, vipi wewe?" yule msaidizi wa mganga akamtupia
swali jingine.
"mi sijisikii vizuri kabisa" sajenti Minja akajibu.
"Minja ebu twende ukapime malaria, ukimaliza utakuja kuongea nae
zaidi" mkuu wa polisi akasema.
Sajenti Minja akashusha pumzi ya kushukuru kwa maana aliona
amepona.
"nakuja ili tuongee zaidi" sajenti Minja akamwambia yule msaidizi
wa mganga huku akiwa anatoka na mkuu wa polisi.
"inaelekea mnafahamiana?" mkuu wa polisi akamtupia swali sajenti
Minja wakiwa wanaelekea katika mabenchi ya kusubiria vipimo.
"hapana, hatakuwa kanifananisha tu, au inawezekana kachanganyikiwa
kutokana na kukoswa koswa kufa, yaani nimekuja Jana tu alafu
nijuane na watu wa huku?" sajenti Minja akajibu kwa kumdanganya
mkuu wa Polisi,
"Ila nadhani endelea kujifanya hivyo hivyo kama unamjua ili umuweke
karibu maana mkiwa marafiki anaweza akakueleza mambo mengi zaidi"
Mkuu wa polisi alimshauri Sajenti Minja,
"Hilo nadhani ni jambo zuri na inaweza kuwa mbinu safi" Sajenti
Minja alijibu,
"Au hii kesi nimpe mtu mwingine ili wewe uifuatilie tu iliyokuleta"
Mkuu wa polisi alimuuliza Sajenti Minja,
"Mi nadhani zinaufanano na kesi iliyonileta, kwa hiyo ni vyema tu
niendelee nayo" Sajenti Minja alijibu,
"ok, we chukua vipimo hapa, acha mi nirudi ofisini, ukishamuhoji
tu, uje unipe taharifa" mkuu wa polisi akatoa maagizo.
"Kwanini tusimpe muda kidogo wa mapumziko, tumuhoji hata kesho ili
akili yake itulie kidogo" Sajenti Minja alitoa ushauri,
"Sawa, ila inabidi haya mambo yaende haraka haraka na yafanikiwe
ili ionekane tunafanya kazi kwa bidii" Mkuu wa polisi alimwambia
Sajenti Minja,
"Kuhusu hilo wala usijali, mambo yataenda sawa tu" Sajenti Minja
alijibu,
"Sawa basi, sasa wewe kachukue vipimo tu tutakutana kesho tena,
maana giza linaanza kuingia" Mkuu wa polisi alimwambia Sajenti
Minja,
"sawa mkuu" sajenti Minja akajibu huku akijifanya anaelekea sehemu
zilipo mahabara za hospitali.
"Huu ushakuwa msala, sasa huyu msaidizi wa Mganga ataniletea balaa
kubwa sana uko mbele" Sajenti Minja aliongea huku akiwa bado
anatembea.
***********************
Wakina Kayoza waliporudi kwa mama yao, walimsimulia yote
yaliyotokea, mama kayoza alisikitika sana,
"mchungaji kashindwa, kwa mganga ndio hivyo tena bahati mbaya, mi
hata sijui nifanyaje?" Kayoza aliongea kwa kulalamika.
"Mchungaji hajashindwa, vuta subira tu utapona" Mama Kayoza
aliongea,
"Mama sio kwa matukio haya, maana hii imeshakuwa kesi nyingine"
Kayoza aliongea,
"Mjomba yenu nae hajafanywa kitu na mzimu huko makaburini?" Mama
Kayoza aliuliza na kufanya Omari aangushe kicheko baada ya
kuzikumbuka zile bakora alizochapwa Sajenti Minja,
"Sasa mbona mimi nauliza wewe unacheka?" Mama Kayoza aliuliza huku
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akiwa amekasirika,
"Mimi sikuona ila Omari alinihadithia" Kayoza nae aliongea huku
akicheka,
"Mbona mnanicheka? omary amekuhadithia nini" Mama Kayoza aliuliza
huku akiwa anawaangalia kwa zamu,
"Mjomba nasikia amekula bakora za kutosha, mpaka kukaa anakaa kwa
shida" Kayoza alimwambia mama yake huku akicheka,
"Sasa ndio kinachowachekesha?" Mama Kayoza aliwauliza,
"Sio tukio zuri, ila inachekesha mama, mtu mkubwa kama mjomba
kutandikwa kama mtoto" Kayoza aliongea na kumfanya mama yake scheme
chini chini,
"Ebu acheni upumbavu" Mama Kayoza aliongea huku akicheka,
Mara wakasikia mlango unagongwa, Mama Kayoza akaenda kuufungua
"karibu mchungaji" mama kayoza akasema huku akiacha nafasi alie nje
apite.
"asante mpendwa" mchungaji alijibu huku akiingia ndani.
"vipi mgonjwa, unaendeleaje?" mchungaji akaongea huku anamtazama
kayoza.
"namshukuru Mungu" kayoza akajibu.
"lazima umshukuru Mungu, kwani ye ndo muweza ya yote" mchungaji
aliongea huku akikaa kwenye kochi.
"Za nyumbani?" Mama Kayoza alimuuliza Mchungaji Wingo,
"Uko ni wazima, bwana yupo pamoja nasi. Sijui nyinyi hapa?"
Mchungaji Wingo alijibu na kuuliza,
"Sisi nasi ni wazima, karibu" Mama Kayoza aliongea,
"kilichonileta hapa ni kitu kimoja tu, leo usiku kutakuwa na
maombi, mnakaribishwa wote mje" Mchungaji Wingo akasema
kilichompeleka.
"haya mchungaji, tunashukuru kwa kutupa taharifa" mama Kayoza
akajibu.
"Ndio kazi yangu" Mchungaji Wingo alijibu,
"Itakuwa usiku wa saa ngapi" Mama Kayoza aliuliza,
"Kuanzia saa mbili" Mchungaji Wingo alijibu,
Kisha mchungaji akaaga, ila alitaka asindikizwe na Kayoza.
Kayoza akaongozana na mchungaji hadi nyumbani kwake,
Pale kwa mchungaji kuna msichana ambae ni mtoto wa kwanza wa
mchungaji, tokea siku ya kwanza alipomuona Kayoza, alijenga upendo
juu yake,
Mchungaji alipofika akaingia chumbani kuchukua biblia, akamuacha
kayoza kakaa peke yake,
mara yule binti wa mchungaji akaja, alipomuona kayoza akatabasamu,
"amani ya bwana iwe nawe" kayoza akamsalimia yule binti.
"sema mambo bwana, mi sio mlokole" yule binti akajibu kwa mbwembwe.
Kayoza akatabasamu, "mambo" kayoza akasema.
"safi, mzima?" yule binti nae akauliza uku akikaa jirani na kayoza.
"mi mzima" kayoza akajibu,
"Kayoza mimi na wewe tunajuana ingawa sio sana, si ndio" Binti
mchungaji alimuuliza Kayoza,
" ndio" Kayoza alijibu.
"Basi kuna kitu kinaitwa hisia, sidhani kama zunazuilika" Binti
Mchungaji aliongea na kumfanya Kayoza awe makini kidogo
kumsikiliza,
"Unataka kusema nin?i" Kayoza aliuliza,
"Sitaki kupoteza muda, ninachotaka kusema ni kwamba Kayoza
nakupenda" Binti akajivika ujasiri, kisha akamueleza Kayoza jinsi
anavyojisikia juu yake,
"Sawa, nashukuru" Kayoza aliongea huku akimuomba Mungu amuepushe na
huo mtihani,
"Ukisema unashukuru unamaanisha nini?" Binti Mchungaji aliuliza,
"Nimekuelewa" Kayoza alijibu,
"Naomba unijibu ili nijue hisia zako kwangu" Binti mchungaji
aliongea,
"Usijali, kesho tutaongea vizuri" Kayoza alijibu huku akitabasamu,
"nibusu basi ili nishinde vizuri mwenzio" mtoto wa mchungaji
akaongea kwa mahaba.
"kesho rafiki yangu, hivi huogopi kusema hayo maneno katika nyumba
takatifu kama hii?" kayoza akamjibu kwa busara,
"si unibusu jamani wewe." yule binti akakomalia kwa sauti ya juu
kidogo.
"unamwambia nani akubusu?" Mchungaji Wingo aliuliza huku akiwa
anaingia Sebuleni.....
.."hakuna kitu baba" binti mchungajibu akajibu.
"kwa hiyo nimesikia vibaya?" Mchungaji Wingo akauliza huku
anamuangalia binti yake.
"nilikuwa namsimulia filamu moja hivi ilioneshwa jana ." binti wa
Mchungaji akajibu huku akiangalia chini kwa aibu,
"Umekalia kuangalia filamu tu, badala ukazane kusoma biblia ili
uongeze imani unakalia kuongeza ujinga tu" Mchungaji Wingo
alimwambia binti yake aliyekuwa amesimama mbele yake
"Nisamehe baba, ila hiyo filamu ilikuwa na Mafundisho tu mazuri"
Binti Mchungaji alijitetea,
"Ebu tupishe bwana" Mchungaji Wingo akamwambia mwanae na binti
akaondoka haraka,
"Huyu mwanangu ni muongeaji sana, yupo tofauti na wenzake kabisa"
Mchungaji Wingo aliongea huku akimgeukia Kayoza na usoni akikunjua
tabasamu,
"Ila ni mcheshi sana, yaani amenizoea muda mfupi sana" Kayoza nae
alijibu,
Kisha mchungaji na kayoza wakawa wanaongea, ila jambo kubwa ambalo
mchungaji alimsisitiza Kayoza asikose katika maombi ya usiku.
Kayoza akarejea kwao kujumuika na mama yake.
"vipi mwenzetu, mchungaji alikuwa anakuambia nini?" mama kayoza
alimuuliza mwanae.
"tulikua tunaongea mambo ya kawaida tu" kayoza akajibu.
Kisha mama kayoza akaenda jikoni kutayarisha chakula.
"eh, mwana leo nimekutana na vituko" Kayoza alianza namna hiyo
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kumuelezea Omari.
"wapi tena shee" Omari akauliza kwa shauku .
"si kwa mchungaji mwanangu, kuna binti yake mkubwa amedata na flag
yangu"Kayoza aliongea huku akitabasamu
"kwa hiyo unataka kufanyaje?" Omari akauliza huku amekunja sura.
"nitafanyaje ndugu yangu, na hili dubwana linanibana" Kayoza
alijibu kwa upole
"aah, ok, we mshiti au kama ana mahamu nitajaribu kumseti mimi"
Omari aliongea, na kusababisha wote wakacheka.
"Poa mi ntakupigia pande, we si mwanangu bwana" Kayoza aliongea
huku akicheka...
*****************
Sajenti Minja hakwenda kupima, alimfuatilia mkubwa wake mpaka
alipomuona anapanda gari na kuondoka, naye akarudi ndani moja kwa
moja hadi katika kitanda cha msaidizi wa mganga..
"vipi, unaweza kukaa" Sajenti Minja alimuuliza yule msaidizi wa
mganga.
"kwanini nisiweze?, naweza tu" Msaidizi wa mganga akajibu,
"kuna maswali machache nataka nikuulize" Sajenti Minja akaongea kwa
upole.
"kwani wewe ni polisi" Msaidizi wa mganga aliuliza ili apate
uhakika, kwa sababu alimuhisi.
"ndio" sajenti Minja alijibu.
"sasa unataka kuniuliza nini wakati tulikuwa wote kuanzia mwanzo
hadi mwisho" Msaidizi wa mganga alijibu huku akionekana akimshangaa
Sajenti Minja,
"najua ndugu yangu, ila naomba unisaidie kitu kimoja" Sajenti Minja
aliongea huku akisubiri sauti itakayomruhusu aendelee .
"endelea" Msaidizi wa mganga alijibu.
"naomba polisi yeyote atakaekuuliza kuhusu yale mambo yaliyötokea
kule, mjibu hujui chochote, sawa?" Sajenti Minja aliwasilisha ombi
lake huku akiwa hana uhakika wa kukubaliwa,
"kwanini tufiche ukweli?" Msaidizi wa mganga aliuliza kwa mshangao,
"Ukiongea ukweli utakuwa umeniharibia kila kitu katika maisha
yangu, yaani hata kufungwa nitafungwa" Sajenti Minja aliongea kwa
huruma ili kumshawishi Msaidizi wa Mganga akubaliane nae,
"Kwa maana hiyo wewe umependa lile tukio lililotokea siku ile?"
Msaidizi wa Mganga alimuuliza Sajenti Minja,
"Tukio sasa, maana yalikuwa mengi" Sajenti Minja aliuliza,
"La wenzangu kuuawa kinyama?" Msaidizi wa Mganga aliuliza,
"Hapana, nitalifurahia vipi wakati lilikuja kuharibu tiba ya ndugu
yangu na nikampoteza mtu ambaye ndiye nilikuwa nategemea yeye
atamponya ndugu yangu?" Sajenti Minja aliongea kwa upole na machozi
yakimtoka kwa mbali ili kumshawishi tu Msaidizi wa Mganga asiseme
ukweli mbele ya Polisi wengine,
"Sasa kwanini nifiche?" Msaidizi wa Mganga akauliza tena ila
kipindi hiki aliuliza kwa upole,
"Kuwa na utu ndugu yangu, maana unachotaka kukifanya ni kuniharibia
maisha tu" Sajenti Minja aliendelea kumlalamikia Msaidizi wa
Mganga,
"Sio nakuharibia maisha, mbona mimi maisha yangu yameshaharibika?"
Msaidizi wa Mganga aliongea huku anamkodolea macho Sajenti Minja,
"Yameharibikaje sasa wakati upon hai na upon huru?" Sajenti Minja
alimuuliza,
"Hill sio tatizo, tatizo ni kwamba yule Mganga nilimchukulia kama
mkombozi wangu kutokana na maisha yangu" Msaidizi wa Mganga
aliongea,
" kivipi yaani?" Sajenti Minja alimuuliza,
"Yaani nilikuwa sina mbele wala nyuma, ila yule mzee aliniokota tu
mjini na kunichukua kisha akawa ananifundisha uganga na akawa
ananipa kipato kidogo angalau nikajiona mtu" Msaidizi wa Mganga
aliongea,
"Hilo sio tatizo, ngoja upone tutaongea zaidi, mimi nitakusaidia"
Sajenti Minja aliongea kwa huruma huku akichomoa noti nyingi kutoka
katika mfuko wake wa suruali na kumpa msaidizi wa Mganga,
"Za nini hizi?" Msaidizi wa Mganga aliuliza huku akiwa anaziangalia
zile hela akiwa hataki kuzipokea,
"Zitakusaidia kununua vitu vidogo vidogo kipindi upo hapa
Hospitali" Sajenti Minja aliongea huku akiwa bado amezishikilia
zile pesa,
"Wewe ni ndugu yangu bwana, tusaidiane" Sajenti Minja aliongea kwa
upole,
"Ngoja nitoke hospitali tutaongea vizuri ndugu yangu" Msaidizi wa
Mganga aliongea huku akizitia pesa zile mfukoni,
"Nikununulie chakula gani kabla sijaondoka" Sajenti Minja
alimuuliza,
"Chochote tu, mimi mswahili bwana sichaguagi chakula" msaidizi wa
Mganga aliongea,
"Wewe mgonjwa bwana, itabidi ule minyama nyama, ngoja nikakutafutie
kuku bosi" Sajenti Minja aliongea kwa furaha huku akitoka nje na
akiamini tayari ameshamteka hisia yule Msaidizi wa Mganga.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**"***********
Babu wa monchwari alivyopigwa ule mtama ile asubuhi kumbe aliteguka
mguu maeneo ya nyuma ya paja chini ya kiuno ila alivumilia na
hakuwaambia kitu chochote wale polisi kwa sababu walikuwa na hasira
muda ule, ila ilivyofika jioni maumivu yalimzidia na Babu wa
monchwari akawaambia polisi ila walimpuuza tu, masikini Babu wa
watu maumivu yalimzidia mpaka akawa Amalia kwa sauti kubwa kama
mtoto, kilio kikamfikia mkuu wa polisi na kuja kuangalia kuna nini,
" mbona huyo mzee analia?" Mkuu wa polisi aliwauliza askari
aliowakuta hapo ambayo walibaki wakitazamana bila kutoa jibu,
"Anamaumivu nadhani" Askari mmoja alijibu,
"Babu una tatizo gani?" Mkuu wa Polisi aliamua amuulize mwenyewe,
"Mguu nahisi umevunjika, nawaambia wanisaidie ila wananitukana"
Babu alijibu huku akiendelea kulia,
"Umevunjikaje, umeanguka?" Mkuu wa Polisi aliuliza,
"Hao wenyewe walinipiga asubuhi" Babu alijibu,
"Hata mambo ya kuwapiga watuhumuwa si tulishawakataza?, tena
mnampiga mzee kabisa..ebu chukueni gari ya doria mumpeleke
hospitali" Mkuu wa Polisi aliongea kwa ukali na vijana wake
wakanyanyuka haraka,
"Kwani yupo hapa kwa kosa gani" Mkuu wa polisi akauliza,
"Huyu ndiye yule mlinzi wa monchwari" Askari mmoja akajibu,
"Hata mumpeleke hospitali akapatiwe matibabu na mumrudishe hapa,"
Mkuu wa polisi aliongea na kuondoka huku akiwaacha vijana wake
wakimbeba Babu monchwari na kumpeleka kwenye gari na safari ya
hospitali ikaanza.
Iliwachukua dakika chache kufika hospitali, walimshusha Babu na
kumpeleka kupata matibabu.
Babu akapatiwa huduma kisha kwa Saa nzima na akaonekana ni mfupa tu
ulikuwa umehama eneo lake, madaktari wakafanya jitihada na kumtibu
bila tatizo na kuwaruhusu askari waondoke nae.
Askari walipotoka nje walienda moja kwa moja mpaka kwenye gari yao,
wakapanda gari ili warudi kituoni, kwa bahati mbaya gari yao
ilipata itilafu ikawa haiwaki, ikabidi wapige simu kwa mkuu wao ili
wapate msaada, mkuu wao akawapa namba ya sajenti Minja na kuwaambia
yuko pale hospitali kwa hiyo wampigie awape msaada wa kuwarudisha
kituoni kwa maana Sajenti ana gari.
Sajenti Minja baada ya kupigiwa simu akawaelekeza mahali gari lake
lilipo, wale askari na Babu wa mochwari wakafika mahali gari
lilipo, kisha wakawa wanamsubiri sajenti Minja atoke ndani ili
awarudishe kituoni, na Babu wa monchwari ndio kabisa alikuwa
anaangalia katika mlango wa kutokea hospitali ambayo ndio njia
anayokuja nayo Sajenti Minja..
...Sajenti Minja wakati anatoka ndani ya hospitali, akawaona wale
polisi na yule babu wa mochwari kupitia dirishani, akasita, kisha
akili yake ikafanya kazi haraka.
akarudi kisha akawapigia simu wale askari na kuwaambia kuwa yeye
bado ana shughuli anazifanya katika eneo like la hospitali, kwa
hiyo askari mmoja amfuate ndani ili akampe ufunguo,
mmoja kati ya wale polisi akaenda alipoelekezwa na sajenti Minja,
akapewa ufunguo, kisha akaambiwa arudishe gari pale hospitalini
baada ya kazi zao
***********************
Sajenti Minja aliingia katika nyumba ya dada yake saa mbili usiku,
baada ya salamu wakakumbushana mambo yaliyowakuta usiku uliopita,
wakafurahi na kuhuzunika pia,
Ila habari iliyowashtua wote ni kupatikana kwa wale maiti na mtu
mmoja akiwa mzima, pia sajenti Minja akawaambia namna
alivyofundisha yule msaidizi wa mganga kukana kujua lolote.
Mama kayoza kidogo akashusha presha baada ya kusikia hivyo,
"Kitu kingine kibaya ni kwamba hata yule babu wa monchwari
aliyetusaidia kuiba ile maiti nae amekamatwa ila sijajua kwa kesi
gani?" Sajenti Minja aliendelea kutoa habari mbaya,
"Ni hiyo hiyo ya kupotea kwa maiti, asubuhi si nilikuwa hospitali
nilienda kumuona mtu, ndio nikakutana na hizo habari, ila maiti
yenyewe imeshapatikana uko makaburini ilikutwa pamoja na hiyo miili
ya waganga wenu" Mama Kayoza aliwapa habari,
"Kama maiti imepatikana itakuwa afadhali kwa Babu" Kayoza aliongea,
"Hujui sheria mjomba, Babu hawezi kuachiwa mpaka ipatikane au
ijulikane sababu za kuuza ile maiti" Sajenti Minja aliongea huku
akimuangalia Kayoza,
"Sababu iliyomfanye auze si ni pesa?" Kayoza alijibu kiutani na
wenzake wacheke,
"Haya mambo mazito msiyachukulie kiutani utani hivyo" Mama Kayoza
aliongea huku akionekana kutofurahishwa na jibu la Kayoza,
"Mama inabidi tujifurahishe tu, ukisema uegemee sana upande wa
yanayotukuta, tutakuwa watu wa machozi kila siku" Kayoza alimwambia
Mama yake,
"Ujinga huo, badala uangalie namna ya kujisaidia unakalia kuongea
vitu visivyo na kichwa wala miguu" Mama Kayoza aliendelea
kumshambulia mwanaye,
"Vitu vya maana kama vipi?, ngoja nijiandae niende kanisani" Kayoza
aliongea kwa hasira huku akiondoka sebuleni,
"Ana hasira kama babu yake, mzee John Minja" Sajenti Minja aliongea
huku akicheka,
"Mjinga tu, hasira ananiletea Mimi badala ya kumpelekea bibi yake
uko kijijini" Mama Kayoza aliongea,
"Kayoza anaenda kanisani?" Sajenti Minja aliuliza,
"Leo kuna maombi, tena na wewe itabidi uende ili bwana akakupe
wepesi uenda kazi ya kumsaidia mjomba wako itatimia haraka" Mama
Kayoza alimwambia Sajenti Minja,
"Sawa itabidi tuongozane, kwani maombi yataisha saa ngapi?" Sajenti
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Minja akauliza,
"Tunakesha" Mama Kayoza alijibu,
"Mh..sasa si itabidi niende nyumbani nikabadili nguo" Sajenti Minja
aliongea,
"Kwani hizo ulizovaa zina ubaya Gani? Mama Kayoza aliuliza,
"Mimi naona sio vizuri kwenda Nazi kwa sababu nimeshinda nazo kutwa
nzima" Sajenti Minja alijibu,
"Hiyo sio sababu, nenda kaoge uende kanisani" Mama Kayoza aliongea,
"Sawa basi, nirudi baada ya muda gani?" Sajenti Minja aliuliza huku
akiinuka,
"Hakuna kuondoka, nilipokwambia ukaoge nilimaanisha uingie bafuni,
sasa unavyotaka kuondoka unadhani bafu lipo kwako tu?" Mama Kayoza
aliuliza,
"Sawa bwana, basi ngoja nikajitayarishe" Sajenti Minja aliongea
huku akielekea vilipo vyumba vya wakina Kayoza,
Baada ya saa moja na nusu wote walikuwa wamejiandaa mpaka Omary
wakaanza kwenda eneo la maombi.
Walienda kwa miguu tu kwa maana ni eneo jirani na wanapoishi.
Walifika na muda ulipofika waumini walikuwa wengi sana kanisani,
walianza kwa kuimba nyimbo mbalimbali za kutukuza.
Baada ya saa zima Mchungaji Wingo aliingia, akakaa katika kiti
anachopaswa kuwepo. Nyimbo ziliimbwa kisha waimbaji wakamaliza,
sala zilianza, walisali muda mrefu sana mpaka kayoza akachoka
kutokana na kwamba yeye sio mtu aliyezoea sana kwenda kanisani,
"oya kaka, tusepe" kayoza alimwambia Omari ambae alikuwa anasinzia
tu muda wote.
"wapi sasa" Omari akauliza kivivu huku akijinyoosha,
"maskani dogo, we unasinzia tu bila ya mpango, usije ukaharibu hewa
bure" Kayoza aliongea kwa utani.
"aah wapi, mimi nina kontroo wewe" Omari akajibu kisha wote
wakacheka.
Wakatoka nje ya kanisa wakawa wanaelekea nyumbani, ilikuwa kama saa
saba usiku hivi, kwa mbali wakaona msichana anawakimbilia, alikuwa
yule binti wa mchungaji,
"habari jamani" Binti akawasalimu.
"nzuri" wakajibu kwa pamoja.
"Kaka unaweza kutupisha kidogo?" Binti Mchungaji aliongea huku
akimuangalia Omary,
"Sawa" Omary alijibu huku akitangulia mbele na kuwaacha Kayoza na
Binti Mchungaji wakiwa wamesimama,
"vipi jibu langu Kayoza" Binti Mchungaji alimuuliza kayoza huku
akiwa hana chembe ya aibu.
"kesho nitakujibu" Kayoza akajibu kwa ufupi.
"jamani mbona unanifanyia hivyo, au kwa kuwa nimekwambia
nakupenda?" Binti Mchungaji alilalamika kwa huruma.
"sikia binti, hapa unapoteza muda wako bure, kiukweli kabisa mi
siwezi kukubalia ombi lako" Kayoza aliongea kwa ujasili kwa maana
aliona bora amueleze ukweli tu kuliko kumpotezea muda, Binti
Mchungaji alijishusha sana, alafu akajenga chuki kali sana kwa
Kayoza.
"Kwanini umeamua kufanya hivyo? au kwa kuwa nimeamua kukueleza
hisia zangu?" Binti Mchungaji aliongea huku machozi yanamtoka,
"Nimefanya hivi kwa sababu nakupenda na najipenda pia" Kayoza
aliongea kwa sauti ya chini kisha akaondoka kumfuata Omary,
"anajiona mzuri kumbe hana lolote, ni shetani tu ananyonya damu za
watu, na kesho nitaitoa taharifa polisi ili nipate yale mapesa
waliyotangaza" Binti Mchungaji aliongea kimoyo moyo huku akiwa
anarudi kanisani na hasira kibao zikiwa zimemtawala.
*******
"kaka umeniangusha" Omari aliongea huku akitabasamu
"achana nae, mtoto wa mchungaji alafu anaendekeza ukicheche" Kayoza
alijibu.
"Ila mpaka mwanamke akuambie maneno nayo, ujue anakupenda kweli"
Omary alimwambia Kayoza,
"Akampende baba yake na mama yake, mimi sina taimu nae" Kayoza
alijibu kijeuri,
"Sawa bwana, kufanya hivyo umemuepusha na kifo",Omary aliongea,
"Sijamuepusha, sema nimemsogezea mbele kifo kwa maana kifo
hakiepukiki" Kayoza aliongea wakati wanafika eneo la nyumbani kwao.
**""""***************
Ilipofika alfajili, Sajenti Minja aliondoka kanisani na kuelekea
moja kwa moja nyumbani kwake kupumzika, kwa kuwa alichelewa sana
kulala alijikuta anautandika usingizi mzito.
Mida ya saa nne akakurupuka kitandani kwake, ni kawaida yake
kujisachi anapoamka, hasa pale anapolala na nguo alizotoka kutembea
nazo,
alipojisachi, akakuta hana kitambulisho cha ofisini,
"mh, kitakuwa wapi, ila ngoja nikakicheki kwa dada kule na nidoee
chai kabisa" sajenti Minja alijiongelesha peke yake.
Akaenda kuoga na kujisafisha kinywa kisha akajiandaa ili aende kwa
Dada yake.
Akatoka nje akawasha gari, akaondoka
**********************
Binti wa mchungaji aliamka ana hasira sana siku hiyo, aliamka saa
tatu, ila mpaka saa nne alikuwa ameshawapiga makofi wadogo zake
wawili kutokana na hasira alizonazo. Tena aliwapiga kwa makosa
madogo madogo tu yasiyo na msingi.
Binti Mchungaji alipomaliza kazi zake, akaenda kuoga, kisha akanywa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
chai, akavaa viwalo vyake vilivyompendeza, akamuaga mama yake kuwa
anaenda kununua nguo.
"leo ndio mwisho wake, anaringa kama hana dhambi!" Binti Mchungaji
aliongea kimoyo moyo wakati akitoka ndani ya geti la nyumba yao na
kuishika barabara iendayo sehemu kilipo kituo kikubwa cha polisi
cha mkoa,
"nikifika pale polisi namueleza askari yeyote, hata wasiponipa hela
sawa, nataka tu nimkomeshe" Binti Mchungaji aliendelea
kujiongelesha Mwenyewe, mara akasikia gari inapiga breki miguuni
kwake, alishtuka na kuruka pembeni mpwa barabara, maana alikuwa na
mawazo kiasi kwamba hakujua kama anatembea katikati ya barabara,
"punguza mawazo dada, mbona we bado mdogo tu" yule dereva wa ile
gari alimwambia binti wa mchungaji.
"samahani kaka yangu" binti wa mchungaji alijitetea.
Kisha yule dereva wa gari akashuka ili kuiangalia gari yake iko
salama, maana breki aliyoipiga ilikuwa Kali sana.
"aha! Kumbe polisi!" Binti Mchungaji alijikuta anahamaki baada ya
kumuona yule dereva wa ile gari amevaa gwanda za polisi.
"ee, kwani vipi?" yule polisi aliuliza huku akimuangalia Binti wa
Mchungaji,
"kuna habari njema nataka kukwambia" Binti Mchungaji alisema huku
furaha yake ikionekana dhahiri machoni pake,
"habari gani hiyo?" yule polisi akamuuliza huku akiwa na shauku ya
kutaka kujua,
Yule binti akageuka nyuma kuangalia kama kuna mtu anakuja,
aliporidhka kuwa hakuna mtu, akasema,
"yule kijana anayenyonya damu za watu anakaa palee" Binti Mchungaji
akasema huku akiionyeshea nyumba ya Mama kayoza ambayo ilikuwa
inaonekana kwa mbali kidogo.
"Una uhakika binti?" Askari aliuliza huku akiwa ahamini
anachoambiwa,
"Twende unipeleke" askari aliongea huku akimfungulia Mlango binti
Mchungaji ambayo aliingia kwenye gari kwa madaha kwa maana
alishaimaliza kazi aliyokusudia kuifanya....
Binti Mchungaji akaingia ndani ya gari na kukaa siti ya mbele,
"Wewe umejuaje kuwa huyo kijana ndiye mnyonya damu?" Askari
aliuliza huku akimuangalia Binti Mchungaji machoni,
"We hutakiwi kuniuliza, unachotakiwa ni kwenda kumkamata" Binti
Mchungaji aliongea,
"Akikataa kuwa sio yeye unafikiri tutafanyaje, inatakiwa uniambie
umejuaje kuwa ndiye yeye ili ninapoenda kumkamata niwe na ushahidi"
Askari aliuliza,
"Ameshawahi kuja kanisani kwetu ili tumuombee ili apone na ahachane
na hayo mambo ya kuua kwa kunyonya damu" Binti Mchungaji alijibu,
"Kumbe hata yeye hapendi we kunyonya damu na kuua?" Askari aliuliza
huku akimtazama,
"Itakuwa hapendi, na ndio maana alikuja kanisani kuombewa" Binti
Mchungaji alijibu,
"Sasa kama hata yeye hapendi kuua kuna haja gani ya kumkamata na
wakati anaonekana ni mtu mwema?" Askari aliuliza,
"Wewe kaka ni hakimu au askari? Maana unauliza tu badala ya kwenda
kumkamata mtuhumiwa, au unaogopa kunyonywa damu?" Binti Mchungaji
aliuliza kwa hasira,
"Samahani, naomba nikuulize swali la mwisho kabla sijaenda
kumkamata" Askari alitoa ombi,
"Sitaki swali, kama hauendi niambie nishuke, mbona askari mpo wengi
tu, nitaenda kuwaambia Askari wengine" Binti Mchungaji aliongea kwa
jeuri huku akiangalia pembeni,
"Naomba uniruhusu tu nikuulize hill swali, baada ya hapo
sitokuuliza tena" Askari aliongea kwa upole,
"Na liwe la mwisho kweli, haya uliza" Binti Mchungaji aliongea kwa
mbwembwe,
"Je huyo mnyonya damu angekua ndugu yako ungetoa taharifa polisi?"
Askari aliuliza huku akiwasha gari,
"Inategemea na undugu wenyewe, kama ni wa mbali namchomea tu" Binti
Mchungaji aliongea huku akifurahi gari kuwashwa kwa maana alipata
uhakika wa kutimiza malengo yake,
"Angekuwa mtoto wa Dada yako au wa kaka yako je?" Askari aliuliza
huku akiliondoa gari,
"Huo ni undugu wa karibu kabisa, siwezi kwenda kumsemea polisi
kamwe" Binti Mchungaji aliongea huku akijitengeneza nywele vizuri,
akiwa bado anajiweka vzuri alishangaa yule askari akisimamisha gari
na kumpiga Kofi zito la usoni,
"Unanipigia nini sasa?" Binti Mchungaji aliuliza huku akiwa
amejishika uso, ila yule Askari hakumjibu, akamuongeza jingine la
uso tena pale pale alipopapiga mwanzo,
"Unanipigia nini sasa?" Binti Mchungaji aliuliza huku akisikilizia
maumivu,
"Hiyo tabia yako ndio imekuponza" Askari aliongea huku akitabasamu,
"Tabia gani jamani" Binti Mchungaji alilamika huku akiwa amejishika
shavu,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Umbea, sio kila kitu kinatolewa taharifa" Askari aliongea huku
akimuongezea kofi na kisha akafungua mlango wa gari ili yule
msichana ashuke.
Binti akatelemka haraka haraka na yule Askari akaiondoa gari kwa
spidi ya juu.
Gari la yule askari lilipopotea, yule binti mchungaji nae
akahairisha safari yake,
"akha mwenzangu, huyu mmoja tu nimekutana nae njiani kanipiga vibao
namna hii, je nikienda huko polisi si wataniua kabisa?" yule binti
wa mchungaji aliongea huku akiwa ameshika njia ya kwenda kwao.
***********************
Sajenti Minja aliingia kwa Dada yake asubuhi na kuwakuta wakiwa
wamekaa,
"Hivi huyu Mchungaji wenu ana binti mkubwa?" Sajenti Minja aliuliza
baada ya salamu,
"Anae binti mkubwa kabisa, kwani vipi?" Mama Kayoza aliuliza,
"Aisee yule sio mtu mzuri kwetu, so nimekutana nae hapo njiani
akanisimamisha na kuanza kunipa habari za Kayoza" Sajenti Minja
aliongea,
"Eeeh, makubwa, amekwambiaje?" Mama Kayoza aliuliza,.
"Ooh Mara mnyonya damu namjua, alikuja kanisa kwetu na kuombewa,
ooh Mara sijui nini, yaani inaonekana anamjua vzuri Kayoza" Sajenti
Minja aliongea,
"Ikawaje sasa?" Mama Kayoza akauliza,
"Aisee nimemuwasha mabanzi, sijui hata kama atarudia tena kusema"
Sajenti Minja aliongea huku akicheka,
"Usiseme hivyo, anaweza kwenda kituoni yule, maana ameshaonekana
sio mtu mzuri" Mama Kayoza aliongea,
" hata akienda atakuwa hana Maelezo ya kutosha" Sajenti Minja
aliongea kwa dharau,
"Tatizo lako wewe ni mpuuzi" Mama Kayoza aliongea kwa hasira baada
ya kumuona Sajento Minja ana dharau
"Sasa Dada mbona unanitukana tena?" Sajenti Minja aliuliza,.
"Mpuuzi sio tusi, mtu anayepuuza jambo ndio huitwa mpuuzi" Mama
Kayoza alimjibu ndugu yake,
"Sijapuuza hill jambo, mimi bado namfuatilia huyo binti ila sidhani
kama ataenda kutoa taharifa polisi" Sajenti Minja aliongea,
"Haya bwana" Mama Kayoza aliongea kinyonge,
"Jana niliangusha kitambulisho changu, alafu hata sijui
nilipokiangushia" Sajenti Minja aliamua kubadilisha mada,
"Kipo ndani, ulikiangushia hapa" Mama Kayoza alijibu,
"Afadhali, maana nilishapatwa na wasiwasi wa kukipoteza" Sajenti
Minja aliongea.
Baada ya kukichukua kitambulisho chake aliaga na kwenda moja kwa
moja hospitali kwa ajili ya kwenda kumuona Msaidizi wa Mganga.
Alifika mapema na moja kwa moja akaenda kumjulia hali Msaidizi wa
Mganga, baada ya kumjulia hali mgonjwa wake, Sajenti Minja
alifarijika kumuona mgonjwa wake amepata nguvu na anatembea kama
kawaida.
Bila kupoteza muda, sajenti Minja akamtafuta daktari, kisha akapewa
ruhusa ya kuondoka na mgonjwa wake, akamchukua hadi nyumbani kwake.
Kisha akampa taharifa mkuu wa polisi kuwa yule msaidizi wa mganga
ametoka hospitali na anakaa nae nyumbani kwake, mkuu akafurahi
kusikia hivyo.
***********************
Kayoza na Omari walijua sababu kubwa ya binti wa mchungaji kutaka
kwenda polisi ni kutokana na kukataliwa na Kayoza kuwa mpenzi wake,
Omari akaamua amchukue yeye, ikawa kila siku ni lazima aende kwa
mchungaji, tena gia aliyokuwa anaenda nayo ni kununua maziwa,
taratibu mazoea yakaanza hadi wakazoeana kabisa, mwisho kabisa
Omari akamtongoza binti wa mchungaji, bila iyana alikubaliwa kwa
roho safi, na sasa Omary na Binti Mchungaji wakawa Wapenzi rasmi.
***********************
Siku moja mkuu wa polisi alikuwa anafungua mlango wa ofisini kwake,
ndio akawaona askari watatu wakiwa wameongozana na babu aliyefungwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
pingu. Alikuwa ni yule Babu wa monchwari, akawaita, kisha akaingia
ofisini, wale askari na yule babu nao wakaingia,
"hii kesi ya huyu mzee mbona mnaiendesha pole pole sana". Mkuu wa
polisi aliwauliza wale askari.
"ushaidi ndio unatuchelesha mkuu" Askari mmoja alijibu
"niambieni katika uchunguzi wenu mmefikia wapi" Mkuu wa Polisi
akawatupia swali jingine,
"hakuna mwanga wowote tuliopata" yule askari akamjibu tena mkuu wa
polisi.
"nyie wazembe kweli, ile maiti iliyoibiwa si iliokotwa pamoja na
zile maiti zilizonyonywa damu?" Mkuu wa polisi akauliza kwa jazba,
"ndio mkuu" wale askari wakajibu kwa pamoja,
"mlienda kumuhoji yule mtu aliekutwa hai?" Mkuu wa Polisi akawapa
swali jingine.
"hapana mkuu" akajibu yule Askari ambae siku zote uso wake
utawaliwa na hasira.
"kwanini" mkuu wa polisi akaendelea kuwabana na maswali.
"yule anahusika na kesi ya sajenti Minja" yule askari akajitetea
kipumbavu.,
"ok, sasa hii kesi ya huyu babu nampa sajenti Minja kwa sababu
mmesema zinaingiliana, basi atazishughulikia zote" Mkuu wa polisi
alimaliza kisha akawaamuru watoke ofisini kwake, wamuache babu wa
monchwari peke yake, wakamtii kisha wale askari wakaondoka.
Kisha mkuu wa polisi akachukua simu yake ya mkononi alafu akapiga,
"hallow Minja uko wapi?"mkuu wa polisi aliuliza. Baada ya kujibiwa
akaendelea,
"Nipo ofisini kwangu" Sajenti Minja alijibu huku akishangaa ile
simu ya ghafla kutoka kwa mkubwa wake,
"ok, njoo ofisini kwangu" Mkuu wa Polisi aliongea kisha akakata
simu.
"nakukabidhi kwa mtu anaejua kazi" Mkuu wa polis alimwambia babu wa
mochwari,
"Nashukuru sana kwa kunijali mwanangu" Babu wa monchwari aliongea
huku akiangalia chini.
"Sio nakujali, huo ndio utaratibu wa kazi" Mkuu wa Polisi aliongea.
************
Sajenti Minja baada ya simu aliyopigiwa na mkuu wake kukatwa,
akatoka ofisini kwake huku akiwa na maswali kibao juu ya kuitwa
kwake na Mkuu wa Kituo.
Akawa anaelekea ofisi ya mkuu wa polìsi, alipofika mlangoni
akagonga hodi,
"yes, come in" sauti ya mkuu wake kutoka ndani ilimjibu,
Sajent Minja akashika kitasa cha mlango akanyonga kwa nia ya
kufungua mlango.....
...sajenti Minja akanyonga kitasa, haikuonekana dalili ya mlango
kufunguka, mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, mara akasikia mlango
unafunguliwa, akatoka mkuu wa polisi,
"minja nisubiri ndani mara moja, naenda msalani dakika moja", mkuu
wa polisi alipofungua mlango aliongea maneno hayo huku akiwa
anatembea kumuacha sajenti Minja, mlango ulikuwa bado uko wazi,
Sajenti Minja akanyanyua mguu wa kulia ili kuingia ndani,
"jesus christ" alijikuta anasema kwa sauti ya chini baada ya
kugundua kuwa aliekuwa ndani ni babu wa mochwari, ila bahati nzuri
ni kwamba yule babu alikuwa ameinamia chini, kwa hiyo hakuweza
kumgundua Sajenti Minja.
Sajenti Minja alirudi nje kwa kasi, kisha akaurudishia mlango huku
anahema kwa fujo kama katoka kukimbia mbio ndefu,
"vipi Minja, mbona unaonekana hauko kawaida", sauti ya mkuu wa
polisi ilimshtua Sajenti Minja,
"nimepigiwa simu, nyumbani kuna matatizo" Sajenti Minja alitumia
uongo,
"ila kulikuwa na kazi nataka kukupa, tuingie ndani kuna kesi nataka
kukupa, alafu utaendelea na ratiba zako", Mkuu wa Polisi alimwambia
Sajenti Minja,
"samahani mkuu, niko chini ya miguu yako, naomba hiyo kesi unipe
baadae, uko nyumbani sio kwema kabisa", Sajenti Minja aliongea uku
akiwa ameweka sura ya huzuni,
"mmmh, ok, sawa, ukimaliza ya nyumbani, unijulishe, maana nataka
nikupe kesi ya mzee mmoja hivi", Mkuu wa polisi alimkubalia,
"Nikimaliza nitakujulisha na asante mkuu kwa kunikubalia niende
nyumbani, nikirudi nitakufahamisha" , Sajenti Minja alijibu huku
akiwa anaanza kuondoka,
"Minja" Mkuu wa Polisi aliita tena wakati Sajenti Minja anaanza
kuondoka,
"naam mkuu" Sajenti Minja aliitikia baada ya kuitwa,
"unaondoka tu, ila hujaniambia nyumbani kuna tatizo gani", Mkuu wa
Polisi alihoji,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"kuna kajomba kangu, ambacho ni katoto ka dada yangu ambae
nilikuambia anaishi hapa, nimeambiwa amegongwa na gari na hali yake
sio nzuri", Sajenti Minja aliendelea kutunga uongo mbele ya bosi
wake,
"ooh, poleni sana, haya bwana wahi,"Mkuu wa Polisi alimruhusu
sajenti Minja kwa mtindo huo.
Sajenti Minja aliondoka kwa mwendo wa haraka haraka mpaka gari yake
ilipokuwepo,
"mhm, nimesevu so hadi raha, leo nilikua nahaibika mbele ya bosi",
Sajenti Minja aliongea wakati anajipakia kwenye gari yake.
********************
"duh, mama ujue mi nashindwa kuelewa, naona kama ndio mmeniacha
niendelee kuwa katika hali hii", Kayoza alimwambia mama yake wakiwa
wanapata chakula cha mchana,
"ebu, acha uwendawazimu uko, mzazi gani anaependa mwanae awe katika
matatizo?, we msubiri mjomba ako arudi labda atakuwa na mpya", Mama
kayoza alimjibu mwanae huku akiwa anasafisha mikono yake kwa maji,
"lakini mama", Kayoza kabla hajamaliza kuongea, ilisikika sauti ya
mtu ikigonga mlango,
"sukuma, mlango uko wazi", Mama Kayoza aliongea kwa sauti ya juu
kidogo, ili mgongaji amsikie,
"hodi mpaka ndani, eeh, nina mguu mzuri kweli, yaani nimefika
wakati wa mahakuli", Sajenti Minja aliongea huku akiurudishia
mlango
,"karibu anko, ingawa ndo kinaisha", Omari alimwambia sajenti
Minja, kisha wote wakacheka,
"ebu tuachane na hayo, leo kidogo nipate aibu ya mwaka mbele ya
bosi wangu", Sajenti Minja alibadilisha stori,
"ehe, nini tena?", Mama Kayoza aliuliza kwa shauku.Sajenti Minja
aliwaeleza mwanzo mpaka mwisho,
"kwa hiyo inavyoonekana anataka na kesi ya yule babu wa mochwari
iwe chini yako?" Mama Kayoza aliuliza,
"ndio hivyo" Sajenti Minja alijibu kinyonge,
"sasa utafanyaje" Mama Kayoza aliuliza,
"nitamkimbia kimbia hivyo hivyo mpaka achoke", Sajenti Minja
alialiongea,
"Mimi naona bora uichukue na hiyo kesi hili uweze kuwadhibiti
vizuri wahusika" Omary alichangia
"Hapana, mimi nitajitahidi niikwepe tu" Sajenti Minja aliongea,
"Ichukue hiyo kesi kwa maana huwezi jua mipango ya Mungu" Mama
Kayoza aliongea,
"Tutajua uko mbele ya safari. jamani kuna kaugali kalichobaki?"
Sajenti Minja aliuliza,
"ugali upo, ila mboga ndo imeisha, ngoja wajomba zako wakakununulie
maziwa kwa mchungaji", Mama kayoza alimjibu Sajenti Minja huku
akimpa kayoza hela ya maziwa,
"Kwani hatuwezi kununua mboga nyingine zaidi ya maziwa" Sajenti
Minja aliuliza,
"Mbona tunaweza kununua hata maharage au nyama, tatizo tukiinjika
mpaka viive si utakuwa umeshakufa na njaa yako?" Mama Kayoza
aliongea,
"Kweli Dada, basi nyie wahini, maana njaa niliyonayo ni ya
hatari...
baada ya wakina kayoza kutoka, Sajenti Minja na dada yake
waliendelea na maongezi yao.
"afadhali umekuja mwenzangu, maana mjomba ako kanichachamalia
hapa", Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja
"kachachamaa na nini tena?"Sajenti Minja akauliza,
"eti anadai tuko kimya katika kufuatilia matatizo yake", Mama
Kayoza akajibu,
"kuna askari niliongea nae jana, akaniambia kuna mtaalam wa jadi
ana uwezo mkubwa wa kusaidia watu", Sajenti Minja alimwambia dada
yake
,"kwa hiyo ulimwambia una ndugu yako ananyonya damu?", mama Kayoza
aliuliza kwa mshtuko,
"kwani mi sina hakili mpaka nimwambie hivyo?, nilimdanganya
natokewa na mauzauza kila nikitaka kulala", Sajenti Minja akamjibu
dada yake,
"ataweza kweli kumtibia kayoza?", Mama kayoza akamtupia mdogo wake
swali jingine,
"dada nawe kwa maswali!, tutajua uko uko kama ataweza au lah",
Sajenti Minja alimjibu dada yake,
"lini mtaenda uko", mama Kayoza akauliza tena
"nafikiri kesho, kama nitapata nafasi", Sajenti Minja alijibu
"haya bwana, wacha nikakutayarishie chakula jikoni", mama kayoza
aliongea huku akinyanyuka kwenye kochi,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"hayo ndo mambo sasa, kama kuna pilipili niwekee", Sajenti Minja
alisema na kumfanya mama kayoza ahangue kicheko.
"Sasa hiyo pilipili utaiweka katika maziwa?" Mama Kayoza aliuliza
huku akicheka,
"Nitaitafunia tu na ugali" Sajenti Minja alijibu,
"Ngoja nikutafutie kama ntaipata" Mama Kayoza aliongea huku
akiingia jikoni.
"Sema siku hizi umekuwa mswahili kweli Dada yangu" Sajenti Minja
aliongea huku akitabasamu,
"Kwanini unasema hivyo?" Mama Kayoza aliuliza huku akisimama,
"Naona nawe unakubali tu tumpeleke mwanao kwa waganga sio kama
zamani ulivyoshikilia msimamo wako wa kanisani" Sajenti Minja
alimwambia Dada yake,
"Ujue Mungu hana njia moja ya kukupa mafanikio, unatakiwa upitie
njia nyingi lakini ukimuamini yeye tu na sio vitu vingine" Mama
Kayoza alimwambia Sajenti Minja,
"Sawa mama mchungaji, inabidi na wewe ujenge kanisa lako sasa"
Sajenti Minja alimwambia Mama Kayoza,
"Ebu kwenda zako uko, kwanza ulivyosema mchungaji umenikumbusha awa
wendawazimu waliofuata maziwa, mbona wamechelewa hivyo?" Mama
Kayoza aliuliza,
"Wana mambo mengi wale vijana, usikute wanamnyatia yule binti wa
mchungaji" Sajenti Minja aliongea kwa utani huku akicheka,
"Acha uwendawazimu wako, watoto wa mchungaji wana maadili wewe"
Mama Kayoza aliongea,
"Sio wote, kama yule binti mcharuko niliekutana nae juzi ni bure
kabisa, bora angeishi uswahilini tu" Sajenti Minja aliongea huku
akicheka,
"Kwani ana kosa gani? Si alikuwa anaenda polisi kusema habari za
ukweli" Mama Kayoza aliongea huku akitabasamu,
"We si ni mlokole? Nenda na wewe polisi kaseme hizo hizo habari
kuwa mwanao muuaji" Sajenti Minja alimwambia Mama Kayoza,
"Mtoto anauma bwana, mtoto mwenyewe ndio huyo huyo mmoja kama roho"
Mama Kayoza aliongea huku akicheka,
"Nenda jikoni bwana, maana story zimezidi mpaka unasahau kuwa mimi
njaa inaniuma" Sajenti Minja alimwambia Dada yake,
"Hata baba, usije ukanifia bure kwa njaa" Mama Kayoza aliongea huku
akielekea jikoni.
*********************
Baada ya mkuu wa polisi kurudi ndani, alimpgia simu askari mwingine
na kumwambia amrudishe rumande Babu wa mochwari,
"jamani nitakaa huku mpaka lini, nina mke na watoto mimi",Babu wa
mochwari aliongea huku machozi yakimtoka,
"usijali mzee wangu, upepelezi utakamilika hivi karibuni", Mkuu wa
polisi alimjibu Babu wa mochwari kwa huruma.
"Mwanzo askari wako waliniambia nikiri kosa ili niachiwe, nikakiri
kosa kuwa ni kweli mwili umeibwa, lakini hawajaniachia, naambulia
kipigo tu mpaka viungo vinateguka" Babu wa monchwari alilalamika,
"Mzee ujue upelelezi sio kitu cha kukurupuka tu, inahitajika muda
mrefu wa kuchunguza na kujiridhisha na jibu la kile
kilichopelelezwa, na hapo sasa ndipo sisi tutaachana na wewe na
kesi yako itakuwa mahakamani" Mkuu wa polisi alimuelewesha Babu wa
monchwari,
"Mahakamani tena?, si nitafungwa jamani mie?" Babu wa monchwari
aliuliza huku akilalamika,
"Sasa sisi hatutaki ufungwe, na ndio maana tunaendelea kukuhifadhi
ili utusaidie kumpata huyo aliyeichukua hiyo maiti" Polisi
alimwambia Babu wa monchwari,
"Sasa mbona sioni juhudi zozote ukizifanya kumtafuta huyo mtu na
nilishawahi kumuona eneo hili huyo mtu mwenyewe" Babu wa monchwari
aliongea na kumfanya Mkuu wa polisi ashtuke kidogo,
"Alikuwa anafanya nini na kwa nini hukuwaambia Askari?" Mkuu wa
polisi aliuliza huku akimshangaa,
"Kitu ninachokishangaa ni kwamba alipotea ghafla, inawezekana
kabisa yule bwana si mtu wa kawaida, atakuwa mshirikina tu" Babu wa
monchwari aliongea,
"Kumbe ukimuona kwa sura unamjua vizuri tu?" Mkuu wa polisi
aliuliza,
"Vizuri sana tu, hata akiwa mbali namtambua" Babu wa monchwari
aliuliza,
"Ulivyomuona alivaaje, au alivaa kiaskari?" Mkuu wa polisi
alimdadisi Babu wa monchwari,
"Hajavaa kiaskari, na kwanza hawezi kuwa askari yule, ana ndevu
kabisa" Babu wa monchwari alijibu,
"Basis usijali babu, tunaendelea kufuatilia" Mkuu wa Polisi
aliongea,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kisha yule askari aliepigiwa simu aliingia na kisha akamchukua Babu
wa mochwari na kumrudisha rumande.
***********************
Wakina kayoza walipofika kwa Mchungaji Wingo, walimkuta Binti wa
mchungaji anafagia fagia
"karibuni", Binti wa mchungaji aliwakaribisha alipowaona,
"asante, za hapa?", Omari alijibu alafu akamjulia hali,
"poa my husband, Kayoza mambo?", baada ya kujibu salamu ya Omari,
binti wa mchungaji akamgeukia Kayoza,
"poa, kuna maziwa ya mtindi?" Kayoza akamjibu kwa mkato, kisha
akasema kilichompeleka,
"yapo, mnataka kiasi gani?" Binti Mchungaji akauliza,
"nusu lita" Kayoza alijibu huku akimpatia pesa, Binti wa mchungaji
akachua hela kisha akaingia ndani kuwapimia maziwa.
"kaka uko siriazi, hutaki hata kucheka nae", Omari alimwambia
kayoza huku akijichekesha
"boya sana huyu demu", Kayoza aliongea akiwa na chuki za wazi kwa
binti wa mchungaji.
Baada ya dakika tano binti wa mchungaji alitoka, akawapa maziwa
,"Omari baki, kuna kitu kizuri nataka kukwambia", Binti wa
mchungaji alisema,
"nibaki?, kwani ndani uko na nani?", Omari alimuhoji Binti wa
mchungaji,
"niko peke yangu, wote wameenda mjini, ila baba kaenda kanisani",
ndivyo alivyojibu,
"Boy we tangulia, mimi ninakuja" Omary alimwambia Kayoza,
"Sasa nikifika peke yangu mama si ataniuliza?" Kayoza alihoji,
"Utajua namna ya kumdanganya, ila hata sitochelewa" Omary aliongea,
"Poa, jitahidi kuwahi bwana" Kayoza aliongea huku akianza kuondoka.
"Twende ndani basi" Binti Mchungaji alimwambia Omary huku akimvuta
mkono,
"Huogopi?" Omary aliuliza huku akijatahidi kutosogea zaidi ya pale
alipo,
"Twende ommy, utaniudhi ujue" Binti Mchungaji aliongea sauti ya
kudeka na kumfanya Omary alegeze msimamo,
"Una hatari sana" Omary aliongea huku akipiga hatua kumfuata binti
mchungaji
"Twende usiogope, awa hawarudi sasa hivi" Binti Mchungaji aliongea
huku akifungua mlango wa chumbani kwake,
"Bora ungenipeleka sebuleni, huku ndio pabaya kabisa" Omary
aliongea huku akiingia katika chumba cha Mchungaji,
"Kelele bwana, kaa hapo mimi nakuja sasa hivi" Binti Mchungaji
aliongea huku akimkalisha Omary kitandani,
"Uwahi basi" Omary aliongea wakati Binti Mchungaji akitoka,
"Nakukuja sasa hivi, kuna kazi naenda kuimalizia chap chap" Binti
Mchungaji aliongea na kisha akatoka nje baada ya kuurudishia
mlango, Omary akabaki chumbani peke yake huku macho yake yakitalii
katika kila kona ya chumba kile cha Binti Mchungaji.
Baada ya Binti mchungaji kumaliza kazi, akaenda kujisafi mwili,
kisha akarudi chumbani kwake na kufunga mlango kwa ndani,
"we mtoto huogopi?, Omari alimuuliza huku akiwa na sura ya
wasiwasi, Binti wa mchungaji badala ya kujibu, yeye akaitoa ile
khanga aliyotokanayo kuoga na kubaki mtupu kama alivyozaliwa, Omari
akili ilimruka na uoga wote ukamtoka, bila kutarajia akamvuta binti
wa mchungaji kitandani, na kuamia katika ulimwengu mwingie.
Mchungaji Wingo aliporudi nyumbani kwake, akakuta mlango wa mbele
uko wazi, video sebuleni inawaka, akamuita binti yake, lakini
hakupata jibu, akaamua aende akamuangalie chumbani kwake,
alipokaribia mlango wa chumba cha binti yake, alisikia mlio wa
kitanda cha binti yake kikilalamika kwa fujo,
"mh..", mchungaji Wingo aliguna...
...mh", mchungaji aliguna, kisha akagonga mlango, mlio wa kitanda
ukakoma, kisha ukimya ukatawala,
we happy", Mchungaji Wingo akamuita binti yake,
"abee baba", happy akaitika,"una shughuli gani umo ndani?",
Mchungaji Wingo akamuuliza, kimya kikatawala tena, ila cha sasa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hivi kilikuwa kirefu kidogo,
"mbona hujibu?", Mchungaji Wingo akauliza baada ya ukimya,
"nilikuwa naa...naa...naa.., sijakusikia ulichosema baba", Happy
akashindwa kujibu akawa anajiuma uma tu,
"nimekuuliza una shughuli gani umo ndani, mbona kitanda kinapiga
kelele hivyo?", Mchungaji Wingo akarudia swali katika sauti ya
ukali,
"nafunga neti baba", happy akajibu huku sauti ikiwa na
wasiwasi,"neti tu, ndo kitanda kipige kelele namna hiyo?",
Mchungaji Wingo aliongea huku akiwa anarudi sebuleni, pia
alionekana hakuridhishwa na jibu la binti yake
.***************
Ndani baada ya kusikia mtu anagonga hodi, wote walishtuka, ila
hawakukurupuka, wakatulia tuli, baada ya kugundua kuwa anaegonga ni
mchungaji, happy aliteremka chini taratibu kisha akavaa kanga yake,
akawa anamjibu baba yake, kipindi hicho chote, Omari alikuwa
anajing'ang'aniza kupita dirishani bila mafanikio, baada ya
majibizano ya muda mfupi, kati ya happy na baba yake, Mchungaji
aliondoka mlangoni kwa happy, hapo ndipo Omari akapata sauti,
"Sasa nitatokaje nje?", Omari alimuuliza happy kwa sauti ya chini
sana,
"subiri kidogo, sasa hivi anaenda kuoga", Happy alimtoa Omari hofu.
"Happy umeniponza mwenzio" Omary aliongea huku akitaka kulia,
"Acha ujinga wewe, kwani baba amejua kinachoendelea?" Happy
aliuliza kwa ukali,
"Hata kama hajui, wewe unadhani nitatokaje nje?" Omary aliuliza
huku akiwa anafunga vifungo vya shati yake,
"Si nimekwambia ataenda kuoga muda si mrefu" Happy aliongea,
"Sasa mimi nitaaminije?" Omary alijikuta anauliza swali la kipuuzi,
"Mimi hapa ni kwetu, najua ratiba za watu wote hapa, ebu niamini
acha ujinga" Happy alimuelewesha Omary.
"Dah, tamaa nyingine mbaya sana" Omary aliongea peke yake huku
akijifuta jasho ingawa ndani hakukuwa na hali ya joto,
"Unasemaje" Happy alimuuliza Omary baada ya kumuona akiongea ingawa
hakumuelewa,
"Sijasema kitu bwana" Omary alijibu huku akionekana ana hasira I
logic hang any in an a na hofu.
"Mwenzangu ushaanza kuwa chizi" Happy aliongea huku akimcheka Omary
chinichini.
*********************
Mchungaji Wingo alipotoka mlangoni kwa binti yake, alienda
sebuleni, kisha akazima luninga, alafu akamuita happy,
"Umeshamaliza kufunga chandarua?" Mchungaji Wingo alimuuliza binti
yake,
"Tayari, alafu sijisikii vzuri" Happy alimwambia baba yake,
"Kwa hiyo umehisi itakuwa malaria na ndio maana ukafunga
chandarua?" Mchungaji Wingo aliuliza huku akitabasamu,
"Ndio hivyo, mimi nadhani itakuwa ni malaria tu" Happy alijibu huku
nae akitabasamu,
"Kuna maji ya moto?" Mchungaji Wingo aliamua kubadili mada,
"Ndio, yapo...yatakosaje wakati najua watumiaji mpo?" Happy
aliuliza,
"Ebu niandalie nikaoge mie" Mchungaji Wingo aliongea huku
akinyanyuka,
"Sawa mzee" Happy alijibu,
"Mama bado hajarudi?" Mchungaji Wingo aliuliza huku akisimama,
"Wakiendaga mjini wanawahigi kurudi kwani?, hiyo ni mpaka saa kumi
na mbili jioni" Happy alijibu baba yake,
"Huyu nae bwana, si ahache kwenda uwage unaenda wewe?, yeye
ameshaanza kuzeeka" Mchungaji Wingo aliongea kwa kulalamika,
"Wivu tu huo, muache aendage yeye, maana ndio anajua mahitaji ya
watoto" Happy aliongea wakati baba yake anaelekea chumbani.
Happy akaenda bafuni akachukua ndoo na kwenda nayo jikoni ambapo
aliiwekea maji ya moto na kuirudisha tena bafuni.
"Maji yapo tayari baba" Happy alipaza sauti kumwambia baba yake
aliyekuwepo chumbani,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Oooh nakuja, umeshayachanganya na maji ya baridi?" Mchungaji Wingo
aliuliza huku bado akiwa ndani,
"Utachanganya mwenyewe, maana Jana nilivyokuchanganyia ulilalama
nimezidisha ubaridi" Happy alimwambia baba yake,
"Bora hujachanganya, maana Sikh hizi nahitaji maji ya uvugu vugu
mkali kidogo" Mchungaji Wingo aliongea huku bado akiwa chumbani,
"Umeshaanza kuzeeka ndio maana unataka maji yenye joto Kali" Happy
alimwambia Baba yake huku akiwa bado amesimama mlangoni,
"Kweli aisee, naona umri unanitupa mkono" Mchungaji Wingo aliongea
huku akitoka ndani akiwa amejifunga taulo lake kiunoni na moja kwa
moja akanyoosha mpaka bafuni.
Alipoingia, akatoa taulo lake mwilini,
"mh..kumbe sabuni imeisha?", mchungaji aliongea peke yake, baada ya
kuangalia sehemu ya kuwekea sabuni ikiwa tupu mule bafuni,
Mchungaji Wingo akakata shauri la kurudi kutoka bafuni na kurudi
chumbani ambapo ndipo huifadhi sabuni nyingine.
********************
Happy Binti Mchungaji alipoona kuwa baba yake kaingia bafuni,
akaingia chumbani haraka,
"Tayari baba ameingia bafuni, twende nikutoe nje" Happy aliongea
kwa sauti ya chini ambayo ilisikika vyema masikioni mpwa Omary,
''Sasa njia tunayotokea si ndipo lilipo bafu, akisikia hatua za
watu wawili zinatembea si atagutuka?" Omary alimuuliza happy Binti
Mchungaji,
"Hawezi kugundua bwana, twende acha uoga" Happy aliendelea
kumwambia Omary,
"Sasa si bora nisubiri Stoke bafuni aende chumbani?" Omary
aliuliza,
"Acha ujinga, mama anarudi sasa hivi na wadogo zangu, wakikukuta
humu, je itakuwaje?" Happy nae aliuliza,
"He!!!! Leo kweli siku yangu, haya twende" Omary aliongea kinyonge
huku akisikitika.
Happy akamshika mkono Omary, kisha akaanza kutoka nae nje kwa
mwendo wa kunyata, yaani mwendo wa taratibu usiokuwa na vishindo.
Walipofika usawa wa mlango wa baf na ndio muda huo Mchungaji Wingo
alikuwa anafungua mlango ili akachukue sabuni chumbani.
Ghafla tu Omary na Happy binti Mchungaji wakashuhudia mlango wa
bafu ukifunguliwa na wote macho yakawatoka pima mithili ya mtu
aliekwamwa na kitu kooni...
Happy akauwai mlango wa bafuni, akaushikilia, tena kwa kuwa mlango
wenyewe ulikuwa unafunguka kwa nje akaamua aulalie kabisa, Omari
kuona hivyo akahisi kitakachomsaidia ni nduki tu. Akatoka mbio
kuelekea nje,
"we happy vipi, una nini leo?", Mchungaji Wingo alimuuliza binti
yake kwa sauti yenye mshangao huku akiusukuma mlango kwa utaratibu
mzuri ili asimdhuru binti yake aliyekuwa amelala,
"baba sijisikii vizuri, naona kizunguzungu", Happy aliongea huku
akiwa bado amelala chini.
Baba yake akamnyanyua, kisha akamrudisha chumbani kwake,
"nikupelekee hospital mwanangu?", Mchungaji Wingo alimuuliza binti
yake kwa sauti ya huruma,
"hapana baba, nafikiri ni tatizo la muda", Happy alijibu huku
akijifunika shuka,
"Hapana, lazima uende hospitali, ngoja nimalize kuoga nikupeleke"
Mchungaji Wingo alimwambia mwanae,
"Baba hii hali ya kawaida tu, itaisha" Happy alijibu baba yake,
"Usichukulie vitu kirahisi rahisi, we jiandae tu nikupeleke"
Mchungaji Wingo aliongea huku akitoka nje.
"hii ya leo balaa, sijui baba angenichukuliaje?", Happy alijiuliza
mwenyewe huku akiwa na tabasamu la mshangao na pia akimshukuru
Mungu kwa kumuepusha na dhahama hii.
*******************
Omari alipotoka kwa mchungaji mbio mbio mpaka alipofika nyumbani,
akasukuma mlango akaingia kwa fujo hadi ndani,
"ehe, vipi mwenzetu?", Omari alipokewa na sauti ya Sajenti Minja
aliyekuwa anamshangaa,
"nilikuwa nakimbia kimbia, kuweka mwili fiti", Omari alijibu akiwa
katika tabasamu la uongo huku akipumua bila mpangilio,
"haya bwana, mi nilifikiri umefumaniwa na mke wa mtu uko, maana
mbio ulizokuja nazo si mchezo", Sajenti Minja aliongea na kufanya
vicheko vilipuke sebule yote.
"Hanna mjomba, huku ugenini siwezi kufanya hivyo" Omary alijibu
huku akijilazimisha kutabasamu,
"Sisi tutajuaje bwana, nyie vijana mna mambo mengi" Mama Kayoza
aliongea,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hakuna mama" Omari aliongea huku akiingia ndani, akamwita Kayoza,
wakaingia ndani,
"duh, jomba uko noma", Omari alianza kwa mtindo huo,
"vipi tena baab?", Kayoza akauliza kwa mshtuko,
"mchungaji kanikuta juu ya mwili wa mwanae kaka", Omari akapasua
lililomkuta,
"naisi kama sijakusikia vizuri vile, ebu rudia", Kayoza akauliza
kwa stahajabu,
"nimesema kuwa, mchungaji kanikuta ndani kwake", Omari akaongea
tena alichomaanisha,
"ikawaje kaka?", Kayoza akauliza huku akiwa bado haamini
anachoambiwa.
Omari akamsimulia yote, mpaka alipofanikiwa kukimbia.
"duh, pole mwanangu", Kayoza akampa pole Omari,
"Cha kushukuru ni kuwa nimetoka salama" Omary aliongea huku akivua
fulana yake,
"Sasa huyo Happy kwa hali uliyomuacha nayo si itakuwa baba yake
amejua?" Kayoza aliuliza,
"Sijui bwana, kama baba yake atahisi labda inaweza kuwa tatizo, ila
kuniona hajaniona" Omary alimjibu mwenzake,
"Ila usirudie kufanya ujinga kama huo tena, yule mwanamke ni
shetani angalia usiwe unamsikiliza kila anachokushawishi" Kayoza
alimshauri Omary,
"haina noma, kuna mpya gani hapa?", Omari akauliza,
"kesho saa nne tutaenda kwa mganga", Kayoza akamtaharifu Omari.
"maeneo gani",Omari akauliza,
"mi mwenyewe sijajua bado", kayoza akajibu,
"Dah, Mimi nina wasiwasi yasije yakatokea kama ya kwa yule mganga"
Omary aliongea,
"Sasa usiseme hivyo, cha muhimu ni kumuomba Mungu tu atusaidie"
Kayoza alimwambia Omary,
"Mungu tunamuomba ila pia tahadhari lazima" Omary alimwambia
Kayoza,
"Basis usiende, nitaenda Mimi na mjomba" Kayoza aliongea huku
akionekana hajafurahishwa na maneno ya Omary,
"Nitaenda tu" Omary aliongea kwa upole baada ya kugundua Kayoza
amepaniki,
"Sasa kama utaenda kwanini unaleta maneno ya kutishana?" Kayoza
aliuliza,
"Basi yaishe kaka, nisamehe kwa maana sikudhani kama utamaindi"
Omary aliamua kujishusha ili mambo yaishe,
"Hatugombani hapa, tunaeleweshana tu" Kayoza alimwambia Omary,
"Sawa nimekuelewa ndugu yangu" Omary alijibu,
"Kama umenielewa sawa, Mimi nipo sebuleni" Kayoza aliongea huku
akielekea nje na kumuacha Omary akiwa amejimwaga kitandani.
.*******************
Kesho yake asubuhi Sajenti Minja aliwapitia wakina Kayoza, na
safari ya kwenda kwa mganga ikaanza.
Njia nzima hakuna alieongea, ndani ya gari kulikuwa na mziki laini
wa unbreak my heart ulioimbwa na mwanamama wa kimarekani
anayejulikana kama Tony braxton.
Sajenti Minja alikuwa akiufatilia ule wimbo kwa sauti ya chini,
Omari yeye alikuwa na mawazo yake, Kayoza pia alikuwa anafikiria
anachokijua.
"Huo wimbo vipi?" Kayoza aliuliza baada ya Sajenti Minja kurudia
zaidi ya mara tatu kuupiga ule wimbo,
"Si naupenda tu" Sajenti Minja alijibu kwa kifupi,
"Mimi najua mtu akiupenda wimbo lazima kuna tukio linahusihana na
huo wimbo" Omary alichangia,
"Ebu acheni ujuaji, sasa mnataka niweke nyimbo gani? au niweke hayo
manyimbo yenu yenye yo yo nyingi?" Sajenti Minja aliuliza,
"Wewe tuambie tu kuhusu huo wimbo, acha kujikanyaga" Kayoza
alimwambia mjomba ake huku akicheka,
"Au shangazi hasomeki?" Omary akaongeza na swali,
"Ebu niacheni bwana" Sajenti Minja aliongea huku akizima redio ya
gari.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa mganga waliingia mishale ya saa sita kasoro robo, wakapokelewa
na msaidizi wa mganga, ila kwa bahati nzuri hawakukuta foleni
ndefu, watu walikuwa wachache tu.
Baada ya nusu saa, zamu yao ikafika wakaingia ndani, kile kitendo
cha kayoza kuingiza mguu katika mlango wa nyumba ya mganga, pale
pale akabadilika na akawa katika taswira ya kutisha sana, ila
alikuwa hawezi kutembea, aliganda pale pale, Sajenti Minja alipata
uoga huku akidhani kuwa zile bakora za kipindi kile zinarudi tena
kwa hiyo akakaa mbali kabisa na Kayoza hata alipogundua kuwa Kayoza
ameganda pale, bado alikuwa anaogopa kumsogelea. Unacheza na viboko
nini.
Mganga akapelekewa taharifa kuhusu lile tukio, Mganga ikambidi
atoke katika chumba chake cha kazi na kwenda mahali alipo Kayoza,
alipofika akamuangalia zaidi ya dakika kumi, kisha mganga akafunga
macho yake, alafu akatoa pumzi kumuelekea kayoza kwa njia ya mdomo,
pale pale Kayoza akadondoka chini huku akiwa katika ile ile taswira
ya kutisha.
"Mtoeni nje" Mganga akawaamuru wamtoe nje, wakambeba wakampeleka
nje, wateja waliokuwa nje wanasubiria tiba wote walikimbia
walipomuona Kayoza katika hali ile ya kutisha.
"Aliyekuja na huyu kijana yupo Wapi?" Mganga aliuliza huku
akimuangalia msaidizi wake,
"Yule kule" Msaidizi wake aliongea huku akinyoosha kidole kuelekea
alipo Sajenti Minja,
"Mbona amekaa mbali sana?" Mganga aliuliza huku akishangaa,
"Hata sisi hatujui, labda anamuogopa" Msaidizi wake alijibu,
"Kamuite" Mganga alimtuma msaidizi wake na yule bwana akaenda
kumuita.
Sajenti Minja alipofika alimsalimia mganga kisha mganga akawaambia
aliefuatana na Kayoza amfuate ndani, Sajenti Minja na Omari
wakamfuata mganga.
Mganga alikuwa ni mwanamke wa makamo, alikuwa na macho mekundu
sana, akamkazia macho Sajenti Minja, kisha mganga akasema,
"Minja mna tatizo kubwa sana" Mganga aliongea na Sajenti Minja
alishtuka kusikia mganga kamtaja jina lake, ila akapata matumaini
ya kumaliza tatizo,
"ila kwako naamini litaisha", Sajenti Minja alijitutumua na kumjibu
mganga,
"bibi yake mzaa baba yupo hai", Mganga akamtupia swali Sajenti
Minja,
"ndio mama", Sajenti Minja akajibu,
"anaishi wapi?", Mganga akauliza tena huku akiwa amemkazia macho
Sajenti Minja,
"anaishi Bukoba vijijini", Sajenti Minja akajibu,
"Sasa itabidi huyo kijana apelekwe uko", Mganga akawaambia Sajenti
Minja,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"tumpeleke wapi?", Sajenti Minja akauliza ili apate ufafanuzi
zaidi,
"mpelekeni kijijini, kijijini kwa bibi yake" Mganga aliongea akiwa
amefunga macho.........
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment