Search This Blog

SIRI ZA GIZANI - 3

 





    Simulizi : Siri Za Gizani

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ibra akasema "baba usibishe nimemuona dada Nasra kwa macho yangu akiogeshwa na bibi chumbani kwake", baba yake akasema "yaani kumbe wewe na mama yako sio watu wazuri kabisa hivi mnathubutu kumuita mama yangu mchawi" shemeji akasema, "mme wangu sio kwamba tunamuita mchawi jamani, mbona unataka ukuze maneno baba watoto lakini, uwezi jua ya mungu mengi labda mtoto kweli kaona, tufatilie zaidi" baba nasra akasema, "weeeeh, koma uchunguzi wa nini, mama yangu hawezi kuwa mchawi bhana sijawai ata kumuona na mzizi tangu nikiwa mdogo mimi, iweje mseme ni mchawi alafu wewe Ibra nikifanya uchunguzi nikakuta unaleta uongo uongo wako hapa naweza ata kukuua, sipendi masihala na mzazi mimi" baada ya kaka kuongea vile ndipo akamwambia mke wake amuitie bibi nasra ili wamwambie kuhusu tatizo lililo tokea. Kweli bibi nasra alitoka akiwa amevaa kanga zake mwilini.

    Baba nasra akamwambia, "mama habari za usiku, samahani mama yangu tumepata habari za kusikitisha, eti kwamba Nasra hajafa na wewe ndiyo upo nae ndani unamuogesha na kucheza nae humo chumbani kwako" bibi nasra alipo ambiwa hivyo akaanza kulia akisema, "mwanangu nimekuzaa na kukuweka tumboni miezi 9 leo hii unaniita mchawi kisa familia yako hii, kama ningekuwa mchawi ningekulea mpaka umri huu, sawa najua m'menichoka mi naondoka kijijini usiku huu huu na sitorudi tena hapa kwenu" baba nasra alipo sikia yale maneno alipiga magoti chini akasema, "mama yangu naomba msamaha tafadhali, ni huyu ibra katuamsha usiku usiku anatwambia huu upuuzi, kwamba kamuona Nasra chumbani kwako na amesisitizia kweli kwamba amekuona unamuogesha ndiyo maana nikakuuliza mama yangu, nakuomba sana usiondoke kwangu mama yangu" bibi Nasra akasema, "we ibra kwanini unakua muongo namna hiyo we Nasra umemuona kwangu lini, Nasra si ameisha fariki mjukuu wangu" ibra akasema, "bibi wewe ni mchawi, Nasra unae ndani, kama kweli hayupo ndani turuhusu tukakukague" bibi nasra akasema, "Mama nasra huyu mtoto unamleaje mbona hana heshima kabisa masikini" Ibra alichapwa sana siku hiyo kisha wakaenda kulala bila kugundua chochote.Bibi Nasra aliwaza sana jinsi ya kumzuia Ibra asigundue siri zake za usiku, ndipo akapata wazo la kumpofua macho ibra ili asione tena katika maisha yake....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Ibra alikuwa anakosa raha sana pale nyumbani, maana wazazi wake walijua kuwa Nasra kafariki lakini yeye kilicho kuwa kina muuma ni pale alipo kuwa akimuona dada yake anaogeshwa na usiku kaburi la Nasra alionekani bali linaonekana mchana tu.

    Siku moja mida ya saa nane usiku, Ibra alianza kusikia joto kali sana kwenye mwili wake, yaani ni usiku lakini joto lake ni kama la mchana hivi. Ibra alikosa usingizi kabisa masikini aka amka kisha akakaa kitandani.

    Joto lilipo zidi Ibra akaamua kuamka ili achukue kitambaa ajifute jasho, wakati amesimama sakafuni akasikia mtu anamshika begani, "wehh wehh" alipo geuka haraka akaona sura ya bibi yake mala ghafla ikaja sura ya mdogo wake, ibra akamwambia " dada Nasra mbona siku hizi utaki kucheza na mimi" Nasra akaachama mdomo wake kisha akamuonyesha ibra kuwa hawezi kuongea bibi yake tayari ameisha mkata ulimi kwa mbele, ibra aliogopa kumtazama dada yake akiwa vile akaamua kumshika kwanguvu Nasra alafu akaanza kupiga kelele "mamaaaa, babaaa, Nasra huyu hapa nimemkamata njooni" wazazi wake waliamka upesi kisha wakaenda chumbani kwa Ibra ili waweze kumuona Nasra mwenyewe, sasa kilicho washangaza ni kwamba, wanamuona Ibra kama kashika mtu kwa nguvu lakini mtu mwenyewe alie shikwa hawamuoni, wakamuuliza, "Ibra mbona kama umeshika hewa mwanetu, nasra yuko wapi" ibra akasema "baba si huyu hapa nimemshikilia" baba akasema, "hatumuoni sisi mtu mwenyewe ebu acha ndoto za kishirikina rudi ulale", Ibra akasema, "mama njoo umshike Nasra bibi atamchukua, mama nisaidie kumshika"

    mama nasra alikuwa analia tu, "mwanangu simuoni nasra, simuoni kweli baba angu" Nasra alikuwa kawekewa madawa mengi sana na bibi yake hivyo kuonekana kwake kulikuwa kwa shida sana masikini, ila nasra alikuwa anawaona wazazi wake lakini hasingeweza kuwaongelesha maana ata ndimi yake ilikuwa imepunguzwa tayari, Ibra aliendelea kumvuta dada yake bila kumuachia huku akiwa analia na Nasra pia analia maana hawawezi kucheza tena masikini, sasa kumbe nasra alitoroka bibi akiwa amelala, bibi alipo shituka akakuta nasra ameingia kwa Ibra hapo hapo akamvuta kichawi nasra akapotea ghafla tu, ibra akasema "mama, Nasra amepotea tena" wazazi wa Nasra walilia sana mule ndani..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sasa Nasra alivyo vutwa kighafla na bibi yake kutoka chumbani, bibi yao alikasilika akasema, "hivi we Nasra kwanini hutulii, unataka nikudhoofishe mwili mzima usiweze kusimama au, sasa toka tena umo uone" Nasra alipo ambiwa vile alikuwa analia tu, maana yale mateso yalikuwa mazito sana, kwasababu alikuwa hatoki ndani na asingeweza kuonekana n'je kama zamani. Bibi Nasra alikuwa amenuna mpaka jicho likawa jekunduuu, akasema, "hivi unajua mwanangu akinigundua mimi ni mchawi nita aibika sana, sasa huyo kaka yako lazima na yeye nimkomeshe atakiona cha moto" Kumbe chumbani mwa ibra wazazi walikuwemo bado wanalia tu, maana kila walipo jitahidi kusahau kifo cha mtoto wao, Ibra alikuwa ana wakumbusha tu kwa matukio ya ajabu ajabu tu, mama Nasra akasema, "mme wangu hii ni mikosi gani jamani, nitazame mguu wangu ulivyo haribika, nusa harufu initokayo sehemu zangu za siri, haya sasa ebu kumbuka mtoto wangu Nasra alivyo fariki kimaajabu tu, hivi tutaishi kwa amani kweli jamani, alafu kila tukio linatokea usiku kuna siri gani za giza humu baba Nasra" Ibra akasema, "wazazi wangu mimi nateseka sana, maana kila ninapo lala tu dada nasra ananitokea ndotoni analia, na bibi ndiye amemficha dada Nasra yaani dada yangu hajafa mama" baba Nasra akasema, "weee husimtaje mama yangu katika hili nakuomba sana, alafu wewe mtoto umeisha kuwa muhuni sana, hivi hutambui kuwa yule bibi yako, ni kama mzazi wako, ata kama hajakuzaa lakini yeye ndiye mzizi bila yeye kunizaa mimi, tungekuzaa vipi sasa" mama Nasra akasema, "mme wangu tatizo lako humsikilizi mtoto unazalau maono yake mme wangu" Ibra akasema "wazazi wangu kama mnataka kuamini kuwa Nasra hajafa, twendeni kabulini kwake, mkiliona kaburi lake usiku mjue amekufa, na msipo liona muamini ninacho wambia hajafa, kipindi wanapanga kutoka nje kumbe bibi nasra alikuwa anawasikia tu, akapuliza dawa haraka sebureni! Sasa wakati wanafungua mlango wa sebreni kutoka nje, hakuna alie weza kufungua, maana baba alijikuta anachoka ghafla tu, Ibra alilala kabisa pale mlangoni na mama Nasra uvimbe wa mguu ulizidi maumivu ata kutembea alishindwa, kwa sababu ya dawa iliyo pulizwa na bibi Nasra.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kipindi Ibra na wazazi wake wameishiwa nguvu pale sebreni, hakuna ata mmoja alie weza kugundua kama kuzidiwa nguvu kule ni bibi Nasra alisababisha, na alifanya vile kusudi wasiweze kugundua kuwa kaburi la Nasra alionekani usiku. Mama nasra alilia sana siku hiyo kwasababu ule mguu ulimuuma sana, baba nasra alikuwa anasema, "vumilia mke wangu utapona mama Nasra" ibra akasema "baba hamka tukaangalie kaburi sasa" baba Nasra akasema nimechoka sana mwanangu tuta angalia kesho" kweli walilala pale mpaka saa 2 asubui, bibi Nasra alipo toka chumbani kwake akajifanya kama haelewi akasema, "vipi wanangu mbona kama mmelala hapa sebreni tatizo nini" wote wakajishangaa wakaamka na kuendelea na shughuri zingine. Ibra hakulizika kabisa na maisha ya pale nyumbani kwao akakaa na kuwaza kwamba "mhh hivi kwanini bibi anatufanyia hivi lakini, ata kama yeye ndiyo mzizi baba anavyo sema, lakini kwanini anatuloga, hatuishi kwa raha kama zamani tunateseka tu ngoja nimfate nimueleze, kama atanipiga sawa" ibra akaenda mpaka chumbani kwa bibi yake bila kugonga hodi, alivyo ingia tu masikini, akamkuta Nasra amepakwa dawa nyingi sana usoni na anasukwa nywere na bibi yake, bibi alikuwa bado hajamuona Ibra, ila kutokana na ibra kuona mambo kama yale alishindwa kuvumilia kabisaa, akapiga kelele, "bibiii unamsuka dada Nasra kwanini unafanya hivi lakini" bibi aligeuka kwa hasila jicho lekunduu, akasema "We ibra kwanini unaingia bila kugonga" Ibra akasema, "namtaka dada Nasra huyo hapo unamsuka" bibi nasra akasema naona umezidi kunifanyia ushenzi lazima nikukomeshe" Nasra hakuweza kuongea chochote yeye alikuwa kimya tu, ila ibra alishangaa tena kuona Nasra haonekani maana bibi yake alimficha kishirikina, Ibra hakukaa kimya akawafata wazazi wake kisha akawambia "baba na mama nataka kuwambia jambo" mama yake akasema, "twambie" kipindi Ibra ana achama mdomo anataka kusema alivyo muona Nasra, wazazi wake walishangaa, kuona ibra anashindwa kutoa sauti kabisa mdomoni mwake, ibra alijitahidi kuongea ila ikashindikana, kumbe tayari bibi yake alikuwa ameisha mfanya Ibra bubu, na asinge weza kuongea katika maisha yake yote, na bibi Nasra akapanga kumpofua macho Ibra ili asione na kusema chochote tena...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog