Search This Blog

SIRI ZA GIZANI - 2





    Simulizi : Siri Za Gizani

    Sehemu Ya Pili (2)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Harufu ya shemeji ilipo zidi kwenye kikao, ndugu na jamaa wakashindwa kuvumilia ikabidi waongee tu, "shemeji hiyo harufu mbaya inatokea wapi, yaani kama mizoga ya wafu kunanuka sana hapa" mkwe wake shangazi alie mfanya shemeji awe vile akaanza kucheka "hahahah, ata mimi nahisi harufu mbaya",mme wake shemeji yaani kaka, akasema, "hii harufu kila siku nikiwa nimelala na mke wangu uwa nahisi kwa mbali, sijui ni kitu gani kimeoza maeneo ya hapa nyumbani" shemeji akauliza "mke wangu kitakuwa nini hicho maana balaa zimezidi kwenye familia yetu" shemeji akaanza kulia maana ukweli alikuwa anaujua yeye kwamba harufu inatokea sehemu zake za siri, kaka akasema, "mke wangu unalia nini mbona hatukuelewi" shemeji akasema, "mimi najua wote mnajua kuwa mimi ndiye nanuka, maana n'zi wamenijaa na kunizunguka mimi" kila mtu akaguna, "mhhh" shemeji akasema tena,

    "mme wangu kwa sasa hivi hatua niliyo fikia ni bora tu nife, maana nimepata kidonda cha ghafla sehemu zangu za siri, na hii harufu mbaya mnayo hisi nyie inatoka kwenye hichi kidonda changu kwa ndani, nakosa raha ya maisha nakosa amani, maana kila mda mimi naenda bafuni, na kinacho nikwaza, ni pale ninapo waona wadudu wadogo aina ya funza wanatembea kwenye kidonda, sijui ni nani ananifanyia hivi, maana natembelewa na funza kabla sijafa, nikifa je?" wakati wanaongea mda ule na hewa pia ilikuwa inaendelea kuchafuka, hivyo shemeji akaomba aende bafuni kujimwagia maji kwanza. Wale walio kuwa wamebaki kwenye kikao wakamwambia kaka kwamba, "itabidi ukamuangalie mke wako hicho kidonda kina fananaje ili utwambie tujue jinsi ya kumsaidia, maana sio kwa harufu hiyo, hiyo harufu sio ya kawaida kwenye mwili wa binadamu alie hai"ikabidi kaka aende chumbani kumuangalia mke wake amekuwaje, wakati huo mkwe wa shemeji amekaa kimya tu na anaonyesha sura ya huzuni uwezi ata kumgundua kama ni yeye anafanya mabaya hayo usiku gizani tena kisiri. Kaka alipo ingia chumbani akamkuta mke wake anajipulizia marashi kwa ndani ili harufu isije kwa ulahisi, kaka akamwambia, "mke wangu naomba nione hicho kidonda kilivyo" shemeji akaogopa na akakataa katakata, maana alihisi mme wake akiona tu jinsi alivyo oza, anaweza kumuacha na akaoa mke mwingine...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kaka yangu hakufanikiwa kabisa kuona ule uvimbe kwenye sehemu nyeti za mke wake, hivyo kaka hakutaka kabisa kumlazimisha mke wake maana alikuwa anampenda sana mkewe na kwakuwa alikuwa anaumwa akaona sio vyema kumlazimisha kitu ambacho hataki. Siku hiyo ikapita bila mafanikio yoyote, sasa kesho yake usiku mida ya saa nane kamili, mkwe wa shemeji aliamka mida hiyo kukiwa na giza sana akaenda kwenye chumba cha mjukuu wake wa kike binti Nasra, alipo fika chumbani akiwa amejifunga kitambaa chekundu kichwani, akafungua mkono wake wa kushoto kisha akapuliza unga alio kuwa ameushikilia kuelekea kwenye uso wa mjukuu wake, palepale nasra akaamka na kupanda kwenye mgongo wa bibi yake akiwa hajitambui na hasikii chochote, mama alimbeba Nasra watu wote wakiwa wamelala ndani, kisha akamuweka kwenye diaba chumbani kwake alafu akaweka na dawa mule kwenye diaba ili Nasra asiweze kabisa kuongea, sasa kulipo kucha kila mtu aliamka lakini cha kushangaza Nasra siku hiyo hakuamka, na wakati Nasra alizoeleka kuamka mapema kila siku pale nyumbani. Ikabidi waende chumbani kwake kumuangalia, walipo fika wakamkuta amelala, akiwa amejinyoosha, alafu akiwa na unga unga usoni, shemeji alijaribu sana kumuamsha binti yake lakini alikuwa haamki, kumbe mwili wa Nasra ulikuwa umewekwa kwenye diaba chumbani kwa bibi yake, na ule ulio onekana umelala hakuwa yeye Nasra mwenyewe bali ilikuwa ni kama egesho tu kuonekana Nasra amefariki, mama Nasra alijaribu kumuamsha Nasra ila ikashindikana ndipo mkwe wake akasema "mkwe usilie hii ni mipango ya mungu tu, huyu mtoto ameisha fariki tayari" shemeji alianguka chini hapohapo mpaka akajitonesha vidonda vya mguu wake, alilia akasema, "hii ni mikosi gani jamani nani anatufanyia hivi, binti yangu bado mdogo hajaona hata ndoto zake wameisha mchukua tayari, ehh mungu wangu nisaidie, bora nife ata leo lakini watoto wangu wasife, nime wazaa kwa uchungu sana" dahh kaka yangu alipo ona mke wake analia na mtoto kafariki alichoka sana, ilimuuma mnoo, kumbe hakujua ubaya wote ule alikuwa anaufanya mama yetu mzazi. Nasra alizikwa lakini kumbe hakufa yeye ni egesho tu, yeye alikuwa kwenye diaba chumbani na amekatwa ulimi alafu analishwa unga tu na bibi yake..



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nasra aliendelea kulishwa unga wa ugali tu mule kwenye diaba, na kila ilipo fika saa nane za usiku mda alio chukuliwa na bibi yake, Nasra alikuwa anatolewa kwenye diaba kisha anaanza kucheka na kuimba na bibi yake, na mala tu baada ya kuimba na kucheka bibi yake anamrudisha kwenye diaba kama kawaida. Ila kaka yake Nasra yaani Ibra kila alipo kuwa akilala alikuwa anaota ndoto za ajabu sana, na mala nyingi alikuwa anaota kuwa mdogo wake yupo hai hajafa, lakini kila alipo kuwa akimwambia baba na mama yake walikuwa hawamuelewi kabisa maana mtoto walimzika na msiba ulifanyika, mda mwingine Ibra alikuwa anachapwa kwa sababu ya usumbufu wake wa kila siku kwamba "dada Nasra hajafa, dada nasra hajafa uwa namsikia akiimba usiku, yaani namsikia kabisaa, akiimba usiku" hayo maneno alikuwa anayataja sana mpaka mama yake akaanza kumgombeza, lakini ibra kila siku alikuwa anaongea hivyo, maana kumbe bibi yake alivyo kuwa anaimba na kucheza usiku na nasra, ibra alikuwa anasikia maana yeye na nasra wote walizaliwa tumbo moja hivyo damu ilikuwa nzito, siku moja Ibra akiwa amelala aliota sauti ya dada yake imemuijia ikisema, "kaka ibra nenda kwenye kabuli langu" Ibra alikuwa muoga sana kutoka nje usiku, lakini ile ndoto ilimsumbua sana Ibra ikabidi afungue mlango aende nyuma ya nyumba yao kuangalia kabuli la mdogo wake maana ndipo walipo kuwa wamemzika kule kwa nyuma. Ibra alipo fika kwenye kabuli alishangaa sana maana alikuta ile sehemu ipo tambalale kabisa na hakuna kabuli lolote mda ule, ndipo Ibra akakimbia haraka kuingia ndani, akiwa analia huku watu wote wamelala, isipo kuwa bibi yake maana walikuwa ndani na Nasra wanacheza na kuimba ila hakuna alie kuwa anasikia zile sauti zaidi yao wawili.

    Siku moja usiku sana bibi yake nasra alikuwa anamuogesha nasra ili asitoe harufu mbaya chumbani maana tangu amfungie hakuwai kuoga ata siku moja. Sasa wakati anamuogesha ibra akawa amesikia sauti za maji kutoka kwenye chumba cha bibi yake huku bibi akisema kwamba "nasra geuka nikusugue na mgongoni kuchafu" ibra alipo chungulia vizuri kwenye kitasa cha mlango akawa amemuona Nasra anaogeshwa kama mtoto mdogo wakati ni dada tu anaeweza kuoga mwenyewe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ibra alipo muona ndugu yake anaogeshwa na bibi yake usiku kama ule, kiukweli hakuamini kabisa ikabidi asogeze jicho vizuri ili amuone kama kweli ni Nasra anaogeshwa na wakati kila mtu ameisha msahau akijua ni marehemu tayari. Ibra alipo mtazama vizuri kwa ukaribu akamuona kweli ndugu yake, dahhh alichoka maana Nasra alikuwa amekonda sana, sababu ya chakula kibaya, alafu zile nywere zake alizo kuwa amesuka kipindi anakufa ndo hizo hizo alizo kuwa nazo bado na zimechakaa kweli kweli.

    Sasa bibi Nasra alihisi kama kuna mtu anamchungulia mlangoni, hapo hapo akamrudisha Nasra kwenye diaba haraka sana. Kumbe Ibra alikimbia kuwa amsha wazazi wake waamke ili waje kumuona Nasra chumbani kwa bibi, Ibra akasema, "baba, baba, babaaa amka njoo umuone Nasra yupo chumbani anaogeshwa na bibi, baba amka nasra wetu hajafa baba", baba yake alitoka akaanza kumchapa Ibra akimwambia, "hivi we mtoto unamatatizo gani kwanini unapenda kutusumbua tukiwa tumelala lakini, mi nina mawazo yangu kibao hapa, mama yako anaumwa kansa naangaika na mawazo bado na wewe unaniletea za kuleta, mshezi kweli, kalaleee" kipindi baba yake anaongea vile, mke wake akasema "mme wangu unaweza kumchapa mtoto bila kujua labda mambo anayo yasema niya ukweli, ebu tumruhusu atwambie alicho kiona usiku wa leo" baba yake akasema, "umeona nini kwani" Ibra akasema, "baba bibi yetu ni mchawi, maana Nasra hajafa bibi ndiye anae chumbani" baba yake akasema, "we mtoto unawazimu gani lakini, hivi hizi laana utaziweka wapi wewe, yaani unamuita bibi yako mchawi una akili kweli" mke wake akasema " mme wangu usikasilike unajua watoto wetu hatukuwazoesha kukaa na bibi zao, labda wakiwaona walivyo zeeka wana hisi ni uchawi au uganga labda tumuelekeze aelewe na sio kumkalipia" Ibra akasema, "baba bibi ni mchawi, kama sio mchawi kwanini anaishi na Nasra peke yake, mwambie amtoe nasra nataka kucheza nae na mimi, kila siku yeye tu anacheza nae" mama Nasra akasema "yaweza kuwa kweli mme wangu" baba nasra akasema "we we we! Naomba msirudie kumuita mama yangu mchawi, yeye amenizaa mimi kama angekuwa mchawi si angeniua nikiwa mdogo, iweje aiteketeze familia yangu, acheni kumsingizia mama yangu bhana, Ibra akasema..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog