Search This Blog

SIRI ZA GIZANI - 1

 





    IMEANDIKWA NA : FRANK DAVID



    *********************************************************************************



    Simulizi : Siri Za Gizani

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Naitwa Awa, mtoto wa kwanza katika familia ya mzee Shaheem, mama yangu mzazi alifariki dunia nikiwa mdogo sana hivyo nilikuwa katika malezi ya mzazi mmoja yaani baba yangu tu. Ila nilikuwa namshangaa sana baba kipindi nipo mdogo! maana baba alikuwa anapenda sana kuswali, yani alikuwa hapitwi na swala maana kila baada ya mda anaenda msikitini, sasa kilicho kuwa kina niumiza zaidi ni zile swala za jioni ambazo baba alipenda tuswali pamoja kabla ya kulala, sasa hapo ndipo nilikuwa sipendi kabisaaaa, yaani nili tamani

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kujifungia chumbani na kulala mapemaaa ili asiniite. Uvumilivu ulinishinda ikabidi niwe muwazi tu, ili kumuuliza baba kwanini ana swali kila siku, anafaidika nini sasa? maana mimi nilikuwa naona kama upotezaji wa mda. Nikamuuliza kwamba, "baba hivi kwanini unapenda kuswali faida gani unaipata baba yangu" baba akasema, "weee, unaongea nini hicho, kwahiyo wewe hupendi kuswali au" baba akasema, "mwanangu kuswali ni muhimu, unapo mkumbuka mungu na yeye pia anakukumbuka na anakuepusha na mengi sana, maana dunia ya sasa ni ya laana, ushetani, uzinzi, na matukio mengi ya ajabu na sio hivyo tu, ndugu zangu wengi nimewapoteza kishirikina tu kwa sababu ya uzembe wao wa kumkumbuka mungu, maana mfano kama baba yako mkubwa alie fariki mwaka jana, yeye huyo angekuwa ana swali kwa imani yeye na familia yake nzima wasinge fariki kizembekizembe vile" nikamuuliza baba kwamba, "kizembekizembe kivipi baba" baba akasema ni hadithi ndefu sana hatuwezi kuimaliza sahivi maana tayari ni usiku ila kesho mapema nikumbushe nikusimulie. Kweli kesho yake mapema nikam'bana sana baba anisimulie nijue kwanini baba mkubwa alifariki kizembe. Baba akasema "dahh Awa binti yangu, usahau tu, haya sawa ebu keti kwenye kiti nikusimulie" nilipo kaa ndipo baba akaanza kunisimulia kwamba. "baba mkubwa wako alikuwa anaitwa Abdaal, yeye alikuwa na mke wake pamoja na watoto wawili, sasa kaka Abdaal pamoja na mke wake walikuwa wasomi sana na wote walikuwa wanajiweza kifedha, hivyo familia yao ilikuwa ya upendo sana na furaha pia, walikuwa na nyumba nzuriii, magari matatu na biashara mbalimbali, siku moja, Afra yaani mke wa kaka Abdaal, alikuwa ametembelewa na wageni nyumbani kwake..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wageni walipo mtembelea mke wa kaka yangu, baada ya mda wakaitaji kuondoka, kwasababu ilikuwa tayari ni usiku mida ya kama saa mbili hivi. Shemeji akaamua kuwa sindikiza ili awatoe nje kidogo kisha waendelee na safari yao. Sasa wakati shemeji yangu anarudi nyumbani bahati mbaya kiatu chake cha kushoto kikakatika, maana kilikuwa ni kiatu cha wazi, shemeji hakuwa na jinsi hivyo akaamua kukibeba ili arudi nacho nyumbani kisha kipelekwe kwa fundi kushonwa. Sasa wakati shangazi anatembea mguu ukiwa peku, bahati mbaya akakanyaga mdudu bila kujua ila alihisi kama amekanyaga kitu kisha kikabonyea, ila kutokana na lile giza hakuweza kuangaika kutazama amekanyaga nini wakati ule. Sasa kumbe ulikuwa ni uchawi tu, majirani zake wamemtumia kusudi tu ateseke na familia nzima iwe katika majonzi, kipindi kaka amerudi kutoka kazini akakuta familia yake ipo na furaha na walikuwa na upendo sana. Kibaya zaidi ni pale ilipo fika saa nane usiku sasa, yule mdudu ambae shemeji alimkanyaga ndiyo akaanza kufanya kazi, huwezi kuamini shemeji yangu alianza kuchemka sana mwili, yaani jasho lina mtiririka sana, kaka akajaribu kumkanda na maji ya baridi ila hari iliendelea kuwa mbaya, kipindi shemeji analia maana alikuwa anaogopa sana ugonjwa, kakidonda kadogo tu, kakaanza kujitokeza mguuni, shemeji hakuhisi chochote akaendelea kukaa tu anajua labda kidonda ni kidogo kitapona, lakini kila kulipo kuwa kunakucha mguu unauma, unawasha, anapata maumivu makali mpaka akaacha kwenda kazini, kaka akaamua kumpeleka mke wake hospitali, alipo fika wakampa dawa na kumchoma sindano, kumbe hapo pia ndipo wakawa wamearibu kila kitu, maana uchawi ukichanganya na madawa ya kawaida unakuwa unaua kabisa, mguu wa shemeji ulianza kuvimba, ulivimba sana ukawa mkubwa kuzidi ata mwili wake, ata watoto wakaanza kuogopa! kaka yangu akashangaa kumuoa mke wake vile, ikabidi arudi hospitali, alipo fika huko, daktari akasema "hii itakuwa kansa hivyo itabidi tumkate mguu wake ili asiendelee kuvimba hivi maana anaweza akafariki tukiendelea kusubilia". Shemeji alipo ambiwa kukatwa mguu alianza kulia sana akasema, "mme wangu ni bora tu nife, siwezi kutazama nakatwa mguu, nimemkosea mungu mimi nimekosa nini jamani ehh"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shemeji alilia sana pale hospitalini, maana alihisi kukatwa mguu wake itakuwa ni kama kapoteza kitu kikubwa sana katika maisha yake na isitoshe alikuwa ni mwanamke mrembo alie vutia sana na alipenda kupendeza mda wote, hivyo ilikuwa inamuuma sana. Kaka akamwambia, "mke wangu, naomba ukubali tu ukatwe huo mguu, kwani wewe hujioni mguu ulivyo kuwa, kila siku mguu unaoza, kila siku unauma, usiku hatulali mke wangu unalia tu ndani, naomba ukubali tu kukatwa, mimi siwezi kukuacha nitakuwa na wewe kwenye changamoto zozote za dunia" huwezi kuamini shemeji alikataa kabisa kukatwa ule mguu, sasa kutokana na ule ugonjwa ikabidi kaka amuite mama kutoka kijijini aje kukaa nyumbani kwake ili amuuguze mke wake, maana biashara zao zilianza kuyumba kutokana na kukosa mda wa kuziangalia, maana walitumia mda mwingi kumuuguza shemeji. Mama yetu alisafiri kutoka kijijini akaenda kukaa pale nyumbani kwa kaka kumuuguza shemeji. mama alienda na kuku wawili moja jogoo nyingine kuku wa kutaga kawaida.

    Watoto wa kaka yaani Ibra na Nasra walifurahi sana kumuona bibi yao. Ila kumbe bibi yao alikuwa mchawi na alitoka amefungasha dawa za kutosha kutoka kijijini akaja nazo mjini, kuisumbua familia ya kaka, sisi hatukujua kama ni mchawi maana alitulea vizuri tu tangu tukiwa wadogo. Alafu na wale kuku wawili, kumbe jogoo alikuwa ni Ibra, alafu kuku wakutaga kawaida alikuwa ni Nasra, hivyo kuku ambayo ingechinjwa kwanza basi mtoto wa kaka mmoja angekufa na kama zinge chinjwa zote pia wangefariki wote. Hakuna alie fahamu kabisa kama mama angeweza kufanya mambo kama yale, maana tulikuwa tuna muheshimu sana sisi.

    kaka alipo kuwa anaenda kazini, mama alikuwa anaonyesha upendo sana mchana kwa mkwe wake, wakawa marafiki sana, lakini kumbe mama hakupenda ata mkwe wake apone alitamani kuona ata anakufa tu, Sasa kwa sababu ya ule mguu kumuuma sana shemeji, hivyo ata kujisaidia kwake ilikuwa ni ngumu sana, sasa bibi alicho kuwa anafanya ni kuchukua kopo kisha analiweka karibia na sehemu nyeti za shemeji ili aweze kujisaidia, lakini ilikuwa aisadii kabisa maana mkojo wake wote ulikuwa unaishia chini. Shemeji alikuwa analia tu, maana hakuamini kama angeweza kujikojolea na utu uzima wake wote,



     Shemeji yangu alikata tamaa na maisha, maana ule uozo wa mguu ulianza kupanda juu kwenye goti, hivyo unge enea mpaka mapajani. Mama mkwe wake akamwambia "mwanangu usilie utapona nitajitahidi upone tafadhali nakuomba usiwe na mawazo" shemeji akajibu "sawa mama" shemeji alihisi labda mama ni msaada mkubwa kwake, ila kumbe mama yetu alikuwa anafurahia kumuona mkwe wake katika ile hali na alipanga aangamize familia nzima. Siku moja usiku wakiwa wote wamelala taa zimezimwa kuna gizaaa, mama akaamka polepole kisha akachukua mkojo wa shemeji alafu akatoka nao n'je kisiri bila mtu yoyote kujua. Kwasababu ule mkojo ulikuwa kwenye kopo ndipo mkwe wake shemeji akaka juu ya lile kopo kisha akaanza kucheka kichawi, haha! Haha! Huku akiwa anaimba nyimbo zisizo tambulika, baada ya hapo akatema mate kwenye ule mkojo alafu akaumwaga mlangoni, sasa wakati yupo nje ya nyumba ana ruka ruka, mtoto wa kaka mmoja yule Ibra akasikia kama kuna kitu kwa nje, ikabidi achungulie dirishani, alipo chungulua akaona kuna mtu yupo uchi kabisa arafu anarukaruka, kiukweli yule mtoto aliogopa kutazama mambo kama yale, hapo hapo akarudi kitandani kisha akajifunika shuka kabisa ili asione tena, maana

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ilimshtua na kibaya zaidi hakuweza kugundua kama ni bibi yake, kumbe masikini, yale mambo aliyo yafanya mama yalikuwa mabaya maana yalipelekea sehemu nyeti ya shemeji yetu kubadilika na kupata vidonda na akikaa nusu saa tu bila kuoga anatoa harufu mbaya sana, shemeji alihisi labda ni kansa imepanda hadi kwenye umbile lake, hivyo akawa anaogopa kusema, ila walikuwa wanamshangaa sana maana alikuwa anapenda kuoga yaani kila mda yeye anaenda bafuni tu. Mkwe wake alikuwa anajua kuwa yeye ndiyo kafanya vile lakini alikuwa anacheka tu na kufurahia maovu yake. Ndugu na jamaa wa shemeji kila walipo kuwa wanakuja kumtazama ndugu yao wanakuta hali inaendelea kuwa mbaya, kila siku haponi tu. Ikabidi ndugu na shemeji wakae kikao kuangalia ni jinsi gani wanaweza kumsaidia, sasa kwasababu kikao kilikuwa kimechukua mda, hivyo shemeji asinge weza kuoga kila mda,kama kawaida yake, ikabidi ajikaze tu ili asigundulike, sasa kutokana na kukaa sana kwenye kikao, harufu mbaya ikaanza kumtoka shemu mbele za watu.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog